Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

THE INSTITUTE OF ADULT EDUCATION

P.O. BOX 162 Karagwe, Kagera,Tanzania ;


Contact : Office-0784543156,0767586763.
KARAGWE

Tarehe…………………..
JINA LA MWANAFUNZI……………………………………………………………………
YAH: KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (STAGE I) YENYE
KIDATO CHA KWANZA NA CHA PILI KATIKA SHULE YA SK OPEN SCHOOL 2024.

UTANGULIZI
Uongozi wa shule pamoja na jumuiya ya shule ya sekondari SK Open school chini ya Institute of
Adult Education (IAE) wanayo furaha kukupongeza na kukufahamisha kuwa umechaguliwa kujiunga na
elimu ya sekondari kidato cha kwanza na cha pili kwa mwaka mmoja. Mwanafunzi atasasoma na kupata
cheti cha kidato cha Nne na sita (Form IV & Form VI). Mgawanyiko wa mafunzo ni kuanzia (Kidato
cha I na II) kwa mwaka mmoja,kidato cha III na IV kwa mwaka mmoja, na kidato cha V na VI kwa
mwaka mmoja. Pia tunapokea wanafunzi wenye haja ya kurudia Mtihani wa QT, kidato cha Nne na
kidato cha Sita (Re- sitters).
SK Open school inapatikana mkoa wa Kagera, wilaya ya Karagwe, kata ya Bugene, eneo la
Omurushaka karibu na stendi ya magari yaendayo Bushangaro.

QT (QUALIFYING TEST) maana yake ni mafunzo ya kidato cha kwanza na cha pili, Mwanafunzi
atapatiwa mafunzo hayo kwa muda wa mwaka mmoja na kupata sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha
Nne. Kwa hiyo mfumo wa kusoma kupitia QT ni mzuri sana hasa kwa wale waliokosa nafasi katika
shule za serikari.

RATIBA YA VIPINDI KWA KIDATO CHA KWANZA

Ratiba ya masomo imegawanyika katika sehemu mbili, masomo ya asubuhi na jioni.

MASOMO YATAKAYO FUNDISHWA.

Kwa mwaka wa masomo wa 2024 masomo yatakayo fundishwa ni ya mchepuo wa Sanaa (Arts)
Sayansi,Kompyuta.

MASOMO YA ASUBUHI:

Muda wa vipindi ni Saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana

MASOMO YA JIONI:

Muda wa vipindi ni Saa 8:30 jioni hadi saa 01:00 Jioni Baada ya vipindi vya darasani Mwanafunzi
anaruhusiwa kubaki na kuendelea kujisomea, pia anaweza kupata msaada wa Mwalimu pindi
unapohitajika .Ratiba ya masomo inaweza kubadilika kwa kuongeza muda wa vipindi usiozidi saa moja
au masaa mawili hasa inapokaribia kipindi cha mtihani wa Taifa.

Page 1
KUSAJILIWA KWA MWANAFUNZI:

Ili mwanafunzi asajiliwe na kupewa kitambulisho cha shule, sharti ahudhurie mafunzo ya semina ya
siku moja itakayofanyika shuleni kwa lengo la kumwezesha mwanafunzi kujitambua na kuyatambua
vyema mazingira yake pamoja na kuelekezwa na kushauriwa jinsi ya kuchagua masomo ya kufanyia
mitihani ili Mwanafunzi aweze kutimiza ndoto zake. Utaratibu wa semina utatolewa kwa mwanafunzi
pindi atakapomaliza kufanya malipo yote kama utaratibu unavyoeleza. Mafunzo yatafanyika kwa
wanafunzi wote watakaojiunga kwa kipindi cha January na February MAFUNZO HAYA NI BURE,
HAKUNA MALIPO.

I. ADA, CHAKULA NA MALAZI (BWENI) YA MASOMO KWA WANAFUNZI WA


KIDATO CHA KWANZA NA CHA PILI KWA MWAKA MMOJA.

MAHITAJI MUDA GHARAMA

ADA AWAMU YA KWANZA JANUARI- MARCHI 150,000/=


ADA AWAMU YA PILI
AWAMU YA KWANZA

FGGGGGGGGGGJHJJJ
APRIL - JULAI 180,000/=
ADA AWAMU YA TATU
AGOSTI - NOVEMBA 150,000/=

JUMLA KWA MWAKA 480,000/=

KUMBUKA: kila mwanafunzi atatakiwa kuja na mahindi kiasi cha kgs 156 kwa mwaka mzima na
maharage kgs 60 kwa mwaka.

Awamu ya kwanza ataleta kgs 70 za mahindi na maharage kgs 30 mengine atamalizia awamu ya
mwezi wa saba.

