Maswali Ya Mapambazuko Ya Machweo

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 27

MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE

Swali 1
Kifo cha Suluhu maswali na majibu
...iwapo penzi hili litatia doa,basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu
kama jongoo na mti wake..."

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)


b. Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (alama 4)
c. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
d. Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alama 6)

Majibu

"...iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu
kama )ongoo na mti wake...

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)


 Haya ni maneno ya Suluhu kwa Abigael kama yanavyokumbukwa na
Abigael. Walikuwa katika chumba walichozoea kwenda kuzituliza nafsi
zao wakiwa na Suluhu. Aliyakumbuka maneno haya wakati alikuwa
amekwisha kichomoa kisu kwenye mfuko alionunuliwa na Suluu huku
akitaka kumuua.
b. Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (alama 4)

i. Nahau - tia doa.


ii. Tashbihi - kulitupa penzi langu kama jongoo na mti wake.
c. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)

 'Ni muasherati - japo ana mke ana wapenzi wa kando kama Abigael.
 'Ni katili alifikiria namna ya kumuangamiza mkewe abaki na Abigael.
 'Ni msaliti - anaisaliti familia yake kwa kuitelekeza.
 .Ni mlezi mbaya- anamwachia mkewe Bi. Suluhu mzigo wa kuwalea
watoto wao na kumwambia ni wake pekee.
 .Ni kiongozi mbaya - haleti maendeleo katika eneobunge lake kw alitumia
pesa za umma kuwalipa mabinti wa Chuo kikuu kwa kula uroda nao.
d. EIeza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alam 6)
 Msemewa ni Abigael.
 Kupitia kwa Abigael tunaonyeshwa namna Bw. Suluhu alivyokuwa
ameoza kitabia kwa kula uroda na mabinti wa Chuo kikuu.
 Kupitia kwa Abigael tunajua kuwa Bwana Suluhu alikuwa tajiri mwenye
mali na pesa nyingi zilizosababisha utovu wa amani kwa mkewe.
 Kupitia kwa Abigael kuisoma barua ya Bi. Suluhu tunajua kuwa Bwana
Suluhu alikuwa ameitelekeza familia yake na kumtwika Bi. Suluhu mzigo
wa kuwalea wanawe.
 Kupitia kwa barua aliyoisoma Abigael, tunajua kuwa Bwana Suluhu
alinyakua shamba la mamake Abigael na kumuua.
 Kupitia kwa Abigael kuisoma barua ya Bi. Suluhu kwa bwanake tunajua
Suluhu alikuwa na nakama.
 KupitiakwaAbigael tunaonyeshwabaadhiyamatatizoyanayowakumba
wanafunzi wa Chuo kikuu kama ukosefu wa chakula, uozo wa jamii,
utegemezi n.k.

Swali 2
Sabina maswali na majibu
Swala la elimu limepewa kipaumbele katika hadithi ya Sabina. Jadili (alama 20)

Majibu

 Sabina ni mwanafunzi wa darasa la none. Jumapili ya mwisho kabla ya Elimu


mtihanai wa kitaifa, Sabina anaonekana mwenye hisia mseto moyoni. (uk. 34)
 Anawaza kuhusu mtihani huo ambao iwapo angepita ungemwezesha kupata
ufadhili katika Shule ya upiti ya bweni. (uk. 34)
 Anawaza vilevile, iwapo angefeli mtihani huo, hatima yake ingekuwa ipi? (Uk.
34)
 Sabina anakumbuka maneno ya mwalimu mkuu kuwa mizizi ya elimu ni chungu
ila matunda yake ni matamu. (uk. 34)
 Kauli ya mwalimu mkuu pia inashauri kuwa ikiwa mtu anataka kuonja
matunda ya elimu lazima atie bidii. (uk. 34)
 Sekta ya elimu inakumbwa na changamoto mbalimbali kwa mfano mimba za
mapema. Nyaboke - mamake Sabina- alimzaa akiwa kidato cha pili. (Uk. 35)
 Changamoto nyingine ni kuacha Shule kabla ya kuhitimisha kiwango fulani.
Nyaboke anapojifungua anakatiza masomo yake ili kuanza ulezi. (uk. 35)
 Vilevile baadhi ya desturi potovu za jamii kama kuwaoza wanao mapema
huweza kukatiza masomo ya watoto. (uk. 39)
 Elimu huwahakikishia watu mustakabali mwema maishani. Wazazi wake
Nyaboke wanakata tamaa ya maisha mazuri kwa sababu mwanao
waliomtegemea kusoma hadi Chuo kikuu anakomea kidato cha pili. (uk. 35)
 Binamu yake Sabina, Mike, anasomea katika Shule ya msingi ya bweni. Alizoea
kubeba vitabu vya kudurusu ambavyo walidurusu na Sabina wakiwa katika kazi
yao ya uchungaji. Hii inaashiria tamaa yao ya kutafuta elimu. (Uk. 36)
 Werevu wa Sabina haukutiwa doa na hali yake ya ujakazi. Kila muhula aliibuka
wa kwanza darasani kana kwamba nafasi hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili
yake.
 Mwalimu mkuu anawahutubia watahiniwa ukumbini kama sehemu ya
maandalizi kabla ya mtihani wa kitaifa. (uk. 37)
 Majukumu mengi nyumbani wanayopewa watoto hueza kutatiza masomo yao.
Kazi ya kuuza maziwa inamfanya Sabina kuchelewa shuleni mara
 Wanahabari wanamtafuta Sabina hadi nyumbani kwao ili kumhoji kwa kufanya
vyema katika mtihani. Anaibuka mwanafunzi wa nane bora nchini. (uk. 39)
 Kufanya vyema katika mtihani kunafanya kila mtu kujinasibisha na Sabina
akiwemo Yunuke na Ombati. (uk. 40)

Swali 3
Fadhila za Punda maswali na majibu

“Isije ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mlango;
itakuwa balaa bin beluwa”
i. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4)
ii. Jadili umuhimu wa mwenye nyumba anayerejelea (ala 6)
iii. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji. Thibitisha ( ala 10)

Majibu

“Isije Ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mpangaji
itakuwa balaa bin beluwa.”

i. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)


 Maneno ya msimulizi
 Anarejelea Lilia
 Lilia alikuwa nyumbani
 Lilia anamngojea mumewe Luka huku akiwa na mawazo mengi kutoka
mateso ambayo amepitia kutoka kwa Luka.
ii. Jadili umuhimu wa mwenye nyuMba anayerejelea. (alama 6)
 Anabainisha maudhui ya unyanyasaji wa kijinsia – Luka anamchapa
Lilia.
 Anaendeleza maudhui ya uongozi mbaya kwa kutotimiza ahadi alizowapa
wananchi.
 Pia anachimuza maudhui ya usaliti kwani analiuza kanisa aliloachiwa na
babamkwe Lee Imani.
 Pia anaendeleza maudhui ya elimu kwa kuwa yeye na mkewe Lilia
wanasoma katika chuo kimoja.
 Anaendeleza maudhui ya ukandamizaji hasa katika kituo cha polisi. Ana
marafiki kituoni wanaomjuza kuhusu kwenda kwa mkewe pale.
 Ni kielelezo cha wanaume katili licha ya mkewe kuwa na ujauzito, Luka
anataka waandamane naye katika siasa.
 Ni kiwakilishi cha viongozi wanaotumia mamlaka yao vizivyo. Baada ya
kuwa gavana anasema kuwa ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na
batili kuwa haki.
(zozote 6 x 1)
iii. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji.Thibitisha.
 Ana mawazo na wasiwasi – mumewe harejei nyumbani.
 Kutusiwa na mumewe anamfananisha na nguruwe anapokataa
kuandamana naye katika siasa.
 Anakanwa na mumewe kuwa akiwa kazini yeye si mumewe.
 Kupigwa – Luka anampiga Lilia si mara moja tu. Anamshika nywele na
kumbururura, anapopigwa teke tumboni….
 Kuharibikia kwa mimba – Mimba yake inaharibika na hili linamliza
sana.
 Anakatazwa kufika ofisini.
 Ana hofu ya kutochukua simu inapopigwa.
 Wakati alipigwa na kuanguka chini, alikuwa anashindwa ampigie nani.
 Baada ya kufiwa na wazazi wote anahisi hana mtetezi.
 Lilia alikuwa na wasiwasi wakati Luka aliingia kanisani na kuketi karibu
naye.
 Alikuwa na wasiwasi kwa wale waliomtembelea Luka hospitalini kwani
hakukuwa na jamaa yeyote.
 Lilia alikuwa na wasiwasi kuhusu yule mgonjwa,”Luka’ aliyetambulika
na mamamkwe lakini yeye hakumjua.
(zozote 10 x1)

Swali 4
Msiba wa Kujitakia Maswali na Majibu

a. Machoka alikumbuka kauli ya jirani yake, Zuhura, aliyeishi kumkumbusha, “wetu ni


wetu, hata akiwa mbaya … wetu. Hatuna budi ila kumchagua yeye. Lisilobudi hubidi.
Awe amesoma ama hajasoma, angali wetu.”leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa
anajutia kumchagua huyo wetu.

Kwa muda mrefu, Machoka na Zuhura walikuwa kama fahali wawili hawakai katika
zizi moja. Kisa na maana, ni wafuasi wa watu wawili tofauti. Leo hii kinachowaleta
pamoja Machoka na Zuhura ni udhikinifu, hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei za
bidhaa muhimu na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali hiyo hiyo ya ‘watu
wao’. Zuhura alisuta nafsi yake.

