Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 51

1|Page

SURA YA KWANZA

ILIKUWA ni mara ya kwanza katika maisha yangu kupanda ndege. Licha ya


kuwa na wasiwasi juu ya maisha ninayokwenda kuishi katika nchi ngeni ya
Kiarabu, nchi yenye utamaduni na sheria tofuati na nchi yangu, hilo halikunifanya
kutoona fahari kuwa ndani ya Fly Emirates Airlines iliyokuwa ikikata mawingu
kwa kasi ya ajabu.
Nikiwa nimeketi katika siti ya dirishani ndani ya ndege hiyo kubwa. Niliyatupa
macho nje, kupitia dirisha dogo ndani ya dege hilo. Niliona tupo katikati ya
mawingu meupe yaliyozagaa katika anga na kuleta taswira kama shamba la pamba
lililomea.
Nilijisikia raha isiyoelezeka.
Masikioni mwangu nilikuwa nimevaa visikilizio, nikisikiliza muziki mzuri wa
Craig David uitwao ‘Walking Away’ uliokuwa unatokea kwenye Ipod yangu
kupitia kwenye visikilizo hivyo vya masikioni.
Sikumbuki tulitumia muda gani kusafiri angani, ninachokumbuka baada ya muda
mrefu kupita sauti ya mhudumu wa ndege kupitia spika zilizokuwa ndani ya ndege
ilisema:
“We are about to land, all passangers of fly Emirates Airlines, wake up and make
sure your belt is close”
Sauti laini ya kike ilisikika, aliongea kwa kimombo akimaanisha abiria tunatakiwa
kufunga mikanda kwani ndege inakaribia kutua.
Ni sauti hiyo ndiyo iliyonistua, nikaangalia saa yangu ya mkononi ikanionyesha
ilikuwa ni saa mbili usiku, nilifunga mkanda kama tulivyotakiwa, kisha nikatulia
kwenye kiti, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi, hofu ikanijaa moyoni
mwangu.
Maneno niliyoambiwa na mama kabla ya kupanda ndege hiyo yakijirudia akilini
mwangu.

2|Page
“Wasichana wanaokwenda kufanya kazi Oman, mara nyingi baadhi yao
wanabakwa, wanamwagiwa maji ya moto, na hata kuuawa, kubwa kuliko vyote
nchi ile inasheria kali dhidi ya makosa mbalimbali. ”
Sauti ya mama yangu ilikuwa ikijirudia akilini mwangu mara kadhaa tangu
mwanzo wa safari hiyo.
Taswira ya mandhali ya kijiji cha Makose huko mkoani Tanga ilinijia kichwani, na
wakati taswira ya kijiji inapita ubongoni mwangu ilikwenda sanjari na picha halisi
ya maisha yangu nikiwa miongoni mwa wenyeji wa kijiji hicho kinachokaliwa
zaidi na wakazi wa makabila ya Wasambaa na wapare waliojipenyeza wakitokea
mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Baada ya kumaliza kidato cha nne nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari ya
Benjamini Mkapa iliyoko jijini Dar.
Zilikuwa ni nyakati za furaha maishani mwangu pengine kuliko nyakati nyingine
zozote, lakini ni nyakati hizohizo furaha yangu iligeuka na kuwa majonzi
yasiyoweza kusahaulika kichwani mwangu.
Ilikuwa ni pale wazazi wangu niliponieleza hawawezi kunisomesha kwa kuwa
hawakuwa na uwezo huo, tena mbaya zaidii nikiwa mbali na nyumbani.
“Hutuwezi kumudu gharama za kukusomesha mwanangu. Shule uliyofaulia ni
shule ya kutwa. Hii inamaana kwamba, upangishiwe chumba, na upate huduma
kama mwanamfunzi. Hiyo ni mbali na ada, sizungumzii nauli na mambo mengine
ya shule...
Jambo baya zaidi, jiji la Dar lina sifa kuwa na gharama kubwa ya maisha.”
Sikubishana na ukweli wa maneno yale. Alichokisema mama kilikuwa sahihi
kabisa, familia yangu ilinuka ufukara, mara kadhaa nilikuwa nikishuhudia
tukishinda na kulalia uji usiyokuwa na sukari.
Sio mara moja kuchekwa nikiwa shuleni, lilikuwa ni jambo la kawaida
kudharauliwa, hata kutengwa kwa kuvaa nguo za kuchanikachanika kiasi cha kutoa
picha kamili ya kiwango cha ufukara ulionizingira.

3|Page
Wala halikuwa jambo la kushangaza kuacha kwenda shule na kufanya vibarua
kwenye mashamba ya wanakijiji, pesa kidogo iliyoipatikana ndiyo ilitumika kwa
kula, kununulia madaftari na sare za shule.
Niliishi maisha ya kifukara tangu nazaliwa hadi nilipokuwa binti. Nikiwa msichana
mrembo wa miaka 21 nilikuwa ni mtu mwenye ndoto na matarajio makubwa sana
kama vijana wengine.
Nilisumbuliwa na wanaume wakware pale kijijini na baadhi yao, walitumia
umasikini wangu kama njia rahisi ya kunipata. Ajabu nilikuwa na misimamo
isiyoyumba. Niliamini mwanaume pekee atakayeujua mwili wangu ni yule
atakayekuwa mume wangu. Kwa kweli nilikuwa ni mwanamke mwenye matarajio
makubwa sana, lakini ndoto zote zilizimishwa na ufukara ulionizingira.

***
Niliyakumbuka hayo nikiwa nimetulia ndani ya ndege iliyotarajiwa kutua dakika
chache katika nchi ya Oman. Nilitokwa na jasho lililotokana na hofu huku nikihisi
tumbo likichemka kadiri tulivyokuwa tukiusogelea uwanja wa ndege wa Jijini
Mascut nchini Oman.
Dakika chache badaye, ndege ilikuwa ikiserereka kwa kasi kwenye ardhi ya nchi
ya hiyo. Baada ya kusimama, tulianza kuteremka abiria mmoja mmoja.
Nilipoikanyaga aridhini, nilijiona nikiwa kiumbe mdogo mithili ya sisimizi, utitiri
wa magorofa yaliyojichomoza kama uyoga sambamba na barabara za flyover
zilinifanya nijione kama ndiyo nakwenda kupotelea katikati ya Jiji hilo.
“Are you Agripina?” nilisikia sauti moja akinisemesha, nilipogeuka nilimwona
mama mmoja mnene wa umbo, aliyevaa baibui sehemu yote ya mwili wake
isipokuwa machoni pekee, mkononi akiwa na bango lililoandikwa jina langu.
“Yes. I’m Agripina, who are you?” nilimjibu nikimuuliza, mimi ndiye Agripina na
yeye alikuwa ni nani.
“Naitwa Mariam Rashidi, ninataarifa za ujio wako, mimi ndiye nitakuwa mwenyeji
wako hapa Oman.”
Yule mama alisema kwa Kiswahili huku akipokea begi langu la nguo.
“Kumbe unazungumza Kiswahili?” Niliuliza kwa wahaka

4|Page
“Ndiyo, mimi ni Mbongo kama wewe, tena ni Msambaa wa Milimani, natokea
maeneno ya huko Lushoto kijiji cha Mlalo,”alisema.
Kwa kweli nilifurahi kukutana na mwanamke yule anayezungumza Kiswahili
kwenye taifa lile la Kiarabu tena akiwa anatokea kijiji jirani na chetu.
Hata hivyo, kwa muda mchache sana niliotumia kutambuna na yule mwanamke
aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Rashidi, kuna mambo niliyoyagundua kutoka
kwakwe, mambo ambayo yalinitisha vibaya mno.
Kwakweli nilifurahi kukutana na mwanamke yule anayezungumza Kiswahili
kwenye taifa hilo la Kiarabu.
Lakini hata hivyo, kwa muda mchache sana niliotumia kutambuna na yule
mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Rashidi, kuna mambo
niliyoyagundua kutoka kwakwe. Mambo ambayo yalinitisha vibaya mno.
Pamoja na kuwa na wasiwasi dhidi ya yule mtu, sikutaka kabisa kuonesha hali ya
hofu waziwazi, wakati wote nilitengeneza uso wenye tabasamu bandia mbele ya
macho ya mwanamke huyo.
Tulitoka nje ya uwanja ule na kuchukua teksi kisha tukaanza safari ya kuelekea
mahali nisikokujua.
Tulitumia nusu saa kufika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi, ambazo siyo tu
hazikujengwa kiramani lakini pia zilikuwa ni nyumba zilizochoka. Nachelea
kusema, ilikuwa ni ‘Uswahilini’ ya Oman.
“Hapa panaitwa Deira,” Mariam alisema, tukiwa mbele ya nyumba moja
iliyoonekana kuchakaa kwa kukosa ukarabati wa muda mrefu.
“Ndipo ninapoishi, lakini kwa sasa tutaishi wote kwa siku mbili. Nitatumia muda
huo kukueleza sheria na taratibu za nchii hii kabla ya kwenda kuanza kufanya kazi
za ndani.”
“Watu wanasema sheria za Uarabuni ni ngumu na kali sana?” nilimuliza.
“Hapana. Siyo ngumu. Inategemeana na wewe utakavyozipokea. Ukizipoea sheria
za hapa katika mtazamo wa ugumu, kwa kweli utashindwa, lakini ukizichukulia
kwa wepesi na ukazitekeleza, huwezi kupata tabu.”

