Notes Kiswahili Iiila

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 10

SOMO LA XIII.

AINA ZINGINE ZA VIRAI

1. VIRAI VIVUMISHI

Kirai kivumishi ni kundi la maneno ambalo neno laken kuu ni kivumishi. Ifahamike
kwamba,vivumishi hukaa pembeni ya nomino ama kiwakilishi cha nomino ili
kuvifafanua.
Mifano :
-Duka lake kubwa limefungwa.
-Mashirika mengi ya Serikali yatabinafisishwa.
-watoto wake wengi walisajiriwa katika kiwanda cha chumvi
-Yule mrefu sana kuliko wengine ndiye anakimbia sana.
- Vile vyote vipya vinahitajika hapa.
-shule nyingi za kibinafsi zimefungwa na wizara ya Elimu

2. VIRAI VIELEZI

Kirai kielezi ni kirai ambacho neno lake kuu ni kielezi.

Mifano :
-Ni vizuri kuyasoma maswali vizuri sana ili kuyaelewa.
-Sherehe zilikamilika (zilimalizika) usiku wa manane.
-Watu hawa wamefika leo asubuhi.
-Tutakutana huko sokoni jioni.
N.k

3. VIRAI VIHUSISHI

Kirai kihusishi ni kundi la maneno ambalo neno kuu lake ni kihusishi.


Vihusishi ni kama vile : kwa, na, kwenye, katika,ndani,juu,chini,n.k
Mifano :
-Sitaki kulala tena kwa shangazi yangu.
-Anasoma katika kitengo cha sayansi.
-Mkate upo kwenye meza sebuleni.
-Wale wanaishi karibu na mto.
-Bama ameleta nguo za watoto.
-Hiki si chakula cha watu wakubwa.

4. VIRAI VIUNGANISHI

Kirai kiunganishi ni kundi la maneno ambalo neno kuu lake ni kiunganishi.

Mifano :
-Amechelewa shuleni kwa sababu anaishi mbali sana.
-Baba na mama pamoja na mjomba wangu wanaishi Umarekani.
-sili wala sinywi chochote kile.
-Umeharibu tena vitabu vyangu ?
N.k.
Somo la XIV. FASIHI

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa kuwasilisha ujumbe kwa hadhira (msomaji au jamii
inayonuiwa). Fasihi hutumia lugha kwa kufafanua tabia za watu na athari zake.
Kuna tofauti kati ya fasihi na sanaa. Fashi, hutumia lugha kwa kuwasilisha ujumbe.
Sana nayo hutumia vifaa kwa kuwasilisha ujumbe.

Kuna aina mbili za fasihi :


-Fasihi Simulizi (hupitishwa kwa njia ya mdomo /matamshi)
Mifano : methali, vitendawili,nyimbo,n.k
-fasihi Andishi (hupitishwa kwa njia ya maandishi)
Mifano : riwaya, hadithi fupi, tamthilia, ushairi, n.k

RIWAYA

Riwaya ni hadithi ndefu iliyoandikwa kimethali. Ni utungo, kisa au hadithi ya kubuni


inayoelezea matukio mbalimbali katika jamii.
Katika riwaya, wahusika husimulia mada iliyochaguliwa na mtunzi.

Tofauti kati ya Riwaya na Hadithi fupi ni kwamba,


-Riwaya ni ndefu kuliko hadithi fupi,
-Katika riwaya, wahusika ni wengi na wanashirikiana katika tabia na masha yao ila -katika
hadithi fupi,wahusika ni wachache sana na huwakilisha tabia na matendovya wanadamu,
-Mazingira ya riwaya ni tofauti na yake ya hadithi fupi,
-Mtiririko wa matukio ni wa moja kwa moja katika hadithi fupi,

Vijengo vya Riwaya

Katika riwaya,

-Simulizi huenda hatua kwa hatua( matukio, visa na mikasa)


-Riwaya haianzi au kukamilika kwa namna moja.

Somo la XV. AINA ZA MANENO

1. VINYUME (Antonimu)

Vinyume ni maneno ambayo huwa na maana inayopingana. Vinyume hupatikana


katika hali tofauti kama vile : vitenzi, baadhi ya vivumishi na dhana nyingine.

