Download as rtf, pdf, or txt
Download as rtf, pdf, or txt
You are on page 1of 38

MCHANGO WA LISHE YA WANAFUNZI KATIKA UTENDAJI WAO KATIKA

SHULE ZA UPILI ZILIZOTEULIWA KATIKA DIVISHENI YA KAKOBA

WILAYANI MBARARA

BYAMUKAMA JOHN BAPTIST

16/BSU/BAED/149

TASNIFU ILIYOWASILISHWA KATIKA KITIVO CHA ELIMU KUTOSHELEZA

BAADHI YA MAHITAJI YA KUKAMILISHA SHAHADA YA SANAA KATIKA

ELIMU YA CHUO KIKUU CHA BISHOP

STUART MBARARA.

MEI, 2019
IKISARI

Mimi, Byamukama John Baptist, nathibitisha kuwa hii ni kazi yangu halisi, haijawasilishwa

katika Chuo kikuu kingine kwa ajili ya kufanikiwa shahada hii au nyingine.

Saini…………………………. Tarehe……………………………………

BYAMUKAMA JOHN BAPTIST

Mtafiti

ii
IDHINI

Nathibitisha kuwa nimeisoma kazi hii na ninaidhinisha ikubaliwe kwa utahini na kitivo cha

Elimu Chuo kikuu cha Bishop Stuart.

Saini……………………………. Tarehe……………………………………….

BWANA KUBAKURUNGI ABRAHAM

Msimamizi

iii
TABARUKU

Kazi hii naitabaruku kwa mwenyezi Mungu aliyenifanikisha katika shughuli zangu zote za

kusoma hadi mwisho. Ningependa pia kuitabaruku kwa Mamangu Bi-Kemitanda Gaudensia

aliyeniwezesha kufaulu katika shughuli za masomo yangu na kufanya kazi hii bila yeye kazi

hii haingemalizika.

iv
SHUKRANI

Ningependa kuwashukuru sana wazazi wangu wapendwa kwa kunizaa na kunipa malezi

mazuri, Mungu awabariki katika kazi zao za kila siku. Ninashukuru pia msimamizi tena

akiwa mhadhiri wangu mpendwa Bwana Kubakurungi Abraham kwa kunielekeza na

kunikosoa hapa na pale katika utafiti huu. Siwezi kuwasahau wahadhiri wangu wote katika

kitivo cha elimu chuoni.

Pia ningependa kuwashukuru kaka na dada zangu wote ambao ni Tabaro Godfrey, Kemizana

jane Scovia na popote walipo mungu awabariki bila kuwasahau marafiki zangu kama

Tumwesigye Nicholas, Arigumaho John Poul, Tumukunde Wilbroad, Amutukundire Pennah,

Aryatuzoora Rodgers na Akampurira Saphura na Mpenzi wangu Bi- Tusingize Allen na

wengine wengi walionishauri na kunisaidia katika utafiti huu Mwishoni na zaidi

ninamshukuru Mwenyezi mungu kwa kunijalia vipawa kadhaa na kunibariki maishani

mwangu hadi kumaliza masomo yangu mpaka shahada yangu ya kwanza.

v
YALIYOMO

vi
IKISIRI

vii
SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

1.0 Utangulizi

Sura hii inazingatia Usuli wa utafiti, Tatizo la utafiti, Malengo ya utafiti, Maswali ya utafiti, Upeo

wa utafiti na umuhimu wa utafiti.

1.1 Usuli wa utafiti

Lishe ni tawi la sayansi ambalo hufafanua uwiano wa virutubishi na madini katika vyakula.

Uwiano huu huangaliwa kati ya uzazi, kukua kwa kimo, afya na magonjwa. Lishe huhusisha

kuliwa kwa chakula, madini na virutubishi kuchukuliwa mwilini, madini na virutubishi kutumiwa

na seli za mwili, hali kadhalika kuondolewa kwa uchafu katika mwili.

Lishe ni chakula ambacho mnyama yeyote hula huambatana na jinsi kinavyopatikana.katika

binadamu lishe huhusisha maandalizi ya chakula, jinsi ya kukihifadhi na jinsi ya kuzuia chakula

kupata hali mbovu ambayo yanaweza kuleta maradhi kwa binadamu.

Kila familia na jamii inapaswa kufahamu nini huhusu lishe, Duniani kote, karibu nusu ya vifo vya

watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kila mwaka hutokana na ukosefu wa lishe bora na ya

kutosha, unaosababisha kudhoofika kwa kinga mwili dhidi ya magonjwa. Endapo mama hakupata

lishe ya kutosha wakati wa ujauzito au mtoto wake hakupata lishe ya kutosha ndani ya siku 1000

za mwanzo wa maisha yake, ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili pamoja na maendeleo yake

hudumaa. Hali hiyo hairekebeshiki pale mtoto atakapokuwa mkubwa – itamuathiri mtoto kwa

kipindi chote cha maisha yake.

Utapiamlo hujitokeza pale mwili unapokosa kiasi cha kutosha cha nishati (kalori), protini, wanga,

mafuta, vitamini, madini na lishe nyingine zinazohitajika kwa ajili ya kufanya viungo vya mwili

1
vikue na kufanya kazi vizuri. Mtoto au mtu mzima anaweza kupata tatizo la utapiamlo kwa kukosa

lishe ya kutosha au kupewa lishe zaidi ya inavyohitajika.

Mpango wa chakula mashuleni ulianzishwa tangu mwaka 1956 na wakoloni na kuimarishwa

kidogo mara baada uhuru chini ya serikali za mitaa,ambayo ilijumuisha utoaji wa chakula cha

mchana na huduma za afya kama vile upimaji na huduma ya kwanza. Taarifa zilizopo zinaonyesha

kwamba hadi mwishoni mwa miaka ya 1970 huduma hizi zilikuwa zimeachwa. Mwaka 1981/1982

TFNC ilianzisha jamii kuchangia chakula shuleni ambapo mpango huu ulizinduliwa Mkoani

Singida na Dodoma.Hivi sasa mpango huu wa huduma ya chakula shuleni unaendelea katika

wilaya chache Tanzania Bara ukiwa unafadhiriwa na mashirika kama WFP na jamii za wilaya ya

Moshi na Hai Mkoani Kilimanjaro. (Juu ya toleo la 12,2008).

