Shule Ya Upili-Wps Office

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

SHULE YA UPILI YA KUTWA YA NAKURU

KIDATO CHA TATU

MUHULA WA PILI 2024

KARATASI YA KWANZA

MAAGIZO

1. Jibu swali lifuatalo katika nakala uliyopewa.

2. Insha yako isipungue maneno 400.

Swali

Fadhila ni miongoni mwa wanafunzi waogombea nafasiya kiranja katika shule ya upili ya kumekucha .
Hekima anamhoji kuhusu mikakati atakayoweka ili kuboresha hali ya maisha shuleni . Andika mahojiano
hayo .

Mwongozo

1.Hii ni insha ya mahojiano. Vipengele vifuatavyo vijitokeze:

a.Muundo

Kichwa

Kiandikwe kwa herufi kubwa. Kichwa kitaje ni mahojiano baina ya Fadhila na Hekima, yanafanyika wapi
na yanahusu mada gani. Kwa mfano, MAHOJIANO KATI YA HEKIMA NA FADHILA KUHUSU MIKAKATI YA
FADHILA YA KUBORESHA HALI YA MAISHA SHULENI.

Utangulizi

i.Maamkuzi yajitokeze

ii.Makaribisho kutoka kwa mhoji - Hekima.

iii.Kiini cha mahojiano kijitokeze hapa

. iv.Mhoji anaweza kumhongera mhojiwa ama kwa kufika kwenye mahojiano au kwa kujitosa kwenye
kinyang'anyiro.

Mwili

Hoja zijadiliwe hapa. Kila hoja kwenye aya.

c.Maudhui Baadhi ya hoja ni:


i.Kuimarisha nidhamu shuleni kupitia kwa shughuli za ushauri nasaha

. ii.Kuleta mshikamano miongoni mwa wanafunzi.

iii.Kuboresha uhusiano kati ya wanafunzi na walimu.

iv.Kuhimiza kushiriki katika michezo na ukuzaji wa talanta.

v.Kukuza uhusiano kati ya walimu, wafanyakazi na wanafunzi.

vi.Kuimarisha juhudi za usafi. Kwa mfano, kuweka ratiba ya kufanya usafi shuleni.

vii.Kuhimiza huduma kwa jamii kwa mfano, kutoa ufadhili/ kuwahudumia wenye uhitaji kwa kuanzisha
mfuko wa kuchangia

. viii.Kuhimiza usimamizi wa shule kuzingatia lishe bora.

ix.Kuhimiza usimamaizi wa shule kuboresha miundomsingi. x.Kuimarisha mawasiliano shuleni.

xi.Kuboresha utendakazi wa viranja

xii.Kuhakikisha usalama shuleni kwa kuwahimiza wadau kuweka mikakati mwafaka.

(xiii) Kupigania haki/ kuwatetea wanaodhulumiwa.

Hitimisho

1.Kuhusu mada na wa kimuundo- ajumuishe mawazo yake.

2.Mhoji anaweza kutoa muhtasari wa hoja zilizojadiliwa au msimamo wake kuhusu hoja zilizojadiliwa.
3.Mhoji anaweza kumshukuru mhojiwa kwa kufika.

Tanbihi: Mtindo

i.Hoja zijadiliwe kwa mtindo wa kimazungumzo.

ii.Upashanaji zamu ufaao udhibitiwe na mhoji.

iii.Mahojiano yazingatie lugha rasmi. Maneno ya misimu yanapotumiwa yatiwe kwenye nukuu.
iv.Mahojiano yawe na dayalojia ya kidrama; majina ya mhoji na mhojiwa yaandikwe pambizoni na
kufuatwa na koloni kabla ya kauli halisi.

You might also like