Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 77

HUWEZI

KUUA
MAITI

ERIC J. SHIGONGO

Page 1 of 77
SURA YA KWANZA

INGAWA ilikuwa mchana hali katika msitu wa Kungoni nchini Kongo ilikuwa
ya kiza nene! Mawingu yalitanda angani. Ni asubuhi ya siku hiyo tu ilinyesha
mvua kubwa tena ya mawe na kusababisha baridi kubwa! Wanyama wengi
walijikunyata sababu ya kulowa.
Milio ya ndege na wanyama mbalimbali ilisikika kila pembe ya msitu huo
uliokuwa kilometa kama 520 kutoka Jiji la Kinshansa, ulikuwa ni msitu wenye
tembo wengi kuliko msitu mingine yote barani Afrika na uliwavutia watalii wengi
lakini waliogopa kuutembelea sababu tembo wa msitu huo waliua watalii.

Kila mtu aliamini hakuna mtu aliyeishi katika msitu huo jambo ambalo halikuwa
sahihi hata kidogo, kwani mtu mmoja tena bibi kizee mwenye umri wa miaka 80
aliishi katika msitu huo kwa miaka mingi.
Alikuwa ameishi katika msitu huo kwa muda wa miaka isiyopungua thelathini
akifanya utafiti wa maisha ya tembo na wanyama wengine kama ndege, Nzige na
Mbungo! Alipofika Kongo kwa mara ya kwanza alikuwa na umri wa miaka 30,
aliingia nchini humo akitokea Tanzania.

Kinshansa chini ya Patrice Lumumba ilimpokea mwanamke huyo kama mtafiti wa


wanyama bila kudadisi sana kilichomfanya aondoke Tanzania na kumpa kibali cha
kwenda kuishi msituni Kungoni.
Ni bibi huyo pekee aliyeishi katika msitu huo akizungukwa na wanyama wengi
wao wakiwa ni tembo! Aliishi na wanyama hao kwa miaka thelathini mpaka
wanyama wote wakamwona ni kama mnyama mwenzao, aliijua lugha za tembo,
nzige, mbung’o na ndege mbalimbali! na kuwasiliana nao kama binadamu.

Kulipokuwa na hatari aliitambua kwa kuwasikiliza tembo, nzige, mbung’o na


ndege! Alipohitaji kitu chochote porini alitoa mlio fulani mdomoni mwake na
Tembo wote walikuja na aliwaagiza kufanya kitu chochote alichotaka! Kifupi
wanyama wote walimwona kama malkia wao!
Kila sehemu aliyokwenda alizungukwa na tembo wakimlinda, ilikuwa si rahisi
kwa wanyama wengine wa porini kama simba, chui, kumdhuru sababu ya ulinzi
aliopewa na tembo alioishi nao kwa miaka mingi na aliwafahamu tembo kwa

Page 2 of 77
majina. Kila mtu aliyesikia habari za bibi huyo alishangaa na Wazungu wengi
walikwenda msituni ili kumwona lakini hawakurudi salama, wengi walikufa kabla
ya kumfikia.

****
Bibi huyu aliitwa Nyanjige Ndaki, hakuwa Mkongo bali Mtanzania tena kutoka
Mkoani Mwanza, alikuwa msomi wa chuo kiku cha Edniburgh, nchini Uingereza
alikopelekwa na gavana kama zawadi kwa mama yake aliyekuwa mpishi wa
Gavanna huyo kwa kipindi kirefu!
Gavana alipotaka kuondoka chini alimchukua bibi Nyanjige wakati huo akiwa na
umri wa miaka mitano tu ili akamsomeshe nchini Uingereza. Aliishi Uingereza
kwa miaka karibu ishirini na tano bila kurudi Tanzania na aliporejea nchini mwaka
1967 alikuwa tayari ana digrii mbili za elimu ya viumbe badala ya kufanya kazi
aliushangaza ulimwengu alipofanya mauaji ya watu 150 kwa mpigo na hakuna
aliyeelewa sababu ya mauaji hayo!
Tangu siku ya kwanza aliyoingia Kongo na kupewa kibali cha kuishi porini
Kungoni hakurudi tena mjini kwa kuogopa kukamatwa, siku zote aliishi na
wanyama porini, akila matunda kama wanyama, wakati mwingine aliua swala na
kula nyama! Hayo ndiyo yakawa maisha yake siku zote, hakutaka kabisa kukutana
na binadamu yeyote.
Patrice Lumumba alipokufa serikali ya Kongo chini ya Mabutu Seseko ilimsahau
kabisa bibi huyo, hakuna mtu aliyetaka kujua habari zake. Serikali ya Tanzania
nayo baada ya kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio iliamua kuachana na
swala hilo ikiamini bibi Nyanjige alikufa! Ingawa msako wa chini chini uliendelea
kwa usaidizi wa nchi nyingine kama Marekani, Ufaransa, Ujerumani ambazo pia
Raia wake walikufa katika tukio la mauaji hayo.
Ilikuwa si rahisi kumwona bibi Nyanjige kwa ulinzi mkali uliokuwepo nyumbani
kwake porini, nyumba yake ilizungukwa na Tembo wasiopungua kumi,
waliomlinda usiku na mchana! Wazungu wengi waliojaribu kumfikia ili kupata
picha yake waliuawa kwa kunyangwa na Tembo!
Mzungu mmoja aliyekwenda porini kwa helkopta alifanikiwa kuipata picha ya bibi
Nyanjige akiwa katikati ya tembo!

Page 3 of 77
Ni picha hiyo iliyoleta matatizo kwani ilipochapishwa katika magazeti na majarida
mbalimbali nchini Uingereza na Marekani serikali ya Tanzania ilishtuka na
kuamini kuwa mtu aliyekuwa akitafutwa alikuwa porini nchini Kongo.
Bila kuchelewa ilituma wanajeshi wapatao ishirini waliopewa msaada na askari
wengine kumi wa Kongo! Walifika hadi msituni lakini hawakufanikiwa
kumkamata bibi Nyanjige na pia hawakufanikiwa kurudi salama nyumbani! Wote
walikufa kifo hichohicho cha kukanyagwa na Tembo!
Mpaka mwezi moja baada ya askari hao kuondoka hapakuwa na mawasiliano
yoyote kutoka msituni, simu zao za upepo ziliendelea kuita bila majibu! Hilo
lilionyesha wazi watu hao hawakuwa hai!
Ilibidi serikali za Tanzania na Kongo kwa kushirikiana ziandae jeshi kubwa lenye
askari wasiopungua elfu tano waondoke kwenda msituni kumsaka bibi Nyanjige!
Maaskari wote 5000 walilizunguka pori wakiwa na silaha kali mikononi mwao na
ndege za kivita zilipita angani!
Askari ndani ya ndege hizo walipoangalia chini ka kutumia viona mbali waliziona
maiti za askari wenzao zikiwa ardhini na tembo wengi wakiwa wamezunguka
kibanda kidogo kilichoonekana kuwa kama nyumba.
Ghafla mamia kwa maelfu ya ndege walionekana angani, hawakujulikana
walikotokea! Wengi walitua kwenye vioo vya mbele vya ndege hizo na kuwafanya
marubani washindwe kuendesha ndege zao vizuri kwa sababu hawakuona mbele.
“Tufanya nini sasa?”
“Turudi tukatue kwanza, vinginevyo hawa ndege watasababisha tuangushe ndege
ni wengi mno na sielewi wametoka wapi!”
“Sawa geuza basi!”
Wakati wanageuza ndege nyingine ilishafika karibu yao ikipita katikati ya
makundi ya ndege, zote mbili ziligongana na kuwaka moto zikiwa angani! Askari
waliokuwa wakitembea kwa miguu walishangaa kuona ndege zikigongana.
“Tusongeni mbele! Mpaka tumtie nguvuni huyu bibi, kazi hii tumepewa na serikali
zetu ni lazima tumkamate na kumfikisha Tanzania akiwa hai, ajali hii imeniongeza
hasira zetu unanipata lakini, ovaaa!”

Page 4 of 77
“Ndiyo ninakupata mkuu! Hata sisi tumeishuhudia ajali hiyo na tunazidi kusonga
mbele ila kuna kitu cha ajabu kidogo kimetokea hapa!”
“Kitu gani?”
“Kundi kubwa sana la mbung’o na nzige wamejitokeza na wanatuuma sana!
Maaskari wengi wameshindwa kabisa kuendelea wa safari na wameanguka chini!
Hivi ninavyoongea wanashambuliwa na mbung’o hata mimi mwenyewe mwili
wangu wote umezingirwa na mbung’o pamoja na nzige wanakula magwanda
yangu!” “Kweli?” Aliuliza Meja Jenerali Job Lupilya aliyekuwa mkuu wa
operesheni hiyo, hakupata jibu kutoka upande wa pili!
Alizidi kuita kwa muda mrefu bila kutikiwa, hali ilimtisha na kumwamuru mmoja
wa wapiganaji wake awashe kifaru cha vita na wakaondoka kuelekea upande wa
pili kulikokuwa na kikosi alichowasiliana nacho!
Iliwachukua kitu kama dakika ishirini kufika eneo hilo, hawakuamini
walichokiona walipofika, miili ya zaidi ya maaskari mia moja ililala chini ikiwa
imeliwa nyama zote na Nzige pamoja na Mbung’o! Ilikuwa ni mifupa tupu
iliyolala chini ambayo wazungu huiita Skeleton! Nzige na Mbung’o wengi wasio
na idadi walitapakaa kila mahali wakiendelea kula miili ya maaskari waliokufa.
“Hivi hawa ni Nzige gani yaani wamewaua askari wetu wote?” Aliuliza
mwanajeshi mmoja na kabla hajafanya lolote walishangaa kuona kundi kubwa la
Nzige kama wingu au kundi la nyuki wakihama kutoka sehemu moja hadi nyingine
likiwafuata!
“Ina maana wanatufuata sisi?”
“Inavyoonekana!”
“Hebu ngoja!” Alisema mkuu wa kikosi na kutoa baruti na akawalipulia, nzige
wengi walikufa lakini dakika moja tu baadaye kundi jingine la Nzige na Mbung’o
lilitokea upande wa pili na kuanza kuwashambulia! Yalikuwa ni maumivu makali
mno, magwanda yao ya jeshi yalitafunwa na kujikuta wakiwa uchi katika muda wa
sekunde chache ndipo minofu yao ilipoanza kuliwa kwa kasi ya ajabu.
Ghafla Meja Jenerali Lupilya akiwa amekata tamaa kabisa alisikika kitu kama
mluzi ukipigwa pembeni yake

Page 5 of 77
“Pswiiiiiiiiiiii!” Kufuatia mluzi huo Nzige wote wakasimamishwa zoezi lao la kula
minofu yake! Mluzi mwingine tena ulifuata lakini katika mtindo tofauti kidogo!
Kufuatia mluzi huo Nzige wote waliruka na kuondoka zao.
Meja jenerali Lupilya alipogeuza uso wake na kuangalia pembeni alikiona kibibi
kizee kikitembea taratibu kuelekea mahali alipolala, Tembo wengi walikizunguka
na mmoja wao alipomfikia alizungushia mkonga wake shingoni mwa Meja
jenerali, alimnyanya na kuanza kumzungusha hewani, Lupilya alipiga kelele na
kulia.
“Wiiiiii!” Bibi alitoa mlio mdomoni kwake na Tembo akamweka chini Lupilya,
alikuwa akitoka jasho mwili mzima na mkojo ulimpenya! Tembo wote walikaa
chini na kulaza vichwa vyao ardhini kama ishara ya kuonyesha heshima kubwa
kwa bibi Nyanjige.
“I’m the queen of the forest who are you?”(Mimi ni malkia wa msitu wewe ni
nani?)
“I’m ...ma...jor gene...ral Lupi...lya fro..m Tan..zania!”(Mimi ni Me...ja jene....rali
Lupil....ya natoka Ta....nzania)
“Tanzania? From what tribe are you?”(Tanzania? Wewe ni kabila gani?)
“Su…ku..ma!” Alijibu Lupilya huku akilia na kutetemeka! Hakuamini kulikuwa na
binadamu aliyekuwa na uamuzi mkubwa kiasi hicho mbele ya wanyama wa
mwituni!
“Ule Nsukuma getegete?”(Wewe ni Msukuma kabisa?) Bibi Nyanjige alimuuliza
meja kwa kabila ya Kisukuma, Lupilya alibaki mdomo wazi akishangaa.
“Ngh’ana gete mama! Nu bebe gashi uli wa Kukaya?”(Kweli kabisa bibi kumbe na
wewe ni mtu na nyumbani!) Alijibu Lupilya huku akiendelea kulia machozi, mwili
wake wote ulimuuma sababu ya kuliwa na Nzige, alipomwangalia mwenzake
alikuwa kimya nyama zote hazikuwepo mwilini! Alibaki mifupa.
“Mnataka nini hasa nyinyi?” Bibi aliuliza kwa kiswahili.
“Nduhu mhayo mama! Nilekejage natalashogeja kabili!(Hakuna neno bibi
nisamehe sitarudia tena) Meja Lupilya aliendelea kuongea kwa Kisukuma.
“Ongea kiswahili mpumbavu wewe! Unafikiri Kisukuma kitakusaidia hapa?”
“Nisamehe bibi na mimi nilitumwa tu!” Lupilya alibadilisha lugha.

Page 6 of 77
“Sasa wewe nakuachia nenda kawaeleze ndugu zako kuwa hapa ni moto wa kuotea
mbali! Mimi ndiye malkia wa msitu huu! Jeshi langu si mchezo nitawamaliza!
Ondokaaaa upesi!” Aliongea kwa ukali bibi Nyanjige na Lupilya ulinyanyuka na
kukimbia kuelekea porini akiwa uchi wa mnyama kila alikopita alikuta miili ya
watu ikiwa imelala chini bila nyama! Na Nzige walikuwa kila mahali lakini
hawakumgusa amri aliyoitoa bibi ilionekana kusambazwa kila mahali.
“Mh! Huyu bibi si mchezo ni heri upambane na dunia nzima lakini si yeye!”
Alisema meja Lupilya. Baada ya kutembea kwa nusu saa hivi aliikuta helkopta
imeegeshwa watu wengi walikuwa pembeni yake wakiwa mifupa mitupu,
aliwaruka na kuingia ndani ya helkopta, mifupa mingine ya watu wawili
ilikuwemo ndani ya helkopta hiyo.
“Hii acha niondoke nayo ili wakaelewe vizuri nitakachokuwa nawaeleza, maana
ninajua itakuwa si rahisi kuamini yaliyotokea! Huyu bibi si mchezo jamani!”
Alisema meja jenerali Lupilya akiwasha ndege ili aondoke.

Page 7 of 77
SURA YA PILI

KWA muda wa miezi kama mitatu ya mwisho kabla Nyanjige hajaondoka


Uingereza alikoishi kwa miaka 30 kurudi nyumbani Tanzania, alipoteza kabisa
mawasiliano na mama yake na alishindwa kuelewa ni kitu gani kilimpata mpaka
akawa kimya kiasi hicho kwani kwa kawaida alipokea barua moja kila mwezi
kutoka kwa mama yake lakini kwa miezi mitatu mfululizo yote hakupata taarifa
yoyote juu ya hali ya mama yake.
Ni jambo hilo ndilo lilifanya Nyanjige aamue kuondoka Uingereza mapema kabla
ya muda aliopanga, lilimtia wasiwasi mwingi sana moyoni mwake na kumpa
kumbukumbu nyingi sana juu ya mama yake na alitaka kuwa naye wakati huo.
Katika miaka yote 30 ambayo Nyanjige aliishi nchini Uingereza akisoma na
hatimaye kufanya kazi ni mara mbili tu aliwahi kuonana na mama yake na mara ya
mwisho ilikuwa miaka kumi kabla ya kufikiria kurudi Tanzania.
“I have got to go home! Tanzania is my country! Tanzania is my home! My people
are in Tanzania not here in the UK! I have to go and serve my own people rather
than serving Britains (Ni lazima nirudi nyumbani, Tanzania ndiyo taifa langu,
Tanzania ndiyo nyumbani kwetu, Tanzania ndiyo asili yangu, watu wangu wako
huko ni lazima niende kuwatumikia wao kuliko kuendelea kuwatumikia
Waingereza) Alisema Nyanjige akiwa mwenye mawazo mengi.
Alikuwa mwanamke mzuri sana lakini katika miaka yote aliyoishi Uingereza
hakujaliwa kupata mtoto wala mchumba wa kumuoa! Si kwamba sura yake
ilikuwa mbaya mno la hasha! Bali hakuwa na bahati ya kuolewa na hiyo ilitokana
na shughuli nyingi alizokuwa nazo! Nyanjige alitamani sana kuwa na mtoto lakini
haikuwa hivyo.
Kabla ya kuondoka nchini Uingereza alimnunulia mama yake zawadi nyingi za
nguo za Kiingereza, alitaka mama yake apendeze na kuwa tishio mtaani kwao na
ikiwezekana hata mkoa mzima wa Mwanza na vitongoji vyake wamfahamu!
Siku ya kuondoka London ndiyo ilikuwa siku ya furaha zaidi katika maisha yake,
alipanda ndege ya shirika la ndege la Alliance Airlines iliyoondoka London kuja
Dar es Salaam kupitia Paris, Uturuki, Misri, Ethiopia, Nairobi na hatimaye kuingia
Dar es Salaam. Safari hiyo ilimchukua masaa zaidi ya ishirini na nne, wakati
anaingia Dar es Salaam saa nne ya asubuhi alikuwa amechoka kupita kiasi lakini
Page 8 of 77
hakutaka kulala Dar es salaam kabisa na kuamua kuunganisha siku hiyo hiyo
kuelekea Mwanza ambako aliwasili saa 10 jioni.
Alikuwa na hamu kubwa ya kuonana na mama yake hivyo alikodisha teksi kutoka
uwanja wa ndege ambao upo kama kilometa nane kutoka Mwanza mjini hadi
kijijini kwao Usagara kilometa kama sabini kutoka Mwanza mjini, ambako mama
yake aliishi baada ya kustaafu kazi ya upishi nyumbani kwa gavana.
Iliwachukua zaidi ya masaa mawili kufika kijijini Usagara, sababu ya ubovu wa
barabara uliokuwepo mjini Mwanza. Alishangazwa na hali aliyoikuta nyumbani
kwa mama yake, nyumba ya mama ilikuwa imebomoka na kuanguka upande
mmoja, nyasi ziliota hadi mlangoni mwa nyumba hiyo iliyojengwa kwa udongo!
Mlango ulikuwa wazi na ilikuwa rahisi sana kufikiri watu walioishi katika nyumba
hiyo walihama miezi michache kabla.
Hali hiyo iliufanya moyo wa Nyanjige upige kwa nguvu na kasi ya ajabu alihisi
kuna tatizo lilitokea ambalo hakuwa na habari nalo! Hakutaka kuteremsha mizigo
yake ndani ya gari na kuamua kuusukuma mlango na kuingia hadi ndani ya
nyumba ya mama yake ambako alianza kuita jina la mama yake lakini hakuitikiwa
hatimaye aliamua kusukuma mlango wa chumbani na kukuta umefungwa kwa
komeo kutoka ndani, alijua kwa hakika ndani kulikuwa na mtu!
“Mama! Mama! Mama!”Aliendelea kuita lakini hali ndani ya nyumba ilikuwa
kimya! Baada ya kuita sana hatimaye ilibidi amwite dereva ajaribu kumsaidia
kuuvunja mlango wa chumbani ili waigie na kuangalia! Alipokuja dereva
walifanikiwa kuuvunja mlango na kuingia hadi ndani! Ingawa giza lilikuwa
halijaingia chumba hicho kilikuwa kiza tupu na ilikuwa si rahisi kuona kitu
chochote kilichokuwemo ndani.
“Dereva una tochi?’
“Tochi dada sina ila nina kiberiti!”
“Basi nisaidie hicho hicho kiberiti nataka kuangalia humu ndani!”
“Kwani kuna nini dada?”
“Mama yangu aliishi hapa lakini dalili zilizopo zinanitisha sijui kahama? Sijui
yupo wapi? Naomba hicho kiberiti nijaribu kuangalia vizuri humu chumbani!”
Dereva aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kiberiti na kumkabidhi Nyanjige,
alipokiwasha tu kwa mwanga mdogo uliokuwepo aliweza kukiona kitanda cha

Page 9 of 77
mama yake na kukisogelea, juu kulitandikwa shuka jeupe lakini hapakuonekana
kuwa na kitu chochote chini ya shuka hilo cha kufanya afikirie mama yake alikuwa
kitandani amelala!
Alikibeza kitanda na kuendelea kukagua sehemu mbalimbali za chumba huku
akiwasha njiti nyingine ya kiberiti kila moja ilipozimika.
Alizunguka chumba kizima bila kuona kitu, akahamia chumba kilichokuwa
kimebomoka upande huko nako pia hakuona kitu chochote! Nyanjige alizidi
kuchanganyikiwa, ghafla wakati akirudi kwenye chumba cha mama yake aliona
kitu kama karatasi chini ya kitanda aliinama na kuiokota, akaikunjua vizuri na
kuanza kuisoma.
“Ng’wanone Nyanjige, nene nalisatu no! Ubusatu wenubu ndibona bukunibulaga!
Bale bizile banhu bunisola bahayaga angu ndi nogi nakabulagaga bana babo! Aho
banisola Bunitwala Kwibanza Lya sungusungu, bunitula mpaga nudeda getegete,
Nushoka kukaya nalagula giti kanegene! I hali yane ya bubi no natumanaga nulu
ukunisanga nali mhola! Aliyu mhayo untale ukonisanga nachile ng’wanone
nalibona atiho nu munho wakunijeka leka nikundikile shuka ulagasanga maguhwa
gani habulili wenubu! Nacha ng’wanone wikate mhola.
Nini.
Noko!
Barua hiyo iliandikwa kwa kisukuma lakini ilimaanisha maneno yafuatayo:
“Mwanangu Nyanjige, mimi naumwa sana na ugonjwa huu naona utaniua!
Walikuja hapa watu wakanichukua hadi kwenye kikao cha sungusungu wakidai eti
mimi ni mchawi, wakanipiga mpaka nikaja hapa nyumbani natambaa kama mtoto!
Hali yangu ni mbaya mno mwanangu sijui kama utanikuta hai ukirudi lakini
kikubwa najua utanikuta nimekufa na ninaona hakuna mtu wa kunizika hivyo
najifunika shuka utaikuta mifupa yangu chini ya shuka hili hapa hapa kitandani,
nakufa mwanangu naomba ubaki salama!
Mimi,
Mamayo!
Nyanjige alimaliza barua hiyo mwili wake ukiwa umekufa ganzi alitembea taratibu
kuelekea kitandani na alipofunua shuka ilikuwa ni mifupa ya mama yake ikiwa
chini ya shuka! Alishindwa kuvumilia akanguka chini na kuzirai! Dereva kuona

Page 10 of 77
hivyo alimbeba na kumtoa hadi nje na kuchukua maji yaliyokuwemo kwenye
galoni ndani ya gari lake na kummwagia usoni na mwilini! Haikuchukua muda
mrefu akazinduka na kuanza kulia machozi. Pamoja na kilio hicho hakuna hata
jirani mmoja aliyejitokeza kuja kumsaidia au kuuliza ni kitu gani kilitokea
Nyanjige na dereva walishangaa.
Baada ya kitu kama masaa mawili hivi bila kuona jirani akitokeza Nyanjige
aliamua kwenda nyumba ya jirani kuulizia lakini alipofika watu wote walikimbilia
ndani na kufunga milango ya nyumba zao na wengine kuongea naye kupitia
dirishani.
“Nyanjige nitwa kwambilija, aliyo ikaya ying’we ituligije konguno na bulogi
(Nyanjige tungekusaidia lakini familia yenu imetengwa na kijiji sababu ya uchawi)
“Hata kama mmenitenga ndiyo mnaweza mkamwacha mtu akafa mpaka kuwa
mifupa? Huu ni unyama ni lazima niwaonyeshe nimechukia kiasi gani!
Isitoshe mama yangu hakuwa mchawi au mlimwita mchawi kwa sababu ya macho
kuwa mekundu? Mmesahau kuwa alikuwa mpishi wa gavana?”
“Kwa kweli sio sisi ni serikali ya kijiji iliyoamua hivyo, hata sisi tumesikitika
mno!” Alisema mama mmoja kupitia dirishani.
Nyanjige akiwa amepandisha hasira kupita kiasi alirudi nyumbani kwao huku
akilia, hakuwa na la kufanya kwani hakufahamu ndugu hata mmoja nchini
Tanzania wazazi wake walitokea Kongo miaka mingi walipofika Mwanza
walichukua majina ya Kisukuma na kujifunza kabila hiyo wakaonekana
Wasukuma wakati walikuwa Wabembe kutoka Zaire.
Ndugu pekee aliyekuwa nae pale alikuwa ni dereva aliyemleta kutoka mjini huyo
ndiye aliyemtegemea kumpa kila aina ya msaada!
“Siki...li...za ka...ka mimi nime..pa..twa na ma..tati..zo nafi..kiri ume..ona, hivi
una...weza kunisaidia vipi?’
“Kwa tatizo gani?”
“Nataka kuzika mifupa ya mama yangu!”
“Hilo tu lisikumbue dada yangu nitakusaidia mimi ni binadamu kama wewe!”
“Nisaidie nitakulipa kiasi chochote cha pesa!”