Mwalimu na mtaalamu wa lishe, Halima Chamosi anasema japo baadhi ya vyakula kidhana

vinaweza kuwa na virutubisho sahihi kiafya, ana shaka na mazingira ya kuandaliwa na kuuzwa

kwake. “Ubuyu kwa mfano kwa dhati yake ni mzuri, ila tatizo linaweza kuwa ile rangi nyekundu

inayowekwa. Pia kuna ice cream, maji yanayotumiwa sio salama na vile vifungashio mwandaaji

anavipuliza kwa mdomo, hivyo anaweza kusambaza vijidudu hatari. Lakini pia mazingira ya

kuuzia vyakula hivi ni machafu na yanahatarisha afya, “anasema”. ‘Wanafunzi wanapaswa kula

chakula bora, mzazi badala ya kumpa fedha mkononi, amuandalie chakula, amfungashie aende

navyo shuleni. Kweli ni kuwa nchini Uganda hakuna mfumo maalumu wa kudhibiti vyakula

vinavyouzwa shuleni. Hii ni kwa kuwa hakuna utaratibu wa kutoa chakula cha pamoja kwa

wanafunzi, jambo linalotoa fursa kwa wanafunzi kula wanachopenda hata kama ni hatari kwa afya

zao. Kwa upande mwingine Serikali inakiri kuwa asilimia 50 mpaka 75 ya watoto wa shule za

msingi na hata shule za sekondari wanakwenda shule wakiwa hawajapata mlo wowote wa asubuhi

nyumbani na pia hawali kitu chochote wakiwa shule. Kwa hivyo utafiti huu utafanywa

2
kuchunguza namna lishe kwa wanafunzi inavyochangia katika utendaji bora wa wanafunzi wa

shule za upili katika tarafa la Kakoba wilayani Mbarara.

1.2 Tatizo la utafiti

Huduma ya chakula ni huduma muhimu inayomwezesha mtu kupata mahitaji yake ya msingi ya

kimwili na ya kisaikolojia.

Ulaji usiofaa wa vyakula umekuwa kama ada katika shule nying za Bweni ziwe za Serikali au za

binafsi. Uzoefu unaonyesha kwamba katika Shule nyingi za sekondari katika tarafa ya Kakoba

wanafunzi wanalishwa vyakula vya aina moja kwa muda mrefu na bado vyakula hivyo vinakosa

sifa ya ubora. Katika shule nyingi ugali na maharage ndiyo chakula kikubwa, huku mara chache

wanafunzi wakiabadilisha vyakula vyenye virutubisho mbadala kama nyama, mbogamboga na

vinginevyo. Ingawa kuna simulizi kuwa zamani katika baadhi ya shule siku ya ratiba ya wali na

nyama, ilichulikuliwa kama sherehe au sikukuu. Hii ni kwa kuwa vyakula hivyo vilikuwa adimu

kupikwa. Jambo linalowafurahisha wanafunzi hawa. Lakini kulingana na uelewa wa mtafiti,

hakuna utafiti wowote uliofanywa kuchunguza namna lishe ya wanafunzi inavyochangia katika

utendaji wa wanafunzi katika shule za upili zinazopatikana katika tarafa ya Kakoba wilayani

Mbarara.

1.3 Malengo ya utafiti

Utafiti huu una malengo mawili, yaani; lengo kuu na malengo mahususi. Sehemu ifuatayo inajadili

malengo hayo;

1.3.1 Lengo kuu.

Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza uhusiano liopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji

bora wa wanafunzi wa shule za upili katika tarafa ya Kakoba wilayani Mbarara.

3
1.3.2 Malengo mahususi

i. Kutambulisha utendaji wa wanafunzi wa shule za upili zinazopatikana katika tarafa ya

Kakoba.

ii. Kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji bora wa wanafunzi

wa shule za upili.

iii. Kujadili changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa shule

za upili.

1.4 Maswali ya Utafiti

i. Je wanafunzi wa shule za upili wanatenda vipi katika masomo yao?

ii. Je ni uhusiano upi uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji wao?

iv. Ni changamoto zipi zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa shule za

upili?

1.5 Upeo wa Utafiti

1.5.1 Upeo wa kijiografia

Utafiti huu ulifanyiwa katika Divisheni ya Kakoba katika Manispali ya Mbarara wilayani Mbarara

ambapo mtafiti alichagua shule mbili za upili.

1.5.2 Upeo wa mada

Utafiti huu ulifanywa kuchunguza mchango wa lishe bora katika utendaji wa wanafunzi wa shule

za upili katika Divisheni ya Kakoba wilayani Mbarara. Kwa hivyo mtafiti alilenga kutambulisha

utendaji wa wanafunzi wa shule za upili zinazopatikana katika tarafa ya Kakoba, kuchunguza

uhusiano uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji bora wa wanafunzi wa shule za upili na

kujadili changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa shule za upili.

4
1.5.3 Upeo wa wakati

Utafiti ulifanywa kwa miezi minne kuanzia Februari hadi mwezi wa tano Muda huu ulimsaidia

mtafiti kupata data kuhusu mchango wa lishe bora katika utendaji wa wanafunzi wa shule za upili.

5
SURA YA PILI

MAPITIO YA MAANDISHI

2.0 Utangulizi

Kazi Tangulizi ni jumla ya utafiti uliyofanyika, ambao unalingana na mada ya utafiti husika. Omari

(2001), Kazi tangulizi hutoa ujuzi na maarifa ya wanazuoni waliowahi kufanya kazi yenye

mwelekeo na lengo la mtafiti. Pia kazi tangulizi, humsaidia mtafiti kutambua mambo yapi

yamefanyiwa utafiti na yapi bado. Sura hii ilikuwa na maandishi ya waandishi wengine

yanayohusu mchango wa lishe katika utendaji bora wa wanafunzi wa shule za upili katika tarafa la

Kakoba wilayani Mbarara.

2.1 Uhusiano uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji bora wa wanafunzi wa shule za

upili.

Chakula ni ugawaji wa chakula na fitafunwa shuleni kwa wanafunzi wakiwa shuleni na kupeleka

nyumbani kwa ajili ya familia zao.(www.tenmet.org). Huduma ya chakula ni huduma muhimu

inayomwezesha mtu kupata mahitaji yake ya msingi ya kimwili na ya kisaikolojia.

Perry, C., & Story, M. (2003). Wanasema kwamba mpango wa chakula mashuleni ulianzishwa

tangu mwaka 1956 na wakoloni na kuimarishwa kidogo mara baada uhuru chini ya serikali za

mitaa,ambayo ilijumuisha utoaji wa chakula cha mchana na huduma za afya kama vile upimaji na

huduma ya kwanza. Taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba hadi mwishoni mwa miaka ya 1970

huduma hizi zilikuwa zimeachwa. Mwaka 1981/1982 TFNC ilianzisha jamii kuchangia chakula

shuleni ambapo mpango huu ulizinduliwa Mkoani Singida na Dodoma.Hivi sasa mpango huu wa

huduma ya chakula shuleni unaendelea katika wilaya chache Tanzania Bara ukiwa unafadhiriwa

na mashirika kama WFP na jamii za wilaya ya Moshi na Hai Mkoani Kilimanjaro. (Juu ya toleo la

12, 2008).

