Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 200

1

SURA YA KWANZA

ILIKUWA ni taarifa mbaya, iliyoshtua ambayo ilianza kwa kusikika katika


sehemu mbalimbali jijini Las Vegas nchini Marekani kabla ya kuwafikia polisi.
Kila aliyezisikia taarifa hizo, hakuamini, wengi wakahisi hazikuwa taarifa za
kweli, labda kulikuwa na mtu mwingine aliyetaka kuivumisha habari hiyo ambayo
ilimsisimua kila mtu aliyeisikia.
Msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la Stacie Lawrence, msichana aliyebahatika
kunyakua taji la Urembo wa Dunia, alikutwa amekufa ndani ya chumba kimoja cha
Hoteli ya Vikings Hill iliyokuwa Las Vegas, Nevada nchini Marekani alipokuwa
amepanga huku akisubiri kuonana na Mkurugenzi wa Mtandao wa Google kwa
ajili ya kusaini mkataba wa picha zake kutumika katika programu moja ambayo
ingetumiwa katika simu zote zinazotumia system ya android.
Stacie aliyekuwa gumzo kwa kipindi hicho duniani kutoka na uzuri wake, alikutwa
amekufa baada ya kujiovadosi madawa ya kulevya aina ya Heroine kwa kujichoma
sindano katika mkono wake wa kulia wakati kitandani ndani ya hoteli hiyo.
Hiyo ndiyo ilikuwa habari ya mjini, kila aliyeisikia, hakuamini, swali la kwanza
kabisa walilojiuliza watu ni juu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Kila mtu
alijua Stacie hakuwahi kutumia madawa hayo, si kipindi hicho tu, hata kabla ya
kutwaa taji hilo, hakuwa mtumiaji, sasa ilikuwaje mpaka leo hii akutwe chumbani
kitandani akiwa amejidunga madawa hayo? Hilo lilikuwa swali lisilokuwa na
majibu.
Waandishi wa habari kutoka katika mashirika mbalimbali ya televisheni habari
kama CNN, BBC, Sky News na hata wale wa magazeti kama New York Times, 24
News tayari walikuwa nje ya hoteli hiyo, vitendea kazi vyao vyote vilikuwa
mikononi mwao, walitaka kupiga picha na kupata habari kuhusu kifo cha msichana
huyo mrembo ambaye bado uzuri wake ulikuwa gumzo duniani.
Polisi walitanda kila sehemu nje ya hoteli hiyo, mkanda wa njano ulioandikwa Do
Not Cross yaani ‘Usivuke’ ulizungushiwa katika hoteli hiyo kwa muda.
Magari ya wagonjwa mawili yalikwishafika katika hoteli hiyo, kilichosubiriwa ni
kuingia ndani na kuuchukua mwili huo.

2
Waandishi hawakuruhusiwa kabisa kuingia ndani ya hoteli hiyo, waliambiwa
wasubiri hapo nje wakati polisi wakiingia ndani kwa ajili ya kufanya kazi yao,
hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri.
Polisi wakaingia ndani ya chumba kile. Huko wakaukuta mwili wa Stacie ukiwa
kitandani, mkono wake wa kushoto kulikuwa na sindano iliyochoma mshipa wake,
aliishikilia kwa kutumia mkono wake wa kulia mbali na hivyo, pembeni yake
kulikuwa na noti za Dola, Paundi, Yeni na Euro.
Udenda ulikuwa ukimtoka, pale alipokuwa, hakutingishika, kilikuwa kifo kibaya,
kilichozua maswali mengi kwa watu wengi, maswali hayo yote, hapakuwa na mtu
aliyekuwa na majibu zaidi ya Stacie mwenyewe ambaye kipindi hicho alikuwa
marehemu.
“This is the fifth one, what the hell with the drugs?” (Huyu ni mtu wa tano, kuna
nini na haya madawa?) alisikika akiuliza mwanaume mmoja huku akionekana
kushangaa.
“I don’t know. What the hell with these teenagers, they always test each and every
goddamn thing, why?” (sifahamu. Nini kinaendelea kwa hawa vijana, mara nyingi
wanapenda kujaribu kila kitu, kwa nini?) aliuliza mzee mmoja huku akionekana
kukasirika.
Kila mmoja alishangaa, huyo hakuwa mtu wa kwanza, supastaa aliyejiua baada ya
kujiovadozi kwa madawa ya kulevya, huyo alikuwa mtu wa tano, kijana supastaa
ambaye aliamua kujiua kwa kujidunga sindano ya madawa hayo.
Mtu wa kwanza kabisa kujiua kwa kujidunga shindano alikuwa Paul McKenz.
Huyu alikuwa mcheza kikapu aliyekuwa akichipukia, mwenye sura nzuri,
alijitengenezea jina kubwa katika Timu ya La Lakers, akaanza kupata mashabiki
wengi, alipendwa na kila mtu aliyekuwa akiupenda mchezo huo, jina lake likaanza
kuwa kubwa, akapata mikataba mingi lakini mwisho wa siku, Paul akaja kujidunga
sindano yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine chumbani kwake.
Watu wengi walisikitika kwani ndiye alikuwa kijana aliyekuwa akichipukia katika
mafanikio makubwa. Hiyo haikuishia hapo, pia kulikuwa na kijana mwingine
aliyekuwa na kipaji cha uigizaji. Katika filamu yake ya kwanza ya Fallen Tree,
alishinda Tuzo ya Oscar, Global na nyingine nyingi, huyu aliitwa Todd Lewis.
Bahati ikaanza kuonekana upande wake, akapendwa sana, kila kona alisikika yeye
tu. Kadiri jina lake lilivyovuma ndivyo alivyozidi kujitengenezea mashabiki.

3
Wakati akiwa amenunua gari yake ya kwanza ya thamani kabisa aina ya Ferrari
Testarossa nyekundu, akakutwa naye akiwa amejidunga madawa ya kulevya ndani
ya gari lake nje ya klabu moja huku pembeni kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan
na Euro. Watu walisikitika na kulia, vilio vyao, huzuni zao hazikuweza
kuwarudisha watu hao duniani.
Mtu mwingine kabla ya Stacie kujiua kwa madawa ya kulevya alikuwa kijana
aliyeitwa kwa jina la Carter Phillip. Huyu alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa
wakichipukia katika muziki wa Pop. Alikuwa na sauti kali, yenye nguvu ambapo
kila alipokuwa akiitumia katika nyimbo zake, wanawake walichanganyikiwa.
Alikuwa mzuri wa sura, mwili uliojengeka. Kibao chake cha kwanza kabisa cha
Come and Get Me Shawty alichokitoa kilitingisha kila kona duniani. Uwezo wake
ulionekana, si hapo tu hata kwenye Shindano la American Got Talent, mpaka
aliposhinda, watu waliona kipaji kikubwa ndani yake.
Wengi wakatabiri Carter angekuwa mrithi sahihi wa Michael Jackson, wengi
wakamtabiria mema, njozi njema ikaonekana mapema kabisa kwani ngoma zake
mbili alizozitoa, zote zilishika nafasi za juu kabisa katika orodha ya Billboard.
Akatengeneza fedha nyingi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na tisa.
Akapendwa, akawa kipenzi kikubwa cha watu ila baada ya kwenda nchini
Uingereza kwenye Tamasha la UKIMWI lililokuwa likifanyika katika Jiji la
Southampton, akakutwa akiwa amejiua ndani ya chumba alichochukua hotelini
baada ya kujidunga sindano iliyokuwa na madawa ya kulevya aina ya
Dextromethorphan huku pembeni kukiwa na noti za dola, paundi, yuan na euro.
Hapakuwa na aliyejua sababu ya vijana hao kujidunga madawa hayo ya kulevya,
kila mtu aliyepata habari za vijana hao alishtuka. Mpaka katika kipindi ambacho
msichana mrembo, Stacie kujiovadozi madawa hayo.
Bado watu hawakujua sababu ilikuwa nini, ni afadhali kama wangekuwa
wamepigika katika maisha yao, ila kilichoshangaza, walikuwa wakianza kupata
umaarufu, kupata fedha, na ndipo kipindi hichohicho nao waliamua kujidunga
madawa ya kulevya.
Dunia ikatetemeka, watu wakaogopa kuwa mastaa, wengi walisikia kwamba
unapokuwa staa, ilikuwa ni lazima kutumia madawa ya kulevya.
Wazazi walipowaona vijana wao wanaanza harakati kupitia vipaji vyao,
waliwazuia kwa kuona mwisho wa siku wangejiua kama hao wengine.

4
Swali kubwa ambalo waandishi wa habari walihoji, mitaani ni sababu gani
zilizopelekea vijana hao kujidunga madawa ya kulevya? Kila aliyeuliza swali hilo,
alikosa jibu kabisa.
“You are a killer,” (Wewe ni muuaji)
“No! I am not a killer officer, I am not,” (Hapana! Mimi si muuaji ofisa, mimi si
muuaji)
“You killed them, why? Why did you kill them? Why?” (Umewaua, kwa nini?
Kwa nini umewaua? Kwa nini?)
“I killed nobody officer,” (Sijamuua yeyote ofisa)
Yalikuwa ni mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba kimoja katika
Kituo Kikuu cha Polisi jijini New York. Ndani ya chumba kile, kulikuwa na kijana
mmoja, kwa kumwangalia, alikuwa na miaka isiyozidi ishirini na tano, alikuwa
mtu mwenye mchanganyiko wa rangi, mama yake alikuwa Mzungu na baba yake
alikuwa mtu mweusi.
Polisi wanne waliovalia makoti makubwa ambayo nyuma yaliandikwa NYPD
yaani New York Police Department walikuwa wakifanya naye mahojiano kwa
sauti kubwa, walimuuliza maswali na kumwambia kwamba yeye alikuwa muuaji
lakini alikataa, alikataa katakata lakini polisi hawakuacha, waliendelea
kumwambia alifanya mauaji.
Polisi hao walizungumza naye kwa zaidi ya dakika arobaini, neno lao lilikuwa
lilelile kwamba mtu huyo alikuwa muuaji. Kijana huyo aliyeitwa Benjamin
Saunders hakukubali, aliwaambia wazi hakuwa amemuua mtu yeyote na katika
maisha yake hakuwahi kuua hata siku moja.
Polisi hawakuridhika, waliendelea kumwambia hivyohivyo mpaka baada ya dakika
kadhaa walipotoka ndani ya chumba hicho. Benjamin alikuwa kimya, pingu
zilikuwa mikononi mwake, alilia, kila alipokiangalia kile chumba, moyo wake
ulimuuma mno, hakuwahi kufikiria kama kuna siku angeitwa ndani ya jumba hilo
kubwa la polisi na kuambiwa aliua.
Wakati akiwa humo huku akilia, mara mlango ukafunguliwa, wanaume wawili
waliovalia suti nyeusi wakaingia ndani, mmoja alikuwa na begi dogo, wakachukua
viti na kukaa mbele yake.

5
Hawakuzungumza kitu kwanza, walibaki wakimwangalia kwa muda,
waliporidhika, wakachukua vitambulisho vyao na kumuonyesha Benjamini,
walikuwa ni maofisa kutoka katika Shirika la Kijasusi la FBI (Federal Bureau of
Investigation).
“Naitwa Brett Phillip,” alisema mwanaume mmoja.
“Naitwa Ryan Cashman,” alisema mwingine na kunyamaza.
Benjamin akawaangalia wanaume hao usoni, walionekana kuwa makini na kazi
yao. Walipoona kijana huyo ameangalia vitambulisho vyao na kujiridhisha
kwamba walikuwa maofisa kutoka FBI, wakavirudisha vitambulisho vyao
mifukoni.
“Tunajua hukuua, tunajua hilo Benjamin,” alisema Brett huku akimwangalia
Benjamin usoni.
“Ndiyo! Sijaua, sijawahi kuua, na kamwe sitoua,” alisema Benjamin kwa sauti ya
chini huku akijifuta machozi.
“Ila alama zote zinaonyesha kwamba uliua,” alisema Brett.
“Sijajua nini kilitokea ila sijamuua mtu yeyote,” alisema Benjamin.
“Kweli?”
“Ndiyo! Sijamuua yeyote yule.”
Alichokifanya Brett ni kuchukua begi lake aliloingia nalo humo ndani, akalifungua
na kutoa karatasi fulani kisha kuiweka mezani huku akimtaka Benjamin aichukue
na iangalie.
“Mungu wangu!” alisema Benjamin huku akianza kulia.
“Kweli mpaka hapo unasema hujaua?”
Benjamin akabaki kimya, kile alichokiona kwenye karatasi ile hakuamini, hakujua
kitu gani kilitokea, mbele yake aliona giza na kuona maisha yake yakienda kuisha
gerezani kama si kuchomwa sindano ya sumu au kunyongwa.
Mdomo wake ulikuwa mzito mno, hakuamini alichokuwa akikiangalia katika
karatasi ile, akawaangalia maofisa waliokuwa mbele yake, walionekana kuwa
makini na kazi zao, mtazamo waliokuwa wakiutumia kumwangalia Benjamin,

6
ulionyesha walikuwa na uhakika kwamba kijana huyo alifanya mauaji waliyokuwa
wakimshuku.
“Una lolote la kujitetea kabla hatujakwenda mahakamani?” aliuliza Brett.
“Sikuwahi kufanya mauaji, sijui nini kilitokea...”
“Lakini alama zako zimekutwa kama ushahidi.”
“Najua, ila sijafanya mauaji......ninaanza kukumbuka, ninaweza kuwatajia
aliyefanya mauaji haya, ila si mimi. Nakumbuka niliambiwa nifanye mauaji haya,
nikakataa, nililazimishwa sana, niliendelea kukataa, nikaambiwa kama ninakataa,
basi kuna mtu atafanya mauaji, baada ya hapo, nitaonekana mimi ndiye nimefanya
mauaji. Mungu wangu! Kwanza mchumba wangu Vivian yupo wapi? Walimuua,
kwa nini walimuua msichana ninayempenda?” aliuliza Benjamini huku akilia.
Maofisa wale walibaki wakimwangalia, alionekana kukumbuka kitu, kwa jinsi
alivyokuwa akijitetea, hata muonekano wake ulionyesha kabisa hakuwa amefanya
mauaji.
Kitendo cha kusema kwamba alimfahamu muuaji, kwa maofisa hao kilionekana
kuwa nafuu kwao, hicho ndicho kitu walichokihitaji kwani kwa jinsi mauaji
yalivyofanyika, ilikuwa ni vigumu kumgundua muuaji.
“Sawa! Sasa muuaji ni nani?” aliuliza Brett huku yeye na mwenzake
wakimwangalia Benjamin usoni.

****
Julai 4, 2010, Washington DC
Zaidi ya watu elfu tatu walikuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya Ikulu ya
Marekani, White House kwa ajili ya kusikiliza hotuba kutoka kwa rais wa nchi
hiyo, Barack Obama ambaye ndiye alikuwa akitimiza mwaka wa pili tangu aingie
madarakani na kuwa rais wa nchi hiyo.
Watu wote waliokuwa hapo, walikuwa na bendera za nchi yao, waliipenda,
waliitukuza na kuiona kuwa na thamani kuliko nchi zote duniani.
Siku hiyo ya kusherehekea Uhuru wa nchi yao tangu mwaka 1776 ambapo George
Washington aliuchukua kutoka kwa Waingereza, ndiyo siku ambayo Wamarekani
wote duniani huithamini kuliko siku yoyote ile.

7
Wanafunzi hawakwenda shuleni, wanachuo hawakwenda vyuoni, wafanyakazi
hawakwenda kazini, yaani kila mtu alitakiwa kukaa nyumbani kwake, kwa wale
waliokuwa mbali na Jiji la Washington, walitakiwa kubaki nyumbani na kuangalia
kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko kupitia runinga zao ila kwa waliokuwa
Washington tena waliokuwa na nafasi, walitakia kufika katika uwanja wa Ikulu ya
Marekani, White House.
Miongoni mwa watu wengi waliokuwa katika eneo la uwanja wa Ikulu hiyo
alikuwepo kijana msomi kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard, Benjamin
Saunders ambaye alibakiza mwaka mmoja kabla ya kuhitimu masomo yake.
Benjamin hakuwa peke yake, alikuwa na mpenzi wake, Vivian ambaye alisafiri
kutoka Los Angeles mpaka hapo Washington kwa ajili ya kumsikiliza rais wao
mweusi ambaye alitaka kuzungumza na Wamarekani wote duniani.
Kama walivyokuwa wengine, hata na wao walikuwa na bendera za nchi hiyo
mikononi mwao. Muda wote walikuwa wakishangilia, walionekana kuwa na
furaha mno huku wakati mwingine wakikumbatiana, hakukuwa na kitu
kilichowapa furaha kama kuwa wote katika kipindi kama hicho.
Walipendana mno, hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kuwatenganisha.
Japokuwa walikuwa kwenye mafarakano ya mara kwa mara lakini muda mwingi
walionekana kuwa na furaha kana kwamba hakukuwa na kitu kibaya kilichokuwa
kikiendelea.
“Tukitoka hapa?” aliuliza Vivian.
“Twende nyumbani!”
“Kwako?”
“Kwani unaogopa nini?”
“Siogopi chochote, ila naweza kuchelewa masomo,” alijibu Vivian.
“Wala usijali, utawahi tu,” alisema Benjamin.
Benjamin alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichokuwa jijini
Cambridge ndani ya Jimbo la Boston hapohapo nchini Marekani, mbali na kutoka
katika familia iliyokuwa na fedha, Benjamin alikuwa na uwezo mkubwa chuoni.
Alikuwa akichukua masomo ya uuguzi, ndoto yake kubwa iliyokuwa mbele yake
ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Marekani.

8
Hiyo ilikuwa ndoto yake, hakutaka kuiona ikipotea, katika maisha yake, alimuahidi
mama yake kwamba kuna siku angekuwa daktari mkubwa wa magonjwa ya moyo
nchini Marekani, baba yake alikufa kwa ugonjwa wa moyo, hakutaka kuona watu
wengine wakifa na ndiyo maana alisoma sana kufanikisha ndoto hiyo aliyojiwekea.
Mpenzi wake alikuwa akisomea masomo ya uandishi wa habari katika Chuo cha
UCLA (University of California, huko Los Angeles). Kama alivyokuwa Benjamin,
hata naye Vivian alikuwa na uwezo mkubwa darasani, aliwaongoza wanachuo
wenzake na kuonekana kufanya mambo makubwa hapo baadaye kupitia uandishi
aliokuwa akiusomea.
“Ngriii...ngriii...ngriii...” ulisikika mlio wa simu ukiita, mbali na kuita, simu hiyo
ilikuwa katika mtetemo.
Mlio wa simu hiyo waliusikia kwa mbali kutoka na kelele zilizokuwa mahali hapo
lakini baada ya Benjamin kuhisi mtetemo huo kutoka mfukoni mwake,
harakaharaka akaichukua simu hiyo.
Alishangaa, haikuwa simu yake lakini aliikuta katika mfuko wa koti lake, si yeye
tu aliyeshangaa, hata msichana wake, Vivian alishangaa pia. Walibaki
wakiangaliana kwa sekunde kadhaa, hawakujua ni nani aliiweka simu ile katika
koti lake na wala hawakujua lengo la huyo mwekaji lilikuwa nini.
“Hiyo simu umeitoa wapi?” aliuliza Vivian.
“Sijui, ndiyo kwanza nimeikuta mfukoni mwangu!”
“Nani amekuwekea?”
“Sijui pia.”
“Hebu pokea.”
Alichokifanya Benjamin ni kuipokea simu ile na kuita. Japokuwa mtu wa upande
wa pili alikuwa akizungumza lakini Benjamin hakuweza kumsikia kutokana na
kelele zilizokuwa mahali pale.
Wakati akiwa na simu hiyo sikioni, mara wanaume wawili waliovalia suti
wakamsogelea, wakaanza kumwangalia na kumshika mkono huku wakimtaka
wamfuate.
“Kuna nini?”

9
“Wewe twende tu,” alisema mwanaume mmoja, Benjamin hakuwa na wasiwasi,
akaanza kuwafuata kama alivyoambiwa, hata Vivian naye hakutaka kubaki mahali
hapo, naye akaanza kuwafuata huku akionekana kuwa na hofu kubwa, kichwa
chake kikaanza kujiuliza mambo mengi kuhusu watu wale, walikuwa wakina nani?
Akakosa jibu.
Benjamin akaongozana na watu wale mpaka walipofika katika gari moja kubwa
ambalo hakujua ndani kulikuwa na nini, akaambiwa aingie na mpenzi wake kisha
kukaa katika kiti kimoja, ndani ya gari hilo, kulikuwa na televisheni nyingi
zilizokuwa zinaonyesha matukio yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano ule.
Hakukuwa na mtu aliyezungumza lolote lile, kila mmoja alikuwa bize akifanya
mambo yake. Benjamin na mpenzi wake, Vivian walikuwa karibukaribu, msichana
huyo alionekana kuwa na wasiwasi mno, hakuwa na amani wala furaha, kwake
alichokiona mbele yake kilikuwa ni tatizo kubwa.
Huku wakiwa wametulia katika viti, mwanaume mmoja akafika mahali hapo,
akawatupia macho, hakuonyesha tabasamu lolote lile, macho yake yalionyesha ni
jinsi gani mtu huyo alikuwa siriazi.
“Unaitwa Benjamin Saunders, si ndiyo?” aliuliza mwanaume huyo.
Kabla ya kujibu swali hilo, Benjamin akashtuka, hakujua mtu huyo alikuwa nani
sasa ilikuwaje alijue jina lake? Akajiuliza, labda alikwishawahi kuonana na
mwanaume huyo sehemu fulani, hakupata jibu, alivuta kumbukumbu zake,
zikamwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa mgeni machoni mwake.
“Ndiyo!” alijibu baada ya ukimya wa sekunde kadhaa.
“Ulikuwa unawasiliana na nani kwenye simu?” aliuliza mwanaume huyo.
“Mimi?”
“Najua unajua nazungumza na nani!”
“Hata mimi sifahamu!”
“Hufahamu nini?”
“Niliyekuwa nazungumza naye, simfahamu!”
“Kwani hiyo simu ni ya nani?”

10
“Hata hilo pia sifahamu! Nilisikia simu ikiita kwenye koti langu, nikaichukua na
nilipotaka kuzungumza kuna watu wakaja kunichukua, ni watu wako bila shaka,”
alijibu Benjamin.
Alichokifanya jamaa yule ni kuichukua simu hiyo na kuondoka nayo huku
akiwaambia kwamba kunapokuwa na mkutano wa rais, hakutakiwi mtu yeyote
yule kupokea simu hasa kwa namba ambayo haipo kwenye simu yake.
Benjamin akashindwa kufahamu ni kwa sababu gani lakini jibu ambalo alikuwa
nalo, inawezekana kwa sababu ya masuala ya usalama ndiyo maana waliamua
kumchukua na kuondoka naye.
Huko kwenye mkutano, hakuwa na raha hata kidogo, alibaki akikodoa macho yake
huku nakule, hata rais alipokuja na kuanza kuhutubia taifa, hakuwa makini
kumsikiliza, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule.
Baada ya rais kumaliza na kuondoka, yeye mwenyewe akamchukua Vivian na
kuondoka naye mahali hapo huku akionekana kuwa na mawazo lukuki.
Alipokwenda mpaka sehemu alipoliegesha gari lake, akalifungua mlango na
kuingia ndani.
“Hii bahasha ya nani?” aliuliza Vivian mara baada ya kuingia ndani ya gari na
kukuta bahasha kwenye dashibodi.
“Bahasha ipi?”
“Hii hapa!”
Benjamin akaichukua ile bahasha na kuifungua ili kujua humo ndani kulikuwa na
nini. Alipoifungua, alikikuta kikaratasi kidogo kikiwa kimeandikwa ‘Crowne Plaza
1930’ huku kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan na Euro.
“Hii ni nini?” aliuliza Vivian huku akionekana kushangaa.
“Ni ujumbe...”
“Ujumbe gani?”
“Huyu mtu anataka kuonana na mimi!”
“Nani? Kuonana naye wapi?”
“Sijajua ni nani! Ila anataka nionane naye Crowne Plaza saa moja na nusu usiku,”
alijibu Benjamin.

11
“Na vipi kuhusu hizo noti?”
“Sifahamu chochote kile. Huyu ni nani? Anataka nini kutoka kwangu?” aliuliza
Benjamin pasipo kupata kitu chochote kile.
“Tukatoe taarifa polisi,” alishauri Vivian.
“Unahisi itasaidia?”
“Ndiyo!”
Hilo ndilo walilokubaliana kwamba ilikuwa ni lazima wakatoe taarifa polisi.
Hakukuwa na cha kujiuliza tena, walichoshauriana ndicho walichokifanya.
Benjamin akawasha gari na kuondoka mahali hapo, breki ya kwanza kabisa
ilikuwa katika kituo cha polisi hapo New York na kuwaambia kile kilichokuwa
kimetokea.
Walichomwambia polisi hao ni kwenda huko kwenye miadi kama alivyoambiwa
na wao wangekuwa nyuma wakifuatilia ili atakapokutana na huyo mtu wamkamate
kwani hali ilionyesha dhahiri kuwa mtu huyo hakuwa mzuri hata kidogo.
“Wewe nenda kama alivyokwambia, ukifika hapo, subiri, akija, tutamkamata,
umesikia?” aliuliza polisi.
“Sawa!”
Alitakiwa kufanya kama alivyoambiwa, hivyo ilivyofika saa moja kamili usiku
akaanza kuondoka alipokuwa akiishi kwenda kwenye hoteli kubwa ya Crowne
Plaza ambapo kulikuwa na baa pia.
Polisi walikuwa pamoja naye, hawakuwa kwenye gari moja ila walianza kufuatilia
tangu mchakato ulipoanza huku wengine wakiwa tayari wamekwishafika ndani ya
baa iliyokuwa katika hoteli hiyo. Alipoegesha gari lake, akateremka na kuanza
kuelekea ndani ya baa hiyo.
Macho yake hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule kama mtu aliyekuwa
akimtafuta mtu fulani. Kila aliyekuwa humo alikuwa bize, wengine walikuwa
wakinywa na marafiki zao, wapenzi wao na hakukuwa hata na mtu mmoja
aliyeonekana kumjali.
Akaifuata meza moja na kutulia, hakuonekana kujiamini, bado alikuwa akiiangalia
huku na kule. Muda ulizidi kukatika, saa moja na nusu ikaingia, hakukuwa na mtu

12
aliyetokea, saa mbili ikaingia lakini bado hakukuwa na mtu yeyote kitu
kilichoonekana kumshangaza.
“Yupo wapi?” alijiuliza huku akiangalia saa yake.
Mpaka inafika saa tatu na nusu usiku, hakukuwa na mtu aliyemsogelea, hakutaka
kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akiwa na mawazo tele.
Polisi ambao aliongozana nao na wale waliokuwa ndani ya baa ile walipoona
hakuna kitu chochote kilichoendelea, nao wakaondoka na kuhisi kwamba
inawezekana mtu huyo aliwaona na ndiyo maana hakutaka kabisa kujitokeza.
“Imekuwaje huko?” aliuliza Vivian.
“Hakutokea mtu yeyote!”
“Kweli?”
“Nd...” alijibu Benjamin lakini hata kabla hajamaliza kutoa jibu lake, hapohapo
simu yake ikaanza kuita, harakaharaka akaipokea.
“Halo!”
“Kwa nini umekuja na polisi?”
“Wewe nani?”
“Hujajibu swali langu! Kwa nini ulikuja na polisi?” ilisikika sauti hiyo ikiuliza
Sali.
“Wapi?”
“Nilipokwambia uje!”
“Sikuja na polisi!”
“Acha kunidanganya. Sasa sikiliza. Nataka tukutane kesho saa mbili asubuhi
kwenye mgahawa wa KFC jirani yako, kama utashindwa, nitakutumia mkanda wa
msichana wako Vivian akiwa anauawa. Umesikia?” alisema mtu huyo na kuuliza.
“Ila wewe ni nani?”
“Mimi ni Dola, Paundi, Yen na Euro.”
“Unamaanisha nini?”

13
“Fanya unachotakiwa kufanya. Kama unampenda mpenzi wako, njoo, tena ukiwa
peke yako, vinginevyo, tutamuua,” alisikika mwanaume huyo.
Simu ikakatika. Mazungumzo yale, hata msichana Vivian alikuwa akiyasikia, wote
wakaogopa, hawakujua mtu huyo aliikuwa nani na alihitaji nini kutoka kwa
Benjamin.
Wote wawili wakakosa amani, hofu zikawajia mioyoni mwao, hawakujua ni kitu
gani walitakiwa kufanya, kutoa taarifa polisi lilionekana kuwa tatizo jingine
kabisa, alitakiwa kufanya kila kitu alichoambiwa pasipo kuwashirikisha polisi
kwani vinginevyo mpenzi wake Vivian angeuawa kama alivyoambiwa.
Usiku mzima Benjamin hakuwa na furaha, moyo wake ulikuwa na hofu tele, simu
aliyoipokea ilimtisha, alitamani kwenda kutoa taarifa polisi lakini maneno
aliyoambiwa na vitisho hasa dhidi ya mpenzi wake, vilimfanya kukosa amani
kabisa.
Alibaki akizungumza naye, jambo lililokuwa mbele yao liliwatisha wote wawili.
Hawakujua hao watu walihitaji nini kutoka kwake, alitoka katika familia ya
kitajiri, alifikiri labda watu hao walihitaji fedha kutoka kwake, ila kila alipofikiria
hilo, hakupata jibu.
Kama kweli wangekuwa wanahitaji fedha, basi wangemteka mpenzi wake na kisha
kumwambia kwamba awapelekee fedha lakini kwa kile walichokifanya cha kutaka
kuonana naye, hakikumpa uhakika kama watu hao walihitaji fedha kutoka kwake.
“Watakuwa wanahitaji nini?” aliuliza Vivian.
“Sijui! Haina jinsi ngoja niende...” alijibu Benjamin.
“Lakini wanaweza kukuua!”
“Unafikiri nitafanyaje? Naweza nikagoma kwenda halafu wakaja kukuua. Vivian
mpenzi, sipo tayari kuona ukifa, acha niende nitasikia wananiiambia nini,” alisema
Benjamin.
Hakuwa na jinsi, alitamani kumuona mpenzi wake akiwa mzima kila siku,
alitamani kumuona akiwa na afya tele katika maisha yake yote hivyo kwenda huko
katika mgahawa wa KFC wala halikuwa tatizo.
Asubuhi ilipofika, akajiandaa na kisha kwenda katika mgahawa huo huku tayari
ikiwa ni saa mbili asubuhi. Alipofika, akasimama na kuanza kuangalia huko na
huku, alionekana kuwa na hofu tele moyoni mwake, na hata mhudumu aliyekuja

14
kuzungumza naye kuhusu kifungua kinywa, aliweza kugundua hofu aliyokuwa
nayo.
“What can I help you?” (Nikusaidie nini?) aliuliza mhudumu huo.
“A cup of coffee, please,” (Kikombe cha kahawa, tafadhali)
Macho yake yaliendelea kuangalia huku na kule, alihisi kwamba angeweza
kumuona mtu yeyote ambaye angekuwa akimwangalia ili agundue kwamba mtu
huyo ndiye alikuwa akitaka kuzungumza naye, aliangalia kila kona, kila mmoja
alikuwa bize na mambo yake.
Baada ya dakika kadhaa, Benjamin akaletewa kikombe cha kahawa na kuanza
kunywa. Aliangalia saa yake, muda alioambiwa akutane na huyo mtu ndani ya
mgahawa huo ulipita lakini cha kushangaza, hakuweza kuja mtu yeyote pale
alipokuwa.
Huku akiwa anaelekea kumaliza kikombe kile, ghafla akaanza kuhisi maumivu ya
tumbo, hali hiyo ilimshangaza kwani alikumbuka kwamba hakuwa akiumwa
ugonjwa huo, akashindwa kuvumilia, moja kwa moja akasimama na kuelekea
chooni.
“Benjamin...” alisikia mtu akimuita wakati yupo ndani ya choo kile.
Aligeuka na kumwangalia mtu huyo aliyemuita, hakuwa ametoka nje, alimkuta
mtu huyo humohumo ndani akiwa anaosha mikono yake katika sinki la maji.
Benjamini alibaki akimwangalia, alimuita jina lake, aliimfahamu vipi?
Alimwangalia kuhisi kwamba inawezekana aliwahi kumuona kabla, sura yake
ilikuwa ngeni.
“Wewe ni nani?” aliuliza Benjamin.
“Tumbo linakuuma, kunywa hii dawa,” alisema mwanaume huyo.
“Wewe ni nani?”
“Kwani simu ilikwambiaje?”
“Kumbe ndiyo wewe...unataka nini kwangu jamani?” aliuliza Benjamin huku
akimwangalia mwanaume huyo.
“Sikiliza Benjamin, tumbo linakuuma, kunywa hii dawa nikupe maelekezo
mengine,” alisema mwanaume yule.

15
Benjamin hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kuchukua hiyo dawa na kuinywa. Hata
dakika mbili nyingi, tumbo likatulia kabisa. Akakiangalia kikopo cha dawa ile,
kikopo kile alikifahamu, kiliandikwa Merthamponic, hiyo ilikuwa ni dawa ya
minyoo, aliifahamu lakini ile aliyokunywa, haikuwa dawa hiyo.
“Nisikilize kwanza...” alisema mwanaume huyo.
“Sawa!”
“Najua una akili sana, mimi na wewe, tutakuwa tunawasiliana kwa alama tu,”
alisema mwanaume huyo.
“Unamaanisha nini?”
“Kwa sababu una akili!”
Benjamini alibaki akimwangalia mwanaume huyo, sura yake ilionyesha kama
alikuwa mchangamfu fulani lakini kwa mbali ilionyesha kwamba mwanaume huyo
hakuwa na masihara hata mara moja.
“Unataka nifanye nini?”
“Uue..”
“Niue?
“Ndiyo! Kuna mtu anatakiwa kuuawa haraka sana,” alisema mwanaume huyo.
“Nani?”
“Carter Jackson...” alijibu mwanaume huyo.
“Sijakuelewa...”
“Sikiliza. Nenda nje ya mgahawa huu, utakutana na mwanaume anaendesha
baiskeli, mfuate huyo, atakwenda mbele kisha ataipaki baiskeli yake katika
mgahawa unaoitwa Bavarian, ingia humo, agizia kikombe kimoja cha kahawa.
Mhudumu atakayekuletea, mwambia kwamba unataka simu ya mawasiliano,
atakupa, ichukue, toka nje, utaikuta ile baiskeli, ichukue, nenda nayo mpaka
kwenye uwanja wa NFL wa Timu ya Buffaroes, ingia humo, nenda mpaka kwenye
kiti namba 20 floo ya juu, kaa hapo na usiondoke,” alisema mwanaume huyo.
“Laki...”
“Fanya hivyo,” alisema mwanaume huyo na kutoka chooni mule.

16
Benjamin alibaki ndani ya choo kile, alikuwa na mawazo mengi, maneno
aliyoambiwa na mwanaume yule kwamba alitakiwa kumuua Carter
yalimchanganya kichwa chake.
Alimfahamu Carter, alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliokuwa wakichipukia
kipindi hicho, alikuwa na mashabiki wengi, alipendwa kila kona na watu
waliokuwa wakizipenda kazi zake alikuwa mpenzi wake, Vivian.
Kumuua Carter ilikuwa kazi kubwa sana, hakuwahi kuua na wala hakufikiria kama
kuna siku angekuja kuua, mbaya zaidi mtu aliyeambiwa amuue katika kipindi
hicho alikuwa mwanamuziki aliyependwa sana.
Mbele yake ilionekana kuwa kazi kubwa, alikataa katakata kufanya hivyo lakini
kila alipokumbuka kwamba kulikuwa na mpenzi na angeweza kuuawa, hakuwa na
jinsi ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.
Alichokifanya ni kutoka ndani ya choo kile, hakurudi katika kiti chake, akaondoka
na kuelekea nje, kama alivyoambiwa, kweli akamuona mtu mmoja akipita huku
akiikokota baiskeli yake, akaanza kumfuata kwa mwendo wa taratibu.
Mwanaume huyo aliyekuwa na baiskeli hakuonekana kuwa na habari yoyote ile
kama nyuma alikuwa akifuatiliwa, aliendelea kumfuata mpaka katika mgahawa
uleule wa Bavaria ambapo aliipaki baiskeli yake na kuingia ndani, alichokifanya
Benjamin, na yeye akaingia ndani na kutulia kwenye meza moja.
“Nikusaidie nini?”
“Nahitaji kikombe kimoja cha kahawa,” alijibu Benjamin, msichana huyo
akaondoka, aliporudi, alikuwa na kikombe cha kahawa.
“Unahitaji nini kingine?”
“Simu ya mawasiliano,” alijibu, hapohapo msichana huyo akatoa simu mfukoni na
kumgawia simu hiyo, Benjamini hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kutoka nje,
akachukua baiskeli ile na kuanza kuondoka kuelekea katika uwanja wa Timu ya
Buffroes ambao aliambiwa kabla.
Alipofika huko, nje hakukuwa na watu wengi, kulikuwa na walinzi ambao
walikuwa wakiwazuia waandishi wa habari na watu wengine kuingia ndani kuiona
timu hiyo ikifanya mazoezi, kitu cha ajabu, alipokwenda yeye, hakuzuiliwa na mtu
yeyote yule hali iliyoonyesha kwamba watu hao walijua kama angefika mahali
hapo.

17
Akaingia ndani, akaelekea mpaka katika floo aliyoambiwa na kutafuta kiti namba
ishirini, alipokiona, akatulia huku akisubiri ninii kingefuata. Wakati akiwa hapo
kusubiri, simu yake ikaanza kuita, alipopokea, akaambiwa aangalie chini ya kitu,
kuna fedha, achukue na aende akanunue baga katika mgahawa wa hoteli hiyo,
hakubisha.
Alipoangalia chini ya kiti kile, akaona noti ya dola mia moja, akaichukua na
kwenda kununua baga, alipofika huko, akapewa na kwenda sehemu kula, ghafla,
macho yake yakaanza kuona giza, alijitahidi kuyafumbua zaidi lakini
yakashindikana, kama mzigo, akajikuta akianguka chini, kilichoendelea baada ya
hapo, hakukijua.
Mara baada ya saa mbili, Benjamin akayafumbua macho yake, akajikuta akiwa
katika chumba kidogo kilichokuwa na mwanga hafifu, hakujua ilikuwa sehemu
gani, aliangalia huku na kule lakini hakuwa akiona vizuri.
Kumbumbuku zake zikaanza kurudi nyuma tangu pale alipokula baga na mwisho
wa siku kujikuta akipoteza fahamu. Hakujua ni kitu gani kilitokea, hakujua kama
ile baga aliyokuwa amekula ndiyo iliyomfanya kupoteza fahamu au la.
Akasimama kutoka katika kitanda alichokuwa amelazwa na kuanza
kuzungukazunguka ndani ya chumba hicho, alitaka kuondoka lakini hakujua ni
wapi alitakiwa kuanzia, kulikuwa na mlango mmoja ila alipoushika na kujaribu
kuufungua, haukuweza kufunguka.
“Where Am I?” (Nipo wapi?) alijiuliza huku akiendelea kujaribu kuufungua
mlango ule.
“Someone help...someone help...” (Nisaidie, nisaidie...) alibaki akipiga kelele tu.
Baada ya dakika kadhaa, akasikia vishindo vya watu vikielekea kule alipokuwa,
alichokifanya ni kuupigapiga mlango ili watu hao wasikie na hivyo kumfungulia.
Watu hao hawakuwa wakielekea sehemu yoyote ile, walikuwa wakienda katika
chumba kilekile, wakaufungua mlango.
“Let me go....let me go, pleaseee....” (acheni niondoke...acheni niondoke, tafadhali)
alisema Benjamin huku akiwaangalia watu wale wa miraba minne ambao waliingia
ndani ya chumba kile.
“Benjamin, just wait, there is someone wanna talk to you,” (Subiri Benjamin, kuna
mtu anataka kuzungumza nawe) alisema mwanaume mmoja.

18
“Who is that?” (Nani huyo?)
“Dollar, Euro, Pound and Yuen,” (Dola, Euro, Paundi na Yeni) alijibu mwanaume
huyo.
“Who is that man?” (Ndiye nani huyo?)
“Wait, he is coming but let’s go somewhere,” (Subiri, anakuja. Ila twende sehemu
nzuri,” alisema mwanaume huyo.
Wakamchukua na kuondoka naye ndani ya chumba hicho. Benjamin alibaki
akishangaa tu, alikuwa akiangalia huku na kule ndani ya nyumba hiyo, ilikuwa
kubwa na ilionekana kuwa ya kifahari sana.
Safari yao fupi ikaishia ndani ya chumba kimoja kikubwa, kulikuwa na meza ndefu
mbele yake ambayo ilizungukwa na viti kumi na mbili, akaambiwa atulie hapo,
kuna mtu angekuja na kuzungumza naye.
Watu hao wakaondoka na kumwacha peke yake mahali pale. Benjamin hakuwa na
amani, alikuwa na wasiwasi tele, hakujua sababu iliyomfanya kuletwa mahali pale
lakini pia alishangazwa na jina la mtu huyo aliyekuwa akimuihitaji. Ndani ya
chumba kile kulikuwa na kamera ndogo tatu za CCTV ambazo zilifungwa katika
kona tatu za chumba hizo ambazo zilihakikisha kunakuwa na usalama ndani ya
chumba hicho.
Katika maisha yake hakuwahi kusikia mtu akiitwa majina ya fedha, kwake ilikuwa
ni ajabu kubwa mno. Alibaki akijiuliza mtu huyo alikuwa nani, hakupata jibu.
Baada ya dakika kadhaa, mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuingia.
“Karibu sana Benjamin,” alisema mwanaume huyo huku akionekana kuwa na
furaha mno.
Alimwangalia mwanaume huyo, hakuwa akimfahamu kabisa na hakukumbuka
kama aliwahi kumuona mahali fulani. Kichwa cha Benjamin kilikuwa na maswali
mengi, akaona huo ndiyo muda wa yeye kumuuliza maswali hayo mwanaume
huyo.
“Kwa nini nipo hapa?” aliuliza.
“Kwa sababu kuna kazi kubwa ya kufanya...” alijibu mwanaume huyo, sura yake
ilikuwa kwenye tabasamu pana.
“Kazi gani?”

19
“Usiwe na haraka, subiri...” alijibu mwanaume huyo, hapohapo akaondoka na
kumwambia kwamba angerudi muda mchache ujao hivyo alitakiwa kusubiri hapo.
Benjamin akabaki akijiuliza juu ya kazi hiyo ambayo alitakiwa kufanya. Hakujua
ilikuwa kazi gani na kwa nini alichaguliwa kuifanya kazi hiyo. Wakati akijiuliza
maswali hayo, mlango huo ukafunguliwa na mwanaume huyo kurudi tena,
akakifuata kiti na kutulia, wakati huu alikuwa na karatasi mkononi mwake.
Watu walikusanyika ndani ya uwanja mkubwa wa mchezo wa NFL wa Metroposa
ambao ulikuwa ukimilikiwa na Timu ya New York Ville ambayo ilikuwa ikishiriki
mchezo huo.

20
SURA YA PILI

WATU hao walijazana kuliko siku nyingine ambapo mechi kubwa ya mchezo
huo zilipokuwa zikichezwa. Siku hiyo watu hawakukusanyika kwa wingi kwa ajili
ya kuiona timu hiyo ikicheza, walikusanyika kwa ajili ya kumuona mwanamuziki
aliyekuwa akichipukia kipindi hicho, mwenye jina dogo na uwezo mkubwa,
aliyekuwa akiimba nyimbo za Pop, Carter Phillip.
Wanawake ndiyo walikuwa kwa wingi mahali hapo, wengi walimpenda Carter, si
kwa sababu ya nyimbo zake kali ikiwemo Come and Get Me Shawty bali hata
muonekano wake ulikuwa mzuri mno, alikuwa na sura iliyovutia, mwili
uliojengeka vizuri kimazoezi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na nane tu.
“I am free tonight, come to me, Carter,” (Nipo huru usiku wa leo, njoo kwani,
Carter) lilikuwa bango moja lililoshikwa na msichana mrembo uwanjani hapo.
Mbali na bango hilo, kulikuwa na mabango mengine mengi yaliyoshikwa na
wanawake ambayo yalionyesha hisia nzito walizokuwa nazo juu ya mwanamuziki
huyo mwenye sauti nzuri na ujuzi wa kucheza.
Muda huo, watu walikuwa wakishangilia sana, hakukuwa na mtu aliyetulia, kelele
zilikuwa kila kona. Carter hakuwa amefika jukwaani hapo lakini kila mtu alikuwa
na hamu ya kumuona mwanamuziki huyo akitumbuiza jukwaani.
Baada ya dakika kadhaa, Carter akafika jukwaani hapo kwa mbwembwe, uwanja
ukalipuka, wale waliokuwa mbali, wakaanza kuwasukuma wa mbele yao ili nao
waweze kuona vizuri, hakukuwa na mtu aliyetaka kumwangalia Carter kupitia
kwenye televisheni kubwa iliyokuwa uwanjani hapo, kila mtu alitaka kumuona
‘live’
“Come and Get Me Shawty,” Carter alisema kwa sauti kubwa jina la wimbo wake
uliokuwa ukivuma kiipindi hicho.
Hiyo ilikuwa ni kama kuwachengua mashabiki zake, kelele zikazidi kusikika
mahali hapo, watu wakachanganyikiwa mno, wanawake wakawa kama
wamepagawa, wengine wakakosa hewa ya kutosha kutokana na wingi wa watu
hivyo kuzimia.

21
Uwanjani ilikuwa purukushani, wengine wakapanda jukwaani na kutaka kugusa tu
Carter kwani walichanganyikiwa mno. Mabaunsa ambao ndiyo walionekana kuwa
walinzi mahali hapo wakawawahi watu hao na kuwazuia, hiyo haikutosha,
wakawashusha kutoka jukwaani.
“I wanna introduce my new hit, this is How Am I Suppose To Say,” (Ninataka
kutambulisha ngoma yangu mpya, hii ni Nisemeje) alisema Carter maneno
yaliyowafanya watu uwanjani hapo kushangilia kwa sauti kubwa.
****
Jina la Carter halikuwa nchini Marekani tu, kila kona katika dunia hii, watu
walimfahamu huku wengi wao wakimuita kama The ‘New Michael Jackson’
wakiwa na maana ya Michael Jackson Mpya.
Watu walimtabiria makubwa, katika wimbo wake wa kwanza alioutoa, ulikimbiza
vilivyo na kumfanya kuwa tajiri mkubwa. Watu wengi walimpenda, makampuni
mbalimbali yakajitolea kumfanya biashara kwani watu wengi waliokuwa
wakimfuata, walipenda kufanya kile alichokuwa akikifanya.
Kama leo alinyoa hivi, mitaani hiyo ilionekana kuwa fasheni mpya hivyo nao
waliiga, leo alivyovaa hivi, kesho asubuhi nao watu wakaiga. Alikuwa nembo kila
sehemu aliyokuwa akipita, barabarani, hakuwa na raha, kila alipotembea watu
walimfuata kwa wingi na kutaka wasainiwe vitabu vyao, kwa kifupi, maisha ya
Carter yalikuwa yenye usumbufu mkubwa.
Siku zikaendelea kukatika, akaunti yake ikasoma kiasi kikubwa, zaidi ya dola
milioni mia mbili kwa kipindi kifupi mno. Fedha hizo, kwa umri wake, jina lake
zilikuwa nyingi mno ambazo kwa fedha za Kitanzania zilikuwa ni zaidi ya bilioni
mia nne.
Maisha yake yakabadilika, hakutaka kuishia hapo, hakutaka kuridhika,
alichokifanya ni kuendelea kufanya mambo makubwa, akazidi kutoa nyimbo kali,
zilizomfanya kushika nafasi za juu kabisa katika chati ya Billboard kitu
kilichomfanya kuwa tajiri zaidi.
“We have the deal on the table,” (Tuna dili mezani) alisema meneja wake.
“What deal?” (Dili gani?)

22
Meneja huyo akamwambia kwamba kulikuwa na kampuni ya simu za mkononi,
Samsung walitaka kuweka naye mkataba wa kuvuna mamilioni ya fedha kwa
kuitangaza kampuni hiyo.
Kiasi kilichotolewa kilikuwa ni dola bilioni moja, zilikuwa fedha nyingi
mnoambazo zingemfanya kuogelea katika dimbwi la fedha. Pamoja na kupata kiasi
kikubwa cha fedha lakini hakubweteka hali iliyomfanya kila siku kujikusanyia
kiasi kikubwa cha fedha.
Baada ya kuingia dili hiyo, akaambiwa aelekee nchini China, huko na safari
nyingine ilikuwa ni kuitangaza kampuni kubwa ya Samsung na vifaa vyake kitu
kilichowafanya watu wengi kununua vitu kutoka katika kampuni hiyo kubwa
duniani.
“Nina wasiwasi mpenzi...” alisikika msichana mmoja akizungumza kwenye simu.
“Wasiwasi wa nini?”
“Umekuwa na jina kubwa sana, unahisi nitastahili kuwa pamoja nawe?” aliuliza
msichana huyo.
“Kwa nini usistahili?”
“Naona nitaibiwa, naona nitaumizwa hapo baadaye,” alisema msichana huyo.
“Wala usijali, hakuna atakayekuibia, najielewa sana...”
“Ila wanawake wengi wanakupenda.”
“Si tatizo Mariana, unatakiwa kuniamini tu.”
“Kweli?”
“Hakika!”
Japokuwa alikuwa akipendwa na wanawake wengi lakini Carter hakuwa
akiwatamani kimapenzi wanawake hao, katika maisha yake, msichana ambaye
alikuwa naye beneti alikuwa mmoja tu, huyu aliitwa Mariana.
Alikuwa msichana mzuri, mwenye macho madogo yenye ubluu, umbo zuri,
nyonga zake zilijengeka vilivyo hali iliyofanya hipsi zake kuonekana sawasawa,
alikuwa mrefu kidogo huku akiwa na nywele nyingi zilizomfanya kupendeza mno.
Lipsi za mdomo wake zilikuwa nene, alikuwa na pua ndefu kidogo, kwa jinsi
alivyokuwa, kulikuwa na wanaume wengi waliomtaka lakini kwake, mtu pekee

23
aliyempenda alikuwa mmoja tu, naye ni mwanamuziki chipukizi mwenye jina
kubwa, Carter.
Uhusiano wao wa kimapenzi ulianza zamani, wakati walipokuwa wakisoma shule
ya msingi. Walipendana mno, walikuwa pamoja na hata wazazi wao walilifahamu
hilo.
Alijua kwamba katika kipindi alichopata jina, wasichana wengi wangempenda,
wengi wangetamani kuwa naye lakini siku zote katika maisha yake, alimthamini
msichana huyo tu, hakukuwa na mwingine katika maisha yake, kumpenda
msichana huyo ilikuwa moja ya vitu vya thamani katika maisha yake, kwani
hakumpenda kwa kuwa alikuwa na jina, alimpenda tangu kipindi cha nyuma.
“Nilipokuwa na jina, ulinipenda, sasa kuna haja gani ya kukuacha katika kipindi
hiki, sidhani kama ni sahihi,” alisema Carter.
Maisha yalikuwa ya raha kila siku, aliendelea kupata mashabiki wengi duniani
huku nyimbo zake zikiendelea kushika chati ya juu duniani kote. Vijana ambao
walikuwa mitaani, nao wakaanza kujaribu kuimba, kutokana na Carter kuwa
muimbaji, vijana wengi waliamini kwamba wangeweza kuwa kama yeye kitu
kilichowafanya kila siku kukaa ndani na kujifunza kuimba.
“Kuna dili jingine,” alisema meneja wake mara baada ya kumaliza ziara ya
Samsung huko Asia.
“Dili gani?”
“Kampuni ya Smadav Telecom inataka kufanya mazungumzo na wewe,” alisema
meneja wake.
“Kuhusu nini?”
“Bila shaka mkataba utakaotufanya tuchume fedha nyingi zaidi,” alijibu meneja
wake.
“Hakuna tatizo!”
Kampuni ya Smadav Telecom ilikuwa miongoni mwa kampuni kubwa nchini
Marekani ambayo ilijihusisha na mitandao ya simu za mikononi. Ilikuwa miongoni
mwa kampuni zilizokuwa na wateja wengi.

24
Mbali na Nike, Apple ambazo zilikuwa zikiingiza mamilioni ya fedha, nayo
Smadav ilikuwa juu kabisa huku ikimilikiwa na mtu aliyekuwa akishika nafasi ya
ishirini kwa utajiri duniani, Bwana David Seppy.
Utajiri wa mzee huyo mwenye miaka hamsini ulitisha, kila siku alikuwa akiingiza
kiasi kikubwa cha fedha hali iliyomuongezea utajiri mkubwa kila siku. Alifahamu
kwamba wasanii ndiyo watu waliokuwa na ushawishi mkubwa katika dunia ya
sasa na hivyo kuwatumia katika kuzitangaza kampuni zake.
Masupastaa wakubwa duniani kama Kobe Bryant, James LeBron, Tiger Woods na
wengine wengi walikuwa miongoni mwa masupastaa ambao walitumika katika
kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha.
Mbali na Smadav, mzee huyo alikuwa akimiliki kampuni nyingine nyingi,
majengo makubwa ya kupanga, migodi, vituo vya mafuta na miradi mingine
mingi. Jina lake lilikuwa kubwa kwa kuwa alikuwa miongoni mwa matajiri
wakubwa ambao walijulikana kutoka na ukaribu wake na wasanii hao.
Baada ya kuingia mikataba na watu wengi, aliyekuwa mbele yake alikuwa ni
Carter, aliamini kwamba kama angemtumia kijana huyo katika kampuni zake
zingewafanya watu wengi kununua bidhaa zake kitu ambacho kingempa kiasi
kikubwa cha wateja, hivyo akaanza kumtafuta kwa kuwatuma wafanyakazi wake.
“Amesemaje?” aliuliza.
“Nimezungumza na meneja wake kwamba tuonane, baada ya hapo tutazungumza
naye,” alijibu mfanyakazi aliyetumwa.
“Sawa. Naomba ukakutane naye halafu utaniambia kipi kitakachojiri,” alisema
Bwana Seppy huku akikenua kwa kuona kwamba mbele yake kulikuwa na
mafanikio makubwa kwa kumtumia mwanamuziki huyo ambaye kadiri siku
zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo alivyozidi kujulikana duniani kote.
Watu wanne walikuwa mezani, walikuwa wakizungumzia mambo ya kibiashara,
kiu kubwa iliyokuwa moyoni mwa Bwana Seppy ni kuona akifanikiwa
kumsainisha mkataba kijana huyo kuitangaza kampuni yake ili kuwavuta wateja
wengi zaidi.
Kiasi ambacho alikiweka mezani kilikuwa ni dola milioni tano. Kilikuwa kiasi
kidogo mno hasa kwa mtu kama Carter ambaye siku kadhaa zilizopita alisaini
mkataba wa dola bilioni moja.

25
Alipousoma mkataba huo, Carter akakenua, akamwangalia meneja wake kisha
kumgawia mkataba huo na kuanza kuuangalia. Kiasi cha fedha ambacho
kiliwekwa, kilikuwa kidogo mno kulinganisha na jina lake.
“Hii fedha ndiyo ya mkataba?” aliuliza meneja wake aliyejulikana kwa jina la
Smith.
“Ndiyo!” alijibu Bwana Seppy kwa kujiamini.
“Huu ni upuuzi...”
“Upuuzi?”
“Ndiyo! Kiasi gani hiki? Unamchukuliaje Carter? Unadhani nyuma yake kuna
watu wangapi? Ana mashabiki zaidi ya bilioni moja duniani kote, halafu leo
umeweka kiasi cha dola milioni tano! Hebu kuweni siriazi kidogo,” alisema Smith
huku akionekana kuchukizwa na mkataba huo.
“Ila yeye ni msanii mchanga!”
“Mchanga! Yaani mpaka leo unamuita Carter msanii mchanga! Acheni zenu.”
Hakukuwa na maelewano, kiasi cha malipo ya mkataba ambacho kiliwekwa
kilikuwa kidogo mno kulinganishwa na jina lake. Bwana Seppy alionekana
kukasirika, kwake, japokuwa Carter alikuwa na jina kubwa lakini bado alionekana
kuwa msanii mchanga.
Alichokifanya ni kuongeza mpaka kufikia dola milioni ishirini, bado Carter
alikataa, alichokiangalia yeye ni idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa nyuma
yake, hakukubali kuona akinyonywa, hivyo aliwaambia wazi kwamba asingesaidi
mkataba mpaka iwekwe dola milioni mia tano mezani.
“Unasemaje?”
“Ufanyieni marekebisho mkataba wenu, milioni mia tano mezani, nitasaini, chini
ya hapo, mtanisamehe,” alisema Carter kwa kujiamini kabisa.
Kutoka dola milioni ishirini mpaka mia tano ilionekana kuwa kiasi kikubwa mno,
ni kweli alikuwa na fedha nyingi lakini Bwana Seppy hakutaka kutoa kiasi hicho
cha fedha.
Walibaki wakibishana na mwisho wa siku, msimamo wa Carter ukabaki palepale
kwamba mkataba hausainiwi na hivyo kuondoa zake bila kugeuka nyuma.