MCHANGANUO WA MALIPO YA USAJILI:

 Kitambulisho cha Mwanafunzi Tsh.10,000/= (shilingi elfu kumi tu)


 malipo haya ya usajili yanapaswa kuwa ya kwanza Mapema kabla ya kuanza masomo,
Mwanafunzi asipolipa hatosajiliwa na asiposajiliwa hatoruhusiwa kuingia ndani ya shule.
(Mwanafunzi aliyesajiliwa lazima awe na kitamblisho cha shule)
 Malipo ya usajili kwa Wanafunzi Watakaojiunga kuanzia mwezi January hadi April
Tsh.25,000/=

Utaratibu wa kulipa ada ya muhula wa januari hadi juni 2024 kwa awamu ni kama ilivyo hapa
chini:

1) Malipo ya kuanzia yasiwe chini ya Tsh.120,000/= ( Shilingi laki m o j a na ishirini)

2) Kufikia mwezi Machi tarehe 30, kila mwanafunzi anapaswa awe amekamilisha malipo yote ya
awamu ya kwanza Januari hadi Machi.

MALIPO YA MTIHANI WA UTIMILIFU (MOCK) TAASISI YA ELIMU

 Mwanafunzi wa form II Tsh25,000/-(shillingi elfu ishirini na tano tu)


 Matibabu Tsh.20,000/= kwa mwaka au aje na Bima ya afya.

Page 2
MALIPO YA SARE ZA SHULE/UNFORM:

 Tishet 1 Tsh. 10,000/=


 Sweta Tsh.15000/=
 Sketi Rangi Nyeusi
 Suruali kwa( wavulana) Rangi Nyeusi
 Shati Rangi nyeupe(mikono mifupi wote)
 Viatu vyeusi Kisigino kifupi
 Track Rangi ya blue(kwa ajili ya michezo)

NB:

 Kwa wasichana wanaopenda kuvaa ijabu nyeupe wanaruhusiwa kuvaa shati nyeupe zenye mikono
mirefu.

MAHITAJI MENGINE YA MWANAFUNZI:

1. Madaftari ya kutosha na kalamu


2. Rimu 1 A4.
3. Aje na Cheti cha kuzaliwa kama hana atalipia kiasi cha sh. 20,000/= na kupatiwa shuleni.
4. Kamusi ya kiingereza kwa Kiswahili au kiingereza kwa kiingereza.
5. Godoro ndogo mita 2.5x3 (hata kama limetumika)
6. Kikombe cha mfupa
7. Sahani1 moja ya mfupa,Bakuli naKijiko
8. Ndoo mbili ndogo
9. Mashuka jozi 2 (Bluu bahari kwa wavulana) na (pink kwa wasichana).
10. Blanketi 1
11. Taulo na kanga pair 1.(wasichana)
12. Chandarua
13. Kandambili
14. Sabuni za kufulia na kuogea za kutosha muhula.
15. Mswaki.
16. Dawa ya meno
17. Pads kwa wanafunzi wa kike

SHERIA ZA SHULE/SCHOOL REGULATIONS:

1. Lugha ya mawasiliano ni kiingereza, Hairuhusiwi kuzungumza Kiswahili au kusoma magazeti,


majarida au machapisho yoyote ya Kiswahili (isipokua kwa somo la Kiswahili) katika eneo la
shule.
2. Kila mwanafunzi ni lazima awe na kitambulisho cha shule na avae shingoni muda wote, Ikiwa
mwanafunzia amepoteza kitambulisho atapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi kisha alipie shuleni
Tsh.10, 000/= ili apatiwe kingine.
3. Ni lazima kila mwanafunzi kuhudhuria vipindi vya dini kulingana na dini yake.

Page 3
Sheria za mavazi

i. Mavazi yasiyo ya heshima hayaruhusiwi mfano suruali kwa wanawake, sketi fupi juu ya
magoti, nguo zina zoonyesha maungo ya mwili, kufunga vilemba kichwani.
ii. Hairuhusiwi kuvaa hereni, kuvaa kikuku miguuni, mikufu na kuvaa kaptura kwa
wavulana nk.
iii. Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa malapa au viatu vya wazi (open shoes). Mwanafunzi
akiwa na tatizo la mguu atapewa kibali maalumu na uongozi wa shule.
iv. Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa kofia ya aina yoyote katika eneo la shule, kama kuna
sababu ya kumlazimu kuvaa kofia atapewa ruhusa na uongozi wa shule

a) Hairuhusiwi kuvaaa vilemba au ijabu za rangi nyingine tofauti na nyeupe. Ikiwa