6
Kulingana na Zhang, J. (2008), Ukosefu wa lishe bora kwa watoto umewaathiri wanafunzi shuleni

wakishindwa kujifunza darasani kwa kukosa vyakula vinavyoimarisha ubongo na mwili kwa

jumla. Ukosefu wa lishe bora umeathiti nguvukazi kwa taifa na kusababisha umaskini wa kipato

katika jamii nyingi.

Zao la viazi vitamu ndilo limeonekana kuliwa kwa wingi Zaidi likitegemewa na asilimia 60 ya

watanzania kama chanzo cha lishe na kipato. Zaidi ya hekta 760000 sawa na tani 3.8 milioni

huvunwa kila mwaka (tani 5.03 kwa kila hekta). Wataalamu wa lishe wameviongezea vitamin A na

madini mengine viazi vitamu ili vinapoliwa mlaji apate virutubisho muhimu kwa pamoja na hivyo

kupambana na utapiamlo.

Kwa kuwa viazi vitamu vimekuwa vikilimwa kwa muda mrefu, juhudi sasa zimeelekezwa kwenye

usambazaji wa mbegu zilizoboreshwa (viazi lishe) kwa wakulima wadogo, ikiwa ni pamoja na

kushawishi mabadiliko ya mitalaa ya shule, ili kuwawezesha wanafunzi kusambaza, kulima

nakujua kupika viazi na jinsi ya kuandaa mlo kamili wakiwa shuleni. Meyer, M. (2005)

Hata hivyo imeonekana kuwa uelewa mdogo wa masuala ya lishe miongoni mwa walimu wa shule

za msingi na sekondari. Kwa mfano, tathmini iliyofanywa na jukwaa la kilimo la Aasi zisizo za

kiraia (Ansaf) kuhusu mtalaa wa elimu ya msingi wa 2015 kama unahusisha masuala ya lishe

najinsia katika silabasi ya mwaka 2016, ilionekana bado kuna upungufu.

Tathmini hiyo ilifanywa katika shule tano kutoka wilaya ya mkuraga mkoani pwani na wilaya ya

Gairo, mkoa wa morogoro ikihusisha wanafunzi 30 na walimu 12. Imeonekana kwamba

ufundishwaji unafanyika kwa nadharia badala ya vitendo. Vile vile sala la umiliki wa ardhi,

majukumu ya jinsia katika uzalishaji, utayarishaji na uandaaji wa chakula hayakupewa kipaumbele

katika silabasi hiyo. Fulkerson, J. (2005).

Tathmini hiyo ilibaini kuwepo kwa tofauti ya viwango vya elimu katika ubora, uzoefu na masomo

wanayofundisha, japo wameonyesha uelewa mzuri kuhusu lishe na mlo kamili. Walimu

7
waliohojiwa wakati wa kufanya tahmini hiyo walishauri masomo ya mlo kamili na lishe yawekwe

kwenye masomo ya sayansi na ya ukuaji na uzalishaji wa mazao ya chakula na uandaaji pamoja na

upikaji wake ndiyo yafundishwe kama stadi za kazi. A., & Houser, R. (1995).

Utafiti mwingine uliofanywa na Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) na kuwasilishwa hivi

karibuni Dar es Salaam, umeonyesha umuhimu wa kusambaza mazao ya mzizi yaliyoongezewa

lishe kwa wakulima wadogo kupitia wanafunzi. Kwa mfano katika mikoa ya kanda ya ziwa kama

vile mwanza, tabora na Geita wanafunzi wametumika katika kusambaza mbegu za viazi kwa

wazazi na walezi wao kiasi cha kurahisisha upatikanaji wa mbegu za viazi zilizoboreshwa. Ni

wakati sasa kwa serikali kuingalia sekta ya elimu kama kichocheo cha kukuza lisha saha kwa

watoto. Wazazi wapatiwe elimu ya kutosha ya lishe ili kuepusha utaopiamlo kwa watoto na jamii

nzima. Wright, A., & Libonati, J. (2008).

Ukosefu wa elimu ya kutosha ya lishe umesababisha watoto kupata utapiamlo na hatimaye

kudumaa. Imeonekana kuwa watoto wengi huondoka nyumbani kwenda shule bila kupata staftahi

na hata wanapofika shule hukaa muda mrefu wakiwa na njaa. Matokeo yao wanashindwa kuelewa

masomo darasani na mwishowe kufeli mitihani. Muldoon, M. (2005).

Aidha, shule zinapaswa kuandaa milo kwa wanafunzi ikiwamo uji au chai ya asubhi na chakula

cha mchana, mlo huo unapaswa kuwa na virutubisho vya kutosha na siyo kujaza matunda. Watoto

washirikishwe katika uandaaji wa chakula ikiwa ni sehemu ya masomo ya stadi za kazi. Vilevile,

suala la lishe lipewe kipaumbele kama moja ya mikakati ya kuimarisha elimu. Ni aibu kwa

Tanzania inayojitosheleza kwa chakula, lakini bado utapiamlo unabaki kuwa tatizo sugu.

Tuondokane na hali hii kwa kuweka mikakati kwa wanafunzi wakiwa wadogo. Haiwezekani taifa

letu ambalo vyakula vinalimwa kwa wingi tukashindwa kuwahudumia watoto wetu shuleni kwa

chakula. Wolpert, S., Wheeler, M. (2008).

8
2.2 Changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa shule za upili.

Huduma ya chakula ni kitu muhimu na ni hitaji la lazima kwa wanafunzi ,huwajengea uwezo

mzuri katika tendo la kujifunza.Ingawa huduma hii ni muhimu lakini imekabiliwa na changamoto

nyingi katika utoaji wake kwa shule za msingi nchini Tanzania. Licha ya changamoto hizo inabidi

kutafuta mbinu za kuzitatua. Zifuatazo ni changamoto na mbinu za kukabiliana na changamoto

hizo ambazo ni:-

Upungufu wa rasilimali fedha (WET, 1995). Upungufu wa rasilimali fedha ni changamoto

mojawapo ya huduma ya chakula ambayo inasababisha kurudisha nyuma tendo zima la huduma ya

chakula shuleni. Nitawashirikisha wazazi kupitia vikao vya shule kuchangia huduma hii ya

chakula shuleni kwa kuchangia fedha kwa kila mzazi aliye na mtoto shuleni Kwani fedha zina

hitajika katika uendeshaji wa huduma hii ya chakula. Mfano fedha inahitajika kwa ajiri ya

kununulia vifaa vya kuendeshea huduma hiyo kama vile vyombo vya kupikia chakula kwa ajiri ya

kulipa mpishi wa kupika chakula na kukarabati baadhi ya majengo ya kutolea huduma hiyo

shuleni.