Page 11 of 77
Dereva alirudi nyuma na kufungua buti la gari na kutoa jembe na koleo ambavyo
alitembea navyo wakati wa mvua kumsaidia kila anapozama katika tope! Baada ya
kuvichukua alivua shati lake na kukunja suruali.
“Ni wapi tuchimbe kaburi dada?”
“Chimba tu hapa hapa mbele!” Alijibu Nyanjige akilia machozi kwa uchungu,
moyo wake uliuma sana na hasira ilimkaba kooni aliamini asilimia mia kuwa
mama yake hakuwa mchawi ila aliponzwa na macho mekundu sababu ya moshi wa
miaka mingi nyumbani kwa gavana.
“Haiwezekani ni lazima nilipe kisasi kwa wananchi wa kijiji hiki hawawezi
kumuua mama yangu mpendwa kinyama namna hii wanastahili adhabu tena
adhabu ya kuchukua maisha yao!” Aliwaza Nyanjige huku akiendelea kulia
machozi na dereva akiendelea kuchimba kaburi.
Masaa mawili baadaye shimo lilikuwa tayari na dereva alimpa Nyanjige taarifa
hiyo na wote wawili wakaingia hadi ndani ambako Nyanjige alibeba mwili wa
mama yake uliokuwa mifupa tupu katika mikono yake na kuanza kutembea hadi
nje! Baadhi ya mifupa ilikatika na kudondoka chini akalazimika kurudi kuiokota
ndipo shimo likafunikwa!
Yalikuwa mazishi ya watu wawili tu! Katika maisha yake yote Nyanjige hakuwahi
kuumia moyo kama siku hiyo, walipomaliza mazishi hayo tayari ilikuwa saa sita
ya usiku na dereva aliomba ruhusa ya kuondoka lakini Nyanjige alikataa na
kuahidi angemlipa pesa za siku zote ambazo angekaa naye.
Kwa usiku mzima Nyanjige alilia akimlilia mama yake, moyo wake ulijaa kisasi
alitaka kulipa kisasi kwa unyama aliofanyiwa mama yake! Asubuhi siku iliyofuata
waliondoka hadi mjini Mwanza kwenye maduka ya madawa ya mifugo ambako
Nyanjige alinunua sumu ya kuulia wadudu aina ya DDT bila dereva kugundua
kilichonunuliwa na wote wawili walirejea tena hadi kijijini Usagara!
Jioni Nyanjige alizunguka kijijini bila kuongea na mtu yeyote akijaribu kutafuta ni
wapi kilipokuwa kisima ambacho wanakijiji walitumia kwa maji ya kunywa,
alipogundua mahali kilipokuwa alirudi nyumbani na usiku wa siku hiyo dereva
akiwa usingizini alitoka na kutembea hadi kwenye kisima akaimiminina sumu yote
kwenye maji.
Usiku huohuo alitoroka na dereva wake kuelekea Kigoma kupitia Kibondo, Kasulu
hadi Kigoma mjini ambako alimlipa dereva kiasi cha shilingi laki tano na kuagana

Page 12 of 77
nae! Ni siku hiyo hiyo aliyoingia Kigoma ndiyo siku aliyovuka na boti hadi mji wa
Kalemie nchini Kongo ambako alipanda basi lililompeleka moja kwa moja hadi
Kinshasa ambako alijitambulisha kama mtafiti wa wanyama na kuruhusiwa kuishi
porini.
Alijua aliyoyaacha nyuma yake yalikuwa makubwa na kweli watu mia moja na
hamsini walikunywa maji ya kisimani asubuhi ya siku aliyomwaga sumu walikufa!
Uchunguzi ulipofanyika sumu aina ya DDT iligundulika katika maji na kila
mwanakijiji alikua na uhakika sumu hiyo ilimwaga katika kisima na Nyanjige na
kutoroka ni hapo ndipo msako kumsaka ulipoanza.
Askari aliyenusurika msituni Kungoni:
“Jamani huko hali ni mbaya kupita kiasi, jeshi lote mlilonipa limemalizika kuna
mbung’o na nzige wa hatari sijapata kuona, wanakula miili ya watu kama mchezo!
Watu wote mlionipa wameliwa na kubaki mifupa tupu! Njooni muone mfano wake
huku kwenye helkopta!” Alisema Meja Jenerali Lupilya na kuwachukua wakuu wa
majeshi hadi kwenye helkopta aliyowasili nayo! Kila mtu alishika mdomo kwa
mshangao jinsi wanajeshi wawili walivyoliwa nyama za mwili wao.
“Waliofanya hivi ni mbung’o na nzige?”
“Ndiyo na vijana wote niliokwenda nao wapo kama unavyoiona hii mifupa!”
“Duh! Na wewe umeokoka vipi?” Mkuu wa majeshi aliuliza.
“Huyo bibi kanihurumia tu kwa sababu niliongea Kisukuma!”
“Anaongea Kisukuma?”
“Ndiyo tena vizuri tu! Ila jeshi lake si mchezo ni la wanyama na wadudu tupu na
wote wanamtii anaishi peke yake msituni, mlishawahi kuona binadamu anazuia
nzige kula kitu?”
“Hapana!”
“Basi mie nimeona kwa macho yangu nzige walikuwa wanile lakini bibi huyo
alipofanya “Psyiiiiii” nzige wote wakatulia!”
Siku hiyo hiyo kikao kilikaa na kuamriwa kuwa jeshi jingine lenye askari 10,000/=
lipelekwe haraka msituni kwa mapigano mengine makali zaidi ili kuhakikisha bibi
Nyanjige anakamatwa na kurejeshwa nchini Tanzania kwa mashtaka ya mauaji ya
halaiki ya watu na Lupilya alitakiwa tena kuliongoza jeshi hilo.

Page 13 of 77
Wakuu wa majeshi walishangaa kumwona Meja Jenerali Lupilya akivua
magwanda yake pamoja na silaha akakabidhi kwa mkuu wa majeshi akawa
ameacha jeshi! Kujiuzuru kwa Lupilya kuliwafanya wengi waamini jeshi la bibi
Nyanjige hakuwa mchezo.
“Jamani mimi naona ni heri muombe msaada umoja wa Mataifa nina hakika nyie
wote mnaokwenda hamtarudi hapa Tanzania!” Alishauri Lupilya lakini hakuna
mtu aliyesikiliza, siku hiyo hiyo alifukuzwa kambini na mkuu wa majeshi aliamua
kuongoza kikosi hicho kwenda Kongo kupitia Kigoma kushuhudia mwenyewe!
Alisomea mambo ya jeshi nchini Cuba na Israel hivyo alikuwa na uhakika wa
kupata ushindi dhidi ya jeshi la wadudu na wanyama wa bibi Nyanjige.
...Msituni:
Tembo zaidi ya elfu tano walikusanyika kumzunguka bibi Nyanjige! Mbung’o
pamoja na Nzige wasio na idadi walizunguka angani na kufanya eneo hilo liwe na
kivuli ingawa ilikuwa ni hali ya jua kali! Ulikuwa ni kama mkutano wa hadhara wa
wanyama na wadudu na bibi Nyanjige alikuwa akiwasiliana na wadudu na
wanyama wote katika lugha zao akiwatahadharisha juu ya uvamizi mwingine na
kuwaomba wakae tayari.
Wanyama na wadudu waliomchukulia bibi Nyanjige kama Malkia wao waliahidi
kutoruhusu mtu yeyote amdhuru labda wote wawe wamemalizika! Lugha ya
wadudu na wanyama aliojifunza ilimsaidia sana kuwasilina sana kuwasiliana na
wanajeshi wake.Baada tu ya mkutano huo Tembo, Nzige na Mbung’o wote
walisambaa na kuanza ulinzi msituni.

Page 14 of 77
SURA YA TATU

MELI zipatazo ishirini kubwa zikiwa zimebeba askari pamoja na vifaa


mbalimbali vya kivita zilikuwa safarini kuelekea Kongo! Ndege zaidi ya hamsini
ziliruka moja baada ya nyingine kutoka uwanja wa ndege wa Kigoma kwenda
Kongo, helkopta zilizojazwa madawa ya kuua wadudu zilikuwa hewani zikielekea
msituni kwa lengo la kuwaua Nzige na mbung’o wote kabla ya kumkamata bibi
Nyanjige!
Kulikuwa na kila dalili kuwa isingechukua masaa hata mawili kabla msitu huo
haujafutwa katika uso wa dunia Tembo wote wakiwa wameteketezwa kwa
makombora!
Askari wote walifurahia vita hiyo na walikuwa na uhakika wa kumkamata bibi
Nyanjige na kumrudisha Tanzania akiwa maiti au hai! Vifo vya wenzao zaidi ya
5000 viliwatia hasira kali sana na walitaka kulipiza kisasi!
...Asubuhi ya siku hiyo msitu ulikuwa kimya kabisa, ni ndege tu waliopiga kelele
wanyama wengine walikuwa kimya! Tembo wengi walikusanyika katikati ya msitu
wakiwa wameiweka nyumba ya bibi Nyanjige katikati kuhakikisha usalama wake.
Ndege aina ya Tai ambao idadi yao ilikuwa si rahisi kuifahamu walionekana
wakiruka angani, walikuwa tayari kwa hatari yoyote ambayo ingetokea na
walikuwa na ufahamu kuwa wakati wowote msitu ungeweza kuvamiwa tena.
Kwa amri waliyopewa na bibi Nyanjige kama wangevamiwa Tembo na nzige
wangeendelea na vita vya nchi kavu na ndege aina ya Tai, Kunguru na mwewe
wangeendelea na vita vya angani wakipambana na na ndege zilizotegemewa
kuuvamia msitu. Hali ya vita ilinukia kila mahali,kilichokuwa kikisubiriwa wakati
huo ni kuwasili kwa maadui.
Masaa machache baadaye miungurumo wa ndege za kivita ilisikika angani upande
wa mashariki, bibi Nyanjige aliponyanyua uso wake kuangalia angani aliziona
ndege kumi zikipita na alipozisoma kwenye mabawa yake aliliona neno TAN na
zilikuwa na nembo ya Twiga nyuma yake alijua ndege hizo zilikuwa ni za jeshi la
Tanzania.
Bila kuchelewa alipiga mluzi kwa sauti ya juu ili kuashiria kuwa sasa mambo
yalikuwa tayari na palepale makundi yote ya ndege waliokuwa wakizunguka

Page 15 of 77
angani walizizingira ndege zote tatu na kuziweka katikati kisha wakaanza kutoboa
vioo vya ndege hizo kwa mbele na kuingia hadi ndani ambako walianza
kuwashambulia marubani kabla hawajafanya jambo lolote.
Ndege walifanya hivyo kwa ndege ya kivita moja baada ya nyingine hatimaye
ndege zote kumi zilianguka chini na kulipuka! Mamia ya ndege pia walilipuliwa na
moto.

*****
Bibi Nyanjige aliyekuwa bado yu katikati ya kundi kubwa la tembo alishuhudia
mashambulizi ya ndege wake na kuhisi ushindi! Lakini ghafla alishtuka alipoona
helkopta tano zikiruka kutoka upande mwingine wa msitu na vitu kama mipira ya
maji ilichungulia kutoka ndani ya helkopta hizo, alijua tayari vita nyingine ilikuwa
imefika.
Kwa mara nyingine alipiga tena mluzi na kundi jingine kubwa la ndege aina ya Tai
liliibuka na kuanza kuzizingira helkopta hizo lakini muda mfupi baadaye bibi
Nyanjige alishangaa kuona ndege wengi wakianguka ardhini wakiwa wamekufa na
kuijaza ardhi! Alishindwa kuelewa ni kitu gani kilitumika kufanya mauaji hayo ya
ndege wake.
Alipomuokota ndege mmoja na kumnusa ndipo aligundua ndege wake waliuawa
kwa sumu kali aina ya DDT! Helkopta zilizidi kusogea eneo alilokuwa na
alishuhudia mipira ya maji ilimwaga aina Fulani ya maji maji na mvuke angani
ndege wake wakazidi kuporomoka na hatimaye anga ikabaki wazi bila ndege hata
mmoja.
Kifo cha ndege kilimtisha na alipoona hivyo alipiga mluzi kuamuru jeshi jingine
liingie kazini na nzige wengi walivamia anga kwa makundi makundi lakini kama
ilivyokuwa kwa ndege nzige nao waliporomoshwa kwa makundi makundi hadi
ardhini.
Kuona hivyo bibi Nyanjige alianza kukata tamaa kwani aliona ni kiasi gani jeshi
lake lilikuwa limepuputika, alikuwa amebaki na jeshi la tembo peke yake na
hakujua kama tembo hao wangeweza kuhimili vishindo vya vita kali iliyokuwa
mbele yake.
Wakati akiwaza hayo ghafla alianza kuwaona Tembo wakiduwaa na kuketi chini
na hata yeye mwenyewe alianza kuhisi kulewa na muda mfupi baadaye bibi
Page 16 of 77
Nyanjige alipoteza fahamu kabisa na kulala ardhini, madawa yaliyokuwa
yakimwaga na helkopta angani yalimlewesha bibi Nyanjige pamoja na Tembo
wake. Kabla hajapoteza fahamu zake zote ni kitu kimoja tu alichowaza kichwani
mwake. angefanywa nini baada ya kukamatwa KWA VIFO
ALIVYOSABABISHA.

*****
Meli zilizobeba askari wa nchi kavu wa Tanzania ziliingia katika mji wa Kalemii
nchini Kongo na kubebwa katika magari tayari kwa safari ya kwenda msituni!
Kulikuwa pia na vifaru vipatavyo sabini kwa ajili ya vita hiyo pia vilishushwa na
kuendeshwa kuelekea msituni tayari kwa mapambano.
“Ni lazima akamatwe” Alisema kiongozi wa majeshi ya kongo yaliyojitolea
kuyasaidia majeshi ya Tanzania mara baada ya kuwapokea askari wa Tanzania.
Tayari vita hiyo ilishachukuwa sura kubwa kuliko ilivyotegemewa kila askari
alikuwa na hasira kali dhidi ya bibi Nyanjige na wengi walitamani kumwona huyo
bibi aliyeitingisha dunia kwa uwezo wake mkubwa wa kushawishi wanyama
kufanya mauaji ya kikatili, lilikuwa si jambo rahisi kuamini.
“Baada ya helkopta kumwaga sumu na kuwaua wadudu na pia kuwalewesha
Tembo, ndege za kulipua mabomu zitapita na kuusambaratisha msitu baada ya kazi
hiyo jeshi la nchi kavu litaingia msituni na kukamilisha kazi!” Alisema mkuu wa
majeshi ya Tanzania.
Wakati jeshi la nchi kavu likiingia msituni ilitolewa amri kuwa helkopta zote
zilizokuwa zikipita angani na kumimina sumu zisitishe zoezi hilo kwanza ili kutoa
nafasi kwa ndege za kudondosha mabomu na ndege kama kumi hivi ziliruka na
kuingia msituni ambako milipuko ya mabomu ilisikika kila mahali, wakati huo
askari wa miguu waliendelea kutembea taratibu kuingia msituni.
Kwa jinsi mabomu yalivyolipuka hakuna mtu hata mmoja aliyeamini bibi
Nyanjige angekuwa hai mpaka wakati jeshi la waenda kwa miguu linaingia
msituni, kwani msitu ni kama uligeuzwa nje kuingia ndani! Ulifukuliwa kila
mahali hapakuwa na mahali pa mtu kujificha.
“Ni lazima huyu bibi atakuwa amekufa lakini maiti yake ni ni lazima itafutwe
twende nayo hadi Tanzania Rais wetu akaione bibi huyu amesababisha vifo vya

Page 17 of 77
watu wengi mno” Hayo ndiyo maongezi yaliyoendelea midomoni mwa askari
wengi waliotembea kuingia msituni.
Baada ya mashambulizi ya mabomu yaliyodondoshwa na ndege nyingi angani,
ilifuata hatua ya mwisho ya jeshi la nchini kavu kwa lengo la kwenda kupambana
na tembo kama wangekuwa hai na kumkamata bibi Nyanjige ama kuitafuta maiti
yake hadi ipatikane na kuondoka nayo! Kwa fikra za askari wengi vita hiyo
ilikuwa imefika mwisho
Jeshi la askari wasiopungua elfu tano liliuvamia msitu huo mkubwa kwa ajili ya
kazi hiyo, kila mahali walikopita walishangaa kuona idadi kubwa ya tembo
wakiwa wamekufa na kusambazwa kabisa na mabomu lakini hawakumwona bibi
Nyanjige mahali popote kila mtu aliamini bibi huyo alikufa katika mashambulizi
hayo.

*****
Hakikuwa kitu rahisi kwa bibi Nyanjige kufa kama walivyotegemea kwani dakika
kama ishirini hivi kabla ya jeshi la nchi kavu halijauvamia msitu, bibi alirejewa na
fahamu zake na kukuta kila upande wa mwili wake kuna Tembo mkubwa mnene
aliyekufa na aliponyanyuka na kukaa kitako macho yake yalipambana na shimo
kubwa lililochimbuliwa alijua hiyo ilikuwa ni kazi ya mabomu.
Aliendelea kusikia milipuko sehemu mbalimbali msituni, ndege zilikuwa
zikidondosha mabomu, kwa hali hiyo ingawa alikuwa amelewa aliweza
kunyanyuka na kujikongoja akipita katikati ya msituni chini ya miti michache
iliyokuwa imebaki mbele alisimama alipoiona helkopta iliyoungua huku pembeni
mwake kukiwa na maiti za wanajeshi wawili waliokuwa.
Wazo la kujiokoa lilimwijia kichwani mwake kwa sababu alijua wakati wowote
angekamatwa, aliivamia moja ya maiti hizo na kuivua magwanda na kuyavaa na
akachukua pia kofia na kuivaa kichwani mwake, alipomaliza tu kufanya hivyo
alisikia nyasi nyuma yake zikitingishika na aliamini haukuwa upepo.
Walikuwa ni maaskari wa nchi kavu wa Tanzania! Walioibuka kutoka katikati ya
nyasi wakiwa na silaha zao mikononi, moyo wa bibi Nyanjige uliingiwa na hofu
kubwa na alianza kutetemeka akijua ni lazima angetiwa nguvuni na kuuawa.
Pamoja na kuwa bibi kizee lakini alikuwa shupavu kuliko umri wake, alijiangusha
karibu kabisa na maiti aliyoivua magwanda.

Page 18 of 77
Kwa jicho la pembeni aliwashuhudia askari wakitembea kuelekea mahali
ilipokuwa helkopita iliyoungua, kila mmoja wao alisikika akiongea kwa huzuni
hasa walipoziona maiti zikiwa zimelala pembeni, wao waliamini miili yote mitatu
iliyolala chini ilikuwa maiti hawakujua kama mtu waliyekuwa wakimsaka alikuwa
miongoni mwa miili hiyo.
“Masikini hawa ni askari wetu kabisa. Hakyanani huyu bibi tukimtia mikononi
tutamchanana vipande viwili!” Alisema mmoja wa askari hao kwa hasira huku
akirukaruka kuonyesha hasira aliyokuwa nayo.
Wengi wa maaskari walipoziona maiti hizo walilia machozi kwa uchungu na kila
mmoja wao alionyesha hasira aliyokuwa nayo juu ya bibi Nyanjige.
Bibi Nyanjige alisikia kila kitu kilichoongelewa na askari hao na kuzidi kuingia na
hofu! Alibana mbavu ili asionekane akihema, alijua kama angegundulika ni lazima
wangemuua kikatili kuliko ilivyowahi kutokea duniani.
“Sasa tufanye nini?” Mmoja wa maaskari alimuuliza mkuu wa jeshi.
“Tusonge mbele vijana wengine wachukue hizi maiti tatu wazipeleke hadi
tulipoyaacha magari, wazipakie wakati tukisubiri utaratibu wa kuzirudisha
nyumbani baada ya vita ya leo, sawa?” Alisema mkuu wa majeshi na vijana watatu
walijitokeza wakaimana na kuibeba miili hiyo begani hakuna hata mmoja aliyehisi
kuwa mmoja kati ya miili waliyoibeba ulikuwa ni wa mtu hai! Bibi Nyanjige
alizidi kubana pumzi.
Alilala begani kwa mmoja wa maaskari hao bila kujitingisha huku akihema mara
moja kila baada ya dakika moja ili asingundulike! Alijua kama mbavu zake
zingecheza ni lazima askari angeshtuka na kupiga kelele na huo ndio ungekuwa
mwisho wake.
Mpaka wanafika yalipokuwa magari na kuitupa miili hiyo ndani ya gari hakuna
askari hata moja aliyehisi mwili mmoja kati ya walioipakia ulikuwa ni wa bibi
Nyanjige tena akiwa hai.
Maaskari waliondoka mbio kuwafuata wenzao msituni na muda mfupi baadaye
maiti zilizidi kusombwa na kurundikwa ndani ya gari huku bibi Nyanjige
akiendelea kugandamizwa na kuumia! Maiti zaidi ya hamsini zilipangwa juu yake.
“Hawanipati ng’o”Aliwaza bibi Nyanjige huku akizididi kutiririkiwa na damu
kutoka katika miili ya watu waliokufa.

