Professional Documents
Culture Documents
Semantiki Na Sintaksia Katika Fasihi
Semantiki Na Sintaksia Katika Fasihi
Winne Mtega
Mtegawinnie19@gmail.com
Sintaksia ni nini?
Aidha, Habwe na Karanja (2004) wanaeleza kuwa sintaksia kuwa utanzu wa isimu
unaoshungulikia muundo wa sentensi na elementi zingine zinazounda sentensi kategoria za
maneno, vikundi ann vishazi.
MAWANDA YA KISINTAKSIA
Semantiki
Semantiki hujikita kuchunguza lugha ya kitamathali na miundo ya lugha ambayo ni sifa muhimu
ya kuchunguza matini ya kifasihi tunapotumia nadharia ya Umitindo. Ni jinsi matumizi ya lugha
yanavyoathiri maana kwa njia fulani. Ukiushi wa aina hii unahusu matumizi ya maneno na jinsi
maana hiyo inavyofasiriwa katika hali za kawaida. Mara nyingi huhusisha matumizi ya maneno
Huchunguza maana kwa njia ambazo si za kawaida kimaana. Darajia hii hujikita katika matumizi
ya tamathali za usemi: Mbinu za kinaya, kejeli, mbinu ya kweli-kinzani (paradoksi,) sitiari,
balagha, ndoto, majazi, jazanda , taswira, taharuki, kisengere nyuma, kisengere mbele, takriri,
kejeli, chuku, sadfa, tashhisi, tashbihi
Vilevile, huhusisha matumizi ya jazanda, yaani lugha ya picha aidha za kimaelezo au za kiishara.
Maelezo haya ni kulingana na; (Leech na Short 2007:101, Wamitila 2008:518).
• tawi la semantiki kwa sababu ndilo tawi huchunguza lugha katika kiwango cha maana.
Huchunguza maana ya maneno yanayopatikana katika lugha husika, iwe ya kifasihi au ya
kiisimu. Pia tulizingatia viwango vingine viwili vya ukiushi ambavyo ni: Kiwango cha
maandishi/grafolojia na kiwango cha umbo.
• Kiwango hiki kilitufaa sana kwa sababu kama tulivyoeleza, mtindo ni jinsi lugha
ilivyotumiwa na kuathiri maana kama inavyotumika kwa njia ya kawaida.
• Kwa muhtasari mtindo unaweza kuelezwa kama mazoea ya matumizi ya lugha ya mtu au
jamii-lugha fulani. Nayo nadharia ya Umitindo hujihusisha na uhakiki na fasiri ya matini
katika mtazomo wa Kiisimu kama taaluma ambao una uhusiano wa karibu na mtazamo
wa Kifasihi.