26
Bwana Seppy akakasirika mno, hakuamini kama kweli msanii huyo, tena mdogo
kiumri alikataa kusaini mkataba huo uliokuwa na fedha alizoziona kuwa nyingi.
Akaondoka huku akiwa na hasira tele, nyumbani kwake hakukukarika, alipokuwa
akimuona Carter katika magazeti na televisheni, alishikwa na hasira mno,
hakumpenda hata kidogo. Aliamini kwamba kupitia msanii huyo angeweza
kujikuanyia wateja wengi lakini mwisho wa siku mtu huyo alikataa.
Kipindi hicho ndipo akagundua kwamba pombe hazikuwa tamu, zilikuwa chungu,
mawazo yalimjaa na kila alipokaa, alikuwa akipiga mikono yake kwa hasira hasira.
Roho mbaya ikaanza kumuingia na kuona kwamba mtu huyo alitakiwa kuuawa,
kama yeye alikuwa kiburi, sasa yeye alikuwa jeuri na alitaka kumuonyeshea
kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile kutokana na uwezo
mkubwa aliokuwa nao, hapo ndipo alipoanza kusuka mipango.
“Kwa hiyo unataka afe?” aliuliza kijana wake mwenye sura mbaya, huyu aliitwa
Dragon na ndiye aliyekuwa akihusika kwa matukio mengi ya mzee huyo, hasa
kwenye kuwaua maadui wa mzee huyo.
“Ndiyo! Tena haraka iwezekanavyo.”
“Sawa! Nitafanya kazi hiyo!”
“Hapana! Hautakiwi kuifanya wewe...”
“Sasa aifanye nani?”
“Hii ni kazi inayotakiwa kufanywa na watu wenye akili nyingi sana, kama
ukifanya wewe, niamini kwamba utakamatwa tu kwani huyu si mtu mdogo, ni mtu
mwenye mamilioni ya watu nyuma yake, hivyo ni lazima tumtume mtu mwenye
akili nyingi,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Dragon.
“Ni nani sasa?”
“Subiri, nitakupa jibu!”
Hiyo ilikuwa kazi kubwa, alichokiangalia ni wingi wa watu waliokuwa nyuma ya
Carter, kulikuwa na watu wengi, kila alipokwenda kulikuwa na watu wengi hivyo
kumuua kwake ilitakiwa kuwa kwa ufundi sana, yaani hata watu watakapojua
kwamba amekufa, wasihisi kama aliuawa.
Alichokifanya ni kuingia katika mitandao na kuanza kumtafuta mtu mwenye akili
nyingi. Alihangaika sana, alikiamini Chuo Kikuu cha Harvard kwamba kulikuwa

27
na wanafunzi wengi wenye akili, sasa alitaka kuona ni nani aliyekuwa
akiwaongoza wanafunzi hao wenye akili, chaguo lake likatua kwa Benjamin,
mwanaume aliyeaminika kuwa na uwezo mkubwa mno kipindi hicho.
“Huyuhuyu! Ni lazima apatikane,” alisema Bwana Seppy huku akikenua,
alimhitaji mtu huyo kwa gharama zozote zile. Hivyo wakaanza kumtafuta kwa ajili
ya kufanya kazi hiyo.

****
“Tunahitaji kukulipa kiasi cha dola milioni moja kwa kutufanyia kazi moja tu,
yaani kazi moja tu,” alisema Dragon mara baada ya kumrudia Benjamin.
“Kazi gani?”
“Najua ushaijua, tunataka huyu Carter kuuawa haraka sana!” alisema Dragon.
“Carter kuuawa?”
“Ndiyo! Na tumeona hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo zaidi yako!”
alisema Dragon huku akimwangalia Benjamin usoni.
“Kwa nini mimi?”
“Kwa sababu una akili! Benjamin, kati ya vijana wote hapa Marekani, hakuna
mwenye akili zaidi yako! Tumeamua kukupa kazi hii kwa kuwa tunaamini
utaifanya kiakili na isigundulike kabisa,” alisema Dragon.
“Hapana! Siwezi kuua!”
“Benjamin! Umesahau tulichokwambia! Unataka Vivian auawe?” aliuliza Dragon.
Benjamin akabaki kimya.
Siku hiyo, Benjamin hakukubali kabisa kufanya mauaji hayo, hakutaka kuona
akitenda dhambi ya kuua, kwake, alikuwa tayari kufanya kitu chochote lakini si
kuua.
Hakuumficha Dragon, alimwambia kweli kwamba hakutaka kuua na wala
hakutegemea kufanya kitu kama hicho maishani mwake. Jibu hilo lilimkera
Dragon, akachukua simu yake na kwenda pembeni, huko, akampigia simu bosi
wake, Bwana Seppy na kumwambia kwamba Benjamin alikataa kufanya
walichomtaka kukifanya.

28
“Una uhakika amekataa?”
“Ndiyo bosi! Amekataa katakata!”
“Kamtekeni Vivian, hakuna zaidi ya hilo,” aliagiza Bwana Seppy na kisha kukata
simu.
Hayo yalikuwa maagizo ambayo yalitakiwa kufanyika haraka sana. Alichokifanya
Dragon ni kuwapigia simu vijana wengine na kuwaambia kile kilichotakiwa
kufanyika. Walimfahamu Vivian hivyo walichokifanya ni kuahidi kwamba
msichana huyo angetekwa haraka iwezekanavyo!
****
Japokuwa alibembelezwa sana lakini Benjamin hakutaka kukubaliana nao hata
kidogo, hakuwa radhi kumuua mtu yeyote yule kwa kipindi hicho. Mbali na hiyo
yote, hakutaka kuamini kama watu hao wangeweza kumteka mpenzi wake.
Dragon hakutaka kuzungumza naye sana, akamruhusu kuondoka huku akimtakia
maisha mema. Benjamin akasimama na kutoka nje ya chumba kile, alipofika nje,
akakuta gari likiwa linamsubiri na hivyo kuamriwa kuingia, alipoingia tu,
akafunikwa macho yake kwa kutumia kitambaa na kisha safari kuanza upya.
Safari hiyo ilichukua dakika arobaini, gari likasimama na kisha kuteremshwa.
Sehemu aliyoteremshiwa ilikuwa kwenye uwanja uleule ambao alikula baga na
kisha kupoteza fahamu, baada ya kushushwa, watu hao hawakutaka kusubiri,
wakaondoka zao.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Benjamin ni kuchukua simu yake na kisha
kumpigia mpenzi wake, Vivian, alitaka kusikia kama alikuwa salama lakini pia
alitaka kumwambia kuwa ni lazima kuondoka kuelekea Los Angeles kwani hapo
Washington DC walipokuwa hakukuwa salama kabisa.
Simu ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikuwa ikipokelewa. Hali hiyo ikamtia
hofu Benjamin kwa kuhisi kwamba inawezekana mpenzi wake huyo tayari
alitekwa na watu hao. Hofu ikamjaa moyoni mwake lakini huku akiwa anafikiria
mambo hayo yote, mara simu hiyo ikapokelewa.
“Upo wapi mpenzi? Unanitia wasiwasi mwenzio?” aliuliza Vivian kwenye simu.
“Kuna sehemu nipo, nimekuwa na hofu sana, upo salama hapo nyumbani?”
aliuliza Benjamin.

29
“Ndiyo!”
“Kweli?”
“Ndiyo! Kuna nini kwani?”
“Hakuna mtu aliyekuja hapo nyumbani?”
“Hakuna! Kwani kuna nini?”
“Subiri! Nakuja!”
“Unanitia wasiwasi mpenzi!”
“Usijali! Nakuja!”
Benjamin akakata simu, akashusha pumzi nzito, kidogo moyo wake ukawa katika
hali ya kawaida, kumsikia mpenzi wake akiwa mzima wa afya, kwake ilikuwa ni
furaha tele.
Alichokifanya ni kukikodi taksi na kisha kuanza kuelekea mahali alipokuwa
akiishi, kwenye apartment ambazo hazikuwa mbali sana kutoka mahali hapo
alipokuwa.
Ndani ya gari alionekana kuwa na mawazo mengi, kichwa chake
kilichanganyikiwa, maneno aliyoambiwa na mwanaume yule aliyemfuata pale
chumbani yalimchanganya sana, hakuamini kama kweli kulikuwa na watu
waliokuwa wakifanya mpango wa kumuua msanii Carter ambaye kwa kipindi
hicho, yeye ndiye alikuwa top.
Kutokana na foleni za hapa na pale, teksi ilichukua dakika ishirini ndipo ikaingia
katika eneo lililokuwa na apartment alizokuwa amepanga. Kwa harakaharaka
akateremka kutoka ndani ya teksi ile na kuanza kuelekea ndani.
Kitu ambacho kilikuwa akilini mwake kwa wakati huo ni kumwambia mpenzi
wake kwamba walitakiwa kuondoka kwani mahali hapo hakukuwa salama tena.
Baada ya kupandisha ngazi, akaufuata mlango wa chumba chake, kitu
kilichomshtua ni pale alipoukuta mlango ukiwa wazi. Kwanza akashtuka, mapigo
ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi, hakuamini alichokuwa akikiona, hapohapo
akaufuata mlango na kuingia ndani.

30
Mito ya makochi ilikuwa chini, sebule ilikuwa shaghalabaghala, akaanza kumuita
Vivian lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeitikia. Hakuishia hapo sebuleni,
akaenda chumbani, bafuni mpaka jikoni, kote huko mpenzi wake hakuwepo.
“Vivian...Vivian...” aliita kila hatua lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeitikia.
Benjamin akatoka ndani ya vyumba hivyo na kuelekea nje kabisa, alizunguka
katika eneo zima lililokuwa likizunguka apartment hiyo, tena huku akimuita
mpenzii wake lakini hakuitikiwa, msichana huyo hakuwepo kabisa.
Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kumpigia tena, simu haikuwa
ikipatikana kabisa kitu kilichomchanganya kupita kawaida. Hakuwa na jinsi,
akapiga polisi na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea.
“Where are you?” (Upo wapi?) ilisikika sauti ya polisi kutoka upande wa pili.
“West Mania Street, block number 45,” (Mtaa wa West Mania, nyumba namba 45)
alijibu Benjamin.
“We are on our way,” (Tupo njiani)
Ndani ya dakika sita tu, tayari polisi wakafika mahali hapo na kuanza kumuuliza
Benjamin juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Aliwaelezea vizuri lakini katika
maelezo yake yote hakutaka kuwataja watu waliokuwa wamemteka.
“Wewe ulikwenda wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Kununua vyakula...”
“Ulichukua muda gani kwa kwenda mpaka kurudi?”
“Nusu saa tu!”
“Na mara ya mwisho kuzungumza naye?”
“Kama dakika ishirini kabla ya kufika nyumbani!”
“Alikwambiaje?”
“Hakuna chochote, alikuwa akinisubiri tu,” alijibu.
Polisi wale walikuwa wakimuuliza huku macho yao yakiangalia huku na kule,
walichokifanya nao ni kupiga simu kituoni na kutoa taarifa kwa kifupi juu ya kile
kilichokuwa kimetokea kisha kuondoka mahali hapo.

31
Usiku haukuwa na amani tena, muda wote Benjamin alikuwa akimfikiria mpenzi
wake, alikosa furaha, kuna kipindi alikuwa akiona kama alifanya kosa kukataa
kufanya kile alichoambiwa akifanye lakini kuna kipindi aliona ni bora alivyokataa
kwani moyo wake haukuwa radhi kabisa kuua.
Alijilaza kitandani huku akiwa na mawazo tele, muda mwingi polisi walikuwa
wakimpigia simu na kuzungumza naye, walitaka kufahamu nini kilikuwa
kikiendelea.
Ilipofika saa tano usiku, simu yake ikaanza kuita, harakaharaka akaipokea na
kuanza kuongea na mtu wa upande wa pili.
“Upo tayari?” lilikuwa swali aliloulizwa mara baada ya simu kupokelewa, kwa
mbali akaanza kusikia sauti ya mpenzi wake, alikuwa akilia huku akiomba msaada.
“Mpenzi wangu yupo wapi?” aliuliza Benjamin.
“Yupo salama, hajapigwa wala kujeruhiwa. Upo tayari au tumuue?” aliuliza mtu
huyo aliyekuwa akizungumza kwenye simu.
Benjamin hakujibu kitu, alibaki kimya huku simu yake ikiwa sikioni mwake.
Alichanganyikiwa, alimpenda sana mpenzi wake lakini kwa upande wa pili,
hakuwa tayari kuua, hakutaka kudaiwa damu ya mtu mikononi mwake.
“Tunakupa dakika ishirini za kujifikiria, baada ya hapo, tutajua nini kinachofuata,”
alisema mwanaume huyo na kisha kukata simu huku akiahidi kupiga tena baada ya
dakika ishirini. Benjamin akashusha pumzi nzito.
Benjamini alibaki kimya chumbani kwake, hakuamini kwamba mwanzo wa kila
kitu ungekuwa namna ile, alibaki akiiangalia saa yake ya mkononi, muda ulikuwa
ukikimbia mno, tena zaidi ya siku nyingine.
Alitamani kuwapigia simu polisi na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea lakini
hakutaka kufanya hivyo kwani watu ambao alitaka kuwapa taarifa polisi kuhusu
wao tayari walikuwa na mpenzi wake, hivyo alitakiwa kubaki kimya huku akiwa
na muda wa kufikiria nini cha kufanya.
Hakujua sababu ya watu hao kutaka kumuua Carter, kwake, kijana huyo
alionekana kuwa mpambanaji, alipambana katika maisha yake yote ili apate
umaarufu na hatimaye atengeneze pesa, sasa iweje aje amuue mtu kama huyo na
wakati kulikuwa na watu ambao walikuwa wakila kwa mgongo wake? Moyo wake

32
ukamhukumu, hakutakiwa kufanya hivyo ila kila alipofikiria kwamba mkewe
alishikiliwa mateka, hakujua nini alitakiwa kufanya.
Baada ya kujifikiria kwa muda, kichwani mwake likaja wazo moja kwamba ni
lazima alifanye haraka iwezekanavyo na hatimaye kukimbia. Dakika ishirini
zilipofika tu, akasikia simu yake ikianza kuita, hapohapo akaipokea.
“Umefikiria nini?” aliuliza mwanaume aliyekuwa upande wa pili.
“Nitamuua kwa ajili ya mpenzi wangu! Ila nitajuaje kama mpenzi wangu atakuwa
salama baada ya kufanya kazi yenu?” aliuliza Benjamin.
“Usijali, hatuwezi kukusaliti katika hilo!”
Benjamin alijiamini, watu hao waliamua kumtafuta kwa kuwa walimuona kuwa na
akili mno hivyo naye akataka kulidhirisha hilo, alitaka kuwaonyeshea kwamba
yeye alikuwa na akili hata zaidi yao.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kumpigia simu rafiki yake, David
Belshaaz, Musraeli aliyekuwa akisoma naye, yeye alikuwa akichukua masomo ya
kompyuta, na alikuwa mtu hatari sana.
“Vipi?” aliuliza David.
“Naweza kukutana nawe sehemu fulani kuongea?” aliuliza Benjamin.
“Ngoja niangalie ratiba yangu ya kesho!”
“Si kesho, nataka tuonane sasa hivi tuzungumze,” alisema benjamin.
“Kuna nini tena?”
“Naomba tuonane David, kuna kitu.
“kipi?”
“Wewe tuonane kwanza!”
“Mbona unanitisha?”
“Usijali!”
“Kuna usalama?”
“Ndiyo! Wewe tuonane!”
“Sawa!”

33
Baada ya kukubaliana kwamba wangeonana usiku wa siku hiyo, simu ikakatwa.
Benjamin bado alikuwa na mawazo tele, hakujua kama katika kipindi hicho
mpenzi wake alikuwa salama au la.
Baada ya dakika ishirini, akapigiwa simu na David na kumwambia kwamba
alikuwa katika mgahawa wa KFC ambao haukuwa mbali kutoka katika apartment
alizokuwa amepanga Benjamin, hiivyo akatoka na kwenda kuonana naye.
“Kuna nini?”
“Yaani nimechanganyikiwa!”
“Kuna nini?”
Hapo ndipo Benjamin alipoanza kumuhadithia David kile kilichokuwa kimetokea,
wakati wote wa kusimulia alionekana kuwa na majonzi tele, kitendo cha mpenzi
wake kutekwa kilimuumiza sana moyoni mwake.
Hakutaka kuficha kitu chochote kile, alimwambia wazi David ili kama kusaidiwa,
asaidiwe kutokana na tatizo lililokuwa mbele yake. David alimsikiliza kwa makini,
suala hilo lilikuwa kubwa kwani aligundua kwamba mtandao ambao ulimteka
Vivian ulikuwa mkubwa na wenye watu wengi, hivyo walitakiwa kuwa makini.
“Itawezekana kweli kumpata Vivian?” aliuliza Benjamin.
“Kama tukiungana, tutampata tu. Ninataka unisaidie!”
David alikuwa mtaalamu wa mambo ya kompyuta, alijua kucheza nazo, alisomea
mpaka pale alipopata PhD. Hakuipenda kompyuta alipokuwa mkubwa, tangu
alipokuwa mdogo, alikuwa mtundu na hivyo kumfanya kugundua mambo mengi
katika kompyuta.
Yeye ndiye alitengeneza virusi vilivyojulikana kama Y2K ambavyo viliaminika
kuzima kompyuta zote duniani mwaka 2000, yeye ndiye aliyekuwa akiingia
kwenye system za Urusi, anaiba data na kuwapa Wamarekani. Yeye ndiye
aliyewaambia Wamarekani kwamba Iraq ilikuwa ikitengeneza mabomu ya nyuklia,
kipindi cha kwanza walikataa lakini baada ya kuwaonyeshea data alizoziiba
kwenye komyuta zao, wote wakaamini.
Alikuwa mtaalamu sana, sasa kitu ambacho Benjamin alikitaka ni kujua mahali
alipokuwa mpenzi wake na vilevile kumgundua mtu aliyekuwa akihusika katika
mpango wa kumuua Carter.

34
“Don’t worry, this is tracking issues, I will let you know, give me the damn
number,” (Usijali, haya ni mambo ya kutraki, nitakutaarifu, naomba hiyo namba)
alisema David na Benjamin kumpa namba hiyo.
Baada ya kukubaliana kwamba kazi ingefanyika, kila mmoja akaondoka huku
Benjamin akiwa na uhakika kwamba rafiki yake huyo angefanya kila liwezekanalo
kuhakikisha kwamba mpenzi wake anajulikana mahali alipokuwa na hata mtu
aliyekuwa nyuma ya mchezo mzima anajulikana.
Usiku mzima Benjamin hakulala, alikuwa na mawazo tele, bado alichanganyikiwa,
alimpenda sana mpenzi wake lakini hakuwa tayari kuona akiua, tena kumuua mtu
kama Carter.
“Nitafanya ujanja, subiri...” alijisemea Benjamin.
Ilipofika asubuhi, akapigiwa simu na kuulizwa kama alikuwa tayari, akampa
taarifa kwamba alikuwa tayari kitu kilichohitajika ni kuambiwa namna ambayo
ingefanikisha kumpata huyo Carter.
“Unakumbuka nilikwambia nini?” aliuliza mwanaume aliyekuwa akizungumza
naye kwenye simu.
“Nini?”
“Una akili sana!”
“Nimekumbuka, kwa hiyo?”
“Wewe unajua ni jinsi gani unaweza kumpata Carter, naomba ufanye hivyo,
hakikisha anapatikana na unamuua...au unataka tumuue Vivian?” aliuliza
mwanaume huyo kwa sauti ya mkwara.
“Hapana mkuu! Naomba usifanye hivyo!”
“Basi fanya kazi yako!”
Kilichokuwa kikihitajika ni kuonana, Benjamin hakutaka kutumia kiasi chake cha
fedha hivyo ilikuwa ni lazima apewe kiasi cha pesa ambacho ndicho angekitumia
katika harakati zake za kumuua Carter.
Hilo wala halikuwa tatizo hata kidogo, akaonana na mwanaume mmoja ambaye
akamgawia kiasi cha dola laki tano ambacho angekitumia katika kumuua Carter au
vinginevyo kuuawa yeye.

35
Alipozipata hizo fedha, kitu cha kwanza ni kuanza kufuatilia ratiba ya Carter
ilisemaje. Katika ufuatiliaji wake huo akagundua kwamba baada ya wiki moja
msanii huyo angekwenda Miami kwa ajili ya kupiga shoo na angefikia katika
Hoteli ya Samson And Delilah, hivyo naye akaenda huko haraka sana kwa ajili ya
kukamilisha mchakato wake, baada ya hapo, mpenzi wake angeachiwa huru.
****
Carter hakuwa mtu wa kutulia, kila siku ilikuwa ni kwenda huku na kule akifanya
shoo. Alichoka sana lakini hakutaka kuacha, ilikuwa ni lazima kufanya hivyo
kwani maisha yake ndivyo yalivyotaka kufanya hivyo. Kuna kipindi alikuwa
akionekana mgonjwa, alipoteza hamu ya kula na alipokwenda hospitali, daktari
alimwambia kwamba alichoka.
Watu walimuonea huruma Carter lakini hakukuwa na mtu aliyemwambia asubiri,
asiende sehemu kupiga shoo na wakati kila mtu alikuwa na hamu ya kumuona.
Kila siku alipokea shoo mbalimbali, tena nchini Marekani na hata nje ya nchi hiyo.
Baada ya kuzunguka kwa kipindi kirefu, akaamua kupumzika nyumbani kwake
jijini New York kabla ya kuanza tena ziara zake kama kawaida.
Katika kipindi hicho cha mapumziko ndipo alipopokea mwaliko wa kwenda
kufanya shoo katika shule yake aliyosoma kipindi cha nyuma iliyokuwa huko
Miami. Kwanza alichoka, hakutaka kwenda huko lakini kila alipotaka kuwaambia,
hakuona kama lingekuwa jambo jema.
Hakutaka kulipwa kiasi chochote kama sehemu nyingine, Shule ya St. Peter
ilikuwa ni kama yake, alipendwa sana huko na kila mwanafunzi alijisikia fahari
kusoma shule ambayo Carter alisoma hivyo kwenda huko, hata kama alikuwa
amechoka hakuwa na jinsi, ila wao walitakiwa kuingia gharama, hasa hoteli ya
kufikia.
“Nataka nifikie kwenye hoteli nzuri tu ambayo itakuwa na ulinzi hasa kwa
mashabiki zangu,” alisema Carter.
“Hakuna tatizo! Samson And Delilah itafaa?”
“Ndiyo! Hakuna tatizo!”
Baada ya siku mbili, alikuwa ndani ya ndege yake binafsi akielekea Miami. Ndani
ya ndege alikuwa na meneja wake na marafiki zake watatu, hakutaka kwenda na
mpenzi wake kwani msichana huyo hakuwa mpenzi wa safari na alijua kwamba

36
kama angekwenda huko, basi angeumia moyo wake kutokana na wanawake
kumpapatikia sana mpenzi wake.
Hawakuchukua muda mrefu angani wakawa wamekwishafika Miami ambapo
wakateremka na kisha kutoka nje ya uwanja huo. Watu wengi walikuwa
wamejazana nje, walimsubiria tangu asubuhi mpaka mchana wa siku hiyo.
Mikononi walikuwa na mabango yaliyoonyesha kumkaribisha ndani ya Miami.
Moyo wake ukafarijika sana, hakuamini kama kweli wale waliokuwa
wamejitokeza walitoka katika shule ambayo alisomea.
Wengi wakamsogelea na kuanza kupiga naye picha, si wao tu bali hata wasafiri
wengine waliokuwa na safari zao, walimfuata, wakampiga picha na kisha kujipiga
pamoja naye.
Baada ya shamrashamra za hapo kumalizika, safari ya kuelekea hotelini ikaanza.
Ulinzi wa magari ulikuwa mkubwa, wengi hawakuamini kama kweli Carter alifika
hapo Miami na alikuwa tayari kwa kufanya shoo moja kubwa jijini hapo.
Hotelini, watu wengi walikusanyika, kila mmoja alitaka kumuona Carter, wengine
waliposikia kwamba mtu huyo alikuwa katika hoteli hiyo, hawakutaka kupitwa,
nao harakaharaka wakasogea na kutaka kuingia ndani ya hoteli hiyo.
“Subiri! Tukutane kesho uwanjani...” alisema mpambe wake huku akiwaangalia.
“Hatuondoki, kama kubaki, ngoja tubaki, tunataka kumlinda Carter wetu,”
alisikika mwanaume mmoja mwenye mwili mkubwa, wengine nao wakamsapoti,
hawakutaka kuondoka, walikuwa radhi kulala hapohapo nje, kama kupigwa na
baridi, walikuwa tayari lakini si kuondoka mahali hapo.
Wakati hayo yote yakiendelea, tayari Benjamin alikuwa amekwishafika ndani ya
hoteli hiyo, alikuwa mteja ambaye alifanya juu chini kuzoeana na dada wa
mapokezi pamoja na msafisha vyumba.
Alikuwa mzungumzaji sana, mcheshi ambapo watu hao wawili walimsifia sana na
muda mwingi walitamani kuwa karibu naye. Katika kipindi cha wiki moja
alichokaa katika hoteli hiyo, alizoeleka sana.
“Unajua u msichana mzuri sana Rose,” alimwambia dada a mapokezi.
“Nani? Mimi?”

37
“Ndiyo! Una tabasamu zuri sana, macho ya goroli, umbo namba nane, hakika
namuonea wivu sana shemeji,” alisema Benjamin huku akimwangalia msichana
huyo wa mapokezi.
“Hahaha! Usitake nicheke! Kwenye wazuri na mimi nipo!”
“Ndiyo hivyo! Hebu subiri nikupige picha,” alisema Benjamin, hapohapo akatoa
simu na kumpiga picha kisha akamgawia.
“Hebu itazame hiyo picha, ushawahi kukutana na msichana mrembo kama huyo?”
aliuliza Benjamin huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Jamani! Unanionea hivyo!”
“Kweli! Natamani siku nijikute nikiwa nawe...yaani ghafla tuwe chumbani, hakika
hautojuta, nitakufanya uhisi kama siku hiyo ni siku yako ya kuzaliwa!” alisema
Benjamin.
“Kweli?”
“Huwa sitanii! Utani kwangu dhambi!”
Walibaki wakicheka kwa dakika kadhaa kisha kuondoka kuelekea chumbani
kwake. Wakati amefika katika korido, akakutana na msichana Mercy, msichana wa
usafi aliyekuwa amezoeana naye kama ilivyokuwa kwa Rose.
“Kwa mbali namuona mrembo wangu...” alisema kwa sauti huku uso akiwa
ameuachia kwa tabasamu pana.
“Hahah! Umeanza!”
“Kweli tena! Unajua sana kufanya usafi, ningekuwa na msichana kama wewe,
hakika ningejiona kuwa mtu mwenye bahati sana,” alisema Benjamin huku akiwa
amemsogelea msichana huyo.
“Mmh!”
“Ndiyo hivyo! Una ngozi nzuri sana, nywele ndefu, unanukia sana, hivi unatumia
manukato gani?” aliuliza Benjamin.
“The Prince!”
“Waoo!”

38
Kama kawaida yake alitafuta uhuru, alitaka kufanya mambo yake huku akiaminiwa
kwa asilimia mia moja. Baada ya kumsifia sana Mercy, akaingia ndani ya chumba
chake na kutulia.
Chumbani alikuwa na mawazo tele, kitu kilichobaki mbele yake kilikuwa kimoja
tu, kumuua Benjamin na kisha kuendelea na mambo yake likiwepo la kumpata
mchumba wake na kuondoka naye.
Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kusuka mipango yake, alitaka kuhakikisha siku
inayofuata anamuua Carter na kuondoka zake. Hilo lilionekana kuwa kazi kubwa
lakini alikuwa na uhakika kwamba angefanikiwa kama kawaida. Alipokuwa
kwenye mawazo hayo, mara simu yake ikaanza kuita.
“Vipi?” alikutana na swali hata kabla ya salamu!
“Nimefanikiwa kufika, na yeye amefika!”
“Umemuona?”
“Ndiyo!”
“Kwa hiyo unakamilisha lini mchakato huo?” aliuliza mwanaume huyo.
“Nafikiri kesho baada ya shoo!”
“Sawa! Fanya hivyo Bwana, ukishindwa, kama kawaida tunamuua huyu!”
“Msijali, nitafanikisha. Ila baada ya kumuua, nitampata Vivian kwa muda gani?”
aliuliza Benjamin.
“Baada ya kifo chake kutangazwa.”
“Basi hakuna tatizo! Kesho namuua...” alisema Benjamin, hapohapo simu
ikakatwa.
***
“Umefikia wapi David?” aliuliza Benjamin kwenye simu.
“Nilisahau, ila hilo si tatizo kaka, muda wowote ule nitalifanyia kazi,” alijibu
David.
“Umejisahau sana kaka, wanataka kumuua Vivian,” alisema Benjamin.
“Unasemaje?”

39
“Ndiyo hivyo, ninataka kujua alipo kwa sasa na ndiyo maana nikakwambia lile
jambo linatakiwa kufanyika kwa haraka sana,” alisema Benjamin.
“Basi sawa, nipe saa moja tu.”
Simu zikakatwa, Benjamin akatulia kitandani huku akionekana kuwa na mawazo
tele, bado kichwa chake kilichanganyikiwa mno, hakuamini kilichokuwa
kikiendelea maishani mwake.
Wakati mwingine aliwaza kutoroka lakini hilo lisingekuwa suluhisho hata kidogo,
ilikuwa ni lazima kama kuondoka, aondoke na Vivian lakini si kumuacha.
Kumuua Carter lilikuwa jambo gumu sana lakini mpaka kufikia kipindi hicho,
hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kumuua ili aweze kuyaokoa maisha ya mpenzi
wake ambaye mpaka kipindi hicho bado alikuwa mateka.
Watu hawakupungua hotelini hapo, walilala huku kila mmoja akitaka kumuona
Carter ambaye ndiye alikuwa gumzo duniani kwa kipindi hicho. Benjamin
akasimama dirishani na kisha kuchungulia nje, watu waliolala pale nje ya hoteli ile
walimfanya kuwa na huruma kumuua Carter, alijua ni kwa namna gani
angewaumiza watu hao, si wao tu bali hata watu wengine duniani kote, hakika
yangekuwa maumivu makubwa sana mioyoni mwao.
Kwa hatua aliyofikia, hakutakiwa kujali kitu chochote kile, kama alivyoambiwa
kwamba asipofanikisha kumuua Carter basi mpenzi wake angeuawa, hivyo
alitakiwa kupambana mpaka mwisho wa siku kuhakikisha kwamba mtu huyo
anauawa.
Siku iliyofuata ilikuwa ni ya kihistoria hapo Miami, watu walikusanyika katika
Ukumbi wa Carthebian uliokuwa katika ufukwe wa Salvador hapohapo Miami
kwa ajili ya kuangalia shoo iliyoandaliwa na wanafunzi waliowahi kusoma na
Carter.
Shoo ilikuwa nzuri, watu waliifurahia sana tena wengine wakichukua nafasi hiyo
kupiga picha na msanii huyo huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha mno.
Wakati shoo hiyo ikiendelea huko, huku hotelini Benjamin alikuwa bize, alitamani
sana kuingia chumbani kwa Carter lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza
kuingia.

40
Milango yote haikuwa ikitumia ufunguo, kulikuwa na kadi maalumu ambayo
ulitakiwa kuichukua na mlangoni kulikuwa na sehemu ya kupitishia kadi hiyo na
hatimaye mlango kufunguka.
Alichokihitaji kilikuwa ni kadi malaya ambayo angeweza kufungua kila chumba
na kufanya kile alichotaka kufanya. Kabla ya kuitafuta, akaandaa sindano yake
iliyokuwa na sumu ambayo aliiona kufaa sana kuchomwa Carter, baada ya
kuiweka vizuri, akaanza mishemishe za kumtafuta msichanaMercy kwa kuamini
kwamba alikuwa na kadi ya kufungulia milango yote kwani ndiye msichana
aliyekuwa akifanya usafi wakati wageni hawapo vyumbani mwao.
Huyo ndiye alikuwa mtu muhimu, ilikuwa ni lazima kumtafuta, alichokifanya,
akatoka chumbani humo na kuanza kumtafuta Mercy. Hakumuona na hakujua
alikuwa wapi. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, aliamini kwamba msichana wa
mapokezi, Rose alikuwa akifahamu msichana huyo alipokuwa, hivyo akaenda
huko kumuuliza.
“Mercy yupo wapi?” alimuuliza Rose.
“Wewe wa nini?” aliuliza Rose huku akionekana kuona wivu, kwa kifupi
alishaanza kumpenda Benjamin.
“Nataka nimuone tu.”
“Kuna nini?”
“Kwani si kumuona tu jamani, au kuna tatizo?” aliuliza Benjamin.
“So ili mkeo nijue jamani,” alisema msichana huyo, Benjamin akamwangalia kwa
macho makini, uzuri wake yeye mwenyewe ulimchanganya, ila hakutaka
kujionyesha kama alipagawa.
“Kumbe tatizo lipo wapi? Si nataka kumuona shemeji wangu,” alisema Benjamin.
Rose akashusha pumzi, alimwangalia Benjamin kwa umakini, alimpenda
mwanaume huyo na hakujua alikuwa akiishi wapi na alifika mahali hapo kufanya
nini.
Kwa sababu kwa maneno ya Benjamin alionekana kama kukubaliana naye,
akamwambia kwamba inawezekana Mercy alikuwa katika chumba cha usafi akifua
mashuka kwa mashine pamoja na vitu vingine. Chumba hicho kilikuwa ghorofa ya
sita, hakutaka kusubiri, akaelekea huko.

41
Alipandisha ngazi, hakutaka kutumia lifti kwa kuhisi kwamba angeweza kukutana
naye hata kwenye korido za ghorofa nyingine. Alipofika katika ghorofa hiyo
aliyoambiwa, akaelekea katika chumba kilichoandikwa laundry mlangoni,
akafungua.
Mbele yake kulikuwa na mashuka mengi yakiwa yameanikwa, yalikuwa zaidi ya
mia moja. Kumuona mtu wa upande mwingine ilikuwa ngumu sana hivyo
alichokifanya Benjamin ni kuanza kuita.
“Mercy...Mercy...” aliita mwanaume huyo.
“Helo...” aliita msichana huyo.
Benjamin akaenda huko alipoitikiwa, alipofika, akamkuta Mercy akiwa peke yake,
alikuwa akitoa mashuka kutoka kwenye tenga na kuweka kwenye mashine moja ya
kufulia, hapohapo akamsogelea.
“What are you doing here?” (Unafanya nini hapa?) aliuliza Mercy huku
akimwangalia mwanaume huyo machoni.
“I am here to see you baby! Is anyone here?” (Nipo hapa kukuona! Kuna
mwingine hapa?) alijibu Benjamin na kuuliza.
“Nobody...” (Hakuna mtu)
Kabla ya kufanya kitu chochote kile alitakiwa kutafuta mahali kadi ilipokuwa,
kwenye kuangalia huku na kule, pembeni akauona mkoba wa Mercy, akajua
kwamba ni lazima ndani ya mkoba huo kulikuwa na hiyo kadi, hivyo akamchukua
msichana huyo na kumpeleka kule kulipokuwa na mokoba ule.
“Kuna nini?” aliuliza msichana huyo.
“Nataka nikuone jinsi ulivyo, umezishtua hisia zangu,” alisema Benjamin huku
akijifanya kuhema juujuu kimahaba.
“Jamani ndiyo unataka hapa?”
“Kwani kuna tatizo? Kuna mtu anatuona?” aliuliza Benjamin huku tayari mikono
yake ikiwa imeanza kazi ya kufungua vifungo vya blauzi ya Mercy.
“Aishiiii...” alianza kutoa kelele za mahaba.

42
Akili ya Benjamin ilikuwa kwenye ule mkoba tu, aliihitaji kadi iliyokuwa katika
mkoba ule na hakukuwa na njia nyingine ya kuipata kadi ile zaidi ya kufanya kile
alichokuwa akikifanya.
Akaanza kumvua msichana huyo suruali ya jinzi aliyokuwa ameivaa na kubaki na
nguo ya ndani tu, akaanza kuutalii mwili wake kwa kupanda huku na kule, kwa
jinsi Mercy alivyochanganyikiwa, akaanza kufumba macho kimahaba,
alichanganyikiwa mno.
“Unanukia vizuri sana...” alisema Benjamin kwa sauti ya chini karibu na sikio la
Mercy.
“As..an..t..e..” aliitikia msichana huyo, mwili wake ulikuwa hoi.
Kitendo cha kufumba macho tu, Benjamin hakutaka kuchelewa, hapohapo
akaupeleka mkono ule kisiri tena huku kichwa chake kuyaficha macho ya
msichana huyo.
“Hii hapa...” alijisemea moyoni mara baada ya kuigusa kadi hiyo mkobani,
alichokifanya ni kuichukua, akaiingiza mfukoni kisiri, kilichofuata ni kufanya
mapenzi na msichana huyo ndani ya chumba hichohicho cha kufulia.
Walichukua dakika arobaini na tano mpaka kumaliza. Mercy alikuwa hoi,
hakuamini kama angeweza kukutana na mwanaume anayeweza kufanya mapenzi
kama ilivyokuwa kwa Benjamin.
Hapohapo wakaanza kuvaa nguo zao na kisha kubaki wakiangaliana tu. Hakukuwa
na mtu aliyesema chochote kile zaidi ya kusogeleana na kukumbatiana tu.
“Ninakupenda...” alisema Benjamin.
“Nakupenda pia.”
Benjamin hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kurudi
chumbani kwake huku tayari akiwa na kadi ile mfukoni mwake, alipofika, akaingia
chumbani na kutulia.
Mpango aliokuwa nao ilikuwa ni lazima akalale chumbani kwa Carter usiku
huohuo ili iwe rahisi kwake kukamilisha mpango wake. Muda ulizidi kwenda
mbele, kuna kipindi alihisi kwamba angeweza kuchelewa, hivyo akaamka,
akachukua kitambaa kilichokuwa na dawa za usingizi na kisha kutoka mule huku
mfukoni akiwa na bomba la sindano.

43
Kwenye korido, hakukuwa na kamera za CCTV hivyo ilikuwa ni rahisi kwake
kuingia humo ndani. Akachukua kadi yake na kuipachika katika kimashine kidogo,
zikawaka taa nyekundu kwa zamu kisha kubadilika na kuwa za kijani, mlango
ukafunguka.
Akaingia chumbani mule, hakikuonekana kuwa tofauti na chumba chake, vyote
vilikuwa vya bei kubwa, alibaki akizungukazunguka mule, aliporidhika, akakifuata
kitandani, kwa sababu kilikuwa na uvungu mkubwa kidog uliomuwezesha
kupenya japo kwa tabu, akaingia humu huku akiwa na bomba la sindano na
kitambaa ambacho alikiwekea dawa za usingizi.
“Ngoja nisubiri...Mungu, sifanyi hivi kwa kupenda, nimelazimishwa kwa ajili ya
mpenzi wangu,” alisema Benjamin kwa sauti ndogo huku akivaa glovu mikono
mwake.
Hakulala hata kidogo, alikuwa macho huku akiendelea kumsubiri Carter ambaye
aliamini hakuwa mbali mpaka kufika mahali hapo. Huko uvunguni, alizima simu
yake, hakutaka kufanya kosa lolote lile na kuonekana kabla hajakamilisha mpango
wake.
Muda ulizidi kwenda mbele, ilipofika saa kumi alfajiri, akasikia sauti za watu nje,
kwa kukadiria zilikuwa kama za watu sita, watu wale wakasogea mpaka mlangoni
na kisha kuufungua.
Alikuwa Carter na wapambe wake, wakaingia ndani huku kila mmoja akionekana
kuwa na furaha. Muda ulikuwa umekwenda sana na hawakuwa na muda wa
kupoteza, Carter akaenda bafuni, akaoga na kisha kurudi chumbani pale.
Wakapiga stori, nyingi walizozipiga hapo zilikuwa ni za kumsifia Carter kwamba
alifanya kazi nzuri sana, aliwaonyeshea watu yeye alikuwa nani. Walikaa kwa
dakika kadhaa mpaka muda ule ambao wengine wakaenda kulala na yeye kutulia
kitandani ambapo baada ya dakika chache, akapitiwa na usingizi.
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi kwa Benjamin kumuua Carter, hakutaka kuchelewa kule
uvunguni, harakaharaka akatoka na kisha kumwangalia Carter kitandani pale,
alichokifanya ni kuchukua kitambaa kile kilichokuwa na dawa ya usingizi na kisha
kumkandamiza Carter kitandani pale huku kitambaa kile kikiwa usoni mwake.
Carter hakukubali, alijitahidi kuhangaika huku na kule ili kujinasua lakini
ilishindikana kabisa, alikandamizwa kitandani pale na kadiri alivyovuta pumzi na

44
ndivyo alivyokuwa akiivuta dawa ile na sekunde chache mbele, akatulia kitandani
pale.
“Kazi imekwisha...” alisema Benjamin.
Mara baada ya kufanikiwa kumlevya kwa yale madawa yaliyokuwa kwenye
kitambaa kile akachukua bomba la sindano aliyokuwa nayo na kisha kumchoma
katika mshipa mmoja mkononi mwake ili aweze kumuua kitandani pale.
Alipohakikisha sumu ile imeingia vilivyo mwilini mwake, akachukua fedha
ambazo aliambiwa aziweke ikiwepo euro, dola, yen na paundi kisha kuanza
kufanya mikakati ya kutoka ndani ya chumba kile.
Hakukuwa na shida kwenye kutoka, akaufungua mlango ule na kutoka. Hakutaka
kuingia chumbani kwake, akaelekea katika chumba kile cha kufanyia usafi kwa
kufua mashuka na nguo kisha akaitupa ile kadi chini, pembenipembeni na kisha
kurudia chumbani kwake, akavuta shuka na kutulia.

****
“Umenionea kadi yangu?” aliuliza msichana Mercy huku akionekana
kuchanganyikiwa.
“Kadi gani?”
“Ya milango!”
“Hapana! Kwani wewe uliiweka wapi?”
“Niliiweka kwenye huu mkoba.”
“Sasa iko wapi?”
“Ndiyo siioni.”
“Umeangalia vizuri?”
“Ndiyo! Hakuna!”
Mercy alichanganyikiwa, alikumbuka vilivyo kwamba aliiweka kadi ndani ya
mkoba wake, lakini katika kipindi hicho alipokuwa akiitafuta, hakuwa akiiona.
Akaondoka mahali hapo na kwenda sehemu zote alizopita lakini huko hakuona
kitu.

45
Mercy alizidi kuchanganyikiwa, hakukumbuka kama aliuacha mkoba ule sehemu
yoyote ile, mtu pekee na wa mwisho kumjia kichwani mwake alikuwa Benjamin.
“Inawezekana anajua...”
Alichokifanya Mercy ni kumpigia simu ya mezani chumbani kwake, kitu
kilichomshtua ni kwamba simu iliita lakini haikupatikana. Mercy hakutaka kukata
tamaa, aliendelea kupiga zaidi na zaidi lakini majibu wala hayakubadilika, bado
simu ile haikupokelewa kitu kilichomtia wasiwasi mwingi.
“Au ameshaondoka?” alijiuliza.
Akaondoka na kuelekea mapokezini na kumuuliza dada aliyekuwepo hapo,
hakuwa Rose, yeye aliondoka na kumuacha msichana mwingine, akamuuliza kama
mteja aliyepanga chumba namba tisini na mbili alikuwa ameondoka.
“Hapana! Bado yupo,” alijibu msichana huyo.
“Mbona nampigia simu simpati?”
“Sijui! Inawezekana amelala, ila hapa inaonyesha yupo, hajaondoka,” aliongeza
msichana huyo.
Mercy hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kwenda wenyewe mpaka katika chumba
kile, alipoufikia mlango, akaanza kugonga kwa nguvu, aligonga zaidi na zaidi
lakini mpango wala haukufunguliwa kitu kilichoendelea kumpa maswali mengi.
“Mmh! Mbona naanza kuwa na wasiwasi...” alisema msichana huyo, akahisi
akichoka, kilichobaki mbele yake kilikuwa ni kufukuzwa kazi tu, hakukuwa na
kitu kingine zaidi ya hicho kwani kupoteza kadi, tena ile masta kabisa lilikuwa
kosa kubwa mno.
Akaondoka na kuelekea nyumbani kwake, hakuwa na raha, alipanga siku
inayofuata kuwa asubuhiasubuhi kuzungumza na Benjamin kwani bado moyo
wake ulimwambia kwamba mwanaume huyo aliiona ile kadi aliyokuwa akiitafuta.
***
Asubuhiasubuhi msichana Mercy akafika hotelini hapo, bado akili yake haikuwa
sawa hata kidogo, alikuwa na mawazo mengi, kadi ambayo aliipoteza usiku
uliopita ilimchanganya mno.
Alipofika hotelini, hata kabla ya kufanya kitu chochote ilikuwa ni kwenda katika
chumba cha Benjamin ili aonane naye na kumuuliza kuhusu kadi hiyo. Alipofika,

46
akagonga mlango ambapo baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafunguliwa,
mwanaume aliyesimama mbele yake alikuwa Benjamin.
“Kumbe wewe...karibu mpenzi,” alisema Benjamin huku akimkaribisha msichana
huyo huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Ahsante! Nimekuja kukuuliza kitu,” alisema msichana huyo.
“Kitu gani?”
“Nilipoteza kadi jana!”
“Kadi gani?”
Alijifanya kutokufahamu chochote kile, hata macho yake yalionyesha kabisa
kwamba hakujua kilichokuwa kikiendelea. Mercy akaanza kumwambia kuhusu
kadi ile ambayo aliipoteza katika mazingira ya kutatanisha huku muda wote huo
akionekana kuwa na majonzi tele usoni mwake.
“Pole sana, ila umeangalia vizuri kwenye kile chumba?” aliuliza Benjamin.
“Nimeangalia kila kona.”
“Umetoa nguo zote na kuangalia vizuri?”
“Ndiyo!”
“Mmh! Sasa iweje isionekane?” aliuliza Benjamin.
“Ndiyo nashangaa!”
Alichokifanya Benjamin ni kumwambia waende kwenye kile chumba cha kufanyia
usafi, alikuwa na uhakika kwamba kadi ile ilikuwa mule kwani alfajiri ya siku hiyo
aliirudisha na kurudi chumbani kwake.
Mercy alikuwa na uhakika kwamba kadi hiyo haikuwepo huko, aliangalia kila
kona, alitoa nguo zote na kuzirudisha lakini hakufanikiwa kuiona kadi hiyo.
Benjamin alipomaliza kujiandaa, wakaelekea katika chumba hicho na kuanza
kuitafuta kadi hiyo.
Kwanza Benjamin hakutaka waende kwenye ule upande alioiweka kadi ile,
alimwambia Mercy waende kwenye upande mwingine kitu ambacho kikafanyika
kikamilifu. Walipokosa na ndipo walipokwenda kwenye ule upande uliokuwa na
kadi, kweli wakaikuta.
“Ni hii hapa,” alisema Mercy huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.

47
“Wewe si ulisema umeikosa?”
“Ndiyo! Nilitafuta sana, nafikiri huku sikuja,” alisema msichana huyo.
Wakabaki wakiangalia tu, tayari miili yao ikaanza kuwasiliana mahali hapo,
walikuwa wawili tu kama jana na kila mtu alionekana kumtamani mwenzake.
Wakiwa wanaangalia kama mbuzi, wakaanza kusikia mlango mmoja huko nje
ukigongwa, uligongwa huku sauti za watu zikisikika mahali hapo.
Kwanza wakashtuka, haikuwa kawaida kabisa, wakatoka chumbani humo na
kwenda kwenye korido, marafiki zake Carter walikuwa katika mlango wa chumba
alichochukua Carter na kuanza kugonga huku wakitaka wafunguliwe.
“Jamani, si jana amechelewa kulala, ataweza kuamka muda huu?” aliuliza Mercy
huku akionekana kuwashangaa.
“Hatuna muda, tunatakiwa kuondoka sasa hivi,” alijibu jamaa mmoja.
Alichokifanya Mercy ni kwenda mapokezini ambapo huko akaanza kupiga simu ya
mezani ndani ya kile chumba cha Carter, alipiga simu, iliita na kuita lakini
haiupokelewa.
Hilohilo ndilo lililotokea kwa Benjamin usiku wa jana, hata naye alipojaribu
kupigiwa simu hakuipokea. Wote wakaanza kushikwa na wasiwasi, wafanyakazi
wa hoteli hiyo hawakutulia, wakaanza kupandisha juu mpaka kwenye korido
iliyokuwa na chumba kile na kuanza kugonga.
Wakati huo Benjamin alikuwa chumbani kwake, alifuatilia kila kitu kilichokuwa
kikiendelea, hakutaka kutoka nje, alitaka kuona kitu gani kingeendelea.
Mara akasikia mlango ukianzakupigwa, watu hao waligonga na kugonga, mlango
haukufunguliwa na hivyo kuanza kuuvunja. Ilikuwa kazi kubwa, mlango ulikuwa
imara sana, walifanya hivyo kwa zaidi ya dakika nne, mlango ukafunguka na
kuingia ndani.
Picha waliyoiona, hakukuwa na mtu yeyote aliyeiamini, Carter alikuwa juu ya
kitanda chake, sindano iliyokuwa na madawa ilikuwa katika mkono wake, tena
ikiwa imechoma katika mshipa wake, kwa jinsi picha ilivyoonekana ilionyesha
kabisa kwamba mtu huyo alikuwa amejidunga madawa ya kulevya.
“What the fuck is this?” (Ndiyo nini hiki?) aliuliza jamaa mmoja huku akionekana
kushtuka.

48
Wakamsogelea kitandani pale, wanawake waliomuona Carter wakaanza kupiga
kelele, waliokuwa wamelala katika vyumba vyao wakaamka na kwenda chumbani
humo kushuhudia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
Mbali na mwili huo, pembeni yake kulikuwa na fedha za noti, dola, yeni, euro na
paundi. Hilo wala halikuwafanya kuhisi chochote kile kwani kwa mtu kama Carter,
kuwa na fedha mbalimbali lilikuwa jambo la kawaida sana.
“Was he cocaine addicted?” (Alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya?) aliuliza
jamaa mmoja huku akimwangalia Carter pale kitandani.
Marafiki zake walibaki wakiashangaa, hawakuamini kile kilichokuwa kikiendelea,
rafiki yao wa muda mrefu, Carter eti alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Hawakutaka kuamini hilo, pale kitandani alipokuwa, alikuwa kimya kabisa na hata
mapigo yake ya moyo hayakuwa yakidunda hali iliyoonyesha kwamba alikuwa
amekufa.
Walichokifanya ni kupiga simu polisi ambapo baada ya dakika ishirini walikuwa
mahali hapo. Moja kwa moja wakaenda mpaka katika chumba hicho huku
wakiwataka watu wote watoke nje na wao kufanya kazi yao.
Tayari mpiga picha wa polisi pamoja na mchoraji walifika mahali hapo na kuanza
kuuangalia mwili wa Carter, alionekana kutumia kiasi kikubwa cha madawa
mpaka kufariki pale kitandani.
Si marafiki zake walioshangaa tu bali hata polisi wenyewe nao walishangaa.
Walimfahamu Carter, alikuwa mmoja wa wanamuziki wadogo ambao walitumika
hata na kampuni mbalimbali kutokomeza utumiaji wa madawa ya kulevya, sasa
iweje mtu huyo leo afe kwa kuzidisha utumiaji wa madawa hayo? Kila
walichojiuliza, walikosa jibu.
Stori juu ya kifo chake zikaanza kusambazwa kwa kasi, hakukuwa na mtu
aliyeamini kwamba mwanamuziki aliyekuwa na jina kubwa, Carter alikuwa
amefariki dunia tena kwa kujidunga madawa ya kulevya kwa kiasi kikubwa.
Kila mtu aliyesikia taarifa hizo alibaki akishangaa, wengi wakajiuliza na mwisho
wa siku kuja na majibu kwamba Carter alifanya siri utumiaji wa madawa ya
kulevya.

49
Ulikuwa msiba mkubwa, kijana huyo, mwanamuziki huyo alikuwa na jina kuubwa,
alikuwa kipenzi cha watuu wengi kitendo cha kusikia kwamba alikuwa amekufa
ndani ya chumba hicho, hakika yalikuwa majonzi makubwa mno kwa kila mtu.
Taarifa hizo ziliendelea kuwekwa katika mitandao ya kijamii, kila aliyeziona,
hakuamini, ndani ya saa moja tu, dunia nzima ilijua kile kilichokuwa kimetokea
nchini Marekani huko Miami.
Watu walilia sana, wengine walijiuliza maswali mengi juu ya sababu iliyomfanya
Carter kutumia madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa hicho mpaka kufa ndani
ya chumba hicho.
Kila mtu alilaumu, wengine wakamuonea huruma. Mpaka mwili wake unaingizwa
katika Hospitali ya St. Martin Luther King, tayari watu wengi walikusanyika
hospitalini hapo, walitaka kusikia kile kilichokuwa kikiendelea, walitaka kuamini
kama kweli msanii huyo alikufa baada ya kutumia madawa ya kulevya kupita
kiasi.
“Nimefanya mlichotaka nikifanye, naomba mmuachie mpenzi wangu,” alisema
Benjamin, alikuwa akizungumza na mtu fulani katika simu.
“Sawa! Tumeona, umefanya kazi nzuri sana...” ilisikika sauti upande wa pili.
“Kwa hiyo?”
“Kuhusu?”
“Mpenzi wangu! Si tayari nimekwishafanya kazi yenu, muachieni sasa,” alisema
Benjamin.
Alikuwa akizungumza na mwanaume wa upande wa pili, alikuwa akimpa taarifa
kwamba kazi aliyokuwa amepewa tayari ilikuwa imefanyika na hivyo alitaka
mpenzi wake aachiwe huru kama yalivyokuwa makubaliano yao kabla.
Kwanza mwanaume huyo alikataa, kwa jinsi ilivyoonekana, alitaka kumuongezea
kazi nyingine, ila alipotaka kufanya hivyo, aliona haikuwa sahihi kwani
makubaliano ambayo waliwekeana mwanzo yalikuwa ni kumuua Carter na
hakukuwa na jingine.
Walichokifanya huko walipokuwa ni kumfunga kitambaa cheusi Vivian na
kumpakiza ndani ya gari, wakaanza kuondoka naye huku waliomsindikiza wakiwa
wanaume wawili, waliokuwa na miili iliyojazia.

50
Njiani, Vivian alikuwa akilia, moyoni mwake aliumia mno, hakujua sababu
iliyomfanya kutekwa na watu hao, kila alipouliza, hakupewa jibu bali aliambiwa
asubiri mpaka atakapokutana na mpenzi wake.
Safari hiyo iliendelea mpaka walipofika katika kituo cha mafuta cha Total ambapo
hapo ndipo walipomkabidhi Benjamin msichana Vivian ambaye hakuonekana
kuwa sawa kabisa, kila wakati alikuwa akilia tu.
“Wamekufanya nini? Wamekupiga?” aliuliza Carter.
“Hapana! Kwa nini wamefanya hivi?” aliuliza Vivian.
“Sijajua! Acha tuondoke,” alisema Benjamin huku akionekana kutokujiamini.
“Benjamin, bosi amesema uchukue hii simu,” alisema mwanaume huyo huku
akimpa simu aina ya iPhone 7.
“Ya nini?” aliuliza Benjamin huku akiichukua simu hiyo.
“Kama zawadi yako!”
“Nashukuru!” alisema Benjamin na kisha kumrudishia mwanaume huyo kwani
alihisi kwamba simu hiyo ilikuwa na kifaa cha GPS ambacho kingemfanya
kuonekana kila alipokuwa.
“Basi hakuna tatizo!”
Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuingia ndani ya gari na
kuanza kuondoka mahali hapo. Alichokifikiria Benjamin ni kuondoka na mpenzi
wake kwenda mbali kabisa kujificha, hakutaka kuonekana kwani kile alichokuwa
amekifanya chumbani kwa Carter, alikuwa na uhakika kwamba watu hao
wangemtafuta na kumuua tu.
Walipofika katika apartment waliyokuwa wakiishi, Benjamin akamwambia Vivian
wachukue kila kitu chao na kuondoka mahali hapo, kweli wakafanya hivyo.
“Ila kwa nini?” aliuliza Vivian.
“Wewe tuondoke, watatutafuta hawa.”
“Kisa?”
“Nimewachezea mchezo!”
“Mchezo gani?”

51
“Usijali, nitakwambia nini kilitokea,” alisema Benjamin huku akiendesha gari kwa
kasi ya ajabu, alikuwa katika barabara ya St. Johnson ya magari yaendayo kasi kwa
zaidi ya 180, ilikuwa ni lazima waondoke na kuelekea Alexandria, mji uliokuwa
pembeni mwa jiji hilo la Washington DC.

52
SURA YA TATU

MADAKTARI waliendelea na tiba yao kama kawaida, mwili wa Carter


uliwekwa kitandani huku ukiwa umetundikwa na dripu kadhaa. Japokuwa taarifa
za awali zilisema kwamba mwanamuziki huyo alikuwa amekufa lakini
walipomchunguza, wakagundua kwamba hakuwa amekufa bali mwili wake
uliwekewa dawa Declophine, dawa ambayo mtu akiwekewa katika mishipa yake
husimamisha mapigo ya moyo kwa muda.
Madaktari walikuwa wakiingia kwa zamu, walikuwa bize wakiendelea kumpa
matibabu mwanamuziki huyo kwa kumwekea dawa iitwayo Anti-Declophine
ambayo ndiyo ilikuwa na uwezo wa kuyarudisha mapigo ya moyo ya Carter.
Mpenzi wake alifika hospitalini hapo, muda wote alikuwa mtu wa kulia tu,
hakuamini kama kweli siku ile aliyoagana naye na kwenda Miami ndiyo ingekuwa
siku ya mwisho kuonana naye.
Ndugu zake ndiyo waliokuwa msaada, walimshika huku na kule, kila alipotaka
kufanya jambo baya, walimzuia kwani walijua kabisa kwamba katika kipindi kama
hicho angeweza kufanya jambo lolote baya.
Kama dunia ilivyokuwa ikishangaa, hata naye alikuwa akishangaa, mpenzi wake
kufa huku akiwa amejidunga madawa ya kulevya ilimshangaza sana. Alikuwa naye
kwa kipindi kirefu, walifanya mambo mengi walizoeana sana lakini hakukuwa hata
na siku moja ambayo alimuona mpenzi wake akitumia madawa ya kulevya, si
kutumia tu, hata kumuona akiyasifia madawa hayo, hakuwahi kusikia kitu kama
hicho.
Kazi ilikuwa kubwa, kiasi cha dawa hiyo ambacho alipewa Carter ilionyesha
kwamba angechukua saa arobaini na ndipo angerudiwa na fahamu hivyo. Nje ya
hospitali hiyo, kulikuwa na watu wengi wakiwemo waandishi wa habari, kila mtu
alitaka kusikia madaktari wangesemaje kuhusu afya ya Carter ambayo ilikuwa tata
sana.
Madaktari hawakutaka kuzungumzia chochote kile, walikwishajua kile
kilichokuwa kimetokea lakini hawakutaka kumwambia mtu yeyote kwa kuhisi
kwamba kama wangefanya hivyo basi amtu aliyekuwa amemchoma sindano hiyo
angeweza kumrudia hapo hospitalini na kufanikisha mpango wake.

