Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

09-06-24

ST. STEPHEN CATHOLIC CHURCH, MWIRERI


MADA YA DOMINIKA: YESU NA ROHO YA UOVU- MAADUI WAWILI
WASIOPATANA
SOMO LA KWANZA
Mwanzo 3:9-15
Nitaweka uadui kati ya uzao wako na uzao wake.
Somo katika kitabu cha Mwanzo
[Baada ya Adamu kula tunda la ule mti,] Bwana Mungu alimwita, akamwambia: Uko wapi?
Naye akaitika, "Nilisikia kishindo chako katika bustani, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi,
nikajificha." Akamwambia: Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Basi umekula tunda la ule mti
niliokukataza usile! akajibu, "Mwanamke uliyemweka kuwa mwenzi wangu ndiye aliyenipa
tunda la mti ule, nikala." Bwana Mungu akamwambia mwanamke: Umefanya nini? Naye
mwanamke akajibu, "Nyoka ndiye aliyenidanganya, nikala." Bwana Mungu akamwambia nyoka:
Kwa kuwa umefanya hayo, ulaaniwe katika wanyama wote, wa kufugwa na wanyama wote wa
mwituni; Kwa tumbo lako utatambaa, utakula uvumbi siku zote za maisha yako. Nitaweka uadui
kati yako wewe na mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake: huyo atakuponda kichwa, nawe
utamuuma kisigino cha mguu. Neno la Bwana.

ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 130:1-2 , 3-4, 5-6, 7-8 (Κ. 7)
K. Kwa Bwana kuna fadhili, kwake kuna wokovu mwingi.

Toka shimoni nakulilia, ee Bwana; / ee Bwana, uisikie sauti yangu!


Masikio yako na yasikilize
sauti ya maombi yangu. K.

Kama wewe, ee Bwana ungeweka kumbukumbu ya dhambi zetu, ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha, / ili wakutumikie kwa uchaji. K.

Ninamngoja Bwana, roho yangu inamngoja,


na ninalitumainia neno lake. / Roho yangu inamngoja Bwana kuliko walinzi waingojavyo
asubuhi. K.

Ee Israeli, umngoje Bwana. / Kwa maana kwa Bwana kuna fadhili,


kwake kuna wokovu mwingi.
Yeye ataiokoa Israeli na maovu yake yote. K.

SOMO LA PILI
2 Wakorintho 4:13-5:1
Tunasadiki, kwa hiyo tunasema.
Somo katika barua ya pili ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho
Ndugu zangu: Roho ya imani tuliyo nayo ni sawa kwetu na kwenu kama ilivyoandikwa:
"Nilisadiki, kwa hiyo nimesema." Nasi tunasadiki tukisema. Tunajua ya kuwa yeye aliyemfufua
Bwana Yesu atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka pamoja nanyi mbele yake. Hayo
yote nayavumilia kwa ajili yenu, ili kwa shukrani ya wengi zaidi neema iongezeke na kumtukuza
Mungu zaidi. Kwa hiyo hatulegei hata tukichakaa nje katika ubinadamu wetu, maana ndani yetu
tunafanywa upya siku kwa siku. Kwa maana taabu nyepesi na ya muda mfupi inatupatia utukufu
mkuu unaopita kila kiasi, sisi tusiokazia macho vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana.
Maana vinavyoonekana ni vya muda, bali visivyoonekana ni vya milele. Kwa maana tunajua ya
kwamba, hema yetu iliyo kikao chetu cha duniani inapong'olewa, tunalo jengo litokalo kwa
Mungu, ndiyo nyumba isiyofanywa kwa mikono, bali iliyo nyumba ya milele mbinguni. Neno la
Bwana.

SHANGILIO LA INJILI
Yohane 12:31-32
K. Aleluya. W. Aleluya.
K. Sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje, asema Bwana; Na baada ya kuinuliwa mimi juu
ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
W. Aleluya.

INJILI
Shetani amefika mwishoni.
Marko 3:20-35
+ Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Marko
Wakati ule: Yesu alienda nyumbani na wafuasi wake. Umati wa watu ulikusanyika tena, hata
wasipate nafasi ya kula. Jamaa zake walipopata habari, walitoka wamkamate, maana walisema,
"Amerukwa na akili." Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, "Amepagawa na
Beelzebuli, na kwa msaada wa mkuu wa pepo wabaya huwatoa pepo wabaya." Akawaita na
kuanza kuwaambia kwa mifano, "Awezaje Shetani kumtoa Shetani? Ufalme wawezaje
kusimama ukiwa umegawanyika wenyewe? Kadhalika nyumba ikiwa imegawanyika yenyewe,
nyumba hiyo haiwezi kusimama. Na kama Shetani akijipinga mwenyewe na kugawanyika,
hawezi kusimama, bali amefika mwishoni. Hakuna awezaye kuingia katika nyumba ya mwenye
nguvu na kupokonya vitu vyake, isipokuwa amemfunga kwanza yule mwenye nguvu. Hapo tu
aweza kupokonya vitu nyumbani mwake. Amin, nawaambieni, wanadamu huondolewa dhambi
zote na kufuru zao. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu, hana maondoleo hata milele, bali
atastahili hukumu ya milele." Alisema hayo kwa sababu walisema, "Ana pepo mchafu." Kisha
mama na ndugu zake walifika. Nao wakisimama nje, walituma habari kwake, kwa maana
alizungukwa na watu wengi. Basi wakamwambia, "Tazama, mama yako na ndugu zako wapo
nje, wanakutafuta." Lakini aliwajibu, "Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?"
Akawatazama wale waliomzunguka, akasema, "Hawa ni mama yangu na ndugu zangu. Kwa
maana kila afanyaye mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama
yangu." Injili ya Bwana.
THANK YOU FOR YOUR SUPPORT!

You might also like