5|Page
Pamoja na maelezo ya Mariam, bado hayakunifanya kutoogopa, matukio ya
mabinti wa kitanzania kubakwa, kuunguzwa kwa maji ya moto wakati mwingine
hata kusukumwa juu ya majengo marefu.
Sambamba na hayo yote, kila nilivyofikiria familia yangu. Familia iliyozingirwa
na umasikini wa kupindukia. Nilijikuta napata nguvu hata kutoogopa lolote.
Taratibu za kisheria juu ya wasichana wa Kitanzania wanaokwenda kufanya kazi
za ndani nchini Oman, tasisi ya ubalozi ilikuwa haiusishwi kabisa. Mambo mengi
yalifanyika kinyamela.
Masaa arobaini na nane badaye, mimi na Marimu tulikuwa kwenye teksi
tukielekea sehemu moja iitwayo Suwaiq kilometa 50 kutoka mjini Mascut. Huko
ndipo mahali nilipotakiwa kwenda kufanya kazi ni huko ambapo kulikuwa na
familia ya tajiri aliyeitwa Abdallah Mustapha ambaye ndiye niliyetakiwa kwenda
kuanza kazi nyumbani kwakwe.
“Karatasi za majibu yako ya vipimo vya hospitali unazo?” Mariam aliniuliza
wakati gari likikunja kushoto na kuiacha barabara kubwa ya lami na kuingia
kwenye barabara iliyokuwa na changarawe nyingi.
“Karatasi zipo kwenye begi, kwani majibu ya vipimo, bado yanahitajika hadi
huku?”
“Ndiyo” alinijibu kwa ufupi. Nilijiuliza moyoni inaamna huko niendako, wao
waajiri hawajui kuwa siwezi kuwa kwenye nchi hiyo pasina kupima, vipi tena
wahitaji majibu ya vipimo.
Wakati nikiwa bado najiuliza, gari lilikata kona na kuiacha ile njia yenye
changarawe na kuingia kwenye njia nyembamba iliyokuwa na marumaru, pembeni
ya njia hiyo kukiwa na miti mingi iliyopandwa kwa mpangilio mzuri.
Gari lilikwenda kwa mwendo wa taratibu. Mita kama ishirini tukawa mbele ya
nyumba kubwa iliyokuwa na sifa zote za kuitwa nyumba ya kifahari.
Baada ya dereva teksi kulipwa ujira wake na kuondoka , tukasogea kwenye geti la
jumba lile. Mariam alibonyeza Swich ya kengele iliyokuwa pale getini na muda
mfupi badaye, alikuja mvulana wa Kisomali kufungua.
Nilipogonganisha macho na yule mvulana kitu fulani kisichoelezeka lilipita
kichwani mwangu. Macho yangu yalinata kwa yule mvulana kwa nukta kadhaa.

6|Page
Alizungumza na Mariam kama watu wenye kufahamiana kwa muda mrefu
kilichonishangaza zaidi aliongea kwa Kiswahili. Alikuwa ni mtu mcheshi na
makalimu. Kiswahili chake kilikuwa na lafudhi ya Kimombasa, kwa kweli
alionekana ni mtu mwenye kufurahia maisha wakati wote.
Baada ya maongezi ya hapa na pale, alitufungulia geti na kuingia ndani.
Ndani ya lile jumba lile kifahari kulikuwa na eneo kubwa la wazi ambalo
lilipandwa bustani ya maua na nyasi fupi za kijani kibichi, upande wa kaskazini
kukikuwa na bwawa dogo la kuogelea sanjari na viti vichache vya kukalia
vilivyokuwa chini ya miavuli midogo mahususi kwa kimvuli, mbele ya nyumba
hiyo kulikuwa na magari ya bei mbaya yaliyopaki kwenye ‘parking’ maalumu
iliyojengwa kiustadi.
“Hapa ndipo utakapo fanya kazi” hatimaye Mariam aliniambia.
“Pazuri sana”
“Ndiyo ni pazuri, hata mshahara utakaolipwa utakuwa mnono, mradi uwe tayari
kukabiliana na changamoto zitakazo kukabili” aliposema hayo taswira ya kubakwa
ikanijia.
Kabla sijatia neno wakati huohuo, alitokea mwanamke mmoja wa kiarabu
aliyekuwa na sifa zote za kuitwa mrembo. Pamoja na uzuri wake lakini midomo na
macho yake yalinijulisha kuwa mtu yule alikuwa na majivuno na dharau.
“Asalam aleykum,” alitusalimia
“Waleykum salama.”
“Huyu ndiye yule mtu mweusi kutoka Tanzania?” alisema. kauli ile ilinifanya
niendelee kuamini kuhusu fikra zangu juu ya tabia ya yule mwanamke wa Kiarabu.
“Ndiye” Mariam alimjibu.
“Mmepima na mmeona hana Ukimwi”
“Hana?”
“Ebola na TB je?”
“Hana pia”
“Piteni ndani” alisema yule mwanamke.

7|Page
“Huyu anaitwa Zakia Al Majid mke wa Abdallah Mustapha.” Mariam
alininong’oneza tukiwa tunaingia ndani, nilishusha pumzi ndefu na kwa mara ya
kwanza nafsi yangu ikikiri kuwa nipo kwenye uwanja wa vita.
Pamoja na kukarahishwa na maswali yaliyokuwa katika dhana halisi ya kibaguzi,
lakini nilivyoingia tu ndani ya lile jumba, akili yangu ikahamia kwenye mandhari
ya mule ndani. Niwe mkweli, tangu nizaliwe hadi leo hii, sijawahi kuona sebule
nzuri kama lile la jumba la kifahari la tajiri Abdallah Mustapha lililopo Suwaiq nje
kidogo ya Jiji la Mascut nchini Oman.
Macho yangu yalikuwa hayatulii, niligeuza shingo huku na kule, nikivutiwa na
fenicha ghali zilizokuwa mule ndani. Nilikuwa mtulivu wakati Marimu akifanya
mazungumzo na yule msichana wa Kiarabu utaratibu wa mkataba wangu.
“Shika hii,” yule msichana wa Kiarabu alinipa karatasi.
“Agripina Soma vizuri huo mkataba wako wa kazi mama, kisha tia saini hapo
chini, ” Mariam ambaye alikuwa kama wakala wangu alishadadia baada ya kuwa
nimepokea karatasi ile.
Nilipitia ule mkataba ulioandikwa kwa lugha ya Kingereza. Pamoja na kwamba
sijui lolote kuhusu mambo ya sheria, hasa sheria za mikataba ya ajira. Nilihisi tu,
mkataba ule ulikuwa na mapungufu fulani ambayo nashindwa kuyabainisha hapa
moja kwa moja.
Nilipogota kwenye nukta ya mwisho ya mkataba ule, sikuamini nilipoona
nitalipwa kiasi cha Riyal 100 ambayo kwa pesa za kwetu ilikuwa ni karibu shilingi
laki sita na ushee.
Yanii kufanya usafi, kuosha vyombo, kufua na kupika, hivyo tu. Nalipwa laki sita
na ushee!!!
Niliona ni pesa nyingi nilizo takiwa kulipwa ukilinganisha na kazi nitakazokuwa
nikifanya. Niliamini wakati wa kupunguza umasikini kwenye familia yangu ndiyo
huo.
Sikutaka kuchelewa. Nilimwaga saini kwenye ile karatasi na nikawa nimeingia
mkataba wa miaka miwili Kwa makubaliano ya kuongezewa mkataba endapo
mwajiri wangu atakubaliana na utendaji wangu wa kazi.
Muda mfupi badaye, nilielekezwa mazingira ya jumba lile sanjari na
kutambulishwa kwa wafanya kazi wenzangu wawili mmoja mwanamke aliyeitwa