53
Saa ziliendelea kusonga mbele, saa arobaini zilipofika, Carter akaanza kutingisha
viungo vyake pale kitandani alipokuwa. Kiungo cha kwanza kabisa
alichokitingisha kilikuwa ni vidole kisha kuyafumbua macho yake.
“He is back...” (Amerudi...) alisema Dk Phinias.
Kila mmoja akaonyesha tabasamu pana, kitendo cha Carter kurudiwa na fahamu
kiliwafurahisha mno na hivyo kuwasiliana na wazazi wake ambao walikuwa nje na
kuwapa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Unasemaje?” aliuliza baba yake huku akionekana kutokuamini.
“Carter amerudiwa na fahamu!” alijibu Dk. Phinias.
“Inawezekana vipi?”
“Subirini kwanza, tunahitaji kuzungumza na polisi!”
Kila mmoja aliyesikia jibu la daktari alibaki akiwa na furaha mno, hawakuamini
kile walichokisikia kwamba Carter alikuwa amerudiwa na fahamu. Ilikuwaje
arudiwe na fahamu na wakati ukweli ulijulikana kwamba alikufa baada ya
kujidunda madawa ya kulevya hotelini?
Hawakuamini hivyo wakataka kumuona. Kutokana na furaha walizokuwa nazo,
wakashindwa kuvumilia na hivyo kuwataarifu watu wengine, hapo ndipo stori
zilipoanza kuvuma kwamba kumbe Carter hakufa bali alikuwa amezimia.
“Sasa kwa nini polisi walisema kwamba alikufa? Kama alikufa si inamaana
walisikiliza mapigo ya moyo lakini hayakuwa yakidunda, kama hayakuwa
yakidunda, kwa nini yupo hai?” yalikuwa maswali kadhaa waliyojiuliza watu
mitaani, maswali yalikuwa mengi mengi lakini hakukuwa na aliyepata jibu.

****
Bwana David Seppy alikasirika, hakuamini kile alichokisoma kwamba mtu
aliyetaka afe, hakuwa amekufa, alichukuliwa kutoka hotelini na kupelekwa
hospitalini na madaktari wakamtibu na hatimaye kupona.
Hakujua ni kitu gani kilitokea, hapo ndipo alipogundua kwamba Benjamin hakuwa
mtu wa kawaida, alitumia ujanja ambao mpaka wao wenyewe hawakuuelewa
ulikuwa ujanja upi ambao ulivizuga mpaka vyombo vya habari na kuripoti
kwamba Benjamin alikuwa amekufa.

54
Hapohapo akawapigia simu vijana wake, kwa jinsi walivyomuona siku hiyo,
hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida hata kidogo, alionekana kuwa na hasira
sana na hata alivyokuwa akizungumza alionekana kuwa mtu ambaye hakuleta
utani hata mara moja.
Aliwaangalia vijana hao kwa zamu, aliwalaumu kwa kuwa walipewa taarifa
kwamba Carter alikufa, hawakutaka kujiridhisha, wakakubaliana na Benjamin
kwamba kijana huyo alikufa.
“Nani ana uhakika kwamba Carter amekufa?” alianza kwa kuuliza swali huku
akiwaangalia vijana hao watatu kwa zamu, wote wakanyoosha mikono juu.
“Mna uhakika kwamba amekufa?” aliuliza Bwana Seppy.
“Ndiyo bosi!”
“Umesikia wapi?”
“Kwenye vyombo vya habari, na hata wewe tulikuja kukwambia kwamba kijana
huyo amekufa, ukatuambia tumeona wapi, tukakuonyesha picha katika mitandao,
ilionyesha kabisa kwamba alikufa, ukakubaliana nasi,” alisema kijana mmoja huku
akimwangalia Bwana Seppy usoni.
Mzee huyo hakutaka kuzungumza kitu, akabaki kimya, ni kweli alikumbuka
kwamba aliwaambia vijana hao maneno hayo kwamba mtu huyo alikuwa
ameuawa, lakini kwa nini naye alikubaliana moja kwa moja kwamba mtu huyo
alikuwa ameuawa, kila alipojiuliza, akakosa jibu.
“Sasa sikilizeni, ninataka muhakikishe kwamba hawa watu wawili wanauawa
haraka iwezekanavyo,” alisema Bwana Seppy huku akiwaangalia vijana wake hao
kwa zamu.
“Wawili tena?”
“Ndiyo! Carter na Benjamin, hakikisheni kabla mwezi huu haujakwisha,
wanauawa wote,” alisema mzee huyo.
“Sawa mkuu!”
Maofisa wa upelelezi nchini Marekani, FBI (Federal Bureau Investigation)
walitaka kufuatilia kuona ni kitu gani kilitokea mpaka hali iliyomkuta Carter
imkute huku ulimwengu mzima ukijua kwamba mwanamuziki huyo alikufa
hotelini baada ya kujiovadozi madawa ya kulevya.

55
Walitaka kupata ripoti kamili kutoka kwa madaktari, walikuwa na uhakika
kwamba walijua kuwa mtu huyo alikufa kutokana na mapigo yake ya moyo
kusimama, sasa ilikuwaje mpaka awe hai kipindi hicho, wakahisi kwamba
kulikuwa na kitu kilitokea ambacho nao walitaka kukifahamu.
Harakaharaka wakawasiliana na uongozi wa Hospitali ya Martin Luther King na
kutaka kuzungumza na daktari mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Terry. Walitaka
kusikia kila kitu, walijua kwamba piga ua madaktari walifahamu ni kitu gani
kilikuwa kimetokea mpaka hali hiyo kuwa hivyo.
Hawakutaka kuchelewa, wakawatuma maofisa wawili ambao walikwenda moja
kwa moja mpaka katika hospitali hiyo na kukutana na Dk. Terry ambaye mara
baada ya kuambiwa dhumuni la maofisa hao kufika hospitalini hapo, akaahidi
kutoa ushirikiano wote.
“Tunahitaji kufahamu kuhusu Carter,” alisema ofisa mmoja.
“Hakuna tatizo! Kipi mngependa kufahamu?” aliuliza Dk. Terry.
“Kuhusu kile kilichotokea, kuna ripoti yake?”
“Ndiyo! Ila bado sijaletewa ofisini!”
“Tunahitaji kuiona, na tunataka kujua nini kilitokea, ikiwezekana tuzungumze na
madakatri wa kwanza ambao waliupokea mwili wake,” alisema ofisa mmoja.
Hilo wala halikuwa tatizo, alichokifanya daktari huyo ni kuwasiliana na daktari
mmoja miongoni mwa madaktari waliompokea Carter na kumuhitaji ndani ya ofisi
yake huku akiwa na ripoti kamili mara baada ya mwili wake kuchunguzwa na
madaktari wa hospitali hiyo.
Ni ndani ya dakika kumi tu, mlango wa ofisi hiyo ukaanza kugongwa, Dk. Terry
akamkaribisha mgongaji, mwanamke mmoja wa makamo akaingia ndani ya ofisi
hiyo huku akiwa amevalia koti refu jeupe, shingoni alining’iniza mashine ya
kusikilizia mapigo ya moyo, alipoingia ndani ya ofisi hiyo, akasalimia na kisha
kumpa ripoti ile Dk. Terry ambaye akaanza kuiangalia.
“Mmh!” aliguna Dk. Terry.
“Kuna nini?” aliuliza ofisa mmoja.

56
“Ripoti inaonyesha kwamba alichomwa sindano iliyokuwa na Declophine, hii ni
dawa ya kusimamisha mapigo ya moyo kwa muda,” alisema daktari huyo, maofisa
wale wakajiweka vizuri vitini.
“Declophine! Ina maana alichomwa?”
“Hatuna uhakika, inawezekana alijichoma pia, hatuwezi kufahamu hilo,” alijibu
daktari huyo.
“Kuna kingine?”
“Ndiyo! Sasa hapa nimepata uhakika kwamba alichomwa kwa sababu ripoti
inaonyesha kwamba puani alipuliziwa dawa kali ya usingizi,” alisema daktari
huyo.
“Na nani?”
“Hilo hatufahamu! Limetokea huko hotelini!’
“Kwa hiyo kulikuwa na mtu alitaka kumuua?”
“Sijajua! Mpaka hapa ripoti inashangaza! Hivi kweli mtu ambaye alitaka kumuua
angeweza kumchoma sindano yenye Declophine?” aliuliza daktari huyo.
Hakukuwa na mtu aliyejibu swali hilo, kila mmoja alikuwa kimya. Swali alilouliza
Dk. Terry lilikuwa kweli kabisa, kama kulikuwa na mtu aliyekuwa ameingia ndani
ya chumba hicho kwa ajili ya kumuua, asingeweza kumchoma sindano iliyokuwa
na Declophine, kama kweli alidhamiria kuua, basi angemuua kwa kumchoma
sindano yenye sumu kali.
“Kwa nini huyo mtu alifanya hivi?” aliuliza ofisa mmoja.
“Hatujui!”
“Au Carter mwenye alitaka kutengeneza jina zaidi?”
“Nalo hatujui!”
“Ni lazima tufanye naye mahojiano, nadhani kuna jambo kubwa limejificha nyuma
ya pazia,” alisema ofisa huyo, hawakutaka kubaki ofisini humo, wakaondoka zao
kurudi makao makuu huku wakiwa na kopi ya ripoti hiyo.
“Hapana! Haiwezi kuwa hivi!” alisema mkuu wa upelelezi kitengo cha FBI.
“Hiyo ndiyo ripoti tuliyopewa!”

57
“Yaani mtu atokee tu na kumchoma sindano yenye Declophine, hivi inawezekana
kweli? Ausimamishe moyo ili iweje? Kama angetaka kumuua si angemuua tu!”
alisema mkuu huyo.
Ripoti hiyo ikaanzisha maswali mengi vichwani mwa FBI hao, kila mmoja
alijiuliza sababu ya mvamizi kutumia sindano yenye Declophine lakini wakakosa
jibu kabisa.
Walijua kwamba inawezekana mvamizi huyo alikuwa akimfuatilia Carter tangu
kitambo lakini swali kubwa lilikuwa ni sababu gani ilimfanya kutumia Declophine
kuusimamisha moyo wake na wakati alikuwa na uwezo mkubwa wa kumuua?
Hapo ndipo wakapata jibu kwamba wamfuate Carter hospitali na kuzungumza
naye, awahadithie ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka kuchomwa sindano
iliyokuwa na Declophine.
FBI hao hawakutaka kuchelewa, harakaharaka wakaondoka na kwenda hospitalini
huko, walipofika, kwa kuwa tayari Carter alikuwa akijisikia nafuu, wakaruhusiwa
kwenda kuzungumza nao, Carter alipowaona tu, akashtuka.
“Unaweza kutuambia nini kilitokea ndani ya chumba kile cha hotelini?” aliuliza
ofisa mmoja mara baada ya salamu, muda huo, macho yake yalikuwa usoni mwa
Carter tu.
“Naweza!”
“Nini kilitokea?” aliuliza ofisa huyo na Carter kuanza kuelezea kila kitu
kilichotokea siku hiyo, mpaka aliporudi hotelini, alipolala na kisha kushtukia
akiwa ameshikwa na mtu na kuanza kuvutishwa madawa ya usingizi, baada ya
hapo, hakujua kitu gani kiliendelea kwani alipofumbua macho, alijikuta akiwa
hospitalini.
****
Carter akaanza kuhadithia kila kitu kilichotokea hotelini katika usiku ambao
alimaliza shoo yake na kurudi huko. Hakutaka kuficha, yeye mwenye alibaki
akishangaa mara baada ya watu kumwambia kwamba alikufa, alikufa vipi na
wakati alipewa tu madawa ya uzsingizi?
Wakati akisimulia hivyo, maofisa wa FBI walikuwa kimya wakimsikiliza, simulizi
yake ilisema kwamba alivamiwa chumbani na mtu ambaye alikuwa na uhakika
alikuwa ndani ya chumba hicho, baada ya kumvamia kitandani, akamkamata

58
vilivyo na kumnusisha kitambaa kilichokuwa na madawa, baada ya hapo, hakujua
nini kiliendelea zaidi ya kujikuta akiwa hospitali.
“Kwa hiyo hukumuona kabisa huyo mtu?” aliuliza ofisa mmoja wa FBI.
“Kwa kweli sijamuona.”
“Kuna nini kilitokea kabla, kuna ugomvi wowote, labda na mtu yeyote
unayemuhisi?” aliuliza ofisa huyo.
“Hapana! Sina ugomvi na mtu yeyote yule, nina urafiki mkubwa na kila mtu, sijui
kama kuna mtu niligombana naye, kilichotokea, inawezekana ikawa wivu tu wa
watu wengine,” alijibu Carter.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli, Carter alikuwa mtu wa watu, alipendwa na kila mtu,
hakuwa mgomvi, watu wengi walimheshimu kwa kuwa hakuwa mbaguzi kama
watu wengine.
Kila kona jina lake lilisikika na ndiyo maana hata taarifa za kifo zake zilipoanza
kusikika kila kona, kila mtu alikuwa na huzuni tele. Aliendelea kubaki hospitalini
hapo, hakuwa mzima kiafya na alitakiwa kusubiri kwa siku tano na ndipo arudi
nyumbani.
Watu waliendelea kumiminika hospitalini hapo, wengine walileta maua, kadi na
vitu vingine huku wakimpa pole kwa kila kitu kilichotokea.Mpenzi wake, kila siku
ilikuwa ni lazima afike hospitalini hapo, alimpenda sana carter na hakuwa tayari
akimuona akipitia katika kipindi kigumu peke yake, alimpenda na kumthamini
zaidi ya mtu yeyote yule.
****
Bwana Seppy alituli chumbani kwake, alionekana kukasirika mno, mchezo
aliofanyiwa na Benjamin ulimfanya kujona hana akili, kuwaona vijana wake
hawakuwa siriazi kwa kazi kubwa aliyokuwa amewapa.
Alichotaka kuona ni Carter anakufa, tena hapohapo hospitalini kwani kama
angeendelea kubaki hai ilimaanisha kuwa kuna siku angekuja kugundulika kwani
huyo Carter angesema kilichotokea na hatimaye kufungwa pingu na kupelekwa
jela.
“Ni lazima auawe hapohapo kitandani,” alijisemea.

59
Tayari aliwaambia vijana wake kwamba kitu hicho kilitakiw akufanywa haraka
iwezekanavyo, ila alitaka kuwasisitizia kwamba kifo cha Carter kilikuwa muhimu
sana kwa wakati huo kuliko kitu chochote kile. Hata alipowapigia simu,
aliwasisitizia kwamba jambo hilo lilitakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo, hata
kama lingehitaji kiasi kikubwa cha fedha, bado lilitakiwa kufanyika.
Vijana hao, watatu wakajiandaa, iliwapasa waingie ndani ya hospitali hiyo na
kujifanya madaktari, wajifanye wanakwenda katika chumba alicholazwa Carter na
hatimaye kumuua, hivyo ndivyo walivyotakiwa kufanya.
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kununua makoti makubwa ya kidaktari,
mashine za kupimia mapigo ya moyo na mafaili ambayo yangewafanya kuonekana
kama madaktari na kuingia ndani ya chumba hicho kirahisi.
Wakafanikiwa kupata vitu vyote na hivyo kufanya kile walichotaka kukifanya.
Kabla ya kwenda hospitalini huko kutekeleza kile walichotaka kukifanya, kwanza
wakampigia simu Bwana Seppy.
“Ndiyo tunakwenda kiongozi, kuna lolote?” aliuliza kijana mmoja, huyu alijiita
Dracula, kijana mwenye roho mbaya, mwanaume mwenye kuua watu kama
alivyoua panzi.
“Kwa sababu huyu Benjamin alijifanya mjanja, sasa inabidi mkimuua muhakikishe
mnaacha alama za vidole vyake, mmenielewa?” alisema na kuuliza.
“Ndiyo mkuu!”
Suala la kupata alama za vidole vya Benjamin wala halikuwa tatizo, walikuwa
nazo katika kinailoni kidogo. Walizichukua alama hizo kipindi kile
walipomkabidhi mpenzi wake kwake, walimpa simu aina ya iPhone 7, alipoishika,
alama za vidole vyake zilibaki katika kioo cha simu.
Hawakukigusa kioo hicho, waliishika simu kwa tahadhali kubwa, walipofika
katika chumba ha wataalamu wao, zile alama zikaanza kutolewa kifundi na
mwisho wa siku kufanikiwa, wakawa nazo na hivyo kuziweka kwenye nailoni,
yaani hapo popote pale ambapo wangefanya kitu chochote, wangeweka kile
kinailoni katika sehemu yoyote, alama za mikono za Benjamin zingeonekana.
“Fanyeni hivyo, ni lazima dunia ijue kwamba yeye ndiye aliyehusika,” alisisitiza
Bwana Seppy.
“Sawa mkuu!”

60
“Na kingine msisahau kuacha fedha, hiyo ni kwa ajili ya kuwachanganya FBI,”
alisema mzee huyo.
“Sawa mkuu!”
Hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa. Kinailoni ambacho kilikuwa na alama za
vidole vya Benjamin (Fingerprints). Walipoanza kuingia ndani ya hospitali hiyo,
wakajigawa, isingekuwa rahisi kufikiri kwamba watu hao hawakuwa madaktari
kwani mavazi yao, muonekano ulionyesha kabisa kwamba walikuwa madaktari.
Waliwekeana muda kwamba ndani ya hospitali hiyo kubwa wangetumia dakika
ishirini na kisha kuonana nje, wangeingia ndani ya gari lao na kisha kuondoka
pasipo kugundulika, wakaelewana.
Muda ulikuwa ni saa moja usiku, muda ambao si watu wengi waliokuwa
hospitalini hapo. Ndugu wa Carter walikuwepo mahali hapo, si ndugu bali hata
polisi nao walikuwepo kuhakikisha ulinzi unafanyika, asiingie mtu yeyote ambaye
si mhusika.
Wakati Dracula anapiga hatuia kuelekea katika chumba kile, hakuonekana kuwa na
wasiwasi wowote ule, hata ndugu zake Carter walipomuona akisogea kule
walipokuwa, hawakuwa na hofu hata kidogo, walijua kwamba naye huyo alikuwa
daktari kwani hospitali kubwa kama hiyo, ilikuwa na madaktari wengi mno.
“Poleni sana jamani...” alisema Dracula hata kabla ya kuingia ndani ya chumba
hicho. Kwa kumwangalia tu, usingejua kama alikuwa muuaji, na kama
ungeambiwa umpe kazi, harakaharaka ungempa uchungaji au upadri, alijiweka
katika sura ya kipole mno.
“Asante sana...”
Hakutaka kubaki hapo nje, kila mtu aliyemwangalia, alikiri kwamba hospitali hiyo
ilikuwa na daktari aliyekuwa na huruma kuliko madaktari wote duniani. Kabla ya
kuingia ndani ya chumba kile, akaonyesha alama ya msalaba kama wanayofanya
Waroma, yaani kwenye paji, kifuani na mabegani.
Alipofanya hivyo tu, watu wote wakajawa na tabasamu pana, mbali na kuwa
daktari, wakagundua kwamba Dracula aliyekuwa na kichuma kilichoandikwa Dr.
Kevin kifuani alikuwa mtumishi wa Mungu, hivyo walikuwa na uhakika kwamba
mambo yangekwenda salama.

61
“Unajisikiaje Carter?” aliuliza Dracula mara baada ya kuingia ndani ya chumba
hicho, Carter alikuwa kitandani akisubiri muda wa kuona wagonjwa ufike ili
ndugu zake waingie.
“Najisikia vizuri kidogo...”
“Sawa! Ngoja nipime mapigo ya moyo,” alisema Dracula na hapohapo akatoa
mashine ya kupimia mapigo ya moyo, stethoscope na kuanza kumpima.
“Mapigo ya moyo yapo vizuri kidogo,” alisema Dracula na kumwambia Carter
ageuke, mgongo uwe juu.
Carter hakubisha, alimwamini Dracula na kuona kwamba alikuwa daktari wa
ukweli hivyo akageuka. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kulifanya, hapohapo
Dracula akaanza kumkaba Carter palepale kitandani.
Carter alijitahidi kuitoa mikono ya Dracula, akashindwa, alijitahidi kupita kelele,
sauti haikutoka kabisa. Alihangaika na kuhangaika lakini hakufanikiwa hata
kidogo.
Dakika moja nzima bado Dracula alimkaba mahali pale vilivyo. Nguvu zikaanza
kumuisha Carter, akachoka na hapohapo pumzi ikaanza kukata, mbele yake akaona
giza, hazikupita sekunde nyingi, akafa hapohapo kitandani.
Dracula hakutaka kuchelewa, akachukua kile kinailoni, akakiweka shingoni mwa
Carter, akakikandamiza vilivyo na alama zile kubaki shingoni mwa Carter,
alipomaliza, hakutaka kubaki, akatoka nje ya chumba kile, akawaambia ndugu
zake Carter kwamba mgonjwa wao aliendelea vizuri hivyo wasubiri, wote
wakamshukuru Mungu, Dracula akaondoka zake huku akiwa amekwishakamilisha
kazi yake.
“It’s done,” (Kazi imefanyika) alimwandikia ujumbe mfupi Bwana Seppy ambapo
alipoisoma, tabasamu pana likajaa usoni mwake.
Kila mtu alikuwa na uhakika kwamba Carter alikuwa amepona na hivyo alitakiwa
kurudi nyumbani. Watu walimkumbuka, kazi zake alizokuwa akizifanya
zilimfurahisha kila mmoja na hivyo kutamani kuona mwanamuziki huyo akirudi
tena nyumbani na kuendelea kuwabuirudisha.
Hakukuwa na mtu aliyejua kwamba kulikuwa na kitu kimetokea ndani ya chumba
alicholazwa Carter, hata madaktari na manesi wa hospitali hiyo hawakuwa wakijua
chochote kile.

62
Baada ya dakika kadhaa tangu Dracula aondoke ndani ya chumba kile na kufanya
mauaji, Dk. Rafael akatokea na kwenda ndani ya chumba kile, kama kawaida
aliwakuta ndugu zake Carter wakiwa nje, nyuso zao tu zilionyesha furaha tele,
mioyo yao ikajazwa na nguvu.
Dk. Rafael akawasalimia na kisha kuingia humo ndani, kwanza jinsi alivyomkuta
Carter kitandani pale, akashikwa na wasiwawasi kwa kuhisi kulikuwa na kitu
kimetokea, akasoegea na kumwangalia vizuri, hakuwa akipumua, macho yalimtoka
na muonekano wake tu ulionyesha kwamba alikuwa amekufa.
Akajaribu kuvipeleka vidole vyake karibu na pua ya Carter, hakuwa akipumua,
hakuridhika, akachukua mashine yake na kusikiliza mapigo ya moyo ya
stethoscope na kuanza kuyasikiliza mapigo ya moyo wa Carter, hayakuwa
yakidunda.
“Mungu wangu!”
Hakutaka kubaki chumbani humo, alichokifanya ni kutoka huku akikimbia, ndugu
waliokuwa nje walipomuona, wakashangaa, hawakujua sababu ya daktari yule
kukimbia hivyo.
Kule alipokwenda, karudi na madaktari wawili ambao wakaingia ndani ya chumba
kile, walichoambiwa ndicho walichokutana nacho ndani, Carter alikuwa kimya
kitandani, wakampima kila kipimo lakini hakushtuka, dalili zote zilionyesha
kwamba alikufa.
“Nani amefanya hivi?” aliuliza Dk. Michael.
Madaktari waliulizana lakini hakukuwa na mtu mwenye jibu, walichanganyikiwa,
hawakujua kama kulikuwa na mtu mwingine alikuwa ameingia ndani ya chumba
kile au la.
Mbali na mwili ule, pembeni kulikuwa na fedha za nchi tofauti, yaani dola ya
nchini Marekani, paundi ya Uingereza, Euro ya Ulaya na Yeni ya China.
Hawakujua kwa nini fedha zile zilikuwa mahali pale.
Walichokifanya ni kutoka nje na kuwauliza ndugu wale ni nani alikuwa ameingia
ndani ya chumba kile, ndugu wale wakasema kwamba kulikuwa na daktari mmoja
aliyekuwa ameingia kabla.
“Yupi?”

63
“Ni daktari mmoja, mrefu, ana shingo ndefu, ana sura ya kipole sana,” alijibu
ndugu mmoja.
Jinsi walivyomzungumzia huyo daktari, hakukuwa na daktari aliyekuwa na sifa
hizo hivyo wakajua kwamba kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa ameingia.
Hawakutaka kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea ndani bali wakawasiliana na
polisi, baada ya dakika kadhaa, polisi wakafika hospitalini hapo.
Kitu cha kwanza kabisa, hawakutaka mwili uguswe kwa ajili ya kutokupoteza
alama za vidole kama zipo, madaktari walilifahamu hilo na tangu walipohisi
kwamba alikuwa ameuawa, hawakuugusa mwili huo.
Walipoona kwamba mwili haujaguswa, hawakutaka kuchelewa, wakaharakaiisha
vipimo vichukuliwe harakaharaka na kama kuna alama za vidole viangaliwe ni vya
nani ili muuaji huyo atafutwe haraka iwezekanavyo.
Kilichowashangaza polisi ni kwamba walikuta fedha kitandani, hawakujua
zilikuwa na maana gani lakini walipokumbuka, hata siku ambayo Carter
alisadikiwa kuwa aliuawa kwa kuchomwa na sindano, pia palepale kitandani
kulikuwa na fedha, hilo likawapa maswali, je kulikuwa na mtu aliyekuwa akifanya
hivyo?
“Hivi mmejiuliza kuhusu hizi fedha?” aliuliza polisi mmoja.
“kivipi?” akauliza mwingine.
“Siku ile taarifa ziliposema kwamba Carter alijidunga sindano, pembeni kulikuwa
na fedha kama hizi, leo ameuawa, pia kuna fedha, hamuhisi kitu chochote hapa?”
aliuliza polisi huyo.
“Mmh!” Polisi wengine wakaishia kuguna tu.
Kama Carter kuuawa, aliuawa, mtu wa kwanza kabisa aliyeshukiwa ni mlinzi
ambaye aliwekwa mahali hapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila kitu
kinakuwa sawa, akachukuliwa na kupelekwa kituoni kwa mahojiano maalumu.
Ndugu zake waliokuwa nje, wakaambiwa kweli kile kilichotokea, kwanza
hawakuamini, inakuwaje ndugu yao auawe na wakati muda wote wao walikuwa
nje ya chumba kile na hakukuwa na adui yeyote aliyeingia zaidi ya madaktari tu?
“Mmoja wa watu walioingia hawakuwa madaktari, alikuwa muuaji,” hilo ndilo
jibu alilolitoa daktari hivyo kuibua vilio mahali hapo.

64
Taarifa zilitolewa kwamba mwanamuziki Carter alikuwa ameuawa ndani ya
chumba cha hospitali, kwanza watu hawakuamini, walihisi kwamba taarifa hizo
zilikuwa ni uongo kwani kipindi cha nyuma, taarifa zilitoka hivyohivyo kwamba
alikuwa amejichoma sindano na kujiovadozi madawa ya kulevya.
Katika kuuchunguza mwili ule wakagundua kwamba muuaji wa mauaji hayo
hakuwa amevaa glavu kitu kilichoifanya alama za vidole vyake kubaki shingoni
mwa mwili wa Carter.
Walichokifanya madaktari ni kuwasiliana na polisi ambao wakafika mahali hapo
na kuchukua alama zile na kurudi nazo ndani ya kituo chao. Huko, kwa msaada wa
mashine walizokuwa nazo, wakaziscan alama zile na kisha kuziingiza katika
kompyuta zao, kilichoendelea ni kuanza kutafuta Marekani nzima juu ya mtu
aliyehusika katika mauaji yale.
Picha zilipita nyinginyingi na tena kwa haraka mno, zilikwenda na kwenda, kama
dakika kumi na tano hivi na ndipo picha moja ikasimama huku neno 100%
MATCH likionekana kuonyesha kwamba picha ya mtu aliekuwa akionekana na
alama alizoziweka wakati akisajiri kitambulisho cha taifa, alama zile alizokuwa
nazo ndizo zilizoonekana katika mwili wa Carter.
“Anaitwa nani huyo?” aliuliza ofisa wa FBI.
“Benjamin Saunders.”
“Yupo wapi?”
“Cambridge, Boston ni mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Harvard,” alijibu ofisa
mmoja.
“Ni lazima twende huko, ni lazima huyu muuaji apatikane. Wasiliana na polisi wa
Cambridge, inawezekana hayupo huko ila ni lazima tuweke mitego, mbali na
hivyo, pelekeni picha zake kila kona, kwenye vituo vya habari na sehemu
nyingine. Gideon, hakikisha mtu huyu anapatikana,” alisema mkuu wa FBI, Bwana
Solomon Kane, hivyo picha zake kuanza kutumwa sehemu tofautitofauti, kila mtu
akajua kwamba Benjamin ndiye aliyemuua Carter.
****
Watu walilia na kuhuzunika, taarifa zilizokuwa zimesambaa kwamba muimbaji
mkali wa miondoko ya Pop, Carter aliuawa ndani ya chumba cha hospitalini
ilimshtua kila mtu.

65
Wengi walijiuliza maswali kwamba ilikuwaje muuaji kuingia ndani ya chumba
hicho na kumuua Carter huku kukiwa na ulinzi ulioimarishwa ndani ya hospitali
hiyo? Kila mtu aliyejiuliza, alikosa jibu ila ripoti ambayo ilitoka hospitali ilisema
kwamba muuaji aliingia ndani ya chumba hicho baada ya kujifanya daktari.
Maofisa wa FBI walichokitaka ni kuangalia kwenye kamera za CCTV ambazo
walizifunga humo ndani, walitaka kumuona mtu aliyeingia alikuwa nani.
Wakaenda katika chumba kilichokuwa na televisheni na kuhitaji kuona hizo video
ambazo zilipigwa, wakawekewa, walifanikiwa kumuona muuaji, sura yake ilikuwa
ngeni na haikuonekana vizuri kutokana na udogo wa upigaji picha wa kamera hizo
hivyo kila mtu akaamini kwamba yeye ndiye huyo Benjamin, kwani walifanana
ngozi, wote walikuwa weusi.
Picha za Benjamin zikaanza kuwekwa mitaani, kila mtu aliyemuona, hakuamini,
alikuwa kijana mzuri, mdogo lakini kitu kilichowashangaza watu kwa nini alifanya
mauaji, tena kwa mtu waliyekuwa wakimpenda mno?
Benjamin alitakiwa kutafutwa kila kona, hakutakiwa kuachwa kwani yeye ndiye
aliyefanya mauaji kwa mtu aliyekuwa kipenzi cha watu. Mitaani, picha zake
zikasambazwa, si kwenye vituo vikubwa vya kwenye mabasi bali hata kwenye
vituo vya treni, kote huko picha za sura yake zikabandikwa.
FBI walitaka kuionyeshea dunia kwamba walikuwa siriazi katika kila
wakifanyacho, hivyo wakatengeneza ‘apprication’ maalumu na kuziweka katika
simu zote za Android na iPhone, apprication hiyo ilikuwa ni kuwahamasisha watu
kumtafuta huyo Benjamin ambaye kwa kipindi hicho alipata umaarufu mkubwa
hata zaidi ya rais.
Baada ya wiki, hatimaye watu wakakusanyika nyumbani kwa Carter, kila mmoja
alikuwa akilia, walihuzunika lakini hakukuwa na kitu kilichomrudisha hai
mwanamuziki huyo, ukweli ulibaki palepale kwamba aliuawa na asingeweza
kurudi tena.
Mpenzi wake na ndugu zake, kila mmoja alionekana kuwa na huzuni mno, kama
kulia mpaka kuzimia, hiyo ilitokea mara nyingi sana lakini bado ukweli wa kifo
chake ukaendelea kubaki palepale.
Siku mbili baadaye, ndugu, marafiki na watu wengine wachache wakakusanyika
katika makaburi ya First Calvary Cementary yaliyokuwa katika mji wa Brooklyn
jijini New York nchini Marekani. Hapo, mchungaji aliyeandaliwa kwa ajili ya
ibada ndogo akaanza kutoa maneno ya mwisho na hatimaye mwili wa Carter

66
kuzikwa, huo ukawa mwisho, yule mwanamuziki mdogo, mwenye umaarufu
mkubwa akawa amezikwa huku akiwa na ndoto nyingi kichwani mwake.
Siku iliyofuata, magazeti yote nchini Marekani na nchi nyingine zilitoa taarifa juu
ya kifo cha mwanamuziki huyo, watu hawakuwa wakiamini, walihisi kwamba
angeweza kurudi tena kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
Tasnia ya muziki Marekani ikapata pengo, hakukuwa na msanii ambaye alikuwa
na jina kubwa ambaye aliupaisha muziki wa Pop kama alivyofanya Carter, leo hii,
Carter huyohuyo akaondoka na muziki wake, tuzo zake alizochukua katika
mashindano mengi zikabaki kama mapambo ndani ya nyumba yake.
“Huyu Benjamin ni lazima apatikane, kuna taarifa yoyote?” aliuliza Bwana Kane.
“Bado ila taarifa zinasema kama alionekana chuoni, bado tunaendelea kufuatilia
mkuu!” alisema ofisa mmoja wa FBI.
Ilikuwa ni lazima Benjamin aondoke kuelekea Boston kuendelea na masomo yake,
hakutaka kubaki New York kwa kuamini kwamba watu wale waliokuwa
wamemteka wangeweza kumrudia tena.
Mara ya kwanza alimwambia mpenzi wake, Vivian waondoke na kuelekea Los
Angeles lakini huko hakukuonekana kuwa na usalama wa maisha yao, hivyo
ilikuwa ni lazima arudi Boston ambapo angechukua apartment sehemu fulani na
kisha kuendelea na maisha yake na si kukaa chuo kama alivyokuwa akifanya.
Kutoka New York mpaka Boston ilikuwa ni mwendo wa saa tano kwa treni ya
umeme, hiyo ilimaanisha kwamba kama wanaondoka muda huo ambao ulikuwa ni
saa tatu asubuhi basi wangeweza kufika Boston majira ya saa saba.
Wakaingia ndani ya treni, macho yao hayakutulia, kila wakati walikuwa
wakiangalia huku na kule. Waliogopa, hawakutaka kumuamini mtu yeyote kwa
kipindi hicho, kila aliyeonekana mbele yao, walimuona kama muuaji ambaye
walikuwa na uhakika kwamba wangetafutwa sana mara baada ya kugundua
kwamba Benjamin hakuwa amefanya kile alichokuwa ameambiwa akifanye.
Baada ya saa nne, wakaingia Boston, ilionekana kuwa furaha kwao, kidogo kwa
Benjamin akaonekana kujiamini kwa kuhisi kwamba asingeweza kuonekana kwani
wauaji hao wasingediriki kusafiri kutokana New York mpaka Boston kumtafuta
yeye tu.

67
Baada ya siku mbili, masomo yakaanza kama kawaida, hakumwambia Vivian
arudi jijini Los Angeles kwa kuhisi kwamba kama angekuwa mbali naye basi binti
huyo angeweza kuuawa, alichomwambia ni kwamba aishi naye hapo Boston huku
akifanya mipango ya kumtoa hapo na kumpeleka Atalanta walipokuwa wazazi
wake.
“Hautakiwi kuwa na hofu yoyote ile, wewe kaa hapa, baada ya miezi kadhaa,
itakubidi uende Atalanta, huko, nitakupangia apartment,” alisema Benjamin hivyo
kukubaliana na Vivian.
Siku tatu baada ya kufika Boston, wakiwa chumbani wamekaa ndipo wakapigwa
na mshtuko mara baada ya kuona taarifa ya habari katika Kituo cha CNN ikisema
kwamba mwanamuziki aliyekuwa na jina kubwa, Carter alikuwa ameuawa ndani
ya chumba alichokuwa amelazwa.
Wakashtuka, hawakuamini walichokuwa wakikiangalia, Benjamin akatulia na
kuiangalia taarifa ya habari ile kwa umakini, aliangalia picha, kweli alikuwa Carter
na taarifa za awali zilisema kwamba aliuawa baada ya kukabwa kitandani tena
huku pembeni kukikutwa fedha za za mataifa mbalimbali.
“Wamemuua Carter,” alisema Benjamin huku akionekana kushtuka.
“Mungu wangu!” alisema Vivian huku akionekana kuumia moyoni mwake.
Benjamin akachukua simu yake na kuanza kumpigia rafiki yake David,
akamuelekeza kila kitu alichokifanya hivyo kutaka afanye kila liwezekanalo
kuhakikisha ile namba aliyokuwa amempa ilikuwa ikipatikana wapi.
“Ila Vivian si umempata?” aliuliza David.
“Ndiyo! Ila nataka nijue ni nani anahusika katika mauaji haya, David, tafadhali
naomba unisaidie,” alisema Benjamin.
“Usijali, nipe muda,” alisema David na kisha kukata simu.
Hiyo ilikuwa ni taarifa ya majonzi waliyokuwa wameipata, hawakuamini kama
kweli watu hao baada ya kugundua kwamba Carter hakuwa ameuawa basi
wangemtafuta mpaka wampate na kumuua, hakujua tatizo lilikuwa nini ila kitu
alichohisi ni kwamba kulikuwa na siri kubwa sana nyuma ya pazia.
Baada ya kukaa kwa huzuni usiku huyo, asubuhi ikaja taarifa nyingine, hii ilikuwa
ni juu ya muuaji aliyekuwa amemuua Carter. Benjamin na Vivian wakabaki
wakiangalia, hawakuamini walichokuwa wakikiona kwamba Benjamin ndiye

68
aliyemuua Carter tena huku alama za vidole vyake zikiwa zimeonekana katika
shingo ya Carter, picha zake zilionyeshwa kwenye kila televisheni, alipoziona,
hakuamini, akapiga magoti na kuanza kulia.
“Sikuua, sikuua,” alisema Benjamin, alikuwa akimwambia mpenzi wake huku
akilia kwa uchungu.
“Ngo ngo ngo...” mlango ulisikika ukigongwa, kila mtu akaogopa kwa kuhisi
kwamba aliyekuwa akigoga mlango alikuwa polisi.
****
Maofisa wa FBI wakafika katika Chuo cha Harvard kilichokuwa Cambridge jijini
Boston kwa ajili ya kumkamata Benjamin ambaye alihusika katika mauaji ya
Carter. Walivalia suti nyeusi, miwani myeusi, kwa kuwaangalia tu ilikuwa rahisi
kugundua kwamba watu hao walikuwa maofisa wa FBI kwani hata masikioni
mwao walikuwa na vispika ambavyo viliunganishwa moja kwa moja mpaka
kwenye maiki zilizokuwa mdomoni.
Wakaelekea mpaka katika ofisi ya mkuu wa chuo ambapo baada ya kufika huko,
wakamwambia kitu walichokifuata kwa kuamini kwamba taarifa kuhusu muuaji,
Benjamin zilikuwa zikijulikana kila kona.
“Alikuwa hapa...” alijibu mkuu wa chuo.
“Bado yupo au?”
“Hapana! Aliondoka!”
“Kwenda wapi?”
“Anapoishi! Hakuna anapopajua kwani tangu arudi kila kitu amekuwa akikifanya
kwa siri sana, hayupo kama zamani, nahisi kuna kitu kinaendelea,” alisema mkuu
wa chuo.
“Una namba yake ya simu?”
“Ndiyo! Niliichukua kwa ajili ya kuzungumza naye juu ya kilichokuwa
kikiendelea kwani alibadilika, alionekana kuwa na mawazo kitu ambacho hakuwa
nacho kabla, ila bahati mbaya sikuweza kuwasiliana naye,” alisema mkuu wa chuo
na hivyo kuwapa namba yake ya simu.
Hawakutaka kuendelea kubaki hapo ndani, walichokifanya ni kuondoka na
kuelekea ndani ya gari lao. Ilikuwa ni lazima waitraki simu yake, wajue mahali

69
alipokuwa hivyo kuchukua laptop yao na kuiunganisha na simu zao kisha kuanza
kumpigia.
Kitendo cha simu kuita tu, ilionekana kuwa kosa kwani tayari kompyuta yao
ikaanza kusoma, ikaanza kuwapa maelekezo juu ya mahali alipokuwa Benjamin
kwa kipindi hicho. Waliangalia vizuri, hakuwa mbali na mahali hapo alipokuwa,
hivyo wakaanza safari ya kuelekea huko, GPS ilionyesha kwamba alikuwa katika
chumba kimoja kilichokuwa katika apatimenti za St. Monica ambazo hazikuwa
mbali kutoka hapo chuoni.
“Tumfuateni,” alisema ofisa mmoja, wakaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea
huko.
****
Kila mmoja ndani ya chumba kile alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa, kitendo
cha kugongwa hodi ndani ya chumba kile kila mmoja akahisi kwamba walikuwa ni
polisi.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Benjamin ni kuanza kutafuta sehemu ya
kujificha, hakutaka kuchelewa, ilikuwa ni lazima afanye haraka kwani pasipo
kufanya hivyo ilikuwa ni lazima kukamatwa.
Akachukua simu yake iliyokuwa mezani, akaona kulikuwa na mtu aliyekuwa
akimpigia, namba ilikuwa ngeni, hakujali, alichokifanya ni kuanza kuangalia
sehemu nzuri ya kujificha, hata kama ingekuwa kuruka dirisha na kutokea upande
wa pili, ilikuwa sawa ingawa chumba hicho kilikuwa katika ghorofa ya tatu.
“Who is it?” (Nani?) aliuliza Vivian.
“Me!” (Mimi!)
“You got no name buddy?” (Huna jina mshikaji?)
“Marie...”
“Who is Marie?” (Marie ndiye nani?)
Maswali yote hayo alikuwa akiuliza Vivian, mtu huyo bado aliendelea kupiga hodi
ili mlango ufunguliwe. Hakukuwa na aliyekuwa radhi kuufungua mlango huo, kitu
ambacho kilikuja moja kwa moja vichwani mwao ni kutoroka ndani ya chumba
hicho, hivyo wakafanya hivyo.

70
Wakaufungua mlango wa nyuma ambapo kulikuwa na sehemu kubwa ya
kupumzikia, walichokifanya ni kuanza kutembea pembezoni mwa ghorofa hilo
kwa kwenda upande wa chumba kingine ambapo pembeni yake kulikuwa na
bomba refu la choo lililoelekea mpaka chini.
“Ni lazima tuteremke kwa kutumia bomba lile,” Benjamin alimwambia Vivian.
“Nitaweza?”
“Utaweza tu, hatuna jinsi, mtu anayegonga mlango hatumfahamu, inawezekana
akawa mmoja wa wale wauaji,” alisema Benjamin, tayari walilifikia bomba lile na
hatimaye kuanza kuteremka nalo chini.
Ilikuwa ni lazima kuondoka mahali hapo, hawakutakiwa kumuamini mtuu yeyote
yule. Hawakuwa wakiiogopa serikali ila watu waliokuwa wakiwaogopa zaidi
walikuwa hao wauaji na ilikuwa ni lazima kuwakimbia.
Walipotua chini tu, hawakutaka kukimbia kwani kwa mbali waliliona gari moja
likiingia mahali hapo hivyo kujificha. Gari liliposimama, wanaume wawili
waliovalia suti nyeusi wakateremka.
Benjamin aliwajua, mavazi mengi hayo huvaliwa na maofisa wa FBI, hivyo
akamwambia Vivian wajifiche zaidi kwani watu waliokuwa wamefika hawakuwa
watu salama kwao, walikuwa FBI.
Walibaki wakiwaangalia mpaka walipokwenda ndani, walijuaje kama walikuwa
humo na wakati hawakuwa wamemwambia mwanachuo yeyote yule? Wakajua
kwamba watu hao walitraki simu yake, hivyo alitakiwa kuiacha hapohapo.
Huo ndiyo ulikuwa umamuzi waliochukua, hawakutaka kwenda na simu ile
sehemu yoyote kwa kuona kama wangekamatwa, hivyo Benjamin akaiacha
hapohapo walipokuwa wamejificha huku akifuta meseji zote, simu zilizotoka na
kuingia, akazikariri namba zile za wauaji na kisha kuondoka huku akiwa na laini.
Bwana Seppy alizidi kuchanganyikiwa, hakuamini kama kweli vijana wake
walishindwa kabisa kumpata Benjamin japokuwa walikuwa wametega mitego
mbalimbali kumnasa.
Alichanganyikiwa kwa sababu kumuacha mtu huyo akiwa hai lilikuwa kosa
kubwa, inawezekana likawa kubwa kuliko makosa yote aliyowahi kuyafanya tangu
azaliwe.

71
Aliwaagiza vijana wake waendelee kumtafuta Benjamin lakini kila siku majibu
yalikuwa yaleyale kwamba hakupatikana, ilikuwaje wasimpate na wakati walijua
hakuwa mjanja, atakuwa amejificha wapi kwani nchi nzima ilikuwa ikimtafuta
yeye.
“Hakikisheni mnampta kabla ya FBI kumpata,” aliagiza Bwana Seppy.
“Sawa mkuu!” alisikika Dracula.
Bado kazi ilikuwa kubwa, Marekani ilikuwa kubwa sana na hawakujua ni mahali
gani walitakiwa kwenda. Kwa sababu fedha ilikuwepo, walichokifanya ni kuwapa
kazi vijana wengi wamtafute Benjamin na kumpata kisha wangepewa malipo
makubwa ya fedha, vijana hao kutoka sehemu mbalimbali wakaingia kazini na
kuanza kumtafuta.
Zoezi hilo lilidumu kwa kipindi cha wiki nzima, hakuwa amepatikana wala kusikia
tetesi kwamba likuwa sehemu fulani, hiyo iliwachanganya sana na hivyo Bwana
Seppy kuamua kujiongeza kwamba kulikuwa na kitu kilitakiwa kufanyika.
“Naamini kwamba kuna watu wanawasiliana na Benjamin,” alimwambia Dracula
aliyekuwa na vijana wenzake.
“Kivipi? Kwenye simu hapatikani kabisa!”
“Najua ila naamini kuna sehemu yupo, anawasiliana na ndugu zake bila hofu! Sasa
naagiza kwamba ninamhitaji kijana yeyote anayejua sana kimpyuta aletwe mbele
yangu, kuna kazi nataka kufanya naye,” alisema Bwana Seppy, hayo yalikuwa
maagizo hiyo yalitakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo.
Baada ya saa tatu Dracula akarudi mahali hapo huku akiwa na kijana mmoja
mtanashati, alivaa kwa kuchomekea shati lake, uso wake ulikuwa na miwani, kwa
kumwangalia tu ungegundua kwamba kijana huyo alikuwa na uwezo mkubwa sana
kichwani mwake.
“Huyu ni Cosmas, mmoja wa vijana wenye ujuzi sana katika masuala ya
kompyuta,” alisema Dracula.
“Sawa! Mlete ndani!”
Muda wote Cosmas alionekana kuwa na hofu moyoni mwake, hakuamini kama
sehemu aliyokuwepo mahali hapo ilikuwa salama kwa maisha yake au la.
Alimwangalia Dracula, alimfahamu kupitia kaka yake na ndiye alikuwa mtu pekee

72
ambaye kila wakati alimtoa hofu kwa kumwambia kuwa sehemu hiyo ilikuwa
salama kwake kwa asilimia mia moja.
“Una uwezo gani wa kutumia kompyuta?” aliuliza Bwana Seppy huku
akimwangalia Cosmas kwa macho yaliyoonyesha kutaka kupewa jibu lae haraka
iwezekanavyo.
“Nina ujuzi mkubwa sana, wewe niambie unataka nini na mimi nitakufanyia,”
alisema Cosmas huku akionekana kuwa makini na majibu yake.
“Kuna mtu ninataka kufahamu anawasiliana na nani katika simu yake,” alisema
Bwana Seppy.
“Nani?”
“Anaitwa Benjamin Saundres!”
“Huyu anayetafutwa?”
“Ndiyo!”
“Mungu wangu! Yupo wapi?” aliuliza Cosmas huku akionekana kushtuka.
“Hatujui! Ndiyo tunataka wewe utuambie yupo wapi,” alisema Bwana Seppy.
“Nitajuaje?”
“Tuna namba yake ya simu, tunataka tujue mawasiliano yote aliyowahi kufanya
kwa njia ya simu,” alisema Bwana Seppy.
“Hakuna tatizo!”
Alichokifanya Cosmas ni kuchukua begi lake na kisha kutoa laptop yake na
kuiwasha. Kitu alichokihitaji kilikuwa ni namba ya mtu aliyekuwa akihitajika,
akapewa na kisha kuiingiza katika kimpyuta yake.
Kitu pekee alichokuwa akicheza nacho kilikuwa ni codes mbalimbali za kompyuta,
alikuwa akiingia katika system mbalimbali na kuanza kucheza na codes hizo.
Haikuwa kazi nyepesi, ilikuwa ngumu lakini mwisho wa siku akakamata namba
zote ambazo zilikuwa zimeingia katika simu ya Benjamin kwa mara ya mwisho
ambayo kwa tarehe iliyoonyesha, ilikuwa kama wiki moja iliyopita.
“Namba ambayo mara kwa mara imekuwa ikiwasiliana naye ni hii hapa,” alisema
Cosmas huku akiwapa namba hiyo.
“Ni ya nani?”

73
“Mnataka niangalie?”
“Ndiyo!”
“Sawa.!”
Hilo nalo halikuwa tatizo hata kidogo, kwa Cosmas hiyo ilionekana kuwa kazi
ndogo mno hivyo alichokifanya ni kuanza kuangalia usajiri wa namba ile ambayo
mwisho wa siku ikamuonyesha kwamba ilikuwa ni ya mtu aliyejulikana kwa jina
la David Belshaaz.
“Anaishi wapi?”
“Washington DC!”
“Sehemu gani?”
“Livingstone. System inaniambia yupo katika nyumba moja namba 2789W
ambayo pia imepakana na hoteli kubwa ya Salander Hill!” alijibu Cosmas.
“Ni lazima huyo mtu apatikane, bila shaka atakuwa anafahamu mahali Benjamin
alipo. Watume vijana waliopo Washington waende, tena hakikisha na wewe
unachukua ndege na kwenda huko! Huyu David naye ni mtu muhimu, hakikisha
anakamatwa, anateswa na kutambia Benjamin yupo wapi,” alisema Bwana Seppy.
“Sawa mkuu!” aliitikia Dracula, hapohapo akachukua simu na kuanza kuwapigia
vijana wake waliopo Washington pia kumpigia simu rubani na kumwambia aandae
ndege kwani kulikuwa na safari ya dharura ya kwenda Washington DC.
****
“Nimekuja kutoa taarifa...”
“Taarifa ya nini?”
“Ya huyu Benjamin Saunders...”
“Unajua alipo?”
“Hapana! Ila kama mkimpata mtu fulani, kazi ya kumpata itakuwa rahisi sana...”
“Nani?”
“Rafiki yake anaitwa David Belshaaz, yupo Washington Dc.”
“Una uhakika?”

74
“Asilimia mia moja, alikuwa akiwasiliana naye sana!”
“Wewe umejuaje?”
“Kwani nyie mnahisi nimejuaje? Kwanza niambieni, hela zipo?”
“Hizo zipo, ila mpaka ufanikishe kukamatwa kwake!”
“Hakuna tatizo! Fedha kwanza...”
“Fedha kabla ya mzigo?”
“Mzigo kabla ya fedha?”
“Sisi ni serikali, wewe tuamini! Tuambie tunaweza kumpata vipi!”
“Sawa! Ila mkichelewa, hamtompata huyu David kwani kuna mtu pia anamuhitaji
kwa nguvu zote...”
“Nani?”
“Nyie fanyeni haraka! Ngoja niwape maelekezo,” alisema kijana mmoja.
Huyo alikuwa Cosmas ambaye aliamua kwenda polisi na kutoa taarifa katika
kitengo cha FBI na kuwaambia kila kitu kuhusu kupatikana kwa rafiki wa
Benjamin, David ambaye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwasiliana na Benjamin,
bila shaka alikuwa akijua mtu huyo alikuwa mahali gani.
Alipowapa maelezo waliyokuwa wakiyahitaji, wakawapigia simu maofisa wa
kitengo hicho waliokuwa Washington kwa ajili ya kwenda walipoelekezwa kwa
ajili ya kumpata David, sehemu hiyohiyo ndipo nao vijana wa Bwana Seppy
walikuwa wakienda kwa ajili ya mtu huyohuyo.
****
David alikuwa ametulia chumbani kwake, alikuwa mbele ya kompyuta yake huku
akihangaika kufanya kazi aliyopewa na Benjamin, ilikuwa kazi kubwa lakini
ilikuwa ni lazima ahakikishe anampatia majibu juu ya mahali mpigaji wa namba
aliyompa alipokuwa akiishi.
Hakuwa akiwasiliana naye kupitia namba yake, alimwambia mapema kwamba
angeitupa simu na hata kuwasiliana naye asingewasiliana kwa kupitia namba yake
bali angeitumia namba ya mpenzi wake, Vivian, hivyo ndivyo alivyofanya.
Hiyo ilikuwa siku ya saba, bado alikuwa na kazi moja ambayo ilikuwa ngumu na
hakujua ni kwa wakati gani angeweza kuikamilisha. Kilichokuwa kikimshinda,

75
hakuweza kuipata namba hiyo ikiwa hewani, ilikuwa imezimwa jambo ambalo
lilimpa ugumu mkubwa mno.
Wakati akiendelea na kazi hiyo, ghafla akasikia kama vishindo vya mtu kwa nje,
akashtuka, haikuwa kawaida kwani nyuma aliyokuwa akikaa, kwa muda kama
huo, saa saba usiku ilikuwa vigumu sana kuwa na mtu mwingine nje.
Haraka sana akaifunika laptop yake, akazima taa na kisha kuelekea chumbani
kwake ambapo kwa juu kulikuwa na tundu, akalifungua na kuingia humo.
Hicho kilikuwa chumba kingine cha kujificha, huku hakukuwa kama dali la
nyumba za Afrika, kulionekana kama chumba kingine ambapo kulikuwa na
kitanda na vitu vingine, akatulia huku akisikilizia kuona ni kitu gani kingetokea
huko chini alipokimbia.
“Hebu subiri!” alijisemea, harakaharaka akawaisha kompyuta yake ya huko
ambapo aliiunganisha na kamera ndogo za CCTV ambazo aliziweka kwenye kona
kadhaa ndani ya nyumba hiyo.
Akaanza kuona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, wanaume watatu waliovalia
nguo nyeusi tupu walisimama katika mlango wa kuingilia ndani, walikuwa
wakijadiliana ni kwa namna gani wangeweza kuingia ndani.
Hakujua watu hao walikuwa wakina nani na walikuja hapo kufanya nini, aliogopa,
alibaki akitetemeka kule juu kwani kwa jinsi alivyowaona, watu hao
hawakuonekana, hawakuonekana kuwa watu wazuri hata mara moja kwani
mikononi mwao walikuwa na bastola.
“Ni wakina nani?” alijiuliza lakini hakupata jibu.
Watu hao wakafungua mlango na kuingia ndani, kule alipokuwa, David alikuwa
akitetemeka lakini alikuwa na wasiwasi wa kukamatwa na watu hao, kuwa huko
dalini hakukusaidia, alichokifanya ni kujificha chini ya kitanda kilichokuwa
hukohuko huku kompyuta ile akiielekezea kule alipokuwa kwa ajili ya kufuatilia
kilichokuwa kikiendelea.
“Yupo wapi?" aliuliza jamaa.
“Hebu tutafuteni,” alisema jamaa mwingine na hivyo kuanza kumtafuta.
Waliangalia kila kona, hakukuwa na mtu yeyote, walikuwa na maswali mengi
kwamba David alikuwa wapi kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana ndani ya nyumba
ile, alikuwa sehemu fulani ambayo hawakuifahamu ilikuwa sehemu gani.

76
Walimtafuta kwa zaidi ya dakika tano lakini hawakuweza kumuona kabisa. Wakati
wakiendelea kuchunguza huku na kule, ndipo mmojawao akasema kwamba
inawapasa kuangalia juu ya dali kwani kulikuwa na nyumba nyingi hapo Marekani
ambapo juu kulikuwa na sehemu nyingine ya kukaa.
“Tuangalieni juu kule, nahisi anaweza kuwa huko,” alisema mwanaume mmoja.
“Una uhakika?”
“Tunatakiwa kujaribu, tutafuteni mlango wa kuingilia juu,” alisema mwanaume
huyo.
Hakukuwa na cha kusubiri, ushauri huo uliotolewa ulitakiwa kufanyiwa kazi
haraka iwezekanavyo hivyo kuutafuta mlango wa kuingilia huko. Wala
hawakupata kazi kubwa, wakaupata na kisha kuufungua.
Kama walivyohisi na kama ilivyokuwa kwa nyumba nyingine, hata huko juu
kulikuwa na chumba kingine kikubwa, mmojawapo akapanda na kuingia huko
kisha kuanza kumtafuta david.
“Najua upo humu! Najua upo humu, jitokeze mwenyewe,” alisema mwanaume
huyo, alikuwa huko huku bastola ikiwa mikononi mwake.
“Hutaki kutoka?” aliuliza huku akiikoki bastola ile.
Kule uvunguni alipojificha David alikuwa na presha kubwa, mapigo ya moyo
yalikuwa yakimdunda mno, kitendo cha kusikia bastola ile ikikokiwa, tayari jasho
lilimtiririka kwa kuhisi kwamba mwanaume huyo angeanza kupiga risasi ovyo.
Hakutaka kusubiri huko, ili kujiokoa, harakaharaka akajitoa huku akimuomba
asimpige risasi.Hicho ndicho alichokuwa akikitaka, hapohapo akamchukua na
kumwambia ashule chini, David akafanya hivyo haraka sana, huko chini,
akapokewa na wale wanaume wawili.
“Safi sana....hebu piga magoti hapo,” alisema mwanaume mmoja, David hakutaka
kubisha, akapiga magoti huku machozi yakianza kumtiririka mashavuni kwani
hakujua kama angeweza kupona mahali hapo.
“Unaweza kutuambia mahali alipokuwa Benjamin?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Benjamin yupi?” aliuliza David.
“Humfahamu?”

