Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 10

MWOLHOBERYA BOAZ

Swali: Uchanganuzi makosa na uchanganuzi utendaji katika


ujifunzaji wa lugha ya pili.

Dhana ya uchanganuzi inahusu mchakato wa kuangalia, kuvunja, na


kuelewa vipengele tofauti vya kitu au suala ili kupata ufahamu wa kina
na maelezo juu yake. Uchanganuzi unaweza kufanywa katika muktadha
mbalimbali, iwe ni katika uchambuzi wa data, uchambuzi wa maandishi,
uchambuzi wa sera, au uchambuzi wa masuala ya kijamii.

Dhana ya Makosa

Corder (1967) anadai kuwa kama ilivyo katika ujifunzaji wa aina yoyote
ile, watu wanapojifunza lugha ya pili hufanya makosa.

Kamusi la Kiswahili Fasaha (2010) inaeleza makosa kama, jambo


lisilokubalika kisheria na taratibu ya mila na desturi za jamii fulani.
Kutokana na maelezo haya tunapata kuwa makosa yatasemekana
kutokea iwapo kuna kutozingatia sheria zilizowekwa. Aidha kwa kuwa
utafiti huu unahusu ujifunzaji wa lugha, ni muhimu kufafanua dhana ya
makosa kwa muktadha wa ujifunzaji wa lugha. Dhana hii imefafanuliwa
na wanaisimu mbalimbali hasa katika uwanja wa ujifunzaji wa lugha ya
pili.
Dulay (1982) anaeleza makosa kama miundo ya lugha ya kimaandishi
au maongezi ambayo inakiuka kanuni za lugha lengwa. Tukizingatia
maelezo yao ni kwamba makosa yatasemekana kuwepo iwapo lugha ya
mwanafunzi itakuwa tofauti na miundo sahihi ya lugha anayojifunza.
Yeye Norrish (1987) anasema kwamba makosa ni ukiukaji wa kanuni
ambao hutokea wakati mwanafunzi hajajifunza. Hii ina maana kuwa
makosa yatatokea iwapo kanuni za lugha lengwa hazijazingatiwa.

Naye Richards na Schmidt (2002:184) wanaeleza makosa kama


matumizi ya lugha ambayo mzawa wa lugha itaitaja kutokuwa sahihi.
Kutokana na maelezo yao ni mzawa wa lugha ya Kiswahili au mtu
mwenye umilisi sawa na mzawa wa lugha lengwa anayeweza kutambua
makosa. Aidha mwanaisinu Corder (1967) katika kueleza dhana ya
makosa katika ujifunzaji wa lugha ya pili alizua dhana mbili ambazo
anazirejelea kwa lugha ya Kiingereza kama errorsandmistakes. Katika
utafiti huu dhana hizi zimetafsiriwa kama makosa na kuteleza mtawalia.
Aidha wanaisimu mbalimbali wamezitofautisha dhana hizi mbili kwa
muktadha wa ujifunzaji wa lugha.

Makosa kwa mujibu wa Corder (1967), (Miller, 1966), (Richards,


1974:24) na Ellis (1994) makosa hutokana na umilisi alionao
mwanafunzi na huwa na ruwaza fulani.

Umilisi kulingana na Holt (1975) ni ujuzi alionao mzawa wa lugha


kuhusu lugha yake ujuzi ambao humwezesha kuzalisha sentensi nyingi
zisizo kikomo za lugha yake. Aidha mzawa wa lugha huwa na ujuzi huu
bila kufahamu kuwa anao. Hii ina maana kuwa mwanafunzi hufanya
makosa kwa sababu bado hajapata ujuzi kamili wa lugha anayojifunza
yaani lugha lengwa. Kulingana na Holt makosa hudhihirisha kiasi cha
lugha alichojifunza mwanafunzi katika lugha ya pili. Aidha anaeleza
kwamba kwa kuwa makosa hutokana na umilisi basi mwanafunzi
hatambui anapofanya makosa haya na binafsi hawezi kuyarekebisha.
Corder ambaye (keshatajwa) anabaini kuwa makosa hujitokeza kwa
wingi na si rahisi mwanafunzi kuyatambua.

