Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 72

Novela ya Gredi ya 7

Mshale
Matumaini

John Habwe
400
Mshale
wa
Matumaini
Novela ya Gredi ya 7
CCCSS Publishers
Limíted
Kimechapishwa nchini Kenya na:
Access Publishers Limited
Barabara ya Kangundo
Eneo la Kayole Junction, Jengo la Junction Plaza
s.L.P 7610 - 00200 Nairobi, Kenya
Simu: +254 701 836 846
Baruapepe: accesspublishers19@gmail.com

@Hakimiliki ni yaJohn Habwe, 2022

Haki zote zimehifadhiwa.


Ni hatia kutoa Chapa, kufasiri, kuiga au kunakili kwa njia
yoyote kitabu hiki au sehemu yoyote ya kitabu hiki bila
idhini ya Access Publishers Ltd.

Chapa ya kwanza 2022

ISBN 978-9914-729-93-1
Kimepigwa chapa na:
Printwell Industries
Ltd, Road A,
Industrial Area,
Nairobi, Kenya.
Yaliyomo
Sura ya Kwanza

Sura ya Pili

Sura ya Tatu 13
Sura ya Nne 18
Sura ya Tano 24
Sura ya Sita 30
Sura ya Saba 35
Sura ya Nane 42
Sura ya Tisa46

Sura ya Kumi 56
Faharasa 61
Sura ya Kwanza
Mnong'ono wa kwanza ulikuwa umechipuka kama miaka
mitano nyuma. Watu wengi hawakuwa na wasiwasi wala
kuchukua tahadhari yoyote. Hakuna mtu hata mmoja
aliyetulia na kuuwazia kwa taamuli. Walibaki
kuuchekelea bila kuchukua tahadhari yoyote au
kuonyana dhidi ya athari zake. Watu wengi walidhani
ilikuwa ni shughuli ya malofa na makundi ya watu
waliokosa kazi za kufanya; watu waliokuwa wakipoteza
muda barabarani. Watu waliopiga soga na kueneza
uvumi na habari za uongo katika vituo vya magari. Hata
mama yangu alipousikia mnong'ono huo, hakuutilia
maanani hata kidogo. Aliupuuza kama watu wengine
mtaani kwetu.
Mnong'ono ulizidi kuvuma lakini watu bado
hawakuuchukulia kwa makini. Ungewasikia
wakiambiana, "Aaah! Acha huo uzushi bwana. Tunajua
ni uongo mtupu. Hayo ni mambo yaliyopitwa na wakatf.
Mtu yeyote atakayeleta fujo hapa tutamripoti kwa polisi.
Polisi watamkamata na kumfungulia mashtaka.
Tutahakikisha amepewa kifungo kirefu gerezani."
Mnong'ono haukukoma mara moja. Ulikita mizizi na
kuendelea kusambaa mbali na karibu. Hata sisi watoto
tuliusikia njiani na mabarazani ukiongelewa na watu kila
tulipotoka michezoni na shuleni.
S
iku moja niliwasikiliza wazazi wangu wakiongelea
m
nongono huo. Mama yangu hakutaka nizungumze

1
kuhusu suala hilo Ia ukabila. Hakutaka nisikie habari
hizo. Wao pia walihofia habari hizo za kutisha. Aghalabu
walizungumzia şuala hilo usiku ama wakati ambao
sikuwa karibu nao. Sikupata kuwasikia wazazi wangu
hata siku moja wakiliongelea jambo hilo sebuleni kama
walivyofanya mazungumzo mengine. Hawakutaka mtu
yeyote hasa mimi, niwasikie wakiongelea şuala hilo nyeti.
Nilihisi walikuwa na uoga fulani. Sikujua kwa nini şuala
hili liliwatia wasiwasi mwingi, hasa mama yangu.
Mwanzoni nilidhani lilikuwa şuala la utani tu. Hatimaye,
nilifahamu kuwa şuala la tofauti za kikabila nchini
mwetu lilikuwa donda sugu katika jamii yetu.
Wazazi wangu walitoka katika makabila tofauti
yaliyokuwa na uhasama na chuki za kikabila. Baba yangu
alikuwa Mlanga naye mama yangu Mreba. Mimi nilikuwa
zao lililotokana na uhusiano wao. Sikujua kama nilifaa
kujiita Mlanga ama Mreba. Lakini kutokana na itikadi ya
jamii yetu kuamini kwamba mtu lazima achukue mbari
yake kuumeni, ilibidi nijitambulishe kama Mlanga.
iliniumiza sana siku hizo za mikasa. Sikutaka
kujinasibisha na ukoo wa wazazi wangu. Nilitaka
kujinasibisha na mbari nyingine tofauti na mbari za
wazazi wangu zilizochukiana. Sababu za chuki ya
makabila hayo mawili sikuwahi kuzibaini siku hizo.
ilinichukua miaka mingi baadaye ili kupata sababu za
mzozo huo.
Baba yangu alikuwa mwalimu katika shule ya msingi ya
Nakitare naye mama yangu alikuwa mfanyabiashara mkuu

2
wa kuuza nguo za mitumba katika şoko la Namuyange.
Tofauti za makabila ya wazazi wangu zilileta taharuki
fulani nyumbani kwetu, Mama yangu hakuamini katika
uvumi huo kamwe. Kila wakati mama alikuwa akimpinga
na kumwonya baba yangu dhidi ya uvumi huo.
"Sidhani kama habari hizi ni kweli," nilimsikia mama
akimweleza baba siku moja.
Mama yangu alikuwa miongoni mwa wanawake jasiri
niliowafahamu wakati huo nikiwa mdogo. Alikuwa
mkakamavu kuwashinda hata baadhi ya wanaume pale mtaani.
Alipozungumza, alikuwa na hakika na alichokisema kila
wakati. Nilimwona kuwa na busara nyingi. Alijiamini.
Wanawake wengine walimsikiliza na kumwamini. Hata
baadhi ya wanaume hali kadhalika. Baba alikuwa kinyume
chake. Kila mara mama hakukoma kumkosoa na kumwelekeza
baba kila ilipofaa.
Ilikuwa vigumu kuelewa tabia ya baba. Kuna wakati
angekuwa mpole na wakati mwingine akawa mkali
kupita kiasi. Nyumbani kwetu kulijulikana kama kwa
mama Zahara kutokana na kujulikana sana kwa mama
yangu na uhusiano mzuri aliokuwa nao na watu.
"Unajuaje kama habari hizi si kweli, kwani huoni jinsi
nyinyi Wareba mnavyotukandamiza kila mahali; si
uongozi, si biashara, hata kazi zote nzuri na zenye
mishahara mizuri mnazifanya nyinyi. Sisi mmetuachia
kazi zisizotamanika wala kutazamika. Lazima tuwe na
haki sawa. Nyinyi Wareba mnatuonea sana," baba
alimlalamikia mama siku moja.
3
Kutokana na uchache wa miaka yangu siku hizo,
sikung'amua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Hata
hivyo, licha ya utoto wangu, niling'amua kwamba baba
yangu alikuwa akijipendelea sana na alikuwa mwingi wa
ubinafsi; tabia ambayo mama yangu aliichukia na
kuipinga kwa jino na ukucha.
Mama hakupenda
kujibizana sana na
baba yangu hasa
katika masuala ya
ukabila. Siku hiyo
mama aliniangalia
nilipokuwa nimeketi.
Nilikuwa nikidurusu
somo la Kifaransa.
Nilijifanya kutosikia
jambo lolote
lililokuwa
likiongelewa. Mama alikuwa akinionya vikali dhidi
ya kusikiliza mazungumzo ya watu walionizidi umri.
Vilevile, hakupenda niingiwe na mbegu ya uasi
aliyokuwa akiihubiri baba yangu. Hata hivyo, siku
hiyo nilisikia maongezi yote kuhusu uhasama wa
kikabila baina ya wazazi wangu. Nisingeweza
kuyaziba masikio yangu.
kweli uyasemayo. Huo ni uzushi tu wa watu. Kila mtu
anafaa ajibidiishe katika maisha ndipo afike mahali pazuri

4
anapotamani badala ya kuliwekea Iawama kabila fulani.
Hii haitasaidia kitu,” mama alimweleza baba.
”Kwa hivyo unamaanisha kwamba Sisi Walanga ni wavivu,
sio?” Baba alidakia. Maneno ya mama yalikuwa
yamemtanza.
Nilivyomwona baba hakutaka ubishi sana na mama siku
hiyo wala sikuwahi kumsikia akimshinda mama katika
mjadala wowote. Siku hiyo baba yangu alitulia tuli kama
maji ya bwawani. Sikujua ni kipi alichokuwa akikiwazia
kwa kweli.
"Nadhani kuna ukweli fulani katika fununu hizi,” baba
alisema hatimaye. Alinyamaza kidogo kabla ya kusema
tena.
”Uvumi huu si wa bure, Iazima lisemwalo lipo na kama
halipo lipo njiani laja,” baba alisisitiza huku akiwa
amefadhaika.
"Alaa!” Mama alimaka. Alishtushwa kwa maneno ya
baba na ambayo yalimtoka kwa mazingatio.
"Ni kweli,” baba aliendelea kusisitiza.
”Unajuaje wewe mambo haya?” Mama alimdadisi baba
kwa ukakamavu.
”Habari hizi zipo kila mahali, hata katika vyombo vya
habari. Lazima nyinyi tuwaonyeshe kilichomtoa kanga
manyoya ya shingo mwaka huu. Hamwezi kutukandamiza
miaka nenda miaka rudi. Habari hizi zimesambaa kila

5
mahali. Lazima kutawaka moto. Lazima yatalimatia,”
baba alisisitiza bila wasiwasi wala kiwewe.
"Hizo ni porojo zenu za ulevini. Hao ni malofa wa
mitaani wasambazao porojo hizo. Kwa nini msambaze
habari ambazo zitaathiri kila mtu? Huu ni kama mtego wa
panya ushikao waliomo na wasiokuwemo,” mama
alieleza, kisha akaendelea kumpasha baba habari. ”Vita
vina hasara, eti! Tutahadhari kabla ya hatari jamani.”
"Ni porojo hizi? Sawa tusubiri tuone yatakayojiri," baba
alisema akiwa amekasirika sana.
"Kama si porojo ni nani aliye na u.shahidi wa kutosha
kuthibitisha hivyo? Ni bora mtu aendc mahakarnani
kutafuta haki badala ya kupigana Vita vis,ivyo na rnaana
wala msingi," mama alimwclcza baba.
Kwa namna fulani baba alionckana akiunga mkono
rnzozo uliovumishwa. Hii ilitokana na kuwa baba yangu
aliarmni kwamba kabila lake lilikandamizwa na kabila la
upande wa mama, dai ambalo mpaka sasa naona
halikuwa na ukweli wowote.
Mazungumzo ya mama na baba yalinitia wasiwasi
mwingl. Hakika sikupenda kuona watu wakipigana.
Nilikuwa nikichukia vita hata katika vipindi vya runinga.
Muda mwingi nilipotazama runinga, niliepuka kutazama
vipindi vilivyoonyesha Vita. Nilipenda kutazama
michezo ya kandanda au vipindi vya dini vilivyojenga
amani, upendo na uhusiano mwema.

6
Sura ya Pili
Mimi na wazazi wangu tulikuwa tukiishi Kisamalc. Hapo
ndipo palikuwa na mji wetu. Nilizaliwa hapo, nikakulia
hapo hadi kujiunga na shule ya msingi. Udogoni nilikuwa
nikitangamana na kila mtu bila kuwa na ubaguzi wa
kimbari wala kikabila. Wakati huo niliamini kwamba
binadamu wote tulikuwa sawa.
Muda ulisonga huku tukiendelea na shughuli zetu. Uvumi
wa vurugu ulitulia kwa muda na maisha yakarejelea hali
yake ya kawaida. Binafsi nilishukuru sana. Nilikuwa na
marafiki wengi Walanga na Wareba. Sikutaka kukosana
nao. Ningekosana nao, ningecheza mpira na nani? Shuleni
ningesoma vipi bila marafiki? Sikutaka mzozo baina yetu.
Nilishukuru kuona kuwa amani ilirejea na watu waliendelea
na shughuli zao za kawaida. Wakristo walienda makanisani
nao Waislamu wakaenda misikitini. Wanasiasa walifanya
siasa zao nao wakulima wakapanda mashambani mwao.
Mavuno yalinawiri na kuvunwa. Jua lilichomoza mashariki
na kutua magharibi. Kuku waliotaga mayai waliyaatamia
na kuangua. Wa kunadi sala katika misikiti walinadi.
Ndege wa mwituni waliimba. Upepo wa kusi ulivuma. Jua
liliwaka na mvua kunyesha. Watu walizaliwa na wengine
wakafa. Maji ya bahari yalijaa na kupwa. Siku zilisonga
kama kawaida.
Ghafla bin vuu, uvumi ulibisha hodi tena kwa kishindo.
Mara hii ulikuwa na kishindo kikuu. Kila mtu aliyeusikia
alifadhaika. Watu wengi walitapatapa kwa woga.