Mifano :

Neno Kinyume
Msichana Mvulana
Mwanaume Mwanamke
Mjomba Shangazi
Jogoo Koo
Mfalme Malikia
Nyanya/bibi Babu
Furaha Huzuni
Ubaya Uzuri/Wema
Ukubwa Udogo
Faida Hasara
Pata Kosa
Choma Chomoa
Funga Fungua
Kavu Nyevu
Kaa Simama
Chimba Chimbua
Tiifu Kaidi
Safi Chafu

2. VISAWE (Sinonimu)

Haya ni maneno yanawakilisha dhana moja. Visawe huwa na maana sawa au maana
ambayo inakaribiana.
Sinonimu ni muhima katika kuboresha uandishi wa insha kwani hukinga kurudiarudia
neno lile lile mara nyingi.

Mifano ya visawe/sinonimu :

Kizunguzungu = kizunzi
Dalili = ishara
Makini = uangalifu
Wajimu = jukumu
Wasiwasi = shaka. Wahka, tewengu
Shida = tatizo
Hasira = hamaki, ghadhabu
Aibu = soni, haya, tayahuri, izara
Goigoi = mzembe, mvivu, mpetevu
Bendera = beramu
Matata = fujo, ghasia, sokomoko, ugomvi, kimondo
Chelewa = kawia, limatia, ahirika
Gereza = jela, kizimba
Fikiri = waza, dhani, tafakari
Busara = hekima, akili, tabasuri
Mtu = mja, mwanadamu,adinasi
Mwizi = pwangu, mdokozi, pwanguzi
Rika = umri, hirimu
Ugali = sima
Udhi = kirihi

3. VITAWE ( Maneno yenye maana zaidi ya moja)


Neno moja hupewa fasiri tofauti kulingana na muktadha (mazingira ya neno) wa
matumizi.

Yapo maneno yenye maana nyingi ambazo zinahusiana na zingine ambazo hazina
uhusiano.

Mifano :
Rai :
-maoni
-sihi

Unga :
-leta pamoja
-kitu kilichosagwa
-tia viungo ndani ya chakula ili kuboresha ladha

Sita :
-namba(ri)
-babaika

Kaa :
-keti
-kipande cha kuni kilichochomwa

Vua :
-toa vazi(nguo,viatu,n.k)
-toa samaki majini
-okoa, toa kwenye matatizo

Chungu :
-isiyo tamu
-mdudu mdogo mweusi
-kifaa cha udongo cha kupikia(pot)

Ua :
-toa uhai wa kiumbe
-ugwe(kamba au waya) unaozunguka nyumba(enclos)
-sehemu ya mmea unaozaa(une fleur)

Kata :
-kifaa cha kutekea maji(ingata)
-tenganisha kitu(couper)
-sehemu ndogo kuliko tarafa(quartier)

Taka :
-hitaji,tamani
-takataka(uchafu)

Tupa :
-kifaa cha kunolea visu
-puuza
-rusha mbali

Jaa :
-furika
-mahali pa kutupa takataka(jalala)

Kinga :
-zuia
-jambo au dawa ya kujikinga na madhara
-kipande cha kuni chenye moto au kilichoungua

Nyanya :
-bibi mzaa mama/babu
-tunda la mnyanya ambalo hutumika kama kiungo.

4. VITATE

Vitate ni maneno ambayo hutatiza wakati wa kuyatamka. Maneno hayo, kwa kawaida
huundwa kwa sauti tatanishi. Sauti tatanishi hukaribiana kimatamshi.

Mifano :

Neno Kitate chake


Vua fua
Dada tata
Chali shali
Jana chana
Pata bata
Dai tai
Sima zima
Koma goma
Goti Koti
Tawa dawa
Mbishi mpishi
wasiwasi waziwazi
Ridhi rithi
Vunda funda
Tua dua

Somo la XVI. UKANUSHI

Ukanushi ni hali ama tendo la kukataa, kukana, kukiri jambo fulani.


Ukanushi unahusi, vitenzi, nyakati(hali) na nafsi.

Kwa kuzingatia neno « silabi », kuna aina mbili za vitenzi :


1. Vitenzi vya silabi moja, kwa mfano : kula, kunywa, kuja,kufa,kupa,kucha,n.k
2. Vitenzi vya silabi nyingi, kwa mfano : kuimba,kucheza,kulalamika,n.k
Ifahahamike
Lugha ya kiswahili ina nyakati kdhaa :
Wakati wa sasa(njeo ya wakati(-na-)
Wakati mtimilifu au hali timilifu(-me-)
Wakati uliopita (-li-)
Wakati ujao (-ta-)
Wakati wa mazoea (hali ya mazoea) =>hu-
Nafsi :
Mimi = > ni-
Wewe => u-
Yeye => a-
Sisi = > tu-
Ninyi/Nyinyi = > m-
Wao => wa-
Viambishi : ni-, u-, a-,tu-,m-,wa- vinaitwa Viambishi vya nafsi viambata.
Katika hali kanushi, viambishi hivyo hugeuka kama ifuatavyo :
ni-huwa si-
u- huwa hu-
a-huwa ha-
tu-huwa hatu-
m-huwa ham-
wao- huwa hawa-

1. Wakati wa sasa au wakati uliopo

Wakati wa sasa au wakati uliopo unatambulisha na kiambishi(njeo ya wakati) -na- katika


hali yakinishi(yali ya kukubali, hali ya kuthibitisha).
Katika hali kanushi, kiambishi hicho hutoweka na mwishoni mwa kitenzi huja kiishio–i kwa
vitenzi vinavyoishia kwa –a.

