Kijana Na Kesho Yake

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 45

KIJANA NA KESHO YAKE

ISACK.S.MASATU

2022

Kitabu hiki kimechapishwa na kudhaminiwa na

1
ISACK.S.MASATU

Email:Stephenmasatu@gmail.com

Whatsapp : 0655597525

Toleo la mwezi October mwaka: 2022

Haki zote zimehifadhiwa na ni marufuku kunakili sehemu ya kitabu hiki kwa


namna yeyote ile bila ya idhini ya mwandishi Isack.S. Masatu

YALIYOMO

2
1. Utangulizi

2. Kijana ni nani na ana Sifa gani?

3. Changamoto za ujana na jinsi ya kuzikabili

4. Mahusiano ya hisia na akili ya Kijana

5. Jinsi gani kijana Aifikie Kesho yake

6. Mwisho

7. Shukrani

UTANGULIZI

Awali ya yote ninamshukuru Mungu kwa kunipa afya njema na Baraka tele.Kitabu hiki
kimeandaliwa na Isack Steven Masatu ni kitabu kizuri sana kwa vijana wote wa

3
Tanzania na Watu wazima pia wanaweza kufaidika nacho kwa kiasi kidogo.Kutokana na
Ukweli nina mapenzi ya dhati na nchi yangu au Taifa langu teule ndani ya Moyo wangu
naandika kitabu hiki kwa lengo la kutaka kuwafumbua macho vijana wenzangu ambao
mara nyingi wanashindwa kufikia malengo yao kwa kukosa ushauri na maarifa au ujuzi
utakaowaezesha kupiga hatua.

Kitabu hiki kinachoitwa ``KIJANA NA KESHO YAKE`` kimebeba uchambuzi juu ya


kijana,changamoto zake na kwa namna gani anaweza kuzitatua ili kuweza kuziishi ndoto
zake au malengo yake.Kitabu hiki ni mwanga na taa kwa vijana wa Tanzania kwani
kitakufungulia na kukupa majibu ya maswali mengi unayojiuliza au unayoyasikia.Aidha
siandiki kazi hii kwa lengo la kutafuta pesa bali kwa lengo la kuwaelimisha vijana
wezangu wa Tanzania ili waweze kuwa imara katika kufanya kazi iendelee chini ya Raisi
wetu mpendwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasani.

Mgawanyo wa kitabu hiki hupo katika sehemu nne.Sehemu ya kwanza inaonesha Kijana
ni nani? Sifa za Kijana,Mafundisho ya ujana na Mambo ambayo Kijana anatakiwa
kufanya.Sehemu ya Pili imebeba uchambuzi juu ya changamoto za ujana na jinsi ya
kuzikabili.Sehemu ya Tatu inaonesha mahusiano ya hisia na akili ya Kijana pamoja na
hisia za kimapenzi kwa kijana.Sehemu ya nne inaelezea Jinsi gani Kijana aifikie kesho
yake.

SEHEMU YA KWANZA

KIJANA NI NANI NA ANA SIFA GANI?

A.Kijana ni nani?

Wapo wengi ambao wanajiita vijana bila ya kujua maana halisi ya kijana na kutambua
wana sifa na uwezo gani? Ila wapendwa,Kijana ni mtu yeyote Yule aliyepo kati ya

4
kipindi cha utoto na utuuzima kwa makadirio ya miaka ni kati ya miaka 18 na 40.Tambua
ya kuwa katika maisha mwanadamu anapita katika vipindi vikuu vinne(4) ambavyo ni;-

 Utoto,hapa mwanadamu anakuwa kati ya miaka 0 hadi 17,ambapo katika kipindi


hiki mwanadamu anakuwa na hisia za chini sana hivyo ni vigumu kwake kuweza
kuishi katika hisia.Hata hivyo katika kipindi hiki mwanadamu anakuwa na uwezo
mdogo wa kupambanua jambo zuri na baya.
 Ujana,Katika kipindi hiki mwanadamu huwa kati ya miaka 18 hadi 40 na
anakuwa na hisia kali ambazo huzitawala akili zake.Wakati huu kijana huwa
anatamani kufanya maamuzi yake.
 Utuuzima,kipindi hiki huanzia kati ya miaka 41 hadi 55 ambapo mwanadamu
anakuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha seli na hata hisia zake zina anza kushuka.
 Uzee,kipindi hiki huanzia kati ya miaka 56 na kuendelea.Hapa mwanadamu
anakuwa hana tena hisia au matamanio ndani ya mwili wake.Hata hivyo nguvu za
kiakili,kiroho na kimwili zinapungua kwa kiasi kikubwa.

Kila kipindi ambacho mwanadamu anapitia kina mambo yafuatayo;-

 Sifa zake
 Changamoto zake
 Mafundisho yake
 Kuna mambo yanayopaswa yafanyike katika hiko kipindi
 Kina mambo yake

Hata hivyo kuna changamoto ambazo kijana upitia,mafundisho ambayo kijana anatakiwa
apatiwe,mambo ambayo anapaswa kufanya kwa nyakati hizo na mambo yake.Watalamu
wa Kiswahili wanaeleza kuwa neno Kijana limetokana na Muunganiko wa Ki na
jana,ambapo tukichukua neno jana maana yake ni siku iliyopita kabla ya leo.Hivyo kijana
pia anaweza kuelezewa kama ni Mtu aliyeinuka jana hivyo anatakiwa kujifunza mengi
lakini kwa uangalifu mkubwa vinginevyo anaweza kupotea.

Baiolojia inaeleza kuwa kijana ni Yule mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha
seli mbalimbali kwa haraka,ambapo kibailojia tunapata kujua kuwa kijana huanza kati ya
miaka 14 hadi miaka 40.Katika kipindi hiki mwanadamu anakuwa na uwezo mkubwa wa
kuzalisha vichocheo mbalimbali vya mwili na ubongo wake huanza kupanuka na kutaka
kujifunza mambo mengi zaidi na uhitaji muongozo mzuri.Hivyo kijana anatakiwa
apatiwe ushauri mara kwa mara pale anapokosea ili asije akaona kile alichokifanya
hakina athari kumbe zipo.Kijana yeyote Yule na awe mwangalifu.

B.Sifa za Kijana

Wakati nikiwa na umri wa miaka 15,Bibi alikuwa akipenda kuniambia kuwa nimekuwa
kijana.Nilikuwa siku zote najiuliza kuwa kijana ana sifa zipi? Na kwa nini ananiita mimi
kijana? Maswali yangu hayakuwa na majibu mwisho niliamua kufanya tafiti na kuja na

5
majibu ambayo yataweza kuwasaidia vijana wenzangu ambao hawajapata kujua wana sifa
gani.Kijana anakuwa na sifa kuu mbili ambazo wengine uzichambua na kuzalisha sifa
nyingine nyingi,ambapo kimsingi kijana anatambulika kwa kutumia sifa zifuatazo na si
vinginevyo;-

1. Kijana huwa na Nguvu nyingi


2. Kijana huwa na hisia kali

Natamani uzitambue sifa hizi kwa undani zaidi ili uweze kujitambua wewe mwenyewe,au
mtoto wako au ndugu yako.

1.Kijana huwa na Nguvu nyingi

Nguvu maana yake ni uwezo wa kufanya kitu au kazi Fulani katika kiwango
kinachotakiwa na kwa ufanisi.Kijana huwa na sifa ya kuwa na uwezo mkubwa wa
kufanya kazi kwa muda mrefu bila ya kuchoka hii ni kwa sababu mwili wake unazalisha
seli ambazo zinaratibu shuguli mbalimbali katika mwili ikiwemo kuchochea ongezeko na
uimara wa misuli itakayofanya awe na nguvu.Utakubaliana nami kuwa kijana ana nguvu
lakini nguvu hizo zipo katika makundi makuu matatu ambayo ni;-

 Nguvu za Kiakili
 Nguvu za Kiroho
 Nguvu za Kimwili

Nguvu za Kiakili,Kijana huwa na uwezo mkubwa sana wa akili yake kufanya kazi kwa
ufanisi kama akiweza kuitumia vizuri na katika kufikiria jambo Fulani au kuhifadhi kitu
Fulani katika akili yake kwa haraka.Kwa ushahidi au uhakika kijana anaweza akasikia
nyimbo ya Diamond,Zuchu,Zabron singers au Rose Muhando na akaweza kuishika kwa
muda mfupi sana jambo ambalo ni gumu kwa mtu mzima na mzee au mtoto.Kijana huwa
na uwezo mkubwa sana wa kiakili lakini itategemea uwezo huo anataka autumiaje na
ndio maana kuna mtu anajua nyimbo nyingi kichwani lakini kushika mada za mitihani
kashindwa hii ni kwasababu akili yake ameielekezea katika mziki na sio darasani.

Nguvu za Kiroho,huu ni uwezo wa kufanya huduma mbalimbali za Mungu kwa ufanisi


na uwezo wa hali ya juu.Kijana amebarikiwa pia kuwa na uwezo mkubwa wa
kuomba,kuhubiri,kufundisha na kufanya mambo mbalimbali ya kidini.Ni rahisi sana
kijana kucheza dufu,kuswalisha,kuhubiri kwa muda mrefu bila ya kuchoka jambo ambalo
haliwezekani kwa mzee na ndio mana mtume alipewa kazi yake akiwa bado kijana na
kwa Yesu pia ilikuwa hivyo.

Nguvu za Kimwili,kijana pia huwa na uwezo mkubwa ndani ya mwili wake wa


kunyanyua,kuhamisha hata kuzuia kitu Fulani.Mfano kijana ana uwezo wa kupigana au
kubeba kitu kizito bila hata kuchoka kwa haraka kama mtoto,mtu mzima na mzee.

6
2.Kijana Huwa na Hisia Kali

Hii ni sifa kubwa ya kijana anayokuwa nayo,hapa kijana anakuwa ni mtu wa kuongozwa
na hisia zaidi katika kila anachofanya.Kwa sababu ya hisia kijana huanza kujihisi ya
kwamba amekuwa na baada ya kujiona amekuwa,anataka kufanya maamuzi mengi ya
maisha yake na hapo ndipo wazazi huchanganyikiwa,na kama wasipokuwa imara
wanaweza kupelekeshwa na watoto wao.Hata hivyo,kutokana na hisia kijana huanza
kujiona yeye ni mjanja sana kuliko hata wazazi wake hali inayomfanya ajifunze vitu vingi
sana na kujaribu kila anachokiona na ndicho kipindi ambacho mtu huishi maisha ya
kuigaiga.Hii ni kwa sababu ametoka utoto na anaanza kuiona dunia sasa,hivyo anaona
kila kitu kwake kipya na kutaka kujifunza kitu hicho.

C.Mafundisho ya Ujana

Kama ilivyo kawaida kuwa kila kipindi ambacho mwanadamu hupitia huwa na
mafundisho yake.Hata hivyo kijana pia anatakiwa kupatiwa mafundisho yake ili aweze
kujikinga na kujilinda mwenyewe hata kuzalisha kipawa au kukiibua akiwa bado kijana
kabla hakija potea au kufa.Mafundisho hayo ni kama vile;-

 Mafundisho ya Kiroho,kijana anatakiwa apatiwe mafundisho ya kiroho kwani


yeye ana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo ya kiroho.Hapa Watumishi
wa Mungu wanatakiwa kutoa semina za mara kwa mara kwa vijana ili kuweza
kuwalinda na kuwakinga.Aidha kijana anatakiwa kuhudhuria katika ibada na
mikutano ya Kiroho au semina za Kiroho ili kuweza kujifunza mengi kuhusu yeye
na dunia inayomzunguka.

 Mafundisho ya kielimu,hapa kijana anatakiwa kwenda shule na kuwa na juhudi


nyingi katika kusoma.Elimu anayotakiwa kupatiwa kijana ni ile inayomuhusu kwa
wakati huo mfano Elimu ya msingi,sekondari au vyuo pamoja na elimu ya afya
ya uzazi itakayo mwezesha kujilinda dhidi ya ngono zembe na magonjwa ya
zinaa.Elimu ndiyo itatoa mwanga juu ya maisha ya kijana kuwa yatakuwaje,na
kupitia elimu kijana ataweza kufanya mambo mengi kwa usahihi.
 Mafundisho ya Kijamii na Uchumi,Kijana pia anatakiwa kupewa mafundisho
juu ya jamii inayomzunguka inataka yeye aishije na namna ya kuweza kuendana
nayo bila ya matatizo ikiwemo kujua ni changamoto gani zinaikumba jamii hiyo?
Lakini pia wakati wa ujana pia mtu anatakiwa kufundishwa mbinu au namna ya
kuweza kuandaa uchumi wake pamoja na namna ya kuyandaa maisha yake ya
utuuzima yaje kuwa mazuri

D.Mambo ambayo Kijana anatakiwa kufanya

7
Yapo mambo ambayo kijana anatakiwa kufanya katika kipindi cha ujana wake,mambo
hayo ni;-

a. Kuishi na Watu Vizuri Katika Jamii

Kijana anatakiwa kuishi na watu vizuri ili ajenge mazingira ya kukubalika katika
jamii.Hii itamfanya kijana apate Baraka za Wanajamii pamoja na neema nyingi kutoka
kwao.Vijana wengi wameshindwa kwa kiasi kikubwa kuishi na jamii vizuri au watu
vizuri.Inafikia hatua badala ya kupendwa na kuwa chachu ya maendeleo katika
jamii,jamii inawachukia vijana kwani wamekuwa chanzo cha kutokufanikiwa kwa
jamii.Vijana katika jamii wamekuwa Vibaka,Wizi,Walevi,Wanyang’anyi na mzigo
mkubwa katika jamii unaopelekea kukwamisha maendeleo ya Taifa letu teule la Tanzania.