7
-Ala! Umerudi tena huu uvumi jamani,- baba alimweleza
mama jioni moja.
"Potelea mbali. Si kweli. Nikwambie mara ngapi ndipo
unisikie? Hizo ni kelele za chura zisizomzuia tembo
kunywa maji," mama alimwambia baba-
"Ninapendekeza mhamie Azania au Jamhuri ya
Demokrasia ya Tcreka kwa muda," baba alimshauri
mama yangu.
"Sioni haja ya kuwa na wastwasi namna hii. Habari hizi
zjtapjta kama nl;vyoptta av.-alt.- mama aliendelea kupinga
Ill.hauri wa baba.
Laiti angctambua marcm.i •.va maneno ya baba na
kuyatjli.l mambo nyongo kama yaljvyotokea. Labda
tutt*ciunua At.tnia au Jamhuri ya Demokrasia ya Terrk.i
kama al n»pendeket.i baba yangu tungekuwa salamx
Lakini mama yangu aiikuwa mshindani mno, Alikataa
katakat.' kusaku ushauri aliopewa.
llaikuchukua Siku nyingi. baba yangu aljtoweka
nyumbani tusiwahi tena maishani. Simutamba yake
ilikuwa haipaukani kila tulipompigia. Tulipowauliza
marafiki zake wa shuleni alikofunzia, hakuna aliyetupa
habari za kutusaidia kumpata. Hakuna aliyejua mahali
alipokuwa baba yangu. Licha ya mama yangu kumtafuta
kila mahali, hakumwona Tulipiga ripoti katika vituo vya
polisi kusaidia kumtafuta lakini juhudi zote zilikuwa
sawa na bure, Tulikata tarnaa kuendelea kumtafuta mtu
asiyepatikana. Hazikupita siku nyingi baada ya kupotea
kwa baba yangu kabja ya vita vikali vya kikabila kuzuka.
Watu walipigana damu *ikamwagika kama maji. Watu
wengi walikufa na
wengi waliobahatika kupona waliachwa na vilema vya
kudumu. Ni maelezo ya kuliza. Ninapoelezea kisa hiki
inanigharimu ujasiri mwingi, japo ninavumilia ili watu
wapate mwanga wa umuhimu wa amani na utangamano
baina ya jamii mbalimbali.
Mimi na mama yangu tuliponea kwa tundu Ia sindano.
Siku hiyo tulikuwa tumejifungia ndani ya nyumba yetu.
Hatukuwahi kutoka nje katu kwa kuwa nyumba yetu
ilikuwa ya kisasa. Mahitaji yote muhimu yalikuwemo;
maji safi ya kunywa, choo na vyakula ambavyo
vingetustahi kwa siku na majuma. Mama yangu baadaye
alionelea kuwa haikuwa suluhu kujifungia ndani kwani
ilionyeshwa katika runinga nyumba zilivyokuwa
zikiunguzwa. Nilistaajabu kuona katika runinga nyumba
ya akina Deno, rafiki yangu, ikiteketea kwa ndimi za
moto. Tuliomba Mungu atunusuru hadi siku ambayo
ingefuata.
Tuliamka alfajiri mbichi siku iliyofuata. Tulikuwa
tumekata shauri kutorokea mahali kokote ambako
tungepata usalama. Nilikuwa na wasiwasi mwingi siku
hiyo. Sikujua nichukue nini niache nini. Niliuangalia
mpira wangu, lakini ningeuchukua ningecheza katika
uwanja gani? Nilimwangalia mbwa wangu. Alikuwa
akiniangalia kwa huruma nyingi. Nilimwonea imani. Paka
wetu pia hakusazwa katika kadhia ile ya majonzi. Naye
alitaka auni kutoka kwetu lakini auni itoke wapi? Sikujua
nimchukue yupi nimwache yupi. Wote walinihitaji. Wote
walinitazama kwa macho ya huruma. Nilitaka kuwaeleza
tungewatoroka siku hiyo. Laiti wangejua jinsi gani vita
vilikuwa vimetuathiri, wangeshangaa. Nilitaka
kuwaambia wanyama hao lakini wasikie wapi maneno ya
wanadamu?
9
Njiwa wangu waliokuwa katika matundu yao walikuwa
wakitoa sauti zao tamu ambazo siku ile nilizitafsiri kama
sauti za dhiki. Nilitaka nipate angalau muda mfupi wa
kuwasikiliza ndege wangu wakiimba lakini sikuwa na
muda huo. Niliangalia friji yetu kubwa mle jikoni.
Ilikuwa imeshiba vyakula vya kila aina; nyama, samaki,
matunda tofautitofauti, maziwa, sharubati na vyakula
vingine vingi,
"Tsiiiii! Tsuuuu! Tsiitsiiii!" ilisikika ikitoa mngurumo
wake. Ilishiba vyakula nusura ivitapike na ambavyo
wakati ule tulikuwa tunaviacha. Hatukujali vingeliwa na
nani.
Macho yangu hatimaye yaliangukia kitabu cha John
Kimale chenye anwani, Mshale wa Matumaini.
Nilikuwa nimekipekuapekua kurasa chache juzi.
Niliamua kukichukua na kukiingiza ndani ya begi langu
la mgongoni. Kilibakia kuwa liwazo tosha katika
kipindi kile cha dhiki. Mara yangu ya kwanza kukisoma,
kilinivutia sana. Utangulizi wa kitabu hicho uliwavutia
sana wasomaji. Nina hakika kwamba kitabu hicho
kitabaki kuwa miongoni mwa vitabu bora zaidi•
nilivyowahi kuvisoma. Ninakumbuka kilianza hivi:
"Kila mwanadamu anao uwezo wa kufanikisha ndoto
zake ikiwa atajiamini katika chochote afanyacho.
Ufanisi wa mtu yeyote unatokana na mtu mwenyewe
wala si juhudi za watu wengine wanaomzunguka.
Mwanadamu yeyote ni shujaa kama atatambua uwezo
alionao na kuuwezesha...
Nilirudisha fikra zangu kwenye tabu iliyotukumba.
"Zingo! Zingo! Zingooo!" mara sauti ya mama ililipuka kama
fataki mara tatu mfululizo.
"Naam, mama," niliitika kwa mshtuko ulionipata saa ile.
"Toka mara moja," sauti ya mama ilipasua hewa kama radi
ya mvua ya kidindia. Ilikuwa yapata kitu saa kumi asubuhi.
Nilitoka
nyumbani
kama mwizi.
Sikuwa na
viatu
miguuni
kutokana na
taharuki.
Potelea
mbali!
Nilitoka navyo mikononi. Moyo ulinidunda dududu!
Tulishika njia kuelekea barabara kuu. Njiani tulipatana
na milolongo ya watu ambao walikuwa wakitoroka
kama sisi. Tulikuwa radhi kuitoroka nchi yetu, nchi
kipenzi chetu iliyokuwa na milima na mito ya kuvutia.
Macho yangu yaliangukia umati wa watu waliokuwa
wamebeba vitu migongoni na vichwani. Kuna
waliobeba masanduku. Kuna waliobeba magodoro.
Kuna waliobeba mablanketi. Kuna waliobeba mitungi
na karai za plastiki. Kuna waliobeba magunia. Almradi
kila mtu alibeba alichoweza kubeba. Nilitembea nyuma
ya mama. Nilijitahidi kuandamama naye

sako kwa bako. Sikutaka kumpoteza katika halaiki ya


watu asubuhi ile.
Wakimbizi tulikuwa wengi ajabu. Walikuwepo Wanaume.
Walikuwepo wanawake, Walikuwepo watoto waliobebwa
tnigongoni na tuatna ?.ao na wenginc waliobcbwa
mabcgani na baba zao. Pia, walikuwcpo wakongwe;
mashaibu na ajuza. Wapo walioshindwa kutcmbca lakini
wakajikaza il i kunusuru roho zao katika vita vilc vikali.
Rila mtu alishika roho yake nikononi. Rila mtu alitaka
kuiokoa. Sote tulikuwa tukielekea mpakani Gora. Sauti za
bunduki Zilisikika zikialika hapa na pale. Sauti hizo
pamoja na sauti za kite za wahasiriwa zilinitia wasiwasi
mwingi. Miili ya wafu ilikuwa imetapakaa hapa na pale
ungedhani walikuwa kuku waliojifia kwa ugonjwa hatari
wa kideri. Mingi ilikuwa imeanza kutoa harufu ya uozo.
Huo ulikuwa ukatili uliopita kiasi. Nilifikiria jinsi gani
binadamu tulivyokuwa tumeporomoka kiutu.
Safarini mvua ya manyunyumanyunyu ilikuwa ikinyesha.
Ilifanya miili yetu kuzizima kwa baridi kwa kuwa
hatungeweza kusubiri mvua ipuse ilhali hatari
ikitutumbulia macho. Barabara iliyojaa tope ilifanya
safari kuwa ngumu kupitiliza. Hata hivyo, licha ya dhiki
tulizopitia hatukuvunjika moyo wala kusimama.
Tulijikaza.

12
Sura ya Tatu
Gera ilikuwa umbali wa kilomita mia mbili kutoka eneo
tulilokuwa. Hatukujua kama tungcfika siku gani lakini
tulijikaza. Mara kwa mara tulisoma mabango
yaliyoonyesha umbali uliokuwa umebakia kufika mpakani
Gera.
Ilikuwa nadra kuona watu wakizungumza, Ni kana
kwamba kila mmoja alikuwa katika ulimwengu wake wa
mawazo. Kila mmoja alisema na Mola wake. Kila mmoja
wetu alikuwa na wasiwasi wa yanayoweza kutokea mbele
ya safari yetu. Nilikumbuka hadithi aliyotufundisha
mwalimu wetu wa somo Ia Dini. Alikuwa ametueleza jinsi
Waisraeli walivyofuatwa nyuma na jeshi Ia Misri ili
kuwaangamiza. Alitueleza kwamba kama si kwa msaada
wa Mungu kuwaokoa basi wangeangamizwa wote.
Nilipokumbuka kisa hicho, niliomba dua fupi ili Mungu
atunusuru kama alivyowanusuru Waisraeli. Sikutaka
tupatwe na janga Iolote.
"Mungu tukumbuke," hivyo ndivyo nilivyoomba sala yangu
fupi.

Kwa kuwa hayakuwa mazoea yangu kutembea kwa


miguu, safari ilinilemea kila wakati. Nilitaka kupumzika
lau kidogo lakini hatukuwa na muda wa kufanya hivyo.
Nilikuwa na uchovu mwingi mwilini, Mama yangu
alitanabahi nimebaki nyuma wakati mmoja, Nilimwona
akiniangalia huku na kule kwa wasiwasi mwingi.
Alininyooshea kidole cha shahada aliponiona hatimaye,
Macho yake yalinikemea. Nilichapua miguu na kukaza
mwendo. Nikamkaribia.
Manyunyu ya mvua yaliendelea kunyunyiza. Baridi ilikuwa
ya mzizimo. Ukungu nao uliwamba barabarani tulikopitia.
Ilikuwa vigumu kuona mtu aliyekuwa mbele yetu. Watoto
wachanga walilia kutokana na baridi na uchovu, Wazazi
nao hawakujali kitu, waliendelea kukaza mwendo.
Ilikuwa safari ndefu. Asubuhi jua lilichomoza tukiendelea
na safari kwenye msitu na nyika. Ilikuwa safari ya
wakimbizi wa kikabila. Tuliamua kupumzika mara chache
tulipochoka. Watu ambao walikuwa na vyakula walivitoa
mikobani na kula. Wale ambao hawakuwa navyo
walijikaza. Kila kitu kilikuwa kimeadimika. Si maji si
chakula. Hata hivyo, tulikuwa na matumaini ya kufika
Gera. Huko tuliamini tungepata auni. Mshale wa
matumaini ulikuwa umetufuma sote.
Giza lilianza kuingia. Wasiwasi ulijichora katika nyuso za
watu wengi. Kina mama na kina baba walionekana
kulemewa na mwendo. Mzee mmoja kwa jina Musambale
alipendekeza tutafute mahali salama ili tulale hadi asubuhi.
Hatukuwa na uhakika kama kulikuwa na usalama wa
kutosha wa sisi kufanya makao walau kwa siku moja.
Tulifika katika kijiji kimoja kilichokuwa mlimani.
"Tutawaambia sisi ni wakimbizi," Mzee Musambale
alitushauri.

