Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 137

1

SURA YA KWANZA

Manyunyu ya mvua yalikuwa yakiendelea kudondoka taratibu kuashiria


kumalizika kwa mvua kubwa iliyonyesha mfululizo usiku kucha. Tofauti na siku
zote, watu walikuwa wachache sana barabarani japokuwa tayari
kulishapambazuka. Ubaridi ulioambatana na mvua hiyo, ulimfanya kila mmoja
kutamani kuendelea kuvuta shuka na kuuchapa usingizi.
“Hee! Tayari ni saa moja? Mungu wangu, nitachelewa kazini,” Edmund Katera
‘Mundi’, kijana mdogo aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni kubwa ya
mawasiliano ya Hashcom Mobile kwenye kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano
(Information Technology) alikurupuka kutoka usingizini na kukimbilia kwenye
kabati lake la nguo kwa lengo la kuchukua taulo.
Harakaharaka akatoka mpaka nje na kuchukua ndoo ya maji ya kuoga huku
mswaki ukiwa mdomoni, akatembea kwa hatua za haraka mpaka bafuni ambapo
alijimwagia maji bila kujali ubaridi uliokuwepo asubuhi hiyo kutokana na mvua
iliyokuwa inaishia.
Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa amerejea chumbani kwake, akavaa na baada
ya dakika chache, alikuwa ameshajiandaa, akajitazama kwenye kioo kikubwa cha
‘dressing table’ iliyokuwa ndani ya chumba chake na baada ya kuridhishwa na
mwonekano wake, alitoka na kufunga mlango wa nyumba aliyokuwa anaishi,
akatoka na kuianza safari ya kuelekea kazini.
Kwa jinsi barabarani kulivyokuwa na matope na foleni kubwa ya magari
barabarani kutokana na mvua hiyo kama ilivyo desturi ya Jiji la Dar es Salaam
hasa nyakati za mvua, ukizingatia kwamba tayari alikuwa nyuma ya muda
kutokana na kuchelewa kuamka, hakuwa na ujanja zaidi ya kukodi bodaboda.
“Naenda Bamaga, Mwenge.”
“Buku nne tu mwanangu.”
“Aaah! Buku nne mi sina, nitakupa buku mbili jero.”
“Unaua mwanangu, ok poa twenzetu,” dereva wa bodaboda alimwambia Edmund
ambaye bila kupoteza muda, alikwea kwenye bodaboda na safari ikaanza. Dereva
huyo wa bodaboda akawa anapenya kwenye foleni, wakati mwingine akilazimika

2
kupita katikati ya magari yaliyokuwa yamefungana kwa lengo la kumuwahisha
mteja wake sehemu aliyokuwa anaenda.
Hata hivyo, haraka hizo zilienda kuishia eneo la Sinza Afrika Sana ambapo magari
kutoka kila upande, yalikuwa yamefungana eneo hilo lililokuwa na makutano ya
barabara nne, moja inayotokea Shekilango, nyingine inayotokea kwenye taa za
kuongozea magari za Bamaga, inayotokea kituo cha polisi cha Mabatini na ile
iliyokuwa inatokea Mwenge kwa kupitia ofisi za TRA.
Kwa jinsi magari hayo yalivyokuwa yamefungana, haikuwa rahisi hata kwa
mwenda kwa miguu kukatisha katikati ya magari hayo, manyunyu ambayo
yalikuwa yamepungua yakaanza kuongezeka na kusababisha kero kubwa kwa
wasafiri waliokuwa wakitumia bodaboda, akiwemo Edmund ambaye tayari shati
lake nadhifu alilokuwa amelivaa lilianza kulowa.
“Pipiiii! Pipiiii... Poooopooo!” milio ya honi nyingi za magari iliendelea kusikika
eneo hilo, kila dereva akijiona yeye yupo sahihi isipokuwa wengine ndiyo
wanavunja sheria za barabarani, hali iliyosababisha taharuki kubwa eneo hilo.
Ilibidi Edmund aanze kumshinikiza dereva wake afanye kila linalowezekana
kuhakikisha wanajinasua eneo hilo kwani ukiachilia mbali ukweli kwamba alikuwa
anaendelea kuloa, alikuwa pia anaendelea kuchelewa kazini.
Wakati dereva wa bodaboda akihangaika kuitoa pikipiki pale ilipokuwa
imezingirwa na magari, kwa bahati mbaya alijikuta akilikwangua gari lililokuwa
nyuma yao na kulibonyeza eneo kubwa na kukwangua rangi.
“Mungu wangu, tumeharibu gari la watu,” alisema dereva wa bodaboda huku
akiendelea kuhangaika kutafuta upenyo wa kukimbia kabla mwenye gari hajashuka
lakini alikuwa amechelewa kwani mwenye gari alishashtukia kwamba amegongwa
na bodaboda.
Msichana mdogo mwenye umri wa kati ya miaka ishirini na mbili hadi ishirini na
tano, mrefu wastani, mwenye umbo lenye mvuto wa aina yake, akiwa amevalia
mavazi ya kisasa kama mtu anayefanya kazi kwenye ofisi moja kubwa mjini, chini
akiwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa iliyomshika kisawasawa maungo yake
makubwa na shati jeupe nadhifu, usoni akiwa amevaa miwani ya kisasa ya rangi
nyeusi, aliteremka kwenye gari la kifahari, Jeep Grand Cherokee la rangi ya fedha
na kuzunguka upande ule bodaboda iliyokuwa imembeba Edmund ilipokuwa.

3
“You stupid poor boys, do you know how much it cost to buy this type of car?”
(Nyie wavulana maskini wapumbavu, mnajua inagharimu kiasi gani kununua gari
kama hili?) alisema msichana huyo kwa jazba huku akivua miwani yake aliyokuwa
amevaa, akainama kuangalia pale dereva wa bodaboda alipoligonga gari lake
wakati akirudi nyuma.
Kwa kuwa Edmund na dereva wake ndiyo waliokuwa na makosa na ni kweli
kwamba waliharibu gari hilo ambalo hata wangeambiwa walipe gharama za
kutengeneza sehemu waliyoigonga hawakuwa na fedha, ilibidi waufyate mkia.
Wakawa wanatazamana huku kila mmoja akijisikia aibu kubwa kutokana na jinsi
msichana huyo alivyokuwa akiendelea kuwachambua, akichanganya lugha,
Kiingereza cha Kimarekani na Kiswahili.
“Please forgive us ladyboss, its just an accident,” (Tafadhali tusamehe bosi, ni ajali
tu) alisema Edmund, kauli iliyomfanya yule msichana amgeukie na kumtazama
kwa jicho la ukali.
“Ajali? Unazijua ajali wewe? Mtazame kwanza, nikikwambia ulipe gharama za
uharibifu alioufanya huyo maskini mwenzio utaweza? Go to hell! (Nenda
kuzimu!)” alisema msichana huyo kwa hasira, kauli iliyomfedhehesha mno
Edmund.
Tayari madereva wa magari mengine walikuwa tayari wameteremka kwenye
magari yao na kuanza kumsihi msichana huyo awasamehe Edmund na dereva
wake. Kwa nyodo na dharau akageuka na kuanza kutembea kuelekea kwenye gari
lake huku akiivaa miwani yake. Akaingia kwenye gari na kukaa nyuma ya usukani.
Edmund aliyekuwa ameshuka kwenye bodaboda, aliendelea kulitazama gari lile,
hasa pale bodaboda yao ilipopagonga. Akiwa anaendelea kushangaa, aliona kitu
chini kwenye lami chini ya gari, bila kuonekana na mtu yeyote akainama na
kukiokota.
Ilikuwa ni simu ya kisasa iliyokuwa imedondoka chini, bila hata kuuliza akajua
kwa vyovyote lazima yule msichana aliiangusha alipoinama kuangalia gari lake.
Tayari askari wa usalama barabarani walikuwa wameshafika eneo hilo kusaidia
kufungua njia ambayo ilikuwa imefungwa na magari yaliyofungamana kila
upande.
Wakati Edmund akiwa bado anajishauri kama amrudishie msichana yule simu
yake au la, tayari barabara ilishafunguliwa na magari yakaanza kuondoka kwa kasi.

4
Akashuhudia yule msichana naye akibadili gia kwenye gari lake la kifahari na
kuondoka kwa mbwembwe za hali ya juu.
“Oyaa twende mwanangu!” dereva wa bodaboda alimuita Edmund kwa sauti ya
juu ambayo ilimzindua kutoka kwenye hali aliyokuwa nayo, akaiweka simu hiyo
mfukoni na kusogea hadi pale dereva wa bodaboda alipokuwa anamsubiri,
akapanda na kuendelea na safari.
Kwa kuwa eneo hilo halikuwa mbali na ofisini kwao, dakika chache baadaye tayari
walishawasili Bamaga, akashuka kwenye bodaboda na kumlipa dereva fedha zake
kisha akaanza kutembea harakaharaka kuelekea kazini kwao huku akiwa
anaendelea kutafakari juu ya tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita na jinsi
alivyotolewa nishai na msichana yule mrembo.

Kila alipokuwa akikumbuka jinsi msichana huyo alivyowatolea maneno ya


shombo, Edmund au Mundi kama wengi walivyozoea kumuita, alijikuta
akipandwa na hasira kali ya maisha.
Aliamini umaskini wake ndiyo uliosababisha msichana huyo amtusi kwani kama
angekuwa tajiri, na yeye angekuwa akiendesha gari lake, tena la kifahari kuliko la
msichana huyo na kamwe asingekumbana na dharau kama hizo.
Edmund alishusha pumzi ndefu na kuwasha kompyuta yake aliyokuwa anaitumia
kazini, akatoa kitambaa na kuanza kujikausha maji ya mvua iliyomnyeshea huku
kichwa chake kikiwa bado hakijatulia.
Dakika chache baadaye, aliinuka sehemu anayokaa siku zote kazini na kwenda
kutengeneza kahawa kwani baridi aliyokuwa anaisikia asubuhi hiyo, ukichanganya
na kipupwe (AC) ya ofisini humo, alijiona kama mwili wake unaganda.
Akarudi kwenye kiti chake akiwa na kikombe cha kahawa, akakaa na kuanza
kuchangamsha tumbo huku bado akionesha kutotulia kiakili.
“Mundi vipi mwanangu? Mbona leo hata salamu hakuna? Yaani umefika
kimyakimya na kula bati kama hujatuona wanao,” Clarence, mfanyakazi
mwenzake na Edmund, waliyekuwa wakifanya kazi kwenye kitengo kimoja cha
Teknolojia ya Mawasiliano (IT) kwenye Kampuni ya Hashcom Mobile, alimuuliza
Edmund baada ya kumuona hayuko kwenye hali yake ya kawaida.

5
Swali hilo lilimzindua Edmund kutoka kwenye lindi la mawazo, ikabidi aanze
kuvunga na kusingizia kwamba mvua iliyomnyeshea asubuhi hiyo wakati akienda
kazini ndiyo iliyosababisha akili zake zihame. Wakaendelea kuzungumza mawili
matatu kisha Edmund akatulia tena. Ni hapo ndipo alipokumbuka kwamba
mfukoni alikuwa na kitu cha thamani.
Akaingiza mkono na kutoa simu kubwa ya kisasa iliyokuwa mfukoni, kwa mara
nyingine akaitazama na kujikuta akishusha pumzi ndefu. Ilikuwa simu ya thamani
kubwa mno ambapo kwa makadirio yake ya harakaharaka, aliamini dukani lazima
itakuwa inauzwa zaidi ya shilingi milioni mbili.
“Duh! Mundi umenunua iPhone 6? Umepata wapi hela mwanangu? Hizo simu za
washua, wewe maskini mwenzangu umeipata wapi?” Clarence alimuuliza Edmund
kwa masihara baada ya kumuona akiitazama simu hiyo.
Wafanyakazi kadhaa waliokuwa wamekaa jirani naye, waliacha kila walichokuwa
wanakifanya na kumsogelea, kila mmoja akitaka kuiona simu hiyo ambayo kwa
kipindi hicho ndiyo ilikuwa ikiongoza kwenye soko la simu kwa kuwa na bei ya
juu na ubora kuliko simu zote.
“Hebu tuone? Hebu na mimi niione?” wafanyakazi kadhaa walikuwa wakigombea
kuishangaa simu hiyo. Wakati wao wakigombea simu hiyo, akili ya Edmund
ilikuwa mbali kabisa, akiendelea kumfikiria yule msichana na jinsi
alivyomdhalilisha mbele za watu.
Baada ya muda, Edmund aliichukua simu hiyo na kuanza kuikagua vizuri,
akagundua kuwa ilikuwa imefungwa kwa namba maalum (security codes).
Kwa kuwa alikuwa na uelewa mkubwa wa namna ya kuchezea simu na kompyuta,
muda mfupi baadaye alifanikiwa kuifungua simu hiyo, juu kabisa akakutana na
picha ya msichana yule aliyemtoa nishai, jambo lililomfanya awe na uhakika
kwamba ni kweli ile simu ni yake na aliiangusha pale alipoikuwa anaangalia jinsi
gari lake la kifahari lilivyogongwa na bodaboda.
Katika hali ambayo hakuitegemea, Edmund alijikuta macho yake yakiganda juu ya
picha ya yule msichana, akawa anamtazama huku akiwa ni kama haamini
alichokuwa anakiona. Mwisho alishusha pumzi ndefu na kuendelea kuishangaa
simu hiyo.
Kitu kingine kilichozidi kumshangaza, licha ya kufanikiwa kuifungua simu hiyo
sehemu ya kwanza, kila kitu ndani ya simu kilikuwa kimefungwa kwa namba

6
maalum za usalama, kuanzia kwenye meseji, kwenye picha, kwenye majina na kila
kitu.
***
Gari la kifahari, Jeep Grand Cherokee (New Model), lilikuwa likipasua lami kwa
mwendo wa kasi, wakati mwingine dereva akilazimika kuyapita magari mengine
yaliyokuwa yanasuasua mbele yake kuelekea Mikocheni. Dakika kadhaa baadaye,
tayari lilikuwa limewasili Mikocheni, dereva akapiga honi, walinzi wawili wenye
bunduki wakafungua geti kisha likaingizwa mpaka sehemu ya maegesho, nje ya
ghorofa refu la kisasa lililokuwa na mandhari ya kuvutia mno.
“Mungu wangu, simu yangu nimeiweka wapi tena?”
“Simu gani bosi? Mbona hapo umeshika simu mbili mkononi?”
“Ile simu yangu ninayoitumia siku zote, siyo hizi,” alisema msichana mrembo
wakati akiteremka kwenye gari, na kusababisha walinzi waache kila walichokuwa
wanakifanya kwa ajili ya kumsaidia bosi wao huyo.
Licha ya kusaidiana kupekua kwenye gari karibu kila sehemu, hawakufanikiwa
kuiona simu hiyo, jambo lililosababisha msichana huyo aanze kutokwa na
machozi.
“Ina vitu vyangu vingi sana vya siri, siwezi kuruhusu ipotee, haiwezekani,”
alisema msichana huyo akionesha kuchanganyikiwa mno.
“Hebu jaribu kuipiga,” alishauri mlinzi mmoja, wazo ambalo msichana huyo
aliona linafaa, kwa kutumia simu yake nyingine, aliipiga simu hiyo. Kwa bahati
nzuri, bado ilikuwa hewani, ikawa inaita.
“Inaita! Inaita,” alisema msichana huyo akionesha kuwa na shauku kubwa ya
kusikia nani atapokea.
***
Edmund aliendelea kufanya kazi zake lakini bado akili yake ilikuwa haitulii.
Alitamani kufahamu vitu vingi zaidi kuhusu yule msichana mrembo aliyemtoa
nishai asubuhi hiyo na njia pekee aliona ni kupitia simu ya msichana huyo.
Akaamua kuanza kuishughulikia, kabla hajafungua sehemu nyingine, alikopi
mafaili yote yaliyokuwa kwenye simu hiyo (back up) na kuhamishia kwenye
kompyuta yake.

7
Akiwa Anahangaika kuifungua kwa kutumia mbinu alizokuwa anazijua
mwenyewe, simu hiyo ilianza kuita. Akashtuka na kuanza kila alichokuwa
anakifanya, akawa anaitazama inavyoita huku akijishauri kama apokee au la.
Mwisho aliamua kuipokea.
“Haloo!”
“Haloo, samahani sana kakaangu naomba msaada wako. Mimi ni mwenye hiyo
simu nimeipoteza hata sijui niliiangushia wapi. Nakuomba unielekeze popote ulipo
nakuja na nakuahidi kuwa nitakupa shilingi milioni moja ‘cash’ ukinisaidia kuipata
simu yangu,” ilisikika sauti upande wa pili ambapo bila hata kuuliza Edmund
alijua ni ya yule msichana aliyemtoa nishai asubuhi. Kwa kuwa lengo lake
halikuwa kuichukua simu hiyo, aliamua kumuelekeza ofisini kwao, Hashcom
Mobile, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam. Baada ya kukata simu, msichana
yule aliingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi kubwa, akiwaacha wale
walinzi wakitazamana.
Dakika chache baadaye, tayari alikuwa amewasili Bamaga, akafuata ramani
aliyoelekezwa na kutokezea kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi Edmund.
Akapaki gari lake na kwenda kujitambulisha kwa walinzi kisha akaruhusiwa
kuingia ndani. Alipoingia tu getini, alitoa simu yake na kuipiga tena ile namba,
ikawa inaita.
“Edmund kuna mgeni wako mapokezi,” sauti ya mfanyakazi mwenzake ilisikika,
alipotazama simu iliyokuwa inaita, Edmund akajua lazima ni yule msichana
amewasili. Harakaharaka akainuka na kujiweka vizuri nguo zake ambazo bado
hazikuwa zimekauka vizuri, akatoka kuelekea mapokezi.

“Mambo!” Edmund alimsalimia yule msichana baada ya kumkuta mapokezi,


akiwa amejiinamia akiiwaza simu yake. Salamu hiyo ilimfanya ainue uso wake,
macho yake na ya Edmund yakagongana.
Mshtuko alioupata ulionekana waziwazi kwani ni kama hakutegemea kwamba mtu
aliyemuokotea simu yake ni Edmund, kijana ambaye muda mfupi uliopita
alimuonesha dharau ya kupindukia.
“Po..a,” alijibu msichana huyo kwa kubabaika, Edmund akamuonesha ishara
kwamba amfuate kwani mapokezi palikuwa na wageni wengine wengi,

8
wakaongozana mpaka kwenye chumba maalum cha mazungumzo, yule msichana
akiwa bado haamini macho yake.
“Wewe ndiye uliyeniokotea simu?” alisema msichana huyo kwa upole mno, tofauti
kabisa na alivyokuwa mwanzo.
“Yaah! Naitwa Edmund, bila shaka unanikumbuka,” alisema Edmund, kauli
iliyozidi kumuweka yule msichana kwenye wakati mgumu.
“Naomba unisamehe sana kakaangu kwa kilichotokea asubuhi. Nilitoka nyumbani
nikiwa nimevurugwa ndiyo maana nikawa mkali sana kwenu. Tafadhali nakuomba
unisamehe,” alisema yule msichana kwa upole huku mara kwa mara akikwepesha
macho yake yasigongane na ya Edmund aliyekuwa ametulia anamtazama kwa
makini.
Edmund alishusha pumzi na kumwambia asiwe na wasiwasi ameshamsamehe
ndiyo maana ameamua kumpa ushirikiano ili aipate simu yake.
“Ooh! Ahsante sana kakaangu, yaani hata sijui namna ya kukushukuru, simu yangu
ina vitu vingi sana vya muhimu, yaani umenikoa kweli,” alisema msichana huyo
huku akimpa mkono Edmund, tabasamu hafifu likiwa limechanua kwenye uso
wake.
Kitendo cha kupeana mkono na msichana huyo, kilimfanya Edmund ahisi kama
amepigwa na shoti ya umeme, akabaki amezubaa mpaka msichana huyo alipoamua
kutoa mkono wake mwenyewe.
“Una akaunti benki?”
“Yaah ninayo, vipi kwani.”
“Nataka nikuhamishie fedha zako kama nilivyokuahidi. Shilingi milioni moja
‘cash’ kwa msaada ulionipa.
“Hapana, sihitaji malipo kutoka kwako dadaangu, nimekusaidia tu.”
“Hapana Edmund, chukua tu kwa sababu mimi ndiyo niliyeahidi kukupa, nitajie
namba yako ya akaunti tafadhali,” alisema msichana huyo lakini Edmund
akaendelea kushikilia msimamo wake.
Ni kweli Edmund alikuwa na shida ya fedha na kupewa shilingi milioni moja
katika siku kama hiyo, tarehe za mshahara zikiwa mbali kabisa kungemsaidia sana
lakini hakutaka kuonesha udhaifu, akashikilia msimamo wake.

9
“Ngoja nikakuchukulie simu yako,” alisema Edmund na kuinuka, akawa anatoka
kwenye chumba hicho cha mazungumzo na kumuacha yule msichana amekaa
palepale alipokuwa amekaa awali.
Alipofika mlangoni, aliufungua na kugeuka nyuma, akashangaa kumuona yule
msichana akimtazama kwa macho ya wizi, macho yao yakagongana kisha
harakaharaka yule msichana akakwepesha macho yake. Edmund akatoka, muda
mfupi baadaye akarejea akiwa na simu hiyo.
“Hii hapa,” alisema huku akimkabidhi, msichana huyo akaipokea huku tabasamu
pana likiwa limechanua kwenye uso wake.”
“Siamini! Jamani ahsante we kaka,” alisema msichana huyo huku akinyoosha tena
mkono wa shukrani kumpa Edmund, wakashikana tena. Hali kama iliyomtokea
awali alipopeana mkono na msichana huyo ikajirudia tena, akabaki kujishangaa
kwani haikuwa kawaida yake.
“Basi chukua hii utakunywa hata soda naona zawadi yangu umeikataa,” alisema
msichana huyo huku akiingiza mkono mwingine kwenye pochi yake ya kisasa,
Edmund akataka kukataa tena lakini alikuwa amechelewa kwani msichana huyo
alimuwekea noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi kwenye mfuko wa shati lake.
“Mbona hujaniuliza jina langu? Au bado una hasira na mimi?” msichana huyo
aliuliza huku tabasamu lake likizidi kuchanua na kuupamba uso wake, akazidi
kuonekana mrembo. Edmund alishindwa cha kujibu zaidi ya kutabasamu, ni kweli
tangu msichana huyo afike, hakuwa amemuuliza jina lake na huenda kama
mwenyewe asingeanza, angeondoka bila kumuuliza.
“Hii ni ‘business card’ yangu na hilo hapo ndiyo jina langu,” alisema huku
akimkabidhi Edmund kadi ya kisasa ya mawasiliano. Akaipokea na kuitazama
vizuri.
“Samantha!”
“Yes! That’s my name.” (Ndiyo! Hilo ndiyo jina langu) alisema msichana huyo
kwa lafudhi laini, Edmund akazidi kujikuta katika wakati mgumu.
“Nisikupotezee muda wako najua upo kazini, narudia tena kukuomba radhi kwa
yote yaliyotokea asubuhi na nakushukuru sana kwa wema wako,” alisema
msichana huyo huku akiinuka, akachukua kila kitu chake na kuagana na Edmund.

10
SURA YA PILI

“Ngoja nikutoe mpaka nje,” alisema Edmund huku naye akisimama, wakatoka
kwenye chumba cha maongezi, wakaelekea mapokezi kisha Edmund akamsaidia
kufungua mlango wa nje, wakatoka na kuelekea kwenye gari la kifahari alilokuja
nalo msichana yule.
“Hebu jaribu kuibipu simu yangu,” alisema msichana huyo na kumtajia Edmund
namba, bila kuelewa lengo la msichana huyo, Edmund alifanya kama
alivyoambiwa, simu ikaita.
“Haya kazi njema kaka, nakushukuru sana,” alisema Samantha na kubonyeza
rimoti aliyokuwa ameishika, gari likawaka taa za pembeni na kutoa mlio wa
kuashiria kwamba milango imejifungua.
Msichana huyo akatembea kwa maringo hadi kwenye gari, akaingia na kukaa
nyuma ya usukani, akawasha gari na kutetemsha kioo, akawa anampungia mkono
Edmund ambaye bado alikuwa amezubaa, akiwa ni kama haamini alichokuwa
anakiona mbele ya macho yake.
Akaondoka eneo hilo akiwa ndani ya gari lake la kifahari, Jeep Grand Cherokee
(New Model) na kumuacha Edmund amesimama palepale.
“Mundi vipi mshkaji wangu, mbona umepigwa na butwaa kiasi hicho? Naona
ulikuwa na chombo cha ukweli kinoma,” Sam, mlinzi wa kampuni aliyokuwa
akifanyia kazi Edmund alimtania baada ya kumuona bado amezubaa palepale nje,
Edmund akatabasamu na kurudi ofisini kuendelea na kazi zake.
“Ebwana eeh! Yule malaika uliyekuwa naye ni nani arifu? Nipigie pande na mimi
nijiweke,” Clarence, rafiki yake Edmund alimtania baada ya kurejea, wote
wakaishia kucheka tu. Edmund akakaa kwenye kompyuta yake na kushusha pumzi
ndefu, akakumbuka kwamba msichana yule mrembo alimuwekea fedha kwenye
mfuko wake wa shati.
“Shilingi laki moja? Mungu wangu, huyu dada anafanya kazi gani kwani?” alisema
Edmund baada ya kuhesabu fedha hizo. Akajikuta akishindwa kuzuia tabasamu
lisiupambe uso wake. Muda mfupi baadaye, simu yake ilianza kuita, harakaharaka
akapokea.

11
“Nashukuru sana kakaangu nimefika ofisini, kama utapata muda baadaye naomba
nije kukuchukua tukapate lanchi pamoja kama shukrani yangu kwako,” alisema
Samantha.

“Ok hakuna shida dada’angu,” alijibu Edmund kisha simu ikakatwa, tabasamu
pana likachanua kwenye uso wake kwani licha ya ukweli kwamba msichana huyo
alikuwa amemfanyia kitendo cha kumdhalilisha sana asubuhi ya siku hiyo,
alijikuta akimsamehe kirahisi na kutamani kumjua zaidi, akaona hiyo ndiyo nafasi
yake.
“Ebwana mbona mudi yako imebadilika ghafla? Tabasamu pana muda wote
utafikiri umeokota pochi ya Mzungu?” Walungasa, mfanyakazi mwingine
waliyekuwa akifanya kazi na Edmund alimuuliza baada ya kumuona muda wote
akiwa na tabasamu pana, akaishia kucheka tu bila kueleza chanzo cha furaha yake.
Saa zilizidi kuyoyoma, hatimaye muda wa chakula cha mchana uliwadia, Edmund
akawa anaitazama simu yake kwa shauku kubwa akisubiri Samantha ampigie
kwani walikubaliana kwenda kula chakula cha mchana pamoja.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yake,
harakaharaka akaufungua na kuusoma.
“Sorry! Nimeshindwa kuja kuna kazi zimenibana. Naomba nikupitie jioni baada ya
muda wa kazi tukakae sehemu tubadilishane mawazo,” ulisomeka ujumbe huo
kutoka kwa Samantha, Edmund akashusha pumzi ndefu na kumjibu kwamba
asijali.
Akaendelea kufanya kazi huku mawazo yake yakiendelea kumuwaza msichana
huyo. Hatimaye muda wa kutoka kazini ukawadia, Edmund akiwa
ameshakamilisha karibu kazi zote alizopaswa kuzifanya kwa siku hiyo. Akazima
kompyuta yake na kuwaaga wenzake kisha taratibu akatoka mpaka mapokezi.
Kabla hajatoka kwenye geti kubwa, alisikia simu yake ikiita, harakaharaka akaitoa
mfukoni na kutazama namba ya mpigaji, hakuwa mwingine bali Samantha,
akaipokea huku tabasamu likiwa limeupamba uso wake.
“Umeshatoka kazini?”
“Ndiyo najiandaa kutoka.”

12
“Ok basi nisubiri hapohapo, nipo jirani nakuja,” alisema Samantha kisha akakata
simu, Edmund akashusha pumzi ndefu na kurudi kwenye chumba cha
mazungumzo, akawa anajitazama kwenye vioo vya chumba hicho na kujiweka
vizuri.
Baadaye alitoka mpaka nje lakini kabla hajakaa kwenye benchi lililopo nje ya ofisi
yao, alisikia simu yake ikiita mfululizo, alipotoa aligundua kuwa ni Samantha.
“Napaki gari hapa nje ya ofisi yenu, uko wapi?” alisema msichana huyo,
harakaharaka Edmund akasimama na kuanza kuangalia gari lililokuwa linapaki,
akaliona Jeep Grand Cherokee (New Model) la msichana huyo likiingia eneo la
maegesho, akatembea kulifuata huku akipunga mkono.
“Mambo!” Samantha alisema kwa sauti nyororo huku akishusha kioo cha gari lake.
“Poa! Vipi za kazi,” Edmund alijikakamua na kuuvaa uchangamfu wa kulazimisha.
Alishindwa kujielewa kwa nini kila alipokuwa akimuona msichana huyo alikuwa
akiishiwa nguvu kabisa.
“Nzuri! Zunguka upande wa pili uingie kwenye gari,” alisema msichana huyo,
tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake. Edmund akazunguka mpaka
upande wa pili na kufungua mlango, akapokelewa na harufu ya manukato mazuri
yaliyokuwa yamepuliziwa ndani ya gari hilo.
Akaingia na kukaa pembeni ya Samantha, kipupwe kilichokuwa kinapuliza ndani
ya gari hilo, ukichanganya na muziki laini uliokuwa unapiga kwa sauti ya chini,
vilimfanya Edmund ajihisi kama yupo kwenye ulimwengu mwingine wa tofauti
kabisa.
“Vipi za tangu asubuhi,” alisema Samantha huku akimtazama Edmund, tabasamu
likiwa limeujaza uso wake.
“Poa kabisa, sijui wewe.”
“Niko poa kabisa, sasa naomba twende Kunduchi, kule kuna hoteli nzuri huwa
naipenda sana,” alisema msichana huyo, Edmund akatingisha kichwa kuonesha
kukubaliana naye, akawasha gari na kuingiza gia, akalitoa eneo la maegesho na
kuingia barabarani, akaongeza kidogo sauti ya muziki na kuelekea kwenye
barabara ya lami.
“Ooh! Samahani naomba ufunge mkanda,” alisema Samantha baada ya kugundua
kuwa kumbe Edmund hakuwa amefunga mkanda. Kijana huyo akiwa anahangaika

13
kufunga mkanda, Samantha alisimamisha gari na kumsaidia, hali iliyowafanya
wawili hao wasogeleane miili yao. Mapigo ya moyo wa Edmund yakaongezeka
kasi ghafla.
Baada ya kumaliza kumsaidia kufunga mkanda, safari iliendelea huku Samantha
akimuonesha Edmund uchangamfu ambao hakuutegemea. Dakika kadhaa baadaye,
tayari walikuwa wamewasili Kunduchi, msichana huyo akaenda kupaki gari
sehemu ya maegesho kisha wakateremka na kutafuta sehemu nzuri ya kukaa.
“Nimefurahi sana kufahamiana na wewe japokuwa tumekutana kwenye mazingira
ya ajabu,” Samantha alivunja ukimya baada ya kuwa ameshamuagiza vinywaji,
Edmund akatabasamu bila kusema neno lolote.
“Naomba uniambie kama umenisamehe.”
“Nimekusamehe wala usiwe na wasiwasi Samantha,” alisema Edmund huku
akijitahidi kupambana na hofu ndani ya moyo wake. Kila kitu kilikuwa kigeni
kwake, japokuwa alikuwa akiishi Dar es Salaam hakuwahi kuingia kwenye hoteli
hiyo hata mara moja, akawa anaona kila kitu kilichokuwa kinatokea kama muujiza
kwake.
“Kwani we unaishi wapi?” Samantha alimuuliza Edmund ambaye alimuelekeza
mpaka mtaa anaoishi.
“Unaishi na nani?”
“Peke yangu.”
“Kwa nini unaishi peke yako? Kwani huna mke?” Samantha alimuuliza Edmund
kimasihara huku akivuta juisi taratibu kwa kutumia mrija, akacheka sana na
kumjibu kwamba hakuwa ameoa bado.
“Ila una mchumba?”
“Hapana, bado sijabahatika, najipanga kimaisha kwanza,” alisema Edmund na
kuanza kumuuliza msichana huyo kuhusu maisha yake.
“Mimi naishi na wazazi wangu Upanga, nafanya kazi ya kusimamia kampuni
kadhaa za baba kwani mimi ni mtoto wake wa pekee,” alisema Samantha huku
akiendelea kunywa juisi taratibu.
Wakaendelea kuzungumza mambo mbalimbali ambapo msichana huyo alimueleza
Edmund vitu vingi kuhusu maisha yake. Ungeweza kudhani wawili hao

14
wamefahamiana siku nyingi zilizopita kutokana na jinsi walivyokuwa wakipiga
stori.
Baadaye, walikula chakula cha usiku pamoja kisha wakaondoka hotelini hapo
baada ya kuwa msichana huyo amelipia gharama zote.
“Nataka niende kupaona nyumbani kwako,” alisema Samantha huku safari
ikiendelea, Edmund akamgeukia na kumtazama, macho yao yakagongana.
“Hakuna tatizo Samantha,” alijibu Edmund, wote wakatabasamu. Safari iliendelea
na baadaye Edmund akaanza kumuelekeza msichana huyo mtaa waliokuwa
wanaishi. Edmund alitegemea kwamba baada ya kufika na kuiona nyumba
anayoishi, msichana huyo ataaga na kuondoka kutokana na ukweli kwamba
nyumba aliyokuwa anaishi ilikuwa na hadhi ya chini ukilinganisha na maisha ya
msichana huyo.
Cha ajabu, walipofika, Samantha naye alitaka kushuka ili akakione chumba
alichokuwa anaishi Edmund, kijasho chembamba kikaanza kumtoka kijana huyo
akihofia msichana huyo atamdharau baada ya kuona maisha aliyokuwa anaishi.
Samantha hakujali kitu, wakaingia kwenye nyumba aliyokuwa amepanga kijana
huyo na hatimaye wakaingia mpaka ndani, ikiwa tayari imeshatimia saa tatu za
usiku.
“Ka..karibu sa..na,” Edmund alimkaribisha Samantha kwa kubabaika, msichana
huyo akaachia tabasamu pana kwani alishagundua hofu iliyokuwa ndani ya moyo
wa Edmund.
“Unaishi na nani?” Samantha alirudia kuuliza swali ambalo tayari alishajibiwa
huku akiwa anazunguka huku na kule ndani ya chumba hicho.
“Naishi mwenyewe,” alijibu Edmund huku akiendelea kujisikia aibu kubwa ndani
ya moyo wake. Kwa hadhi aliyokuwa nayo Samantha, alijikuta akishindwa kabisa
kujiamini kwani maisha yake yalikuwa ya kawaida sana ukilinganisha na ya
Samantha, japo bado hakuwa amefika nyumbani kwao lakini mwonekano wake tu
ulitosha kutoa picha kamili.
“Huku ndiyo chumbani kwako?” Samantha aliuliza huku akisukuma mlango wa
kuingilia chumbani, kabla hata Edmund hajajibu kitu, tayari msichana huyo
alikuwa ameshafungua mlango.

15
“Unawashia wapi taa,” aliuliza kwa sauti ya chini, Edmund akamfuata kwa nyuma
na kuwasha taa ukutani huku akiendelea kujisikia aibu kwani asubuhi ya siku hiyo
alikurupuka kuwahi kazini na hakukumbuka hata kutandika kitanda wala kupanga
vitu vyake vizuri.
“Ahahaaa!” Samantha alicheka sana baada ya kuona chumba cha Edmund
kilivyokuwa kimekosa mpangilio mzuri.
“Inabidi uoe mke atakayekuwa anakusaidia hata kutandika kitanda na kupanga
nguo vizuri kabatini,” alisema msichana huyo huku akikaa kwenye kitanda cha
Edmund, macho yake yakawa yanaendelea kuangaza huku na kule, tabasamu pana
likiwa limechanua kwenye uso wake.
Edmund naye alianza kuhangaika kupangapanga vitu vizuri, akaanza kwa kuokota
nguo zilizokuwa zimezagaa sakafuni na kuziweka kwenye kapu la nguo chafu
kisha akatoa shuka safi kabatini na kuanza kutandika, ikabidi Samantha amsaidie
kwani alimuona alivyokuwa anahangaika.
“Mh! Mbona humu ndani kwako kuna joto sana? Huna feni?” aliuliza Samantha
wakati akimalizia kutandika kitanda, Edmund akaanza kubabaika tena kwani
ukweli ni kwamba feni yake ilikuwa imeharibika na aliipeleka kwa fundi siku
mbili zilizopita lakini akakosa muda wa kwenda kuichukua.
“Sasa nitakaaje? Mwenzio nasikia joto sana?” alisema Samantha huku akianza
kufungua vifungo vya shati jeupe alilokuwa amevaa, akabaki na sidiria nyeupe na
kufanya kifua chake kilichojaa vizuri kianze kuonekana na kusababisha Edmund
azidi kukosa uvumilivu.
Japokuwa hakuwa akiishi na mwanamke na hakuwa na mpenzi kwa kipindi kirefu
baada ya kuumizwa na aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza, takribani miezi kumi
iliyopita, Edmund alikuwa mwanaume aliyekamilika kila idara.
Ukichanganya na ukweli kwamba alikuwa akivutiwa sana na msichana huyo licha
ya alichomfanyia asubuhi ya siku hiyo, Edmund alijikuta akizidi kuwa kwenye
wakati mgumu mno kihisia.
“Basi ngoja nifungue dirisha,” alisema Edmund huku akijitahidi kuyakwepesha
macho yake yasitue kwenye mwili wa Samantha ambaye alikuwa akijigeuzageuza
kimitego pale kitandani huku akiendelea kulalamika kwamba anasikia joto kali.
“Hapana! Usifungue nitavumilia tu, ila naomba kama hutajali nivue shati labda
nitajisikia vizuri,” alisema msichana huyo, Edmund akakosa cha kujibu. Msichana

16
huyo akasimama na kumuomba Edmund amsaidie kumfungua vifungo vya shati
vilivyobakia, akatii bila shuruti.
Wakati akiendelea kumfungua vifungo vya shati, Samantha alikuwa akimtazama
Edmund kwa macho yaliyobeba ujumbe mzito, akamsaidia kulivua na kulitundika
ukutani.
“Edmund! Naomba sogea nikwambie kitu,” alisema msichana huyo kwa sauti
iliyokuwa inatokea puani, Edmund akatii alichoambiwa ambapo katika hali
ambayo hakuitegemea, msichana huyo mrembo kupindukia alimkumbatia kwa
nguvu kifuani huku akipumua kwa fujo mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio za
marathon, ngozi yake laini iliyokuwa na joto la huba vikazidi kumchanganya
Edmund.
“Nakupenda sana Edmund, hata sijielewi mwenzio, nimejikuta nakupenda tu
ghafla wakati siyo kawaida yangu,” alisema Samantha kwa sauti ya kudeka,
akaanza kumwagia mvua ya mabusu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Ni kama Edmund alikuwa akiusubiri kwa hamu muda huo kwani hakutaka kulaza
damu, naye akawa anamuonesha ushirikiano mkubwa msichana huyo,
wakagandana kama ruba huku mapigo ya moyo ya kila mmoja yakizidi
kuongezeka kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, miguno ya raha
ikawa inasikika kutoka kwa kila mmoja.
Waliendelea kupasha miili yao tayari kwa mechi ya kirafiki isiyo na refa wala jezi,
huku mara kwa mara msichana huyo akirudia kumuomba radhi Edmund kwa
kilichotokea asubuhi ya siku hiyo kwa sauti yenye uwezo wa kumtoa nyoka
pangoni, kufumba na kufumbua wakajikuta wote wakiwa kama walivyoletwa
duniani.
“Unazijua love bites?” Samantha alimuuliza Edmund kwa sauti ya chini mno huku
akiendelea kumfanyia vituko vya hapa na pale, akawa anatingisha kichwa
kuonesha kukubali kwani japokuwa hakuwa mzoefu sana kwenye ulimwengu wa
mapenzi, Edmund alikuwa akijua baadhi ya vitu.
“Naomba unitoe hapa,” alisema Samantha huku akimuoneshea Edmund shingo
yake, kijana wa watu akatii, naye akamng’ang’ania Edmund shingoni, kazi hiyo
ikaanza.
Hata hivyo, tofauti na Edmund alivyokuwa anafahamu, Samantha alikuwa
akilifanya zoezi hilo kwa nguvu kiasi cha kumfanya Edmund aanze kuhisi

17
maumivu makali kwenye shingo yake lakini akawa anajikaza kwani alikuwa na
uhakika kuwa muda mfupi baadaye wataingia ‘msambweni’ , jambo alilokuwa
analisubiri kwa hamu kwani mpaka muda huo hakuwa akijielewa tena.
Kufumbana kufumbua, Samantha alikurupuka kama mtu aliyezinduka usingizini,
akajitoa kwenye kifua cha Edmund, kwa kasi ya ajabu akasimama huku mapigo ya
moyo wake yakimuenda mbio kuliko kawaida. Akaanza kutafuta nguo zake
ambazo kila moja ilikuwa imeangukia upande wake.
“Vipi tena?” Edmund aliuliza kwa mshangao lakini Samantha hakumjibu kitu,
akaendelea kuvaa nguo zake na muda mfupi baadaye, tayari alikuwa amemaliza,
akawa anataka kuondoka.
Kwa kuwa tayari Edmund alikuwa kwenye hali mbaya, hakutaka kukubali kirahisi
Samantha aondoke na kumuacha kwenye hali ile kwani kile alichokuwa
anakisubiri kwa hamu hakikuwa kimekamilika.
Akajaribu kumzuia huku akitaka kujua ni jambo gani limetokea mpaka Samantha
abadilike ghafla kiasi kile lakini tayari alikuwa amechelewa, Samantha alitoka
mbiombio mpaka nje alikopaki gari lake la kifahari. Wakati Edmund akihangaika
kutafuta nguo zake ili amuwahi kabla hajaondoka, alisikia muungurumo wa gari la
kifahari la msichana huyo likiondoka kwa kasi eneo hilo, akabaki amepigwa na
butwaa, akiwa haelewi kabisa kilichotokea.
Ni hapo ndipo alipoanza kuhisi maumivu makali kwenye shingo yake, alipopeleka
mkono wake pale alipotolewa ‘love bite’ na Samantha, hakuyaamini macho yake
baada ya kugundua kuwa palikuwa na kidonda huku damu zikianza kumchuruzika
kwa wingi.
“Mungu wangu, hiki nini tena?” alisema Edmund huku akisogea kwenye kioo
kikubwa kujiangalia.
Alipojiangalia shingoni, mahali alipotolewa ‘love bite’ na Samantha, alishtuka
kugundua kuwa kumbe msichana huyo alikuwa amemng’ata na kumtoa kidonda
kikubwa kilichokuwa kikiendelea kutoka damu kwa wingi.
Harakaharaka alikimbilia kwenye kabati na kutoa kiboksi kidogo cha huduma ya
kwanza, akatoa pamba na ‘spirit’ na kurudi kwenye kioo, akawa anajisafisha huku
akiwa ameuma meno kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia.
Kidogo ‘spirit’ ilimsaidia kupunguza kuvuja kwa damu ingawa maumivu
yaliendelea kuwa makali kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Akakata

18
kipande kikubwa cha pamba na kukiweka juu ya kidonda hicho huku akiendelea
kuugulia maumivu, akameza vidonge vya kupunguza maumivu huku akiendelea
kujiuliza maswali yaliyokosa majibu.
Aliporudi kitandani, aligundua kuwa shuka safi alilolitoa muda mfupi uliopita,
lilikuwa limeingia madoa makubwa kutokana na damu iliyokuwa inamvuja,
akapata kazi nyingine ya kuanza kubadilisha mashuka. Kila kilichokuwa
kinaendelea, alikifananisha na ndoto ya kutisha, akawa anatamani ndoto hiyo ifike
mwisho haraka lakini haikuwa hivyo.
Muda mfupi baadaye, pamba aliyokuwa amejiweka juu ya jeraha lake, ilikuwa
imelowa damu chapachapa, ikabidi aitoe na kukata nyingine, akaiweka huku bado
akiwa haamini kilichokuwa kinatokea.
“Kwani Samantha ni nani hasa? Kwa nini ameniumiza hivi na kukimbia? Kosa
langu kwake ni lipi? Ina maana haya ndiyo malipo ya wema wangu kwake?”
Edmund aliendelea kujiuliza huku akifuta damu iliyochafua vitu mbalimbali ndani
ya chumba chake.
Alitoka mpaka nje na kupatazama pale msichana huyo alipokuwa amepaki gari
lake. Hakuwepo wala hapakuwa na dalili zozote za uwepo wake, akarudi ndani na
kufunga mlango mkubwa wa nje, akachukua simu yake na kujaribu kumpigia
Samantha, mara simu ikaanza kuita.
“Haloo!” Haloo! Samantha! Samantha!” Edmund aliita baada ya simu kupokelewa
lakini hakuitikiwa, akaendelea kuita lakini hakusikia majibu yoyote, akakata simu
na kujaribu kupiga tena.
“Namba ya simu unayopiga haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadaye,”
sauti ilisikika kwenye simu yake ikimaanisha kwamba simu ya Samantha
imezimwa. Akazidi kujikuta kwenye wakati mgumu.
Alipotazama saa ya ukutani, aligundua kuwa tayari ilishatimia saa sita za usiku.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kwenda
kulala, huku akiendelea kuugulia maumivu makali.
***
“Mbona umechelewa kurudi? Ulikuwa wapi?”
“Kuna sehemu nilikuwa nimepitia.”
“Ndiyo uchelewe mpaka muda huu?”