Aidha Selinker na Gass (2008) wanaeleza kuwa makosa yanaweza


kutambuliwa tu na mwalimu au mtafiti na wala sio mwanafunzi
mwenyewe. Hii ni kwa sababu mwanafunzi hajazielewa kanuni za lugha
lengwa. Corder (1993) anasisitiza kuwa makosa ni muhimu wakati wa
ujifunzaji wa lugha kwa kuwa:

i) Ni ishara ya mikakati anayotumia mwanafunzi katika kujifunza


lugha japokuwa mikakati hiyo si sahihi
ii) ii) Humjulisha mwalimu kiasi cha lugha ambacho amejifunza
mwanafunzi na ni kipi ambacho anahitaji kufunzwa.
iii) iii) Ni muhimu kwa mwanafunzi anayejifunza lugha ya pili kwa
kuwa huenda ikawa njia mojawapo au kifaa anachotumia
kujifunzia lugha.
Kwa ujumla, makosa ni vitendo vinavyokiuka sheria, kanuni, maadili au
taratibu zilizowekwa katika jamii au taasisi fulani. Matokeo ya makosa
yanaweza kuwa adhabu, kurekebishwa kijamii, kutoa fidia, au hatua
nyingine za kisheria au kimaadili zilizoanzishwa kwa lengo la kurejesha
utaratibu na kudumisha usalama na haki katika jamii.

Mtazamo wa Uchanganuzi makosa uliasisiwa na Corder na wenzake


miaka ya 1960. Mtazamo huu uliibuka kukidhi upungufu wa
uchanganuzi linganuzi uliotumiwa na wanaisimu kutofautisha lugha ya
kwanza na ya pili ya mwanafunzi ili kukisia makosa.

Uchanganuzi makosa ni mbinu itumiwayo kuthibitisha makosa


yanayopatikana katika lugha ya mwanafunzi. Walimu wa lugha
wanaowasikiliza wanafunzi wao wakizungumza hutambua makosa.
Ukweli ni kuwa kila mtu hufanya makosa anapoongea hata walimu na
wazawa wa lugha hufanya makosa. Wazawa wa lugha hawafuati kanuni
za sarufi zilizoandikwa vitabuni.

Uchanganuzi makosa, huchunguza aina ya makosa na visababishi vya


makosa hayo. Kulingana na mwanaisimu Corder, mtafiti hufuata hatua
zifuatazo katika uchanganuzi makosa:

Kukusanya sampuli ya kazi ya wanaojifunza lugha. Hapa inamhitaji


mwalimu kukusanya kazi za wanafunzi mbalimbali wanaojifunza lugha
ili aweze kuchunguza ikiwa kuna makosa yoyote. Akiwa anakusanya
sampuli za wanaojifunza lugha, ni lazima asiegemee upande mmoja
kama wa wanafunzi wasiofanya vizuri darasani, lazima ahusishe kila
aina ya mwanafunzi yaani wale weruvu na wale wasiowerevu sana.

Hatua inayofuata baada ya kukusanya sampuli ni kutambua makosa.


Hapa, mwalimu ataanza kusoma kazi za wajifunzaji lugha ili atambue
makosa yaliyoandikwa na wanafunzi. Anaweza kulipiga msitari kosa
ambalo ametambua ili asisahau au kuacha mokosa mengine wakati wa
kumwelekeza mwanafunzi.

Baadaye, mwalimu atachambua na kurekodi makosa. Makosa


yanawekwa katika makundi na kuelezwa kisarufi. Hivyo makosa
yenyewe ndiyo hutumiwa katika kuainisha kategoria za kisarufi.