15
Musambale alisema kana kwamba alikuwa na hakika na
aliyoyasema. Nilimpenda sana kwa ukakamavu wake.
Sote tuliomba Mungu tukitumai kuwa wangetuelewa.
Mara Musambale kama aliyesoma akili zetu akasema,
"Tutawarai hadi watuelewe. Hatuwezi kuendelea na
safari katika gin hili."
Sikujua kwa nini Muşambale hakuwa na wasiwasi kama
tuliokuwa nao wcngi wetu. Alionekana kuchukulia kila
jambo kijuujuu. Labda ilikuwa hulka yake pamoja na
busara aliyokuwa nayo.

Bikizee mmoja, Zulu, alikuwa na fimbo mkononi. Sura


yake ilikuwa imekunyaa kwa mikunjo. Miguuni hakuwa
na viatu kama mimi. Nyayo zake zilikuwa na mianya
ungedhani bonde la ufa. Alikuwa na kea za ajabu
miguuni na sugu nyingi mikononi mwake. Kila
nilipomtazama nilimhurumia sana bikizee huyo. Daima
alitumia fimbo yake ya mwanzi ili kuuhimili mwilj wake
uliolegezwa kwa uzee. Alikuwa amejifunga leso kuukuu
ambayo ilichakaa sana. Alionekana kuishi maisha ya
tabu. Sikuwa na uhakika kama angeweza kufika mpakani
Gera japo alikuwa na matumaini mengi ya kufika huko.

17
Kumbe maisha ndivyo yalivyo. Alijikaza. Alijihimu. Alijua
fika kuwa lisilo budi hutendwa. Bak bandika bak bandua,
tuliflka katika kijiji kilichokuwa karibu na mlima. Wakazi
wake walikuwa wafugaji wa mbuzi na kondoo. Vilevile,
walilima mawele, mtama, miwa na mahindi. Mashamba
yao yalikuwa yamestawi vizuri. Kijiji hicho kilikuwa
hakijaathirika kabisa na vurugu hiyo. Wakazi wake waliishi
kwa amani na utangamano. Mioyo yetu ilitulia kidogo.
Tulikuwa na matumaini makubwa ya kupata mahali salama
pa kupumzika. Kijiji hicho kiliitwa Mokowe.
Mzee Musambale aliulizia alikopatikana mzee wa mtaa.
Tulimpata.
"Sisi ni wakimbizi. Tumetoka Ktsamale," Mzee Musambale
alimweleza baada ya kumwamkua.
Alituelekeza hadi enco wanakosatdiwa wakimbizi.
Tuliomba kukaa na tukaruhusiwa usiku mmoja tu. Jamaa
hao walikuwa na ukarirnu wa kupigiwa mfano.
Tuliwashukuru kwa ukarimu wao.
Tulielekezwa katika mabanda mawili yaliyokuwa
katika sehemu ile. Tulipangwa katika makundi mawili,
wake kwa waume. Ilibidi kukarabati mahema mengine
ili yatusitiri sote tuliokuwepo. Wanawake walikaa
sehemu moja ya mahema na wanaume upande
mwingine.

18
Tulisongamana wakati wa kulala kwa kuwa sehemu
tuliyolala ilikuwa ndogo kwa sote kutoshea. Lakini nani
alijali msongamano?
Akili yangu ilinirudisha nyumbani. Niliona nyumba ya
mama ilivyofujwa, samani zote kuchukuliwa na Vitu
kuharibiwa. Niliona pia picha ya moto ukiuteketeza utajiri
uliokuwa nyumbani. Pia, niliona jinsi friji ilivyokuwa na
vitu lakini sikuwa na uwezo wa kuvifikia. Nisingeweza
kurudi. Nyumbani huko nilikuona kama msitu wa simba
usioishi swara. Nilipiga moyo konde.
Mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu ikiambatana na
upepo mkali wa kusi. Upepo ulipeperusha lile hema
tulimokuwa tumelala. Hata hivyo, lilikuwa hema kubwa
lenye mihimili imara ya vyuma. Halingeweza
kuangushwa kwa urahisi na upepo uliovuma kwa hasira
kubwa. Mioyo yetu ilijizika tena katika sala. Ungesikia
baadhi ya watu wakiomba kwa sauti za juu. Wengine
waliomba kwa sauti za chini. Kila mmoja aliamini
kwamba Mungu angemsaidia katika taharuki ile. Baada
ya saa moja, mvua ilipusa.
Tuliletewa maharagwe na mahindi tuchemshe kwa ajili
ya chakula cha jioni. Musambale aliwaagiza akina mama
Sita wapike chakula hicho. Tulikaa kusubiri chakula.
Nilipokuwa nikingojea chakula cha jioni nilihisi uchovu wa
ajabu. Sikuwahi kuchoka namna hiyo maishani mwangu.
Sikujua ningetembeaje kilomita nyingi zilizosalia hadi
kufika mpakani Gera.

19
"Kwa nini Musambale asiombe ruhusa ili tukae hapa hata
kwa wiki moja?" nilijiuliza.
"Labda hakuruhusiwa," sauti fulani ilinieleza.
Sura ya Nne
Niliwaza kuhusu safari iliyobakia. Miguu tayari ilikuwa
ikiniuma nyayoni na magotini. Pia nilihisi maumivu fulani
ya kifuani na nyongani. Sikutaka mama yangu ajue
nilikuwa na maumivu. Sikutaka kumwongezea mama
yangu adha zaidi. Alikuwa na matatizo ya kutosha.
Nilichukua kitabu changu cha Mshale wa Matumaini ili
kujiliwaza. Nilifungua ukurasa niliokuwa nimeachia awali
na kuendelea.
"Hakuna mwanadamu aliyeumbwa na akili isiyofikiria,
labda awe na hitilafu ya ubongo. Kama unaweza kuwaza
na kuamua basi unaweza kutumia akili yako kujiinua na
kujiendeleza. Mtu yeyote yule afanyaye mambo ya
kihayawani kama vile ukatili wa kumwaga damu,
unyang'anyi, uporaji na unyanyasaji wa wanyonge; mtu
huyo hana tofauti na hayawani kwani hatumii akili yake
vyema ili kuboresha maisha yake na ya watu
wanaomzunguka..."
Wakati nil ipokuwa nikisoma, wakimbizi wengi
walionekana wakiwa wamechoka tiki. Kuna wale
waliolala fofofo. Wengine wachache walizungumza kwa
sauti za chinichini lakini ungeweza kukadiria uchovu
waliokuwa nao. Maisha yalikuwa ya tabu. Lakini kila mtu
alin#ng'ana kuishi• Hapana aliyetamani kuachwa nyuma.

20
Chakula hatimaye kiliiva. Tulipakuliwa katika sahani za
plastiki zilizotoka katika ofisi ya chifu. Ilikuwa vigumu
kuonana vizuri kwa sababu ya mishumaa iliyotumika.
Nilikuwa nishazoea taa za umeme kwetu nyumbani. Siku
hiyo ilinibidi kutumia mwanga wa mshumaa. Ilikuwa
vigumu kwangu kuutumia.
Chakula kilikuwa kimepikwa vibayavibaya. Hakikuwa na
ladha yoyote ya chakula. Nilikula tu kwa kuwa lisilo budi
hutendwa. Niliungama kwamba siku zote mhitaji habagui.
Nililala usingizi wa pono usiku huo. Sikupinduka wala
kuamka kwenda haja usiku kucha. Ninadhani hali ile
ilitokana na uchovu mwingi niliokuwa nao usiku ule.
Niliota nikiwa katika Uwanja wa Ntaijuka nikiichezea
kandanda timu yangu ya Nomads. Timu ya Nomads
ilishindana na timu ya Ngorongoro mara kwa mara.
Ngorongoro ilikuwa timu ya kijijini lakini ilikuwa hodari
sana. Ilikuwa imeshinda timu nyingi mjini Madena.
Ilishinda timu ya Lulu, timu ya Zawadi na timu ya Ngazija.
Kwenye ndoto hiyo nilikuwa nikicheza nambari mbili.
Katika kipindi cha kwanza, nilifunga bao la penalti.
Nilitegemewa sana katika ulingo wa penalti. Kila mtu
aliniamini. Baada ya dakika kadhaa nilifunga bao la pili.
Tulicheza tukiwa na hakika ya ushindi.
Katika dakika kumi na tano za mwisho ndipo wachezaji
wa timu ya Ngorongoro walipotuzaba mabao matatu
mfululizo na kuibuka washindi. Kipindi kilipofika
mwisho, tulitaka refa atupe muda zaidi lakini alikataa
katakata. Hali ile iliibua fujo mle uwanjani. Wachezaji
21
wa upande wetu walianza kumshambulia refa kwa
ngumi na mateke. Timu pinzani ilipoona hivyo, iliamua
kumtetea refa na hivyo ikawa fujo moja kwa moja.
Wachezaji walikuwa wanapigana wenyewe kwa
wenyewe.
Mchezaji
mmoja
alikuwa
ameshika
gongo kubwa
na kuanza
kunishambulia.
Nilitoka shoti
na kutoroka
lakini
hakukoma,
akawa
ananifukuza himahima.
Nilimwomba anisamehe kwa kunyanyua mikono
yangu juu lakini hakunielewa. Aliponikaribia
alikuwa tayari kunipasua kichwa. Hapo nilipiga
ukemi mkubwa.
Ghafla niliamka! Dah! Nilishtuka nilipojiona katika
ulimwengu halisi badała ya ulimwengu wa kutisha wa
ndotoni. Wału waliokuwa karibu nami walisikia ukemi
nilioupiga ndotoni.
"Una shida gani?” waliniuliza.
22
"Ni ndoto tu,” niliwajibu.
Jasho lilikuwa likinitoka chepechepe mwilini. Wakati ule
kulikuwa kumepambazuka kabisa. Wakimbizi wengine
walikuwa wakijitayarisha ili kuendelea na safari. Maaskari
wa chifu walikuwa wakiamsha wału waliokuwa bado
wamelala. Hakukuwa na idhini ya kuendelea kukaa pale
kambini.
Nilijiunga na msafara wa wakimbizi wenzangu. Watu
walikuwa wameamka na nguvu mpya. Mwendo ulikuwa
wa kasi. Ungesikia miguu yao ilivyoumana na barabara
usingeamini. Binadamu ana uwezo mwingi ambao wakati
mwingi hautambui hadi apatikanapo na changamoto.
Nilishangaa kuona kuwa baadhi ya watu walitupa vitu vyao
walivyovibeba kwa tabu nyingi. Hasa mizigo ya nguo.
Mizigo hiyo iliongeza jitimai katika safari.
Katika safari ile nilikuwa nikiwazia sana nyumbani.
Nilimkumbuka rafiki yangu wa chanda na pete Deno.
Tulicheza naye kandanda siku nyingi. Uhasama baina ya
makabila yetu ulikuwa umejenga ukuta wa chuki. Deno
alikuwa Mreba kama mama yangu. Nilimwazia sana
rafiki yangu huyo. İle picha ya nyumba yao kuteketea
ilinijia tena akilini. ilinitia huzuni na kumwazia kama
naye aliteketea kwenye moto ule ama alijiopoa.
Nilimwombea apone ili tupate kuonana tena. Nilitamani
ilhasama wa makabila yetu uishe ili turudi katika hali ya
kawaida na amani idumu majumbani mwetu.