19
“Nilikuwa nafanya kazi ya muhimu baba.”
“Kazi gani ya muhimu? Hivi siku hizi umekumbwa na nini wewe mtoto?
Majukumu ninayokupa hutimizi kila siku visingizo.”
“Baba! Hivi unafikiri hizo kazi zako unazonipa ni rahisi sana, si ndiyo? Kwanza
kwa taarifa yako mimi nimechoka, sitaki kuendelea kuwa mtumwa?” Samantha
alisema kwa sauti ya juu wakati akijibizana na baba yake.
“Unasemaje? Hebu rudia tena?”
“Jamani kwani kuna nini tena?” mama yake Samantha aliingilia ugomvi huo kati
ya baba na mwanaye, Samantha alipomuona mama yake akamkimbilia na
kumkumbatia huku akiendelea kulia.
“Kwani kuna nini mwanangu?”
“Eti baba ananifokea kisa nimechelewa kurudi wakati nilikuwa kufanya kazi
aliyonipa mwenyewe, kwanza mama mimi nimechoka kuendelea kuwa mtumwa,
sitaki,” alisema Samantha huku akijitoa kwenye mikono ya mama yake,
akakimbilia ndani na kuwaacha wazazi wake wakitazamana.
“Na wewe mume wangu, kwa nini unamfokea Samantha? Unafikiri huyo bado ni
mtoto mdogo?”
“Amekuwa jeuri sana siku hizi, kazi hafanyi kama ninavyomuelekeza kila siku
visingizio kibao, na leo umemsikia mwenyewe anasema amechoka. Sasa unafikiri
itakuwaje?”
“Huenda ameongea kwa hasira tu mume wangu, tumuache atulie kwanza,” alisema
mama yake Samantha, akamuita dereva wao na kumuamuru alipaki vizuri gari
alilokuja nalo Samantha, harakaharaka dereva huyo akatii alichoambiwa,
akaliingiza gari hilo kwenye maegesho kulikokuwa na magari mengine ya kifahari.
“Nisamehe Edmund! Nisamehe jamani, halikuwa kusudi langu kukufanyia hivyo,
naomba sana unisamehe kwani hukustahili kulipwa ubaya,“ alisema Samantha
huku akilia kwa uchungu, akiwa amejifungia chumbani kwake.

20
SURA YA TATU

Hakukumbuka hata kubadilisha nguo, akawa anajigalagaza kitandani huku akiwa


amekumbatia mto wake, machozi mengi yakiendelea kumtoka. Alikuwa anajua ni
jambo gani litakalomtokea Edmund, akawa anajisikia vibaya mno ndani ya moyo
wake. Hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kufanya kazi hiyo lakini hata yeye
alijishangaa kumuona huruma Edmund kiasi hicho, akawa anaendelea kulia kwa
kwikwi.
***
Muda ulizidi kuyoyoma, Edmund akiendelea kuugulia maumivu makali mno.
Usingizi ulimpaa kabisa, kwa mbali akaanza kuhisi mwili wake ukimchemka
kuashiria kwamba tayari alishapata homa.
Kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo homa hiyo ilivyokuwa
inazidi kuwa kali, akawa anatetemeka kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi.
Mpaka inafika alfajiri, Edmund alikuwa hoi mithili ya mtu aliyeugua kwa muda wa
wiki nzima mfululizo.
Kwa kuwa alikuwa anaishi peke yake, alijua endapo akiendelea kujilegeza,
anaweza kufia chumbani humo bila msaada, akajikongoja na kuamka mpaka
mlangoni, akafanikiwa kufungua mlango lakini kabla hajatoka nje, alianza
kutapika mfululizo mpaka akaishiwa nguvu. Kilichozidi kumtia hofu, ni pale
alipogundua kuwa kumbe alikuwa anatapika damu.
Akajikongoja mpaka kwenye mlango wa chumba cha jirani, akamgongea mpangaji
mwenzake aliyeamka haraka kutaka kujua kulikoni agongewe mlango alfajiri hiyo.
“Edmund?!!” aliita jirani huyo huku akionesha kushtushwa mno na hali aliyokuwa
nayo kijana huyo.
“Ni...sa..idie na...ku...” Edmund alishindwa kumalizia kauli yake, akaanza tena
kutapika damu mfululizo na muda mfupi baadaye, akadondoka chini kama mzigo,
puuh!
Akapoteza fahamu, jambo lililosababisha jirani yake arudi ndani haraka
kubadilisha nguo kwani alikuwa amejifunga taulo tu, akatoka na kuanza
kuwaamsha majirani wengine kwa lengo la kumsaidia Edmund ambaye mpaka
muda huo hakuwa na fahamu.

21
“Kwani kumetokea nini?” baba mwenye nyumba aliuliza lakini hakuna aliyekuwa
na majibu.
“Amekuja kunigongea mlango, nilipotoka nimemkuta kwenye hali mbaya mno
akitapika damu na muda mfupi baadaye ndiyo akadondoka na kupoteza fahamu,”
alisema yule jirani aliyekuwa wa kwanza kumuona Edmund.
“Kwa hiyo tufanye nini jamani?”
“Tumkimbize hospitali, hali yake inaonesha siyo nzuri kabisa, anaweza kupoteza
maisha huku tukishuhudia,” baba mwenye nyumba na wapangaji wake
walikubaliana, alfajiri hiyohiyo pilikapilika zikaanza.
Kwa kuwa kulikuwa na mpangaji aliyekuwa akifanya kazi ya udereva wa teksi na
alikuwa akilala na gari la bosi wake hapohapo nyumbani, ilibidi teksi hiyo ndiyo
itumike.
Wakasaidiana kumbeba Edmund na kumpakiza kwenye teksi hiyo, muda mfupi
baadaye, tayari walishaondoka, dereva akawa anajitahidi kukanyaga mafuta kwa
kasi ili kumuwahisha hospitalini.
Kwa bahati nzuri, alfajiri hiyo hakukuwa na foleni, dakika kadhaa baadaye
wakawa tayari wameshawasili kwenye Hospitali ya Mwananyamala, akapokelewa
na wahudumu waliokuwa zamu na kumlaza juu ya kitanda chenye magurudumu,
harakaharaka akakimbizwa wodini.
“Amepatwa na nini?” aliuliza daktari kwa mshangao baada ya kuona hali
isiyokuwa ya kawaida kwenye mwili wa Edmund.
“Hata hatuelewi, tumeshtukia akianguka na kupoteza fahamu.”
“Mungu wangu! Hebu nipisheni kwanza, tokeni nje,” alisema daktari huku akiinua
simu ya mezani iliyokuwa ndani ya wodi hiyo na kupiga namba fulani, wale
wapangaji wenzake Edmund na baba mwenye nyumba wakatoka huku nao
wakiendelea kuulizana maswali yaliyokosa majibu. Mshtuko aliouonesha daktari
ulizidi kuwachanganya, wakawa wanasubiri miujiza tu kwani kwa hali aliyokuwa
nayo Edmund, chochote kingeweza kutokea.
Muda mfupi baadaye, madaktari wengine wawili waliingia harakaharaka kwenye
wodi aliyokuwa ameingizwa Edmund, wakasogea na kukizunguka kitanda
alichokuwa amelazwa huku wakimtazama daktari mwenzao aliyewaita.

22
“Kuna huyu mgonjwa ameletwa lakini hali yake inashangaza sana, inaonesha kama
ameng’atwa na nyoka au mdudu mwenye sumu kali lakini ukiangalia jeraha jinsi
lilivyo, halifanani na jeraha la kung’atwa na nyoka.”
“Mh! Mbona anabadilika rangi na kuwa mweusi kama mkaa?”
“Halafu mbona mishipa yake ya damu mwili mzima imevimba kiasi hiki?”
“Tangu nianze kazi sijawahi kukutana na hali kama hii, mpaka naogopa,” alisema
daktari yule, kila mmoja akawa amepigwa na butwaa, hakuna aliyekuwa anajua
waanzie wapi kumtibu.
“Mapigo yake ya moyo yapo chini sana na kadiri muda unavyozidi kwenda mbele
ndivyo yanavyozidi kushuka,” alisema daktari aliyekuwa anampima Edmund
kifuani kwa kutumia kifaa maalum cha kupimia mapigo ya moyo kiitwacho
Stethoscope.
“Atundikiwe dripu za maji kwanza wakati tukiendelea kuchunguza ni sumu ya aina
gani iliyopo kwenye damu yake,” alisema mwingine, wazo lililoungwa mkono na
wenzake.
Edmund ambaye bado hakuwa na fahamu akatundikiwa dripu lakini kilichozidi
kuwashangaza madaktari hao, dripu ilikuwa ikitiririka kwa kasi kubwa kuingia
kwenye mishipa yake, hali iliyoashiria alikuwa na upungufu mkubwa mno wa
maji.
Dakika chache tu baadaye, tayari dripu ya kwanza ilikuwa imeisha, ikabidi
atundikiwe nyingine ambayo nayo licha ya madaktari hao kujaribu kuiseti
kitaalamu, iliendelea kutiririka kwa kasi kubwa mno, kila mmoja akazidi kupigwa
na butwaa huku hofu ikianza kuingia ndani ya moyo wa kila mmoja kwani
kulikuwa na dalili zote kwamba ugonjwa aliokuwa nao Edmund, haukuwa wa
kawaida.
***
Samantha aliendelea kulia kwa kwikwi chumbani kwake, akiwa amejifungia
mlango kwa ndani huku akijilaumu sana kwa kitendo alichomfanyia Edmund.
Alikuwa anajua fika nini kitakachomtokea baada ya saa chache kupita, hata hivyo
hakuwa na cha kufanya. Alitamani muda urudi nyuma ili arekebishe makosa
aliyoyafanya lakini hilo halikuwezekana.

23
“Hustahili Edmund, wewe ni mwanaume wa kipekee, hustahili kabisa mateso ya
kiasi hicho,” alisema msichana huyo huku akiendelea kulia. Alipotazama saa ya
ukutani, tayari ilikuwa imefika saa kumi za usiku lakini hakuwa amepata hata lepe
la usingizi, macho yake yakiwa yamevimba na kuwa mekundu sana kutokana na
kulia kwa muda mrefu.
Ghafla, akiwani kama aliyekumbuka kitu muhimu, Samantha alikurupuka pale
kitandani kwake. Kwa kuwa hakuwa amebadilisha nguo alizokuwa amevaa siku
iliyopita, alichukua viatu vyake na kuvishika mkononi kwani hakutaka mtu yeyote
amsikie.
Akafungua mlango na kunyata kwenye korido ndefu mpaka sebuleni, akafungua
kwenye droo zilipokuwa zinawekwa funguo za magari, akachukua funguo ya gari
analopenda kutembelea, Jeep Grand Cherokee (New Model) na kunyata kuelekea
kwenye mlango wa kutokea.
Alipofika mlangoni, aliingiza namba maalum za kufungulia mlango kisha
akafungua na funguo, akatoka nje na kuangaza huku na kule.
“Vipi dada mbona mapema namna hii?” mlinzi aliyekuwa na bunduki, akiwa
amevalia sare maalum, alimuuliza kwa mshangao kwani haikuwa kawaida ya
Samantha kutoka nyumbani muda huo.
“Shhh! Njoo nikwambie,” alisema Samantha na kumvutia mlinzi huyo karibu
yake, akamdanganya kwamba amepatwa na dharura na ni lazima aondoke alfajiri
hiyo lakini hataki baba yake au mama yake ajue chochote.
Mlinzi akawa anatingisha kichwa kuashiria kumuelewa, akaingiza mkono kwenye
pochi yake na kumtolea noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi, harakaharaka
mlinzi akaenda kufungua geti, Samantha akaingia ndani ya gari lake na kuliwasha
kisha akatoka kwa kasi kubwa, akaingia barabarani na kutokomea gizani,
akamuacha mlinzi akihangaika kufunga geti.
“Sijui kama nitamuwahi kabla hali haijawa mbaya,” alisema Samantha huku
akitazama saa yake ya mkononi, gari likikimbia kwa kasi kubwa ajabu. Bahati
nzuri asubuhi hiyo hakukuwa na magari mengi barabarani kwani kwa mwendo
aliokuwa akiendesha, ingekuwa rahisi mno kusababisha ajali.
Hakuwa akijali chochote barabarani, hata sehemu zenye matuta au kona kali
alikuwa akipita bila kupunguza mwendo, dakika chache baadaye, tayari aliwasili

24
nyumbani kwa Edmund. Akapaki gari palepale alipopaki usiku uliopita na
kutembea harakaharaka kuelekea kwenye chumba cha Edmund.
Mazingira aliyoyakuta yalizidi kumchanganya kwani alikuta mlango ukiwa wazi
huku matapishi ya damu yakiwa yametapakaa kila sehemu. Kwa bahati nzuri,
alimkuta mama mwenye nyumba akiwa nje, akiwaandaa wanaye kwa ajili ya
kwenda shule. Alipomuuliza, mwanamke huyo alimueleza kwamba Edmund
amekimbizwa Mwananyamala baada ya kuzidiwa ghafla.
Bila hata kuaga, alikimbilia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi kubwa mithili
ya madereva wa mbio za magari. Dakika kumi baadaye, tayari alikuwa amewasili
Hospitali ya Mwananyamala, akateremka kwenye gari na kuanza kutembea
harakaharaka kama aliyechanganyikiwa mpaka mapokezi.
“Samahani nesi naomba kuuliza,” alisema Samantha huku akihema mithili ya
mwanariadha aliyetoka kukimbia mbio za mita mia moja. Japokuwa ilikuwa ni
alfajiri na kulikuwa na kiubaridi cha asubuhi, Samantha alikuwa akitokwa jasho,
jambo lililomshangaza yule nesi aliyekuwa pale mapokezi.
“Kuna mgonjwa anaitwa Edmund, eti ameletwa hapa alfajiri hii?”
“Mh! Kuna mgonjwa mmoja tu aliyeletwa alfajiri hii, ngoja niangalie jina lake,”
alisema nesi huyo huku akipekua kwenye daftari kubwa la usajili wa wagonjwa
wanaoingia hospitalini hapo.
“Ndiyo! Amepelekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi, hali yake ni mbaya
sana na madaktari wote wameelekea huko kumsaidia,” alisema nesi huyo, majibu
yaliyozidi kumpandisha Samantha presha.
“Samahani sana nesi, niko chini ya miguu yako, naomba uniruhusu nikamuone.”
“Dada! Mgonjwa ndiyo kwanza ameletwa na amepelekwa wodi ya wagonjwa
mahututi, unataka ukamuone ili iweje? Hakuna anayeweza kukuruhusu, waache
madaktari wafanye kazi yao,” alisema nesi huyo huku akifunika daftari hilo na
kuendelea na shughuli nyingine.
Samantha akaona asipotumia nguvu za ziada, kweli Edmund anaweza kupoteza
maisha muda wowote kwani mapambazuko yalikuwa yamekaribia sana na endapo
asingefanya jambo mpaka jua litakapochomoza, tafsiri yake ni kwamba huo ndiyo
ungekuwa mwisho wa Edmund, jambo ambalo hakutaka kuona likitokea.

25
Harakaharaka akaingiza mkono kwenye sidiria yake na kutoa noti tatu za shilingi
elfu kumikumi, akampa yule nesi na kumtaka amuoneshe wodi ya wagonjwa
mahututi ilipo.
“Lakini madaktari hawatakuruhusu.”
“We nioneshe nikifika nitajua mwenyewe,” alisema Samantha huku akiendelea
kuhema kwa nguvu. Nesi akazisunda zile fedha kwenye mfuko wa gauni lake
jeupe na kuinuka, akamuelekeza Samantha sehemu ilipo wodi hiyo.
Harakaharaka akawa anatembea kuelekea wodini, hakuwajali watu kadhaa
aliowapita kwenye korido ya kuelekea kwenye wodi hiyo, akapita kwa kasi na
kuelekea mpaka kwenye mlango, akaanza kugonga kwa nguvu.
***
Dakika chache baadaye, dripu ya pili aliyokuwa ametundikiwa Edmund pale
kitandani nayo iliisha, ikabidi atundikiwe dripu ya tatu huku hali yake ikazidi kuwa
tete. Bado madaktari hao hawakuwa wanajua wafanye nini.
Wakati dripu ikiendelea kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake, majibu
ya damu tayari yalishatoka, madaktari wote wakawa wanayajadili kwani licha ya
kuonesha kwamba damu ya Edmund ilikuwa na sumu kali, vipimo vilishindwa
kuonesha ni sumu ya aina gani, jambo lililosababisha wasijue dawa sahihi ya
kuitumia.
“Why can’t we use trial and error method?” (Kwa nini tusitumie njia ya kujaribu
na kujifunza kupitia makosa?) alisema daktari mmoja, wazo lililokubaliwa na
wenzake wote.
Harakaharaka daktari aliyekuwa anahusika na kitengo hicho akatoa orodha ya
dawa zinazotumika kutibu watu walioumwa na nyoka na kwa pamoja
wakakubaliana kuanza kutumia dawa ya Polyvalent Anti–Snake Venom Serum
ambayo ilikuwa na uwezo wa kupambana na sumu kali zaidi.
Hata hivyo, wakati dawa hiyo ikiendelea kuandaliwa, Edmund alianza kuonesha
dalili zilizozidi kuwachanganya madaktari wote mle wodini.
Alianza kutapatapa, akirusha mikono na miguu kama anayekaribia kukata roho
huku akitokwa na povu lililochanganyikana na damu puani na mdomoni, jambo
lililoashiria kwamba tayari sumu iliyokuwa ndani ya mwili wake ilishafika kwenye
moyo.

26
Kifaa maalum cha kumsaidia kupumua alichokuwa amevalishwa puani na
kuunganishwa na kompyuta, kilianza kupiga kelele kwa nguvu kuashiria kwamba
mapigo ya moyo ya Edmund yalikuwa yakishuka kwa kasi na hakuwa tena na
uwezo wa kupumua.
Wakati madaktari wakiwa wanahangaika kumsaidia, walishtuka baada ya kusikia
mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi waliyokuwa ndani yake, ukigongwa kwa
nguvu, jambo ambalo halikuwa la kawaida. Walimpuuza aliyekuwa anagonga,
wakaendelea na kazi ya kumhangaikia Edmund ambaye dalili zote zilionesha
kwamba yupo kwenye hatua za mwisho kabisa za uhai wake.
Walipoona mtu huyo anazidi kugonga, ilibidi mmoja wao aache kazi na kwenda
kufungua.
“Unasemaje binti?” aliuliza daktari aliyefungua mlango lakini cha ajabu, Samantha
alimpiga kikumbo na kusababisha mlango wote ufunguke, kufumba na kufumbua
tayari Samantha alikuwa ndani ya wodi hiyo.
“Ninayo dawa ya kumsaidia kupona! Naomba mniamini! Ninayo dawa,” alisema
Samantha huku akihema kwa nguvu, mikono yake akiwa ameiinua juu kama ishara
ya kuonesha kwamba hakuwa na lengo baya.
Tayari yule daktari aliyempiga kikumbo alishamsogelea na kutaka kumtoa kwa
nguvu lakini alipoendelea kusisitiza kwamba alikuwa na dawa ya kumsaidia
mgonjwa huyo aliyekuwa kwenye hatua za mwisho za uhai wake, madaktari
walitazamana kwa sekunde chache kisha wakapeana ishara ya kumruhusu
awasaidie kwani nao walishaonesha kushindwa.
Aliporuhusiwa tu, harakaharaka alisogea mpaka kwenye kitanda alichokuwa
amelazwa Edmund ambaye bado alikuwa akiendelea kutapatapa, akamchomoa
mpira wa kumsaidia kupumua aliokuwa amevalishwa puani na mdomoni kisha
kwa kasi ya ajabu akaanza kumpuliza mdomoni.
Aliendelea kumpuliza kwa nguvu, baada ya takribani sekunde thelathini za
kufanya hivyo, Edmund aliacha kutapatapa, akaendelea kumpuliza na katika hali
ambayo hakuna aliyeitegemea, mapigo ya moyo wake yalianza kupanda.
Yalipofika katika kiwango ambacho Samantha aliona kinafaa, aliacha kumpuliza
na kumvalisha tena ile mashine ya kupumulia, akamgeuza kidogo ili apate nafasi
ya kuiona vyema shingo yake.

27
Muda mfupi baadaye, aliliona jeraha alilomsababishia kijana huyo shingoni muda
aliojifanya anamtoa ‘love bite’. Harakahaharaka akapeleka mdomo wake eneo hilo
na kuanza kulinyonya jeraha la Edmund kwa nguvu, madaktari wakawa
wanashangaa wakiwa hawaamini walichokuwa wanakiona. Urembo wa Samantha
na alichokuwa anakifanya, vilikuwa vitu viwili tofauti.
Mara Samantha akasimama huku mdomo wake ukionesha kujaa, akachukua
kikarai kidogo kilichokuwa pembeni na kutema kile kilichokuwa mdomoni
mwake, madaktari wakashtuka mno. Ilikuwa ni damu ambayo ilibadilika rangi na
kuwa nyeusi kutokana na sumu iliyokuwa imeingia ndani ya mwili wa Edmund.
Akarudi tena kwenye shingo ya Edmund na kuendelea kumnyonya kisha akaenda
tena kutema kwenye kile kikarai, aliendelea kufanya hivyo mfululizo, nguo
alizokuwa amevaa zikachafuka vibaya kwa damu lakini mwenyewe hakujali.
Kadiri alivyokuwa anaivuta sumu hiyo kwa mdomo, ndivyo Edmund alivyokuwa
anazidi kubadilika, ile mishipa ambayo ilikuwa imevimba kama inataka kupasuka,
ikaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida, ngozi yake ambayo ilikuwa nyeusi
kama mkaa, nayo ilianza kubadilika rangi na kurudi kwenye hali yake ya kawaida,
madaktari wakawa bado wanashangaa, kila mmoja akijihisi yupo kwenye ndoto.
Samantha aliendelea kufanya hivyo mpaka kile kikarai kikakaribia kujaa, tayari nje
kulishaanza kupambazuka, lile giza la alfajiri likawa linafifia taratibu na kumezwa
na mwanga wa jua lililoanza kuchomoza kwa mbali.
“Endeleeni na kazi yenu lakini msimwambie yeyote juu ya hiki nilichokifanya,
nitakuja baadaye kumuona,” alisema Samantha huku akiwaelekeza madaktari hao
kukisafisha vizuri kidonda kilichokuwa kwenye shingo ya Edmund.
Akachukua kile kikarai kilichokuwa na damu iliyochanganyikana na sumu mpaka
nje, akainamisha uso wake ili mtu yeyote asimuone sura yake na kuondoka
harakaharaka eneo hilo mpaka kwenye gari lake ambapo alichukua chupa
iliyokuwa na maji, akayamwaga na kumimina ile damu yote.
Kama alivyoingia hospitalini hapo, alitoka kwa kasi kubwa akiwa ndani ya gari
lake la kifahari, dakika chache baadaye, tayari alishatoka nje ya uzio wa hospitali
hiyo, akawa anakanyaga mafuta kwa nguvu huku akishusha pumzi ndefundefu.
“Ni lazima nikulinde Edmund, sijali kitakachonipata kutoka kwa baba yangu,
nahisi kukupenda sana kutoka ndani ya moyo wangu,” aliwaza Samantha huku
akiendelea kukanyaga mafuta.

28
Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa amewasili kwenye jumba lao la kifahari,
hakutaka kupiga honi ili mlinzi afungue geti kama kawaida yake kwani alihisi baba
yake atasikia, akapaki gari pembeni ya geti na kushuka, akabonyeza kengele ya
mlango mdogo wa geti. Sekunde chache baadaye, tayari mlinzi alishafungua
mlango.
“Mungu wangu! Umefanya nini mbona umelowa damu kiasi hicho?” mlinzi alihoji
huku akionesha kupatwa na mshtuko mkubwa mno. Hakujua atamjibu nini bosi
wake kwa kumruhusu Samantha atoke halafu arejee akiwa kwenye hali kama hiyo.
“Sijaumia popote wala usiwe na wasiwasi, baba aliniulizia?”
“Kweli hujaumia? Na hizo damu zimetoka wapi?” mlinzi alisema huku akimgeuza
Samantha kwa hofu.
“Niamini mimi, hapa nikienda kubadilisha nguo hakuna atakayejua chochote.
Nakuuliza baba hajaniulizia?”
“Ulipotoka alisikia muungurumo wa gari, akaamka na kuja kuniuliza kwa nini
nimekufungulia geti wakati bado hakujapambazuka, nikamwambia umepatwa na
dharura. Amekasirika sana, bado kidogo aninase vibao,” alisema mlinzi huyo,
kauli iliyomfanya Samantha aanze kutetemeka.
Alikuwa akimfahamu vyema baba yake alivyo mkali, akajua lazima moto utawaka.
Hata hivyo, kwa sababu alishajiapiza kumlinda Edmund, alipiga moyo konde na
kuingia ndani, akatembea harakaharaka mpaka kwenye mlango wa kuingilia ndani,
akaingiza namba maalum kisha mlango huo ukafunguka.
Akavua viatu vyake na kuvishika, akawa ananyata kuelekea chumbani kwake huku
hofu ikiwa imeutawala moyo wake.
“Umetoka wapi?” sauti kali ya baba yake ilimshtua mno Samantha, akajikuta viatu
vikimponyoka mikononi na kuanguka chini. Hakutegemea kama baba yake
anaweza kuwa sebuleni muda kama huo, akabaki anatetemeka.
“Nazungumza na wewe, umetoka wapi? Halafu mbona uko hivyo?”
“Ni..me..toka ku..fanya ka..zi uliyonituma,” alisema Samantha huku akitetemeka,
tayari baba yake alishamsogelea, akawa anamtazama machoni kwa umakini.
“Kazi gani muda huu.”

29
“Ya kafara ya da...mu ba..ba,” Samantha alisema uongo ambao baba yake
aliushtukia mapema.
“Tangu lini kafara ikafanyika alfajiri? Halafu mbona unaonesha kuwa na wasiwasi
kiasi hicho? Unanidanganya si ndiyo?”
“Hapana baba, ni kweli,” alisema Samantha, mzee huyo akaendelea kumbana na
kumwambia asijaribu kumdanganya kwa sababu anaujua ukweli wa kila kitu
alichokifanya, kauli iliyomshtua sana Samantha.
“Jana kuna kijana tulikuandalia mazingira ya kukutana naye, kila kitu kikaenda
vizuri mpaka usiku ulipotimiza kazi yako lakini ghafla ukabadilisha mawazo kwa
sababu ya mapenzi. Umenisikitisha sana mwanangu! Unafikiri sijui kwamba
umetoka Hospitali ya Mwananyamala kumsaidia huyo kenge mwenzio?
“Ni mwezi wa pili sasa unaisha hujafanya kazi hata mara moja. Jana tumetumia
nguvu kubwa kukutengenezea mazingira lakini matokeo yake umetanguliza
udhaifu mbele. Hujui kwamba mapenzi ni udhaifu? Unataka huu utajiri wetu
uishe? Kwa nini unavunja masharti? Unaijua hatari ambayo iko mbele yetu kwa
ujinga unaoufanya?”
“Lakini baba...”
“Lakini nini? Sasa kwa taarifa yako, mimi siwezi kukubali ujinga unaoufanya
unigharimu, kama umeshindwa kufanya kazi itabidi wewe ndiyo utolewe kafara,
hujui ni kwa namna gani nimekupigania mpaka hapo ulipofika? Nitakuua.
“Nakupa saa 24 ya kwenda kumuua huyo mshenzi anayekufanya uvunje masharti
vinginevyo damu yako ni halali yangu,” alisema mzee huyo kwa ukali kisha
akageuka na kutembea kwa kasi kuelekea chumbani kwake, akamuacha Samantha
amepigwa na butwaa akiwa ni kama haamini alichokisikia kutoka kwa baba yake.

30
SURA YA NNE

Kwa jinsi alivyokuwa anamfahamu, alijua endapo hatafanya jambo haraka,


anaweza kwenda kummalizia Edmund mwenyewe kule hospitalini kwani nguvu za
giza alizokuwa nazo zilikuwa zinaweza kumfanya akajua kila kitu kinachoendelea
na kuamua nini cha kufanya.
“Na akigundua kwamba nimeshamtoa sumu mwilini, anaweza kweli kuniua na
mimi kama alivyofanya kwa kaka Samuel,” aliwaza Samantha akiwa bado
amesimama palepale koridoni, kijasho chembamba kikimtoka.
Japokuwa alikuwa anapenda maisha ya kifahari waliyokuwa wanaishi kama wapo
peponi, Samantha alikuwa hakubaliani kabisa na mchezo wa baba yake wa
kuwatoa kafara watu wasio na hatia, wakati mwingine hata ndugu zake wa damu
wakiwemo watoto wake wa kuwazaa ili kulinda utajiri wake mkubwa.
Mara kwa mara alijaribu kujitoa kwenye mtego huo lakini alikuwa akishindwa
kwani baba yake alikuwa akijua kila kitu anachokifanya au anachokaribia
kukifanya na kumkwamisha.
“Lazima nikuokoe Edmund, hata kama itanigharimu maisha yangu, nimechoshwa
na maisha haya,” alijisemea Samantha na kutembea harakaharaka kuelekea
chumbani kwake. Hakutaka kupoteza muda, harakaharaka alivua zile nguo na
kukimbilia bafuni, akaoga kisha akarudi na kuvaa baibui na nikabu iliyouficha
kabisa uso wake na kuyaachia macho tu.
Akatoka na zile nguo zilizokuwa zimelowa damu na kwenda kuzitupa kwenye pipa
la takataka nje. Harakaharaka akatoka mpaka nje na kumuacha mlinzi akitingisha
kichwa chake kwa masikitiko. Sekunde chache baadaye, muungurumo wa gari
ulisikika nje ya geti na Samantha akaondoka kwa kasi akiwa ndani ya gari lake.
Tayari kulishapambazuka, barabarani kukawa na watu na magari mengi, hali
iliyomzuia Samantha kuendesha kwa kasi kama ilivyokuwa awali.
Baada ya kuhangaika sana, alifika Hospitali ya Mwananyamala akiwa amevaa
vilevile, akapita mpaka mapokezi ambapo ilibidi avue nikabu, yule nesi aliyemkuta
akamkumbuka kwani muda mfupi uliopita walikuwa pamoja.

31
“Nina shida nyingine dadaangu, nataka mgonjwa wangu ahamishwe hospitali, kwa
jinsi hali yake ilivyo anahitaji huduma bora zaidi kwa hiyo nataka kumpeleka
hospitali ya kulipia,” Samantha alidanganya.
“Inabidi ukazungumze na madaktari wanaomtibu,” alisema yule nesi na kumsaidia
kupita hadi wodini ambako aliwakuta madaktari wakiwa wameshamsafisha
Edmund kidonda na kumfunga vizuri.
Akazungumza nao kuhusu mpango wake ambapo walimkubalia, akaandikiwa
barua ya rufaa na kusaidiwa kumtoa mgonjwa wodini, akiwa bado hajitambui.
Samantha alikuwa akishinikiza kila kitu kifanyike harakaharaka kwani alijua muda
wowote baba yake anaweza kufika hospitalini hapo na kuvuruga kila kitu.
“Ambulance imepeleka wagonjwa wengine Muhimbili, inabidi usubiri.”
“Hapana, sihitaji ambulance, nimekuja na gari langu,” alisema Samantha huku
akivaa tena ile nikabu yake na kuuficha uso wake, manesi na madaktari
wakasaidiana kumpakiza mgonjwa kwenye gari kisha baada ya hapo daktari mkuu
akataka manesi wawili waongozane naye lakini Samantha alikataa, jambo
lililowashangaza wote.
Harakaharaka akaingia kwenye gari na kupiga ‘starter’ kisha akawasha taa za
mbele za gari hilo, akaondoka kwa kasi mpaka getini. Akiwa anataka kutoka na
kuingia barabarani, alishtuka baada ya kuliona gari la baba yake nalo likiwa
linakata kona ya kuingia hospitalini hapo.
“Mungu wangu!” alisema Samantha kwa hofu kubwa.
Harakaharaka msichana huyo alipandisha vioo vya gari lake, akamuona baba yake
akivua miwani na kulikodolea macho gari hilo akiwa ni kama haamini. Akaingia
barabarani na kukanyaga mafuta kwa nguvu, gari likawa linakimbia kwa kasi
kubwa.
“Dereva hebu geuza gari mara moja, lile gari siyo analoendesha mwanangu
Samantha?” alisema baba yake Samantha baada ya gari alilokuwa akiliendesha
Samantha kuwapita kwa kasi pale getini wakati wakitaka kuingia Hospitali ya
Mwananyamala.
Harakahara dereva akaanza kuhangaika kugeuza gari na kusababisha madereva
wenzake wawe wanampigia honi kwa fujo kwani alikuwa akisababisha foleni.
Hatimaye akafanikiwa kugeuza na kuelekea kule lile gari lilikoelekea huku baba
yake Samantha akimsisitiza kuongeza mwendo.

32
Kwa mbali wakawa wanaliona gari hilo ambapo walipotazama namba waligundua
kuwa ndiyo lenyewe, mzee huyo akawa anamhimiza dereva kuhakikisha
anaongeza kasi mpaka alifikie.
***
Samantha akiwa anakanyaga mafuta na kusababisha gari liwe linaenda kwa kasi
kubwa, alishtuka zaidi baada ya kuona gari la baba yake nalo likigeuza na kuanza
kumfuata kwa nyuma. Akazidi kuchanganyikiwa, akawa anaendelea kuendesha
gari kwa kasi huku akitazama nyuma kwa kupitia vioo vya pembeni, akaona gari la
baba yake likizidi kuongeza kasi, hofu ikazidi kumjaa.
Japokuwa barabara ilikuwa na magari mengi, Samantha alizidi kuongeza kasi,
akawa anazipita daladala kwa namna ambayo ilikuwa rahisi sana kusababisha ajali,
muda mwingine akawa analazimika ‘kutanua’ na kutoka nje ya barabaraba,
madereva wengine wakawa wanapunguza mwendo ili kuepusha ajali.
Japokuwa kulikuwa na matuta makubwa kwenye eneo la Mwananyamala
Komakoma, Samantha aliyapita bila kupunguza mwendo hata kidogo na
kusababisha gari liruke juu na kuzua taharuki kwa watumiaji wengine wa barabara,
dakika chache baadaye akawa ameshapotea kabisa eneo hilo.
“Ongeza mwendo! Inawezekanaje akushinde wakati wewe umesomea udereva?
Nitakufukuza kazi.”
“Lakini mzee, hili gari lipo chini na huwezi kupita kwa kasi kwenye matuta haya
makubwa kama yeye alivyofanya, tutaharibu gari au tutapata ajali,” dereva
alijitetea lakini utetezi wake haukuwa na maana kwa mzee huyo ambaye tayari
kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka.
Akamlazimisha dereva kusimama haraka, akateremka na kukaa mwenyewe nyuma
ya usukani, akaondoa gari kwa kasi lakini tayari alishachelewa kwani Samantha
alishapotea kwenye upeo wa macho yao, walipofika eneo la Kinondoni Studio,
kwenye makutano ya Barabara za Mwananyamala na Kawawa, walishindwa
kuelewa kama Samantha ameelekea kulia au kushoto, wakajikuta wakikwama.
***
Baada ya kuendesha gari kwa kasi kubwa, akinusurika kupata ajali mbaya zaidi ya
mara nne, hatimaye Samantha aliwasili Mlingotini, Bagamoyo, nyumbani kwa
mzee Tenson Shiwinga, mganga wa baba yake ambaye alizoea kumuita babu.

33
Akafunga breki kali na kusababisha gari liseleleke na kutoa mlio uliomshtua Mzee
Shiwinga ambaye alikuwa ndani ya kibanda chake cha miti, udongo na makuti,
akatoka akiwa amejifunga shuka jekundu na kupigwa na butwaa kumuona
Samantha akishuka kwenye gari huku akihangaika kumteremsha mtu ambaye
ilionesha wazi alikuwa hajitambui.
“Babu nahitaji msaada wako, nisaidie niko chini ya miguu yako.”
“Samantha? Kuna nini tena mjukuu wangu? Baba amekutuma?”
“Hapana babu, nisaidie kwanza nitakueleza kilichotokea. Huyu ni mchumba
wangu nataka umsaidie kumtoa sumu, nimemng’ata kwa bahati mbaya, fanya kila
liwezekanalo akipona nakuahidi nitakupa zawadi kubwa sana,” alisema Samantha
huku machozi, jasho na kamasi vikimtoka kwa wakati mmoja.
Mzee Shiwinga alimtazama Samantha usoni na kugundua kuwa alikuwa analia,
akawa hana namna zaidi ya kumsaidia. Akamsaidia kumbeba mtu huyo ambapo
kutokana na jinsi mzee huyo alivyokuwa na nguvu licha ya umri wake mkubwa,
alimbeba kwenye mikono yake na kutembea naye haraka kuingia ndani ya kibanda
chake.
Samantha akawa anafuata kwa nyuma huku baibui aliyovaa akiiona kama mzigo,
alitamani aivue na kuitupa mbali lakini haikuwezekana, akawa anaendelea kulia
huku akimsisitiza mzee huyo kufanya kila linalowezekana kumsaidia kijana huyo.
Baada ya kumuingiza ndani ya kibanda chake kilichojaa matunguli, pembe, kwato,
mikia na ngozi za wanyama mbalimbali wa porini, mzee huyo alimlaza juu ya
ngozi ya chui aliyokuwa akiitumia kuwatibu wagonjwa wake, akachukua kibuyu
kimoja na kukitingisha kwa nguvu kisha akakifungua ambapo kilitoa gesi kama
soda inayofunguliwa.
Akanywa dawa zilizokuwa ndani yake kisha akaanza kumnywesha mgonjwa wake
kwa kutumia mdomo huku mkono mmoja akiutumia kufungua bandeji kwenye
jeraha la kung’atwa lililokuwa shingoni. Baada ya kumnywesha, alichukua kibuyu
kingine chenye dawa na kumwagia juu ya jeraha, akaanza kuliminyaminya huku
akitamka maneno ambayo Samantha hakuyaelewa.
Sekunde chache baadaye, mganga huyo alitoka mbio na aliporejea alikuwa na
majani kadhaa mkononi ambayo aliyatafuna harakaharaka na kuanza kumtemea
mwili mzima.
”Anaitwa nani?”

34
“Edmund!” alisema Samantha huku akijifuta machozi, mganga huyo akaanza
kulitaja jina la Edmund huku akichanganya na maneno mengine ambayo
hakuyaelewa, akaendelea kuchakarika, akitumia karibu vibuyu vyote vilivyokuwa
na dawa, muda mfupi baadaye, wote walishtuka baada ya kusikia Edmund akipiga
chafya mfululizo kisha akafumbua macho.
“Ooh! Edmund wangu jamani, siamini,” alisema Samantha na kuanza upya
kuangua kilio huku akimkumbatia Edmund kwa nguvu. Bado Edmund alikuwa
amepigwa na butwaa, akawa anashangaashangaa akiwa haelewi kinachoendelea.
“Sa...ma..ntha...” alisema kwa tabu huku akijaribu kuinuka lakini maumivu makali
shingoni yakamfanya arudi tena pale chini.
“Ni..ni kime..tokea? Ha..pa ni wa...pi?” alihoji Edmund huku akiendelea
kushangaa, maswali mengi yakipita ndani ya kichwa chake.
“Tupo kwa mganga Edmund, nisamehe kwa yote yaliyotokea, nitakueleza kila kitu
kilichotokea,” alisema Samantha huku akiendelea kulia, ikabidi mganga amsogeze
pembeni kwani bado alikuwa na kazi kubwa ya kuendelea kumhudumia, Samantha
akakubali kusogea pembeni lakini bado alikuwa akiendelea kulia kwa uchungu.
Mganga Shiwinga aliendelea kumfanyia dawa Edmund na baada ya takribani saa
mbili kupita, Edmund alikuwa na uwezo wa kuinuka mwenyewe na kukaa
japokuwa bado alikuwa akilalamikia maumivu makali.
“Una bahati sana kijana, tayari ulishafariki, ni kama muujiza tu! Umshukuru sana
Samantha kwani asingekuwahisha pengine tungekuwa tunaongea mengine hivi
sasa,” alisema Mganga Shiwinga wakati akiendelea kumkanda Edmund jeraha
lake.
“Samantha,” aliita Edmund, harakaharaka msichana huyo aliyekuwa amekaa juu
ya kiti cha miguu mitatu akiwa amejikunyata, aliinuka na kumsogelea Edmund,
akambusu kwenye paji la uso kisha akakaa juu ya ile ngozi aliyokuwa amekalia
Edmund.
“Unajisikiaje mpenzi wangu?”
“Bado shingo inauma, hebu niambie nini kimetokea? Halafu kwa nini jana
uliondoka ghafla nyumbani kwangu? Kwa nini uliniumiza shingoni kiasi hiki?
Kwa nini... mbona sielewi kinachoendelea? Na hapa nimefikaje? Kwa nini mganga
anasema nilikuwa nimeshakufa?” Edmund aliuliza maswali mengi mfululizo
akionesha kuchanganyikiwa kabisa.

