A. Pata watu kadhaa ambao utafanya nao maombi juu ya
mradi wako – shughuli yako ni vema ukaiweka mikononi mwa Mungu tangu awali. Mara nyingi tunamshirikisha Mungu tukiwa tayari katika magumu. Anza nae , endelea nae hatakupungukia hata kidogo.
II. KUTAFUTA SOKO:
A. Chagua utakachofanya au bidhaa unayotaka kuzalisha au
huduma unayotaka kutoa
1. Chagua unachotaka kuzalisha, pia fahamu WATEJA wako
2. Jua au fahamu WASHINDANI wako
3. Tengeneza BEI za bidhaa zako au huduma yako
B. Andika maelezo ya bidhaa au huduma hizo
2
1. Ainisha njia ambazo utatumia katika usambazaji wa
bidhaa zako au huduma yako
2. Ainisha faida au umuhimu wa bidhaa zako au huduma
yako utakayozalisha
III. TENGENEZA BAJETI KUONYESHA GHARAMA ZAKO ZA
KWANZA / MWANZO/ AWALI
A. Gharama za vifaa / vitu – uzalishaji wa awali
B. Gharama za vitendea kazi – kama vipo
C. Ghara za vitu vingine – kiasi kidogo
D. Gharama za nguvu kazi – pamoja na wewe mwenyewe
IV. TENGENEZA HATI YA AWALI YA MAPATO NA MATUMIZI
A. Mwaka wa kwanza – Ni muhimu sana
B. Mwaka wa pili – Ni vyema ukawa nayo
C. Mwaka wa tatu – kama ukipenda ili kupata picha ya mradi
3
V. TAFUTA FEDHA
A. Toka ndugu na marafiki
B. Mabenki yanayohudumia wateja wa kati
C. Mchango binafsi – Ni muhimu sana
D. Tengeneza mpango wa malipo
VI. TANGAZA BIASHARA / HUDUMA YAKO
A. Kwa mdomo au kwa maneno
B. Njia ya vyombo vya habari – magazeti, redio tv nk.
C. Vipeperushi – kwa njia ya urafiki katika maeneo ya biashara
VII. WEKA MALENGO NA UWEKE MUDA MAALUM
A. Weka mauzo yote katika karatasi
B. Lenga kutafuta wateja wapya – biashara ni wateja
C. Lenga kuongeza aina mpya ya bidhaa / huduma
4
VIII. OMBA NA WANA MAOMBI WENZAKO NA ANZA SHUGHULI
A. Shauriana na marafiki na wana maombi wenzako
IX. UFUATILIAJI
A. Pima malengo kama yamefikiwa
B. Pima muda uliochukua mpaka mwisho
X. SHEREHEKEA USHINDI / KUFAULU
A. Msifu Bwana kwa ushindi
B. Toa ZAKA yako – fungu la KUMI – hata kama ni 10%+