23
Zilibaki takriban kilomita arobaini kufika mpakani Gera.
Mzee Muşambale alichukua uongozi wa kundi letu la
watu wasiopungua ishirini. Makundi mengine
yaliongozwa na viongozi wengine. Mzee Muşambale
alituhimiza kila wakati tusikate tamaa wala kufa moyo.
Wengi wetu tuliokuwa tumechoka tulipata motisha
kutokana na himizo lake.
"Tuko karibu kufika, msichoke," Mzee Muşambale alihimiza.

"Subirini. Tumsubiri mwenzetu kwanza," Mzee


Muşambale alitwambia wakati mmoja.
Kuna bikizee aliyekuwa amelemewa na mwendo.
Alikuwa Bi, Zulu. Alilala pale chini. Alikuwa akipumua
kwa shida. Watu walimpepea ili apate kuzinduka lakini
wapi. Musambale alikimbia hapa na pale akiulizia yeyote
aliyebakisha maji ya akiba lakini hakuna aliyekuwa nayo.
Mto ulikuwa mbali nasi. Midomo yake ilianza kuumana,
halafu akatulia tuli, hafurukuti kama awali. Akajinyoosha
twaa kama sanamu ya kuchonga.
"Keshakufa jamani mwenzetu," Musambale alitamka kwa
huzuni.

Baadhi ya akina mama walianza kulia na kuomboleza


lakini hatukuwa na muda huo.
Mama yule alikuwa tayari ameshakufa na chendacho
mavani hakina marejeo.
Wanaume wachache waliuchukua mwili wake na kuuweka
vizuri kichakani. Mwili wake ulikuwa hauna thamani.
24
Mwili wake ulikuwa gimba. Dakika chache zilizopita mwili
wake ulikuwa na uhai. Aliuogesha ukapendeza. Aliutunza
na kuulinda. Alitoroka kifo nyumbani ili kuulinda uhai
wake lakini sasa mwone anatupwa kama mbwa, kama pande
la nyama lililooza. Labda mwili wake ungeliwa na mbwa au
fisi.
Thamani ya maisha niliiona duni sana siku ile. Nilitaka
kuwafuata wanaume waliompeleka kichakani lakini
mama yangu alininyoshea kidole na kunionya kupitia
macho yake makali. Nikajirudi na kupoa moto.
Rifo cha bibi yule kilinidunga mwiba mchungu kifuani.
Nilishangaa jinsi maisha yanavyoweza kuisha namna ile•
Maisha ya Bi. Zulu yalizimika ghafla kama taa ya kibatari
kwenye upepo mkali. Nilijawa na maswali mengi moyoni.
Maskini Bi. Zulu hakuzikwa kaburini. Nilishtuka sana kwa
kifo chake. Sikuwa nikimjua Bi. Zulu vizuri lakini
nilijipata nikilia nilipofikiria kuhusu kifo chake. Mkono wa
kifo kwa kweli hauna huruma. Nilijawa na maswali mengi
moyoni.
"Kwani binadamu si sawa?" nilijiuliza.
"Eeh binadamu si sawa," sauti iliniambia.
"Alaa!" Nilishangaa.
"Kwa nini?" Nilijiuliza tena.
"Hata misimu si sawa," ile sauti ilisema.
"Alaa!" Nilishangaa tena. Tuliendelea na safari, ya Bi. Zulu
tukayatupilia mbali.

25
Ilipotimu saa kumi jioni tulikuwa tumefika mpakani
Gera. Kulikuwepo na uwanja mkubwa tambarare.
Mahema ya wakimbizi yalikuwa mengi. Tulipofika eneo
hilo, tulikaribishwa na kila mmoja wetu akajiandikisha
katika orodha kwenye kitabu kikubwa cha wakimbizi.
Tulipomaliza usajili, tulikabidhiwa mahema yetu ili
kuweka makao yetu. Hatimaye, tulishukuru kufika
salama. Maisha ya ukimbizi yakaanza rasmi.

26
Sura ya Tano
Maisha ya Gera yalinitisha kwelikweli. Hayakufanana na
maisha ya nyumbani kwetu Kisamale. Baridi ya jioni
pekee ilikuwa dhiki tosha kwangu. Jua la mchana
lilikuwa na usumbufu usiosemeka. Mchana jua
lingetuchoma na kututoa jasho. Kambini, tulikuwa na
wasiwasi kwa kuhofia kuingiliwa na wezi au wabakaji.
Hali hiyo ilinikera kabisa. Hayo ndiyo yaliyokuwa
maisha yetu mapya ambayo ilitubidi tuyakubali. Kila
mtu alikuwa amelemewa na mzigo wa fikra. Watu
tuliowajua kuwa wacheshi walipoteza ucheshi wao. Kila
mara walivaa sura za huzuni. Walikuwa kama
waliorushwa kwenye moto wa jehanamu. Niliwahurumia
kuliko nilivyojihurumia. Mama alikuwa miongoni mwa
waathiriwa hao.
Kila siku alikuwa na msongo wa mawazo. Aliwaza
asubuhi. Aliwaza mchana. Aliwaza usiku. Hali hiyo
iliathiri sana hali yake kiafya. Ilifikia wakati rangi ya
ngozi yake ya maji ya kunde ilisawijika na kuwa na
mabakamabaka mwilini. Mwili wake wenye afya nzuri
ulidorora na kuwa duni. Alikonda kama Alitembea
kinyonge ungedhani alikuwa mgonjwa taabani. Mtu
asiyemjua angedhani labda alikuwa ajuza wa miaka tisini.
Binafsi nilipomtazama, nilishindwa kubaini hasa ni kitu
gani kilichokuwa kikimla mama yangu• Nilishuku hali
ngumu ya maisha ambayo hakuwa ameizoea ilimletea
msongo wa mawazo na kuifanya afya yake kudorora. Hayo

27
hayakuwa maisha ya mama yangu. Maisha ya raha
mustarehe aliyozoca kuishi yalimpasha simanzi kila
alipoyakumbuka.
Nywele zake za singa zilibadilika zikawa kama za paka.
Zilijilalia ovyo na kusokotana kwa kukosa matunzo, Nguo
zake zilikuwa mbili kama mboni za macho; chafuka
nikufue, chanika nikushone. Daima zilikuwa chafu.
Hangeweza kubadili kama alivyofanya awali. Nguo za
kubadili angezitoa wapi? Hakuwa mama yangu pekee
aliyepitia kipindi kile kigumu. Walikuwa watu wengi sana.
Mimi nilijisemea kimoyomoyo, 'Zingo, lazima uwe jasiri
ndiposa uishi vyema. Usiwe legelege.' Nilijikakamua. Muda
mwingi nilikuwa nikisoma riwaya yangu ya Mshale wa
Matumaini ili kujipa tumaini. Nilipenda usimulizi na vitushi
vyake vya kusisimua. Lugha yake pia ilikuwa sahili na
rahisi kueleweka. Nilimkumbuka mhusika mkuu
alivyokuwa akipitia changamoto nyingi za maisha ili
kutimiza ndoto zake za kuwa msanii hodari na wa
kutambulika. Mhusika huyo mwanzoni aliumbuliwa kwa
kudhaniwa kwamba hakuwa na kipaji chochote cha sanaa.
Watu wengi walimzomea na kudhihaki juhudi zake lakini
hakukata tamaa wala kufa moyo. Hatimaye, mhusika huyo
alifanikiwa na kuwa miongoni mwa wasanii maarufu
duniani. Wakati nilipochoka kusoma riwaya hiyo nilisoma
B
iblia. Niliyapenda mafunzo ya Yusufu, Danieli na Daudi
k
wenye Biblia. Yalinitia nguvu katika maisha yangu.
Mama aliamua kuniingiza shuleni pale kambini.
Nilijiunga na kidato cha kwanza, Shule hiyo iliitwa Gera
Secondaryfor Refugee Children.
Masomo yalikuwa na changamoto nyingi pale shuleni.
Wanafunzi wengi waliokuwa pale hawakupenda
masomo. Wengi walienda kwa kulazimishwa na
kushinikizwa tu. Wao walitaka kufanya mambo
waliyoyapenda.
Siku moja nilikutana na rafiki yangu Deno pale kambini.
Alikuwa ameketi peke yake. Aliponiona alinikimbilia.
"Zingo! Kumbe uko hapa?” aliniuliza.
î'Ndiyo,
niko hapa pamoja na mama yangu. Wazazi wako
wako wapi?” niljmuuliza.
Nilipomuuliza swali hilo, alianza kusinasina kwa kilio.
"Mbona unalia I)cno, kwani nimekukosea nini?”
nilimuuliza. Deno hakukoma kulia bali tnachozi yalikuwa
yakimtoka kapakapa machoni.
Tole, naomba unisamehe kama nimekukosea,” nilimsihi.
Deno alitoka mbio bila kunieleza chochote. Alikimbia na
kutorokea kwenye mahema mengine. Nilimwita lakini
hakuitika. Hakutaka kabisa kuongea na mimi siku hiyo.
Niliketi nikijiuliza ni kosa gani nililokuwa nimemfanyia.
Au ni kwa kuwa baba yake alikuwa Mreba na baba yangu
Mlanga? Sikupata jawabu.

29
Mama aliendelea kuugua. Kila wiki nilikuwa na jukumu
la kumpeleka katika zahanati moja hapo Gera. Wauguzi
walipompima waligundua kuwa alikuwa akiugua msongo
wa mawazo. Kichwa kilimuuma daima. Alilalamika kila
kukicha. Mwili wake ulikosa nguvu. Aidha, alipoteza
hamu ya chakula. Alishindwa kufanya kazi yoyote. Konde
aliyopewa kuilima ilimshinda kuifanyia kazi. Ilinibidi
kujisabilia kila nilipotoka shuleni ili kusaidia kazi zote
zilizomshinda.
Siku iliyofuata niliamua kumtafuta Deno pale kambini.
Nilibahatika kukutana naye karibu na hema moja.
Aliponiona alitaka kunikimbia.
"Deno tafadhali usinikimbie mimi rafiki yako,"
nilimwambia. Basi nilipomwambia hivyo alisimama.
"Mbona siku hizi unanikimbia? Kwani nilikukosea lini?"
nilimuuliza.
"Ukinitajia kuhusu wazazi wangu huwa unaniliza," Deno
aliniambia kwa upole.
"Pole jamani," nilimwambia.
"Nimeshapoa," alinijibu.
Siku hiyo tulizungumza mambo mengi kuhusu mkasa
uliotukumba kwetu Doneka na safari ngumu ya miguu
hadi kufika Gera katika Jamhuri ya Demokrasia ya
Tereka.
"Mbona baba yako aliamua kuiteketeza nyumba yetu?"
Deno aliniuliza siku moja. Swali hilo lilinifanya kuemewa
kidogo.
"Unasemaje?" nilimuuliza Deno kana kwamba sikuwa
nimesikia kauli yake.
"Babako aliteketeza nyumba yetu na kuwaunguza wazazi
wangu," Deno alitamka baina ya kwikwi za kilio.
"Hapana, huyo hakuwa babangu Deno. Babangu alipotea na
labda kujifia hata kabla ya vita kuanza," nilimweleza Deno.
"Nilimwona babako kwa macho yangu pamoja na genge
lake, Wameshika panga na bunduki wakiimwagia nyumba
yetu petroli. Babako aliwasha kiberiti na kuitia moto
nyumba yetu. Siku hiyo nilikuwa nimejificha nje.
Nilishuhudia kila kitu."
Deno hangeweza kujizuia kwa kilio. Aliamua kuingia
hemani kujifungia. Nilipoona hivyo, niliamua kurudi
kwenye hema letu huku nikiwa nimeemewa.
Nilikuwa na mawazo mengi siku hiyo. Sikuwa na hakika
kama Deno alimwona baba yangu au mtu mwingine
aliyemfananisha naye. Lakini Deno alimjua baba yangu
toka kitambo. Bila shaka lazima alikuwa yeye.
Jioni hiyo sikutaka kumweleza mama yangu kuhusu suala
hilo. Sikutaka kumwongezea jitimai zaidi kwa sababu ya
ugonjwa wake.