8|Page
Fatuma emeke kutoka Liberia na yule mvulana wa Kisomali, ambaye
nilitambulishwa kwa jina la Hussein Jabal, baada ya mambo hayo kukamilika
Mariam aliniaga:
“Mimi naondoka.”
“Sawa...Lakini kuna ajambo nilitaka kukuuliza Mariam.”
“...kuhusu?”
“Kuhusu uvumi wa wasichana wa kazi kufanyiwa ushenzi wakiwa huku ikiwemo
kubakwa.”
“Kubakwa!!!” Mariam alishangaa.
“Ndio, kubakwa”
“Kubakwa ni sehemu ndogo sana ya changamoto zilizopo huku, kwanza ni jambo
la kawaida tu, kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa tayari kuipokea hali hiyo
pale itakapokutokea.” Mariam aliongea kauli hiyo kiwepesi sana.
“Niwe tayari kubakwa pale hali hiyo itakapo tokea?”niliuliza nikiwa nimemkazia
jicho.
“Siyo uwe tayari kubakwa...”
“Bali?”
“Uwe tayari kufanya mapenzi kwa hiyari.”
“Sijaja huku kufanya mapenzi na mtu wa aina yeyote. Lakini pia, sikuja huku ili
ninyanyasike kwa namna yeyote ile Mariam, hukunieleza mambo hayo kabla ya
kupanda ndege, kwa nini unanigeuka?” nilisema kwa sauti kavu lakini yenye
viashiria vya hofu kubwa.
“Ngoja nikupe siri moja...” Mariam alisema. Kabla hajamaliza mara Zakia alitokea
na kunitaka nianze majukumu yangu.
Mariam aliniaga, akanipa miadi ya kuonana wakati mwingine. Nikabakia nikiwa
na mashaka na wasiwasi moyoni.
Mashaka yalikuwa makubwa sana. Sikuwa na imani tena na Mariam. Kama
nilivyosema awali, mwanamke huyo nilimwona ni mtu aliyejaa hila usoni mwake,
tangu siku ya kwanza aliponipokea uwanja wa ndege wa Muscat.

9|Page
Siku hiyo, nilianza kazi kwa nidhamu na umakini. Mwenyeji wangu akiwa ni
Fatuma Emeke msichana mweusi na mzuri wa umbo kutoka nchini Liberia.
Siku kadhaa nikiwa ndani ya ile nyumba ya kihafahari, kama mfanya kazi wa
ndani (house girl) nilibaini jambo jipya.
Yule mwanamke wa kiarabu. Zakia Al Majidi mke wa Abdallah Mustapha alikuwa
ni mke wa pili wa tajiri huyo ambaye alikuwa na watoto wawili wa kiume kutoka
kwa mke wake waliokuwa wakiishi na mama yao katika mji wa Al Jibrih
mashariki mwa Jiji la Mascut nchini Oman.
Niliendelea kufanya kazi nikiwa ni mtu mwenye mori na ari. Sikuwahi kukutana
na matukio kama yalivyokuwa yakivumishwa nikiwa Tanzania. Ama nilivyokuwa
nikihisi. Hapakuwa na mtu aliyewahi kunisumbua kimapenzi aidha kuninyanyasa
kwa namna yoyote ile ingawa majivuno na ubaguzi wa rangi wa Bi Zakia, sikuwa
napendezwa nao.
Nilimaliza mwezi mmoja salama, nililipwa mshahara wa kwanza vizuri bila tatizo
lolote. Siku napokea pesa kama malipo ya kazi zangu lilikuwa ni jambo la furaha
mno kwenye maisha yangu. Niliamini huo ndiyo muda wa kukamilisha ndoto
zangu za kupunguza hali ya maisha duni kwenye familia yangu.
Hapa kuna jambo moja nimesahau kulieleza: Nimesahau kueleza kwamba, moja ya
sheria ambazo ziliwekwa na Bi Zakia pale nyumbani kwake, dhidi ya wafanyakazi
wa ndani ilikuwa ni kutotumia simu za mkononi. Hadi leo sijui yule Mwarabu kwa
nini alituwekea sheria ya kijinga vile.
Nakumbuka Kila mwisho wa wiki, nilikuwa nikifunga safari hadi Mascut. Huko
nilipiga simu nyumbani, nikawasiliana na na familia yangu. Lakini pia, nilikuwa
nikiwatumia pesa kwa njia kama ‘mape-xpress’ ‘western union’ ‘telegram’ na
kadhalika.
Katika kipindi chote cha maisha yangu ndani ya nyumba ya tajiri Abdallah
Mustafa, mtu wa karibu kwangu alikuwa ni yule mvulana Hussein Jabal, raia wa
Somalia. Ukiachilia mbali Fatuma ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu wa
wa kike tuliyeshirikiana kwenye kazi zote za ndani. Ukaribu wangu na mvulana
huyu ulitokana na uwezo wake wa kuzungumza Kiswahili.
Mbali na hilo, Hussein alikuwa ni mtu mcheshi na msikivu, Kila siku baada ya
kazi, tulikaa kwenye bustani ya majani na kuzungumza mambo mengi, nilipata

10 | P a g e
kuelewa mambo mengi kuhusu mtu yule. Hata yeye alijua mambo kadhaa kuhusu
maisha yangu.
Ukaribu wangu na Hussein ulinifanya nimzoe. Kumzoea kukazaa hali ya
kumuwaza kila wakati. Hali ile ya kumuwaza kila wakati, kukatengeneza hali
nyingine ya kummisi hususani pale awapo mbali na mimi.
Taswira ya sura ya Hussein Jabal ilianza kuniganda kichwani mwangu. Sikutaka
kujiongopea kabisa kwamba moyo wangu hauvutiwi na uso wenye pua ndefu,
macho makubwa sanjari na meno yaliyojipanga vizuri mithili ya punje za muhindi.
Sikutaka kabisa kujifariji kuwa nafsi yangu haikuvutika na umbo kakamavu la yule
mvulana.
Lakini hata hivyo, akili yangu haikuwa tayari kuukubali ukweli uliotoka moyoni
mwangu, ukweli wenye viashiria vyote vya mapenzi kwa mvulana yule.
Nilijikumbusha na kujionya juu ya msukumo huo. Sauti moja kichwani iliniambia
jiepushe na mapenzi, yatakuletea matatizo mapenzi, fuata kilichokuleta Agripina.
Sauti hiyo ilikuwa ikigonga kichwa changu kama kengele, lakini pamoja na hilo,
bado moyo wangu ulikumbwa na wazimu dhidi ya mvulana yule. Taa nyekundu
ilikwisha waka moyoni.
Nilijikumbusha na kujionya juu ya msukumo huo. Sauti moja kichwani iliniambia
jiepushe na mapenzi, yatakuletea matatizo mapenzi, fuata kilichokuleta Agripina.
Sauti hiyo ilikuwa ikigonga kichwa change kama kengele, lakini pamoja na hilo,
bado moyo wangu ulikumbwa na wazimu dhidi ya mvulana yule. Taa nyekundu
ilikwisha waka moyoni.
Bila kutarajia nikajikuta mimi na mvulana yule tunaanzisha mahusiano ya
kimapenzi. Mapenzi ambayo yalikuja kuleta madhila makubwa mno kwenye
maisha yangu hadi leo hii ninaposimulia mkasa huu.
Mahusiano yetu yalianza kama mzaha. Awali nilichukulia kama nimepitiwa na
jinamizi la mahaba na tamaa za mwili kwa bahati mbaya. Niliamini mwisho wa
penzi lile ni kupotea kama lilivyokuja, akini kadri siku zilivyokuwa zikiyoyoma
ndivyo mapenzi yangu na mtu yule yalivyozidi kustawi na kukua kwa kasi.
Hussein Jabal alikuwa ndiyo mvulana wa kwanza kuujua mwili wangu.
Nakumbuka siku ya kwanza kugaragara nae kitandani, ilikuwa ndiyo mara yangu
ya kwanza kuingia kwenye sayari ya mahaba kunako sita kwa sita. Huwa siwezi
kuisahau siku hiyo.
11 | P a g e
“Asante Agripina,” Hussein alisema akiwa amelala chali. Kichwa changu kikiwa
juu ya kifua chake. Tukiwa kama tulivyozaliwa.
“...kwa?”
“Kwa penzi tamu...na...Kwakuwa mwanaume wa kwanza kufungua bikira yako.”
“Usijali Hussein ila jambo moja....”nilisema huku nikigeuza shingo yangu na
kumwangalia machoni. Tukawa tunatizamana.
“Usiniache tafadhali.”
“Siwezi kukuacha Agripina, nataka siku moja tukaishi Mogadishu, huko kwetu
Somalia.”
“Kweli?”
“Kabisa.”
Huo ulikuwa ni mwanzo wa mimi kuingia kwenye mambo ya kiutu uzima.
Uhusiano kati yangu na mvulana yule ulikuwa ni siri ya watu watatu. Kwa maana
ya mimi mwenyewe, Hussein pamoja Fatuma Emeke, ambaye alikuwa ni
mfanyakazi mwenzangu kutoka Liberia.
Usiri wa penzi langu na mvulana yule, raia wa Somalia ulitokana na jambo moja
kuu. Tuliogopa sheria kali ya nchi ya Oman iliyokuwa ikisimamia misingi ya
‘sharia’
Ilikuwa hairuhusu vijana ambao hawajaoana kuwa kwenye uhusiano wa
kimapanzi. Adhabu yake ilikuwa ni kuchapwa viboko hadharani au kufukuzwa
nchini humo kwa wageni.
Tuliendelea kufanya kazi kwa bwana Abdallah Mustapha kwa nidhamu kubwa
huku mahusiano yangu na Hussein yakiendelea kwa kasi lakini yakiwa kwa siri
kubwa.
Kila siku usiku nilikuwa nikiondoka chumbani kwangu na kwenda chumbani kwa
Hussein. Huko nilifanya nae mapenzi usiku kucha na alfajiri kabla ya adhana,
nilirejea chumbani mwangu.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu huko Suwaiq nchini Omani kabla ya siku moja
kutokea tukio moja lililobadili dira ya maisha yangu!