35
Samantha alishusha pumzi ndefu na kumuomba mganga atoke na kuwapisha ili
wazungumze kwa uhuru zaidi, mganga Shiwinga akafanya kama alivyoombwa,
Samantha akashusha tena pumzi ndefu na kumtazama Edmund usoni.
“Naomba unisamehe sana kwa kilichotokea Edmund, halikuwa kusudio langu.
Najua itakuwa vigumu kuniamini lakini naomba uelewe kwamba nimelijua kosa
langu na nimeamua kukulinda kwa sababu naamini wewe ndiye utakayenitoa
kwenye hiki kifungo Edmund!
“Sijawahi kufurahia maisha hata mara moja, usinione niko hivi napata kila
ninachokitaka ukajua nina furaha, nateseka sana mwenzio! Nipo chini ya miguu
yako.
“Naomba uniahidi kwamba hata nikikuambia ukweli bado utaendelea kuwa nami
na kamwe hutaniacha, nakupenda Edmund,” alisema Samantha huku akilia kwa
uchungu mkubwa na kumlalia Edmund kifuani, machozi yakawa yanamtoka na
kutiririka kupitia kona za macho yake mpaka kwenye mwili wa Edmund.
Kwa jinsi msichana huyo alivyokuwa akilia kwa uchungu, kabla hata Edmund
hajajua anataka kumwambia nini, kitendo cha kushtuka na kujikuta nyumbani kwa
mganga wa kienyeji huku msichana huyo akiwa pembeni yake, kilimfanya aamini
kwamba hawezi kuwa na nia mbaya naye.
Kwa taabu alinyanyua mkono wake mmoja na kumshika Samantha mgongoni,
akampigapiga kama ishara ya kumbembeleza na kumwambia yupo tayari
kumsikiliza na atakuwa naye kwa hali zote. Kauli hiyo ilimfurahisha mno
Samantha, akambusu Edmund mdomoni na kuanza kumueleza kilichotokea.
Akamwambia kwamba baba yake anamiliki utajiri mkubwa lakini kwa njia zisizo
halali na kwamba kwa kipindi chote cha maisha yake tangu azaliwe, Samantha
ndiyo kichocheo cha utajiri huo.
“Sijakuelewa unamaanisha nini,” Edmund alimkatisha Samantha, ikabidi aanze
kumfafanulia kila kitu kwa kina.
Akamueleza kwamba wazazi wake wamepata utajiri walionao kwa njia za
kishirikina na kwamba walikuwa wakiwachukua watu misukule na wengine
kuwatoa kafara kwa kumtumia Samantha ili utajiri wao uzidi kuchanua siku baada
ya siku.

36
Licha ya kujitahidi kufafanua, bado Edmund alikuwa hamuelewi msichana huyo,
huku muda mwingine akijihisi pengine yupo kwenye ndoto ya kutisha na muda
mfupi baadaye atashtuka na kujikuta akiwa amelala chumbani kwake.
Samantha alikuwa na kazi ya ziada ya kumuelewesha Edmund, akamwambia
kwamba tangu akiwa mdogo, wazazi wake walimpeleka kwa waganga
waliomuwekea tego mwilini mwake kupitia sehemu zake za siri kwamba
mwanaume yeyote atakayejaribu kufanya naye mapenzi, achukuliwe msukule au
akatolewe kafara.
“Nimeshawaua wanaume wengi sana Edmund, hata wewe ilikuwa ufe kwa njia
hizohizo, nimekuokoa kwa sababu kwa mara ya kwanza maishani mwangu
nimetokea kukupenda Edmund, nimechoka kuwa muuaji! Nimechoka naomba
unisaidie kuondokana na hali hii,” alisema Samantha huku akianza upya kuangua
kilio kwa uchungu.
Maelezo hayo yalimshtua mno Edmund, bado akawa anajihisi yupo ndotoni kwani
ilikuwa vigumu sana kuamini kwamba Samantha alikuwa akiongea ukweli.
“Kwa hiyo... kwa hiy..o nini huwa kina...to..kea,” Edmund alimuuliza kwa sauti ya
kukatakata huku akitetemeka mno kutokana na hofu kubwa iliyokuwa imemuingia,
hasa baada ya kuambiwa kwamba hata yeye alitakiwa kufa ila akaponea kwenye
tundu la sindano.
Samantha akamwambia kwamba anapotongozwa na wanaume, wakishakubaliana
kwenda kukutana kimwili, kuna dawa huwa anaitafuna muda mfupi kabla ya tendo
na kusababisha mwili wake wote uwe na sumu kali.
“Mwanaume akijaribu kuingia na mimi chumbani tu, hatafanikiwa kufanya
mapenzi na mimi na huo ndiyo utakuwa mwisho wake kwani lazima nitamng’ata
au kumchubua sehemu, kinachotakiwa ni damu yake kutoka hata kidogo tu!
“Ikitokea hivyo sumu yangu humuingia na kusababisha apoteze maisha ndani ya
muda mfupi sana na baada ya hapo kazi yote hubakia kwa baba,” alisema
Samantha huku akijifuta machozi na kamasi vilivyokuwa vinamtoka mfululizo.
“Kwa hiyo na mimi hicho ndicho kilichonitokea?”
“Ndiyo Edmund, naomba unisamehe mpenzi wangu, halikuwa kusudio langu
ndiyo maana nimeamua kukusaidia, nimekuwahi mpenzi wangu,” alisema
Samantha kwa hisia za hali ya juu, Edmund akashusha pumzi ndefu na kukosa cha
kusema, ukimya ukatawala kati yao.

37
Ghafla, walishtushwa na kelele za mlango uliobamizwa kwa nguvu, mganga
Shiwinga akaingia mbiombio na kumueleza Samantha kuwa ameliona gari
linalofanana na la baba yake likija eneo hilo kutokea mbali.
“Mungu wangu, babu naomba nisaidie kutoroka na Edmund wangu,” alisema
Samantha huku akianza kuhangaika, Mzee Shiwinga akamtuliza na kumwambia
kuwa isingekuwa rahisi kumtoroka baba yake katika mazingira hayo kwani
hakukuwa na njia nyingine ambayo angeweza kupita zaidi ya ile ambayo baba
yake alikuwa akija nayo.
“Labda ninachoweza kukusaidia ni kwenda kumficha Edmund porini lakini jua
kwamba ni hatari sana endapo akishtukia mchezo, bila shaka baba yako unamjua
vizuri,” alisema mganga Shiwinga huku akimuinua Edmund pale alipokuwa
amelala, harakaharaka akatoka naye na kuzunguka nyuma ya kibanda chake,
vishindo vikasikika wakati akikimbia naye kutokomea porini.
Huku nyuma, Samantha alifuta ushahidi wote wa uwepo wa Edmund eneo hilo,
akawa anapanga uongo wa kumwambia baba yake. Dakika chache baadaye,
muungurumo wa gari lililoonesha lipo kwenye kasi kubwa ulisikika nje ya kibanda
cha mganga Shiwinga kisha sekunde chache baadaye mlango ukawa unagongwa
kwa nguvu.
Huku akitetemeka kuliko kawaida, Samantha aliinuka na kufungua mlango,
akakutana uso kwa uso na baba yake aliyekuwa amefura kwa hasira kama nyoka
cobra!
“Ulijua sitakupata si ndiyo?”
“Hapana baba, nimekuja kwa babu Shiwinga kuja kutibiwa, naona mambo yangu
hayaendi sawa na mimi sipendi kukuudhi,” alisema Samantha huku akitetemeka
kuliko kawaida.
Haikuwa rahisi kwa baba yake kuuamini uongo wa kitoto alioutoa kwani kwa
macho yake alimshuhudia kuanzia anatoka hospitalini na jinsi alivyomkimbia
alipojaribu kumfuatilia.
“Unanifanya na mimi ni mtoto mwenzako si ndiyo?”
“Kweli baba, kama huamini kamuulize hata babu Shiwinga.”
“Yuko wapi?”

38
“Ameenda kunitafutia dawa,” alisema Samantha lakini baba yake hakutaka
kuamini, akamwambia dereva wake aliyekuja naye kusimama mlangoni na
kuhakikisha hakuna mtu anayetoka ndani ya nyumba hiyo ya mganga. Akazunguka
nyuma ya nyumba ya mganga na kuanza kuangaza huku na kule kama atamuona
mganga huyo.
Muda mfupi baadaye, aliona vichaka vikitingishika mita kadhaa kutoka pale
alipokuwa amesimama, akajua lazima kuna mtu. Alipoendelea kutulia huku macho
yake akiwa ameyakaza, alimuona mganga Shiwinga kichakani
Mganga Shiwinga akiwa na rundo la majani ya porini na mizizi kadhaa, alitokeza
kichakani huku akipiga ‘mbinja’ kwa nguvu, akajifanya hajamuona baba yake
Samantha wala hana taarifa zozote za uwepo wake. Ni mpaka alipomkaribia ndiyo
akajifanya kushtuka kumuona!
“Ni wewe baba?”
“Ni mimi mzee, shikamoo.”
“Marahabaa! Naona umeamua kuja mwenyewe, umefanya jambo zuri sana, nipo
na Samantha,” alisema mzee huyo huku akimpita baba yake Samantha na kumpa
ishara kwamba amfuate. Kwa jinsi alivyokuwa anamheshimu na kumuogopa
mganga Shiwinga, zile hasira zote alizokuwa nazo baba yake Samantha ziliyeyuka
kama siagi kikaangoni.
“Samahani kabla hatujaingia ndani, naomba nikuulize jambo.”
“Uliza tu baba.”
“Mwanangu Samantha amekuja na nani huku kwako?”
“Amekuja mwenyewe kama anavyofanya siku zote akiwa na tatizo lolote.
Ameniambia kwamba anahisi nguvu zake zimepungua kwa sababu hawezi tena
kufanya ile kazi tuliyompa kama ilivyokuwa zamani!
“Hivi hizi dawa unazoziona ni kwa ajili yake, nataka kumuongeza nguvu,”
alidanganya mganga Shiwinga, baba yake Samatha akashusha pumzi ndefu kwani
uongo alioambiwa na binti yake ulikuwa ukifanana na uongo wa mganga huyo.
Kwa kuwa hakuwahi kumdanganya hata siku moja, baba yake Samantha aliamini
kwamba alichoambiwa na mganga ni ukweli mtupu, akashusha tena pumzi ndefu
kisha wakaendelea kutembea kuelekea ndani ya kibanda chake.

39
“Naomba uzungumze na mjukuu wako, ukiachilia mbali kupungua kwa nguvu
zake, siku hizi amekuwa mzembe sana. Hafanyi kazi na badala yake anaendekeza
ujingaujinga tu. Hata ujio wangu hapa haukuwa wa heri kwa sababu kuna jambo
amelifanya na yeye mwenyewe analijua.
“Ni kwa sababu ya heshima yako mzee ndiyo maana nimeamua kumsamehe, ila
akirudia tena tusilaumiane,” alisema baba yake Samantha akiwa amekaa kwenye
kiti cha miguu mitatu ndani ya kibanda hicho cha mganga, akiwa amefura kwa
hasira.
“Samantha, kwani umemfanya nini baba yako?” alihoji mganga huku akijifanya
hajui chochote kilichotokea, Samantha ambaye muda wote alikuwa amekaa kimya,
hofu kubwa ikiwa imeutawala moyo wake, alishusha pumzi ndefu na badala ya
kueleza alichoulizwa, alianza kulia na kumuomba baba yake amsamehe.
“Mueleze babu yako ulichokifanya, kulia hakukusaidii chochote,” alisisitiza baba
yake Samantha lakini binti yake hakuwa tayari kueleza chochote, ikabidi yeye
ndiyo aanze kumueleza mganga kilichotokea.
Kwa kuwa tayari walishakula njama, mzee Shiwinga naye alijifanya kushtuka
kusikia kwamba Samantha alikuwa amemtorosha mtu aliyekuwa ameandaliwa kwa
kafara.
“Ni makosa makubwa uliyoyafanya, baba yako ana kila sababu ya kukasirika,
umekosea sana,” alisema mganga Shiwinga, akaacha hata kuchambua dawa na
kuendelea kumsema Samantha. Kwa jinsi walivyokuwa wamepangilia vyema
njama zao, haikuwa rahisi kwa mzee huyo kushtukia chochote.

40
SURA YA TANO

Samantha akawa amejiinamia muda wote huku akiyalazimisha machozi ya uongo.


Ilibidi baba yake asubiri mpaka binti yake huyo amalize kushughulikiwa na
mganga Shiwinga. Alipomaliza tu, alimtaka waongozane naye kurudi jijini Dar es
Salaam, nyumbani kwao.
Kwa jinsi alivyokuwa amembana, Samantha alishindwa jinsi ya kumtoroka,
akaondoka kwa shingo upande huku akijiapiza kuwa ni lazima atarudi kuja
kumfuata Edmund hata iweje.
Hatimaye msafara wa magari mawili uliianza safari ya kuelekea jijini Dar es
Salaam, Samantha akiwa amepanda kwenye gari alilokuwa anaendesha baba yake
na dereva wao akiwa anaendesha gari la Samantha.
Mganga Shiwinga aliwasindikiza kwa macho mpaka walipopotea kabisa kwenye
upeo wa macho yake, harakaharaka akaacha kila alichokuwa anakifanya na
kukimbilia nyuma ya nyumba yake, akapotelea vichakani.
Edmund aliendelea kukaa kwenye pango alimofichwa na mganga Shiwinga, hofu
kubwa ikiwa imetanda ndani ya moyo wake. Maelezo aliyopewa na Samantha
kuhusu kilichomtokea usiku uliopita, yalimfanya ajihisi maisha yake yapo kwenye
hatari kubwa mno.
Akiwa bado amezama kwenye dimbwi la mawazo ndani ya pango hilo lililokuwa
na giza totoro, alisikia vishindo vya mtu akija mbiombio, hofu ikazidi
kumuongezeka akihisi huenda baba yake Samantha ameshtukia mchezo na sasa
alikuwa anataka kuja kummalizia mwenyewe.
Japokuwa alikuwa ameacha kwenda kanisani kwa kipindi kirefu, alijikuta akihitaji
ulinzi wa Mungu wake kuliko kitu kingine chochote, mapigo ya moyo yakawa
yanazidi kumuenda mbio huku akisubiri muujiza utokee.
Mara aliona jiwe kubwa lililokuwa kwenye sehemu ya kuingilia ndani ya pango
hilo likisogezwa pembeni, akakazia macho sehemu hiyo akitaka kujua ni nani
aliyekuwa anafungua. Alipogundua kwamba ni mganga Shiwinga, alishusha pumzi
ndefu na kuinua mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu wake.
“Una bahati sana, yule bwana amekasirika mno, yaani kama angekukuta pale
kwangu angekutafuna mzimamzima,” alisema mganga huyo huku akimsaidia

41
Edmund kuinuka pale alipokuwa amekaa, akaupitisha mkono wake mmoja nyuma
ya mabega ya Edmund na kuanza kumsaidia kutembea kwani bado mwili wake
haukuwa na nguvu za kutosha.
Akamtoa nje ya pango hilo na kufunga sehemu ya kuingilia kwa jiwe kubwa,
wakawa wanarudi nyumbani kwake huku bado Edmund akiwa haamini kama
amesalimika.
“Nakushukuru sana babu.”
“Usinishukuru mimi, mshukuru Samantha, sijui umempa nini kwani kwa jinsi
alivyo katili sijui kwa nini ameamua kukuokoa wewe,” alisema mganga huku
akiendelea kumuandalia Edmund dawa nyingine kwa ajili ya kuitoa kabisa sumu
iliyokuwa imeingia mwilini mwake.
Bado Edmund alibaki na maswali mengi yaliyokosa majibu kuhusu Samantha,
akawa anajaribu kumdodosa mganga Shiwinga kama alikuwa anamjua vizuri
msichana huyo.
“Namjua tangu akiwa kachanga, mimi ndiye niliyeshirikiana na wazazi wake
kumfanya awe kama unavyomuona leo.”
“Mbona amesema kwamba kila mwanaume anayejaribu kufanya naye mapenzi ni
lazima afe. Ni kweli?”
“Ni kweli, pale alipo hamjui kabisa mwanaume, yeye alizaliwa kwa sababu ya kazi
moja tu, kumletea baba yake utajiri.”
“Sasa mbona ananiambia ananipenda ndiyo maana ameniokoa?”
“Hajawahi kupenda hata siku moja ndiyo maana nakuuliza kwamba sijui umempa
nini.”
“Sasa itakuwaje na umeshasema kila mwanaume anayejaribu kufanya naye
mapenzi ni lazima afe?” Edmund aliuliza huku akionesha kuwa na shauku kubwa
ya kutaka majibu. Licha ya yote yaliyotokea, alishindwa kuuficha ukweli uliokuwa
ndani ya moyo wake kwamba anampenda sana msichana huyo.
“Jiandae kufa,” alisema mganga huyo huku akiangua kicheko cha kizee, Edmund
akajiinamia chini.
“Ipo njia moja tu ya kuwasaidia wote wawili lakini ni ya hatari sana, hata mimi
sipendi kumuona akiendelea kuua watu wasio na hatia, natamani nimuone akiwa

42
na mume anayempenda, ajenge familia na hatimaye atulie lakini siyo rahisi,”
alisema mganga Shiwinga, kauli iliyomfanya Edmund ainuke pale alipokuwa
amejiinamia na kumsogelea mganga akitaka kujua ni mbinu gani hiyo ya
kuwasaidia.
“Inabidi Samantha atolewe nguvu za giza na tego aliloingiziwa mwilini mwake
tangu akiwa mtoto lakini suala hilo ni lazima yeye mwenyewe aridhie kwa sababu
litakuwa na madhara makubwa kwake na kwa familia yake.
“Lakini pia baba yake hatakiwi kabisa kujua kwa sababu anaweza hata kutupiga
risasi wote, Samantha ndiyo kitega uchumi chake,” alisema mzee Shiwinga na
kumfanya Edmund ashushe pumzi ndefu na kujishika shavu.
Alizama kwenye dimbwi la mawazo, akawa anatafakari mambo mbalimbali
yaliyotokea, akawa anajiuliza kama inawezekana msichana huyo akatolewa nguvu
mbaya zilizopandikizwa ndani ya mwili wake na akawa binadamu wa kawaida.
Hofu ya kifo ilimfanya amuogope mno Samantha, akaendelea kutafakari kwa
muda mrefu bila kupata majibu. Hakuna kitu kilichokuwa na maana kwake zaidi
ya uhai wake kwani mpaka muda huo ilikuwa ni miujiza ya Mungu tu ndiyo
iliyomfanya awe hai.
“Mbona umekuwa kimya kiasi hicho?”
“Babu sidhani kama nitaweza kuwa na amani na Samantha. Moyo wangu
unamuogopa mno hata kama ni yeye ndiye aliyeniokoa,” alisema Edmund na
kumfanya mganga Shiwinga aachie tabasamu.
“Siyo kazi nyepesi, moyo wako umeshaingiwa na hofu, ni binadamu anayeweza
kuzitawala hisia zake pekee ndiye anayeweza kuuona upendo wa kweli alionao
Samantha na kumsaidia kutoka kwenye shimo la mauti aliloishi kwa kipindi kirefu
tangu akiwa mdogo.”
“Kuzitawala hisia? Ndiyo kufanya nini?”
“Namaanisha mtu anayejitambua, anayefahamu yeye ni nani na kwa nini yupo
duniani ndiyo anayeweza kuishinda hofu ya kifo. Mtu akishaishinda hofu ya kifo
anaweza kuzitawala hisia zake na anaweza pia kuwasaidia wengine wenye uhitaji,”
alisema mganga Shiwinga na kumfanya Edmund akune kichwa kwani kimsingi
hakuwa amemuelewa.
“Kwa hiyo unataka kusema inabidi nijifunze uchawi?”

43
“Uchawi? Sijazungumzia suala la uchawi hapa, nazungumzia elimu ya utambuzi.
Haina uhusiano wowote na uchawi.”
“Lakini nimewahi kusikia kuwa waganga na wachawi peke yao ndiyo wanaoweza
kuishinda hofu dhidi ya kifo.”
“Tangu uzaliwe umesikia mambo mengi sana yasiyo sahihi, ni jukumu lako
kuutafuta ukweli kwani ndiyo kitu pekee kitakachokuweka huru. Hata vitabu vya
dini vinazungumzia suala la kuutafuta ukweli, mimi siyo muumini lakini
nayafahamu vizuri maandiko matakatifu,” alisema mganga Shiwinga huku
akiendelea kumuandalia Edmund dawa.
Maelezo yake yalimfanya Edmund aanze kujiuliza maswali mengi yaliyokosa
majibu. Alitamani kumuuliza maswali mengi sana mganga huyo lakini alishindwa
hata aanzie wapi.
Mganga Shiwinga ni kama alielewa kilichokuwa kikipita ndani ya mawazo yake,
akamwambia asiwe na wasiwasi akimaliza kumuandalia dawa atamjibu maswali
yote aliyokuwa akihitaji majibu.
Kazi ya kuandaa dawa iliendelea ambapo baada ya kumaliza, mganga huyo
alimnywesha Edmund huku nyingine akimpaka kwenye jeraha lake. Kutokana na
ukali wa dawa hiyo, Edmund alianza kuhisi usingizi mzito, mzee huyo
akamuandalia sehemu ya kupumzika ambapo muda mfupi baadaye alipitiwa na
usingizi.
***
Saa chache baada ya Samantha kuondoka pamoja na baba yake na dereva wao,
mganga Shiwinga alishtuka kusikia mlio wa pikipiki ikija kwa kasi nyumbani
kwake, akabaki anajiuliza maswali yaliyokosa majibu kwani haikuwa kawaida kwa
wagonjwa wake kwenda kwake kwa kutumia aina hiyo ya usafiri.
Akatoka nje na kusimama juu ya jiwe kubwa, akawa anatazama kule mlio ule wa
pikipiki ulikokuwa unatokea. Muda mfupi baadaye, tayari pikipiki hiyo ilikuwa
imeshafika, akabaki amepigwa na butwaa kumuona Samantha akishuka kwenye
bodaboda na kufungua pochi yake, akatoa fedha na kumpa yule dereva wa
bodaboda kisha harakaharaka akaondoka na kumuacha mganga Shiwinga akiwa
bado amepigwa na butwaa.
“Samantha! Imekuwaje tena?” aliuliza mganga Shiwinga kwa mshangao, msichana
huyo akatembea harakaharaka mpaka pale alipokuwa amesimama.

44
“Nataka kumuona Edmund, nataka kuhakikisha kama yupo salama,” alisema
Samantha huku akionesha kuwa na hofu kubwa.
Ilibidi mganga Shiwinga amtulize na kumtoa wasiwasi, akamuingiza ndani ya
kibanda chake na kwenda kumuonesha Edmund ambaye alikuwa amepitiwa na
usingizi mzito. Samantha akashusha pumzi ndefu na kumgeukia mganga.
“Nashukuru kwa msaada wako babu, sina imani na baba najua anaweza kufanya
kila kinachowezekana kumuondoa duniani Edmund, naomba usinisaliti,” alisema
Samantha huku akilengwalengwa na machozi.
Mganga huyo akamhakikishia kwamba asiwe na wasiwasi, na yeye akaanza
kumuuliza kilichotokea kwani hakutarajia kumuona muda huo hasa baada ya kuwa
amefuatwa na baba yake akiwa na jazba kali.
“Tumeenda naye mpaka nyumbani lakini nikafanya ujanja na kuondoka bila mtu
yeyote kujua. Wanajua nipo chumbani kwangu nimelala. Muda si mrefu baba
atajua Edmund mahali alipo kwa sababu nimemuacha akiandaa rada zake za
kichawi kwa ajili ya kuanza kazi ya kumtafuta, anataka kumuua,” alisema
Samantha huku akihema kwa nguvu.
“Usiwe na wasiwasi, hakuna rada zinazoweza kunasa chochote kinachoendelea
hapa nyumbani kwangu, mimi ndiyo Shiwinga mwenyewe kutoka Lyamba Lya
Mfipa, niamini,” alisema mganga huyo huku akijipigapiga kifuani kwa kujiamini.
Samantha alikaa kwenye kiti cha miguu mitatu na kuanza kuzungumza na mganga
huyo ambaye alimueleza kilichoendelea baada ya yeye kuondoka.
“Nataka kujua kuhusu msimamo wako, huyu kijana wa watu anaonesha kuwa na
hofu kubwa juu yako na mimi sitaki kuja kuonekana nimemsaliti, nataka uniambie
unafikiria nini juu yake.”
“Kama nilivyokudokeza babu, mi nampenda Edmund na nataka kujenga naye
familia. Wewe ni shahidi, sijawahi kumpenda mwanaume yeyote zaidi yake,
naomba unisaidie babu.”
“Mimi sina tatizo, cha msingi ni utayari wako mwenyewe kwa sababu ili uweze
kuwa naye, inabidi ukubali hizo nguvu za giza ndani ya mwili wako zitolewe,
jambo ambalo baba yako hawezi kulifurahia hata kidogo.”
“Babu nimeshakwambia, nimechoka kuwa mtumwa wa baba, nimechoka kuwa
kaburi la wanaume, na mimi nina haki ya kupenda na kupendwa! Nampenda

45
Edmund na nipo tayari kufanya chochote kwa ajili ya penzi lake,” alisema
Samantha kwa msisitizo huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
“Una uhakika na unachokisema?”
“Nina uhakika wa asilimia mia moja, mimi nimeshakuwa mkubwa babu, isitoshe
Mungu kanijalia urembo, kwa nini niendelee kuishi maisha ambayo siyataki?
Nataka kuwa mke wa Edmund,” alisema Samantha kwa sauti ya juu ambayo
ilimfanya Edmund aliyekuwa amelala, kuzinduka na kuyasikia maneno hayo.
Akawa anajihisi kama yupo ndotoni kwa sababu hakutegemea kwamba Samantha
anaweza kurudi kwa mganga muda huo, harakaharaka akainuka pale alipokuwa
amelala.
Akajaribu kusimama lakini kutokana na dawa alizopewa na Mganga Shiwinga,
Edmund alijikuta akianza kupepesuka mithili ya mlevi, akagonga vyombo
vilivyokuwa pembeni na kuwashtua Samantha na Mganga Shiwinga.
Akiwa bado anapepesuka, harakaharaka Samantha aliinuka na kumkimbilia,
akawahi kumdaka na kumvutia kifuani kwake.
“Samantha! Ni wewe?”
“Ni mimi Edmund, najua huwezi kuamini lakini ndiyo hivyo, nimerudi kwa ajili
yako,” alisema Samantha huku akizidi kumbana Edmund kwenye kifua chake
kizuri, akamtazama Edmund kwa macho yake yaliyokuwa mithili ya mtu
anayesikia usingizi, Edmund akashindwa kuzizuia hisia zake na kujikuta mapigo
ya moyo wake yakianza kwenda mbio.
Ni kweli alikuwa anaumwa na dawa alizopewa na mganga Shiwinga zilimlevya
sana lakini kitendo cha kukumbatiwa na Samantha, kilimfanya ajihisi kama tayari
ameshapona. Wakabaki kutazamana usoni huku kila mmoja akizisikiliza pumzi za
mwenzake.
“Nakupenda sana Edmund, sijawahi kupenda kama ninavyokupenda wewe,
tafadhali naomba nisamehe kwa yote yaliyotokea,” alisema Samantha kwa sauti ya
kudeka huku akianza kulengwalengwa na machozi, Edmund hakumjibu kitu zaidi
ya kumbusu kwenye paji lake la uso, kitendo kilichomfanya msichana huyo
mrembo asisimke mwili mzima.

46
Mganga Shiwinga aliyekuwa amesimama hatua kadhaa akiwatazama, aliishiwa cha
kuzungumza, kwa akili za kiutu uzima ikabidi akohoe kidogo na kutoka nje,
akawaacha wawili hao bado wamegandana kama ruba.
“Niambie kama umenisame...” alisema Samantha lakini alishindwa kumalizia kauli
yake, wawili hao wakajikuta wamegusanisha ndimi zao na kuanza kuelekea
kwenye ulimwengu wa tofauti, kila mmoja akionesha kuwa na hisia nzito juu ya
mwenzake.
Muda mfupi baadaye, walijikuta wakiwa juu ya kitanda cha kamba alichokuwa
amelala Edmund muda mfupi uliopita. Usingeweza kudhani kwamba Edmund
alikuwa anaumwa kwa jinsi alivyoonesha ushirikiano.
Kama isingekuwa nguvu za giza zilizokuwa ndani ya mwili wa msichana huyo,
huenda wawili hao wangefika mbali zaidi na kuvuka mipaka lakini Edmund
alipokumbuka kilichotokea mara ya mwisho alipojaribu kukutana kimwili na
Samantha, alijikuta akiwa mpole ghafla.
“Kweli unanipenda Samantha?” aliuliza Edmund kwa sauti ya chini, msichana
huyo akaitikia kwa sauti ya kunong’ona na kumueleza Edmund kwamba
anajishangaa nini kilichomtokea kwa sababu hajawahi kuhisi hali hiyo hata siku
moja tangu azaliwe.
“Babu Shiwinga amesema hatuwezi kuwa pamoja kutokana na nguvu zako
vinginevyo nitapatwa na madhara makubwa zaidi.”
“Hata mimi nimezungumza naye na kuna mambo tumeshakubaliana. Nimechoka
kuwa mtumwa Edmund, na mimi nataka nijisikie kama mwanamke niliyekamilika,
nipo tayari kwa chochote,” alisema Samantha kwa sauti iliyoonesha kutokuwa na
hata chembe ya masihara.
“Edmund! Muda wa kunywa dawa umefika,” mganga Shiwinga alikatisha
mazungumzo ya wawili hao, wote wakajivuta kichovu na kuamka huku Samantha
akiendelea kuonesha waziwazi hisia nzito za kimapenzi alizokuwa nazo kwa
Edmund.
“Na wewe Samantha inabidi urudi nyumbani ili baba yako asije akashtukia, inabidi
ujue namna ya kula na kipofu,” alisema mganga Shiwinga kwa msisitizo. Ikabidi
Samantha akubali kwa shingo upande kuondoka lakini kabla hajaondoka alitaka
mganga ampe maelekezo ya nini cha kufanya.

47
“Nikizitazama nyota zenu naona kuna tofauti kubwa sana, Edmund nyota yako
inang’ara sana na wewe Samantha nyota yako ina giza nene, hamuwezi kuoana
mpaka nyota zenu ziwe zinashabihiana kwa hiyo kabla ya kukutoa hizo nguvu
zako inabidi kwanza tufanye kazi ya kutafuta uwiano wa nyota zenu.”
“Tutafute uwiano kivipi? Sijakuelewa babu.”
“Inabidi nyote muanze kufanya ‘meditation’.”
“Meditation? Ndiyo nini?” Edmund aliingilia kati mazungumzo hayo huku naye
akionesha kutoelewa kabisa kilichokuwa kinazungumza na mganga Shiwinga.
Licha ya kuwa mganga huyo alikuwa akitibu kwa mitishamba na dawa za kienyeji
kama walivyo waganga wengine, ndani ya muda mfupi tu ambao Edmund alikuwa
amekaa naye, aligundua kwamba mzee Shiwinga alikuwa na kitu kingine kikubwa
zaidi ambacho pengine ndicho kilichokuwa kinamfanya ajiamini kiasi hicho.
“Mtaelewa tu wala msiwe na wasiwasi, meditation ni neno la Kiingereza ambalo
linamaanisha tahajudi kwa Kiswahili. Kwa kifupi, ni kitendo ambacho mtu anakaa
kwenye mkao maalum na kutafuta utulivu wa mwili na akili, ukishaweza kukaa na
kutulia kwenye meditation, unakuwa na uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na
roho yako.”
“Kuwasiliana na roho? Mbona sikuelewi babu?”
“Ni vigumu kunielewa lakini ninachotaka kuwaambia ni kwamba kila mtu, awe
anajua au hajui, anazalisha nguvu ambazo ndiyo zinazofanya aendelee kuishi.
“Hakuna anayejua moja kwa moja nguvu hizo zinazalishwa wapi ndani ya mwili
wa binadamu lakini baadhi ya watu husema kwamba zinazalishwa kwenye kile
ambacho tumezoea kukiita roho,” alisema mganga Shiwinga na kuwachanganya
kabisa Edmund na Samantha.
“Ili kuwasiliana na roho yako, siyo lazima uwe mchawi au uwe muumini wa jamii
za siri au umuabudu shetani kama wengi wanavyoamini, ukifanya meditation tu
utaona matokeo yake.
“Na ukiweza kuwa unawasiliana na roho yako mara kwa mara, utakuwa na uwezo
wa kuchagua ni nguvu gani unazalisha na hizo ndiyo zinazoweza kufanya nyota
yako ing’ae au ififie, uishi maisha ya kimaskini au ya kitajiri, ufanikiwe au ufeli,
kimsingi nguvu hizo ndiyo zitakazoamua maisha yako yaweje.

48
“Tatizo ambalo nyote wawili mnalo, linaanzia kwenye roho zenu, ni lazima
nilishughulikie hilo kwanza kabla ya mambo mengine yote. Ni safari ndefu lakini
nawahakikishia mkiweka juhudi za kutosha, mtaanza kujitambua ninyi ni akina
nani na kwa nini mmeletwa duniani,” alisema mzee Shiwinga, wote wakashusha
pumzi ndefu na kutazamana. Ilikuwa ni elimu mpya kabisa kwao.
“Pengine hamjanielewa, hivi nikiwauliza swali jepesi tu, nianze na wewe Edmund,
mtu akikuuliza wewe ni nani utamjibu nini?”
“Aah! Babu mbona swali jepesi hilo? Mimi ni Edmund.”
“Mnaonaa? Hilo ni swali jepesi lakini lenye maana kubwa ambalo ni wachache
sana wanaoweza kulijibu. Wengi tunaamini kwamba sisi ni hii miili yetu
tunayoiona lakini ukweli upo tofauti kabisa ndiyo maana nataka mjifunze kwanza
kufanya meditation kisha mengine yatafuatia.
“Natamani kuwaona mkioana na kuishi kwa amani kama mume na mke lakini
kuna vikwazo vingi sana katikati yenu ambavyo vinahitaji nguvu za ziada
kuvivuka,” alisema mganga Shiwinga lakini kabla hajamalizia, wote walishtushwa
na muungurumo wa pikipiki iliyokuwa inakuja kwa kasi nyumbani kwa mganga
huyo.
“Mungu wangu, siyo baba huyo?” alisema Samantha kwa mshtuko mkubwa.
“Ni yeye! Mungu wangu, hata sijui itakuwaje! Njooni huku,” alisema mganga
Shiwinga huku akikimbilia kwenye chumba chake kidogo alichokuwa anahifadhia
dawa na tunguli zake.
Harakaharaka akafunua ngozi aliyokuwa ameitandika chini kisha akainama, akawa
anafukua kitu ambacho hakuna aliyejua ni nini. Edmund na Samantha wakapigwa
na butwaa kuona mganga Shiwinga akifungua kitu kama mlango uliokuwa
umechimbiwa ardhini.
“Kunatisha lakini hakuna namna, inabidi muingie. Msifike chini, kaeni hapa jirani
kwenye ngazi,” alisema mganga huyo, Edmund na Samantha wakatazamana
wakiwa ni kama hawaamini.
Tayari mlio wa pikipiki ulikuwa unasikika jirani kabisa na pale nyumbani kwa
mganga, wakawa hawana namna zaidi ya kuingia kwenye shimo hilo lenye giza
totoro lililokuwa limechimbwa chini ya ardhi, ndani ya chumba cha mganga
Shiwinga.

49
“Naogopa.”
“Usiogope, jikaze,” Edmund alisema huku akimkumbatia Samantha ambaye
alionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake. Mganga Shiwinga akafunga
mlango kisha wakamsikia akirudisha kila kitu katika mpangilio wake wa kawaida.
“Mbona kama kule chini kuna watu?”
“Shhh!” Edmund alimnyamazisha Samantha aliyekuwa anaendelea kutetemeka.
Japokuwa Edmund naye alikuwa akiogopa mno kutokana na mazingira ya shimo
hilo, alijikaza kisabuni kwani alijua endapo baba yake Samantha atagundua
kwamba yupo pale, huenda huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yake.
“Karibu! Karibu ndani,” Edmund na Samantha walimsikia mganga Shiwinga
akimkaribisha mtu, wakawa na shauku kubwa ya kusikia ni nani. Japokuwa
walikuwa ndani ya shimo hilo la kutisha, waliweza kusikia kila kilichokuwa
kinaendelea ndani ya nyumba ya mganga huyo.
“Ahsante, nimerudi tena. Nina tatizo mzee wangu,” Edmund na Samantha
almanusra wafe kwa kihoro baada ya kuisikia sauti hiyo. Hakuwa mwingine bali
baba yake Samantha.
“Tatizo gani tena?”
“Kila nikijaribu kumtafuta yule mshenzi kwenye rada zangu simuoni.”
“Nani tena?”
“Yule kijana ambaye Samantha alileta uzembe kwenye kukamilisha kafara lake.
Mambo hayaendi vizuri, biashara zimekuwa nzito. Nahitaji kufanya kafara ili
mambo yanyooke na tayari Samantha alishamuandaa japo alifanya uzembe.”
“Mh! Kwa hiyo ulikuwa unasemaje mwanangu?”
“Nataka unisaidie kuniongezea nguvu kidogo ili rada zangu ziweze kumnasa vizuri
mahali alipo, nahitaji kukamilisha kazi yangu leoleo,” alisema baba yake
Samantha, kauli ambayo ilisikika vyema kwenye masikio ya Edmund na
Samantha.
“Hilo tu, mbona kazi ndogo sana hiyo,” alisema mganga Shiwinga na kumwambia
amsubiri kidogo, akaingia ndani ya chumba chake cha kuhifadhia tunguli,
akachukua baadhi ya vifaa na kusogea pale kwenye mlango wa kuingilia kwenye
lile shimo alimokuwemo Samantha na Edmund.

50
SURA YA SITA

“Msiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema mganga Shiwinga kwa
kunong’ona, Samantha na Edmund wakamsikia vizuri. Kauli hiyo kidogo
ilipunguza wasiwasi kwenye moyo wa Edmund, akashusha pumzi ndefu na
kumbusu Samantha kwenye paji la uso, wakaendelea kukumbatiana.
Mganga Shiwinga akatoka na kurudi pale alipomuacha baba yake Samantha,
akaanza kupiga manyanga huku akiimba nyimbo ambazo si Edmund wala
Samantha aliyezielewa.
“Huyu kijana inaonesha ni mzito.”
“Mzito kivipi baba.”
“Inaonesha ameaga kwao, rada zangu hazimuoni kabisa. Amefanyiwa zindiko kali.
Hata nikikuongeza nguvu itakuwa ni sawa na kazi bure.”
“Sasa itakuwaje?”
“Mi nakushauri uachane naye, tafuta mtu mwingine, huyu anaweza kukuletea
matatizo zaidi. Samantha si yupo? Mwambia afanye kazi yake.”
“Samantha yupo, nimemuacha nyumbani, hata hajui kama nimekuja huku.
Nimeona nikimshirikisha katika hili atanikwamisha kwa makusudi maana hata
simuelewi,” alisema baba yake Samantha.
“Basi inabidi muandae tukio jingine ili kutimiza hicho unachokitaka. Huyu kijana
sijui anatokea wapi maana yuko vizuri sana,” alisema mganga Shiwinga, baba yake
Samantha akainamisha kichwa na kutafakari kwa muda kisha akamgeukia mganga
Shiwinga.
“Basi itabidi nifanye kama ulivyoniambia, Samantha amenigharimu sana kwa
sababu ya ujinga wake. Akirudia tena itabidi nimtoe yeye mwenyewe kafara,
nampenda mwanangu lakini naupenda zaidi utajiri, nitakuwa sina namna,” alisema
baba yake Samantha, akaingiza mkono mfukoni na kumtolea fedha mzee huyo,
akamkabidhi kisha akatoka mpaka nje ambako dereva wa bodaboda alikuwa
anamsubiri.

51
Akaaga na kupanda bodaboda, akaondoka kwa kasi. Ni mpaka mlio wa bodaboda
ulipopotelea mbali kabisa ndipo Samantha na Edmund walipoamini kwamba
hatimaye wapo salama.
“Namchukia baba.”
“Hapana Samantha, usiseme hivyo.”
“Namchukia sana, si umesikia mwenyewe anachokisema, eti yupo tayari hata
kuniua ilimradi apate utajiri, hivi ni haki kweli hii! Eti babu ni haki kweli?”
alisema Samantha huku akianza kulia, muda mfupi baada ya mganga Shiwinga
kuwafungulia kutoka pale mafichoni. Edmund akawa na kazi ya ziada ya
kumbembeleza.
“Baba yako amebadilika sana siku hizi, yaani tamaa ya utajiri imemfanya aone
kupoteza uhai wa mtu kuwa kazi nyepesi sana, afadhali kama Mungu ameanza
kukubadilisha. Mimi huwa namsaidia tu lakini kiukweli sifurahishwi na
anachokifanya,” alisema mganga Shiwinga kwa msisitizo.
“Ahsante kwa kunitetea babu, yaani hata sijui nitawalipa nini wewe na Samantha,”
alisema Edmund huku akiwa bado amemkumbatia Samantha.
“Usijali kijana, nilishakwambia nitakusaidia, furaha yangu ni kuona unamkomboa
Samantha kutoka kwenye shimo la mauti alilozama,” alisema mganga Shiwinga.
“Naomba basi utufundishe meditation maana naona mambo yanazidi kuwa
magumu.”
“Mpo tayari?”
“Ndiyo babu.”
“Mbona naona mwenzako bado analia? Mbembeleze kwanza halafu inabidi
tufanye harakaharaka huyu arudi nyumbani. Najua baba yake akifika lazima
ataenda kumtafuta.”
“Sawa babu, halafu nilitaka kukuuliza jambo. Mbona kwenye lile shimo
ulilotufungia kama kuna watu kule chini?” alihoji Edmund, kauli iliyomfanya
mganga huyo ashtuke sana, akakosa cha kujibu.
“Edmund, mbona una maswali mengi namna hiyo? Kamuulize Samantha ndiyo
anayejua kila kitu,” alisema mganga huyo huku akiendelea kuandaa mahali pa

52
kuwafundishia wawili hao namna ya kufanya tahajudi (meditation) kama
walivyokuwa wamemuomba.
Ilibidi Edmund amfuate Samantha na kuanza kumbembeleza, akatumia uwezo
wake wote kumshawishi na hatimaye akafanikiwa kumfanya atulie. Akamshika
mkono na kumuinua pale alipokuwa amekaa, akamkumbatia na kumbusu kwenye
paji lake la uso.
“Usijali, haya yote yatafikia mwisho,” alisema na kumuongoza Samatha kuelekea
kule mganga Shiwinga alikowaandalia sehemu ya kujifunzia tahajudi.
“Piteni mkae,” alisema mganga Shiwinga na kuanza kuwaelekeza namna ya kukaa.
Wakakaa kwa kukunja miguu yao vizuri kama alivyokuwa akiwaelekeza.
“Lazima miguu yako uikunje vizuri kama hivi,” alisema baada ya kuona mkao huo
unawashinda wote wawili, baada ya kuelekezana sana, hatimaye wote waliweza
kukaa mkao huo.
“Hakikisha mgongo unanyooka kabisa ili kuwezesha nguvu kuingia na kutoka
vizuri kwenye mwili wako wakati wa kufanya tahajudi,” alisema mganga Shiwinga
kisha kabla ya kuanza kuwaelekeza hatua iliyokuwa inafuatia, akaanza kuwapa
maelezo muhimu kuhusu tahajudi (meditation).
“Kama nilivyowaambia, ni vigumu kujibu swali la wewe ni nani na kwa nini upo
hapa duniani lakini kupitia tahajudi, ni rahisi kujijua wewe ni nani.
Nimeshawaambia, sisi siyo hii miili yetu tunayoiona, wala siyo majina yetu, kazi
zetu wala vitu vinavyofanana na hivyo.
“Wengi hawajui thamani zao ndiyo maana wanaishi maisha ya ajabu. Baba yako ni
miongoni mwa watu ambao hawajui thamani zao wala hawajui thamani ya maisha
ndiyo maana amefikia hatua ya kuwa kama mnyama. Sitaki na nyie muwe
miongoni mwa mamilioni ya watu wasiojitambua, wanaoishi duniani leo hii.
“Tahajudi ni chombo ambacho kitakusaidia kusafiri vizuri safari yako ya kuelekea
kujitambua. Zipo aina nyingi za tahajudi lakini ambayo tutaanza nayo ni tahajudi
ya pumzi au kwa Kiingereza wanaita ‘breath meditation’. Mkiifanya hiyo vizuri
kwa uaminifu, hatua ya pili inaitwa Mantra.
“Bila shaka kila mmoja wenu anajua kwamba anapumua,” aliuliza mganga
Shiwinga, wawili hao wakatazamana kwani waliliona swali hilo kuwa jepesi sana.
“Babu kwani kuna mtu ambaye hajui kwamba anapumua?”