31
Kila siku
nilikuwa
nikimtafuta
Deno ili
turudishe urafiki
wetu uliokuwa
unaelekea
kutumbukia
nyongo. Kadri
siku zilivyozidi
kusonga ndivyo
ukaribu wetu ulivyoongezeka.
Siku moja niliamua kumkaribisha hemani mwetu.
"Huyu ni nani?" mama aliniuliza.
"Ni rafiki yangu," nilimjibu.
"Rafiki yako yupi?" mama alinidadisi.
"Rafiki yangu wa shuleni kule nyumbani," nilimweleza.
"Karibu, karibu sana," mama alimkaribisha.
Niliomba sana mama asimuulize kuhusu wazazi wake kwa
kuhofia kumliza tena Deno na kuleta habari za ukatili wa
baba yangu. Kwa bahati nzuri mama hakumuuliza chochotc
kuhusu habari hizo.

33
Sura ya Sita
Urafiki wangu na Deno ulizidi kuimarika kila uchao.
Nilimshauri siku moja ahamie kwenye hema letu badala
ya kuishi na watu asiowafahamu. Nilipomuuliza mama
yangu kuhusu suala hilo aliniunga mkono. Aliniambia
nimlete nyumbani, tukaishi sote.
Baada ya miezi kadhaa kupita, tulipewa vishamba vya
kujenga nyumba za kuishi kwa muda. Mimi na Deno
tulisaidia katika kujenga nyumba hiyo. Ilikuwa nyumba
ndogo iliyokandikwa kwa udongo na kuezekwa paa Ia
madebe. Sakafu ilikuwa ya mchanga. Muda ulizidi
kusonga lakini mama yangu hakupata afueni ya ugonjwa
wake. Ugonjwa ulizidi kumlemaza hadi kufikia hatua
ambapo shughuli ndogondogo za nyumbani zilimshinda.
Kazi zote za nyumbani ziliniangukia mimi na Deno.
Tulipika, tulifagia, tulifua nguo na kuosha vyombo.
Deno hakutaka kujiunga na shule yoyote hata baada ya
Mzee Musambale kumshauri. Mimi niliendelea kusoma
licha ya changamoto zilizokuwepo wakati ule. Siku
nyingi Deno alikuwa akimsaidia mama yangu
nilipokuwa shuleni. Mama alitokea kumpenda Deno
sana. Alimpenda kama mmoja wa watoto wake.
Jioni moja, Mzee Musambale alifika kwetu kibandani.
Mama alikuwa ameanza kuhisi nafuu kidogo. Angalau
siku hiyo alikuwa anaweza kutembea na kujifanyia kazi
ndogondog0•
"Karibu Mzee Musambale," mama alimkaribisha.

30
Musambale alionekana mnyonge kiasi. Sauti yake ilijaa
majonzi fulani.

"Ahsante Zahara," Mzee Musambale alijibu. "Habari za

"Kidogo nina nafuu. Angalau sasa naweza kuamka na


kula. Siyo kama awali nilipokuwa siwezi hata kuinuka
35
kitandani," mama alisema huku akijaribu kukaa vizuri
kitini.

"Umepata habari zozote kumhusu mumeo Kadurenge?"


Mzee Musambale alimuuliza mama.
"Hatuna habari hizo. Tujuze, kwani alionekana?" mama
alimuuliza.

"Mumeo amepatikana. Sasa yuko Doneka, ila chini ya


ulinzi. MUsambale alitueleza. "Kadurenge pamoja na
wengine
wamekamatwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa kwa kuhusika
katika ukatili na unyama. Anashukiwa kuhusika katika
mauaji ya halaiki ya watu."
Habari hizo zilinipa mshangao. Nilikumbuka maneno ya
Deno aliyonieleza awali. Kusikia vile, sikuwa na sababu
za kumtetea baba yangu tena. Nilimwazia. Mwalimu
mzima anawezaje kujihusisha katika kitendo cha kikatili
kama kile. Nilimtazama Deno. Alikuwa ameemewa
alipokuwa ameketi. Macho yetu yalipokutana niliangusha
uso wangu kwa haya. Niliamini kuwa baba alikuwa chui
aliyevaa ngozi ya kondoo.
"Ulizisikia wapi habari hizo," mama alimuuliza tena huku
akipumua kwa shida. Alikuwa akihema kwa nguvu.
"Habari hizo zi tele redioni," Mzee Musambale alijibu.
"Nimeona ni bora kuwataarifu."
Nilipomtazama mama yangu, machozi yalikuwa
yakimdondoka machoni. Alishindwa kuizuia simanzi
kutokana na habari hizo za kuudhi.
Mama alishusha pumzi kama mtu aliyekuwa akikata roho.
Nilishtuka.
Niliomba kimoyomoyo mama awe salama maana
nilimhitaji sana.
Mzee Musambale alituaga na kuondoka kuelekea
nyumbani kwake. Macho yangu yalijaa gharika ya
machozi. Sio machoti pekee yaliyonitoka siku hiyo. Hata
makamasi yalinidondoka usiku kucha kutokana na kulia.
Baba tuliyedhani amekufa kumbe alikuwa hai.
Kilichoniudhi zaidi ni kule kusadikisha maneno ya Deno
kwamba alimwona na bastola na upanga•

32
Je, ilikuwa kwamba baba yangu alihusika katika kifo cha
wazazi wa rafiki yangu Deno? Nilijiuliza lakini sikupata
jawabu.
Mama alikuwa ameketi kwenye kiti cha kukunja;
amepiga mbizi katika mawazo mengi. Sikujua aliwaza
nini kwa yakini. Alikuwa katika masikitiko makuu.
Alikuwa akilia kwa kite.
Jioni ile nilipomtazama Deno, naye hakuwa na furaha
hata kidogo. Alikuwa na mawazo mengi. Kwa kweli
habari alizozileta Mzce Musambale siku ile
ziliporomosha furaha yetu. Nakumbuka jioni hiyo

37
hatukupika chajio. Mama alikuwa amcrejclewa na
ugonłwa. Kila mtu alikuwa katika huzuni kuu.
Tangu mama alipopata habari mbaya kumhusu baba
yangu hakuwa salama tena. Mara kwa mara nilimsikia
akijisemesha mwenyewe.
"Ningalijua jamani!" Mama alisema huku akiguna.
Kadri siku zilivyosonga ndivyo afya yake ilivyozidi
kudhoofika hata zaidi. Aliendelea kukonda na kukondeana.
Tulipomrudisha hospitali, madaktari walitueleza kwamba
ugonjwa wa shinikizo la damu ulikuwa umemzidia
maradufu. Madaktari walijitahidi kurntibu na kumpa
matumaini lakini mama yangu hakupata afueni yoyote ya
ugonjwa wake. Kipindi hicho kilikuwa kigumu sana
kwangu. Maisha yalikosa ladha kwa kukosa kuwa na
kipenzi mama yangu. Siku nyingi nilimtembelea
hospitalini alikolazwa ili kumtakia shufaa. Hazikupita siku
nyingi, ugonjwa
ulimlemea akawa hawezi kupumua bila usaidizi wa mipira.
Jioni moja nilipomtembelea nikiwa na Deno, nilipata mshtuko
kupata habari za mauti yake. Nilihuzunika sana. Siku iliyofuata,
mama alisitiriwa katika mava ya umma katika mji wa Gera.
39
Sura ya Saba
Kifo cha mama kiliniumiza sana kwa sikil nyingi zilizofuata.
Nilikuwa kanıa mgomba wenye mkungu wa ndizi uliokosa
nguzo ya kuuhimili. Nilikesha siku nyingi nikimwaza mama
yangu. Pia, nilimwaza baba japo kidogo. Licha ya yeye kuwa
nduli, nilitamani japo siku moja nikutane naye ana kwa ana.
Damu ni nzito kuliko maji ati. Nililaani bahati yangu mbaya
duniani. Niliona kuwa kwa namna fulani maisha yalinionea.
Nilipoona vijana wenzangu pale Gera, nilitamani ningalikuwa
wao. Walikuwa wakicheza na kufurahia maisha. Nilitamani
maisha yao. Nilijiuliza kwa nini nilizaliwa nchini Doneka.
Mbona sikuzaliwa nchini Tereka, Gandua, Yenka au Azania
ambako amani ilikuwa imedumu? Kifo cha mama yangu
kiliniumiza sana. Sikuwa na matumaini yoyote ya maisha
bora. Hata hivyo, kitabu changu, Mshale wa Matumaini,
kilibaki kuwa liwazo kwangu. Nilikisoma kila wakati. Kuna
sehemu moja katika kitabu hicho iliyonigusa sana kipindi hiki.
Ilisema:
"Maisha siku zote yana pandashuka kama ilivyo dunia
yenyewe. Dunia ina milima na mabonde, huzuni na furaha,
vilio na vicheko, kusherehekea na kuomboleza; mambo
haya ni sehemu ya maisha ya kila mwanadamu. Hapana
mtu yeyote ambaye atawahi kuyaepuka. Yeyote awezaye
kuyaepuka si mwanadamu wa kawaida. ili kuielewa dunia
vilivyo, lazima upitie changamoto zote za maisha kama vile
kufiwa na uwapendao, kukataliwa na marafiki wa chanda
na pete unaowathamini, kukimbiwa na kudharauliwa;

40
hivyo ndivyo maisha yalivyo. Kubwa zaidi ni kujiclcwa na
kujithamini katika kila hali ikupatayo.”
Denondiyealiyekuwarafikiyangu wakaribuniliycmchukulia
kama ndugu yangu wa toka nitoke. Alinisaidia kwa siku
nyingi na kunipa moyo kwamba kila mtu alikuwa na uwezo
wa kuishi hata wazazi wasipokuwepo. Alinicleza kuwa pia
yeye alipitia hali zaidi ya yangu na hivyo nilipaswa kuvumilia
na kukubali kuwa maji yakimwagika hayazoleki. Siku
ningekataa kula kutokana na majonzi ya kufiwa na mama,
Deno angenihimiza hadi nikakubali kula.
”Kaka kula nawe upate nguvu. Kula usimwaibishe mama
yako,” Deno alinihimiza kila siku.
"Nitakula kaka,” ningemhakikishia Deno. Ningekula japo
kwa kujilazimisha.
Suala la shule lilianza kunitoka akilini polepole. Hapakuwa
na mtu yeyote wa kunihimiza. Sikuona haja ya kuendelea
na masomo baada ya majanga yote yaliyonisibu. Kama
ningeendelea na shule ni nani angeyashughulikia maslahi
yangu mengine? Baba hakuwepo. Mama hakuwepo.
Deno alipokutana na Mzee Musambale siku moja alimsimulia
hali yangu. Mzee Musambale alinijia nyumbani kwa kishindo.
Aliniletea chakula cha mgao kutoka kambini. "Unaendelea na
masomo?” Mzee Musambale aliniuliza.
"Nimeamua kuacha shule," nilimweleza kwa masikitiko
makuu.
"Kwa nini?” Mzee Musambale aliniuliza huku akinikazia
macho. Haikuwa kawaida yake kunikasirikia.

