Form 2 Mid 2023

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 1

a) Tunga sentensi kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kibainishi/ritifaa.

(Alama 2)

b) Ainisha maneno katika sentensi hii; (Alama 4)


Mgomba mrefu zaidi ulikatiwa ng'ombe.
c) Andika sentensi ifuatayo katika wingi: (Alama 2)
Seremala aliulainisha ubao huo ili kutengeneza kasha wamuuzie mlinzi huyo.
d) Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa; (Alama 2)
Mtu huyo alifuata njia hiyo iliyomwelekeza mjini.
e) I) Eleza maana ya mofimu. (Alama 1)
II)Ainisha mofimu katika sentensi; (Alama 4)
Nilimsomea.
f) Tumia neno “Panda” katika sentensi kama: (Alama 2)
i) Kitenzi
ii) Kivumishi
g) Tunga sentensi mbili kutumia Visawe vya maneno yafuatayo; (Alama 4)
a) Doa.
b) Omba.
h) Tunga sentensi kuonyesha ngeli zifuatazo; (Alama 4)
1) A-WA.
2) U-I.
i) Sahihisha sentensi ifuatayo kisha uandike katika wingi; (Alama 2)
j) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi; (Alama 3)
Mtaalamu alisema kwamba alifahamu Chandon cha uvimbe aliokuwanao.
k) Onyesha shadda katika maneno yafuatayo; (Alama 2)
i) Walakini.
ii) Haraka.
l) Kanusha sentensi ifuatayo; (Alama 2)
Waziri atafungua maonyesho.
m) Andika sentensi ifuatayo upya katika kauli ya kutendwa; (Alama 2)
Serikali imetoa ripoti kuhusu kashfa ya mafuta.
n) Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii; (Alama 2)
Kariuki alipigiwa mpira.
o) Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno “kaa”. (Alama 2)

ISIMU JAMII. (ALAMA 20)

a) Ni nini maana ya is tilapia zifuatazo; (Alama 4)


i) Isimu jamii.
ii) Lugha
iii) Sajili
iv) Dhima.
b) Umri ni mojawapo wa kaida zinazotawala matumizi ya lugha. Eleza zingine nne. (Alama 8)
c) Taja na ufafanue sifa nne za lugha ya vijana/mtaani. (Alama 8)

You might also like