Uelewa mdogo wa jamii kuhusu utoaji wa huduma ya chakula shuleni (MANTEP, 1995) Hii ni

changamoto mojawapo katika utoaji wa hudumaya chakula. Jamii nyingi Zina ukosefu wa maarifa

ya kutosha kuhusu huduma hii ya chakula. Kwa kutumia uzoefu nilionao mimi kama mwalimu

kuwashawishi na kuwaelimisha wazazi ,walimu wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kupitia

mikutano ya kijiji ,ili watambue umuhimu wa huduma ya chakula shuleni kwa kuwaambia kuwa

chakula ni muhimu sana kwa wanafunzi kwani tafiti nyingi zimeonyesha kuwa waanafunzi

wanaopata chakula shuleni walau hata mlo mmoja wanafanya vizuri katika mitihani yao kuliko

wale ambao hawapati chakula shuleni akili yao huwa chini kwani asilimia kubwa ya watoto

ambao hawapati chakula shuleni husinzia darasani kutokana na kutokupata chakula cha kuwapa

9
nguvu. Hivyo watoto wana hitaji vyakula venye virutubisho vya kutosha ili wawe na afya nzuri ili

waweze kusoma na kupokea kile wanachofundishwa kwa ustadi zaidi.

Hali duni ya kiuchumi. Changamoto hii inasababisha huduma ya chakula shuleni kutoendelea

mbele kutokana na wananchi kuwa na kipato kidogo. Changamoto hii nitaitatua kwa kuweka wazi

mchakato mzima wa utoaji huduma ya chakula kwa kuwashirika wadau mbalimbali kama vile

mashirika ya kiserikali na mashirika yasiyo ya kiserikali,tasisi mbalimbali za kidini nasizo za

kidini kuchangia huduma hii ya chakula kwa kutoa fedha au kuchangia chakula katika shule.

Shule itafute njia mbalimbali zitakazowezesha kupata vyakula vyenye lishe bora kwa kuwasiliana

na mashirika mbalimbali kama vile mashirika ya dini, Taasisi mbalimbali kama vile,WFP na

OxfamGB kwani mashirika hayo yatakapofadhili huduma hii ya chakula shuleni itaongeza

uandikishaji wa wanafunzi la kwanza kiasi kikubwa ,ongezeko la mahudhurio, kupungua kwa

viwango wanafunzi wanaoacha shule na maendeleo ya kimasomo huimarika. (WEU, 1998).

Kukosekana kwa mvua (ukame). Hii ni changamoto mojawapo inayosababisha kukwamisha

huduma ya chakula shuleni. Nitaawambia wadadu mbalimbali kama wazazi, jamii kupitia

mikutano mbalimbali ya serikali ya kijijij kwa kuwaelimisha Elimu ya mazingira kwa kupanda

miti ili kukabiliana changamoto hiyo ya ukame na vilevile kuwa shawishi kulima mazao

yanayoendana na hali ya hewa ya eneo hilo .Kwa mfano katika Mikoa ya yenye ukame kama

Mikoa ya Shinyanga ,Dodoma na Singida ili waweze kukabiliana na changamoto hiyo kwani

mvua zinazonyesha huwa zinanyesha kwa msimu. Vile vile nitashirikisha shule itafute njia

mbadala zitakazowezesha kupata vyakula vyevye lishe bora kwa kuanzisha kilimo cha bustani na

ufugaji wa samaki, ili kukabiliana na changamoto hii ya chakula shuleni. kufanya tendo la

ufundishaji na ujifushaji uwe wa bora na wenye mafanikio.(MANTEP,1995).

Mgongano wa kisera. Hii ni changamoto mojawapo inayosababisha huduma hii kuwa chini na

hakuna sera iliyo kamili ya serikali kuhusu chakula cha shule. Vilevile jamii nyingi inauelewa

10
mdogo kuhusu sera hii ya huduma ya chakula. Sera zinazotolew a haziwi wazi kwa wadau kuhusu

chakula cha shule. Kwani sera hizo hazionyeshi namna na mipango ya uendeshaji ya uendeshaji

hivyo kusababisha kutoelewana katika uchangiaji upande wa jamii na taasisi nyingine .Hivyo

nitawashirikisha kamati ya shule,na wazazi kupitia vikao mbalimbali vya wazazi shuleni

kuwaelezea manufaa ya huduma ya chakula cha wanafunzi shuleni.Kwani sera hizo zinatungwa

kwa manufaa Ya Taifa ila zinaweza kuumiza jamii ya sehemu husika. Mfano katika uchangiaji wa

fedha, sera inasema wazazi hawaruhusiwikuchangia kitu chochote shuleni. Ukifuata sera hiyo

itasababisha watoto kutopata chakula angalau mlo mmoja wa chakula shuleni ili kufanya tendo

zima la ufundishaji na ujifunzaji liwe lenye mafanikio. (MANTEP 1991).

Hivyo basi changamoto zipo nyingi hizo nibaadhi tu ya changamoto endapo za kutatua

changamotot hizo zitazingatiwa na kufuatwa ipasavyo zitasaidia tendo zima la ufundishaji

ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule za msingi, kwani chakula bora kwa mwanafunziinaongeza

ufaulu inaboresha utambuzi, umakini na mahudhurio mazuri shuleni. Hivyo chakula cha shule si

kama kitu muhimu tu bali ni mahitaji ya lazima na haki kwa mwanafunzi.

11
SURA YA TATU

MBINU ZA UTAFITI

3.0 Utangulizi

Sura hii inawasilisha mbinu za utafiti zilizotumika katika kukusanya na kuchambua data. Kothari

(2008) anaeleza kwamba, utafiti wowote ule wa kitaaluma ni lazima ufanywe kwa kuongozwa na

mbinu mbali mbali za utafiti ili uweze kutoa matokeo yasiyo na shaka ndani yake. Kwa msingi huo

basi, zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zilitumika katika kukusanya data za utafiti huu kama

zinavyoelezwa hapa chini.