Page 19 of 77
wa ndege na nzige walioifunika.
Siku hiyohiyo jioni iliamriwa maiti zote zilizokuwa zimekusanywa zisafirishwe
kurudi Tanzania wakati kukiwa na mpango kamambe wa kuendelea na operesheni
kumsaka bibi Nyanjige siku ya iliyofuata.
Baada ya kauli hiyo ya mkuu wa majeshi maiti zote zilianza kuhamishwa kutolewa
kwenye gari na kufungwa katika mifuko maalum ya nailoni tayari kwa
kusafirishwa kurudishwa Tanzania, bila kugundulika bibi Nyanjige alifungwa
ndani ya mfuko na kupakiwa katika ndege maalum iliyoandaliwa.
Dakika kama mbili hivi baada ya kuwekwa katika mfuko wa nailoni akiwa
amepangwa ndani ya ndege bibi Nyanjige alianza kukosa hewa! Alihisi angekufa
sababu ya kukosa hewa safi, Kwa kutumia meno yake makali alitoboa tundu katika
mfuko wake na kuitega pua yake kwenye tundu hilo akawa anavuta hewa taratibu
kutoka nje.
*****

Ndege ilipoingia Dar es Salaam saa nne ya usiku maiti zote zilipakuliwa na
kupakiwa ndani ya gari maalum lililoandaliwa tayari kwa kuzipelekea chumba cha
maiti cha hospitali ya jeshi iliyoitwa Military General Hospital kuhifadhiwa katika
chumba chenye baridi ili zisiharibike zikisubiri operesheni imalizike na wote
waliokuwa wazikwe siku moja kwa heshima ya jeshi.
Masaa matatu baada ya kuingizwa katika chumba cha maiti baridi kali
iliyokuwemo ndani ya chumba hicho ilimfanya bibi Nyanjige ahisi mwili wake
ukiganda aligundua asingeweza kuendelea kuwa ndani ya chumba hicho kwa muda
mrefu kabla roho yake haijatoka.
Msako wa kumsaka bibi Nyanjige porini uliendelea kwa masaa karibu kumi na
mbili bila mafanikio yoyote! Nyumba yake ilisambaratishwa na mashimo mengi
yalifukuliwa akitafutwa lakini bado hakuonekana mahali popote wanajeshi
walikata tamaa na kuamini alikuwa amekufa.
Miili mingi ya tembo wakiwa wamekufa ilionekana kila mahali msituni, ndege na
nzige waliokauka pia walionekana ardhini ilikuwa si rahisi kuiona ardhi sababu ya
wingi wa ndege na nzige walioifunika.

Page 20 of 77
Siku hiyohiyo jioni iliamriwa maiti zote zilizokuwa zimekusanywa zisafirishwe
kurudi Tanzania wakati kukiwa na mpango kamambe wa kuendelea na operesheni
kumsaka bibi Nyanjige siku ya iliyofuata.
Baada ya kauli hiyo ya mkuu wa majeshi maiti zote zilianza kuhamishwa kutolewa
kwenye gari na kufungwa katika mifuko maalum ya nailoni tayari kwa
kusafirishwa kurudishwa Tanzania, bila kugundulika bibi Nyanjige alifungwa
ndani ya mfuko na kupakiwa katika ndege maalum iliyoandaliwa.*
Ndege ilipoingia Dar es Salaam saa nne ya usiku maiti zote zilipakuliwa na
kupakiwa ndani ya gari maalum lililoandaliwa tayari kwa kuzipelekea chumba cha
maiti cha hospitali ya jeshi iliyoitwa Military general hospital kuhifadhiwa katika
chumba chenye baridi ili zisiharibike zikisubiri operesheni imalizike na wote
waliokuwa wazikwe siku moja kwa heshima ya jeshi.
Masaa matatu baada ya kuingizwa katika chumba cha maiti baridi kali
iliyokuwemo ndani ya chumba hicho ilimfanya bibi Nyanjige ahisi mwili wake
ukiganda aligundua asingeweza kuendelea kuwa ndani ya chumba hicho kwa muda
mrefu kabla roho yake haijatoka.
Kwa nguvu zake zote za kizee alijitahidi na kuutoboa mfuko wa nailoni
uliomfunga akatoka nje na kupenya katikati ya maiti nyingine na kusimama wima
ndani ya chumba cha maiti huku akitetemeka mwili mzima. Alijitahidi na
kuusogelea mlango mkubwa wa kuingilia chumba cha maiti na kujaribu
kuutingisha lakini ulikuwa mgumu alitaka atoke nje na kuondoka zake!
Aliposhindwa kuufungua alibaki ameduwaa.
Kwa masaa karibu sita aliketi pembeni ya mlango akiendelea kupigwa na baridi,
alijaribu kufikiri ni kwa njia gani angeweza kujiokoa kutoka ndani ya chumba
hicho lakini alishindwa, mara ghafla alisikia jogoo likiwika akafahamu tayari
ilikuwa ni alfajiri na kuamini masaa machache baadaye mlango ungefunguliwa.

Page 21 of 77
SURA YA NNE

BAADAE alianza kuona mwanga wa jua ukipenyeza kwenye madirisha na


muda mfupi baadaye aliusikia mlango wa chumba cha maiti ukitingishwa akajua
kulikuwa na mtu aliyetaka kuufungua! Bibi Nyanjige alikimbia na kwnda kujificha
nyuma ya kabati kubwa iliyokuwemo ndani ya chumba hicho.
Akiwa nyuma ya kabati alishuhudia mlango ukifunguliwa na mtu aliyevaa mavazi
ya kijeshi aliingia na kwenda kuketi nyuma ya meza iliyokuwa mbele ya kabati
alilojificha! Mtu huyo alichukua kalamu na daftari na kuanza kuandika mambo
ambayo bibi Nyanjige hakuyaelewa.
Dakika chache tena baadaye aliingia mwanamke aliyevaa mavazi ya kijeshi akiwa
na fagio kubwa mkononi, bibi Nyanjige alielewa mwanamke huyo alitaka kufanya
usafi na ni lazima angemwona alishindwa angefanya kitu gani kujiokoa, alifikiria
kukimbilia upande mwingine alijua angeonekana na kuamua kubaki hapo hapo.
Askari wa kike alianza kufagia taratibu akielekea nyuma ya kabati kubwa, bibi
Nyanjige alitetemeka mwili mzima akijua mwisho wake tayari ulikuwa umefika!
Alibaki akitetemeka wakati mfagiaji akielekea nyuma ya kabati, bibi Nyanjige
hakujua ni kitu gani kingetokea.
Huku akitetemeka bibi Nyanjige alinyata taratibu na kuizunguka kwa mara ya pili
kabati kuelekea upande mwingine ili kumkwepa muuguzi akapanda kwenye ngazi
na kulala katikati ya maiti mbili bila muuguzi kugundua, alimwona muuguzi
akiendelea kufagia kuizunguka kabati, bibi alijua kama angebaki nyuma ya kabati
ni lazima angekamatwa.
“Mungu amesaidia swali ni kwamba
nitatokaje humu ndani?” Alijiuliza bibi Nyanjige bila kupata jibu.
Alitaka sana kutoka chumba cha maiti mapema kabla maiti za wanajeshi
hazijakaguliwa asubuhi hiyo jambo ambalo kwa uhakika alijua lingehatarisha
usalama wake! Kwa idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi alivyosababisha alikuwa
mtu aliyesakwa kuliko hata gaidi Carlos!
Baada ya kumaliza kufagia muuguzi alitoka nje na kuufunga mlango wa chumba
cha maiti nyuma yake na giza likarejea tena! Bibi Nyanjige aliutumia muda huo
kuvua nguo za kijeshi alizokuwa nazo mwilini mwake na kubaki na gauni lake la
Page 22 of 77
kawaida, alizitupa nguo hizo sakafuni na kuendelea kulala katikati ya maiti akizidi
kutafakari njia ya kujiokoa na kifo kilichokuwa mbele yake.
Mara mlango ulifunguliwa safari hii hakuingia muuguzi peke yake aliongozana na
kundi la wanaume kumi na mbili.
“Maiti yenu ipo palee kwenye zile ngazi pembeni ya kabati!” Alisema muuguzi
huku akizionyesha maiti ambazo bibi Nyanjige alilala katikati yake! “Hapa lazima
nijikaushe vinginevyo mtu mzima nitaabika!” Aliwaza bibi wakati wanaume wale
wakizidi kuikaribia ngazi aliyolala.
“Nyie wanaume hebu mmoja wenu aje atie kwanza saini kwenye kitabu cha
kuchukulia maiti yenu!” Muuguzi aliwaeleza na wanaume wote walisita na mmoja
wao alikwenda hadi kwenye meza na kutia saini kwenye kitabu!
“Haya nendeni mkachukue zipo maiti mbili moja ndiyo yenu!”
“Sawa!”
Wanaume hao waliondoka kuelekea kwenye ngazi na walipozifikia walishangaa
kuona kukuta kuna maiti tatu moja ya mwanamke ikiwa imelala katikati ya maiti
mbili na sakafuni kukiwa na mavazi ya kijeshi!
“Nesi!”
“Mnasemaje?”
“Mbona kuna maiti tatu wakati wewe umesema ni mbili?”
“Mungu wangu wee!” Bibi Nyanjige aliwaza moyoni mwake na kujua tayari
mambo yalishaharibika alizidi kubana pumzi na mbavu kama mtu aliyekufa siku
tatu kabla ya siku hiyo!Macho yake aliyafunga vizuri na mdomo wake kuuacha
wazi! Ilikuwa si rahisi hata kidogo kuamini kuwa mtu aliyekuwa mbele yao
alikuwa mzima.
“Nyie chukueni maiti yenu muondoke, hata kama zipo nne nini
kinachowasumbua?” Muuguzi alijibu, jibu hilo lilimfurahisha sana bibi Nyanjige.
Baada ya jibu hilo wanaume hao waliushika mwili wa bibi Nyanjige na kuuweka
pembeni kisha wakachukua maiti yao na kuishusha chini, wakaibeba na kuanza
kutoka nayo nje ya chumba cha maiti!
Akili ya bibi Nyanjige ilifanya kazi kwa haraka haraka kama kompyuta! Alitaka
kuitumia nafasi hiyo kuokoa maisha yake. Alipomwangalia muuguzi mezani

Page 23 of 77
alikuta ameinamisha kichwa chake akiandika mambo fulani kwenye vitabu vyake
bila kuwaangalia watu waliokuwa wakitoka na maiti.
“Huu ndio wakati wenyewe!”, Alisema bibi Nyanjige na kuruka na kutua sakafuni
bila mlio wala kelele.
“Yes! Hiyo inaitwa staili ya paka mwizi maarufu wa mboga!” Alisema bibi
Nyanjige akiisifia staili aliyotumia kuruka.
Alinyata kwa kasi ya Chui akiwafuata wanaume waliobeba maiti kwa nyuma!
Moyo ulikuwa ukimdunda kwa kasi ya ajabu wasiwasi wake ulikuwa ni muuguzi
kunyanyua uso au watu aliokuwa akiwafuata kugeuka nyuma na kukuta
mwanamke akiwafuata, alijua ni lazima wangeshangaa na kupiga makelele na hilo
lingemaanisha kukamatwa.
Alitembea mpaka nje ya chumba cha maiti bila kugundulika hakuna mtu kati ya
wanaume wote waliokuwemo ndani ya chumba cha maiti aliyegeuka na kuangalia
nyuma. Maiti ilipofikishwa nje watu wote waliokuwepo waliangua kilio kwa
uchungu hakuna mtu aliyeonekana kujali kitendo cha bibi Nyanjige kuonekana
akitoka chumba cha maiti.
Ilionekana wazi mtu aliyekufa alikuwa tegemeo la watu wengi na alikuwa kipenzi
cha watu! Ili kuficha tatizo lake bibi Nyanjige aliangua kilio kikali kuwazidi hata
wafiwa waliokuwepo nje ya chumba hicho watu wote waligeuka na kujiuliza bibi
huyo alikuwa nani! Ni hapo ndipo alipogundua kilio chake kilikuwa kikali na
kupunguza kidogo sauti.
“Mh! Wasije wakanishtukia bure!” Aliwaza bibi Nyanjige lakini mpaka hatua hiyo
aliamini tayari alishanusurika kifo!

*****
Maiti ilipakiwa ndani ya gari na watu wengine walipanda katika mabasi mawili
yaliyokodishwa kwa ajili ya kubeba watu kwenda chumba cha maiti, bibi Nyanjige
hakutaka kuipoteza nafasi hiyo alipanda ndani ya basi mojawapo akiwa mtu wa
tano tu kabla ya watu wengine kupanda.
“Siwezi kupanda daladala wakati usafiri upo! Na kwa staili hii hawanipati ng’o na
hata wakinipata watakuwa wamehangaika vya kutosha!”Aliwaza bibi Nyanjige
wakati akitembea kuelekea kwenye kiti cha nyuma kabisa cha basi na kuketi.

Page 24 of 77
Wanawake wengine watatu walimfuata na kukaa karibu naye, walionekana
kumshangaa kwa sababu hakuwa na khanga wala kitenge zaidi ya gauni chafu
alilovaa! Bibi Nyanjige aliishtukia hiyo na kuamua kukizamisha kichwa chake
katikati ya mikono kama mtu aliyekuwa akilia kwa uchungu, watu wengi ndani ya
basi walihisi alikuwa shangazi au mama wa marehemu kwa uchungu alioonekana
kuwa nao!
“Nikifika huko nyumbani kwao, nitateremka na kwenda zangu stesheni ya treni na
kama lipo nitaondoka leo hii hii kwenda Mwanza nataka nikajifiche kwenye kisiwa
cha Rubondo pia kuna wanyama wengi sana nataka niunde jeshi jingine ili
nipambane nao tena upya! Nataka niifundishe dunia somo ambalo haitalisahau,
safari hii nitamwaga Tembo na Nzige mjini watu wabanane!” Aliwaza bibi
Nyanjige.
“Bibi!” Aliita msichana mmoja aliyekaa kiti jirani na bibi Nyanjige tayari gari
ilishaanza kuondoka hospitalini.
“Mbona huna khanga?”
“Nimedondosha mjukuu wangu!”
“Wapi bibi?”
“Sikumbuki!”
“Haya chukua hii hapa ikusaidie kidogo!”Alisema binti huyo wakati akimkabidhi
bibi Nyanjige khanga aliipokea na kujifunika nayo kichwani badala ya sehemu
nyingine za mwili! Hakutaka kuonekana sura kwa kuogopa kujulikana!”

*****
Basi lilikwenda kwa kasi likipita maeneo ya Mwenge, Morocco kuelekea kivuko
cha kwenda Kigamboni.
“Jamani kuna mtu kazidi nini humu ndani, mbona mwenzenu kakosa kiti?” Utingo
wa gari hilo aliuliza baada ya kuona kijana mmoja amesimama wima wakati gari
ilikuwa na uwezo wa kubeba watu ishirini na waliopanda basi hilo kwenda chumba
cha maiti walikuwa shirini na hakuna aliyesimama!
Abiria walianza kuangaliana ili kujua ni nani alikuwa amezidi! Bibi Nyanjige
alizidi kutetemeka ndani ya khanga aliyojifunika alijua ni lazima angegundulika na

Page 25 of 77
si ajabu wangemfikisha polisi! Aliendelea kuomba Mungu amsaidie ili
asigundulike.
“Acha tu braza mimi nitasimama!” Alisema kijana huyo huku akisogea mbele
kuelekea kwa dereva.
“Njoo ukae hapa!” Alisema dereva akimwita kijana huyo akakae kwenye eneo la
karibu na gia ya basi alikaa na kujisikia vizuri! Watu wote ndani ya gari walikuwa
kimya, kwikwi za bibi Nyanjige tu ndio zilisikika ndani ya khanga aliyojifunika
kichwani.

*****
Dakika tano tangu magari yaondoke chumba cha maiti, wanajeshi wakiwa na
mkuu wao wa hospitali ya jeshi waliingia chumba cha maiti na kuanza kuzikagua
maiti za wanajeshi, zilipohesabiwa walishangaa kukuta maiti moja haipo!
Walipojaribu kuzunguka chumba cha maiti wakitafuta maiti moja walishangaa
kukuta mavazi ya kijeshi yametupwa sakafuni, walipomuuliza muuguzi mtunza
chumba cha maiti alionekana kutofahamu lolote juu ya mavazi hayo wasiwasi
mwingi uliwaingia.
“Kuna watu wamechukua maiti mpaka sasa hivi?”
“Ndiyo!”
“Ni wa wapi?”
“Ni wenyeji wa Kigamboni!”
“Balozi wao ni nani?”
“Kessa Mwambeleko!”
“Wana simu yoyote waliyokuachia?”
“Ndiyo!”
“Hebu tupatie hiyo namba yao tujaribu kuuliza!”
“Ni 0744 382856!”
Mmoja wa wanajeshi hao alikuwa na simu ya mkononi palepale alibonyeza namba
zilizotajwa na kuanza kusikiliza sikioni mwake.

Page 26 of 77
“Mko wapi?” Ndilo swali aliloanza kuuliza.
“Tupo feri tunasubiri boti wewe ni nani?” Aliuliza upande wa pili.
“Mimi ni mwanajeshi wa jeshi la ulinzi nipo chumba cha maiti cha hospitali ya
Jeshi, nina wasiwasi mtakuwa mmechukua maiti tofauti!”
“Maiti tofauti! Kivipi?”
“Tunahisi mmechukua maiti ya mwanajeshi aliyeuawa Kongo!”
“Hapana hiyo si kweli tuliyemchukua ni ndugu yetu kabisa na mimi ni mdogo
wake kabisa!”
“Hebu subirini hapa hapo mlipo!” Mwanajeshi huyo aliamuru na muda mfupi
baadaye yeye na wenzake waliingia ndani ya gari la jeshi kuelekea kivukoni,
ilichukua kama muda wa dakika kumi kufika na kuomba jeneza lifunguliwe ili
maiti ikaguliwe.
Yalitokea mabishano makali wanajeshi wakidai maiti irudishwe chumba cha maiti
lakini mdogo wa marehemu hakukubaliana nao mpaka mtu mmoja alipotoa picha
ya marehemu na kuifananisha na maiti iliyokuwa ndani ya jeneza ndipo
walipokubali na kuondoka!
Muda wote huo bibi Nyanjige alikuwa amejifunika khanga kichwani akitetemeka
hakutaka sura yake ionekane na alimshukuru Mungu kuwa mpaka wakati huo
hapakuwa na mtu aliyekwisha mshtukia! Alipanga wakifika kigamboni
achoropoke na kutoroka msibani kurudi mjini ambako angetafuta usafiri wa treni
kumpeleka Mwanza.

Page 27 of 77
SURA YA TANO

KAMA kuna makosa aliyowahi kuyafanya katika maisha yake bibi Nyanjige ni
kitendo chake cha kuzihamisha karatasi alizoandika matukio yote muhimu akiwa
porini huko Kongo kutoka katika gauni lake na kuziweka katika magandwa ya
jeshi aliyojivisha ili kuepuka kugundulika na kusahau kuzitoa karatasi hizo wakati
wa kuyavua magwanda.
Ni karatasi hizo zilizofanya wanajeshi wagundue ni nani aliyetoroka! Ziliposomwa
kila mtu alijua bibi Nyanjige aliingia nchini akiwa katika maiti zilizoletwa kutoka
Kongo na kutoroka akiwa chumba cha maiti.
“Aisee nimeamini huyu bibi ni hatari sijui anatumia uchawi pia?”Aliuliza jenerali
Mwita Mitiro katika kikao cha wakuu wa jeshi la polisi na jeshi la Wananchi
kilichoitishwa kulijadili suala la bibi Nyanjige haraka.
“Sasa tufanye kipi maana tayari huyu bibi keshatutoroka!”
“NI LAZIMA AKAMATWE!” Alisema mkuu wa jeshi la polisi na kuagiza simu
ipigwe haraka sana huko kongo ili zoezi la kumsaka bibi Nyanjige lisimamishwe
wanajeshi waliokuwa Kongo hawakuamini walichokisikia, walifikiri ni uongo.
“Kafika vipi Tanzania?” Alihoji kiongozi wao.
Viwanja vyote vya ndege, stesheni za reli, vituo vya mabasi, bandari vyote
viliwekwa chini ya ukaguzi mkali, iliagizwa mabasi yote yaliyosafiri
yasimamishwe na kukaguliwa bibi Nyanjige akitafutwa kwa udi na uvumba!
Msako mkali mno kila mahali wanajeshi waliingia mitaani na kusaidiana na polisi
kufanya msako wa nyumba hadi nyumba!
Watu walipigwa na vibibi vizee zaidi ya mia moja waliofanana kidogo na bibi
Nyanjige walitiwa mbaroni na kuhojiwa katika vituo mbalimbali vya polisi, vituo
vya televisheni na redio vilitangaza juu ya kuingia kwa bibi Nyanjige nchini na
picha yake ilionyeshwa, ili kurahisisha kukamatwa kwake zawadi ya shilingi
milioni hamsini ilitangazwa.
Msako ulikuwa mkali mno kila sehemu ya jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake,
magari yote yalisimamishwa na kukaguliwa, abiria wote katika stesheni ya reli
walikaguliwa na wanajeshi hamsini walipangwa kuondoka na treni siku hiyo na

Page 28 of 77
wengine ishirini kusafiri na meli ya kwenda Mtwara ikifikirika bibi Nyanjige
angeondoka na usafiri huo! Bibi Nyanjige alitafutwa kama Osama Bin Laden.
Mpaka wanafika kigamboni bibi Nyanjige hakuwa na habari kuwa maiti ilipelekwa
huko kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho peke yake! Akiwa huko aligundua
kuwa maiti ilikuwa isafirishwe kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi, taarifa
hizo ndizo zilimfanya abadilishe mawazo yake ya safari badala ya kwenda
Mwanza aliamua kwenda Moshi na magari ya msiba lengo lake likawa kwenda
kwenye mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti ambako angetulia na
kuaanzisha jeshi jingine jipya na wanyama.
“Tena huko kuna wanyama wengi zaidi ninafikiri jeshi langu safari hii litakuwa
kubwa sana kuna uwezekano hata wa kuwapata Tembo wengine kutoka Kenya
kwenye mbuga za Maasai Mara! Wasiponikamata katika muda wa wiki mbili
nitakuwa nimekwisha unda jeshi kubwa kuliko nililokuwa nalo Kongo!”Aliwaza
bibi Nyanjige.
Mpaka Chalinze basi lao lilishasimamishwa zaidi ya mara tatu kwenye vizuizi
barabarani lakini maaskari walipogundua kuwa lilibeba watu waliokuwa safarini
kwenda kwenye mazishi waliliachia liendelee na safari.
Bibi Nyanjige alifurahi kupita kiasi lakini wakati wanakaribia kuimaliza Chalinze
askari polisi na wanajeshi watano wakiwa na bunduki mikononi walisimama
katikati ya barabara na kulisimamisha gari lililobeba maiti pamoja na basi
lililobeba abiria, waliingia ndani ya basi na kuliacha gari lililobeba maiti! Moyo wa
bibi Nyanjige ulibadilisha kasi.
“Jamani sisi tunawahi mazishi hawa wote unaowaona humu ndani ni watu
tunaowapeleka mazishi huko Marangu Moshi!”
“Sawa lakini kuna mtu tunamtafuta ni lazima tukague mzee! Tumeagizwa hivyo na
mkuu wetu wa kazi!” Alisema mmoja wa maaskari.
“MAMA YANGU!” Bibi Nyanjige aliongea ndani ya khanga aliyojifunika
aliyasikia maongezi yote ya maaskari na dereva, mkojo ulitaka kumpenya kwa
woga na aliomba Mungu ili muujiza utokee wanajeshi hao wasipande ndani ya basi
lakini haikuwa hivyo walipanda na kusimama ndani ya basi.
“Jamani tunawaomba wote mtoe ushungi na vilemba vichwani mwenu ili nyuso
zenu zionekane wazi kuna mtu tunamtafuta samahani sana kwa usumbufu
utakaojitokeza, tusipompata mtaendelea na safari yenu!”