53
“Nilijua mtasema hivyo lakini ukweli ambao hamuujui, watu wengi sana
wanapumua lakini hawajui kama wanapumua mpaka uwakumbushe. Najua hata
nyie mlikuwa mmesahau kama mnapumua mpaka nilipowauliza swali hili.
“Msingi wa tahajudi ya pumzi, ni kuzifuatilia pumzi zako kwa utulivu
zinavyoingia na kutoka. Ukikaa na kutulia kisha ukawa unapumua kwa uhuru,
ukitoa pumzi ndefu na kuvuta pumzi ndefu japo kwa nusu saa tu, huku ukijitahidi
kutowaza jambo jingine lolote zaidi ya kuzitazama pumzi zako tu, ukiwa
umefumba macho, hiyo ndiyo inaitwa tahajudi ya pumzi.
“Unapoanza huwa inakuwa ngumu kama mtakavyoona lakini ukizoea unaweza
hata kukaa saa tatu au nne ukiwa kwenye hali hiyo. Unajua watu wengi wanakufa
kwa magonjwa mbayo yanasababishwa na msongo wa mawazo, presha au vitu
vinavyofanana na hivyo, wengine wanaugua magonjwa ambayo hata vipimo
mahospitalini havioneshi ni ugonjwa gani kumbe tatizo linaanzia kwenye akili.
“Tahajudi hii ina uwezo wa ajabu wa kutuliza kabisa akili yako, kama ulikuwa na
msongo wa mawazo, ulikuwa na hasira, hofu, mashaka au huzuni kali na umekata
tamaa ya kuishi, ukifanya zoezi hili japo mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni,
utaweza kuondokana kabisa na matatizo yote hayo na taratibu utaanza kuona
maisha yako yanabadilika kuanzia ndani ya mwili wako mpaka nje.
“Sitaki niwe mzungumzaji mkubwa, nataka kila mtu ajionee mwenyewe, wote
fumbeni macho na anzeni kuzifuatilia pumzi zenu kwa utulivu kabisa, mawazo
yakiwa yanakuja ndani ya vichwa vyenu msiyazuie ila elekezeni ufahamu kwenye
pumzi, haya moja, mbili, tatu...” alisema mganga huyo kisha wote wakafumba
macho na kutulia, wakifuatilia maelekezo waliyopewa na mganga huyo.
Utulivu wa ajabu ukatawala ndani ya nyumba hiyo, hakuna sauti wala kelele
yoyote iliyosikika, kila mtu alikuwa kimya kabisa. Dakika thelathini baadaye,
mganga Shiwinga alitoa ishara akiwaamuru wote wafumbue macho yao, wakatii
walichoaambiwa.
“Haiwezekani! Haiwezekani babu.”
“Hata siamini kilichotokea, siamini... babu unataka kutufundisha uchawi?”
Samantha na Edmund walikuwa wakizungumza kwa pamoja, walichokishuhudia
ndani ya muda huo mfupi kiliwashangaza mno na hakuna aliyewahi kufikiria
kwamba anaweza kutokewa na hali kama hiyo.

54
“Leo sitaruhusu mjadala wa aina yoyote, Samantha muda umeenda sana, jiandae
urudi nyumbani, kama una maswali yahifadhi utakuja kuniuliza kesho au siku
nyingine, na wewe Edmund huu ni muda wa kunywa dawa,” alisema mganga
Shiwinga akionesha kutotaka majadiliano nao kwani alijua kwa wakati huo hakuna
ambaye anaamini alichokiona.
“Lakini babu...”
“Lakini nini Samantha, muda umeenda sana, rudi nyumbani baba yako atakuwa
anakutafuta.”
“Kwa hiyo naruhusiwa kwenda kufanya kama hivi tena hata nikiwa nyumbani
kwetu?”
“Ndiyo, fuata masharti kama nilivyokwambia,” alisema mganga Shiwinga,
Samantha akaachia tabasamu hafifu na kumgeukia Edmund ambaye naye bado
alikuwa amepigwa na bumbuwazi.
“Umejisikiaje?”
“Nahisi kama nilikuwa napaa angani, nimeogopa sana, sijawahi kujisikia hali kama
hii hata siku moja tangu nimezaliwa.”
“Mimi nahisi kama nilikuwa kwenye ndoto, ngoja nikifika nyumbani nitaenda
kurudia tena ili nihakikishe kama ni kweli au ni ndoto,” alisema Samantha huku
akianza kujiandaa.
Japokuwa walikuwa wakilalama, ukweli ni kwamba kilichowatokea kilikuwa
kigeni kabisa na kila mmoja alitamani kuendelea kuwa kwenye hali hiyo,
japokuwa nafsi zao pia zilikuwa na hofu kwani walihisi kama wanafundishwa
ushirikina, jambo ambalo mganga Shiwinga hakutaka kabisa kulizungumzia.
Baada ya kumaliza kujiandaa, Samantha alimpigia simu yule dereva wake wa
bodaboda ambaye walikubaliana kwamba akamsubiri kwenye barabara ya lami ili
isiwe rahisi kwa mtu yeyote kugundua kuwa Samantha alikuwa nyumbani kwa
mganga huyo.
Wakati akiendelea kumsubiri dereva huyo wa bodaboda, Samantha na Edmund
walipata nafasi ya kuzungumza kwa kina kwani sasa Edmund alikuwa na nafuu
kubwa tofauti na alivyokuwa mwanzo.
“Unanihakikishia kweli upo tayari kuondokana na mambo yote ambayo baba yako
alikuwa anakutumikisha?”

55
“Jamani Edmund, mpaka nimekubali kuanza kujifunza tahajudi huamini tu
kwamba nahitaji kuachana na kila kitu? Nakupenda sana mwenzio, hata sielewi
umenipa nini lakini amini nakwambia nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako.
Nataka hili tatizo likiisha, wewe ndiyo mwanaume wa kwanza kuujua mwili
wangu,” alisema Samantha kwa sauti ya kubembeleza.
Akawa anayazungusha macho yake mazuri huku na kule kuonesha msisitizo wa
kile alichokuwa anakisema, Edmund akashusha pumzi ndefu na kutabasamu,
akamkumbatia, akambusu shavuni, msichana huyo naye akafanya hivyohivyo.
“Naomba usije kunigeuka mbele ya safari, nayakabidhi maisha yangu mikononi
mwako, ni wewe pekee ndiye unayeweza kuniokoa.”
“Usijali Edmund, ilimradi upo kwenye mikono ya babu Shiwinga, amini upo
kwenye mikono salama,” alisema Samantha na kuingiza mkono kwenye pochi
yake ndogo, akatoa noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi na kumkabidhi Edmund.
“Na hizi ni za nini?”
“Zitakusaidia kwa matumizi madogomadogo, hata kama siyo leo,” alisema
Samantha huku akimshikisha Edmund fedha hizo, akaachia tabasamu pana,
wakawa wanatazamana.
“Nataka unizalie watoto wazuri kama wewe jinsi ulivyo,” Edmund alisema huku
akimkumbatia tena msichana huyo, kauli hiyo ikaonesha kumfurahisha mno
Samantha, akaangua kicheko cha furaha.
“Enhee! Kuna jambo nilitaka kusahau.”
“Jambo gani tena mpenzi wangu?”
“Muda ule wakati tumejificha kule kwenye lile shimo wakati baba yako amekuja,
kule chini si uliona kama kuna watu wengi ndani ya lile shimo? Nimemuuliza
mganga Shiwinga wale ni akina nani ameniambia wewe ndiyo una majibu. Hebu
naomba unieleze ukweli,” alihoji Edmund huku akiwa anamtazama Samantha
machoni.
Katika hali ambayo hakuitegemea, alishangaa kuona swali hilo limemfanya
Samantha abadilike kabisa usoni, uso wake ukajaa huzuni na muda mfupi baadaye
akaanza kuangua kilio. Akabaki amepigwa na butwaa. Kwa mbali, muungurumo
wa bodaboda ukaanza kusikika kuashiria kwamba yule dereva alikuwa jirani akija.

56
“Mbona sikuelewi? Nisamehe kama nimekosea kukuuliza,” alisema Edmund,
msichana huyo akamkumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia kwa huzuni,
Edmund akazidi kuchanganyikiwa.
“Najisikia vibaya sana Edmund, kama ningekuwa naweza kurudisha siku nyuma ili
niweze kurekebisha makosa yangu ningefanya hivyo.”
“Huna haja ya kujilaumu sana Samantha, kila jambo huja kwa sababu maalum.
Isitoshe mi najua wewe hupendi kuwadhuru binadamu wenzako bali
unalazimishwa na baba yako.”
“Ahsante kwa kuwa mwelewa, nakupenda sana Edmund ila naomba uniahidi
kwamba hata utakapoyajua mambo yangu yote niliyowahi kufanya hutanikimbia.”
“Usiwe na wasiwasi Samantha, nilishakwambia kwamba hata iweje siwezi
kukuacha.”
“Kweli Edmund?”
“Kweli kabisa.”
“Basi wale watu kwenye lile shimo kule ndani kwa mganga ni miongoni mwa
wanaume waliofiakwenye mikono yangu,” alisema Samantha, kauli iliyosababisha
Edmund ashtuke mno.
“Kama sijakuelewa hivi?”
“Unajua mtu akitolewa kafara, anakuwa hajafa kabisa mpaka sikualizoandikiwa na
Mungu zifike.”
“Unataka kusema wanakuwa bado wanaishi?”
“Ndiyo lakini hawawi kama binadamu wa kawaida, wanaitwa misukule.”
“Mungu wangu! Halafu inakuwaje?”
“Ndiyo wanatumika kufanya kazi mbalimbali, wengine baba anawatuma kwenda
kuiba hela kichawi kwenye mabenki na maduka makubwa,” alisema Samantha na
kumfanya Edmund ahisi kwamba yupo ndotoni.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana na tayari yule dereva wa bodaboda
alishafika, ilibidi Samantha aondoke. Akamuacha Edmund amesimama palepale,
akiendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.

57
“Vipi ameshaondoka?” sauti ya mganga Shiwinga ndiyo iliyomzindua Edmund
kutoka kwenye dimbwi la mawazo.
“Ndiyo, ameshaondoka,” alijibu Edmund na kushusha pumzi ndefu.
“Vipi mbona umeduwaa? Amekujibu?”
“Ndiyo amenijibu,” alisema Edmund na kumsogelea mganga Shiwinga,
akaendelea kumdadisi maswali mengi, akitaka kujua kama alichoambiwa na
msichana huyo mrembo ni kweli.
Mganga Shiwinga alimfafanulia kila kitu, akajikuta akipatwa na hofu kubwa ndani
ya moyo wake.
“Wala huna sababu ya kuogopa, hawawezi kukudhuru kwa chochote.”
“Sasa huwa wanakula nini?”
“Chakula chao kikuba ni pumba,” alijibu mzee huyo, Edmund akaendelea
kumdadisi kwa muda mrefu.
“Inatosha sasa, maswali mengine utauliza siku nyingine,” mganga Shiwinga
alimkatisha Edmund ambaye alikuwa akiendelea kuuliza maswali mengi kuhusu
jambo hilo.
Siku hiyo ilipita, mganga Shiwinga akawa anaendelea kumpa dawa mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuuzindika mwili wake ili baba yake Samantha asiweze
kumdhuru kwa chochote. Pia aliendelea kumkazania kufanya tahajudi (meditation)
mara kwa mara.
Siku mbili baadaye, Samantha alienda tena kumtembelea nyumbani kwa mganga
huyoambapo mbali na mambo mengine, walipanga watakavyokuwa wakiendesha
mapenzi yaoa kwani siku za Edmund kukaa kwa mganga zilikuwa zimeisha.
“Babu Shiwinga anasema mpaka baada ya siku arobaini ndiyoi tunaweza kukutana
kimwili na wewe, anasema uchawi uliowekwa mwilini mwako utakuwa umeisha
kabisa.
“Jamani siku arobaini zote hizo, nakuhitaji Edmund, nataka nikupe zawadi yako,”
alisema Samantha na kumkumbatia Edmund kimahaba.
“Halafu nataka uhame pale unapoishi, leo nikirudi Dar nitaenda kuongea na
madalali watutafutie nyumba nzuri, inabidi upate nyumba nzima mpenzi wangu ili
tuwe huru,” alisema msichana huyo na kumfanya Edmund aachie tabasamu hafifu.

58
Kama alivyomuahidi, kweli Samantha alivyorejea Dar, alipitiliza moja kwa moja
mpaka benki ambapo alitoa fedha za kutosha kupanga nyumba nzima pamoja na
kununua samani za ndani kwa ajili ya Edmund.
Akaenda kuonana na madalali wa nyumba ambapo alipelekwa mpaka kwenye
nyumba nzuri iliyopo Masaki. Kwa kuwa fedha hazikuwa tatizo kwake, siku
hiyohiyo alilipa na kukabidhiwa funguo.
Hakutaka kulaza damu, akaelekea kwenye maduka ya fenicha za kisasa ambapo
alinunua vitu vingi vya thamani na kukodi gari la kuvibeba na kuwachukua watu
maalum wanaofanya kazi ya kubuni mpangilio mzuri wa fenicha ndani ya nyumba.
Ilipofika jioni, kila kitu kilikuwa kimekamilika, akafunga nyumba hiyo na kurejea
nyumbani kwake, akitumia gari la kifahari, Jeep Grand Cherokee.
“Leo umetoa fedha nyingi sana benki, umezifaanyia nini?”
“Eeh! Baba kwani fedha si zangu au mi siruhusiwi kuchukua pesa?”
“Mi nimekuuliza tu kwa sababu siyo kawaida yako. Halafu leo kazini hukuwepo
kabisa, ulikuwa wapi?”
“Kuna vitu nilikuwa nimeenda kununua,” Samantha alimdanganya baba yake,
muda mfupi tangu aliporejea kutoka kwenye mizunguko yake. Hakutaka
kumwambia chochote kuhusu Edmund na alipanga kuendelea kufanya kila kitu
kuwa siri yake. Harakaharaka akapitiliza mpaka chumbani kwake kwani hakutaka
baba yake aendelee kumhojihoji akihofia kwamba anaweza kujichanganya kwenye
maelezo yake.
“Nataka uwe na furaha mpenzi wangu, nitafanya kila kitu ili nikuone unafurahi,”
Samantha alijisemea mwenyewe akiwa amejilaza kitandani kwake. Penzi la
Edmund lilikuwa likifukuta ndani ya moyo wake.
Siku hiyo ilipita, kesho yake Samantha akawahi kuamka kama kawaida yake na
kuanza kujiandaa kuelekea kazini. Ilikuwa ni lazima afike kwanza ofisini kwake
kwani alijua baba yake ameshaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu nyendo zake
hivyo anaweza kuwa anamfuatilia.
Kama kawaida yake, alitumia muda mrefu nyuma ya kioo, akajipamba na
kuufanya uzuri wake wa asili uzidi kuongezeka. Akachagua nguo nzuri za ofisini
na kuvaa, akamalizia kwa kujipulizia manukato mazuri ya bei mbaya, akatoka
akiwa ananukia mithili ya jini.

59
Akaenda mpaka kwenye maegesho ya magari yao ambapo aliingia kwenye gari
lake alilokuwa akilipenda zaidi, Jeep Grand Cherokee (New Model) na safari ya
kuelekea Mikocheni iliko ofisi yake ikaanza.
Njia nzima alikuwa akiendelea kumfikiria Edmund, kila alipokuwa anakumbuka
hali inayomtokea anapokumbatiana au kubusiana na kijana huyo, alikuwa akiachia
tabasamu pana na kugongagonga usukani.
Akawa na kazi ya kubadilisha nyimbo nzuri za mapenzi kwenye gari lake, hasa
zile alizokuwa akizipenda zaidi, mmoja wa V- Bozeman uitwao What is Love na
mwingine wa Good Enough, zote zikipatikana pia kama ‘soundtracks’ ya filamu
maarufu ya mwendelezo (series) iitwayo Empire ambayo nayo alikuwa akipenda
sana kuitazama anapokuwa nyumbani kwao.
Safari iliendelea, akafika mpaka eneo la Sinza Afrika Sana, eneo ambalo kwa mara
ya kwanza alikutana na Edmund baada ya dereva wa bodaboda aliyekuwa
amembeba kijana huyo kuligonga gari la Samantha kwa nyuma.
“Ama kweli mapenzi yana namna nyingi za kukutana, ajali imesababisha
nimempata mwanaume wa maisha yangu, nakupenda sana Edmund,” alisema
Samantha huku safari hii akishindwa kujizuia kuangua kicheko.
Kama gari lake lisingekuwa na vioo vyeusi (tinted) huenda watu ambao
wangefanikiwa kumuona wangehisi msichana huyo mrembo amechanganyikiwa
kwani alikuwa anacheka wakati hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya gari.

60
SURA YA SABA

Akaendelea na safari, alipofika eneo la Bamaga, mahali Edmund alipokuwa


akifanyia kazi, aliachia tena tabasamu na kuendelea na safari yake mpaka
Mikocheni. Akaingiza gari lake mpaka sehemu ya maegesho ambapo mlinzi wa
kike alifika haraka na kumpokea mkoba wake uliokuwa na ‘laptop’ na kumsaidia
kuuingiza mpaka ofisini kwake.
Kwa kuwa hakufika kazini hapo kwa siku kadhaa, alikuta kazi nyingi zikiwa
zimerundikwa kwenye meza yake, jambo ambalo lilimkasirisha kwani alijua
atachelewa kutoka kwa ajili ya safari ya kumfuata mpenzi wake Edmund.
“Naomba akija mtu yeyote kuniulizia mwambie niko bize,” alisema Samantha kwa
ukali akimpa maelekezo katibu muhtasi (secretary) wake, kisha akaanza kufanya
kazi harakaharaka. Alikagua mafaili ya mizigo iliyoingia na kutoka kwa siku zote
ambazo hakukaa ofisini, akakagua pia ripoti ya mhasibu kuhusu fedha zilizoingia
pamoja na zile zilizotumika.
Alihakiki oda za wateja na kuidhinisha wapelekewe bidhaa walizokuwa
wanazihitaji kisha baada ya hapo, akiwa ameshapunguza karibu nusu ya mafaili
aliyotakiwa kuyakagua, alimuita sekretari wake.
“Nimepunguza kazi kidogo lakini nina dharura nataka kutoka mara moja, baba
akiniulizia mwambie nimeenda kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi, hizo kazi
nyingine nitakuja kumalizia nikirudi,” alisema Samantha huku
akichezeshachezesha funguo ya gari mkononi.
Baada ya kumpa maelekezo hayo sekretari wake, alitoka mpaka kwenye maegesho
ya magari, akaingia kwenye gari lake na safari ya kuelekea Bagamoyo ikaanza
mara moja. Kabla hajafika mbali aliingia kwenye ‘supermarket’ na kununua
zawadi mbalimbalai kwa ajili ya Edmund kisha akaendelea na safari.
Njia nzima aliendelea kumuwaza Edmund, baada ya safari iliyochukua takribani
dakika arobaini, tayari Samantha alikuwa ameshawasili Bagamoyo. Akaenda
kupaki gari lake kwenye hoteli moja maarufu kwa ajili ya usalama kisha akakodi
bodaboda iliyompeleka mpaka kijijini kabisa alikokuwa anaishi mganga Shiwinga.
Baada ya kuwasili, Samantha na Edmund kama kawaida yao, waligandana kama
ruba kwa dakika zisizopungua tano, wakibusiana na kukumbatiana huku kila

61
mmoja akiwa na furaha ya ajabu. Mganga Shiwinga aliwaachia nafasi, yeye
akaendelea na shughuli zake za kuandaa dawa huku tabasamu pana likiwa
limechanua kwenye uso wake.
Baada ya kila mmoja kutulia, mganga Shiwinga hakutaka kupoteza muda,
aliwaingiza sehemu ya kufanyia tahajudi na kazi ikaanza. Tofauti na jana yake
ambapo wawili hao walianza kufanya ‘meditation’ kwa mara ya kwanza, safari hii
walionekana kuwa watulivu zaidi, wakionesha kuelewa walichokuwa wanakifanya.
Mganga Shiwinga aliwaongezea muda, wakafanya kwa saa moja mfululizo,
alipowaambia wafumbue macho, kila mmoja alionesha kuwa na mabadiliko
makubwa mno.
“Babu mbona najisikia hivi?”
“Unajisikiaje kwani Edmund.”
“Najiona kama nimekamilika mno, zile hofu, wasiwasi, mashaka na hisia za namna
hiyo hazipo tena. Akili yangu imetulia sana na nahisi kujiamini mno kuliko kipindi
chochote kwenye maisha yangu.”
“Sasa wewe hupendi kuwa hivyo?”
“Napenda sana babu, lakini mbona sijawahi kuwa hivi?”
“Kwa sababu hukuwahi kufanya tahajudi. Wewe Samantha unajisikiaje?”
“Na mimi najihisi hivyohivyo, halafu naona kama mwili wangu unakuwa mwepesi
sana, utafikiri mwanzo nilikuwa nimebebeshwa gunia la mchanga, kwa kifupi
najisikia raha sana, nataka tufanye tena,” alisema Samantha na kusababisha wote
waangue vicheko.
Mganga huyo akaendelea kuwaambia kuwa wakiendelea na utaratibu huo, kwa
muda wa wiki moja tu, nguvu zote mbaya zilizokuwa kwenye mwili wa Samantha
zitakuwa zimefifia kabisa kiasi kwamba hataweza kumsababishia tena madhara
Edmund hata wakikutana kimwili, jambo ambalo wote walilichekelea.
“Sijamaanisha mnaruhusiwa kukutana kimwili kabla hamjaoana, itabidi mjizuie
mpaka mipango yote ya ndoa itakapokamilika maana vijana wa siku hizi
hamuaminiki nyie,” alisema mganga Shiwinga, Edmund na Samantha wakatazama
na kukonyezana.

62
Mganga Shiwinga aliendelea kuwafundisha mambo mengi ambayo hakuna
aliyewahi kuyasikia hata mara moja.
“Binadamu tumeumbwa kwa namna ambayo nafsi zetu zinatafuta sana ukamilifu.
Na inapotokea nafsi yako inaanza kutafuta ukamilifu, ndipo unapoanza kujiuliza
maswali mengi yasiyo na majibu. Kwa mfano utajiuliza kwa nini ulizaliwa, lengo
la kuishi kwako hapa duniani ni nini na vitu vya mfano huo.
“Pia utajiuliza maswali mengi kuhusu mazingira yanayokuzunguka, kwa mfano
milima ilitokeaje? Inakuwaje mpaka mbegu inaota na kuwa mmea mkubwa,
utajiuliza kwa nini maua yanakuwa na rangi nyingi tofautitofauti na utajiuliza ni
nani anayesimamia mambo yote haya yanayoendelea kwenye ulimwengu.
“Ukifikia hatua hiyo, tunasema kwamba nafsi yako inakuwa imeanza kuamka au
kwa Kiingereza inaitwa ‘spiritual awakening’. Huu ni mwanzo wa safari ya kiroho
ambayo ni binadamu wachache sana wanaofikia. Wengine wanaifikia kwa kupitia
dini, kwamba unakuta mtu anakuwa ni wa maombi sana au anaswali sana, basi
huyo naye anakuwa amefikia hatua ya nafsi kuamka.
“Nafsi ikiamka inakufanya utambue kwamba kumbe mambo yote yanayoendelea
kwenye hii dunia, hayatokei kwa sababu yametokea tu, kwa lugha nyepesi
tunasema hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya. Watu wanazaliwa, watu
wanakufa, mimea inaota, inachanua na kutoa mbegu, upepo unavuma, mvua
zinanyesha, jua linawaka na mambo mengine chungu nzima, hakuna linalotokea
kwa bahati mbaya.
“Lazima ipo nguvu ambayo ndiyo inayoratibu mambo yote haya, swali ambalo
nafsi ya mtu iliyoanza kuamka inakuwa inajiuliza mara kwa mara ni je, ni nguvu
gani au ni nani anayeratibu mambo yote haya? Kwa wanaoamini katika dini,
wanaamini kwamba Mungu ndiye anayeratibu yote haya na ni katika kipindi hiki
ambacho hujisogeza karibu zaidi na Mungu wao.
“Kwa ambao hawaamini katika dini, pia huamini kwamba kuna nguvu kuu au kwa
Kiingereza huitwa ‘universal power’; ambayo ndiyo inayoamua nini kitokee wapi
na kwa sababu gani. Vyovyote ambavyo utaiita nguvu hii, iwe ni Mungu, nguvu
kuu au vyovyote, hii ndiyo nguvu inayoamua aina ya maisha utakayoishi, uwe
unajua au uwe hujui.
“Kwa kawaida kila binadamu anazalisha nguvu kwa hiyo ukiona mtu anafanikiwa
sana maishani mwake, maana yake ni kwamba anazalisha nguvu chanya na ukiona
mtu anaishi maisha ya kimaskini au anaandamwa na mabalaa ya kila aina, ujue

63
anazalisha nguvu, iwe anajua au hajui,” alisema mganga Shiwinga na kusababisha
wote wawili washushe pumzi ndefu, Samantha na Edmund wakatazamana kwani
walichokisikia kilikuwa kitu kipya kabisa kwao.
Mganga Shiwinga aliwafundisha vitu vingi mno, akaendelea kuwafanyia dawa
mpaka aliporidhika kwamba Samantha hawezi tena kumdhuru Edmund.
Akawaruhusu kuondoka huku akiwasisitiza kufuata maelekezo aliyowapa.
Wakaondoka na safari ya kurudi Dar es Salaam ikaanza. Kwa jinsi Samantha
alivyokuwa na shauku, aliona kama wanachelewa kufika. Hatimaye waliwasili Dar
na kwenda moja kwa moja mpaka Sinza Vatican.
“Edmund.”
“Nambie mpenzi wangu.”
“Yaani nimefurahi sana mganga Shiwinga alivyotusaidia na kurahisisha kazi.
Unajua nilipokuwa nafikiria kuendelea kukusubiri kwa siku arobaini nilikuwa
najisikia vibaya sana.”
“Siyo wewe tu mpenzi wangu, hata mimi pia nilikuwa najisikia vibaya lakini
nashukuru ameturahisishia kazi, si unaona hata hazijafika na tayari tupo huru!
Niambie unajisikiaje kuwa na mimi?”
“Yaani maneno ya kutosha kuelezea jinsi ninavyojisikia hayapatikani. Nakupenda
sana mwenzio,” alisema Samantha na kumkumbatia Edmund kwa nguvu, kila
mmoja akajihisi mkondo wa ajabu ukitembea ndani ya mishipa yake ya damu.
“Nakupenda pia mke wangu mtarajiwa.”
“Edmund! Umeniitaje?”
“Mke wangu mtarajiwa.”
“Whaoo! Nimefurahi sana kusikia ukiniita hivyo, natamani ufike muda ambao
utakuwa unaniita mkeo tena kihalali kabisa.”
“Usijali, hilo litatimia. Ila kuna kitu kimoja naomba nikuulize.”
“Uliza tu mpenzi wangu,” alisema Samantha huku akimtazama Edmund kwa
macho kama ya mtu anayesikia usingizi.”

64
“Siku ile uliniambia umepata nyumba Masaki lakini hapa ni Sinza Vatican.
Imekuwaje? Halafu unanihakikishiaje usalama wangu? Baba yako akijua kwamba
nipo hapa huoni kwamba huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yangu?”
“Ni kweli kuna nyumba nyingine nimepanga Masaki na ina kila kitu ndani lakini
nahisi kama baba alituma watu wanichunguze siku wakati nahamishia samani
nilizonunua kwa ajili yako. Machale yakanicheza kwa sababu namfahamu baba
yangu, akishatilia shaka jambo lazima ataufahamu ukweli ndiyo maana nimeamua
kutafuta huku kwenye mchanganyiko wa watu.”
“Maskini mpenzi wangu, si unatua fedha nyingi sana kwa ajili yangu?”
“Usijali kuhusu fedha, kwanza nilipanga ukirudi wewe ndiyo utafute madalali wa
kuipangisha ile nyumba ya kule kwa mteja mwingine mpaka kodi yangu
itakapoisha, baada ya hapo tutatafuta nyumba kubwa zaidi ili tuchanganye vitu vya
kule na huku, nataka kujenga familia na wewe mpenzi wangu.”
“Kwa hiyo na kule kuna vitu kama hivi?”
“Ndiyo, kama hivihivi, halafu unauliza kama hivi kwani umeviona vyote? Hebu
njoo nikutembeze ujionee mwenyewe,” alisema Samantha na kumpiga Edmund
kimahaba mgongoni kisha akamshika mkono Edmund, akaanza kumtembeza
kuanzia jikoni, wakaenda sehemu ya kulia chakula, wakaenda bafuni na chooni,
wakarudi tena sebuleni na mwisho wakaingia kwenye chumba cha kulala.
“Hapa ndiyo tutakapokuwa tunalala.”
“Whaoo!” Sijawahi kulalia kitanda kikubwa na kizuri kama hiki,” alisema Edmund
na kujirusha juu ya kitanda kikubwa na cha kisasa, Samantha naye akamfuata kwa
juu, wakawa wananesanesa juu ya godoro kubwa huku kila mmoja akionesha kuwa
na furaha kubwa ndani ya moyo wake.
Samantha ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza ‘uchokozi’, akamsogelea Edmund
wakiwa wamejilaza palepale juu ya kitanda, taratibu akausogeza mdomo wake
karibu na wa Edmund, wakagusanisha ndimi zao, kitendo kilichosababisha
Samantha aanze kuhema kwa nguvu mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio za
mita mia moja.
Hali haikuwa tofauti sana kwa Edmund, japokuwa nyumba hiyo ilikuwa na
kiyoyozi, alijikuta kijasho chembamba kikimtoka. Hakutaka kuamini kwamba
hatimaye ile siku aliyokuwa anaisubiri kwa hamu kubwa, hatimaye ilikuwa
imewadia.

65
Kwa jinsi alivyokuwa anampenda msichana huyo kwa dhati, kutoka ndani kabisa
ya moyo wake, hakutaka kulaza damu. Akamsogeza karibu zaidi na kumkumbatia
kwa nguvu huku wakiendelea kugandana kama ruba. Japokuwa Edmund hakuwa
fundi kwenye uwanja huo wa kikubwa, alijikakamua kadiri ya uwezo wake.
Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Samantha, japokuwa hiyo haikuwa mara yake ya
kwanza kubaki wawili tu na mwanaume chumbani, lakini mara zote alikuwa
akifanya hivyo kwa ajili ya kazi maalum na hakuwahi kuwa na hisia kama
alizokuwa nazo siku hiyo.
Hata wanaume wote aliowahi kuwa nao mara kadhaa chumbani, waliishia tu
kumbusu na kumkumbatia kisha akatimiza alichotumwa na baba yake lakini siku
hiyo hali ilikuwa tofauti kabisa. Kutoka ndani ya moyo wake alikuwa tayari
kumruhusu Edmund avuke mipaka ambayo hakuna mtu aliyewahi kuivuka tangu
azaliwe, kila mmoja akawa anavuta pumzi ndefu huku mapigo ya moyo
yakiongezeka.
“Edmund,” aliita Samantha kwa sauti ya kunong’ona iliyotokea puani, akajibiwa
kwa sauti ya kugugumia, Samantha akaendelea:
“Unanipenda kweli?”
“Nakupenda sana, tena zaidi ya sana.”
“Nikikupa mwili wangu hutanichezea na kuniacha?”
“Nakuapia Samantha, utakuwa peke yako ndani ya moyo wangu, niamini,” alisema
Edmund kwa sauti ya kubembeleza huku mikono yake ikiendelea kuvinjari sehemu
mbalimbali za mwili wenye mvuto wa kipekee wa msichana huyo mrembo, hali
iliyomfanya awe anaweweseka kama yupo ndotoni.
Kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo hali ilivyokuwa inazidi
kubadilika kwa kila mmoja, Edmund akawa anameza mate kama fisi aliyeona
mfupa, kwa ujanja wa hali ya juu akafanikiwa ‘kumsaula’ Samantha kisha na yeye
akafanya hivyohivyo, muda mfupi baadaye, wote wakawa wamevaa ‘suti za
kulalia’, wakagandana tena kama ruba, safari hii kila mmoja akilihisi vilivyo joto
la ngozi ya mwenzake.
Miguno ya kimahaba ikaendelea kusikika hapa na pale huku hisia tamu zikiendelea
kupita kwenye kichwa cha kila mmoja, kufumba na kufumbua sijui Edmund
alifanya nini, akampindua Samantha na sekunde chache baadaye, msichana huyo

66
alionekana kuuma meno kama mtu anayeugulia maumivu makali kuliko kawaida
lakini Edmund hakujali chochote.
Alitumia nguvu kubwa na hatimaye akafanikiwa kuivunja ‘ngome’ imara ya
mpinzani wake, Samantha akashindwa kujizuia na kupiga kelele kwa nguvu
akiugulia maumivu makali aliyokuwa anayahisi lakini bado Edmund hakujali,
akaendelea kufanya alichokuwa anakifanya. Ilibidi Samantha atumie nguvu,
akamtoa na kumsukumia Edmund pembeni huku akiendelea kuugulia maumivu
makali.
“Mungu wangu, kumbe ulikuwa unasema kweli? Ahsante Samantha kwa zawadi
hii,” alisema Edmund huku akionesha kushtushwa mno na alichokiona pale
kitandani. Eneo lote lilikuwa limebadilika na kuwa kama machinjioni, rangi
nyekundu ilisambaa kila sehemu.
Samantha hakumjibu chochote zaidi ya kuendelea kuugulia maumivu makali,
ikabidi Edmund aanze kazi nyingine ya kumbembeleza lakini haikuwa rahisi.
Samantha alionesha kumchukia mno Edmund kwa wakati huo na hakutaka hata
kumsikia, Edmund akawa anaendelea kumbembeleza kwa maneno ya upole
yaliyoonesha kumuingia msichana huyo, taratibu hasira zake zikaanza kupungua
lakini bado hakutaka Edmund amguse huku akimlaumu kwa kutomuonea huruma.
“Sasa unafikiri nitarudije nyumbani?” alisema Samantha kwa sauti ya chini
iliyoonesha bado yupo kwenye maumivu makali. Kabla hata Edmund hajajibu
chochote, simu ya msichana huyo ilianza kuita mfululizo, awali hakutaka hata
kuisikia lakini alipoona inaendelea kuita, ilibidi amuagize Edmund amchukulie
kwani hakuwa hata na uwezo wa kuinuka pale alipokuwa.
“Uko wapi wewe mtoto? Nataka urudi nyumbani haraka iwezekanavyo, nakupa
dakika kumi,” aling’aka baba yake Samantha na kabla hajajibu chochote, tayari
simu ilikuwa imeshakatwa.
“Vipi!”
“Baba! Anafoka hatari.”
“Sasa itakuwaje?”
“Hebu fanya haraka nenda hapo dukani kaninunulie dawa inaitwa Flamar-X,
inasaidia kupunguza maumivu, ni lazima niende nyumbani sasa hivi, inaonesha
kuna tatizo kubwa,” alisema Samantha kwa sauti iliyoonesha kwamba bado

67
anaugulia maumivu, harakaharaka Edmund alikimbilia bafuni na muda mfupi
baadaye, alitoka akiwa ameshaoga.
Akajiandaa harakaharaka na kutoka kuelekea dukani. Kwa kuwa alikuwa mgeni
mtaani hapo, ilimlazimu kuuliza kwa wenyeji, akaelekezwa ambapo muda mfupi
baadaye tayari alikuwa ameshapata alichoagizwa. Akarudi ndani na kumkuta
Samantha naye ameshaenda kuoga.
Akawa anajiandaa na muda mfupi baadaye, tayari alishamaliza, akanywa dawa.
“Inabidi ujifunze kuendesha gari bwana, huoni kama sasa hivi ungenisaidia
kunipeleka mpaka nyumbani? Yaani naumwa hapa najikaza tu,” alisema
Samantha, akamkumbatia Edmund na kumbusu mdomoni kimahaba kisha
wakaagana.
“Usiende popote, funguo zile pale mezani,” alisema Samantha na kutoka huku
akijivuta mpaka kwenye gari lake lililokuwa limepaki nje ya nyumba hiyo.
Akaingia na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwao.
Huku nyuma, Edmund alibaki akichekacheka mwenyewe kama mwendawazimu.
Hakutaka kuamini kwamba kweli Samantha, licha ya uwezo mkubwa wa kifedha
na urembo usio na kifani, hakuwa akimjua mwanaume mpaka umri huo. Kwake
huo ulikuwa ni zaidi ya ushindi, akajiapiza kumpenda kwa moyo wake wote na
kujiepusha na jambo lolote ambalo lingeweza kumuumiza moyo.
Harakaharaka alibadilisha mashuka chumbani na kwenda kuyaloweka bafuni kwa
ajili ya kuyafua kisha kwa mara nyingine akaanza kukagua kitu kimoja baada ya
kingine ndani ya nyumba hiyo.
Maisha aliyokuwa akiishi awali yalikuwa tofauti kabisa na maisha mapya. Kila
kitu kilikuwa kigeni kwake, akajikuta akipiga magoti na kuinua mikono juu kama
ishara ya kumshukuru Mungu kwani japokuwa alikuwa na ndoto za siku moja
kuishi maisha ya kifahari kama hayo, alikuwa anajua isingekuwa rahisi kuyafikia
kama ilivyotokea.
Baada ya kuridhika, alienda kukaa kwenye masofa ya kifahari pale sebuleni na
kuwasha runinga kubwa ya ukutani (flat screen). Akawa anaendelea kuchekacheka
mwenyewe, wakati mwingine akijihisi yupo kwenye ndoto tamu ambayo itaisha
muda wowote.
***

68
“Umefanya nini Samantha!”
“Kwani vipi baba?”
“Unaweza kuniambia ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini? Usinifiche kwa
sababu najua kila kitu.”
“Nilikuwa kwa rafiki yangu Aneth, leo ni ‘bethidei’ yake.”
“Usinidanganye Samantha, najua kila kitu,” alisema baba yake Samantha huku
akionesha kuchanganyikiwa kuliko kawaida. Licha ya ukali wake wote, Samantha
hakuwahi kumuona baba yake akiwa kwenye hali kama hiyo.
Alionesha kuchanganyikiwa mno, akawa anaongea peke yake kama
mwendawazimu huku akitembea kutoka kona moja ya sebule mpaka nyingine.
“Mama kwani nini kimetokea?”
“Maduka mawili ya baba yako yameungua katika mazingira ya kutatanisha, tena
yote kwa wakati mmoja. Lile la Kariakoo na jingine la Posta,” alisema mama yake
Samantha, kauli ambayo ilimshtua mno Samantha, akajua kazi imeanza.
Harakaharaka alikimbilia chumbani kwake na kujifungia. Alijua lazima baba yake
amejua kwamba ameingiliwa na mwanaume kwani siku zote alikuwa akimuonya
kwamba kitendo cha kufanya mapenzi na mwanaume yeyote, kingemaanisha
kuanza kupotea kwa utajiri mkubwa walioutafuta kwa kipindi kirefu.
Samantha aliendelea kuwaza kwa muda mrefu lakini baadaye akaamua kupiga
moyo konde kwani alichokuwa anakitaka kwa kipindi kirefu, ilikuwa ni
kuondokana na maisha ya kitumwa, jambo ambalo hatimaye lilikuwa limetimia.
Akili zake zilitua kwenye tukio walilolifanya muda mfupi uliopita na Edmund,
japokuwa alikuwa kwenye maumivu makali, alishindwa kulizuia tabasamu pana
lisiupambe uso wake.
Kwa kitendo walichokifanya na Edmund, alijikuta akizidi kumpenda kijana huyo
na kutamani muda wote awe pembeni yake. Aliendelea kuwaza huku tabasamu
pana likiwa limemtawala, hakutaka kuumiza kichwa chake kwa kuendelea kuwaza
matatizo ya baba yake kwani aliona kama amejitakia.
Kutokana na jinsi alivyokuwa amechoka, alijikuta akipitiwa na usingizi mzito.
Akalala fofofo mpaka alipokuja kuzinduliwa na kelele za mlango uliokuwa

69
unagongwa na mama yake. Harakaharaka akafungua mlango, mama yake akaingia
chumbani kwake.
“Samantha.”
“Abee mama.”
“Mbona umelala muda huu wakati siyo kawaida yako?”
“Najihisi kuchoka mama. Vipi baba amefikia wapi?”
“Ameondoka, yaani amechanganyikiwa kuliko kawaida. Hakuna kitu
kilichookolewa kwenye maduka yote mawili, vitu vyote vimeteketea kabisa.
Lakini kwa sababu ya ubishi wa baba yako, kila siku mimi namwambia aachane na
huu utajiri wa kishirikina hanisikii, ngoja yamkute,” alisema mama yake Samantha
huku akikaa vizuri kwenye kitanda cha binti yake.
Samantha hakuwahi kumsikia mama yake akizungumzia jambo hilo hata siku
moja. Mara zote, alikuwa anajua kwamba mama yake anamuunga mkono baba
yake, kauli hiyo ikamfanya ashushe pumzi ndefu huku akijishauri kama amueleze
ukweli kuhusu Edmund au la!
“Vipi, mbona unaonekana una mawazo?”
“Nafikiria matatizo yaliyomtokea baba.”
“Achana naye, anazeeka vibaya huyo. Halafu hivi wewe hujawahi kufikiria
kutafuta mwanaume wa kukuoa hata mara moja? Natamani kuwa na wajukuu
kama wanawake wenzangu, huu utajiri si lolote kwani tutakufa na kuuacha,”
alisema mama yake Samantha, kauli iliyozidi kumuweka njia panda mwanaye.
Kuna wakati alihisi huenda mama yake anamtega akitaka kuujua ukweli lakini
upande mwingine ukamfanya kuamini kwamba alikuwa anamaanisha kile
anachokisema.
Mwisho aliamua kupiga moyo konde, akakaa pale kitandani vizuri na kumgeukia
mama yake.
“Mama.”
“Abee mwanangu.”
“Kuna jambo nimekuwa nataka kukwambia kwa kipindi kirefu lakini nimekuwa
naogopa.”