3.1 Mpango wa utafiti

Mbinu ya utafiti huu ilikuwa ni ya maelezo. Mbinu ya maelezo kama ilivyofafanuliwa na Punch,

(2004) ni kupanga, kutoa sababu na kuzieleza data kama zilivyoelezwa na walengwa wa utafiti.

Mtafiti huzipanga kutokana na maudhui au makundi yanayofanana. Mtafiti alikuwa makini katika

kueleza, kufafanua, kuhakiki, kuvumbua, kufanya majaribio, kutafsiri taarifa alizozipata kupitia

muundo huu wa utafiti. Sehemu ndogo ya utafiti ilitumia takwimu kama kielelezo.

3.2 Eneo la utafiti

Utafiti huu ulifanyika katika tarafa ya Kakoba Wilayani Mbarara. Eneo hili limechaguliwa kwa

sababu ndilo eneo lenye uwezo wa kutoa data stahilivu kwa utafiti huu. Aidha eneo hili

limeteuliwa kutokana na muda wa utafiti kuwa mdogo na ufinyu wa bajeti ambayo ilisababisha

mtafiti kutoweza kuzunguka katika Manispali nzima, vile vile mtafiti alizunguka katika Divisheni

ya Kakoba ambapo alijihushisha na shule za sekondari mbili ambazo zilikuwa Mbarara Allied

school, na Global High school.

12
3.2 Populesheni itakayolengwa

Utafiti huu ulilenga walimu wakuu, walimu na wanafunzi wa shule za upili zinazopatikana katika

divisheni ya kakoba wilayani Mbarara. Katika utafiti huu mtafiti alilenga walimu 10 wa shule za

upili, walimu wakuu 2, wanafunzi 38 na wazazi 20 ambao kwa ujumla walikuwa watafitiwa 70

kutoka katika shule mbili za sekondari kutoka katika Divisheni ya Kakoba.

3.3 Uteuzi wa sampuli

Katika utafiti huu, sampuli iliyotumika ilikuwa ya walimu wakuu, walimu, wazazi na wanafunzi

wa shule za upili. Shule hizi ziliteuliwa katika usampulishaji ili kuwakilisha wahojiwa wote bila

kutegemea shule moja.

Watafitiwa thelathni na watano (35) kutoka katika kila shule zilizochaguliwa walitumika ambapo

walimu 5, mwalimu mkuu na wanafunzi 19 na wazazi 10 walichaguliwa kutoka katika kila shule

kwa hivyo ujumla ya watafitiwa 70 walichaguliwa kutoka katika shule mbili. Jambo lililomsaidia

kupata data stahilivu na ya kutosha katika utafiti wake.

3.4 Usampulishali wa populesheni

Usampulishaji tabakishi na nasibu ulitumiwa kuhusisha populesheni yote ya wahojiwa. Wahojiwa

walitolewa kutoka sehemu mbalimbali katika Divisheni ya Kakoba ili kupata data ya udedushi

kiidadi na siyo kiidadi ambayo ilihusisha populesheni yote ya Kakoba na data iliyolengwa

kupatikana. Mtafiti alichagua sampuli yake kwa kuunda vikundu vidogo vidogo kutoka kwa

kikundi kimoja kikubwa yaani wanafunzi na walimu, kisha mtafiti alichagua sampuli kutoka kila

kikundi ili aweze kupata data ya utafiti wake, usampulishaji nasibu ulisaidia mtafiti katika

kuchagua sampuli yake kwa sababu kila mtu katika Shule za sekondari ako na nafasi ya

kujumuishwa katika utafiti huu kwa hivyo mtafiti aliorodhesha majina yote na baadaye alichagua

sampuli yake kinasibu. Usampulishaji huu ulifanyika kwa kuandika kila sampuli inayowezekana

13
katika vipande vya karatasi, halafu alichanganya karatasi hizo katika boksi baada ya hapo

alitikisha boksi hilo ili vipande vya karatasi vichanganyike halafu ndio mtafiti aliweza kuchagua

chochote kile bila kufuata kigezo chochote. Walimu wakuu na wazazi waliteuliwa kwa kutumia

usampulishaji lengwa.

3.5.0 Vifaa vya kutumia katika utafiti

Vifaa vingi vilitumiwa katika utafiti ambavyo vilikuwa, mwongozo wa mahojiano, hojaji na hati za

maandishi. Hayo yote yalitumiwa kukusanya data kwa udedushi wa kiidadi na siyo kiidadi.

3.5.1 Mwongozo wa mahojiano

Hiki kilitumiwa kukusanya data ya msingi kwa kuunda maswali yaliyoulizwa kwa wahojiwa

ambao walijibu barabara na mtafiti alikuwa anaandika katika daftali yake na majibu mengine

aliyahifadhi. Zana hii ilimsaidia mtafiti katika ukusanyaji wa data yake kwa sababu wahojiwa

walikuwa wanajibu maswali ya mtafiti palepale na mtafiti alikuwa anawafafanulia zaidi wale

ambao hawakuweza kuelewa maswali ya mtafiti kwa hivyo zana hii ilimsaidia mtafiti kupata data

stahilivu kwa sababu mtafiti alikuwa anauliza kila jambo alilotaka kujua kutoka kwa wahojiwa

wake.

3.5.2 Hojaji

Hii ni mbinu ambayo mtafiti alitumia katika ukusanyaji wa data ya utafiti kutoka nyanjani. Mtafiti

aliunda maswali yenye uhusiano na mada ya utafiti. Kulikuwa maswali ambayo yaliandikwa na

kompyuta na kunakilishwa kwa karatasi na kuchukuliwa wahojiwa. Wahojiwa walijibu maswali

hayo na baadaye mtafiti aliyapokea na kuyachunguza kama ilivyoonyeshwa katika sura ya nne.

Mbinu hii ilitumiwa kwa sababu wahojiwa walikuwa na muda wa kutosha kujibu maswali ya

mtafiti pia katika kutumia hojaji mtafiti alikuwa na wakati wa kufanya shughuli nyingine kama

kuhoji watafitiwa ambao walikuwa hawajui kuandika na kusoma.

14
3.5.3 Hati za maandishi

Mtafiti alitumia vitabu vya kiada, magazeti, ripoti, karatasi za habari na machapisho yenye

uhusiano na utafiti. Haya yaliangalia data yenye uhusiano na mada na shabaha za utafiti ambayo

yameshaandikwa. Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kujua mambo ambayo watafiti na waandishi

wengine walivyoandika kuhusu mada yake.