12 | P a g e
SURA YA PILI

“TA, TA, TA...” sauti ndogo ya mshale wa saa ya ukutani ilisikika. Ilikuwa
yapata saa sita na nusu usiku, nilikuwa nimelala chali huku macho yangu
yakitizama kwenye dari.
Hakuna kilichosikika zaidi ya sauti ndogo ya saaa ya mshale sanjari na mkoromo
mdogo uliokuwa ukitoka kwa Fatuma aliyekuwa kwenye usingizi wa pono.
Nilijinyanyua kitandani na kuketi kitako, macho yangu yalihamia kwenye kipimo
cha kupima ujauzito, bado moyo wangu ulishindwa kukubaliana na ukweli
kwamba nilikuwa mjamzito. Niliogopa. Muda wa kuwa na mtoto haukuwa sahihi.
Nilivuta pumzi kwa ndani na kuzitoa kwa mkupuo. Kwa mujibu wa saa ile ya
ukutani ilikuwa yapata saa sita kasoro, usiku.
Nilavaa nguo, nikatoka nje. Nikatembea kwa kunyata kukifuata kibanda
alichokuwa akilala Hussein, ndani ya nyumba ile ya tajiri Abdallah Mustapha.
Kulikuwa na ukimya eneo lote la nyumba ile ya kifahari. Nilisogea hadi mlangoni
mwa chumba cha Hussein na kusukuma mlango.
Alaa!
Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.
Haikuwa kawaida kwa Hussein kufunga mlango hasa kwa kipindi ambacho
tunakuwa tumekubaliana kuwa nitakwenda chumbani kwakwe.
Nikasukuma tena. Mlango haukufunguka.
Kuna nini? Nilijiuliza kimoyomoyo.
Nikayatembeza macho kulia na kushoto nikichukua tahadhali ya kubambwa.
Nikarudi tena mlango, sasa nikataka niugonge kidogo kumwamsha Hussein nilihisi
huenda alipitiwa na usingizi na alijisahau akafunga mlango.
Lakini kabla sijatekeleza hilo, ghafla nikasikia sauti kutokea mule ndani.
Ilikuwa ni sauti ya kilio cha mwanamke, nikamakinika na hali hiyo. Nikatega
sikio.

13 | P a g e
Toba!
Nikaendelea kugundua kuwa ilikuwa ni sauti ya kimahaba ya mwanamke
aliyekuwa ndani ya chumba cha Hussein Jabal.
Ndani ya chumba kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya mapenzi.
Hussein ananisaliti!....
Ndiyo wazo la kwanza kupita kichwani mwangu.
Mwili ukanitetemeka. Donge zito likanikaba kooni, nikahisi uchungu wa ndani
kwa ndani. Wivu ukanivaa.
Nikaugonga mlango kwa nguvu. Sikujibiwa zaidi ya kuendelea kusikia sauti ya
mwanamke aliyekuwa akilia. Kilio cha raha.
Kitendo hicho kikazidisha wahaka ndani ya nafsi yangu. Kichwa changu kikawa
na maswali lukuki.
Ndani ya lile jumba la kifahari, tulikuwa wanawake watatu. Fatuma Emeke, Zakia
ambaye ni mke wa Abdallah Mustapha pamoja na mimi.
Kivyovyote vile Hussein ndiye alikuwa akifanya mapenzi na mwanamke mule
ndani. Swali kuu ni Je mwanamke huyo ni nani?
Ni Fatuma au ni Zakia? Fatuma nilimwacha chumbani akikoroma. maana yake ni
kwamba siyo Fatuma. Ni nani? Zakia.
Nilipo muwaza tu mwanamke huyo, hapo hapo taswira ya tabia zake zikanijia
akilini.
Mbali ya wivu dhidi ya mumewe, Alikuwa ni mwanamke mwenye dharau na
majivuno, mtu mweusi kwakwe alikuwa ni kikatuni kisicho na maana yoyote.
Alikuwa ni mbaguzi asiye na mfano. Hakupenda kuchangia meza moja ya chakula
na watumishi wake wa ndani. Siku zote alimini mtu mweusi yupo duniani kwa ajili
ya kumtumikia mtu mweupe.
Kwa mantiki hiyo anawezaje kuwa ndiye mtu aliye ndani wakifanya mapenzi na
Hussein Jabal mvulana asiye na mbele wala nyuma kutoka huko Mogadishu nchini
Somalia.
Sasa kama ni hivyo mwanaume huyo anafanya mapenzi na nani?

14 | P a g e
Nilijihoji huku nikijawa na wivu mwingi kifuani kwangu, donge zito lilinikaba
kooni kila nilivyozisikia kelele za kilio cha mahaba kutoka mule ndani.
“Yanii huyu bwana anipe mimba halafu kama haitoshi ananisaliti!! Nilifadhaika
san.
kwa nguvu zangu zote niliusukuma mlango na kuingia ndani.
Sikuamini macho yangu....
“Yanii huyu bwana anipe mimba halafu kama haitoshi ananisaliti!! Nilifadhaika
san.
kwa nguvu zangu zote niliusukuma mlango na kuingia ndani.
Sikuamini macho yangu....

Hussein Jabal na Zakia mke wa Abdallah Mustapha walikuwa uchi wa mnyama


kitandani.
Niliduwaa mbele yao, macho yalinitoka pima. Mikono yangu ilifunika mdomo
wangu uliokuwa wazi kwa mshangao!
Wao pia, walipatwa na taharuki, wakakurupuka kitandani na kunyakua nguo
zilizokuwa kando na kujiziba. Tukatizamana bila yeyote kati yetu kusema kitu.
Ilikuwa ni picha mbaya kwenye macho yangu.
“Unaona sasa. Haya yote nilikueleza.” Hussein aliongea kibwege akiwa na
wasiwasi usoni. Zakia hakutia neno zaidi ya kuanza kuvaa nguo zake upesi upesi.
“We mbwa umetoka chumbani kwako kuja kunifumania humu chumbani?” Zakia
alisema, safari hii macho yake hayakuwa na wasiwasi tena, yakawa ni macho
yenye chuki na hasira dhidi yangu.
Nakuuliza wewe Malaya mweusi....” alisema. Na pale pale alinichapa kibao
ambacho hakikunifanya niyumbe wala kupepesa macho.
Nilikosa cha kumjibu yule mke wa bosi wangu, nikabaki nimeganda kama sanamu
huku moyo wangu ukiteketea kwa dhuruma ile.
Yanii nidhulumiwe penzi langu na mitusi nitukanwe na makofi nipigwa!! Niliwaza
kimoyomoyo nafsi yangu ikizidi kukaangika kwa maumivu.