77
“Ndiyo! Sina rafiki anayeitwa Benjamin!”
“Acha utani kijana, hebu tuangalie vizuri, unatuonaje? Tuna utani au?” aliuliza
mwanaume mmoja.
“Kweli tena, simfahamu!” alisema Benjamin.
Watu hao waliona kama wanataniwa, walimwangalia vizuri David, majibu yake na
uso wake ulionekana kuwa tofauti na kile alichokisema. Kitu cha kwanza kabla ya
kuuliza zaidi ilikuwa ni kumpiga kofi zito shavuni mwake, David akaanguka chini.
“Tuambie ukweli!”
“Huo ndiyo ukweli!”
“Upi?”
“Kwamba simfahamu m...” alisema lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake,
akashtukia akipigwa tena.
“Umekataa?”
“Kweli simjui!”
“Basi sawa...” alisema mwanaume huyo na kisha kuikoki bunduki yake.
Kitendo cha bunduki ile kukokiwa, tayari David alijua ni kitu gani kilitakiwa
kufuata mahali hapo, alibaki akitetemeka kwani hakujua kabisa kama watu hao
wangeweza kuchukua uamuzi wa harakaharaka wa kummaliza hapohapo
nyumbani kwake.
Akaomba sana msamaha lakini hakukuwa na aliyemjali, ili wasimuue, basi ilikuwa
ni lazima aseme mahali Benjamin alipokuwa, vinginevyo, roho yake ilikuwa
mikononi mwao.
“Muue haraka tuondoke zetu, hatuna muda wa kupoteza,” alisema mwanaume
mwingine ambaye tangu aingie ndani ya nyumba hiyo hakuwa amezungumza
lolote lile.
“Hakuna noma...” aliitikia huyo mwenzake, hapohapo akamnyooshea bunduki
David tayari kwa kumuua mahali hapo.
Filamu nyingi ziliigizwa kila mwaka, watu walifuatilia filamu hizo katika kumbi
mbalimbali, kila mtu alizipenda, kuna wengine, kabla ya kuagiza filamu hizo

78
katika makampuni husika, kazi yao ilikuwa ni kwenda kwenye majumba ya
kuangalia na kuziangalia filamu hizo.
Achana na za mapenzi, kulikuwa za mapigano ambazo kwa kipindi hicho ndizo
ziliteka hisia za watu wengi, kulikuwa na waigizaji wengi, wenye uwezo ambao
waliigiza filamu za mapigano na kupendwa sana lakini filamu ya Knock Out 3D
iliyoigizwa na muigizaji chipukizi, Todd Lewis ndiyo ilionekana kuwa kali zaidi
ya filamu za mapigano zilizotangulia.
Todd Lewis alikuwa kijana mdogo lakini kutokana na matangazo ya filamu hiyo
(Trailers), watu wengi nchini Marekani walitaka kuiona, mapigano aliyokuwa
akiyatumia ndani ya filamu hiyo yalimchengua kila mtu ambaye alitazama
matangazo ya filamu hiyo.
Siku ambayo ilipangwa kuzinduliwa kwa filamu hiyo watu waliona ikiwa mbali,
waliiona ikichelewa kufika hivyo kutaka ifike haraka ili waingie na kisha
kuiangalia.
Si Marekani tu waliobabaika na matangazo ya filamu hiyo bali hata katika nchi
nyingine, kote huko waliisubiria filamu hiyo kwa hamu kubwa, tiketi zaidi ya
milioni kumi, sehemu zote duniani ziliuzwa na kuisha na bado watu walihitaji zaidi
kwani matangazo ya filamu hiyo katika sehemu mbalimbali zilionyesha kabisa
kwamba hiyo haikuwa filamu ya kukosa kuiyazama.
Siku zilikatika na hatimaye siku hiyo kuwaidia, watu walijazana katika Ukumbi wa
Stapple Center, Los Angeles nchini Marekani tayari kwa kuishuhudia filamu hiyo
ambayo ilisubiriwa kwa kipindi kirefu na ndiyo filamu ya kwanza kuuza tiketi
nyingi katika siku ya kwanza ya uzinduzi wake.
Filamu ilipoanza kuonyeshwa katika mfumo wa 3D, kila mtu alisisimka, miwani
ilikuwa nyusoni mwao huku wakiangalia namna Todd alivyoigiza kwa umahiri
mkubwa.
Mpaka filamu hiyo inamalizika, kila mtu aliridhika, hawakuamini kama
kungekuwa na muigizaji chipukizi ambaye angeweza kuigiza kwa ustadi mkubwa
kama ilivyokuwa kwa Todd.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mafanikio yake, alikuwa na miaka kumi na saba tu
lakini alitabiriwa kuwa muigizaji mkubwa hapo baadaye. Kila sehemu alipopita
watu walimuita, walimpa vitabu vyao kwa ajili ya kuvisaini, alipendwa na kila
mtu, yaani kila alipokuwa, alinukia fedha.

79
Siku zikaendelea kukatika, huo ulikuwa mwanzo wa mafanikio yake mengi,
akaigiza filamu ya pili na ya tatu, ya nne na ya tano, mpaka anafikisha umri wa
miaka ishirini, alikuwa na jina kubwa, alitengeneza sana fedha na watu wengi
walitamani kuwa kama yeye.
“Inakuwaje?” aliulizwa na mwandishi wa habari, tena alikuwa amekaa ndani ya
gari lake.
“Safi...”
“Mimi ni mwandishi wa habari...”
“Najua, unaitwa Ester kutoka Independent...” alisema Todd huku akitabasamu.
“Ndiyo! Nimesikia umenunua gari jipya, ni kweli?”
“Umesikia wapi?”
“Ni taarifa tu kutoka sehemu mbalimbali, kuna ukweli?” aliuliza Ester.
“Ndiyo! Ila umezipata wapi?”
“Hii ndiyo kazi yangu Todd...” alisema msichana huyo.
Baada ya kupata mafanikio makubwa, alichokifanya Todd ni kununua jumba la
kifahari lililokuwa Los Angeles hapohapo nchini Marekani, lilikuwa jumba la
kifahari lililomgharimu dola milioni nne, zaidi ya bilioni nane za Kitanzania.
Hakuishi hapo, alichokifanya ni kununua gari la kifahari aina ya Ferrari Testarossa
kutoka nchini Italia. Gari hilo alilinunua baada ya kutoa oda kwani katika kipindi
hicho magari hayo yalikuwa nane tu, yeye akawa miongoni mwa watu waliokuwa
wakimiliki gari hilo.
Kuwa na gari hilo, tayari aliandikwa kila kona, hakukuwa na siri tena, alikuwa staa
hivyo kila kitu alichokifanya, watu walikifahamu. Todd hakuwa mtu wa starehe,
hakuwa mtu wa kwenda klabu au kutumia pombe yoyote ile, pamoja na ustaa wake
huo, alikuwa mtu wa kusali sana, alikwenda kanisani kila Jumapili kitu
kilichowashangaza watu wengi.
Wanawake walimpapatikia, hakuwa na nafasi nao, aliwajua, aliwakumbuka watu
wengi ambao walipoteza fedha zao, umaarufu wao mara baada ya kuweka ukaribu
wanawake, hakutaka kitu hicho kitokee kwake na ndiyo maana kila siku alijitahidi
kuwaepuka.

80
Baada ya siku kadhaa, yeye na Kampuni ya Filamu ya Marvel wakaondoka na
kuelekea nchini Ukraine kwa ajili ya kuingiza vipande vya filamu iliyotarajiwa
kutoka baada ya miezi sita, filamu kali iitwayo Around ambayo ilisemekana kuwa
filamu kali kuliko zile zilizopita.
Watu walitulia majumbani mwao, walitaka kufahamu filamu hiyo ilikuwaje na
ilifananaje kwani waliiamini kampuni ya Marvel, ilikuwa kampuni kubwa,
iliyotengeneza filamu nyingi kama Spiderman, Captain America, Thor na nyingine
nyingi, hivyo waliamini kwamba hata Around ingekuwa moja ya filamu kali, tena
iliyokuwa ikiigizwa na muigizaji mwenye jina na uwezo mkubwa, Todd.
****
David alikuwa akitetemeka, kitu alichokuwa akikiona mbele yake kilikuwa kifo tu,
hakuamini kama watu wale wangeweza kumuacha kwani walimtaka kusema
ukweli juu ya mahali alipokuwa Benjamin, ila hakutaka kusema, alifanya siri kitu
kilichowakasirisha wanaume hao.
Bado walimtaka kuzungumza, kusema ukweli juu ya mahali alipokuwa Benjamin
lakini bado msisitizo wa David ulikuwa palepale kwamba hakuwa akimfahamu
mtu huyo, ndiyo kwanza alimsikia siku hiyo.
Hawakutaka kusubiri zaidi, David alionekana kuwa jeuri hivyo walichoamua ni
kummaliza tu. Huku bastola zikiwa zimekokiwa tayari kwa kufyatuliwa, ghafla
wakasikia dirisha la kioo likivunjwa, risasi mfululizo zikaanza kupigwa kuelekea
ndani humo, tena kwa ustadi mkubwa kabisa.
Wanaume wawili miongoni mwa wale watatu wakaanguka chini, damu zilikuwa
zikiwatoka migongoni mwao, walirusharusha miguu na mikono yao, walihangaika
katika hatua za mwisho kabla ya kukata pumzi na kufariki dunia.
Mwanaume mmoja, yeye na David ndiyo waliobaki ndani ya nyumba ile, alikuwa
na wasiwasi mkubwa, bastola ilikuwa pembeni yake na hata kuichukua, hakudiriki.
Alikuwa akitetemeka muda wote, macho yake yalipotua kwa wenzake ambao
walipigwa risasi na kufa, alizidi kuogopa na kuona kwamba muda wowote ule hata
yeye mwenyewe pia angeweza kufa.
Wakati wote wawili wakiwa wamelala chini, ghafla mlango ukafunguliwa na
maofisa watatu wa FBI kuingia huku wakiwa na bastola zao mikononi mwao, kitu
cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuwaweka wote chini ya ulinzi.

81
“Sijafanya kitu,” alisema David huku akitetemeka, ndiyo kwanza walikuwa
wakimfunga pingu.
“Tutajua...”
“Lakini hawa ndiyo walikuja kunivamia,” alisema.
“Tutajua tu, twendeni!”
Wote wakafungwa pingu na kutolewa ndani ya nyumba ile, muda wote David
alikuwa akilia, hakuamini kama kweli alifungwa pingu. Watu walioingia walikuwa
ni maofisa wa FBI, walijuaje kama alikuwa amevamiwa? Na wale watu waliokuwa
wameingia na kumuweka chini ya ulinzi wao, walijuaje kama yeye alikuwa
akimfahamu Benjamin? Kila alilojiuliza, alikosa jibu kabisa.
****
Wote wakachukuliwa, wakaingizwa ndani ya gari na safari ya kuelekea katika
kituo cha polisi kuanza mara moja. Njia nzima David alionekana
kuchanganyikiwa, hakujua kitu gani kilichokuwa kikiendelea, mawazo mengi,
maswali yalimtinga lakini yote hayo hayakuwa na majibu yoyote yale.
Walichukua muda wa dakika ishirini ndipo gari lao likaanza kuingia katika jengo
ambalo alikuwa na uhakika halikuwa jengo la polisi. Kwa muonekano wake tu,
kwa kuliangalia harakahara lilionekana kujengwa kwa ajili ya kazi maalumu, nje
hakukuwa na magari, na sehemu hiyo ilionekana kuwa tofauti kabisa na sehemu
nyingine.
Hakukuwa na mtu aliyezungumza kitu chochote kile, wakalipeleka gari katika
sehemu ya kuegeshea na kisha kuwataka wote wateremke, wakafanya hivyo.
Wakawachukua na kwenda nao ndani, huko, wakatenganishwa vyumba, David
alipelekwa katika chumba kingine na yule mwanaume mwingine akapelekwa
katika chumba kingine.
Huko, David alikuwa akitetemeka, hakujua ni kitu gani kilichowafanya maofisa
hao wa FBI kumchukua na kumuingiza ndani ya chumba hicho badala ya
kumuacha nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa amevamiwa.
Akawekwa mbele ya meza kubwa, kulikuwa na viti viwili chumba kizima, mbele
yake kulikuwa na kioo kikubwa, akajua tu kwamba nyuma ya kioo kile kulikuwa
na watu waliokuwa wakimwangalia.

82
Mbali na hivyo, pia kulikuwa na kamera ndogo mbili za CCTV zilizokuwa
zimewekwa katika pembe mbili ndani ya chumba hicho. Alikaa huku akionekana
kuwa na hofu, akahisi kwamba kulikuwa na jambo zito mbele yake.
Wakati akiwa kwenye mawazo, mara wanaume wawili wakaingia ndani ya
chumba hicho, mmoja akakaa katika kiti kimoja na mwingine kusimama huku
bastola ndogo aina ya 45 Automatic ikiwa kiunoni mwake.
“Unamfahamu mtu anaitwa Benjamin?” aliuliza ofisa huyo aliyejitambulisha kwa
jina la Gregory.
“Hapana!” alijibu.
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“David Belshaaz, hatupo hapa kama watu wabaya, unajua dhahiri kwamba
tunamtafuta mtu huyo, kwa nini unatuficha, kuna nini? Hutuamini?” aliuliza
Gregory.
“Simfahamu! Watu wale walionivamia, walikuja na kuniuliza kuhusu Benjamin,
mmewaua, na nyie mnakuja na kuniuliza kuhusu Benjamin, huyu Benjamin ni nani
na amefanya nini?’ aliuliza David huku akimkazia macho Gregory.
“Ina maana haumfahamu Benjamin?”
“Ndiyo! Au naweza nikawa namfahamu kwa kumwangalia, ila jina, ni geni
kwangu,” alijibu David.
“Una uhakika?”
“Ndiyo ofisa...”
Alijua fika hakuwa na kosa lolote lile, hata kama angekataa kusema mahali
alipokuwa Benjamin, asingepigwa wala kuuawa, au hata kutishiwa. Alizungumza
kwa kujiamini kwani alijipa uhakika kwamba mahali alipokuwa palikuwa salama
kabisa.
“Unamfahamu marehemu Carter?” aliuliza Gregory.
“Ndiyo! Kuna mtu asiyemfahamu mtaalamu wa Pop?”
“Unajua nini kuhusu yeye?”

83
“Kwamba alikuwa mwanamuziki mkali, labda kingine, alipenda sana kucheza
chess,” alijibu David.
“Na kuhusu kifo chake?”
“Nitajua nini kuhusu hilo? Nafuatilia vyombo vya habari, nadhani waandishi
watakuwa wanajua zaidi kuliko mimi,” alijibu David.
“Sawa. Naomba simu yako!”
“Ya nini?”
“Hakuna ubaya. Naweza kuipata?”
“Unaweza ukaipata kama ukiniambia ya kazi gani, ila vinginevyo, hautoweza
kuipata,” alijibu David.
Gregory akabaki akimwangalia David, kwa namna alivyokuwa akizungumza,
alionekana kuwa mtu makini, hakuingiza utani, kila alichokiongea, uso wake
ulimaanisha kila sentensi kwamba hakuwa akileta utani hata mara moja.
Gregory akabaki akimshangaa, katika kufanya naye kazi hakuwahi kukutana na
mtu aliyekuwa akijiamini kama ilivyokuwa kwa David. Si yeye tu aliyeshangaa
bali hata wale waliokuwa wakifuatilia nyuma ya kioo, walishangaa, huyu David
alikuwa mtu mwingine kabisa.
“Si kwa lengo baya!”
“Najua ofisa. Naweza kuondoka?”
Gregory akashusha pumzi nzito, akayapeleka macho yake kwa mwenzake
aliyekuwa amesimama pembeni, wakapeana ishara fulani, David aliiona ila
hakutaka kujali kwani bado akili yake ilimwambia kwamba alikuwa katika mikono
salama kabisa.
“Oooh! Samahani ofisa, mlisema kwamba mnaitaka simu yangu, si ndiyo?’ aliuliza
David.
“Ndiyo!”
“Mtaweza kuitumia?”
“Ndiyo!”
“Sawa! Naombeni niwape kwa masharti.”

84
“Yapi?”
“Nikiwapa niondoke zangu, mtaniletea mkishamaliza kazi nayo,” alisema David,
maofisa hao wakaangaliana.
“Sawa!”
Alichokifanya David ni kuichukua simu hiyo kutoka mfukoni na kisha kumgawia
Gregory ambaye akaipokea huku macho yake yakiwa usoni mwa David.
Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani mwake, kwamba ilikuwaje David
atake kumpa simu baada ya kujifikiria kwa muda mrefu lakini pia kumuuliza kama
angeweza kuitumia?
Hakupata jibu ila alijua kwamba kwenye kutumia simu hakukuwa na tatizo lolote
lile na ndio maana akakubaliana naye. Alipopewa, hakuwa na jinsi, alitakiwa
kutekeleza ahadi yake hivyo wakamruhusu kuondoka na kuahidi kumrudishia simu
ile pindi watakapomaliza kuitumia.
Kitu cha kwanza kabisa walichotaka kukifanya ni kuipekua simu ile. Haikuwa
rahisi kama walivyofikiria, kwanza sehemu ya simu zilizopigwa na kuingia
hazikuwa zikionekana. Walishangaa, haikuwa simu ya kawaida, ilionekana
kuingizwa programu ambayo hawakuwa wakiifahamu.
Wakaipeleka kwa watu wao wa masuala ya kompyuta (IT), walipowapa ile simu
na kuanza kuichezea ili kujua ni simu zipi zilikuwa zimepigwa na kutoka,
hawakuweza kuona chochote kile.
Walihitaji muda wa saa moja huku wakiishughulikia simu ile, maofisa wengine wa
FBI waliwasubiri zaidi lakini mpaka saa moja linafika, hakukuwa na
kilichowezekana, bado majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikuweza
kufunguka sehemu ya simu zilizoingia na kutoka.

85
SURA YA NNE

ILIKUWA ni usiku sana, walikuwa safarini kuondoka walipokuwa wakiishi na


kuelekea sehemu ambayo hawakuifahamu. Walembea kwa mwendo wa
harakaharaka, hawakutaka kusimama, kila walipoangalia nyuma, walihisi kwamba
kulikuwa na watu walikuwa wakiwafuata hivyo ilikuwa ni lazima kukimbia.
Walikwenda mpaka walipofika sehemu iliyokuwa na kituo cha mafuta, kitu
walichokihitaji ni chakula, kilipita kipindi fulani hawakuwa wamekula chakula
chochote kile, walihisi njaa hivyo ilikuwa ni lazima kununua chakula.
Wakaingia katika supamaketi iliyokuwa katika kituo hicho cha mafuta na kuanza
kuzunguka huku na kule kutafuta chakula. Hakukuwa na mteja yeyote, walikuwa
wao na muuzaji mwanamke ambaye kila wakati alibaki akimwangalia Benjamin
kama mtu aliyekuwa akimfahamu.
Benjamin hakujua hilo, alikuwa bize kuangalia huku na kule, walipomaliza
kuchagua vyakula walivyovitaka, wakaenda mpaka katikasehemu ya kulipia tayari
kwa kumlipa mwanamke huyo.
“Kuna nini?” aliuliza Benjamin kwa sauti ya chini, alikuwa akimuuliza Vivian.
“Kivipi?”
“Huoni jinsi anavyotuangalia huyu mwanamke?”
“Mmh!”
“Nahisi kuna kitu!”
Wakati wamesimama hapo, mwanamke huyo hakuonekana kuwa na haraka,
alikuwa akiwahudumia taratibu huku chini ya meza yake kukiwa na kitufe
ambacho kama ungekibonyeza, kilipeleka taarifa katika kituo kidogo cha polisi
kilichokuwa karibu na supamaketi hiyo kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa
kikiendelea.
Alimfahamu Benjamin, picha yake ilikuwa maarufu hata zaidi ya Gazeti la New
York Times na zilibandikwa kona nyingi hapo Marekani. Alikuwa akimchelewa
mahali hapo kwa kuwa alijua kwamba tayari polisi walipokea taarifa hivyo
wangefika mahali hapo muda wowote ule.

86
“Tunaweza kuondoka?” aliuliza Benjamin, alimshangaa namna mwanamke huyo
alivyokuwa akijichelewsha.
“Subirini kwanza...”
“Tusubiri nini?” aliuliza Vivian, mwanamke huyo hakujibu, aliendelea kujifanya
anapanga baadhi ya bidhaa zake, hivyo Benjamin na Vivian wakasubiri pasipo
kujua kwamba polisi walikuwa njiani kufika mahali hapo.
Walionekana kukasirika lakini hawakutaka kuondoka, kwa jinsi mwanamke huyo
alivyoonekana bize, ilionyesha kuwa hakuwa akifanya kusudi, kweli alikuwa bize.
Huku wakiendelea kuwa mahali hapo, ghafla wakaanza kusikia ving’ora vya gari
la polisi likija kule walipokuwa. Kwanza wakashtuka, walipoyapeleka macho yao
kwa mwanamke yule, alionekana kabisa kushtuka.
“Umeita polisi?” aliuliza Benjamin.
“Nani?”
“Umeita polisi...umeita polisi wewe...” alisema Benjamin huku akimshika mkono
Vivian na kuanza kuondoka naye mahali hapo.
Tayari gari la polisi lilikaribia kabisa karibu na kituo hicho cha mafuta, waliona
kabisa kama wangepita kwa kutumia mlango wa mbele ingekuwa rahisi sana
kuonekana, hivyo ilikuwa ni lazima waondoke kwa kupitia mlango wa nyuma.
Hakukuwa na muda wa kujifikiria mahali hapo, wakaanza kuondoka kupitia
mlango wa nyuma, mwanamke yule akatoka nje, alionekana kuwa na haraka,
akaanza kuwahimiza polisi wale wafike haraka mahali hapo kwani mtu
waliyekuwa wakimtaka, alikuwa akikimbia.
Baada ya polisi kufika mahali hapo, wakasimamisha gari lao na kisha kuteremka,
hawakutaka kuzungumza na mwanamke yule, walichokifanya ni kuingia ndani
moja kwa moja, bastola ndogo zilikuwa mikononi mwao, wakaanza kuangalia
huku na kule wakimtafuta.
“Yupo wapi?’ aliuliza polisi mmoja huku akiwa makini kuangalia huku na kule.
“Aliondoka kupitia mlango ule,” alisema mwanamke yule, polisi wakaanza
kuelekea huko.

87
Sehemu walipotokea ilikuwa ni stoo, kulikuwa na bidhaa nyingi, hawakutaka
kusimama mahali hapo, ilikuwa ni lazima wakimbie, mbele yao kulikuwa na
mlango mkubwa wa chuma, wakaufuata na kisha kuufungua.
Sehemu waliyotokea ilikuwa na mifuko mingi iliyokuwa imefungwa, wakapita
katikati mpaka walipokutana na mlango mwingine ambapo baada ya kuufungua,
wakakutana na gari aina ya Jeep.
“Tuingie garini,” alisema Benjamin huku akilifuata gari hilo.
“Hatuna ufunguo...”
“Wakati mwingine si lazima uwe na ufunguo...” alisema Benjamin huku
akikivunja kioo cha gari lile.
Akaingia ndani, akamfungulia mlango Vivian na kuingia ndani. Alichokifanya ni
kuifungua sehemu iliyokuwa chini ya usukani na kisha kuanza kuziunganisha
nyaya zilizokuwa mahali hapo, tena kwa kasi ya ajabu.
“Fanya haraka....wanakuja...”
“Najitahidi...nipe sekunde tano...” alisema Benjamin huku akizichuna zile nyaya
kwa meno yake na kisha kuanza kuziunganisha, yote hiyo ilikuwa ni harakati za
kuwasha gari hilo.
Wakati akiendelea kuliwasha lile gari kwa kutumia nyaya kadhaa, polisi wale
walikuwa wakikaribia, muda huo nao walikuwa stoo, walikimbia kuelekea kule
walipoelekea Benjamin na mpenzi wake, Vivian.
Wakati wameufikia mlango, ghafla wakasikia mlio wa gari likiwa limewashwa,
wakati wameufungua mlango huo, wakaliona gari hilo likiondoka kwa kasi mahali
hapo, hata mlango mkubwa wa nyuma haukufunguliwa, Benjamin akaufunja
mlango huo kwa gari lile na kuanza kuondoka.
“Tuwakimbize, twende garini,” alisema polisi mmoja.
Wakatoka nje, wakalifuata gari lao, wakaingia na kuanza kuondoka kulifuata gari
lile ambalo lilikuwa mbali kama mita mia moja na hamsini kwani injini yake
ilikuwa na nguvu kubwa.
“Tunahitaji msaada Barabara ya St. Joseph 45W, tumemuona mtuhumiwa wa
mauaji, Benjamin, tunahitaji msaada....ova..” alisema polisi mmoja, alikuwa
ameshika redio call, mwenzake alikuwa akiendesha gari hilo kwa kasi kubwa.

88
Bwana David Seppy alichanganyikiwa, hakuamini zile taarifa alizokuwa amepewa
kwamba vijana wake waliokuwa jijini Washington DC waliuawa huku mmoja
akikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi chini ya maofisa wa FBI.
Hakutaka kuona hilo likitokea, alijua vilivyo jinsi maofisa hao walivyojua
kuzungumza na mtu, kumuuliza maswali ya mitego na hatimaye kuwaambia mtu
aliyekuwa amewatuma.
Kwa kijana huyo kushikiliwa na FBI lilionekana kuwa jambo bata sana, hakutaka
kuona akigundulika kwamba yeye ndiye aliyekuwa akihusika na mauaji
yaliyokuwa yakitokea, hivyo ilikuwa ni lazima ahakikishe kijana huyo anauawa.
Akawasiliana na Dracula ambaye naye tayari alifika huko, akampa amri kwamba
iwe isiwe ilikuwa ni lazima kijana huyo auawe kwa kuwatumia baadhi ya maofisa
waliokuwa ndani ya jengo hilo kumuua kijana huyo kwa kumchoma sindano.
Hilo likachukuliwa na Dracula, akawasiliana na maofisa wawili wa FBI ambao
walikuwa upande wao na kuwalipa kiasi kikubwa cha fedha, akawaambia kwamba
kijana huyo alitakiwa kuuawa haraka iwezekanavyo, hivyo mishemishe zikaanza.
“Imekuwaje?” aliuliza Bwana Seppy.
“Vijana wanafuatilia, bila shaka watafanikiwa,” alijibu Dracula.
Alikaa na kusubiri, alitaka kujua kama maofisa hao walifanikiwa au la, baada ya
saa nne, akapigiwa simu na kupewa taarifa kwamba kijana yule aliyenusurika
kuuawa, aliuawa katika chumba kimojawapo katika kituo cha polisi baada ya
kuchomwa sindano.
“Safi sana,” alisema Bwana Seppy huku akionekana kuwa na furaha kubwa.
Baada ya wiki moja, akaamua kumuita kijana wake, Dracula na kumpa mpango
kabambe uliokuwa mbele yake, alimwambia wazi kwamba alitaka kuzitangaza
biashara zake kupitia watu maarufu hivyo mtu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa
juu ambaye ilikuwa ni lazima kuonana naye, alikuwa muigizaji, kijana mdogo,
mwenye uwezo mkubwa, Lewis Todd.
Kumpata Todd halikuwa tatizo hata kidogo kwani kwa sababu mambo ambayo
walitakiwa kuzungumza naye yalikuwa ni biashara, wakawasiliana na meneja
wake na kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea hivyo aliakiwa
kuzungumza mtu wake.
“Hakuna tatizo, nitazungumza naye,” alisema meneja huyo, Bwana Oswald Genz.

89
Genz alikuwa mtu wa fedha, kila alipokaa, kitu alichokifikiria kilikuwa fedha tu.
Kulikuwa na madili mengi yaliyokuwa yakija mezani kwake kwa ajili ya mtu
wake, hivyo kupewa taarifa kwamba Bwana Seppy alitaka kuingia mkataba wa
kufanyiwa matangazo na mwanamuziki aliyekuwa akimsimamia, kwake ilikuwa
dili nzuri.
Kitu cha kwanza akawasiliana na Todd na kumwambia kila kitu kilichokuwa
kikiendelea, akampa mchakato mzima kuhusu dili hilo ambapo kwa upande wa
Todd, hakukuwa na tatizo lolote lile, alitakiwa kurudi kutoka nchini Ukraine na
ndipo angesaini mkataba huo.
“Ila walikwambia ni kiasi gani?” aliuliza Todd kwenye simu.
“Hapana!”
“Ni lazima tujue. Bila dola milioni ishirini, hakuna biashara hapo,” alisema Todd.
“Nadhani inaweza kuwa zaidi ya hapo, si unajua jinsi Seppy alivyokuwa na
fedha?”
“Ndiyo! Najua hilo! Kama itakuwa ni zaidi, basi hilo ni bonge la dili,” alisema
Todd na simu kukatwa.
Baada ya wiki tatu, Todd akafika nchini Marekani, kitu cha kwanza kabisa
kukifanya ni kupanga mikakati ya kuonana na Bwana Seppy, mikakati hiyo
ikafanyika na ndani ya siku mbili, walikuwa katika hoteli ya kifahari ya Leopard
Vile iliyokuwa ikimilikiwa na mzee huyo kwa ajili ya kuingia mkataba.
“Nitakulipa dola milioni tano,” alisema Bwana Seppy.
“Unasemaje?” aliuliza Todd huku akionekana kutokuamini kile alichokisikia.
“Dola milioni tano! Unaonaje?” aliuliza.
Todd akaangaliana na meneja wake, hawakuamini walichokuwa wamekisikia
kutoka kwa mzee huyo. Walitegemea kwamba wangepata zaidi ya dola milioni
ishirini kutokana na jina kubwa alilokuwa nalo kipindi hicho, sasa iweje apewe
milioni tano na wakati nyuma yake kulikuwa na watu wengi, waliofanya
alichokifanya?
“Haiwezekani,” alisema Todd.
“Kivipi?”

90
“Bila milioni thelathini, hakuna kinachofanyika,” alisema Todd, alionekana
kumaanisha haswa.
“Nisikilize Todd.....”
“Hakuna suala la kusikiliza. Kiasi hicho nilikuwa nikipokea miaka miwili iliyopita,
si sasa, kuna watu wengi mno nyuma yangu, kiasi hicho kidogo,” alisema Todd.
Bwana Seppy akakasirika kama kawaida yake, kwake, mtu kukataa kuingia
mkataba na yeye, tena kwa fedha alizozitaka yeye ilionekana kuwa dharau kubwa,
akabaki akimwangalia kijana huyo, hasira kali iliyomkaba kooni ikamwambia
kwamba ilikuwa ni lazima amuue kijana huyo, yaani kama ilivyotokea kwa Carter.
Bwana Seppy alitumia muda huo kumbembeleza Todd akubaliane naye lakini
kijana huyo akakataa kabisa kwa kusema kwamba kiasi kilichotolewa, kisingeweza
kumfikisha kokote kule kwani mbali na yeye, kulikuwa na watu wengi nyuma
yake.
Bwana Seppy hakutaka kuzungumza tena, moyo wake ulimuuma sana kwa kuona
kama akilazimishwa kumuua kijana huyo, hivyo alichokifanya ni kuondoka
kuelekea nyumbani kwake.
Alikuwa na mawazo mengi, hata mkewe alipomuona, aligundua kwamba mume
wake hakuwa sawa kichwani hivyo akamlazimisha kumwambia ukweli lakini
akasema kwamba kulikuwa na vitu vidogo vya kibiashara vilivyokuwa
vikimsumbua.
“Kweli?” aliuliza mkewe.
“Ndiyo mke wangu! Kichwa changu hakipo saa, biashara zangu zinasumbua sana,”
alisema mzee huyo.
Hakutaka kupoteza muda, alichokifanya ni kumwambia Dracula kwamba Todd
alitakiwa kuuawa kama kawaida, hakutaka kumuona mtu huyo akiendelea kuishi,
alimpa muda wa mwezi mmoja kijana huyo afe.
“Tumuue kwa risasi?” aliuliza Dracula.
“Itagundulika kama ameuawa...” alijibu.
“Au ajali?”
“Napo itagundulika kama ilivyokuwa kwa Princess Diana...”

91
“Sasa tumuue vipi?”
“Kama ilivyokuwa kwa Carter. Mfanyeni aonekane kama amejidunga madawa ya
kulevya, tena iwe ndani ya nyumba yake,” alisema Bwana Seppy.
“Sawa! Tutafanya hivyo mkuu!”
“Tena ni vizuri ikiwa ndani ya gari lake,” alisema Bwana Seppy.
“Ila....”
“Ila nini bosi?”
“Isiwe mwezi huu, acheni mpaka mwezi ujao,” alisema.
“Sawa!”
“Natumaini mtaifanya kazi yangu ipasavyo!”
“Ndiyo mkuu! Hela zitahitajika kuwekwa?”
“Kama kawaida. Kama ilivyokuwa kwa Carter, acha iwe kwa Todd pia, na
msisahau kuweka na alama za vidole vya Benjamin,” alisema Bwana Seppy.
“Hakuna tatizo!”
****
Benjamin alikuwa akiendesha gari kwa kasi kuwakimbia polisi ambao nao
walikuwa wakija nyuma yake, alichanganyikiwa, kitendo cha kukimbizana na
polisi barabarani lilikuwa kosa kubwa ambalo lingemfanya kuadhibiwa kwa
kupigwa faini au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
Ilikuwa ni afadhali kwa kipindi hicho kukimbizwa na polisi hao kuliko kukamatwa
na kufikishwa mahakamani. Dunia nzima ilijua kwamba yeye ndiye alikuwa
muuaji, hakukuwa na aliyejua lolote kwamba kilichokuwa kimetokea nyuma ni
yeye kuyaokoa maisha ya Carter na hata zile alama za vidole vyake, zilikuwa zake
ila hakuwahi kuingia ndani ya chumba kile.
Akakanyaga mafuta, gari ile ilikuwa na injini kubwa hivyo aliweza kuwaacha
mbali polisi wale, hakutaka kusimama na kujisalimisha, alipoona kwamba
inawezekana polisi wale walikuwa wamewasiliana na polisi wengine,
akamwambia Vivian kwamba ashikilie usikani.
“NA wewe?” aliuliza msichana huyo.

92
“Ni lazima niondoke garini, siwezi kuendelea mbele,” alijibu.
“Uondoke?”
“Ndiyo! Vinginevyo nitakamatwa...” alisema Benjamin.
“Unataka kuniacha?”
“Ndiyo! Vivian, unajua ukweli, nataka unisaidie kuiambia dunia ukweli,” alisema
Benjamin.
“Sawa! Ila unakwenda wapi?”
“Popote pale, nitajifiicha, sitotaka kuonekana mpaka hapo dunia itakapofahamu
ukweli kwamba sikuua,” alisema Benjamin.
Hakukukuwa na muda wa kupoteza, mahali walipokuwa, ilikuwa ni kwenye kijiji
cha Hertrown ambacho kilikuwa pembezo mwa Jiji la Boston, barabarani
kulizungukwa na miti, sehemu hiyo ilikuwa kama na pori fulani.
Gari likasimamishwa, harakaharaka Benjamin akamsogelea Vivian, akambusu na
kisha kuteremka, alichokifanya ni kuingia ndani ya pori lile, Vivian akapiga gia na
kuondoka mahali hapo.
Benjamin akaanza kukimbia kwa kasi kubwa, akiwa huko, akasikia king’ora cha
polisi, akajua kabisa kwamba tayari gari hilo lilikuwa likipita mahali hapo.
Benjamin akaondoka mpaka katika mlima mmoja mkubwa, huko, kulikuwa na
mawe mengi kama milima ya jijini Mwanza, akasimama kwenye kilele na kuanza
kuangalia chini, aliliona gari lile alilopanda na Vivian likiwa limesimamishwa na
magari matatu ya polisi yaliyokuwa mbele, aliweza kumuona mpenzi wake, Vivian
kwa mbali akiwa ameteremka garini na kuongea na polisi waliokuwa
wamemsimamisha, hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kuanza kushusha mlima ule
upande wa pili na kutokomea zake, hakutaka kujua ni kitu gani kilichokuwa
kikiendelea huku nyuma.
Vivian aliendesha gari lile huku akiwa na maumivu makubwa moyoni mwake,
kitendo mcha mpenzi wake, Benjamin kutafutwa kwa kosa la mauaji kilimuumiza
sana kwani aliujua ukweli kwamba mpenzi wake hakuhusika katika mauaji hayo
bali nyuma ya pazia kulikuwa na watu wengine ambao walihusika.
Hakuendesha gari kwa mwendo wa kasi kama ilivyokuwa kwa Benjamin,
aliendelea kusogea mbele mpaka pale alipokutana na magari ya polisi ambapo

93
akapigwa mkono na kuambiwa apaki pembeni, hakubisha, akafanya kama
alivyoambiwa.
Polisi wale walipoliangalia gari lile, lilikuwa lilelile waliloambiwa kwamba ndani
yake kulikuwa na Benjamin, mwanaume aliyekuwa akitafutwa sana kipindi hicho,
wakaingia ndani ya gari na kuanza kupekua kila kona, mtu huyo hakuwepo.
“Benjamin yupo wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Benjamin yupi?”
“Ulikuwa na nani kwenye gari?”
“Peke yangu!”
“Haukuwa na mtu?”
“Hapana!”
Wakati mahojiano yakiendelea, lile gari la polisi lililokuwa likiwakimbiza likafika
mahali hapo, moja kwa moja polisi hao wakateremka na kuanza kuelekea kule
walipokuwa polisi wenzao na Vivian.
“Alikuwa humu,” alisema mmoja wa polisi waliofika mahali hapo.
“Benjamin alikuwa humu, huyu binti ni lazima atuambie yupo wapi,” alisema
polisi mwingine, alikuwa miongoni mwa wale waliofika mahali hapo ambao ndiyo
waliokuwa wakiwafukuza.
“Hakukuwa na mtu zaidi yangu!”
“Hapana! Tuambie yupo wapi!”
Japokuwa walimlazimisha Vivian kusema mahali alipokuwa Benjamin lakini
msichana huyo hakutaka kuzungumza kitu chochote kile, msimamo wake ulikuwa
uleule kwamba hakukuwa na mtu mwingine ndani ya gari lile zaidi yake.
Walichokifanya ni kumchukua na kumpeleka kituoni, walidhani kwamba
angebadilisha msimamo wa majibu yake lakini aliendelea kusisitiza kwamba
hakukuwa na mtu yeyote ndani ya gari zaidi yake kitu kilichowaweka polisi katika
wakati mgumu wa kumpata Benjamin.
****

94
David hakutaka kutulia, bado mbele yake kulikuwa na kazi kubwa ya kujua yule
mtumiaji wa namba iliyokuwa ikitumika kuwasiliana na Benjamin ilikuwa ni ya
nani na ilitoka wapi.
Japokuwa simu yake ilichukuliwa lakini data zote za simu ile alikuwa
amekwishazituma katika email yake hivyo akaingia na kuanza kuangalia.
Alipoipata namba ile, akachukua programu aliyoitengeneza mwenyewe iliyoitwa
Davy Hack kisha kuanza kuipekua simu iliyotoka namba ile.
Hukondipo alipopata majibu ya maswali yote aliyokuwa akijiuliza, akakutana na
namba nyingi zilizokuwa zikiingia na kutoka ila kitu kilichompa uhakika kwamba
mtu aliyekuwa akihusika zaidi alikuwa ni mtu ambaye namba yake inaishia na 69
kwani ndiye mtu aliyekuwa akipiga mara kwa mara.
“Huyu ni nani?” alijiuliza.
Hakutaka kuchelewa, kila swali alilokuwa nalo kichwani mwake ilikuwa ni lazima
kupata majibu yake hivyo alichokifanya ni kuanza kuangalia usajili wa namba ile.
Kazi wala haikuwa kubwa, japokuwa watu pekee ambao wangeweza kuangalia
namba ya usajili kwa undani zaidi walikuwa ni wale wenye mtandao husika lakini
yeye akafanikiwa kwa asilimia mia moja, mtumiaji wa namba hiyo iliyokuwa
ikipigwa mara kwa mara katika namba ya simu ya huyo aliyekuwa akimsumbua
Benjamin aliitwa David Seppy.
Taarifa hizo hazikuishia hapo, ziliendelea kutoa zaidi taarifa na kuonyesha mahali
alipokuwa akiishi, kila kitu kuhusu yeye ambacho hakikuwa na siri yoyote
vilionekana.
David akashusha pumzi ndefu, hakuamini kwamba matukio mengi yaliyokuwa
yakitokea yalipangwa na mzee huyo. Hakujua tatizo lilikuwa nini, alimfahamu
rafiki yake, hakuwa mtu mwenye ugomvi na mtu yeyote, na hakujua kama
kulikuwa na ulazima wa Benjamin kufahamiana na mzee huyo kwani walikuwa
watu tofauti kabisa, sasa kwa nini kulikuwa kama na ukaribu fulani?
Alichokifanya cha zaidi ni kuangalia meseji zilizokuwa zikiingia na kutoka katika
namba hizo mbili. Alipoziona, akashtuka kwani meseji hizo ndizo zilizoonyesha
kila kitu kilichokuwa kikiendelea, David akashusha pumzi ndefu, akachoka,
hakuamini kama mzee aliyekuwa akiheshimika, David Seppy ndiye aliyekuwa
akihusika kwenye mauaji ya Carter, pia, mbali na hivyo, alijipanga kumuua Todd
baada ya mwezi mmoja.

95
****
“Benjamin, niambie ukweli kuhusu hili linaloendelea,” alisema Harry, rafiki
mkubwa wa Benjamin.
“Hakuna jipya, sikuhusika kumuua Carter.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
“Mbona alama zako za vidole zimeonekana katika mwili wa Carter?” aliuliza
Harry.
“Huwezi kuamini Harry, ila jua kwamba sikuhusika na chochote kile,” alisema
Benjamin.
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
Benjamin aliamua kufunga safari kuelekea katika Mtaa wa Augestberg uliokuwa
hapohapo Boston nchini Marekani. Hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi
ya hapo.
Alimwamini sana Harry, alikuwa rafiki yake mkubwa, walikuwa pamoja kila kona
katika kipindi walichokuwa chuo. Hakuwa na sehemu nyingine ambayo aliona
kustahili kukimbilia zaidi ya hapo, kwa Harry ndipo kulikuwa kila kitu kwa kipindi
hicho.
Maneno aliyosema Benjamin bado yalimuweka Harry katika wakati mgumu,
hakujua kama alitakiwa kumwamini Benjamin kama kweli hajaua au la, kila
alipojiuliza swali hilo, alikosa jibu.
“Kwa hiyo tufanye nini?” aliuliza Harry.
“Nahitaji unisaidie.”
“Nikusaidie nini?”
“Nataka niwe na nawasiliana na David mara kwa mara, kuna kazi nimemwambia
anisaidie. Harry, nimechanganyikiwa, sina hatia, sijui ni kwa nini muuaji aliamua
kumuua Carter,” alisema Benjamin huku akionekana kuvurugwa kabisa.
Hakuwa na jinsi, kwa sababu alikuwa rafiki yake na alikuwa akikumbana na
matatizo mengi, akaamua kuishi naye kwa kumficha, humo alipokuwa, hakutaka

96
hata marafiki zake wengine wafahamu kama Benjamin alikuwa ndani kwake, si
hao tu, bali hata mpenzi wake, Shakira naye hakutakiwa ufahamu kitu chochote
kile.
Siku ziliendelea kukatika, Benjamin akaamua kuwasiliana na David juu ya mahali
alipofikia hasa baada ya kumpa namba ile ambayo alitakiwa kuifuatilia, majibu
aliyopewa, hakuyaamini kwamba nyuma ya kila kitu, alikuwepo mzee mwenye
utajiri mkubwa nchini Marekani, Bwana David Seppy.
“Unasemaje?” aliuliza Benjamin huku akionekana kushtuka, Harry alikuwa
pembeni yake.
“Nimefuatilia mawasiliano, nimegundua hilo, ushahidi upo, tena nikwambie kitu?’
aliuliza David.
“Niambie!”
“Anayefuata ni muigizaji Todd!”
“Unasemaje?”
“Hiyo ndiyo taarifa, kila kitu kinachoendelea kinajionyesha hapa, wanatumiana
meseji pasipo kugundua kwamba ninafuatilia kila kitu,” alisema David kwenye
simu.
Maneno aliyoyaongea yalikuwa mazito mno, yaliwachanganya wote wawili lakini
pia walitaka kufuatilia kama kweli walivyokuwa wamewasiliana kwenye simu,
Todd angeuawa kweli au la.
Wote wakabaki kimya, wakaenda pembeni ya chumba hicho na kubaki kimya
kabisa. Vichwa vyao vikaanza kuwafikiria watu wawili, Bwana Seppy na Todd.
Kulikuwa na maswali mawili yaliyokuwa yakivitesa vichwa vyao, sababu ya
Bwana Seppy kufanya mauaji hayo kwa watu waliopendwa na watu wengi,
hawakujua kitu chochote kile.
“Kwa nini?” aliuliza Benjamin.
“Hata mimi najiuliza hilohilo! Kwa nini?”
“Ni lazima tukatoe taarifa polisi,” alisema Benjamin.
“Hapana! Ukifanya hivyo tutakuwa tunakosea,” alisema Harry.

97
“Kwa nini? La sivyo Todd atakufa, huoni kama itanisaidia hata mimi mwenyewe
kuwa huru?” aliuliza Benjamin.
“Una ushahidi kama Bwana Seppy ndiye muuaji?” aliuliza Harry.
“Si David anao!”
“Sawa! Wewe unao?”
“Sina, mpaka David atakaponipa!”
“Nisikilize Ben, hatutakiwi kufanya mambo kwa kukurupuka, ni lazima twende
kama wasomi, tukusanye ushahidi wa kutosha, hata kama Todd atauawa, si tatizo
kwani kupitia kifo chake tutazidi kujikusanyia ushahidi wa kutosha, tukicheza,
hatutoweza kumtia hatihani huyu mtu, tuwe na subira,” alisema Harry.
“Mpaka lini?”
“Sijui! Ila tuwe na subira!”
“Kwa hiyo tuache Todd auawe?”
“Kama inawezekana, tuache, haina jinsi,” alisema Harry, Benjamin akashusha
pumzi ndefu.
Kuanzia siku hiyo, hakukuwa na mtu mwenye furaha, wlaimchukia sana Bwana
Seppy ambaye mara kwa mara alikuwa mtu wa kuwasaidia watoto yatima na
kufungua taasisi zake za kuwasaidia masikini huku nyuma ya pazia akiwa mtu wa
matukio ya kikatili.
Hakukuwa na mtu aliyemshtukia, ilikuwa ngumu kugundua kwa sababu muda
wote alijifanya kuwa mtu wa watu. Matendo yake maovu aliyaficha kwa kutumia
kivuli cha misaada kwa watu masikini na wengine ambao hawakujiweza.
Serikali iliendelea kumwamini huku ikimpa tenda nyingi. Kwa watu watatu,
Bwana Seppy alionekana kuwa mtu katili ambaye iliwabidi wamfikishe
mahakamani haraka iwezekanavyo.
“Ni lazima huyu mtu ahukumiwe,” alisema Benjamin.
Kuanzia siku hiyo, wala hawakukaa sana, wakapata taarifa ambayo waliitegemea
kuisikia siku za karibuni kwamba muigizaji chipukizi aliyekuwa na kipaji cha hali
ya juu katika mapigano, Todd Lewis alikutwa akiwa amejiua ndani ya gari lake
baada ya kujidunga dawa za kulevya aina ya Cocaine.

98
Taarifa ziliendelea kusema kwamba mara baada ya polisi kuingia ndani ya gari
hilo, pembeni ya mwili wa Todd kulikuwa na fedha za noti, dola, yeni, euro
napaundi.
Hawakujua sababu ya Todd kujidunga sindano hiyo, mwili wake ulichukuliwa na
kupelekwa katika Hospitali ya Calvary ambapo huko ndipo madaktari pamoja na
polisi wangejua ni kitu gani kilichokuwa kimemuua, kama ni madawa ya kulevya
peke yake au kulikuwa na kingine.
Todd Lewis, muigizaji aliyekuwa na jina kubwa duniani alikuwa akitoka katika
Uwanja wa Kikapu wa Stapple Center kuangalia mechi ambayo iliwakutanisha
wenyewe, La Lakers ikiongozwa na Shaq O’ Neil ambayo ilikuwa ikipambana na
Chicago Bulls.
Alikuwa ameamua kusafiri kutoka jijini New York mpaka Los Angeles kwa ajili
ya kuangalia mechi hiyo. Alipenda mchezo wa kikapu na hakutaka kabisa kukosa
mchezo huo ambao ulikuwa ukizikutanisha timu kongwe, kali ambazo zilikuwa na
nguvu mno katika kipindi hicho.
Nje ya uwanja huo, watu wengi walikuwa wakimsubiri, alikuwa na jina kubwa,
ukiachana na mastaa wengi wa mchezo wa kikapu, pia siku hiyo Todd alikuwa
gumzo kubwa, ndani ya uwanja huo, watu wengi walitaka kupiga naye picha, pale
alipokuwa amekaa, watu walimsogelea na kuanza kujifotoa picha kadhaa na mpaka
mchezo huo unamalizika, kulikuwa na watu wengi waliopata nafasi ya kupiga naye
picha.
Wengine hawakuridhika, hata walipokuwa wakitoka, bado mashabiki walikmfuata
Todd, walitaka kupiga naye picha huku wengine wakitaka kusainiwa vitabu vyao.
Hayo yalikuwa maisha ya usupastaa, walimheshimu kwa kuwa aliifanya kazi yake
ipasavyo, wengi walipenda kutazama filamu zake, kwa kifupi, Todd aliwavutia
watu wengi mno.
Alipomaliza kuwasainia watu vitabu vyao na hata kupiga nao picha, kama kawaida
akaifuata gari yake ya kifahari, Ferrari nyekundu na kisha kuingia, kilichofuata ni
kuanza safari ya kuelekea hotelini kabla ya kurudi New York alipokuwa akiishi
siku inayofuata.
Akaliwasha gari hilo na kuondoka mahali hapo. Moyo wake ulijisikia faraja,
hakuamini kwamba mwisho wa siku angekuwa na umaarufu mkubwa kama
aliokuwa nao katika kipindi hicho.

99
Katika kipindi cha nyuma alipokuwa akianza, mambo yalikuwa magumu mno,
alipambana usiku na mchana lakini mwisho wa siku, alifanikiwa kuwa kama
alivyokuwa, hakukuwa na kitu kingine kilichokuwa kikiendelea zaidi ya
kukusanya fedha na kuwa nazo zaidi ya zile alizokuwa nazo.
Wakati safari ikiendelea na kuyakuta makutano ya Barabara za St. Barnaba na
Morovian ambayo ilikuwa ikienda mpaka katika Mtaa wa Butterfly uliokuwa
umbali kama wa kilometa tatu, akashtuka baada ya kuona gari moja likija kwa kasi
nyumba yake, lilikwenda mbele yake kwa mwendo wa kasi na kisha kusimama
kwa katikati ya barabara, tena kiubavuubavu.
Kama haukuwa umakini wake mkubwa, basi angeweza kuligonga gari hilo. Kwa
ustadi mkubwa, Todd akafunga breki na kisha kusimama, alibaki akihema kwa
nguvu, mbele yake ilionekana ajali kubwa ambayo pasipo kutumia uwezo wake
basi angeweza kuligonga gari hilo.
Huku akijiuliza ni kitu gani kinaendelea, wanaume wawili wakateremka kutoka
kwenye ile gari na kuanza kuelekea kule alipokuwa. Hakujua watu hao walikuwa
wakina nani na walihitaji nini kutoka kwake.
Mahali hapohakukuwa na magari, ilikuwa usiku sana na magari hayakuwa yakipita
mara kwa mara, hasa katika barabara hiyo ya magari yaendayo kasi. Akashindwa
kuliwasha gari lake, watu wale walikwenda kwa kasi mpaka pale lilipokuwa gari
lake, wakamwambia afungue mlango vinginevyo wangempiga risasi humohumo.
Hakuwa na jinsi, hakutaka kupinga, kitu cha kwanza kabisa, akashusha kioo cha
mbele cha mlango wa upande mwingine, mwanaume mmoja akaingia na
kumwamuru aendeshe mpaka sehemu waliyotaka wao waelekee.
“Naomba uniache, kama unataka gari chukua,” alisema Todd huku akitetemeka.
“Unadhani sisi tunataka gari?” aliuliza mwanaume huyo huku akiwa na bastola
mkononi mwake.
“Hata kama unataka kiasi chochote cha fedha, nitakupa, naomba uniache...”
alisema Todd, tayari machozi yakaanza kububujika mashavuni mwake.
Mwanaume yule mwingine akapita upande wa pili, akaufungua mlango na
kumshusha Todd kisha kumpeleka katika gari lao walilokuja nalo huku yule
mwingine akiachwa katika gari lile kwa ajili ya kuondoka nalo.

100
Kila kitu kilichokuwa kikifanyika mahali hapo, kilifanyika kwa haraka sana, tukio
zima lilichukua sekunde arobaini na tano tu, tayari wakaondoka huku wakiwa na
Todd ndani ya gari.
“Naombeni mniacheee...” alisema Todd.
“Hutakiwi kupiga kelele...” alisema mwanaume mmoja huku akimnyooshea
bastola.
“Nimefanya nini? Naombeni msiniue..” alisema Todd.
“Kwani kila anayeuawa kuna baya amelifanya? Hakuna kitu kama hicho, kuwa
mpole,” alisema mwanaume huyo.
Baada ya hapo, hawakutaka kuongea kitu chochote kile, wakaondoka naye huku
garini wakiwa kimya, kwani hata Todd naye aliyetaka kuzungumza maneno mengi
aeleweke na hivyo kuachwa, aliambiwa akae kimya kwani suala la kumuua
lisingeweza kuzuilika hata kidogo.
Walikwenda mpaka katika barabara nyingine ya Queen Elizabeth I ambayo
ilikuwa ikienda moja kwa moja mpaka kwenye jumba la makumbusho ya Lincoln,
hawakufika huko, wakakata kulia na kisha kuchukua barabara nyingine ambayo
iliwapeleka mpaka katika sehemu ambayo haikuwa na watu, giza lilitawala, gari
likasimamishwa mahali hapo.
“Naomba mnisamehe....”
“Halafu?”
“Niondoke, nitawalipa kiasi cha fedha chochote mnacholkitaka....”
“Halafu?”
“Naomba mnisamehe...”
Hawakutaka kupoteza muda, saa zao zilionyeshwa kwamba tayari ilikuwa ni saa
nane za usiku hivyo walitakiwa wafanye haraka, wamuue na kisha kuendelea na
mambo yao.
Walichokifanya ni kumkaba kooni, tena kwa nguvu kuhakikisha anakufa na kisha
kufanya kile walichoambiwa kukifanya. Mwanaume mmoja mwenye nguvu ndiye
aliyetumika kumuua Todd ndani ya gari hilo.

101
Dracula hakutaka kwenda katika lile gari kwani aliamini kwamba vijana wale
wangefanya kama jinsi alivyowapa maagizo, kweli wakafanya. Kilichofuata baada
ya kuhakikisha kwamba Todd amekufa ni kumchoma sindano iliyokuwa na
madawa aina ya cocaine, walipomaliza, wakachukua nailo zenye unyevuunyevu
ambazo kwa kutumia utaalamu wao waliweza kuweka alama za vidole za
Benjamin na kisha kuziweka katika shingo ya Todd na sehemu nyingine za mwili.
“Vipi?”
“Tayari!”
“Mbebeni mkamuweke ndani ya gari lake, pia wekeni na hizi fedha,” aliagiza
Dracula huku akiwapa noti ambazo zilitakiwa kuwekwa ndani ya gari hilo, vijana
wale wakafanya kama walivyoagizwa, wakaubeba mwili wa Todd na kisha
kuupeleka garini mwake na kuziweka noti zile.
“Tuondokeni!” alisema Dracula baada ya kumaliza kila kitu. Wakaondoka mahali
hapo huku kila mmoja akiwa na furaha ya kukamilisha kazi waliyokuwa
wamepewa.
****
Hakukuwa na mtu aliyeamini mara baada ya taarifa juu ya kifo cha Todd
zilipotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani. Wengi
walipigwa na bumbuwazi, kile walichokisikia, hakikuaminika kwao kwamba yule
muigizaji, mwenye jina aliyekuwa akivuma sana kipindi hicho, Todd Lewis
alikutwa amejidunga madawa ya kulevya kwakujiovadozi.
Watu wakapigiana simu, kila aliyesikia, hakutaka kukubaliana na habari hiyo
kwani miongoni mwa watu waliokuwa wakifanya vizuri kipindi hicho, alikuwa
huyo Todd, sasa kwa nini afe mapema hivyo? Tena mbaya zaidi alikutwa akiwa
amejiovadozi madawa ya kulevya kitu ambacho kiliwachanganya watu wote kwani
Todd hakuwa mtumiaji wa madawa hayo hata mara moja.
Wengi wakaenda katika Hospitali ya Calvary kujionea, huko, watu walikuwa
wakilia kwani ndipo walipopata taarifa kamili kwamba muigizaji huyo alikutwa
ndani ya gari yake ya kifahari ya Ferrari akiwa amejiovadozi madawa ya kulevya.
“Haiwezekani Bwana! Huyu jamaa hakuwa mlevi kabisa,” alisema jamaa mmoja.
“Ndiyo! Hata mimi nimeshangaa sana, yaani Todd awe mlevi wa madawa ya
kulevya! Haiwezekani hata kidogo,” alisikika jamaa mwingine.