Alikuwa akiitazamia nchi nzuri na maisha bora baada ya uchaguzi. Alitazamia ‘watu
wake’ wangezitimiza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni zao. Leo hii imebakia
kujuta. Kujuta ghya ya kujuta! Tayari alikuwa amekwishafanya kosa. Kosa ambalo
alifahamu lilikuwa la kujitakia. Ulikuwa mwiba wa kujidunga usiokuwa na kilio wala
kuambiwa pole. Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza kuzoleka…”
Chambua maudhui katika dondoo hili. (ala 12)
b. Eleza sababu nne zinazochangia jimbo la Matopeni kutoshuhudia maendeleo ya
kisiasa tangu nchi kupata uhuru . (ala 8)

Majibu

a. Maudhui katika dondoo


 Mgogoro- Machoka na Zuhura walikuwa fahali wawili hawakai zizi
moja.
 Ukabila – “Wetu ni wetu, ata akiwa mbaya….wetu.
 Umoja – Leo hii kinachowaleta pamoja Machoka na Zuhura ni
udhikinifu, hali ngumu ya maisha.
 Hali ngumu ya masiha – mfururiko wa bei za bidhaa muhimu na kutozwa
ushuru wa kiwango cha juu.
 Majuto – Leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa anajutia kumchagua
huyo wetu.
 Utamaushi – Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza
kuzoleka…
 Usaliti- waliochaguliwa kama watu wao walikosa kuendeleza uongozi
wenye manufaa.
 Unafiki – Ahadi zilizotolewa kwa kampeni hazikutimizwa.
(zozote 6 x 2)
b. Sababu za matopeni kutoshuhudia maendeleo.
 Usaliti – Jimbo la Matopeni linawachagua viongozi kwa matumaini ya
kuboresha maisha ya wananchi.
 Viongozi wanapochagulia wanatupikia mbali ahadi walizotoa kama vile
kuimarisha sekta ya afya, kutengeneza barabara, kuimarisha ukulima
n.k.
 Ukabila na unasaba- Wakati wa kampeni Zuhura anamwambia Machoka
kuwa wanastahili kumchagua mtu wao. Matopeni imetawaliwa na familia
moja; Sugu Senior na Sugu Junior.
 Ujinga – kutoshuhudia maendeleo ndiyo malipo ya kumpigia kura
kiongozi kwa kutumia matumbo yao badala ya akili.
 Ufisadi – Wanamatopeni wanawachagua viongozi kwa sababu wakati wa
kampeni, wanaowania wanawanunulia unga, khanga, sukari na mafuta.
 Viongozi kuendeleza udikteta na ukoloni mamboleo. Kahindi Mlalama
anadai kuwa vizingiti hivi haviishi daima matopeni licha ya kuwa bado
wana ndoto ya kesho njema.
 Ubadhirifu wa mali ya umma, mali ya umma inayotumiwa kugharamia
safari za ndege za viongozi wa majimbo jirani.
 Utabaka – Viongozi kwenye hafla ya kuapisha Sugu Junior wameketi
vyema kwenye hema zilizotandikwa vyema, ilhali wananchi wameketi
kwenye jua kali.
 Uvunjaji wa sheria- kupiga kura si kazi, kazi ni kuhesabu kura.
 Wanasiasa kukosa sera za kimaendeleo.
 Wananchi kutuwazia sera za wanasiasa.
 Propaganda – Wananchi kushindwa kufikiria ahadi za wanasiasa.
(zozote 8 x 1)

Swali 5
Msiba wa Kujitakia Maswali na Majibu

a. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)


"Jimbo la matopeni lilikuwa limegeuzwa ngome ya watu fulani binafsi. Watu wenye
ushawishi mkubwa serikalini! Watu wasiojali maisha ya wapiga kura kama Machoka
na Zuhura. Wapiga kura walioamka siku hiyo asubuhi ya majogoo, wakastahimili
baridi kali ya bukrata. Wakavumilia jua kali la mchana. Zuhura alikumbuka namna
yeye na wenzake walivyotunga foleni ndefu kwenye vituo vya kupigia kura. Yote
haya wakiwa na matumaini ya maisha bora ya baadaye, si bora maisha! Kumbe
wajinga ndio waliwao! Mzigo mzito wa maisha haukuwatisha wala kuwakosesha
usingizi viongozi wao. Ama kweli, mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi. "
b. Onyesha namna wanamatopeni wanavyokumbwa na madhila kwa kurejelea hadithi ya
"Msiba wa kujitakia" (alama 14)

Majibu

a.
i. Takriri - watu, wapiga kura.
ii. Nidaa/siyahi - hawajui leo wala kesho!
iii. Tashbihi - Maisha ya Wanamatopeni yalikuwa kama mchezo wa karata.
iv. Msemo - asubuhi ya majogoo.
v. Mbinu rejeshi - Zuhura anakumbuka namna yeye na wenzake walivyotunga
foleni ndefu.
vi. Methali - Wajinga ndio waliwao.
 mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
vii. Jazanda - Mzigo mzito wa maisha. (zozote 6 x 1 =6)
b.
i. Maisha ya udhikifu
ii. Mfumuko wa bei
iii. Kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali.
iv. Uamuzi wa mpiga kura hauheshimiwi.
v. Kupewa mishahara duni.
vi. Mishahara inachelewa kulipwa
vii. Wanatawaliwa na viongozi wasio na sera bora.
viii. Shughuli za uchaguzi zinaendeshwa kwa njia isiyo huru wa haki.
ix. Ndoto na nia za vijana zimebanwa, zikafinywa na kuzimwa.
x. Njaa - Machoka hajatia chochote kinywani tangu asubuhi kiasi matumbo yake
kushindwa kuhimili makali ya njaa.
xi. Ukosefu wa ajira - Machoka anatafuta kibarua mchana kutwa bila mafanikio.
xii. Ukabila – Zuhura anampigia kura Sugu Junior kwa sababu ni wa kabila lao.
xiii. Viongozi waliochaguliwa hawawatimizii raia ahadi walizotoa.
xiv. Ufisadi - wapiga kura wanahongwa kwa kupewa khanga, sukari, unga wa
sima, mafuta na visenti vya kununua tembo.
(zozote 7 x 2 = 14)

Swali 6
Fadhila za Punda Maswali na Majibu

. “Katika hali ile ya uchungu, kilio na mtanziko wa mawazo, akaiona simu yake imeanguka
chini ya kitanda….. Haidhuru hata kama atamuunga mkono mwanawe.”

i. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)


ii. Fafanua mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
iii. Eleza sifa nne za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 4)
iv. Eleza jinsi “taasubi ya kiume” inavyoshughulikiwa na mwandishi wa “fadhila za
punda”. (alama 10)

Majibu

i. Msemaji ni mwandishi.
 Anayerejelewa ni Lilia
 Mahali ni nyumbani kwa Luka/Lilia.
 Ni baada ya kupigwa na mumewe kwa kumripoti katika kituo cha polisi.
(alama 4)
ii. Taswira (hisi) - hali ya uchungu/ kilio /mtanziko
 Nahau/msemo - unga mkono (alama 2)
iii. Sifa za Lilia
 Mwenye mapenzi ya dhati - anampenda mumewe
 Ni mtiifu - anawacha kazi baada ya kushauriwa na mumewe.
 Ni mwaminifu - mbele ya mumewe
 Ni mwenye heshima - anamwita mama mkwe kwa heshima.
 Ni mwenye huruma - anamtetea mumewe kupewa ufadhili.
 Mtulivu - hapendi ugomvi.
 Mwenye bidii - anasoma hadi chuo.
(za kwanza 4 x 1 =4)
iv. Taasubi ya kiume
 Luka anampiga mkewe Lilia kwa ngumi, teke, kofi na hata kumfokea.
 Baada ya kuanza uzinzi na hawara zake, Luka anakuwa mkali kwa mkewe.
 Luka anashinikiza Lilia kuacha kazi kwa madai kuwa anamhitaji kudhibiti
fedha za kanisa.
 Lilia hana usemi nyumbani mbele ya Luka.
 Luka anampuuza Lilia anapomshauri asiingilie siasa.
 Luka analiuza kanisa lao bila kumshauri wala kumwuliza mkewe Lilia.
 Luka kurithi mali ya babake Lilia badala ya bintiye (Lilia)
 Luka haoni umuhimu wa kuandamana na mkewe; anamwacha kijijini.
 Luka kutaka miadi kabla ya kutembelewa na mkewe.
 Wanawake hawafai kuwastaki waume zao. Lilia anahofia kujulikana kwamba
alikuwa na nia ya kumshtaki mumewe.
 Luka kuwa na hawara. Kitendo hiki kinamkosesha Lilia hadhi yake katika
ndoa.
(zozote 5 x 2 = 10)

Swali 7
Fadhila za Punda Maswali na Majibu

“Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala upitao.
Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”

a. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)


b. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c. Bainisha toni ya dondoo. (alama 1)
d. Fafanua sifa zozote tatu za mzungumziwa. (alama 3)
e. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa fadhila za
punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka. (alama 10)

Majibu

“Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala upitao.
Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”

a. Yaweke maneno haya katika muktadha wake.


 Ni maneno ya mamake Luka.
 Anamwambia Luka.
 Yumo katika hospitali (Luka).
 Ni baada ya gavana Luka kuhusika kwa ajali na yule kirukanjia wake
akakosa kuja kumwona baada ya kumsaliti Lilia alipokuwa gavana.
Zozote 4x1=4
b. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
 Methali – usiache mbachao kwa msala upitao.
 Swali la balagha – yu wapi kirukanjia wako?
 Takriri - …wapi…wapi
 Nidaa - …mashuzi! 2x1=2
c. Bainisha toni ya dondoo.
 Huzuni, Majuto, uchungu.
 Dhihaka,dharau 1x1=1
 Umuhimu wa toni ni kuonyesha hisia za mzungumzaji.
d. Fafanua sifa zozote tatu za mzungumziwa.
 Mwenye bidii.
 Ni laghai.
 Msaliti.
 Mzinzi.
 Ni katili.
 Mnafiki.
 Ni msomi.
 Mwenye dharau. Zozote 3x1=3
e. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa fadhila za
punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka.
 Luka anaachiwa kanisa na pastor Lee Imani baadaye anauza kanisa ili
awanie gavana.
 Lilia anampenda Luka na anamshawishi babake akubali kuwabariki
lakini Luka anamsaliti Lilia anapokuwa gavana kwa kumpiga makofi na
teke la tumbo.
 Luka anamsaliti pastor Lee baada ya kumkubali na kufadhili elimu,
baadaye anakuwa na uhusiano na mtoto wake anayemtesa baadaye.
 Luka anawasaliti waumini kwa kuuza kanisa na kuingia siasani.
 Luka anamtendea uovu mkewe anapokosa kuandamana naye kwenye
kampeni na kumtusi kuwa amenona kama nguruwe na kwamba
wanawake ni wengi.
 Luka anawasaliti wananchi waliomchagua kwa kutotimiza ahadi
alizowatolea wakati wa kampeni.
 Luka anamsaliti mkewe kwa kuwa na uhusiano ka kiruka njia.
 Kirukanjia anamsaliti Luka kwa kukosa kumtembelea hospitalini baada
ya kujulishwa na daktari huenda asiweze kutembea tena licha ya kuwa na
uhusiano wa kimapenzi naye.
 Lilia anamsaliti babake kwa kuacha kazi ya meneja wa benki baada ya
babake kumsomesha na kupata kazi ili awe akipokea wageni wa Luka.
 Lilia anamsaliti babake kwa kushinikiza aolewe na Luka, ingawa babake
hakutaka.
 Lee anamsaliti Lilia kwa kumrithisha Luka Kanisa 10x1=10