Nitakuwa nalikosea sana Taifa langu la Tanzania,kama nikikuacha bila ya kukwambia


wewe kijana mwenzangu kanuni na mbinu muhimu za kuishi na watu vizuri.Kwa mujibu
wa Isack Masatu inaonekana kuna kanuni na mbinu 24 zitakazomwezesha kijana aweze
kuishi na Watu vizuri katika jamii inayomzunguka.Kanuni na mbinu hizo ni kama
ifuatavyo;-

i. Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya


ii. Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu
iii. Shukuru kwa kila jambo jema linapotendeka
iv. Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya
kumsaidia na kumjenga
v. Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe
vi. Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu
vii. Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe
watakupenda
viii. Heshimu kila mtu,na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana
ix. Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake hata akiwa ni masikini n.k
x. Usiseme uongo
xi. Zungumza kufuatana na mambo ambayo mtu anayoyapenda
xii. Usiwe mzungumzaji sana bali kuwa msikilizaji
xiii. Kumbuka majina ya watu unaokutana nao
xiv. Usiwe mwepesi wa hasira
xv. Tunza siri zako na za wengine
xvi. Jipende na kujikubali
xvii. Usiwe unachonganisha watu
xviii. Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote
xix. Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki
xx. Usilipize kisasi bali tenda wema kwa aliyekukosea
xxi. Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu
xxii. Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu
xxiii. Usipende mabishano na kama yakitokea usitake kila mara kushinda
xxiv. Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu wakubwa

8
Nakusihi sana kijana mwenzangu,zingatia sana haya katika kuhakikisha unaishi vizuri na
watu katika jamii.Lakini tambua wapo watu utafanya yote hayo lakini bado hawatataka
kukupenda,kimsingi hawakosekani lakini kwanza watakuwa wachache sana na chuki zao
binafsi,lakini pili wewe usijali endelea kuziishi kanuni hizo siku zote za maisha yako
katika jamii.

b. Kuuthamini Ujana wake


c. Kuwa Mcha Mungu (Mtauwa)

SEHEMU YA PILI

CHANGAMOTO ZA UJANA NA JINSI YA KUZIKABILI

Wapo watu wengi na wa rika mbalimbali ambao hukabiliwa na changamoto mbalimbali


lakini nimefanya tafiti kwa muda sasa kwa kujitazama mwenyewe Isack Masatu na
vijana wenzangu akiwemo Joyce Joseph.Sasa kwa uchungu na hisia kali nataka kila
kijana azijue changamoto hizi zinazotukumba katika kipindi hiki cha ujana na tutawezaje
kuzikabili. Zijue changamoto zinazomkabili kijana kama ifuatayo;-

1.Kuenenda na Wakati

Vijana wengi sana wanakabiliwa na changamoto ya kutaka kuenenda na wakati katika


njia ambayo si sahihi.Kijana huvutiwa sana na kushawishika kuenenda na wakati katika
maeneo yafuatayo;-

 Kuvaa,hapa kijana huwa na kiu ya kutaka kuvaa nguo za kisasa hata kama
zinachochea mmomonyoko wa maadili mfano kuvaa modo au nguo za kubana
wakiamini kuwa wanaenda na wakati
 Kusuka,pia kijana huwa na tabia ya kutaka kusuka mitindo mbalimbali bila ya
kujali gharama na kupelekea wasichana kupoteza pesa nyingi katika kusuka kila
baada ya muda mchache.Hii inapelekea kutokuwa na maendeleo
 Kunyoa,Vijana hupenda kunyoa denge au kiduku na mitindo mingine ambayo
wanaamini ni ya kisasa,ambapo huwa na gharama na haina faida kwao
 Kutembea,Vijana hupenda kuiga miondoko ya kutembea mitandaoni na kwa
wasanii,hali inayopelekea kuanza kuiga tamaduni za kigeni mfano kudunda n.k
 Kusema,Kijana pia hupenda kuiga namna ya kuongea au kusema kulingana na
wakati huo,watu wengi wanaongea kwa namna gani kama vile kubana sauti
 Kutenda sawa na wakati,vijana wengi wanataka kila wanachokifanya kiwe
kinaendana na wakati huo bila ya kujali kina madhara gani
 Kumiliki vitu vinavyoenenda na wakati,kama vile smartphone,gari na
kompyuta hali ya kuwa hawana uwezo navyo au hawajui thamani yake

9
Namna ya Kuikabili

Ili kijana aweze kuepukana na changamoto ya kuenenda na wakati,ipo haja ya kijana


kuukomboa wakati katika kila nyanja za maisha yake.

Kuukomboa Wakati,maana yake ni kuutumia vizuri wakati tuliopewa kama fursa ya


pekee.Wakati wa ujana ndicho kipindi muhimu,ambapo mwanadamu anatakiwa
kukitumia vizuri katika kuyaandaa maisha yake.Ipo haja ya kijana kuutumia wakati au
muda vizuri katika nyanja zifuatazo;

 Ki-elimu,kijana unatakiwa kuwekeza katika kusoma kwa bidii ili kufikia malengo
yako uliojiwekea katika elimu
 Ki-uchumi,Kijana anatakiwa ahakikishe kuwa anatumia vizuri wakati wake kwa
kufanya mambo yatakayoimarisha uchumi wake
 Kiroho,Kijana anatakiwa kutumikia muda wake katika maisha ya kiimani kwa
kumtumikia Mungu,kwani yeye ananguvu sana za kufanya huduma za ki-
Mungu.Hii itamfanya awe na maisha ya furaha na amani ya Mungu duniani

Ninakusihi sana wewe kijana wa Tanzania,ipo haja ya kuukomboa wakati wako katika
nyanja zote ili tuweze kuleta maendeleo katika Taifa letu pendwa la Tanzania.Hakika
mafanikio yako yamebebwa na uwezo wako wa kutumia muda vizuri.Katika tafiti ya
Isack Masatu anakuja na imani anayoiweka na kuwa uhalisia ambapo anasema
``Right time consuming makes success`` ikiwa na tafsiri ``Matumizi sahihi
ya muda hutengeneza mafanikio``

Ukifuatilia historia ya watu wakubwa duniani au waliofanikiwa katika nyanja tofauti


tofauti utagundua kuwa chanzo cha mafanikio yao ni kuutumia muda vizuri katika
kutafuta wanachokitaka.Nakusihi sana wewe kijana anza kuutumia muda wako vizuri
sasa katika kutafuta kile unachokitaka kama unahitaji kufanikiwa.

2:Kupenda Anasa na Starehe

Anasa maana yake ni raha na starehe au kitu kisichokuwa na faida katika maisha ya
mwanadamu kama vile vigodoro na utumiaji wa pombe.Starehe ni hali ya kutokuwepo
kwa shida wala usumbufu wowote,raha,furaha,anasa,amani na utulivu.Vijana wengi
wanapenda kufanya mambo ya anasa na kuishi maisha ya starehe bila ya kuwa na sababu
za msingi.Utamkuta Kijana anapenda kwenda kwenye kumbi za starehe na makasino
kufuata mambo ya anasa tu.Hii inakwamisha mafanikio ya vijana wengi kwani
wanajisahau sana kuwa wanatakiwa watafute maisha yao.

Namna ya Kuikabili

Vijana hatuna budi kuachana na mambo ya anasa na starehe kwa kuhakikisha tunakuwa
bize katika kutafuta maisha yetu ya mbeleni.Tuache kusikiliza vishawishi vya watu na
kuiga ujinga ambao unaweza kusababisha kujiingiza katika anasa na starehe zisizo za

10
msingi,na zitakazoweza kufanya ushindwe kufikia mafanikio yako.Fanya mambo kwa
faida ya maisha yako na usipende kuonekana_onekana na watu.

3.Tamaa za Ujanani

Hili ni tatizo linalowakumba zaidi ya asilimia 95% ya vijana wa Tanzania na wa


Afrika.Moyo wa kijana huwa umebeba matamanio kwa kiasi kikubwa kwani uhai wa
milango yake ya fahamu ni tofauti kabisa na rika nyingine.Hata hivyo kijana huwa na
hisia kali sana kuliko rika nyingine zote hii ni kutokana na mabadiliko ya kibaiolojia
ndani ya mwili wake.Hivyo basi kijana akiona,akisikia,akinusa,akihisi au akilamba ni
rahisi sana kutamani.Vijana wengi wamejawa na tamaa za kimapenzi hali inayopelekea
kushindwa kuendelea kiuchumi na kielimu,kwa kutumia muda wao mwingi katika
kufikiria ngono.Tamaa za mwili husababishwa na kijana kushindwa kuzitawala hisia
zake.Katika kipindi hiki Mvulana anaweza kuwa na wasichana zaidi ya wanne bila ya
kujali miaka yao wengine wanaweza kuwa ni wakubwa kuliko yeye au wadogo sana hata
msichana naye anaweza kuwa na wavulana zaidi ya wanne bila ya kujali umri.Hii ni kwa
sababu kila msichana anayepita mvulana atamtamani na kila mvulana anayepita msichana
atamtamani na katika kipindi hiki kukataa kufanya mapenzi au kuwa katika mahusiano
inakuwa ni kazi ngumu sana kwa kijana.

Namna ya Kuikabili

Kwa kuzingatia ukweli kwamba tamaa za ujanani ni matokeo ya mtu kushindwa kutawala
hisia zake na kuishi kwa matamanio,ni lazima kijana ahakikishe kuwa anatawala hisia
zake pamoja kukataa matamanio ya moyo.Hii inawezekana kupitia kuwa bize,kuwa
mtakatifu,kuepuka marafiki wabaya pamoja na vishawishi vyao.Siku zote siri ya
mafanikio ipo ndani ya hisia zako,kupitia hisia unaweza kushinda kila jaribu au kupitia
hisia ukajikuta unashindwa,hivyo basi kamwe usiruhusu hisia zikutawale.

4:Utandawazi

Utandawazi ni mfumo wa mawasiliano rahisi unaoziwezesha nchi nyingi duniani


kuwasiliana na kushirikiana katika masuala ya biashara,siasa na teknolojia kwa njia ya
mtandao uliounganishwa kwenye kompyuta,aipadi au simu.Utandawazi unajumuisha na
intaneti,Vijana wengi wanaathiriwa na matumizi mabaya ya simu kubwa,aipadi au
kompyuta kupitia intanenti au mtandaoni.Intanenti inaonekana haina maana kwa sababu
vijana wengi wanaitumia vibaya katika kutafuta mambo yasiyofaa,kwa maisha yao na
kutumia muda mwingi bila ya kuwa na sababu ya msingi.Hapa utamkuta kijana,kisa ana
simu kubwa wakati wote ana post picha au video zisizo na msingi mtandaoni bila ya

11
kufikiria kwa undani matokeo ya picha au video ambayo amevituma.Au utamkuta analike
na kukomenti picha za ngono na video za ngono pamoja na kuzidownload kwenye
simu,aipadi au kompyuta yake.Hii inapelekea mmomonyoko wa maadili kwa
kijana.Wazazi wamefikia wakati hawataki kuamini kuwa simu hazina madhara kwa
mtoto makini,mimi nimeanza kutumia simu kubwa nikiwa darasa la pili hadi sasa na
hakuna madhara yoyote niliyoyapata.

Namna ya Kuikabili

Njia pekee ya kuikabili changamoto hii ni kuwa na hekima na busara katika matumizi ya
mitandao yaani utandawazi au intanenti,iwe chachu ya kufanya tujue namna ya kufikia
malengo tuliojiwekea na kupata taarifa mbalimbali.Hakikisha unapotumia simu,aipadi au
kompyuta kwa kufungua intaneti basi unakuwa na sababu ya msingi nay a maana kwako
na usipoteze muda mwingi bila ya faida yoyote.Aidha kuwa mjanja wa kutumia intanenti
kwa faida ya maisha yako ya mbeleni.Epuka kufuatilia mambo yasiyo ya msingi na
lazima kwako.

SEHEMU YA TATU

MAHUSIANO YA HISIA NA AKILI YA KIJANA

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa hivi karibuni na Isack Masatu inaonesha kuwa kuna
uhusiano wa karibu kabisa kati ya hisia na akili ya kijana.Kwanza tuangalie maana fupi
ya akili na hisia.

Neno hisia huwa na maana nyingi sana kwa kila msomi lakini kwa maana rahisi kabisa
Hisia ni mihemko inayotokea ndani ya mwili wa mwanadamu.Awali ya yote
nilikuwambia kuwa,mwanadamu huwa anapitia vipindi vikuu vinne vya ukuaji katika
maisha,katika vipindi vyote hivyo ni kipindi cha ujana pekee ambapo mwanadamu huwa
na mihemko hiyo kwa kiasi kikubwa zaidi.Hii ni kwa sababu katika kipindi cha ujana
mwanadamu huwa na uwezo wa kuzalisha homoni zinazoweza kuchochea hisia ndani ya
mwili.Pamoja na ukweli kwamba kila kijana huwa na hisia nyingi sana lakini hisia hizo
haziwezi kuibuka bila ya kuchochewa.Lakini pia unaweza ukaeleza Hisia maana yake ni
matamanio ya kitu baada ya kuona,kusikia,kufanya au kukumbuka au kutafakari juu ya
jambo Fulani.Matamanio hayo huleta vichocheo vya hisia katika mwili.

12
Uzuri na ubaya wa hisia unaweza kuonekana juu ya kile mtu anachokitamani katika
kufanya au kuwa nacho.Hisia zinaweza kutawala akili ya mwanadamu na kumwendesha.