70
SURA YA NANE

“Wewe na baba yako lenu si moja! Mnaona utajiri ndiyo jambo la maana. Angalia
hata hutaki kuwa karibu na mimi mama yako, wewe na baba yako tu! Haya
niambie nini kimekusibu,” alisema mama yake Samantha huku na yeye akijiweka
sawa kutaka kusikia mwanaye anataka kumwambia nini.
“Naomba unisamehe lakini kama nitakuwa nimekukosea mama.”
“Usijali mwanangu, kuwa huru kuzungumza kitu chochote unachotaka. Mimi
ndiyo mama yako.”
“Mi nina mpenzi mama.”
“Mpenzi? Nilivyokwambia kuhusu suala la mchumba nilitaka uniachie mimi ndiyo
nikusimamie kukutoa hayo mashetani yanayoua wanaume kwanza ndiyo mengine
yafuatie. Wewe si unajua matatizo yako? Sasa naye si atakufa kama hao wengine
walivyokufa?”
“Hapana, hawezi kufa mama. Kuna jambo nimefanya ila nakuomba sana
usimwambie baba,” alisema Samantha kwa sauti ya chini, akaanza kumsimulia
mama yake kila kitu, kuanzia jinsi alivyokutana na Edmund, alivyomkosakosa
kumuua na yote yaliyofuatia baada ya hapo.
“Mh! Makubwa, hebu kaniletee maji ya kunywa kwanza nishushie,” alisema mama
yake Samantha huku akishusha pumzi ndefu. Samantha akajikaza kisabuni na
kuinuka pale kitandani kwani bado alikuwa anahisi maumivu makali kutokana na
tukio lililotokea kati yake na Edmund, saa chache zilizopita.
Mabadiliko ya namna alivyokuwa anatembea, yalimshtua mno mama yake, kwa
kuwa yeye ni mtu mzima, akawa ameshaelewa kilichotokea ingawa bado alikuwa
na shauku kubwa ya kutaka kusikia kutoka kwa Samantha mwenyewe.
Muda mfupi baadaye, Samantha alirejea akiwa na chupa ya maji baridi pamoja na
glasi, akammiminia mama yake kisha akarudi kukaa kitandani. Mama yake
akayanywa maji hayo huku akiendelea kumchunguza kwa macho ya udadisi.
Alipomaliza akakaa vizuri tena pale kitandani na kumgeukia Samantha.
“Kuna jambo moja bado hujaniambia ukweli.”
“Jambo gani mama?”

71
“Hujamaliza kuniambia kuhusu wewe na huyo Edmund wako. Mmeshawahi
kukutana kimwili mara ngapi?” alihoji mama yake Samantha huku akiwa
amemkazia macho mwanaye. Swali hilo lilimshtua mno Samantha kwani alijua
mama yake ameshamshtukia na miongoni mwa mambo aliyokuwa akimuonya
mara kwa mara, ilikuwa ni kutokutana kimwili na wanaume.
“Mbona hujibu?” mama yake Samantha alizidi kumbana binti yake kwa maswali,
Samantha akawa anang’atang’ata kucha huku akiogopa hata kumtazama mama
yake usoni. Baada ya kumbana sana, ilibidi Samantha awe mkweli, akamwambia
kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yao ya kwanza.
“Nilijua tu! Niliposikia maduka mawili ya baba yako yameungua nilijua ni kwa
sababu gani, si ajabu hata yeye mwenyewe anajua na ndiyo maana
amechanganyikiwa sana. Umekosea mwanangu! Umefanya kosa kubwa sana.”
“Nisamehe mama!”
“Mimi sina tatizo, ila baba yako anaweza hata kukuua, ilibidi uniambie kabla!
Majanga makubwa sana yanakuja,” alisema mama yake Samantha huku naye
akionesha kuchanganyikiwa mno. Ukimya mkubwa ukapita kati yao.
Walikuja kuzinduliwa na kelele za mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu,
wakajua kazi imeanza kwani hakuwa mwingine zaidi ya baba yake Samantha.
“Fungua kabla sijauvunja huu mlango,” alifoka baba yake Samantha, ikabidi mama
yake Samantha ndiyo ainuke na kuufungua mlango huo ambao Samantha aliufunga
kwa ndani alipompelekea mama yake maji.
“Kumbe wewe na mwanao ndiyo mnafundishana ujinga si ndiyo?” alifoka baba
yake Samantha baada ya kumkuta mkewe akiwa ndani ya chumba cha binti yao.
“He! Mwenzetu vipi? Mbona umekuwa hivyo? Hebu tulia utueleze nini
kimetokea.”
“Wewe ni binti yako mnajua! Mnajua kabisa mlichokifanya, ‘sheli’ yangu ya
Kibaha nayo imewaka moto,” alizidi kufoka baba yake Samantha. Kila mmoja
akapatwa na mshtuko kufuatia habari hizo kwani ndani ya muda mfupi tu, vitega
uchumi vitatu vilikuwa vimeteketea kwa moto.
Duka la Kariakoo na jingine la Posta yote yalikuwa yameungua na sasa ilikuwa ni
kituo cha mafuta cha Kibaha.

72
“Umeanza umalaya si ndiyo? Sasa leo nitakukomesha,” alisema baba yake
Samantha huku akikunja mikono ya shati alilokuwa amevaa na kuvua tai yake
lakini kabla hajafanya chochote, mama yake Samantha aliingilia kati kwani alijua
mumewe alivyokuwa na hasira chochote kinaweza kutokea.
Kitendo cha yeye kuingilia kati na kuanza kumtetea Samantha ilikuwa sawa na
kumwagia petrol kwenye moto, kwa jazba kama faru aliyejeruhiwa, baba yake
Samantha alimkamata mkewe na kuanza kumshushia kipigo kwa hasira.
Samantha alitumia upenyo huo kuchoropoka, alichokumbuka kubeba ilikuwa ni
pochi yake ndogo tu, akatoka mbio mpaka nje akiwa pekupeku, akikimbia mpaka
getini, jambo lililomshangaza sana mlinzi wao.
“Kuna nini Samantha?”
“Baba anamuua mama, nifungulie geti,” alisema Samantha, harakaharaka mlinzi
huyo bila kufikiria mara mbili akamfungulia Samantha mlango. Japokuwa alikuwa
anasikia maumivu makali, Samantha alijikaza na kukimbia mpaka barabarani. Kwa
bahati nzuri, kuna pikipiki ilikuwa inakuja, akaipungia mkono kwa nguvu huku
akiwa amechanganyikiwa, ikasimama.
Kabla hata hajapanda, alisikia geti lao likifunguliwa, akamuona baba yake akitoka
mbio kumfukuza, harakaharaka akapanda na kumhimiza dereva huyo kuondoka
kwa kasi kubwa, jambo alilolitii. Akaondoa pikipiki kwa kasi kubwa na kumuacha
baba yake Samantha mita chache nyuma, akiendelea kutoa vitisho vya hali ya juu.
Alipoona Samantha amemkimbia, harakaharaka alirudi ndani na kuwasha gari,
wakiwa umbali wa takribani mita mia tatu, Samantha aligeuka nyuma na kuona
gari likitoka kwa kasi kwenye geti, akajua ni baba yake ameamua kumfuatilia.
Kwa jinsi alivyokuwa anamfahamu baba yake, alijua akizembea anaweza
kumdhuru vibaya, akamhimiza dereva kuongeza kasi na kumtaka wapite njia za
vichochoroni, jambo ambalo alilitii.
“Kwani tunaenda wapi sista?”
“Sinza Vatican, pita vichochoroni baba anakuja, ukinifikisha nitakupa kiasi
chochote cha fedha unachokitaka,” alisema Samantha huku akihema kwa nguvu,
utulivu ukiwa umemuisha kabisa.
Kwa bahati nzuri, dereva huyo wa bodaboda alikuwa na uzoefu wa kutumia
pikipiki hiyo, akafanya kama mteja wake alivyomuelekeza, muda mfupi baadaye

73
wakawa wameshampoteza kabisa baba yake Samantha. Bodaboda ikawa inakatiza
vichochoro kwa kasi kubwa, hali iliyomshtua kila aliyeiona.
***
“We kijana! Kijanaa!”
“Naam bosi, unahitaji usafiri?”
“Kuna bodaboda imepita sasa hivi kwa kasi kubwa imeelekea huku vichochoroni,
umeiona?”
“Ndiyo mzee.”
“Nataka ufanye kila unachoweza kuhakikisha tunaikimbiza mpaka tunaipata.
Nitakupa kiwango chochote cha fedha unachokitaka. Hili gari naweza kulipaki
hapa?”
“Hakuna tatizo, lipaki tu kuna ulinzi wa kutosha ingawa itabidi ulipie.”
Sekunde chache baadaye, baba yake Samantha naye alikuwa juu ya bodaboda,
akifuata njia ileile ambayo yule dereva aliyempakiza mwanaye amepitia, akawa
anamhimiza dereva kuzidi kuongeza kasi.
Sekunde chache baadaye, baba yake Samantha naye alikuwa juu ya bodaboda,
akifuata njia ileile ambayo yule dereva aliyempakiza mwanaye amepitia, akawa
anamhimiza dereva kuzidi kuongeza kasi.
Dereva bodaboda aliyekuwa amempakiza Samantha alizidi kuchanja mbuga,
akawa anakatiza mitaani kwa kasi kubwa huku akitumia uwezo wake wote
kuhakikisha anatimiza alichoambiwa na mteja wake.
Huku nyuma, dereva mwingine aliyekuwa amembeba baba yake Samantha naye
alikuwa akikimbiza pikipiki kwa kasi kubwa akijaribu kuwafuata akina Samantha.
Kila alipohisi amepotea, alikuwa akisimama na kuuliza kwa wenyeji kama
wameiona bodaboda yoyote iliyopita kwa kasi eneo hilo, wakawa wanaelekezwa.
Safari iliendelea kwa kasi kubwa utadhani madereva wapo kwenye mashindano ya
mbio za pikipiki maarufu duniani, MotoGP lakini haikuwa hivyo. Baada ya
kukimbizana kwa umbali mrefu, dereva aliyekuwa amembeba Samantha
alifanikiwa kuwapoteza ‘maboya’ baada ya bodaboda nyingine kadhaa kuingia
katikati yao.

74
“Washenzi kabisa hawa lakini najua wameelekea wapi, hebu geuza tuelekee
Masaki,” alisema baba yake Samantha kwa hasira baada ya kugundua kuwa tayari
wamewaacha kwenye mataa. Dereva huyo wa bodaboda alifanya kama
alivyoambiwa, safari ya kuelekea Masaki ikaanza.
Upelelezi wa chini kwa chini alioufanya mzee huyo kwa kuwatumia vijana wake,
ulimfanya afahamu kwamba siku mwanaye alipotoa fedha nyingi benki kwa mara
ya kwanza, alionekana akizungumza na madalali wa nyumba wa Masaki.
Baada ya kufuatilia sana, alifanikiwa kuifahamu mpaka nyumba aliyopangisha
japokuwa hakutaka kuonesha dalili zozote kwamba anafahamu mwanaye anafanya
nini. Alichokuwa anakisubiri ilikuwa ni kwenda katika muda ambao Samantha
hajategemea ili abaini ukweli wa alichokuwa anakifanya.
Baada ya bodaboda kukimbia kwa umbali mrefu, hatimaye waliwasili Masaki,
akamuelekeza dereva huyo kwenda moja kwa moja mpaka kwenye nyumba
ambayo alikuwa na taarifa kwamba Samantha ndiye aliyepangisha.
“Huyu si anajifanya mjanja? Sasa leo nitamdhihirishia kwamba mimi nina akili
zaidi yake,” alisema baba yake Samantha, akashuka kwenye bodaboda akiwa
amevimba kwa hasira kama faru aliyejeruhiwa.
Akatembea harakaharaka na kwenda mpaka kwenye mlango wa nyumba hiyo,
akaanza kugonga kwa nguvu huku akilitaja jina la Samantha.
***
Baada ya kufanikiwa kuwaacha dereva wa bodaboda na baba yake, Samantha
alimuamuru dereva wake kupita njia ya kuzunguka na hatimaye wakawasili Sinza
Vatican bila kushtukiwa.
Kwa kuhofia kwamba dereva huyohuyo akibanwa anaweza kueleza ukweli mahali
alikompeleka, Samantha alijifanya kuelekea upande mwingine kabisa.
Alipohakikisha dereva huyo wa bodaboda ameshaondoka, harakaharaka alikimbia
mpaka pale kwenye nyumba aliyopanga.
Edmund aliyekuwa akitazama runinga kwa ‘kujiachia’, akiwa amejilaza kwenye
masofa sebuleni, alishtuka baada ya kusikia mlango ukigongwa kwa nguvu,
harakaharaka akainuka na kwenda kufunua pazia, akachungulia nje.
“Samantha! Mungu wangu,” alisema Edmund baada ya kumuona mpenzi wake
huyo akiwa katika hali isiyo ya kawaida. Harakaharaka akafungua mlango ambapo

75
Samantha aliingia kwa kasi, miguuni akiwa pekupeku na akiwa hajajipamba kama
ilivyo kawaida yake kila wanapokutana, Edmund akajua lazima kuna tatizo kubwa.
“Vipi mpenzi wangu?”
“Funga milango yote, funga kwa funguo na uzime kila kitu,” alisema Samantha na
kupitiliza mpaka chumbani, Edmund akazidi kupigwa na butwaa. Hata hivyo,
ilibidi afanye kama alivyoelekezwa, akafunga milango yote na kuzima runinga na
redio, akamfuata Samantha chumbani.
“Vipi nini kimetokea kwani?” alisema Edmund kwa sauti ya upole, Samantha
akamkumbatia kwa nguvu huku akitetemeka. Ilimchukua dakika kadhaa kutulia na
kurudi kwenye hali yake ya kawaida ambapo alianza kumueleza kila kitu
kilichotokea.
Taarifa hizo zilimshtua pia Edmund lakini akajikaza kisabuni na kuendelea
kumbembeleza Samantha ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.
“Nahatarisha maisha yangu kwa sababu yako Edmund, siku ukiniumiza moyo
wangu basi huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yangu,” alisema Samantha
huku akiendelea kulia lakini Edmund kwa kutumia ushawishi wa hali ya juu,
aliendelea kumbembeleza mpaka akatulia.
“Naona umechafuka sana na mwili wako wote umelowa jasho, twende
nikakuogeshe mpenzi wangu,” alisema Edmund, kauli ambayo ilimfurahisha sana
Samantha, akamkumbatia Edmund kwa mahaba mazito. Edmund alitimiza wajibu
wake kwani alijua ni mambo gani yanayoweza kumfanya Samantha akarudi
kwenye hali yake ya kawaida.
Baada ya kumaliza kumuogesha Samantha kama mtoto mdogo, walirudi chumbani
na kuendelea na mazungumzo yao ya hapa na pale, huku mara kwa mara msichana
huyo mrembo akimsisitiza kwamba siku akigundua kwamba ana mwanamke
mwingine, atayakatisha maisha yake kwa kujiua.
Ndani ya muda mfupi tu aliokaa na Edmund, Samantha alisahau kabisa kila kitu
kilichotokea, wakawa wanapiga stori na kucheka kwa furaha, muda ukawa
unayoyoma na hatimaye giza likaingia.
“Leo nataka kulala na wewe, siwezi kurudi nyumbani kwa sababu najua bado baba
ana hasira kali juu yangu, anaweza hata kunimeza mzimamzima,” alisema
Samantha, wazo ambalo Edmund aliliunga mkono kwani na yeye alikuwa

76
akijisikia raha sana kukaa karibu na msichana mrembo kiasi hicho, aliyekamilika
kwa kila kitu.
***
Baada ya kugonga mlango kwa muda mrefu bila kupata majibu yoyote, baba yake
Samantha aliamua kusogea pembeni na kuanza kuichunguza vizuri nyumba hiyo.
Hata hivyo hakuona kama kulikuwa na dalili ya kuwepo kwa mtu yeyote ndani
yake, akamfuata yule dereva wa bodaboda ambaye bado alikuwa akimsubiri.
Akamuelekeza kumpeleka mpaka kwenye mgahawa mmoja uliokuwa jirani na
eneo hilo ili wawe wanafuatilia kama kuna mtu yeyote ataingia kwenye nyumba
hiyo. Hata hivyo, baada ya kukaa kwa zaidi ya dakika arobaini, hakukuwa na dalili
za mtu yeyote kuingia wala kutoka kwenye nyumba hiyo.
“Twende nirudishe pale uliponitoa, tutarudi tena baadaye,” alisema baba yake
Samantha huku akionesha kuwa na hasira kali. Safari ya kurejea Upanga ikaanza
huku njia nzima akiendelea kuangaza macho huku na kule kama atamuona
Samantha.
Dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wameshawasili pale alipoacha gari lake,
akamlipa dereva wa bodaboda fedha zake kisha akachukua gari lake na kurudi
nyumbani kwake.
Alipoingiza gari na kuingia ndani, alishtushwa na hali aliyomkuta nayo mkewe
ambaye alikuwa amelala sebuleni akiugulia maumivu makali ya tumbo
aliloumizwa na mumewe katika purukushani chumbani kwa Samantha.
Kwa hali aliyomuona nayo, alijikuta hasira zote zikimuisha na kuanza kujilaumu
kwa alichokifanya. Japokuwa alikuwa akisifika kwa ukali, hakuwahi kumfanyia
vitendo vya udhalilishaji mkewe hata mara moja tangu walipooana miaka mingi
iliyopita, akajikuta akijilaumu sana kwa kilichotokea.
Ilibidi awe mpole na kumuomba radhi mkewe ambaye bila hiyana alikubali
kumsamehe, ikabidi ampigie simu daktari wa familia hiyo ambaye alifika haraka
nyumbani hapo na kuanza kumpima mama Samantha kabla ya kumpa dawa za
kutuliza maumivu.
Dawa alizopewa zilisaidia kumpunguzia maumivu, mumewe ambaye sasa hasira
zote zilikuwa zimeisha na kumfanya abaki na majuto, alimsaidia kumuinua na
wakaelekea chumbani kwao.

77
“Mke wangu narudia tena kukuomba msamaha lakini naomba unisaidie kuniambia
ukweli, najua lazima Samantha atakuwa amekwambia ni mwanaume gani
anayemzuzua.
“Nakuomba uniambie au unielekeze huyo mwanaume ni nani na anaishi wapi, nipo
tayari hata kutuma watu wakampige risasi afe, siwezi kukubali utajiri wangu
niliouhangaikia kwa kipindi kirefu leo hii upotee kirahisi namna hii,” alisema baba
yake Samantha huku akionesha kumaanisha kile alichokisema.
Mama yake Samantha akashusha pumzi ndefu na kumtazama mumewe.
***
Baada ya kumpoteza maboya baba yake, hatimaye Samantha alifika karibu na
nyumba ambayo alimpangishia Edmund. Kwa kuhofia kujulikana kwa siri hiyo,
aliamua kutofika kabisa nyumbani hapo akiwa na yule dereva wa bodaboda.
“Nishushe hapahapa kaka,” alisema Samantha huku akimpigapiga begani dereva
huyo wa bodaboda ikiwa ni ishara ya kumhimiza asimamishe bodaboda.
“Shilingi ngapi itakuwa?” aliuliza Samantha na kufungua mkoba wake ambapo
kabla hata hajajibiwa alichomoa noti zaidi ya nne na kumkabidhi dereva huyo wa
bodaboda, bila hata kumuaga alianza kutembea kwa harakahara kuelekea kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi Edmund.
Kwa kuwa alikuwa na ufunguo wa ziada, hakubisha hodi zaidi ya kufungua na
kumkuta Edmund akiwa amejilaza kwenye kochi sebuleni akitazama mpira kupitia
runinga kubwa iliyokuwa ukutani sebuleni hapo.
“Waoh! Karibu sana jamani, karibu kipenzi cha roho yangu,” alisema Edmund
baada ya kumuona Samantha akiingia sebuleni hapo na kunyanyuka kwenda
kumlaki kwa furaha ya ajabu.
“Ahsante, vipi mzima hujambo Edmund wangu?” aliitikia Samantha na kumjulia
hali Edmund huku akimbusu shavuni na kumkumbatia kwa nguvu zote.
“Mbona unaonekana kutokuwa na furaha Samantha, kuna nini tena mama?”
“Si baba, sina furaha tena na maisha yangu”
“Kafanya nini tena?”
“Yaleyale ya kuingilia uhuru wa maisha yangu, hataki kuelewa kabisa kuwa kwa
sasa nahitaji kuishi maisha ya ajabu ya kitumwa,” alisema Samantha huku

78
akimlalia kifuani Edmund na kuanza kutokwa na machozi yaliyolowanisha kifua
cha Edmund.
Bila kupoteza muda, Edmund alianza kumfuta machozi Samantha kwa kutumia
kiganja na kisha kumshika mkono na kuingia naye chumbani ambapo alimkalisha
kitandani na kuanza kumbembeleza.
“Alipokuita alikwambia nini?” aliuliza Edmund huku akimshika Samantha kiunoni
hali iliyoamsha hisia kali kwa msichana huyo na kuanza kujinyonganyonga badala
ya kujibu swali alilokuwa ameulizwa na Edmund.
“Unajua Edmund umemtia hasara kubwa sana baba?”
“Mimi? Kivipi?” aliuliza Edmund kwa hamaki kubwa huku akimtazama Samantha
kwa macho yenye maswali mengi.
“Kitendo cha mimi kufanya mapenzi na wewe kimesababisha kuungua kwa
maduka yote ya Kariakoo na Posta, ndiyo maana alinipigia simu kwa hasira,”
alisema Samantha na kumtazama machoni Edmund huku akilegeza macho na
kumuweka katika wakati mgumu Edmund.
“Mmh, sasa ikawaje?”
“Hivi ninavyokuambia nimemkimbia baba, hata hivyo alikuwa akinifuatilia lakini
tumempoteza njiani nikiwa na bodaboda,” alisema Samantha na kumsimulia kwa
kirefu kisa chote kilichotokea katika familia yake.
Edmund alishusha pumzi ndefu na kuanza kutafakari mambo mbalimbali, haraka
sana Samantha alimshika mikono na kumkumbatia huku akimtaka kutokuwa na
hofu kwani alikuwa amejitolea mhanga kwa ajili ya penzi la kijana huyo.
Wakibaki wamekumbatiana huku kila mmoja akisikiliza joto la mwenzake, hali
iliyosababisha wote kujikuta wakishikwa na mhemko wa ajabu.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, Edmund alianza uchokozi kwa
kumtekenya Samantha maeneo mbalimbali ya mwili, hali iliyomsisimua msichana
huyo mrembo kwa kila idara, umbo hadi sura na kujikuta akimsukumia Edmund
kitandani.
Harakaharaka bila kupoteza muda, walijikuta wakiwa kama walivyotoka kwenye
matumbo ya mama zao, wakipashana joto kwa staili mbalimbali na kuanza
kulisakata kabumbu bila uwepo wa refa.

79
***
“Hutaki kusema siyo?” alizidi kufoka Baba Samantha hali iliyozidisha hofu kwa
mkewe, kwani alimjua vyema mumewe linapokuja suala la mali hakuwa na utani
hata kidogo.
“Jamani baba Samantha, binti yako hutumia muda mwingi kuwa na wewe, mimi
nitajuaje mambo yake?” alijibu mama Samantha na kumwangalia mumewe kwa
macho ya hofu.
Wakati mazungumzo yakiendelea, mara simu ya baba Samantha iliita na kuitoa
haraka mfukoni ambapo namba ya mpigaji ilikuwa ngeni na kuipeleka haraka sana
sikioni baada ya kuipokea.
“Unasema kweli?”
“Eeh, Mungu wangu, aaah, ahsante kwa taarifa, ahsante sana,” alisema Baba
Samantha huku machozi yakianza kumchuruzika.
“Nini tena mume wangu?” aliuliza Mama Samantha baada ya kuhisi kitu kisicho
cha kawaida.
“Unaona sasa Mama Samantha, unaona?”
“Nimeona nini tena jamani mume wangu, mbona sikuelewi jamani?”
“Yote haya kasababisha mwanao, nasema safari hii namwaga ubongo wa mtu.
Sikubali,” alizidi kulalama Baba Samantha.
“Kuna nini?” Mama Samantha aliuliza tena huku safari hii akinyanyuka alipokuwa
amekaa na kumsogelea zaidi mumewe.
“Mabasi yangu mawili yamegongana uso kwa uso na kuua abiria zaidi ya 30,
mbaya zaidi hapa nimepigiwa simu na afisa wa Sumatra akinijulisha kuwa baada
ya trafiki kufanya uchunguzi wamebaini kuwa ajali hiyo inatokana na uzembe wa
madereva, hivyo kampuni yangu ya usafirishaji imefungiwa kwa muda
usiojulikana,” alisema Baba Samantha na kuendelea kulia kwa kwikwi nzito.
“Basi mume wangu jikaze, hakuna haja ya kulia kwa sababu pesa zinatafutwa.”
“Inauma mke wangu, nikikumbuka maisha niliyoishi kabla sijapata utajiri sitaki
kabisa kuamini kwamba naelekea kuyarudia tena.”

80
SURA YA TISA

“Hatuwezi kurudi kwenye umaskini mume wangu, hata ikitokea hivyo ni suala la
kumshukuru Mungu kwani yeye ndiye anayepanga kila kitu,” alisema mama
Samantha lakini mumewe hakumuelewa kabisa, akawa anazunguka huku na kule
ndani ya chumba hicho akiwa ni kama amechanganyikiwa.
***
Kitendo cha Samantha na Edmund kukutana tena kimwili, hakikusabisha madhara
kwenye utajiri wa baba yake Samantha pekee bali madhara yalikuwa makubwa
zaidi.
Kitendo cha wawili hao kufanya mapenzi, kilisababisha wanaume ambao
walitolewa kafara baada ya kujaribu kufanya mapenzi na Samantha na baadaye
kuhifadhiwa kwenye pango maalum ndani ya nyumba ya mganga Shiwinga
aliyekuwa nyuma ya utajiri wa kishetani wa mzee huyo, watoroke katika mazingira
ya kutatanisha na kuingia mitaani.
Kibaya zaidi, kutokana na kafara nzito walizokuwa wakifanyiwa wanaume hao,
hawakuwa binadamu wa kawaida tena na baada ya kutoroka kwa mganga
Shiwinga, kila mmoja alikuwa akitorokea kwenye mazingira aliyokuwa anaishi
kabla ya kutolewa kafara, jambo lililosababisha taharuki kubwa kwenye kila mtaa
walipokuwa wakionekana.
Kila mmoja aliyepatikana, alionesha kukonda sana, akiwa na nywele na kucha
ndefu na chafu, huku karibu wote wakiwa hawana kabisa uwezo wa kuzungumza
kama zamani, wakionesha pia kuwa na matatizo ya kiakili.
“Maskini Mohamed, huwezi kuamini kama ndiyo yule kaka sharobaro, aliyekuwa
anajipenda kiasi cha kufanya awe kipenzi cha mabinti hapa mtaani, ukimuona
huwezi kuamini.”
“Mimi nimemuona asubuhi, anatia huruma sana. Nasikia alitembea na mke wa
mtu, mumewe akamuendea kwa mganga, wake za watu sumu jamani,” watu
kadhaa walikuwa wakijadiliana, saa chache baada ya kijana maarufu, Mohamed au
Muddy kama wengi walivyozoea kumuita, kupatikana jirani na nyumbani kwao
akiwa na hali mbaya sana, ikiwa ni baada ya karibu mwaka mmoja na nusu tangu
alipopotea katika mazingira ya kutatanisha.

81
Taarifa za kuonekana kwa misukule kadhaa kwenye mitaa ya Jiji la Dar es Salaam
zilimshtua kila aliyezisikia huku kila mtu akizungumza lake. Hata wale ambao kwa
kipindi kirefu hawakuwa wakiamini kuhusu habari za misukule, nao walianza
kuamini kwa kilichokuwa kinatokea.
Wachungaji, viongozi mbalimbali wa dini na waganga wa kienyeji, waliitumia
vyema fursa hiyo, wengi wakawa wanatangaza kwamba wanao uwezo wa
kuwaponya na kuwarudisha misukule hao katika hali yao ya kawaida, jambo
lililosababisha ndugu wa watu hao waliokuwa na tatizo hilo kuanza kuhangaika
huku na kule kwenye nyumba za ibada, kila mmoja akitaka kumsaidia ndugu yake.
Hata hivyo, hakuna aliyeonesha kupata ahueni wala kuwa na dalili za kupona,
gumzo likazidi kuwa kubwa mitaani.
***
“Unasema tukae tumshukuru Mungu, hivi una akili kweli mke wangu?”
“Sasa mume wangu unafikiri tutafanya nini?”
“Lazima tufanye kitu, au hujasikia habari za misukule inayoonekana huko
mitaani?”
“Sasa kwani wewe unahusika vipi na hiyo misukule?”
“Usijifanye hujui mke wangu, hao ni wanaume wote waliojaribu kufanya mapenzi
na Samantha na kujikuta wakiingia kwenye mtego wangu.”
“Haa! Sasa si uliniambia kwamba wanakufa? Inawezekana vipi mtu aliyekufa
akaonekana mitaani?”
“Hawakuwa wakifa moja kwa moja bali wanachukuliwa misukule kwa ajili ya
kutusaidia kwenye biashara, sasa inaonekana wanatoroka kule walikohifadhiwa,
inabidi sasa hivi niende Bagamoyo kwa mganga Shiwinga kutaka kujua nini
ninatokea, nahisi kuhujumiwa,” alisema baba yake Samantha kwa hasira, taarifa
iliyomuacha mkewe akiwa mdomo wazi.
“Sasa wakipona si wataeleza ukweli wa kilichotokea? Unafikiri tutaficha wapi sura
zetu?”
“Wewe si umeamua kushirikiana na mwanao kunihujumu? Mkae mkijua kwamba
hili tatizo siyo langu peke yangu, ni letu sote kwa hiyo kama mtaendelea
kufichiana siri na mwanao kitakachotokea tusilaumiane, nipo tayari kuua,” alisema

82
baba yake Samantha huku akiichomeka bastola yake kiunoni, akatoka na kuingia
ndani ya gari, safari ya kuelekea nyumbani kwa mganga Shiwinga, Bagamoyo
ikaanza.
“Mungu wangu, kumbe ndiyo mambo yenyewe yalivyo makubwa hivi,” alisema
mama yake Samantha wakati akimsindikiza mumewe kwa macho wakati akitoka
kwa kasi getini na kuianza safari ya kuelekea Bagamoyo, akionesha wazi kuwa na
jazba kali kuliko kawaida.
***
“Samantha.”
“Abee mume wangu.”
“Ni siku ya pili sasa hujarudi nyumbani, unafikiri wazazi wako watakuwa kwenye
hali gani?”
“Edmund, kumbe hunipendi eeh! Yaani yote niliyokuelezea kuhusu baba leo
unataka nirudi tena? Unataka nikafe?”
“Siyo hivyo mpenzi wangu, najua kama wazazi lazima watakuwa kwenye wakati
mgumu sana, si ajabu wakaenda hata kutoa taarifa polisi.”
“Achana nao. Mimi nina wazo Edmund, hatuwezi kuendelea kukaa kwa amani,
unaonaje kama tukiondoka Dar kwa muda mpaka mambo yatulie?”
“Twende wapi?”
“Popote, Arusha, Mbeya au Mwanza, pesa siyo tatizo kwangu,” alisema Samantha,
wazo ambalo Edmund alikubaliana nalo lakini wakakubaliana kwamba kabla
hawajaondoka, ni lazima waende kwa mganga Shiwinga kumpa taarifa ya uamuzi
wao na pia kupewa dawa nyingine za kuendelea kutumia huko watakakokimbilia.
“Wazo zuri na inabidi twende sasa hivi Bagamoyo, moyo wangu hauna amani
kabisa kwa sababu najua baba anatusaka kwa udi na uvumba na muda si mrefu
atajua mahali tulipojificha,” alisema Samantha, bila kupoteza muda wakajiandaa
kwa safari ya kuelekea Bagamoyo, bila kujua kwamba baba yake Samantha naye
muda huo alikuwa njiani kuelekea Bagamoyo, kiunoni akiwa na bastola.
Kwa kuwa safari hii Samantha hakuwa na gari, waliamua kukodi teksi ya
kuwapeleka mpaka Bagamoyo, wakahakikisha wamefunga vizuri nyumba yao na
kutoka mpaka mtaa wa pili kulipokuwa na maegesho ya teksi.

83
Wakaingia ndani ya teksi moja na kuzungumza na dereva, baada ya kukubaliana,
safari ya kuelekea Bagamoyo ilianza, wawili hao wakiwa wamekaa siti ya nyuma,
Samantha akiwa amejilaza kwenye miguu ya Edmund kimahaba.
Safari iliendelea mpaka walipowasili Bagamoyo, wakamuelekeza dereva kuiacha
barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea
nyumbani kwa mganga Shiwinga.
Dakika kadhaa baadaye, waliwasili nyumbani kwa mganga huyo, wakamlipa
dereva fedha zake na kumwambia aende kuwasubiri kwenye barabara ya lami,
wakachukua namba zake za simu kisha wakaingia nyumbani kwa mganga huyo
ambaye aliwakaribisha kwa uchangamfu.
Muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani hapo, wakiwa wanapiga stori za hapa na
pale, walisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba hiyo, Samantha na Edmund
wakahisi yule dereva teksi atakuwa amesahau kitu, ikabidi watoke kwa lengo la
kwenda kumsikiliza.
Katika hali ambayo hakuna aliyeiamini, walipotoka tu, walikutana uso kwa uso na
baba yake Samantha ambaye tayari alikuwa ameshashuka kwenye gari lake na
kuliacha likiendelea kunguruma.
“Nilijua tu lazima nitawapata, kumbe wewe ndiye unayempa jeuri mwanangu si
ndiyo?” alisema mzee huyo huku akipeleka mkono kiunoni, kufumba na kufumbua
akachomoa bastola na kuikoki, akamnyooshea Edmund.
“Tukimbie, Edmund tukimbie, atakuua, namjua baba yangu,” alisema Samantha
kwa hofu na kumshika mkono Edmund aliyekuwa ameduwaa, asijue la kufanya,
wakaanza kukimbia kuelekea nyuma ya nyumba yam ganga Shiwinga lakini kabla
hawajafika mbali, mlio wa risasi ulisikika, paah!
Mganga Shiwinga akiwa ndani ya nyumba yake, alishtuka kusikia mzozo mkubwa
nje ya nyumba yake, akaacha kila alichokuwa anakifanya na kutoka nje lakini
alipofika mlangoni, alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia mlio mkubwa wa risasi,
akajikaza kiume na kutoka nje.
Akashindwa kuyaamini macho yake kwa alichokiona, baba yake Samantha
alikuwa ameshika bastola, huku naye akionesha kupigwa na bumbuwazi, akiwa ni
kama haamini kilichotokea.
“Edmund! Kimbia mpenzi wangu, kimbia atakuua.”

84
“Hapana Samantha, siwezi kuondoka bila wewe,” alisema Edmund huku naye
akiwa ni kama haamini alichokuwa anakiona. Samantha alikuwa amedondoka
chini, huku damu nyingi zikimtoka mithili ya bomba lililopasuka.
Risasi iliyofyatuliwa na baba yake, badala ya kumpata Edmund kama mwenyewe
alivyokuwa amepania, ilipenya na kuingia kwenye paja la mguu wa kushoto la
mwanaye na kusababisha adondoke chini kama mzigo, damu nyingi zikiwa
zinamtoka.
Licha ya Samantha kuendelea kumsisitiza Edmund aondoke, kijana huyo hakuwa
tayari, akaona ni bora apigwe risasi na kufa kuliko kukimbia na kumuacha
Samantha akiwa kwenye hali hiyo.
Kitendo cha kumpiga risasi mwanaye, kilimfanya baba yake Samantha abaki
amepigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa, huku akiwa bado ameishika bastola
yake vilevile. Ni mpaka mganga Shiwinga alipotoka nje ndipo mzee huyo
alipozinduka na kujikuta akijilaumu mno kwa kitendo alichokifanya.
Baba yake Samantha na mganga Shiwinga wakakimbia mpaka pale Samantha
alipokuwa ameanguka, huku Edmund akijaribu kuzuia damu zisiendelee kumtoka
kwa wingi. Baada ya wawili hao kufika, kufumba na kufumbua baba yake
Samantha alimpiga Edmund konde zito lililomfanya adondoke chini kama mzigo,
akamfuata na kuanza kumpiga mateke ya tumboni huku akimtolea matusi ya
nguoni, hali iliyosababisha zoezi la kumuokoa Samantha lisitishwe kwa muda.
“Unakosea baba Samantha, tumsaidie kwanza huyu, atakufa huku tunamuona,”
alisema mganga Shiwinga, baba yake Samantha akamalizia kupiga teke lingine
kwa nguvu na kusababisha Edmund augulie maumivu makali.
Wakaanza kumsaidia Samantha ambapo walimbeba juujuu na kumsogeza eneo
lenye nafasi, mganga Shiwinga akakimbilia ndani na muda mfupi baadaye alitoka
akiwa na dawa ya maji, akaanza kumpaka Samantha pale kwenye jeraha lake huku
akimpa Edmund kazi ya kutwanga dawa nyingine ya majani.
“Huyu mshenzi sitaki afanye kazi yoyote, kwanza ondoka hapa nisije nikakupiga
risasi,” alifoka baba yake Samantha lakini mganga Shiwinga akaingilia kati na
kumsihi mzee huyo atulize hasira zake kwanza kwa sababu kwa wakati huo, jambo
la muhimu lilikuwa ni kuokoa maisha ya Samantha kwanza.
Edmund ambaye alikuwa akitokwa na damu mdomoni kutokana na ngumi
aliyopigwa na baba yake Edmund huku mikono yake pia ikiwa imetapakaa damu

85
alizozishika wakati akimsaidia Samantha, alitii alichoambiwa na mganga
Shiwinga, akaanza kutwanga dawa kwenye kinu kikubwa huku mara kwa mara
baba yake Samantha akimkata jicho baya.
Walipofanikiwa kuzuia damu zisiendelee kutoka, mganga Shiwinga na baba yake
Samantha walisaidiana kumpakiza Samantha kwenye gari kwa ajili ya
kumuwahisha hospitali.
“Na wewe mshenzi ingia ndani ya gari,” alisema baba yake Samantha kwa ukali
akimwambia Edmund ambaye alisitasita kwa sekunde kadhaa, alimpomtazama
Samantha alivyokuwa akiendelea kuugulia maumivu, hakuwa na cha kufanya zaidi
ya kutii alichoambiwa.
Akakaa kwenye siti moja na Samantha ambaye japokuwa alikuwa kwenye
maumivu makali, alishindwa kuficha furaha yake kumuona Edmund akiwa amekaa
pembeni yake. Kwa kasi kubwa baba yake Samantha aliondoka gari na kumuacha
mganga Shiwinga akiwa amesimama nyuma ya nyumba yake. Kila kitu kilikuwa
kimetokea kwa kasi kubwa mno mithili ya filamu ya kusisimua ya Hollywood.
Baba yake Samantha alikuwa na kazi moja tu nyuma ya usukani, kukanyaga
mafuta! Gari likawa linakimbia utafikiri lipo kwenye mashindano. Takribani
dakika thelathini baadaye, tayari walikuwa wamewasili jijini Dar es Salaam, mzee
huyo akaenda moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha polisi Oysterbay.
Edmund akashikwa na mshangao kwani alitegemea breki ya kwanza ingekuwa
hospitalini, mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda mbio kuliko kawaida.
Kwa muda wote huo, Samantha alikuwa amepitiwa na usingizi mzito kutokana na
kuugulia maumivu kwa muda mrefu.
Kwa kupitia vioo vya gari la kifahari walilokuwa wamepanda, Edmund alimuona
baba yake Samantha akizungumza jambo na askari kadhaa waliokuwa
wamemzunguka, akawa anawaeleza jambo huku akiwaoneshea kwenye gari lake.
Askari watatu wenye silaha wakatembea harakaharaka mpaka kwenye gari,
Edmund akashtukia akishushwa chini na kukokotwa msobemsobe mpaka kaunta.
“Afande kani nimefanya kosa gani?”
“Umefanya jaribio la kuua kwa kutumia silaha,” alisema askari mmoja huku
akimuamuru Edmund kuvua viatu na mkanda kisha kusalimisha kila kilicho chake
kaunta.

86
Baba yake Samantha aliyekuwa akiandikiwa fomu ya matibabu (PF3) na askari
mmoja pembeni, alijifanya kutosikia chochote kilichokuwa kinaendelea, sekunde
chache baadaye alitoka na fomu yake, akaenda kwenye gari lake, akapanda na
kuondoka kwa kasi kubwa na kumuacha Edmund akiwa chini ya ulinzi mkali.
“Mungu wangu! Kwani nimefanya kosa gani?” alihoji Edmund lakini kama
ilivyokuwa mwanzo, hakuna aliyemjibu, baada ya kumaliza kukabidhi vifaa vyake
kaunta, alibebwa msobemsobe na kuingizwa mahabusu.
Akiwa nyuma ya nondo, Edmund alilia kwa uchungu sana, aliona kama baba yake
Samantha anamuonea bila sababu yoyote ya msingi kwa sababu kama ni mapenzi,
binti yake ndiye aliyekuwa akimpenda yeye.
“Sasa mimi kosa langu nini? Nimemkosea nini Mungu kustahili mateso kama
haya? Sijawahi kuingia selo hata siku moja, leo kwa sababu ya mapenzi nimeingia,
kwa nini lakini?” Edmund alikuwa akijisemea mwenyewe kama mwendawazimu,
akiwa amekaa kwenye kona moja ya mahabusu hiyo iliyokuwa imejaa wahalifu
wengi huku kukiwa na hewa nzito.
“Dogo vipi mbona unalialia?” mwanaume mmoja mwenye mwili mkubwa,
aliyekuwa amevua shati na kubaki kifua wazi, alimuuliza Edmund huku
akimgongagonga begani. Edmund alipomgeukia na macho yao kugongana,
alijikuta akikosa cha kujibu kwani bila hata kuuliza, mwanaume huyo alionekana
kuwa miongoni mwa wahalifu wazoefu kutokana na jinsi uso wake ulivyokuwa na
makovu mengi makubwa.
“Aah! Mambo ya kawaida tu braza.”
“Ukishaingia humu inabidi uwe mgumu, mambo ya kulialia kama mtoto wa kike
wenzako watakuoa, shauri yako,” alisema mwanaume huyo kwa sauti ya
kukwaruza na kusababisha mahabusu wengine wacheke kwa nguvu. Ikabidi
Edmund ajikaze kisabuni, akawa anaugulia maumivu ndani kwa ndani.
***
“Hapa ni wapi? Nimefikaje hapa na Edmund yuko wapi?” Samantha aliongea kwa
taabu baada ya kuzinduka na kujikuta akiwa sehemu tofauti kabisa ambayo
hakukumbuka amefikaje.
“Samantha, ooh! Ahsante Mungu. Nesi! Nesi! Ameamka,” mama yake Samantha
aliyekuwa amekaa pembeni ya kitanda alicholazwa mwanaye alimuita nesi huku
akiinua mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu wake.