15 | P a g e
“Hussein, why this black bitch come in here ?” Zakia alimuuliza Hussein kwa
ghadhabu, kwamba kwa nini mimi Kahaba mweusi niko pale.
“Kahaba ni wewe Kisonoko wa Kiarabu.” nilisema huku nikimwangalia Zakia kwa
jicho la chuki.
Alinitandika kibao kingine. Nilipepesuka na kuhisi shavu likifukuta kwa joto kali
la maumivu, lakini safari hii na mimi sikukubali, kwa wepesi wa ajabu nilimrukia
nikampiga kibao cha uso kilicho mpeleka chini, sura yake ikawa imejaa mshangao
wa kutotegemea jambo lile.
Akanitizama kwa ghadhabu na kunifuta kwa hasira huku akiunguruma kama paka
vidole amechanua tayari kwa kuniparua kwa makucha. Ndani ya sekunde zilezile
mlango wa chumba kile ulisukumwa, bila kutegemea mumewe aliingia.
Tukabaki tumeduwaa, ndani ya nukta chache sana. Akili ya Zakia alifanya kazi
mithili ya kompyuta, hapohapo alimkimbilia mahali aliposimama mumewe
Abdallah Mustapha na kumkumbatia kifani, akaongea kwa mideko:
“These two people want to kill me just because I found them sexing” alisema kwa
Kingereza chepesi kwamba tunataka kumua kisa ametukuta tikifanya mapenzi.

Lilikuwa ni shambulio la moja kwa moja kwa upande wangu, na ikawa zamu
yangu kutaharuki.
“What!.” Abdallah alihamaki. Akatutizama mimi na Hussein kwa zamu, macho
yake yakiwa na hasira. Ghafla alinirukia na kunipiga ngumi ya uso, nikaanguka
chini huku damu zikinitoka puani. Akamvaa Hussein na kumpiga mateke ya
tumboni.
“Mnazini ndani ya mji wangu, kama haitoshi mnataka kuondoa uhai wa mke
wangu!!!..” alisema kwa ukali ndita zilizojichora kama mkeka wa kizaramo
zilionekana.
“Watu weusi mnataka kuua mtu mweupe..! tena kwenye ardhi ya nchi yake..!Hii ni
kali kuliko zote nilizowahi kuziona!” jitu hilo la Kiarabu liliunguruma.
Mefanya makosa makubwa sana, hili ni taifa la Warabu, siyo Afrika... huko kwa
wapumbavu...” alisita, akaacha kumpiga Hussein, akatutizama kwa zamu kisha
akasema tena:

16 | P a g e
“Jiwekeni tayari kunyongwa hadhalani washenzi weusi ninyi,” sauti yake ilikuwa
ya kunong’ona lakini yenye kutisha.
Walitoka mule ndani kisha wakatufungia mlango kwa nje na kutia kufuli.
“Get ready for wriggle! Black bitch” Akiwa nje ya chumba walichotufungia
alirudia rudia kusema hayo maneno kwa msisitizo, akiwa na maana kwamba tuwe
tayari kufa.
“Ulijuaje kuwa hawa washenzi wako huku wakifanya huu ujinga?” nilisikia
Abdallah akimuliza mkewe.
“Niliona dalili za mahusiano tangu zamani, ndipo nilipoanza uchunguzi wa siri.”
“Lazima tuwasiliane na polisi na kuwaeleza juu ya haya ili watu hawa wapewe
adhabu ya kifo.”
“Lini?”
“Sasa hivi.”
Nilisikia mazungumzo hayo yaliyozungumzwa kwa sauti kubwa, kila neno
nililisikia vizuri kabisa.
Muda mfupi badae nilimsikia tena Abdallah akiwasiliana na polisi na kuwaeleza
kisanga chote kilichotokea pale nyumbani kwakwe.
“Ndio...Wamo ndani.......hawawezi....kutoroka....Tanzania na Somalia” Abdallah
aliendelea kutoa maelezo kwa polisi, kisha nikasikia akiwamiza polisi kufika ndani
ya dakika ishirini.
Niliketi chini, donge zito likinikaba kooni, machozi yalinitoka, nilijiona ni kimbe
niliyedhulumiwa haki yangu kwa kiwango kikubwa, kwa wakati huo sikuwaza
madhala yanayoweza kutokea kutokana na lile tukio, lililokuwa akilini mwangu ni
MAPENZI.
“Alinilazimisha....” hatimaye Hussein alisema kwa sauti ya upole akiniangali kwa
macho ya upole.
“Nini!”
“...alinilazimisha kufanya mapenzi...” alisema tena huku akinitizama kwa huruma.

17 | P a g e
“Unafikiri naweza kuwa hayawani wa kiwango hicho? tangu lini mwanaume
akalazimishwa kufanya mapenzi na mwanamke! tafuta uongo mwingine wa
kuniongopea siyo huo”
“Haki ya Mungu nakuapia, Zakia amekuwa akinitaka kimapenzi kwa siku nyingi
sana na nimekuwa nikitishiwa kwa mambo mengi, najua ni ngumu kunielewa,
muhimu kwa sasa tufanye mpango wa kujinasua kwenye hili songombingo kwani
nijuavyo sheria za nchi hii, kesho asubuhi tutanyongwa hadhalani kwa makosa ya
uzinifu na kutaka kuua.”
Kauli ile ndiyo iliyozindua ufahamu wangu na kuelewa hatari iliyokuwa
inaninyemelea. Wivu uliokuwa umegubika nafsi yangu uliyeyuka kama bonge la
balafu kwenye jua, hofu ikachukua nafasi.
“Hussein umeniponza, ona maisha yangu ulivyoyaingiza matatani...”
“Hayo tutayaongea badaye, muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunatoweka eneo
hili”
Huko nje tuliendelea kuwasikia Zakia na mumewe wakiendelea kutujadili kwa
namna kifo chetu kitakavyokuwa funzo kwa watu wengine hususani wafrika
waliko nchini Oman.
Dakika chache nilisikia ngurumo za magari ambayo haikuhitaji kuuliza ni magari
ya nani, upesi nilifahamu yalikuwa ni magari ya polisi.
“Wako wapi?” nilisikia sauti ikisema huko nje.
“Tumewafungia chumba hiki” Abdallah alijibu, mlango wa chumba ulifunguliwa
askari kama saba wenye bunduki wakaingia mule ndani.
Hatukuulizwa chochote na wale askari zaidi ya kupigwa, tulipigwa na kupigwa
tukapigika kweli kweli.
Kila sehemu ya mwili wangu kulikuwa na maumivu. Sikuweza kusimama kwani
nilikuwa na maumivu makali.
“Wasilianeni na ndugu zao waliopo huku kwa ajili ya kuja kuchukua maiti zao.”
Askari mmoja aliyeonekana kama kiongozi wao alisema.
Tuliondolewa mule ndani tukiwa tumefungwa pingu mikononi, tukapandishwa
kwenye gari la polisi, safari ya kuelekea mahali ambapo sikupaelewa ikaanza,

18 | P a g e
muda wote nilikuwa nikilia kwa uchungu, maisha yangu yalikuwa yamebadilika
ghafla mno.
“Nisamehe Agripina” Hussein alisema, akionekana kukata tamaa. Aliongea hayo
tukiwa ndani ya ‘defender’ la polisi
“Najua hadi kesho, muda kama huu, miili yetu itakuwa mochwari ndani ya friji
lenye baridi kali, ikingojea kuzikwa kwenye makaburi mawili tofauti. Nataka
moyo wako ufahamu kuwa sikukusudia safari ya mahusiano yetu iwe hivi.
Ndoto zangu za kukupeleka Mogadishu zimegonga mwamba. Naumizwa na hilo
Agripina, lakini naumizwa zaidi na mtoto aliye tumboni mwako” alisema huku
akinionyesha kipimo changu cha mimba alichokuwa amekimata mkononi, machozi
yakijikusanya machoni mwake.
Sikujibu chochote, zaidi ya kutiririkwa na machozi, polisi walikuwa wametuweka
kati huku mitutu ya bunduki ikitutizama kwa uchu.
Tulipelekwa hadi kwenye eneo moja lenye uwazi mkubwa, kukiwa na majengo
yaliyokuwa kama mabweni, ukingoni mwa eneo hilo kukizungushiwa ukuta mrefu
wenye mitambo yenye shoti za umeme.
“Teremka” tuliamriwa.
Taswira ya kunyongwa ikawa inanitesa akilini, kwakweli niliogopa sana, tukiwa
kwenye lile eneo ambalo badae nilifahamu kuwa ilikuwa gereza.
Tuliingizwa kwenye ofisi ndogo tuliyo andikisha majina yetu na kuandikiwa
makosa mawili yanayotukabili, kwa maana ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa,
sanjari na kujaribu kuua.
Baada ya hapo, Hussein alichukuliwa na kupelekwa eneo ambalo sikujua ni wapi.
Nilitolewa mule kwenye kile kiofisi kidogo na kuingizwa kwenye chumba pweke
ambacho hakikuwa na kitu chochote, kulikuwa na mwanga hafifu wa njano
uliotokea kwenye balbu ndogo iliyokuwa ikining’inia kwenye dari.
Niliegemeza mgongo ukutani, taswira ya kijiji cha Makose mkoa wa Tanga huko
nchini Tanzania ikanijia, kwa mara nyingine nililia mno kuona ndoto zangu za
kuikomboa familia yangu katika maisha duni zimegonga mwamba huku nikisubiri
kunyongwa hadi kufa masaa machache yajayo.
Niliegemeza mgongo wangu kwenye ukuta, taswira ya kijiji cha Makose mkoa wa
Tanga huko nchini Tanzania ikanijia, kwa mara nyingine nililia mno kuona ndoto