VICHOCHEO VYA HISIA

Hali ya mwili kutamani kitu Fulani huwa haiji hivi hivi bila ya kuchochewa na mambo au
vitu Fulani kupitia mchakato maalumu ndani ya mwili,hisia zinaweza kuamshwa au
kuchochewa na mambo yafuatayo;-

a) Kuzitafakari Hisia za Mwili

Mara nyingi kijana anapokaa anapenda sana kutafakari jambo ambalo linaleta msisimko
wa mwili ambao huchochea kutokea kwa hisia mfano unakuta kijana anatafakari hivi
kwanini Juliana ananichekea chekea sana? Au Hivi kwanini Devi
anapita mara kwa mara nyumbani kwetu?

b) Kusoma Makala za Mapenzi

Uhalisia wa vijana wengi ni kusoma vitabu au makala zinazohusu mambo ya


mapenzi.Kijana anaposoma makala za mapenzi anapata hisia au matamanio ndani ya
mwili,maana uhai wa mihemko ya mwili huchochewa kwa haraka zaidi kupitia milango
ya fahamu ambapo hapa kijana hutumia macho kusoma hizo makala.Hali inapelekea pia
kuchochewa kwa hisia

c) Kutazama Kanda za Ngono

Kijana anashawishika sana katika kutazama kanda za ngono kama vile kanda za X
ambazo humfanya kijana kuzalisha homoni kwa haraka zitakazochochea hisia ndani ya
mwili.

d) Mazingira hatarishi

Pindi vijana wanapokutana au kukaa jinsia mbili tofauti katika mazingira ambayo ni
hatarishi,kama vile vichochoroni,chumbani au mahali popote ambapo pametulia peke yao
kwa muda,hii pia uchochea hisia ndani ya mwili kwa haraka zaidi.

e) Mavazi

Mavazi pia ni kichocheo kizuri tu cha hisia kwa kijana.Wasichana ndio hasa huelezewa
hapa pindi wanapovaa mavazi yasiyo na stara,hatarishi na yakuvutia wavulana
kimapenzi,mfano kuvaa sketi au gauni fupi au nguo yoyote inayobana hii pia hupelekea
kuchochewa kwa hisia ndani ya mwili.

f) Zawadi

Kwa kawaida unaweza kusema kuwa zawadi ni kitu cha kawaida lakini mtu anapotoa au
kupokea zawadi huweza kuleta hisia kali ndani ya mwili wake.Zawadi huangalia

13
nimepewa au kupokea zawadi ya thamani gani,mara ngapi na kwa kiasi gani.Kijana huwa
na tabia ya kumkumbuka mtu aliyempa au kupokea zawadi hasa wakiwa jinsia mbili
tofauti.Hali hii huweza kuamsha hisia za kijana.

g) Mikao ya Picha

Pindi vijana wawili wenye jinsia tofauti wanapopiga picha katika mikao hatarishi,kama
vile kugusana,kujitega au kukumbatiana na mengineyo ndani ya hiyo picha,na ikiwa watu
hao si ndugu,basi picha ambayo watapiga kwa mikao hatarishi kama hiyo itakuwa ni
kichocheo kizuri cha hisia.

h) Kushikana

Ngozi ndio kiungo muhimu sana katika mwili wa kijana ambacho ndicho kinauwezo
mkubwa sana wa kuchochea hisia za kijana.Hivyo basi,pindi vijana wawili wenye jinsia
tofauti wanapogusana wana huwezo mkubwa wa kuchochea hisia hasa wakiwa si ndugu
au marafiki wa karibu.

i) Kuongea mambo yanayohusu ngono

Vijana wanapokutana na kuongea stori kuhusu maswala ya ngono mfano unaweza


kuwakutana vijana wawili wa kiume wakisema `` Oya Yule mwanamke fundi,mmh! Kila
anapoenda anazungusha`` ,au vijana wa kike ``Shoga yangu,unajua Yule kaka wa jana
kumbe ni fundi sana na mjuzi wa mambo.Nimempenda bure hata sitaki pesa yake kwa
staili ile`` Hii inaweza kuchochea kwa kiasi kikubwa hisia za kijana.

Jiulize

 Akili maana yake ni nini?


 IQ maana yake ni nini?

AKILI NA IQ

Akili ni uwezo wa kujifunza,kuelewa na kutafakari kitu au jambo Fulani kwa usahihi


zaidi.Kiuhalisia mtu mwenye akili ni Yule mtu anayefanya kitu kwa usahihi zaidi.IQ
{Intelligence Quotient} huu ni uwezo wa kutafakari au kufikiria juu ya kitu Fulani na
kukitolea ufumbuzi.Ndani ya ubongo wa mwanadamu kuna IQ na Akili,Mtu anaweza
akawa na akili nyingi sana mfano msomi au mwanafunzi ambaye mnaamini kuwa ana
akili darasani, lakini mtu huyohuyo anaweza akawa anafanya mambo ya ajabu sana
mpaka mkawa mnashangaa lakini yote hayo hutokea kwa sababu ya kuwa na uwezo
mdogo wa kufikiria na kutafakari katika ubongo au IQ.Hata hivyo Mtu anaweza akawa
na IQ kubwa lakini hana akili mfano unaweza ukamwona mtu Fulani hana akili darasani

14
kwani kila mtihani yeye anapata sifuri lakini akiwa katika mambo mengine tofauti na
darasani anafanya kwa ufasaha zaidi mambo yote hayo tunasema ana IQ kubwa lakini
akili yake ni ndogo.Au unaweza ukaona mtu kichaa lakini hatembei uchi huyo tunasema
sawa hana akili lakini ndani ya ubongo IQ yake bado ipo vizuri.

Swali

 Kuna mahusiano gani kati ya akili na hisia za Kijana?

Mahusiano kati ya Akili na Hisia za Kijana

Mara nyingi nilikuwa nikiwasikia Walimu wangu wa shule ya Sekondari pamoja na


Mama Mchungaji Esther Manyama kuwa Isack ukiwa na hisia za kimapenzi au hisia
zozote zile kali tofauti na hisia juu ya kusoma basi utafeli au ufanisi wa akili yako
utapotea.Nilikuwa na maswali mengi sana nikijiuliza bila ya majibu kama vile kuna
mahusiano gani kati ya akili na hisia za mwanadamu na kivipi akili ya mwanadamu
huweza kuathiriwa na hisia zake.Baada ya miaka kupita nikagundua kuwa upo ukweli
ndani ya maneno yao kwani vijana wengi wa shule huanza kupotea pindi wanapoingia
katika mapenzi na hupoteza ndoto zao.

Kutokana na upendo mkubwa nilionao na uchungu wa Taifa langu niliamua kufanya tafiti
kuweza kubaini mahusiano yaliyopo kati ya akili na hisia za kijana.Leo nataka nikupe
haya wewe kijana mwenzangu uyatambue.

Kibaiolojia Hisia huzalishwa na homoni,ambazo ndizo zinazohusika katika kuchochea


hisia na kuzalisha,lakini ili hisia zitokee ni lazima mtu ahusishe akili au ubongo kwani
akili itampa mtu uwezo wa kuelewa na kutafakari kile ambacho
amekiona,amekisikia,amekinusa,amekilamba au amekila ambapo matukio hayo matano
ambayo kwa pamoja uhusisha milango ya fahamu ndiyo yanayopeleka taarifa katika akili
iliyopo katika ubongo wa mwanadamu na hapo mwanadamu huchambua na kuelewa
kimenigusa nini au nimeona nini.Kama mtu huyo ameona,amesikia,amenusa,amelamba
au amekula kitu ambacho ni kizuri na kinamvutia ndani ya moyo wake basi ataanza
kukitamani.Hivyo kama ni mdomo ndio umeonja basi utajaa mate kuonesha unataka tena
au kama ameona mvulana au msichana mrembo homoni zitaratibu msisimko wa damu

15
kuelekea kwenye uume au uke wa mwanadamu na kimiminika chepesi kinaweza kuwa
maeneo hayo.Hapa waswahili wanasema mvulana Yule kadisa ikiwa na maana uume
umesimama.Hisia zinaweza kuja wakati ndiyo anamuona huyo mtu au unakutana nae na
kuongea naye au kufanya naye mapenzi au baada ya kumaliza kukutana nae na kuongea
naye au kufanya naye mapenzi.Ila cha kuzingatia ni kuwa huyo utakayekutana naye ni wa
jinsia tofauti nawe na si ndugu yako wala rafiki yako wa karibu.Hivyo tunaona akili
inahusika katika kuchambua taarifa zilizoletwa na milango ya fahamu
( Macho,Pua,Mdomo,Ngozi na Sikio) na baadae uruhusu kuzalishwa kwa hisia.Hayo ndio
mahusiano yaliyopo kati akili na hisia za kijana.

Swali

 Kivipi hisia zinaweza kutawala akili ya Kijana?

Namna Hisia zinavyoweza kutawala Akili ya Kijana

Pale ambapo kijana anapotamani kufanya kitu Fulani au kukutana na mwanamke mara
kwa mara hujenga mazoea ndani ya akili yake.Labda kila asubuhi yeye huwa na wakati
wa kukutana na mtu Fulani au kila wiki ushiriki katika ngono na msichana Fulani.Hii
huwa kama ndio hali yake ambayo hujengeka na kuwa tabia yake.Mwanzoni ataona kuwa
ni kitu cha kawaida,lakini itafikia wakati akikosa kufanya au kwenda anapoenda mara
kwa mara anakuwa anafikiria sana na mara nyingine kile anachokifanya kwa kiasi
kikubwa kinabaki kama kumbukumbu katika akili yake.Hivyo basi akiwa amekaa tu bila
ya kazi yoyote inayohitaji umakini,anaanza kufikiria ile tabia yake au mtu wake.Hapa
ndio wakati ambapo kijana anaanza kupoteza malengo yake kwani anakosa kabisa muda
wa kutafakari juu ya maisha yake,na katika hatua hii hataki hata kushauriwa kinyume na
vile anavyotaka,huwa anahisi kuwa kile anachokifikiria ndiyo sahihi au kile
anachokifanya ndiyo sahihi.

Kwa kiasi kikubwa akili yake huwa imebeba hisia kali juu ya huyo mtu au hicho
kitu,kama ni Mvulana hapo kutwa anawaza juu ya msichana wake na kama ni msichana
naye kutwa anamuwaza mtu wake.Hii inapelekea kijana kuanza kuwa na mawazo mengi
pindi anapokaa peke yake,na kila atakachokifikiria atakuwa anakijengea namna ya
kufanana na mchumba wake au kitu ambacho anahisia nacho sana .Hali hii huathiri akili
yake kwani kila anapotaka kufikiri ndani ya akili yake yanakuja mawazo ya kile kitu au
Yule mtu ambaye anahisia naye au mpenzi wake.Mwisho ushindwa kuwa na mawazo
mazuri na ya mbali.

Hisia za Kimapenzi Kwa Kijana

Waswahili wanasema ``Uchungu wa mwana aujuae mzazi`` hii ni kweli kabisa


kwani matatizo ya kijana anayeyajua ni Yule aliyekuwa kijana au aliyepo ujanani.Mimi
ni kijana mdogo sana hivyo najua nini ambacho kijana kinaweza au kina mkuta katika

16
maisha yake.Najua sasa unajua hisia ni nini? Ila nataka ni kuelezee juu ya hisia za
kimapenzi kwani hili limekuwa janga kubwa linalotafuna vijana ndani ya Tanzania na
hata Dunia kwa ujumla.Kutokana na vichocheo nilivyovitaja hapo juu kijana anaweza
kuingia katika hisia za kimapenzi na kama asipoweza kujitawala mwenyewe atajikuta
anafanya mapenzi bila hata ya stara.Mfano unakuta mvulana mmoja ana wasichana
watano au saba mtaani au msichana mmoja anatembea na wavulana zaidi ya watatu au
wanne kwa wakati mmoja.Hii ni kwa sababu ameshindwa kuzitawala hisia zake kama
kijana.Jambo hili linawakumba sana vijana wa shule za sekondari,vyuo vya kati pamoja
na vyuo vikuu.Mwanafunzi akishafika kidato cha pili au cha tatu anataka kuanza kujaribu
kutongoza au kutongozwa.Mara nyingi wavulana ndiyo wanaokuwa wachokozi katika
jambo hili,kwani hisia za mvulana zinaweza kujichochea zenyewe kwa haraka kuliko za
msichana ambapo msichana hadi zishtuliwe.

Hii inapelekea kijana kushindwa kuwaza juu ya maisha yake ya mbeleni na kuanza
kuwaza juu ya mapenzi.Hapa utakuta kijana muda wote anataka kuchati,kulike,kucoment
au kuangalia picha za ngono.Tafiti niliyoifanya mwaka 2020 ilibainisha kuwa vijana
ndiyo waliosababisha kuletwa kwa mikanda,makala na picha za ngono mitandaoni na
ndiyo wadau wakubwa sana.Mwingine anajiingiza katika mapenzi kwa sababu ameona
Fulani akifanya au anataka aonekane na yeye pia ana mpenzi.Kijana unapaswa kutambua
kuwa katika mapenzi kuna watu wa namna mbili kwa mujibu wa tafiti yangu.

Mtu wa kwanza ni Yule ambaye anaweza kuingia kwenye mapenzi na asi athiriwe na
chochote kiakili au kuendeshwa na hisia,hata akiwa na wasichana au wavulana
wengi.Hapa namaanisha kuwa awezi kupoteza muda mwingi kufikiri juu ya mpenzi
wake.Watu hawa jina lao ni SHEKIS.Watu kama hawa wapo wachache katika jamii zetu.

Watu wa pili ni wale ambao wakijiingiza katika mapenzi wanakuwa na ulimbukeni.Yaani


muda wote unakuta anataka kuwa na mpenzi wake au kumuwaza tu.Mtu wa namna hii
anashindwa kuzizuia hisia zake.Hata hivyo watu wa namna hii wakiingia kwenye
mapenzi basi lazima watafeli kufikia malengo yao ipasavyo.Watu wa namna hii wanaitwa
DEVIS.Kundi kubwa la wanafunzi wanaangukia hapa.

Kijana hasa Yule wa shule,kama unataka hisia zisikutawale na wala kuwa na matamanio
yoyote kimapenzi basi zingatia mambo haya;-

i. Kuwa Mtakatifu

Hapa unatakiwa kuwa mcha Mungu yaani mtu unayeishi katika misingi ya imani
thabiti.Hii itakuwezesha kuwa na hofu ya Mungu ambayo itakukinga dhidi ya vichocheo
vya mapenzi.Penda sana kumuomba Mungu na Kumtukuza yeye basin naye hatakuacha.

17
ii. Epuka vichocheo vyote vya Mapenzi/Hisia

Kijana kama unataka kuzitawala hisia zako na zisikuendeshe basi ni lazima ujiepushe na
vichocheo vya mapenzi au hisia yaani mambo yote yale yanayoweza kuamsha hisia ndani
ya mwili wa kijana kama vile kuangalia kanda za ngono,kupiga picha za mikao hatarishi
n.k

iii. Kuwa bize

Hii pia ni njia muhimu sana kwa kijana unatakiwa uwe bize na mambo ambayo
yatakufanya huishi kesho yako.Hali hii itakuondolea mawazo ndani ya akili yako juu ya
mapenzi kwani muda mwingi utakuwa unawaza juu ya maisha yako au masomo yako.

iv. Namna ya mazungumzo yako

Pindi hunapokutana na Msichana au Mvulana basi unapoongea naye,ongea kama vile


unaongoea na Dada yako au kaka yako au ndugu yeyote wa kike au kiume wa nyumbani
kwenu.Kama hutaongea naye kama ndugu yako wakaribu basi hutaweza kumfikiria
kabisa kuwa naye kimapenzi.Mana kijana huwa na tabia ya kukumbuka aliyekutana naye
leo kutwa na mazungumzo yao na kupelekea kumfikiria basi fanya hivyo ili uwe na
amani.

v. Omba Ushauri

Kijana unatakiwa kuomba ushauri pale ambapo utaona mimi mwenyewe siwezi kumudu
bila ya ushauri.Basi mambo yakiwa magumu mtafute mwalimu wa baiolojia au wa
sayansi,mwanasaikolojia au daktari kwajili ya kuomba ushauri,kutokana na utaalamu
wao wanaweza kukusaidia sana na tatizo lako likaisha kabisa.