Baada ya kueleza kosa baada ya linguine, hatua inayofuata ni kufafanua


chanzo cha makosa haya. Kwa hivyo, atafanya uchambuzi wa kila kosa
kwa kina na kugundua sababu zake hivyo, mchunguzaji makosa ataeleza
chanzo cha makosa hayo. Kwa mfano mwanafunzi akiandika setensi
kama nilikura chakula kitamu jana, mwalimu ataelewa kwamba chanzo
cha kosa hili ni athari ya lugha mama. Kwa hivyo, chanzo cha makosa
hayo kinaweza kuwa ni utamaduni mwanafunzi anakotoka, athari ya
lugha mama na kadhalika.

Hatua ya mwisho ni kutathmini/ kuyasahihisha makosa haya ili kujua


jinsi ya kukabiliana nayo. Tunapowasikiza wanafunzi wakizungumza
tunafahamu makosa wayafanyayo. Kwa sababu hii ni vyema kujiuliza
kile mzungumzaji alikusudia kukisema na angekisema vipi.

Kusahihisha makosa haya sio jambo rahisi kwa sababu kuna zaidi ya
njia moja ya kufanya hivyo.

Kusahihisha makosa kunategemea kile msikilizaji anafikiri


mzungumzaji alikusudia kukisema na kosa lenyewe. Ni vyema kufikiri
namna nyingi tofauti za kusahihisha makosa. Kwa sababu huna uhakika
wa kilichokusudiwa, mwache mwanafunzi akusaidie kuamua sahihisho
sahihi.

Kufafanua makosa haya, na kutaka kujua kisababishi. Makosa yanaweza


kutokana na kuhamisha kanuni au ruwaza za lugha ya kwanza. Makosa
mengine yanaweza kusababishwa na jinsi mwalimu au vitabu vya kaida
vinavyoeleza kanuni fulani. Au inaweza kuwa mikakati ya mawasiliano
anayotumia mwanafunzi hata kama anajua kanuni anazotumia sio sahihi.

Uchanganuzi wa makosa unahusika na mchakato wa kurekebisha na


kuboresha shughuli na michakato kwa kujifunza kutokana na makosa
yaliyofanyika. Kwa hivyo ili mwalimu kumkosoa mwanafunzi wake, ni
vyema mwalimu aanze kutambua makosa yanayopatikana katika kazi ya
mwanafunzi na baadaye aweze kumkosoa.

Uchanganuzi Utendaji
Utendaji ni jinsi ambavyo mtu au kitu kinavyotekeleza, kufanya, au
kufanikisha kazi fulani. Inahusiana na ufanisi na uwezo wa kutekeleza
majukumu au malengo kwa njia iliyoridhisha.

Uchanganuzi wa utendaji ni mchakato wa kuchunguza na kuelewa jinsi


shughuli au mfumo unavyofanya kazi ili kubaini mafanikio
yaliyopatikana au mapungufu yanayohitaji kuboreshwa. Lengo la
uchanganuzi wa utendaji ni kuchambua na kuelewa jinsi shughuli
zinavyotekelezwa na kutathmini ikiwa zinafikia malengo na viwango
vilivyowekwa.

Uchanganuzi wa utendaji ni mchakato wa kuchunguza na kuelewa jinsi


shughuli, michakato au mfumo fulani unavyofanya kazi na kufikia
malengo yaliyowekwa. Malengo hayo ni Pamoja na kiwango cha sarufi.
Kiwango cha sarufi ni lengo muhimu la utendaji katika ujifunzaji wa
lugha ya pili. Sarufi inahusika na muundo na sheria za lugha ikiwa ni
pamoja na matumizi sahihi ya maneno, sentensi, viambishi na kanuni za
tafsiri.