102
Kila mmoja alikuwa sahihi kabisa, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa na shaka na
Todd kwamba alikuwa mtumiaji wa madawa hayo, taarifa hizo zikaendelea
kusambaa kila kona mpaka ndani ya saa moja tu, dunia nzima ilijua nini kilitokea
nchini Marekani.
Hofu zikaanza kutanda, taarifa zilizosema kwamba ndani ya gari la marehemu
kulikutwa noti za fedha kutoka nchi mbalimbali ziliwashtua sana kwani hata siku
ambayo Carter alikutwa akiwa amekufa ndani ya chumba cha hoteli, fedha kama
hizo zilikutwa kitu kilichowafanya watu kuona cha kawaida ila baada ya fedha
hizo kukutwa ndani ya gari hilo, wakagundua kwamba inawezekana hizo fedha
zilibeba ujumbe fulani.
“Kama huyu Benjamin ndiye aliyemuua Carter, basi inawezekana akawa amemuua
na Todd pia,” alisema jamaa mmoja wakati alipokuwa supamaketi, katika sehemu
ya kuuzia magazeti na majarida mbalimbali.
“Inawezekana kabisa...hebu tuwasikilizie polisi tuone watasemaje,” alisema jamaa
mwingine.
Hilo ndilo lililokuwa vichwani mwa watu wengi, kila aliyesikia namna gari hilo
lilivyokutwa, alikuwa na uhakika kwamba muuaji alikuwa yuleyule, kijana wa
chuo mwenye akili nyingi, Benjamin Saunders.
Hilo ndilo lililotokea, baada ya siku mbili, taarifa zikatolewa kwamba alama za
vidole vya Benjamin vilikuta katika mwili wa Todd, yaani kabla ya kumchoma
sindano, alimkaba kooni na kumuua na ndipo alipofanya mambo mengine likiwepo
lile la kumchoma sindano ya madawa ya kulevya ili ionekane kwamba alikuwa
amejiovadozi.
Hakukuwa na mtu aliyejua sababu ya Benjamin kuwaua watu maarufu, wengi
waliuliza, kwenye mitandao wakatoa maoni yao lakini hakukuwa na mtu
aliyefahamu lolote lile juu ya sababu ya Benjamin kuwaua watu maarufu na kisha
kuacha noti za fedha mbalimbali karibu na miili yao.
“Ila kwa nini anawaua watu maarufu?’ aliuliza mwanamke mmoja.
“Hata mimi sifahamu! Kwanza nashangaa...”
“Halafu nasikia huyu Benjamin mwenyewe ana akili sana darasani.”

103
“Hata mimi nimesikia hivyohivyo na watu walipokwenda, wakakuta kweli ana
akili sana, inawezekana ndiyo ikawa sababu ya kuwasumbua polisi na wananchi
kumtia nguvuni,” alisema jamaa mmoja.
Bado watu walitakiwa kumtafuta Benjamin lakini hakukuwa na yeyote aliyempata,
kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya dola milioni ishirini na tano ambazo zilikuwa ni
zaidi ya bilioni hamsini kilitolewa lakini bado majibu yalikuwa yaleyale kwamba
mitaani hakuonekana kabisa.
Maofisa wa FBI walikuwa na kazi kubwa, hakukuwa na aliyeamini kwamba
mpaka muda huo Benjamin hakuwa amepatikana. Taarifa zilizopelekwa katika
meza ya mkuu wa kitengo chao zilisema kwamba walitakiwa kupewa muda zaidi
kwani inawezekana kulikuwa na mtu hatari ambaye alikuwa akimlinda Benjamin
ili asiingie katika mikono yao.
“Kwa hiyo tumeshindwa?” aliuliza mkuu wa FBI, Bwana Connery Gibson.
“Hapana!”
“Sasa mbona hapatikani?”
“Ngoja tuendelee nadhani kuna kipindi tutampata tu.”
Hakukuwa na muda mwingine wa kupoteza, kama kusubiri, walisubiri kwa kipindi
kirefu lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale, kuna kipindi walijiona kama
kushindwa hivyo walitakiwa kuwasiliana na Shirika la Kijasusi la FBI ili
wawasaidie kwani huyu Benjamin, japokuwa walijua kwamba hakuwa polisi au
mtu yeyote mwenye uwezo wowote wa kijeshi lakini alikuwa mgumu mno
kupatikana.
Walichokifanya ni kujiongeza tu, wakawagawa vijana wao katika miji mingine
kama Los Angeles, Miami, Texas na sehemu nyingine ili kuhakikisha Benjamin
anapatikana haraka iwezekanavyo.
“Nadhani hatotushinda tena, si ndiyo?”
“Tutegemee hilo mkuu!”
****
Harry alichanganyikiwa, hakuamini kile alichokuwa amekiona kwamba muigizaji
maarufu duniani kwa kipindi hicho, Todd Lewis aliuawa ndani ya gari lake huku

104
wauaji hao wakitaka kuionyeshea dunia kwamba alijiovadozi madawa ya kulevya
kitu ambacho hakikuwa kweli kabisa.
Kilichomchanganya zaidi ni alama za vidole zilizopatikana ndani ya gari lile na
hata katika mwili wa Todd ambazo zilionyesha kwamba ni Benjamin ndiye
aliyefanya mauaji hayo.
Hapo ndipo alipoamini kwamba Benjamin hakuhusika katika mauaji, kulikuwa na
watu wengine waliokuwa wakiyafanya huku wakiweka alama za vidole vyake
katika kila tukio walilolifanya.
Alimwangalia Benjamin mara mbilimbili, hakuamini kilichokuwa kimetokea,
alimuonea huruma sana kwamba inawezekana vipi mtu auwe na kisha kuweka
alama za vidole vyake? Alimuuliza Benjamin lakini mwanaume huyo alimwambia
ukweli kwamba hakujua kitu chochote kile.
“Sifahamu!” alisema Benjamin.
“Kuna kitu unajua!”
“Harry! Sifahamu chochote, huyu mzee Seppy ndiye anahusika, yaani ni lazima
dunia ijue kwamba yeye ndiye anahusika, vinginevyo, nitahukumiwa kwa mauaji
ambayo sikuyafanya,” alisema Benjamin.
“Tutatoa vipi taarifa polisi? Watakukamata!”
Huo ndiyo ulikuwa mtihani mwingine, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya,
hawakuwa na ushahidi wa kutosha hivyo kama wangekosea sehemu moja basi
lingekuwa tatizo kubwa kwao, walitakiwa kujipanga ili hata kama watakwenda
kutoa taarifa polisi basi kusiwe na tatizo lolote lile.
David ndiye alikuwa na ushahidi kamili lakini bado kulikuwa na kitu kimoja
kilichokuwa kikiwatatiza, kila mauaji yalipotokea, kulikuwa na fedha zilizokuwa
zikiachwa, zile fedha zilimaanisha nini? Kila walichojiuliza, walikosa jibu.
“Sijui zinamaanisha nini, ila kama nikipewa muda, nitaweza kufahamu tu, kuna
kitu,” alisema Benjamin huku akionekana kama mtu aliyekuwa akijifikiria sana.
“Hili ndilo la msingi, sidhani kama hata FBI watakuwa wanajua maana, huu
utakuwa ni ujumbe, ujumbe gani sasa? Hebu tuhangaike mpaka tufahamu,”
alisema Harry.

105
Wote wakakubaliana na kuingia kazini kuhakikisha wanajua kwanza maana ya zile
fedha za noti zilizokuwa zikiwekwa katika mauaji yaliyokuwa yakitokea.

Moyo wa Bwana Seppy haukuridhika kabisa, japokuwa aliendelea kufanya mauaji


lakini uwepo wa Benjamin ulimkosesha amani kabisa. Alikosa furaha kabisa, kuna
kipindi alikuwa akikaa chumbani kwake na kujifikiria sana.
Mtu huyo alikuwa muhimu sana, kila kilichokuwa kikiendelea, aliona kama
Benjamin alikifahamu hivyo kama mtyu huyo asingekufa haraka iwezekanavyo
basi ilikuwa ni lazima kujulikana na hivyo kumletea matatizo katika maisha yake.
Hakuwa na mfariji yeyote yule zaidi ya demu wake mwenye asili ya Urusi
aliyeitwa Maria Kontekov, msichana mrefu, mrembo mwenye macho ya bluu
ambayo yaliwachanganya wanaume wengi kipindi hicho.
Mara kwa mara alikuwa akionana na huyu msichana wake, alioa na kubahatika
kupata watoto wawili lakini kipindi kirefu cha maisha yake alipenda kukaa na
Maria zaidi ya mke wake ambaye naye umri ulikwenda sana kama alivyokuwa.
Nyumbani hakukulalika, kama alitaka kuonana na vijana wake, alikuwa na jumba
jingine la kukutaniana na kupanga vitu vingine. Alipokuwa na mawazo mengi
kama kipindi hicho, kimbilio lake pekee lilikuwa Maria ambaye alikuwa akitoka
Urusi na kwenda Marekani, wanafanya mambo yao na kisha kurudi huko.
Fedha iliongea, Maria hakuwa akiongea chochote mbele ya Bwana Seppy, alipata
chochote alichokitaka lakini kwa sharti kwamba hakutakiwa kuwa na mwanaume
yeyote zaidi yake.
Hilo, kwa Maria wala halikuwa tatizo, alikuwa radhi kumridhisha mzee huyo tu
kwani kitu pekee alichokihitaji kilikuwa ni fedha tu. Alipewa fedha za kutosha na
hata pale ambapo alikuwa na fedha nyingi, nyingine akaongezewa, akaunti yake
benki ikajaa fedha nyingi, akanunuliwa jumba la kifahari jiji Moscow nchini Urusi,
akanunuliwa magari ya kifahari pamoja na kufunguliwa biashara kubwa.
Mawazo juu ya Benjamin yalipomzingua kichwani mwake, harakaharaka
akamwambia Maria afike haraka iwezekanavyo nchini Marekani. Hakukuwa na
umbali mkubwa kutoka Marekani mpaka Urusi lakini mzee huyo akaamua
kumtumia ndege yake na hatimaye wakutane jijini New York, wazungumze kama
kawaida yao na kuingia chumbani kufanya mambo yao.

106
Ndani ya saa tatu, tayari msichana huyo alikuwa mikononi mwake, walikuwa
chumbani, wakafanya kila kitu huku muda mwingi mzee huyo akihitaji kuchuliwa
mgongo wake kitu ambacho wala hakikuwa tatizo kwa Maria.
“Kuna nini mpenzi?” aliuliza Maria kwa sauti ndogo iliyojaa mahaba.
“Hakuna kitu kipenzi!”
“Hapana! Huwezi kunidanganya, ninakujua, nimekaa nawe kipindi kirefu,
unapokuwa kwenye mawazo, najua, hebu niambie, tatizo nini,” alisema Maria
huku akiwa kifuani mwa Bwana Seppy.
“Hakuna kitu!”
“Kweli?”
“Ndiyo mpenzi! Hebu nichue kidogo mgongo,” alisema mzee huyo, haraka sana
Maria akaanza kazi hiyo.
Siku hiyo walishinda chumbani tu, Bwana Seppy alijisikia amani moyoni mwake,
msichana huyo ndiye alikuwa kila kitu katika maisha yake, ilikuwa ni rahisi
kugombana na mkewe ila si Maria, hata kama ungetaka kumchukiza, mtongoze
Maria, alikuwa radhi kukuua ila si kama ambavyo ungemtongoza mkewe wa ndoa.
Wiki nzima Bwana Seppy hakurudi nyumbani, alikuwa akijifariji na Maria tu
chumbani. Fedha ilikuwa kila kitu, ilibadilisha kila muonekano wa kitu, kile
kilichokuwa hakiwezekani, ilikifanya kiwezekane, tena kwa urahisi kabisa.
Maisha yalikuwa ni ya raha na starehe, vijana wake waliendelea na kazi kubwa ya
kumtafuta Benjamin huku yeye akiwa hotelini akila raha kabisa. Hakutaka kusikia
lolote kuhusu familia yake, hakutaka kusikia kuhusu watoto wake, Jericho na
Vanessa, kitu alichotamani kusikia ni kuhusu Maria tu.
“Umekuwa mnyonge kwa kipindi kirefu sana, naomba leo usiku unitoe mtoko,”
alisema Maria kwa sauti ndogo huku akiwa kifuani mwa mzee Seppy.
“Unataka twende wapi?”
“Tukaangalie mechi ya kikapu, leo La Lakers anacheza,” alisema msichana Maria.
“Sawa! Tutakwenda kutazama, ninataka uwe na furaha kipindi chote mpenzi,”
alisema mwanaume huyo.

107
Haraka sana Bwana Seppy akampigia simu Dracula na kumwambia kwamba siku
hiyo alihitaji kwenda kuangalia mchezo wa kikapu baina ya Timu ya LA Lakers na
Memphis ambazo zilitarajiwa kucheza katika mchuano mkali wa timu za
Magharibi.
Hilo wala halikuwa tatizo, haraka sana Dracula akaenda kukata tiketi mbili, tena
katika upande wa VIP, alipozipata akampelekea mzee huyo hotelini kitu
kilichomfanya Maria kuwa na furaha sana.
“Nakupenda mpenzi,” Maria alimwambia Bwana Seppy.
“Nakupenda pia.”
Walilala mchana huo na usiku wakaamka na kuanza safari ya kwenda katika
uwanja wa La Lakers, Staple Center. Ndani ya gari ulikuwa ni muda wakupeana
mahaba motomoto. Japokuwa Bwana Seppy alikuwa mtu mzima kama baba yake
lakini halikuwa tatizo kwa Maria kubadilishana naye mate na kufanya mambo
mengine ya aibu, alifanya hivyo kwa sababu nyuma ya pazia kulikuwa na fedha.
Walipofika, wakataremka na kisha kuingia ndani. Ilikuwa vigumu kumgundua
Bwana Seppy kwamba alikuwa yeye, kichwani alivalia kofia, akavaa fulana kali,
jinzi na raba zilizokuwa na chata ya Nike, kwa muonekano, alionekana kama
kijana mwenye miaka thelathini.
Wakaingia mpaka katika sehemu ambayo walitakiwa kukaa. Huko, ni watu wenye
fedha ndiyo waliokuwa wakikaa, tiketi zao zilikuwa ni dola elfu themanini ambazo
zilikuwa ni sawa na milioni mia moja sitini, na watu walilipia bila malalamiko.
Kule walipokuwa wakikaa, mbele yao kulikuwa na kioo kikubwa, walikaa kibosi
na wote waliokuwa huko walikuwa na wasichana wao wadogo, ni mambo ya
kifuska ndiyo yaliyokuwa yakiendelea huko.
Katika kipindi hicho, mchezaji aliyekuwa na jina ambaye alikuwa akichipukia
alikuwa Paul McKenzie, miongoni mwa wachezaji waliokuwa mwiba kipindi
hicho, huyu jamaa alikuwa akitisha. Alikuwa na umri wa miaka kumi na tisa tu
lakini uwezo wake ulikuwa mkubwa kana kwamba alikuwa na miaka thelathini.
Mpaka katika kipindi hicho, alivunja rekodi nyingi mno na rekodi moja tu ndiyo
alikuwa akiifukuzia, ya kufunga pointi nyingi kama ilivyokuwa kwa mkongwe wa
mchezo huo, Michael Jordan, au MJ kama alivyojulikana na watu wengi.

108
Mafanikio makubwa ndiyo yaliyomfanya kujituma kila siku. Timu ya La Lakers
ikapata mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya mkali mwingine, Shaq O’Neil ambaye
alistaafu kipindi kilichopita huku akiwa ameipa timu hiyo mafanikio makubwa.
Mbali na uwezo mkubwa aliokuwa nao, Paul alikuwa na sura nzuri, aliwavutia
wasichana wengi, katika kipindi hicho ndicho alisemekana kuwa mwanaume
mwenye sura nzuri zaidi ya wanaume wote chini ya jua. Wanawake walimpenda
kwa sababu hakuwa na makuu, hakuwa na kashfa yoyote ile, kitu alichokuwa
akikiangalia ni mpira wa kikapu ambao ulimpa magari, majumba ya kifahari na
vitu vingine vingi, hata akaunti yake benki ilikuwa ikisomeka na kutuna kila siku.
Wakati Tv kubwa iliyopachikwa ukumbini hapo ilipomuonyesha Paul kwa karibu,
tena kwa kumvuta, msichana Maria akashtuka, hakuamini kama kweli duniani
kulikuwa na mwanaume mwenye sura nzuri kama yule aliyemuona.
Mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, akajikuta akianza kuangukia
katika penzi la mwanaume huyo, hakuishia kuangalia kwenye televisheni ile tu,
akayatupa macho yake uwanjani, kila aliposhika mpira, wanawake walisikika
wakipiga kelele hali iliyoonyesha kwamba hata wanawake waliokuwa humo
walimpenda mno.
Moyo wake ukamia mno, kwa jinsi Paul alivyokuwa mzuri, hakutaka kumuona
mwanamke yeyote anakuwa naye zaidi yake yeye, hakutaka kubaki kule juu,
akajifanya kuvurugwa na tumbo hivyo alitakiwa kwenda chooni, Bwana Seppy
hakuwa na wasiwasi wowote ule, akamruhusu msichana huyo aende huko.
Maria akaanza kutembea kwa harakaharaka, akashuka chini mpaka kule katika viti
vya chini kabisa, alitaka kumuona Paul kwa ukaribu kabisa kwani alihisi telvisheni
ile ilikuwa imemdanganya, alipofika huko, akajipenyeza katikati ya watu mpaka
katika kiti ambacho hakikuwa na mtu na kukaa hapo.
Macho yake yakaanza kumwangalia vizuri Paul, aliuona uzuri wa mwanaume
huyo, wanawake ambao walikuwa jirani yake, muda wote walikuwa wakimsifia
mwanaume huyo, tena huku wakimuita kila alipogusa mpira.
Maria alikasirika, alitamani kuwaambia wasimuite kwani alimuona kama kuwa
mpenzi wake. Wakati mpira ukiwa umepigwa na kuelekea nje katika upande
aliokuwa Maria na wanawake wengine.
Paul akaufuata, wanawake wote wakasimama, wakazidi kuliita jina lake, Paul
akawaangalia, tabasamu pana lilikuwa usoni mwake, alipomuona msichana Maria

109
tu, hakufanya kitu chochote zaidi ya kumkonyeza kitu kilichowafanya wanawake
wote waliokuwa hapo kumuonea wivu msichana Maria, kwani kwa muonekano tu,
hata naye Paul alionekana kuvutiwa naye, ila hakujua kama angeweza kuonana
naye baada ya mechi hiyo kumalizika.
Maria hakutaka kuondoka, akanogewa kukaa mahali hapo, baada ya dakika kumi
na tano ndipo akakumbuka kwamba alikuwa ameaga anakwenda chooni hivyo
kama angechelewa zaidi kungekuwa na tatizo, harakaharaka akasimama na kuanza
kuondoka kuelekea juu alipomuacha mwanaume wake.
Alipandisha ngazi harakaharaka mpaka juu ambapo akaingia katika chumba hicho.
Bwana Seppy wala hakuwa na wasiwasi, ndiyo kwanza akawa anazungumza na
wazee wenzake wenye fedha, Maria akakaa katika kiti na kuendelea kuufuatilia
mchezo huo.
Mawazo yake yalikuwa kwa Paul tu, kila aliposhika mpira, alitetemeka, mapigo
yake ya moyo yalimdunda mno, mwanaume huyo alimtetemesha kupita kawaida.
Hata Paul mwenyewe, muda mwingi alikuwa akiangalia katika sehemu aliyokuwa
Maria, pale, hakuweza kumuona, hakujua kama mwanamke huyo aliondoka au
alitoka na angerudi baada ya muda fulani.
Kipindi cha kwanza kilipofika, wakiwa mapumziko, Maria alikuwa akimfuatilia
Paul kwa karibu kabisa, macho ya Paul hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na
kule, kwa muonekano wake tu ilionyesha kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani,
alitamani kujitokeza lakini alishindwa kabisa kufanya hivyo.
“Au nimfuate?” alijiuliza huku akiendelea kumwangalia mwanaume huyo.
Paul alichanganyikiwa, tayari moyo wake ulitekwa na msichana huyo, hakuwa
radhi kuendelea kucheza na wakati moyo wake ulichanganyikiwa, kipindi cha pili
hakuingia, alifikiria kuingia kipindi cha tatu.
Alikaa kwenye benchi lakini macho yake yaliendelea kutalii huku na kule,
alitamani kumuona msichana huyo ambaye aliutetemesha moyo wake kwa kipindi
hicho.
Wanawake walikuwa wakimuita lakini hakuwa na habari nao, alikuwa akimtaka
msichana mmoja tu, alikuwa Maria ambaye hakujua aliondoka na kuelekea wapi
na wala hakujua kama alikuwa akifuatiliwa na msichana huyo.

110
Mchezo uliendelea, La Lakers hawakuwa wakali kipindi hicho, staa wao alikuwa
nje, ila kipindi cha tatu kilivyoingia, akaingia, timu ikapata uhai na kujikuta
akifunga pointi nyingi sana.
Mpaka mchezo unamalizika, bado Paul alikuwa na mawazo tele, alishindwa
kuvumilia, hakutaka kuingia chumbani kuzungumza na wachezaji wenzake, alibaki
akizunguka huku na kule.
Watu wakaanza kutoka, naye akatoka uwanjani, alipofika kwenye korido tayari
kwa kwenda chumbani walipokuwa wenzake, akakutana na mchezaji mwenzake
wa akiba, akamfuata na kisha kumpa kikaratasi kilichokuwa na namba,
alipoiangalia namba hiyo, hakuifahamu ila chini kulikuwa na jina la Maria,
akaisevu na kisha kuangalia picha katika mtandao wa Whatsapp, picha aliyokutana
nayo, ilikuwa ni ya msichana huyo aliyekuwa akimtafuta sana kipindi hicho.
Msichana Maria.
****
Mpaka mechi inamalizika, Maria alichanganyikiwa, hakujua ni kwa jinsi gani
angeweza kuwasiliana na Paul. Hakutaka kubaki humo, alijua kwamba kama
angeendelea kubaki asingeweza kuonana na mwanaume huyo, ilikuwa ni lazima
ateremke ili aende akaonane naye huko huko.
Hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kumuaga Bwana Seppy kwamba anakwenda
tena chooni kwani tumbo lilikuwa likimsumbua. Mzee Seppy hakuwa na tatizo,
alikuwa amenogewa na maongezi na mzee mwenzake tena huku wakinywa pombe
kali, akamruhusu.
Maria akaondoka kuelekea chini, huko, alimsubiri Paul lakini hakutokea, hakujua
nini cha kufanya, kitu kilichomjia kichwani mwake ilikuwa ni lazima amwachie
namba mwanaume huyo ili kama kumtafuta, amtafute kwani kuonana naye tayari
ilionekana kuwa tatizo kubwa.
Akachukua kikaratasi, akaandika jina lake na namba yake ya simu. Kwa sababu
hakumuona mwanaume huyo, alichokifanya ni kumgawia mchezaji mmoja na
kumwambia kwamba ampe Paul kwani alitaka kuwasiliana naye, hilo halikuwa
tatizo, mchezaji huyo akachukua kikaratasi hicho na kumuahidi kwamba angeweza
kumpa.
“Naomba usisahau, nakuomba,” alisema Maria.
“Usijali! Nitaifikisha...”

111
“Nakuomba usikose...tafadhali nakuomba!”
“Usijali dada!”
“Nitashukuru sana!”
****
Muda wote Maria alikuwa akiiangalia simu yake, alikuwa na presha kubwa ya
kuona akipigiwa na Paul na kumwambia kwamba alikuwa akimpenda kama
alivyokuwa akimpenda.
Hakuwa na raha, hata ndani ya gari alikuwa kimya kabisa, moyo wake ulikuwa
kwenye mawazo tele, hakumfikiria Bwana Seppy tena, mtu aliyekuwa akimfikiria
alikuwa Paul tu ambaye aliuburuza vibaya moyo wake.
Bwana Seppy aliyaona mabadiliko, akajaribu kuuliza sababu ya mpenzi wake
kuwa vile lakini wala hakupata jibu lolote lile, ilimuuma kwani kati ya watu ambao
hakutaka kabisa awaone wakiwa na majonzi mioyoni mwao, alikuwa huyu Maria.
Alijaribu kumuuliza tatizo lilikuwa nini lakini hakupewa jibu la kuridhisha kwani
msichana huyo alimwambia wazi kwamba alikuwa poa na hakukuwa na tatizo
lolote lile.
Upande wa pili, bado Paul alikuwa akikiangalia kikaratasi kile, japokuwa hakuwa
akimfahamu msichana huyo lakini akahisi kwamba ndiye yule aliyemuona
uwanjani wakati mechi ikiendelea na ghafla akapotea.
Naye kuanzia kipindi hicho akawa na mawazo tele, alikuwa na namba lakini
alihofia kuipiga na kuzungumza na msichana huyo. Alibaki akijiuliza, kujiuliza
huko hakukuisha mpaka alipolala usiku.
Kesho, kitu cha kwanza kabisa kukikumbuka kilikuwa ni namba ya Maria,
hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kumpigia simu
Maria. Simu ilianza kuita, ikaita, hapohapo ikakatwa.
Mara ya kwanza alihisi kwamba ni network, alichokifanya ni kupiga tena na tena
lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu ilikatwa kila alipopiga, na baadaye
alipojaribu kuipiga tena, haikuwa ikipatikana kitu kilichouumiza moyo wake
kupita kawaida.
****

112
Nahitaji kurudi nyumbani nikapumzike mpenzi,” alisema Maria huku
akimwangalia Bwana Seppy usoni.
“Mbona mapema jamani! Si ulisema unakaa mwezi mzima?” aliuliza Bwana
Seppy huku akionekana kushtuka.
“Kuna mambo mengi natakiwa kufanya, ila wiki ijayo nitarudi tena, si unajua
mama atakuwa amenikumbuka sana,” alisema Maria.
Kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, ilikuwa ni vigumu sana kugundua kwamba
msichana huyo alikuwa na lake kichwani. Aliiona simu ngeni ikiingia, haikuwa
kawaida simu ngeni kuingia katika simu yake, akajua kwamba moja kwa moja
mpigaji alikuwa Paul.
Alitamani kupokea lakini ilishindikana kabisa kwani alikuwa jirani na Bwana
Seppy hivyo kuikata kila ilipokuwa ikiita. Baadaye alipoona kwamba inasumbua
sana na angeweza kushtukiwa, akaizima kabisa.
Moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria zaidi
ya kumpigia mwanaume huyo ili azungumze naye na ikiwezekana wakutane
sehemu, hata kama angemuomba penzi, kwake hakuwa na kinyongo, alikuwa
tayari kumpa kwani hakukuwa na mwanaume aliyekuwa akimpenda kama
ilivyokuwa kwa Paul.
Alihakikisha anaondoka siku hiyo, hakutaka tena kuendelea kukaa nchini
Marekani, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuondoka. Hilo wala halikuwa tatizo,
Bwana Seppy akakubaliana naye, hivyo mchana wa siku hiyo akapanda ndege
ambayo ilimrudisha mpaka nchini Mexico.
“Nitakukumbuka mpenzi,” alimwambia Bwana Seppy.
“Nitakukumbuka pia, ila usisahau kurudi wiki ijayo!”
“Nitarudi tu,” alisema Maria na kisha kummwagia mabusu mfululizo.
Wakati ndege ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Benito Juarez
nchini Mexico, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumpigia simu Paul. Wakati
simu inaita, moyo wake ulikuwa na presha kubwa, alitamani kuisikia sauti ya
mwanaume huyo. Simu wala haikuita sana, ikapokelewa.
“Nazungumza na nani?”

113
“Mimi! Maria, yule binti wa uwanjani,” aliitikia Maria huku akiachia tabasamu,
fikra zake zilimwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa akimwangalia.
“Nimefurahi sana kusikia sauti yako! Kumbe upo Mexico?” aliuliza Paul kwa
mshangao, kwani code ya simu ile ilionyesha kwamba mpigaji alikuwa Mexico.
“Ndiyo!”
“Ninatamani nikuone, naweza kuja?”
“Naweza!”
Walizungumza mengi, siku hiyo, Paul hakutaka kabisa kukaa nchini Marekani,
kutoka hapo mpaka Mexico haikuwa mbali, siku hiyohiyo akapanda ndege na
kuelekea huko ambapo alipokelewa na msichana huyo kisiri.
Hawakutaka kwenda kwenye hoteli kubwa kwani walihisi kwamba huko
wangeshtukiwa mapema, kwa kuwa ilikuwa usiku, wakaenda katika hoteli ya
chini, tena uswahili kabisa ambapo walikuwa na uhakika kwamba wasingeweza
kugundulika kwa urahisi.
“Ninakupenda Paul,” alisema Maria huku tayari wakiwa kitandani.
“Nakupenda pia na ndiyo maana nimesafiri kuja huku, kwa ajili yako tu,” alisema
Paul huku akimmwagia mabusu mfululizo msichana huyo.
“Una mchumba?” aliuliza Maria.
“Hapana! Wewe?”
“Ninaye, ni mzee mmoja hivi, sina jinsi, ilinipasa kuwa naye,” alijibu Maria.
“Kwa nini?”
“Basi tu! Maisha yalinipasa kuwa na mzee huyo.”
“Yupi?”
“Bwana Seppy!”
“Yule bilionea?”
“Ndiyo! Ila moyo wangu haupo kwake kabisa, ninakupenda Paul, ninataka uupoze
moyo wangu!” alisema Maria kwa sauti ya kulalamika kimahaba.
“Akija kujua je?”

114
“Sidhani na ndiyo maana ninataka tufanye vitu kisiri sana.”
“Basi hakuna tatizo!”
Usiku huo ulikuwa ni usiku wa raha, hakukuwa na karaha, walianza kubusiana
hapa na pale na mwisho wa siku wakajikuta wakiwa watupu kabisa, kilichofuatia
ni miguno ya mahaba na kelele za chumbani kitandani humo.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kila kitu, mara kwa mara walikuwa wakikutana,
safari za Paul kwenda nchini Mexico hazikukata, mara kwa mara alikuwa akisafiri
kwenda huko.
Kwa Maria, naye alichanganyikiwa mno, kila alipopata nafasi ya kwenda nchini
Marekani, alihakikisha anakutana na Paul na kufanya mambo yao kimyakimya
pasipo mtu yeyote kufahamu.
Safari za Maria kwenda nchini Marekani kumuona Bwana Seppy zikaanza
kupungua, kila alipoambiwa aende, akajifanya kuwa bize. Bwana Seppy akaanza
kupatwa na machale, haikuwa kawaida kabisa, Maria alionekana kubadilika, alihisi
kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
Kuna kipindi aliamua kumtafuta Maria, simu yake haikuwa ikipatikana lakini
alipojaribu kumtumia ujumbe katika Mtandao wa Whatsapp, meseji ilikwenda na
kusomwa.
“Upo wapi?” aliuliza Bwana Seppy.
“Nyumbani!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mpenzi! Mama anaumwa!”
“Haupo Marekani?”
“Mimi? Marekani! Nije bila taarifa! Inawezekana vipi?” aliuliza Maria.
“Kweli upo Mexico?”
“Ndiyo mpenzi! Halafu nimekumisi sana, nataka wikiendi hii nije kukuona,”
aliandika Maria.
“Sawa! Karibu,” alijibu Maria. Hakujua kama Bwana Seppy alikuwa akimfuatilia
hatua kwa hatua kupitia simu yake kwa kitu kiitwacho GPS na alijua kwamba

115
kipindi hicho hakuwa nchini Mexico, alikuwa Marekani katika Hoteli ya
Greenland iliyokuwa Kaskazini mwa Jiji la New York.
“David, niambie nini kinaendelea,” alisema Benjamin kwenye simu.
“Nimeendelea kufuatilia mawasiliano kwa njia ya simu,” alijibu David.
“Umegundua nini?”
“Kuhusu nini?”
“Juu ya hizo fedha, unajua hizi zitakuwa na maana yake, nini umegundua?”
aliuliza Benjamin huku siku ikiwa sikioni mwake, Harry alikuwa pembeni
akimsikiliza.
“Bado! Nitaendelea kufuatilia, hata mimi ninahisi kwamba kuna kitu,” alisema
David.
Hilo ndilo lililowasumbua kichwa kipindi hicho, hawakujua ni kitu gani
walitakiwa kufanya kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, ilionyesha kabisa kwamba
huyo muuaji ambaye waliamini ni Bwana Seppy alitumia noti zile za fedha huku
akiwa na maana yake.
Benjamin akakata simu na kisha kwenda kutulia kwenye kochi, kichwa chake
kilikuwa na mawazo mengi, moyo wake ulimwambia wazi kwamba kulikuwa na
maana kubwa juu ya zile noti lakini hakujua zilikuwa na maana gani.
Alisimama kutoka pale alipokuwa na kuanza kutembea huku na kule, alikuwa na
akili nyingi, alitumia muda wake mwingi kufikiria maana ya fedha zile lakini bado
hakupata jibu lolote lile.
Alichokifanya ni kuchukua kalamu na karatasi na kisha kuziandika fedha zile kwa
majina, alikumbuka, ilikuwa ni noti ya Yen, Dola, Paundi na Euro. Akaziandika
zote na kisha kuanza kuziangalia kwa makini.
“Umegundua nini?” alimuuliza Harry.
“Bado sijagundua lolote lile,” alijibu Harry.
“Kweli?”
“Ndiyo!”

116
Mtu aliyekuwa akihusika na mauaji walikuwa wakimfahamu, alikuwa Bwana
Seppy lakini tatizo lilitokea ni kwamba hawakujua sababu iliyompelekea kutumia
fedha zile kuficha kilichokuwa kikiendelea.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Benjamin ni kuandika jina la mzee huyo,
tena yote mawili, David Seppy na kisha kuanza kuyaangalia kwa umakini kabisa.
“Harry, hebu yaangalie haya majina vizuri,” alisema Benjamin, akayatumbulia
macho.
“Umegundua lolote?”
“Hapana!”
“Kweli?”
Alichokifanya Harry ni kuyaangalia tena majina yale, tena kwa wakati huu kwa
umakini mkubwa kabisa, aliangalia vya kutosha lakini hakubahatika kitu.
Alichokifanya Benjamin ni kulifuta jina la David, likabaki jina la Seppy.
“Na hapo?”
“Bado sijapata kitu.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Benjamin akatoa tabasamu pana, hakuamini kama mwisho wa siku angepata jibu
kutokana na zile fedha zilizokuwa zikiwekwa kila tukio lilipokuwa likifanyika.
Harry alikuwa kimya, kila alipomwangalia rafiki yake, alikuwa akitabasamu tu
kitu kilichompa wakati mgumu kama kweli alijua maana ya fedha zile au la.
“Inamaanisha nini?” aliuliza Harry.
“Ni jina lake, alitaka kila mtu ajue kwamba yeye ndiye anafanya mauaji haya,”
alijibu Benjamin.
“Unamaanisha Bwana Seppy?”
“Ndiyo!”
“Hebu nifafanulie...”
“Sawa. Hebu niandikie hizi alama za fedha kwenye karatasi...”
“Alama kivipi?”

117
“Kama dola ina alama gani?”
Alichokifanya Harry ni kuandika kama alivyoambiwa, fedha zote, yaani dola, euro,
rubui na paundi, na alama zake zote kisha kumuonyeshea Benjamin. Benjamin
akaichukua karatasi hiyo, akachukua kalamu na kuanza kumuonyesha.
“Alama hii ni alama ya dola ($), ukitoka hapa, kuna alama hii pia (£) ambayo ni
paundi, ukiachana na hiyo, kuna hii (₽), hii ni fedha ya Urusi, ila pia kuna (¥) hii ni
fedha kutoka nchini Urusi, hizi zimekuwa fedha ambazo amekuwa akizitumia mara
kwa mara. Sasa ziunganishe, yaani $+£+₽+¥ ambayo unapata $£₽¥, yaani SEPPY.
Bado hujapata kitu hapo?” aliuliza Benjamin baada ya kutoa maelezo ya kutosha.
Harry alipigwa na mshangao, hakuamini kile kilichokuwa kimemaanishwa juu ya
fedha zile zilizokuwa zikiwekwa kila tukio lilipokuwa likitokea. Moyoni mwake,
aliamini kwamba Benjamin alikuwa na akili sana kwani kugundua kitu kama
hicho, kwamba mtu alikuwa akifanya mauaji na kuweka fedha kama alama ya jina
lake, hakika ilimshangaza sana.
“Mmh! Nimekuelewa, na hii noti ya euro vipi?” aliuliza Harry.
“Aliiweka kwa kuwa kitambo jina lake lilikuwa Seepy, ila baadaye akaamua kutoa
E moja na kubaki Seppy, kwa hiyo alitumia euro kama kuongezea alama yake
ambayo ni € ili watu wasielewe kile alichokimaanisha,” alijibu Benjamin huku uso
wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Nimekuelewa. Kilichobaki?”
“Ni kuwataarifu polisi tu, akamatwe na afungwe gerezani,” alijibu Benjamin.
Wakagongesheana mikono na kuahidiana kwamba asubuhi ya siku inayofuatia,
ilikuwa ni lazima kwenda katika kituo cha polisi kutoa taarifa.
****
Moyo wa Bwana Seppy uliwaka kwa hasira, hakuamini kile kilichokuwa
kikiendelea kwamba msichana aliyekuwa akimpenda, alikuwa akitembea na
mwanaume mwingine.
Hakuamini, alichanganyikiwa, kila wakati alikuwa akitembea peke yake ndani ya
nyumba yake huku akizungumza kama kichaa. Hakumjua mwanaume aliyekuwa
akitembea na mpenzi wake ila aliambiwa kwamba mara kwa mara wawili hao
walikutana katika hoteli moja iitwayo Greenland iliyokuwa huko New York.

118
Alichokifanya ni kuwaandaa vijana wake, ilikuwa ni lazima mwanaume huyo
ajulikane ili kama kumuua amuue kwani asingeweza kumuua msichana Maria kwa
kuwa alikuwa akimpenda mno kutoka ndani ya moyo wake.
Siku ziliendelea kusogea mbele, alijua ukweli lakini kila alipomwambia Maria
kwamba alikuwa mdanganyifu katika uhusiano wao msichana huyo alimwambia
wazi kwamba hakuwa akimdanganya kabisa na alimpenda yeye tu, nyuma yake
hakukuwa na mwanaume yeyote yule.
Bwana Seppy akajipanga, ilikuwa ni lazima ajue ukweli wa kile kilichokuwa
kikiendelea. Kijana wake wa kompyuta bado alikuwa na kazi kubwa ya
kuhakikisha anafahamu mahali anapokuwa msichana huyo ili aweze kutoa taarifa
inayotakiwa kutolewa.
“Mkuu! Maria amekuja tena Marekani,” Tim, kijana wa kompyuta alimwambia
bosi wake.
“Amekuja lini?”
“Leo hii! Ila hayupo New York.”
“Yupo wapi?”
“Los Angeles kwenye hoteli iitwayo Scandnavia Hill,” alijibu Tim.
Bwana Seppy hakutaka kuchelewa, harakaharaka akawatuma vijana wake
waliokuwa Los Angeles kwenda kuhakikisha kile walichokuwa ameambiwa. Huku
nyumbani, moyo wake ulizidi kuuma, alimpenda sana Maria, hakutaka kumpoteza,
aliuburudisha moyo wake vilivyo hivyo kumuwia vigumu sana kumfanya lolote
baya.
Alijua kwamba msichana huyo alihitaji uhuru wake, alitakiwa kuwa na mwanaume
mwingine kwani yeye, kwa jinsi alivyokuwa na umri mkubwa, kitandani hakuwa
na uwezo mkubwa wa kufanya mapenzi, kama msichana ambaye damu inachemka,
ilikuwa ni lazima kutafuta kijana machachari, mwenye nguvu ya kufanya mapenzi
hata kwa zaidi ya saa mbili kitandani.
Yote hayo alikubaliana nayo lakini tatizo likawa ni kusalitiwa huku akijua kwamba
anasalitiwa. Hakutaka kuona hilo likitokea na hivyo alikuwa tayari kwa kila kitu,
alimgharamia sana msichana huyo, hakukuwa na mtu mwingine aliyeingiza mkono
katika kumpa fedha na kumjengea nyumba, sasa iweje mwanaume mwingine
amchukulie msichana huyo?

119
Kitu alichokuwa akikisubiria ni kuhusu mwanaume aliyekwenda na mpenzi wake
hotelini, hakujua kama alikuwa na fedha kuzidi yeye, hakujua kitu chochote kile,
kitu alichokisubiri kilikuwa ni taarifa tu.
Vijana hao walifanya uchunguzi wao katika hoteli hiyo tena kwa kutumia
wahudumu ambao walilipwa vizuri na kutoa jibu kwamba msichana Maria alikuwa
na mwanaume, supastaa wa mchezo wa kikapu, Paul McKenzie, hivyo kumpa
taarifa mzee huyo.
“Nani? Paul?” aliuliza mzee huyo huku akionekana kutokuamini.
“Ndiyo!”
“Hapana!”
“Ndiyo mzee, tumeangalia vizuri! Ni yeye,” alisema kijana wake.
Bwana Seppy alipigwa na butwaa, hakuamini alichokisikia, alikuwa shabiki namba
moja wa Paul, alimpenda sana kwa kuwa alionyesha kuwa kijana anayesaka
mafanikio kwa nguvu kubwa, kila siku katika maisha yake alipambana, alimpenda
lakini mwisho wa siku ndiye huyohuyo aliyekuwa akitembea na mpenzi wake.
Kabla ya kutoa uamuzi wa nini cha kufanya, akatulia kwenye kochi lake, akaanza
kufikiria kitu kwamba ni uamuzi gani alitakiwa kuuchukua, machozi yalikuwa
yakimbubujika, alijifikiria kwa muda na mwisho wa siku, akaamua kutoa uamuzi
wake.
“Muueni kama wengine,” alisema mzee huyo.
“Hakuna tatizo!”
“Kesho, Dracula atasafiri mpaka huko kuja kuwasaidia kukamilisha kazi hiyo,”
alisema Bwana Seppy.
“Sawa bosi.”
****
Hawakuwa wakijua kama walikuwa wakifuatiliwa, Paul na Maria walikuwa
chumbani huku wakiyafurahia maisha kama kawaida yao. Hawakutaka kwenda
katika Hoteli ya Greenland jijini New York bali walichokifanya ni kubadilisha
hoteli na kwenda Los Angeles na kuingia katika Hoteli ya Scandnavia Hill.

120
Huko, walikuwa huru, waliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye
angefahamu kama walikuwa humo. Hawakujua kama wahudumu wa humohumo
ndiyo waliwapa taarifa vijana wa Bwana Seppy hasa baada ya kupewa kiasi
kikubwa cha fedha.
Walijiachia usiku kucha na ilipofika asubuhi, Paul hakutaka kuondoka, bado
alitamani kuwa na mpenzi wake huyo kwa kuwa hakukuwa na mechi yoyote na
hata mazoezi hayakuwepo pia.
“Naomba ukae huku wiki nzima,” alisema Paul huku akimwangalia Maria usoni.
“Kwa ajili yako tu, hakuna tatizo!”
Kweli, hicho ndicho alichokifanya, hakutaka kurudi nchini Mexico, aliamua kukaa
humohumo hotelini huku Bwana Seppy akiwasiliana naye kwa kutumia Whatsapp
tu, tena huku akiwa ameifunga simu yake.
Hakujua kama mzee huyo alifahamu kila kitu, tayari Dracula ambaye alikuwa
akisubiriwa alikwishafika na hivyo ni mipango ya mauaji ndiyo yaliyotakiwa
kufanyika.
“Hakuna taarifa zilizosambaa kwamba tunakuja?” aliuliza Dracula, alikuwa
akimuuliza dada wa mapokezi.
“Hakuna!”
“Sawa. Chukua kwanza hii,” alisema Dracula huku akimpa bahasha iliyokuwa na
dola elfu ishirini.
Wakapewa kadi iliyokuwa na uwezo wa kufungua kila mlango ndani ya hoteli
hiyo, kitu kingine walichokifanya ni kuwasiliana na watu wa IT ambao walikuwa
wakisimamia kamera zote zilizokuwa humo hotelini, kuhitaji ulinzi wa hali na mali
ili wasiweze kukamatwa, kwani walitaka kuingia ndani wakati msichana Maria
alipokwenda bafuni kuoga.
Walichokifanya ni kuondoka na kwenda katika korido iliyokuwa na chumba hicho,
walipoifikia, kwa kuwa kwenye mlango kwa chini kulikuwa na nafasi fulani hivyo
wakachukua kamera ndogo waliyokuja nayo na kuipitisha kwa chini ambayo
iliunganishwa na kichuma kirefu, kamera ile ambayo kama zilizokuwa zikitumiwa
na FBI, zikaanza kuonyesha kilichokuwa kikiendelea ndani, tena huku wao
wakifuatilia kila kitu kwa nje.
“Wamelala....” alisema jamaa mmoja.

121
“Usingizi?”
“Hapana! Wamekumbatiana,” alijibu jamaa huyo, baada ya dakika kadhaa,
wakamuona msichana Maria akiamka, akachukua taulo lake, akampiga Paul kibao
cha kimahaba na kuelekea bafuni kuoga.
“Amekwenda kuoga.”
“Nani?”
“Msichana...”
“Basi tuingieni,” alisema Dracula huku kila kitu alichokuwa ameambiwa awe
nacho akiwa nacho. Hakukuwa na muda wa kupoteza, hicho ndicho walichokuwa
wakikitaka, kwa haraka sana, wakaingia ndani kwa kutumia kadi ile waliyopewa
na mhudumu kama funguo ya kuingia katika chumba chochote kile.

122
SURA YA TANO

HAWAKUTAKA kupoteza muda hapo mlangoni, walishakubaliana kuingia


ndani hivyo wakaingia. Paul aliyekuwa kitandani, akakurupuka lakini Dracula
akamuwahi palepale kitandani na kumbana vilivyo, akauziba mdomo wake, kijana
mwingine akasogea na kumshikilia miguu ili asilete purukushani kitandani pale.
Walipoona wameweza kumzuia, mwingine akaufuata mlango wa bafuni na
kuufunga kwa nje ili Maria asiweze kutoka ndani ya bafu lile. Huku kitandani,
Dracula akachukua mto na kisha kuufunika uso wa Paul ili amuue kwa kumziba
pua na mdomo, akose hewa na kufa, ndivyo ilivyotokea.
Paul alikukuruka na kukuruka lakini ilishindikana kabisa, hakuweza kujinasua
kutoka katika mikono ya wanaume hao waliokuwa wamemkandamiza vilivyo
kitandani pale, zoezi hilo lilifanyika kwa dakika tano mpaka walipohakikisha
amekufa hapo kitandani ndipo Dracula alipotoa mto ule na kumwangalia Paul.
“He is gone,” (Amekufa) alisema Dracula huku uso wake ukianza kutoa tabasamu
pana.
Kama kawaida yao, Dracula akachukua bomba la sindano lililokuwa kwenye
mfuko aliokuwa nao, akalitoa, akachomeka sindano, akavuta madawa ya kulevya
yaliyokuwa katika majimaji na kisha kumchoma Paul huku akimshikiza kwa
mkono wake mwingine, alipohakikisha imekuwa poa, akachukua kiplastiki
kilichokuwa na alama za vidole vya Benjamin na kisha kumuwekea katika shingo
ya mwili wa Paul na katika sehemu zingine za mwili, kabla ya kuondoka, pia
wakaweza zile noti ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya utambulisho wa mauaji yale.
Hawakutaka kupoteza muda, waliingia harakaharaka na kufanya kazi yao haraka
sana, walipomaliza, wakaondoka zao huku wakiwa wamekamilisha kazi hiyo kwa
mafanikio makubwa.
“How was the work?” (Kazi ilikwendaje?) aliuliza Bwana Seppy kwenye simu.
“Simple as usual,” (Nyepesi kama kawaida) alijibu Dracula.
Ndani ya bafu lile, wakati mlango ukifungwa, Maria hakuwa akijua kitu chochote
kile, hakujua kama kulikuwa na watu walikuwa wameingia na kumuua mpenzi
wake.

123
Aliendelea kuoga huku akiimba, alipomaliza, akachukua taulo lake akajifuta na
kisha kuufuata mlango. Akakishika kitasa ili aufungue, mlango haukuwa
ukifunguka, ulionyesha kwamba ulifungwa kwa nje.
Akaanza kuugonga huku akiliita jina la Paul, mara ya kwanza alifikiri ni utani na
hata uitaji wake ulikuwa ni wa kiutani sana lakini mlango haukufunguliwa na wala
hakusikia sauti yoyote ile kutoka ndani ya chumba hicho.
“Paul, just open the door,” (Paul, fungua mlango) alisema Maria huku akiugonga
mlango ule lakini hali iliendelea kuwa kimya.
Aliendelea kusubiri kwa dakika thelathini, alipoona Paul hafungui mlango ndipo
alipoanza kuugonga kwa nguvu huku akikitekenya kitasa kile. Ilikuwa kazi kubwa
lakini hakuacha kwani pasipo kufanya hivyo, basi angeendelea kuwa ndani ya
chumba kile tu.
Alichukua dakika zaidi ya thelathini nyingine, kukipiga kitasa kile mpaka
kilipovunjika ndipo akafanikiwa kutoka ndani ya bafu lile. Alichokutana nacho
kitandani, hakuamini, mwili wa mpenzi wake, Paul ulikuwa tuli kitandani.
Maria hakuweza kuvumilia, akaanza kupiga kelele, wala hazikupita dakika nyingi,
mlango ukafunguliwa, watu wa kwanza kuufungua mlango hawakuwa wahudumu
bali walikuwa wageni kutoka katika vyumba vingine ndani ya hoteli hiyo.
Wao wenyewe wakapigwa na butwaa, walichokutana nacho, hawakuamini hata
mara moja, mwili wa Paul ulikuwa kitandani, alivyoonekana, ni kama mtu
aliyejiovadozi madawa ya kulevya kwani sindano ilikuwa mwilini mwake, katika
mkono wake wa kushoto, udenda ulikuwa ukimtoka.
Hakukuwa na mtu aliyeugusa mwili ule, wakapiga simu mapokezini ambapo
wahudumu wakafika haraka sana. Wao wenyewe hawakuamini kile walichokiona,
wakaona jambo la busara kumuita meneja wa hoteli ile ambaye haraka sana
akafika.
“Mungu wangu!” alisema meneja huku akionekana kutokuamini, hivyo kupiga
simu polisi.
Japokuwa hoteli hiyo ilikuwa na wahudumu wengi, lakini kulikuwa na mhudumu
mmoja ambaye alihusika, yeye ndiye aliyewapa kadi ya kufungulia mlango na hata
kuwaelekeza chumba alichochukua Paul na Maria.

124
Muda wote wakati watu wapo hapo chumbani, Maria alikuwa akilia tu, hakujua ni
kitu gani kilikuwa kimetokea, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makubwa.
Hakutoa maelezo yoyote yale kwani aliamini chochote kile ambacho angekisema
mahali hapo, kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angemuelewa.
Baada ya dakika kumi, polisi wakafika hotelini hapo, moja kwa moja
wakapandisha ngazi na kuanza kuelekea kule kilipokuwa chumba kile, kwa kuwa
kilikuwa ghorofa ya tatu, hawakuchukua muda mrefu, wkaafika.
“Nani alikuwa humu chumbani tofauti na marehemu?” aliuliza polisi mmoja.
“Mimi hapa!” alijibu Maria huku akijifuta machozi.
“Hakuwepo mwingine?”
“Hakuwepo.”
“Nini kilitokea?”
“Hata mimi sijui, nilikuwa naoga, nilipotoka, nikakuta hiki kilichotokea,” alisema
Maria.
Walichokifanya ni kumfunga pingu kwani yeye ndiye alikuwa mshukiwa namba
moja wa mauaji yale. Wakamchukua na kuondoka naye kwenda kituoni huku
polisi wengine wakiangalia kitu cha kufanya.
Waandishi wa habarai tayari walikuwa wamefika, hawakuamini kile kilichokuwa
kimetokea, mtu aliyekuwa amekufa chumbani humo, walimfahamu, alikuwa staa
mkubwa wa kikapu, alipendwa na wasichana wengi kutokana na uzuri wa sura
yake.
Hakuwa mtu wa kashfa, aliishi na watu vizuri, alipendwa kutokana na upole wake
pia. Siku hiyo, hakukuwa na aliyeamini kama kweli Paul alikuwa amekufa,
majonzi yasiyokwisha yakaikumba mioyo yao na hivyo watu haohao waliokuwa
ndani ya chumba hicho, wakaanza kusambaza taarifa hizo katika mitandao
mbalimbali ya kijamii.
Njia nzima Maria alikuwa akilia, polisi hawakutaka kusikia lolote lile,
kilichowaambia ni kwamba msichana Maria alikuwa akijua kilichotokea hivyo
walitaka kushirikiana naye ili kujua nini kilitokea.
Mauaji yale, yalikuwa yaleyale ambayo yalitokea kwa masupastaa waliopita.
Walikufa vilevile, wengi walihisi kwamba walijidunga madawa ya kulevya lakini

125
baada ya miili yao kuchunguzwa, wakagundua kwamba kulikuwa na mtu aliyeitwa
Benjamin ambaye ndiye alikuwa amehusika katika mauaji yale.
Hawakujua kuhusu Paul lakini bado mioyo yao iliwaambia kwamba inawezekana
muuaji alikuwa huyohuyo ambaye mpaka kipindi hicho hakuwa amepatikana
japokuwa alitafutwa sehemu yote nchini Marekani.
Kuna watu wengine walihisi kwamba Benjamin aliondoka na kukimbilia Mexico,
nchi iliyokuwa na wauzaji wengi wa madawa ya kulevya. Hakukuwa na dalili za
kupatikana kwake, kila watu walipokwenda huku na kule, hawakupata kitu.
Taarifa juu ya kifo cha Paul zikaanza kutangazwa kila sehemu, watu waliambiana
kwenye mitandao ya kijamii, kila mtu aliyezipata, hakuamini kama kweli
aliyekuwa ameuawa alikuwa Paul, yule mcheza kikapu mwenye jina, sura nzuri
aliyekuwa akifagiliwa na wasichana wengi.
“Hebu tuambie nini kilitokea,” alisema ofisa wa FBI ambaye alikuwa katika
chumba cha mahojiano na msichana Maria ambaye muda wote alikuwa akilia tu.
Pembeni mwa ofisa huyo, alikuwepo mwingine ambaye naye alivalia suti kama
aliyokuwa nayo.
“Sikumuua Paul,” alisema msichana Maria huku akiyafuta machozi yake.
“Nini kilitokea?”
Hapo ndipo Maria alipoanza kusimulia kile kilichotokea, hakutaka kuficha kitu,
alikamatwa na kitu pekee ambacho kingemuweka huru kwa wakati huo ni
kuzungumza ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Kwa hiyo muuaji haumfahamu?” aliuliza ofisa mmoja.
“Hapana! Simfahamu kabisa.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Polisi hawakutaka kumuachia Maria, ilikuwa ni lazima kumshikilia kwani
mshukiwa namba moja wa mauaji yale alikuwa yeye, akawekwa sero, huko,
alikuwa akilia sana, alijuta hatua aliyochukua ya kuwa na Paul na kwenda naye
katika hoteli ile.
Hapo ndipo lilipokuja jina la Benjamin. Aliwahi kusikia mastaa wengi wakiwa
wameuawa na mtu aliyeitwa Benjamin, hakumfahamu mtu huyo na hakujua

126
sababu iliyomfanya kuwaua mastaa. Alimchukia Benjamin ambaye kwa kipindi
hicho, alikuwa adui wa nchi nzima, yaani Enemy of the State.
****
Walipanga kwamba siku inayofuata ilikuwa ni lazima kwenda kituyo cha polisi na
kuwaeleza polisi juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Benjamin hakuwa muuaji,
hilo ndilo ambalo lingeweza kuzungumzwa kwani pasipo kufanya hivyo, Benjamin
alikuwa katika wakati mgumu.
Tayari Benjamin na Harry waliwasiliana na David na kumwambia juu ya kile
kilichotakiwa kufanywa, yaani piga ua ilikuwa ni lazima wakutane katika kituo cha
polisi kwani yeye ndiye alikuwa na mawasiliano ya Bwana Seppy, Dracula na
watu wengine katika upangaji wa mipango yao ya mauaji.
Wakakubaliana lakini ilipofika saa nne usiku wakapata taarifa zilizowashtua
kwamba supastaa wa mchezo wa kikapu, Paul McKenzie alikuwa ameuawa ndani
ya chumba cha hoteli, mauaji yake yalikuwa yaleyale, yaani kama Todd, Carter.
Walichanganyikiwa, hata kama majibu ya vipimo vya mwili ule havikutolewa,
walijua fika kwamba taarifa zingesema kwamba Benjamin ndiye aliyeua, yaani
kama ilivyokuwa katika mauaji mengine.
Hilo ndilo lililowafanya hata ule mpango wao wa kwenda kituo cha polisi
kuusitisha, ilitakiwa wajipange upya wajue ni kitu gani wangetakiwa kufanya
kwani pasipo kufanya hivyo, mambo yangekuwa mabaya zaidi.
“Tufanye nini?” aliuliza Harry.
“Dah! Hapa nimechanganyikiwa. Hebu subiri kwanza, naomba dakika kama tano
hivi peke yangu,” alisema Benjamin huku akionekana kuwa na mawazo mengi.
Harry akamuacha, Benjamin akasimama na kwenda chumbani, alihitaji muda wa
kuwa peke yake kwani kulikuwa na mengi ya kujifikiria, hakutaka kukurupuka
katika kufikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya.
“Nini cha kufanya?” alijiuliza huku akitembea huku na kule.
Alikuwa akiishi kwa hofu, hakuwa na amani, alijua kwamba kila kitu kilichokuwa
kikitokea, Bwana Seppy alijua kwamba ilikuwa siri, kwa sababu yeye mwenyewe
hakuwa na furaha, ilikuwa ni lazima hata Bwana Seppy naye akae akiwa na hofu
kama alivyokuwa yeye.