ANGALIZO:

Kijana anaweza kuishi bila ya kuwa na mpenzi bila ya shida yeyote,maana nilipokuwa
nafundisha semina kule Makete Njombe,Mvulana mmoja akasema haiwezekani mtu
kukaa bila mpenzi,ila kiukweli inawezekana na hakuna matatizo yoyote ya kibaiolojia
yanayoweza kutokea.Lakini pia Kijana anaweza kuwa na mpenzi na kamwe asiathiriwe
kwa namna yeyote,hapa kinachotakiwa ni umakini tu katika mahusiano.Ambapo
hatakiwa kutumia muda mwingi sana kuwaza juu ya mpenzi wake kama bado
hajafanikiwa kimaisha.

18
ATHARI ZA KUSHINDWA KUTAWALA HISIA KWA KIJANA

Endapo Kijana akishindwa na akakubali kutawaliwa na hisia,basi hisia hizo zinaweza


kumwendesha hata kupelekea athari mbalimbali ndani ya mwili au maisha yake.Zipo
athari nyingi sana za kijana kushindwa kutawala hisia zake,lakini zifuatazo ni baadhi ya
athari hizo:-

1. Mawazo

Kama kijana akishindwa kuzitawala hisia zake kabisa,basi anaweza kukumbwa na tatizo
la kufikiri juu ya ngono mara kwa mara.Hii inatokea mara tu baada ya kukutana na mtu
wa jinsia tofauti naye na wakafurahi na kuongea vizuri basi akipata muda kidogo tu basi
anaanza kuwaza.Hivi Yule kaka ananitaka nini? Au Yule Dada mbona ananichekea sana?
Hali hii inaweza kumfanya kuwa dhaifu kimawazo.

2. Punyeto

Punyeto ni kitendo cha kujichua misuli ya uume au uke.Hili limekuwa tatizo kubwa na
moja ya matokeo ya kijana kushindwa kuzitawala hisia zake.Mara kijana baada ya
kuzichochea hisia za kimapenzi ndani ya mwili,huwaka tamaa ya kushiriki katika
ngono.Wakati akiwa katika tamaa ya kufanya ngono,na hana mtu wa kufanya naye kwa
wakati huo basi huchukua sabuni au mafuta au kilainishi chochote kile na kuchua misuli
yake.Wapo vijana wengi wanaoshiriki katika jambo hili hasa wanafunzi wa boarding na
hosteli bila ya kujua madhara yake.Mtu ambaye amekubali kuendeshwa na hisia zake basi
ataangukia katika janga hili.

Jiulize

 Je,Punyeto ina madhara gani?

Kijana mwenzangu Punyeto ina madhara mengi.Kwa wale ambao wanajichua misuli ya
uume au uke wao,basi wanaweza kupata madhara yafuatayo;-

a. Husababisha udhaifu ndani ya mwili,kwa sababu ya kupotea kwa Protini na


Kalsiamu
b. Husababisha matatizo katika neva nyurolojia na kupelekea macho kutoona
c. Uume kushindwa kusimama (Uhanithi)
d. Kuwa mtumwa au teja wa kujichua
e. Kujichua husababisha mafadhaiko (Stress) kwenye akili na roho yako pia
f. Huleta matatizo ya kisaikolojia,huzuni na majonzi na kukufanya kujilaumu nafsi
mara baada ya kujichua
g. Haifutiki kirahisi,ubaki kichwani

19
h. Kufanya makutano haramu
i. Kuwahi kufika kileleni
j. Kupungua kwa wingi wa mbegu
k. Kuvunja maadili/thamani na nidhamu
l. Inapoteza muda wako na kukufanya kuwa mtu usiye na faida
m. Raha ya kujichua haibaki akilini kwa muda mrefu
n. Husababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu
o. Kujichua sio mwisho wa kumaliza haja
p. Haina faida
q. Inaongeza aibu
r. Kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa
s. Huchochea mapenzi ya hisia moja
t. Kupungua au kuisha kwa nguvu za kiume.

Kijana unatakiwa ujiepushe na tatizo hili maana si zuri,na la fedhea kabisa.Kama


umeshindwa kuzitawala hisia zako kabisa,ni heri ukatafuta mpenzi wako mmoja ukatulia
naye kuliko kufanya hili tendo.

3. Matatizo ya Akili

Hisia zinaweza kuathiri mfumo wa fahamu wa kijana na kumsababishia matatizo ya


kiakili.Nakumbuka Mwalimu wangu wa kemia Nadhiru Mkungura aliwahi kunihadithia
stori ya msichana mmoja ambaye alikuwa na hisia kali sana juu ya kijana mmoja hivi kwa
muda mrefu.Baada ya miaka mingi kupita Yule mpenzi wake akafa,sasa pale alipokuwa
anakaa Yule mvulana pakabaki kama ghofu na watu wakipita wanaona ghofu lakini
kutokana na hisia kali alizokuwa nazo Yule binti,aliona kama Yule jamaa yake yupo na
kila siku alikuwa akienda na kukaa na kucheka pamoja na kula peke yake lakini yeye
aliona kama yupo naye.Hii yote ilisababishwa na Yule binti kushindwa kuzitawala hisia
zake.

4. Zinaa

Zinaa ni moja ya neno kubwa kimaana,ila zinaa maana yake ni kufanya mapenzi au kuwa
na mpenzi nje ya ndoa au kabla ya ndoa.Wakati mwingine neno zinaa linatumika kwa
wale walioko katika ndoa tu,lakini wale watakaoshiriki katika mapenzi kabla ndoa basi
watakuwa wamefanya uasherati.Katika zama hizi zinaa imekuwa ni jambo la kawaida
sana,hasa kwa vijana,miaka ya zamani watu wazima ndiyo waliokokuwa wakifanya
zinaa,lakini dunia ya sasa hadi vijana wanajihusisha katika zinaa.Hii ni kwa sababu ya
kushindwa kutawala hisia na kufuata matamanio ya mwili.Ukiwa unashiriki katika moja
ya mambo haya basi tunasema wewe unashiriki katika zinaa;-

20
a. Ushoga

Hiki ni kitendo cha wavulana kwa wavulana kuingilia na kumwaga mbegu za uzazi.Hili
limekuwa tatizo linalowakumba sana vijana,hasa makamo ya shule na vyuo wanakutana
wanafirana wavulana kwa wavulana.Wakati mwingine unakuta mtu mzima anenda
kumlawiti mtoto mdogo.Hii inaonesha namna zinaa inavyofanyika katika jamii,lakini pia
haya ni matokeo ya kupenda urahisi au pesa kwa wavulana.

b. Usagaji

Hiki ni kitendo kinachohusisha kuingiliana kwa msichana kwa msichana ili kutimiza haja
ya mapenzi.Katika kitendo hiki msichana mmoja anajifanya kuwa yeye ni mvulana na
anamuingilia mwenzie,wakati mwingine wanatumia vidole,ndimi au ndizi.Dunia
ilivyokuwa ya ajabu sasa hivi,kuna uume wa kutengenezwa ambao uvaliwa kama
mkanda,ambao wanautumia kuingiliana wenyewe kwa wenyewe.

c. Ndoa ya jinsia moja

Vijana tunafanya uchafu ambao hauna maana na unaweza kusababisha laana kwa
jamii.Sasa hivi utakuta mvulana kwa mvulana wameoana au msichana kwa msichana
wameoana,na wanaishi kama mke na mume pasipo kuwa na shida yeyote.

d. Ngono kati ya mwanadamu na mnyama

Hili pia limekuwa tatizo kubwa tu kwa jamii kwani vijana wanazichochea hisia zao
wakati hawana pa kuzituliza,hali hii hupelekea kutamani wanyama na kufanya nao
ngono.Wapo wengi ambao mpaka sasa wamekamatwa na kupelekwa jela kwa kuingiliana
na mbwa,mbuzi,ng`ombe au kuku.

e. Kukosa Uaminifu katika ndoa (Uzinzi)

Moja ya kitu muhimu sana katika ndoa ni uaminifu kati ya wawili wapendanao.Ndoa
nyingi zinavunjika kwa kukosa uaminifu ndani yake,hapa utakuta mume au mke anakuwa
na mpenzi mwengine nje ya ndoa yake.Mara nyingi wanaokuwa wahusika ni wanaume na
ni mara chache sana kumkuta mwanamke anafanya hivyo,labda kama amesalitiwa au
ameumizwa sana.

f. Ngono kabla ya kuoa au Kuolewa (Uasherati)

21
Vijana wengi wanafikiri kuwa kufanya ngono mapema ndiyo ulijari au sifa,kitu ambacho
si kweli.Hapa utakuta kijana mdogo tu tayari ametoa mimba mara nyingi tu,na
kusababisha vifo vya viumbe visivyo na hatia.Au binti au Mvulana mdogo anawapenzi
zaidi ya wawili na anajiona yuko sawa, na kama akitokea mwengine amempenda anapita
naye.Utakuta mtoto wa darasa la pili tayari anafanya mapenzi,ebu tukae tutafakari
tunatengeneza kizazi cha aina gani? Kufanya ngono au mapenzi ndani ya umri mdogo si
sifa na yanaweza kusababisha athari zifuatazo:-

 Kupata magonjwa ya zinaa.Vijana wengi tunakuwa na magonjwa ya zinaa


pamoja na mengineyo kwa sababu ya kufanya ngono zembe mara kwa
mara.Kwani mara nyingi mkikutana hakuna kwenda kupima, wala uangalifu
katika kufanya ngono,hii inaweza kuleta maambukizi ya magonjwa ya zinaa,kama
vile kaswende,gonorea na UKIMWI

 Mapenzi ya mapema yana gharimu.Hapa utaona kijana akisha anza


mahusiano,basi ananza kutumia pesa nyingi.Utakuta anataka kuhonga,kuwa na
nguo kali au kumiliki vitu ambavyo anafikiri katika akili yake vitamvutia mpenzi
wake.Wakati huu ndio ambao kijana anatakiwa asikose pesa,kama akikosa
anaweza hata kuiba kwaajili ya kwenda kufanya mambo yasiyo na maana

 Kupata matatizo ya uzazi.Hii inatokea kwa sababu ya kufanya mapenzi pasipo


uangalifu,hali inayopelekea kupotea kwa mbegu nyingi kabla ya wakati
wake.Matokeo yake ni kwamba ukifika wakati wa ndoa unakuta mwanamke
hawezi kuzaa au mwanaume hawezi kuzalisha

 Uanisi.Hii ni hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake


au kusimamisha kwa muda mfupi tu.Haya pia ni matokeo ya kufanya ngono
zembe kwa muda mrefu na kupelekea kukosa nguvu za kiume

 Kupoteza thamani.Kwa upande wa mwanamke thamani anaweza kuikosa kwa


kuonekana kuwa ametumika sana,yani ni mzoefu wa mapenzi.Kwa mwanaume
unakuta ndani ya ndoa anakosa thamani kwa sababu ya kutoweza kumridhisha
kimapenzi mkewe.Hapa utakuta wanasema kuwa mtu mwenyewe safari moja tu
hoi

 Kupoteza muda.Ngono kabla ya kuoa au kuolewa inapoteza muda sana,wakati


unakutana na mpenzi wako mara kwa mara pasipo na sababu ya msingi.Lakini pia
unakuta mnaishi bila kuwa na malengo ya kuwa pamoja mbeleni,hivyo baada ya
muda mchache unajikuta umebadilisha mwengine naye unapoteza muda

22
g. Kuangalia au kuweka picha au video za utupu hadharani

Zinaa imesababisha kanda za ngono na picha kuwa maarufu sana duniani.Vijana wengi
wanaangalia X na picha za ngono mtandaoni haya ni matokeo ya zinaa

h. Mavazi ya Mtego

Zinaa pia imebeba tabia ya mtu kuvaa mavazi ya mtego,mara nyingi wanawake ndio
wanavaa mavazi ya mtego kwa wanaume.Inawezekana kwa kusudia au
kutokukusudia,hali inayopelekea kutongozwa au kufuatwa na wanaume mara kwa
mara.Unakuta mwanamke amevaa nguo inamchora kabisa yani hakuna alichojistiri

i. Matumizi ya Vipodozi

Hii inaweza kutokea mara tu baada ya mwanamke kuingia kwenye zinaa, huanza kuona
haja ya kujitengenezea mvuto kwa mwanaume,hali inayopelekea matumizi ya vipodozi
kama vile losheni n.k

Kwa kuongezea kwa namna moja au zaidi zinaa inaweza kupelekea yafuatayo;-

j. Mziki unaohamasisha na kuchochea kunengua viuno


k. Ndoa kuvunjika (Talaka)
l. Ngono kati ya ndugu wa damu (incest)
m. Kujimalizia tamaa za mwili
n. Kunyonyana ndimi na sehemu za siri
o. Kujamiana kwa njia ya ulimi

Kijana unatakiwa uwe makini na kutawala hisia zako,ili uweze kujiepusha na zinaa
ambayo inaweza kupelekea maambukizi ya magonjwa ya ngono kama vile
Kaswende,Gonorea na UKIMWI.Wakati mwingine hupelekea kifo au mwili kuwa dhaifu
na kuchoka kabla ya kuzeeka.

5. Kushindwa Kujiamini

Hisia za kimapenzi zinamfanya kijana kushindwa kujiamini katika mambo


mbalimbali.Mara nyingi anakuwa hana amani anapokuwa na watu wengi hasa ambao
hawajui au hana mazoea nao.

