Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

TAMTHILIA: WEMA HAUOZI - TIMOTHY

AREGE

MWONGOZO

UCHAMBUZI WA JALADA

Enovate CBC Revision App


UCHAMBUZI WA JALADA

PICHA KWENYE JALADA

Jalada la tamthilia ya Wema Hauozi linaleta mawazo mazito kuhusu Kazi yake Timothy Arege.

Rangi nyeupe ambayo imetumika kuandika anwani ya kitambu. Rangi nyeupe katika kazi ya fashihi

huashiria Amani, utu au wema. Mabula katika tamthilia hii ni muhusika ambaye ana utu kwa jamii.

Anafichua uozo wa viongozi kwa sababu anapenda Amani na wema.

Picha iliyochorwa inabainika kuwa ya mwanamke kwa sababu ya Nywele.Mwanamke huyu

anaelekea kuwa Mishi. Mwanamke huyu ana weusi mwingi kwenye sehemu ya kichwa. Weusi huu

unaonyesha hali ngumu ambayo anapitia kutokana na tatizo la mmewe la kuachishwa kazi.

Amesimama kama mtu anayenyenyekea. Mwanamke huyu amevaa mavazi ya kiafrika nay a heshima

kuonyesha ni mke mwema mwenye maadili.

Rangi ya chani kiwiti ambayo kulingana na fasihi huashiria uahi, rutuba na mafanikio. Japo kuna

matatizo katika familia ya mabula. Ipo siku wema wake utaleta rutuba katika maisha yao. Maana ya

rangi hii inajulikana wakati Mabula anapata kazi mbili mara moja kutokana na wema wake.

Maneno ‘Tamthili ya Gredi ya nane’ yameandikwa kwa rangi ya manjano. Rangi ya manjano

huonyesha ukomavu. Mwandishi wetu Timothy Arege. Amekomaa katika kazi ya uandishi. Ameandika

taamthilia nyingi kama vile, Mstahiki Meya, Kijiba cha Moyo,Majira ya Utasa, Duara, Si shwari na

Bembea ya maisha.

Revision materials:cbcresources.co.ke Enovate CBC Revision App


ANWANI

Anwani ya tamthilia hii ni WEMA HAUOZI. Limeundwa na maneno mawili; wema na neno hauozi.

Wema ni neno linaloashiria ukarimu,fadhila na uadilifu. Kuna baadhi ya wahusika ambao wana

ukarimu, utu, uadilifu na fadhila.

Muhusika Mabula ni mwenye wema. Anatetea haki za raia kwa kufichua kwamba fedha zinaenda kwa

mifuko ya viongozi.

Neno hauozi linaashiria kwamba licha ya changamoto nyingi, mateso na shida, ipo siku wema utashinda

uovu. Muhusika mabula anaachishwa kazi, familia yake imapitia wakati mgumu, watoto wake

wanapitia hali ngumu ila baadaye ule wema alitenda unaonekana na kumlipa kwa kazi tena. Hata kama

kuna juhudi za kuukomesha wema kuna wakati wema hushinda uovu.

Revision materials:cbcresources.co.ke Enovate CBC Revision App


DHAMIRA

Dhamira ni lengo au sababu la kufanya jambo. Mwandishi wetu timothy Arege alikuwa na malengo

makuu ya kuandika tamthilia hii.

Malengo haya ni kama vile;

1.Kuonyesha mgongano kati ya wema na ubaya. Tamthilia inaagazia mgongano ambao hutokea katika

jamii kati ya wema na ubaya. Baadhi ya wahusika kama vile Mabula wanakumbwa na matatizo kwa

sababu ya kutenza wema.Viongozi katika mataifa hukabiliwa na chaguzi kati ya kutenda wema kwa raia

na kujilimbikizia mali.

2.Kuhimiza uadilifu na ukarimu. Mwanishi alilenga kuonyesha kuwa kuwa maadili yanaweza kulipa.

Hili linadhihirika kupitia mabula ambaye anapata kazi kutokana na ukarimu wake. Isitoshe, familia yake

inasaidiwa na watu kufuatia ushujaa wake wa kutetea haki.

3. Alilenga kuonyesha madhara ya ubinafsi. Madhara ya ufisadi na ubinafsi ni kama vile watu kukosa

ujira, hali ngumu ya maisha na mizozo katika familia.

4. Mwandishi alilenga kuhamasisha jamii kuhusu matumaini. Licha ya kuipoteza kazi yake,

mabula ana matumaini kwamba ipo siku atapata kazi. Wazee wenzake kama vile temba wanamwimiza

awe na matumaini ipo siku wema wake utashinda uovu.

5. Mwandishi alilenga mumwelimisha msomaji kuhusu masuala kama vile wema, ufisadi, ubinafsi,

ukarimu bidi na maswala mengine.

Revision materials:cbcresources.co.ke Enovate CBC Revision App

You might also like