Swali 8
Huku ukirejelea hadithi zifuatazo tano jadili maudhui ya migogoro kwa kutoa mifano
maridhawa. (alama 20)

a. Fadhila za punda
b. Msiba wa kujitakia
c. Mapambazuko ya machweo
d. Harubu ya maisha

Majibu

Huku ukirejelea hadithi zozote tano jadili maudhui ya migogoro kwa kutoa mifano
maridhawa.

a. Fadhila za punda
 Lilia na Luka wana mgogoro unaosababisha vita k.m anapojitazama
kwenye kioo anaona kovu shavuni na donda.
 Mapenzi ya Lilia na Luka yanaleta mgogoro kati ya Lilia na babake-
hapendi uhusiano ule.
 Kuna mgogoro wa kinafsia kwa babake Lilia anayemshuku Luka kuwa
na uhusiano na mwanawe Lilia.
 Luka kumvamia mkewe na kumvuta nywele kumwelekeza kwenye
chumba cha kulala, ambapo anampiga ngumi na mateke.
 Luka anamtawisha Lilia na hata kumlazimisha kuandamana naye
kwenye kampeni na hii inawafanya wakosane – Luka anamwambia
wanawake ni wengi.
b. Msiba wa kujitakia
 Kati ya viongozi na raia ambao wako tayari kupigania haki zao-
hawapewi huduma na viongozi.
 Zuhura na Machoka-Zuhura angependa kumchagua kiongozi kwa
misingi ya kikabila kinyume na Machoka.
 Sugu Junior na Fumo Matata – Fumo anaona dai la serikali kwamba
kuna maendeleo ni porojo tu.
 Mgogoro kati ya tume ya uchaguzi na wananchi.
 Mgogoro wa ushindi wa Sugu Junior dhidi ya Fumo matata.
 Kati yam zee Sugu Senior na Zuzu Matata; ambapo mzee Sugu senior
alitwaa uongozi baada ya kuondoka kwa wakoloni.
c. Mapambazuko ya machweo
 Mzee Makutwa kumtifulia mzee Makucha vumbi na kumdhihaki
kuhusiana na kazi yake.
 Bi Macheo anajikuta katika mgogoro na mumewe kwa vile hapendi jinsi
mzee Makutwa anavyomfanyia stihizai mumewe.
 Mzee Makucha anakuza mgogoro anapomwitia polisi mzee Makutwa
kwa kuwahujumu vijana.
 Mzee Makutwa ana mgogoro na sheria kwa vile anaendesha biashara
haramu.
 Migogoro kati ya vijana waliosoma na serikali kwa mfano Sai alidai kuwa
vijana wanaachiwa kazi za hadhi ya chini.
 Mzee Makutwa na polisi wakijaribu kumwingiza pangoni.
 Mzee Makucha na shirika la reli-kukataa kumlipa pesa.
d. Harubu ya maisha
 Mama Mercy amtaka mumewe aeleze sababu ya kutofika ilhali motto
anaelekea kulala. Mama Mercy analalamika kuwa mumewe hatimizi
wajibu wake.
 Familia ya Kikwai ina mgogoro na fundi wa nyumba hajalipwa kwa
mwezi mzima.
 Kikwai anagongana na Bosi kwa kuacha gari nyumbani kwa kukosa
mafuta.
 Nilakosi ana mgogoro wa mpangishaji wake kwa vile hajamlipa na mwezi
unaenda kuisha.
 Kikwai kutoleta chakula.
 Kikwai kufika amechelewa.
 Mercy kulalamikia njaa na upweke.

Swali 9
Nipe Nafasi Maswali na Majibu

a. Eleza tafsiri mbalimbali za kichwa cha hadithi hii, ‘Nipe Nafasi’ (alama 7)
Pupa (F. M. Kagwa)
b. Fafanua umuhimu wa mandhari ya Chenga-ways katika kujenga hadithi Pupa. (alama
5) Toba ya Kalia
(Douglas Ogutu)
c. “Ni kutokana na mchango wako kupitia twitter na facebook katika maswala
mbalimbali ambapo iliamuliwa upewe fursa ya kuzungumza moja kwa moja na
watazamaji wetu.”
Eleza nafasi ya vijana kwa mujibu wa hadithi Toba ya Kalia. (alama 8)

Majibu

Nipe Nafasi – Mzamane Nhlapo

a. Eleza tafsiri mbalimbali za kichwa cha hadithi hii, ‘Nipe Nafasi’ (alama 7)
 Kuchukua nafasi ya kuboresha maisha yake. Kazili anapoona mumewe
amemdhalilisha vya kutosha, anaamua kuondoka. Hajali kuomba ruhusa
kama anavyotakiwa.
 Kuchukua hatua wanapoona waume zao hawawajibiki. Bi. Kazili
anajisemea kuwa atarudi kufanya kazi kuwakimu, na siku hiyo lazima
wale chajio.
 Nafasi ya kuishi atakako. Kazili anawakumbusha wanaume kuwa yeye ni
raia halali wa Lesotho kupitia kwa ndoa, na hakuna anayeweza
kumlazimisha kurudi Swaziland, hata mumewe.
 Kupinga maamuzi kuhusu maisha yake ambayo hajahusishwa kufanya.
Mama Kazili anakana maamuzi ya wanaume kwenye kraal ambayo awali
yanachukuliwa kuwa sheria isiyoweza kupingwa.
 Wanawake kupewa nafasi na nyadhifa. Kazili anaeleza jinsi wanawake
wanavyohiniwa nafasi na wadhifa katika jamii kwa kusingizia Biblia,
kuwa mwanamke anafaa kuwa mnyenyekevu.
 Nafasi ya kuheshimiwa. Kazili anapinga swala la mwanamke
kuchukuliwa kama mtoto ambaye anafaa kuomba ruhusa kwa kila kitu
kutoka kwa mumewe.
 Nafasi ya ajira na kazi. Mwisho wa mwaka huo, Kaizili anafanya kazi ya
ualimu bila ruhusa kutoka kwa yeyote, na wanawe wanapata chakula kila
siku.
 Kupatiwa nafasi ya usemi. Wanawake wa makamo wanakubaliana na rai
ya Kazili, wanaona kuwa amaesema ukweli mchungu. Wako tayari
kubadili mkondo huu wa dhuluma dhidi yao.
 Kufanya maamuzi ya kibinafsi. Mama Kazili anawambia wanaume
kwamba aliondoka bila kuomba ruhusa kwa mumewe kwa sababu alijua
hangekubaliwa. Anawajuza kuwa hawezi kukaa tu kuwatazama wanawe
wakihangaika kwa njaa.
 Nafasi ya kusema ukweli. Wanaume wanahisi kwamba Kazili amewatusi,
na kwamba lazima arudi kwao Swaziland kwa kuwakosea heshima.
Hatarajiwi kusema ukweli.
Pupa (F. M. Kagwa)
b. Fafanua umuhimu wa mandhari ya Chenga-ways katika kujenga hadithi Pupa. (alama
5)
 Kufichua mitandao ya uhalifu inavyofanya kazi / biashara haramu
zinazoendeshwa katika jamii na madhara yake.. Ni danguro.
 Kusawiri maudhui ya masaibu yanayoandama mtoto wa kike katika
jamii.
 Kuendeleza ploti. Baadhi ya matukio yanatokea katika mandhari haya.
 Kuwaibusha wahusika na sifa zao kama Mashaka.
 Kuchimuza matabaka katika jamii. Kuna tabaka la wateja matajiri na
wanyonge kina Mwakuona, Mashaka ambao ni bidhaa ya matajiri
Toba ya Kalia (Douglas Ogutu)
c. “Ni kutokana na mchango wako kupitia twitter na facebook katika maswala
mbalimbali ambapo iliamuliwa upewe fursa ya kuzungumza moja kwa moja na
watazamaji wetu.”
Eleza nafasi ya vijana kwa mujibu wa hadithi Toba ya Kalia. (alama 8)
 Kukuza vipaji. Jack na Siri wanashiriki katika shindano linaloandaliwa
na wahandisi kutoka Uchina na kuibuka katika nafasi tatu za kwanza.
Jack anaandaa kazi ya kupigiwa mfano na hata fomyula zake zinaingizwa
kwenye vitabu, japo kwa jina la Siri
 Kuendeleza lugha na utamaduni. Jack akiwa Uchina anaendeleza elimu
ya lugha ya Kiswahili kwa wakazi wa huko, na anasema kwamba baadhi
yao wanapata umilisi hata kuliko wazungumzaji wa nchi yake ya
nyumbani.
 Ujasiriamali. Jack anapokamilisha masomo yake ya shule ya upili kukosa
karo anaanzisha biashara ya kuuza nguo.
 Siri huwasiliana na wazazi wake kupitia skype, na Jack ndiye
huwaunganishia mitambo kuhakikisha mawasiliano yanafaulu vizuri.
Wanapatana naye vyema akiwa Uchina.
 Urafiki wa dhati. Urafiki wake na Siri ni wa kipekee. Wanasaidiana sana,
hata wanawafikiri kuwa ndugu. Hata kuhiniwa fursa yake na kupewa
Siri hakuwatenganishi.
 Usamehevu. Anawasamehe wote waliomkosea mwishoni.
 Kukuza teknolojia kupitia kwake Jack , nafasi ya teknolojia na
mawasiliano inabainika.
 Kukuza uzalendo. Siri anakipigania Kiswahili na kukifunza Uchina.
 Ushauri. Mwishoni mwa kipindi, Siri anawapa watazamaji wosia kuwa
wasiwadhulumu mayatima na maskini
 Siri na Jack wanawakilisha teknolojia ya mawasiliano na umuhimu wake
katika kuunganisha jamii.
 Watetezi imara wa haki na ukweli. Siri
 Kukuza mahusiano ya kimataifa na umuhimu wake katika jamii
unadhihirika. Siri