6. Umaskini

23
Kijana ambaye atakubali hisia zimwendeshe basi atakuwa na uwezo mdogo sana wa
kufikiri juu ya namna ya kupambana na janga la umaskini pamoja na athari zake.Hii ni
kwa sababu ya kukosa muda wa kufikiri juu ya maisha yake,na kuzipa hisia zake nafasi
ya kwanza.

SEHEMU YA NNE

JINSI GANI KIJANA AIFIKIE KESHO YAKE

Mimi Isack Masatu kama Kijana Mzalendo wa Taifa langu teule la Tanzania, ambalo
linanipa mimi pamoja na vijana wenzangu elimu bure,kwa kutambua changamoto
wanazokumbana nazo vijana wenzangu,kabla hawajafikia malengo yao na kushindwa
kuifikia kesho yao.Si kwa sababu hawataki bali kwa kutokujua namna gani ya kuweza
kuifikia kesho yako au kuyaishi malengo yako.Lakini nataka kupitia sura hii basi kila kitu
uwe umeelewa juu ya kesho yako,changamoto zake na namna ya kuzikabili.

Kesho yako maana yake ni yale maisha ambayo unatamani kuyaishi katika utuuzima hata
kufikia uzee.Yamkini unatamani maisha yako yajekuwa ni ya siasa,unatamani uwe Raisi
wa Taifa hili au Uwe mwana Muziki mkubwa ndani ya Tanzania,basi hayo matamanio
yako ya kutaka kuwa na maisha hayo ndiyo kesho yako.Wengi tunashindwa kuiandaa
kesho yetu na hata kuifikia kesho yetu.Inawezekana unatamani kuwa Daktari lakini
unashindwa kufanya maandalizi yako mapema.

Lakini mpendwa yapo mambo muhimu ya kufanya ili uweze kuifikia kesho yako.Mambo
hayo ni;-

1. Omba Mungu Akufanyie Wepesi

Ni ukweli usiopingika kuwa Mungu ndiye mwenye mamlaka na kibali ndani ya


ulimwengu.Wewe kama kijana ipo haja ya kumuomba Mungu akuwezeshe kufikia
malengo uliojiwekea,kwani ziko roho za kishirikina na chuki na mitego ya watu ambayo
kimsingi huwezi kupambana mwenyewe bila ya Mungu.Kijana mwenzangu ni lazima
tumpe Mungu nafasi ya kwanza katika kuipigania kesho yetu ili yeye naye asituache,bali
atusimamie katika kila hatua ya maisha yetu.

2. Kuwa na Maono

Kwa tafsiri ya kawaida Maono ni kile kitu ambacho unatamani ukifanye au uwe nacho
ndani ya akili yako na hujirudia mara kwa mara.Maono huwa na tabia ya kuona kitu cha
mbeleni sana,hapa kijana kwanza anatakiwa kuyatambua maono yake yeye ni kuwa nani?
Wengi wanashindwa kujua maono yanapatikana wapi,na wanawezaje kuwa na mipango
ya mbali kwani Maono pia yana maana ya malengo au mipango unayotaka kuifanya

24
mbeleni.Waingereza wanasema ``Failure to plan,You plan to Fail`` ikiwa na
maana kuwa kushindwa kupanga kunaleta kushindwa katika kila kitu.Kumbe basi ni
lazima tuwe na maono.

Namna au Njia za Kupata Maono

i. Kuota Ndoto

Hapa unaangalia ile ndoto ambayo inajitokeza mara nyingi pindi unapolala au kupumzika
kwa muda.Mfano mara kwa mara unaota upo jeshini basi tambua maono yako wewe ni
kuwa mwanajeshi,au unaota unafundisha basi wewe maono yako yawe ni Ualimu.

ii. Mawazo

Kufikiria au kuwaza pia ni njia mojawapo ya kupata maono au mipango.Kijana


anatakiwa akae kwa utulivu kwa muda mara kwa mara na kuwaza kuhusu maisha
yake ya mbeleni,hii inaweza kumpatia kijana mipango ya maisha yake au kujua kesho
atakuwa nani?

iii. Elimu

Kupitia elimu kijana anaweza kupanga mipango ya mbeleni yamkini kulingana na hali
halisi ya uwezo wake wa kiakili shule pamoja na ufaulu wake.Mfano kijana akijua kabisa
kuwa uwezo wake ni masomo ya sanaa basi hawezi kupanga kuwa Mhandisi,hivyo
kulingana na masomo anayo yaweza atapanga anataka kuwa nani?

iv. Kupitia Watu Wengine

Kupitia watu ambao tayari wamefanikiwa unaweza ukapenda na wewe kuwa kama
yeye.Mfano umemuona Daktari bingwa na makini kama Charles Bathon ambaye ni
Daktari wa kwanza ulimwenguni kutenganisha mapacha,ukatamani nawe uje kuwa
Daktari Bingwa.Kumbe kupitia watu waliofanikiwa nawe unaweza kushawishika na
kupanga mipango ya kuwa kama wao.Mtu aliyekushawishi unaweza ukamfanya kuwa
Role Modal wako.

v. Kupitia Mafundisho ya Dini

Unapokuwa ukisikiliza mahubiri na mafundisho ya dini unaweza ukapata mipango juu ya


maisha yako ya mbele.Yamkini ukatamani kuwa Mchungaji,Shekhe au kuifanya kazi ya
Mungu katika Kanisa au Msikiti kwa namna Fulani.

Unapogundua kuwa una maono ni lazima kwanza uyaandike,kisha jiulize maswali


yafuatayo;-

a. Nataka kufanya nini? (Kutayarisha malengo)

25
b. Nitafanya kwa njia gani? (Kuelezea hatua-Mbinu)
c. Wakati gani nitaanza na nitamaliza?
d. Nitakumbana na changamoto gani na faida gani?

Kwa kuzingatia hayo na kuweka kumbukumbu vizuri,basi wewe tunasema tayari


unamaono ni hatua muhimu katika kuifikia kesho yako.Kwani Wanatheolojia wanasema
``Huwezi Kuishi Kesho Yako,Kama Usipoitengeneza Kesho Yako Kupitia
Leo Yako`` .Leo inatumika kwa kuandaa mipango mapema.Ngoja nikupe historia fupi
ya hayati Patrick Aron Mpilima Masatu Mfugale pamoja na maono yake.

Patrick Aron Mpilima Masatu Mfugale amezaliwa tarehe 01/12/1953 katika


kijiji cha Ifunda mjini Iringa.Alichukua elimu yake ya msingi katika shule ya
Consolatha Fathers Primary school mjini Iringa.Mwaka 1975 alichukua elimu
ya Upili katika shule ya Upili Moshi.Lakini tangu akiwa kidato cha pili mwezi wa tano
alikuwa na maono ya kuwa Mhandisi bora Tanzania na Kazi yake isifanane na yeyote
Tanzania.Wakati akiwa sekondari alikuwa akiandika maono na maisha yake anavyotaka
yawe aidha alitamani kusoma nje ya nchi.Alianza safari yake ya Uhandisi katika serikali
mwaka 1977 katika Wizara ya Ujenzi.Mnamo mwaka 1983 serikali iliona juhudi zake na
kuamua kumpeleka akachukue shahada ya 1 ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha
Rocky nchini India.Mnamo mwaka 1989 alipata shahada yake ya 2 ya uhandisi katika
Chuo Kikuu cha Loughbourough Braunshweing nchini Uingereza pia kwa msaada wa
serikali ya Tanzania.Mwaka 1991 Mfugale alisajiliwa kama Mhandisi Mtaalamu
nchini.Mwaka 1992 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Barabara za Mikoani.Akiwa
Chuoni mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Mhandisi Mkuu wa Madaraja na Wakala wa
Barabara Tanzania wa serikali TANROADS.

Katika shughuli zake Kama Mhandisi Mkuu wa Serikali amefanikiwa kubuni na


kutengeneza madaraja zaidi ya 1400 yakiwemo Daraja la Magufuli,daraja la
Mkapa,daraja la Kikwete,daraja la Rufiji,daraja la TAZARA,daraja la Ubungo,daraja la
JPM,daraja la Tanzanite,SGR n.k.Hata hivyo amesimamia na kutengeneza barabara
nyingi hapa nchini zikiwemo Mfugale Flyover (Buguruni-Dar es salaam),Bwawa la
Nyerere Rufiji megawati 2,115.Kutokana na mchango wake mkubwa katika kuokoa fedha
za serikali,kupotea katika mambo ya ujenzi kwani alifanya kazi kizalendo,mnamo tarehe
27/09/2022 serekali iliamua baadhi ya maeneo muhimu nchini yapewe jina la Mfugale
kama vile,Airport ya Chato,Daraja la TAZARA Dar es salaam pamoja na Ikulu ya
Chamwino.Lakini nyumbani kwake utakuta ameweka picha za maono yake,kila
nilipokutana naye moja ya maneno muhimu aliyonambia ni kuwa na maono na aliweza
kuninunulia Diary na kuniambia niandike mipango yangu ya siku,wiki,mwezi,mwaka na
miaka katika kila nyanja ya maisha yangu.

Mfugale alifariki tarehe 29/06/2021 akiwa ofisini kwake mjini Dodoma, aliumwa ghafla
na kupelekwa Hospitali ambapo umauti ulimkuta.Hakuna Mhandisi aliyezikwa kwa
heshima kama yeye na mazishi yake yamezidi hata baadhi ya viongozi na vigogo wa
serikali ya Tanzania.Aidha kabla ya mazishi, mwili wake ulianza kuagwa jijini Dodoma
na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu

26
Hasani pamoja na viongozi wengine wa serikali,siku ya Alhamisi.Ijumaa mwili wake
ulipelekwa Dar es salaam kwaajili ya kuagwa katika viwanja vya karimje kwa misa na
salamu,jumamosi mwili wake ulitolewa nyumbani kwake mbezi na kupelekwa kijijini
kwetu Ifunda Iringa ambapo Jumapili wanafamilia tuliuaga mwili kwa misa na jumatatu
akazikwa katika makaburi ya familia Ifunda mjini Iringa.

Kupitia historia hii Kijana unatakiwa kujifunza kwanza,kuwa na maono na yaandike


kama kumbukumbu ili kila ukisoma maono upate nguvu ya kuyapigania.Kwani Mfugale
tunaona kuwa alipigania maono yake kwa sababu aliyaandika.Pili weka juhudi katika
kupigania malengo yako na hata baada ya kupata unachokihitaji hakikisha unaendelea
kuwa na bidii,ili uweze kupanda juu kama ilivyokuwa kwa Mfugale.Vijana wengi sana
hatuna maono,ila nakusihi sana wewe kijana,anza kuweka maono yako sasa

3. Usiudharau Ujana Wako

Kuudharau ujana maana yake ni kuutumia vibaya ujana wako katika mambo mabaya na
yasiyo na faida kwako,na kwa jamii inayokuzunguka.Vijana wengi sana wanapenda
kudharauliwa,hali inayopelekea laana na kushindwa kufikia mipango ya kesho yake.Ila
nataka nikwambie kuwa uwezo wa kijana kudharauliwa au kuheshimiwa upo ndani yake
mwenyewe.Aina ya maisha unayoishi na mambo unayoyafanya,ndiyo yanayoamua ujana
wako uheshimiwe au udharauliwe.Yapo mambo ambayo yanasababisha kijana
kudharauliwa au kuheshimiwa,mambo hayo ni:-

i. Kusema/Kuongea kwako

Aina ya maongezi na maneno yako yanaamua uheshimiwe au udharauliwe.Kuna vijana


ambao ongea yao imejaa matusi kila kona! Yaani hawezi kuweka msisitizo wa sentensi
yake bila kutukana.Rafiki,hakuna mtu yeyote atakayemuheshimu kijana wa namna
hii.Kijana wa namna hiyo anatukana sana kwa sababu ya vitu ambavyo amevijaza ndani
ya akili yake kama vile miziki ya kidunia,picha za uchi,mazungumzo mabaya n.k

ii. Mwenendo wako

Hii inajumuisha mambo mbalimbali unayoyafanya kiroho na kimwili kama vile:-

27
 Uvaaji wako

Unavaaje…..kuvaa kwako kunaamua uheshimiwe au udharauliwe..Nani atakaye


kuheshimu ikiwa wewe mwenyewe hauheshimu mwili wako? Unakutana na kijidada
kimekuvalia suruali imembana mpaka kuonesha viungo vyake vya siri..Sasa wewe
mwenyewe hujiheshimu utaheshimiwa na nani? Hapo dada anaona sifa kuvaa mavazi
yanayozigeuza sehemu zake za siri kuwa mali ya uma na maonesho kwa jamii.Cha ajabu
mwenyewe anajiona mjanja hatari!Unakutana na kijana wa kiume naye kavaa kisuruali
kimembanaaaaa.. Na makalio yapo nje!! Lakini hapo anajiona yuko vizuri mtaa
mzima.Kijana unatakiwa kuvaa mavazi ya heshima katika jamii.

 Kutembea kwako

Unatembeaje…Baadhi ya vijana ukiona tembea yao utadhani anaruka matuta


Barabarani..Pia kutembea kwako kunaweza kuamua uheshimiwe au udharauliwe..

 Kunyoa/Kusuka kwako

Kijana unayejielewa na kutafuta maisha usiwe una nyoa mitindo ya ajabu na kusuka
mitindo ambayo si sahihi kwa jamii zetu.

iii. Upendo wako Kwa Watu

Siku zote upendo unakupa kujali na kuthamini.Kijana ukikosa upendo ni lazima utakuwa
na kiburi na kujiona ni bora kuliko wengine.Hakuna mtu atakaye mheshimu kijana wa
staili hiyo.Upendo wako unaamua uheshimiwe au udharauliwe..

iv. Imani yako

Hali ya kijana kuwa na imani na hofu ya Mungu kunamfanya aheshimiwe katika


jamii.Kutokuwa na imani kunakufanya ufuatishe namna ya dunia hii,na ukifuata namna
ya dunia hii lazima utafanya mambo yasiyopendeza katika jamii.Hivyo unapoamua
kutengeneza heshima katika ujana wako usisahau kumpa Mungu maisha yako.

v. Usafi Wako

Hapa tunazungumzia usafi wa kimwili na Kiroho.Usafi wako wa Kiroho ukoje? Au ndo


unakutwa vichochoroni na Mabinti wa Watu? Usafi wa Kimwili nao vipi? Usijeanza

28
kusumbua Wachungaji na Maostadhi wakuweke mkono ili uolewe kumbe Mchawi ni
wewe mwenyewe!...Mpangilio wa chumba unachoishi ukoje? Au Tukiingia tunaweza
kukuta soksi kwenye hotpot? Jichunguze katika maeneo hayo yote kama kijana.Aina ya
Maisha yako yatakufanya udharauliwe au uheshimiwe.