mwanafunzi anasababu ya kumfanya afunge kilemba atapewa kibali na mkuu wa
shule.
b) Hairuhusuwi kusuka rasta bali wanaweza kunyoa au kusuka mistari ya kawaida
ya kutoka mbele kurudi nyuma.
c) Kuvaa hereni haitakiwi
d) Hairuhusiwi kuvaa mikufu (Neckless)
4. Wanafunzi wanatakiwa kunyoa nywele katika uwiano (size) moja, baadhi ya aina za unyoaji
kama vile kunyoa nusu kichwa (kiduku) hairuhusiwi. Pia hairuhusiwi kwa wavulana kuweka
dawa kwenye nywele, Wanafunzi wote wanaoingia vipindi vya asubuhi hawapaswi kupaka
nywele zao rangi
5. Mwanafunzi anatakiwa kuwahi shuleni na kukaa kwa utulivu darasani. Hairuhusiwi mwanafunzi
kuwa nje ya darasa bila ruhusa ya mwalimu wakati wa vipindi vinaendelea.
6. Kutii na kuwaheshimu walimu na viongozi wote wa wanafunzi.
7. Mwanafunzi anaposhindwa kufika shuleni kwa sababu ya ugonjwa au sababu nyinginezo,
anapaswa kutoa taarifa ya maandishi kwa uongozi wa shule.
8. Unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara, bangi, utumiaji wa dawa za kulevya, wizi wa aina yoyote
havitakiwi.
9. Ni marufuku kupigana na kutumia lugha chafu au kuandika maandishi yenye lugha chafu ubaoni
au kuandika maandishi yoyote kwenye viti au meza nk.
10. Mwanafunzi haruhusiwi kuingia darasani na chakula/vitafunwa (bites) au vinywaji kama soda au
juice.
11. Mwanafunzi anatakiwa kuomba ruhusa ikiwa anataka kutoka nje ya shule wakati masomo
yanaendelea.
12. Ni lazima kila mwanafunzi afanye mazoezi yote atakayopewa na mwalimu darasani,pamoja na
mitihani yote itakayotolewa na shule.
13. Mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanafunzi na Mwanafunzi au mwanafunzi na mwalimu au na
mfanyakazi yeyote wa shule ni marufuku kabisa.
14. Hairuhusiwi kubeba au kuweka spika za simu masikioni (earphone) pamoja na kutumia simu
darasani.
15. Ni lazima mwanafunzi atii na kufuata sheria zote zilizoorodheshwa hapo juu na zile nyingine
atakazoendelea kupewa pindi awapo shuleni.

Page 4
NB:/ANGALIZO: ukurasa huu ujazwe na kusahiniwa kati ya mwanafunzi na mzazi kurudishwa
shuleni.

Uvunjifu wa sheria mojawapo kati ya hizo zilizoorodheshwa hapo juu, zitamweka Mwanafunzi
kwenye hatari ya kufukuzwa shule. Ikiwa mwanafunzi atafukuzwa, ada iliyokwisha lipwa
haitarudishwa.

Mimi ......................................................................................... nimesoma na nimekubaliana na utaratibu


wote wa shule na nimeamua kwa dhati kujiunga na masomo katika shule hii na kwamba nitatii masharti
yote.

SEHEMU A

1. Jina kamili la mwanafunzi (kama ilivyoandikwa katika mtihani wa taifa wa darasa la


saba)
………………………………………………………………………………………………………………

2. Tarehe ya kuzaliwa: …………………….………………………………………………………….


3. Mtaaa / Mahali anapoishi: .......................................................Wilaya:
…………………………………….mkoa……………………………………
4. Anwani ya Familia:
………………………………………………………………………………………………………….........
b) Dini: ………………………………………………………………
6. Hali ya Familia: - (Weka alama ya vema 
ndani ya kisanduku.)Nina wazazi wote wawili
Nina mama pekee

Nina baba pekee Mimi ni yatima


Ninatunzwa na ndugu zangu

7. Hali ya Afya: ( Weka alama ya vema  ndani ya kisanduku; kama alama hiyo
imewekwa katika kisanduku chochote, maelekezo yatolewe katika sehemu au
nafasi ambayo imeachwa hapo chini )
1) Ulemavu au mapungufu yanayohitaji uangalifu au maelewano

2) Nina mzio (allergy)

3) Nina ugonjwa usiotibika ambao unahitaji kutibiwa mara kwa mara


4) Maelezo:
………………………………………………………………………………………………………………..................
....................................................................................................................................
....................................................................................................................................
....................................................................................................................................
....................................................................................................................................

Page 5
…………………………………. ……………………………

Sahihi Tarehe

SEHEMU B

1. Jina la Baba/Mlezi:.............................................................. Namba ya simu:


……………………………
2. Kazi: ……………………………………………………………………………………..
3. Jina la Mama/Mlezi ............................................................ Namba ya simu
……………………………..
4. Kazi: ……………………………………………………………………………………..
5. Namba nyingine ya simu kwa mawasiliano ................................ Uhusiano:
………………………………
6. Ahadi ya Mzazi/Mlezi
a) Nakubali kumlipia karo (ada) ya shule na kumpa mahitaji
mengine yanayohitajika shuleni mwanzoni mwa kila
muhula, ili asiache masomo na kufuata hivyo vifaa
nyumbani.

Sahihi: …………………………. Tarehe: …………………………………..

(Kwa matumizi ya ofisi tu)

Jina la mpokeaji wa form hii au kwa niaba

Jina: …………………………….… Saini……………………Tarehe………………………

Page 6

You might also like