41
"Sina sababu maalumu mzec wangu. Pia, sidhani kama
nitaweza kujikidhia mahitaji yangu menginc bila kupewa
msaada,” nilimwelcza.
Mzee Muşambalc alinishauri sana jioni hiyo. Nilimsikiljza
alivyonieleza kwa upole huku nikimwitikia. Alinjshauri
kwamba nisifikirie kuhusu kususia shule. Aliniahidi
kunisaidia ili nisipate tabu niwapo shuleni au nyumbani.
Niliwazia ushauri wa Mzee Muşambale. Niliungama
kwamba jungu kuu halikosi ukoko. Niliridhi kufuata ushauri
wake. Siku iliyofuata nilirejea shuleni, Hapo shuleni
nilitokea kupenda kandanda sana. Walimu walinipenda na
kunitia moyo kila wakati. Ushauri wao ulinifanya kutia
juhudi masomoni mwangu.
Ninakumbuka idara zote za shule kwa jumla. Idara hizo
zilikuwa mfano mwema kwangu. Kwa msaada wao ningepata
ufadhili wa masomo yangu Uswizi. Mwanzoni, sikuamini
masikio yangu nilipoelezwa kuhusu mpango huo. Lakini
nilitiwa moyo kila siku kuwa mpango huo lazima ungenifaidi,
Nilikuwa na matumaini makubwa ya maisha mema ya
mbeleni.
Siku ya Jumapili tuliamua kumtembelea Mzee Muşambale
nyumbani kwake. Deno alipenda sana kumtembelea Mzee
Muşambale kila alipokuwa huru. Mzee Muşambale
alipenda kutuhadithia mambo ya kale na historia nzima ya
Doneka. Alitueleza jinsi alivyokuwa askarigongo wa
Mwingereza na mshahara wake ukiwa peni tatu na nguo za
mitumba kwa mwezi. Alipenda kutusimulia visa kuhusu
ukoloni na jinsi Wazungu walivyowanyanyasa na
kuwanyang'anya

42
Waafrika rasilitnali '/,ao enzi za ukoloni. Mzcc Musambale
alikuwa chetnchetni ya ushauri na hadithi za kupcvusha akili.
Siku hiyo tulilnpata Mzee Musambalc akiwa pckc yake
nyutnbani. Alikuwa kanisani jioni ilc. Alikuwa na furaha
sana.
"Habari za nyumbani?" alituuliza.
"Salama," tulimjibu.
"Mara hii mmepanda nini?" Mzee Musambale alituuliza.
"Tumepanda mboga na mahindi," nilimwambia.
"Na viazi," Deno aliongeza.
"Japo si vingi sana," nilidakia kusema huku nikichekacheka.
"Mbona hamjaniletea hata kidogo?" Mzee Musambale
alituuliza.
"Bado havijakomaa. Vikikomaa tutakuletea bila shaka." Deno
imweleza Mzee Musambale.
Mzee Musambale alichukua redio yake ili kusikiliza taarifa za
habari za saa kumi na mbili jioni. Alifungulia idhaa ya BBC
Swahili. Ilikuwa redio ndogo nyekundu yenye umbo la
mviringo. Ninakumbuka wakati tulipokuwa njiani tukielekea
Gera alikuwa na redio ile. Alitembea nayo mahali popote
alipoenda. Alipenda kusikiliza habari na muziki wa Kidoneka,
Redio ya BBC Swahili ilikuwa ikitangaza
habari za ulimwengu. Wakati alipofungua,
simulizi za Afrika zilitangazwa kwa
Kiswahili fasaha. Masimulizi
yalizungumzia kuhusu miji mikongwe

43
iliyokuwa na asili ya Lugha ya Kiswahili
kama vile Zanzibar, Pate na Mombasa.
Baada ya maelezo hayo, taarifa za habari zilifuata.
Zilizogonga vichwa vya habari zilikuwa ni taarifa kuhusu
kushikwa kwa magaidi sugu. Magaidi hao walihusika katika
maangamizi ya maelfu ya watu nchini Doneka. Habari zilidai
kuwa Umoja wa Mataifa uliingilia kati katika kuwanasa
wahusika wote wa kigaidi nchini humo. Wote waliopanga
uvamizi na uteketezaji wa makanisa na maboma ya watu
walishikwa. Hali hiyo iliwaacha wananchi wakiwa maskini
ombaomba na wengine wakiachwa na vilema vya kudumu.
Majina ya majambazi sugu yalitajwa. Jina la baba yangu
liliongoza katika orodha hiyo, Kadurenge Mlawatu. Dah!
Nilishangaa sana.
Pale nilipokaa nilizizima kwa wasiwasi na jekejeke. Hata
Deno alikosa maneno ya kusema, Alionekana kama
jisanamu lililoketishwa kitini. Mzee Musambale
aliniangalia
kwa hasira. Sikuwa na mahali pa kuuficha uso wangu. Baba
yangu alikuwa ameniumbua na kunivua nguo kadamnasi. Mzee
Musambale aliniangalia kwa muda. Ile tabasamu yake ya kila
siku ilifutika ghafla usoni pake. Nilihisi akinielekezea chuki
iliyomvaa usoni. Nadhani habari za baba zilimshtua zaidi siku
ile.
Nilitamani kutoroka niishi peke yangu lakini nilijirudi.
Nilitamani kuuvua uhusiano na baba yangu. Nilisikitika sana.
Nilijichukia. Hata nilitamani ningekuwa nimejifia kama
mama au Bi. Zulu. Maisha yalimaanisha fedheha. Nilijua

44
ingekuwa vigumu sana kwangu kutangamana na mtu yeyote.
Watu waliniona kama zimwi fulani kutokana na unyama
alioufanya baba yangu.
Mawazo yangu yalinirudisha Doneka. Niliangazia maisha
yetu ya nyuma tulipokuwa tukiishi kwa furaha. Tulitangamana
vizuri na majirani. Hata baba, licha ya unyamavu wake,
alipendwa na watu kutokana na cheo chake cha ualimu pale
Nakitare. Sikuelewa kwa nini alikubali kuwa mwanamgambo
na kuiletea familia yetu donda la lawama. Nilielewa kwa nini
baba alikuwa na hakika ya vita hivyo kutokea wakati mama
alipokuwa akimpinga.
Nilirejesha akili zangu kwa Mzee Musambale. Alikuwa
akitokwa na machozi saa ile. Sikuelewa kwa nini alikuwa
akilia. Nilihofu kuona mtu mzima akilia mbele yangu. Sasa
alithibitisha mambo yote aliyokuwa akidhani ni uvumi tu.
Nilitaka kutoka mara moja mahali pale lakini nilishindwa
ningewaaga vipi. Nilijisemea kimoyomoyo kwamba
nisingerudi tena kwa Mzee Musambale.
Nilitaka kujifungia peke yangu au nitorokcc mbali nisjwahi
kuonekana tena. Lakini sikuwa na mahali popote nilipopajua
wala ndugu niliyekuwa na uhakika wa kunisaidia, Niliarnua
kujiondokea.
"Nakwenda zangu," niliwaaga.
Sikujibiwa. Ububu ulitawala. Nilipoondoka, Deno alinifuata
nyuma. Aliona huzuni iliyoniandama wakati ule míthjli ya
mfiwa. Mawazo yalituzonga. Sikujua Deno naye alifikíria nini.
Sikutaka kumuuliza. Sikuwa na uwezo wa kumzuia

45
alivyofikiria. Deno hakuwa na ile furaha yake ya kawaida.
Alikuwa amezama katika mawazo.

46
Sura ya Nane
Siku zilizidi kusonga tukiwa tunaishi kwa msaada wa
chakula cha mgao kutoka kambini. Tuliishi kwa mchele na
maharagwe au pojo na ngano.
Nilipenda kufukuza mawazo yangu kwa kucheza kandanda.
Ningeenda uwanjani kucheza kandanda au kutazama
wenzangu wakicheza. Ingawa nilikuwa mchezaji mwenye
uzoefu tokea nilipokuwa Doneka, hawakutaka nijumuike nao
kuichezea timu yao. Baadhi waliniita muuaji pale uwanjani.
Nilishangaa kwa nini vijana wengine walikuwa wakinichukia
bila sababu. Hata Deno alipunguza uhusiano wake na mimi.
Nilichukia hali hiyo. Iliathiri masomo yangu kwa kiasi
kikubwa. Baadhi ya walimu walishangaa kusikia kwamba
nilikuwa mtoto wa jambazi sugu huko Doneka. Nilisikia
kauli kama 'mtoto wa nyoka ni nyoka.'
Maisha ya Gera yalinikera sana. Nilitamani kurudi kwetu
licha ya tabu zilizokuwepo. Nyumbani ni nyumbani
ingawa pangoni.
Niliomba Mungu azidi kuonyesha wengine, Mzee
Musambale akiwemo, tofauti kati yangu na Kadurenge,
baba yangu. Maswali mengi kumhusu yalizuka. Kwa nini
aliingia katika harakati kama hizo? Alikuwa amekosewa
na nani? Ni nani aliyemuudhi? Mbona hakulalamikia
vyombo vya usalama? Maswali haya na mengine yalinijia
akilini. Nilipigana nayo kuyaelewa, Nilitamani mama
yangu angekuwa hai ili anisaidie kuyajibu. Hata kana

47
asingenisaidia angekuwa rafiki yangu wa karibu lakini
hakuwepo sasa. Maisha yalisonga japo kwa dhil<i nyingi.
Siku ziliendelea kusonga. Niliona Gera pakicndclca kuwa
mahali pagumu kwangu kuishi. Silguwa na ndugu, jamaa
wala marafiki. Mzce Musambalc aliyekuwa rafil<i na
niliyemchukulia kama baba kwangu, sasa sikuwa na uhusiano
mwema naye. Nilimwomba Deno arudi shuleni lakini alikaidi
ushauri wangu. Alianza kuvuta gamu na kutumia dawa
zingine za kulevya. Nilimwona Deno nyumbani mara
mojamoja.
Nilipata liwazo kidogo nilipokuwa shuleni. Ilikuwa familia
kubwa na muhimu kwangu kwani ilinipenda na kunijali licha ya
hali yangu.
Halmashauri ya shule ilikuwa imetoa taarifa kwamba
kungekuwa na mradi wa kuwanufaisha vijana wote wakimbizi.
Mradi huo ulikuwa ni ufadhili wa kusomea Uswizi. Kila siku
nilikuwa nikiomba nafasi hiyo ije haraka kwani ingenitoa
katika lindi la dhiki iliyoniandama. Siku niliziona ndefu
kuliko kawaida. Sikuwa na marafiki wengi wa kucheza nao.
Nilishinda pweke. Nilihuzunika na hali hiyo ya huzuni na
majonzi. Ilinibidi muda mwingi nijisomee vitabu badala ya
kutangamana na wenzangu.
Mawazo ya kuacha shule yalikuwa yakinirudiarudia kila siku.
Lakini ningeacha shule ningeenda wapi? Sikutaka kuwa
kijana wa mtaani kama alivyochagua Deno. Nilijikanya
kufanya hivyo. Nilijikaza shuleni. Kila mara niliomba ushauri
kutoka kwa idara mbalimbali za shule. Niliziona idara hizo
kama zilizochukua nafasi ya wazazi Wangu, Pengo la wazazi
wangu lilizibika japo kidogo.

48
Ni wakati huu ambapo nilijifunza kuomba Mungu zaidi. Kila
Jumapili nilienda kanisani. Ingawa
baadhi ya macho ya waumini pale
kanisani yalinitazama kwa jicho la
kunichuja, sikujali. Ninakumbuka
siku moja nilipokaa kwenye ubao,
muumini mmoja alisimama.
Alinitazama kwa dharau kisha
akanipigia kidoko. Labda alijua
nilikuwa mtoto wa Kadurenge.
Kila Jumapili ningefika kanisani
kusali. Nilifanya toba yangu na ya baba yangu mzazi.
Ningesimama karibu na mchoro wa Yesu Kristo. Ningefanya
sala ndefu ya kuomba msamaha kwa ajili ya wazazi wangu.

Siku moja nilijikuta nikifunga safari ya kwenda Uswizi.


"Kweli kuinamako ndiko kuinukako," nilishtukia kutamka
maneno hayo nilipokuwa nikiketi kwenye ndege ya Umoja
wa Mataifa.
Nilipokuwa mle ndegeni, niliwaza kero nilizokuwa nimepitia
Doneka na Gera.
Jana nililala chini, juzi nikalala vichakani. Siku nyingine
nililala chini mkekani. Lakini siku hiyo nilikuwa ndani ya
nyuni wa bati aliyeelea angani. Mbawa zake zilitanuka kama
za njiwa na kupasua anga. Machozi yalinidondoka licha ya
kujikaza nisilie. Sijui ni vipi ningejizuia katika hali kama ile ya
mseto wa mawazo.