4. Kujitambua

Hauwezi kufanikiwa bila ya kujitambua kama kijana.Kijana unayetaka kufanikiwa kwa


kufikia malengo uliyojiwekea,ni lazima uwe unajiuliza mara kwa mara maswali haya;-

 Mimi ni nani?

Kijana anapaswa kujifahamu yeye mwenyewe kuwa yeye ni nani? Ametoka katika
familia tajiri au maskini? Ni changamoto zipi uliwahi na unazipitia?

 Kwa nini nipo hapa?

Kijana anapaswa kutambua kuwa mahali alipo anafanya nini na anapaswa kufanya nini
kwa wakati gani?

Kijana unatakiwa kuifahamu haiba yako (tabia,imani,hisia n.k) na namna ya kutawala


hisia zako pamoja na tamaa za mwili wako,Usije ukaruhusu hata kimoja kikatawala akili
yako kwani ikiwa hivyo basi unaweza kupoteza malengo yako na kushindwa kuifikia
kesho yako.Yapo mambo ambayo unatakiwa kuyajua kama kijana juu ya haiba
yako.Kwanza haiba ni jumla ya mwenendo wa mtu Fulani ikizingatia tabia,hisia,imani na
mitazamo yake,mara nyingi tunapozungumzia neno haiba tunamaanisha ni tabia ya
mtu.Basi nataka uchukue maana ya haiba kama tabia ya mtu.Pili tambua kuwa haiba yako
au tabia yako inaweza kuathiriwa yaani kuwa nzuri au mbaya kwa kuzingatia vigezo
hivi;-

a. Hali za Urithi Kutoka kwa Wazazi

Hii huanza wakati wa mtungo wa mimba (Zygote).Mtoto kuwa wakike au wakiume


huamuliwa na chromosomes.Rangi ya nywele,macho,urefu,umbo la mwili,ustadi na
vipawa vyake huamuliwa na genes.Ila makuzi ya kiumbe huamuliwa wakati wa mtungo
wa mimba mfano utoaji wa meno,uwezo wa kutembea,uwezo wa kupokea au kuelewa n.k
katika sehemu mbalimbali mtoto akichelewa kupevuka au akiwa ni mrefu sana wakati
wazazi wake ni wafupi basi huwa anachekwa.Hata anaweza kukataliwa na jamaa! Na hali
hii huathiri haiba ya mtoto.

b. Mazingira aliyokulia Mtu

29
Mazingira pia yanaweza kuathiri hali ya mtoto au kijana mbeleni.Mfano Kijana
aliyelelewa katika mazingira ya ubaguzi,kubezwa,kunyanyaswa,kushambuliwa hii
inaweza kuathiri kabisa hali ya baadaye ya maisha yake.Kijana au mtoto kulindwa kupita
kawaida pia kunaweza kuathiri maisha yake ya mbeleni.

c. Mafunzo (Learning)

Elimu pia huchangia kubadili hali na tabia ya kijana au mtu.Hatua mojawapo ya kujifunza
ni pale Kijana anapofikia hatua ya kuonyesha mabadiliko katika maisha.Elimu au
kuelimika ni hatua inayoendelea.Mtu anapozaliwa akiwa mkamilifu ndani yake anakuwa
na misukumo ya kujifunza.Tabia ya mtu huumbika wakati anapoendelea kufanya tendo
Fulani jema au baya kwa kulirudia rudia mara nyingi.

Aina Nne za Hali Ya Watu

Kutokana na ukweli kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kijana kujitambua basi ngoja
nikupe uchambuzi juu ya saikolojia ya aina za watu au uchambuzi wa aina za watu kwa
mujibu wa Mchungaji Douglas.C.Mwosi.Ziko aina kuu nne za hali na tabia za
watu.Ingawa hakuna mmoja awezaye kusema ana aina moja tu kati ya aina hizo
nne.Utakuta kuna moja inatawala na nyingine hazitawali.Sisi tupo mchanganyiko wa aina
nyingi.Lakini utaona dhaidi ya aina moja au mbili katika hali yako au ile ya rafiki
yako.Tuangalie aina hizo za hali za mwanadamu

I.Mwenye urafiki sana,Mchangamfu (Sanguine)

A. UWEZO WAKE
i. Huwapenda watu na ana marafiki wengi
ii. Hapendi kuwa pekee na analeta furaha kila mahali anapoenda
iii. Huweza kusimulia,hadithi kucheka na kufanya ubishi kwa urahisi
iv. Huwajali watu,furaha na huzuni zao
v. Hujaa nguvu na mipango mingi
vi. Ni mtu anayetaka kuongea yeye tu hataki kushindwa

B. UDHAIFU WAKE
i. Vigumu kwake kuwa mwaminifu kanisani,kwa Mungu,Kazini,kwa wenzake na
kwenye ndoa
ii. Huwa na choyo
iii. Huwezi kumtegemea,husahau ahadi na wajibu wake
iv. Hufanya matendo bila ya kufikiria na hupenda kujivuna
v. Hukasirika kwa haraka lakini hupoa kwa haraka
vi. Hawezi kujitawala mwenyewe na anaingia kwenye majaribu mengi

30
vii. Hutubu mara nyingi kwa sababu ya makosa yake

II.Mwenye ushujaa na talanta ya uongozi (Choleric)

A. UWEZO WAKE
i. Huweza kujitawala sana
ii. Huweza kukata shauri kwa haraka na katika hali nzuri
iii. Ana ushujaa na nguvu
iv. Hupenda kushughulika na mambo mengi
v. Ana talanta ya utawala na uongozi
vi. Hushawishi moyo kirahisi.
vii. Hutazama kusudi lake tu na haoni matatizo mbele yake
B. UDHAIFU WAKE
i. Huweza kuwa mkali na kukaa hivyo kwa muda mrefu
ii. Huweza kujilipizia kisasi mara nyingi
iii. Mwenye choyo na akitaka kitu huwapita wengine
iv. Ni vigumu kwake kuonyesha huruma na upendo wake
v. Anataka mashauri kwa haraka na mara nyingi huwa yale yasiyofaa
vi. Huweza kusema maneno makali lakini hawezi kumwelewa mtu anayechukizwa na
maneno hayo
vii. Ni vigumu kwake kuomba msamaha
viii. Ni vigumu pia kutambua kuwa anahitaji msaada wa Mungu sana

III.Mwenye akili na talanta nyingi (Melancholy)

A. UWEZO WAKE
i. Huwaza sana juu ya maisha,makusudi na maono yake
ii. Hutaka ukamilifu katika kila kitu
iii. Hufanya kazi bora
iv. Wengi wana talanta ya muziki,kuchora picha.hadithi
v. Huweza kupambana na mambo au matatizo ya mbele
vi. Ni rahisi kabisa kwake kujitoa kwa Mungu na kazi yake

B. UDHAIFU WAKE
i. Hujifikiria nafsi yake mno~mwenye choyo
ii. Huweza kuchukizwa kwa haraka na kirahisi

31
iii. Ni vigumu kwake kumsamehe mwingine
iv. Hufadhaika sana na kujisumbua juu ya mambo mengi
v. Huogopa kukata shauri,anaona wasiwasi
vi. Hutumaini mambo mabaya kila mara ni mchunguzi na kumhukumu mwengine
vii. Mwenye moyo mzito.Anaona furaha siku moja huzuni kesho
viii. Asipotawala mawazo yake anaweza kuiharibu ndoa yake
ix. Anaweza kuwafukuza rafiki zake

IV.Mwenye Utulivu (Phlegmatic)

A. UWEZO WAKE
i. Huenda pole pole
ii. Hana hasira na mchangamfu
iii. Huweza kuona upende wa kuchekesha katika mambo mengi
iv. Mstadi,hutumia akili yake
v. Hufanya kazi nzuri sana
vi. Mwaminifu,mwenye hekima
vii. Huweza kutegemewa na ni hodari
viii. Wengi wenye matatizo huvutiwa kwake kwa ajili ya ushauri

B. UDHAIFU WAKE
i. Mvivu wakati mwingine,atachukua muda mrefu kukamilisha kazi
ii. Mwenye choyo na hataki kujitolea kabisa kwa wengine
iii. Huweza kuwa mshupavu;hatapenda kusaidia katika kazi yaw engine.Atakataa na
ubishi na kuchekelea
iv. Hataki kukata shauri mara moja.Hukawia mno,huogopa.Hutambua haja ya
maombi ya utaratibu lakini hukawia kufanya hayo
v. Kama mtu huyo ni mume,mke atapata shida kumwacha awe kichwa nyumbani
mwao kwa sababu hataki kukata shauri

5. Kutumia Muda Vizuri

32
Miongoni mwa mambo yanayokwamisha malengo ya kijana ni kutotumia vizuri
muda,kwa sababu katika maisha ya mwanadamu uwezo wa kufanikiwa au kutofanikiwa
upo katika muda.Nasema hivi nikiwa na maana kwamba kila jambo analolifanya mtu ili
liweze kuleta matokeo ni lazima lipitie kwenye kipengele cha muda.Mfano ukiona mtu
amefanikiwa kiroho au kimwili,tambua ya kuwa mafanikio hayo yamekuja kwa sababu
aliutumia vizuri,muda wake katika kuhakikisha anafanikisha jambo hilo.Ukiona jambo
ambalo ni zuri linatokea kwenye jamii au hata kwenye maisha yako tambua ya kuwa
muda ulihusika katika kulifanikisha jambo hili.Kwa sababu kila ukipandacho sasa hivi ni
mbegu ambayo inategemea muda ili ije kuzaa.Inawezekana hujanielewa ni hivi kama
muda wa kuijenga ndoa yenu mliutumia kwenye kuchunguzana na kuangaliana
mapungufu au kasoro, moja kwa moja tambua ya kuwa mnatumia muda wenu
kuchunguzana mlikuwa mnajijengea kesho ambayo ndiyo iliyoko sasa hivi.Matokeo ya
vijana wengi kuzama kwenye ngono na zinaa ni kwa sababu muda wao mwingi
umewekezwa kwenye kuhakikisha mchakato wa kuifikia zinaa unafanikiwa.Ndio maana
si ajabu kumkuta mtoto mdogo wa primary anamiliki simu ambayo ndani yake imejaa
picha za ngono.

Ila kama kijana unatakiwa utambue kuwa kile unachokipanda ndani yako leo ndicho
kitakachokuja kuzaliwa baada ya muda wa kuzaa kufika.Hili ni jambo ambalo
linawaangusha vijana wengi,badala ya kuwa wanapambania kesho yao wanatafuta starehe
na anasa za dunia.Tambua ya kuwa muda mwingi unapotea katika kile ukipendacho yani
kama wewe unapenda simu na huna nidhamu nayo,yaani ukilala simu ukiamka
simu.Wakati mwingine unakaa online pasipo chochote cha maana zaidi ya udaku na
kulike wadada na wakaka.Kumbe suluhisho la kijana kufanikiwa ni kuutumia wakati
(muda) kwa kutenda mambo yatakayomwezesha kuiishi kesho yako.

Hiki ni kitendawili kigumu mno hasa kwa mtu aliye na uhitaji wa kufika sehemu
Fulani.Wafanyakazi wengi wamejikuta wakipoteza kazi zao kwa sababu ya kutaka
shortcut,wadada/wakaka wamejikuta wakiingia kwenye ndoa haramu kwa sababu ya
kutaka shortcut.Waingereza wanasema `` IT’S BETTER TO WAIT LONG THAN TO
MARRY WRONG``.Kijana unatakiwa kutambua kuwa muda ndio ufunguo wa
mafanikio yako kwani ``No success without time management`` ikiwa na maana
hakuna mafanikio bila ya kutumia muda vizuri.Kama wewe ni mwanafunzi,hakikisha
muda wako mwingi unautumia katika kusoma na kupitia mitihani na si kufanya uzembe,
kwani mafanikio yanakuja pale ambapo unapotumia muda sana kwa kusoma.Mfano
ukiwa unapoteza muda mwingi sana katika mapenzi na wewe ni mwanafunzi au
mwajiriwa,basi ufanisi na mafanikio yako yatakuwa katika mapenzi na si elimu wala
kazi,kwani hukiutumia muda wako vizuri kwenye elimu au ajira yako.Kama unataka
kuwa mwanafunzi bora basi hakikisha unatumia muda wako mwingi katika kusoma au
kama unataka kuwa mchezaji bora wa mpira,basi tumia muda wako vizuri kwenye
mazoezi.

33
Aidha kama unatamani uje kuwa Mtumishi wa Mungu,basi tumia sasa muda wako vizuri
katika kusoma maandiko Matakatifu na kufanya ibada sana.Kama unataka kuwa Daktari
au Mwalimu halafu unatumia muda shuleni katika michezo,basi tambua hautaweza
kufanikiwa kuiishi kesho yako kwani haujatumia muda wako vizuri katika kuiandaa.Kwa
hiyo jifunze kuutumia muda (wakati) vizuri kwa sababu maono yaliyopo ndani yako
yatafanikiwa kulingana namna ulivyotumia muda wako katika kuhakikisha yanafanikiwa.

6. Uchaguzi Sahihi

Ili kijana aweze kufikia kesho yake ni lazima awe makini katika kuchagua.Maana kila
kitu ambacho mtu anakifanya na kinamletea faida ama hasara kinatokana na uchaguzi
wake.Ukiona Mtu ni Mwalimu,Mtumiaji wa Madawa,Daktari au Kibaka ujue huo ni
uchaguzi wake.Uchaguzi wa mtu unatokana na kile ambacho anakiwaza katika kichwa
chake.Kwanza kijana huanza kuwaza juu ya kitu Fulani,kisha akili yake itakichambua
kile ambacho anakiwaza na kutoa majibu kama kinafaa au hakifai.Kama itaona kinafaa
kitamuongoza kijana kufanya hicho kitu lakini kama akili itaona hakifai kitatoa ishara
kwa kijana ili asikifuatilie.Kwa kupitia matokeo ya kitu au jambo ambalo kijana
ameamua kufanya,tunaweza kupata makundi mawili ya uchaguzi ambayo ni;-

 Uchaguzi sahihi
 Uchaguzi usio sahihi

Jiulize

Uchaguzi sahihi ni nini? Na uchaguzi usio sahihi ni nini?