127
“Umefikiria nini?” aliuliza Harry baada ya kukaa kwa dakika kumi nzima.
“Sioni sababu ya Bwana Seppy kuwa na furaha na wakati mimi nina hofu, kwa
nini naye asiishi na hofu moyoni mwake?” aliuliza Benjamin.
“Unamaanisha nini?”
“Nataka niwasiliane naye!”
“Ben! Umechanganyikiwa?”
“Hapana! Hii ni njia ya kwanza, lazima akae kwa presha, ajue kwamba ninajua kila
kitu, yaani hapo ndipo tutafanikiwa, kwanza tutakusanya ushahidi wa kutosha
kwani atafanya maamuzi ya ghaflaghafla kitu ambacho kinaweza kuwa ushindi
mkubwa,” alisema Benjamin.
“Umefikiria nini mpaka kusema hivyo?”
“Wala usijali! Nipe muda, nataka kwenda kumpigia simu, nitatumia simu ya
barabarani,” alisema Benjamin.
Jambo alilozungumza halikumuingia akilini kabisa, hakujua alimaanisha nini,
hakuona kama kulikuwa na sababu ya kufanya kile alichotaka kukifanya ila kwa
sababu yeye mwenye mhusika ndiye aliamua kufanya hivyo, hakuwa na jinsi.
Alichokifanya Benjamin ni kuchukua namba ya simu ya Bwana Seppy na kisha
kuondoka nayo kwenda mtaani. Kwa sababu ilikuwa usiku wa saa tano hakukuwa
na mtu yeyote aliyemtambua kwani mbali na mwanga hafifu pia alivalia kofia
kubwa aina ya pama.
Hakutaka kutumia simu ya mtaani hapo, alijua kwamba mara watakapogundua
simu ambayo ilitumika ilikuwa ni lazima kumtafuta kuanzia hapo. Alichokifanya
ni kupanda basi na kwenda katika mji mwingine ambao ulikuwa mbali na hapo,
kama kilimeta thelathini kutoka hapo.
Huko ndipo alipotafuta kibanda cha simu za mitaani, alikipata katika kituo cha
mafuta cha Total, akakifuata na kuanza kupiga namba ya Bwana Seppy. Wala simu
haikuita muda mrefu, ikapokelewa.
“Bwana Seppy hapa, nani mwenzangu?”
“Benjamin Saunders...” alijitambulisha Benjamin, Bwana Seppy aliyekuwa upande
wa pili, akashtuka.

128
****
Bwana Seppy akahisi kama mtu akija kumkaba kooni mwake, alichanganyikiwa
sana kusikia sauti ya Benjamin, mwanaume aliyekuwa akimsumbua katika kipindi
chote hicho, mtu ambaye alitaka afe haraka iwezekanavyo.
Mwanaume huyo alizungumza kwa kujiamini, hakuonekana kuwa na wasiwasi
wowote ule mpaka wakati mwingine Bwana Seppy kuhisi kwamba Benjamin
alikuwa na ulinzi wa kutosha huko alipokuwa.
“Ni lazima ufungwe maisha yako yote, ni lazima unyongwe kwa mauaji
unayoendelea kuyafanya,” alisema Benjamin kwa sauti ya juu iliyosikika vizuri
masikioni mwa Bwana Seppy.
“Hahaha!” akabaki akicheka.
“Cheka, ni vizuri kucheka kwa sababu siku ya hukumu yako inakaribia,” alisema
Benjamin.
“Nani atajua? Wewe ndiye muuaji, vipimo vya madaktari na polisi vimeonyesha
alama za vidole vyako, unahisi nani atakuamini?” aliuliza Bwana Seppy kwa
dharau.
“Uwepo wa fedha katika kila tukio!”
“Hilo linaweza kuwa ushahidi tosha?”
“Ndiyo!”
“Zina maana gani?”
Benjamin hakutaka kuchelewa, hapo ndipo alipomwambia mzee huyo maana ya
fedha zile zilizokuwa zikiwekwa katika kila eneo la tukio la mauaji lilipofanyika.
Bwana Seppy akachanganyikiwa, hakuamini kama kungekuwa na mtu ambaye
angegundua kile kilichokuwa kimetokea kwamba Benjamin agundue maana ya
uwekaji wa fedha zile.
Hilo lilikuwa jambo la kwanza ambalo hakutaka mtu yeyote afahamu, si mke
wake, hata Dracula mwenyewe ambaye alikuwa akimtumia katika mauaji
hakumwambia maana ya kuweka fedha zile katika kila tukio la mauaji aliyokuwa
akiyafanya.

129
Hakutaka kuzungumza kitu, alichokifanya ni kukata simu na hapohapo kumpigia
simu Dracula, kitu cha kwanza kabisa kumuuliza ni mahali gani walipofikia tangu
waanze kumtafuta Benjamin ambaye bado aliendelea kutafutwa kila kona.
“Ndiyo tunaendelea, kuna nini kwani?” aliuliza Dracula.
“Amenipigia simu!”
“Amekupigia simu?”
“Ndiyo! Hebu niambie ukweli! Hivi atapatikana kweli?” aliuliza Bwana Seppy,
kwa kumsikiliza tu, alinekana kuchanganyikiwa, hakuwa sawa kama siku
nyingine.
“Atapatikana tu! Tuvute subira.”
****
Baada ya kuzungumza na Bwana Seppy na simu kukatwa, Benjamin akatulia huku
akimwangalia Harry, alikuwa akitabasamu tu, mbele yake aliyaona mafanikio
makubwa, alikuwa akifanikiwa kwa kila kitu alichokuwa akikifanya.
Walichokifanya, usiku huohuo ulikuwa ni wa kutoka na kwenda katika kituo cha
polisi, huko, wangezungumza ukweli juu ya kile kilichotokea kwani tayari
ushahidi walikuwa nao.
Wakatoka na kuanza safari ya kwenda huko. Japokuwa walikubaliana kwenda
huko saubuhi lakini wakaiona mbali, ilikuwa ni lazima ifanyike siku hiyohiyo.
Walitembea mitaani, Benjamin hakutaka kuuficha uso wake kwani hata kama
angekamatwa, bado alikuwa akienda kituo cha polisi. Walipishana na watu wengi,
cha ajabu kabisa watu hawakumgundua kutoka na mwanga hafifu hasa katika
kipindi hicho cha usiku.
“Tukifika, ni kutoa maelezo, hata kama nitapelekwa mahakamani, nitaeleza
ukweli,” alisema Benjamin huku wakiendelea kwenda huko.
Walitembea kwa mwendo wa haraka, wakati wakikaribia kufika, simu ya Harry
ikatoa mlio kwamba kulikuwa na ujumbe ulikuwa umeingia, harakaharaka
akaichukua simu yake na kuangalia nini kilikuwa kimeingia, ilikuwa ni habari
iliyoingizwa kutoka katika programu ya Shirika la Habari la CNN ambayo ilieleza
kwamba kulikuwa na mauaji yalikuwa yametokea katika Hoteli ya Scandnavia
Hill.

130
“Hebu subiri...” alisema Harry.
“Kuna nini?” aliuliza Benjamin.
“Paul McKenzie ameuawa,” alisema Harry, Benjamin akashtuka.
“Unasemaje?”
Hawakutaka kuendelea na safari, walichokifanya ni kwenda pembeni na kuanza
kuisoma habari hiyo. Kwa jinsi mauaji yalivyotokea, walijua fika kwamba mzee
huyo ndiye aliyehusika kwani mauaji yale yalifanana sana na yale mengine
yaliyowahi kutokea.
Walibaki wakiangaliana tu, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya kwani kwa
jinsi hali ilivyoonyesha, basi polisi wangeanza kumtafuta tena kwa nguvu kubwa.
Hawakuwa na sababu ya kuendelea mbele, safari yao iliishia hapo na hivyo kurudi
nyumbani. Vichwani mwao walikuwa na mawazo tele, walijua fika kwamba mara
baada ya mwili ule kupimwa, ilikuwa ni lazima alama za vidole vya Benjamin
vionekane kwa sababu ndivyo Bwana Seppy alivyokuwa akifanya kwenye kila staa
aliyekuwa akiuawa.
“Kwa hiyo tufanye nini?” aliuliza Hans.
“Subiri, nafikiri mpaka asubuhi nitakuwa na majibu, wala usijali,” alijibu
Benjamin.
****
Msako mkubwa wa Benjamin ulikuwa ukiendelea, kamera ziliongezeka mitaani
kwa ajili yake, ilikuwa ni lazima apatikane kwani kitu alichokuwa amekifanya,
hakikuweza kuvumilika, ilikuwa ni lazima akamatwe na kufikishwa katika
vyombo vya sheria na kuhukumiwa kwa yale yote aliyokuwa ameyafanya.
Maofisa wa FBI walikuwa wakihangaika, walitoa uangalizi kwa watu waliohusika
na kamera mpya za barabarani ambazo walikuwa wamezifunga ili kuhakikisha
Benjamin anakamatwa na mambo mengine kuendelea. Watu waliowekwa kwa ajili
ya kuziendesha kamera zile, kila siku hawakuona kitu, waliendelea kufuatilia kwa
wiki nzima lakini hakukuwa na mtu aliyeitwa Benjamini, yaani hata dalili zake
kuwepo sehemu fulani, hazikuwepo.

131
“Na jana uliangalia?” aliuliza Bwana Swan, kiongozi aliyepewa kusimamia
kamera hizo mpya ambazo zilifungwa sehemu nyingi nchini Marekani na taarifa
kupelekwa moja kwa moja makao makuu.
“Ndiyo!”
“Na hamjamuona?”
“Ndiyo! Ila bado tunaendelea...”
Hivyo ndivyo alivyoambiwa. Wakati mwingine aliona kama hakukuwa na
umuhimu wa kuwa na watu hao kwani alijitahidi kuwapa maneno mengi ya
kuwafanya waone kwamba kulikuwa na umuhimu wa kumkamata mtu huyo lakini
hiyo wala haikusaidia kabisa.
Ilimuumiza, hakupenda kuwasimamia watu ndiyo kazi ifanyike, kwa
kumwangalia, alionekana kuwa mwanaume mpole, na hivyo ndivyo alivyokuwa ila
alipotaka kitu fulani kifanyike, alikuwa kwenye presha kubwa sana.
“Hebu angalieni kamera vizuri, haiwezekani sehemu nzima asionekane,” alisema
Bwana Swan.
“Sawa mkuu!”
Hakukuwa na kitu kilichobadilika, yaliendelea kuwa yaleyale kwamba Benjamin
hakuonekana. Hawakujua alikuwa watu, ilikuwa vigumu sana mtu kutafutwa na
nchi nzima, FBI halafu asionekane, hilo lilikuwa jambo gumu sana.
Wakati mwingine walihisi kama Benjamin alikimbia nchi, akaenda kujiunga na
kundi la Kiislamu la ISIS, wakati mwingine waliisi kwamba Benjamin alikwenda
kujiunga na Kundi la Born To Kill la nchini Cuba, yaani kumkosa Benjamin nchi
nzima lilikuwa jambo lisilowezekana kabisa.
“Bosi...njoo uone hii,” alisema kijana mmoja, alikuwa mbele ya kompyuta yake,
tangu asubuhi hakuwa ameondoka ofisini, yeye ndiye aliyepambana kwa nguvu
zote kumtafuta Benjamin kila kona.
Alianzia jijini New York, akaenda Washington, akaenda Los Angeles na sehemu
nyingine kwa kutumia kamera zilizowekwa lakini kote huko hakuambulia kitu.
Dakika za mwisho kabisa, alimuona mtu kama Benjamin, alipouona uso wake,
akatafuta picha ya Benjamin na kuambatanisha na picha ile aliyoiona kwenye

132
kamera, maneno yaliyotokea ni 100 MATCH, yaani imefanana kwa asilimia mia
moja, hapo akajiona kuwa mshindi, ilikuwa ni lazima kumpa taarifa Bwana Swan.
“Yupo wapi?”
“Nawaona vijana wawili wakiwa wamesimama, mmoja yupo ndani ya kibanda cha
simu na mwingine yupo nje, Benjamin ni huyu aliyekuwa ndani, aliyekuwa nje
simfahamu,” alisema kijana huyo aliyejiita Genius.
Alichokisema Bwana Swan ni kuunganishwa kwa kompyuta ile katika televisheni
kubwa iliyokuwa ndani ya chumba hicho huku akimtaka kila ofisa wa FBI
aliyekuwa humo ndani aangalie kile kilichokuwa kikiendelea.
Sehemu iliyoandikwa Location ikiwa na maana ya eneo ilionyesha kwamba
ilikuwa ni Macberth 25W, sehemu ambayo ilikusanya watu wenye maisha ya kati
katika Jiji la Boston, huko ndipo ambapo huyo Benjamin alipokuwa.
Kumuona tu hawakuridhika, waliamini kwamba wangeweza kutorokwa kwani
huyo Benjamin hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo. Walichokitaka ni
kumfahamu mtu ambaye alikuwa naye, alikuwa nani na alikuwa akiishi wapi.
Hiyo wala haikuwa kazi kubwa, alichokifanya Genius ni kuivuta sura ya Harry,
akaruhusu sura kadhaa zianze kupita katika kompyuta yake huku ikiitafuta sura ya
mwanaume huyo aliyekuwa pamoja na Benjamin.
Ilikuwa kazi kubwa, kila mtu aliyekuwa ndani ya jengo hilo alikuwa kimya,
Bwana Swan alibaki akiwa amesimama, mkono wake mmoja ulikuwa mfuko na
mwingine aliupeleka katika shavu lake, alikuwa akifuatilia kwa ukaribu sana.
Zaidi ya sura milioni mbili zilipita kwa kasi kubwa mno, ndani ya dakika ishirini,
kompyuta ikasimama katika sura moja na kujiandika 100 MATCH kwamba sura
ya mtu huyo ilifanana na huyu aliyekuwa ametafutwa.
“Ni nani huyo?” aliuliza Bwana Swan, jamaa mwingine akachukua kalamu na
karatasi.
“Anaitwa Harry Hoff, kijana mwenye asili ya Ujerumani, anaishi jijini Boston,
nyuma namba 278 katika Mtaa wa Vivien View Barabara ya St. Peters, anasoma
katika Chuo cha Kikuu cha Harvard,” alisema Genius, maelezo ya wananchi wote
wa Marekani, data zao zilikuwa zimechukuliwa kutokana na vitambulisho wa taifa
walivyokuwa wamepewa.

133
“Safi sana...ninahitaji maofisa kumi waende huko anapoishi Harry. Hakuna kuua,
mnachotakiwa ni kuwapata wote wakiwa hai,” alisema Bwana Swan na maofisa
wote kuitikia na hivyo kuanza kwenda huko.
****
Vivian hakuwa na raha, moyo wake ulikuwa na majonzi tele, hakuamini kile
kilichotokea kwamba mpenzi wake alikuwa akitafutwa kila kona huku sababu
kubwa ikiwa ni kufanya mauaji.
Alijua kwamba hakuwa muuaji bali kulikuwa na mtu ambaye alifanya mauaji,
hakumfahamu na hivyo ndivyo alivyowaeleza maofisa wa FBI lakini hakukuwa na
mtu aliyemuelewa.
Aliruhusiwa kwenda nyumbani, hakukukarika, kila alipokaa, alimkumbuka mpenzi
wake tu. Maofisa wa FBI hawakutaka kumuacha, walihakikisha wanamfuatilia kila
hatua.
Nje ya nyumba hiyo kulikuwa na gari lao, ndani ya gari hilo kulikuwa na
kompyuta nyingi pamoja na kamera zilizokuwa na uwezo wa kupiga picha na
kuona kile kilichokuwa kikiendelea ndani.
Mbali na hivyo, waliendelea kufuatilia mpaka mawasiliano ya simu zake, kuanzia
ile ya mezani mpaka ya mkononi kwani waliamini kwamba msichana huyo
alikuwa na nafasi ya kuwasiliana na mpenzi wake ambaye alikuwa akitafutwa kwa
udi na uvumba kipindi hicho.
“Nini kinaendelea?” aliuliza Bwana Swan ambaye aliwagawa vijana wake sehemu
mbalimbali.
“Bado tunaendelea kufuatilia, tunamuwekea ulinzi wa kutosha huyu msichana
wake,” alijibu ofisa mmoja.
“Simu zake?”
“Tumeziwekea ulinzi pia.”
“Sawa.”
****
Maofisa wa FBI wakaelekea nyumbani kwa Harry, walikwenda na gari lao,
ilikuwa asubuhi sana muda ambao waliamini kwamba hata watu hao hawakuwa
wameamka, walitaka kuwavamia na kisha kumchukua mtu wao ambaye aliwatesa

134
sana huku usiku uliopita tu akiwa amefanya mauaji katika hoteli moja huko Los
Angeles.
Walifika katika nyumba hiyo huku wakiwa na bunduki zao mikononi mwao,
waliamini kwamba wangeweza kumpata kwani kwa jinsi walivyoona siku
iliyopita, wawili hao wangeendelea kuwa ndani ya hiyo nyumba na ilionyesha
kwamba kwa kipindi kirefu Benjamin alikuwa mahali hapo ila tu hawakuwa
wakijua hilo.
Walipofika nje ya nyumba hiyo, kitu cha kwanza kabisa walichokifanya ni
kuizunguka nyumba hiyo na ndipo mmoja wao akaanza kuugonga mlango na
kutaka kufunguliwa.
Nyumba ilikuwa kimya, japokuwa alipiga kelele na kusema “FBI, FBI” lakini
hakukuwa na mtu yeyote aliyefungua mlango. Hawakutaka kuendelea kubaki hapo
ndani, walikuwa na hofu kwamba inawezekana Benjamin angekimbia hivyo
walichokifanya ni kuingia ndani ya nyumba hiyo kwa kuuvunja mlango.
Bunduki zilikuwa mikononi mwao, walioingia hawakuwa wao peke yao bali
kulikuwa na askari wa SWAT ambao kazi yao ilikuwa ni kuvamia sehemu
zilizokuwa na hatari, yaani kule ambapo kulikuwa na watu waliokuwa na silaha
nzito, walitumika hao kwa ajili ya kuwalegeza kwanza.
Ndani, hakukuwa na mtu, walijaribu kuingia humu na kule, walitembea huku na
kule lakini hawakukuta mtu yeyote. Mwisho kabisa wakaamua kukifuata chumba
kimoja, kilikuwa chumba cha Harry, walipokifikia, wakaingia ndani,
hawakumuona Benjamin, mtu pekee waliyemuona humo alikuwa Harry.
“You are under arrest....” (Upo chini ya ulinzi...) alisema ofisa mmoja huku wote
kwa pamoja wakimnyooshea bunduki Harry ambaye aliamka na kuanza
kuwaangalia.
“What the hell is going on?” (Nini kinaendelea?) aliuliza huku akiwaangalia.
Hawakutaka kumjibu swali lake, walichokifanya ni kumshika na kumlaza chini
kisha kumfunga pingu huku wakimtaka kuwaambia mahali alipokuwa Benjamin.
“Benjamin, I don’t know where he is,” (Benjamin, sijui yupo wapi) alisema Harry
huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.
“Tell us where he is,” (Tuambie yupo wapi)

135
“I dont know men, he left last night,” (Sijui jamani, aliondoka usiku uliopita)
alijibu Benjamin, kwa kumwangalia tu, alionyesha dhahiri kwamba
aliwadanganya.
****
Benjamin alikuwa kama mtu mwenye machale, usiku wa siku hiyo hakulala,
alibaki macho huku akiwa na wasiwasi mno, alijua kama kulikuwa na kitu
ambacho kingetokea hivyo asingeweza kulala kabisa.
Alikesha, mpaka mwanga unaanza kuchomoza asubuhi, alikuwa macho, akatoka
kitandani na kwenda jikoni ambapo akaandaa kahawa na kisha kuelekea sebuleni
kuangalia televisheni.
Kipindi hicho televisheni ndiyo ilikuwa faraja yake, hakuwa na cha kufanya,
hakuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote kile, alipokuwa kwenye televisheni,
ndiyo ulikuwa muda wa kujua kitu gani kilikuwa kikiendelea katika ulimwengu
aliokuwa akiuogopa.
Mara kwa mara alijiona kwenye televisheni, alikuwa mtu maarufu kwa sababu ya
matukio yaliyokuwa yametokea. Watu wengi walihojiwa, kilio chao kilikuwa ni
kumuona Benjamin akikamatwa na kufikishwa mahakamani na kisha kushtakiwa
kwa makosa ambayo dunia nzima ilijua kwamba aliyafanya.
“Ila kwa nini huyu mzee anafanya hivi?” alijiuliza pasipo kupata jibu.
Akasimama, akaanza kutembea ndani ya sebule ile huku akiwa na mawazo lukuki,
aliongea peke yake kama kichaa, akatoka pale alipokuwa mpaka katika dirisha
kubwa, akafungua pazia na kuanza kuangalia nje.
Alitamani kuwa huru, aliwaona watu wakitembea barabarani huku wakiwa
wamejiachia, alitamani na yeye kuwa vile lakini ilishindikana kabisa, hakuweza
kuwa huru kama watu wale walivyokuwa huru kipindi kile.
Wakati akiwa amesimama katika dirisha lile ndipo alipoliona gari moja likija na
kusimama karibu na eneo la nyumba ile barabarani. Kwanza akaanza kuwa na
wasiwasi, hakutaka kujipa uhakika kwamba watu waliokuwa ndani ya gari hilo
walikuwa watu wazuri, akagundua kwamba kulikuwa na kitu.
Hakutaka kuwa na wasiwasi mwingi, akasubiri kuona ni watu gani wangeteremka
kutoka ndani ya gari lile. Wakati akiwa amelikodolea macho, likatokea gari jingine
ambalo kwa ubavuni liliandikwa S.W.A.T.

136
Harakaharaka wanajeshi waliokuwa na mavazi yaliyoandikwa S.W.A.T wakatoka
ndani ya gari lile, walikuwa na bunduki kubwa hasa AK 47 ambazo ndizo zilikuwa
maalumu kwa kazi yao.
Mavazi yao, yalikuwa yale mazito ambapo tumboni mpaka kifuani walikuwa na
vazi jingine lililokuwa na uwezo wa kuzuia risasi. Benjamin alipowaona watu hao,
hakutaka kusubiri, alijua fika kwamba walikuwa mahali hapo kwa ajili yake.
Hakutaka kujiuliza, wanajeshi wale na FBI tayari walianza kuelekea kule
ilipokuwa nyumba ile, aliamini kwamba kama angekwenda jikoni na kutoka nje
kupitia mlango wa nyuma, angechelewa na hivyo kukamatwa, wazo pekee
lililomjia kichwani ilikuwa ni lazima aingie ndani ya ‘chimney’.
Sebuleni hapo kulikuwa na sehemu maalumu ambayo nyumba nyingi za Marekani
na Ulaya au hata sehemu zenye baridi kali huweka kama jiko kwa ajili ya kuchoma
kuni na kuleta moto ambapo moshi wake ulipita katika bomba kubwa lililokwenda
juu ya bati na kupotelea huko.
Yeye alitaka kuingia katika bomba hilo, halikuwa kubwa sana lakini lilitosha kwa
mwili wake kuenea kwani hakuwa mnene ila alikuwa mrefu. Hakutaka kuchelewa,
haraka sana akaelekea katika sehemu ile, kulikuwa na kuni, akazisogeza pembeni
na kisha kuanza kujiingiza, hakuanza kukiingiza kichwa, alibinuka na kuanza
kuiingiza miguu yake kwenda kwenye bomba lile kwa juu.
Ilikuwa kazi kubwa lakini haikumsumbua sana, hakuchukua sekunde nyingi,
akafanikiwa kuingia ndani ya bomba lile na kutulia, masikio yake yalikuwa ni
hapo sebuleni, tangu maofisa wa FBI walipoanza kuugonga mlango na kuuvunja,
yeye alikuwa ndani ya bomba lile sebuleni pale huku akisikiliza kila kitu
kilichokuwa kikiendelea.
Maofisa wa FBI walijua fika kwamba Harry alikuwa akijua mahali alipokuwa
Benjamin ila hakutaka tu kuwaambia ukweli. Walichokifanya ni kumchukua na
kumpeleka kituoni.
Huko wakamuingiza ndani ya chumba cha mahojiano na kuanza kuzungumza
naye, walitaka aeleze ukweli mahali alipokuwa Benjamin, vinginevyo
wangemfanya kitu kibaya.
“Nina haki ya kusikilizwa pia,” alisema Benjamin kwani tayari aliona maofisa
wale walikuwa wamekasirika.
“Sawa. Benjamin yupo wapi?”

137
“Sijui! Kwani nyie wa nini?”
“Amefanya mauaji!”
“Hapana! Benjamin hakuwahi kuua,” alisema Harry.
“Usibishane na sisi, aliua na hata jana aliua pia,” alisema ofisa huyo.
“Jana kuna mauaji yalitokea huko Los Angeles, wote mnasema kwamba Benjamin
ndiye aliyehusika, si ndiyo?” aliuliza Harry.
“Ndiyo!”
“Sawa! Kwenye maelezo yenu mlisema kwamba jana usiku mliniona nikiwa naye,
ilikuwa saa tano usiku, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Mauaji yalitokea saa nne na nusu, si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Sasa jamani! Huyo Benjamin awe ameua saa nne na nusu usiku, atatumia usafiri
gani kutoka Los Angeles mpaka hapa Boston kwa mwendo wa nusu saa? Kwa
ndege haiwezekani, alitumia usafiri gani sasa?” aliuliza Harry huku akiwaangalia
maofisa wawili aliokuwa nao humo ndani.
“Labda niwaulize kitu kimoja. Nyie mnaamini Benjamin ni yupi? Yule aliyefanya
mauaji huko Los Angeles au huyu aliyekuwa pamoja nami?” aliuliza Harry.
Maofisa wakabaki wakiangaliana tu.
Alichokisema Harry kilikuwa ni ukweli mtupu. Kutoka Los Angeles mpaka hapo
Boston ilikuwa ni mwendo wa saa moja na nusu kwa ndege, sasa ilikuwaje huyo
Benjamin afanye mauaji Los Angeles halafu ndani ya nusu saa aonekane jijini
Boston? Hilo likawapa wakati mgumu maofisa hao, hawakujua washike lipi, kama
Benjamin alionekana hapo Boston majira ya saa tano usiku, je aliyefanya mauaji
saa nne na nusu usiku huko Los Angeles alikuwa nani? Wakabaki na maswali
kibao.
****
Dunia ilikuwa ikijiandaa kwa ajili ya kumuona msichana mrembo ambaye
angeibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Dunia ambayo kwa kipindi hicho
yalitegemewa kufanyika jijini Texas nchini Marekani.

138
Watu walitaka kushuhudia ni msichana yupi angeibuka mshindi kwani wasichana
wote ambao walitegemewa kushiriki walikuwa wale warembo, waliowavutia watu
wengi nchini mwao.
Kila mtu anawa na uhakika kwamba msichana Angelica Sanchez kutoka nchini
Mexico angechukua taji hilo lililokuwa likishikiria na mrembo kutoka nchini
Venezuel, Maria alejandro.
Kwa kumwangalia, Angelica alikuwa msichana mrembo mno, alikwenda juu, hipsi
zake zilionekana vilivyo, alikuwa na sura nzuri uliopendezeshwa na vishimo viwili
vilivyokuwa mashavuni mwake. Muda wote, alikuwa kwenye tabasamu pana kana
kwamba hakujua maana ya kukasirika.
Huyo ndiye alikuwa gumzo kipindi hicho. Tangu alipochukua taji la urembo nchini
Mexico, kila mtu alitokea kumpenda, kampuni mbalimbali zinazojihusisha na
mambo ya mitindo ikamtafuta, yeye alijiona mrembo, watu wengine wakamuona
mrembo lakini makampuni hayo yaliona fedha.
Walijua kwamba kama wangemtumia msichana huyo katika matangazo yao
mbalimbali, wangepata fedha nyingi, hivyo wakaingia naye mikataba mingi kwa
kutegemea kuwa angeweza kuchukua taji hilo.
Mbali na Angelica, pia kulikuwa na msichana aliyeitwa Jenny Chu, msichana
kutoka nchini China, alikuwa mrembo, alisoma na kuwa na PhD ya udaktari,
hakuangalia elimu yake, alichokuwa akikiangalia kilikuwa ni masuala ya urembo
tu, tangu zamani aliwaahidi wazazi wake kwamba kuna siku angekuwa mrembo
wa dunia, na muda huo, aliona ndiyo kipindi chenyewe.
Kulikuwa na wasichana wengi, japokuwa wengi waliwafikiria wasichana hao
warembo lakini wakasahau kwamba mbali na wasichana hao kulikuwa na
msichana mmoja aliyekuwa mrembo mno, inawezekana kuliko wote hao, msichana
huyo aliitwa Stacie Lawrence.
Kwa kumwangalia msichana huyo kutoka nchini Australia, alikuwa mrembo
haswa, sura ya kitoto, lipsi pana kidogo, macho ya goroli, shingo ya upanga,
aliumbika, alijua kutembea, yaani kwa kumwangalia harakaharaka, ingekufanya
kudhani kwamba umekutana na mzimu wa mwanamke mrembo kuliko wote,
Cleopatra.
Stacie hakuwa mzungumzaji, alikuwa kimya, alionekana kama kuwa na wasiwasi,
hakuonekana kujiamini kabisa. Alikuwa msomi, alikuwa na PhD ya mambo ya

139
uandishi, alitamani kusoma lakini pia alipenda sana mambo ya urembo na huo
ukawa ndiyo muda wake wa kukamilisha kile alichokuwa akikiota kila siku.
Alimuogopa msichana Angelica kwa kuwa alitangazwa sana, hakuwa na uhakika
kama angeweza kushinda kinyang’anyiro hicho, kila wakati alipokuwa akimuona
Angelica, alitamani kumsogelea na kumsalimia kisha kumwambia kwamba
alitamani sana kuwa kama yeye.
Hakujua watu walimfikiria vipi. Wasichana wengi waliokuwa katika
kinyang’anyiro hicho walimpa ushindi, alionekana kustahili hata zaidi ya Angelica
ambaye mara kwa mara alikuwa akipigiwa promo kutoka sehemu mbalimbali.
Wasichana wengine wakashindwa kujizuia, walimsogelea na kumwambiia wazi
kwamba alikuwa mrembo, kila msichana alitamani kuwa kama yeye lakini kila
alipoambiwa, aliwajibu kitu kimoja kwamba inawezekana hawakumuona
Angelica.
“Unajua wewe mzuri sana,” aliambiwa na msichana Priscilia, mrembo kutoka
nchini Italia.
“Nani? Mimi?”
“Ndiyo! U mrembo sana...”
“Hapana! Labda hujamuona Angelica...”
“Nimemuona lakini wewe, hakika unastahili kuwa mshindi katika shindano hili,”
alisema msichana Priscilia.
Kwa kumwangalia, alionekana kutokutania, alimaanisha kile alichokuwa
akikizungumza. Hiyo haikuwa kwa msichana huyo tu, alipoondoka walimfuata
wasichana wengine na kumwambia jinsi alivyokuwa mrembo.
Alipoambiwa, alijisikia aibu, hakujiamini hata kidogo. Kwa Angelica, tayari
alianza kuona wivu, jinsi wasichana wengine walivyokuwa wakimzungumzia
Stacie, moyo wake uliuma kupita kawaida.
Walikaa kambini huku wakiendelea na mazoezi kama kawaida, saa zilizidi
kukatika, siku zikaenda mbele mpaka siku ya tukio kufika. Kila mtu alitaka kuona
msichana Angelica akichukua taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kushinda
kutoka nchini Mexico.

140
Wakati Angelica akiendelea kuwa gumzo ndipo watu wakafanikiwa kumona
msichana Stacie. Kwanza kila mmoja akashtuka, hawakuamini kile walichokiona,
hawakuamini kama kulikuwa na msichana mwingine mrembo hata zaidi ya
Angelica ambaye alikuwa gumzo.
Mioyo ya watu ikaanza kubadilika, ikatoka kwa msichana Angelica na kuhamia
kwa Stacie, watu wakaanza kumtafuta katika mitandao mbalimbali, picha zake,
urembo wake ukawadatisha sana, hakukuwa na aliyeamini kama dunia hiihii
ingekuwa na msichana mrembo kama alivyokuwa Stacie.
Watu wakaanza kutumiana picha za msichana huyo katika mitandao ya kijamii,
kila mtu aliyemuona Stacie katika picha zile, alitaka kumuona uso kwa uso kwani
mioyo yao ilikataa kabisa kwamba katika dunia hiihii, kipindi hikihiki kungekuwa
na msichana mrembo kama Stacie.
“Ni lazima nitakwenda kutazama kinyang’anyiro,” alisema jamaa mmoja, alikuwa
ameshika simu yake akimwangalia Stacie.
“Si ulisema hauendi!”
“Nitakwenda, nimebadili mawazo,” alisema jamaa huyo.
Watu walitaka kuona ushindani mkubwa kutoka kwa wasichana wawili warembo,
mmoja kutoka nchini Australia na mwingine kutoka nchini Mexico. Kila kona,
wawili hao walawa gumzo, japokuwa kipindi cha nyuma Angelica alikuwa
akizungumziwa sana lakini katika kipindi hicho upepo ukabadilika kabisa,
hakuzungumziwa Angelica peke yake bali alizungumziwa Stacie, tena kadiri muda
ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele, aliendelea kusikika zaidi.
“Unahisi nani atachukua ushindi?”
“Mmh! Wala sijui manake nishanchanganyikiwa!”
Watu walisubiri mpaka pale kinyang’anyiro kilipoanza. Mwana huo, watu
walifuatilia kinyang’anyiro hicho kuliko vipindi vingine vyote, kila kona, watu
walikuwa wakifuatilia katika televisheni zao na kitu kilichokuwa kikiwavuta zaidi
ni urembo wa wasichana hao wawili.
Vipengele vyote vikapita na mwisho wa siku mshindi kutarajiwa kutangazwa.
Katika tatu bora alibaki Stacie, Angelica na mrembo mwingine kutoka Afrika
Kusini, ThandiMbokani.

141
Ukumbi mzima ulibaki kimya, mtu aliyetakiwa kutangaza matokeo, akasimama,
akachukua matokeo kutoka kwa majaji na kisha kusimama, hakuanza na mtu wa
kwanza, alianza na mtu wa tatu.
Lilipotajwa jina la Thandi, kila mtu alikaa kimya, walilitegemea hilo, walijua
kwamba msichana huyo angeshika nafasi hiyo na mbili za juu zingekuwa kwa hao
warembo waliowafanya watu wengi kujaa ndani ya ukumbi huo.
Mtangazaji, hakutaka kutangaza kwa pupa, alitaka kila mtu awe na presha mahali
hapo, kwanza akarekebisha tai yake, akajikoholesha, akafanya mambo mengi
yasiyokuwa na msingi ili kuwafanya watu kuwa na presha ndani ya ukumbi huo.
Kila mmoja alikuwa akimwangalia, mapigo yao ya moyo yalikuwa yakidunda
sana, wote walikuwa na mshindi wao mioyoni mwao, walitaka kumsikia
mtangazaji huyo alikuwa nani kwani kama ni urembo, wote walikuwa warembo
japokuwa msichana Stacie alizidi kidogo.
Moyo wa Bwana Seppy ulikuwa mweupe kabisa, alichokuwa akitaka kukiona ni
kuwa peke yake katika penzi la msichana Maria, kuua, kwake hakukuwa na tatizo
lolote lile, kitu pekee alichokitaka ni kuwa na furaha kipindi chote.
Alipata taarifa kutoka kwa watu wengine kwamba yule mchezaji wa mpira wa
kikapu aliyekuwa akitamba sana kipindi hicho, Paul alikuwa amekufa chumbani
katika hoteli moja huko Los Angeles, hakutaka kujali sana kwani yeye ndiye
aliyekuwa nyuma ya mpango wake.
Hakutaka kumuuliza Maria kuhusu Paul, alijua kwamba msichana huyo alikuwa na
hofu kubwa kwa kuhisi kwamba angejua, akamuacha na uzuri ni kwamba kila
taarifa iliyokuwa ikiandikwa, hakutajwa msichana, ilitajwa kwamba kama kawaida
Benjamin alikuwa amekwenda chumbani humo na kumuua kijana huyo.
“Hakikisheni huyo msichana anakuwa huru, si mnajua kwamba huyo ni msichana
wangu?” alizungumza Bwana Seppy katika simu, alikuwa akizungumza na polisi.
“Ndiyo mkuu!”
“Basi fanyeni hivyo!”
Hela zilikuwa kila kitu, alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa, aliheshimika
kila kona, polisi wengi waliokuwa na tamaa ya fedha walikuwa chini yake na
ndiyo maana wakati mwingine alikuwa huru kufanya kitu chochote alichotaka

142
kukifanya kwa kuwa alijua hakukuwa na mtu aliyekuwa akimbabaisha hata mara
moja.
Polisi walipewa maelekezo juu ya nini cha kufanya na wao walitakiwa kufanya
vilevile, harakaharaka wakamuita Maria katika chumba cha mahojiano, wakaanza
kuzungumza naye, hawakuchukua muda mrefu wakaamua kumwachia huku
wakimwambia kwamba angehitajika kituoni hapo mara kwa mara.
Hilo ndilo alilolitaka Bwana Seppy, akawasiliana na Maria ambaye alimwambia
kwamba yupo nyumbani, akamwambia kuwa alitaka kumuona wiki hiyo lakini
msichana huyo akasema kwamba hakujisikia vizuri, alihitaji muda wa kupumzika.
“Si utakuja kupumzika huku mpenzi!” alisema Bwana Seppy.
“Hapana mpenzi! Naomba wiki moja ya mapumziko!”
“Sawa. Upo poa lakini?”
“Ndiyo! Najisikia kuchoka tu,” alisema Maria.
Bwana Seppy aliusoma mchezo, alijua fika kwamba msichana huyo alikuwa katika
kipindi cha majonzi, alimpenda sana Paul na hakuona kama kungekuwa na mtu
ambaye angelivuruga penzi lake, hata mapenzi aliyokuwa nayo juu ya Bwana
Seppyy alipungua kwa kiasi kikubwa kwani hata kama fedha, Paul alikuwa nazo
japokuwa hazikuwa nyingi kama za Bwana Seppy.
Siku zikaendelea kukatika, wiki ikakatika lakini msichana Maria hakufika nchini
Marekani, kila alipopigiwa simu, alisema kwamba alikuwa kwenye kipindi
kigumu, matatizo ya kifamilia yalikuwa yakimwandama hivyo asingeweza kabisa
kwenda nchini Marekani.
Kwake, hayo yalikuwa majibu makali, yaliyouumiza moyo wake kupita kawaida,
hakutaka kuona akishindwa, alichokifanya ni kuondoka Marekani na kuelekea
nchini Mexico kwa kuamini kwamba uwepo wake mbele ya msichana huyo
ungeweza kubadilisha kila kitu.
“Kisa nini Maria?” aliuliza Bwana Seppy huku akimwangalia msichana huyo
usoni.
“Sipo vizuri kiafya,” alisema.
“Najua na ndiyo maana naona umekonda sana. Tafadhali mpenzi, kama kuna
tatizo, naomba uniambie.”

143
“Hakuna tatizo lolote lile.”
“Kweli?”
“Hakika!”
Siku hiyo Bwana Seppy alitumia muda wake wote kuwa chumbani na msichana
Maria, hata walipofanya mapenzi, haikuwa kama kipindi cha nyuma, hakupewa
ushirikiano kama ilivyokuwa kipindi kingine. Moyoni mwake aliumia lakini
hakuwa na jinsi, alimpenda msichana Maria na kama kuzunguka, alizunguka
sehemu nyingi, aliwaona wasichana wengi lakini alikiri kwamba hakuwahi
kumuona msichana kama Maria kwa jinsi alivyokuwa mzuri.
“Hii yote ni kwa sababu nakupenda Maria?” aliuliza Bwana Seppy ilipofika
asubuhi.
“Kivipi?”
“Kwa unavyonifanyia!”
“Kwani nimekufanyaje mpenzi?”
“Sawa. Si umesema una matatizo ya kifamilia, ngoja nikuache uendelee nayo,”
alisema Bwana Seppy.
Moyo wake ulikasirika, alimfahamu Maria, hakuwa namna ile, alijua kwamba
kulikuwa na kitu kilichokuwa kikimuuma, kitendo cha mwanaume aliyekuwa
akimpenda kuuawa, ndicho kilichomfanya kuwa katika hali ile.
Alikasirika kwa kuwa yeye kama yeye alikuwa na nafasi yake lakini pia
hakutakiwa kukasirikiwa au kuonyeshewa hali yoyote ya kutokujali kwa sababu
yeye ndiye aliyekuwa akimuweka mjini msichana huyo.
Uamuzi wa mwisho kabisa kuupanga ulikuwa ni kuondoka mahali hapo, hakutaka
kurudi tena, kama kuumia, aliumia vya kutosha na huo ulikuwa muda wa kuulizwa
moyo wake huku akijitahidi kutafuta msichana mzuri ambaye angempenda kama
alivyokuwa akimpenda Maria.
****
Hakukuwa na aliyeamini kama Stacie alikuwa amembwaga Angelica katika
kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss World ambacho kilifanyika nchini Marekani
katika jiji la Texas.

144
Ukumbi mzima ulipiga makofi, watu wengine walibaki midomo wazi, wapo
wengine waliocheza kamari na kubashiri kwamba msichana Angelica angeibuka
mshindi kutokana na kunyakua taji hilo.
Stacie alikuwa na furaha kubwa moyoni mwake, alipita huku na kule akiwapungia
watu mikono, ndoto yake aliyokuwa nayo tangu kipindi cha nyuma hatimaye
Mungu aliifanikisha na kuwa kweli.
Machozi ya furaha yalimbubujika, kuna kipindi hakuwa akiamini, alihisi kwamba
alikuwa katika moja ya ndoto yenye msisimko ambapo baada ya kipindi fulani
angeamka na kujikuta akiwa kutandani kitu ambacho hakikuwa kweli, kila kitu
kilichokuwa kikitokea, kilikuwa katika maisha halisi.
Jina lake siku hiyo likapata umaarufu, waandishi wa habari wakampiga sana picha
na wengine kuiweka habari yake katika mitandao ya kijamii, jina lake, yaani kwa
kipindi cha dakika kadhaa, lilikuwa maarufu mno.
Uzuri wake uliendelea kuwatetemesha wanaume wengi, hawakuwa wakiamini
kama kweli duniani kulikuwa na msichana aliyekuwa na sura nzuri kama
alivyokuwa Stacie, wanaume wenye fedha wakajipanga, kila mtu alihitaji kuwa na
msichana huyo, hawakujua kama angekubaliana nao au la, kitu walichokihitaji ni
kuwa naye kimapenzi, yaani hata kama ni kutumia fedha, watumie lakini mwisho
wa siku wampate msichana huyo.
Siku hiyo Stacie akapelekwa katika hoteli kubwa ya nyota saba na kukaa huko.
Usiku mzima alikuwa na furaha tele, hakuamini kama kweli angefanikiwa
kunyakua taji hilo lililokuwa na heshima kubwa duniani katika masuala ya
urembo.
Siku iliyofuata akawasiliana na rafiki yake wa kipindi kirefu, Robert Steph ili awe
meneja wake kwani mbele yake aliyaona mafanikio makubwa hasa ya kuingia
mikataba minono.
Kama alivyohisi ndivyo ilivyotokea, siku hiyihiyo akapigiwa simu na watu wa
Jarida kubwa la Forbes ambao walitaka kuonana naye na kuzungumza naye kuhusu
masuala ya kibiashara, hilo wala halikuwa tatizo, alichoangalia kwanza ni kupiga
pesa tu.
****

145
Fedha zikaanza kunukia kwa msichana Stacie, hakukuwa na kitu alichokiona
mbele yake zaidi ya mafanikio makubwa, alijiona akiwa mtu mkubwa, mwenye
fedha na heshima kubwa.
Kitendo cha kunyakua tuzo na kuwa mrembo wa dunia kilimpa uhakika wa kuishi
maisha ya kuwa na fedha mpaka anakufa, kupitia uzuri wake, alishinda tuzo hiyo
na hivyo kumshukuru Mungu kila siku kwa kile alichokuwa amempa.
Baada ya kusaini mkataba na Jarida la Forbes na kulipwa kiasi cha dola milioni
mbili ambazo zilikuwa zaidi ya bilioni nne za Kitanzania, makampuni mengi
yakamfuata, hakuwa na hiyana, alichokifanya ni kuendelea kukusanya fedha kama
kawaida.
Jina lake halikushuka, liliendelea kuwa juu na kwa sababu tayari alikuwa na jina,
aliona kuwa na umuhimu wa kuwa na mbunifu wake wa mavazi. Kulikuwa na
watu wengi walioomba nafasi hiyo, kila siku alipokea barua pepe, watu walikuwa
wakimuomba nafasi ya kuwa mbunifu wake wa mavazi kiasi kwamba
akachanganyikiwa amchukue yupi kwani kila mmoja alionekana kuwa mtaalamu
kwa kazi hiyo.
“Kwa hiyo utamchukua nani?” aliuliza Robert.
“Labda huyu Muitaliano, Alejandro Petrescu,” alijibu Stacie.
Alichokifanya ni kuwasiliana na mbunifu huyo wa mavazi na kumtaka kufika
nchini Marekani haraka iwezekanavyo, alimtumia tiketi ya ndege, gharama za
kukaa hotelini lakini mwisho wa siku walitaka kuona kila kitu kinakuwa kama
kinavyotakiwa.
Tangu achukue taji hilo alikwenda nyumbani kwao Australia mara mbili tu, baada
ya hapo, maisha yake yakaendelea kuwa nchini Marekani ambapo aliishi kwa
kuheshimika kupita kawaida.
Alejandro ndiye aliyemfanya Stacie kupendeza zaidi, kila siku alikuwa mtu wa
kumbunia mavazi mbalimbali, na kila alipovaa, alivutia kiasi kwamba wanaume
wengi wakazidi kumpenda.
Jina lake lilikuwa kubwa, ni ndani ya miezi sita tu tayari aliingiza kiasi kikubwa
cha fedha kwa sababu tu alikuwa mrembo na hata mastaa wa filamu walitamani
kuigiza naye kitu kilichowafanya kuwaomba waongozaji wafanye kitu.
“Hakuna tatizo, nitamuita kwenye hii filamu!”

146
Muongozaji kutoka katika Kampuni ya Filamu ya Marvel alikuwa akizungumza na
muigizaji wake mwenye jina kubwa, Tom Hardy ambaye alikuwa akihitaji kuigiza
na msichana Stacie.
Hilo wala halikuwa tatizo, kwa sababu wao wenyewe walikuwa wakitafuta fedha,
waliamini kuwa kama wangemruhusu msichana huyo ashiriki katika muvi yao
hakika wangepata kiasi kikubwa cha fedha, hivyo bila ubishi, wakawasiliana naye
na kumuita.
Stacie hakuamini, hakuwahi kufikiria hata mara moja kwamba ingetokea siku
angepokea simu kutoka kwa mmoja wa waongozaji katika kampuni hiyo na
kumtaka kuigiza filamu, hakukataa, kwa kuwa naye alizitaka hizo fedha na kuwa
maarufu zaidi, akakubaliana nao.
Baada ya siku kadhaa, wakaanza kuigiza filamu mpya ya Black Panther. Japokuwa
alikuwa muigizaji mchanga lakini alifanya vizuri sana kitu kilichoonyesha kwamba
angekuwa muigizaji mkubwa sana hapo baadaye.
Hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa mafanikio makubwa aliyoanza kuyapata. Kila
siku akawa mtu wa kuingiza fedha, uzuri wake uliwachanganya watu wengi na
hivyo kuanza kumfutailia bila mafanikio makubwa.
Miongoni mwa watu wengi waliokuwa wakimfuatilia alikuwa Bwana Seppy. Mzee
huyu alimpigia simu Stacie na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye kwa
kuwa kulikuwa na mambo mengi ya kuzungumza.
Jina la Bwana Seppy halikuwa geni, alimfahamu mzee huyo, alikuwa miongoni
mwa watu wenye fedha ambao waliitetemesha Marekani kipindi hicho. Kwake
ilikuwa furaha tele hivyo kupanga mipango ya kuonana.
Siku mbili zilizofuata, walikuwa katika Mgahawa wa SamSam ambapo hapo
Bwana Seppy alikuwa na walinzi wake waliokuwa kimya kila wakati.
Bwana Seppy alibaki akimwangalia msichana huyo, alikuwa mrembo sana, tangu
aachane na mpenzi wake, Maria miezi kadhaa iliyopita hakupata mtu ambaye
angeziba pengo kubwa lililoachwa na msichana Maria.
Alimtafuta msichana wa kuziba pengo hilo ila kwa kipindi chote hicho,
hakufanikiwa kabisa. Kila alipomwangalia Stacie, aliona kabisa kwamba msichana
huyo alikuwa akielekea katika kuliziba pengo hilo lililomtesa kwa kipindi kirefu.

147
Kuhusu kutumia fedha, kwake halikuwa na tatizo lolote lile, kitu pekee
alichokihitaji kilikuwa ni mapenzi kutoka kwa msichana huyo tu. Macho yake tu
yalionyesha kila kitu, mapenzi aliyokuwa nayo moyoni hayakubaki huko bali
yalizunguka mpaka machoni mwake.
Alitaka kumwambia ukweli lakini hakujua mahali pa kuanzia, alivuta pumzi huku
akiagiza kahawa, kipindi chote hicho msichana Stacie alikuwa akimwangalia tu
machoni mwake.
“Nashukuru sana kwa kuitikia wito wangu,” alisema mzee huyo huku
akimwangalia msichana huyo.
“Usijali...”
“Nimekuita kwa jambo moja...”
“Lipi hilo? Biashara?”
“Ndiyo! Lakini sidhani kama la biashara linatakiwa kuzungumzwa leo, nadhani leo
tunatakiwa kuzungumzia jambo jingine kabisa,” alisema mzee huyo.
“Lipi hilo?”
Bwana Seppy akashusha pumzi ndefu na kuangalia pembeni kama kulikuwa na
watu waliokuwa wakiyafuatilia mazungumzo yao, alipoona hakukuwa na mtu
aliyekuwa akifanya hivyo, hapo ndipo alipoamua kutumbua jipu.
Hakutaka kuteseka moyoni mwake, ilikuwa ni vigumu mno kuendelea kuumia,
kuwa na mawazo na wakati alikuwa na uwezo mkubwa wa kumwambia msichana
huyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Hakutaka kuficha, kama ni siri, aliamua kuitoa na hivyo kumwambia jinsi
alivyokuwa akimpenda. Muda wote msichana Stacie alikuwa kimya, alibaki
akimwangalia mzee huyo usoni, uso wa Stacie ulikuwa kwenye tabasamu pana
ambalo lilimpa matumaini mzee huyo kwamba angefanikiwa kile alichokuwa
akikitaka.
“Umemaliza?” aliuliza Stacie baada ya kumsikiliza mzee huyo kwa dakika tatu.
“Ndiyo!”
“Haitowezekana!” alijibu kwa kifupi.
“Kwa nini tena jamani?”

148
“Jua kwamba haitowezekana, hakuna sababu, jua tu kwamba haitowezekana,”
alisema Stacie na hapohapo kusimama, hakutaka kusubiri, japokuwa mzee huyo
alionyesha muonekano uliomtia huruma, hakutaka kujali, akachukua kila kilicho
chake na kuondoka zake huku Bwana Seppy akiishia kula kwa macho tu.
Benjamin hakutaka kutoka kule alipokuwa, alikuwa kimya, japokuwa katika
bomba lile kulikuwa na joto kali na uchafu mwingi hasa moshi hakutaka kutoka,
alibaki humohumo akiendelea kusubiri mpaka maofisa wale wa FBI waondoke
ndiyo atoke ndani ya bomba lile.
Alimsikia rafiki yake, Harry alivyokuwa akiwaambia maofisa hao kwamba yeye
hakuwepo, alikuwa amekwishaondoka na hakujua mahali alipokuwa. Maofisa wale
walimtafuta, muda wote mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kule
alipokuwa lakini hakutaka kutoka.
Walimtafuta bila mafanikio yoyote na kuamua kuondoka ndani ya nyumba hiyo.
Hapo ndipo Benjamin alipoona ni muda muafaka kutoka ndani ya bomba lile,
alianza kuangalia huku na kule, hakuwa akijiamini hata kidogo.
Hakukuwa a mtu nyumbani hapo, alikuwa peke yake, senhemu hiyo haikuonekana
kuwa salama tena, kama maofisa wa FBI walikuja na kuondoka, aliamini kwamba
wangerudi tena mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kutoka.
Alitembea kwa mwendo wa tahadhali, alihofia kukamatwa, alitembea huku
kichwani akiwa na kofia yake, hakuwa na usafiri, ingekuwa rahisi sana kama
angefanikiwa kupata usafiri, magari yalikuwepo lakini hilo halikuwezekana.
Akachukua simu yake na kuanza kumpigia mpenzi wake, Vanessa, alitaka kuonana
naye na kupanga ni kwa namna gani angeweza kuwa naye na mwisho wa siku
kuondoka nchini hapo na kuelekea Urusi ambapo hakukuwa mbali sana.
Simu ikaanza kuita, alikuwa mvumilivu, wakati akipiga simu hiyo, alihakikisha
anakuwa katika sehemu ambayo itakuwa vigumu kuonekana, alijibanza sehemu na
watu wote waliokuwa wakipita pale alipokuwa, hakukuwa na aliyemgundua.
“Upo wapi?” aliuliza Benjamin mara baada ya simu kupokelewa.
“Nipo nyumbani!”
“Kuna usalama huko?” aliuliza.
“Nadhani. Hakuna mtu, nipo peke yangu!”

149
“Na FBI je?”
“Hawapo!”
“Hebu chungulia dirishani, angalia kwa umakini, kweli hawapo?” aliuliza
Benjamin na Vanessa kufanya hivyo.
“Hakuna mtu!”
“Sawa! Nakuja!”
Japokuwa aliambiwa na msichana wake kwamba hakukuwa na maofisa wa FBI
pale nyumbani alipokuwa lakini alishindwa kabisa kujiamini, mapigo yake ya
moyo yalikuwa yakidunda na kuona kwamba kama angekwenda huko ilikuwa ni
lazima kukamatwa.
Wakati anafikiria hayo, upande mwingine wa moyo wake ukamwambia kwamba
hakukuwa na tatizo lolote lile, kama alitaka kwenda huko, aende na kila kitu
kingekuwa vizuri.
Kutoka hapo alipokuwa mpaka alipokuwa akiishi Vanessa, katika nyumba ambayo
aliamua kuipanga kwa muda haikuwa mbali sana, hakuchukua muda mrefu akawa
amefika katika mtaa huo.
“Ni lazima tuondoke na kuelekea nchini Urusi, hapa Marekani si salama tena,”
alijisemea Benjamin.
****
Wakati Benjamin akiwasiliana na Vanessa, vijana wa Bwana Seppy walikuwa
wakifahamu kila kitu na walikuwa wakifuatilia neno moja baada ya jingine. Bado
Benjamin alionekana kuwa mtu muhimu sana, walijua kwamba kama
wasingefanikiwa kumpata mtu huyo na kumuua basi bosi wao angekuwa kwenye
wakati mgumu sana.
Mawasiliano yale wakamuonyeshea Bwana Seppy ambaye alionekana kuwa na
mawazo mno ya kukataliwa na msichana Stacie, alichoagiza ni kwamba Benjamin
na mpenzi wake, Vivian watafutwe na kuuawa haraka iwezekanavyo.
“Hakuta tatizo mkuu! Tunawafuata hukohuko,” alisema Dracula na kisha
kuwakusanya watu wake kuelekea kule ambapo Benjamin alitakiwa kuonana na
mpenzi wake, Vanessa.
****

150
Benjamin alianza kupiga hatua za taratibu kuifuata nyumba aliyokuwemo Vanessa,
hakujiamini kabisa na alijua fika kwamba inawezekana kuna sehemuu maofisa wa
FBI walikuwa wamejificha.
Aliangalia huku na kule, hakuona mtu, hakujua kama maofisa hao walikuwa
kwenye gari ambalo mbele hakukuwa na mtu, walikuwa kwa nyuma huku
wakimfuatilia katika televisheni walizokuwa nazo na hata mazungumzo yake na
Vanessa waliyasikia kwani tayari walikuwa wakimfuatilia msichana huyo tangu
siku ile walipomruhusu kutoka katika kituo cha polisi.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza jamaa mmoja.
“There is no time, let’s roll,” (Hakuna muda, twendeni)
Hicho ndicho walichokifanya, hawakutaka kusubiri mahali hapo, wakateremka
huku wakiwa na bunduki zao mikononi. Wakati Benjamin akiendelea kupiga hatua
kuelekea katika nyumba ile, ghafla akaliona gari likija kule alipokuwa, alionekana
kuogopa, hakujua gari hilo lilikuwa la kina nani, alichokifanya ni kuanza kukimbia
kuelekea katika nyumba ile.
Hao waliofika hawakuwa maofisa wa FBI, walikuwa ni vijana kutoka kwa Bwana
Seppy, walifika hapo na kuhisi kwamba walikuwa peke yao, kitendo cha Benjamin
kukimbia kuelekea ndani, wakaanza kumkimbiza huku wakiwa na bunduki.
Benjamin akaingia ndani, nao wakamfuata na kuingia ndani. Msichana Vanessa
ambaye alikuwa ndani ya nyumba hiyo, akaanza kupiga kelele, watu wale
hawakutaka kujali, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumkamata Benjamin na
kisha kumkamata na Vanessa ambaye muda wote alikuwa akiomba msamaha tu
kwamba aachwe.
“Mlidhani mtatusumbua miaka yote, kwisha habari yenu,” alisema Dracula huku
akiachia tabasamu pana, uso wake ulionyesha jinsi gani alikuwa na furaha.
Wakawachukua na kuanza kutoka nje. Hawakujua kama maofisa wa FBI walikuwa
hapo nje, kitendo cha kutoka tu, milio ya risasi ikaanza kusikika, walichokifanya ni
kujificha pembezoni mwa nyumba hiyo.
“Who are they?” (Ni wakina nani?) aliuliza jamaa mmoja.
“I don’t know.” (Sifahamu)
“They are cops,” (Ni polisi) alisema Dracula.