19 | P a g e
zangu za kuikomboa familia yangu katika maisha duni zimegonga mwamba huku
nikisubiri kunyongwa hadi kufa masaa machache yajayo.
Nilikaa ndani ya kile chumba hadi asubuhi, mwanga wa jua la asubuhi ukapenya
kupitia matobo ya kwenye bati na kuingia hadi ndani ya chumba kile.
Niliumia nilipo baini kuwa jua hilo ndio jua la mwisho kuliona duniani, masaa
mawili badaye, mlango ulifunguliwa. Wakaingia askari wawili na wakanitaka
nitoke nje.
Nilitolewa nje na kupelekwa tena kwenye ile ofisi ndogo ambayo niliingizwa jana
usiku nikiwa na Hussein Jabal.
“Yuko wapi Hussein?” niliuliza.
“Unamuuliza nani maswali ya kijinga, nyamaza kimya” askari mmoja alinifokea.
“Nifanyie ikhisani ya jambo moja,” nilimwambia kwa upole huku machozi
yakinilenga.
“Jambo lipi?”
“Naombeni msaada wa kuwasiliana na ubalozi wa nchi yangu ili nipate msaada wa
kisheria. Pia yupo mwenyeji wangu aitwaye Mariam ambaye anaishia hapa hapa
Mascut maeneo ya Deira...”
“Tunasikitika hilo pia hatuwezi kufanya , taarifa zitakazo mfikia huyo Mariam ni
kuja kuchukua maiti yako.” alisema tena yule askari.
Nililia nikalia na kulia, hofu ya kunyongwa kwa kamba ilisambaa ndani ya kifua
changu vibaya sana.
Walinifunika kitambaa cheusi usoni, mikono yangu ikiwa kwenye pingu.
Nikachukuliwa na kupelekwa mahali ambapo nilisikia wakipataja kuwa panaitwa
‘slaughuter place’
Nilifikishwa ‘slaughuter place’ na kufunguliwa kitambaa, mbele yangu nikajiona
nipo eneo lenye uwazi kama uwanja wa mpira, kulikuwa na jukwaa kubwa ambalo
lilitengenezwa kama goli la mpira wa miguu, kamba nyingi zenye vitanzi zilikuwa
zikining’inia kwenye goli lile nikabaini eneo hilo ndipo eneo lililohusika kwa
kunyongea watu.

20 | P a g e
Katika kutazama huko nikaendelea kuona kitu kingine kilicho upasua moyo wangu
vibaya mno, nilimwona Hussein akiwa kando ya jukwaa lile la kunyongea akiwa
anafanya ibada kwa imani ya dini ya Kislamu.
“Husseiiiin!!” niliita kwa nguvu huku nikiamini kivyovyote vile Hussein amepewa
nafasi ya kusali sala ya mwisho kabla ya kuning’ininzwa kwenye kitanzi. Wale
askari wa kijeshi walinikaba shingoni.
“Wewe!!!. Kuleta ghasia kwa mtu anaye fanya ibada ni jambo baya...Eeh!!”
Nilishindwa kujibu kwa kuwa tayari nilikuwa nimefungwa kitambaa mdomoni,
nikaishia kulia, wakati huo nilimwona Hussein akiwa amemaliza kufanya ile ibada
na sasa askari walimfunga pingu mikononi mwake. Aligeuka akanitizama huku
akitoa tabasamu lenye kila dalili ya kukata tama.
“Agripina naenda kunyongwa, nisamehe kwa kushindwa kukupeleka Mogadishu,
nisamehe hata kwa kukusababishia kifo ilihali ukiwa na mtoto tumboni mwako.
Nisamehe kwa kukusaliti na kutembe na mwanamke mwingine, nisamehe kwa kila
kitu Aglipina.
Naamini tutaonana badaye. Inshallah...” Hussein alipaza sauti kunieleza.
Nibubujikwa na machozi mdomo wangu ukiendelea kuzibwa kwa tambala gumu.
Walimvalisha soksi nyeusi usoni wakamwongoza kumpandisha kwenye jukwaa la
kunyongea. Askari wawili walimvisha kitanzi cha kamba ngumu shingoni na
kuhakikisha wamekaza vizuri kisha wakashuka chini wakimwacha peke yake
kwenye jukwaa.
Niliendelea kulia nikimwomba Mungu kimoyomoyo afanye mujiza wake
kubadilisha kile kilichokuwa kikiendelea wasaa ule, lakini haikuwa hivyo. Askari
aliyehusika na kubonyeza swichi ya kupandisha kamba juu alikuwa akingojea amri
kutoka kwa kamanda mkuu.
“Kill him.”
Amri ya kunyonga ilitoka.
Mnyongaji alibonyeza swichi, kamba ikaanza kujiviringisha taratibu kwenda juu.
Ilivyokuwa ikijivingirisha ndivyo ikawa inamnyanyua Hussein taratibu na hapo
ikawa inamkaba shingoni kwa nguvu.

21 | P a g e
Sekunde kumi badaye Hussein alikuwa akining’inia juu na kutapatapa huku na
kule. Miguu yake ilikuwa ikirukaruka huku kiwiliwili chake kikitetemeka kama
anapigwa na shoti ya umeme. Hussein alijikojolea na wakati mkojo huo unapita
sekunde tano zilizofuata Hussein alitulia tuli.
Tayari alikuwa MAITI!!!!!.
Bila kutegemea nilijikuta na mimi nikijikojolea kwa mara ya pili, nilikuwa na
woga usiyo mithilika, niliona mwili wa Hussein ukiendelea kubembea kwenye
kamba. Maisha ya Hussein hapa duniani yaliashia hapo. Kilichokuwa kimebaki
kwakwe ni kushushwa kupelekwa mochwari kisha kuzikwa.
“Anayefuata kunyongwa ni wewe,”
Sauti ya kamanda ilisikika nyuma yangu. Tumbo likinichafuka nikahisi kutapika,
bila kutarajia nikajisaidia haja kubwa na ndogo kwa pamoja.
Nilifunguliwa kile kitambaa mdomoni na kusogezwa eneo lilitandika zuria dogo
kando kukiwa na maji kwenye ndoo ambayo nilitakiwa kunawa kabla ya kusali
sala zangu za mwisho kisha kunyongwa kama ilivyokuwa kwa mpenzi wangu
Hussein Jabal.
“Niacheni nirudi nyumbani, sitaki kufa mimi...sitaki.” nilisema kwa hamaniko
kubwa huku nikilia. Hakuna aliyenijali, wote walinitaka nijinawishe kwa maji
kisha waninyonge.
Niliendele a kuwasihi waniachie nirudi nyumbani kwetu Tanzania, lakini nao
waliendela kunisihi nisali sala zangu za mwisho kwani muda wa mimi kufa
utakapo wadia hawatakuwa na cha kusubiri zaidi ya kunitundika kweye kamba na
kuninyonga.
Muda wa kunyongwa ulifika. Walinikamata askari wawili waliokuwa na nguvu na
kunisukumiza kwenye jukwaa tayari kwa kunivisha kitanzi na kunyongwa.
“Mungu uko wapi wewe Mungu...Fanya kitu kwa ajili yangu baba, fanya sasa hivi
Mungu wangu, nisaidie.” nilitamka maneno hayo kwa nguvu nikiwa
nimechanganyikiwa vibaya sana.
Hata hivyo, fikra hizo zilibakia kuwa kichwani mwangu tu. Nilivishwa kitambaa
cheusi kisha kitanzi, kamba ikakazwa shingoni mwangu na askari anayebonyeza
swichi inayoruhusu kamba kunivuta kwa juu aliiendea swichi na kuibonyeza.

