Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Aina za Biashara.

Kwa kuzingatia maana ya biashara ambayo tumezungumzia hapo awali, ni dhahiri


kwamba biashara zimegawanyika katika maeneo tofauti ila katika kitabu hiki
nitakueleza maeneo mawili muhimu ambayo ni.

 Biashara ya kuuza bidhaa


 Biashara ya kutoa huduma
Kwa kuzingatia haya maeneo muhimu, tambua biashara pia imegawanyika katika
sehemu tofauti ambayo wewe kama mfanyabiashara utachagua eneo gani la
biashara litakufaa zaidi na utaweza kulimudu.

i. Kuuza bidhaa

Hii ni biashara ambayo mfanyabiashara atajikita katika kuuza bidhaa ambazo


tayari zinakuwa zimezalishwa na zipo tayari kwa ajili ya matumizi, asilimia kubwa
ya biashara nyingi zinazofanyika ni biashara za nguo, simu, bidhaa za chakula n.k

Bei za bidhaa hizi kwa asilimia kubwa huwa ni ngumu kupangwa na muuzaji
mwenyewe kwa sababu bei ya bidhaa inapangwa na soko husika. Hii ni matokeo
ya uwepo wa wafanyabiashara wengi katika soko moja wenye bidhaa
zinazofanana.

Uuzaji wa bidhaa haubagui mtaji, uwe na mtaji mdogo au mtaji mkubwa unaweza
kufanya shughuli hizi.

ii. Kilimo na Ufugaji

Kilimo biashara ni kilimo ambacho kinafanywa kwa kiwango kikubwa mfano


mashamba makubwa ya mahindi, mpunga n.k kwa asilimia kubwa ni kwa ajili ya
biashara. Biashara ya kilimo inahitaji uelewa kuhusu kilimo na kupata ushauri
kutoka kwa wataalamu.

Kilimo biashara kinahitaji mitaji mikubwa ya kuendesha shuhuli za kilimo, kwa


hapa Tanzania kuna mikoa mitano ambayo inajulikana kwa kuilisha Tanzania
yaani ni mikoa inayozalisha chakula kwa kiasi kikubwa mikoa hiyo ni Ruvuma,
Mbeya, Iringa, Morogoro.

Hivyo basi kwa wakulima wakubwa wanaotaka kufanya kilimo biashara ni vizuri
kufikia katika hayo maeneo kwa uzalishaji mkubwa wa mazao.

iii. Utoaji wa huduma.

Hii ni aina nyingine ya biashara ambayo mfanyabiashara hatausika na utoaji wa


bidhaa ila atajikita na utoaji wa huduma mfano ushauri, msaada.

Kwa kutumia elimu yake kutaleta chachu ya kutoa mwanga katika maeneo tofauti,
lakini cha kuzingatia ni kwamba yote unayofanya ni kwa sababu ya kutoa
suluhisho kuhusu magumu au changamoto wanazopitia watu au makampuni

Imeandaliwa na Paul Makubi (Pro Business Consultant)


0743028952

You might also like