3.6 Utaratibu wa utafiti

Mtafiti alitoa barua ya utambulisho kutoka kwa mkuu wa kitivo cha elimu Chuo kikuu Bishop

Stuart ambayo ilimwezesha na kukubaliwa kufanya utafiti wake katika shule za sekondari zilizo

changuliwa katika Divisheni ya Kakoba wilayani Mbarara.

3.7 Utengenezaji na uchambuzi wa data

Mtafiti alitengeneza na kuchambua moja kwa moja data aliyoipata kutoka uwandani, wahojiwa na

kuiweka kwenye jedwali ili yaorodheshwe kwa utaratibu halafu msimamo wa kuchunguza

mchango wa lishe ya wanafunzi katika utendaji wa wanafunzi wa shule za upili uliangaliwa

Barabara.

3.8 Masuala ya maadili

Mtafiti alizingatia maadili ya jamii kwa kuwahoji wale waliokubali kutoa habari kuhusu utafiti,

majina yao yalihifadhiwa na hayakuandikwa katika karatasi yoyote ya utafti. Pia karatasi za hojaji

ziliwekwa bara’bara ili mtu asije akakuta jina lake katika umma kutokana na maarifa aliyompa

mtafiti. Mtafiti alifafanua umuhimu na shabaha za utafiti na masuala ambayo hayakueleweka kwa

wahojiwa yaliwafafanuliwa ili kuyaelewa zaidi na kuweza kumtolea taarifa mtafiti kwa

madhumuni ya kufanikiwa kwa utafiti wake.

3.9 Vizuizi vya utafiti

Katika muda wa utafiti, mtafiti alikumbwa na vizuizi, miongoni mwa vizuizi hivyo, vifuatavyo

vilikuwa juu ya mamlaka ya uongozi wake;

15
Ukosefu wa fedha za kutosha za kutumia katika utafiti, pesa hizo zingetumiwa kuchapisha makala

ya hojaji na mwongozo wa mahojiano. Pia nauli ya kutembelea wajibu na zakutumia katika kupiga

simu kuuliza ikiwa wajibu wamejibu maswali yake. Kizuizi hiki kilitatuliwa kwa kuomba watu wa

familia yake usaidizi wa pesa.

Kuchelewa kukusanya data, hii ilitokana na wajibu kutojibu maswali ya hojaji mapema. Mtafiti

alitatua hiki kwa kuwakumbusha kila mara aidha kwa kuwatembelea au kuwapia simu.

16
SURA YA NNE

UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA

4.0 Utangulizi

Sura hii inaonyesha ugunduzi wa utafiti. Mtafiti hutoa utafiti wake ambao alioupata kutoka

uwanjani.

SEHEMU A

4.1 Data za watafitiwa

Mtafiti alichunguza na kuchanganua data za watafitiwa kulingana na kiwango cha jinsia na umri

katika shule za upili. Kwahivyo, Mtafiti alichunguza vigezo hivi ili kutosheleza matokeo ya

uwanjani.

4.1.1 Jedwali 1 kuonyesha jinsia ya washiriki.

Wajibu/watafitiwa katika utafiti wa uwanjani.

Jinsia Marudio Asilimia (%)

Kiume 30 43 %

Kike 40 57 %

Ujumla 70 100

Asilia: Data za msingi 2019

Kulingana na jedwali 1 inaonyesha kuwa utafiti ulitumia watafitiwa wa jinsia ya kike na kiume pia

inaonyesha kuwa wanaume walikuwa wengi kuliko wanawake. Matokeo pia yanaonyesha kwamba

wanaume walikuwa 40 yaani asilimia 57 % na wanawake walikuwa 30 yaani asilimia 43 %. Jinsia

ya wahojiwa ilikuwa kama ilivyo kwa kuwa mtafiti alilinganisha jinsia zote mbili ili ajue mawazo

ya wanawake na wanaume kuhusu uhusiano uliopo baina ya lishe bora na utendaji wa wanafunzi

wa shule za upili bila kubagua katika jinsia. Hii ni maana kwamba mtafiti hakutaka kubagua jinsia

17
kwa hivyo mtafiti alitumia wanaume 40 yaani asilimia 57% na wanawake 40(43%) ambapo kwa

ujumla walikuwa wahojiwa 70(100%) walioshiriki katika utafiti uliofanywa kuchunguza mchango

wa fasihi simulizi katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili.

4.1.2 Umri wa watafitiwa.

Jedwali 2 linaonyesha umri wa watafitiwa.

Umri Marudio Asilimia (%)

14-20 54 77 %

21-25 4 6%

26-30 3 4%

31- 35 5 7%

36 na zaidi 4 6%

Ujumla 70 100

Asilia: Data za msingi 2019.

Jedwali la 2 linawakilisha kwamba watafitiwa 54 wanaowakilisha asilimia 77% ya watafitiwa

walikuwa na umri wa miaka 14-20, ambao wengi wao walikuwa wanafunzi, watafitiwa 4

wanaowakilisha asilimia 6% walikuwa kati ya 21-25, watafitiwa 3 wanaowakilisha asilimia 4%

walikuwa kati ya miaka 26-30, watafitiwa 5 wanaowakilisha asilimia 7% walikuwa kati ya miaka

31- 35 na watafitiwa 4 waliowakilisha asilimia 6% walikuwa kati ya miaka 36 na zaidi.

Kutokana na jedwali hili, tunaona kwamba watafitiwa kati ya miaka 14-20 wanachukua asilimia

kubwa yaani 77 %. Hii ni kwa kuwa wanafunzi wengi walipatikana katika umri wa miaka hiyo.

Pia kuna na wale wenye miaka 26 na zaidi ambao walichukua asilimia ndogo kuliko wangine hii ni

kwa sababu walimu wengi walikuwa katika kiwango hicho.

18
Umri ulikuwa katika makundi ili kurahisisha kwa watafitiwa kwa sababu kinajulikana kwamba

baadhi ya watu hawapendi kuonyesha umri wao wenyewe hasa jinsia ya kike.

4.2 Kutambulisha utendaji wa wanafunzi wa shule za upili zinazopatikana katika tarafa ya

Kakoba.

Katika utafiti huu wahojiwa zaidi sana wanafunzi waliulizwa kama wanapewa chakula mara ngapi

kwa siku na matokeo yalikuwa kama inavyoonyeshwa katika jedwali la 3 hapo chini.

Maoni ya wanafunzi Marudio Asilimia

Tunapwewa chakula mara tatu kila siku 26 55

Tunapewa chakula mara moja kwa siku 16 34

Tunapewa chakula mara mbili kila siku 5 11

Ujumla 47 100

Asilia: Data za msingi 2019.