49
Ndege ilikuwa inavuka bahari ya Atlantiki. Ilikuwa inapambana
na mawingu angani. Abiria wengi walikuwa wamelala.
Nilijaribu kulala nisiweze. Sikujua dakika ya pili ingeleta hali
gani. Niliishi katika ulimwengu wa mabadiliko. Lolote
lingetokea. Niliomba mabadiliko yangu yawe mema. Nilimwaza
Deno. Kama Deno angependa elimu, leo tungekuwa tunavuka
naye bahari ya Atlantiki, Deno hakupenda masomo. Nami
sikumlaumu. Mazingira ya Gera hayangefanya mtu kupenda
elimu. Yalikuwa ya dhiki na mateso mengi. Vijana wengi
walitamauka kutokana na dhiki walizopitia.
Nilianza kuwazia ndoto ya Uswizi. Sikujua kungekuwaje huko
Uswizi. Nilisikia watu wengi wakisema kungekuwa kuzuri.
Kungekuwa na nafasi nyingi kwa wale watu wa kujituma.
Niliomba nifikapo Uswizi, watu wasianze kunihusisha tena na
Kadurenge. Ingawa nilikuwa na jina hilo kwenye kadi yangu ya
kitambulisho, sikutaka kulitumia jina hilo. Kama ningekuwa na
uwezo ningelifutilia mbali. Niliomba Mungu azidi kunifundisha
na kunielekeza jinsi ya kuchagua maisha mema ya kuishi.
Niliomba Mungu afanikishe mshale wangu wa matumaini.
Nilikurupuka kutoka katika usingizi. Loo! Kumbe ilikuwa ni
ndoto tu. Nilikereka sana moyoni lakini sikuwa na budi
kukubali ukweli huo. Nilipiga moyo konde na kuendelea na
maisha ya ukimbizi.
Sura ya Tisa
Maisha ya Gera yalizidi kuwa magumu kila siku. Nilijikaza
katika masomo yangu huku Musambale akinihimiza kila
wakati kutia bidii. Maisha ya upweke yaliendelea kunisonga
Pia. Ingawa tuliishi na Deno, urafiki wetu ulididimia kila siku.

50
Uliingia doa. Tulizungumza kwa nadra sana. Tuliishi katika
nyumba moja bila kupendana wala kuwa na ushirikiano
wowote. Tulikosa utangamano waliokuwa nao watu walioishi
katika nyumba moja. Ungedhani nyumba hiyo kulikaa fisi na
mbuzi. Aibu iliyoje!
Sikujua kwa nini kipindi hiki nilimkumbuka marehemu mama
yangu zaidi. Labda upweke niliokuwa nao ndio ulionifanya
nimkumbuke. Haikupita siku hata moja bila picha ya mama
kunijia katika kumbukumbu zangu. Nilitamani kumwona tena
na kumweleza hali ya mambo ilivyokuwa.
"Nimechoka na hii dunia. Nichukue nije huko uliko
nikapumzike na mimi Pia. Huwa ninasikia watu huja huko
kupumzika madhila ya dunia," mawazo yalinipitikia akilini
siku baada ya siku.
Licha ya matatizo mengi yaliyonizonga, bado niliona nilitaka
kuishi duniani japo kidogo. Shule iliniwia ngumu kila siku.
Wakati fulani nilijihisi kulia hasa nilipokumbuka ndoto
niliyoota majuzi yale. Nilitamani ingekuwa kweli lakini
sikuwa na uwezo wa kubadili ndoto kuwa kweli• Siku moja
Mzee Musambale alinipata nikiwa nimekaa peke
yangu na kujishika tama. Alinishauri, "Usikae peke yako hivyo."
"Sawa, ila nafurahi kuwa peke yangu kuliko kuwa na marafiki
wengi," nilimweleza.
"Hata kama utakaa peke yako jaribu usome ili ubongo wako
uwe angalau unashughulika na kitu fulani. Sitaki upatwe na
maradhi ya akili," alinieleza

51
Niliamua kutii ushauri wake. Niling'ang'ana shuleni kufa
kupona. Nikang'ang'ana nyumbani.
Kila siku tulisikia habari za athari za vita nchini Doneka. Kila
habari tuliyoisikia ilitutia kiwewe. Vita hivyo vilikuwa kama
moto uliozimwa ukakataa kuzimika. Tulisikia kuwa maelefu
ya watu waliokufa walisitiriwa katika makaburi ya halaiki na
wengine waliobahatika kama sisi walitoroka wakahamia
ughaibuni. Ajabu ni kuwa licha ya vita kuendelea Doneka,
niliendelea kushikwa na hamu ya kurudi nyumbani. Nilisadiki
waliosema nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni.
Siku moja Deno alifunganya virago vyake akaondoka
nyumbani. Alipokuwa akitoka sikumwambia kitu. Nilitaka
kusema kitu lakini kinywa changu kilikataa kufunguka.
Alikuwa amebadilika si haba. Alimiliki saa na simu za bei
ghali. Sikujua alizitoa wapi. Yeye, kama mimi tuliishi kwa
misaada ya wahisani.
Jioni moja nilipata habari za Mzee Musambale kuugua. Tangu
nitoke kwa Musambale siku niliyosikia habari mbaya
kumhusu baba yangu, niliogopa kurudi tena kwake.

52
Mara kwa nłaľ•a nilitaka kwcnda kumwomb;ĺ ľnqaľnaha
kwa niaba ya baba yangu. Lakinĺ nilihisi M7.í'í'
Mtłqarnbnlo angenikatalia. Alionekana kuwa na haqira
nyingi qiktí hiyo hasa baadaye aliposikia jinsi ml«' wake na
rnwanawľ' wa pekee walivyokufa katika tnapigano ya
í)onoka, Watu walisełna alikuwa kanŇa aliycshikwa na
wazimu, Aliongpa pcke yake alipotennbea barabarani. í lata
wakati alipokuwa na watu angeanza kulia watu wasijuc
alililia nini. Liwe liwalo. Niliamua kwenda kumwona.
Nilifika kwa Mzee Musambale saa tisa za mchana.
Alikuwa katika nyumba yake ndogo. Kwa kwcli Mzee
Musambale alikuwa akiugua. Nilikaa kwenye kigoda.
Mzee Musambale hali kadhalika. Macho yake yalikuwa
yamefumbwa kama mtu anayefanya sala. Usingejua sala
yake ilihusu nini. Labda ilihusu maradhi yake ya sasa.
Labda alitaka Mola ampe uponyaji. Labda ilihusu janga la
vita vya Doneka. Ni nani aliyejua? Mungu tu ndiye
aliyejua yaliyokuwa katika kina cha moyo wa kila mmoja
wetu. Nilimtazama Mzee Musambale hapo alipokuwa,
alikonda na kukondeana. Kando yake kulikuwa na
kikombe cha chai
alichotiliwa lakini
hakuwa
amekunywa chai
hiyo.
Mkononi alikuwa
amefungwa bendeji.
Chini ya bendeji hiyo kulikuwa kumechomekwa sindano
mbili za kuingizia dawa. Mara Mzee Musambale alifunua
macho yake. Alizungumza maneno yasiyoeleweka. Alisema
kama mtoto aliyekuwa anajifundisha kusema. Nilipokuwa
katika nyumba ya Mzee Musambale, akili yangu ilijaribu
kuitathmini hasara ya vita na maisha ya kukaa ughaibuni.
Niliamini vita vilikuwa na hasara kubwa. Vita vilionyesha
upande wa binadamu uliokuwa na uozo mkubwa. Kama si
vita, Mzee Musambale angekuwa kwake nyumbani. Nami
pia ningekuwa nyumbani nikiyaendesha maisha yangu.
Lakini vita vilitutosa katika mkondo wa maji machafu.
Humo mkondoni tulipigana ili kuishi, nayo maisha hayo
hayakuwa rahisi.
Baada ya kukaa kwa muda wa saa mbili kwa Mzee
Musambale, niliondoka. Muda huo niliokaa kwa Mzee
Musambale nilinyamaza tu, sikusema kitu. Hali ya Mzee
Musambale ilinitia wasiwasi sana. Moyo wangu ulijaa
huruma. Nilimwombea kimoyomoyo. Nilitumaini Mungu
anayejaalia waja wake angemjaalia na kumpa afya ya
haraka ili apambane na pandashuka za maisha akiwa
mzima wa afya.
Siku moja tuliamka kwa wasiwasi mkubwa. Kulikuwa na
uvumi kuwa mlima wa Gera ungelipuka tena baada ya
miaka kumi ya kulipuka hapo nyuma. Kama ungelipuka
ungerusha jivu la volkeno ambalo lingesababisha
madhara makubwa. Watu walikuwa na wasiwasi.
Nilianza kufananisha wasiwasi huo wa jivu la volkeno na
wasiwasi wa vita tulivyokuwa navyo nyumbani, Doneka.
54
Maisha yalikuwa na changamoto tele. Tulitakiwa kuwa na
moyo na bidii ili kufaulu kuyaishi. Sikutaka kulegea katika
safari yangu ya maisha. Licha ya changamoto nyingi,
niliamua kujikaza kwani baada ya dhiki ni faraja. Niliamua
kujikaza kila siku. Ninakumbuka siku za mwisho marna
alipokuwa anakaribia kufa. Alinishika mkono akanieleza,
"Wewe Zingo ni kijana wa kisasa. Ujikaze. Maisha si rahisi.
Hayaendi ila kwa nyenzo. Na nyenzo ni wewe na akili
zako."
Sikumjibu mama. Macho yake yaliyofifia kwa ugonjwa
yalinitazama kwa makini. Ni kana kwamba alitazama
ndani ya nafsi yangu. Siku hiyo nilikumbuka wosia huo.
Sikujua nikimbilie wapi. Ingawa shirika la wakimbizi
kutoka Canada Iilitaka kutuhamishia mahali salama,
nilihiari kubaki nyuma. Wenyeji walikataa kuhama na
kuacha nchi yao kama sisi tulivyohama kwetu. Baadaye,
tulisikia kuwa zilikuwa tetesi tu. Nilimshukuru Mola wangu
kwa neema hiyo.
Baada ya kupoa kwa hangaiko la mlima kulipuka,
niliyapiga darubini maisha yangu ya mbeleni. Nilishukuru
kwa misaada na vifaa vya masomo shuleni, mavazi na
usaidizi tuliopewa na mashirika ya kusaidia wakimbizi.
Sasa nilitazamia kuwa mwanasheria. Nilitaka kusomea
uanasheria ili niweze kurudi Doneka siku moja kutetea
haki za binadamu, hususan watoto wadogo. Azma hii

55
ilinikaa moyoni hata siku moja nikaona nimweleze Mzee
Musambale. Niliamua kumwendea.
"Shikamoo!" nilimwamkua.
"Marahaba, Zingo!" aliitika. "Habari za masomo?"
"Ninaendelea vizuri na masomo," nilimjibu.
"Ungependa kusomea nini pindi ukimaliza shule ya upill?
aliniuliza.
"Ningependa kuwa mwanasheria wa kutetea haki za
binadamu," nilimweleza Mzee Musambale.
"Sawa Zingo lakini lazima usome kwa bidii ndipo ufaulu
kufanya hivyo. Tunaendelea kukutafutia msaada katika
mataifa ya ughaibuni," Mzee Musambale alisema kwa
msisitizo fulani.
"Ninawashukuru kwa juhudi zenu. Mimi nitajitahidi,"
nilimhakikishia Mzee Musambale.
"Ahsante," alisema. Niliondoka.
Nilichuana na vitabu bila kuchoka. Kule kukataliwa
nilikokataliwa na vijana wenzangu kulinifanya kutia juhudi
zote katika vitabu. Nilivizamia kama mchwa katika ujenzi.
Kila nilikokwenda nilikuwa na kitabu mkononi. Kila
nukta niliyoipata niliitumia kupanua maarifa na elimu
yangu. Wale vijana walionibagua wakaanza kunisema,
"Anajifanya msomi sana. Tutaona atafika wapi. Ni
duduvule wa vitabu." Maneno yao yaliponifikia
yalinikera mwanzoni lakini baadaye yalinijengea