87
“Mama! Kwani hapa ni wapi?” aliendelea kuhoji Samantha huku akiishangaa
chupa ya damu iliyokuwa ikitiririka kuingia kwenye mishipa yake.
“Ni hospitali mwanangu. Uliletwa ukiwa hujitambui,” alisema mama yake
Samantha huku akitokwa na machozi ambayo Samantha hakuelewa kama ni ya
furaha au ya huzuni.
Akataka kuinuka pale kitandani kwani bado hakuwa akikumbuka nini
kimesababisha akawa kwenye hali kama hiyo lakini maumivu makali ya mguu
yakamrudisha kitandani. Kwa mbali akaanza kukumbuka kilichotokea.
“Nimefanya nini mguu mama?”
“Edmund alitaka kukuua mwanangu, amekupiga risasi lakini usijali tayari
ameshakamatwa hivi tunavyoongea yupo mikononi mwa polisi.”
“Whaaat?” (Niniii?)
“Ndiyo hivyo, baba yako amesema hatakubali, atahakikisha yule kijana anapotea.”
“Baba muongo! Mama baba kakudanganya,” alisema Samantha huku akianza kulia
kwa uchungu.
Kumbukumbu za yote yaliyotokea zilijirudia ndani ya kichwa chake, akakumbuka
jinsi alivyokuwa amepanga kutoroka na Edmund na kukimbilia mbali ili isiwe
rahisi kwa baba yake kuendelea kuwafuatilia, alikumbuka jinsi walivyofunga safari
mpaka kwa mganga Shiwinga, Bagamoyo.
“Alikumbuka pia jinsi baba yake alivyowafuata mpaka kwa mganga huyo na jinsi
alivyochomoa bastola kiunoni kwake kwa lengo la kumpiga risasi Edmund na jinsi
msichana huyo alivyojitoa sadaka na kujikuta akipigwa risasi ya mguuni na baba
yake.
“Edmund! Kimbia mpenzi wangu, kimbia atakuua.”
“Hapana Samantha, siwezi kuondoka bila wewe,” Samantha aliyakumbuka
maneno ya mwisho aliyozungumza na mpenzi wake huyo, damu nyingi zikiwa
zinamvuja mguuni.
“Baba ndiye aliyenipiga risasi mama, alikuwa anataka kumuua Edmund,” alisema
Samantha, kauli ambayo ilimshtua mno mama yake Samantha.

88
“Unasema? Samantha utakuwa umechanganyikiwa mwanangu. Unajua umepoteza
damu nyingi na isitoshe umechomwa sindano kali za kuzuia maumivu, hizo ndizo
zilizokuchanganya.”
“Hapana mama, nina akili zangu timamu, niamini ninachokizungumza. Hata
mganga Shiwinga anaweza kuwa shahidi.”
“Hapana mwanangu, inabidi upumzike, nesi muongeze dawa ya usingizi aendelee
kupumzika,” alisema mama yake Samantha akiamini mwanaye atakuwa
amechanganyikiwa kwani hakuamini kama mumewe anaweza kufanya kitendo
hicho.
Kwa kuwa nesi alikuwa jirani, alimchoma sindano Samantha ambaye bado
aliendelea kusisitiza kwamba anachokizungumza ni kweli mpaka alipopitiwa na
usingizi mzito. Maneno yaliyosemwa na mwanaye yaliendelea kujirudia ndani ya
kichwa cha mama yake Samantha.
Japokuwa upande mmoja alikuwa akibisha kwamba mumewe hawezi kufanya
hivyo, upande mwingine alikubali kwamba anaweza kwa sababu tangu aanze
kukumbwa na misukosuko ya utajiri wake kuanza kupukutika, alikuwa ni kama
amechanganyikiwa mpaka kufikia hatua ya kumpiga mkewe, jambo ambalo
hajawahi kulifanya hata siku moja.
Muda mfupi baadaye, mumewe alifika hospitalini hapo huku akionesha kukosa
kabisa utulivu, akaenda mpaka kwenye wodi maalum ya VIP aliyokuwa amelazwa
Samantha.
“Anaendeleaje huyu!” alisema baba yake Samantha huku akikaa pembeni ya
mkewe.
“Anaendelea vizuri, amerejewa na fahamu zake lakini inaonesha bado akili zake
hazijatulia,” alisema mama yake Samantha huku akikaa vizuri pale kitandani kwa
lengo la kumchunguza vizuri mumewe kwani alikuwa na uwezo mkubwa wa
kumtambua kwamba anaongea ukweli au anadanganya.
Akawa anaendelea kumhoji maswali ya hapa na pale ambapo kwa kumtazama tu
aligundua kwamba kuna jambo alikuwa analificha. Hata hivyo, hakutaka kuonesha
kwamba ameshtukia jambo lolote, wakaendelea kuzungumza mambo yao ya
kawaida huku akimuunga mkono kila alichokuwa anakisema.
“Umesema huyo kijana umempeleka kituo gani?”

89
“Yuko Oysterbay, mshenzi sana yule kijana,” alisema baba yake Samantha huku
akionesha kudhamiria kweli kumpoteza ili kulinda utajiri wake ambao tayari
ulishaanza kusuasua. Baadaye aliondoka na kumuacha mama yake Samantha
akiwa pembeni ya Samantha.
Baada ya dawa za usingizi kuisha nguvu, Samantha alizinduka tena usingizi
ambapo kama ilivyokuwa mara ya mwisho kabla hajachomwa sindano ya usingizi,
aliendelea kumsisitiza mama yake kwamba Edmund hakuwa na kosa lolote.
“Nakuomba umsaidie Edmund mama, anateseka bure kwa kosa ambalo
hajalifanya,” alisema Samantha huku akilia, mama yake akamtaka atulie kwanza
kwa sababu hata yeye ameanza kuwa na wasiwasi kwamba kijana huyo hana hatia.
Akamtaka Samantha amuelezee kwa kirefu kilichotokea.
Lengo la kumwambia amuelezee upya ilikuwa ni kutaka kufananisha maelezo
aliyompa awali na ambacho angekisema muda huo kwa sababu kama alikuwa
anadanganya, isingekuwa rahisi maelezo ya awali na ya muda huo kufanana.
Hata hivyo, Samantha alieleza kama alivyoeleza awali bila kuongeza wala
kupunguza jambo lolote, jambo lililomfanya mama yake Samantha aamini
kwamba mwanaye alikuwa anazungumza ukweli.
“Basi nisikilize mwanangu, mimi nitamsaidia Edmund na nakuhakikishia nitaenda
kumtoa mahabusu lakini ni lazima nikusimamie wewe upone kwanza.”
“Mama! Mpaka mimi nipone unafikiri itakuwa lini? Kamtoe kwanza Edmund,
nataka kumuona, nakuomba mama.”
“Usiwe na haraka mwanangu, kuwa mpole.”
“Haiwezekani mwanangu, afya yako ni muhimu zaidi.”
“Mama usipoenda kumtoa leo nachukua uamuzi mgumu wa kujiua,” alisema
Samantha kwa sauti ya juu huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Kauli hiyo ikapenya kwenye ngoma za masikio ya baba yake Samantha ambaye
alikuwa mlangoni akitaka kuingia, mkononi akiwa amebeba matunda na juisi
alivyoenda kumnunulia mwanaye.
“Anasemaje huyu? Eti Samantha unasemaje?” alihoji baba yake Samantha akiwa
ameshafungua mlango na kuingia wodini humo, macho yake na ya mwanaye
yakagongana.
“Usipoenda kumtoa Edmund polisi najiua.”

90
SURA YA KUMI

“Mtoto mshenzi sana wewe! Yaani matatizo yote yanayotutokea kumbe ni yule
mshenzi ndiye anayesababisha na leo unadiriki kufumbua mdomo wako kuongea
upuuzi kama huo? Jiue hata sasa hivi.”
“Mh! Jamani mume wangu, mbona unashindwa kutumia busara,” ilibidi mama
yake Samantha aingilie kati kutokana na mumewe kuonesha kutojali tishio kubwa
lililotolewa na binti yao.
“Kwanza Edmund siyo aliyenipiga risasi, wewe ndiyo ulikuwa na bunduki na
ukataka kumuua kaka wa watu…”
“Ishia hapohapo! Mimi ni baba yako na ndiye niliyekuzaa, kwa hiyo utachagua
mwenyewe usimame upande gani, kama unataka kushirikiana na huyo mshenzi
mwenzako niambie sasa hivi nitamke kwamba kuanzia leo wewe siyo mtoto
wangu.”
“Samantha hebu acha kubishana na baba yako, nisikilize mwanangu. Na wewe
mume wangu, kwa nini tusitafute muda mwingine wa kuyazungumzia haya
matatizo? Sidhani kama hapa ni sehemu sahihi,” alisema mama yake Samantha
kwa upole, baba yake Samantha akashusha pumzi ndefu na kuweka matunda na
juisi alivyomnunulia mgonjwa kisha akatoka bila kuzungumza chochote.
“Mwanangu jikaze usibishane na baba yako kwa chochote, anaonekana
amechanganyikiwa, msije mkasababisha matatizo mengine zaidi.”
“Mama mimi nimeshasema, kama hamuendi kumtoa Edmund polisi tusilaumiane
kwa kitakachotokea,” alisema Samantha huku akiangua kilio cha kwikwi.
Mama yake akawa na kazi ya ziada ya kumtuliza lakini bado alishikilia msimamo
wake uleule.
***
Siku ya kwanza ilikuwa ngumu mno kwa Edmund kwani maisha yake yote
hakuwahi kuingizwa mahabusu hata siku moja wala hakuwahi kufikiria kama
inaweza kutokea siku akawekwa nyuma ya nondo. Kitendo hicho kikamvuruga
kabisa kichwa chake, akajikunyata kama kifaranga cha kuku kilicholowanishwa na
mvua.

91
Aliona kama saa zinakwenda taratibu mno, muda ukawa unazidi kuyoyoma huku
taratibu akianza kuzoea mazingira ya selo. Ile hewa nzito iliyompa sana shida
kupumua wakati anaingizwa, akaanza kuiona kuwa ya kawaida.
Siku hiyo ilipita lakini mpaka adhana ya alfajiri inasikika kuashiria mwanzo wa
siku mpya, Edmund hakuwa amelala hata kidogo. Muda wote alikuwa akiendelea
kusumbuliwa na mawazo machungu ndani ya moyo wake, muda mwingine
akijikuta anashindwa kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake.
Baadaye mahabusu wengine walianza kuamka mmoja baada ya mwingine na
kumkuta Edmund akiwa kwenye mkao uleule waliomuacha nao kabla ya kulala.
Wakawa wanamzodoa na kumchokoza kwa maneno ya hapa na pale lakini
mwenyewe hakujali.
Muda ulizidi kuyoyoma na baadaye, wafungwa wote walitulia baada ya kusikia
mlango wa mahabusu ukifunguliwa. Kama ulivyokuwa utaratibu wa askari
wanapoachiana zamu kuhakiki kama mahabusu wote wapo, ndicho kilichofuatia
ambapo mmoja baada ya mwingine alianza kuitwa jina ili kuhakikisha kama yupo.
Baada ya kukabidhiana, wale askari waliokuwepo usiku waliondoka kwenda
kupumzika na wakaingia askari wengine ambapo taratibu za kazi ziliendelea kama
kawaida, mahabusu walioletewa chai wakawa wanaitwa mmoja baada ya
mwingine na kwenda kupokea mizigo yao.
Edmund alijua hakuna mtu anayeweza kwenda kumuona kutokana na jinsi tukio
lenyewe lilivyokuwa kwa sababu hata kazini alikuwa haendi kwa siku kadhaa,
tangu siku aliponusurika kufa baada ya kukutana na Samantha kwa mara ya
kwanza. Akajua itakuwa vigumu sana kwa taarifa za mahali alipo kuwafikia watu
wake wa karibu, alichokuwa anasubiri ikabaki kuwa muujiza tu.
Muda ulizidi kuyoyoma na majira ya kama saa sita mchana, Edmund alishtuka
baada ya kusikia jina lake likiitwa na askari aliyekuwa mlangoni, harakaharaka
akainuka na kumfuata yule askari.
Akatolewa mpaka nyuma ya kaunta bila kusemeshwa chochote. Akashangaa
anarudishiwa viatu na mkanda wake pamoja na vitu alivyovuliwa jana yake wakati
akiingizwa.
“Mheshimiwa, kijana mwenyewe ndiyo huyu?” askari yule aliyemfuata Edmund
selo alihoji, Edmund akawa anageuka huku na kule kuangalia ni nani atayejibu
swali hilo kwa sababu hakukuwa na mtu yeyote anayemjua.

92
“Ndiyo yeye!” alisema mwanaume wa makamo aliyekuwa ndani ya gari lenye vioo
vyeusi vilivyokuwa vimeshushwa kidogo.
“Shikamoo!” Edmund alimsabahi mwanaume huyo kwa hofu huku akiwa makini
kumchunguza kama alishawahi kumuona sehemu lakini kumbukumbu zake
hazikumpa majibu.
“Ingia ndani ya gari!” alisema mwanaume huyo bila hata kujibiwa salamu yake,
Edmund akatafakari kama aingie au la kwa sababu hakuwa na imani na usalama
wake tena, akawa anahisi jambo lolote linaweza kumtokea, hata kuuawa kinyama
kutokana na jinsi baba yake Samantha alivyoonesha kuwa na hasira.
Akiwa bado anasuasua, Edmund aliingizwa kwenye gari na yule askari aliyemtoa
mahabusu, akashangaa naye akiingia kwenye gari na safari ya kuondoka eneo hilo
ikaanza. Kitendo cha yule askari naye kuingia ndani ya gari, kidogo kilimpa amani
Edmund ndani ya nafsi yake, akawa na uhakika kwamba hakuna jambo lolote baya
linaloweza kumtokea.
Safari iliendelea, dereva akawa anaendesha gari kwa kasi kama anayewahi tukio
muhimu, muda mfupi baadaye waliwasili Kinondoni, gari likaiacha barabara
kubwa ya lami na kuingia kwenye barabara za mitaani, likazidi kukata mitaa kabla
ya baadaye kutokezea mbele ya jengo kubwa la ghorofa kadhaa ambalo ndani yake
kulikuwa na Hospitali ya Planet Health au PH kama wengi walivyozoea kuiita.
Sifa kubwa ya hospitali hiyo ilikuwa ni huduma za daraja la kwanza za afya
ambapo licha ya gharama zake kuwa kubwa, watu wengi kutoka familia tajiri
walikuwa wakipenda kwenda kutibiwa hapo kutokana na ubora wa huduma zake.
Japokuwa Edmund hakuwahi kutibiwa hapo lakini alikuwa akizifahamu vyema
sifa za hospitali hiyo.
Hata hivyo, tofauti na siku nyingine zote, eneo lote la hospitali lilikuwa
limezingirwa na umati mkubwa wa watu kuashiria kwamba kulikuwa na tukio
kubwa lililogusa hisia za wengi, kiasi cha kuwalazimu kuacha kazi zao na kubaki
wakishangaa.
“Kuna nini tena hapa?” Edmund alijiuliza akiwa anaendelea kushangaa jinsi umati
wa watu ulivyokuwa mkubwa. Miongoni mwao, aliwaona waandishi wengi wa
habari waliokuwa bize kupiga picha huku na kule huku wengi macho yao yakiwa
juu kabisa ya jengo hilo lililokuwa na ghorofa kumi.

93
“Tumefika, kijana hebu shuka,” alisema yule dereva, askari aliyekuwa amekaa na
Edmund akafungua mlango na kumshika mkono Edmund, yule dereva naye
akateremka na ‘kulock’ gari, yule askari akawa anamuongoza Edmund kupenya
kwenye umati mkubwa wa watu uliokuwa eneo hilo kuelekea mapokezi huku yule
mwanaume mwingine akiwafuata kwa nyuma.
“Mungu wangu, kwani kuna nini hapa? Mbona mapigo ya moyo yananienda kasi
kiasi hiki?” Edmund alijiuliza wakati wakielekea mapokezi. Mpaka muda huo,
bado hakuwa anaelewa kilichokuwa kinaendelea eneo hilo. Wingi wa watu na jinsi
walivyokuwa na taharuki vikazidi kumchanganya kichwa chake.
“Mhusika huyu hapa tumekuja naye, tunaomba msaada wa kumfikisha juu haraka
iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika,” yule mwanaume alizungumza na
askari wengi wenye silaha waliokuwa wametanda mapokezi, Edmund akazidi
kupigwa na butwaa hasa baada ya kusikia akitajwa kwamba yeye ndiye mhusika.
Akiwa bado anaendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu, Edmund aliingizwa
kwenye lifti chini ya ulinzi na yule mwanaume akabonyeza kitufe ukutani. Lifti
ikaanza kupanda juu mpaka ilipofika kwenye ghorofa ya mwisho.
Harakaharaka wakateremka huku Edmund akiendelea kushaangaa huku na kule,
akashangaa yule mwanaume akielekea kwenye ngazi ndogo zilizokuwa zinaelekea
upande wa juu kabisa wa jengo hilo, mahali ambako hakukuwa kukitumika.
“Nifuate harakaharaka,” alisema yule mwanaume, wakawapita askari wengine
wawili waliokuwa wamesimama eneo hilo, kila mmoja akiwa na silaha mkononi,
wakapanda ngazi hizo na kutokeza upande wa juu kabisa wa ghorofa hilo.
“Mungu wangu,” alisema Edmund kwa mshtuko mkubwa baada ya kukutana uso
kwa uso na baba yake Samantha aliyekuwa amemshikilia mama yake Samantha
aliyekuwa analia kwa uchungu huku akilitaja jina la mwanaye kama anayemsihi
jambo fulani.
Edmund akiwa bado anatazamana na mzee huyo huku kijasho chembamba
kikimtoka, aligundua kwamba macho yake yalikuwa yamevimba na kubadilika
rangi na kuwa mekundu kuonesha kwamba naye alikuwa akilia.
“Amekuja,” alisema baba yake Samantha kwa kifupi na kusababisha mkewe
aliyekuwa akiendelea kulia apatwe na mshtuko mkubwa, akajitoa mikononi
mwake na kusimama wima, akawa anamkodolea macho Edmund akiwa ni kama
haamini.

94
“Ahsante kwa kuja Edmund, tuko chini ya miguu yako tunaomba utusaidie,”
alisema mwanamke huyo na kumvaa Edmund mwilini huku akiendelea kulia. Bado
Edmund hakuwa anaelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, ikabidi waanze
kumfafanulia kwa kina.
“Samantha anataka kujirusha ghorofani, ameweka mgomo kwamba kama
asipokuona basi leo ndiyo mwisho wa maisha yake,” alisema mama yake
Samantha huku akiendelea kulia.
“Mungu wangu, yuko wapi?” alihoji Edmund huku na yeye akionesha
kuchanganyikiwa kuliko kawaida. Alikuwa anatambua jinsi msichana huyo
mrembo alivyokuwa anampenda lakini hakuwahi kudhani hata siku moja kwamba
anaweza kuchukua uamuzi mgumu kiasi hicho.
“Yupo nyuma ya haya matanki ya maji, hataki mtu yeyote amsogelee ndiyo maana
tumekaa mbali, tunakuomba nenda kazungumze naye,” alisema mama yake
Samantha huku akiendelea kulia. Yule mwanaume aliyeongozana na Edmund
kutoka kituo cha polisi, akatingisha kichwa kuashiria kuunga mkono kilichokuwa
kinazungumzwa na mwanamke huyo.
Edmund akaelekezwa upande aliokuwepo Samantha na kutakiwa kuwa makini
kwani kwa hali ilivyokuwa, Samantha alikuwa tayari kufa muda wowote. Huku
akitetemeka, Edmund alianza kutembea kwa kunyata kuelekea upande ule
alioelekezwa.
Baada ya kuyavuka matanki yale makubwa ya maji yaliyokuwa yakisambaza maji
kwenye jengo zima, alitokezea kwenye uwazi ambapo aliweza kumuona vizuri
Samantha, akiwa amesimama kwa msaada wa magongo kutokana na mguu wake
mmoja kujeruhiwa kwa risasi.
Alikuwa amesimama kwenye kingo za ghorofa hilo, akiwa amevalia nguo
wanazovaa wagonjwa wanaolazwa kwenye hospitali hiyo huku akionesha
kutokuwa na hata chembe ya hofu.
“Samantha! Samantha!” Edmund aliita kwa sauti ya upole huku akiendelea
kutembea taratibu kumfuata msichana huyo ambaye muda wote alikuwa
akiwatazama mamia ya watu waliokuwa wamefurika chini ya ghorofa hilo,
wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kuona ni jambo gani litakalotokea.

95
“Ni mimi Edmund, nimekuja mpenzi wangu,” alisema Edmund kwa sauti ya
kubembeleza lakini msichana huyo hakutaka kugeuka, akaendelea kutulia vilevile
kama hasikii chochote.
“Samantha, niko chini ya miguu yako mpenzi wangu, naomba ugeuke unitazame,
nimekuja kukuchukua. Nakupenda sana na sipo tayari kuona jambo lolote baya
linakutokea,” Edmund aliendelea kumbembeleza msichana huyo, taratibu akaanza
kugeuza shingo yake na muda mfupi baadaye alikuwa akitazamana uso kwa uso na
Edmund.
“Ooh! Mungu wangu, kumbe kweli ni wewe mpenzi wangu? Siamini! Siamini,”
alisema msichana huyo na kuanza kuangua kilio kwa nguvu. Edmund akazidi
kumsogelea huku akimuonesha ishara kwamba na yeye asogee ili wakutane
katikati, jambo ambalo Samantha alilitii na kuanza kujikongoja na magongo yake
huku akiendelea kulia kwa uchungu.
Hatimaye wakakutana ambapo Samantha alitupa magongo yake, akamrukia
Edmund na kumkumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia kwa sauti kubwa.
Kufumba na kufumbua askari kadhaa waliokuwa na silaha waliwazunguka na
kuhakikisha Samantha hasogei tena kule alikotaka kujirusha.
Wazazi wa Samantha nao walisogea eneo hilo, kila mmoja akitokwa na machozi
ya furaha kwani hawakuamini kwamba hatimaye Edmund alifanikiwa kumuokoa
kutoka kwenye shimo la mauti. Waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma, kila
mmoja alikuwa akipiga picha kwa kasi kuhakikisha hakosi tukio hata moja.
“Nini kimekusibu mpenzi wangu?”
“Siwezi kuishi bila wewe Edmund na ndiyo maana nikafikia hatua ya kutaka
kuyakatisha maisha yangu baada ya kujua kwamba wameenda kukufunga kwa
makosa ambayo hujafanya,” alisema Samantha kwa uchungu kisha akambusu
Edmund mdomoni huku akionesha kuwa kwenye hisia nzito.
“Usijali mpenzi wangu, niko salama kabisa,” alisema Edmund huku naye
akimbusu Samantha sehemu mbalimbali za mwili wake. Hakuna aliyejali kwamba
walikuwa wamezungukwa na askari, wazazi wa Samantha na waandishi wa habari.
Kila mmoja alimuonesha kwa vitendo mwenzake jinsi alivyokuwa anampenda.
Muda mfupi baadaye, madaktari wawili na manesi walifika eneo hilo na kusimama
pembeni kusubiri maelekezo yatakayotolewa.
“Afande, naomba arudishwe wodini kwa sababu hali yake bado siyo nzuri.”

96
“Hapana daktari, inabidi usubiri kwa sababu si unajua kujaribu kujiua ni kosa
kisheria?” alisema askari mmoja aliyeonesha kuwa na mamlaka kuliko wenzake.
Baba yake Samantha akamvuta pembeni askari huyo na kuanza kuzungumza naye.
Muda mfupi baadaye, amri ikatolewa kwamba Samantha arudishwe wodini kisha
Edmund arudishwe alikokuwa.”
“Siendi sehemu yoyote bila Edmund, kama mnataka nirudi wodini lazima niende
naye,” alisema Samantha huku akimng’ang’ania Edmund mwilini, askari
wakatazamana kisha yule kiongozi wao akaomba kuzungumza tena na baba yake
Samantha. Wakawa wanajadiliana nini cha kufanya.
“Mzee unampenda binti yako?”
“Nampenda sana lakini sipo tayari kumuona akiwa na huyu mshenzi,
haiwezekani.”
“Kwani kikubwa kinachokufanya umchukie huyu kijana ni nini?”
“Anamtumia mwanangu kimapenzi na kama hiyo haitoshi, alijaribu kumuua kwa
kumpiga risasi na tayari kesi yake imeshafunguliwa.”
“Lakini mbona inavyoonesha ni kama wanapendana sana? Huyu kijana anaweza
kweli kujaribu kumuua msichana anayempenda kiasi hiki?”
“Kwa hiyo unafikiri mimi naongopa, si ndiyo?”
“Hapana, siyo hivyo mzee, najaribu kuzungumza na wewe ili kuzuia lisitokee tukio
jingine kama hili lililotokea. Unafikiri kama juhudi kubwa za kwenda kumtoa
mahabusu huyu kijana zisingefanyika mwanao angekuwa hai mpaka hivi sasa?
Angeshakuwa amejirusha ghorofani. Hulioni hili?”
“Kwa hiyo unataka kusemaje afande?”
“Najua una hasira lakini nakuomba uongozwe na busara katika hili, utasababisha
madhara makubwa kwa binti yako mwenyewe. Kama kweli unampenda kwa muda
huu mpe uhuru wa kufanya anachokitaka mpaka atakapopona, kwa sababu kwanza
siyo mtoto mdogo kama unavyofikiri,” alisema askari huyo na kuendelea
kumsisitiza baba yake Samantha kwamba kitendo cha kuendeleza ubabe wake
dhidi ya Edmund kingesababisha madhara makubwa zaidi.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, hatimaye mzee huyo aliamua kuruhusu kwa
shingo upande Edmund akae wodini na Samantha lakini kwa maelezo kwamba ni

97
lazima aendelee kuwekwa chini ya ulinzi. Baada ya askari kujadiliana, nao
walikubaliana kwamba kwa sababu ya hali halisi ilivyo, Edmund aachiliwe kwa
dhamana huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa.
“Ahsante Samantha! Ahsante sana.”
“Ahsante kwa lipi Edmund? Mimi ndiyo natakuwa kukushukuru wewe.”
“Msimamo wako thabiti umesababisha niachiwe kwa dhamana. Mahabusu kubaya
mpenzi wangu, usiombe yakukute, bora usimuliwe tu,” alisema Edmund huku
akitingisha kichwa chake kwa ishara ya kuhuzunika.
“Usijali Edmund, nikisema nakupenda namaanisha kweli nakupenda, ni bora nife
kuliko kuishi bila wewe,” alisema Samantha huku akionesha kumaanisha kile
alichokuwa anakisema. Wakaendelea na mazungumzo ya hapa na pale huku
Edmund akimsihi asirudie kufanya jaribio lingine la kuyakatisha maisha yake kwa
sababu Mungu hajaribiwi.
“Nimekuelewa mpenzi wangu lakini mimi nina wazo.”
“Wazo gani mke wangu mtarajiwa.”
“Kabla hatujatokewa na haya matatizo tulikuwa tumepanga tutoroke na kwenda
kuishi mbali na jiji hili ili tuwe huru. Bado nataka mipango yetu iendelee.”
“Mpaka upone Samantha, unafikiri tutaondokaje ukiwa na hali kama hiyo? Isitoshe
mimi nimeachiwa kwa dhamana, huoni kama itakuwa ni tatizo jingine?”
“Sasa tufanyeje mpenzi wangu?”
“Kwa hapa tulipofikia, inabidi tuwe wapole haya mambo yatulie kwanza kisha
baada ya hapo ndiyo tutajua nini cha kufanya,” alisema Edmund lakini Samantha
akaonesha kutokubaliana na maelezo hayo. Wakaendelea kujadiliana kwa muda
mrefu lakini bado hawakufikia makubaliano.
“Halafu huu ni muda wa mimi kwenda kazini kuripoti, unajua tangu nilipopatwa
na matatizo sijaenda hata siku moja.”
“Wala huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kazi, hata ukiacha naamini kwa
fedha nilizonazo tutaishi kwa raha mustarehe kwa kipindi kirefu wakati tukiangalia
upya namna ya kuyajenga maisha yetu,” alisema Samantha, Edmund akamuitikia
ili kumridhisha lakini moyoni alipanga kuwa ni lazima aende kazini kwao
atakapopata nafasi. Baada ya wawili hao kukaa pamoja wodini kwa muda mrefu

98
huku Samantha akionesha kuchangamka sana tofauti na kabla ya ujio wa Edmund,
mama yake Samantha aliingia akiwa na mfanyakazi wake wa nyumbani, wakiwa
na vyakula kwa ajili ya wawili hao.
“Nakushukuru sana baba’angu kwa kutusaidia kumtuliza huyu mwenzio.
Nakuomba usimsikilize baba yake, nisikilize mimi na Samantha, upo kwenye
mikono salama,” alisema mama yake Samantha, Edmund akaitikia kwa adabu na
kumshukuru kwa yote.
Chakula kikaandaliwa ambapo tofauti na siku zote, Samantha alikula sana huku
akiendelea kupiga stori za hapa na pale na Edmund, wakawa wanacheka kwa
furaha.
“Mwanangu, naomba kila muda wa chakula ukifika uwe unahakikisha unakula na
Samantha. Unajua siku zote huwa anatusumbua lakini leo amekuona pembeni yake
mpaka nimeshangaa jinsi alivyokula, akiendelea hivi atapona haraka,” alisema
mama yake Samantha na kusababisha wote waangue kicheko.
***
Baada ya kuona mpango wake wa kuwatenganisha Samantha na Edmund
umeshindikana kwa njia za kawaida, baba yake Samantha aliondoka hospitalini
hapo bila kuaga, huku akiwa na hasira kali ndani ya moyo wake.
“Lazima kile kibabu Shiwinga kitakuwa kinajua kila kitu na kiliamua kunificha,
sasa leo naenda kukifunza adabu,” alisema baba yake Samantha akiwa kwenye gari
lake, akichanja mbuga kuelekea Bagamoyo, nyumbani kwa mganga Shiwinga
huku kiunoni akiwa na bastola.
Kwa kilichotokea, alihisi kama Shiwinga amemsaliti sana na adhabu pekee
ambayo alikuwa akistahili ilikuwa ni kifo. Hakuna kitu ambacho hakuwa tayari
kuona kinatokea kama utajiri wake kupukutika kwa sababu ya makosa ya
mwanaye kuruhusu kuingiliwa kimwili na mwanaume.
“Nitafanya kila kitu kulinda utajiri wangu, hata ikibidi kuua watu wote
wanaonikwamisha,” alijisemea baba yake Samantha huku akikanyaga mafuta na
kusababisha gari liwe linakimbia kwa kasi kubwa.
Baada ya takribani dakika thelathini, tayari alikuwa amewasili Bagamoyo,
akaiacha barabara ya lami na kuingia upande wa kulia na kuanza kuifuata barabara
nyembamba ya vumbi iliyokuwa ikielekea nyumbani kwa mganga huyo.

99
Akawa anazidi kukanyaga mafuta kuelekea nyumbani kwa mganga Shiwinga huku
mara kwa mara akiikagua bastola yake kama ipo sehemu husika. Kwa jinsi
alivyokuwa amekasirika, alikuwa tayari kufanya chochote, roho ya akishetani
ilishampanda na hakukuwa na kitu chochote cha kumzuia kutimiza azma yake.
Mganga Shiwinga akiwa anaendelea na majukumu yake ya kawaida ya kuandaa
dawa za mitishamba na tunguli za kufanyia shughuli zake za kiganga, alishtuka
kuona nywele na vinyweleo vinamsisimka mwili mzima.
“Hiki nini tena,” alisema huku akiacha kila alichokuwa anakifanya na kukimbilia
kwenye chumba chake cha uganga. Kusisimkwa nywele na vinyweleo mwili
mzima, kwake ilikuwa ni ishara tosha kwamba kuna jambo halikuwa sawa.
Harakaharaka akakaa kwenye mkao maalum na kuseti mitambo yake ya kiganga
kwa lengo la kutaka kuona kilichokuwa kinakaribia kutokea. Ndani ya muda mfupi
tu baadaye, tayari rada zake zote zilikuwa zimewashwa na kumuonesha
kilichokuwa kinataka kutokea.
Kwa kutumia nguvu zake za giza, alifanikiwa kumuona baba yake Samantha akija
kwa kasi kubwa, hali iliyoashiria kwamba lazima atakuwa anakuja kwa shari,
akashusha pumzi ndefu na kuanza kutafakari nini cha kufanya.
Japokuwa alikuwa amefanya kazi kwa kipindi kirefu na baba yake Samantha,
alikuwa anazijua akili zake zinavyobadilika anapokuwa na hasira, hasa kwa
mambo ambayo yalikuwa yakihusu utajiri wake. Akajua asipochukua tahadhari,
anaweza kumdhuru kweli kama alivyofanya kwa Samantha wakati akijaribu
kumdhuru Edmund.
Harakaharaka aliinuka na kutungua furushi lililokuwa kwenye paa la nyumba yake,
akalitoa na kuanza kupekuapekua, akatoa kimfuko kidogo cha ngozi ya mnyama
wa porini ambacho ndani yake kulikuwa na unga mweusi.
Akachukua shuka jekundu na kujifunika nalo huku katikati ya miguu yake akiweka
kitezo kilichokuwa na mkaa, akaanza kunyunyiza ule unga mweusi kwenye mkaa
huku akizungumza kwa lugha aliyokuwa anaielewa mwenyewe. Moshi mwingi
mweusi ukaanza kufuka na kusambaa eneo lote la nyumba yake, akaendelea
kunuiza kwa muda mrefu.

100
SURA YA KUMI NA MOJA

Upande wa pili, baba yake Samantha alizidi kukanyaga mafuta lakini tofauti na
siku zote, alishangaa akizidi kuchanja mbuga tu bila kufika nyumbani kwa mganga
huyo.
“Nimepotea nini? Mbona sijawahi kufika huku?” alijiuliza baada ya kuona anazidi
kuchanja mbuga tu bila kufika. Ikabidi atafute nafasi na kugeuza gari lake,
akakanyaga mafuta kwa kasi kurudi alikotoka huku akiwa makini kuangalia njia ya
kuchepuka kuingia nyumbani kwa mganga huyo.
Hata hivyo, mpaka anafika kwenye barabara ya lami ya kuelekea Bagamoyo mjini,
hakufanikiwa kuiona njia hiyo, akabaki amepigwa na butwaa. Akatafuta sehemu
ya kugeuza na kuanza tena safari ya kwenda kwa mganga huyo.
Kama ilivyokuwa mara ya kwanza, alisafiri umbali mrefu bila kufika nyumbani
kwa mganga huyo, akashangaa anazidi kuzamia porini bila dalili zozote za kufika
kwa mganga huyo. Mara kwa mara alikuwa akiikagua bastola yake huku shauku ya
kukutana ana kwa ana na mganga huyo ikizidi kumpanda.
Hata hivyo, licha ya kupiga ‘mark time’ kwa muda mrefu, hakufanikiwa kufika
nyumbani kwa mganga huyo, baadaye akakata tamaa na kuamua kurudi jijini Dar
es Salaam huku akiwa na maswali mengi yaliyokosa majibu juu ya kilichotokea.
“Au amenifanyia dawa ya kunipoteza nini? Maana hashindwi yule,” aliwaza baba
yake Samantha wakati akiendelea na safari ya kurejea jijini Dar es Salaam. Kwa
kuwa mkewe alikuwa akimuuguza Samantha, nyumbani hakukuwa na mtu zaidi ya
walinzi na wafanyakazi wa ndani.
Alipowasili, moja kwa moja alienda mpaka kwenye chumba chake alichokuwa
anafanyia shughuli zake za kiganga ambacho hakuna mtu mwingine yeyote
aliyekuwa anaruhusiwa kuingia zaidi yake yeye mwenyewe. Akakaa humo kwa
muda mrefu akijaribu kufanya dawa za hapa na pale ili kunusuru mali zake
zisiendelee kuteketea.
Baada ya kujifungia kwa zaidi ya saa mbili, alitoka na kuendelea na shughuli
nyingine za pale nyumbani. Kwa kitendo alichooneshwa na binti yake, alijiapiza
kwamba hatarudi tena hospitalini hapo kumjulia hali.

101
“Nahisi kuna ulazima wa kusafiri kwenda Kasumbalesa, Sumbawanga kuongeza
nguvu za giza, maji yamenifika shingoni,” aliwaza baba yake Samantha wakati
akitafakari kuhusu uharibifu mkubwa wa vitega uchumi vyake uliotokea katika
mazingira ya kutatanisha.
Alipofikiria wazo hilo, alishusha pumzi ndefu kwani aliamini, kama ilivyotokea
kipindi alichokuwa anahangaika kutafuta utajiri kabla hajakutana na mganga
Shiwinga, lazima mambo yake yatanyooka tu kama mwanzo.
Masharti ya safari ya Kasumbalesa, mpakani kabisa kati ya Tanzania na Zambia
upande wa Sumbawanga, nyumbani kwa mganga Kiswigo Kachele, ilikuwa ni
lazima aondoke bila kuaga, jambo ambalo kwake halikuwa gumu kutokana na jinsi
alivyokuwa akiishi kibabe na familia yake.
Hakutaka kupoteza muda, harakaharaka akawasiliana na kampuni ya usafiri wa
ndege ya Katavi Airlines aliyokuwa akiitumia sana kwa safari za Sumbawanga,
akakamilisha taratibu zote kwa ajili ya safari ya kuelekea huko alfajiri ya siku ya
pili.
“Mtaalamu Kiswigo anaweza kunisaidia, sijui kwa nini sikupata wazo la
kukimbilia kwake haraka nilipoona mambo yameanza kwenda ndivyo sivyo,”
aliwaza baba yake Samantha. Siku hiyo ilipita, kesho yake alfajiri na mapema
aliwahi kuamka na kutoka na dereva wake aliyemuwahisha uwanja wa ndege.
“Usimwambie mtu yeyote kwamba umenileta uwanja wa ndege, tumeelewana?”
“Ndiyo bosi, nimekuelewa,” alijibu dereva kwa unyenyekevu, wakaagana ambapo
dereva huyo alirudisha gari nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kawaida.
Baba Samantha aliingia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na baada
ya taratibu zote kukamilika, aliingia ndani ya ndege na abiria wengine.
Baada ya abiria wote kukaa kwenye siti zao, sauti ya mhudumu wa ndege ilisikika
ikiwataarifu abiria wote kufunga mikanda, muda mfupi baadaye, ndege iliondoka
na kuanza kupasua mawingu kuelekea Sumbawanga.
“Lazima yule mtoto afe, na mganga Shiwinga naye anatakiwa kufa vilevile,
uchawi wa ‘Lyamba Lya Mfipa’ ndiyo dawa yao,” aliwaza baba yake Samantha
wakati ndege ikiendelea kupasua mawingu.
Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa angani, hatimaye ndege iliwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, tangazo likasikika kutoka kwenye vipaza

102
sauti vilivyokuwa ndani ya ndege hiyo, likiwataarifu abiria wote kufunga mikanda
wakati ndege ikijiandaa kutua.
Dakika kadhaa baadaye, ndege ilikuwa imeshasimama kabisa, abiria wote,
akiwemo baba yake Samantha wakaanza kuteremka. Baada ya kushuka tu, baba
yake Samantha alitembea harakaharaka na kuwapita abiria wengine, akatoka
mpaka nje ya uwanja huo na kukodi teksi.
“Nipeleke Kasumbalesa haraka,” alisema baba yake Samantha, dereva wa teksi
akawa ni kama anatafakari kidogo kwa sababu safari hiyo ilikuwa ndefu na ugumu
ulikuwa unaongezwa na ubovu wa barabara, hasa katika kipindi hicho ambacho
mvua kubwa zilikuwa zinaendelea kunyesha.
Hata hivyo, kwa kuwa pesa haikuwa tatizo kwa mzee huyo, alimuahidi kumpa
kiwango chochote atakachokitaka, cha msingi wafike. Baada ya dereva
kutangaziwa dau, alikubali na safari ya kuelekea kijijini huko ikaanza.
Njia nzima, baba yake Samantha alikuwa akiendelea kufikiria kuhusu adhabu
itakayomfaa Edmund, hakuna kitu alichokuwa tayari kukipigania kwa kadiri ya
uwezo wake wote, kama utajiri wake.
Safari haikuwa nyepesi, mara kwa mara gari lilikuwa likikwama kwenye matope
yanayonata, hali iliyosababisha wawili hao wawe wanashuka na kusaidiana
kulisukuma. Mpaka wanafika kwa mganga, baba yake Samantha alikuwa
amechafuka mwili mzima kwa matope ya udongo mwekundu.
“Itabidi unisubiri turudi wote mjini, kama nitachelewa sana basi nitakuongeza dau,
usiondoke tafadhali,” baba yake Samantha alimwambia dereva huyo, baada ya
kufika sehemu ambayo gari lisingeweza kuendelea na safari kutokana na
kukosekana kwa barabara, ikabidi yeye aanze kutembea kwa miguu kuelekea kwa
mganga huyo na kumuacha dereva teksi kwenye gari lake.
“Utajiri mgumu, yaani mzee huyu na heshima zake zote kumbe anakuja kwa
mganga wa kienyeji?” aliwaza dereva huyo wakati akimtazama baba yake
Samantha alivyokuwa anahaha kutafuta njia ya kupenya kuelekea nyumbani kwa
mganga maarufu, Kiswigo Kachele aliyekuwa anaishi katikati ya pori kubwa la
Kasumbalesa, mpakani kabisa mwa Tanzania na Zambia.
“Hahahaaa!” sauti nzito ya mtu aliyekuwa anacheka ilisikika baba yake Samantha
alipoukaribia mti mkubwa wenye matawi mengi yaliyofungana kiasi cha
kusababisha kigiza chini yake, ndani ya eneo la mganga huyo. Kutokana na uzito

103
wa sauti hiyo, ndege wengi waliokuwa kwenye mti huo walianza kuruka huku na
kule kukimbia.
“Nilijua utakuja! Mimi ndiyo fundi Kiswigo Kachele, mfalme wa ‘Lyamba lya
Mfipa’, vua viatu fuata njia ya upande wa kushoto,” ilisikika sauti hiyo na
kumfanya baba yake Samantha atetemeke kwa hofu. Japokuwa haikuwa mara yake
ya kwanza kufika kwa mganga huyo, mauzauza aliyokuwa anakutana nayo kila
akija, yalimfanya awe muoga sana.
Baada ya kuvua viatu kama alivyoelekezwa, baba yake Samantha aliifuata njia
nyembamba iliyokuwa upande wake wa kushoto, akawa anapita katikati ya majani
marefu yaliyokuwa na umande, akazidi kusonga mbele mpaka alipotokezea
sehemu yenye uwazi.
Kwa mbali, akaiona nyumba ya tembe ya mganga huyo iliyokuwa imejengwa kwa
miti na kuezekwa kwa nyasi. Akiwa bado anashangaashangaa, bundi wawili
walianza kumzunguka baba yake Samantha huku wakitoa milio ya kutisha,
akajikaza kiume na kutulia, akawa anawatazama bundi hao ambao baada ya
kumzunguka mara kadhaa, wote waliruka na kuelekea kwenye mlango wa ile
nyumba ya tembe, wakaenda kutua mlangoni, mmoja kushoto na mwingine kulia.
Bila hata kuuliza, baba yake Samantha alijua kwamba wale ni wasaidizi wa
mganga Kiswigo waliotumwa kwenda kumpokea, akatembea kufuata uelekeo wale
bundi walikoelekea na hatimaye akausogelea mlango wa ile nyumba ya tembe.
“Geuka nyuma na uingie kwa kutanguliza mgongo,” ile sauti iliyosikika kule
kwenye mti mkubwa, ilisikika tena, baba yake Samantha akatii maelekezo na
kuingia kinyumenyume mpaka ndani, ile sauti ikampa maelekezo mengine na
hatimaye akakaa juu ya ngozi ya mnyama wa porini ambaye hakumtambua ni
mnyama gani.
Baada ya kukaa na kutulia, vishindo vizito vya mtu vilianza kusikika kutokea
nyuma ya pale alipokuwa amekaa, akatulia kimya kwani alijua ndiyo mganga
Kiswigo alikuwa anatoka kwa ajili ya kuja kuonana naye
Mwanaume mzee mwenye umri wa kati ya miaka 80 na 85, mwenye nywele
nyingi zilizobadilika rangi na kuwa nyeupe kutokana na mvi, akiwa amejifunga
shuka jeusi na kutembelea mkongojo ambao kwa juu ulikuwa na fuvu la mnyama
wa porini, macho yake yakiwa mekundu ya kutisha, alitokeza mbele ya baba yake
Samantha na kukaa juu ya kiti cha miguu mitatu.