Page 29 of 77
“Mtu mwenyewe ni nani?” Aliuliza dereva.
“Bibi Nyanjige!” Alijibu mwanajeshi mmoja.
“Yule aliyeua watu mia na hamsini kwa sumu?”
“Ndiyo! Tena ni zaidi ya mia na hamsini kamaliza wanajeshi wetu wengi sana
huko Kongo!”
“Aisee! Lakini humu ndani hayumo mimi ningemwona!” Alisema dereva.
Bibi Nyanjige akiwa kiti cha nyuma alishindwa kufunua nguo yake kichwani,
machozi yalimtoka humohumo ndani ya khanga aliyojifunika, aligundua hapakuwa
na njia yoyote ile ya kujiokoa! Huo ndio ulikuwa mwisho wa safari yake ya
kukimbia!
Wanajeshi walizidi kumsogelea wakipita na kuangalia mtu mmoja baada ya
mwingine! Tena kwa uangalifu mkubwa kila mmoja wao akiwa na picha ndogo ya
bibi Nyanjige mkononi.
Bibi Nyanjige alizidi kutetemeka ndani ya Khanga aliyojifunika kichwani, alielewa
wazi hapakuwa na njia yoyote ya kujiokoa kutoka mikononi mwa wanajeshi
waliokuwa wakimsaka! Aliamini mwisho wa uhai wake ulikuwa umefika na
kilichokuwa kikimsubiri mbele yake hakikuwa kingine zaidi ya kamba shingoni,
alijua kwa mauaji aliyoyafanya ni lazima angenyongwa na kufa!
“Ehne! Wewe mama hebu jifunuee hicho kilemba chako!” Mwanajeshi mmoja
alimwambia mwanamke aliyekaa kiti kilichokuwa mbele ya kiti cha bibi Nyanjige
na aliyekuwa akifuata baada ya mama huyo alikuwa bibi Nyanjige mwenyewe!
Bila ubishi mama huyo alijifunua kilemba chake na kuuacha uso wake wazi,
hakufanana na mtu waliyekuwa wakimtafuta.
“Haya wewe mwanamke mwenye khanga kichwani hapo kwenye kona hebu ondoa
hiyo khanga yako!” Alisema askari huyo.
Pamoja na ushujaa wake bibi Nyanjige alisikia nguo zake za ndani zikilowana,
tayari mkojo ulishampenya! Alijadili kwa muda mrefu kuhusu kuitoa khanga
kichwani au la kwani alijua kufanya hivyo kungemfanya akamatwe! Na
kukamatwa kwake kungemaanisha kifo.
“Wee mwanamke husikii unajifanya kusinzia siyo?” Askari aliuliza kwa ukali.

Page 30 of 77
“Ah bwanae hebu tuachane nao hawa twende chini tukasubiri magari mengine!”
Askari mmoja alisema baada ya kuona taa za gari zikimulika kutoka kwa nyuma
yao na wote kwa pamoja waliteremka hadi chini kuliwahi gari lililokuwa likija.
Kitendo hicho cha askari kilimfanya bibi Nyanjige ashushe pumzi ndani ya khanga
aliyojifunika, hakuamini kama sakata hilo lilikuwa limekwisha! Kwa mara ya
kwanza katika maisha yake alijikuta akiamini kuwa Mungu husikia kilio cha
wenye shida.
“Hapo ndio nilishakufa!”
Dereva aliliondoa gari huku akilalamika kwa kupotezewa muda wake, walitumia
kama dakika thelathini eneo hilo moja! Hata watu wengine ndani ya basi
walisikika wakilalamikia kitendo hicho, bibi Nyanjige naye aliendelea kuhema
kwa nguvu ndani ya khanga yake, hakuwa tayari kujifunua kwa kuogopa
kugundulika kwani tayari kila mtu ndani ya basi hilo alikuwa na habari juu ya
kusakwa kwake.
“Maaskari wengine bwana yaani walitegemea bibi Nyanjige wampate humu? Yule
bibi ni hatari bwana, yule ni gaidi si mtu wa kukamatwa ovyoovyo! Badala ya
kumtafuta huko huko Kongo eti wanakuja kuweka kizuizi hapa Chalinze!
Wamechanganyikiwa nini?” Alifoka dereva wakati akiliondoa basi kwa kasi ili
kufidia muda uliopotea wakati wa kukaguliwa!
Dereva alikuwa na sababu ya kuondoka kwa kasi kwa sababu maagizo aliyopewa
na tajiri yake yalikuwa ni kuwahi kurudi Dar es Salaam ili kuja kuchukua watalii
kuwapeleka Mbuga za Mikumi, aliliendesha basi kwa kasi ambayo mara nyingi
huwa haitumiwi na magari yaliyobeba maiti.

*****
Macho ya binadamu hayana pazia! Ilikuwa si rahisi kwa watu wote waliokuwa
msibani Kigamboni kutomgundua bibi Nyanjige. Msichana mmoja alimwona bibi
Nyanjige na kumfananisha lakini hakuwa na uhakika sana na macho yake.
Aliporejea nyumbani baada ya gari kuondoka na maiti kuelekea Kilimanjaro,
aliliona tangazo katika luninga likitangaza msako wa bibi Nyanjige, kwa sura
aliyoiona hakuwa na sababu ya kutoyaamini macho yake tena! Alikuwa na uhakika
asilimia mia kuwa mtu aliyemwona msibani alikuwa bibi Nyanjige.

Page 31 of 77
Alipiga kelele kwa nguvu na kushangilia alijua zawadi iliyotolewa kwa mtu yeyote
ambaye angefanikisha kukamatwa kwa bibi Nyanjige ilikuwa yake.
“Baba nimemwona huyu bibi anayetangazwa msibani!”
“Wewe mtoto unaota au unataka kuchanganyikiwa?” Baba yake aliuliza.
“Sio hivyo baba ni kweli alikuwa msibani na tulitoka nae chumba cha maiti!”
“NI lazima utakuwa umefananisha!”
“Hapana baba nina uhakika asilimia mia moja, mimi siyo mtoto!”
“Alivaa nguo gani?”
“Alivaa gauni hilihili lenye rangi ya kijivu na nyekundu analoonekana nalo
kwenye televisheni ila lilikuwa mchafu kupita kiasi!” Alisema binti huyo
akilionyesha gauni pekee la bibi Nyanjige katika Luninga picha yake iligandishwa
ili watu wamwone vizuri.
“Huyu bibi ni mtu hatari popote atakapoonekana basi akamatwe na mtu
atakayewezesha kukamatwa kwake atapatiwa zawadi”Ilisema sehemu ya habari
hiyo.
“Baba tupige simu kwa polisi?” Binti alimweleza baba yake.
“Wewe mtoto una uhakika na unachokisema?”
“Ndiyo!”
“Sasa na hao polisi watampataje kama ameondoka na basi kwenda Kilimanjaro?”
“Wanaweza kulifuatilia basi alilopanda!”
Dakika mbili baadaye msichana huyo alikuwa kwenye simu akiongea na polisi juu
ya mahali alikokuwa bibi Nyanjige, hata polisi wenyewe walionekana kutoyaamini
maneno ya binti huyo.
“Binti una uhakika lakini? Usije kulisumbua jeshi la polisi bure?”
“Ni uhakika!”
“Kwa hiyo yupo wapi?”
“Ameondoka masaa matatu yaliyopita kupelekea maiti huko Marangu Moshi,
kama mtaweza kulifuatilia gari lililobeba maiti basi mtakuwa mmempata!”

Page 32 of 77
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Namba za basi walililopanda unaifahamu?”
“Ni TZO 8507!”
“Ok! Ahsante!” Alishukuru askari na kumuaga binti huyo akimpa uhakika kuwa
kama bibi Nyanjige angekamatwa huko alikosema basi yeye ndiye angepewa pesa
yote iliyoahidiwa kama zawadi, bila kupoteza hata sekunde mbili baada ya
kuongea na simu maaskari walinyanyua simu ya upepo na kuanza kuwasiliana na
maaskari waliokuwa maeneo ya Chalinze.
“Unanipata afande, ova!”
“Ndiyo ninakusoma, ova!”
“Yule bibi! Yule bibi! Yumo ndani ya basi dogo linalosafirisha maiti kwenda
Marangu, ova! Basi dogo lililobeba maiti!”
“Namba zake ni ngapi?”
“TZO 8507,hakikisheni mnamkamata, ova!”
“Mungu wang....!”Alisema askari wa upande wa Chalinze.
“Niniii? Kuna nini kwani?”
Askari aliyekuwa makao makuu hakupata jibu lolote kutoka upande wa pili, askari
aliyekuwa akiongea nae alihisi baridi kali ikipita katikati ya uti wake wa mgongo!
Mikono yake ilikufa ganzi na simu ya upepo ilianguka chini!
“Vipi?” Mwenzake aliyekuwa jirani alimuuliza hata yeye pia hakumpa jibu zaidi
ya kumwambia kuna matatizo yametokea.
Gari lenye namba zilizotajwa ndio lililokuwa limepita kama saa nzima kabla ya
simu hiyo ya upepo kupigwa!
Hawakuamini kama bibi Nyanjige alikuwa ndani ya basi hilo kwani waliwakagua
karibu watu wote ndani ya basi hilo isipokuwa mtu mmoja tu!
“Nafikiri aliyekuwa amejifunika khanga kwenye kiti cha mwisho kabisa nyuma ya
basi, niliyetaka kumwamsha halafu wewe ukasema tuachane alikuwa bibi Nyanjige
sasa tutafanya nini?”

Page 33 of 77
“Hakuna kingine isipokuwa kufuatilia mpaka tulipate basi hilo tumkamate na
kumrejesha Dar es Salaam vinginevyo tutaonekana wazembe na kusababisha
matatizo makubwa!”
Maaskari wote walikubaliana na kuingia ndani ya gari lao lililokuwa limeegeshwa
pembeni na kwa kasi ya ajabu walianza kuondoka kuelekea mbele hofu yao kubwa
ilikuwa kufukuzwa kazi na hiyo ndiyo iliwafanya wawe na usongo wa kulipata
basi hilo na kumkamata bibi nyanjige, walikuwa wamefanya uzembe mkubwa
ambao ungefanya wahusishwe na rushwa na kwa kosa hilo wangepoteza kazi zao.
“Hapana jamani mimi nahisi hiki kibibi ni kichawi, sasa pale kilitokea kitu gani
mpaka tusimfunue kilemba chake kichwani?”:
“Hata mimi sielewi lakini kwa spidi waliyokuwa nayo ni lazima tutawapata tu!”

Page 34 of 77
SURA YA SITA

BARABARA ya Chalinze Segera ni miongoni mwa barabara


zilizotengenezwa vizuri kupita zote nchini Tanzania! Ilikuwa ni barabara ya lami
na aliyeitengeneza lami hiyo alikuwa ni mtaalam kweli kweli kwani ilikuwa ni
mkeka wa nguvu! Magari yote yalipita katika barabara hiyo yalikimbia hadi
kilometa mia mbili kwa saa.
Baada ya basi kuondoka eneo lilipokamatiwa dereva aliliendesha kwa kasi ya
ajabu kiasi cha kuwatisha abiria, abiria wote walikuwa kimya roho zao zikiwa
mikononi ilikuwa si rahisi kuamini gari hiyo ilikuwa ikisafirisha maiti! Dereva
alipoangalia mshale wa kuonyesha kasi aligundua ulikuwa umegota mwisho!
Alishtuka lakini aliziamini tairi za gari lake zilikuwa na siku tatu tu tangu
ziwekwe!
“Kanyaga moto mwanangu!” Kondakta wake alimchochea!
“Usiwe na shaka babu hii ni nenda ugaruke mwanangu!” Aliitikia dereva.
Bibi Nyanjige alikuwa bado amejifunika na khanga yake kichwani, kasi hiyo
ilimshtua lakini hakuwa na la kufanya, aliendelea kumshukuru Mungu kwa
kumuokoa! Mara kwa mara alijitingisha kama vile alikuwa na kwikwi za kilio,
hakuongea kitu na mtu yeyote ndani ya basi, alijifanya mtu mwenye huzuni kupita
wengine wote!
Kilometa kama hamsini na tano mbele yao basi lao lilikuwa likipandisha mlima na
mbele yao lilikuwepo lori kubwa na tela lake lililokuwa likienda kwa mwendo wa
taratibu sana, dereva wa basi lao alikerwa na kasi hiyo ya lori na kuamua kulipita
kwa mwendo wa kasi.
Aliamua kufanya hivyo bila kujua kuwa mbele kulikuwa na lori jingine likija
tayari walikuwa wamefika darajani!
Akiwa katikati ya lori alilokuwa akilipita alishtukia akikutana uso kwa uso na lori
lililokuwa likija mbele yake, alijitahidi kukwepa na kugongwa mbavuni,basi lake
lilianza kuyumba kutoka upande mmoja wa barabara hadi mwingine akielekea
darajani.

Page 35 of 77
Abiria ndani ya gari walianza kupiga kelele, ikabidi bibi Nyanjige ajifunue na
kukuta watu wote ndani ya basi wakiwa wamesimama wima huku wakilia! Dereva
alionekana kuchanganyikiwa.
Ghafla mlipuko mkubwa ulisikika tairi lilikuwa limepasuka! Basi likatoka
barabarani na kuanza kuingia kwenye mtaro, mbele kidogo lilipinduka na
kutumbukia katika daraja refu ambalo chini yake ulipita mto mkubwa uliokauka
maji.
“Jamani ajali imetokea anayeweza kujiokoa afanye hivyo!” Ilikuwa ni sauti ya
dereva.
Dirisha la upande wake lilipasuka, pamoja na uzee aliokuwa nao bibi Nyanjige
alijivuta akatokeza nje na kusimama wima dirishani akiwa ameshika keria ya basi
kwa juu!
“Steringi hauwawi bwana!” Alisema bibi Nyanjige na kabla gari halijfika chini
alirukia upande wa pili na kutua kwenye nyasi, alihisi kiuno chake kuteguka.
Akiwa hapo alishuhudia basi likijibamiza chini na kuzunguka kama mara tatu hivi
ardhini, hakusikia tena kelele ndani ya basi ikawa kimya kabisa!
Hali iliyomfanya aamini kuwa watu wote ndani ya basi walikuwa wamekufa lakini
sekunde chache baadaye alishuhudia watu wawili wakitoka ndani ya basi huku
damu nyingi zikiwavuja, hawakuishi sana kwani walipotembea hatua chache
mbele walianguka chini.
Bibi Nyanjige alisogea hadi eneo walipoangukia na kugundua wote walikuwa
wamekufa! Alitembea kwenda mbele na kuchungulia ndani ya basi lililobondeka
aliona watu wengi wakiwa wamelala ndani ya basi damu nyingi zikiwatoka, maiti
nyingi hazikuwa na viungo muhimu kama vichwa, mikono na hata miguu!

Jeneza lililobebea maiti wakiondoka Dar es Salaam lilikuwa wazi na maiti haikuwa
ndani yake! Ilikuwa ni ajali mbaya kuliko ajali zote ambazo bibi Nyanjige aliwahi
kushuhudia maishani mwake!
Ghafla wazo lilimwijia kichwani mwake lilikuwa wazo la kujiokoa lilikuwa wazo
zuri kuliko mawazo yote aliyowahi kuyawaza!

Page 36 of 77
Alijua ni lazima ingegundulika alisafiri na basi lililosafirisha maiti, hivyo ili
kupoteza kabisa habari zake aliamua kuufanya ulimwengu wote uamini kuwa naye
alikufa katika ajali hiyo.
“Hakuna mtu atakayeamini nimeokoka katika ajali hii hivyo ni lazima niyafanye
mawazo yao yawe kweli!” Aliwaza bibi Nyanjige.
Alipita katika dirisha lililovunjika na kuingia ndani ya basi lililobondeka na
kuivuta moja ya maiti iliyoharibika vibaya haikuwa na kichwa kabisa, alikiona
kichwa cha maiti hiyo pembeni lakini hakukijali, aliubeba mwili na kutoka nao
hadi nje kupitia dirishani, alikuwa bibi kizee lakini mwenye nguvu za ajabu.
Alipoifikisha maiti hiyo nje aliilaza chini na kuruka tena hadi ndani ya basi
ambako alikichukua kichwa na kutoka nacho hadi nje! Ilikuwa ni kazi ya kutisha
lakini aliifanya bila hofu, mikono yake yote ilitapakaa damu kutoka shingoni mwa
kichwa alichokibeba na damu hiyo ilipenya katika vipele alivyokuwa navyo
mikononi mwake lakini hakujali.
Alikiweka kichwa hicho pembeni na bila kuchelewa aliamua kutekeleza mpango
aliokuwa nao, aliivua maiti hiyo nguo ilizovaa na kuzitupa pembeni kisha akavua
gauni lake na kubaki kama alivyozaliwa, kwa haraka aliivalisha maiti hiyo gauni
lake na pia mkufu wake wa shaba ulioandikwa jina lake! Alitaka kuidanganya
dunia kuwa hata yeye alikufa katika ajali hiyo ili aweze kuandaa jeshi zuri zaidi
porini.
Alipomaliza tu kazi ya kuivalisha maiti gauni lake alisikia muungurumo wa gari
nyuma na alipogeuza macho yake kuangalia barabarani aliliona gari la polisi na
maaskari wapatao watatu waliteremka ndani ya gari hilo huku bunduki zikiwa
mikononi mwao.
Alijua wazi watu hao walikuwa wakimtafuta yeye hakuna kilichokuwa mbele yake
zaidi ya kujiokoa tena, ili kutimia lengo lake alikichukua kichwa cha marehemu na
kuanza kukimbia nacho mbio kuelekea vichakani.
“Jamani yule anayekimbia ni mtu au nyani?”
“Mtu yule!”
“Hapana labda ni nyani sidhani kama kuna binadamu mweusi kiasi kile hapa
duniani!” Alijibu mmoja wa maaskari.

Page 37 of 77
Kabla hata hawajalifikia basi walikutana na maiti moja na mmoja wao maaskari
alibaki akiimulika maiti hiyo na tochi, wenzake walinyoosha moja kwa moja hadi
mahali lilipokuwa basi hilo, walipomulika ndani walishuhudia maiti nyingi zikiwa
zimelaliana, hapakuwa na mtu aliyeonekana kuwa hai, maiti nyingi zilikuwa
zimekatikatika vibaya!
“Masikini hii ina maana hata bibi Nyanjige atakuwa amekufa au?”
“Ni lazima itakuwa hivyo!” Maaskari waliokuwa wakilikagua gari waliongea na
ghafla walisikia mwenzao akipiga kelele.
“Huyu hapa?”
“Nani?”
“Bibi Nyanjige!”
Waliokuwa ndani ya basi walitoka ndani ya basi mbio na kurudi hadi mahali
mwenzao alipokuwa akipiga kelele, hawakuamini macho yao kuukuta mwili
uliovaa gauni la bibi Nyanjige ukiwa hauna kichwa!
“Kichwa chake kiko wapi? Ni lazima tuupeleke pamoja na kichwa vinginevyo
hakuna mtu atakayeamini kuwa huyu ni bibi Nyanjige!”
“Lakini ni afadhali amekufa ametuhangaisha sana!”
“Huyu bibi alikuwa hatari mno!”
Walijaribu kukitafuta kichwa cha marehemu bila mafanikio mwisho wakaamua
kupiga simu ya upepo Chalinze kuomba msaada na dakika kama ishirini baadaye
gari kubwa la polisi liliwasili na kupakia maiti zote zilizokuwa ndani ya basi hilo
na kuondoka nazo.
“Na hiyo?” Aliuliza mmoja wa askari waliokuwa wakipakia maiti.
“Hii hapana! Tunakwenda nayo Dar es Salaam makao makuu ni lazima tuipelekea
hospitali kuu ya Jeshi ili wakubwa waione tena usiku wa leo hii hii! Maana huyu
bibi aliisumbua sana dunia!”
“Sasa wataamimi vipi bila kichwa?”
“Alama zote zipo, hii cheni yake imeandikwa jina lake si unaona!” Alisema askari
mmoja na akamwonyesha askari mkufu ulioandikwa neno Nyanjige walioukuta
shingoni mwa maiti!