151
“Who call them?” (Nani aliwapigia simu?)
“I don’t know,” (Sijui) alijibu Dracula.
Hakukuwa na muda wa kuulizana maswali mengi zaidi, kama walivyokuwa
wakirushiwa risasi nao wakaanza kujibu mapigo. Yalikuwa ni mapigano makubwa,
maganda ya risasi yalikuwa yakidondoka chini tu.
Sehemu hiyo ikabadilika na kuwa uwanja wa vita. Vijana wa Bwana Seppy
walikuwa na silaha nzito hivyo kuionekana kuwa na kazi nyepesi kabisa. Kwanza
walianza kulishambulia gari la maofisa wale bila tatizo lolote lile.
Kwa maofisa wale ilikuwa ni kazi ngumu kuwarushia risasi kwani watu hao
walikuwa na Benjamin mtu ambaye walimtaka kwa udi na uvumba. Wasiwasi wao
ndiyo uliosababisha kushambuliwa sana.
Benjamin ambaye alikuwa amekaa nyuma alipoona mashambulizi yanazidi na
wote wamemsahau na kuwa bize na maofisa wale, akarudi ndani haraka sana,
hakutaka kumshtua Vanessa kwani mahali alipokuwa ilikuwa vigumu sana.
Mmoja wa vijana wale alimuona Benjamin akikimbia lakini hawakuwa na muda
wa kumkimbiza kwani bado mashambulizi kutoka kwa maofisa wa FBI yalikuwa
yakiendelea kama kawaida.
“He is running....he is running...” (Anakimbia....anakimbia...) alisema jamaa huyo
lakini hakuna aliyajali, wote walikuwa bize na mapambano.
****
Kulikuwa na watu wawili tu waliokuwa wakikizuzua kichwa cha Bwana Seppy
kila siku, mtu wa kwanza kabisa alikuwa Benjamin na wa pili alikuwa msichana
Stacie ambaye kwa kipindi kifupi tu aliuteka moyo wake na kuuendesha
alivyotaka.
Hakutulia, kila wakati alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi,
alichanganyikiwa na wakati mwingine alihisi kama angeweza kupoteza maisha
kutokana na jinsi alivyokuwa na mawazo lukuki kichwani mwake.
Kwa wakati huo alikuwa akisubiri habari njema kutoka kwa vijana wake
aliowatuma kumteka Benjamin na kuja kumuua kwa mkono wake. Tangu vijana
hao walipoondoka mpaka muda huo, hakuwa amepata taarifa yoyote ile kitu
kilichomshangaza sana.

152
Dracula, mmoja wa vijana wake alikuwa mtu makini sana, kila alipomtuma,
alikuwa mleta taarifa mzuri sana, hata kabla hajauliza kilichokuwa kimeendelea,
tayari alimpa taarifa lakini siku hiyo, hali ilionekana kuwa tofauti kabisa, kila
alipompigia simu Dracula, ilipatikana, ila haikupokelewa kitu kilichomtia
wasiwasi mkubwa.
“Kuna nini? Mbona hapokei simu?” alijiuliza huku akikosa jibu kabisa.
Aliendelea kusubiri zaidi kwani kila alipopiga simu majibu yalikuwa yaleyale
kwamba simu haikupokelewa.
Baada ya saa moja ndipo akaona kulikuwa na simu iliyoingia katika simu yake,
moja kwa moja akayapeleka macho yake katika simu ile, namba aliyokutana nayo
ilikuwa ni ya Dracula, harakaharaka akaipokea.
“Mmefikia wapi?” lilikuwa Swali lake la kwanza kabisa hata kabla ya
salamu.”Ametukimbia...”
“Amewakimbia, yaani kirahisi tu?”
“Hapana mkuu! Tulikutana na tatizo, kulikuwa na maofisa wa FBI nao walikuja
kumchukua, tukawa tunarushiana risasi, tumepoteza mwenzetu mmoja ila FBI
wote wapo chini,” alisema Dracula.
“Kwa hiyo Benjamin mmemkosa?”
“Tulimpata, tulikuwa naye ila mapigano yalivyoanza, akapata nafasi ya kukimbia,
ila tunaye mpenzi wake hapa,” alisema Benjamin.
“Nani? Vivian?”
“Ndiyo!”
“Mleteni huyohuyo.”
Hakutaka kusikiliza mazungumzo zaidi, alichokifanya ni kukata simu huku akiwa
kwenye hasira kali, moyo wake ulikasirika, kitendo cha vijana wake kumpata
Benjamin na kisha kuwatoroka kwake kilionekana kuwa kama uzembe mkubwa
hata kama walikuwa wamezungukwa na maadui.
Kwa sababu Vivian alipatikana, kwake hakukuwa na tatizo, msichana huyo
alikuwa muhimu kwani aliamini kama angekuwa naye basi ilikuwa ni lazima
Benjamin ajipeleke kwani bila kufanya hivyo aliahidi kumuua Vivia ili kumtia
hofu kijana huyo.

153
Wala haukupita muda mrefu, Vivian alikuwa mbele ya Bwana Seppy, kwanza
akamwangalia msichana huyo, hakumpenda kwa sababu mpenzi wake alimsumbua
sana. Akamwamuru Dracula amuweke kwenye kochi na yeye kuanza kuzungumza
naye.
“Ben yupo wapi?” aliuliza mzee huyo.
“Sijui chochote kile,” alijibu Vivian huku akionekana kuwa na kiburi fulani.
“Unanificha?”
“Hapana! Waulize vijana wako, mimi sijui chochote kile,” alisema Vivian kwa
ujasiri mkubwa.
Bwana Seppy hakutaka kuuliza swali jingine, alichokifanya ni kuamuru msichana
huyo achukuliwe na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa ndani ya
nyumba hiyo, chumba hicho kilikuwa na giza kubwa huku kukiwa na buibui
wengi.
Kilikuwa chumba chenye mateso makali, watu wengi waliojifanya jeuri,
walichukuliwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho na kuachwa kwa siku kadhaa.
“Nisikilize Dracula,” alisema Bwana Seppy.
“Ndiyo mkuu!”
“Unamfahamu Stacie?”
“Huyu mrembo wa dunia tuliyekwenda kumuona siku ile?”
“Ndiyo!”
“Amefanyaje?”
“Ninaitaka roho yake!”
“Kwa nini?”
“Dracula! Tangu lini umeniuliza sababu? Nimekwambia ninaitaka roho yake,
unaniuliza kwa nini! Unataka nikujibu nini?” aliuliza Bwana Seppy huku
akionekana kuwa na hasira kubwa.
“Samahani mkuu! Tumuue kama kawaida au kivingine?”
“Kama kawaida!”
“Sawa.”

154
Huo ndiyo ulikuwa uamuzi aliokuwa ameufikia, hakutaka tena kuwa na huruma,
alimpenda msichana Stacie, alimwambia lakini mwisho wa siku msichana huyo
akamletea mapozi na kumkataa.
Hilo lilimkasirisha na ndiyo ilikuwa sababu ya kupanga mauaji, hakutaka
kuumizwa moyoni mwake, kitendo cha kukataliwa kilimfanya kuwa na chuki kali
dhidi ya Stacie, alijijua kwamba alikuwa na fedha nyingi hivyo kuwa na uhuru wa
kuwa na msichana yeyote yule, sasa kwa nini msichana huyo amkatae?
Vijana wake wakaondoka mahali hapo, ilikuwa ni lazima kummaliza msichana
Stacie kama walivyowamaliza watu wengine ambao walimkwaza Bwana Seppy
ambaye alikuwa na utajiri mkubwa mno kipindi hicho.
Kabla ya yote, kitu cha kwanza kabisa ni kuanza kutafuta msichana huyo alikuwa
sehemu gani.
Maisha yalibadilika kabisa, kilichokuwa mbele ya Stacie kilikuwa ni kutengeneza
pesa tu. Mikataba iliendelea kumiminika, aliisaini tena kwa kiasi kikubwa cha
fedha. Alijiona kuwa tajiri mkubwa hapo baadaye, watu walizidi kumpapatikia
kwa sababu alikuwa msichana mrembo, mwenye mvuto wa ajabu ambapo kila
mwanaume alitamani sana kuwa naye.
Hakuwa mwepesi, alitaka kutengeneza pesa kwanza kabla ya kuamua kuwa na
mwanaume fulani. Mtu ambaye alikuwa akimfikiria kipindi hicho alikuwa
mwanaume mmoja tu, huyu aliitwa Alan, mwanaume aliyewahi kuwa naye
utotoni.
Siku zikaendelea kukatika, akasahau kama alitakiwa kurudi nchini Australia, kama
walivyokuwa mastaa wengine, naye akatokomea nchini Marekani kwani ndipo
kulipokuwa na ishu nyingi za pesa, kurudi nchini kwake isingewezekana tena.
Baada ya miezi kadhaa, akaitwa kwa ajili ya kuwa balozi wa watoto katika shirika
la Umoja wa Mataifa kupitia UNICEF. Kazi kubwa ilikuwa ni kuzunguka duniani
kote, kukutana na wanawake na watoto waliokuwa na matatizo kiafya na
kuzungumza nao huku kiasi kikubwa cha dawa kikiwa kimeandaliwa.
Kichwa chake hakikumfikiria Bwana Seppy, hakujua ni maumivu makali kiasi
gani aliyomuachia mzee huyo, aliendelea na maisha yake kama kawaida huku kila
alipokwenda, watu walimheshimu mno.
“Kuna simu nilipigiwa,” alisema meneja wake, Robert.

155
“Na nani?”
“Mkurugenzi wa Google.”
“Amesemaje?”
“Anataka kuingia mkataba na wewe kwa ajili ya kufanya matangazo zaidi juu ya
programu mpya wanayotarajia kuiweka katika simu zote zinazotumia android,”
alijibu.
“Mmh! Wamesema wanaweza kutoa kama kiasi gani?”
“Sijajua ila si chini ya dola milioni hamsini,” alijibu meneja huyo, kiasi hicho
kilikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni mia moja.
“Sawa! Tukitoka huku, tutaonana nao tuwasikie, ila nina furaha sana,” alisema
Stacie huku akiachia tabasamu pana.
Wakati huo walikuwa safarini kuelekea nchini Japan, alikuwa ameingia mkataba
na kampuni ya kutengeneza matairi ya Yokohama, alitakiwa kwenda huko haraka
iwezekanavyo, hakutaka kuchelewa kwani kiasi alichowekewa kilikuwa kikubwa
mno, hivyo akafanya hivyo.
Ndani ya ndege, muda wote alikuwa mtu mwenye mawazo tele, hakuamini kama
kile kilichokuwa kikiendelea kiliendelea katika maisha yake. Hawakuchukua muda
mrefu ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tokyo.
Hapo, kulikuwa na maofisa wa Yokohama ambao walitumwa kumpokea msichana
huyo mrembo. Walipotoka tu nje ya uwanja huo, kundi kubwa la waandishi wa
habari wakaanza kuwasogelea na kuwapiga picha.
Walifanya kile walichokuwa wameitiwa na baada ya siku mbili, safari ya kurudi
nchini Marekani ikaanza. Kichwani mwake alikuwa akifikiria mkataba aliotaka
kuingia nao na Kampuni ya Google. Wakati mwingine aliiona ndege hiyo
ikichelewa kutua, alitamani kufika nchini Marekani na hatimaye asaini mkataba
uliokuwa mbele yake.
Walichukua saa kumi na sita mpaka kufika nchini Marekani ambapo ndege ikatua
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK uliokuwa jijini New York.
“Wamesema wapo jijini Las Vegas,” alisema Robert.
“Las Vegas?”

156
“Ndiyo!”
“Tunatakiwa kupumzika. Mpigie simu Alejandro na umwambie ajiandae, kesho
tunakwenda huko,” alisema Stacie na Robert kufanya hivyo.
Usiku wa siku hiyo hakulala vizuri, kila alipogeuka, alizifikiria fedha ambazo
aliahidiwa kupewa kama tu angesaini mkataba wa kuitangaza kampuni hiyo.
Asubuhi ilipofika, akaamka, tayari tiketi zilishakatwa na hivyo kuonana na
Alejandro kisha kuanza safari ya kuelekea huko Nevada katika Jiji la Las Vegas.
Baada ya saa mbili, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa McCarran. Kitendo cha kufika katika jiji hilo tu kikampa uhakika wa kuondoka
na mamilioni ya dola.
Walipofika nje, wakapanda ndani ya gari maalumu waliloandaliwa na kisha
kuelekea katika Hoteli ya Vikings Hill. Wakapelekwa katika vyumba
walivyotakiwa kulala. Siku hiyo akalala hotelini pasipo kujua kama kulikuwa na
watu walitumwa kwa ajili ya kuichukua roho yake tu.
****
Kujua Stacie alikuwa wapi kipindi hicho halikuwa jambo kubwa, wakapata taarifa
kwamba msichana huyo alikuwa safarini akielekea nchini Japan kwa ajili ya
kufanya matangazo ya biashara na kuwekeana mkataba na Kampuni ya Yokohama
iliyokuwa ikitengeneza matairi ya magari na ndege.
Hawakutaka kuelekea nchini humo kufanya mauaji, kwa kuwa kipindi hicho
ilikuwa ni lazima afike nchini Marekani kwa ajili ya shughuli zake, walihakikisha
wanamsubiri ili siku akiingia, kama kawaida wafanye kile walichoambiwa.
Walijiandaa kwa kila kilichokuwa kikiendelea, waliwaweka watu tayari kwa ajili
ya kufuatilia ishu nzima ya Stacie na baada ya kuondoka nchini Japan siku mbili
baadaye, walipewa taarifa nzima kwamba msichana huyo alitakiwa kwenda Las
Vegas kwa kuwa Kampuni ya Google walitaka kufanya naye biashara kwa kusaini
mkataba mnono ambao ungewatangaza.
“Alisema atafikia kwenye hoteli gani?’ aliuliza Dracula.
“Bado sijajua, ila nikijua tu, nitawapeni taarifa,” alisema mtoa taarifa.

157
Huo haukuwa mwisho, waliendelea kuzipokea taarifa hiyo na taarifa ya mwisho
kabisa kuwafikia ilisema kwamba msichana huyo angefikia katika Hoteli ya
Vikings Hill.
“Ni lazima twende huko kabla yake,” alisema Dracula.
“Hakuna tatizo.”
Baada ya saa mbili, Dracula na wenzake wawili walikuwa ndani ya ndege
wakielekea jijini Las Vegas. Ilikuwa ni lazima kufanikisha kile walichoambiwa
kwani bila kufanya hivyo, walijua kwamba kungekuwa na tatizo kubwa kwani
Bwana Seppy hakutaka washindwe kwenye jambo lolote lile.
Walipofika, wakateremka kwenye ndege na moja kwa moja kuelekea nje ambapo
wakakodi taksi iliyowapeleka mpaka katika hoteli hiyo ya kifahari ambapo ndani
yake kulikuwa na Cassino iliyokuwa na michezo mingi ya kamari.
Hawakuacha kuwasiliana na kijana aliyekuwa akiwapa maelekezo, aliwaambia
kwamba tayari msichana huyo aliingia jijini New York na hivyo kesho asubuhi
angeanza safari ya kwenda Las Vegas ambapo tayari aliweka oda ya vyumba ndani
ya hoteli hiyo.
“Tutafanikiwa, nilihisi kwamba tungekuwa na ugumu, ila inaonekana kuwa kazi
nyepesi sana,” alisema Dracula.
“Kwa hiyo tumuue kama wale wengine?”
“Ndiyo! Hayo ni maelekezo niliyopewa na mzee.”
“Basi hakuna tatizo.
Walichokifanya ni kwenda kutembea, walizunguka sehemu mbalimbali kwa ajili
ya kula raha tu, walikuwa na fedha hivyo kila kitu walichokifanya kiligharimu
fedha kitu ambacho wala hawakuwa na tatizo nacho kwani kama fedha, walikuwa
nazo za kutosha tu.
Muda mwingi walikuwa wakiifikiria kazi hiyo, walitakiwa kupanga mipango
kabambe, walijua kwamba kulikuwa na kamera ndani ya hoteli hiyo ila walitakiwa
kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hawakamatwi na mtu yeyote yule.
Walizunguka kwa zaidi ya saa moja na nusu ndipo wakarudi hotelini ambapo
baada ya kula, wakalala huku wakiisubiri siku inayofuatia kwa hamu kubwa.

158
Asubuhi ilipofika, wakaelekea katika mgahawa uliokuwa chini na kupata kifungua
kinywa. Huko ndipo waliposikia taarifa za ujio wa msichana Stacie kwamba
angefikia katika hoteli hiyo siku hiyo.
Watu kutoka sehemu mbalimbali walianza kufika ndani ya hoteli hiyo, kila mmoja
alitaka kumuona msichana huyo, wengi walimuona katika sehemu mbalimbali,
hasa kwenye televisheni na majarida, siku hiyo walitaka kumuona ana kwa ana.
“Kuna kitu jamani,” alisema kijana mmoja.
“Kitu gani.”
“Nina wazo. Nadhani tukitumia njia kama tuliyowaua watu huko nyuma
tutashindwa kwani watu wanajua hivyo tunaweza kukamatwa,” alisema kijana
huyo.
“Wewe unataka tufanye nini?”
“Ni lazima tumlevye huyu msichana.”
“Kivipi?”
“Kwa kutumia madawa ya usingizi. Tutumieni hata Phenometriphone, sumu yenye
nguvu ambayo ikimpata mtu kwenye ngozi yake, ndani ya dakika arobaini, atalewa
na kulala kwa usingizi mzito,” alisema kijana huyo.
“Baada ya hapo?” aliuliza Dracula.
“Ndipo tutamuua kwa kuingia chumbani kwake bila kipingamizi,” alisema kijana
huyo.
Wazo alilolitoa liliungwa mkono na kila mtu, hakukuwa na mtu aliyekataa,
kumlevya msichana huyo kabla ya kumuua lilionekana kuwa jambo jema ambalo
kama wangelifanya, lingewapa urahisi, na wasingeweza kugundulika kwa urahisi.
Kitu walichokifanya ni kuanza kutafuta sumu hiyo. Waliuona ugumu uliokuwepo
mbele yao, isingekuwa kazi nyepesi kuuziwa dawa hiyo pasipo kuwa na kibali
kutoka kwa daktari ila kwa kuwa walikuwa na fedha, waliamini kwamba kila kitu
kingekuwa chepesi.
Wakaondoka na kwenda kwenye duka la dawa, Dracula ndiye aliyekuwa mteja wa
kununua sumu hiyo, alipofika kwenye duka moja la dawa, muuzaji alikataa
kumuuzia, alichokifanya ni kutoa noti za dola, akaweka mezani dola elfu moja,
harakaharaka akapewa sumu aliyoitaka na glavu.

159
“Ila usinichome,” alisema muuzaji huyo.
“Usijali.”
Dracula akaondoka na kurudi hotelini, huko akaonana na marafiki zake na
kuwaambia kile kilichoendelea ambapo alikuwa na sumu hiyo iliyokuwa kwenye
kikopo kidogo.
Aliwaambia kwamba walitakiwa kuwa na gravu, alikuja nazo hivyo kujiandaa
huku yeye ndiye aliyetakiwa kumpaka msichana Stacie sumu ile.
“Tujadiliane, tutampaka vipi?” aliuliza Dracula.
“Kazi nyepesi sana, niachie mimi. Kitu cha msingi, yule kijana anayepokea mabegi
watu wanaokuja hotelini, ile nafasi tunatakiwa kuwa nayo sisi,” alisema kijana
aliyetoa wazo, kijana mwenye akili nyingi, huyu aliitwa Stephen, ila alipendwa
kuitwa Steph.
Walichokifanya ni kusubiri, waliposikia kwamba msichana huyu alikuwa kwenye
ndege, wakawasiliana na kijana aliyekuwa akihusika kupokea wageni na
kumwambia kwamba walitaka kuzungumza naye, kijana yule pasipo kujua hatari
iliyokuwepo, akawafuata chumbani, hukohuko wakamfunga kamba miguuni na
mikononi huku wakimuwekea plasta kubwa mdomoni.
Steph akachukua mavazi ya kijana yule na kuyavaa kisha kutoka ndani ya chumba
hicho. Kwa kuwa hoteli ilikuwa kubwa, tena ikiwa na wafanyakazi wengi ilikuwa
kazi ngumu sana kugundua kwamba kijana huyo hakuwa mmoja wa wafanyakazi.
Tayari mkono wake wa kulia aliupaka sumu ile na aliyekuwa akimsubiri alikuwa
Stacie tu. Baada ya dakika ishirini, kelele za watu zikaanza kusikika kuonyesha
kwamba msichana huyo alikuwa akikaribia kuingia mahali hapo.
Harakaharaka Steph akapiga hatua, gari liliposimama, akaufungua mlango, watu
wakawa wanampiga picha Stacie, alipoteremka tu, akampa mkono, wakasalimia
tena kwa kushika kiuhakika kana kwamba walikuwa wakifahamiana, baada ya
hapo, akachukua mabegi yake huku tayari akiwa amekwishampaka sumu ile
Stacie.
“Tayari! Kwisha habari yake,” alisema Steph huku akiwa ameshika mabegi ya
Stacie aliyekuwa akiwasalimiana na mashabiki zake, alipofika mapokezi, mizigo
akaitelekeza, akapandisha juu mpaka katika chumba walichokuwepo wenzake na
yeye kuingia.

160
“Imekuwaje?” aliuliza Dracula.
“Kila kitu tayari,” alijibu Steph huku akitoa tabasamu pana.
Kwa kumwangalia, Stacie alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama
kulikuwa na watu waliokuwa wakimpenda kama ilivyokuwa, kila alipowaangalia,
moyo wake ulikuwa na furaha tele.
Ni kweli alipendwa lakini watu waliojitokeza hotelini siku hiyo walikuwa wengi,
ilimshangaza, alichokifanya baada ya kusaini vitabu vya mashabiki hao ni
kuondoka na kuelekea ndani ya hoteli hiyo ambapo tayari kilikwishaandaliwa.
Alipokaa kitandani na kuanza kuvua nguo zake, akaanza kujisikia hali ya tofauti,
mwili ulichoka na macho yake yakawa mazito, alishindwa kujua nini kiliendelea
kwani dakika chache zilizopita wakati akiingia ndani ya hoteli hiyo, alijisikia
vizuri kabisa, hakuwa na uchovu wowote ule.
Akapuuzia, akaendelea kuvua nguo zake lakini ghafla akajikuta akilala kitandani,
usingizi mzito ukampitia, hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
Dracula na vijana wake waliokuwa ndani ya kile chumba, harakaharaka wakatoka
na kuelekea chumbani kule, walijua kwamba mpaka muda huo msichana Stacie
alikuwa amelala kutokana na kuzidiwa sumu ile aliyopakwa.
Mlango haukuwa umefungwa, ulikuwa wazi walichokifanya ni kuufungua na
kuingia ndani. Walimuona msichana huyo akiwa kitandani, hakuwa akijitambua,
alizidiwa na sumu aliyokuwa amewekewa, hawakutaka kuchelewa, walichokifanya
ni kuanza kumnyonga hapohapo kitandani, tena kwa kumziba pua na mdomo.
Wala hawakupata ushindani wowote ule, walifanikiwa kufanya walichotaka
kukifanya kwa asilimia mia moja, baada ya kuhakikisha mapigo ya moyo
yamesimama, wakachukua dawa za kulevya na bomba la sindano kisha kumchoma
kwenye mkono wake na kuziweka alama za vidole vya Benjamin kwa kutumia
plastini yenye unyevuunyevu kama kawaida, baada ya hapo wakaacha fedha
walizotakiwa kuziacha na kisha kuondoka mahali hapo huku wakiwa
wamefanikiwa.
Taarifa zilisikika usiku uleule baada ya mhudumu kufika ndani ya chumba hicho
kwa ajili ya kumhudumia msichana huyo. Alipofika, akaanza kuugonga mlango ili
afunguliwe lakini hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika kutoka ndani, ukimya
mkubwa ulikuwa umetawala.

161
Alichokifanya mhudumu huyo ni kwenda mapokezini ambapo huko akahitaji dada
wa hapo apige simu katika chumba hicho ili azungumze na Stacie na kumwambia
kwamba walitaka kumhudumia kwa kumpelekea chakula.
Simu ya ndani ya chumba alichokuwa Stacie ikaanza kuita, iliita na kuita lakini
haikupokelewa kitu kilichoonekana kuwashangaza sana. Hawakutaka kukubali,
wakampigia simu meneja wake, haraka sana, simu ikapokelewa.
“Upo na Stacie?” aliuliza dada wa mapokezi baada ya salamu.
“Hapana! Yupo chumbani kwake, kwa nini unauliza hivyo?” aliuliza Robert.
“Tunampigia simu, hapokei, unaweza kumpigia kwani tunahitaji kumuhudumia,”
alisema msichana huyo.
“Hakuna tatizo, namfuata hukohuko chumbani,” alisema Robert na kukata simu.
Akatoka chumbani humo na kwenda chumbani kwa Stacie kwa lengo la
kuzungumza naye kwamba wahudumu walitaka kumhudumia, alipoufikia mlango,
akagonga hodi, kama ilivyokuwa kwa wahudumu, naye ilitokea vilevile, hakukuwa
na sauti yoyote iliyosikika kutoka ndani.
“Stacie, fungua mlango,” alisema Robert lakini hakukuwa na majibu yoyote yale.
Alichokifanya ni kuufungua mlango na kuingia ndani, taa zilikuwa zikiwaka,
alipigwa na mshtuko mkubwa baada ya kuangalia kitandani na macho yake kutua
kwa msichana Stacie aliyekuwa amefariki kitandani pale.
Robert akachanganyikiwa, hakutaka kubaki chumbani humo, harakaharaka akatoka
na kumpigia simu mbunifu wa mavazi, Alejandro na kumwambia kile kilichokuwa
kimetokea.
“Unasemaje?” aliuliza Alejandro huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hivyo! Ngoja nikatoe taarifa...”
Robert alionekana kuchanganyikiwa, akatoka hapo na kwenda mapokezini huku
akikimbia, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea, kwake, ilionekana kama ndoto
fulani hivi ambapo baada ya muda angeamka na kujikuta akiwa kitandani.
Alipofika mapokezi, kila mtu akabaki akimwangalia, hawakujua sababu
iliyomfanya kutoka chumbani kwake na kuja mahali hapo huku akionekana kuwa
kwenye presha kubwa.

162
“Kuna nini?”
“Ninataka kuongea na uongozi,” alisema Robert, watu waliokuwa pembeni, nao
wakamsogelea, walitaka kujua kuna nini.
“Kuna nini kaka?”
Hapo ndipo Robert alipoanza kuhadithia kile alichokutana nacho chumbani kwa
Stacie, hawakuamini, walichokifanya wahudumu hao ni kwenda huko chumbani
kuhakikisha.
Kile walichoambiwa ndicho walichokutana nacho, msichana Stacie alikuwa
kitandani, hakuwa akipumua, alikufa kwa kunyongwa lakini kwa jinsi
ilivyoonekana, alionekana kama mtu aliyekuwa akijidunga madawa ya kulevya.
“Alikuwa akijidunga!” alisema mhudumu mmoja.
“Nashangaa! Sikuwahi kumuona akitumia madawa ya kulevya, si hivyo tu, hata
kusikia tetesi sehemu yoyote ile,” alisema Robert.
“Sasa imekuwaje leo atumie madawa ya kulevya?”
“Hata mimi nashangaa.”
Kwa kuwa hawakuwa na maneno yoyote yale, walichokifanya ni kumpigia simu
meneja wa hoteli hiyo ambaye alifika na kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea,
hawakumpigia huyo tu, bali waliwapigia simu polisi ambao kwa haraka sana
wakafika mahali hapo.
Kile walichokiona hakikuwa kigeni katika macho yao, katika kipindi hicho, watu
waliokufa hotelini walikufa kwa staili hiyohiyo na muuaji alikuwa mmoja tu, huyo
alikuwa Benjamin.
Polisi hawakutaka mwili huo uguswe, bado walitakiwa kuuchunguza na kugundua
kifo chake kilisababishwa na nini. Kitendo cha wahudumu kugundua kwamba
msichana Stacie alikuwa amekufa chumbani humo, taarifa hizo wakaanza
kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.
Kila mtu aliyezipata, alishtuka, hawakuamini kile walichokiona kwamba msichana
huyo alikuwa amekufa ndani ya chumba cha hoteli. Hawakutaka kujiuliza sana,
wakajua kwamba muuaji alikuwa yuleyule aliyekuwa akitafutwa kila kona,
Benjamin ambaye mpaka katika kipindi hicho hakukuwa na mtu aliyejua mahali
alipokuwa.

163
“Ila kwa nini anaua jamaniiii?” aliuliza msichana mmoja huku akiwa ameishika
simu yake, kile alichokiona, hakukiamini hata kidogo.
“Mimi mwenyewe nashangaa...halafu yeye anaua masupastaa wanaochipukia, kwa
nini lakini?” alisema msichana mwingine.
Ndivyo ilivyokuwa. Taarifa zile ziliendelea kusambaa kila kona, watu walilia
kwani hakukuwa na msichana ambaye waliamini kwamba angefanikiwa na kuwa
na mashabiki wengi kama Stacie kutokana na mvuto aliokuwa nao.
Baada ya siku mbili mwili kuchunguzwa, taarifa zikasikika kwamba muuaji
alikuwa yuleyule, mtu hatari aliyeogopwa, Benjamin ambapo kwa kipindi hicho,
FBI waliamua kumtafuta kwa nguvu kubwa kwani pasipo kufanya hivyo,
angeendelea kuua.
****
“David! Umefikia wapi?” aliuliza Benjamin kwenye simu.
“Kila kitu tayari, ushahidi upo wa kutosha, nikutumie kwenye barua pepe?’ aliuliza
David.
“Sawa. Nitumie, hata kama kuna sauti nitumie pia,” alisema Benjamin.
“Hakuna tatizo. Ila unajua kwamba keshokutwa pia kuna mauaji yatafanyika?”
aliuliza David.
“Hapana! Imekuwaje tena?”
“Huyu jamaa anataka kumuua mrembo wa dunia.”
“Unasemaje?”
“Ninavyoongea tayari kashatuma watu kwenda Las Vegas kwa ajili ya kufanikisha
mpango huo,” alisema David.
“Kwa hiyo atatumia alama zangu za vidole?”
“Nadhani!”
Benjamin akabaki kimya kwa muda, hakutaka kuendelea na mazungumzo hayo,
hapohapo akakata simu. Alikuwa kwenye mawazo mengi, hapo alipokuwa,
haikuwa sehemu sahihi ya yeye kuwepo kwani alihisi kwamba muda wowote ule
angekamatwa.

164
Alipanga kuondoka Boston na kuelekea New York, alitulia katika viti vya abiria
katika kituo cha treni cha Smallville, alitaka kukimbilia huko kwani hapo Boston
hakukuonekana kuwa salama katika maisha yake.
Japokuwa kulikuwa na watu wengi kituoni hapo lakini hakukuwa hata na mmoja
aliyekuwa amemgundua. Aliendelea kubaki hapo mpaka treni ilipofika, haraka
haraka akasimama na kwenda kuingia ndani, akatafuta kiti na kutulia.
Treni haikusimama sana kituoni hapo ikaanza safari ya kuelekea jijini New
York.Humo ndani ya treni, hakutaka kumwangalia mtu yeyote yule, alikuwa kimya
huku muda wote akiwa anaangalia chini na huku kofia ikiwa kichwani mwake.
Wakati akiwa katika hali hiyo, ghafla akashtukia kuona wanaume wawili
waliokuwa wamevalia suti wamesimama mbele yake, harakaharaka akayainua
macho yake na kuwaangalia watu hao, hawakuzungumza kitu, walibaki
wakimwangalia, walipomuona kama mtu aliyechanganyikiwa, wakatoa beji zao
zilizoonyesha kwamba walikuwa maofisa wa FBI.
“Upo chini ya ulinzi Benjamin. Hatutaki ulete fujo, tulia hivyohivyo,” alisema
ofisa mmoja. Benjamin akatii. Wanaume hao wakakaa pembeni yake, mmoja
upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
****
FBI walikuwa na kazi kubwa mbele yao, hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza
kumpata Benjamin ambaye alionekana kuwa mtu hatari sana, mtu ambaye
hakutaka kuachwa akitanua mitaani hata mara moja.
Mauaji mengi yalitokea, yaliitetemesha Marekani na duniani kote kwa kuwa hao
waliouawa walikuwa watu maarufu sana, watu waliofanikiwa kuiteka mioyo ya
watu wengi duniani.
Walikesha usiku na mchana, walitegesha kamera sehemu nyingi hasa katika Jiji la
Boston ambapo huko ndipo waliamini Benjamin alikuwepo katika kipindi hicho.
Watu waliopewa kazi ya kumfuatilia usiku na mchana hawakutakiwa kulala hata
mara moja, walipewa agizo kwamba walitakiwa kuhakikisha kamera zinafanya
kazi kila saa na kila kitu kitakachokuwa kikiendelea kiwe kinarekodiwa.
Hilo halikuwa tatizo, watu wa IT kutoka katika shirika hilo la kijasusi wakawa
wanafanya kazi zao kama vile walivyoagizwa. Siku ziliendelea kukatika mpaka

165
walipofanikiwa kumuona mtu aliyefanana na Benjamin akiingia katika Kituo cha
Treni cha SmallVile.
Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuivuta picha yake kwa karibu, hakuwa
akionekana vizuri lakini kingine walichokifanya ni kuichukua picha yake nyingine
ambayo alikuwa akionekana usoni na kisha kuilinganisha na picha ile.
Kila kitu kilifanana, kompyuta ikaandika neno 100 Match yaani ikimaanisha
kwamba kila kitu kilikuwa sawa kati ya ile picha ya kichwa na picha ie ambayo
ilipigwa katika kituo cha treni.
Walichokifanya ni kuwasiliana na maofisa wa FBI na kuwaambia kile kilichokuwa
kimetokea, harakaharaka wakawaagiza watu kuelekea huko huku wakiwatumia
picha jinsi alivyovaa ili asiweze kuwapotea.
Hilo halikuwa na tatizo, wakaondoka kuelekea huko. Walikuwa maofisa wawili
waliokuwa na bunduki, kama kawaida yao walivalia suti nyeusi. Walikwenda
mpaka walipofika katika kituo hicho cha treni.
Haikuwa kwenda na kumuona bali walitakiwa kumtafuta na kuona alikuwa wapi,
hivyo ndivyo walivyofanya, wakajifanya kuwa bize, waligawana kila mtu kuwa
kivyake, kwa bahati nzuri wakati treni imefika, wakafanikiwa kumuona akisimama
harakaharaka kuifuata treni, akaingia ndani na safari kuanza.
****
Muda wote msichana Vivian alikuwa akilia tu, hakuamini kama mwisho wa siku
angekamatwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho kilichokuwa na giza totoro.
Alipiga kelele kuhitaji msaada wa kutolewa ndani ya chumba hicho lakini
hakukuwa na mtu aliyejali, hata mtu wa kuufungua mlango huo hakutokea kabisa,
bado chumba kilikuwa kimefungwa.
Saa zilisogea, alipoona amepiga sana kelele pasipo kupata msaada wowote ule
akaamua kubaki kimya na kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea. Baada ya
kukaa ndani ya chumba hicho kwa saa kadhaa, mlango ukafungiliwa, mwanaume
mmoja aliyekuwa na tochi akaingia na kummulika tochi usoni, mkononi alikuwa
ameshika sahani iliyokuwa na chakula, alichokifanya ni kumrushia pale alipokuwa.
“Please let me out of here,” (Naomba unitoe hapa, tafadhali) alisema Vivian huku
akilia.

166
“We can’t let you out of here, you have ten minutes to eat your damn food,”
(hatuwezi kukutoa hapa, una dakika kumi za kula chakula chako) alisema
mwanaume yule kisha kuufunga mlango.
Vivian akaanza kutambaa pale sakafuni, aliona wakati sahani ikisukumwa kule
alipokuwa hivyo alitambaa kwa hisia kwamba sahani ilikuwa sehemu fulani. Hiyo
ilimfanya kuwa rahisi sana kuipata sahani hiyo ambapo akaichukua na kuanza
kula.
Alikuwa kwa kuwa alikuwa na njaa lakini hakuona radha yoyote ya chakula hicho,
alitumia dakika saba tu kula, alipomaliza, akajisogeza pembeni na kuanza kulia
tena.
Hakuona kama angeweza kutoka ndani ya chumba hicho, watu waliokuwa
wamemkamata, hawakumtaka yeye, wao walimtaka Benjamin ambapo hakujua
kama kulikuwa na kosa lolote alilolifanya mpenzi wake mpaka watu hao kumtafuta
na kutaka kumuua kwa gharama zozote zile.
Alitamani kuwapigia simu watu wake wa karibu na kuwapa taarifa lakini
alishindwa kufanya hivyo kwani kipindi alichokuwa ametekwa, hakuwa na simu
yoyote ile, alifikishwa humo ndani akiwa mikono mitupu.
Alichokifanya ni kumuomba Mungu kwani hakukuwa na njia nyingine ambayo
ingemuwezesha kutoka ndani ya chumba hicho kwani hao watu waliomkamata,
walionekana kutokuwa na masihara hata kidogo.
“Wewe ni muuaji,” alisema polisi mmoja aliyekuwa na koti lililoandikwa BPD
yaani Boston Police Department.
“Hapana! Mimi si muuaji,” alisema Benjamin huku akimwangalia mwanaume
huyo usoni, hakuwa peke yake, alikuwa na wanaume wengine, wote walikuwa
polisi.
Walimkamata Benjamin kwa kuwa walihisi kwamba yeye ndiye aliyekuwa
akifanya mauaji ya watu wote waliokuwa wameuawa vyumbani mwao, walikuwa
na uhakika kwa sababu alama za vidole vyake zilikutwa katika miili ya maiti hizo
na baadhi ya vitu ndani ya chumba hicho.
Benjamin alikuwa akilia huku akiendelea kujitetea kwamba hakuwa muuaji,
hakuwahi kuua kama dunia ilivyokuwa ikijua bali kulikuwa na mtu nyuma ya kila
kitu kilichokuwa kikiendelea.

167
Kukamatwa kwake ilikuwa siri kubwa, hakupewa mwandishi wa habari yeyote
yule, waliwaacha Wamarekani waendelee kuwalaumu lakini walitaka kufanya vitu
vyao kwa mpangilio kwani kama taarifa zingetoka na kusema kwamba
walimkamata Benjamin, wangeweza kuharibu kila kitu.
“Tunajua kwamba hujafanya mauaji Benjamin japokuwa alama za vidole vyako
zimekutwa katika maiti zilizokuwa katika vyumba,” alisema polisi mmoja.
“Kweli sijafanya mauaji.”
“Sawa! Ila kama hukufanya, nani alifanya?” aliuliza mwanaume huyo.
Hapo ndipo Benjamin akaanza kusimulia kila kitu kilichotokea tangu siku ya
kwanza alipopigiwa simu na Bwana Seppy na kuambiwa kazi kubwa ya kufanya
mauaji iliyokuwa mbele yake, aliwaambia wazi kwamba alikataa hivyo kumteka
yeye na mpenzi wake, wakamtisha lakini pamoja na hayo yote, alikataa kufanya
mauaji hayo.
“Ikawaje?”
“Walinipa simu ya iPhone, nilipoishika, nafikiri ndipo walipata alama za vidole
vyangu ambazo wamekuwa wakiziweka kila kona,” alisema Benjamin.
“Una chochote cha kushikilia dhidi ya Bwana Seppy?’ aliuliza polisi mmoja.
“Ndiyo! Nina rafiki yangu ambaye amekuwa akizifuatilia meseji na simu za mzee
huyu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kwa maana hiyo ushahidi upo wote,”
alisema Benjamin.
Polisi wale hawakutaka kuzungumza kitu chochote, walitaka kufahamu kama
kulikuwa na ushahidi kwani kumfikisha mahakamani mtu mzito kama Bwana
Seppy haikuwa rahisi, ilikuwa ni lazima ujikamilishe kwa kila kitu.
Mara baada ya kukata walichokitaka, hapohapo polisi hao wakatoka ndani ya
chumba kile. Benjamin akabaki kimya, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele,
hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake.
Hapo ndipo mawazo juu ya mpenzi wake, Vivian yalipomjia kichwani mwake,
hakujua alikuwa wapi baada ya kutekwa, kabla ya kufanya kitu chochote ilikuwa
ni lazima ajue mahali alipokuwa.

168
Wakati akiwa kwenye mawazo lukuki, hapohapo mlango ukafunguliwa na
wanaume wawili waliokuwa na makoti yaliyosomeka FBI wakaingia na kukaa
katika viti vilivyokuwa chumbani humo.
Mwanaume wa kwanza alijitambulisha kwa jina la Brett Phillip na mwingine Ryan
Cashman. Watu hao walifika mahali hapo kwa kuwa walitaka kumuhoji maswali
kadhaa juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Sikuwahi kuua, nililazimishwa kufanya hivyo ila nikakataa,” alisema Benjamin
huku akiwaangalia wanaume hao usoni, tena kwa zamu.
“Kama hukuua, nani aliua?” aliuliza Brett.
Kama alivyowaambia polisi wale ndivyo alivyowaambia hata maofisa hao wa FBI
kwamba hakuhusika katika mauaji hayo bali kulikuwa na mtu mwingine ambaye ni
bilionea ndiye aliyehusika katika mauaji yote yaliyotokea.
“Bwana Seppy! Haiwezekani,” alisema Brett.
“Ndiyo hivyo! Ushahidi upo tayari, kama hamuamini, natumaini kuna siku
mtaamini, hasa tutakapokwenda mahakamani,” alisema Benjamin.
****
Taarifa za ndani kabisa zilisema kwamba yule muuaji aliyekuwa akitafutwa kwa
udi na uvumba, Benjamin alikuwa amekamatwa jijini Boston na hivyo kushikiliwa
na polisi.
Kila aliyezisikia taarifa zile, hakuamini masikio yake kama kweli muuaji huyo
aliyekuwa akichukiwa kila kona alikuwa amekamatwa na polisi. Taarifa hizo
zilisambaa kwa kasi kubwa kama moto wa kifuu, kwenye mitandao ya kijamii,
taarifa hizo zilisambazwa kila kona kiasi kwamba watu wengine wakahisi kwamba
hazikuwa na ukweli wowote ule.
Hapo ndipo watu walipoamua kutaka kumuona huyo Benjamin. Wengi wakahisi
kwamba zilikuwa taarifa za uongo ambazo zilitengenezwa na polisi ili waweze
kujisafisha kutokana na uchafu waliokuwa nao wa kushindwa kumtafuta Benjamin
na kumkamata.
Polisi hawakutaka kuzungumzia lolote lile, walikuwa na msemaji ambaye yeye
ndiye aliyehusika kutoa taarifa kwa wananchi, kwa kuwa taarifa hizo zilivuja,
hawakutaka kuthibitisha juu ya hilo.

169
Baada ya taarifa hizo kusambaa kila kona, siku mbili baadaye ndipo polisi
walipothibitisha kukamatwa kwa Benjamin na hivyo kuwaambia wananchi
kwamba mua wowote ule kuanzia kipindi hicho angefikishwa mahakamani
kusomewa mashitaka kwa kile alichokuwa amekifanya.
Hicho ndicho kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa, watu wakaandaa
mabango yao na kuandika jumbe nzito kwamba mahakama isilete masihara katika
kesi hiyo, ilikuwa ni lazima kumhukumu Benjamin kwa kosa la mauaji kwa kile
alichokuwa amekifanya.
“Just hung him,” (Mnyonge) liliandikwa bango moja.
Watu hawakuishia kuandika mabango hayo tu bali siku iliyofuata wakaanza
kuandamana kuitaka mahakama imuhukumu kifo Benjamin kwa kile kilichotokea.
Muda wote wakati hayo yakiendelea, Benjamin alikuwa sero, huko hakutakiwa
kuzungumza na mtu yeyote yule, alitakiwa kukaa hivyohivyo mpaka pale kesi
ingeanza kusikilizwa.
Mtu pekee aliyeruhisiwa kuingia na kuzungumza naye alikuwa mwanasheria wake
ambaye alimhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea na kwamba hakuhusika
katika mauaji hayo yaliyokuwa yametokea.
“Kwa hiyo unamaanisha Bwana Seppy ndiye aliyefanya mauaji?” aliuliza
mwanasheria wake, Bwana Donald Gilphin.
“Ndiyo! Ushahidi upo wa mawasiliano yake aliyokuwa akiyafanya,” alisema
Benjamin.
“Kama yapo, hakuna tatizo, hapo ndipo ninapopataka,” alisema mwanasheria.
Mitaani hakukukalika hata mara moja, kila kona, watu walikuwa wakiandama
huku wakiishinikiza mahakama kumuhukumu kifo Benjamin kwa kile kilichokuwa
kimetokea kwa kuua watu wengi ambao walitabiriwa kuwa mastaa wakubwa hapo
baadaye.
Maandamano hayo yalikusanya watu wengi, si hapo Boston tu bali katika sehemu
mbalimbali nchini Marekani watu walizidi kuandamana kila siku. Kama kuanza,
walianza hapo Boston, wakaitikia Texas, New Orleans, New York, Washington na
sehemu nyingine nyingi, kote huko walitaka kushuhudia Benjamin akihukumiwa
kifo tu.

170
Siku ziliendelea kukatika, baada ya siku kadhaa, Benjamin akachukuliwa na
kufikishwa mahakamani. Siku hiyo ilikuwa ni hatari mitaani, watu walikuwa na
mabango yaliyoitaka mahakama imuhukumu kifo Benjamin kwa kile kilichokuwa
kimetokea.
Moyo wake uliumia sana kwani alijua kwamba hakuua na wala hakuwahi kuua
lakini hilo watu hawakulielewa, alitamani sana kuwaambia watu wote ukweli juu
ya kilichokuwa kimetokea lakini hakupata muda huo, hasa siku ya kwanza
kusikiliza kesi.
Siku hiyo, alisomewa mashitaka tu na kisha kesi yake kupangwa kusikilizwa baada
ya wiki mbili, baada ya hapo alitakiwa kuwasubiri watu wengine na kisha safari ya
kuelekea rumande kuanza. Pale alipokuwa, hakuwa na amani kabisa, watu walitaka
kuona akihukumiwa kifo tu na si vinginevyo.
Waandishi wa habari hawakuwa nyuma, wakati yeye na watu wengine
wakipelekwa katika basi kubwa la gereza, wakaanza kupiga picha kwani kwa
kipindi hicho, Benjamin alikuwa biashara kubwa sana mitaani.
“I hate him...” (ninamchukia) alisikika mwanamke mmoja aliyekuwa mahakamani
hapo.
“I hate him too, he is not supposed to live,” (hata mimi namchukia, hastahili
kuishi) alisikika mwanamke mwingine.
Hicho ndicho kilichokuwa ndani ya mioyo ya Wamarekani, hawakumpenda kabisa
Benjamin, walimchukia kwa kuwa waliamini kwamba yeye ndiye aliyehusika
katika mauaji yote yaliyokuwa yametokea.
Moyo wake haukuacha kuuma, kila siku maumivu yalikuwa ni sehemu ya maisha
yake. Kwa sababu kitu kilichokuwa kikisubiriwa ni kujitetea mahakamani
kutokana na yale yaliyokuwa yametokea, hivyo wazazi wake na baadhi ya ndugu
zake wakaruhusiwa kuzungumza naye tena huku akiwa chini ya ulinzi mkali.
“Ni kweli uliua mwanangu?’ aliuliza baba yake.
“Hapana baba! Sijaua, niliambiwa niue lakini nikakataa.”
“Nani alikwambia?”
“Bwana Seppy! Sijajua kwa nini alitaka kuua kipindi hicho ila yeye ndiye
aliyehusika katika mauaji yote na kuacha alama za vidole vyangu,” alijitetea
Benjamin.

171
“Ilikuwaje hapo?”
Hapo ndipo Benjamin alipoanza kuhadithia kila kitu, hakutaka kuficha kitu
chochote kile kwani aliamini kupitia wazazi wake na baadhi ya ndugu
waliokuwepo hapo alipokuwa wangeweza kuibadilisha mioyo ya watu wote
duniani ambao walikuwa wakiamini kwamba aliua kumbe hakufanya hivyo.
“Nitasimama kidete mpaka kijana wenu ashinde, hii kesi haina nguvu tena,”
alisema mwanasheria wake ambaye naye alisimama kama wakili wake, Donald.
Siku ziliendelea kukatika mpaka ilipofika siku ya kupandishwa tena mahakamani.
Kama kawaida watu wengi walikusanyika mahakamani hapo, walitaka kushuhudia
kile ambacho kingeendelea na Benjamin angejitetea vipi juu ya yale mauaji
aliyokuwa ameyafanya.
Wakati akiingia mahakamani, watu walianza kuzomea, hawakutaka kabisa
kumuona katika uso wa dunia, walitaka kuona akihukumiwa kifo kwani hata kama
angefungwa kifungo cha maisha gerezani bado watu wasingeridhika kabisa
kutokana na mauaji aliyokuwa ameyafanya.
Maofisa wa FBI walikuwepo mahakamani hapo, walikuwa wakifuatilia kila kitu,
waliufahamu ukweli uliokuwa umejificha, walimwangalia Benjamin, walimuonea
huruma kwani hakuwa ameua kama dunia ilivyokuwa ikiamini.
Baada ya dakika kadhaa, hakimu ambaye alitakiwa kusikiliza kesi hiyo akaanza
kuingia ndani ya mahakama hiyo, watu wote waliokuwa humo ndani wakasimama
kama kumpa heshima, walipomwangalia, wakagundua kwamba alikuwa McRegan,
miongonimwa mahakimu waliokuwa na rekodi kubwa ya kuwahukumu watu vifo.
Kidogo mioyo yao ikaridhika, kitendo cha kumuona McRegan akiingia mioyo yao
ilikuwa na furaha tele kwa kuona kwamba hatimaye kilio chao kilisikika na
mambo yangekwenda vizuri kabisa kama walivyotaka iwe mioyoni mwao.
Baada ya hakimu kukaa, watu wote hapo mahakamani wakakaa na kuanza
kusikiliza. Kesi kwanza ikaanza kusikilizwa kwa muda kisha kupewa nafasi
upande wa mshtaki ambaye ni Jamhuri ya Marekani, wakili wake, Bwana Peters
akasimama na kuanza kumuuliza maswali Benjamin.
“Bila shaka unaitwa Benjamin Saunders,” alisema Peters.
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Unajua kwa nini upo hapa?”

172
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Upo hapa kwa kosa la mauaji, ni kweli?”
“Ni kweli mheshimiwa.”
“Ni kweli uliua?”
“Hapana!”
“Sasa kama hukuua, kwa nini upo hapa?”
“Kwa sababu nimesingiziwa kuua.”
“Ila alama za vidole vyako vilikutwa katika kila mwili wa marehemu,
unalizungumziaje hilo? Tuna majibu ya vipimo vyote, picha zako zilibandikwa kila
kona, kila mtu anajua kwamba wewe ni muuaji, unakataa pia?’ aliuliza Peters.
“Ndiyo mheshimiwa. Ninakataa kwa sababu sikuua!”
“Kama kweli hukuua, kwa nini ulikuwa uunajificha baada ya kugundua kwamba
unatafutwa?” aliuliza Peters.
“Nilikuwa najificha si kwa sababu niliua, ila nilikuwa najificha kwa sababu
nilitakiwa kuuawa muda wowote ule,” alisema Benjamin.
“Ulitakiwa kuuawa! Na nani?”
“Bwana Seppy, huyu bilionea,” alijibu Benjamin, minong’ono ikaanza kusikika
humo mahakamani.
“Kwa nini alitaka kukuua?”
“Kwa sababu nilikataa kuua.”
“Kumuua nani?”
“Wote nilioambiwa kwamba nimeua.”
“Kivipi?”
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake, hakutaka kuchelewa, akaanza kuhadithia kila kitu
kilichotokea katika maisha yake, alianzia tangu siku ya kwanza kabisa alipopigiwa
siku wakati alipokuwa jijini Washington, kipindi ambacho yeye na Wamarekani
wengine walitaka kumsikiliza rais katika hotuba ambayo alitakiwa kuitoa katika
siku hiyo ya uhuru wa Marekani.

173
Hakuishia hapo, alizungumzia namna alivyopigiwa simu na mtu asiyemfahamu
ambaye alimtaka kuonana naye sehemu fulani, alitii kwani kama asingefanya
hivyo mpenzi wake angeuawa.
Ilikuwa ni simulizi iliyochukua zaidi ya dakika ishirini, mahakama ilikuwa kimya
ikimsikiliza. Alisimulia huku akionekana kuumizwa sana na muda wote alikuwa
akilia tu.
Aliiambia mahakama kwamba hakuua bali Bwana Seppy ndiye aliyeua na hata
alama za vidole vyake zilitengenezwa baada ya kupewa simu ya iPhone kwa ajili
ya mawasiliano, kitendo cha kuishika simu ile tu, akawa ameacha alama za vidole
vyake.
“Mheshimiwa hakimu, kwa mamlaka ya mahakama, naomba Bwana Seppy
akamatwe na kufikishwa mahakamani kwani tumegundua kwamba mteja wetu
hana hatia,” aliingilia wakili wake, Bwana Donald japokuwa haikuwa ikiruhusiwa.
Hakimu hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutoa amri Bwana Seppy afikishwe
mahakamani kwani kwenye kesi ile na yeye alitajwa kama mhusika katika mauaji
yale. Mahakama ikawa kimya, mpaka katika kipindi ambacho Benjamin alikuwa
akishuka kizimbani, watu walibaki wakimwangalia kwa huruma kubwa.
Kila kitu kikabadilika, chuki walizokuwa nazo watu dhidi yake zikaanza kupotea
mioyoni mwao baada ya kugundua kwamba hakuwa muuaji bali aliambiwa aue
lakini akakataa na hivyo ujanja kufanyika kwa ajili ya kumuingiza matatani.
“Hii kesi utashinda. Ila ushahidi unao?” aliuliza Bwana Donald.
“Upo! Ni lazima tumtafute David, ana ushahidi wote, kama hatutompata,
tutashindwa,” alisema Benjamin.
“Basi sawa. Nitawasiliana na polisi ili waweze kuwasiliana naye, baada ya wiki
mbili, ushahidi uwe tayari,” alisema Donald.
“Nitashukuru.

174
SURA YA SITA

BWANA Seppy alikuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, Dracula


aliyekuwa mahakamani kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtumia ujumbe mfupi juu
ya kila kitu kilichokuwa kikijiri huko.
Moyo wake ulikuwa na hofu kubwa baada ya Benjamin kupinga kufanya mauaji
hayo na mwisho wa siku kulitaja jina lake. Aliiona dunia ikiwa imemuangukia,
kila mtu mbele yake alikuwa akimzomea na mbaya zaidi aliiona milango ya
gerezani ikifunga na yeye kuchukuliwa na kuingizwa humo.
Alisikitika mno, alijuta na wakati mwingine alikuwa akijiulaumu juu ya sababu
iliyomfanya kufanya mauaji yale na wakati alikuwa na uwezo wa kukaa kimya na
maisha kuendelea kama kawaida.
Siku hiyohiyo akafuatwa na maofisa wa FBI ambao walimtaka kuondoka naye
kutoka hapo New York alipokuwa akiishi na kuelekea jijini Boston. Alijifanya
kutokujua kitu chochote kile, wakamwambia kwamba angepewa taarifa juu ya
kilichokuwa kikiendelea mara baada ya kufika katika kituo cha polisi.
Kipindi hicho polisi hawakuhusika, walijua kwamba mtu huyo alikuwa na jina
kubwa hivyo ingekuwa rahisi kwake kutengeneza watu wake katika vituo
mbalimbali vya polisi na ndiyo maana hata kwenye kumkamata, walikwenda
maofisa wa FBI na si polisi kama ilivyotakiwa iwe.
“Benjamin amekutaja kwamba umehusika katika mauaji, ni kweli?” aliuliza ofisa
wa FBI huku wakiwa wamemuweka ndani ya chumba kilichokuwa na kioo katika
upande mmoja wa ukuta, hakujibu kitu, akabaki kimya.
“Kuna ukweli?” ofisa huyo akauliza tena swali.
“Siwezi kuzungumza kitu chochote kile, namtaka mwanasheria wangu awe hapa,”
alisema Bwana Seppy.
Hilo halikuwa tatizo, walichokifanya ni kumpa simu yake na kumwambia
awasiliane na mwanasheria wake ambaye ndani ya dakika ishirini, alikuwa katika
kituo hicho.

175
Alitajwa na mtuhumiwa wa mauaji kwamba yeye ndiye aliyehusika katika mauaji
hayo, hivyo alitakiwa kujipanga kwani naye angepanda mahakamani na kujibu kesi
iliyokuwa ikimkabili.
“Unaona kama tunaweza kushinda kesi hii?” aliuliza Bwana Seppy, yeye
mwenyewe alikuwa na hofu.
“Kesi tunaweza kushinda kama huo ushahidi hautoweza kupatikana mahakamani,”
alijibu mwanasheria wake ambaye angemfanya kuwa wakili wake hapo baadaye.
“Kwa hiyo huo ushahidi inabidi upotee?”
“Ndiyo hivyo!”
Hilo halikuwa tatizo, kwa sababu Benjamin alisema kwamba kulikuwa na
ushahidi, Dracula na wenzake wakaanza kufuatilia na mwisho wa siku kujua
kwamba kulikuwa na mtu ambaye alifahamu kila kitu na ndiye ambaye alikuwa na
ushahidi, huyu alikuwa David Belshaaz, mmoja wa marafiki wa Benjamin
aliyekuwa akiishi hapo Boston na alikuwa akisomea masomo ya kompyuta katika
Chuo cha Harvard.
“Inabidi mmuue haraka iwezekanavyo,” alisema Bwana Seppy.
“Hakuna tatizo.”
Alichokifanya Dracula ni kuwatuma vijana wake waelekee katika Chuo Kikuu cha
Harvard kwa ajili ya kumtafuta huyo David. Vijana hao hawakutaka kupoteza
muda, harakaharaka wakaondoka kuelekea huko chuo ambapo baada ya kuulizia,
wakaambiwa kwamba kijana huyo alikuwa akiishi West Mania, mtaa uliokuwa na
wahuni wengi hapo Boston.
Mbele yake, David aliiona hatari kubwa, alijua kwamba baada ya Benjamin
kukamatwa na kujulikana kwamba yeye alikuwa na ushahidi wote kuhusu kile
kilichokuwa kikiendelea basi angetafutwa tu.
Alilijua hilo kwa kuwa kwenye kesi ile yeye ndiye alikuwa kila kitu, yaani yeye
ndiye alikuwa na uwezo wa kumfunga Benjamin na yeye ndiye alikuwa na uwezo
wa kumuweka huru kijana huyo.
Aliyapenda maisha yake na hakutaka kabisa kuona akikamatwa na kufikishwa
sehemu mbaya ambayo ingeyaweka maisha yake rehani na hata kuyapoteza kabisa.

