Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

RICHARD LUCIAN KILEWO

20/05/2022

ABBAS SAID MSANGI

S.L.P. 1249,

DODOMA.

+255 654 957 317

HATI YA MADAI NA DHAMIRA YA KUSHTAKI.

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

Tunakuandikia barua hii kwa niaba ya RICHARD LUCIAN KILEWO ambaye ni mteja
wetu na mkazi wa Dodoma, ambaye wewe, SHADRACK KYANDO, pamoja na
STEPHANO PETER mlimuuzia Kiwanja Na.182 KITALU “AZ” Kilichopo eneo la
Mkalama katika Halmashauri ya Jiji Dodoma na chenye ukubwa wa Mita za mraba Elfu
Moja Mia Tatu Hamsini (1350) kama ilivyo kwenye invoice na ramani iliyosajiliwa Julai
2021, ametuelekeza tukuandikie Hati hii ya madai na dhamira ya kushtaki kama
ambavyo tunafanya sasa;

Kwamba, mteja wetu mnamo Julai 2021 wewe, SHADRACK KYANDO, pamoja na
STEPHANO PETER mlimuuzia kiwanja tajwa hapo juu kwa bei ya Shilingi za
Kitanzania Milioni Ishirini (TShs.20,000,000/=) tu na alianza kufanya malipo kidogo
kidogo kutoka Julai, 2021 hadi Disemba,2021 kama makubaliano yenu yalivyokuwa.

Kwamba, tarehe 31.7.2021, 2.8.2021, 7.8.2021, 18.8.2021, 7.11.2021 na 24.12.2021 mteja


wetu alikulipa wewe, Shadrack Kyando, pamoja na Stephano Peter Kiasi cha Shilingi
za Kitanzania Milioni Mbili na Laki Tano (TShs.2,500,000/=) tu, Milioni Mbili na Laki
Tano (TShs.2,500,000/=), Shilingi za Kitanzania Milioni Nne (TShs.4,000,000/=) tu,
Shilingi za Kitanzania Laki Nane (TShs.800,000/=) tu, Shilingi za Kitanzania Milioni
Tano (TShs.5,000,000/=) tu, na Shilingi za Kitanzania Milioni Nne na Laki Mbili
(TShs.4,200,000/=) tu kwa kufuatana na fedha zote zikilipwa kuptia akaunti yako
iliyopo katika benki ya CRDB ambayo ni 0152437476000 na yenye jina la Abbas Said
Msangi.

Kwamba, mara baada ya mteja wetu kukamilisha malipo yote kikamilifu umekuwa
msumbufu na kumekuwa na mkwamo upande wako kuwasilisha nyaraka husika za
kiwanja kwa muda wa miezi saba mpaka sasa. Na Kwamba, Mteja wetu kwa vitendo
na maneno yenu ya ushirika yaliyojaa hadaa, uongo, uovu, na yenye nia ya kuhodhi,
kung’ang’ania nyaraka za kiwanja chake alichonunua kihalali kwenu vinaashiria
chembechembe za jinai na madai.

Tambua kuwa, kwa vitendo na maneno yenu ya ushirika yaliyojaa hadaa, uongo,
uovu, na yenye nia ya kuhodhi na kung’ang’ania nyaraka za kiwanja chake
alichonunua kihalali kwenu zimepelekea kukwama na kuathirika kwa mteja wetu
kiakili, kiuchumi na mipango ya malengo yake kiamii.

Na kwamba, mbali na jitihada zote alizofanya kuhakikisha anakabidhiwa nyaraka za


umiliki wa kiwanja, jitihada hizo hazikuzaa matunda. Hivyo, mteja wetu ametuelekeza
tukuandikie Hati hii ya madai na dhamira ya kushtaki kama tunavyofanya sasa ili
kukufahamisha mambo muhimu yafuatayo:-
1. Kumkabidhi Mteja wetu nyaraka za umiliki wa kiwanja tajwa pamoja
stakabadhi zote za malipo ya kiwanja husika.

2. Kumlipa mteja wetu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini


(TShs.20,000,000/=) tu ikiwa ni gharama ya mauziano ya kiwanja pamoja na
riba ya 25%.

3. Kulipa kiasi cha Shilingi za Kitazania Laki Mbili (TShs.200,000/=) tu ikiwa ni


gharama za kuandaa Hati hii.

Zingatia kwamba, tunakupa muda wa Siku Thelathini (30) kuanzia tarehe ya kupokea
Hati hii uwe umetekeleza matakwa ya hati hii na dhamira ya kushtaki. Kushindwa
kutimiza masharti ya Hati hii kutapelekea hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yako
kwa gharama zako.
Tambua kwamba umetahadharishwa.

Wako katika haki.

……….………..…………
PETER J MASHENENE
Wakili:
MASHENENE & CO.ADVOCATES

NAKALAKWA;
1. RICHARD LUCIAN KILEWO (tafadhali fika ofisini kwetu baada ya siku 30 kuisha
kwa hatua zaidi)

2. AFISA ARDHI (Eneo la Mkalama) HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA-


kwa hatua zako muhimu.

You might also like