Swali 10
Nilitamani (Phibiana Muthama) na Kifo cha Suluhu – Dominic Maina Oigo

Nilitamani Maswali na Majibu

a. “Wakati anaongea kwa simu, nikawa najifungua mkanda. Nikafaulu. Nikajaribu


kufungua mlango. Duh! Ulikuwa ushatiwa loki. Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia
juu yake! Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue niendako.
Nikakimbia. Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia yaliyonikuta. Nilikata katikati ya
misitu sijui nielekeako ila mbali na Romeo na pepo yake. Nimekaza mwendo huku
nahema, pumzi si zangu! ”
i. Fafanua aina za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 5)
ii. “Tamaa mbele mauti nyuma.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi:
Nilitamani. (alama 7)
Kifo cha Suluhu – Dominic Maina Oigo
b. “Aliyaacha machozi yamtoke shibe yake kwani asingeweza kujizuia. Barua ile
ilimfichulia siri si haba”
Thibitisha kauli iliyopigwa mstari ukirejelea hadithi Kifo cha Suluhu. (alama 8)

Majibu

Nilitamani (Phibiana Muthama)

a. “Wakati anaongea kwa simu, nikawa najifungua mkanda. Nikafaulu. Nikajaribu


kufungua mlango. Duh! Ulikuwa ushatiwa loki. Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia
juu yake! Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue niendako.
Nikakimbia. Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia yaliyonikuta. Nilikata katikati ya
misitu sijui nielekeako ila mbali na Romeo na pepo yake. Nimekaza mwendo huku
nahema, pumzi si zangu! ”
i. Fafanua aina za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 5)
 Taswira sikivu – Wakati anaongea kwa simu
 Taswira mguso – nikawa najifungua mkanda / Nikajaribu
kufungua mlango / Duh! Ulikuwa ushatiwa loki.
 Tasira mwendo – Sijui nilipata wapi nguvu za kupitia juu yake!
Nikaponyoka pyu! Nikakimbia mguu niponye. Nilikimbia nisijue
niendako. Nikakimbia.
 Taswira oni – Sitaki kuangalia nyuma kwa kushtukia
yaliyonikuta. Nilikata katikati ya misitu sijui nielekeako ila mbali
na Romeo na pepo yake.
 Taswira hisi - Nimekaza mwendo huku nahema, pumzi si zangu!
ii. “Tamaa mbele mauti nyuma.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi:
Nilitamani. (alama 7)
 Tumaini, anaondoka kwao Kenya hadi nchi ya Wabongo kwa
kutamani maisha mazuri.
 Tumaini anatamani kuwa na milki na mali kama ya Nina.
Anagundua kwamba alimwonea gere Nina.
 Tumaini anapoishi na Nina anaanza kuwaonea wivu na kutamani
kuwa na mume kama huwa Nina.
 Tumaini anahama kwa Nina, kwa matumaini ya maisha mazuri
bila mpangilio maalum: anaishia kuteseka zaidi.
 Tumaini anapanda kutoka kiwango cha kutamani na kuanza
kutaka. Anataka maisha mazuri, anataka mume wake waoane na
kupata watoto wazuri.
 Kwa tamaa yake, Tumaiini anamwona Romeo, kama
mwanamume mtanashati aliyemwaza kwenye lile shairi lake.
Nusra kumtoa kafara na analazimika kutoroka.
 Matatizo ya kisaikolojia. Tumaiini anatamani kila kitu. Katika
ushairi mawazoni, Tumaini anatamani kuwa na kasri afurahie,
kazi ajikimu, na gari la kifahari. Anatamani maisha yawe mepesi
na kumpa burudani.
 Tuamini yuko katika ndoa ya kisaikolojia. Anatamani sana kupata
mume mzuri amwoe, waishi maisha mazuri. Anajiona akiwa
ameolewa, huku wamejaliwa watoto ambao wanawalea kwenye
misingi ya kidini na kuwakuza vyema.
 Unafiki wa kidini. Anapoona mambo yake yameenda kombo,
anamgeukia Mungu na kumpa ahadi ya kumtumikia milele iwapo
atamfungulia milango.
 Ulaghai. Romeo anamhadaa Tumaini kwa kisingizio cha mahaba,
lakini ukweli ni kwamba anataka kumtumia kwa matambiko yake.
 Maamuzi mabaya. Tumaini anaamua kuondoka kwa Nina, japo
hana pa kuishi. Ni ajabu kuwa anachoka kufadhiliwa hali hana
hanani.
 Maisha bandia. Tumaini anapopata hela kutoka kwa Nina,
anaamua kwenda kudanganya moyo Coco Beach. Ananunua
kaukau za mihogo na soda ya pepsi. Anavinjari kama mwenye
vyake hali anateseka.
Kifo cha Suluhu Maswali na Majibu
b. “Aliyaacha machozi yamtoke shibe yake kwani asingeweza kujizuia. Barua ile
ilimfichulia siri si haba”
Thibitisha kauli iliyopigwa mstari ukirejelea hadithi Kifo cha Suluhu. (alama 8)

 Matatizo katika asasi ya ndoa. Suluhu anamsababishia mkewe uchungu


kwa kutengana naye na hapati fursa ya kuzungumza naye.
 Ukatili wa suluhu, ikiwemo kumwua mamake Abigael.
 Usuli na Mabadiliko. Anamkumbusha kazi yake ya kuuza makaa
ilivyofika hatima ya ghafla, kisha akatwaa ubunge kwa mbinu azijuazo.
 Uumilivu wa Bi. Suluhu. Amevumilia kwa ajili ya watoto na kuwalea, na
wa kwanza amekamilisha darasa la nane.
 Uaminifu wa Bi. Suluhu. Anasisitiza jinsi anavyompenda mumewe, wala
hajawahi kumwendea kinyume.
 Bi. Suluhu anaonyesha thamani ya ndoa ya kuweka siri kwa
kumhakikishia mumewe kuwa hajawahi wala hatatoa siri zake anazojua.
 Ufisadi na kutowajibika. Suluhu haleti maendeleo kwa kuwa anawalipa
wasichana wa vyuo vikuu na kula nao uroda. Pesa anamlipa Bwana
Ngoma aliyefadhili siasa zake.
 Ushauri. Anamuasa akome tabia zake kwa kuwa hali yake ni bayana.
 Shukrani za Bi. Suluhu. Anamshukuru kwa mema aliyomtendea kabla ya
kubadilika, na yale aliyotendea wazazi wake.
 Athari za kutowajibika. Bi. Suluhu anamlaumu mumewe kwa kifo chake
anachotarajia kutokana na kukosekana nyumbani na uzinzi,
vinavyomletea msongo wa mawazo.
 Utamaushi. Bi. Suluhu anakiona kifo kama suluhu.
 Kufichua yaliyofichika. Barua hii inategua kitendawili cha kifo cha
mamake Abigael aliyepatikana ameuawa.
 Kuonyeha mustakabali wa jamii mpya. Abigael anajuta kuingilia ndoa ya
Suluhu. Anaona kifo cha Suluhu hakitafaa lolote. Kifo kifaacho ni cha
maovu na kupalilia utu. Anafanya uamuzi wa kutia bidii kujipa riziki na
kumwachia Mungu wajibu wa hukumu.

Swali 11
Mume wangu, hebu zivute fikra zako miaka kumi na mitano iliyopita tulipoingia katika
mkataba wa ndoa. Kwa nini unataka kujitia hamnazo kuhusu ahadi ulizozitoa? Umesahau
namna tulivyohangaika, tukachekwa na watu, tukakosa hata marafiki na hatimaye
tukabandikwa majina ya ajabu? Umesahau, mume wangu? Umesahau namna kazi yako ya
kuuza makaa ilivyofika hatima ya ghafla baada ya serikali kupiga marufuku ukataji wa miti
katika eneo la Dafrao? Naomba ukumbuke. Ninaamini huenda umesahau! Ama cheo chako
cha ubunge ulichokipata kwa mbinu nizijuazo mimi kimekulevya na kukufanya uisahau
familia yako?

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)


b. Fafanua mbinu za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 6)
c. Tambua toni iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
d. Fafanua umuhimu wa ujumbe alitoa mnenaji wa maneno haya. Tumia hoja nane.
(alama 8)

Majibu

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)