176
Alijipanga kwa kila kitu. Kila siku alihakikisha anaondoka nyumbani asubuhi na
mapema kwenda maktaba, huko angekaa mpaka muda wa usiku wa manane
ambapo angerudi nyumbani na kutulia, tena akiwa amejificha mpaka pale wiki
mbili zingekatika na kutoa ushahidi wake mahakamani.
Hiyo ndiyo ilikuwa ratiba yake ya kila siku. Kila siku alipokuwa akirudi usiku wa
manane alikutana na hali ambayo alikuwa na uhakika kwamba kulikuwa na watu
waliingia ndani kwake kutokana na mazingira aliyoyaacha, hayakuwa yale
aliyoyakuta, akagundua kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakiingia.
Wakati alipokuwa akirudi nyumbani, hakuwa akirudi kwa uwazi, alirudi kwa
kificho sana kiasi kwamba hata majirani hawakuwa wakijua kama alikuwa akiishi
ndani ya nyumba hiyo, na ilipofika asubuhi, kama kawaida yake aliondoka kisiri
kuelekea maktaba kama kawaida yake.
“Mambo...” alisikia sauti ya msichana ikimsalimia kwa sauti ya chini kabisa.
David akageuka na macho yake kugongana na macho ya msichana mrembo mno,
alipomwangalia, ilikuwa rahisi sana kusema kwamba msichana huyo alikuwa
chotara, yaani alikuwa na mchanganyiko wa rangi, mzazi wake mmoja alikuwa
mtu kutoka Brazil na mwingine alikuwa Mzungu.
Kabla ya kuitikia salamu hiyo, David alibaki akimwangalia msichana huyo, mbali
na uzuri wa sura aliokuwa nao, alikuwa na umbo zuri, alivutia na ngozi yake
ilimdatisha kupita kawaida.
“Poa..” aliitikia.
“Kuna mtu hapa?” aliuliza msichana huyo.
“Wapi? Hapo? Hakuna mtu, karibu,” alisema David huku akionekana
kuweweseka.
Hakukuwa na kusoma tena, kila wakati macho yake yalikuwa yakimwangalia
msichana huyo kiwizi, alichanganyikiwa kutokana na uzuri aliokuwa nao, wakati
mwingine alihisi kwamba alikutana na malaika kwa jinsi alivyokuwa na uzuri wa
kuvutia.
Alikuwa kama bubu, hakujua ni kitu gani alitakiwa kumwambia msichana huyo
kwani ukweli ni kwamba alimpenda sana na asingeweza kumuacha kabisa,
alijiuliza maswali mengi juu ya namna ya kumuingia msichana huyo mrembo.
“Naitwa David Belshaaz,” alijitambulisha huku akimpa mkono.

177
“Naitwa Veronica Twingle,” alijitambulisha msichana huyo kwa sauti ya chini ili
wasiwasumbue watu wengine waliokuwa kwenye maktaba hiyo.
“Unasoma wapi?”
“Nasoma UCLA, nimekuja huku kwa ajili ya likizo fupi, wewe?” alijibu Veronica
na kuuliza.
“Ninasoma hapo Harvard.”
“Waoo! Inaelekea una akili sana.”
“Hapana! Nipo kawaida sana V.”
“Mmh! Aya!”
Hisia za kimapenzi zilimwendesha puta David, bado hakuamini kama alikuwa na
msichana mrembo jirani yake. Mapigo yake ya moyo kila wakati yalidunda sana
kuna wakati alitamani hata kumwambia Veronica waondoke hapo maktaba na
waelekee sehemu, wazungumze sana.
Muda ulizidi kwenda mbele, ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni, David
hakutaka kuendelea kuvumilia kwani kwa jinsi walivyokuwa wakipiga stori na
kuzidi kuzoeana, aliona hiyo ndiyo nafasi ya kumwambia msichana huyo
waondoke.
“Tuondoke! Kwenda wapi?”
“Sehemu yoyote nzuri! Hata hapo kwenye mbuga ndogo ya wanyama, unaonaje?’
aliuliza David, tabasamu halikumtoka usoni mwake.
“Mmh!”
“Nakuomba, ninahitaji sana kampani yako!”
“Kuna usalama kweli?”
“Ndiyo! Unahisi mimi ni mtekani?”
“Hapana!”
“Basi jua kuna usalama, na nitakulinda pia, amini kwamba upo katika mikono
mikono salama,” alisema David kwa kujiamini.

178
Kwa sababu aliahidiwa ulinzi, Veronica, msichana mpole hakuwa na jinsi,
akakubaliana naye na hivyo kuondoka hapo maktaba na kuelekea huko alipotaka
mwanaume huyo waelekee.
Kwa kuwa yeye hakuwa na gari na msichana huyo alikuwa na gari lake, wakaingia
na kuanza safari ya kuelekea huko walipokuwa wakielekea. Njia nzima David
alikuwa akijichekesha tu, hakutaka kuonekana mkimya, alitaka kuonekana
muongeaji sana ili aweze kumvutia msichana huyo na hatimaye auteke moyo
wake.
Veronica aliendesha gari mpaka pale geji ya mafuta ilipoanza kuonyesha kwamba
gari hilo lilikuwa na mafuta kidogo hivyo walitakiwa kuongeza. Alichokifanya ni
kutafuta kituo cha mafuta kwa ajili ya kulijaza mafuta gari hilo.
Alipokiona, akakifuata kituo hicho, akateremka na kuushika mpira wa kujazia
mafuta ndani ya gari kisha kuanza kujaza mafuta huku David akiwa ndani ya gari
akimwangalia msichana huyo, kila alipomwangalia, alihisi kumpenda tu.
Wakati akiwa amejisahau kumwangalia msichana huyo tena huku kioo kikiwa
wazi kabisa, akashtukia akishikwa shati na mwanaume aliyekuwa nje ya gari, hata
kabla hajaangalia alikuwa nani, akanusishwa kitambaa kilichokuwa na madawa ya
usingizi, hapohapo, hakuchukua hata sekunde kumi, akaanza kuona giza machoni
mwake, hakukuwa na alichokisikia zaidi ya sauti ya mwanaume ikimsifia
msichana Veronica kwa kazi nzuri aliyoifanya, baada ya hapo, akapoteza fahamu.
Veronica ambaye alikuwa akitabasamu tu aliwaangalia watu hao, aliwafahamu na
ndiyo haohao waliomwambia kwamba aifanye kazi hiyo kwani huyo David
alikuwa akihitajika sana.
Akalipwa kiasi chake cha fedha, dola za kimarekani elfu ishirini na kisha wanaume
hao kumchukua David, wakamuingiza ndani ya gari lao na kisha kuondoka naye
mahali hapo.
“Bosi alisema tumuue kupoteza ushahidi,” alisema jamaa mmoja.
“Nakumbuka sana! Tutafanya hivyo tukifika katika jengo la mauaji,” alisema
jamaa mwingine.
“Haina noma.”
****

179
Safari yao ilikuwa ikiendelea kama kawaida, kitu walichokuwa wakikihitaji
kilikuwa ni kufanya mauaji tu. David alikuwa akilia, aliomba msamaha japokuwa
hakujua ni mahali gani alikosea, alitaka kuachwa huru ili aondoke na si kuuawa
kama watu hao walivyotaka.
Hakuacha kulia, alifumbwa macho kwa kitambaa kizito, alihisi kwamba gari hilo
lilikuwa safarini lakini hakujua lilikuwa likielekea mahali gani. Alichokiona mbele
yake kilikuwa kifo tu, alitamani sana aachwe lakini hakukuwa na mtu aliyetaka
kufanya kitu kama hicho.
Safari iliendelea kwa dakika kama ishirini, katika safari nzima walikuwa
wakizungumza kuhusu kumuua David kitu kilichomfanya kuogopa na kuona
kwamba kama asingefanya juhudi zozote zile, watu wale wangeweza kumuua
kama walivyotaka.
“Tukishamuua, inakuwaje sasa?” aliuliza kijana mmoja.
“Baada ya hapo, tumeambiwa tuutumbukize mwili wake ndani ya pipa la
tindikali,” alijibu kijana mmoja.
“Basi hakuna tatizo, kama ni hivyo, ipo poa,” alisema kijana huyo.
Safari hiyo iliendelea mpaka gari hilo lilipofika katika jumba moja na kisha
kuteremka pamoja na David ambaye bado alikuwa amefumbwa macho yake.
Wakamchukua na kumpeleka ndani ya jumba hilo, hawakutaka kumuua haraka
kama walivyoambiwa, iliwapasa kujipanga kwanza kwani mbali na huyo David,
pia kulikuwa na msichana Vivian ambaye alitakiwa kushikiliwa mpaka pale
watakapoambiwa nini cha kufanya juu yake.
“Ingia humo kwanza,” alisema mwanaume mmoja, hapohapo akamsukuma David
ndani ya chumba hicho ambapo humo ndani akatoa kitambaa kile kilichofumba
macho yake, chumba kizima kilikuwa na giza.
****
Kesi haikuonekana kuwa kubwa kwa upande wa Benjamin kwa kuwa kulikuwa na
ushahidi ambao ulimhusisha Bwana Seppy kwamba alikuwa muuaji na ndiye yeye
aliyepanga mauaji kwa watu wote waliokuwa wamekufa ambapo kulionyesha
kwamba watu hao walijiua huku kukiwa na alama za vidole vya Benjamin.

180
Mtu muhimu kwa kipindi hicho alikuwa David tu, ilikuwa ni lazima kumtafuta
popote pale alipokuwa kwani baada ya wiki mbili mtu huyo alikuwa akihitajika
mahakamani.
Alielekezwa na Benjamin mahali alipokuwa akiishi David na kwenda huko lakini
kitu cha ajabu kabisa kukutana nacho, nyumba ilikuwa imefungwa na hakukuwa
na dalili kama kulikuwa na mtu humo ndani.
Hilo lilimshtua sana, alitamani mno kwenda kuwauliza majirani lakini hilo
halikuwezekana kwani katika mtaa huo, hakukuwa na watu waliokuwa
wakionekana nje, wengi walikuwa ndani ya nyumba zao.
Hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka na huko alipokwenda
alijaribu kumpigia simu David lakini kitu kilichomfanya kuwa na wasiwasi, simu
haikuwa ikipatikana.
Moyo wa Donald ukakosa amani, akahisi kwamba inawezekana kuwa kulikuwa na
kitu kibaya kilitokea kwani Bwana Seppy alikuwa na mkono mrefu na alijua
kwamba huyo David ndiye alikuwa mtu hatari hivyo kufanya kila linalowezekana
kummaliza kabisa.
Kwa kile kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni lazima kumpa taarifa Benjamin, hivyo
akarudi na kumwambia kile alichokutana nacho. Kama ambavyo moyo wake
ulivyokuwa na wasiwasi ndivyo ilivyokuwa hata kwa Benjamin.
Haikuwa kawaida kwa David kuzima simu yake, muda mwingi simu yake ilikuwa
hewani, sasa kwa nini siku kama hiyo azime simu yake tena msaa machache baada
ya kusema kwamba alikuwa na ushahidi wa kutosha ambao ungemfanya Bwana
Seppy kutiwa hatihani na hivyo kuhukumiwa kifo au kifungo cha maisha gerezani?
“Nahisi kutakuwa na kitu,” alisema Benjamin huku akionekana kuwa na hofu.
“Unahisi kwamba Bwana Seppy atakuwa amefanya kitu?” aliuliza Donald.
“Nahisi hivyo, ni lazima atakuwa amefanya kitu,” alisema Benjamin huku
akionekana kukata tamaa kwani pasipo David, inamaanisha kwamba yeye ndiye
angehukumiwa kifo au kifungo cha maisha gerezani.
Alichokifanya Benjamin ni kumwambia Donald kwamba ilikuwa ni lazima
kuonana na maofisa wa FBI ili aweze kuwaambia kuhusu umuhimu wa David
katika kesi hiyo.

181
Hilo wala halikuwa tatizo, mara baada ya kupewa taarifa hiyo, maofisa wa FBI
wakaanza kufanya mikakati yao ya kuhakikisha huyo David anapatikana kwani
yeye ndiye alikuwa mtu muhimu kuliko wote katika kesi iliyokuwa ikimkabili
Benjamin.
Kitu cha kwanza kabisa kukifanya ni kwenda nyumbani kwake, kama ilivyomkuta
Donald ndivyo ilivyowakuta hata wao, David hakuwepo na hawakujua alikuwa
mahali gani.
Mara ya kwanza wakahisi kwamba inawezekana alikuwa ndani amelala au
ameuawa hivyo kufanya harakati za kuingia humo, walifanikiwa kupitia mlango
wa nyuma, tena kwa kuvunja kioo na kutoa loki, wakaingilia jikoni, wakaangalia
huku na kule, David hakuwepo.
Hawakutaka kuishia hapo, wakaenda sehemu nyingine za nyumba hiyo ikiwemo
chumbani mpaka bafuni na chooni, kama ilivyokuwa jikoni, napo majibu yalikuwa
yaleyale, David hakuwepo kitu kilichowafanya kuhisi kwamba kulikuwa na watu
kutoka kwa Bwana Seppy ambao walifika na kumteka kijana huyo, hivyo
wakaanza kumtafuta kila kona, tena hasahasa walitumia kamera ndogo za mitaani,
CCTV kwa kuamini kwamba wangepata kitu chochote kile ambacho
kingewasaidia.
****
Mitaani hali ya hewa ilibadilika, watu wote ambao waliitaka mahakama
kumhukumu Benjamin kifo au kifungo cha maisha gerezani, wakabadilika na
kumtaka mwanaume huyo huyo aachiwe huru na bilionea mkubwa duniani, Bwana
Seppy apatikane haraka iwezekanavyo na kupandishwa kizimbani.
Watu walilia mitaani, hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea, maneno
aliyosema Benjamin mahakamani kwamba yeye hakuhusika na mauaji bali Bwana
Seppy ndiye alihusika yaliwafanya kupunguza chuki zao juu yake.
Vichwa vyao vilichanganyikiwa, hawakujua ukweli ulikuwa wapi, hawakujua
kama kweli Benjamin alikuwa amehusika au la, kitu walichokuwa wakikisubiria
kilikuwa ni huyu shahidi ambaye alikuwa na ukweli wote ambao ungemuweka
huru Benjamin.
Baada ya saa kadhaa tangu Benjamin amtaje Bwana Seppy kama mhusika mkuu
katika mauaji hayo, taarifa zilizoanza kusikika katika mitandao ya kijamii ni
kwamba David, huyo shahidi aliyetarajiwa kumwaga kila kitu hadharani, hakuwa

182
akionekana nyumbani kwake, alipotea katika mazingira ya kutatanisha kitu
kilichowafanya watu kuona uwezekano kwamba mzee huyo bilionea alikuwa
amehusika katika mauaji hayo.
“Huyu mzee atakuwa amehusika...” alisema jamaa mmoja.
“Kweli Bwana, haiwezekani baada ya kutajwa yeye, eti shahidi haonekani, hivi
inawezekana hiyo?” alihoji jamaa mmoja.
Hilo ndilo lililosikika mitaani, kila mtu alikuwa na uhakika kwamba Bwana Seppy
ndiye aliyehusika katika mauaji ya watu wote waliouawa kinyama ndani ya hoteli.
Mambo yaliendelea kubadilika na mwisho wa siku kila mtu akataka kitu kimoja tu,
mzee huyo afikishwe mahakamani na kuhukumiwa kwa kile kilichokuwa
kimetokea.
Wenye mabango hawakutaka kusubiri, wakaondoka na kuelekea barabani, polisi
walijitahidi kuwazuia lakini ilishindikana kabisa kwani kadiri muda ulivyokuwa
ukienda mbele ndivyo walivyozidi kuongezeka mitaani na kuendelea kuitaka
mahakama imhukumu kifo Bwana Seppy kwani kile alichokuwa amekifanya,
hakika kiliiumiza mioyo yao.
****
Vivian alikuwa chumbani mule, hakuweza kuona kitu chochote kile, aliletewa
chakula kilichokuwa katika sahani lakini hakuwa na hamu ya kula, muda wote
alikuwa mtu wa kulia tu, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno,
hakuamini kama mwisho wa siku yeye ndiye angekuwa ndani ya chumba hicho
ambapo mpaka hapo hakujua nini ingekuwa hatma yake.
Aliendelea kulia huku akimfikiria mpenzi wake, hakujua alikuwa mahali gani na
nini kiliendelea katika maisha yake. Alisikia huzuni kubwa moyoni mwake na
wakati mwingine alipiga magoti na kumuomba Mungu japo amkomboe kutoka
katika mikono ya watu hao ambao walionekana kuwa na lengo moja, kumuua.
Siku ya kwanza ikapita pasipo kujua kwani ndani ya chumba kile kulikuwa na giza
totoro ambalo lisingemfanya mtu yeyote kugundua kama ilikuwa wakati gani, siku
iliyofuata, huku akiwa amechoka akapanga kuondoka ndani ya chumba hicho,
hakujua angeondoka vipi lakini ilikuwa ni lazima kuondoka.
Hapo ndipo alipoanza kupapasa huku na kule, alikuwa akitafuta upenyo wa
kuondoka chumbani hapo. Kama zilivyokuwa nyumba nyingine nchini Marekani,

183
hata nyumba ile, vyumba vyake vilikuwa vimetenganishwa kwa maboksi magumu
hivyo akaona kwamba hiyo isingekuwa kazi kubwa kuondoka.
Alichokifanya ni kuchukua viatu vyake vilivyokuwa na visigino virefu na kuanza
kugonga kwenye boksi lililotenganisha chumba hicho na chumba kingine.
Hakuwa na jinsi, ilikuwa kazi kubwa lakini ilimbidi kufanya hivyo kwani kama
asingefanya hivyo, angeuawa mara tu watu wale waliomuweka ndani ya chumba
hicho wangerudi kwa mara ya pili.
Kugonga kwake hakukuacha, aliendelea kugonga zaidi na zaidi. Boksi lile lilikuwa
kubwa lakini kutokana na kugonga kwa nguvu tena eneo moja pasipo kuacha,
alama ikaanza kutoka katika boksi hilo.
Hiyo ikampa nguvu ya kugonga zaidi, hakuacha, aliendelea kufanya hivyo zaidi na
zaidi na mwisho wa siku akaona Mungu akiwa upande wake kwani boksi lile
kubwa likaanza kuachia eneo kubwa, alipoendelea zaidi, chumba kikaacha
kupenyezewa mwanga kupitia katika tundu lile lililopatikana.
“Asante Mungu,” alijikuta akisema.
Kabla ya kuendelea akaanza kuchungulia, alitaka kujua kama upande wa pili
kulikuwa na watu wengine, alichungulia, sehemu ambayo alikuwa ametoboa
ilikuwa katika chumba kingine, hakutaka kujiuliza kama kulikuwa na watu
wengine ndani ya nyumba hiyo, jibu alilokuwa nalo ni kwamba ndani hakukuwa
na mtu kwani kama kungekuwa na mtu, ni lazima angefika katika chumba kile
kutokana na kuligonga boksi kwa kipindi kirefu.
Aliendelea zaidi mpaka alipopata tundu kubwa na hatimaye kutoka ndani ya
chumba kile. Moja kwa moja akaelekea katika chumba kile ambacho
kilitenganishwa kwa ukuta wa boksi, akaufuata mlango na kuufungua.
Kitu cha kwanza kabisa alichotaka kujua ni muda. Akatoka ndani ya chumba hicho
na kuelekea sebuleni, nyumba nzima ilikuwa kimya na hakukuwa na dalili za
kuwepo kwa mtu yeyote ndani ya chumba hicho.
Alipofika huko, saa kubwa ya ukutani ilionyesha kwamba ni saa kumi na moja
jioni, hakujali sana, akaufuata mlango na kutaka kuufungua kwa ajili ya kutoka
ndani ya chumba hicho.
“Mbona haufunguki...” alijisemea huku akiendelea kuufungua mlango huo.

184
Mlango ulifungwa kwa ufunguo kwa nje, alijitahidi kuufungua lakini
haukufunguka kabisa. Moyo wake ulikuwa ukidunda kwa nguvu, alichokuwa
akikitaka ni kutoka katika nyumba hiyo tu kwani haikuwa sehemu salama hata
mara moja.
Alipoona mlango haufunguki, akatoka mlangoni na kuelekea katika vioo vya
dirisha, vyote vilifungwa, alijaribu kuvunja vioo hivyo lakini ilishindikana, vioo
vilikuwa vile vigumu ambavyo isingewezekana hata mara moja kuvunjika.
“Nifanye nini?” alijiuliza.
Hakutaka kuishia hapo, ilikuwa ni lazima ahakikishe anatoka ndani ya jumba hilo
kubwa, akaondoka na kuelekea katika vyumba vingine, kama ilivyokuwa kule
sebuleni ndivyo ilivyokuwa huko, alishangaa ni kwa jinsi gani nyumba hiyo
ilikuwa na ulinzi mkubwa kiasi hicho.
Alipita katika vyumba vyote isipokuwa chumba kimoja ambacho kilikuwa kigumu
kufunguka. Hicho ndicho chumba alichohisi kwamba kulikuwa na njia nyepesi ya
kutokea hivyo ilikuwa ni lazima kuingia ndani ya chumba hicho.
Alijaribu na kujaribu kuufungua mlango huo lakini haukufunguka, aliendelea
kujaribu zaidi na zaidi na baada ya dakika thelathini, mlango ukafunguka na
hapohapo kuingia ndani.
Alichokikuta hakuamini. Chumba kilikuwa na kiti kimoja kilichokuwa na kamba
nyingi, pembeni kulikuwa na mkia wa taa uliokuwa ukitumika kuwachapa watu
waliokuwa wakiingizwa ndani ya chumba hicho.
Mbali na vito hivyo, pia kulikuwa na waya mmoja mkubwa uliogawanyika pande
mbili, waya wa kuchajia betri za gari ambao ulitumika kama kuwatisha watu kwa
kuwapiga shoti ya umeme.
Mbali na hivyo, pia kulikuwa na kiti kidogo chini ambacho kilionekana kama
kistuli kilichokuwa na tundu kwa chini sehemu ya kukalia. Hicho kilikuwa
maalumu kwa kumkalisha mateka akiwa mtupu kisha kuanza kuzipiga korodani
zake.
Hicho kilikuwa chumba cha kutisha ambacho pia hata kuta zake zilionekana kuwa
na michirizi ya damu zilizokuwa mpaka chini kabisa. Picha hiyo ilimtisha mno,
hakutaka kubaki humo kwani hata harufu ya damu ilimghasi puani mwake,
harakaharaka akatoka chumbani humo na kuelekea sebuleni.

185
Macho yake yakatua katika simu ya mezani, hatakaharaka akaifuata ili aweze
kuitumia kuwapigia polisi, alipouchukua mkonga wa simu na kupiga, hakuukuwa
na sauti yoyote iliyosikika na alipoangalia, akakuta waya ukiwa umekatwa.
Alichanganyikiwa, kila kitu alichotaka kukifanya ndani ya chumba hicho
kilionekana kumbana sana. Muda ulikuwa umekwenda sana, saa tano zilikatika
huku akiwa hapo sebuleni na saa ya ukutani ilionyesha kwamba ni saa nne usiku.
Wakati akiwa anajifikiria zaidi nini cha kufanya, ghafla akasikia muungurumo wa
gari kutoka nje ya nyumba hiyo, harakaharaka akazima taa na kuchungulia
dirishani.
Geti likafunguliwa na wanaume watatu wakatoka kutoka garini huku wakiwa na
mwanaume mwingine ambaye walimfunga kitambaa machoni. Vivian hakujua mtu
aliyekuwa ametekwa alikuwa nani, alichokifanya ni kwenda jikoni na kujificha
huko.
****
Wanaume wale baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo, wakampeleka David
katika chumba kingine kabisa kilichokuwa na giza nene kama kile chumba
alichowekwa Vivian. Wakamwambia akae huko kwani kulikuwa na kazi kubwa ya
kutaka kufanya.
Walichokifanya ni kutoka na kuelekea sebuleni, walisahau kabisa kuhusu
msichana Vivian, walichokikumbuka ni kwamba walikuwa na jukumu dogo la
kumuua David kama waliyoambiwa na bosi wao.
“Let’s eat,” (tuleni kwanza) alisema mwanaume mmoja.
Chakula kilikuwa kingi katika friji kiasi kwamba hawakuona dalili zozote kama
kulikuwa na chakula kingine kilichokuwa kimechukuliwa na Vivian. Wakachukua
na kukiweka mezani ambapo wakaanza kula huku wakiyafurahia maisha kwamba
baada ya dakika kadhaa wangekwenda kuwa na fedha nyingi kutokana na malipo
ambayo Bwana Seppy angeyafanya.
“I will have my own Ferrari motherfu...” (nitakuwa na Ferrari yangu...)
“Hahaha! What the hell! I will ride back home, Atlanta and smoke some weed
baby, what the hell are gonna do with the damn money?” (Hahah! Nitaendesha gari
langu kurudi nyumbani, Atlanta na kupiga madawa, utazifanyia nini fedha zako?)
aliuliza jamaa mwingine baada ya kujitamba.

186
“I ain’t do a lot of damn things, just spendin’ my time with some fucking bitches,
smoke some weed,” (sitofanya mishe nyingi, nitatanua muda wote na malaya,
kuvuta bangi kwa wingi) alisema jamaa huyo mwingine.
Walikuwa wakizungumza kwa mbwembwe, mbele yao walijiona wakiwa na fedha
nyingi kutokana kwa kile walichotakiwa kukifanya, walifurahia kwa kuwa
hawakuona kama kungekuwa na mtu yeyote yule ambaye angewazuia.
Wakati wakiendelea kula na kunywa huku tena wakivuta bangi, Vivian alikuwa
chumbani kule alipojificha, alikuwa akimuomba Mungu amlinde kwani sehemu
hiyo haikuwa salama hata mara moja.
Aliyasikiliza mazungumzo yao lakini bado hakujua yule mtu aliyeletwa ndani ya
chumba kile alikuwa nani. Alichokifanya, tena kwa mwendo wa kunyata akaanza
kuondoka kuelekea katika chumba kile, kilikuwa na giza totoro kama kilivyokuwa
kile chumba alichoingizwa yeye.
Alipofika humo, akaanza kumuita David kwa kutumia jina la mwanaume huku
akimwambia kabisa kwamba yeye hakuwa mtu mbaya, alikuwa mtu mzuri ambaye
alifika hapo kwa ajili ya kumkomboa.
“Who the hell are you?” (Wewe nani?) aliuliza David.
“Vivian...”
“Vivian...Benjamin’s girlfriend?” (Vivian...mpenzi wa Benjamin?) aliuliza David.
“Yes!”
“What the hell are you doing here?” (Unafanya nini hapa?)
“I was kindnaped like you!” (nilitekwa kama wewe) alijibu Vivian.
Wakati akizungumza hayo, tayari alikuwa amekwishamfikia Benjamin na hivyo
kumfungua kamba alizokuwa amefungwa na kuanza kupanga mipango ya kutoka
ndani ya nyumba hiyo.
Alichokisema David kilikuwa ni kuondoka kupitia vyumba vingine kwani watu
hao walikuwa sebuleni hivyo kama wangefanikiwa kufika katika vyumba vingine
ingekuwa rahisi kwao kutoroka.
“Haiwezekani!” alisema Vivian.
“Kwa nini?”

187
“Kila chumba kina dirisha la kioo kisichovunjika, nilijaribu kutoroka lakini
nimeshindwa,” alisema Vivian.
Ndiyo, kutoroka lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo kwani Vivian
alishajaribu kufanya hivyo lakini akashindwa. David hakutaka kukubali, kwake
aliona kama msichana huyo alimdanganya hivyo kuanza kwenda katika vyumba
hivyo kwa mwendo wa kunyata kwa kuamini kwamba wangeweza kufanikiwa.
Matokeo yalikuwa yaleyale kwamba hawakuweza kutoka ndani hivyo kugundua
kwamba sehemu ya kutorokea ilikuwa moja tu, nayo ilikuwa ni pale sebuleni.
“Lazima tufanye kitu!” alisema David.
“Kitu gani?”
“Kupambana! Hakuna kingine zaidi ya hicho,” alisema David.
“Tutapambana vipi?”
“Subiri kwanza...”
Akili ya David ilicheza harakaharaka, hakuona kama Vivian alikuwa na wazo
lolote lile. Alikumbuka kwamba chumba alichokuwa amehifadhiwa kilikuwa na
giza totoro hivyo ingekuwa rahisi kwake kufanya jambo na hatimaye kujinasua
kutoka katika mikono ya watu hao. Akaanza kuvua nguo zake.
“Unafanya nini?” aliuliza Vivian huku akionekana kushangaa.
“Vua nguo zako pia!”
“Ili?”
“Nipe nivae na wewe uvae hizi,” alisema David.
“Ili?”
“Fanya hivyo Vivian, hatuna muda wa kupoteza,” alisema David.
Kwa sababu yeye ndiye alikuwa amepata wazo juu ya nini cha kufanya, Vivian
hakuwa na sababu ya kukataa, akavua nguo zake harakaharaka kisha kubadilishana
na David na kuelekea ndani ya chumba kile huku David akichukua nondo kubwa
iliyokaa kama fimbo na kuanza kurudi kule ndani.
“Wewe utalala chini, kule pembeni, hakikisha ukilala, unafichan kichwa chako
ukutani, halafu mimi nitasimama nyuma ya huu mlango, umesikia?” alisema David
na kuuliza swali.

188
“Ndiyo!”
“Basi fanya hivyo,” alisema David.
Vivian akaelekea pembeni kabisa, akalala kiubavuubavu, kichwa kilikuwa ukutani
huku David akisimama nje ya mlango. Kila kitu kilipokuwa tayari, David akaanza
kuupiga kelele akiwahitaji wanaume wale waje ndani ya chumba kile.
“Bora nife, mbona mnaogopa kuniua? Mnaniweka humu ndani ili iweje? Kama
wanaume kweli, mliozoea kuua, kwa nini msiniue,” alisema David kwa kupiga
kelele, aliendelea kusema maneno hayo zaidi na zaidi kwa kuamini kwamba ni
lazima vijana wale wangemfuata ndani ya chumba kile.
Wanaume watatu wenye uchu wa fedha walikuwa wamekaa sebuleni, chupa
kubwa za pombe zilikuwa mezani na walikuwa wakinywa mfululizo, maisha yao
yalionekana kubadilika kwani kitu walichokuwa wakikitaka, walikipata na kazi
moja tu ndiyo iliyokuwa ikisubiriwa, kumuua mtu ambaye waliambiwa wamuue.
Mbele yao hakukuwa na kazi kubwa, kazi kubwa ambayo walikuwa nayo ni
kumtafuta mtu huyo, baada ya kumpata, hakukuwa na kazi nyingine yoyote ile
kwani kitendo cha kumuua, wala hakikuwa kazi kubwa, ilikuwa nyepesi sana,
kama kumsukuma mlevi katika mteremko wa mlima Kitonga.
Walipokuwa wakiendelea kunywa pombe kali, ndipo waliposikia kelele kutoka
katika chumba walichomuhifadhi David, walikumbuka kwamba walimsiba mdomo
kwa kutumia gundi hivyo wakajua kwamba kijana huyo alileta ubishi na hatimaye
kutoa gundi hiyo mdomoni.
Hilo liliwakasirisha sana, wawili wakamwambia mwenzao achukue bastola na
kuelekea huko chumbani ili amtulize David, baada ya kunywa pombe ndipo
wamuue kwa kumtumbukiza ndani ya pipa la tindikali.
“Kamtulize, akileta ubishi, mzimishe kwa muda,” alisema Cobra.
“Ila mnanionea sana, tunakunywa na kufurahia maisha, mnaanza kunituma,”
alisema jamaa huyo aliyejulikana kwa jina la Amazon.
“Wewe nenda, kwanza wewe si ndiye mdogo, hatumalizi pombe zote,” alisema
Cobra huku akimwangalia Amazon kwa jicho lililomtaka kufanya kile
alichomwambia.
Huku akionekana kukasirika, Amazon akainuka, akachukua bunduki na tochi kisha
kwenda katika chumba kile alichoambiwa aende. David hakunyamaza, aliendelea

189
kuzungumza maneno yaleyale ya kuwatia hasira kwa kudai kwamba waliogopa
kumuua.
Alipoufikia mlango ule, akawasha tochi na kuingia ndani, alipomulika, mtu
aliyemuona akiwa amelala, hakumuona vizuri, alimuona kwa nyuma tu, kutokana
na mavazi aliyokuwa nayo, aliamini kwamba alikuwa David, akaanza kumfuata
pale chini.
Alipomfikia na kumwangalia vizuri, nywele nyingi alizokuwa nazo zilimshtua,
alipotaka kugeuka tu, akashtukia akipigwa nondo ya kichwa, hapohapo akaanguka
chini na kupoteza fahamu.
“Inuka...inuka Vivian,” alisema David huku akimuinua Vivian.
Vivian akainuka, David akachukua bastola ile na kumwambia Vivian amfuate,
wakaanza kuelekea sebuleni. Walipofika huko, wakamkuta Cobra na mwenzake
wakinywa pombe kali, hapohapo wakawaweka chini ya ulinzi.
“Ukitingishika tu, nakumwaga ubongo,” alisema David huku akionekana kuwa na
hasira.
Wote wakatulia, kwa jinsi David alivyoonekana, alionekana kuwa na hasira nyingi
ambaye hakutaka kabisa kufanyiwa mchezo. Walibaki wakiwa wametulia na
kufanya kile ambacho David alitaka wakifanye.
Alichowaambia ni kwamba wachukue simu na kumpigia mtu ambaye aliwatuma
na kumwambia kwamba kazi ilikuwa imekamilika, yaani yeye na Vivian walikuwa
wamekufa.
Hakukuwa na aliyeleta ubishi kwani walijua kwamba kijana huyo hakuwa na
masihara hata kidogo hivyo wakachukua simu na kumpigia Dracula. Simu iliita
kwa muda mchache tu, ikapokelewa.
“Mmekamilisha?” ilisikika sauti ya Dracula kutoka upande wa pili.
“Kila kitu tayari! Tumewaua wote,” alisema Cobra.
“Safi sana! Ngoja niwasiliane na mzee, kiasi kilichobaki kitatumwa katika akaunti
zenu,” alisema Dracula kisha Cobra kukata simu.
Hiyo wala haikutosha, alichoagiza David ni kwamba Vivian awafunge kamba na
kisha waondoke, hilo wala halikuwa tatizo, Vivvian akarudi chumbani kule
ambapo alimkuta Amazon akiwa hoi chini huku damu zikimtoka kichwani,

190
akachukua kamba na kurudi sebuleni ambapo akawafunga vijana hao na wao
kuondoka huku wakiufunga mlango kwa nje.
****
Dracula alikuwa akizungumza na Bwana Seppy katika kituo cha polisi, muda wote
uso wa mzee huyo ulionyesha tabasamu pana kwani hakuamini kile alichokisikia
kwamba mtu aliyekuwa akimsumbua kwa wakati huo alikuwa marehemu.
Hiyo ilimaanisha kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye angemtisha katika
kesi hiyo kwani kama shahidi aliyekuwa akimtegemea Benjamin alikuwa mmoja
tu, David ambaye mpaka katika kipindi hicho alipewa taarifa kwamba alikuwa
marehemu.
“Una uhakika wamefanikiwa?” aliuliza Bwana Seppy.
“Ndiyo! Wamenipa taarifa, huwa wanafanya hivi kila siku,” alisema Dracula.
“Asante Mungu!”
Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu tu, kwake ulionekana kuwa
kama muujiza mkubwa kwani kwa kipindi hicho alihitaji sana David auawe kuliko
kitu chochote kile.
Alibaki akiiangalia saa yake, aliona muda ukikawia kwenda kwani alitamani
kusimama kizimbani na kuiambia mahakama kwamba hakuwa amefanya mauaji na
kama wanabisha walete shahidi kitu ambacho ingekuwa ngumu kwa Benjamin na
watu wake kufanya hivyo.
Upande wa pili ulikuwa ni kilio tu, taarifa zilianza kusambaa kwamba David
alikuwa ameuawa, hakukuwa na siri tena, kwa Benjamin, tayari alikata tamaa,
muda wote alionekana kuwa na huzuni tele kwani kwa namna moja au nyingine
lazima mahakama ingemhukumu kifo au hata kufungwa kifungo cha maisha
gerezani.
Alizungumza na mwanasheria wake, Donald na kumwambia wazi kwamba
alikuwa na hofu moyoni mwake, kama ilivyokuwa kwa Benjamin, hata kwa
Donald ilikuwa hivyohivyo kwani aliamini kwamba David aliuawa lakini napo
ilikuwa ngumu kusema kwamba Bwana Seppy ndiye alikuwa amehusika kwani
wangeulizwa kama wana ushahidi kitu ambacho kingewapa wakati mgumu.
“Kwa hiyo tufanye nini?” aliulizaDonald.

191
“Duh! Yaani siwezi kuamini kama David ameuawa, na FBI wanasemaje?” aliuliza
Benjamin huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Wamejaribu kumtafuta...”
“Ikawaje?”
“Nao wakamkosa.”
“Hata mwili wake?”
“Nao wameukosa pia,” alijibu Donald.
Benjamin akaona huo ndiyo mwisho wake, alipoambiwa hivyo na Donald,
hakutaka kuendelea kuzungumza naye, akaomba kuondoka kwani kichwa chake
kilichanganyikiwa mno.
Siku hiyo haikuwa nzuri katika maisha yake, alipagawa kwa sababu mtu pekee
ambaye alibaki, aliyekuwa tegemeo lake alikuwa David tu ambaye mpaka muda
huo tetesi zilisema kwamba aliuawa kwani hakuwepo nyumbani na wala
hakuonekana sehemu yoyote ile.
“Mungu nisaidie!” alisema Benjamin huku akiwa amepiga magoti, alionekana
kukata tamaa kwa asilimia mia moja.
****
Siku hazikumsubiri mtu, ziliendelea kukatika, Moyo wa Benjamin ulikuwa kwenye
maumivu makali mno hasa baada ya kugundua kwamba mshikaji wake aliyekuwa
na ushahirdi wote, David alikuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Hakukaa kimya, aliwaambia wazazi wake juu ya hofu aliyokuwa nayo moyoni
mwake, aliwaambia wazi kwamba kila siku alikuwa mtu wa mawazo na hakujua
kama ingetokea siku yoyote ile angeweza kupata furaha aliyokuwa nayo kabla
kama tu huyo David asingepatikana.
“I don’t know what I should do but the world must know that I killed nobody,”
(Sijui ninachotakiwa kufanya lakini lazima dunia ijue sijamuua mtu yeyote yule)
alisema Benjamin huku akiwa ameuinamisha uso wake.
“Everybody knows you killed nobody, but we have to look for the evidence to set
you free,” (Kila mtu anajua hujamuua mtu yeyote yule lakini ni lazima tuutafute
ushahidi) alisema baba yake.

192
“Nobody knows where David is by now, they killed him, why? When I come back,
I’ve to tell the world about what happened although David disappeared” (Hakuna
anayejua mahali David alipo kwa sasa, watakuwa wamemuua, kwa nini?
Nitakaporudi, nitatakiwa kuiambia dunia kila kitu kilichotokea hata kama David
amepotea) alisema Benjamin huku machozi yakianza kumtoka.
Hakukuwa na kilichobadilika, bado Benjamin alitakiwa kukaa jela mpaka pale
ambapo angeitwa tena mahakamani. Ushahidi mwingine ukakusanywa na hivyo
kilichokuwa kikitakiwa ni siku ya mahakama ifike na kila kitu kuwekwa wazi.
Siku ilipofika, tayari watu wengi walikwishakusanyika ndani ya mahakama hiyo.
Hali ilikuwa tofauti na kipindi cha nyuma. Watu walibadilika, hawakutaka tena
kuona Benjamin akifungwa bali Bwana Seppy ndiye alitakiwa kufungwa kutokana
na kile alichokifanya.
Waandishi wa habari walikuwa ndani ya mahakama hiyo, walitaka kuandika kila
kitu kilichokuwa kikiendelea. Mwana huo wa 2011, hakukuwa na kesi iliyovuta
hisia za watu wengi kama hiyo.
Kila mtu duniani alitegesha masikio yake kusikiliza kile kilichokuwa kikiendelea
katika mahakama hiyo huko nchini Marekani. Jaji yuleyule, McRegan ndiye
aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo na kutoa hukumu.
Mahakama ilijaza watu, hakukuwa na nafasi ya watu wengine na hata wale
waliokuwa wamechelewa ambao walikuwa ni zaidi ya watu elfu kumi walitakiwa
kubaki nje na kufuatilia kesi ile kupitia televisheni kubwa iliyowekwa tayari nje ya
mahakama hiyo.
Haukupita muda mrefu, basi kubwa lililobeba watuhumiwa likaanza kuingia ndani
ya eneo la mahakama hiyo. Waandishi wa habari ambao walikuwa nje
wakalisogelea gari hilo na kuanza kulipiga picha.
Basi liliposimama, mahabusu kadhaa wakaanza kuteremka huku wakiwa na pingu
mikononi mwao. Miongoni mwa mahabusu hao alikuwa Benjamin na Bwana
Seppy ambaye muda wote uso wake ulikuwa na tabasamu pana.
Alichokuwa akifahamu, David alikuwa ameuawa kama alivyoambiwa na Dracula,
alijua kwamba Benjamin hakuwa na ushahidi wowote ule ambao ungemuweka
matatani.
Aliwapungia watu mikono, watu wengi walikuwa wakimzomea lakini
hakuonekana kujali mpaka alipoingia ndani ya mahakama. Watu walitaka

193
kuisikiliza kesi hiyo na hukumu kutolewa siku hiyohiyo, hakukuwa na mtu
aliyefika mahali hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine yoyote ile.
Wakati Jaji McRegan anaingia ndani ya mahakama hiyo, watu wote wakasimama
kama ishara ya heshima, jaji akatembea mpaka mbele ambapo akakaa katika kiti
chake kisha kuwaruhusu watu kukaa kwa kupiga nyundo yake.
Muda wote Benjamin alikuwa amekiinamisha kichwa chake chini, alionekana
kuwa na majonzi mazito na muda wote machozi yalikuwa yakimtoka tu. Wakili
wake, Donald ndiye aliyekuwa akimsimamia siku hiyo, mbali na huyo, pia
kulikuwa na wakili wa upande wa Bwana Seppy, wakili huyu aliitwa Tedd,
mwanaume mrefu ambaye muda wote alivalia miwani.
Zilianza kusikiliza kesi nyingine ambazo zilichukua masaa mawili na ndipo
Benjamin akatakiwa kupanda kizimbani. Watu walikuwa wakimwangalia tu,
alionekana kuwa na maumivu makali moyoni mwake kiasi kwamba hata watu
wengine wote wakaanza kumuonea huruma.
“Unaitwa nani?” aliuliza Donald.
“Naitwa Benjamin Saunders.”
“Unajua kwa nini upo hapa?”
“Ndiyo! Ni kwa sababu mahakama inanihusisha na mauaji yaliyotokea,” alijibu
Benjamin.
“Mnamo tarehe ishirini mwezi wa sita mwaka jana, kulikuwa na mauaji
yaliyotokea, mwanamuziki, Carter Phillip alikutwa amekufa katika chumba kimoja
huko Southampton nchini Uingereza, polisi walifanya kazi yao na kugundua
kwamba alama zako za vidole zilikutwa katika mwili wa marehemu, na si kwenye
mwili tu bali hata katika sehemu nyingine chumbani humo, unalizungumziaje
hilo?” alisema Donald na kuuliza swali.
“Kitu cha kwanza ambacho mahakama hii inatakiwa kufahamu ni kwamba
sikuwahi kuua katika maisha yangu. Nilimfahamu Carter kama mwanamuziki
chipukizi. Mnamo tarehe tano mwezi wa saba nilipokea simu ya kuhitajika sehemu
fulani, huko nilipokwenda, nilikutana na Bwana Seppy ambaye alinipa kazi ya
kufanya mauaji ya Carter Phillip. Sikujua sababu ila nilimkatalia kwa kuwa
sikuwahi kuua,” alisema Benjamin.
“Unahisi kwa nini alikuchukua wewe?”

194
“Mimi ni mtaalamu wa kompyuta, aliamini kwamba kama ningeifanya kazi yake
ingekuwa nyepesi na hata kugundulika ingekuwa ngumu. Kwa kweli nilikataa
kabisa,” alisema.
Huo ulikuwa ni muda wa maswali kutoka kwa wakili wake, maswali yake
yalikuwa ya kumpa nafasi ya kuelekezea kile kilichokuwa kimetokea, wakili
Donald alichukua dakika kumi, alipomaliza maswali yake, akakaa chini na wakili
wa Bwana Seppy kusimama.
Maswali yake yalikuwa magumu lakini Benjamin alijitahidi kujibu kwa uelewa
mkubwa, baada ya kuulizwa maswali hayo na kumaliza, hapo ndipo akakaa, watu
wote wakata kuona Bwana Seppy naye akiulizwa maswali.
Hilo halikuwa tatizo, akasimama na kuelekea kizimbani. Mtu wa kwanza kabisa
kumuuliza maswali alikuwa wakili wake, maswali aliyoulizwa yalikuwa mepesi na
yale ya kumuweka katika wakati mzuri wa kushinda kesi, wakili huyo alipomaliza,
akasimama na Donald kusimama.
“Unaitwa nani?” aliuliza Donald huku akimwangalia Bwana Seppy usoni mwake.
“Naitwa David Seppy...”
“Sawa. Una akili?” aliuliza Donald.
“Unasemaje?”
“Una akili?” alirudia swali lake.
“Ndiyo nina akili!”
“Unajua kwa nini upo hapa?”
“Ndiyo mheshimiwa! Nipo hapa kwa sababu nimesingiziwa kwamba nimeua,”
alisema Bwana Seppy.
“Umesingiziwa au umeua kweli?”
“Nimesingiziwa kwa kuwa kama ningekuwa nimeua, basi hata alama za vidole
vyangu zingeonekana,” alijitetea.
“Mshtakiwa ambaye ni Benjamin anasema kwamba wewe ndiye uliyehusika katika
mauaji hayo na wewe ndiye uliyemuita na kumpa kazi hiyo ili akaue, ni kweli?”
aliuliza Donald.
“Si kweli!”

195
“Unamjua Benjamin? Ushawahi kuonana naye kabla?” aliuliza Donald.
“Hapana! Sikuwahi kuonana naye kabla.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mheshimiwa.”
“Tarehe kumi na mbili mwezi wa sita, simu yako ilitumika kutuma ujumbe mfupi
kwenda namba +56 890 672 88 ambayo inamilikiwa na mtu anayejulikana kwa
jina la Petterson Edward ambaye ulikuwa ukimuita kwa jina la Dracula, ujumbe
huo uliuandika kwamba kulikuwa na mtu ambaye alitakiwa kuuawa mara moja,
huyo si mwingine bali ni Carter, ni kweli?” aliuliza Donald.
“Si kweli!” alijibu Bwana Seppy baada ya kukaa kimya kwa muda.
“Mheshimiwa hakimu, naomba niwekewe televisheni na kompyuta kwa ajili ya
kuletea ushahidi ulioshiba kabla ya shahidi wa mwisho kabisa ambaye ni David
kuja na kuthibitisha yote yaliyotokea,” alisema Donald.
Bwana Seppy alipolisikia jina la David, akayapeleka macho yake kwa Dracula
ambaye alikuwa ndani mahakama ile, alichanganyikiwa kwani taarifa ya mwisho
ilisema kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa, je, ni David yupi ambaye alikuwa
akizungumziwa mahali hapo.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, harakaharaka televisheni ikaletwa mahali hapo,
laptop ikaunganishwa na simu simu aina ya iPhone aliyokuwa nayo Donald na
kisha kuanza kuonyesha ushahidi wa kila kitu kilichokuwa kimetokea.
“Kama nilivyosema, ushahidi umeonyesha kufanya mawasiliano hayo kama
inavyoonekana, ujumbe huo ulitumwa kutoka namba hii, naomba kuuliza, je, hii
namba ni yako au si yako?” aliuliza Donald huku akimuonyeshea namba Bwana
Seppy katika televisheni.
“Ni yangu!”
“Kuna mtu aliwahi kuishika simu yako na kutuma ujumbe pasipo kujua?” aliuliza.
“Hapana!”
“Sawa. Mnamo tarehe kumi na tisa mwezi wa tisa, ujumbe wa mauaji ulitumwa
kutoka katika simu yako kwenda katika namba ileile na ulisema kwamba ni lazima
Todd Lewis auawe kwa sababu alikataa kuweka mkataba na wewe ambao
ungemlipa kiasi kidogo cha fedha, hivyo kama kisasi ukaamua kumuua kwa

196
kutuma watu, je, ni kweli?” aliuliza Donald, Bwana Seppy akabaki kimya, alianza
kuweweseka huku akiangalia huku na kule.
“Uliidanganya dunia kwamba Benjamin ndiye aliyekuwa akifanya mauaji. Hiyo
haikutosha, pia ulitumia njia hizohizo kuwaua watu wengine na kumfanya
Benjamin kuingia matatani. Na kwa faida ya mahakama ni kwamba ulikuwa
ukiweka noti kila sehemu uliyoua ili iwe vigumu kugundulika ila noti hizo
zilikuwa na maana kubwa.
“Ile noti ya Dola, alama yake ambayo inawakilisha S, ile Euro ambayo
inawakilisha fedha ya Ulaya, ile Paundi iliyowakilishwa na P, na mwisho ile Yuen
iliyowakilishwa na Y, inaunganisha jina lako la SEPPY, je, bado unataka kubisha
hapo?” aliuliza Donald huku akimwangalia mzee huyo usoni. Bwana Seppy
akabaki kimya.
“Wiki kadhaa zilizopita, kulikuwa na mauaji ya msichana Stacie, mauaji hayo
yalifanyika jijini Los Angeles mnamo majira ya saa nne usiku huku alama za
vidole zikionyesha kwamba ni Benjamin ndiye aliyehusika, saa tano usiku kupitia
kamera za CCTV zilizokuwa Boston zilimuona Benjamin na hivyo polisi kwenda
kumkamata.
“Swali langu ni hili! Kama ni Benjamin ndiye aliyekuwa amefanya mauaji ya
Stacie, je, alitumia usafiri gani kutoka Los Angeles mpaka Boston na wakati
kutoka sehemu hizo kwenda nyingine hutumia muda wa saa tatu kwa usafiri wa
treni na saa mbili na nusu kwa usafiri wa ndege? Wewe ndiye uliyefanya mauaji
hayo, na bahati mbaya sana ulishindwa kujipanga kwa kutumia saa yako,” alisema
Donald huku akiifunga faili lake.
Bwana Seppy alibaki kimya, alikuwa akitetemeka mno, hakuamini kile
kilichokuwa kikiendelea mahakamani hapo, alimwangalia Donald huku
akionekana kuchanganyikiwa.
Minong’ono ilianza kusikika hapo mahakamani, kesi ilionekana kuwa nyepesi mno
kwa upande wa Benjamin. Wakati Donald akilifunga faili lake, hapohapo
akamuomba mheshimiwa jaji kumruhusu kumleta shahidi wa mwisho, huyo
shahidi wa mwisho akaruhusiwa kuingia hapo mahakamani, kitu kilichomshtua
Bwana Seppy, ni David na msichana Vivian wakaingia.
“Aliuawa, nini kinaendelea?” alijiuliza Bwana Seppy, hapohapo akaona huo ndiyo
mwisho wake.

197
“Mheshimiwa jaji, naomba tumpe nafasi shahidi, hii ni kesi nzito ambayo inahitaji
ushahidi wa kutosha kwani kama shahidi hatotoa ushahidi wake hapa mahakamani
sasa hivi, anaweza kuuawa kwani hata alipotajwa kwamba yeye ni shahidi,
alitekwa,” alisema Donald na kumuomba hakimu, hapohapo David akapanda
kizimbani na kuanza kutoa ushahidi wake.
“Mheshimiwa jaji, mara baada ya rafiki yangu Benjamin kupata tatizo, aliniomba
nimsaidie ili kujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia, ilikuwa kazi kubwa
na nzito lakini kwa kutumia kompyuta yangu, niliweza kufanikiwa kunasa ushahidi
wote ambao niliukabidhi kwa Donald.
“Kwa kifupi ni kwamba Bwana Seppy amehusika katika mauaji. Baada ya kujua
kwamba mimi ndiye shahidi kwa kuwa data zote ninazo, akawatuma watu waje
kuniteka, wakaniteka na kunipeleka katika jumba moja lipo sehemu fulani.
“Huko nikakutana na huyu msichana, Vivian ambaye ni mpenzi wa Benjamin,
alinihadithia kilichotokea baada ya kutoroka. Tulipotoroka, kitu cha kwanza
kilikuwa ni kumtafuta Donald ambaye akatupeleka katika jengo la FBI ambapo
tulipewa hifadhi kwani bila kufanya hivyo, tungeuawa.
“Ila mbali na kufanya mauaji ya watu hao, nadhani pia anatakiwa kushtakiwa kwa
kufanya mauaji ya maofisa wa FBI kwani wakati amewatuma vijana wake
kumteka Benjamin, waliua maofisa wa FBI na kumteka Vivian,” alisema David.
David alizungumza mambo mengi yaliyokuwa yametokea, kila alipokuwa
akizungumza, watu walikuwa kimya wakimwangalia tu, jaji McRegan alikuwa
akiandika kila kitu kilichokuwa kikihitajika kuandikwa. Mpaka David
ananyamaza, alikuwa ameridhika na ushahidi.
Jaji akabaki kimya, watu wote walikuwa wakimsikilizia yeye ni kitu gani
angezungumza baada ya kupewa ushahidi uliojitosheleza. Hakutaka kutoa hukumu
moja kwa moja, alichokifanya ni kuliita jopo la wazee wa baraza, wakaomba muda
wa dakika ishirini kwa ajili ya kuijadili kesi hiyo.
Minong’ono haikuisha hapo mahakamani, kila mtu alikuwa akiongea lake huku
wakimtaka jaji amuhukumu Bwana Seppy kifungo cha maisha gerezani au hata
kumnyonga kutokana na kile alichokifanya.
Jopo hilo la wazee wa baraza na jaji lilichukua dakika kumi na tisa, likarudi
mahakamani. Kabla ya kuzungumza kitu chochote kile, jaji akaanza kuwaangalia

198
watu waliokusanyika ndani ya mahakama hiyo kisha kuyapeleka macho yake kwa
Bwana Seppy.
Mwanaume aliyekuwa bilionea, aliyewatetemesha watu wengi kwa ajili ya
ubilionea wake, leo hii alikuwa kizimbani huku akituhumiwa kuua watu kwa
tamaa zake za fedha.
Mbali na yeye, pia kulikuwa na familia yake, muda wote mke wake alikuwa akilia,
hakuwa akiamini kile kilichokuwa kikiendelea mahakamani hapo. Watoto wake
waliokuwa na miaka kumi na tisa nao walikuwa pamoja nao, kitendo cha baba yao
kufikishwa mahakamani tu kisa aliua kiwahuzunisha wote na hawakutegemea
kama kitu kama kile kingetokea.
“Mahakama imejiridhisha kwa kila kitu kilichotokea, ushahidi umekamilika na kila
kitu kilichozungumzwa. Hivyo kwa kupitia kifungu namba 113B kilichowekwa
mwaka 1893, mahakama haikumkuta Benjamin na hatia hivyo inamuachia huru ila
kwa mauaji aliyoyafanya David Seppy, amekutwa na hatia hivyo atahukumiwa
kifo kwa kuchomwa sindano ya cyanide mpaka kifo.
“Hii itakuwa fundisho na pia kwa kupitia maofisa wa FBI, imebainika kwamba
mmoja wa watu wake ambao walikuwa wakifanya mauaji ajulikanaye kwa jina la
Petterson Edward ‘Dracula’ yupo hapa mahakamani akifuatilia kila kitu, hivyo
naye atachukuliwa na kujumuishwa katika adhabu hii,” alisema jaji, hakutaka
kuendelea sana, akapiga nyundo yake, akasimama na kutoka katika kiti kile.
Mahakama nzima ilikuwa shangwe, watu hawakuamini kama kweli kile
walichokisikia ndicho kilichokuwa uamuzi wa mahakama ile. Benjamin hakutaka
kusubiri, hapohapo akachomoka na kuwafuata wazazi wake na kuwakumbatia,
kwake, ilikuwa furaha tele.
Kwa Bwana Seppy ilikuwa ni kilio kikubwa, hakuamini kile ambacho mahakama
ilikiamua, akabaki akilia pale alipokuwa. Hata kabla watu hawajawanyika, tayari
maofisa wa FBI walimfikia Dracula na hapohapo kumpiga pingu na kuondoka
naye.
Siku iliyofuata, magazeti yote nchini Marekani yalitawaliwa na habari hiyo, kifo
cha Bwana Seppy ambaye katika kipindi hicho ndiyo alitakiwa kuanza maandalizi
ya kuiaga familia yake kabla ya kutekelezwa adhabu kali ya kifo ambayo ilikuwa
mbele yake.

199
Alilia na kuhuzunika sana lakini hakuweza kubadilisha kitu chochote kile, hukumu
ilikuwa palepale kwamba ni lazima afe kama hukumu ilivyosomwa mahakamani.
Benjamin akabadilika na kuwa shujaa, yule mtu aliyekuwa akitafutwa usiku na
mchana, akawa mtu aliyekuwa akipendwa na kuzungumziwa kila kona, kila mtu
alitamani kuwa karibu naye japo kupiga picha naye kwani hakukuwa na mtu
aliyeonekana kuwa shujaa kama alivyokuwa yeye.
Alichokifanya ni kuendelea na masomo yake chuoni na baada ya miaka miwili,
akakamilisha miaka yake mitano ya kusomea masuala ya kitabibu na hivyo kuwa
daktari katika Hospitali ya St. Monica iliyokuwa Ohio nchini Marekani.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mafanikio yake, hakumuacha mpenzi wake,
Vivian, baada ya miaka miwili kukatika, akamuoa kwa harusi kubwa na
iliyohudhuriwa na watu wengi maarufu.
Kilichoendelea baada ya hapo, kilikuwa ni historia tu.

MWISHO

200

You might also like