Uchaguzi sahihi ni hali ya kuamua kufanya jambo au kitu ambacho kina matokeo
mazuri.Mfano kuamua kusoma au kwenda ibadani ambapo matokeo yake ni kufaulu
mitihani au kuipata pepo ya Mungu na Baraka.Uchaguzi usio sahihi ni hali ya kuamua
kufanya jambo au kitu ambacho matokeo yake ni mabaya,yamkini hapo kwa hapo au
baada ya muda mara tu baada ya kuamua au mbeleni sana.Mfano kuamua kuacha
shule,kuiba,au kutumia madawa ya kulevya.

Kutokana na uwezo mkubwa wa kiakili wa Kijana tungetamani kuona akifanya uchaguzi


sahihi.Lakini hali ya kuwa na maamuzi mabaya au uchaguzi usio sahihi kwa kijana si
kwamba hana akili bali hisia za tamaa mbaya ndizo zimeiteka akili yake na kuiendesha
katika kuratibu uchaguzi usio sahihi.Ipo haja ya kijana anayetaka kufikia malengo mazuri
ya kesho yake,kuwa na uchaguzi sahihi katika nyanja zifuatazo:-

 Urafiki

34
Moja kati ya watu muhimu sana katika kuyafikia malengo yako kama kijana ni rafiki au
marafiki.Mara nyingi watu tumekuwa tukichagua rafiki bila ya kuwa waangalifu.Kwanza
kuna tofauti kati ya rafiki na watu au mtu wa kupiga nae stori.Rafiki ni Yule mtu wa
karibu nawe ambaye mnashirikiana mawazo na kuwa pamoja katika shida na raha,na mtu
wa kupiga naye stori ni Yule mtu ambaye unakutana naye mara kwa mara na kupiga naye
stori basi lakini hakujui wewe wala mipango.Mara nyingi rafiki yako anaweza akawa
chanzo cha wewe kufanikiwa au kushindwa,hii ni kwa sababu yeye ndiye atakupa
mawazo pale unapohisi changamoto yoyote ile na kumwambia mipango yako kama
kutaka ushauri wako.Kama ukichagua rafiki mbaya basi atakupa ushauri ambao utakuwa
una kuvunja moyo kabisa na kufanya ukate tamaa.Basi wewe kama kijana unayetaka
kufanikiwa basi ipo haja ya kutafuta rafiki ambaye ni sahihi kwako.

 Imani

Mungu ndiyo kila kitu katika kufikia mafanikio yako,hebu jaribu kufuatilia wale ambao
wamefanikiwa zamani,watakwambia walikuwa wacha Mungu.Kama ukiweza kumpa
Mungu nafasi ya kwanza kwa kuwa na imani na mafundisho pamoja na kwenda ibadani
basi utafanikiwa.Kwahiyo ni muhimu sana kama Kijana unayetaka kufanikiwa,kufanya
uchaguzi sahihi wa kuishi katika imani na misingi yake.Ili Mungu akuepushe na matatizo
na mitihani ya kidunia.

 Mahusiano ya Kimapenzi au Ndoa

Siku zote watu wawili Mchumba,mke au Mume wako ndiye mtu wa karibu yako sana,na
kivyovyote vile atakuwa anajua hata mipango uliojiwekea kwenye maisha
yako.Mchumba wako au mwenza wako katika maisha anaweza kukupa mawazo mazuri
na ushauri mzuri juu ya mipango uliojiwekea katika kufikia kesho yako,au akakupa
mawazo au ushauri mbaya juu ya mipango uliyojiwekea ndani ya maisha yako.Kama
umechagua mwanamke ambaye hana mapenzi ya dhati nawe,anaweza kukwamisha
mipango yako.Hivyo basi wewe kama kijana unapotaka kutafuta mtu wa kuwa naye
katika mahusiano,ni lazima uhakikishe unafanya uchaguzi sahihi.Ili uweze kumuowa au
kuwa naye kimapenzi ni lazima ujue tabia,imani,itikadi,mitazamo na udhaifu wake.Kama
ukiona yupo kama nafsi yako inavyotaka,basi sasa unaweza kuwa naye katika mahusiano
hata ndoa kama mwenza wako (mpenzi wako).Epuka sana kuwa na tabia ya kubadilisha
badilisha mchumba,mara nyingi hutokea kwa vijana wa kiume wanakuwa na tamaa sana
na kama wakikwazwa na wapenzi wao huamua kutafuta mwingine,hii inaweza ikawa
kikwazo kwa maisha yako ya kuipigania kesho yako.Aidha lipo wimbi kubwa la vijana
kutaka mchumba, mke au Mume mwenye uwezo mkubwa wa kifedha au mwenye sura
nzuri,mweupe, na mwenye mwonekano mzuri,wakiamini ndiyo watu sahihi kwao.Nataka
nikufahamishe kijana kuwa hakuna mtu mwenye tabia zote unazozitaka,ila unachotakiwa
ni kuangalia yupi mwenye tabia nzuri nyingi na tabia mbaya chache ? Huyo ndiye
anayekufaa.

35
Sifa za Mke,Mume au Mchumba Mwema

Kijana mwenzangu sitaki upate shida sana,

hizi ni baadhi ya sifa muhimu sana ambazo ili mtu Fulani tuseme ni Mke,Mume au
Mchumba mwema anatakiwa awe nazo:-

a) Awe Mcha Mungu


b) Awe anamjali na kumpenda kwa dhati mwenza wake ( Mumewe,Mkewe au
Mchumba wake)
c) Awe na heshima na utii kwa mumewe/Mkewe/Mchumba wake/Wazazi wa pande
zote mbili pamoja na jamii kwa ujumla
d) Awe anajua na kuona thamani yako
e) Asiwe na tamaa za Kimapenzi na pesa

Aidha wapo Vijana wengi waliwahi kuniuliza kuwa wafanye nini ili waweze kuishi vizuri
katika mahusiano yao na ndoa zao? Ila kiuhalisia katika mahusiano au ndoa unatakiwa
uzingatie mambo yafuatayo;-

a) Kumfahamu mwenzi

Kijana unapokuwa na mahusiano na mwanamke au Mwanaume unayempenda kwa dhati


ya moyo wako.unapaswa kumtambua kwa kuzingatia nini anapenda na nini hapendi. Hata
hivyo unatakiwa uweze kumjua akiwa na shida au tatizo au akiwa hayupo sawa.Hii
inaweza kuondoa migongano katika mahusiano au ndoa.

b) Kumjali Mwenzi

Kijana unatakiwa uoneshe hali ya kumjali mwenzi wako au mpenzi wako,kwa kuonesha
huruma,upendo wa dhati na kusaidiana naye anapokuwa na shida au tatizo.Kila mtu
anapenda kuishi na mtu anayemjali,Wanaume tunalo jukumu kubwa la kuwajali
wanawake wetu na Wanawake pia wanalojukumu la kuwajali Waume zao.Ukishindwa
kumjali mwenzi wako anaweza kukukimbia.

c) Kumheshimu Mwenzi

Siku zote heshima huleta furaha na amani katika mahusiano au ndoa.Hivyo basi,ipo haja
ya Kijana aliyepo katika mahusiano au ndoa,kuonesha heshima kwa mwenzi wake wa
maisha

36
d) Kuwajibika Kwa Mwenzi

Mara nyingi ndoa au mahusiano yanavunjwa kwa sababu ya kukosekana kwa uwajibikaji
wa Mume au Mke katika mahusiano au ndoa.Unakuta Mwanamke anataka kushiriki
tendo la ndoa na mumewe vile ipasavyo,lakini mumewe afanyi ipasavyo.Au la
Mwanaume anataka haki yake ya mahusiano au ndoa,yaani kushiriki katika tendo la ndoa
au mahusiano lakini mwanamke hayupo tayari.Hii inaweza kusababisha kutokudumu kwa
mahusiano au ndoa.

Aidha tabia ya ndani inaweza kumvuta mume,Mke au Mchumba wako aliyepotea kama
vile kuwa na wema,upendo,kujitoa,utii na kujali.Wanaume wanatakiwa kuwapenda na
kuwaheshimu wake zao au wachumba zao.Kumbuka kuna aina tano za upendo ambazo
ni;-

i. Eros huu ni upendo unaotokea kati ya mwanaume na


mwanamke.Upendo huleta watu hawa pamoja kama mke na
mume na kuishi katika misingi ya upendo huu ndani ya ndoa.

ii. Storge huu ni upendo unaotokea kati ya wazazi na watoto


wao.Hii inakuwa ndani ya familia moja baba na watoto,mama
na watoto wake au Dada na Baba,au kati ya wanafamilia.

iii. Phileo huu ni upendo uliopo kati ya marafiki wawili lakini ni


lazima wawe ni wa jinsia moja.Kiuhalisia hakuna upendo au
mahusiano ya dhati kati ya jinsia mbili tofauti ambao si
ndugu.Ni mara chache sana kukutana watu wa jinsia mbili
tofauti ni marafiki wa kweli.Ukikuta watu wa namna hiyo
tambua kuna kitu kinaendelea au kitatokea tu.

iv. Agape huu ni upendo wa KiMungu wa kujitoa,usio na


masharti.Huu unatokea na kudhihirika kwa mtu kufanya
matendo mema yanayompendeza Mungu na kufuata amri na
mafundisho ya Mungu kupitia dini yake.

37
Nayaandika haya kwako kijana wa Tanzania kwa sababu ya mapenzi ya dhati niliyonayo
kwa Taifa langu pamoja nawe kwani sitaki upoteze malengo yako uliyojiwekea.Nakusihi
sana uwe makini na uchaguzi sahihi katika kutafuta mwenza wa ndoa au mchumba.

KANUNI ZA MAFANIKIO

Lengo langu na furaha yangu siku zote ni kuona Kijana wa Tanzania kuwa na mafanikio
katika mipango yake ya kimaendeleo.Ila waswahili wanasema kuwa jambo usilolijua ni
sawa na usiku wa giza.Hii inamaanisha huwezi kufanikiwa bila ya kujua siri za
mafanikio.Kwa mara ya kwanza niliwafundisha siri hizi rafiki zangu waliopo Yombo
Kilakala,kisha ndugu zangu wa kidato cha sita wa mwera sekondari mwezi wanne 2022
akiwemo Muivano Richard na Nancy Mnzava.Lakini kutokana na mapenzi ya dhati
kwako wewe msomaji wa kitabu hiki ambaye unataka ufanikiwe pamoja na familia
yako,naomba usome kwa makini kanuni za mafanikio.Kanuni hizo ni;-

A. Ili uwe tajiri,kuwa mtoaji


B. Ili ufanikiwe,Tumika
C. Ili ucheke,mfanye Mungu acheke
D. Ili ustawi,kuwa mwaminifu
E. Ili ufike mbali,amka mapema
F. Ili umbadilishe mtu,badilika wewe kwanza
G. Ili uwe na nguvu,omba sana
H. Ili ufanye mambo mengi,ongea machache
I. Ili uishi vizuri,samehe wanaokukosea
J. Ili uongee vizuri,zuia hasira
K. Ili upendwe,penda
L. Ili uheshimiwe,kuwa mpole
M. Ili umfunge na kumkemea shetani,jitakase kuwa mbali na dhambi
N. Ili ukue katika Imani,tafakari maneno ya Mungu mchana na Usiku

Katika safari ya kuipigania kesho yapo kama Kijana unatakiwa kuachana na imani
potofu,hata hivyo uwe na wivu wa kimaendeleo.Aidha hakikisha una tunza afya yako na
kuishi na stadi za maisha.

AFYA NA STADI ZA MAISHA

Afya ni hali ya mwili au akili kufanya kazi zake za kawaida bila ya kuwa na tatizo lolote
lile na kwa ufanisi.Kijana anatakiwa kujikinga na magonjwa ambayo yanaweza kuathiri
afya yake.Katika harakati za kupigania kesho yako na hatima ya maisha yako kama
kijana,ipo haja ya kuilinda afya yako.Yamkini usipoilinda afya yako inawezekana
magonjwa yakakushambulia na hata kupoteza malengo yako.Au ukiwa ndiyo umepata au
umefanikiwa unajikuta unashindwa kufurahia maisha ambayo ulikuwa
38
ukiyapigania.Mfano unakuta una vidonda vya tumbo,Kisukari au Magonjwa ya
zinaa,,Figo au Ini kushindwa kufanya kazi.

Wapo ambao wamefanikiwa lakini wanashindwa kufurahia maisha kwa sababu


walishindwa kuzilinda afya zao.Una kuta mtu anashinda na njaa kutwa au anakula
vyakula visivyoeleweka.Ili kuilinda afya yako kama kijana zingatia haya;-

 Zingatia usafi wa chakula chako na ubora wake kwa afya yako,mahali unapoishi au
kukaa kuwe safi,mavazi yako na mwonekano wako kijumla

 Epuka kukaa na njaa kwa muda mrefu pasipo na sababu ya msingi.Hata hivyo
usipende kula vyakula na kunywa vinywaji venye kuathiri afya yako

 Epuka kufanya ngono zembe,hakikisha kama hauwezi kukaa peke yako basi unakuwa
na mpenzi mmoja tu na uwe mwaminifu kwake

 Tenga muda wa kufanya mazoezi.Hakikisha unapata angalau dakika 40 hadi lisaa


limoja kwaajili ya kufanya mazoezi,ili kuimarisha afya yako.Mfano wa mazoezi
kukimbia,kutembea-tembea angalau kwa umbali wa kilometa 1 au mita 800 sawa na
viwanja nane (8) vya mpira

 Pata muda wa kupumzisha akili na mwili wako.Akili pamoja na mwili vikifanya kazi
kwa muda mrefu bila ya mapimziko,basi inaweza kuathiri afya yako.

Ndugu zangu magonjwa ni mengi sana ambayo yanawakumba watu tusimame imara
katika kuilinda afya yetu tu.Ili tusije tukawa tunapambania ndoto au maisha ambayo
tutaishi na huzuni au magonjwa hata kifo.