 Maneno haya ni ya Bi. Suluhu kwa Bwana Suluhu katika Barua aliyoitoa
Abigael mfukoni mwa Bwana Suluhu. Bwana suluhu na Abigael walikuwa
wamekwenda kujistarehesha.
b. Fafanua mbinu za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 6)
 nahau/msemo – kujitia hamnazo
 Balagha – umesahau mume wangu?
 Takriri/urudiaji – neno umesahau limerudia.
 Nidaa – naamini huenda umesahau!
 Uhuishi/Tashihisi – cheo kimekulevya
 Mbinu rejeshi – Bi Suluhu anakumbuka maisha yao ya awali – m.f
tulivyohangaika.
 Usambamba – tukachekwa tukakosa tukabandikwa
 Majazi – Dafrao (zozote 6 x 1 = 1)
c. Tambua toni iliyotumika katika dondoo hili.
 Toni ya unyenyekevu – naomba ukumbuke.
 Toni ya mshangao– Bi Suluhu anastaajabu vipi mumewe amesahau maisha
yao ya awali. (yoyote 1x2=2)
 Toni ya huzuni -
d. Fafanua umuhimu wa ujumbe alitoa mnenaji wa maneno haya. Tumia hoja nane.
(alama 8)
 tunafahamu uhusiano wao – hapo awali Bw. Suluhu alimpenda Bi. Suluhu na
kutoa ahadi nyingi kwake. Uhusiano huu umedhoofika sasa.
 Tunafichuliwa maisha yao ya hapo awali. Walikuwa maskini aliuza makaa
kupata riziki.
 Bwana Suluhu ni Mbunge na alipata cheo chake kwa njia isiyo halali.
 Tunafichuliwa kuwa Bw. Suluhu ndiye aliyemwangamiza mamake Abigael ili
ajifaidi na shamba lake.
 Tunafahamu kuwa Bw. Suluhu hafanyi maendeleo katika eneo bunge lake
kwa sababu anafuja pesa za wananchi kwa kuwalipa wasichana wa vyuo vikuu
baada ya kula uroda nao.
 Tunaambiwa kuwa Bw. Suluhu ana deni la Bw. Ngoma aliyemkopesha pesa
za kampeni hivyo akakosa kufanya maendeleo kwa kuwa anatafuta mbinu za
kulipa deni hili.
 Tunafahamishwa kuwa Bw. Suluhu ni mgonjwa. Watu wanazungumza kuhusu
kuabiri gari moshi.
 Bi. Suluhu anahofia Suluhu asimwambukize Abigael nakama
 Tunafahamishwa kuwa Bw. Suluhu alikuwa mwema hapo awali kwani
alisaidia mamake Bi. Suluhu na familia yake.
 Bi .Suluhu pia anatufahamisha kwamba anaugua msongo wa mawazo
uliosababishwa na vitendo vya mumewe vya kihayawani.
 Kupitia kwa barua hii tunafahamu kuwa Bw. na Bi. Suluhu wana watoto
wawili ambao wanaumia kwa sababu ya matendo ya Bw. Suluhu.
(za kwanza 8 x 1 = 8)

Swali 12
“Wewe mke sampuli gani usiyetaka kumuunga mkono mmeo?”

Kwa kurejelea hadithi hii na nyingine zifuatazo, jadili changamoto anazopitia mnenewa
pamoja na wahusika wa jinsia yake. (alama 20)
Ahadi ni deni.
Hadithi ya Nipe nafasi

Majibu

a. Fadhila za punda
 Mwanamke kutawishwa, lilia anaachishwa kazi ya umeneja na mwishowe
kutawishwa. Anaishia kukaa nyumbani na kutishwa asidhubutu kutoka nje ya
lango.
 Mwanamke anatishiwa – Lilia anapodhubutu kumshtaki mumewe
anakumbushwa kuwa yeye ndiye Gavana na ana uwezo wa kufanya haki kuwa
batili na batili kuwa haki.Utajua kichomtoa kanga manyoya.
 Mwanamke anapokezwa vipigo. Lilia anapokea mapigo kutoka kwa mumewe
anapoenda kuripoti kwa polisi.
 Mwanamke kutusiwa: Lilia anaambiwa amenona kama nguruwe.
 Mwanamke kudhalilishwa. Lilia annambiwa kuwa ana umbo kama nguruwe
kwani kazi yake ni kula na kulala tu.
 Mwanamke kuendewa kinyume na mumewe, katika ndoa, Luka anasemekana
kuwa na kiruka njia ambaye waliandamana naye kila mahali. Lilia anapouliza
ni nani anapokea kipigo kinachomlaza kitandani siku mbili.
 Kuachishwa kazi. Lilia anaachishwa kazi na mumewe ili awe mpokezi wa
wageni nyumbani.
b. NIPE NAFASI
 Wanawake kutosaidiwa katika malezi na waume zao. Mama Kazili hatumiwe
pesa na mumewe yeye na watoto wake wanataabika kwa njaa.
 Mwanamke kutosikilizwa. Wazazi wa mama Kazili wanadinda kusikiliza
malalamishi yake kuwa mumewe ana mke mwingine migodini.
 Kutopatiwa pesa za mahitaji – nyanyake msimulizi anakosa kumpa mamake
pesa zinapotumwa na babake.
 Kufiwa na jamaa zao. Mama Kazili anafiwa na mwanawe Mkhathini wakiwa
katika safari yao kwenda Makongeni.
 Wanawake kulaumiwa/kusingiziwa kusababisha kifo. Mama Kazili
analaumiwa kusababusha kifo cha Mkhathini kwa sababu hakuomba ruhusa.
 Wanawake kuuawa – mwanamke katika kijiji cha Habelo anatoroka na
mwishowe maiti yake kufukuliwa na mbwa kondeni mwake. Hii ni baada ya
kumuita mumewe mzembe.
 Wanawake kudhalilishwa – wanawake wanaketi sakafuni nao wanaume
wanaketi vitini.
 Mwanamke kutopewa nafasi ya kujitetea. Mama Kazili ananyamazishwa na
Matweba anapojitetea kwa wazee.
 Kutengwa kwa misingi ya kitaifa. Mama Kazili anaambiwa lazima arudi kwao
Swaziland.
 Mwanamke kuchukuliwa kama mtoto anayetarajiwa kuwa chini ya uelekezaji
na utunzi wa mwanamume katika jamii ya Belo.
 Jamii na serikali imewanyima wanawake uhuru. Wanahitajika kuomba ruhusa
kwa kila jambo wanalolihitaji kufanya.
c. Ahadi ni deni
 Kutoonana na jamaa zao kwa muda mrefu. Fadhumo anakaa kwa muda wa
mihula mitatu bila kuonana na wazazi na jamaa zake.
 Kufiwa na wazazi, Fadhumo anafiwa na babake katika ajali na mamake pia
anafariki baadaye.
 Kuacha masomo – Fadhumo anaacha masomo yake kwa sababu ya ukosefu
wa karo. Anaachia kidato cha pili.
 Kulazimishwa kuwa kimada. Jamaa ya babake Fadhumo anamwambia kuwa
ikiwa anataka kusoma sharti awe kimanda wake.
 Mwanamke kulazimishwa kuolewa akiwa mchanga Fadhumo anaolewa na
Adan akiwa mchanga.
 Mwanamke kutwikwa majukumu. Fadhumo anajukumika kuwalea na
kuwasomesha nduguze ingawa ni mchanga.
 Mwanamke kufanya kazi kunachukuliwa kama kuzurura. Adan anaulizwa na
watu kwa nini mkewe anaenda kazini ilhali anafaa kukaa nyumbani na
kutunza nyumba na watoto.
 Mwanamke kutoruhusiwa kusoma; mjombake Adan anamwambia kuwa
masomo yatamfanya mkewe kuwa jeuri.
 Mwanamke kusingiziwa; mjombake Adan anamwambia Adan kuwa Fadhumo
anaweza kutoroka na walimu wake au wanafunzi wenzake (zozote 20 x 1 =
20)

Swali 13
Nipe Nafasi Maswali na Majibu

a. Baridi ilizidi kututafuna kadri tulivyokazana kupanda Milima ya Maloti. Vidole


vyangu vya miguuni vilikufa ganzi. Mashavu yetu yaliadhibika kwa upepo baridi
huku vipande vya theluji vikitupiga kwenye nyuso zetu.Miili yetu iliathirika;tulihisi
njaa na uchovu. Nikatamani tufike kwa jamaa ya baba yetu ambako tungepata angalau
mchuzi wa papa kabla ya kulala. Bidii ya mama ilitutia moyo wa kuendelea na safari.
i. Tambua nafsi ya usimulizi iliyotumika katika hadithi hii na uthibitishe jibu
lako. (alama 2)
ii. Eleza umuhimu wa mwandishi kutumia nafsi uliyotaja hapo(i) juu. (alama 2)
iii. Bainisha mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili (alama 2)
iv. “Mamake Msimulizi (Richman) ni kielelezo cha wanawake jasiri””Thibitisha
kwa kutolea mifano mwafaka (alama 7)
b. Hadithi “Toba ya Kalia” inahimiza uwajibikaji. Jadili. (alama 7)

Majibu

a.
i. Nafsi ya kwanza
 Vidole vyangu vya miguuni..
 Nikatamani tufike kwa jamaa ya baba yetu.....
 Kututafuna kadri tulivyokazana...nk. (Nafsi-1, Mfano-1)
ii. Umuhimu wa nafsi ya kwanza:

i. Msimulizi humleta msomaji karibu na yeye/masafa baina ya msomaji


na msimulizi yanaf upishwa.
ii. Msimulizi hudhihirisha hisia zake kwa wasomaji na kuwateka hisia
zao
iii. Msimulizi huongezea kisa chake uhalisia ikilinganishwa na kama kisa
kingesimuliwa kwa namna ya kuripotiwa
iii. Mbinu za kimtindo;