Lengo linguine la uchanganuzi utendaji ni muundo. Lengo hili ni


muhimu katika ujifunzaji wa lugha ya pili. Linahusisha kujifunza na
kuelewa muumdo na miundo ya lugha kama vile kanuni za tafsiri,
muundo wa sentensi, matumizi ya viambishi na mifumo ya sarufi.
Kwa hivyo, ni lazima kuwepo uchanganuzi wa utendaji ili kutoa
ufahamu na taarifa muhimu kuhusu utendaji na kuwezesha kufanya
maamuzi sahihi na kuchukua hatua za kuboresha.

Hatua muhimu katika uchanganuzi wa utendaji ni:

Kuweka malengo na viwango vya utendaji: Kwanza, ni muhimu kuweka


malengo na viwango vya utendaji vinavyotarajiwa. Hii inaweza
kujumuisha kuweka malengo ya uzalishaji, ubora, wakati wa utoaji,
huduma kwa wateja, au viashiria vingine vya utendaji.

Kukusanya data na habari kuhusu utendaji wa shughuli au mfumo. Kwa


ajili ya uchanganuzi wa utendaji, data na habari kuhusu utendaji wa
shughuli au mfumo unahitajika kukusanywa. Hii inaweza kujumuisha
kupima na kurekodi data kama vile vipindi vya wakati n.k

Kuchambua data na kutathmini utendaji: Baada ya kukusanya data,


uchambuzi unafanywa ili kuelewa jinsi utendaji unavyofanana na
malengo na viwango vilivyowekwa. Hii inahusisha kutumia zana za
takwimu na mbinu za uchambuzi wa data ili kutathmini utendaji na
kugundua mwenendo, maeneo yenye utendaji mzuri, na mapungufu.

Kugundua maeneo yenye utendaji mzuri na yale yanayohitaji


kuboreshwa au kuboreshwa. Kwa kutumia matokeo ya uchambuzi,
maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa na kuchukua hatua
zinabainishwa. Hii inaweza kujumuisha kurekebisha michakato,
kuboresha mifumo ya teknolojia, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi, au
kufanya mabadiliko mengine yanayolenga kuongeza ufanisi na ufanisi
wa utendaji.

Kupendekeza na kutekeleza hatua za kuboresha utendaji. Ni lazima


baada ya kutambua makosa hayo, mwalimu apendekeze hatua ambazo
atatumia kwa wanafunzi ili wasiyarudie mamkosa hayo. Hapa anaweza
kutumia mbinu mbalimbali za kufundisha ili wanafunzi wake
wasiyarudie kufanya makosa hayo hayo. Mbinu hizo zinaweza kuwa ni
Pamoja na mbinu ya moja kwa moja, mbinu ya tafsiri, mawasiliano na
kadhalika.

Uchanganuzi wa utendaji ni mchakato wa kuchunguza, kuchambua, na


kuboresha utendaji wa shughuli, michakato, au mifumo kwa lengo la
kufikia malengo yaliyowekwa na kuboresha ufanisi na ufanisi. Ni
mchakato muhimu katika kufuatilia na kuboresha utendaji wa kila
shughuli.

Kwa ujumla, uchanganuzi makosa unazingatia kutafuta na kurekebisha


kasoro na makosa iliyosababisha, wakati uchanganuzi wa utendaji
unazingatia kuelewa jinsi shughuli zinavyotekelezwa na kuboresha
utendaji kwa ujumla.

Nahitimisha kwa kusema kwamba kipengele hiki cha uchanganuzi


makosa na uchanganuzi utendaji ni kipengele muhimu sana kwa
mwalimu kwa sababu kipengele hiki kinasaidia mwalimu kutambua na
kuelewa kiwango cha mwanafunzi wake, uelewa wake na upungufu
wake na jambo hili humsaidia mwalimu kujua kwamba mwanafunzi
anajaribu kujifunza lugha ya pili.

Marejeleo

Corder, S. P. (1967). The significance of learner’s errors. 4(5), 161–170.

Dulay, H. (1982). Language two. Oxford University Press.

Richards, J. C., & Schmidt, R. W. (2002). Longman Dictionary of


Language Teaching and Applied Linguistics. Routledge.

You might also like