Jedwali la tatu linaonesha kwamba wanafunzi wengi yaani 26 waliowakilisha asilimia 55% ya

wanafunzi walisema kwamba wanapewa chakula mara tatu kila siku, wahojiwa wanafunzi 16

waliowakilisha asilimia 34% walisema kwamba wanapewa chakula mara moja kila siku na

wanafunzi wahojiwa 5 waliowakilisha asilimia 11% walisema kwamba wanapewa chakula mara

mbili kwa siku. Wahojiwa wanafunzi walipoulizwa aina ya chakula wanachopewa shuleni, wote

walisema kwamba wanapewa ugali na maharagi.

Mtafiti aliendelea na kufanya uchunguzi wake ambapo aliuliza wanafunzi ikiwa wanafurahiya

chakula wanachopewa shuleni na matokeo yalikuwa kwamba wahojiwa wote walisema kwamba

hawafurahi na namna wanavyolishwa wanapokuwa shuleni.

Ili kutambua utendaji wa wanafunzi wa Kiswahili, wahojiwa waliulizwa kueleza namna wanafunzi

wa shule za upili wanavyotenda kitaaluma, matokeo ya utafiti yalionesha kwamba kuna wanafunzi

wanaotenda vizuri na wale wanaotenda vibaya.

19
4.3 Kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji bora wa wanafunzi

wa shule za upili.

Ili kujibu swali la pili la utafiti huu, wahojiwa waliulizwa ikiwa lishe ya wanafunzi inahusiana

utendaji wa wanafunzi wa shule za upili, na matokeo yalikuwa kwamba baadhi ya wahojiwa yaani

62 waliowakilisha asilimia 86% walisema kwamba lishe ya wanafunzi inachangia sana katika

utendaji wa wanafunzi na wahojiwa 08 waliowakilisha asilimia 14% walisema kwamba lishe ya

wanafunzi hainamchango wowote katika utendaji kitaaluma wa wanafunzi wa shule za upili.

Wahojiwa waliulizwa kueleza namna lishe ya wanafunzi inavyochangia katika utendaji wa

wanafunzi wa shule za upili, na matokeo ya wahojiwa yanaoneshwa katika jedwali nne hapo chini.

Jedwali la nne linaloonyesha uhusiano wa lishe katika utendaji wa wanafunzi wa shule za

upili.

Uhusiano Marudio Asilimia

Lishe ya wanafunzi inasaidia katika kupandisha ufaulu na kupungua utoro 22 31

shuleni jambo linalochangia katika utendaji wa wanafunzi wa shule za

upili.

Lishe ya wanafunzi husaidia wanafunzi kuelewa kile kinachofundihwa 14 20

darasani.

Vyakula vyenye virutubisi husaidia wanafunzi kuwa na afya nzuri ambalo 10 14

ni jambo linalochangia katika utendaji bora kwa wanafunzi wa shule za

upili.

20
Wanafunzi wakelishwa chakua kibaya mara nyingi husababisha migomo 24 34

jambo linalokwamiza utendaji bora kwa wanafunzi wa shule za upili.

Ujumla 70 100

Asilia: Data za msingi 2019

Jedwali la nne linaonyesha kwamba wahojiwa wengi yaani 24(34%) walisema kwamba wanafunzi

wakelishwa chakua kibaya mara nyingi husababisha migomo jambo linalokwamiza utendaji bora

kwa wanafunzi wa shule za upili, wahojiwa 22(31%) walisema kwamba lishe ya wanafunzi

inasaidia katika kupandisha ufaulu na kupungua utoro shuleni jambo linalochangia katika utendaji

wa wanafunzi wa shule za upili, wahojiwa 14(20%) walisema kwamba lishe ya wanafunzi husaidia

wanafunzi kuelewa kile kinachofundihwa darasani na wahojiwa 10(14%) walisema kwamba

yyakula vyenye virutubisi husaidia wanafunzi kuwa na afya nzuri ambalo ni jambo linalochangia

katika utendaji bora kwa wanafunzi wa shule za upili.

Matokeo kutokana na mahojiano ya walimu na wazazi yalikuwa kwamba walimu 12(17%)

walisema kwamba ilikuwa unaweza kukuta mwanafunzi anasinzia darasani,na ukimuuliza nini

tatizo, anakuambia njaa! kiuhalisia si rahisi kwa mwanafunzi huyu kumuelewa mwalimu hata

kidogo. Kwa hivyo lishe ya wanafunzi inachangia sana katika utendaji wa wanafunzi wa shule za

upili.

Kutokana na mahojiano ya mtafiti na wazazi, Wazazi 10(14%) walisema kwamba tuligundua

kwamba kumbe si rahisi kwa mwanafunzi kushinda shule kwa waa nane bila chakula. Muda huu

unatosha kudhoofisha afya yake na matokeo ni kushindwa kumudu masomo.

21
Kwa upande wa walimu wakuu waliowakilishwa katika utafiti huu, walisema kwamba licha ya

usaidia uelewa kwa wanafunzi lishe ya wanafunzi umesaidia katika kupunguza utoro kwa

wanafunzi.

Utafiti uligundua kwamba mwanafunzi yoyote anapokwenda shuleni na kushinda huko bila kupata

chakula chochote, hupoteza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoelewa darasani hata kama mwalimu

tajitahidi kufundisha.

Wahojiwa 8(11%) waliohojiwa walisema kwamba uwezo wa kujifunza wa mwanafunzi mwenye

utapiamlo ni mdogo kulinganisha na mwanafunzi mwenye afya nzuri.

4.3 Kuchunguza changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa

shule za upili.

Utafiti huu ulijikita katika kuchunguza changamoto zinazokumba shule za upili kuhusu lishe ya

wanafunzi, na utafiti huu ulilenga walimu wakuu, walimu na wanafunzi pamoja na wazazi. Katika

utafiti huu wahojiwa wote walisema kwamba kuna changamoto zinazokabili shule za sekondari na

maoni yao yanaoneshwa katika jedwali la sita hapo chini;

Jedwali la sita linaloonyesha changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya

wanfunzi wa shule za upili.

Changamoto Marudio Asilimia

Uelewa mdogo kwa jamii juu ya utoaji wa chakula kwa shule za 15 21

upili.