 Tashihisi/uhuishi (uhaishaji- Baridi ilizidi kututafuna/vipande vya


theluji vikitupiga
 Msemo/ Nahau - vilikufa ganzi/ilitutia moyo
 Taswira - miili yetu iliathirika / tulihisi njaa na uchovu
 Usimulizi - dondoo lote limesimuliwa
iv. Mamake msimulizi (Richman) kama kielelezo cha wanawake jasiri;
 Mama Kazili anapoamua kuwapeleka wanawe Makongeni bila idhini
ya mumewe na wakwe zake.
 Licha ya mumewe kukosa kumtumia pesa kwa zaidi ya mwaka sasa,
anajikaza kuwalea wanawe
 Mama Kazili anatoa dukuduku lake la kutaka apewe nafasi ya Kuikimu
familia yaka kwa ukoo wa Belo bila woga
 Mama Kazili anamweleza Msimulizi waziwazi sababu za kuenda
Makongeni baada ya Msimulizi kumuuliza.
 Vilevile, alianza kufanya kazi kama mwalimu wa shule ya msingi bila
ruhusa kutoka kwa mumewe wala ukoo wa Belo.
 Anaingiliana vyema na mama aliyemkopesha pesa za nauli ya gari ili
kusafiri milimani
 Aidha, alijibidisha kupanda milima ya Maloti licha baridi na utelezi
kuwapeleka wanawe Makongeni wasife njaa.
 Anamlenga Matweba usoni sawasawa na kumjibu licha ya Matweba
kumkemea.
 Licha ya kumpoteza mwanawe Mkhathini anaendelea na safari huku
akiwa amembeba.
 vilevile, alijua fika kuwa ukoo wa Belo ungem laumu kwa kusababisha
kifo cha Mkhathini..
 Mama Kazili anawaeleza jamaa ya mumewe kuwa yeye ni raia halali
wa Lesotho kupitia kwa ndoa na hakuna yeyote anayeweza
kumlazimisha kurudi Swaziland ikiwemo mumewe.
 Anawaeleza wazee kuwa yuwajua Biblia namna mwanamke anapaswa
kuwa mnyenyekevu na kuwa sheria za kijamii zinamchukulia
mwanamke kama mtoto aliyepaswa kuwa chini ya utunzaji na uelekezi
wa mwanaume.
 Anaikashifu serikali kwa hila kwa kudai kwamba wamechaguliwa na
wanawake.
 Anasema kuwa kabla hajafa, apewe nafasi ya kuyaboresha maisha
yake na yale ya mwanawe.
 Anakataa kuomba msamaha kwa wazee wa ukoo wa kwa Belo kusema
kuwa alimaanisha kile alichokisema.
b. Uwajibikaji katika hadithi ‘Toba Kalia’
i. Jack anawekeza pesa zake zote kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo.
ii. Jack anawajibika anapowaunganishia wazazi wa Siri mitambo ili kuwasiliana
na mwanao Siri kwa njia ya ‘skype’
iii. Licha ya kuhiniwa nafasi yake katika mashindano na Bwana Kalia, Jack
anampa mkewe Kalia zawadi yake ya hundi za shilingi elfu kumi amhifadhie
iv. Jack anajitengenezea kitanda na kuweka shati lake chini ya mto ili kunyooka .
v. Siri anaidhamini lugha ya kwao licha ya kuwa Uchina na hata amewafundisha
Wachina wengi lugha ya kwao Kiswahili.
vi. Siri akiwa Uchina kila mwezi, husoma riwaya mbili, tamthilia mbili na
angalau diwani ya mashairi kila baada ya miezi miwili kuendeleza ugwiji
wake katika lugha ya Kiswahili
vii. Bi. Mshewa (Mamake Siri) anafundisha Kiswahili katika Shule ya Upili ya
Kayole.
viii. Siri amewafundisha Wachina wengi Kiswahili
ix. Wadhamini ambao ni wataalamu wa uhandisi kutoka Uchina wanachangia
katika elimu kwa kutoa tuzo kila mwaka kwa shule za maeneo mbalimbali
x. Bw. Kalia anakosa kuwajibika anaposhirikiana na Mkurungenzi wa Wizara ya
Sayansi na Teknolojia katika kubadilisha matokeo ya mashindano ya somo la
Sayansi.
xi. Wazazi wa Siri hawakutimiza ahadi waliyotoa kwa wazazi wake Jack
walipofariki katika ajali ya barabarani kwamba wangemtunza Jack hadi afikie
kilele cha masomo yake.
xii. Wazazi wa Siri walikuwa na uwezo wa kumpeleka Jack chuo kikuu bila
ufadhili wowote lakini Bw Kalia anampoka Jack aliyefiwa na wazazi
xiii. Bi. Mshewa anakosa kuwajibika anapoona Jack anaanza kuimarika katika
biashara yake na kumtaka awalipe nusu ya faida ya kila mwezi.
xiv. Siri anawajibika anapozungumzia uovu waliomtendea Jack katika runinga ili
dunia nzima ipate kujua.
xv. Siri anatoa mshahara wake wa mwaka kufadhili Masomo ya Jack ya chuo
kikuu.
xvi. Jane Gatoni anawájibika anapompa Siri fursa ya kumpeperusha siri yake
studioni.
xvii. Jack anawajibika katika biashara yake ya kuuza viatu na kuimarika.
xviii. Jack anawajibika anapowasamehe wote katika familia ya Bwana Kalia na
kumshukuru Siri kwa kusema ukweli
xix. Bw. Kalia anakosa kuwajibika anapojaribu kumpigia simu Siri kumwonya
asipasue mbarika na akatize mahojiano ya runinga.
xx. Jack anawajibika anapoiweka siri ya kutomwambia Bwana Kalia mpango wa
Siri wa kutoa ujumbe muhimu kwa nchi nzima.

Swali 14
Fadhila za punda

“Nitapata wapi mwandani kama mkee wangu marehemu?“

a. Eleza mukthatha wa dondoo hiili ? (alama 4)


b. Fafanua sifa tatu za msemaji. (alama 6)
c. Tambua na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
d. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa kwenye dondo hili. (alama 2)

Majibu

a. Muktadha: Pastor Lee Imani akijiwazia mwenyewe baada ya kupata shinikizo la kuoa
mkw mwingine baada ya kifo cha mkewe. Anaeleza kuwa hangeoa kwa kuwa hayupo
anayelingana na marehemu mkewe 1x4 = 4
b.
 Mcha Mungu - anaanzisha na kuendeleza kanisa
 Mkarimu - anampa mamake Luka ajira
 Mdadisi - Anamwita Luka na kumuuliza nia yake kwa bintiye
 Mwenye mapenzi - Alimpenda marehemu mkewe pia bintiye
za kwanza 2x3=6
Tanbihi"

i. kadiria majibu mengine ya mwanafunzi, maelezo ya sifa yaafikiane na


sifa yenyewe
ii. Akikosea msemaji katika (2a) asituzwe sehemu hii.
c.

i. Ndoa na mapenzi
ii. Kifo/mauti za kwanza 2x2=4
Alama 1 kutaja, 1 ufafanuzi wa kweli
d.
i. Swali balagha
ii. Tashbihi
za kwanza 2
Atoleee maelezo ya kila mbinu, asipoeleza asituzwe chochote.

Swali 15
Sabina

a. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo; (alama 6)


‘Athari ya mawazo yake ilijiandika dhahiri shahiri usoni mwake. Alianza kwa kuachia
tabasamu pana mithili ya msafiri aliyefika salama. Baada ya dakika chache machozi
yalianza kumtoka njia mbilimbili huku kajishika tama. Alifikiria kuhusu mtihani
uliodhamiriwa kuanza siku ya Jumanne. Mtihani ambao ungemwezesha kupata
ufadhili katika shule ya upili ya bweni ikiwa angepita vyema. Hili ndilo wazo lililozua
tabasamu. Lakini, angefeli je?Hatima yake ingekuwa ipi? Maswali haya yalimliza
yakamwacha akisinasina kama mgonjwa wa mafua. Akiwa katika hali hii,
aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu, ‘‘mizizi ya elimu ni michungu ila matunda
yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu, lazima mtie bidii kwani
mtaka cha mvunguni sharti ainame.”
b. Bainisha mbinu mbili zinazoweza kutumiwa kutambua sifa za mhusika Sabina kwa
kurejelea hadithi Sabina. (alama 2)
c. Taja na ueleze aina mbili za taswira zinazojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 2)
d. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza matatizo yanayomkumba mwanamke katika
hadithi Sabina. (alama 10)

Majibu

a.
i. Ayasemayo mhusika
ii. Matendo ya mhusika
iii. Wayasemayo wahusika wengine
iv. Maelezo ya mwandishi kuhusu mhusika mwenyewe
v. Uhusiano wake na wahusika wengineMbinu za kimtindo
b.
i. Taswira – athari kujiandika
ii. Msemo- kajishika tama
iii. Tashbihi- mithili ya msafiri
iv. Balagha- angefeli je?
v. Mbinu rejeshi- aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu
vi. Jazanda- mizizi ya elimu
vii. Methali- mtaka cha mvunguni sharti ainame
viii. Tashihisi- maswali yakamwacha…
ix. Takriri- mtihani, mtihani
c. Aina za taswira kwenye kifungu
i. Oni- usoni mwake
ii. Mwendo- msafiri aliyefika salama
iii. Hisi- kujishika tama
iv. Usikivu- alifikiria
v. Onji- mizizi ya elimu ni michungu (Za kwanza2x1)
d. Matatizo yanayomkumba mwanamke
i. Mimba za mapema- Nyaboke
ii. Kukatiza masomo- Nyaboke
iii. Kufanyishwa kazi nyingi- Sabina
iv. Kukataliwa na wanaowadunga mimba- Nyaboke kukataliwa na janadume
lililompachika mimba
v. Kujukumizwa ulezi wa mapema- Nyaboke
vi. Kukatisha wazazi tamaa
vii. Kukosa malezi ya baba mzazi- Sabina
viii. Kufanya kazi za sulubu ili mtoto apate mahitaji ya kimsingi
ix. Kifo cha mzazi-Sabina
x. Kifo cha walezi- babu na nyanyake Sabina
xi. Kutelekezwa na wanakijiji –Wanakijiji kuapa kukaa mbali naye baada ya
kushuku familia hiyo imelaaniwa.
xii. Kutengwa – Sabina anatengwa na watoto wa mjomba wake (Ombati)
xiii. Dhiki za kisaikolojia-Sabina anapoitwa na mwalimu mkuu
xiv. Kushukiwa- mwalimu mkuu anamshuku Sabina anapinga adhabu ya
kuchelewa kufika shuleni.
xv. Kuchapwa/kuteswa- Sabina anapigwa na shangazi yake.(Yunuke)
xvi. Matusi- Sabina anatusiwa kiokote na Yunuke
xvii. Kunyimwa vifaa vya kimsingi vya matumizi- Yunuke anamzimia Sabina
kibatari alipokuwa akisoma, rinda la Sabina ni kuukuu.