Mifano :

Hali yakinishi(kukubali) Hali kanushi


Mwalimu anaandika ubaoni Mwalimu haandiki ubaoni
Mti huu unaanguka sasa hivi Mti huu hauanguki sasa hivi
Sisi tunahitaji kununua viatu Sisi hatuhitaji kununua viatu
Anatuma ujumbe kwa meneja Hatumi ujumbe kwa meneja
Watoto hawa wanachukiana sana Watoto hawa hawachukiani sana
Yeye ana simu ya kifahari Yeye hana simu ya kifahari
Redio hiyi inalia sana Redio hiyi hailii sana

Fahamu vema(F.V) : Vitenzi vinavyoishia kwa irabu –u, -i, -e havichukui kiambishi cha
ukanushi –i.

Mifano :
Mtoto anaharibu nepi => mtoto haharibu nepi
Baba anasamehe mama => baba hasamehe mama
Ule upepo unarudi tena => ule upepo haurudi tena

2. Hali timilifu

Hali timilifu au wakati mtimilifu unaonyesha na kiambishi (njeo ya wakati) –me- katika
kitenzi. Kiambishi hicho hubadiliki –ja- katika hali kanushi.

Mifano :
Barabara imefungwa hivi punde => barabara haijafungwa hivi punge
Nimesahau funguo zangu => sijasahau funguo zangu
Mti umeanguka leo asubuhi => mti haujaanguka leo asububi

3. Wakati uliopita
Kiambishi ama njeo ya wakati –li- ndicho kinachotambulisha . Kiambishi hicho hugeuka na
kuwa –ku- katika hali kanushi.
Mifano :
Nilimletea pesa zako jana => sikumletea pesa zake jana
Magari haya yaligongana wiki jana => magari haya hayakugongana wiki jana
Viatu vyake vilichanika sana => viatu vyake havikuchanika sana

4. Wakati ujao

Wakati ujao unaonyesha na njeo –ta-. Katika hali kanushi ta hubaki kuwa –ta-.
Mifano :

Ratiba itapatikana kesho kutwa => ratiba haitapatikana kesho kutwa


Mama yenu atarudi mwakani => mama yenu hatarudi mwakani
Wewe utakula haya mayai => wewe hutakula haya mayai
Vitabu vyote vitaletwa na mkutubi => vitabu vyote havitaletwa na mkutubi

5. Hali ya mazoea

Hali ya mozea huonyeshwa na kiambishi ama silabi hu- mwanzoni mwa kitenzi.
Ukanushi wake hufanywa kama ule wa wakati wa sasa.

Mifano :
Wanafunzi huvaa sare za shule => wanafunzi hawavai sare za shule
Nguo za watoto huchafuka sana => nguo za watoto hazichafuki sana
Hali zingine zinastahili kukanushwa :
 Hali ya kuamuru
Mifano :
Angalieni picha hiyo kwa makini ! => msiangalie picha hiyo kwa makini !
Ondoka hapa sasa hivi ! => Usiondoke hapa sasa hivi !

 -nge-, -ngeli-, -ngali-, ndi


Mifano :

Ningekuwa na pesa ningenunua gari => nisingekuwa na pesa nisingenunua gari


Tungalimtafuta mapema tungalimpata = > tusingalimtafuta mapema hatungalimpata
Angelikunywa dawa angelipona = > asingelikunywa dawa asingelipona
Kitumbua hiki ndicho nilichopika => kitumbua hiki sicho nilichopika

 Vitenzi vya silabi moja

Mifano :
Watoto wanakula mikate => watoto hawali mikate
Wamekunywa maji machafu => hawajanywa maji machafu
Mjomba atakuja kesho asubuhi => mjomba hatakuja kesho
Ng’ombe walikula majani mengi jana => ng’ombe hawakula majani mengi jana.