56
mwamba wa matumaini katika moyo wangu. Nilizidi
kutazama mbele na kuomba Mola anijaalie katika safari
yangu.
Maisha yote ya kuwa mkimbizi yalinipitikia katika
kumbukumbu. Kwa muda, nilimwaza Mzee Musambale.
Alikuwamtuhodari.Hatahivyo,uhodariwakeulinyonyolew
a na ugumu wa maisha. Nilikumbuka alivyotuongoza
kutoka
Doneka hadi Gera kwa ujasiri mwingi pamoja na hekima.
Alikuwa mshauri mkubwa lakini sasa aliupa ulimwengu
kisogo. Hakupata fursa ya kurudi nchini mwake kuijenga.
Chuki ya kikabila ilimtorosha kiguu na njia hadi ughaibuni
alikotumbukia katika shimo la mauti. Nilimwaza mama
yangu tena. Nilikumbuka alivyokuwa mwanamke wa vicheko
na furaha nyingi. Lakini alikwisha kuwa mavumbi. Kaburi
lake sasa lilizikwa watu wengine wengi. Alipotea kabisa
tusimwone tena. Machozi yalinidondoka.
Deno alikuwa ametoweka kabisa mfano wa wingu
wakati wa kiangazi. Hata nilipotaka kumtafuta ili tupate
kusuluhisha tofauti zetu sikumpata.
"Potelea mbali," nilisema.
Nilimwacha kuishi maisha yake alivyopenda na
alivyotaka. Kambi za wakimbizi zililalamikia unajisi,
wizi na uchawi. Kwa muda wizi huo uliendelea. Kila
mkimbizi alihisi magenge ya wenyeji ndiyo
yaliyoendesha uvamizi huo. Genge moja maarufu
lilikuwa linajulikana kama Moonlight lilihangaisha
57
wakimbizi usiku na mchana. Lilikuwa genge la vijana
arobaini. Ilikuwa vigumu kwa watawala kuwashika vijana
hao kwa sababu walibadilisha mbinu zao za kufanya
ujambazi. Serikali iliwasaka usiku na mchana. Mkono wa
serikali haukufa moyo, uliendelea kuwasaka. Serikali
iliendelea kuwasaka hadi iwatie majambazi hao nguvuni.
Watoto waliotumwa madukani walinyang'anywa pesa
Wengine walipigwa na wengine kunajisiwa. Ilifika
wakati mpaka ikawa muhali kutembea usiku, Vijana
wakaWa wanatembea katika vikundi vya watatuwatatu.
Mimi nikawa katika hali ya woga. Hata watu wengi
walipojaribU
kuwabaini majambazi hao, baadhi waliclekeza vidole upande
wangu.
"Si mimi," nilijitetea. Nilishikwa na wasiwasi mwingi kwa
kushukiwa huko. Kila jambo baya walikuwa wakinielekezea
kidole cha lawama. Nilimwomba Maulana aniepushe na
mioyo ya binadamu iliyojaa chuki. Kila jioni niliomba Mungu
anifunike dhidi ya mabaya.
Msako mkubwa ulifanywa. Ulikuwa kama neti kubwa
iliyotupwa baharini. Vijana mia moja walinaswa katika msako
huo. Kulikuwa na vijana wenyeji na wasio wenyeji. Wasio
wenyeji wakadai walilazimishwa kuingia katika kundi hilo la
Moonlight. Vijana wengi walionaswa miongoni mwa wezi hao
walikuwa wale waliokataa kusoma. Baadhi yao walijiunga na
shule na kisha baadaye wakatoroka. Wengine hawakujiunga na
shule kabisa. Baadhi yao walifanya biashara rejareja kama Vile
58
kuuza biskuti, peremende, matunda na soda. Deno alipatikana
katika kundi hilo. Watu wengi hawakuamini kuwa Deno,
alivyoonekana mtoto mzuri, angekuwa katika genge la
wavamizi. Lakini ndivyo maisha ya Gera yalivyokuwa,
yangekunoa ukapata makali. Ugumu wa maisha haya ulikuwa
mwalimu tosha.

Watu waliokuwa
wazuri
waligeuzwa na
kuwa wabaya.
Na wale
wabaya
walikuwa
wabaya zaidi.
Lile kundi
liliponaswa
ujambazi

59
ulipungua. Hata
nikashukuru
Deno alivyoondoka nyumbani. Wangedhani nilikuwa
ninashirikiana naye katika uhalifu ule. Deno akatoka
hatua ya kuwa mkimbizi na kuwa mfungwa. Katika
vijana mia moja walionaswa arobaini waliachiliwa huru.
Sitini nao walipelekwa korokoroni. Baada ya muda
wakafanyiwa kesi. Deno alikuwa miongoni mwa vijana
sitini waliojipata katika tope hilo la kufanyiwa kesi huko
Gera. Deno alifungwa miaka kumi. Alipotaka kurejeshwa
Doneka aliirai nchi ya Tereka isimpeleke Doneka ima fa
ima.
Moyo wangu ulimlilia Deno. Alikuwa kijana mzuri.
Mazingira yalimwathiri vibaya. Kwa kuwa alikuwa angali
mbichi, yalimkunja kwa wepesi. Sasa nilimkosa zaidi
kuliko mlivyomkosa zamani. Siku moja nikajieleza,
"Zingo, siku moja nenda ukamwone Deno gerezani."
"Aaa! Kwa nini tena?" nilijiuliza.
"Ni kaka yako yule," nilijieleza.
"Mimi ninaona yule ni mhalifu. Kumtembelea kunaweza
kukuchongea."
Nilikubali. Nikamwachilia Deno hapo kwa mara ya mwisho.
Licha ya kuushauri moyo wangu usimwaze nilijipata kila
siku nikimwaza. Nikawa ninasema, "Jamani! Deno alitoka
kikaangoni akatumbukia motoni." Kama tungeongea
60
ningemshauri kidogo. Hata hivyo, alikuwa ashabadilika
mwenendo. Macho yake, miguu yake na hulka yake nzima
ilibadilika. Hakuwa yule Deno niliyemjua. Ingawa
sikumshuku kwa kosa la ujambazi, niliona mabadiliko ndani
yake yaliyonishinda kufasiri kikamilifu.

61
Wareba, walikuja hata watu wa mataifa mengine waliomjua
Mzee Musambale.
Nilikaa mahali nikatulia tuli. Nisingesema lolote. Walisema
watu wakubwa.
Msemaji baada ya mwingine alisema masikio yakasikia.
Kila msemaji alitaka amani na mpango mzima wa
kurudisha wakimbizi nyumbani.
Mimi nilikuwa kijana mdogo. Nilitaka kuinua mkono
wangu niseme kitu ila nilipomkumbuka marehemu mama
yangu, niliuteremsha chini mara moja. Lau mama
angekuwepo angeniadhibu. Nilimwogopa mama hata katika
mauti. Wakati fulani nilihisi kama alikuwa akinitazama
kutoka juu nilikoamini alikuwa. Pia, nisingependa kuvunja
msingi alionijengea wa kuheshimu watu wazima.
Nilinyamaza kimya. Lakini bila kuamini, nilisimama japo
nilikuwa na woga mwingi.
"Ninataka niseme kitu," nilisema. "Mimi nilikuwa mtoto.
Sikujua asili ya vita vya Doneka. Niliona watu wakipigana
tu. Tulitoroka nyumbani. Nilifuata makundi ya watu
nikafika hapa Gera. Ningeomba nyinyi watu wazima
mnapogombana na hata kupigana msitujumuishe sisi watoto
tusiojua mnagombania nini. Sasa hivi sisi tunahangaika.
Hatuwezi kusoma vizuri. Vita vinaathiri watu wazima lakini
vinaharibu kabisa msingi wa vijana wadogo. Hapa nilipo
sijui nilimkosea nani, Mlanga au Mreba. Mpaka leo sina nia
ya kutomheshimu yeyote kwa ajili ya kabila lake. Sisi
watoto tungependa kurudi Doneka. Ninawatamani sana
marafiki zangu. Ahsanteni kwa kunisikiliza. Mungu
awabariki."

58
Nilirudi kukaa huku nimeinamisha kichwa. Ulimi ulikuwa
umesema mambo yaliyonikaa moyoni.

Mzee Musambale alipoteremshwa kaburini nilikumbuka


hekima yake nikasikitika. Nikakumbuka tena ile siku
tuliyomzika mama. Siku hiyo Mzee Musambale alikuwepo
akiililia roho ya mama. Sasa nasi tulikuwa tunaililia roho
yake. Ni kama baina ya maisha na mauti kulikuwa na pazia
Zito jeusi. Usingeuona upande ule mwingine katu.
Baada ya kifo cha Mzee Musambale, niliishi kwa hofu nyingi.
Haikuwa rahisi kujua ni nani angefuata katika safari ya
kuondoka duniani na kutokomea ahera. Licha ya ufanisi
wangu katika mitihani, sikuwa na raha hata kidogo.
Siku moja nililetewa fomu za kujaza. Nafasi yangu ya
kusomea nchini Uswizi ilikuwa imewadia. Nilijaza fomu za
kwenda kusomea ughaibuni. Nilisubiri. Nilipangiwa kusafiri
baada ya miezi Sita. Hatimaye, siku iliwadia. Nilikumbuka
ndoto yangu ya kusomea ughaibuni. Kumbe hiyo ndoto
ingetokea kweli. Niliwaaga marafiki kwa machozi,
nikaondoka kuelekea Uswizi nilikopania kuendeleza maisha
yangu. Maisha yangu yaliyokuwa yamekatika virakaviraka.
Nilikuwa ninajitahidi kuyaunga upya ili yaweze kukamilika.
Ili kufaulu katika azma hiyo nilihitaji nguvu isiyotetereka na
baraka za Maulana. Sasa niliomba Mungu anijalie katika
hatua hii niliyofika. Nilijua sikuwa bora lakini Mungu
alinionea huruma nami kama mtoto abebwaye mgongoni
nikajikaza. Siku zilisonga. Siku zikawa Wiki, wiki
zikabadilika na kuwa miezi. Azma yangu

59
kubwa ilikuwa kufaulu ili nirudi nchini kwetu Doneka
kutetea haki za wanyonge, hususan watoto.
Nikiwa
kwenye ndege,
sikuwa
nimeacha
nyutna kitabu
changu cha
Mshale wa
Matumaini;
kitabu
ambacho
kilikuwa kama
injini
iliyoendesha
maisha yangu.
Wakati ule nilikuwa katika kumaliza kurasa zake za
mwishomwisho. Nilikitoa wakati ule na kuamua
kukisoma hadi ukurasa wa mwisho. Kifungu chake cha
mwisho kilivuta utulivu wangu nikaamua kukisoma kama
mara tatu hivi. Kilieleza, "Chochote kisichowezekana basi
hakijaamuliwa. Pindi jambo likiisha kuamuliwa basi
jambo hilo linawezekana. Pindi tunapoogopa kufanya
uamuzi katika maisha yetu tujue kwamba kuanguka kwetu
huanzia hapo. Kuamua hutaka juhudi na siku zote kila
juhudi hulipa,"
Fallarasa
dhiki -- usumbuftl.
duduvulc nultldu arnbayc aghalabu hutoboa
Initi na kukaa ndani.
hakijaathirika hakijapata madhara.
hangaiko Wasiwasi.
ikasawijika ikabadilika na kuwa mbaya.
jagina shujaa.
jitimai - huzuni nyingi.
kadamnasi — mbele ya watu; hadharani.
kea — mpasuko kwenye nyayo
unaoacha nafasi kubwakubwa.
kidedea - mbele; ongoza.
kudorora — kuwa mbaya.
kuemewa - kushindwa; kulemewa.
kujinasibisha kujihusisha na watu wengine
kindugu.
kujisabilia — kujitolea.
kupoa moto — kutulia.
kupwa - kupungua kwa maji baharini.
kutumbukia nyongo- kuharibika kabisa.
madhila - tabu.
mnong'ono — mazungumzo ya sauti ya chini
yenye habari za siri ambazo watu
hawazisemi waziwazi.
mvua ya kidindia mvua nyingi sana.
61
hali ya kutoelewana; ugomvi
mkubwa.
uraha na starehe nyingi.
kukaribiana sana; bega kwa
ega.
linilazimu; sikuwa na hiari.
uwezo wa mtu wa kufikiria
kuhusu jambo fulani.
ulikosa matumaini.
benchi ya kukalia.
hali ya mtu kujifikiria yeye tu bila
kujali maslahi ya watu wengine.
ulisambaa; ulienea.
aliyonipata.
amenawiri.
62

You might also like