Swali 16
.“...majira ya magharibi pevu, nilifika tena pale mzimuni. Kama ilivyo ada yangu , nilivaa
guo jeupe lililonifunika kama maiti. Nikaangalia huku na huko, sikuona mtu. Hapo nikasogea
karibu zaidi na ule mzimu. Nilipofika nikauimba ule wimbo wote. Nilipomaliza tu nikajitoma
kichakani mle bila hofu wala kimeme. Mara nikajikuta nimo ndani, kiza tororo! Nikatoa tochi
yangu nikaanza kumulika hukuna huko. Nilichokiona humo, sikuamini macho yangu! Mle
ndani ya mzimu mlikuwa na makanda na makasha ya tumbaku, unga wa kilevi na bang
ikwenye marobota. Kulikuwa na mapipa yaliyojaa chang’aa na tembo ya mnazi. Humo pia,
mlikuwa na kitanda cha besera kilichotandikwa
vizuri. Juu ya kitanda hicho, palitupiwatupiwa asumini na maua ya mlangilangiyaliyonukia
harufu za mahaba kuliko harufuya mapambo ya harusi ya kiharuni! Mle mvunguni mwa
kitanda kile mlikuwa na chetezo kilichojaa udi wa mawaridi. Nikabaki kinywa wazi kwa
bumbuazi na butwaa la uduazi! Butwaa ambalo kwa hakika lilifanya akili yangu isimame
kufikiri kwa muda wa sekunde kadhaa.”

a. Kando na taswira, tambua mbinu zingine za kimtindo katika dondoo hili. (alama 5)
b. Ainisha taswira katika kifungu hiki. (alama 3)
c. Chambua maudhui yanayojitikeza katika kifungu hiki. (alama 4)
d. Eleza umuhimu wa Msimulizi katika mujibu wa hadithi husika. (alama 8)

Majibu

a. Kando na taswira, tambua mbinu zingine za kimtindo katika dondoo hili.


i. Tashbihi - nilivaa guo jeupe lililonifunika kama maiti.
ii. Tanakali za sauti - mara nikajikuta nimo ndani, kiza tororo!
iii. Nidaa - sikuamini macho yangu!
iv. Msemo - nikabaki kinywa wazi kwa bumbuazi na butwaa la uduazi!
v. Utohozi - tochi
vi. Tashihisi - butwaa ambalo kwa hakika lilifanya akili yangu isimame kufikiria
kwa muda wa sekunde kadhaa (alama 5)
b. Ainisha taswira katika kifungu hiki.
i. Taswira oni - nilichokiona humo, sikuamini macho yangu!
ii. Taswira sikivu - nikauimba ule wimbo.
iii. Taswira mnuso - yaliyonukia harufu za mahaba kuliko harufu ya harusi ya
kiharuni.
iv. Taswira hisi - butwaa ambalo kwa hakika lililofanya akili yangu isimame
kufikiri kwa muda sekunde kadhaa. (3x1=3)
c. Chambua maudhui yanayojitikeza katika kifungu hiki.
i. Utamaduni/itikadi - nilipofika nikauimba ule wimbo wote.
ii. Matumizi ya mihadarati/madawa ya kulevya - kulikuwa na mapipa yaliyojaa
chang’aa na tembo ya mnazi.
iii. Anasa/uzinzi - humo pia mlikuwa na kitanda cha besera kilichotandikwa
vizuri. Juu ya kitanda hicho,palitupiwatupiwa asumini na maua ya mlangilangi
yaliyonukia harufu za mahaba kuliko harufu ya mapambo ya harusi ya
kiharuni!
iv. Ujasiri/uwajibikaji/ufichuzi - hapo nikasogea karibuzaidi na ule mzimu.
Nilipofika nikauimba uke wimbo ... (4x1=4)
d. Eleza umuhimu wa Msimulizi kwa mujibu wa hadithi husika.
i. Ni kielelezo cha ujasiri na umuhimu wake katika jamii.
ii. Anadhihirisha migogoro kati ya vijana na wazee hasa kuhusiana na masuala
ya utamaduni.
iii. Kupitia kwake, mchango wa vijana/watoto katika kujenga na kuboresha jamii
unadhihirika.
iv. Anaonyesha umuhimu wa upelelezi katika kuwafichua wahalifu miongoni
mwa wanajamii.

Swali 17
Mzimu wa Kipwerere Maswali na Majibu

…akikiomba radhi kile kitawi cha mti kilichonasa kwenye kazu yake ya rangi ya udongo
iliyoficha kiwingu cha nongo kwa kukosa kuoshwa tangu ainunue! Nikauacha mpambano ule
kati ya mzimu na mwenye dhamana ya mzimu ambao sina shaka ulidumu hadi asubuhi pale
wanakijiji walipofika kushuhudia siri nzito iliyomezwa na mzimu ule waliokuwa wakiogopa
na kuamini kiasi cha kuabudu kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka!

a. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)


b. Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. (alama 4)
c. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo. (alama 4)
d. Onyesha jinsi itikadi ilivyomwezesha ‘mwenye dhamana ya mizimu’ na wenzake
kuwafanya wanakijiji kuogopa na kuamini mzimu wa Kipwerere kiasi cha kuabudu
kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka. (alama 8)

Majibu

a. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)


i. Ni maneno ya msimulizi
ii. Anamrejelea Salihina
iii. Walikuwa katika Mzimu wa Kipwerere
iv. Msimulizi alikuwa amewafumania Bishoo na Salihina katika mzimu na wakati
Salihina alipokuwa akitoroka akashikwa na kitawi cha mti hivyo akapiga
mayowe akiomba msamaha. 4 x 1 = 4
b. Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. (alama 4)
i. Kubainisha mgogoro katika hadithi – mgogoro uliopo unaotokana na itikadi
unaotumiwa na kina Salihina kuwalaghai wanakijiji.
ii. Kuwatambulisha wahusika: Salihina na Bishoo
iii. Kuchimuza maudhui: unafiki – Salihina anajifanya kuwa mdumishaji wa
maadili ilhali yeye ndiye alikuwa akilangua dawa za kulevya.
iv. Kutambulisha sifa za wahusika: Bishoo anabainika kuwa mwongo kwa kuwa
anamdanganya mumewe kuwa alikuwa akienda kumwona mtoto mgonjwa
ilhali alikuwa anaenda kwa Salihina.
v. Kuibua dhamira ya mwandishi: Kuonyesha madhara ya ushirikina na itikadi:
imani kuhusu Mzimu wa Kipwerere unawatia wanajamii hofu ilhali hakukuwa
na mizimu au mashetani yoyote katika kichaka hicho.
vi. Kuendeleza ploti – kusuluhisha taharuki kuhusu kuwepo kwa mashetani katika
mzimu kwa kuonyesha kuwa hakukuwa na shetani yeyote ila wajanja kama
kina Salihina. Zozote 4 x 1 = 4
c. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo. (alama 4)
i. Tashihisi/uhaishaji - akikiomba radhi kile kitawi cha mti
ii. Taswira - kilichonasa kwenye kazu yake ya rangi ya udongo iliyoficha
kiwingu cha nongo kwa kukosa kuoshwa tangu
iii. Nidaa - ainunue! uliotukuka!
iv. Kejeli - Nikauacha mpambano ule kati ya mzimu na mwenye dhamana ya
mzimu
d. Onyesha jinsi itikadi ilivyomwezesha ‘mwenye dhamana ya mizimu’ na wenzake
kuwafanya wanakijiji kuogopa na kuamini Mzimu wa Kipwerere kiasi cha kuabudu
kwa unyenyekevu na uchaji uliotukuka. (alama 8)
i. Kuna itikadi kuhusu chanzo cha kichaka cha Mzimu wa Kipwerere –
inaaminika kuwa kichaka hicho kilitokana na kaburi la mwanamke aliyeitwa
Kipwerere.
ii. Inaaminika kuwa yeyote aliyekiuka miiko kuhusu kutoingia katika mzimu
angetolewa kama kafara kwa mizimu.
iii. Wanajamii wa eneo la Mzimu wa Kipwerere wanaamini kuwa Salihina
angeweza kuwasiliana na mizimu. Hivyo, wanapotaka kuandaa sherehe
kama vile jando wanamtuma Salihina kuzungumza na mizimu.
iv. Wanajamii wa eneo la Kipwerere kutoruhusiwa kupita kichaka hicho saa
sita mchana na usiku wote. Wanajamii hawakupewa sababu zenye mashiko
za kuwanyima ruhusa ya kupitia kichaka hicho bali walitishiwa tu kuwa
wangetolewa kama kafara kwa mzimu.
v. Kuamini kwamba taa zilizowaka usiku katika Mzimu wa
Kipwerere ziliwashwa na shetani wa mzimu ili kuwapa watoto wake chakula.
vi. Kuamini kwamba mwanamke na mwanamume waliozungumza walikuwa
shetani na mkewe. Inadaiwa kuwa waliungumza wakati watoto wao
walikuwa wamelala.
vii. Mashetani wanavuta sigara - Kuamini kwamba harufu ya sigara iliyotoka
katika mzimu ilitokana na shetani aliyekuwa akivuta sigara.
viii. Kuamini kwamba kulikuwa na wimbo uliokuwa kama ufunguo wa kuingia
katika mzimu.

Swali 18
“Mike! Mike! Mike! Njoo! Nilijua utafanya vyema mwanangu…”

a. Tambua na ueleze toni ya dondoo hili. (alama 2)


b. Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 2)
c. Eleza sifa nne za msemaji wa dondoo hili. (alama 4)
d. Eleza mbinu mbili ulizozitumia kutambua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 4)
e. Tambua na ufafanue madhila yanayomsakama mhusika mkuu katika hadithi hii ya
“Sabina”. (alama 8)
Majibu

a. Tambua na ueleze toni ya dondoo hili. (al 2)

