Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 1

Darajia ya Kisemantiki

Semantiki hujikita kuchunguza lugha ya kitamathali na miundo ya lugha ambayo


ni sifa muhimu ya kuchunguza matini ya kifasihi tunapotumia nadharia ya
Umitindo. Ni jinsi matumizi ya lugha yanavyoathiri maana kwa njia fulani.
Ukiushi wa aina hii unahusu matumizi ya maneno na jinsi maana hiyo
inavyofasiriwa katika hali za kawaida. Mara nyingi huhusisha matumizi ya maneno

Huchunguza maana kwa njia ambazo si za kawaida kimaana. Darajia hii hujikita
katika matumizi ya tamathali za usemi: Mbinu za kinaya, kejeli, mbinu ya kweli-
kinzani (paradoksi,) sitiari, balagha, ndoto, majazi, jazanda , taswira, taharuki,
kisengere nyuma, kisengere mbele, takriri, kejeli, chuku, sadfa, tashhisi, tashbihi

Vilevile, huhusisha matumizi ya jazanda, yaani lugha ya picha aidha za kimaelezo


au za kiishara (ambazo si taswira au picha tu bali zina ujumbe wa ziada). Maelezo
haya ni kulingana na; (Leech na Short 2007:101, Wamitila 2008:518).
• tawi la semantiki kwa sababu ndilo tawi huchunguza lugha katika kiwango
cha maana. Huchunguza maana ya maneno yanayopatikana katika lugha
husika, iwe ya kifasihi au ya kiisimu. Pia tulizingatia viwango vingine viwili
vya ukiushi ambavyo ni: Kiwango cha maandishi/grafolojia na kiwango cha
umbo.

• Kiwango hiki kilitufaa sana kwa sababu kama tulivyoeleza, mtindo ni jinsi
lugha ilivyotumiwa na kuathiri maana kama inavyotumika kwa njia ya
kawaida. Kiwango hiki pia kilituwezesha kuhakiki tamathali za usemi
tulizoteua kuzichanganua katika kazi hizi nne teule za Sanja.

• Kwa muhtasari mtindo unaweza kuelezwa kama mazoea ya matumizi ya


lugha ya mtu au jamii-lugha fulani. Nayo nadharia ya Umitindo hujihusisha
na uhakiki na fasiri ya matini katika mtazomo wa Kiisimu kama taaluma
ambao una uhusiano wa karibu na mtazamo wa Kifasihi.

You might also like