Page 38 of 77
“Na hata hizi nguo alizovaa ndio zake kabisa!” Alisema askari huyo.
Magari yote yaliondoka moja likiwa kimbeba maiti zote kuelekea hospitali ya
Tumbi na gari jingine la polisi likiwa limebeba maiti moja lilielekea Dar es
Salaam! Gari hilo la polisi halikusimama Chalinze lilinyoosha moja kwa moja
kuelekea jijini Dar es Salaam ambako lilifika baada ya kama dakika arobaini na
tano!
Maiti ilipelekwa moja kwa moja hadi chumba cha maiti cha hospitali ya jeshi
ambako usiku huohuo wakuu wa jeshi walifika na kuanza kuikagua maiti hiyo.
“Jamani mna uhakika huyu mliyemleta ni bibi Nyanjige kweli?”
“Ni yeye afande si mnaona hata huu mkufu wake afande!!” “Hebu niuone!”
Afande Mwita Mitiro aliuomba mkufu huo, alipokabidhiwa alianza kuukagua,
alipoliona jina la Nyanjige kwenye mkufu huo hata yeye aliamini ulikuwa ni mwili
wa bibi Nyanjige.
“Kweli bwana si unaona hata gauni ndilo lilelile lililopo katika hii picha!” Alisema
mkuu huyo huku akiimulika picha aliyoshika mkononi mwake kwa tochi.
“Hebu ivueni hiyo maiti hizo nguo ili tuikague zaidi!”
Bila kuchelewa vijana waliikamata maiti hiyo na kuivua nguo zote ilizovaa hakuna
aliyekuwa tayari kuamini macho yake walipokuta mwili maiti hiyo una sehemu
nyeti za kiume! Waligundua bibi Nyanjige aliwachezea tena mchezo.
“Ni akina nani walioileta maiti hii?”
“Ni sisi afande!”
“Yaani mmetuletea maiti ya mwanaume?” Aliuliza afande kwa ukali.
“Hatukujua afande!”
“Hebu wawekeni mahabusu hawa haraka na msako ni lazima uendelee!
Bibi Nyanjige atakuwa hai amefanya tena ujanja wake wa kuvalisha nguo maiti,
nataka akamatwe mara moja na kuletwa hapa!” Askari mia mbili waondoke kwa
magari na helkopta tano zifuate usiku huu huu kwenda kuuzunguka msitu wote
ulio jirani na mahali ajali ilipotokea nina uhakika atakuwa maeneo hayo hayo!
Mpaka kesho saa sita kamili namtaka awe hapa akiwa hai mmesikia?” Aliuliza
mkuu wa majeshi hasira zikiwa zimempanda.

Page 39 of 77
“Ndiyo afande!”
Kipenga kilipulizwa wanajeshi wote wakakusanyika na dakika kama ishirini
baadaye mkuu wa majeshi alishuhudia helkopta na magari yakiondoka kwa kasi,
kila askari alikuwa na bunduki yake mkononi!
Hofu kubwa ya wanajeshi ilikuwa ni wadudu na nzige ambao bibi Nyanjige
aliwatumia, ingawa alikuwa nchini Tanzania ambako hapakuwa na nzige wala
mbung’o bado wanajeshi waliogopa vita vya wadudu!
Saa tisa ya usiku bibi Nyanjige akikimbia uchi wa mnyama katikati ya pori
kuelekea asikokujua, alishangaa kuona helkopta tatu zikitokea juu yake “Mungu
wangu wamekuja tena?”
Bibi Nyanjige aliziona helkopta za jeshi zikielekea upande wake bila shaka alijua
zilikuwa zikimfuata yeye!
“Hawaniwezi na nitawamaliza mpaka wajute kwanini walimuua mama
yangu!”Aliwaza bibi Nyanjige.
Alikitupa kichwa cha mtu alichokuwa nacho na kuinama akaweka mikono yake
chini akaanza kutembea kama Sokwe kwa miaka mingi aliyoishi porini na
wanyama alijua muondoko wa kila mnyama! Ilikuwa si rahisi kumtofautisha na
Sokwe halisi.
Alizidi kutokomea katikati ya vichaka huku helkopta zikimmulika kwa mwanga
mkali wa taa uliofanya usiku porini kuonekana kama mchana, mwanga huo ulimtia
hofu na kumfanya aamue kujiangusha ardhini na kunyooka wima kama mti.
Marubani walipomulika na taa zao walimwona kama kipande cha mti
kilichounguzwa na moto! Ilikuwa si rahisi hata kidogo kuamini walichokiona
ardhini kilikuwa binadamu! “Najipumzisha ila hali ikitulia nitaendelea!” Aliwaza
bibi Nyanjige.
Alibaki amelala eneo hilo kwa muda wa masaa zaidi ya mawili, hali ilipotulia
alinyanyuka na kuanza kutembea taratibu akisonga mbele kwenda mahali
kusikojulikana, lengo lake likiwa kufika Serengeti.
Alitembea kwa usiku mzima bila kufika au kutokezea barabarani,kulipokucha
alishindwa kuendelea na safari yake kwa kuhofia kukamatwa na kuamua kujificha
chini ya kichaka akisubiri usiku mwingine uingie ndio aendelee.

Page 40 of 77
“Nitatembea kila siku usiku kama Bundi na asubuhi nitajificha vichakani hadi
nifike ninakokwenda, ninajua ninasakwa sana lakini hawatanikamata hata siku
moja!” Bibi Nyanjige aliongea peke yake huku akitetemeka kwa baridi ndani ya
kichaka alichojificha.
Alikuwa bado hajakata tamaa na hakutaka kufanya hivyo, alikuwa na matumaini
ya kujinasua kutoka mikononi mwa kifo kilichokuwa kimemzunguka! Usiku
ulipoingia alitoka kichakani na kuendelea na safari yake, hiyo ndiyo ikawa staili
yake ya safari!
Kwa siku kama tatu alitembea usiku na mchana alijificha kichakani.Njaa
haikumsumbua sana kwani alishazoea maisha ya porini, alikula matunda na majani
ya miti.
Ilikuwa ni siku ya nne akiwa amejificha kichakani miguu yake ikiwa imevimba
kama matende kwa sababu ya safari, mwili wote ulikuwa umechoka na alikuwa
akijaribu kuwaza angefanya nini ili aendelee na safari yake hadi Serengeti ambako
alitaka kwenda kuunda jeshi kama alilokuwa nalo Kongo ili kupambana na majeshi
ya serikali.

Page 41 of 77
SURA YA SABA

AKIWA katika mawazo hayo ghafla alisikia sauti za watu nyuma ya kichaka
alichojificha! Zilikuwa ni sauti za wanaume wakitembea kuelekea eneo alilokuwa,
alipenyeza macho yake katika majani ya kichaka na kuangalia nje! Aliliona kundi
kubwa la askari waliovaa magwanda ya kijeshi wote walikuwa na bunduki
mikononi mwao alitetemeka akijua tayari alishaingia mikononi mwa wabaya wake.
“Na hizi alama za miguu ni za nani?” Aliuliza mmoja wa askari huku akiangalia
ardhini.
Swali hilo lilimfanya bibi Nyanjige afe ganzi mwili mzima na kuona mwisho wake
ulikuwa umefika, meno yake yaligongana ovyo,alijua ni nyayo zake
zilizoongelewa na maaskari walizigundua sababu ya mvua kubwa iliyonyesha siku
moja kabla.
“Bwana achana na nyayo za wachungaji wa Kimasai tuendelee na msako na siku
nitakayomtia mkononi huyo bibi yenu atanikoma sababu kanisumbua sana!”
Alisema mmoja wa maaskari hao na kupiga risasi kama tatu hivi hewani ili
kuonyesha hasira aliyokuwa nayo dhidi ya bibi Nyanjige.
“Wee acha tu watu tumeacha wake zetu kuja kuhangaika hapa porini na baridi
sababu ya kibibi kijingajinga!” Mwingine alidakia
Lilikuwa kundi la maaskari wengi mno na walizidi kupita pembeni ya kichaka
taratibu hakuna askari hata mmoja aliyefikiria kuchungulia ndani ya kichaka hicho
kuona kilichokuwemo Bibi alizidi kutetemeka kwa hofu.
“Sitakiwi kulaza damu hata kidogo lazima nijiokoe hata nikifa kazi niliyoifanya ni
kubwa!” Aliwaza Bibi Nyanjige na sekunde chache baadaye alipata wazo alitaka
kuitumia nafasi hiyo ya kupita maaskari kuokoa maisha yake, alitaka kumwiiga
Sylivester Stallone Rambo katika sinema zake.
“Nafikiri na mimi nikitumia utaalam ule ule nitamnasa mmoja!” Aliwaza bibi
Nyanjige na kusimama wima akiupima mwili wake nguvu.
“Niko bombaaa!” Alijitapa na kuamua kujaribu kutumia nafasi hiyo

Page 42 of 77
Aliangaza macho yake pembeni na kuona mzizi mkubwa wa mti ukiwa chini,
akajinyoosha na kwa kutumia nguvu nyingi aliukata na kuushika mkononi,
ulikuwa mgumu na ulifanana kabisa na kamba.
Alipatwa na ujasiri wa ajabu na kujisogeza hadi pembeni kabisa mwa kichaka
alichojificha na kuwashuhudia maaskari wakizidi kupita taratibu bunduki zao
zikiwa mkononi, hakuwa na shida nao wote alimtaka mmoja tu! Alitulia akisubiri
wa mwisho apite huyo ndiye alikuwa mlengwa.
Wengi walipita akamuona mmoja wao ambaye aliamini alikuwa wa mwisho akija
taratibu, yeye alibeba mtambo mkubwa zaidi ya wenzake uliomuelemea kwa uzito!
Alitembea peke yake akionekana kuchoka kupita kiasi na alikuwa legelege na
mwenye afya mbovu.
“Huyu huyu ananitosha!” Aliwaza bibi Nyanjige huku akiweka mzizi wake vizuri,
askari alipofika karibu yake bibi Nyanjige aliruka kwa kasi na kuuzungusha mzizi
aliokuwa nao shingoni mwa askari kama ambavyo vibaka hufanya wanapomkaba
mtu.
Mwanajeshi hakupiga kelele hata kidogo bali alianguka chini kimyakimya,macho
yalimtoka vibaya askari, bibi Nyanjige naye akazidi kubana kwa mzizi kwa dakika
kama mbili huku akiwaangalia wanajeshi wenzake waliozidi kutokomea bila kujua
yaliyompata mwenzao! Bibi Nyanjige alijipongeza kwa kazi aliyoifanya.
Kwa haraka alimvutia askari huyo na kumwingiza ndani ya kichaka ambako
alimbana zaidi na mzizi hadi akafa!
“Sasa mambo yameanza upya!” Alisema bibi huku akimvua askari huyo
magwanda yake na kuyavaa mwilini mwake! Ingawa yalimbana sana
aliyalazimisha. Kofia ya jeshi aliyovaa askari huyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba
bibi Nyanjige alipoiweka kichwani ilimfunika uso wake wote, haikuwa rahisi hata
kidogo kumtambua.
Baada ya kumaliza kuvaa mabuti ya jeshi aliuchukua mtambo aliokuwa nao askari
huyo na kuubeba begani mwake, kwa utaalam wa kijeshi aliojifunza akiwa
masomoni huko Uingereza ambako ilikuwa lazima kwa wanafunzi wa chuo kikuu
kupata mafunzo ya jeshi aligundua mtambo huo ulikuwa ni wakutungulia ndege.
“Sasa watanitambua na nina uhakika kwa nilivyovaa hakuna hata askari mmoja
atakayegundua kuwa mimi ndiye bibi Nyanjige wanayehangaika kumsaka! Na kwa

Page 43 of 77
kutumia mtambo huu leo hii nafanya kazi ambayo dunia haijawahi kushuhudia!”
Aliwaza bibi Nyanjige akiwa amebeba mtambo wake begani!
Ulikuwa mtambo mzito kiasi cha kumyumbisha ukizingatia umri wake kuwa
mkubwa, lakini mazoezi ya mwili aliyoyafanya akiwa kijana na aina za vyakula
alivyokula vilimfanya awe imara hata kuwa na uwezo wa kubeba mtambo mzito
kama ule.
Ghafla alishuhudia helkopta mbili zikija angani nyuma yake badala ya kusikitika
kama ilivyokuwa awali alifurahia! Alilala chini na kuuelekeza mtambo angani
akiwa ameilenga vilivyo moja ya helkopta bila kusita aliachia kombora moja zito
lililokwenda moja kwa moja na kuilipua ndege,bibi Nyanjige alichekelea.
Kabla helkopta ya pili haijafika mbali nayo ilipokea kombora jingine na kuanza
kuwaka moto ikielekea ardhini!
“Wamefanya kosa sana kunipa mtambo huu hii ni sawa na kumpa mwehu rungu!
Sasa na hakikisha kila ndege inayopita hapa inapokea kipigo na kulipuka leo ni
le…….!” Kabla hajamalizia sentensi yake alisikia muungurumo mwingine tena
upande wa Mashariki, furaha nyingine tena ilimjaa moyoni na kuunyanyua
mtambo wake na kuitungua helkopta hiyo ilidondoka chini mara moja huku
ikiwaka moto na alifanya hivyo hivyo kwa ndege ya pili pia!
Matukio hayo yalimshangaza karibu kila mtu aliyekuwepo porini, walishindwa
kuelewa ni nani aliyefanya ukatili huo kwani ni ndiyo waliokuwa na mtambo wa
kulipulia ndege katika pori hilo jambo lililoonyesha kuwa mtu aliyekuwa
akizilipua ndege hizo alikuwa mwanajeshi mwenzao, lakini nani? Hilo ndilo
lilibaki swali la kila mmoja wao ikabidi mkuu wa kikosi apige kipenga ili
wanajeshi wote wakusanyike kuhesabiwa.
Bibi Nyanjige aliposikia mlio wa kipenga ha jeshi alijua mambo yameharibika!
Alichukua mtambo wake na kwenda kuuficha porini mahali alipofahamu yeye
mwenyewe alirudi haraka na kujichanganya ndani ya kundi la askari mia mbili bila
kugundulika! Mpaka wakati huo hapakuwa na askari mmoja wa jeshi la nchi kavu
aliyekuwa ameuawa!
“Jamani nani amekabidhiwa mtambo wa kutungulia ndege?”
“Ni afande Laurian!”
“Yupo wapi sasa?”

Page 44 of 77
‘Hatujui afande ila alikuwa anakuja kwa nyuma!”
“Na mtambo wenyewe upo wapi?”
“Alikuwa nao, ila sababu ya uzito wake alitembea taratibu nyuma yetu!”
“Mmekwishajaribu kumtafuta?”
Hakuna mtu aliyejibu swali hilo askari wote walianza kuzungusha macho yao huku
na kule wakimwangalia askari huyo bila mafanikio yoyote.
“Haya hesabuni nambaaaa!” Kamanda wa kikosi aliamuru na maaskari wote
walianza kuhesabu namba zao taratibu wakianzia na moja hadi kufikia mia mbili!
Hesabu ilitimia.
“Jamani mbona hesabu yetu imetimia yupo wapi Laurian?” Aliuliza mkuu wa
kikosi na kuamuru askari wahesabu tena namba zao taratibu lakini bado hesabu
ilikuja ile ile na kumshangaza Kamanda.
“Laurian! Laurian!” Kamanda aliita lakini bado hakuitikiwa na mtu yeyote, kila
askari alishangaa na walishindwa kuelewa kitu gani kilikuwa kimetokea kwani
kama askari huyo asingekuwepo ni lazima idadi ya askari ingepungua mtu mmoja.
“Haya wote kaeni katika mstari ili nikague lakini kama nikimpata huyo Laurian
adhabu yake itakuwa kifo hawezi kunihangaisha kiasi hiki!” Alisema kamanda na
wanajeshi wote walijipanga tena mstari na Kamanda alianza kupita taratibu
akiwakagua mmoja baada ya mwingine juu hadi chini kama vile ambayo mwalimu
mkuu hufanya shuleni anapokagua usafi!
Bibi Nyanjige alikuwa amesimama katika mstari wa nyuma akitetemeka kwa hofu,
alijua tayari alishaingia matatizoni alikuwa na uhakika wa kugundulika kwa
sababu angejulikana ni mwanamke na kugundulika kwake kungemaanisha ni yeye
aliyekuwa akizilipua helkopta.
“Afande simama wima mbona umejikunja hapa mgongoni? Na huo mguu sawa
ulioweka si wenyewe panga vizuri miguu yako hunioni mimi? Huyu kamanda
anaweza kukuletea matatizo makubwa sana sababu amekasirika!”
Askari mmoja aliyekuwa jirani alimwambia bibi Nyanjige lakini alipojaribu
kujinyoosha mgongo ilishindikana kwa sababu mgongo wake ulipindwa na uzee!

Page 45 of 77
“Nyooooka kidogo afande huu mgongo utakuletea matatizo!” Alisema tena askari
huyo lakini Bibi Nyanjige hakujibu kitu alijua kufanya hivyo kungefanya
agundulike na kuhatarisha maisha yake alizidi kuinamisha kichwa chake chini.
“Hebu toeni kofia zenu kichwani upesi ili niwaone vizuri!”Kamanda aliamuru na
kwa sababu ilikuwa ni amri hapakuwa na njia yoyote ile ya kubisha, askari wote
walianza kutoa kofia zao vichwani na mkuu wa kikosi alipita kwa askari mmoja
baada ya mwingine.
Macho ya askari aliyesimama jirani na bibi Nyanjige yalimfuata kamanda kila
alikopita akikagua na kumsahau kabisa bibi Nyanjige, alipogeuza kichwa chake
dakika chache baadaye alishangaa kukuta askari mwenzake hayupo! Hakutaka
kuuliza sababu Kamanda alikuwa amekaribia sana eneo hilo, alizidi kukauka ili
kuonyesha heshima ya jeshi.
“Mbona idadi imebaki ileile 199! Kuna askari amepotea na huyo ndiye anatungua
ndege zetu wenyewe, sijui anatumiwa? Ni lazima asakwe” Alisema kamanda.

*****
Bibi Nyanjige alikuwa katikati ya vichaka akitembea kuelekea mahali alipouacha
mtambo wake wa kulipulia ndege alipokuta bado upo alifurahi kupita kiasi na nusu
saa baadaye akiwa bado katikati ya nyasi alianza kuona maaskari wakipita
kuelekea mahali walikotokea.
Aliiona hiyo kama bahati nyingine kubwa zaidi alinyata taratibu na kujichanganya
katikati maaskari bila kugundulika na kuanza kutembea pamoja nao, hakuna
aliyeligundua jambo hilo! Umbali wa kilometa kama kumi na tano katikati ya pori
walifika kambini na wanajeshi walijipumisha ndani ya mahema waliyojenga.
Usiku huo kwa bibi Nyanjige hakutaka uwe usiku wa bure, alitaka kuutumia kwa
kazi katika zungukazunguka yake bila kutiliwa mashaka alifanikiwa kufika mahali
yalipofichwa mabomu na silaha nyingine za kijeshi, alianza kusomba mabomu
taratibu na kuyatega sehemu mbalimbali za kambi bila kugundulika, aliyaseti yote
yalipuke baada ya masaa mawili.
“Hii ndiyo kiboko yao lazima niwamalize hawa watu, nataka siku moja niingie
katika kitabu cha orodha ya watu maarufu duniani na huu ni wakati wa mimi
kuondoka niwaachie kasheshe yao” Alisema bibi Nyanjige huku akitabasamu.

Page 46 of 77
Aliondoka kama anakwenda kukojoa na kutokomea porini akijua baada ya masaa
mawili kambi lingegeuka tanuru la moto na mamia ya wanajeshi wangegeuka
mkaa au matofali ya kuchoma.
Masaa mawili kama alivyopanga akiwa katikati ya pori aliona moto mkubwa
ukiwaka nyuma yake! Akajua tayari kazi yake imekamilika.

*****
Maaskari walizinduliwa na milipuko ya mabomu na kuanza kukimbia huku na kule
wakijaribu kuokoa maisha yao! Haikuwa rahisi hata kidogo kwani wengi
walilipuliwa na kuwaka kwa moto! Mahema yaliwaka kwa moto na wengi wa
wapiganaji walikufa ndani ya mahema yao!
Mpaka hali inatulia masaa matatu baadaye tayari wanajeshi 150 walikuwa chini
wakiwa maiti! Kamanda alinusurika na alizidi kusikitika na kushindwa kuelewa ni
kitu gani kilikuwa kikiendelea alianza kuhisi kulikuwa na vibaraka wa bibi
Nyanjige kati yao, hakufikiri hata kidogo kuwa bibi Nyanjige ndiye aliyeifanya
kazi hiyo kama kikulacho ki nguoni mwako.

******
Kulipokucha asubuhi bibi Nyanjige alikuwa katika kijiji cha Kiambali mkoani
Tanga, kijiji hiki kilikaliwa na watu wa jamii ya Kimasai peke yao! Kwa
magwanda aliyokuwa nayo alijua ni lazima angewatia wasiwasi na wangetaka
kumwona sura yake jambo ambalo kwa hakika lingesumbua.
Hakutaka kujitokeza mchana alichofanya ni kujificha kichakani mchaka kutwa,
usiku ulipoingia aliyavua magwanda yake na kuanza kutembea taratibu kuingia
kijijini.
Mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa mlevi akitoka kilabuni, mtu huyo alishtuka
sana kuona mwanamke yu uchi.
“We iko nani?”
“Mimi?” “Ndiyo!”

Page 47 of 77
“Bibi Nyanj….!” Alitaka kutaja jina lake lakini alipokumbuka kuwa alikuwa
akitafutwa na tayari jina lake lilikuwa maarufu midomoni mwa Watanzania alisita
kulimalizia.
“Uuuuuuuuuuwiiiiiiii, saidia, jamani saidia! Mchawi! Mchawi huyu hapa!” Alipiga
kelele mzee huyo, alikuwa ndiye mwenye nyumba zilizokuwa jirani na eneo hilo
aliendelea kupiga kelele kwa muda mrefu hatimaye watu wengi walijitokeza
wakiwa na silaha zao mikononi, wengine mapanga, mikuki na mawe..
Wananchi wa kijiji hicho walichukia wachawi hivyo walianza kumshambulia bibi
Nyanjige kwa mawe na marungu na wengine walimrushia hata mikuki yao,
alianguka chini huku akilia.
“Jamani mie siyo mchawi!” Alisema lakini hakuna aliyemsikiliza watu walizidi
kumshambulia kila mtu akiamini bibi Nyanjige alikuwa mwanga!