Uhaba wa maji safi na salama kwa shule za upili 20 29

Uhaba wa mvua za kutosha kwa msimu za kilimo 9 13

22
Uaminifu mdogo wa utunzaji wa chakula cha wanafunzi 16 23

Uhaba wa miundombinu na vifaa vya kupikia na jingo la kupikia 10 14

Ujumla 70 100

Asilia: Data za msingi 2019

Jedwali la sita linaonyesha kwamba wahojiwa wengi 20(29%) walisemakwamba changamoto

kumbwa ni uhaba wa maji safi na salama kwa shule za upili, wahojiwa 16(23%) walisema

kwamba kuna changamoto ya uaminifu mdogo wa utunzaji wa chakula cha wanafunzi, wahojiwa

15(21%) walisema kwamba kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa jamii juu ya utoaji wa

chakula kwa shule za upili, wahojiwa 10(14%) walisema kwamba shule za upili zinatatizwa na

uhaba wa miundombinu na vifaa vya kupikia na jingo la kupikia na wahojiwa 9(13%) walisema

kwamba kuna changamoto ya uhaba wa mvua za kutosha kwa msimu za kilimo. Jambo

linalosababisha ukosefu wa vyakula.

23
SURA YA TANO

MAJADILIANO, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

24
MAREJELEO

Fulkerson, J. (2005). School lunch and snacking patterns among high school students: associations

with school food Nutrition and Academic Performance environment and policies.

Lahey, M., Rosen, S. (2002). Dietary factors affection learning behavior. Retrieved from

http://childrensdisabilities.info.

Li, Y., Dai, Q., Jackson, J., & Zhang, J. (2008) Overweight is associated with decreased cognitive

functioning among school-age children and adolescents.

Mantep (1991), Usimamizi wa Elimu kiongozi cha mwalimu mkuu, Mantep Institute, Bagamoyo

Tanzania.

Mantep (1995), Usimamizi wa Elimu kiongozi cha mwalimu mkuu, Mantep Institute, Dar-es-

Salaam.

Mdee J.S,Shafi k,Njogu A(2013) Kamusi ya Kiswahili karne ya 21,toleo la pili, Longhorn

Publisher Ltd,Dar es salaam.

Meyer, M. (2005). Upper-elementary students’ perception of school meals. The Journal of Child

Nutrition & Management, issue 1, spring.

Mtandao wa Elimu Tanzania (2008), Juzuu ya 3 toleo la 12, www.tenmet.org, Dar-es-Salaam.

Mture Educational Publisher Ltd(2013) Sayansi kwa vitendo kitabu cha mwanafunzi darasa la

tatu, Mture Educational Publisher Ltd, Dar es salaam Tanzania .

Perry, C., & Story, M. (2003). The association of the school food environment with dietary

behaviors of young adolescents.

25
Sampson, A., Dixit, S., Meyers, A., & Houser, R. (1995). The nutritional impact of breakfast

consumption on the diets of inner-city African-American elementary school children.

Shore, S., Sachs, M., Lidicker, J., Brett, S., Wright, A., & Libonati, J. (2008). Decreased scholastic

achievement in overweight middle school students.

TUKI (2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu,Taasisi ua uchunguzi wa Kiswahili (TUKI),Dar es

salaam.

Twaweza (2014) Nini kinaendelea kwenye shule zetu?, Wananchi watafakari juu ya hali ya elimu

Tanzania,ivon Dar es salaam ,Tanzania.

Wizara ya Elimu na Utamaduni (1998), Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya shule Mwongozo kwa

shule za msingi,Wizara ya Elimu na Utamaduni, Dar-es- Salaam.

Wizara ya Elimu ya Taifa (1995), Uongozi wa Elimu katika shule za msingi, Printcare (T), Limited

Moshi Tanzania.

Wolpert, S., Wheeler, M. (2008). Food as brain medicine. UCLA Magazine Online. Retrieved

http://magazine.ucla.edu.

Zhang, J., Hebert, J., & Muldoon, M. (2005). Dietary fat intake is associated with psychosocial and

cognitive functioning of school-aged children in the United States.

26
VIAMBATISHO

KIAMBATISHO 1: HOJAJI YA WANAFUNZI

Chuo kukuu cha Bishop Stuart

Mhojiwa Mpendwa,

Ninaitwa, Byamukama John Baptist, kutoka chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara. Ninafanya

utafiti kuhusu “Mchango wa Lishe ya wanafunzi katika utendaji wao katika shule za upili

zilizoteuliwa katika Divisheni ya Kakoba wilayani Mbarara”. Naomba mchango wako kuhusu

majibu ya maswali yafuatayo na pia katika uchanganuzi huu, Mchango wako na maoni yako

yatahifadhiwa kitaaluma.

1(a) Sehemu ya A: WASIFU

Jina la mhojiwa (si lazima)...........................................................Tarehe …................................

(b) Jinsia ( jibu moja tu)

Msichana

Mvulana

(ch) Umri

14-20

21-25

Mengine (eleza) …..........................................................

(g) Kidato ………………………………………………

27
Sehemu B: Kutambulisha utendaji wa wanafunzi wa shule za upili zinazopatikana katika

tarafa ya Kakoba.

Katika shule hii, mnapewa chakula mara ngapi kwa siku?

Mara moja Mara Mbili Mara tatu

Mengine eleza zaidi………………………………………………………………..

Je ni chakula kipi munachopewa au lishwa katika shule hii?

………………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………………….

Je unafurahiya chakula mnachopewa hapa shuleni?

Ndiyo Hapana

Ikiwa unakubali eleza sababu ya jibu lako?

……………………………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………………………….

Ikiwa haukubali, eleza sababu ya jibu lako?

………………………………………………………………………………………………….…….

…………………………………………………………………………………………….………….

………………………………………………………………………………………………………..

Je wanafunzi katika shule hii wanatenda vipi kitaaluma?

28
1. Vizuri

2. Vibaya

3. Sijui

Kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lishe ya wanafunzi na utendaji bora wa wanafunzi wa

shule za upili.

Je wewe kama mwanafunzi unadhani kwamba kuna uhusiano wowote katika lishe ya wanafunzi na

utendaji wao kitaaluma?

Ndiyo Hapana

Ikiwa unakubali, eleza uhusiano uliopo baina ya lishe na utendaji kitaaluma wa wanafunzi wa

shule za upili?

………………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………………….

Ikiwa haukubali eleza sababu ya jibu lako?

…………………………………………………………………………………………………..

…………………………………………………………………………………………………..

Kujadili changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi wa shule za

upili.

Je unadhani kwamba kuna changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya

wanafunzi?

Ndiyo Hapana

29
Ikiwa unakubali, eleza changamoto zinazokabili shule za sekondari kuhusu lishe ya wanafunzi?

………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………

Ikiwa haukubali, Eleza sababu ya jibu lako?

………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………

Asante sana kwa ushirika wako.

30
31

You might also like