22 | P a g e
“Mungu uko wapi wewe Mungu...Fanya kitu kwa ajili yangu baba, fanya sasa hivi
Mungu wangu, nisaidie.” nilitamka maneno hayo kwa nguvu huku nikilia kama
mtoto, sikuwa tayari kufa, bado niliona nina haki ya kuishi na kuwa mtu huru
kwenye dunia.
Hata hivyo fikra hizo zilibakia kuwa kichwani mwangu tu, nilivishwa kitambaa
cheusi kisha kitanzi, kamba ikakazwa shingoni mwangu na askari anayebonyeza
swichi inayoruhusu kamba kunivuta kwa juu aliiendea swichi na kuibonyeza.

Kamba ilianza kuivuta shingo yangu na kunining’iniza kwa juu. Pumzi ziligoma
kutoka huku maumivu makali ya kubanwa na kamba yakiniumiza. Nikawa
natapatapa huku na kule, nikatamani ninyanyue mikono yangu ili nizuie kamba
isiendelee kunikaba, ila mikono yangu ilikuwa imefungwa pingu.
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu na wakati huohuo nikajiona nikiwa naelea
angani, nikiwa kwenye hali hiyo, nilijiona naanguka kwa kasi kueleka kwenye
shimo ambalo lilikuwa na giza, kwenye shimo hilo sikuona mwisho wake. Hapo
nikaendelea kubaini kuwa zile ni dalili za kifo.
‘Kumbe ndiyo hivi mtu akiwa anakufa inavyokuwaga niliwaza.
Nukta zilezile sikujua tena kilicho endelea ingawa kabla sijajua kilicho endelea
tayari nafsi yangu ikakubali kuwa mimi ni maiti!!!

23 | P a g e
SURA YA TATU

NILISHITUKA ghafla nikajikuta nipo kwenye eneo lenye baridi kali na


ukimya wa ajabu. Nilikuwa nimelala chali huku nikiwa kama nilivyozaliwa,
nilikuwa natetemeka kutokana na baridi.
Niligeuza shingo kutizama kulia na kushoto, nikajiona nipo kwenye kitu kama box
kubwa lenye kuzalisha baridi, sikuhitaji muda mrefu zaidi kutambua kuwa
nilikuwa nimewekwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti ndani ya Mochwari!.
Ndani ya nukta zilezile nilikumbuka kila kitu. Kichwa changu kikabaki na maswali
mengi ambayo majibu yake sikujua pakuyapatia. Katika mengi niliyojiuliza, swali
kubwa lilikuwa ni vipi nipo hai ilihali nilinyongwa kwa kamba hadi kufa!.
Wakati nikiwa naendelea kujiuliza swali hilo mara nilisikia mlango wa Mochwari
ukifunguliwa, nikasikia sauti za watu wawili wakizungumza, mmoja mwanaume
mwingine wa kike.
Almanusura nipige kelele baada ya kusikia sauti ya mtu ninaye mfahamu.
Niliweka utulivu nikajionya kutokurupuka kwa namna yoyote ile. Nilitulia huku
nikifuatilia mazungumzo.
Wakawa wanazungumza huku wakisogea karibu zaidi na jokofu nililokuwa
nimelazwa. Nikasikia yule mwanaume akimuhadithia songombingo lilitokea
nyumbani kwa Abdallah Mustapha hadi kupelekea mimi na Hussein kunyongwa.
“Kikawaida huwa hatuna utaratibu wa wanawake kuingia kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti na kutizama miili, lakini kwa kuwa umeniomba sana, utamwona
ndugu yako.”
“Nitashukuru sana.”
“Uko tayari kuona maiti ya ndugu yako?” mlinzi wa Mochwari alimuuliza Mariam
kwa msisitizo.
“Ndiyo niko tayari,” baada ya jibu hilo kutoka kwa Mariam, ndani ya jokofu, mate
mepesi yakajaa mdomoni, hofu ikanitawala. Wakati huohuo droo ya jokofu
nilimolazwa ikavutwa.

24 | P a g e
Shiiit!!.
Nilijikuta nakosa utulivu ambao nilikuwa nimeutengeneza. Bila kutarajia
nikafumbua macho. Tendo la maiti kufumbua macho mbele ya Mariam na yule
mlinzi wa mochwari iliibua kizaazaa.
“Mamaaaa. Uwiiii!! Maitiiii...Imefufuka..,Waiii...Uwiiii...Mzimu...Mzimuu..”
Mariam na mlinzi yule wa mochwari walipiga kelele huku wakikurupuka na
kuuparamia mlango wa kutokea nje.
Kwa upande wangu nilijitoa ndani ya ile droo ya jokofu nikasimama katika ya
chumba kile nikaona nimezingirwa na maiti nyingi zilizokuwa zimelazwa chini
huku zimefunikwa kwa mashuka meupe.
Wakati huohuo nikasikia kelele nyingi zilizopigwa na Mariam na mlinzi yule
zikishadadiwa na watu wengine huko nje.
Nilibaki nimeduwaa kama teja aliyekosa kidonge cha methadon, katika kuduwaa
huko nikavutiwa na maiti moja iliyokuwa imelazwa chini huku kukiwa na kibao
kidogo kilichowekwa juu ya mwili wa ile maiti kikiwa na maandishi ya kingereza
yaliyosomeka ‘Today buria’
Mpenzi msomaji, hadi leo ninaposimulia mkasa huu nashindwa kuelewa ni
msukumo gani ulionikumba na kufanya kile nilichofanya, kwani pamoja na
kulindima kwa kelele huko nje zenye kushadadia kufufuka kwa maiti ndani ya
mochwari, ndiyo kwanza mimi nilipiga hatua kuusogelea ule mwili, kisha
nikaufunua. Sikuamini nilichokiona.
Kwa mara nyingine nilijikuta nikiduwa baada ya kuona kitu kilichonifanya nihisi
mwili wote ukipata ubaridi. Mpenzi wangu Hussein Jabal alikuwa amelala chali
akiwa amekufa, uso wake ulionyesha kama mtu aliyepatwa na maumivu makali
kabla ya kukata roho.
Shingoni mwake kulikuwa na alama na michumbuko ya kamba iliyomnyongea.
Machozi yalinitoka, donge kavu likanikaba kooni, kwa mara nyingine nilimlaumu
mno Mungu, niliona sitendewi haki kwenye dunia. Maisha yangu yalikuwa
yamevurugika vibaya mno.
Kamasi jepesi lilichungulia kwenye tundu za pua yangu huku machozi yakiendelea
kumiminika mashavuni mwangu.

25 | P a g e
“Mzimu, mzimu, mzimu!!!” ghafla nikashitushwa na kelele zilizoendelea
kulindima kwa kasi ya ajabu kutokea huko nje, hapo akili yangu ikazinduka, bila
kufikiri mara mbili nikachomoka kufuata malango wa kutokea nje na kutoka.
Nilipojitokeza tu nje nikashangaa kukuta mlundo wa watu waliokuwa umbali wa
hatua kama ishirini wakiwa wamezunguka jengo lile la mochwari wakiwa mkao
wa kusubiri kuona mzimu ulioibuka ndani ya mochwari.
Baada ya kujitokeza mbele ya mboni za macho yao nikabutwaa kuona kukizuka
taharuki nyingine ya aina yake.
Kelele na mayowe ya hofu yalilindima huku kila mmoja akishika njia yake, bila
kupoteza muda na mimi nikaanza kutimua mbio bila kujua wapi ninapokimbilia.
Ndani ya nukta hizo hizo nikagundua jambo jingine lililonifanye nizidi
kuchangaikiwa.
Kwenye mwili wangu nilikuwa sina chochote nilicho vaa, nilikuwa uchi wa
mnyama.
Nikazidi kuhamanika, nikageuka na kurudi ndani ya chumba cha mochwari kisha
nikakwapua shuka moja miongoni mwa zile zilizokuwa zimefunika miili ya watu
wengine, nikajifunika na kutoka tena nje.
Nikashika uelekeo wa upande wa kusini mwa hosptali ile, nikawa nakimbia huku
nimejifunika shuka jeupe.
Lile shuka jeupe la mochwari lilinifanya nizidi kufanana dhahili na mzimu,
nilikimbia nikiwa nimechanganyikiwa vibaya sana, katika kukimbia huku na kule
nakajikuta nimetokeza upande wa nyuma wa hosptali ile, eneo lile kulikuwa na
bustani ya mauwa iliyopandwa kiusatadi, bahati nzuri lilikuwa ni eneo ambalo
halikuwa na mtu yeyote.
Kando ya mauwa kulikuwa na pipa la kuhifadhia takataka, nikaamini hapo ndiyo
maficho sahihi kwa wakati ule, nikafunua mfuniko na kutumbukia ndani ya pipa
lile kisha nikajibanza humo.
Nilikuwa nimejikunyata huku nikitweta, nafsi yangu ilikiri kuwa nilikuwa ni kama
mwanakondoo aliyezingirwa na kundi la mbwa mwitu. Sikutaka kujiongepea kama
nikikamatwa tena, nitanusurika kifo kama ilivyo tokea siku hiyo.
Tukio hilo lilinifundisha jambo kubwa kuhusu ukuu wake baba wa mbinguni.
Mungu acheni awe Mungu jamani, utukufu na sifa anastahili yeye. Kama yeye