Stadi Za Maisha

Stadi za maisha ni uwezo wa mtu kutumia akili yake kuishi vizuri katika jamii.Kijana
anatakiwa kuwa na stadi za maisha,kwani zinaweza kufanya maisha yako kuwa bora na
ya kuvutia kwa jamii.Uwezo huu unaweza kumuonesha mtu afanye nini? na kwa wakati
gani? Katika maisha kama kijana unatakiwa kuhakikisha kuwa unakuwa na stadi za
maisha,kwani zitakusaidia kujitambua wewe mwenyewe,Kutengeneza uhusiano mzuri na
watu katika jamii,kuishi katika mazingira magumu hata katika kutatua matatizo.Wakati
mwingine tunatumia stadi za maisha kama ujuzi wa maisha au fani.Katika maisha yako
kama Kijana unatakiwa uwe na stadi zifuatazo;-
39
 Ubunifu

Kijana unatakiwa uwe na uwezo wa kuunda au kutengeneza kitu Fulani, chenye uwezo
wa kukupatia kipato au kukuletea faida katika maisha yako.Vijana wengi sana wamelaza
akili zao katika mambo ya anasa na starehe pamoja na ngono zembe,hali inayowafanya
washindwe kuwa na uwezo mkubwa wa kubuni jambo Fulani.Hapa kijana kama anataka
kufanya biashara utakuta anaiga kwa mtu Fulani kwani yeye hawezi kubuni chake.Kama
kijana unaweza kubuni biashara Fulani au kazi Fulani ambayo inaweza kukupatia
kipato.Unaweza ukabuni namna ya ufugaji wa kisasa au kilimo cha kisasa.Mwalimu
Mkungura ni moja kati ya walimu ambao wanaweza kutoa shamba darasa mara nyingi
yeye anawafundisha wanafunzi wake namna ya kuanzisha miradi mbalimbali.

 Kufikiri

Mwanzoni nilikueleza kuwa kijana ana nguvu nyingi za kiakili,hivyo basi anatakiwa awe
na uwezo mkubwa kufikiri au kutafakari jambo Fulani na kulipatia ufumbuzi wake.Vijana
wengi tumekuwa ni wavivu wa kufikiri juu ya namna ya kufanya maisha yetu kuwa bora
katika jamii na kujikuta tunafanya mambo ya kushangaza jamii kwa kukosa kufikiri.Ili
uweze kufanikiwa ni lazima kuchemsha ubongo,ili kuweza kujua namna ya kutoboa
kimaisha hata ukiwa katika mazingira magumu.

 Kuchagua

Kijana unatakiwa kuhakikisha kuwa unakuwa na uwezo wa kuchagua kitu au jambo


ambalo ni sahihi,bila ya kufanya makosa.Namna ambayo unaishi leo inatokana na
uchaguzi wako wa jana,ukifanikiwa kuchagua vizuri leo basi utafanikiwa kuishi vizuri
mbeleni.Ni lazima vijana tuwe na nguvu ya uchaguzi sahihi.

 Kutatua Matatizo

Ni ukweli kuwa katika kutafuta maisha,kijana ni lazima akumbane na matatizo


mbalimbali.Pamoja na ukweli huo ni lazima kijana awe na uwezo wa kutumia akili yake
katika kutatua matatizo mbalimbali yatakayo mkumba katika kutafuta maisha.Bila ya
kujali ukubwa wa tatizo,dawa ya tatizo si kulikimbia bali ni kulitatua,kama ukilikimbia
je,una uhakika gani kwamba huko uendapo hakuna tatizo kama hilo,na vipi kama

40
likitokea tena?Tumia akili yako katika kutatua matatizo utakayo kumbana nayo katika
harakati za kimaisha.

 Kijana unatakiwa uwe na uwezo wa kutambua hisia zako,mawazo yako,ubora na


udhaifu wako
 Kijana unatakiwa uwe na uwezo wa kutawala hisia na mawazo yako
 Kijana pia unatakiwa kujua nini unataka,na kwanini na kwa njia gani unaweza
ukakipata utakacho?
 Uwe na uwezo wa kuchagua rafiki mzuri ambaye utachangia naye mawazo,furaha
na huzuni.Aidha rafiki mzuri ni Yule mwenye heshima kwa wazazi wako na
wake,ndugu,wazee,jamaa na marafiki.Mwenye kutoa msaada pindi kunapotokea
tatizo
 Uwe na uwezo wa kutengeneza mahusiano mazuri na wanajamii
 Kuwasiliana na watu vizuri
 Uwe na uwezo wa kuelewa na kuwa na uchungu juu ya mawazo na changamoto
za wengine

MWISHO

Mimi ni Isack Steven Masatu ni mwanafunzi wa Kidato cha nne katika Shule ya
Sekondari Mwera,ni Kijana kutoka familia ya maisha ya chini sana.Najua wapo ambao
watachukia juu ya kazi yangu hii,ila naomba wanisamehe.Lengo langu si kuandika

41
mambo ambayo yatakukera,hapana bali ni kukusaidia wewe kijana mwenzangu
kimawazo,ili uweze kufanikiwa.Mara nyingi napenda sana niitwe Mzalendo,kwani nipo
tayari kufanya chochote kile kwaajili ya Taifa langu teule la Tanzania.Ila hakuna mtoto
wala mzee atakaye weza kulijenga Taifa letu la Tanzania,bali wewe Kijana ndiye
utakayoifanya Tanzania iendelee au isiendelee.

Vijana tunatakiwa tutafute maisha na si mapenzi au anasa,kwani tunatakiwa kupigania


nchi yetu,pia tunatakiwa tuandae maisha mazuri ya familia zetu.Maana baada ya kipindi
hiki cha ujana unaenda kuitwa Baba au Mama sijui utalaumiwa au utapongezwa na
watoto wako.Uzembe wako leo wewe kijana unaweza kuathiri kizazi chako,mfano kama
wewe utapambania maisha leo na uzee wako ukawa maskini basi usitegemee watoto
wako watakuja kuwa na maisha mazuri kama wasipopambana,na wakati mwingine
mapambano yao yakaharibiwa kwa kuiga tabia zako.Lakini kama ukiwaandalia watoto
wako sasa hivi maisha mazuri basi hautopata shida wala lawama uzeeni mwako.Simama
sasa hivi wewe bado ni Kijana tafuta maisha yako,usipende kuwategemea wazazi maana
wanaweza kukulemaza

Aidha Kijana kama bado hujafanikiwa,usipende anasa wala kuiga maisha ya mtu,maana
unaweza ukashindwa kufikia malengo yako.Usijali wenzako wanasemaje juu yako,bali
unachotakiwa kujua ni kwamba unachokifanya ni sahihi au si sahihi,kama ni sahihi basi
endelea kupambana.Kama si sahihi basi tafuta namna nzuri kiwe sahihi.

Ndugu zangu Watanzania kuzaliwa maskini si kosa bali kosa ni kufa maskini.Kwani wale
wanaoendesha magari ya kifahari wametoka mbingu gani na sisi mbingu gani? Sote
tumeumbwa na Mungu mmoja bali tunatofautiana katika juhudi za kutafuta
maisha.Usipende kukubali kuwa wachini siku zote,kataa umaskini na ujinga simama
unaweza ukatoboa kabisa.Mheshimiwa Juma Hamidu Aweso Waziri wa Maji ni mtoto
wa mama ntiliye lakini kupambana kwake kumemfanya awe waziri wa maji wa jamuhuri
ya muungano wa Tanzania.

Ndugu yangu,maisha haya yanaenda kwa kanuni pamoja na ujanja.Mara nyingi napenda
kuilezea kanuni yangu ambayo naiamini sana katika kuipigania kesho yangu.Kanuni hiyo
ni PHD ikiwa na uchambuzi ufuatao;-

 Pray for Your Believe (Omba kupitia dini yako kwajili ya Ndoto zako).Katika
imani tunaona kuwa maombi ndiyo kila kitu,na tukiomba Mungu anatusikia
dua zetu na sala zetu naye utufanyia wepesi wa kufanikiwa

 Hardworking in Your Preparation (Juhudi katika kufanya


maandalizi).Unaweza ukawa na mipango mizuri juu ya maisha yako,lakini
ukiwa hauna jitihada katika kupigania malengo yako na kufanya maandalizi
ya kesho yako ya ushindi,basi ni lazima ushindwe.Hivyo kuwa na jitihada
katika kuipigania kesho yako

42
 Despline to the People (Nidhamu kwa watu).Hapa wengi tunaanguka kwa
kukosa nidhamu kwa watu ndani ya jamii.Vijana wengi hatuna heshima wala
utii.Hii inapelekea kukosa Baraka za wana jamii,nakupelekea dua mbaya
kutoka kwao,hali inayoweza kusababisha kutopewa nafasi za kazi kama
zikitokea na kuzibiwa milango yetu ya Baraka.Hivyo tuwe na nidhamu.

Aidha Vijana sasa hivi tumekumbwa na tatizo la kuiga miondoko na tabia za watu
weupe,na kutaka kuishi kama wao kitu ambacho hakiwezekani na hata kikiwezekana
hakina maana,bali kina hasara kwetu.Utakuta kijana anatembea na vinguo vifupi au modo
kisa ameona msanii Fulani amevaa kwenye nyimbo au sanaa yake,wakati mwingine
tunaiga tabia za waigizaji au tabia za watu wa Taifa Fulani.Mfano ukifuatilia mashoga
ambao wamefikia kutoa kabisa uume na kuweka uke wanasema mbona wamarekani
wanafanya.Sawa wanafanya ila tambua ukweli kuwa kila Taifa lina tamaduni zake na
itikadi zake (Norms).Nahisi bado haujanielewa basi ni hivi ``The one which can be
right to you is the one which can be wrong to me and the one which
can be right to me is the one which can be wrong to you`` yani kitu
ambacho ni sahihi kwa Taifa Fulani,sehemu Fulani au mtu Fulani,kitu hiko hiko
kinaweza kuwa si sahihi kwa Taifa lengine,sehemu nyingine au mtu mwingine.Na kitu
ambacho kwa Taifa Fulani,sehemu Fulani au mtu Fulani si sahihi kinaweza kuwa sahihi
kwa mtu mwingine,Taifa au sehemu nyingine.Mfano kuvuta bangi kwa Korea Kaskazini
ni jambo la kawaida lakini kwa Tanzania si ruhusa,ushoga marekani ni jambo la kawaida
lakini kwa Tanzania si jambo la kawaida.Kijana mwenzangu usipende kuishi maisha ya
kuiga si mazuri yanaweza kukupotezea muelekeo.

Vijana wenzangu ni lazima tusimame imara kwajili ya kulitetea Taifa letu, kwani Taifa
litaangamia pasipo sisi.Aidha serikali ni lazima iwaunge mkono na kutoa mafunzo mara
kwa mara ya uzalendo na stadi za maisha kwa kijana.Taifa likiwa linatumia sana watu
wazima kuliko vijana basi inaweza kuwa chanzo cha kudumaa kwa maendeleo ya Taifa
hilo.Lakini pia Taifa bila ya kukosolewa kamwe haliwezi kuendelea.Bunge ni chombo
muhimu sana katika kujadili maendeleo ya Taifa lakini kama kukiwa na wabunge kutoka
vyama tofauti tofauti na si Chama tawala tu.Kama bunge likiwa na chama tawala tu,basi
kila kitu kitapitishwa na kuonekana bora,tunahitaji viongozi wa vyama pinzani pia
wapewe nafasi,ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo.Naandika hivi kama Mzalendo wa
Tanzania na mwenye haki ya kuongea.Vijana ni lazima tupambanie maisha yetu pamoja
na Taifa Letu.

43
Kwa wale ambao watakuwa na maoni au chochote kile kuhusu kitabu hiki wanitafute
Whatsapp namba 0655597525 au Email: Stephenmasatu@gmail.com au
kwenye mitandao mengine ya kijamii kama vile Facebook na
Instagram kwa jina Isack Masatu au Twiter jina Mwinjilisti Isack.

SHUKRANI

Haikuwa rahisi mimi nifike hapa vikwazo vingi nimekutana navyo,niliandika vitabu
viwili lakini baada ya kutafuta msada wakukitoa nikaibiwa na wakabadilisha baadhi ya
taarifa.Ila pia kutafuta pesa za kuchapisha kitabu hiki pia ikawa changamoto pamoja na
hayo yapo mengi niliyopitia mpaka kukamilisha kazi hii lakini kwa kuwa neema ya
Mungu ndiyo iliyoniwezesha basi sina budi kusema ahsante MUNGU wa Mbingu na
nchi.Aidha kwa dhati ya Moyo wangu natoa shukrani kwa watu wafuatao.Kwanza Mama
yangu kipenzi Joyce Lucas kwa kunipa malezi na msada wa mali na hali katika
kuwezesha kazi yangu pamoja na Baba yangu kipenzi Steven Masatu.Pili wale wote
waliyoweza kunipa ushauri na taarifa zao wakati nilipokuwa katika tafiti za kuandaa
kitabu hiki,najua haikuwa rahisi ila nipende kuwashukuru John Dafa,Dr Angel na
Mwalimu Peter Moshi.Lakini pia nawashukuru sana wahakiki wa kazi hii kwa msaada
wao mkubwa wa kitaalamu Dorith John,Upendo Jackson,Happy Elyson na Mariamu
(kidato cha tano HKL Mwera sekondari)

Aidha kupitia maneno na hotuba za kizalendo za mwalimu wangu kipenzi Jahazi Mkali
na Salimu Hamadi zimenifanya mimi niandike kazi hii basi sina budi kuwashukuru kwa
hili.

Natoa shukrani pia kwa wanafunzi wenzangu wote wa shule ya mwera sekondari kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha sita pamoja na Mkuu wetu wa shule Jausia Mziray na wana
Pangani kwa ujumla kwa kunipa chachu ya kuandika kitabu hiki. Lakini pia kwa namna
moja hama nyingine nawashukuru wale wote ambao wameweza kukisoma kitabu hiki na

44
kupata ujumbe uliopo ndani ya kitabu hiki.Tambua kuwa nimetumwa na najiandaa nije
kuisaidia jamii yangu ya Tanzania,I love Tanzania so much.Ahsante Mungu

GOD IS ABLE

AND

CAPABLE

The Patriot ISACK

STEVEN

MASATU

45

You might also like