 Toni ya furaha- Ombati anamwita mwanawe Mike kushangilia matokeo ya


mtihani akidhani ni yake.
b. Changanua mtindo katika dondoo hili. (al 2)
 Nidaa- mike!
 Mdokezo-mwanangu…
c. Eleza sifa nne za msemaji wa dondoo hili. (al 4)
 Ni mwenye tamaa. Ananuia kujinufaisha kutoka kwa dadake kupitia kwa
mahari yake. Anapoyakosa, anaamua kutumia bintiye, Sabina, kwa kumwoza
baada ya darasa la nane ili kupata mifugo.
 Ni mtamaduni. Anaendeleza mifumo ya kijamii kama vile ubidhaaishaji wa
wanawake. Anataka kupata mahari kupitia kwa Nyaboke na anapoyakosa,
anaamua kumwoza bintiye, Sabina, katika umri mchanga na kumwandalia
sherehe. Anasemekana kumlaani Nyaboke kwa kumkosesha mahari.
 Ni kigeugeu. Maripota wanapofika kumhoji Sabina, anaungana naye huku
akijisifia jinsi alivyomlea na alivyo mwerevu, licha ya kuwa awali
anamtelekeza. Anawafukuza waliokuja kumposa Sabina na mifugo wao.
 Ni mwongo/mzandiki/mnafiki. Anamhadaa mwalimu mkuu kuwa Sabina
anapata muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya mtihani. Anadanganya kuwa
Sabina anapenda kazi za shambani hali analazimishwa.
 Msaliti- anaisaliti jamaa yake kwa kumwacha Yunuke kumtesa mwana wa
dadake Nyaboke.
 Mbaguzi- anabagua kati ya wana wake na mtoto wa dadake Sabina. Sabina
anatumikizwa huku wanawe wakikaa starehe.
d. Eleza mbinu mbili ulizozitumia kutambua sifa za msemaji wa dondoo hili. (al 4)
 Usawiri wa mwandishi
 Maneno ya wahusika wengine
 Maneno yake mwenyewe
 Matendo yake kwa wahusika wengine
e. Tambua na ufafanue madhila yanayomsakama mhusika mkuu katika hadithi hii ya
“Sabina”. (al 8)
 Kufiwa na mamake Nyaboke na kuachwa mikononi mwa babu na nyaya yake.
 Babu na nyanyake kufariki akiwa darasa la tano. Hili linamfanya achukuliwe
na mjaombake Ombati na Yunuke.
 Alitumikizwa sana nyumbani kwa mjombake ambako alifanya kazi za kila
nui.
 Anapokea kichapo kutoka kwa Yunuke baada ya kuchelewa kutoka shuleni.
 Anatusiwa sana Yunuke. Anaitwa baradhuli, kiokote,mjalaana n.k.
 Kusingiziwa. Subira anasingiziwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanamume Fulani.
 Kubaguliwa. Binamu zake wanasomea shule za bweni huku yeye akisomea
shule ya kutwa.
 Kunyimwa nafasi ya kudurusu. Yunuke anazima kibatiri hivyo kumnyima
Sabina nafasi ya kumalizia kusoma alichokuwa amebakisha.
 Kuozwa.mjombake Ombati anapanga kumuoza kwa kijana mwendesha
pikipiki hivyo kuzima ndoto yake ya kuemdelea na masomo.
 Kupuuzwa- yunuke na Ombati waliziona juhudi zake masomoni kama za bure.
 Kukosa malezi ya wazazi wote. Babake anamringa mimba mamake Nyaboke
na kumtoroka.

Swali 19
“Poko! Ukiumwa na nyuki haina haja ya kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali.
Hujui faida ya nyuki ulimwenguni? Uliamua kurina asali ya nchi.”

a.
i. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
ii. Tambua tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
iii. Onyesha matokeo ya kuharibu mizinga yote ya asali ukirejelea hadithi
Mapambazuko ya Machweo.
b. Jadili maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto katika hadithi ya;
i. Mapambazuko ya Machweo (alama 10)
ii. Sabina (alama 10)

Majibu

a.
i. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
 Maneno ya Makucha kwa Makutwa mgodini baada ya MAkutwa
kukamatwa kwa kosa kufuja raslimali ya nchi.
ii. Tambua tamathali tatu za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
 Taswira fiche. Ukiumwa na nyuki-kuajibishwa kwa kuhujumu uchumi
wa nchi. Dhihaka. kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali.
 Jazanda. Uliamua kurina asali ya nchi - kuhujumu uchumi wa nchi
iii. Onyesha matokeo ya kuharibu mizinga yote ya asali ukirejelea hadithi
Mapambazuko ya Machweo. (alama 7)
 Makutwa anafanya biashara ya kimagendo ya kuchimba vito katika
mgodi kisiri. Hii ni raslimali ya serikali ambayo mtu anafaa kupata
leseni ya kuchimba
 Ukoloni Mamboleo. Mzee Makutwa anawasomba ijana kwenda
kuwafanyisha kazi ya kusaka vito vya thamani katika mgodi wake.
Wanafanya kazi hii katika mazingira mabovu na kufungiwa mle ndani,
wasiwe na nafasi ya kutokea.
 Makutwa analipoka taifa nguzo yake muhimu kwa kuwachukua vijana
mabarobaro na kwenda kuwatumikisha katika mgodi wake. Vijana
hawa wanafaa kuwa wakiendesha shughuli nyingine muhimu za
kujenga jamii.
 Ajira ya watoto. Vijana kadhaa, ikiwemo watoto wadogo wanafanya
kazi ya kudondoa vijiwe vidogovidogo vinavyong'aa. Wanasimamiwa
na wanyapara wanaowaamrisha kwa sauti za kutisha.
 Mazingira mabovu ya utendakazi. Vijana mgodini wanakumbwa na
hali ngumu ya kimaisha, kwani huko wanakoishi hakuna hali nzuri.
Hewa si safi na kazi wafanyazo ni za sulubu.
 Ukosefu wa ajira. Sai na Dai pia wanawakilisha hali ya vijana ambao
baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, hawajapata kazi wala hawana
matuamini. Wanashinda kuzurura mitaani.
 Wafanyakazi kutimuliwa bila fidia. Mzee Makucha anafanya kazi na
shirika la reli ambalo linamtimua kwa ajili ya kupunguza idadi ya
wafanyakazi wake. Baadaye linasambaratika, hivyo anakosa
marupurupu yake.
 Umaskini. Mzee Makucha anaanguka kwenye lindi la umaskini baada
ya kuachishwa kazi katika shirika la reli bila marupurupu, kwani
shirika hilo linasambaratika pia.
 Kazi duni. Makucha analazimika kuchuuza vitafunio kando ya
barabara kujipatia riziki. Mkewe naye anauza kaimati na vitumbua
kwenye veranda ya nyumba yao.
 Kukimbilia ndoa. Riziki, anawatoroka wazaziwe na kuolewa na
Mhindi ili kuepuka urumo.
b.
i.

i. Haki ya kuishi/ jasho- hakuna hewa mgodini


ii. Ajira ya watoto- watoto wadogo na vijana kuchimba mchanga na
kusomba kwa mikokoteni.
iii. Afya – hakuna miale ya jua kwenye mgodi
iv. Kutishwa na wanyapara- walinzi katili
v. Mazingira duni
vi. Kuchimba gizani- taa za vibatari
vii. Kulala kwenye mabanda
viii. Kutoruhusiwa kuondoka- walinzi wakali, mbwa wakubwa na nyua za
stima
ix. Kukatiziwa masomo- vijana na watoto wadogo
x. Wanakusanywa barabarani kwa probox ya Makutwa
xi. Kufanywa kuwa watumwa- Sai na Dai
ii. Sabina
i. Kunyimwa haki ya kusoma- anaambiwa anaharibu mafuta na Yunuke
ii. Kukatiziwa masomo- Nyaboke kuacha shule katika kidato cha pili
iii. Ndoa za mapema – Nyaboke kukataa posa za wanaume/ Sabina
kuozwa siku ya kutangaza matokeo
iv. Kufanywa mtumwa- kazi zinazozidi umri wa Sabina/ miaka 14
v. Mavazi kuu kuu- Sabina kutoka shambani akiwa na rinda kuu kuu
vi. Mateso- matusi ya Yunuke, kumzimia taa, kumkashifu kwa kutouuza
maziwa Itumbe
vii. Kuchelewa kufika shule- anafika saa tatu na nusu
viii. Kudhalilishwa – kukama ng’ombe, kuwapeleka malishoni, kuzoa
kisonzo, kuuza maziwa asubuhi,kuandaa chajio, kuwafunga ng’ombe
zizini
ix. Kutolindwa dhidi ya hatari – watu kuambaa familia ya Nyaboke/ laana
x. Kudharauliwa na binamu zake Sabina/ Mike ndiye anambebea vitabu
wakiwa malishoni.
xi. Kujaribu kumnyima bahati kwa kumwita Mike kuhojiwa na
wanahabari.

Swali 20
Siku moja alipokataa katakata kuandamana na mumewe, jungu lilifoka. “Wewe mke sampuli
gani usiyetaka kumuunga mkono mmeo?” Haya kaa nyumbani. Kula na kulala tu, hujui
jingine. Ona umbo lako sasa, kama nguruwe. Si mke mrembo niliyeoa! Wanawake ni
wengi…”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b. Bainisha vipengele vinne vya kimtindo katika dondoo hili (alama 4)
c. Fafanua nafasi ya mwanamke katika hadithi hii. (alama 12)

Majibu

a.
i. msemaji ni Luka
ii. msemewa ni Lilia
iii. nyumbani kwao
iv. Luka alimtaka mkewe kuandamana naye katika kampeni – taswira ya kiongozi
anayethamini ndoa na familia ili achaguliwe kuwa gavana, (alama 4x1)
b.
i. Balagha – wewe mke sapuli gani?
ii. Nahau = katakata, unga mkono
iii. Taswira – ona sasa
iv. Tashbiha – kama nguruwe
v. Masimango – kama nguruwe
vi. Nidaa – niliyeoa!
vii. Mdokezo – wengi…
c. Fadhila za punda
i. Mwanamke kutawishwa- lilia anaachishwa kazi ya umeneja na mwishowe
kutawishwa.
ii. kukaa nyumbani na kutishwa asidhubutu kutoka nje ya lango.
iii. Mwanamke anatishiwa – Lilia anapodhubutu kumshtaki mumewe
anakumbushwa kuwa yeye ndiye Gavana na ana uwezo wa kufanya haki kuwa
batili na batili kuwa haki.Utajua kichomtoa kanga manyoya.
iv. Mwanamke anapokezwa kichapo cha mbwa- Lilia anapokea mapigo kutoka
kwa mumewe anapoenda kuripoti kwa polisi.
v. Mwanamke kutusiwa- Lilia anaambiwa amenona kama nguruwe.
vi. Mwanamke kudhalilishwa- Lilia annambiwa kuwa ana umbo kama nguruwe
kwani kazi yake ni kula na kulala tu.
vii. Mwanamke kuendewa kinyume na mumewe katika ndoa- Luka anasemekana
kuwa na kiruka njia ambaye waliandamana naye kila mahali. Lilia anapouliza
ni nani anapokea kipigo kinachomlaza kitandani siku mbili.
viii. Kuachishwa kazi. Lilia anaachishwa kazi na mumewe ili awe mpokezi wa
wageni nyumbani.
ix. Ni chombo cha starehe-
x. Wasaliti – kunyanganywa bwana
xi. Kunyimwa uhuru wa kutangamana
xii. Ku

You might also like