Page 48 of 77
SURA YA NANE

JESHI lilishituliwa sana na vifo vya wanajeshi wake msituni viongozi


hawakuelewa ni nani aliyezitungua ndege zao kiasi hicho ingawa waliamini
mtambo uliotumika kuzitungua ulikuwa wao.
Walioshindwa kuelewa bibi Nyanjige aliwezaje kuwashawishi wapiganaji wao
mpaka wakafikia uamuzi wa kulisaliti jeshi lao! Siku zote waliamini wapiganaji
wao walikuwa waaminifu kupita kiasi.
Hakuna mtu hata mmoja aliyehisi bibi Nyanjige ndiye alifanya ukatili huo baada
ya kuingia katika jeshi lao bila kugundulika.
Msako mwingine mkali zaidi uliitishwa wanajeshi zaidi ya elfu sita walitumwa
kwenda kuuvamia tena msitu kumsaka bibi Nyanjige, bado waliamini alikuwemo
msituni! Ni maaskari katika msako wa mara ya pili walioigundua maiti ya askari
waliyehisi alizitungua ndege zao ukiwa ndani ya kichaka!
Kilichopelekea maiti hiyo igundulike ni harufu kali iliyosikika wakati wakipita
pembeni mwa kichaka, walipoingia ndani walikuta maiti ya mpiganaji mwenzao
ikiwa imelala bila magwanda zaidi ya chupi! Gauni chafu lilikuwa pembeni.
Walipoliangalia gauni hilo waliligundua kwa haraka kuwa lilikuwa la bibi
Nyanjige! Wote walielewa kilichotokea waligundua ni bibi Nyanjige aliyezitungua
ndege zao na ni yeye aliyetega mabomu na kuwaangamiza maaskari wenzao!
Hasira zilizidi kuwapanda wanajeshi na kila mtu alipania kumpata bibi huyo.
“Lazima apatikane!”
Gauni la bibi Nyanjige lilipopelekwa makao makuu ya jeshi, wakubwa
walishindwa kuelewa ni uwezo gani aliokuwa nao bibi huyo kizee hadi asumbue
jeshi kiasi hicho! “Alikuwa na nguvu gani mpaka kumuua askari wetu kisha
kumvua nguo, nafikiri magwanda yake ya askari aliyavaa mwenyewe ndio akaanza
kutungua ndege zetu?” Aliuliza mkuu wa majeshi!
“Nafikiri ni hivyo sijui hivi sasa atakuwa wapi?” Msaidizi wake Brigedia Mwita
alijibu
“Hakuna sehemu yoyote anayoweza kuwa amekimbilia zaidi ya humohumo porini!
Hivyo hakikisheni pori lote linazingirwa ili asipate mahali pa kutokea! Na

Page 49 of 77
mkimpata naomba maiti yake iletwe hapa makao makuu, tunahitaji kuikausha ili
iwekwe makumbusho kwa ajili ya historia ya nchi yetu kwani mpaka sasa siamini
kama kuna bibi kizee anayeweza kufanya maajabu kiasi hiki……!” Mkuu wa
majeshi alimwambia msaidizi wake na kabla hajamaliza simu yake ililia.
“Hallow, nani anaongea?” Aliuliza.
“Ni mimi Brigedia Bukuku!” Alijibu Brigedia aliyekuwa akiongoza msako
msituni.
“Ndiyo Brigedia mnaendeleaje?”
“Tunaendelea vizuri nilitaka tu kukutaarifu kuwa tayari ule mtambo wa kutungulia
ndege tumeupata ulikuwa umefichwa kichakani kabisa!”
“Vizuri, endeleeni na kazi mpaka mmkamate huyo bibi kizee, yupo hapohapo
porini!”
“Sawa afande!”

*****
Habari za msako wa bibi Nyanjige zilishaenea kila mahali mjini na vijijini,
hapakuwa na mtu asiyefahamu juu ya bibi huyo! Hata katika kijiji cha Wamasai
cha Kiambali ambako bibi Nyanjige aliendelea kusambuliwa kwa mawe
akidhaniwa mchawi, kijana mmoja aliikumbuka sura yake na kupiga kelele
akiwaomba wenzake wasitishe zoezi la kumpiga.
“Nimemkumbuka huyu bibi!” Alisema kijana huyo kwa Kimasai.
“Ni nani?”
“Ni bibi Nyanjige!”
“Mama yangu nimekwisha!”Bibi Nyanjige alijisemea moyoni akiwa amelala chini
damu nyingi zikimtoka katika majeraha aliyoyapata sababu ya kipigo kibaya
alichopewa na wananchi wenye hasira, alijua kutambuliwa kulimaanisha kifo!
Alijua tayari alishaingia mkononi mwa wanajeshi na kwa zawadi iliyokuwa
imetolewa na serikali hapakuwa na njia ya kuwshawishi Wamasai wamwachie.
“Bibi Nyanjige ndiye nani?”
“Si anayetafutwa kwa mauaji!”
Page 50 of 77
“Una hakika ndiye huyu?”
“Ni yeye!” Kijana huyo aliendelea kusisitiza.
“Sasa tufanye kitu gani?”
“Mimi naomba tuchague morani watatu ili twende kupeleka taarifa hizi makao
makuu ya jeshi waje wamchukue!” Alisema kijana huyo na maneno hayo
yalimfikia bibi Nyanjige moja kwa moja, aliomba wazee wa Kimasai wamkatalie
kijana huyo lakini haikuwa hivyo, wazee wote walikubaliana na jambo hilo.
Usiku huohuo kwa kutumia baiskeli morani watatu waliondoka kuendesha baiskeli
zao hadi mjini Korogwe ambako waliziacha kwa marafiki na kupanda mabasi
kuelekea Dar es Salaam.
Waliingia jijini saa moja asubuhi na kufika makao makuu ya jeshi saa mbili na
nusu ambako baada ya kujieleza kuwa walikuwa na taarifa za mahali bibi Nyanjige
alikokuwa walipokelewa vizuri na kuonana na mkuu wa jeshi kama walivyoomba.
“Yule bibi tunaye!” Ndivyo walivyosema baada ya salamu zao kwa mkuu wa
majeshi msaidizi aliyewapokea kabla hawajaenda kuonana na mkuu wa majeshi
mwenyewe!
“Bibi gani?” Aliuliza mkuu wa majeshi msaidizi.
“Bibi Nyanjige!”
“Nyanjige?” Aliendelea kuuliza kwa mshangao.
“Ndiyo!”
“Mnae nyinyi? Mmempataje wakati kahangaisha jeshi kiasi kikubwa?”
“Kweli tunaye kama huamini tupatie vijana wako twende nao hadi kijijini kwetu
lakini zawadi itakuwa yetu sisi!” Alisema mmoja wa Morani.
“Hilo si tatizo ili mradi tu awepo kwa sababu mkitusumbua hatutafurahi!”
“Wewe tupe tu vijana na gari twende nao!”
“Si vijana bali mimi mwenyewe nitaondoka nanyi!”
“Tena wewe ndiyo vizuri zaidi!”

Page 51 of 77
“Haya hebu nisubirini kwanza nije!” Alisema mkuu huyo wa majeshi na kutoka
nje ya ofisi na kwenda moja kwa moja kwa mkuu wa majeshi na kumweleza habari
za vijana wa Kimasai walioingia ofisini kwake.
Mkuu wa majeshi hakuiamini habari hiyo aliuona kama uongo fulani na kuomba
awaone vijana wa Kimasai walioleta taarifa, mkuu wa majeshi msaidizi alitoka
kwenda kuwachukua na kuwapeleka ofisi ya bosi wake.
Mkuu wa majeshi alipowauliza vijana hao maswali majibu yao yaliendeela kuwa
yaleyale na walijibu kwa uhakika zaidi, jambo lililowafanya wakuu wa majeshi
waamini kila kitu!Hapakuwa na ubishi wala kusita tena bali mkuu wa majeshi
alimwamuru msaidizi wake pamoja na wanajeshi wengine waongozane na vijana
wa Kimasai kwenda kijijini kuona kama kweli bibi waliyedai kuwa nae alikuwa
bibi Nyanjige!
Magari matatu yakiwa na askari wapatao sitini yaliondoka makao makuu ya jeshi
kwenda kijiji cha Kiambali, kwa sababu walimfahamu bibi Nyanjige na maajabu
yake waliondoka na silaha za kutosha, kila mwanajeshi akiwa na bunduki yake na
pia mabomu.
“Kama ni yeye basi mkamlete akiwa hai!”
“Sawa mkuu!”

*****
Kutoka jijini Dar es Salaam hadi kijiji cha Kiambali kupitia Kibaha, Chalinze
ulikuwa ni mwendo wa masaa manne waliingia kijijini hapo majira ya saa nane
mchana! Wote walishangazwa na hali waliyoikuta, ng’ombe waliokuwa
wakikimbia huku na kule mikia ikiwa imenyooka, walionekana kama wamepatwa
na kichaa mamia ya watu walikuwa wamelala ardhini wakivuja damu na wengine
walikuwa wakichomwa kwa pembe za ng’ombe ardhini, wengi walikuwa
wamekufa.
Dereva aliegesha gari lake na wanajeshi walianza kushuka taratibu kutoka garini
bunduki zao zikiwa tayari kufanya kazi, ghafla walishitukia kundi kubwa la
ng’ombe kama mia mbili likija kwa kasi kuelekea mahali walipokuwa
wamesimama,wanajeshi wote walihisi hatari.

Page 52 of 77
“Jamani hawa ng’ombe hawana kichaa kweli?” Maaskari waliulizana na
kuwageukia vijana wa Kimasai.
“Nyie vijana vipi hawa ng’ombe wenu?”
“Hata sisi hatuelewi kabisa tuliacha hali ni shwari kabisa hapa kijijini sijui
kimetokea nini!”
Wakati wakiongea hayo tayari ng’ombe walishafika na kuanza kuwashambulia
wanajeshi kwa pembe zao kali, walijaribu kupiga risasi lakini haikusaidia ng’ombe
walizidi kuja mbio, baadhi ya wanajeshi walirusha hata mabomu yalipolipuka
yaliua ng’ombe wachache!Makundi mengine makubwa zaidi ya ng’ombe yalizidi
kujitokeza na kuwashambulia wanajeshi! Kifupi hali ilitisha.
Wakati yote hayo yakitokea mkuu wa majeshi alikuwa bado hajateremka garini,
hali aliyoishuhudia ilimtisha, badala ya kushuka alijikuta akifunga mlango wa gari
zaidi! Hakuna kilichokuwepo zaidi ya kujiokoa na alilazimika kumwamuru dereva
aliondoe gari kuokoa maisha yao.
Ni wao tu wawili waliokoka hata vijana wa Kimasai pia walikufa katika
mashambulizi hayo ya ng’ombe! Lilikuwa ni tukio la ajabu katika historia ya
Tanzania.
Dereva aliliendesha gari kwa kasi huku akipiga honi iliyowatisha ng’ombe
waliokimbia kulifuata gari, njiani alizipita maiti nyingi za watu zikiwa zimelala
chini na wengine wengi walikimbia huku na kule kuokota maisha yao.
Mkuu wa majeshi na dereva wake walifanikiwa kutoka kijijini ndani ya gari
wakiwa salama salimini lakini wenzao wote waliokuwa nao walikufa, jambo hilo
liliwasikitisha sana, mpaka wakati huo hawakufanikiwa kuelewa kama kweli bibi
Nyanjige alikuwa katika kijiji hicho au la! Kilikuwa kitendawili.
“Inawezekana kweli yupo na ameitumia elimu yake ya viumbe niliyosikia kuwa
anayo kuwatia ng’ombe vichaa ili wafanye mauaji bibi mimi anatisha jamani!”
Alisema mkuu wa majeshi msaidizi.
“Nafikiri inawezekana sasa kitafanyika kitu gani ili bibi huyu akamatwe maana
anazidi kuua watu!”
“Hata mimi nashindwa kuelewa, acha kwanza tupeleke taarifa hii kwa wakubwa,
nafikiri kutakuwa na kitu cha kuamua!” Alijibu mkuu wa majeshi msaidizi huku

Page 53 of 77
mwili wake ukitetemeka kwa hofu mpaka wakati huo alikuwa haamini kama kweli
alikuwa amenusurika katika janga hilo la kushambuliwa na ng’ombe.
“Hivi kumbe ng’ombe ni hatari eh?”
“Mimi ndio nimegundua leo kuwa ng’ombe wanaweza kuua kikatili! Tunakula
nyama yao kila siku kumbe ni viumbe hatari”

******
Bibi Nyanjige hakuwa tayari kuingia mikononi mwa wanajeshi kwani kitendo
hicho kwake kilimaanisha kifo! Alikuwa tayari kufa kwa kupigwa na wananchi
wenye hasira lakini si kuingia mikononi mwa wanajeshi ambao alijua alishawatia
hasira kali kupita kiasi.
Pamoja na mawazo hayo alishindwa afanye nini ili ajiokoe kwani alizungukwa na
idadi kubwa ya Wamasai wenye silaha za jadi kama mikuki, pinde na mishale!
Alikuwa amepoteza damu nyingi sana lakini bado alihisi kuwa na nguvu mwilini
mwake ambazo zingemwezesha kukumbia lakini alisita kuchukua uamuzi huo
akiogopa kushambuliwa kwa mikuki na mishale.
Jua lilizidi kumchoma akiwa amelala ardhini, muda wote alifikiria namna ya
kujinasua mikononi mwa kifo lakini alikosa njia! Mara nyingi alishawhi
kunusurika vifo katika mazingira magumu lakini siku hiyo alishindwa kuelewa ni
kitu gani angefanya kujiokoa!
Majira ya saa saba ikiwa ni saa moja tu kabla magari ya wanajeshi hajawasili
kijijini, wazo lilimwijia bibi Nyanjige kichwani mwake, wazo la kutumia mifugo
kama ng’ombe iliyokuwa mingi kijijini hapo kujiokoa! Aliielewa lugha ya
ng’ombe na alijua ni maneno gani huwatia ng’ombe vichaa na hasira.
Baada ya fikra hizo alikunja mdomo wake na kutoa muungurumo kama wa
ng’ombe ambao kwa mbele uliishia na maneno “uwooou” watu wote waliokuwa
wamekusanyika eneo hilo kumshangaa bibi Nyanjige walicheka walipomwona
akifanya kitendo hicho! Alirudia kufanya hivyo mara nyingi na kadri alivyozidi
kutoa muungurumo huo ndivyo watu walivyozidi kucheka! Hawakuelewa ni nini
alichokuwa akifanya.

Page 54 of 77
Ghafla bila kutegemea Wamasai walishtukia ng’ombe wengi wakija mbio kuelekea
eneo hilo huku mikia yote ikiwa imesimama wima nyuma yao! Dalili kuwa
ng’ombe walikuwa wamepatwa na kichaa.
Kijiji cha Kiambali kilikuwa cha wafugaji wa Kimasai tupu na kilikuwa na
ng’ombe wasiopungua 10,000 ukiondoa ndama 5,000! Ng’ombe wote waliruka
kutoka mazizini mwao na kukimbilia kuelekea mahali sauti ya bibi Nyanjige
ilikokuwa ikitokea, nao walikimbia huku wakitoa mlio huohuo ambao hatimaye
ulisambaa kijiji kizima!
Mlio huo ulikuwa ni matusi makubwa kwa ng’ombe wote kijijini humo, uliwatia
hasira mbaya sana ng’ombe wote na kukimbia kwenda mlio ulikotokea ili
kupambana! Wanakijiji hawakuelewa lolote kwa sababu wao hawakuelewa lugha
ya ng’ombe pamoja na kuwa waliishi nao, ilihitaji elimu kubwa sana kuelewa
kilichokuwa kikitokea.
Ng’ombe walipofika eneo la tukio bibi Nyanjige alitoa tena mlio mwingine na
ng’ombe wote walianza kuwashambulia Wamasai waliokuwa eneo hilo kwa
kutumia pembe zao zenye ncha, Wamasai wengi walikufa mbele ya macho ya bibi
Nyanjige!

Page 55 of 77
SURA YA TISA

“NIMENUSURIKA tena!” Alisema bibi Nyanjige wakati akinyanyuka


kutoka ardhini ni yeye peke yake ndiye hakushambuliwa na ng’ombe siku hiyo
kila ng’ombe walipomsogelea alitoa mlio ulioishia na “ssssssssss!” na ng’ombe
wote walimwacha na kuwashambulia Wamasai.
Baada ya kunyanyuka bibi Nyanjige alitembea kuelekea msituni huku
akichechemea! Mwili wake wote ulimuuma na ulijaa majeraha sababu ya kipigo
alichopata! Mbele kidogo kama kilometa moja alijikutaka akitokeza barabarani
alikuwa akisikia kizunguzungu sababu ya kupoteza damu nyingi na alihisi
asingeweza kuendelea zaidi na muda mfupi baadaye alianguka chini.
Ghafla alisikia muungurumo wa gari likija kwa mbali na alipojaribu kunyanyua
kichwa chake kuangalia ulikokuwa ukitokea muungurumo huo alishindwa na
kuendelea kulala chini! Giza lilikuwa limeyafunika macho yake
“ Ni kitu gani kile pale!” Dereva alimuuliza msaidizi wa mkuu wa majeshi baada
ya kuona kitu kama mwili wa binadamu umelala chini!
“Au ni mmoja wa watu waliojeruhiwa na ng’ombe?”
“Hapana watu wa kijijini watakuwa hawajafika huku!”
“Sasa ni nani? Halafu naona yupo uchi wa mnyama! Hebu chukua bunduki yako
tukamwangalie!” Mkuu wa majeshi alisema na wote wawili walichukua bunduki
zao na kuanza kusogea mahali ulipolala mwili ule!
Walishangaa kukuta ni mwili wa bibi kizee! Dereva aliusukuma kwa mguu wake
wa kulia ukalala chali, hawakuamini macho yao walipokuta alikuwa ni bibi
Nyanjige!
Bunduki zote mbili zilimlenga bibi Nyanjige ardhini na hasira ilizidi kuwapanda
mkuu wa majeshi na dereva wake, mioyo yao iliwaambia wammiminie idadi
kubwa ya risasi ikilinganishwa na unyama alioufanya bibi kizee huyo lakini
walishindwa kufanya hivyo baada ya kufikiria agizo walilopewa na mkuu wa
majeshi.
“Ikiwezekana mmlete akiwa hai ili akaushwe na kuwekwa jumba la
makumbusho...!” Kauli hiyo ya mkuu wao ilikuja vichwani mwao.

Page 56 of 77
“Nyie mbwa hebu nipigeni hizo risasi zenu ili mimi nife nipumzike! Au hamjui
kutumia bunduki nini? Nyie wapumbavu sana yaani bibi kama mimi
nimewasumbua kiasi hicho?” Bibi Nyanjige alisema maneno ya kutia hasira ili
kuwalazimisha wampige risasi! Alitamani kufa kwa risasi kuliko kuingia mikononi
mwa wanajeshi.
“Para tat lita-pa! Pa! Pa!”Risasi zilisikika zikilia
“Mkuu umefanya nini sasa? Umesahau maneno tuliyoelezwa kuwa tumepeleke
akiwa hai?”Dereva aliuliza.
“Hasira imenipanda sana!” Alisema msaidizi wa mkuu wa majeshi baada ya
kumimina risasi.
“Sijafa bado nipigeni za kichwa!” Alisema bibi Nyanjige huku akicheka kwa
dharau.
Mkuu wa majeshi alijiandaa tena kumimina risasi lakini dereva wake alimuwahi na
kumnyang’anya bunduki yake!
“Ha! Ha! Ha! Mmeshindwa kuniua sasa subirini mimi niwamalize!” Alisema bibi
Nyanjige.
Tukio la bibi Nyanjige kutoroka kwa mara nyingine liliwashangaza viongozi wote
wa jeshi na kuwafanya washindwe kuelewa bibi huyo alikuwa wa aina gani kwani
alifanya mambo makubwa yasiyolingana na umri wake kabisa! Vichwa
viliwagonga wakuu wa jeshi! Ilikuwa ni mara ya tatu bibi Nyanjige kutoroka
mikononi mwao. Jambo hilo liliwakera sana.
Maiti zote zilizokufa kwa kuumwa na nyuki zilitolewa ndani ya chumba na
kufanya idadi ya watu waliokufa katika harakati za kumsaka bibi Nyanjige kuwa
zaidi ya elfu sita! Jambo hilo lilimtia hasira kila mtu katika jeshi, ilikuwa ni aibu
kwa jeshi kubwa kama hilo kushindwa kumkamata kibibi kama bibi Nyanjige!
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa majeshi hakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya
kujiuzuru wadhifa wake mara moja na aliteuliwa mwingine palepale! Hiyo ilifanya
wakuu wa majeshi waliojiuzuru sababu ya bibi huyo kufikia wawili!
“Hii ni aibu tena aibu kubwa sana kwa jeshi lenye watu makini kama mimi,
naahidi nitamtia mbaroni tu! Subirini!’ Alisema mkuu mpya wa majeshi baada ya
kuapishwa na wanajeshi wote walimpigia makofi!

Page 57 of 77
Siku iliyofuata msako mkubwa ulitangazwa nchi nzima kumsaka bibi kizee
aliyeshindikana kutiwa mbaroni! Mikoa yote ilitaarifiwa na ni mchana wa siku
hiyo hiyo taarifa zilifika makao makuu ya jeshi kutoka mbugani Mikumi kuwa gari
alilotoroka nalo bibi Nyanjige lilikutwa limetelekezwa karibu na lango la kuingilia
kwenye Mbuga ya Mikumi! Taarifa hiyo ilimaanisha wazi bibi Nyanjige alikuwa
amekimbilia ndani ya Mbuga ya Mikumi.
“Askari wote waliopo katika kikosi cha jeshi la 201 KJ mkoani Morogoro
waondoke haraka iwezekanavyo kwenda mbugani Mikumi na waliopo Kilosa pia
wapelekwe huko huko Mikumi, jeshi jingine nitaliongoza mimi kutoka hapa Dar es
Salaam nina uhakika kufikia kesho huyu bibi atakuwa amekwishatiwa
mbaroni!”Alisema mkuu wa majeshi baada ya kupokea taarifa hiyo.
Amri hiyo ya mkuu wa jeshi ilitekelezwa kwa haraka, wanajeshi wa kambi ya
Morogoro na wa Kilosa waliondoka katika magari na kupelekwa hadi mbugani na
mamia ya wanajeshi walisafirishwa kwa magari ya jeshi kutoka Dar es Salaam na
Dodoma hadi katika mbuga hiyo hiyo kwa lengo la kumsaka bibi Nyanjige.
Kwa idadi hiyo ya askari wengi walikuwa na uhakika bibi Nyanjige angekamatwa.
Helkopta zisizo na idadi zilipita angani zikimsaka bibi huyo machachari, ulikuwa
ni msako mkali kuliko msako mwingine wowote uliowahi kufanyika katika
historia ya Tanzania! Hata msako wa porini Kongo haukuwa mkali kiasi hicho!
Wanajeshi wote walikuwa na hasira kali ya kutaka kumtia bibi Nyanjige mikononi
mwao na kumuua kikatili, waliamini alikuwa ameliaibisha jeshi.

*****
Kwa siku tatu mfululizo kulikuwa na hekaheka ya aina yake mbugani, kila kichaka
kilichoonekana mbele ya wanajeshi kilifyekwa na kusabararishwa ili mradi
ulikuwa ni msako wa bibi Nyanjige lakini bado hakuonekana mahali popote,
wanajeshi hawakukata tamaa sababu walijua kwa uhakika alikuwa ndani ya pori
hilo.
“Mpaka tumpate haiwezekani hata kidogo jeshi kubwa kama hili lishindwe
kumkamata bibi kizee wa aina hii tu!”
“Ingawa historia yake inashangaza ni lazima atiwe mbaroni, safari hii hatumpeleki
akiwa hai tena, tutamuuua huku huku porini tu!”