104
“Najua kinachokusumbua, mwanao amevunja masharti na kusababisha mwili wake
uchafuliwe na mwanaume, mkuu wa giza amekasirika sana na kama usingewahi
kuja, huenda ndani ya siku chache baadaye, utajiri wako ungekuwa umepukutika
wote na wewe ingebidi uchukuliwe msukule kwa ajili ya kwenda kuwasaidia
wenzako kazi kama ambavyo wamekuwa wakikusaidia wewe kwa kipindi chote
cha utajiri wako.
“Kibaya zaidi, umeshindwa kuitunza misukule inayokusaidia kazi na imeanza
kuingia mitaani, hujui kama wakipatikana wachungaji wenye upako wa ukweli
wanaweza kuwafungua vijakazi wetu na kusababisha watoe siri ya tulivyokuwa
tunawatumikisha? Ukirudia tena uzembe kama huu utaadhibiwa kulingana na
makosa yako,” alisema mganga huyo huku akionesha kuwa na hasira kali.
“Ulinielekeza kwenda kwa mganga Shiwinga wa Bagamoyo, siku za nyuma
alinisaidia sana lakini sasa hivi amenigeuka na yeye ndiyo chanzo cha yote haya.
Nataka yeye na kijana aliyenichafulia binti yangu wafe kwa namna yoyote, hata
ikibidi kuwatumia radi.
“Shiwinga siyo mwenzetu tena, alishasaliti kambi yetu na tunaendelea na mikakati
ya kumpoteza ingawa anatusumbua sana kwa sasa, nguvu zake zimeongezeka
sana,” alisema mganga huyo na kukohoa mfululizo, akafungua upindo wa shuka
alilokuwa amejifunga na kutoa ungaunga fulani ambao aliunusa na kupiga chafya
mfululizo kisha ghafla akayeyuka pale alipokuwa amekaa.
Sekunde chache baadaye, alirejea na kukaa vilevile lakini mkononi mwake alikuwa
na kitabu kilichochakaa sana, akakifutafuta vumbi juu yake na kumgeukia baba
yake Samantha.
“Matatizo yako yamefikia hatua mbaya, ni lazima utumie hiki kitabu kuweka
mambo sawa. Kinaitwa kitabu cha shetani, sijawahi kukitoa kumpa mtu yeyote
tangu niliporithishwa na marehemu babu yangu lakini kwa sababu ya matatizo
yako, nakupa ukakitumie kisha utakirudisha mambo yakiwa sawa, sogea
nikuoneshe namna ya kukitumia,” alisema mganga huyo kwa sauti ya kutetemeka
kisha akapiga tena chafya mfululizo.
Baba yake Samantha alisogea jirani na yule mganga ambapo alianza kumfundisha
namna ya kukitumia kitabu cha shetani, mganga akawa anamsisitiza kwamba ni
lazima afuate masharti yote anayompa vinginevyo anaweza kupata madhara
makubwa.
“Kabla hujakigusa kitabu hiki lazima uwe na udhu.”

105
“Udhu? Udhu ndiyo nini mtaalamu?”
“Kwani wewe unaabudu dini gani?”
“Mimi Mkristo.”
“Ndiyo maana hujui maana ya udhu. Namaanisha kabla hujakigusa hiki kitabu
lazima mwili wako uwe safi. Nitakufundisha namna ya kuchukua udhu. Pia
hutakiwi kuwa umetoka kukutana kimwili na mkeo au mwanamke yeyote ndani ya
kipindi cha saa ishirini na nne kabla ya kukitumia.
“Hutakiwi kunywa pombe au kutumia aina yoyote ya kilevi katika kipindi chote
utakachokuwa unakitumia kitabu hiki. Muda mzuri wa kukitumia kitabu, ni usiku
kuanzia saa saba mpaka alfajiri kabla adhana haijalia.
“Kabla ya kukitumia kwa mara ya kwanza, lazima ufunge kwa saa ishirini na nne,
usile wala kunywa kitu chochote kisha baada ya hapo, utakuwa unakula asubuhi na
mchana tu, usiku hutakiwi kula kitu chochote mpaka utakapomaliza kazi.
“Inachukua siku ishirini na moja kukamilisha mzunguko mmoja wa kutumia kitabu
hiki, kila siku inatakiwa uzifanyie kazi kurasa saba za kitabu hiki, kwa hiyo katika
muda wa siku ishirini na moja utakuwa umezifanyia kazi kurasa 147 na kitabu
chote jumla kina kurasa 441 ambayo ni mizunguko mitatu. Umenielewa?”
“Nimekuelewa mtaalamu.”
“Kingine cha muhimu, katika kila kurasa saba utakazokuwa unazisoma kwa siku
moja, kuna maelekezo ya nini cha kufanya. Lazima kila kitu kifanyike usiku wa
siku husika, hutakiwi kutumia mwanga wa taa za umeme kusomea, inatakiwa
utumie mishumaa mitatu, ukikosea masharti tusilaumiane,” alisema mganga huyo
kwa msisitizo, baba yake Samantha akawa anatingisha kichwa kuonesha kuelewa
alichokuwa anaambiwa.
“Haya njoo huku nikufundishe namna ya kuchukua udhu kisha nianze kukuelekeza
kwa vitendo namna ya kutumia kitabu,” alisema mganga huku akiinuka, baba yake
Samantha naye akainuka na kumfuata. Wakatoka nje kupitia mlango wa nyuma na
kwenda kwenye kisima kilichokuwa ndani ya eneo la mganga huyo.
Akachota maji kwa kutumia kata iliyotengenezwa kienyeji na kujaza maji kwenye
chungu kilichokuwa pembeni kisha akamuelekeza baba yake Samantha kukibeba
chungu hicho hadi bafuni.
“Inabidi kwanza uonge kuondoa janaba.”

106
“Janaba ndiyo nini?”
“Yaani wewe kila kitu hujui, nimechoshwa na maswali yako, nenda kaoge na
uhakikishe unajisafisha kila sehemu ya mwili wako,” alisema mganga huyo huku
akimpa baba yake Samantha mswaki wa mti.
Akabeba chungu kilichokuwa na maji na kuelekea kwenye bafu lililojengwa kwa
miti, akaoga kama alivyoelekezwa na mganga huyo kisha baada ya hapo, alitoka
na kurudi pale kwenye kisima ambapo yule mganga alikuwa akimsubiri.
Akaanza kumuelekeza namna ya kuchukua udhu kisha baada ya hapo, walirudi
tena ndani ambako maelekezo yaliendelea.
“Nimesahau kitu cha muhimu, unapotumia kitabu hiki ni lazima mavazi uliyovaa
nayo yawe safi. Hutakiwi kuvaa nguo yenye jasho au uchafu wa aina yoyote na
ndiyo maana huwa tunashauriwa kuvaa shuka jeupe.
“Inabidi ukifika kwako na wewe ukatafute shuka jeupe, kwa leo nitakuazima
langu,” alisema mganga huyo, akainuka na kuingia chumbani kwake, muda mfupi
baadaye akarejea akiwa na mashuka mawili, moja lake na jingine kwa ajili ya baba
yake Samantha.
“Kabadilishe hizo nguo zako, vua zote kisha ujifunge hili shuka,” alisema mganga
Kiswigo, baba yake Samantha akainuka na kuelekea kwenye chumba
alichoelekezwa, muda mfupi baadaye alirudi akiwa ameshabadilisha nguo na
kujifunga shuka jeupe.
Mganga Kiswigo akamuelekeza namna ya kukaa kisha akachukua kitabu na
kumkabidhi baba yake Samantha. Akamwambia akifungue.
“Mbona hakijaandikwa kitu?” alisema baba yake Samantha, mganga Kiswigo
akawa ni kama amekumbuka kitu, akamuonesha ishara kwamba amsubiri kidogo,
akainuka na kuelekea chumbani. Aliporudi, alikuwa na kichupa kilichokuwa na
unga mweusi, akamsogelea baba yake Samantha na kufungua kile kichupa.
“Itauma lakini inabidi ujikaze,” alisema na kuanza kumnyunyizia unga ule
machoni. Japokuwa alikuwa na roho ngumu, baba yake Samantha alishindwa
kujizuia kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi, akajikuta akipiga kelele kama
mtoto mdogo wakati unga ule ukimuingia machoni.
“Utazoea tu wala usijali, fumba macho na usifumbue mpaka nitakapokwambia,”
alisema mganga huyo, baba yake Samantha akatii, akaanza kuzungumza maneno

107
ambayo hakuyaelewa huku akimzunguka na kumpigapiga na usinga aliokuwa
ameushika. Baada ya kufanya hivyo mara kadhaa, alimwambia baba yake
Samantha afumbue macho.
“Hiki kitabu huwa kinasomwa kuanzia mwisho kuja mwanzo, anzia ukurasa wa
mwisho,” alisema mganga Kiswigo, baba yake Samantha akajifuta kwanza
machozi na kufuata alichoambiwa. Alipofungua ukurasa wa mwisho wa kitabu
hicho, alishangazwa sana na alichokiona.
Zile kurasa ambazo muda mfupi uliopita alikuwa akiziona kama hazijaandikwa
chochote, zilikuwa zimejaa maandishi mengi ambayo yalikuwa
yakibadilikabadilika, kikiwa pia na picha nyingi za kutisha.
“Mbona kipo hivi?”
“Ndiyo hivyo, utazoea tu baadaye.”
“Sasa mbona maandishi yanachezacheza na kubadilika.”
“Kinachochezacheza na kubadilika siyo maandishi, ni akili zako.”
“Akili zangu?”
“Ndiyo! Una udhaifu mkubwa kwenye akili zako. Inaonesha una hofu kubwa,
hujiamini, umejawa na visasi na chuki ndani ya moyo wako. Huwezi kukitumia
hicho kitabu ukiwa katika hali hiyo.”
“Sasa nitafanyaje mtaalamu?”
“Kwani Shiwinga hakukufundisha kufanya tahajudi?”
“Alinifundisha na najua lakini sijafanya kwa kipindi kirefu sana.”
“Ndiyo maana mambo yako yanakuendea kombo, huwezi kukitumia kitabu cha
shetani kama akili yako haijatulia na njia pekee ya kutuliza akili ni kwa kufanya
tahajudi,” alisema mganga Kiswigo na kukichukua kile kitabu kutoka kwenye
mikono ya baba yake Samantha.
“Sasa itakuwaje?”
“Inabidi ufanye kwanza tahajudi kwa dakika thelathini kisha ndiyo mambo
mengine yatafuatia,” alisema huku akiinuka na kumuoneshea ishara kwamba aanze
kufanya tahajudi kama alivyomuelekeza. Akatoka na kufunga mlango kwa nje,
akamuacha baba yake Samantha mle ndani.

108
Baba yake Samantha alikaa juu ya ngozi ya mnyama aliyoelekezwa kufanyia
tahajudi (meditation), akaikunja miguu na kukaa katika mkao uliomfanya atulie
pale chini, akainua shingo katika namna iliyotengeneza nyuzi tisini, mikono
akaiweka juu ya mapaja na kubana kidole cha shahada na kidole gumba kwa
mikono yote na kugeuzia upande wa juu.
Baada ya hapo alifumba macho na kuinua kidevu chake kidogo kama anayetazama
juu kidogo, akavuta pumzi ndefu kwa kutumia tumbo kisha akazishusha taratibu
huku akijitahidi kuelekeza uzingativu wake katika kutuliza akili zake.
Akawa anayatazama mawazo yanavyoingia na kutoka kwenye kichwa chake kwa
kutumia jicho la tatu huku akiendelea kuvuta pumzi ndefu na kuzitoa, akaendelea
kutulia na dakika kadhaa baadaye, alikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa,
ubongo wake ukiachia hisia zote mbaya zilizokuwa zimerundikana ndani ya mwili
wake.
Huku nje, mganga alikaa juu ya gogo la mjohoro lililokuwa nje ya nyumba yake
huku ndege wengi wa kutisha, wakiwemo bundi na popo wakimzunguka na
kupigana vikumbo. Akawa anapiga mbinja na kuongea maneno aliyokuwa
anayajua mwenyewe, wale ndege wakaanza kutua mmoja baada ya mwingine pale
alipokuwa amekaa.
Wengine walitua juu ya kofia kubwa ya mkeka aliyokuwa ameivaa, wengine
wakatua mabegani na wengine juu ya lile gogo alilokuwa amelikalia, kila mmoja
akawa anatoa mlio wake huku akiwa makini kuwasikiliza, akafumba macho na
kuendelea kutulia wakati wale ndege wakiendelea kutoa milio ya kutisha.
Alipokuja kusimama, wale ndege wote walikurupuka na kupotelea kwenye msitu
mkubwa uliokuwa umekizunguka kibanda chake, akajinyoosha na kuvua kofia
yake ya mkeka, akatingisha kichwa chake na kunguruma kama mnyama wa porini
kisha akaingia ndani ya kibanda chake na kugonga kengele kubwa ya kizamani
iliyokuwa ukutani, kuashiria mwisho wa tahajudi ya baba yake Samantha.
“Unajisikiaje?”
“Najisikia mwepesi sana.”
“Wakati unafanya tahajudi na mimi nilikuwa nafanya mambo yangu hapo nje,
nimegundua kwamba umebadilika sana tangu mara ya mwisho ulivyokuja kwangu.
Kwa nini unatumia ushirikina kupata utajiri?” alihoji mganga Kiswigo, kauli
iliyoupasua moyo wa baba yake Samantha kama mkuki wenye ncha kali.

109
Mara ya mwisho alipofika kwa mganga huyo, baba Samantha alielekezwa kwamba
hakuna uchawi mkubwa kama akili zake ambazo kama akizitumia vizuri, zinaweza
kumpatia chochote alichokuwa anakitaka maishani mwake lakini baada ya
kuondoka, aliamua kutumia njia za mkato kwa kushirikiana na mganga Shiwinga
bila mtu yeyote kujua.
“Hebu niambie kikubwa kilichokuleta. Usinifiche kitu kwa sababu najua kila kitu,
nimezisoma fikra zako kwa hiyo ukiwa muongo utakuwa unafanya kosa jingine
kubwa sana,” alisema mganga Kiswigo kwa sauti ya kukwaruza. Ikabidi baba yake
Samantha awe mkweli.
“Nimekuwa nikimtumia binti yangu kama chambo cha kupata misukule ya
kuniingizia utajiri. Tulimfanyia zindiko kwamba kila mwanaume atakayejaribu
kufanya naye mapenzi afe katika mazingira ya kutatanisha kisha tunamgeuza kuwa
msukule.
“Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifanya hivyo, najua ni kinyume na makubaliano
yetu, naomba unisamehe sana, Shiwinga ndiye aliyenishawishi kufanya hivyo,”
alisema baba yake Samantha huku kijasho chembamba kikimtoka licha ya hali ya
hewa ya baridi ya eneo hilo.
Maelezo hayo ya baba yake Samantha yalisababisha mganga huyo apige chafya
mfululizo, hali ya hewa nje ikaanza kubadilika ghafla, wingu zito likaanza kutanda
na muda mfupi baadaye, radi kali zilianza kupiga mfululizo na kupasua miti
mikubwa iliyokuwa kwenye pori lililozunguka nyumba ya mganga huyo.
Miti mikubwa minne ilichanwachanwa vibaya na radi hizo na kufuatiwa na mvua
kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali. Kwa muda wote huo, mganga
Kiswigo alikuwa akizungukazunguka mle ndani huku akiendelea kupiga chafya
mfululizo, machozi mengi yakimtoka utafikiri mtu aliyekula ugoro mkali.

110
SURA YA KUMI NA MBILI

Alipokuja kukaa chini na kutulia, ile mvua kubwa ilikoma kunyesha, wingu
likayeyuka na kwa mbali kijua kikaanza kuchomoza, baba yake Samantha akawa
anaendelea kutetemeka kuliko kawaida.
“Ninyi ni mashetani, wewe na huyo Shiwinga mnapaswa kuadhibiwa vikali kwa
makosa makubwa mliyoyafanya. Una bahati umekuja kukiri kwangu, vinginevyo
hizo radi zote zilizoangusha miti huko nje zilikuwa zinakuja kupiga nyumba yako
wewe na familia yako mkiwa ndani.
“Umepatwa na nini mpaka ukawa na tamaa kali kiasi cha kuamua kuhatarisha
maisha ya wengine ilimradi wewe ufanikiwe? Katika umri wangu huu, sijawahi
kufanya hivyo hata mara moja. Ningeamua kutumia nguvu zangu nilizonazo,
huenda ningekuwa tajiri namba moja duniani lakini unafikiri kwa sababu gani
sijafanya hivyo?
“Na kibaya zaidi, nimegundua kwamba hata safari yako ya kuja huku ilikuwa ni
kwa ajili ya kukatisha maisha ya watu wawili, uongo kweli?”
“Kweli mtaalamu.”
“Mimi huwa siendekezi watu wa aina yako, nataka watu ambao wanatumia nguvu
za akili zao kwa msaada wa elimu mbalimbali kama hicho kitabu cha shetani
kujipatia chochote wanachokitaka, siyo kupata utajiri kwa kutoa watu wengine
kafara.
“Sasa kwa adhabu yako, utajiri wako wote utapukutika na utaanza na moja! Utakaa
na mimi kwa siku saba, ndani ya hizo, tatu utafukiwa kaburini, mbili utalala juu ya
mbuyu na mbili utalala kwenye maji ili kuondoa nguvu zote mbaya zilizokuingia
kwa sababu ya tamaa zako. Vinginevyo siku zako kuishi zinahesabika,” alisema
mganga Kiswigo na kusababisha baba yake Samantha awe mdogo kama Piriton.
Zile mbwembwe zote alizokuja nazo ziliyeyuka, ikafikia kipindi akawa anaijutia
nafsi yake. Hata hivyo, kwa sababu lengo lake lilikuwa ni utajiri, alijiapiza kuwa
liwalo na liwe, hawezi kuacha utajiri wake upotee.
“Nimekuja na dereva teksi nimemuacha kule nje ya msitu, naomba nikamwambie
aondoke tu.”

111
“Unataka kunikimbia si ndiyo? Hebu toka nje uangalie jinsi msitu wangu
ulivyoharibika kwa sababu ya upumbavu wako. Ukijaribu kutoroka
yatakayokukuta utakuwa umejitakia,” alisema mganga huyo huku akionesha
kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Baba yake Samantha akatoka nje lakini alichokutana nacho, kilisababisha aingie
ndani haraka. Akaingia ndani huku akitweta, hofu kubwa ikiwa imetanda kwenye
moyo wake.
“Nimekwambia usijaribu kunitoroka, mimi huwa sikimbiwi kirahisi kama
unavyofikiri. Kama ni huyo dereva wako nimeshatuma vijakazi wangu wakampe
taarifa, atakuwa ameshaondoka,” alisema Mganga Kiswigo huku akikaa vizuri.
Aliendelea kumsema baba yake Samantha kwa ukatili mkubwa aliokuwa
anaufanya kwa lengo la kutaka utajiri kwa njia zisizo sahihi, akamsisitiza kwamba
atamfanyia dawa kali ambazo endapo akithubutu tena kujipatia utajiri kwa njia
kama alizozitumia mwanzo, atakufa kifo kibaya.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, mganga Kiswigo alimuingiza baba yake
Samantha kwenye chumba kilichokuwa na giza, akawasha mshumaa na
kumuonesha sehemu ya kukaa. Chumba kizima kilikuwa kimejaa tunguli, mafuvu
ya wanyama, ngozi, mikia, na mifupa, hali iliyomfanya baba yake Samantha akae
kwa wasiwasi mkubwa.
“Jambo la kwanza inabidi kwanza unyolewe hizonywele zako,” alisema mganga
huyo huku akichukua kisu kikali na kuanza kukinoa kwenye jiwe lililokuwa ndani
ya chumba hicho, akatoka nje na aliporejea, alikuwa na bakuli la bati lenye maji
ndani yake.
Akachanganya na dawa nyeusi ya ungaunga kisha akamwambia baba yake
Samantha ajisafishe kichwa chake. Akamuelekeza namnaya kukaa na muda mfupi
baadaye, kazi ya kumnyoa nywele ilianza. Kwa ustadi mkubwa, mganga Kiswigo
alimnyoa nywele zote baba yake Samantha, kichwa kizima. Baada ya kumaliza
kumnyoa alimpaka dawa nyingine ya maji na kumalizia kumpaka nyingine ya
unga.
Akatoka kwenda kwenye chumba kinginena kumuacha baba yake Samantha mle
ndani, muda mfupi baadaye alirejea akiwa na kimkoba kidogo, akakiweka chini,
mbele ya baba yake Samantha na kukifungua.
***

112
“Kwani baba yako ameenda wapi? Mbona ananiweka roho juu jamani?”
“Siyo kwamba mimi ndiyo nilitakiwa nikuulize wewe? Mimi niko hospitalini
nitajuaje alikoenda? Kwani si mlilala pamoja mama?”
“Ndiyo tulilala pamoja lakini asubuhi wakati naamka nilishtukia mwenzangu
akiwa ameshaondoka.”
“Umejaribu kumpigia simu?”
“Hapatikani hewani, yaani nachanganyikiwa mwenzenu basi tu.”
“Ukimuuliza mlinzi anasemaje?”
“Anasema aliondoka alfajiri na dereva wake.”
“Na huyo dereva ukimuuliza anasemaje?”
“Anasema alimpeleka mjini na kumuacha huko,” mama yake Samantha alikuwa
akijadiliana na mwanaye wakiwa kwenye wodi aliyolazwa Samantha. Tofauti na
alivyotegemea, Samantha alizipokea taarifa hizo kwa hisia tofauti kabisa, akajua
ule muda aliokuwa anausubiri umewadia.
Mama yake alipotoka kwenda kumnunulia matunda baada ya kuwa ameshakula
chakula cha mchana, harakaharaka alimgeukia Edmund ambaye muda wote
alikuwa amekaa kimya, akiwaza yake.
“Umesikia mama alichokuwa ananiambia?”
“Nimesikia vizuri.”
“Wewe unasemaje?”
“Nasemaje kuhusu nini mpenzi wangu!”
“Ninavyomjua baba, akiondoka bila kuaga kama hivi, anaweza kukaa hata siku
mbili au tatu bila kurudi nyumbani. Kwa vyovyote atakuwa ameenda kwa waganga
wake, unaonaje tutumie nafasi hii kutoroka?”
“Mh! Si tulishazungumza mpenzi wangu? Huonikama ni hatari sana? Isitoshe
wewe bado hujapona.”
“Hakuna cha hatari, please usiniangushe Edmund, mbona unakuwa kama siyo
mwanaume?” alisema Samantha, kauli iliyomfanya Edmund ajiinamie kwa
sekunde kadhaa, akatafakari kwa kina na alipoinuka, alimtazama Samantha usoni.

113
“Vipi umeamua nini?”
“Japokuwa ni hatari, nipo tayari kufanya chochote utakachosema mpenzi wangu,
sitaki kukuangusha,” alisema Edmund, kauli iliyomfurahisha sanaSamantha,
akatanua mikono yake kama ishara ya kumtaka Edmund amkumbatie, naye
akafanya hivyo. Wakakumbatiana kwa nguvu huku msichana huyo akimbusu
Edmund sehemu mbalimbali.
“Vipi kuhusu mama?”
“Hatakiwi kujua chochote kwa sasa, anaweza kutuharibia mipango yetu.”
“Na vipi kuhusu huo mguu wako.”
“Utapona mbele ya safari, hapa cha kufanya ni kuchonga dili na daktari wangu
anayenitibu aturuhusu kuondoka, mengine tutajua mbele ya safari,” alisema
Samantha huku akigeuka hukuna kule kuangalia kama hakuna mtu aliyekuwa
anawasikiliza.
Baada ya kukubaliana, bila kupoteza muda Samantha alichukua simu yake na
kuanza kuzungumza na mhasibu wao.
“Naomba uende benki ukahamishe shilingi milioni ishirini kutoka kwenye akaunti
ya kampuni na kuniingizia kwenye akaunti yangu ya Barclays, nina shida nazo
haraka.”
“Lakini mzee alisema kwa fedha nyingi kiasi hicho ni lazima aidhinishe
mwenyewe.”
“Hebu nisikilize ninachokwambia. Nimeshaongea naye na yeye ndiyo ameniambia
nifanye hivyo, kuna dharura,” alisema Samantha, mhasibu huyo akamuitikia na
kuanza utekelezaji wa alichoambiwa mara moja.
“Akituhamishia hizo fedha, nikichanganya na zilizopo kwenye akaunti zangu
nyingine, zitafika karibu shilingi milioni hamsini. Si zinatutosha kabisa kuanza
maisha?” alisema msichana huyo, Edmund akawa anatingisha kichwa kuonesha
kukubaliana na alichokisema Samantha huku akilini mwake akishangaa jinsi
msichana huyo alivyokuwa akizungumzia kiasi kikubwa namna hiyo cha pesa
kirahisi utafikiri anazungumzia fedha za kawaida kabisa.
“Milioni hamsini? Sijawahi kufikiria hata siku moja kwamba naweza kushika kiasi
hicho cha fedha,” aliwaza Edmund. Kama walivyokubaliana, Samantha aliomba

114
kuonana na daktariwake ambapo alipofika, alimueleza mpango wake na kumtaka
awasaidie.
Alipotangaziwa dau la fedha tu, daktari huyo alikubali na kuahidi kuifanya kazi
hiyo siku hiyohiyo kwa usiri mkubwa. Akiwa hana hili wala lile, mama yake
Samantha alirejea wodini akiwa na matunda, akamuandalia mwanaye huku
akiendelea kulalamika kuhusu ishu ya mumewe kuondoka bila kumuaga.
Ilipofika jioni, aliaga na kuondoka kwa makubaliano kwamba atakuja tena
asubuhi, akamuacha Samantha mikononi mwa Edmund huku akisisitiza kwamba
kama kutatokea tatizo lolote, ampigie simu haraka.
Alipoondoka tu, harakaharaka mipango ilianza kufanywa, yule daktari akaingia
wodini akiwa ameongozanana manesi wawiliwaliokuwa wakisukuma kiti cha
magurudumu (wheel chair), wakasaidiana kumkalisha Samantha huku Edmund
akikusanya vitu vyake.
Alipomaliza, walitoka mpaka kwenye maegesho ya magari ya kubebea wagonjwa,
wakaingia kwenye ambulance ambayo tayari ilishaandaliwa. Muda mfupi baadaye,
ambulance hiyo ilitoka hospitalini hapo ikipiga ving’ora, kila mtu akiamini
kwamba ndani yake kulikuwa na mgonjwa aliyezidiwa, aliyekuwa akihamishwa na
kupelekwa kwenye hospitali kubwa.
Breki ya kwanza ilikuwa ni Ubungo Maziwa, gari la kubebea wagonjwa likaiacha
Barabara ya Morogoro na kuingia ndanindani mpaka kwenye hoteli moja ya
kifahari iitwayo Highway View iliyokuwa eneo hilo.
Gari likaingia mpaka ndani ambapo Edmund kwa kusaidiana na wahudumu wa
hoteli hiyo walisaidiana kumteremsha Samantha na kumuingiza hadi mapokezi.
Harakaharaka Edmund alitoa fedha za kumlipa dereva wa ambulance na muda
mfupi baadaye, gari hilo likaondoka.
“Tunataka chumba, kesho asubuhi tunasafiri kwenda mkoani kwa hiyo tumeamua
kuja hapa kwa sababu ni jirani na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani,”
Edmund alijieleza pale mapokezi.
Harakaharaka wakapewa chumba kilichokuwa ghorofa ya chini kabisa, jirani na
mlango mkubwa wa kutokea ili isiwe tabu wakati wa kuingia na kutoka kwa
sababu bado Samantha alikuwa akitumia kiti cha magurudumu. Baada ya
kukamilisha kila kitu, wawili hao waliingia mpaka chumbani.

115
“Siamini kama tumefanikiwa kuondoka kilaini kiasi hiki,” alisema Samantha huku
akitanua mikono yake kama ishara ya kutaka kumkumbatia Edmund ambaye naye
alisomgelea na kumkumbatia msichana huyomrembo, wakagandana kama ruba
kwa dakika kadhaa.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda, wawili hao waliagiza chakula ambacho
kililetwa na wahudumu wa hoteli hiyo, wakala huku wakiendelea kupiga stori za
hapa na pale, kila mmoja akionesha kuwana furaha kubwa ndani ya moyo wake.
Baada ya kumaliza kula, Edmund alienda kumuogesha Samantha kwani bado
hakuwa na uwezo wa kuoga mwenyewe kisha akamrudisha kitandani na kumlaza
vizuri. Naye akaenda kuoga na muda mfupi baadaye, wote wawili walikuwa
kitandani.
“Edmund, utaendelea kunidekeza hivihivi hata ukinioa au ndiyo unaniektia?”
Samantha alihoji akiwa amelala juu ya kifua cha Edmund aliyekuwa
amemkumbatia kimahaba.
“Nitakupenda na kukudekeza siku zote za maisha yangu, siyo leo na kesho tu, bali
katika siku zote za uhai wangu, kifo ndiyo kitakachotutenganisha,” alisema
Edmund na kumbusu msichana huyo mdomoni, kauli iliyomfurahisha sana.
Waliendelea na mazungumzo yao, wakawa wanapanga mipango ya safari yao na
jinsi watakavyoenda kuyaanza maisha mapya.
“Nina marafiki zangu wengi Arusha, na tayari nimeshamwambia mmoja atutafutie
nyumba ya kupanga maeneo ya Njiro, unajua kuishi hotelini ni gharama sana,”
alisema Arianna, wazo ambalo Edmund alikubaliana nalo, moyoni akawa
anajipongeza kwani Samantha alionesha kuwa na akili za kimaendeleo sana.
Baadaye walipitiwa na usingizi wakiwa wamekumbatiana kimahaba mpaka alfajiri
ya siku ya pili walipokuja kugongewa mlango na wahudumu wa hoteli hiyo kama
walivyokuwa wamewaomba. Harakaharaka Edmund aliamka na kuanza
kumuandaa Samantha, akaenda kumuogesha na kumvalisha nguo nzuri, na yeye
akaoga na muda mfupi baadaye alitoka kwenda kutafuta teksi.
Dakika kadhaa baadaye, alirudi na teksi, wakasaidiana na dereva wa teksi pamoja
na wahudumu wa hoteli hiyo kumtoa Samantha na kwenda kumpakiza kwenye
teksi hiyo, wakaaga na kuondoka kuelekea kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi ya
Mikoani cha Ubungo.

116
Baada ya kulipa nauli na kupewa tiketi, Samantha alipandishwa na kwenda
kukalishwa kwenye siti yake, Edmund akasimamia mizigo yao yote nayo
ikapakizwa kisha akaenda kukaa pembeni ya Samantha, ndani ya basi jipya na la
kisasa la Dar Express. Wakawa wanasubiri muda wa basi kuondoka.
***
Baada ya kupambazuka, mama yake Samantha aliwahi kuamka kama kawaida
yake, akasaidiana na msichana wake wa kazi kuandaa kifungua kinywa kwa ajili
ya mwanaye na Edmund. Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa ndani ya gari akiwa
na dereva wao, wakawa wanaelekea hospitalini alikolazwa Samantha.
Walipofika hospitalini, aliteremsha mizigo yake na kuelekea mapokezi moja kwa
moja, akamsalimia nesi aliyemkuta kisha akawa anaongoza kwenye korido ya
kuelekea kwenye wodi aliyolazwa mwanaye.
“Mh! Mama samahani mara moja,” nesi aliyekuwa mapokezi alimuita mama yake
Samantha baada ya kuona kuna jambo halikuwa sawa. Kwa jinsi alivyokuwa
anafahamu, ni kwamba mgonjwa wake tayari alikuwa ameruhusiwa kutoka usiku
uliopita, akashangaa kumuona akileta kifungua kinywa wakati hakukuwa na mtu
wodini.
“Ameruhusiwa? Ameruhusiwa na nani na ameenda wapi? Mbona mimi natokea
nyumbani sasa hivi, isitoshe mwanangu bado hajapona, nani aliyemruhusu?”
alihoji mama yake Samantha huku akionesha kuchanganyikiwa kabisa.
Hakutaka kuamini maneno yanesi huyo, alitaka kuhakikisha mwenyewe, akaenda
mpaka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa mwanaye, alipofungua mlango na
kutazama ndani, mapigo ya moyo wake yalimlipuka mno baada ya kuamini
kwamba ni kweli alichoambiwa.
“Msitake kunitania, nitawafunga nyote nyie, hivi mnanijua au mnanisikia?
Namtaka mwanangu,” alisema mwanamke huyo na kusababisha vurumai kubwa
hospitalini hapo, hali ya sintofahamu ikatanda.
Kwa bahati nzuri, muda mfupi baadaye mganga mkuu wa hospitali hiyo aliwasili,
akashangaa kukuta vurumai kubwa hospitalini kwake, ikabidi amuite mama yake
Samantha ofisini kwake kwa lengo la kutaka kufahamu kilichotokea.
Baada ya kumueleza kilichotokea, ufuatiliaji ulianza kufanyika haraka ambapo
baadaye ilifahamika kwamba msichana huyo aliruhusiwa kimakosa baada ya kula
njama na mmoja wa madaktari hospitalini hapo na dereva wa ambulance.

117
Ilibidi taarifa zitolewe polisi haraka, dakika kadhaa baadaye, askari kadhaa wakiwa
kwenye difenda walifika hospitalini hapo na kumuweka chini ya ulinzi daktari
aliyehusika kumtorosha Samantha pamoja na dereva wa ambulance. Baada ya
kubanwa, ilibidi waeleze ukweli wa mahali walikowapeleka Samantha na Edmund.
Hakukuwana muda wa kupoteza, wale askari wakatoka na difenda yao, wakiwa na
yule daktari, dereva wa ambulance, mganga mkuu na mama yake Samantha
kuelekea Ubungo Maziwa kwenye hoteli wawili hao walikopelekwa.
Njia nzima mama yake Samantha alikuwa akijaribu kupiga simu ya mwanaye
ambayo ilionesha kwamba imezimwa, hata alipopiga ya Edmund majibu yalikuwa
ni yaleyale. Alipompigia mumewe, naye hakuwa akipatikana hewani na hakuwa na
taarifa zozote za mahali alikoenda kwani aliondoka nyumbani bila kuaga.
Mwanamke huyoakazidi kuchanganyikiwa, machozi yakawa yanamtoka kama
mtoto mdogo.
Walipofika hotelini hapo, wahudumu pamoja na meneja wa hoteli waliwataarifu
kwamba wawili hao wameondoka muda mfupi uliopita kuelekea stendi ya mabasi
ya Ubungo lakini hawakuwa wakijua wanasafiri kuelekea wapi.
“Mungu wangu, wameamua kutorokea wapi? Nitamjibu nini mume wangu?”
alisema mama yake Samantha huku akiwahimiza wale askari kuwahi stendi ya
mabasi ya Ubungo kama wanaweza kuwakuta wakiwa bado hawajaondoka.
Difenda iligeuzwa na kwa kasi kubwa safari ya kuelekea stendi ikaanza. Kwa
kuwa hapakuwa na umbali mrefu, dakika chache baadaye tayari walishawasili
kituoni hapo.
Licha ya askari kujitahidi kufika haraka kwenye Stendi ya Mabasi, Ubungo,
hawakufanikiwa kuwapata Samantha na Edmund kwani tayari basi walilokuwa
wamepanda, lilishaondoka muda mfupi kabla askari hao hawajafika.
Kazi kubwa waliyoifanya yakuzuia mabasi yote yasiondoke na kuanza kukagua
moja baada ya jingine, haikuzaa matunda zaidi ya kusababisha usumbufu kwa
abiria wengine waliokuwa wakitaka kusafiri asubuhi hiyo.
“Tumejitahidikadiri ya uwezo wetu lakini wewe mwenyewe ni shahidi,
hatujawapata,” askari aliyeonesha kuwa na mamlaka kuliko wenzake, alimwambia
mama yake Samantha ambaye muda wote alikuwa akilia kama mtoto mdogo.
***

118
Basi liliendelea kuchanja mbuga kwa kasi kubwa kuelekea Arusha huku Edmund
na Samantha wakipiga stori za hapa na pale na kucheka kwa furaha. Hakuna
aliyeamini kwamba walifanikiwa kuondoka kirahisi namna ile.
“Nataka nikipona mguu tu nikubebee mimba, hata wakija kugundua tupo wapi
watakuwa wamechelewa sana maana tayari nitakuwa na kiumbe chako tumboni
mwangu,” alisema Samantha huku akilishika tumbo lake, tabasamu pana likiwa
limechanua kwenye uso wake.
Baada ya safari ndefu, hatimaye waliwasili Arusha, wakatafuta hoteli nzuri kwa
ajili ya mapumziko wakati wakiendelea na taratibu za kutafuta chumba cha
kupanga.
“Nadhani huu ni muda muafaka wa kuzungumza na mama ili asiendelee kuwa na
wasiwasi, washa simu yako basi umpigie,” alisema Edmund, wazo ambalo
msichana huyo alilikubali. Ile anawasha tu simu yake, meseji nyingi zilianza
kuingia mfululizo na kabla hata hajajua aanze kuisoma ipi, simu ilianza kuita.
Alipotazama namba ya mpigaji, hakuwa mwingine bali mama yake.
“Huyo anapiga,” alisema Samantha na kushusha pumzi ndefu, akaipokea. Kitu cha
kwanza alichokutana nacho ilikuwa ni sauti ya kilio ya mama yake.
“Samantha uko wapi mwanangu? Uko salama? Angalia mama yako ninavyolia
kama mtoto mdogo, nielekeze mahali ulipo nakuja kukuchukua sasa hivi,” alisema
mama yake Samantha bila kuweka nukta, ikabidi Samantha amueleze kwamba
yupo salama ingawa hataweza kurudi nyumbani.
Alimueleza kwa kirefu kwamba yupo na Edmund na wameamua kutoroka ili
kumkwepa baba yake ambaye alikuwa akiwakosesha raha. Akamuomba msamaha
mama yake kwa kuondoka bila kutoa taarifa na kumsababishia usumbufu mkubwa
kiasi hicho.
“Unataka baba yako aniue? Unafikiri nitamwambia nini?” alihoji mama yake
Samantha, wakaendelea kuzungumza kwa muda mrefu huku akimsisitiza mwanaye
huyo kurudi lakini haikusaidia kitu.
Mpaka simu inakatwa, hawakuwa wamefikia muafaka zaidi ya Samantha
kuendelea kushikilia msimamo wake kwamba hayupo tayari kurejea nyumbani
kwa kipindi hicho.
***

119
Baada ya kukosa mbinu za kutoroka, ilibidi baba yake Samantha awe mpole,
akakubali kufuata maelekezo ya Mganga Kiswigo ambapo jambo la kwanza
alinyolewa nywele zote kwa kutumia kitu kikali, akapakwa mafuta maalum
yaliyosababisha kichwa chake kiwe kinang’aa sana.
Baada ya hapo, akaondoka na mganga huyo nakuingia kwenye msitu mkubwa
uliokuwa jirani na nyumba yamganga huyo, miti mingi ikiwa imechanwachanwa
na radi, huku maeneo mengine maji yakiwa yanaendelea kumiminika kwani
haukupita muda mrefu tangu mvua ikatike.
Inatakiwa tuchimbe kaburi hapa kufuata usawa huu,” alisema mganga Kiswigo
huku akimuonesha baba yake Samantha kwa vitendo. Bila kupoteza muda, mganga
akazama kichakani na muda mfupi baadaye aliporejea, alikuwa na jembe, sululu na
koleo, kazi ya kuchimba kaburi ikaanza mara moja huku baba yake Samantha
akiendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
“Kwani hili kaburi tunachimba la nini?”
“Nimeshakwambia utalala kaburini kwa siku tatu, hili ni lako.”
“Nilale kaburini? Kivipi?”
“Utajua tu, tuendelee kwanza na kazi, maswali siyo muda wake huu,” alisema
mganga Kiswigo na kazi ya kuchimba kaburi ikaendelea huku baba yake Samantha
akionesha kukosa raha kabisa.
Baada ya kumaliza kuchimba kaburi lililokuwa na urefu wa futikadhaa kwenda
chini, wanaume wawili waliokuwa wamebeba jeneza lililofunikwa kwa shuka
jeupe, walichomoza kutoka vichakani huku wakiimba nyimbo ambazo baba yake
Samantha hakuzielewa. Kitendo cha kuwaona watu hao, kilimshtua mno baba yake
Samantha kwani aliamini wapo wawili tu, yeye na mganga Kiswigo ndani ya msitu
huo.
Watu hao walisogea mpaka pale jirani yao na kulishusha lile jeneza, wakaliweka
pembeni ya kaburi kisha wote wakainama kama ishara ya adabu kwa mganga
Kiswigo ambaye naye alizungumza maneno ambayo baba Samantha hakuyaelewa,
akashtukia wote wakimzunguka.
“Inabidi ujikaze kwa sababu haya mambo umeyasababisha wewe mwenyewe,”
alisema mganga Kiswigo huku akifungua kichupa kilichokuwa na dawa nyeusi,
akamimina kidogo mkononi kisha akamsogelea baba yake Samantha ambaye bado
hakuwa akielewa kinachotaka kutokea.