 Vitenzi-jina

Mifano :
Kuchelewa kwake shuleni kulitushangaza sana => kuchelewa kwake shuleni
hakutushangaza sana.
Kulima kunanufaisha => kulima hakunufaishi

Somo la XVII. INSHA

Insha mfululizo wa sentensi zinazohusiana na mada inayozungumzwa au kuandikwa. Insha


huwa ndefu na pia fupi. Inaweza kuwa na aya moja au zaidi huku kila aya ikibeba wazo
maalumu.

Mambo muhimu katika uandishi wa insha :


- Ufasaha wa lugha
- Matumizi ya alama na vituo mbalimbali
- Mpango wa mazawo na mantiki yake
- Uzingatiaji wa kichwa cha habari na maelekezo kama yapo
- Kutotumia lugha ya mkato kama vile ktk badala ya katika
- Kuandika utangulizi unaovutia wasomaji ama wasililizaji
- Kuandika kiini cha insha kwa mpangilio unaofaa huku kila wazo likipewa aya yake
- Mawazo yote yahusiane
- Mwisho wa insha uvutie wasomaji ili waendelee kusoma
Muundo wa insha :
Insha nzuri inaweza kugawanywa katika sehemu zifuatazo :
- Kichwa cha insha : huandikwa kwa herufi kubwa katikati au juu ya insha. Huandikwa
kwa ufasaha na kwa muhtasari. Hakizidi maneno matano na huzingatia wazoo kuu la
insha

- Mwanzo wa insha : huzingatia fasili ya jambo linalozungumzwa, uhusiano wake na vitu


vingine na muhtasari wa insha inayotungwa. Kwa kawaida, mwanzo hauzidi aya moja.

- Kiini cha insha : hii ni sehemu kuu ya insha. Mawazo hupangwa kwa mtiririko sahihi.

- Mwisho wa insha : hutoa mawazo yanayojadiliwa. Huwa na msimamo, maoni, kauli na


mapendekezo ya mwandishi kuhusu jambo lililotungiwa insha. Kwa ufupi, huonyesha
mhutasari au hitimisho.

Kuna aina tatu za insha

 Insha ya wasifu : hueleza sifa za watu, na vitu kama vile wanyama, majengo, milima, mahali
fulani, n.k
 Insha ya kisanaa : huwa na lugha yenye mvuto na misemo kama vile nahau, methali,
tamthilia za semi
 Insha ya hoja : huletea mawazo ya aina fulani na kupinga mawazo mengine kwa uthibitisho
ulio dhahiri.

Somo la XVIII. AINA ZA SENTENSI KIDHAMIRA

Kumbusho :
Sentensi ni utungo au kundi la maneno ambalo hueleza dhana (maana) iliyokamiliko. Sentensi
ni kundi la maneno ambalo lina muundo wa kiima na kiarifu na ambalo huleta maana kamili.

Zifuatazo ni aina za sentensi kidhamira :

1. Sentensi za taarifa : sentensi hizi hutoa taarifa tena huishia kwa nukta.

Mifano :
Dada yangu ameumwa maleria.
Darasa letu lina wanafunzi wachache kuliko mengine.
Tunasoma Kiswahili kwa vipindi vinne.
Mama yangu hawezi kuosha vyombo.

2. Sentensi ulizi : hizi huuliza swali kuhusu jambo fulani. na huishia na alama ya kuuliza.
Mifano :
-Watu hawa wanahitaji nini ?
-Miti hiyi iliangukaje ?
-Kwa nini unachelewa kila asubuhi kazini ?

3. Sentensi agizi : sentensi agizi hutoa amri na huishia kwa alama ya hisi (alama ya
kushangaa.
Mifano :
-Nenda taratibu usianguke !
-Kaeni wawili wawili !
-Ondoa uchafu huo haraka haraka !
-Andika maswali hayo katika madaftari yenu

4. Sentensi hisihi : Hizi ni sentensi ambazo huonyesha hisia kama vile huzuni, uchukivu,
mshangao, n.k
Mifano :
-Ajabu ! Tarafa nzima kukosa zahanati !
-Lo ! Bikizee kaendesha gari kweli !

5. Sentensi za masharti : katika sentensi hizi, kuna masharti. Yaani jambo fulani ni lazima
litimizwe ili mafanikio yapatikane.
Mifano :
-Kama mvua ingenyesha mapema mavuno yangekuwa mengi
-Ningekuwa na pesa ningenunua gari la kifahari.
-Ukifika mapema tutaondoka pamoja.

Kumbusho :

Kuna aina nyingine za sentensi kimuundo ambazo ni :


-sentensi sahili
-sentensi ambatano
-sentensi changamano

You might also like