Page 58 of 77
“Kweli sababu tukimfisha watataka kumkausha ili wamhifadhi, ninajua
atawatoroka na kutufanya sisi kuacha familia zetu kuja kumtafuta huku porini, hii
haiwezekani hata kidogo ni lazima tumuue!”Wanajeshi waliendelea kuongea huku
wakiendeleza msako wao porini, kwa kutwa nzima walipita kila mahali porini
wakimtafuta bibi lakini hawakufanikiwa kumpata wala kuona dalili yoyote ya
kuonyesha mahali alikokuwa. Ikawa usiku ikawa asubuhi siku ya kwanza ikapita!
Siku ya pili kama ilivyokuwa imepangwa na mkuu wa majeshi aliyekuwa pamoja
na wapiganaji wake msako uliendelea, wanajeshi walikuwa wamechoka lakini
waliendelea na msako wao bila kukata tamaa, azimio lao likiwa ni hakuna kurudi
nyumbani bila bibi Nyanjige, pamoja na kukatakata miti na hata kuchoma hifadhi
kwa moto bado hawakufanikiwa kumwona bibi Nyanjige, walishindwa kuelewa
mahali alipokuwa!
Wanajeshi wasiopungua elfu tatu walimtafuta bibi Nyanjige mbugani kwa siku
zote tatu bila mafanikio hatimaye walianza kupoteza matumaini kabisa lakini siku
ya nne asubuhi waliibukia sehemu iliyokuwa wazi na iliyolundikwa udongo
mwingi kama tripu za mchanga zilizomwagwa tayari kwa ujenzi.
“Mh!”Mmoja wa maaskari aliguna
“Vipi afande?”
“Nashangaa ni nani amerundika mchanga huu hapa?”
“Labda watu wa hifadhi walitaka kujenga hoteli!”
“Hoteli?”
“Ndiyo!”
“Hoteli eneo hili alale nani?”
“Watalii!”
“Hapana, sitegemei hata siku moja kama kunaweza kuwa na mtalii wa kulala
katikati ya pori kiasi hiki!”
“Aisee hebu angalieni pale!” Alisema mmoja wa wanajeshi akiwaonyesha shimo
kubwa lililokuwa mbele yao.
“Shimo?”
“Ndiyo!”

Page 59 of 77
“Sijui la nini?”
“Hebu twende tukalione!” Waliongozana wakitembea kuelekea mahali lilipokuwa
shimo hilo, wote walibaki midomo wazi kukuta shimo refu likielekea ardhini na
mwisho wake haukuonekana, lilikuwa shimo lenye uwezo wa kupitisha mtu mzima
na pembeni yake kulionekana alama za miguu.
“Mh jamani hii si miguu ya mtu?”
‘Ndiyo tena kwa jinsi miguu hii ilivyo midogo lazima ni ya mwanamke!”
“Inawezekana kabisa!”
“Lakini nani alichimba shimo hili?”
“Hata mimi sijui labda ni wachimbaji wa madini walitaka kuufanya huu mgodi!”
“Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuja porini kwenye wanyama wakali
kiasi hiki kuanzisha mgodi labda kama anataka kuliwa na simba!”
Wanajeshi karibu mia mbili walikusanyika eneo hilo na kuendelea kulishangaa
shimo lililokuwa mbele yao halikuwa la kawaida hata kidogo, kifupi lilitisha na
walijua ni lazima ndani yake kulikuwa na kitu, wanajeshi wengine walihisi bibi
Nyanjige alikuwa ndani yake.
“Mimi nafikiri hii miguu ni ya huyu bibi Nyanjige hakuna mwingine, hebu
nifungeni kamba mimi niingie hadi ndani nikachanguze ila nikitingisha kamba basi
mjue nina matatizo mnivute haraka!”Alisema mwanajeshi huyo na kamba ililetwa
haraka na akafungwa kiunoni na kuanza kushushwa taratibu kuingia shimoni!
Kamba ilikwenda hadi ikafika mwisho bila mwanajeshi huyo kufika chini, shimo
lilionekana kuwa refu na lilikuwa na kiza kinene alitumia tochi kuona ndani, ilibidi
wamvute haraka na kumtoa hadi nje.
“Vipi afande?”
“Jamani huko ndani ni kiza kitupu na shimo bado linaendelea sijui ni kitu gani
kimechimba shimo refu kiasi hiki!”
“Huko ndani hujaona dalili yoyote ya bibi Nyanjige?”
“Hapana ila kuna alama za mtu alikuwa akikanyaga ukutani akishuka shimoni!”
“Umeona alama za miguu?”
“Ndiyo tena na mikono!”

Page 60 of 77
“Sasa?”
“Sijakata tamaa unganishe kamba nne ili iwe ndefu zaidi niingie tena, ninafikiri
bibi yupo humuhumu shimoni!”Alisema askari huyo huku akitabasamu, alionekana
jasiri kupita kiasi
“Au tudumbukize bomu ndani ili ateketee?” Aliuliza mkuu wa majeshi na
wanajeshi waligawanyika makundi mawili juu ya suala hilo wengine wakisema ni
sawa lakini wengine walikataa na kufanya afande aliyejitolewa atumbukizwe tena.
Palepaple kamba iliunganishwa na kuwa ndefu, afande huyo aliyeitwa Alphonce
kwa mara nyingine alitumbukizwa shimoni, safari hi alifika hadi chini akimulika
kwa tochi yake lakini alipotua tu chini alishangaa kusikia akikabwa na kitu kama
mzizi mkubwa shingoni.
Pumzi ilianza kupungua baadaye na baadaye alishindwa kabisa kuhema, macho
yakamtoka, kabla hajakata roho alisikia sauti ya mwanamke akicheka kwa sauti ya
juu.
Baada ya kuliacha gari kwenye lango la kuingilia mbugani bibi Nyanjige alikimbia
huku akichechemea hadi katikati ya mbuga ambako alikuta kundi kubwa la
pundamilia, alipiga mluzi mrefu na wa ajabu Pundamilia wote walisogea karibu
yake na kumzunguka!Lengo lake lilikuwa ni kufika katikati ya pori kwenye
wanyama wengi ili ajichimbie huko na kuunda jeshi jingine kali la wanyama na
kupambana na jeshi la serikali kama wangejaribu kumsaka tena. Alimshukuru
Mungu kwa elimu ya viumbe aliyokuwa nayo bila elimu hiyo alijua asingekuwa
hai.
“Jeshi nitakalounda safari hii litaushangaza ulimwengu huu! Nataka niache historia
nyuma yangu nataka dunia inielewe na nikifa watu wote waseme bibi nyanjige
aliishi na kuusumbua ulimwengu nataka nirudishe heshima ya mwanamke
iliyopotea siku nyingi!”Aliwaza bibi Nyanjige akiwa katikati ya kundi kubwa la
pundamilia walioketi chini na kuwazunguka, heshima kutoka kwa wanyama
ilikuwa ni ileile aliyopata msituni Kongo.
Mahali alipokuwa palimhakikishia usalama lakini bado alikuwa na wasiwasi wa
kusakwa! Gari aliloliacha kwenye lango la kuingilia mbugani lilitosha kabisa
kuonyesha mahali alikokuwa na hivyo kuendelea kusakwa.
“Kama ni hivyo inabidi nisogee mbele zaidi na haraka iwezekanavyo hawa
washenzi lazima watakuja, hilo nalijua wazi!”

Page 61 of 77
Alinyanyuka haraka na kumchagua pundamilia mmoja mwenye nguvu kati ya
Pundamilia waliomzunguka na kupanda juu yake kama vile watu wapandavyo
farasi, huo ndio ulikuwa usafiri wake hata wakati akiwa katika msitu huko kongo!
Alimshika mkia na Pundamilia na kuanza kuukunja! Kitendo hicho kilimfanya
Pundamilia aondoke kwa mwendo wa kasi ya ajabu,bibi alizidi kuukunja mkia
wakipita katikati ya mbuga na kupishana na wanyama wengi wakali lakini
hapakuwa na wasiwasi wowote sababu wanyama wote walimtii, mbele zaidi
alitokeza katika sehemu ya wazi na aliuachia mkia wa Pundamilia akasimama.
“Hapa nilipo si rahisi kuniona ila nahitaji kuwa na mahali pa kuishi na safari hii
nitaishi ardhini ambako hakuna mtu awaye yote ataniona hata wakija kunitafuta
hawatanipata ninachohitaji ni maji na chakula, nitakaa ardhini kwa siku nne bila
kutoka nje siku ya tano nitatoka nafikiri hali itakuwa shwari, kazi yangu sasa
itakuwa ni kuunda jeshi tu!” Aliwaza bibi Nyanjige kisha kuanza kutafakari ni kwa
njia gani angeweza kupata mahali pa kuishi.
“Kwanini nisichimbe ardhini?”Aliwaza bibi Nyanjige na kukubaliana na wazo hilo
na bila kuchelewa alipiga mluzi wa ajabu kwa muda wa kama dakika tano hivi,
walitokeza wanyama wawili wadogo na wafupi kimo cha Paka , walikuwana mikia
mikubwa ya rangi nyeupe! Walikimbia mbio hadi miguuni kwa bibi Nyanjige na
mmoja alimrukia mikononi akambeba kama mtoto!

Page 62 of 77
SURA YA KUMI

BIBI Nyanjige alipiga tena mluzi wa aina nyingine na wadudu wale kama
mshale walirukia ardhini na kuanza kuchimba ardhini! Udongo uliruka kama
uliotupwa na mashine ya kuchimba kisima, katika muda wa kama dakika ishirini
hivi hawakuonekana ardhini na shimo refu kupita kiasi lilishachimbwa ardhini!
Kazi hiyo iliendelea kwa muda kama masaa mawili ndipo bibi Nyanjige aliposikia
mlio fulani wa wanyama hao kutoka shimoni aliielewa maana yake na kuanza
kuteremka shimoni taratibu akikanyaga pembezoni mwa shimo hilo na kuzidi
kushuka chini, ilimchukua muda wa masaa mawili kufika chini ambako aliwakuta
wanyama hao wamelala kifundifundi ardhini! Walionyesha kuchoka.
Kulikuwa na kiza kila mahali ndani ya shimo hilo lakini kwa msaada wa macho ya
wanyama hao ambao macho yao yalimulika kama tochi yenye mwanga mkali bibi
Nyanjige aliweza kuona, hakuwa na tatizo la hewa kwani wanyama walitoa aina
fulani ya hewa kutoka katika mapafu yao iliyoondoa gesi na hewa nzito shimoni.
Ni wanyama hao ndio waliomtunza bibi Nyanjige shimoni kwa siku zote tatu
alizokaa shimoni alikula matunda na ni wanyama hao waliokwenda mtoni kunywa
maji na kwenda kumtemea mdomoni aliposikia kiu.
Wanajeshi kumi na mbili waliongizwa shimoni kuchunguza wote hawakurudi juu
wala kutingisha kamba ili watolewe, hali hiyo ilizidi kuwatia wasiwasi wanajeshi
wote.
“Hebu ngojeni niende mwenyewe inawezekana hawa vijana wanafanya mchezo
humo ndani!”Alisema mkuu wa majeshi akafungwa kamba kiunoni na kuanza
kushushwa taratibu kuelekea shimoni, mwili wake ulitetemeka kwa hofu.
Sababu ya mafunzo ya judo aliyoyapata huko China alikuwa tayari kwa lolote
ambalo angekutana nalo ardhini, alipotua tu chini naye mzizi ulimzunguka
shingoni kwa sababu hakuwa legelege alifanikiwa kuuondoa mzizi na kumtupa
mtu aliyeweka mzizi huo shingoni pembeni, mara alisikia kitu kama mluzi na
ghafla ukipigwa viumbe kama Paka vilimrukia usoni na kuanza kumng’ata na
kumrarua vibaya usoni, lakini tayari alishaitingisha kamba na wanajeshi
waliokuwa nje walianza kumvuta kwa nguvu.
“Jamani ni hatari!” Alisema baada ya kufika juu.

Page 63 of 77
“Kuna nini?”
“Bibi……!” Kabla hajamaliza sentensi yake Kamanda alikata roho.
“Yaani bibi Nyanjige ndiye amemfanya hivi kamanda wetu kama yumo humu
ndani basi hakuna la kufanya zaidi ya kutumbukiza bomu na huu ndio uwe mwisho
wake!”
‘Lete bomu?”
“Hili hapa!”
“Na wenzetu waliomo ndani je?”
“Nina uhakika hao hawawezi kuwa hai, weka bomu shimoni tu!”Alisema msaidizi
wa kamanda na bomu lilitupwa ndani ya shimo, kilichofuata hapo ni mlipuko
mkubwa sana.
Risasi za Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi zilichimba sentimita chache kutoka
kwenye kichwa cha bibi Nyanjige. bila shaka alidhamiria kumuua kutokana na
maneno machafu aliyopewa.
Msaidizi yule wa Mkuu alikerwa na bibi Nyanjige kupita kiasi kutokana na
maneno yake ya dharau. Pamoja na kuelewa ukweli kuwa bibi Nyanjige ana uwezo
mkubwa na ameshalisumbua sana jeshi mpaka hapo walipompata, kitendo cha
kuwatambia kwamba atawamaliza kilimchefua zaidi.
Dereva wake alisimama katika namna ya kumchunga bosi wake asichukue hatua
mbaya ya mauaji. Hakuona sababu ya kumuua wakati kulikuwa na kila uwezekano
wa kumchukua na kumpeleka jeshini.
Bibi Nyanjige kama ambaye alikuwa amesoma mawazo ya Msaidizi wa Mkuu yule
wa majeshi. Alimtazama kwa sura ya dharau ya hali ya juu. Nia yake ikiwa ni
kumjaza hasira zaidi Mkuu huyu ili ampige risasi.
Alikuwa radhi kufa kwa risasi, kuliko kufikishwa mbele ya wakuu wa majeshi
ambao kutokana na jinsi alivyowaudhi na kuwachanganya, alijua lazima atapata
mateso makubwa na mabaya sana. Njia bora aliyoiona ilikuwa ni kuendeleza bidii
ya kuwaudhi wawili hawa, pengine lengo la kupigwa risasi na kufa pale pale
lingekamilika na hivyo kumuepushia na sokomoko ambalo angelipata huko jeshini
atakapopelekwa.

Page 64 of 77
“Nyie Manguruwe pori!.. Nasema kama wanaume kweli vifyatueni hivyo
vibunduki vyenu viniue niende zangu peponi. Mbwa wakubwa nyie. Kwanza
vijanaume gani vinakuwa vipumbavu-pumbavu kama hivyo.
Mnamshikia bunduki bibi kizee kama mimi huku mnatetemeka! Niueni sasa
mkione cha moto!-Washenzi wakubwa!!” Maneno haya yalimfanya Mkuu wa
majeshi kukurupuka na kumnyang’anya bunduki dereva wake na kumwekea bibi
Nyanjige kichwani, akataka kufyatua, dereva wake akamsukuma kidogo na
kumnyang’anya bunduki.
Risasi iliyofyatuliwa kwa mara nyingine ikachimba ardhi badala ya kichwa.
“Kwa nini unanizuia?” Mkuu alimjia juu dereva wake ambaye aligwaya ghafla.
“Nasema kwa nini unanizuia? Huoni maneno anayoyasema mshenzi huyu
yanavyochefua? Unafikiri huyu anafaa kufikishwa jeshini-keshatia hasara ngapi?
Nani ana haja ya kumuona akiwa hai?”
Bibi Nyanjige akaingilia kati akimwita Mkuu yule ambaye alielekea kuingia
kwenye mtego wa bibi Nyanjige kwa kupandwa na jazba.
“We mwanamke!! Unamfokea mwenzako wakati nimeshakupa ruhusa ya kuniua
na ...” Kabla hajaongeza neno zaidi, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akatupa teke
zito, likampata chini ya kidevu.
Bibi Nyanjige akatoa mguno mkubwa wa maumivu. Akajinyonganyoga pale
sakafuni huku akihisi ladha yenye chumvi ya damu kutoka kinywani mwake.
Akalia kwa uchungu wa maumivu yale.
Mkuu wa majeshi alimgeukia dereva. “Unaona.. Unaona?”
“Sikiliza Mkuu, huyu usimuue, hebu punguza hasira na ukumbuke maagizo
tuliyopewa, kwamba tumfikishe huyu akiwa hai mbele ya Wakuu.”
“Amenitia hasira sana, hawezi kunidharau namna hii”.
Dereva aliinama kumwangalia bibi Nyanjige kama yu hai, maana teke alilopigwa
na Mkuu wake lilikuwa ni zito kiasi kwamba bibi yule alijinyonga kidogo kisha
akalala kimya.
Akagundua kwamba ameumia mno. Kwa kuchanganya na majeraha mengine
aliyokuwa ameyapata kutokana na kipigo cha Wamasai, Bibi Nyanjige sasa
alikuwa hajiwezi. Alikuwa akivuja damu na kuvimba karibu mwili mzima, hii

Page 65 of 77
ilimfanya aanze kufikiria upya kuhusu namna ya kumpeleka kwa Wakuu wa
Majeshi.
“Mkuu, huyu ameumia sana, tufanyeje?”
“Hawezi kutembea?” Mkuu ambaye alikuwa ameegemea gari na kuangalia upande
mwingine, alionekana kupunguza makali ya hasira zake.
“Nadhani, buti ulilompiga ni kubwa sana kwa mtu kama huyu, anaweza kufa kabla
ya kufikishwa Makao Makuu”.
“Unafikiria nini sasa?” Sauti ya Mkuu ilishapoa.
“Huyu anahitaji matibabu, Mkuu”
“Na akifia hospitali?”
“Tusifikiri hivyo mapema, maana kama suala ni kifo anaweza kufa hata wakati
tuko njiani kumpeleka Makao Makuu.”
Mkuu aliendelea kubaki nyuma ya gari huku akili yake ikifanya kazi haraka haraka
juu ya nini cha kufanya.
Alikumbuka kwamba ni kweli walitakiwa kumfikisha mtu yule mbele ya Wakuu
wa Majeshi akiwa hai na sio vinginevyo. Japokuwa bibi yule anatisha kutokana na
historia za mauaji makubwa na mazito ambayo ameyafanya, lakini kumfikisha kwa
wakuu akiwa amekufa, ni matusi kwa mwanajeshi mwenye cheo kama yeye.
Kumpeleka mtuhumiwa tena mwanamke kizee akiwa amekufa mbele ya wakuu?
Atajielezaje? Kwamba ametusumbua sana? Msumbufu mwenyewe mwanamke!!?
Tena kizee?
Haikumuingia akilini.
Mwili wa bibi Nyanjige ulikuwa kama umekufa ganzi. Maumivu yalikuwa
makubwa na akajikuta akianza kukata tamaa kutoka mikononi mwa watu wale.
Hakujua wakati kama ule anahitaji kutumia mbinu ya namna gani kumuokoa.
Suala la kufa, halikuwa na mjadala, alitambua kwamba ni lazima ndani ya siku
chache zijazo atakuwa amekufa, lakini mateso atakayoyapata yatakuwa mabaya
zaidi ya kifo!
Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akarudi kutoka nyuma ya gari alikokuwa
ameegemea akiwa tayari na suluhisho. “Hebu muingize kwenye gari”. Dereva
akamtazama katika hali ya kutoelewa, lakini Mkuu alishaingia kwenye gari na

Page 66 of 77
kufunga mlango wake. Dereva akatekeleza hilo, alimbeba na kumwingiza kwenye
kiti cha nyuma, akazunguka na kuingia kwenye kiti cha mbele, akawasha gari.
“Wapi Mkuu?”
“Twende Hospitali.”

*****
Umati wa watu ulikuwa umejazana nje ya Hospitali ya mkoa kutaka kumwona
Bibi Nyanjige, mwanamke aliyevuma nchi nzima kutokana na vitendo vya mauaji
ya kushangaza. Watu walitaka kuhakikisha kwamba ni kweli mwanamke
anayelisumbua jeshi la nchi ni mtu mzima kwa kiasi kinachozungumzwa?
Wengi walihisi kwamba huenda mwanamke huyo akawa ni mtu wa makamo au
kijana na sio mtu mzima sana kama inavyotangazwa kwa sababu kutokana na
kiwango cha matatizo anayoyasababisha, inakuwa vigumu kuamini kwamba
kikongwe kama hicho kinaweza kufanya yote hayo.
Polisi walikuwa na kazi ya ziada kujaribu kusuma sukuma wananchi waliokuwa
wakilisogelea lango la hospitali ambako Bibi Nyanjige alikuwa ameingizwa.
Baada ya kufanikiwa kumfikisha hospitali, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi alijihisi
kupumzika. Aliacha wamuingize kwenye chumba ambacho yeye hakufahamu ni
cha nini, kisha akamgeukia daktari wa zamu.
“Ameshazinduka?”
“Hapana, inaelekea amepata kipigo kikubwa sana na itamchukua muda kuzinduka
na.....”
“Hebu nambie, muda gani unafikiri atakuwa ameshazinduka?”
“Sina hakika Mheshimiwa, lakini nitajitahidi iwe haraka kama mnavyohitaji”
Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akavuta pumzi za matumaini, kisha akamgeukia
tena. “Nambie, atapona huyu?”
“Siwezi kusema mapema hivyo, lakini sijaona kama ana majeraha makubwa sana,
labda iwe ni ya ndani kwa ndani, hata hivyo tutafanya uchunguzi”.
“Sikiliza, mimi nataka apone,” baada ya maagizo hayo, mkuu aligeuka akatoka nje
ya jengo. Wapiga picha za magazeti na televisheni pamoja na waandishi wa habari

Page 67 of 77
wakamfuata kwa kasi kutaka kumhoji, lakini hakuwa tayari kuongea kwa muda
ule. Akapiga simu ya upepo ofisini kuwafahamisha mambo yalivyo. Muda mfupi
baadaye, kundi la wanajeshi lilifika hospitalini kuweka ulinzi mkali ili bibi
Nyanjige asitoroke.

*****
Bibi Nyanjige hakuwa amezimia kweli kama ilivyoeleweka. Alikuwa na fahamu
zake kamili, lakini alifanya hivyo akiamini kwamba mbinu hiyo itamsaidia katika
kumfanya apate mapumziko wakati akitafakari la kufanya.
Ukweli aliuona ni kwamba uhai wake uko hatarini kufuatia kuwekewa ulinzi mkali
na wanajeshi. Aliwahi kufikiria kujiokoa kwa kuita wanyama waje pale pale
hospitali na kusambaratisha madaktari na wanajeshi na yeye akapata nafasi ya
kutoroka, lakini ilikuwa vigumu kwa vile kinywa chake kilitawaliwa na maumivu
makubwa kufuatia buti alilopigwa na yule msaidizi wa Mkuu wa Majeshi.
Kufikishwa mbele ya Wakuu wa Majeshi kama alivyosikia wale wanajeshi wawili
wakizungumza ni kitu kilichomuumiza kichwa sana. Juu ya kukata tamaa, lakini
bado alijipa moyo kwamba atapata jibu la tatizo lake kadiri maumivu
yatakavyopungua.

Page 68 of 77
SURA YA KUMI NA MOJA

SIKU TANO BAADAE.


Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Majenzi ya Ulinzi ulikuwa kimya kana
kwamba hakukuwa na watu. Soli za viatu vya Mkuu wa Majeshi pekee ndizo
zilizosikika zikigongagonga sakafu, akiizunguka meza ile kubwa ya duara katika
hali ya kuonyesha kuchanganyikiwa.
Ni kikao ambacho kilianza muda mrefu uliopita, wastani wa saa nzima, huku
Mkuu wa Majeshi akifoka ukumbi mzima kutokana na operesheni ya
kumshughulikia Bibi Nyanjige ilivyokwenda kizembe mpaka kumkamata tena kwa
taabu kubwa.
Ni katika kikao hicho ambapo Makamanda wote waliokuwa wakishughulikia suala
la bibi Nyanjige mpaka kufikia kuuawa kwa wapiganaji walifukuzwa katika jeshi
na pia kutakiwa kuchukuliwa hatua maalum za kijeshi ili iwe funzo kwa wakuu
wengine ambao ni wazembe kama hao.
Kwa muda wa dakika kumi zilizopita, Mkuu wa Majeshi alikuwa akizungumza
kwa hasira mbele ya makamanda wake kutokana na uzembe uliokuwa umefanyika
hata kumfanya Bibi Nyanjige kulinyanyasa jeshi na kuua wanajeshi pamoja na
kufanya mambo mengine ya kishenzi huku jeshi likionekana dhahiri kushindwa
kumkamata.
“Hamko ‘serious!’ Inakuaje jeshi zima linyanyaswe na mwanamke kikongwe? Ni
ujinga gani unafanyika hapa. Tumetuma wanajeshi sitini na magari kwenda
Kiambali kufuatilia taarifa za kuonekana kwa bibi huyu, wanarudi watu wawili!
wengine wote wameuawa na ng’ombe?
Aibu gani hii? Ng’ombe wanafanya wapiganaji washindwe kufanya kazi yao?
Ng’ombe?” Alipomaliza maneno hayo, akarudi kuketi. Kiha akaendelea kusema,
“Ok, sasa tumeshamkamata Bibi Nyanjige na tunatakiwa kumuadhibu kwa adhabu
ambayo itakuwa ni halali yake kwa jinsi alivyotusumbua kwa kipindi chote hiki na
kutufedhehesha.” Alisema Mkuu wa Majeshi
“Hata hivyo, kwa kuwa hali yake inaridhisha, nataka aletwe hapa sasa hivi ili
tuamue la kufanya mbele yake na utekelezaji ufanyike dakika hiyo hiyo ya
makubaliano”.

Page 69 of 77
Hakukuwa na wa kubisha wala kujadili chochote. Wanajeshi kadhaa waliitwa,
wakapewa maagizo hayo kwamba wayatekeleze kwa muda mfupi ujao.
Kama umeme, wanajeshi wale walivaa bunduki zao, wakachukua gari na kwenda
hospitali ya mkoa kumchukua bibi Nyanjige.
Bibi Nyanjige aliletwa pale haraka kama ilivyotakiwa. Safari hii hakuwa uchi
kama alivyokutwa wakati anakamatwa. Alikuwa amevaa gauni lililoraruka-raruka
ambalo alipewa bila kujua lilikotoka.
Mkuu wa majeshi akaendelea na mazungumzo ambayo alikuwa akiyaongea kabla
bibi Nyanjige hajafika pale. “Kwa hiyo kumchoma katika tanuru siamini kama
kutatusaidia sisi na vizazi vyetu. Ni kweli ametuudhi zaidi, lakini tuangalieni
adhabu nyingine ambazo tumezijadili hapa wakati huyu bibi hajafika.
“Au kumkatakata na kumwagia acid kwenye sehemu za majeraha na mateso
mengine makali tuliyokuwa tumeyajadili, pia sijaafiki kwamba ni adhabu
anayostahili.”
Kutokea hapo, zilijadiliwa adhabu nyingine mbaya na za kutisha zaidi, lakini jibu
halikupatikana mpaka ilipotangazwa adhabu ya kumkausha na kumweka katika
jumba la makumbusho.
“Adhabu hii ninakubaliana nayo na anastahili kabisa.” Mkuu wa Majeshi
alizungumza akitabasamu baada ya kazi nzito ya kutafuta jawabu linalostahili.
Bibi Nyanjige alishtuka! Hiyo ilikuwa ni adhabu kubwa na mbaya zaidi
kutekelezwa kwake. Ingawa alijua kwamba wanajeshi wana tabia ya ukatili, lakini
hakudhani kwamba adhabu ya kifo kwa kukaushwa ingepitishwa kwake.
Alijikuta akitetemeka kwa hofu, hasa baada ya kugundua kwamba kwa mazingira
yaliyomzunguka, kujiokoa kilikuwa ni kitu kisichowezekana kabisa.
Eneo lote lilikuwa limezungukwa na wanajeshi wenye silaha nzito nzito.
Wakati akifikiria hivyo, alishtukia ameshikwa mikono na kuvutwa kinyumenyume
mpaka kwenye chumba kipana ambacho hakikuwa na dirisha zaidi ya hewa ya
mtambo wa kiyoyozi.
Moyo ulimdunda bibi Nyanjige. Alifahamu kwamba mbele ya wanajeshi, mwisho
wa maisha yake umefika.

Page 70 of 77
Alifikiri kuita wanyama waje kumsaidia, lakini kutokana na ukali wa silaha
zilizoko pale jeshini, alihisi kwamba hilo halitawezekana, na zaidi kuingia ndani ya
chumba alichowekwa, itakuwa vigumu kwa mnyama yeyote kuingia.
Alifungwa kitaalamu kwenye kiti maalum cha umeme ambacho kwa jinsi kilivyo
madhubuti, hakuweza hata kujitikisa.Donge la hasira lilimkaba kooni.
Chumba alichokuwamo kilifungwa na akabaki peke yake ndani. Baada ya dakika
chache, wanajeshi zaidi ya 20 na wakuu wao wawili waliingia ndani ya chumba
hicho, na kubamiza mlango kwa nyuma. Mlango huo ulikuwa na tundu ndogo kwa
juu yenye nyavu zilizochakaa, tundu ambalo lingemwezesha mtuhumiwa
anayewekwa mahabusu ndani ya chumba hiki, kuwasiliana na mlinzi yeyote
endapo anapata tatizo.
Mwanajeshi mmoja alikuwa amekamata sindano na boksi lenye chupa yenye
sumu. Akaelekea upande mmoja na kuminya sindano akivuta sumu ijae ndani
yake.
Baada ya kumaliza kufanya hivyo, akamrudia bibi Nyanjige na kuinama mbele
yake huku akitabasamu kuonyesha kwamba mwisho wake umefika. Akamshika
mkono na kusogeza ncha ya sindano.
Bibi Nyanjige alipagawa, ghafla akapiga mluzi mkali sana katika namna ya ufundi
iliyowashtua hata wale wanajeshi. Yule aliyeshika sindano alisita. Wale wengine
wakatazamana kuonyesha kutoelewa kinachoendelea. Kusita huko kulimpa
mwanya bibi Nyangije kuendelea kupiga uruzi wake wa ajabu.
Ghafla, kundi la kutisha la nyuki lilipenya kwenye kidirisha kidogo cha mlangoni,
likaingia ndani ya chumba na kuwavamia wale wanajeshi. Bibi Nyanjige
aliendelea kupiga uruzi na wale nyuki hawakumgusa. Wanajeshi walijaribu
kufungua mlango na kukimbia nje, ikashindikana kwani nyuki walitawala chumba
kizima. Pamoja na ujasiri wa kijeshi, lakini walijikuta wakilia na kupiga mayowe.
Haikusaidia, nyuki walizidi kujaa ndani na kuwashambulia. Vishindo vya
kuwakwepa nyuki na kuchanganyikiwa, vilikuwa vikubwa kupita kiasi.
Dakika tano baadaye, wanajeshi wote 20 walikuwa wameshakufa.
Baada ya lile kundi la nyuki kutoka humo chumbani, ndipo Bibi Nyanjige
alipogundua kwamba nyuma ya kiti alichofungwa, kuna swichi ya kuwasha au
kuzima kiti kile. Kwa kutumia mguu wake mmoja, aliigusa swichi ile, na hapo,
kamba maalum zilizofungwa sambamba na kiti cha umeme zikaachia.

Page 71 of 77
Hakuchelewa, akajitoa kwenye kamba na kumvua nguo mmoja wa wale wakuu
wawili waliokuwa wameingia mle ndani, akavaa yeye pamoja na miwani!
Akaufungua mlango kisha akatoka nje.
Wanajeshi wote walipomwona wakampigia saluti. Akaenda mpaka yalipoegeshwa
magari, akachagua mojawapo, akachomeka funguo na kuliwasha. Akaliondoa
taratibu huku wanajeshi wakiendelea kumpigia saluti kwenye kila kizuizi
alikopita!!
Bibi Nyanjige akarudi kuelekea Morogoro. Akapita Chalinze na masaa kadhaa
baadaye, akawa ameshaingia kwenye mbuga za wanyama za Mikumi.
Hapo akaliacha gari na kuingia kwenye msitu mzito.
Ni huko alikoamua kuwa ndiko kutakuwa kambi yake wakati akiunda jeshi la aina
yake litakaloshirikisha wanyama wote kwa mpango kwamba baada ya miaka
mitano arejee kufanya shambulio zito la kuivamia nchi.
Ni kama machale yalimcheza bibi Nyanjige kwani wakati bomu likilipuka hakuwa
eneo hilo wanyama wake wawili walikuwa wakichimba chini kwa kasi kuelekea
upande wa pili moshi wa bomu ulimfikia hadi mahali alipokuwa lakini alizidi
kutambaa akiwafuata chimbachimba wake kwa nyuma , kasi yao ya kuchimba
ardhini hata yeye mwenyewe ilimshangaza .
Walipokuwa wamekwenda kama umbali wa mita ishirini chimbachimba walianza
kuchimba kuelekea juu kwa amri ya bibi Nyanjige, udongo ukawa ukiporomoka
kumfunika lakini bado alipenyenya katikati ya udongo huo na kulipanda …
taratibu kuelekea juu ya ardhi.
Alikuwa amechoka taabani na hakujua nini cha kufanya ghafla alishtukia
minong’ono ya watu ikija nyuma yake! Alipogeuza kichwa kuangalia nyuma
aliwaona maaskari wasiopungua ishirini wakiwa na bunduki aina ya SMG
mikononi mwao na wote walipiga kelele wakimuamuru atulie vinginevyo
wangemuua kwa risasi.
Tulia hapo hapo ulipo vinginevyo tutakumaliza umetusumbua kwa muda mrefu
sana leo mwisho wako umefika!’’
Hilo hata mimi nalifahamu na ninaomba mniue haraka iwezekanavyo nimechoka
kukimbia, lakini hata hivyo niliyowafanyia yanatosha kuwa kisasi kwa waliomuua
mama yangu!’’

Page 72 of 77
Wanajeshi wote walibaki … kwa mshangao kusikia baba Nyangije aliua watu
wengi kiasi hicho kwa kisasi cha mtu mmoja ilikuwa siyo rahisi kwao kuamini
kuwa hatimaye bibi Nyanjige walikuwa wamemtia mikononi mwao.
Leo hakuna ujanja ni lazima ufe tu!’’ Hilo ninalolitaka mimi!’
Hebu lifanyeni haraka basi!” Hasira ilizidi kuwapanda wanajeshi na wote kwa
walijikuta wakiziandaa bunduki zao tayari kwa mashambulizi, hawakutaka
kupoteza muda zaidi walichotaka ni kung’oa roho ya bibi Nyanjige mtu
aliyewahangaisha kwa muda mrefu.
Jamani hebu sikilizeni!” mmoja wa wanajeshi alisema
“Tusikilize nini?” wote waligeuka na kumuuliza
“Ni vema tukafuata maagizo ya mkuu majeshi kuwa tukimkamata hai tumpeleke
kwake akiwa hai“
Haiwezekani kwani huko nyuma tulikwishafanya hivyo akatoroka! Leo kosa hilo
halifanyiki ni lazima tuulie mbali”
Yalitokea mabishano kidogo baadhi ya wanajeshi wakisema haikuwa sahihi
kumuua bibi Nyanjige, wengi walikubali kumbeba na kumpeleka moja kwa moja
hadi makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam ambako mkuu wa majeshi
angeamua kitu cha kumfanyia bibi huyo hatari na machachari aliyetingisha jeshi.
Kwa kauli moja wanajeshi wote walikubaliana juu ya kumsafirisha bibi Nyanjige
akafungwa kwa kamba mikono na miguu yake pamoja , kipande cha mti
kilipitishwa katikati ya mikono na miguu yake na wanajeshi walimbeba kwa
kutumia mti huo kama mzega wa maji au mnyamapori na kutembea naye moja
kwa moja hadi barabarani walikoacha magari yao.
“Jamani hivi kweli mmeshindwa kuniua mpaka mnipeleke kwa huyo mkuu
wenu?”
“Wee kitimoto kaa kimya na ufunge kabisa hilo domo lako!”
“Yaani unaniita mimi kitimoto? Kijana umechoka kuishi siyo? Nguruwe mkubwa
wee!” Bibi Nyanjige alifoka aliwatukana sana wanajeshi lengo lake likiwa ni
kuwatia hasira ili wamshambulie kwa risasi afe kifo cha mara moja! Alijua wazi
mateso yaliyokuwa mbele yake talikuwa makubwa na hakutaka kukutana nayo.

Page 73 of 77
Wewe hata utukane matusi gani Dar es Salaam lazima ufike tu na kwa taarifa yako
unakwenda kukaushwa na kutunzwa katika makumbusho ya taifa ili hata wajukuu
zetu waje kuelewa ulikuwa mtu hatari kiasi gani!”
“Aisee kwa hiyo nitakuwa mtu maarufu kama Vladimir .L Lenin au Mao Zedong
siyo? Hicho ndito nilichotaka, siku zote niliota kuwa maarufu na kweli nimekuwa
Hureeeeeeee!”
Bibi Nyanjige alicheka na kushangilia kwa dharau.
Aliyoyafanya yote yalizidi kuwachefua wanajeshi lakini kwa sababu
walishagundua nia yake walizidi kumvumilia na kumpakia ndani ya gari,
mawasiliano kati ya vikosi vyote yalifanyika magari yalikusanywa na msafara wa
kurudi Dar es salaam ulianza mara moja . Ilikuwa furaha kubwa mno kwa
wanajeshi kumpata mtu aliyehangaisha nchi.
Msafara uliingia jijini Dar es Salaam masaa sita baadaye na kwenda moja moja
hadi makao makuu ambako mbiu ilipigwa wanajeshi wote wakakusanyika na bibi
Nyanjige kukabidhiwa kwa mkuu wa majeshi.
Nawapongezeni sana kwa kumkamata bibi huyu lakini napenda kuwaeleza kuwa
suala hili hivi sasa halikuwa mikononi mwetu tena inabidi tulipeleke mikononi
mwa sheria, pigeni simu polisi waje wamchukue ni lazima ashtakiwe kwa mauaji
mshenzi mkubwa huyu” Alifoka mkuu wa majeshi.
Simu ilipigwa na dakika ishirini baadaye polisi walifika na kumchukua bibi
Nyanjige moja kwa moja hadi kituo cha polisi ambako alitoa maelezo kisha
kutupwa mahabusu!” muda wote alichekelea wala hakuonyesha kuwa na wasiwsi
wowote. Jambo hilo liliwashangaza watu wengi sana ukilinganisha na kosa la
mauaji ya halaiki alilokuwa akishtakiwa nalo.
Siku mbili baadae alichukuliwa na kupelekwa gerezani keko ambako aliendelea
kusota wakati polisi wakiendelea kukamilisha upelelezi wao, kila mwezi
alipelekwa mahakamani mara moja ambako alisomewa shitaka la mauaji na
kurudishwa tena mahabusu! Kila siku ya kesi yake idadi kubwa ya watu walijaa
mahakamani lengo lao ikiwa ni kumuona bibi Nyanjigebibi aliyeushangaza
ulimwengu kesi yake iliwavutia watu wengi sana jijini Dar es salaam.
Polisi walijitahidi kukusanya kila aina ya ushahidi ili kumtia hatiani bibi Nyanjige
lakini walishindwa kuupata ushahidi kwa sababu ilikuwa si rahisi kuthibitisha
mbele ya mahakama kuwa ni yeye aliyewaamuru wanyama na wadudu

Page 74 of 77
kuwashambulia wanajeshi na kuwaua. kesi pekee iliyoonekena kuwa na nguvu ni
ya mauaji ya watu karibu mia na hamsini waliokunywa maji kisima ambamo bibi
Nyanjige angeweza kushinda katika kesi zote ingawa ni kweli alifanya mauaji kwa
kuwaamrisha wanyama .
Ni kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha ndiko kulifanya bibi Nyanjige asote
mahabusu kwa karibu miezi therasini na sita! Mwezi therasini na saba ulipoingia
ghafla alianza kuugua ugonjwa wa ngozi, kikohozi na homa kali ! Walijaribu
kumtibu katika hospitali iliyokuwepo gerezani bila mafanikio yoyote hali yake
ilizidi kuwa mbaya hata mahakamani wakawa hawampeleki.
Miezi miwili baada ya kuugua hali yake ilikuwa mbaya zaidi homa ilizidi kupanda
madaktari walifikiri homa ya matumbo lakini hata walipompa dawa za ugonjwa
huo bado hazikumsaidia! Alizidi kuzidiwa ndipo walipoamua kumpeleka hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ambako alipikelewa na kulazwa.
Alipofanyiwa vipimo aligundulika kuwa na kimeta alioupata sababu ya kuishi na
wanyama porini kwa muda mrefu, alipewa dawa za ugonjwa huo ambazo
alizitumia kwa muda wa mwezi mzima lakini bado hali yake haikutengemaa, homa
ilizidi kuendelea kuwepo ! Madaktari walizidi kuchanganyikiwa na kushindwa
juelewa ni nini kingefenyika kumsaidia.
Kikohozi kilizidi kupamba moto, alikohoa usaha nyakati za usiku pia alitoka jasho
jingi mwilini. Alipoteza sehemu kubwa ya uzito wa mwili wake hilo lilifanya
madaktari wafikirie kifua kikuu na kuamua kumpima makohozi! .
Majibu yalipotoka yalionyesha kweli alikuwa na ugonjwa wa kifua kikuu na
kulazimu aanzishwe matibabu! Lakini hata baada ya matibabu! ya kifua kikuu
kumalizika bado hali yake ilikuwa mbaya mno! Hakuwa hata na uwezo wa
kunyanyuka kitandani ambako halilala akiwa amepigwa pingu yake mikono.
‘Jamani tu mtibu vipi huyu bibi? ”
“Hata mim nashindwa kuelewa kila dawa tumeshampa lakini bado haisaidii!”
“Sasa tufanye nini?
“Hivi ESR yake ilikuwa ngapi?”
“Mara ya mwisho ilikuwa sitini!”
"Sitini?"
"Ndiyo!"

Page 75 of 77
Hiyo iko juu sana na inaonyesha wazi kuna tatizo! Unaonaje tungempima Elisa test
uone kama ana ukimwi maana dalili zote ni za Ukimwi!” Nakuunga mkono daktari
yalikuwa ni maongezi kati ya madaktari wawili waliomshughulikia bibi Nyanjige
kwa karibu zaidi walifikia uamuzi huo na siku iliyofuata alicchukuliwa damu kwa
ajiri ya kipimo cha Ukimwi!
Hakuna aliyekuwa tayari kuamini majibu yalipotoka kuwa bibi Nyanjige alikuwa
na virusi vya ukimwi vilivyokuwa vikitishia uhai wake.
Niliupata wapi jamani ugonjwa huu? Bibi Nyanjige alijiuliza baada ya daktari
aliyekuwa akimpa ushauri nasaha kumueleza wazi juu ya afya yake alishindwa
kuelewa lakini alipotuliza akili vizuri aligundua ni wapi aliupata ugonjwa huo.
Ni siku ile ya ajali ya basi nakumbuka kuna damu ya majeruhi niliyekuwa
nikimvuta magwanda ya jeshi na kumvalisha nguo zangu iligusa kwenye kidonda
changu nafikiri ni siku hiyo nilipoambukizwa! Aliwaza bibi Nyanjige.
Mwisho wa maisha yake aliuona u karibu kupita kiasi alijua wakati wowote ule
angeweza kuaga dunia! Kila alipofikiria roho za watu waliokufa kwa sababu yake
aliogopa sababu yake alijua wazi hukumu kubwa ilikuwa ikimsubiri.
Eee Mungu nisamehe shetani alinidanganya nikaua watu wasio na hatia! Alilia bibi
Nyanjige kwa uchungu.
Septemba 23 1998 ushahidi wote ulikamilika, ilidhibitika wazi mbele ya
mahakama kuwa bibi Nyanjige alitia sumu kisimani na kuwaua wananchi 150 wa
kijiji cha Usagara mkoani Mwanza!
Ingawa hapakuwa na ushahidi wa kutosha juu ya wanajeshi zaidi ya 7000
waliokufa nchini Congo na katika mbuga ya wanyama Mikumi baada ya
kushambuliwa na wanyama jaji alimtia bibi Nyanjige hatiani.
Kitanda chake kilizungukwa na watu wapatao kumi , kati yao alikuwepo jaji
maarufu jijini Dar es salaam kwa kutoa hukumu za vifo , alikuwa jaji mwanamke
asiye na huruma hata kidogo naalikuwa miongoni mwa watu waliochukizwa sana
na kitendo alichofanya bibi Nyanjige .
Huyu alikuwa jaji Angela Ngaiza ilikuwa ni siku ya hukumu ya bibi Nyanjige
ingawa alionekana kuwa katiak hatua za mwisho kabisa za uhai wake , alikuwa
amekonda mno na aliangalia macho yake huku na kule bila matumaini .
“Nyanjiige!” jaji aliita

Page 76 of 77
“Na..am mhe .shi..miwa jaji ” aliitika bibi Nyanjige kwa taabu.
Mahakama inakutia hatiani kwa kosa la mauaji ya watu 150 waliokufa baada ya
wewe kuweka sumu kwenye kisima cha maji huko Usagara ushahidi uliopatikana
kutoka kwa wwatu mbalimbali akiwemo mtu aliyenunua sumu hiyo kutoka dukani
kwake na majibu ya vipimo vya maji ya kisima uliofanywa na madaktari
uonanyesha wazi ulifanya mauaji hayo na kwa sababu hiyo basi kabla ya
kukuhukumu naomba ujitete!
Hakimu alisema akimwangalia kitandani.
Sina la kujitetea!” Kwa sababu hiyo ninakuhukumu kifo cha kunyongwa!” Jaji
alisema bila ya huruma
Jaji naomba nikukumbushe kitu kimoja kuwa huwezi kuhukumu maiti!
Huwezi kuhukumu mtu aliyekufa tayari!
Mimi ni kama mait….! Bibi Nyanjige hajamalizia sentesi yake, shingo yake
ikaanguka pembeni na hasema kitu tena! Daktari alipompima aliguandua tayari
alishaaga dunia.
Afadhali!” Jaji alisema kwa sauti ya chini

MWISHO

Page 77 of 77

You might also like