120
SURA YA KUMI NA TATU

Akampulizia usoni na muda mfupi baadaye, akadondoka chini kama mzigo, akiwa
amepoteza fahamu. Alipokuja kuzinduka, alijikuta akiwa ndani ya jeneza, akaanza
kugongagonga mbao za jeneza hilo na kupiga kelele za kuomba msaada lakini
hakuna aliyemsikia.
Joto kali na hewa nzito vilivyokuwepo eneo hilo, vilimfanya aamini kwamba
mganga Kiswigo ametimiza alichokisema kwa kumzika akiwa hai. Alipokumbuka
kwamba mganga huyo alimwambia atakaa humo kwa siku tatu, alizidi
kuchanganyikiwa, akawa anakiona kifo mbele yake.
Alilia sana kila alipokuwa akifikiria hatima ya maisha yake. Ni kweli alikuwa
akiupenda utajiri lakini kilichokuwa kinamtokea, aliona kama kimemzidi uwezo.
Akiwa anaendelea kulia, alisikia vishindo kwa mbali vikisogea mahali pale,
akatulia na kuanza kuvisikilizia. Vishindo vikawa vinazidi kuongezeka mpaka
jirani kabisa na pale alipokuwa.
“Msaada! Jamani msaada nakufa, nisaidieni,” baba yake Samantha alianza tena
kupiga kelele huku akipigapiga mbao za jeneza lile. Kwa mbali akaanza kusikia
kama lile kaburi alilokuwa amezikwa ndani yake, linaanza kufukuliwa. Akawa
anasikia vishindo vya hapa na pale, jambo lililompa matumaini makubwa kwamba
hatimaye alikuwa anaenda kuokolewa.
Tofauti na mategemeo yake, baada ya vishindo vya muda mrefu, hatimaye jeneza
alilokuwa amelazwa ndani yake lilifunguliwa upande wa kichwani, hali iliyompa
upenyo wa kutazama nje ingawabado hakuweza kutoka.
Mganga Kiswigo, akiwa amejifunga nguo nyeupe mwili mzima, alimuinamia
babayake Samantha pale ndani ya jeneza, akatoa kibuyu na kuanza kukitingisha
kwa nguvu kisha akakifungua na kujimimia unga mweusi kiganjani.
Akawa ni kama ananuiza maneno ambayo baba yake Samantha hakuyaelewa kisha
baada ya hapo akampulizia ule unga usoni. Kama ilivyokuwamara ya kwanza,
ndani ya sekunde chache tu, baba Samantha alijikuta akipitiwa na usingizi mzito,
kwa mbali akasikia jeneza likifungwa tena na kufuatiwa na vishindo vya udongo,
kuonesha kuwa alikuwa akifukiwa tena kwa mara nyingine.
***

121
Mpaka simu inakatwa, Samantha na mama yake hawakuwa wamefikia muafaka
zaidi ya msichana huyo kuendelea kushikilia msimamo wake kwamba hayupo
tayari kurejea nyumbani kwao, jijini Dar es Salaam kwa kipindi hicho.
“Vipi anasemaje?”
“Anasema turudi nyumbani, eti baba hatamuelewa halafu anaonekana ananihofia
sana mimi kwa sababu ya huu mguu.”
“Mama yako anakupenda sana, hataki upate shida hata kidogo.”
“Sasa kwani mimi hapa napata shida? Nikiwa nyumbani ndiyo napata shida.”
“Lakini unajua kama mzazi atakuwa anajisikia vibaya sana, unaonaje ukinipa simu
ili niongee naye na kumtoa wasiwasi?”
“Mh! Unafikiri itasaidia chochote?”
“Itasaidia, naamini itasaidia,” alisema Edmund kwakujiamini, hali iliyomfanya
Samantha akose cha kujibu zaidi ya kumpa simu yake. Muda mfupi baadaye,
Edmund alikuwa akizungumza na mama yake Samantha ambaye bado alikuwa
akilia kwa uchungu.
“Wewe ndiyo umemtorosha mwanangu Edmund, si ndiyo?”
“Siyo hivyo mama, nakuomba unielewe, nipo chini ya miguu yako ndiyo maana
nimeona nikupigie nizungumze na wewe moja kwa moja.”
“Uzungumze ninina mimi Edmund? Nilikuamini nikakuacha na mwanangu kumbe
mlikuwa mnapanga kutoroka?”
“Lakini mama…”
“Lakini nini Edmund?”
“Samantha yupo kwenye mikono salama.”
“Mikono salama ipi? Hujui huyo bado hajapona huo mguu? Unataka uoze?”
“Hapana, nitahakikisha anapata huduma zote za kimatibabu kila siku mpaka apone.
Nakuahidi nitamtunza na kumlea kama ulivyokuwa unafanya wewe wala usiwe na
wasiwasi, kama kukitokea tatizo lolote nitakuwa wa kwanza kukutaarifu,” alisema
Edmund kwa busara, kauli ambayo kidogo ilimtuliza mama yake Samantha.
“Kama ni hivyo naomba msizime simu ili muda wowote nitakaohitaji kuzungumza
nanyi muwe mnapatikana.”

122
“Hakuna tatizo mama,” alijibu Edmund kisha akakata simu. Samantha ambaye
muda wote alikuwa amejilaza pembeni akimsikiliza Edmund, aliachia tabasamu
pana na kutanua mikono yake kama ishara ya kutaka kumkumbatia, naye
akamuonesha ushirikiano.
“Unajua mwenzio mimi wazazi wangu hawataki kuamini kwamba nimeshakuwa
mkubwa na nahitaji kuwana maisha yangu, mpaka leo wananiona kama mtoto
mdogo,” alisema Samantha na kumbusu Edmund mdomoni.
Akaendelea kumshukuru kwa jinsi alivyoweza kuzungumza na mama yake na
kumtoa wasiwasi.
“Usiwe na wasiwasi mpenzi wangu, niliahidi nitakulinda na lazima nikuoneshe
kwa vitendo.”
Siku hiyo ilipita, kesho yake mipango ya kutafuta chumba cha kupanga ikaanza
kufanywa. Kwa kuwatumiamarafiki zake waliokuwa wakiishi jijini Arusha, kazi
ilikuwa nyepesi kwani walifanikiwa kupata nyumba yenye vyumba vitatu, sebule,
jiko na vyoo vya ndani (self container) iliyokuwakwenye mtaa tulivu wa Njiro.
Japokuwa kodi ilikuwa kubwa, Edmund na Samantha walilipa bila tatizo kwa
sababu fedha walizoondoka nazo jijini Dar es Salaam zilikuwa zikiwatosha.
Kilichofuatia ilikuwani kununua samani za ndani, kazi ambayo ilibidi ifanywe na
Edmund kwa sababu Samantha hakuwa na uwezo wa kuzunguka huku na kule
kutokana na jeraha la risasi mguuni kwake.
Siku mbili baadaye, nyumba ilikuwa imekamilika kwa kila kitu, kuanzia sebuleni,
jikoni mpaka chumbani. Ungeweza kudhani waliokuwa wanaishi ndani ya nyumba
hiyo ni vigogo fulani serikalini kwa jinsi nyumba ilivyokuwa na mandhari nzuri
kuanzia nje mpaka ndani.
Kama alivyokuwa ameahidi, Edmund alihakikisha anatafuta daktari maalum
ambaye kila siku alikuwa akienda kumsafisha Samantha kidonda na kumpa dawa
zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kumponesha kidonda chake.
“Ukiendelea hivi itabidi wiki ijayo nianze kukufanyisha mazoezi ya kutembea,
unapona kwa haraka sana,” alisema daktari baada ya kumaliza kumsafisha
Samantha jeraha lake, kauli iliyowafurahisha mno wote wawili. Hakuna kitu
ambacho Edmund alikuwa akitamani kuona kinatokea kama Samantha kupona na
kuwa kama zamani.

123
“Ahsante Edmund kwa kunihudumia vizuri, najua hata mama siku akiniona
ninavyopona kwa spidi atapunguza munkari wake,” alisema Samantha wakati
akisaidiana na Edmund kuandaa chakula cha jioni. Japokuwa Edmund alikuwa
nimwanaume, alikuwa akiweza kufanya shughuli zote za jikoni, kuanzia kwenda
sokoni, kupika, kuosha vyombo na kufanya usafi, jambo lililomfanya Samantha
azidi kuchanganyikiwa na penzi lake.
“Siku zote nilikuwa na ndoto za kuishi maisha kama haya, nakupenda sana
Edmund, sijawahi kudhani kwamba naweza kuja kumpenda mwanaume kiasi hiki.
“Yaani siku chache tu nilizokaa na wewe huku mbali, najihisi kama nipo peponi,”
alisema Samantha kwa hisia, wakiwa wamejilaza kitandani kwao baada ya
kumaliza kula chakula cha usiku, Edmund akaachia tabasamu pana na kumbusu
Samantha.
Wakiwa wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, simu ya Samantha ilianza
kuita, harakaharaka msichanahuyo akaipokea na kuiweka ‘loud speaker’. Alikuwa
ni mama yake Samantha na alichokisema, kilisababisha wote wawili
wabakiwamepigwa na butwaa, wakiwa ni kama hawaamini wanachokisikia.
“Watu kutoka serikalini wamekuja hapa nyumbani wanamsaka baba yako kwa
udina uvumba. Wanasema wana mashaka na namna alivyopata utajiri wake na
kuanzia leo wamezifungia akaunti zake za benki pamoja na kushikilia mali zote
anazomiliki na kuna uwezekano mkubwa wakazitaifisha.
“Kibaya zaidi mwenyewe mpaka leo hajarudi na haifahamiki yuko wapi, nahisi
kuchanganyikiwa,” alisema mama yake Samantha kwa sauti iliyoonesha dhahiri
kwamba alikuwa akilia.
Kwa kuwa simu ilikuwa imewekwa loudspeaker, Edmund naye alisikia kila kitu,
akabaki amepigwa na butwaa akiwa ni kama haamini alichokisikia. Baada ya
kumaliza kueleza, mama yake Samantha alikata simu na kuwaacha wawili hao
wakitazamana kama sanamu.
“Lakini mimi nilikuwa namwambia baba, haya mambo ya kujipatia utajiri kwa njia
zisizo halali mwisho wake huwa siyo mzuri akawa mbishi, sasa hata sijui
itakuwaje,” alisema Samantha huku akionesha kuchanganyikiwa.
“Usijali kuhusu utajiri wa baba yako, hayo ni makosa ambayo aliyafanya
mwenyewe, cha msingi sisi tuangalie namna ya kujenga maisha yetu na kupata
pesa kwa njia za halali.”

124
“Yaani hata hizi pesa tulizoondoka nazo naona kama zinatuletea tu mkosi,
natamani tuzipeleke kanisani au msikitini tukatoe sadaka,” alisema Samantha,
mjadala ukaendelea kwa muda mrefu na mwisho wakakubaliana kwamba
waendelee kuzitumia kuendeshea maisha yao wakati wakitafuta njia nyingine za
kupata pesa kwa njia ya halali kisha baada ya hapo ndiyo wataamua nini cha
kufanya.
***
Kama mganga Kiswigo alivyomwambia awali baba yake Samantha, kweli siku tatu
ziliisha huku akiwa kaburini, jambo ambalo hakuwahi kulihisi hata mara moja
kwamba linaweza kumtokea.
Baada ya siku hizo tatu kuisha, mganga Kiswigo akiwa na wasaidizi wake
walienda kufukua kaburi alilokuwa amefukiwa baba yake Samantha na kumtoa.
Kutokana na dawa kali alizokuwa akipuliziwa kila alipokuwa akirejewa na
fahamu, ukichanganya na njaa ya kutokula chochote kwa siku tatu mfululizo na
kukosa hewa safi, babayake Samantha alikuwa hajitambui.
Baada ya kufukua kaburi, walilitoa jeneza alilokuwa amelazwa ndani yake na
kulifungua, wakamtoa na kumvua sanda aliyokuwa amefungwa kama maiti,
akabebwa kwenye machela ya miti na kupelekwa mpaka nyumbani kwa mganga
Kiswigo akiwa bado hajitambui.
Akaanza kuogeshwa kwa maji yaliyochanganywa na dawa kisha nyingine
akanyweshwa ambapo muda mfupi baadaye, alianza kupiga chafya mfululizo na
kuzinduka, akawa anashangaa pale ni wapi na amefikaje.
“Kunywa hii upate nguvu,” alisema mganga Kiswigo na kumsaidia kuinuka,
akaegamia ukuta na kupewa bakuli lililokuwa na mchuzi uliochanganywa na dawa.
Baada ya kunywa, angalau alipata nguvu za kuweza kuzungumza.
“Leo ni lini?”
“Jumatatu.”
“Kwa hiyo nimekaa kaburini siku tatu?”
“Ndiyo, si nilikwambia tangu mapema? Bado siku nyingine mbili za kulala juu ya
mbuyu na nyingine mbili za kulala kwenye maji. Ulikuwa na nguvu mbaya sana
ndani ya mwili wako kwa sababu ya uovu ulioufanya. Narudia tena kukuonya,

125
ukirudia kufanya uliyoyafanya ujue kaburi linakuita,” alisema mganga Kiswigo
huku akiendelea kumuandalia dawa nyingine.
Siku tatu tu alizokaa kaburini, zilitosha kumbadilisha kabisa baba yake Samantha,
alidhoofika na kuwa mtu tofauti kabisa. Baada ya kumaliza kunywa mchuzi ule,
aliandaliwa chakula chepesi na wasaidizi wa mganga huyo, akawa anakula
harakaharaka utafikiri anafukuzwa kutokana na jinsi alivyokuwa na njaa kali.
Baada ya kumaliza kula, aliendelea kupewa dawa ambazo taratibu zilikuwa
zikimrejeshea nguvu zake mpaka giza lilipoingia.
“Inabidi ujiandae kama nilivyokwambia, kwa siku mbili hizi utalala juu ya ule
mbuyu mkubwa kule porini, inabidi ujikaze ili tumalize kazi, hakuna njia
nyingine,” alisema mganga Kiswigo na kumfanya baba yake Samantha akose cha
kujibu.
Kuna wakati mwingine alikuwa akijilaumu sana kwa makosa makubwa
aliyoyafanya wakati wa harakahati zake za kusaka utajiri kwa njia ya ushirikina.
Wakati mwingine aliona kama hata mateso aliyokuwa anapitia alistahili kutokana
na dhambi zake.
Muda ulizidi kuyoyoma na hatimaye muda wa kwenda kulala uliwadia ambapo
kama ilivyokuwa kwa siku kadhaa nyuma, mganga huyo alimpulizia dawa maalum
usoni na kusababisha alegee kisha kupoteza fahamu.
Alikuja kuzinduka kukiwa tayari kumeanza kupambazuka na kujikuta akiwa
amelala juu ya tawi kubwa la mbuyu. Alipotazama chini, almanusra aanguke kwa
mshtuko kwani alikuwa kwenye umbali mrefu ambao hakujua amepandaje, akawa
anajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
Muda ulizidi kuyoyoma, jua likachomoza kabisa lakini hakukuwana dalili za mtu
yeyote kuja kumshusha, hata alipotazama chini, hakuwa na uwezekano wowote wa
kuteremka, muda ukawa unazidi kuyoyoma huku njaa na kiu vikimtesa baba yake
Samantha.
Hatimaye siku hiyo ilipita akiwa bado juu ya mti, usiku wa pili ukamkuta akiwa
palepale. Kutokana na hofu kubwa ya kuanguka aliyokuwa nayo, usiku kucha
hakulala mpaka majira ya kumi na moja alfajiri ya siku iliyofuata ambapo alijikuta
akizidiwa na usingizi na kujilaza kidogo.

126
Alipokuja kuzinduka kukiwa tayari kumeshapambazuka kabisa, alijikuta akiwa
ndani ya nyumba ya tembe ya mganga Kiswigo, akabaki akijiuliza maswali mengi
yaliyokosa majibu.
“Nadhani kila kitu kinaenda vizuri, bado zoezi la mwisho ambalo siyo gumu kama
haya yaliyopita, mambo yakienda vizuri keshokutwa nitakuruhusu uondoke lakini
narudia kukusisitiza kwamba utakachokutana nacho nyumbani kwako
kisikushangaze, unatakiwa kwenda kuanza upya kabisa, utajiri wa kishirikina
hauna nafasi tena na mali zote ulizozipata kwa njia ya kishirikina zitayeyuka na
kukuacha ukiwa huna kitu,” alisema mganga Kiswigo, baba yake Samantha akawa
anatingisha kichwa kuonesha kukubaliana naye.
Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye baba yake Samantha akamaliza dozi ya nguvu
aliyopewa na mganga Kiswigo. Ndani ya wiki moja tu, mwili wake ulikuwa
umepukutika na kupungua uzito kwa kasi kikubwa. Ukichanganya na nywele
alizonyolewa na mganga huyo, isingekuwa rahisi kwa mtu anayemfahamu
kumtambua haraka.
Ungeweza kudhani ni mtu mwingine kabisa. Baada ya kukamilisha dozi, alipewa
dawa nyingine za kwenda kutumia ili kumaliza kabisa nguvu za utajiri wa
kishirikina aliokuwa nao na badala yake, mganga Kiswigo akamkabidhi kitabu
ambacho alimhakikishia kwamba endapo atafuata yale yote yaliyomo ndani yake,
basi angeweza kupata chochote maishani mwake.
“Kitabu hiki kinataka mtumwenye imani na msafi waroho, ukiwa mchafu wala
maandishi yake huwezi kuyaona. Bila kujali unaabudu dini gani, ni lazima
uendelee kumuabudu Mungu wako nakumtukuza na kufuata yale yote
yaliyoamrishwa kwenye vitabu vyake.
“Unajua watu wengi huwa wanaamini kwamba kitabu hiki ni cha shetani kwa
sababu kinapatikana mikononi mwa sisi watu wenye nguvu za giza lakini ukweli ni
kwamba hiki ni kitabu kitakatifu kama vilivyo vitabu vingine vya dini nyingine.
“Ukianza kusoma utagundua kwamba licha ya kusisitiza kufanya tahajudi
(meditation) za aina zote tatu, kuanzia tahajudi ya pumzi (breath meditation), ya
maneno (mantra meditation) na ya mwanga na sauti (light and sound meditation),
inasisitiza pia mtu kuishi kulingana na misingi ya kibinadamu.
“Upendo ni jambo lililoagizwa na vitabu vya dini zote lakini hata kwenye hiki
kitabu pia tunasisitizwa upendo. Itakuwa haina maana kama utajifanya unampenda
Mungu ambaye humuoni wakati unawatendea mabaya binadamu wenzako.

127
Hakikisha katika kila siku inayopita, angalau unamfurahisha mtu mmoja, hata kwa
jambo ambalo ni dogo.
“Pia ndani ya kitabu hiki, utajifunza namna ya kukabiliana na hisia zako zikiwemo
hofu, hasira, tamaa, wivu na mambo mengine mengi ambayo kimsingi ndiyo
yanayoichafua nafsi ya mtu na kumuweka mbali na Mungu wake.
“Utafuata maelekezo yote hatua kwa hatua na nakuhakikishia ukishaweza
kuutakasa mwili wako ukawa safi kabisa, pia ukatakasa nafsi na akili zako,
unaweza kuomba jambo lolote na hakika litatimia.
“Hata kama utataka tena utajiri, ukifuata kwa umakini mkubwa kilichoandikwa
kwenye hiki kitabu, ambacho kimsingi ndiyo kilichoandikwa kwenye vitabu
vingine vyote vya dini, kila unachokitaka kitatimia kwa haraka sana. Mimi sina
mengi ya kusema, kama una swali lolote unaweza kuniuliza,” alisema mganga
Kiswigo huku akimkabidhi baba yake Samantha kitabu hicho.
Akakipokea na kushusha pumzi ndefu kisha akamuuliza mganga huyo swali.
“Umesema nikishaweza kuutakasa mwili wangu, roho na akili, kila
nitakachokiomba kitatimia! Sasa nataka kujua nawezaje kuutakasa mwili, roho na
akili?”
“Swali zuri na ni rahisi sana. Mwili wako unautakasa kwa kuhakikisha kwanza
unaufanyia usafi wa kutosha kila siku. Hakikisha unaoga kwa maji mengi mara
kwa mara, unafanya mazoezi, unavaa nguo safi, unalala mahali pasafi, unakunywa
maji mengi na mambo mengine ya usafi wa kawaida lakini kubwa, inatakiwa
uhakikishe unakula vyakula ambavyo kiasili binadamu ndivyo anavyopaswa kula.
“Unajua watu wengi wanakosea sana wakiamini kula vyakula vya kukaanga
vyenye mafuta mengi, sukari nyingi, vyakula vya kusindikwa kwenye makopo na
nyama ndiyo ufahari lakini kimsingi binadamu hakuumbwa kula aina hiyo ya
vyakula. Ndiyo maana utashangaa kuona magonjwa ya kutisha hayaishi, mara
kisukari, kansa, presha, kupooza na maradhi mengine ya aina hiyo!
“Binadamu ameumbwa kula mbogamboga, nafaka na matunda. Tena jitahidi kula
vyakula ambavyo havijawekwa mafuta ya viwandani. Mfano mwepesi, mtu
anayekula ugali wa dona na mboga za majani, pembeni akiwa na matunda,
amekula chakula bora kuliko anayekula baga, pizza na nyama za kukaanga.
Ukizingatia hilo, utaufanya mwili wako utakasike na kubwa zaidi, kunywa maji
mengi ya kutosha. Huo ni upande wa mwili.

128
“Upande wa akili, hakikisha kila kinachopita kichwani mwako kipo katika taswira
chanya. Acha kufikiria mambo mabaya kama visasi, wivu, chuki au kuwa na hasira
zinazovuka mipaka.
“Wasamehe wanaokukosea hata kama wamekukosea jambo kubwa kiasi gani,
wasaidie wenye uhitaji, tenda haki kila mara si kwa sababu sheria inasema hivyo
bali kwa sababu tumeagizwa kuishi kwa haki. Usimuonee wala kumkandamiza
mtu yeyote, si mkubwa wala mdogo, si tajiri wala maskini! Wapende watu wote
bila kujali huyu ni nani au atanisaidia nini. Ukifanya hivyo utazitakasa akili zako
na hakikisha unafanya hivyo kila siku.
“Mwisho ni upande wa roho. Hakikisha unajiweka jirani na ulimwengu wa kiroho
muda wote. Amini kwamba kuna nguvu kubwa inayoyaongoza maisha yako na ya
viumbe wengine wote duniani. Fanya tahajudi kila siku, sali, timiza yale yote
yanayoamrishwa katika vitabu vyote vya dini na epukana na anasa za hii dunia
kwa sababu mwili utakapokufa, roho itaendelea kuishi.
“Ishi hapa duniani ukiwa unaelewa kwamba sote ni wapita njia tu na kunamaisha
baada ya kifo, jiandae leo kwa kutenda mema na kuishi kulingana na asili ya
binadamu ili kesho hata zamu yako ya kufa ikifika, usiwe na hofu tena.
“Ukiyatimiza hayo, utakuwa umefikia hatua ya utakaso,” alisema mganga
Kiswigo, baba yake Samantha akawa anatingisha kichwa tu huku akiwa ni kama
haamini kwa sababu alitegemea labda mganga huyo atakuwa anazungumzia habari
za mashetani, majini, misukule na viumbe wa kutisha lakini haikuwa hivyo.
Kwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kukaa nyumbani kwa mganga huyo,
baba yake Samantha alimshukuru sana mganga huyo na kumwambia kwamba
mpaka muda huo, alikuwa anajihisi ni kama amezaliwa upya, akaahidi kwenda
kufanyia kazi mambo yote aliyoelekezwa.
Mganga Kiswigo na wasaidizi wake walimsindikiza baba yake Samantha mpaka
nje ya msituhuo, wakampeleka mpaka sehemu aliyokodishiwa baiskeli kwa ajili ya
kumsogeza mpaka sehemu anayoweza kupata usafiri wa magari madogo au ya
mizigo yatakayomfikisha mjini ili aendelee na safari yake. Walimfungashia zawadi
mbalimbali za kuwapelekea watu wa mjini. Hatimaye safari ye kurejea jijini Dar es
Salaam ikapamba moto.
***

129
Maisha ya Edmund na Samantha jijini Arusha yaliendelea vizuri huku mara kwa
mara wakiwasiliana na mama yake Samantha ambaye naye nafsi yake ilitulia na
taratibu akaanza kuamini kwamba mwanaye yupo kwenye mikono salama kwani
kila alipokuwa akizungumza naye, alikuwa anaonesha kuwa na furaha kubwa.
Edmund naye aliendelea kuhakikisha Samantha anapata huduma zote za kiafya
kama alivyomuahidi mama yake na baada ya wiki mojakuisha, Samantha alikuwa
na ahueni kubwa kwani tayari jerahalake la kupigwa risasi mguuni lilikuwa
likikaribia kupona kabisa.
Ili kuharakisha kuponakwake, Edmund akawa anamfanyisha mazoezi ya kutembea
ambapo safari hii alianza kumudu kutembea mwenyewe ingawa bado alikuwa
akichechemea. Jioni moja akiwa anamfanyisha Samantha mazoezi ya kutembea,
nje ya nyumba waliyokuwa wanaishi, simu ya Edmund ilianza kuita mfululizo,
alipotazama namba ya mpigaji, alishtuka na kumtazama Samantha usoni.
“Vipi?”
“Bosi wetu kazini ananipigia simu, sijui anataka kusema nini? Naogopa hata
kupokea.”
“Pokea tu umsikilize, kwani tatizo liko wapi?”
“Si unajua tangu nilipopatwa nayale matatizo kipindikile sijarudi tena kazini na
wala hawana taarifa kama niko wapi kwa siku zote hizo?”
“Pokea, nakuomba upokee na uzungumze naye,” Samantha alisemakwa sauti ya
upole na kumkumbatia Edmund, ikabidi atii alichowambiwa, akapokea.

“Edmund!”
“Naam mkuu.”
“Uko wapi wewe mbona unatupa wasiwasi? Tumekuja nyumbani kwako
ulikokuwa unaishi karibu mara kumi, haupo wala hakuna taarifa za mahali ulipo,
una tatizo gani?”
“Nina matatizo ya kifamilia.”
“Lakini ulipewa ruhusa kwa sababu ulikuwa unaumwa, kama una matatizo ya
kifamilia kwa nini usitoe taarifa? Karibu mwezi mzima unaisha hujaripoti kazini.
Au kwa sababu unajua unategemewa na kampuni ndiyo maana unaleta dharau?

130
SURA YA KUMI NA NNE

“Sasa sikia, nilichokupigia simu ni kwamba inatakiwa Jumatatu uje kazini,


vyovyote itakavyokuwa lazima uje, kuna kazi maalum umechaguliwa kuifanya, no
excuse! (Hakuna visingizio!)” alisema meneja mkuu wa Kampuni ya Hashcom
Mobile, Erick Salawi kisha akakata simu.
“Edmund alishusha pumzi ndefu na kumgeukia Samantha ambaye muda wote
alikuwa ametulia akimsikiliza Edmund alivyokuwa anazungumza na simu.
“Vipi anasemaje?” alihoji Samantha huku akionesha kuwa na shauku kubwa ya
kutaka kusikia atakachoambiwa, ikabidi Edmund amueleze kila kitu.
“Umeamuaje?”
“Siwezi kuondoka na kukuacha Samantha, nipo tayari kupoteza kila kitu lakini
siyo wewe,” alisema Edmund, Samantha akamvutia kifuani kwake na
kumkumbatia, mazungumzo mazito yakaanza. Huku akizungumza kwa sauti ya
upole, iliyojaa ujumbe mzito, Samantha alimtaka Edmund asafiri mpaka Dar es
Salaam kwenda kusikiliza alichoitiwa na kwamba asiwe na wasiwasi kuhusu yeye.
“Napenda kukuona ukifanya kazi mume wangu mtarajiwa, nataka tuishi kwa
kujitegemea, naamini tunaweza. Wewe ukifanya kazi na mimi nikifanya kazi,
tukiunganisha mshahara wetu tunaweza kufanya mambo makubwa sana, tafadhali
nakuomba usiniangushe,” alisema Samantha, Edmund akawa anatingisha kichwa
kama ishara ya kukubaliana na kilichokuwa kinasemwa na Samantha.
Siku hiyo ilipita, kesho yake Edmund akaanza kujiandaa kwa ajili ya safari ya
kuelekea Dar es Salaam. Alihakikisha anamuacha Samantha katika mazingira
mazuri, akamuandalia kila kitu ili asihangaike atakapoondoka.
Hatimaye muda wa kuondoka uliwadia, akakumbatiana na Samantha kwa muda
mrefu huku wakimwagiana mvua ya mabusu, wakaagana huku msichana huyo
mrembo akimtakia kila la heri.
***
Baada ya safari ndefu na yakuchosha ya basi, kutoka Sumbawanga, hatimaye baba
yake Samantha aliwasili jijini Dar es Salaam majira ya saa tano za usiku.
Alimshukuru Mungu kuwasili usiku kwani kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu
anayefahamiana naye ambaye angemuona, asingeacha kumshangaa.

131
Aliposhuka Stendi ya Mabasi ya Ubungo, alikodi teksi iliyompeleka moja kwa
moja mpaka nyumbani kwake. Kwa muda wote huo hakuwa amewasiliana na
mkewe wala hakumpa taarifa zozote juu ya ujio wake.
Mlinzi wa nyumba ya kifahari waliyokuwa wanaishi, alishtuka baada ya kusikia
kengele ya geti ikigongwa, jambo ambalo halikuwa kawaida. Harakaharaka
akasogea getini na kutazama kupitia kioo maalum kilichokuwepo eneo hilo,
akashtuka kumuona bosi wake huku akionesha kubadilika sana.
Harakaharaka alifungua mlango na kumkaribisha kwa heshima, akaingia na
kupitiliza moja kwa moja mpaka ndani ambako aligonga mlango na kufunguliwa
na mkewe muda mfupi baadaye.
“Mume wangu, ni wewe? Ooh! Ahsante Mungu, siamini macho yangu,” alisema
mama Samantha na kumkumbatia mumewe kwa nguvu huku machozi yakimtoka
kwa wingi.
“Mbona umekonda hivi? Unaumwa?” alimuuliza wakati akimkaribisha ndani, baba
yake Samantha akawa anatingisha kichwa kuonesha kwamba hakuwa akiumwa,
akamwambia mkewe atamuelezea kila kitu. Walipoingia ndani, jambo la kwanza
lilikuwa ni kwenda kuoga kwani udongo mwekundu ulikuwa umemchafua na
kumfanya abadilike kabisa.
Baada ya kuoga kwa zaidi ya dakika ishirini, akitumia sabuni nyingi, alitoka bafuni
na kuelekea chumbani. Muda mfupi baadaye akatoka na nguo alizotoka nazo
safarini na kwenda kuzichoma moto, akarudi ndani ambako alikuta tayari mkewe
ameshamuandalia chakula.
Wakakaa mezani ambapo alianza kukifakamia chakula kwa fujo kutokana na njaa
kali iliyokuwa inamsumbua. Alipomaliza kula walielekea chumbani ambapo mama
yake Samantha alianza kumuelezea kila kitu kilichotokea katika kipindi chote
ambacho hakuwepo.
Alimueleza kuanzia jinsi Samantha alivyotoroka hospitalini akiwa na Edmund,
jinsi mali zao nyingi zilivyoshikiliwa na serikali kwa madai ya kutolipiwa kodi
stahiki kwa muda mrefu na jinsi nyumba hiyo waliyokuwa wanaishi ilivyokuja
kupigwa ‘X’ kwa madai kwamba ilikuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya
barabara.
“Na nyumba nayo imewekwa ‘X’?”

132
“Ndiyo na nasikia tayari watu wengine wameshaanza kubomolewa mtaa wa pili,
inabidi tufanye mpango wa kuhamia kwenye nyumba yetu ya Bunju haraka
iwezekanavyo.”
“Lakini ile bado haijaisha!”
“Sasa unafikiri tutafanya nini mume wangu? Au unasubiri nyumba ije ivunjwe
tukiwa humuhumu ndani?” alisema mama yake Samantha kwa sauti ya upole,
akaendelea kumuelewesha mumewe mambo mbalimbali.
“Utakachokutana nacho nyumbani kwako kisikushangaze, unatakiwa kwenda
kuanza upya kabisa, utajiri wa kishirikina hauna nafasi tena na mali zote
ulizozipata kwa njia ya kishirikina zitayeyuka na kukuacha ukiwa huna kitu,” kauli
ya mganga Kiswigo ilijirudia kichwani mwake mithili ya mkanda wa video.
Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubaliana na kila kitu, wakalala mpaka asubuhi
ya siku iliyofuata ambapo maandalizi ya kuhamia Bunju yalianza. Hata suala la
kuhamisha vitu lilikuwa gumu kwa sababu akaunti zote za benki zilizokuwa na
mamilioni ya fedha zilikuwa zinashikiliwa na serikali.
Ilibidi abangaize kwenye miradi yake mingine ambayo nayo ilikuwa ikisuasua,
fedha zikapatikana na kazi ya kuhamisha vitu ikaanza huku pia mafundi wakilipwa
kwa ajili ya kukamilisha vitu vidogovidogo ambavyo bado havikuwa vimekamilika
kwenye nyumba mpya, ikiwemo madirisha na milango.
Mpaka jioni ya siku hiyo, vitu vyote muhimu vilikuwa vimeshahamishwa. Wazo
alilolitoa mama Samantha lilisaidia sana kwa sababu usiku wa siku hiyo, tingatinga
la serikali liliwasili kwenye mtaa huo na kuanza kubomoa nyumba zote zilizokuwa
zimewekewa alama ya ‘X’.
Mpaka kunapambazuka, eneo kulipokuwa na nyumba ya kisasa ya akina
Samantha, lilikuwa jeupe kabisa. Hakukuwa na nyumba wala bustani nzuri za
maua tena. Kila kitu kilikuwa kikibadilika kwa kasi kubwa kwenye maisha ya
familia hiyo, wakayaanza maisha mapya ya hadhi ya chini, Bunju, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam.
***
Basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha, liliendelea kuchanja mbuga kwa
kasi kubwa na baada ya kusafiri kwa saa nyingi, hatimaye liliwasili Ubungo
ambapo abiria walianza kuteremka, Edmund akiwa miongoni mwao.

133
Akashuka akiwa na kibegi chake kidogo mgongoni na kutoka mpaka nje ya stendi
ambapo alikodi Bajaj iliyompeleka mpaka Sinza. Hakutaka kwenda kulala kwenye
nyumba waliyokuwa wanaishi na Samantha kabla ya kutokewa na matatizo,
akaenda kupanga chumba kwenye nyumba ya kulala wageni iliyokuwa karibu na
kazini kwao ili asubuhi iwe rahisi kuwahi kazini.
Moyoni alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua aliitiwa nini kazini kwani
ilionekana kuna jambo la muhimu sana.
Kesho yake asubuhi, Edmund aliwahi kuamka na kujiandaa, akatoka na kuelekea
kazini ambapo siku hiyo alikuwa miongoni mwa watu wa kwanzakwanza kusaini
na kuingia ofisini.
Kila mfanyakazi mwenzake aliyekuwa akikutana naye alikuwa akimshangaa kwani
kilipita kipindikirefu bila kuonekana kazini. Kingine kilichofanya watu wazidi
kumshangaa, ni kwamba licha ya kuelewa kwamba ametoka kwenye matatizo,
Edmund alikuwa amebadilika sana kimwonekano.
Alikuwa amenawiri, rangi ya ngozi yake ambayo awali ilikuwa imefifia ikawa
inapendeza kuonesha kwamba sasa alikuwa akiishi maisha mazuri. Hata mavazi
yake nayo yalibadilika kwani alipendeza sana kiasi cha kuwafanya mpaka marafiki
zake waanze kumuonea wivu.
Hatimaye meneja mkuu aliwasili ambapo alimkuta Edmund akiendelea kufurahi na
wafanyakazi wenzake, akamchukua mpaka ofisini kwake ambapo alianza
kuzungumza naye. Alimuonya kuhusu tabia yake ya kukaa nyumbani bila kutoa
taarifa yoyote ofisini na kumtaka asirudie tena tabia hiyo.
Edmund alikiri makosa yake na kuomba asamehewe, meneja huyo akamwambia
akaendelee na kazi wakati wakimsubiri mkurugenzi mkuu ambaye kimsingi ndiye
aliyeagiza aitwe haraka iwezekanavyo.
Saa tatu asubuhi juu ya alama, Edmund aliitwa kwenye ofisi ya mkurugenzi wa
kampuni hiyo, alipoingia akashtuka kugundua kuwa karibu viongozi wote
wakubwa wa kampuni walikuwepo, kuanzia mkurugenzi, meneja mkuu, mhasibu
mkuu na maafisa wengine kadhaa.
Meneja ndiye aliyevunja ukimya na kumueleza Edmund kwamba mkurugenzi
alikuwa akihitaji kuzungumza naye, akakaribishwa ambapo alianza kumpa pole
kwa matatizo yaliyomtokea lakini akamsisitiza tena kuacha tabia ya kukaa tu
nyumbani bila kutoa taarifa.

134
“Kikubwa nilichokuitia, kwa kipindikirefu tangu ulipoajiriwa, nimekuwa
nikifuatilia kwa ukaribu mwenendo wako wa kazi na kimsingi nimeridhishwa na
juhudi na maarifa ambayo unayaonesha ili kuhakikisha kampuni inasonga mbele.
“Tumefikiria kufungua tawi letu jingine jijini Arusha na mambo yote ya kimsingi
yameshakamilika. Kampuni imekuteua wewe kwenda kuwa meneja mkuu wa tawi
la Arusha ambapo utakuwa ukiripoti moja kwa moja kwangu.
“Maslahi yako yameboreshwa sana ikiwemo kuongezwa mshahara, kutafutiwa
nyumba ya kuishi na gari la kukuwezesha kufanya kazi zako vizuri. Meneja mkuu
atakupa maelekezo zaidi ya namna ya kupata vitu vyote nilivyovitaja na jinsi
utakavyoenda kuanza kazi.
“Kabla sijahitimisha, unachochote cha kuzungumza?” alihoji mkurugenzi na
kumfanya Edmund ashindwe kuzizuia hisia zake, machozi ya furaha yakawa
yanamtoka ambapo aliushukuru uongozi kwa kumuamini na kuahidi kwamba
atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha tawi jipya la Arusha linachanua kwa kasi.
Baada ya hapo, mkurugenzi alifunga kikao hicho na kumpa mkono wa pongezi
Edmund, akifuatiwa na viongozi wengine ambapo walipotoka, walielekea kwenye
ofisi ya meneja mkuu ambaye alianza kumpa maelezo ya nini anachotakiwa
kufanya akifika Arusha.
Akamkabidhi barua mpya ya kupandishwa cheo na kuongezwa mshahara,
akaambiwa akajiandae mpaka asubuhi ya siku inayofuata ambapo angesafiri na
meneja huyo mpaka jijini Arusha kwa ajili ya kwenda kumkabidhi ofisi rasmi.
Hakuna siku ambayo Edmund alikuwa na furaha kama siku hiyo, akawa
anamshukuru Mungu wake kwa miujiza aliyomtendea.
Kesho yake asubuhi, Edmund na meneja mkuu walisafiri mpaka jijini Arusha
ambapo Edmund alienda kukabidhiwa rasmi ofisi mpya za Hashcom Mobile,
akatambulishwa kwa wafanyakazi kuwa ndiyo meneja mkuu wa ofisi hizo. Kiumri,
Edmund alikuwa bado mdogo ukilinganisha na madaraka aliyokabidhiwa lakini
mwenyewe hakuogopa chochote kwa sababu alikuwa akiuamini utendaji kazi
wake. Ofisi zilikuwa mkabala na Stendi Kuu ya Mabasi ya Arusha wakati nyumba
ya kuishi, ikiwa na kila kitu ndani ilikuwa maeneo ya Njiro, jirani na pale
alipokuwa anaishi kwa siri na Samantha. Alikabidhiwa pia gari la kutembelea,
Toyota Harrier pamoja na dereva ambaye angekuwa akilipwa na kampuni.
Baada ya meneja mkuu kumkabidhi kila kitu, alipanda ndege kurejea jijiniDar es
Salaam ambapo Edmund naye alielekea kwenye makazi yake ya awali,

135
alikomuacha mpenzi wake, Samantha. Alipofika alipokelewa kwa shangwe kubwa
na Samantha ambaye alimtaka amueleze kilichotokea katika safari yake hiyo.
Samantha alipoelezwa, naye alishindwa kuficha hisia zake, akamwaga machozi
mengi ya furaha na kumshukuru Mungu kwa kilichotokea.Siku tatu baadaye, tayari
walishahamia kwenye nyumba ya kampuni na Edmund akaanza kazi rasmi huku
Samantha akiwa ndiyo mshauri wake mkubwa.
***
Maisha mapya ya wazazi wa Samantha, yalimbadilisha kabisa baba yake. Muda
mwingi akawa ni mtu wa kukaa na kujutia mambo yote mabaya aliyowahi
kuyafanya. Hakukuwa na chochote tena baada ya serikali kutaifisha mali zake
karibu zote huku nyingine zikiteketea kwa moto au kuharibika katika mazingira ya
kutatanisha.
Hata hivyo, kama alivyokuwa ameshauriwa na mganga Kiswigo, aliendelea
kufuata maelekezo yote aliyopewa. Taratibu akaanza kubadilika na kurudi kuwa
mtu mwema, kama alivyokuwa mwanzokabla ya kukumbwa na tamaa ya utajiri
haramu.
“Mke wangu!”
“Naam mume wangu.”
“Nimekaa na kufikiria sana kuhusu suala la Samantha na Edmund, nafikiri hakuna
sababu ya kuendelea kuwazuia kuishi pamoja lakini cha msingi lazima wafuate
sheria zote muhimu ili wafunge ndoa na kuishi kihalali, au wewe unasemaje mke
wangu?” alisema baba yake Samantha, kauli ambayo ilimfanya mkewe apigwe na
butwaa, akiwa haamini alichokisikia, akawa anamshukuru Mungu kwa miujiza
yake.
Bila kupoteza muda, mama yake Samantha aliwasiliana na Samantha na Edmund
na mipango ya kuchumbiana ikaanza kufanywa. Wiki mbili baadaye, wawili hao
waliwasili jijini Dar es Salaam ambapo taratibu za kuvalishana pete ya uchumba
zilifanyika. Baadaye wakaoana kwa ndoa ya kawaida, wakala kiapo cha kuwa
mume na mke na huo ukawa mwanzo wa kufungua ukurasa mpya wa maisha yao.
Kwa kuwa Edmund alikuwa akilipwa mshahara mkubwa, alimsaidia baba mkwe
wake mtajiwa kuanzisha upya biashara, jambo ambalo mzee huyo hakuwahi kuhisi
linaweza kutokea hata mara moja!

136
Yaani Edmund yule aliyekuwa anamdharau na kumkosakosa kumuua mara
kadhaa, leo ndiyo anampa mtaji wa kuanza upya biashara baada ya kufilisika!
Ilikuwa ni zaidi ya maajabu kwa mzee huyo. Maisha yalizidi kusonga mbele,
taratibu biashara za baba yake Samantha zikaanza kuchangamka, ukiongeza na
uzoefu aliokuwa nao, kazi haikuwa ngumu.
Akaikarabati vizuri nyumba yake mpya na kurudisha vitu vingi alivyovizoea
kablahajafilisika. Safari hii alikuwa amebadilika mno, hakuwa kama mwanzo,
alikuwa na heshima kwa kila mtu, aliwajali maskini na wenye shida na kila siku
ilikuwa ni lazima amuombe Mungu wake na kutubu dhambi zake zote alizowahi
kuzifanya.
Vijana wengi ambao waliwahi kuchukuliwa misukule enzi za utajiri wake, nao
waliendelea kuombewa na kupatiwa tiba za uhakika na wakaanza kurudi kwenye
hali zao za kawaida kama walivyokuwa mwanzo.
Miezi michache baadaye, Samantha alipata ujauzito, akiwa mke halali wa Edmund
ambapo miezi tisa baadaye, alijifungua watoto mapacha, wa kike na wa kiume
aliowapa majina ya Emanuel na Emanuela, yakimaanisha Mungu yupo pamoja
nasi. Maisha yakaendelea kwa raha mustarehe, huku ufanisi wa Edmund kazini nao
ukizidi kuongezeka kila kukicha.

MWISHO

137

You might also like