26 | P a g e
hajakukadiria jambo fulani, hakuna pigo litakalo kuangusha daima. Jifunze hili
ndugu msomaji.
Uhai wangu ulikuwa mashakani, niliamini kama nitaingia kwenye mikono ya
serikali ya nchi ya Oman kamwe hawawezi kuniacha nikiwa hai, niliendelea
kuamini kuwa endapo nitatiwa nguvuni jeshi la nchi hiyo liitahakikisha
ninanyongwa hadi napoteza uhai wangu.
Kiu ya kuwa mtu huru ilizidi kutanda kwenye fikra zangu, shauku ya kurudi
nyumbani Tanzania ilipozidi kutekenya hisia zangu.
Nilikaa ndani ya pipa lile la takataka kwa makisio ilikuwa ni zaidi ya masaa saba
ama nane, eneo lile liliendelea kuwa kimya, sikusikia michakacho wala
chakarachakara yoyote.
Nilijinyanyua taratibu na kuchungulia, nilishangaa nilipona giza lilikuwa
limeingia, nikajivuta na kuruka nje ya pipa lile. Nitembea kuelekea gizani. Wakati
napiga hatua ya kwanza ya pili, nikabaini jambo jingine lisilo la kawaida mwilini
mwangu.
Njaa kali ilikuwa ikiniuma, nikagundua nilikuwa nina muda mrefu sijapata
chochote, na nilikuwa sina nguvu, kukaa sana kwenye jokofu kukanifanya niwe na
kiu cha maji.
Hata hivyo sikutaka kuwaza sana juu ya njaa niliyo kuwa nayo, nilichokuwa
nahitaji ni kurudi nyumbani kwetu Tanzania.
Akili yangu nikairejesha kwenye kujinasua kuingia kwenye mikono ya serikali ya
nchi ya Omani. Nafsi yangu ikakiri kuwa hatua ya kwanza ya kuwa mtu huru
ilikuwa ni kutoka nje ya hosptali ile.
Nikawa natembea kwa kupepesuka lakini kwa umakini wa kutooenekana na mtu
yeyote, mwilini nikiwa nimejifunika lile shuka nililotoka nalo mochwari,
nilitokeza kwenye eneo ambalo lilinipa faraja zaidi, nikaona kwa kutokea eneo lile
ni hatua nyingine muhimu ya kunitoa ndani ya hospitali.
Ilikuwa ni eneo la kufulia nguo na nguo nyingi zilikuwa zimeanikwa katika kamba.
Nilinyata na kuanua gauni moja na mtandio, upesi nikavaa gauni lile na kujitanda
mtandio kisha nikatoka nikiwa natetemeka, miguuni nilikuwa peku.
Nilipishana na watu wawili watatu hapakuwa na yeyote aliyenijali na hatimaye
nikatokeza kwenye geti kuu la hosptali hiyo.

27 | P a g e
Kulikuwa na wanajeshi wenye bunduki waliokuwa wamezagaa kwenye geti lile.
Nilizidi kutetemeka, lakini sikuacha kujongea kuufauta mlango wa kutokea.
Hatimaye nilifika getini na kutoka nje, jasho liliendelea kunitoka huku mwili wote
ukinitetetemeka, hatua ya kwanza....Ya pili...Ya tatu. Mara nikasikia sauti kali ya
kiume ikiniita nyuma yangu.
“Agripina...”
Bila kufikiria mara mbili, nikageuka. lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ulikuwa ni
mtego, hapo hapo nikaona sura za wale wanajeshi zikimakanika bunduki zao
wakazielekeza mbele yangu.
“Nimekwisha!!!!..”
Na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikipata stafutahi ile nilikuwa
nimekwishapata wazo moja ambalo niliamini kama nikiliweka katika uhalisia ni
wazi litaleta matunda na kuweza kutoroka kabisa katika nchi ile na kurudi
nyumbani Tanzania.
Baada ya kushiba nilinyanyuka na kuanza kuyafanyia kazi mawazo yangu, nilitoka
na kutembea kwa mguu3 ukingoni mwa fukwe ile.
Nilifika katika wigo bandari ya Mascut, uliozungushiwa seng’eng’e. Nilisimama
katika uzio wa bandari hiyo nikawa natizma huku na kule kama nitamwona mtu
yeyote.
Wakati huo kwa makisio ilikuwa yapata kati ya saa nne ama saa tano usiku.
Nikaelendelea kusimama kwa muda hadi badae niliposhituliwa na sauti kali
iliyotokea nyuma yangu:
“We ni nani na unafanya nini?” sauti ya amri ilisikika, nilipogeuka nikamwona
mtu mmoja mzee wa makamo kasimama huku akiwa amekamata bunduki aina ya
‘bolt shotgan’ Kimwonekano alikuwa ni kama mlinzi wa eneo lile la bandari.
“Naitwa Agripina, shida yangu ni kupata meli yoyote inayoelekea Afrika. Nisaidie
baba yangu niko kwenye matatizo makubwa. Nitakupa chochote utakacho.”
Yule mlinzi alinitizama kwa chati tochi yake ikiendelea kunimulika, kisha akavuta
pumzi ndefu halafu akasema:

28 | P a g e
“I’ve never seen you in my life but you seem like you need some help...” Aliongea
kwa sauti ya kukoroma, alionekana ni mzee ambaye amekubuhu kwenye biashara
za magendo.
“We have a cargo ship, Zaghol 153 which travels to Mombasa this night. Captain
can take you there in one condition...” aliongea tena kwa Kingereza, akisema ipo
meli ya mizigo ya, Zaghol 153 inayosafiri kwenda Mombasa usiku huu ila nahodha
anaweza kunipeleka kwa sharti moja.
“Sharti lipi?” niliuliza kwa kiherehere.
“Nifuate. ”
Badala ya kunijibu yule mtu alisema huku akifunua wavu wa seng’eng’e na mimi
kupita ndani ya bandari, tukanza kutembea kuingia ndani ya bandari hiyo.
Niliendelea kumfuata huku nikiwa na mashaka, nilikuwa na wasiwasi kwa sababu
niliona kama jambo nililoliomba kwa mtu yule lilikubalika kirahisi mno. Machale
yakawa yananicheza, nikawa njia panda, nilifikiria kwa muda mwisho wa siku
nikajiambia potelea mbali litakalo kuwa na liwe. Nikamfuata.
Alinipeleka hadi kwenye ofisi moja ndogo ambayo ilionekana ni kama ofisi ya
walinzi waliyoitumia kwa kufanyia mambo yao ndani ya bandari ile.
“Ningoje hapa.” Aliniambie yule mzee na kunipa kiti, aliniacha pale na kwenda
mahali ambako sikujua ni wapi, dakika chache badae alirejea na kunitaka nimfuate.
Nilimfuata. Swali kuu kichwani mwangu lilikuwa ni vipi mtu yule ajitoe
kunisaidia mimi kiasi kile, kwa malipo gani? Kwa ushawishi upi? Na kwa huruma
gani aliyonayo juu yangu mtu ambaye nimekutana naye si zaidi ya dakika ishirini.
Pamoja na kuyawaza hayo, bado sikutaka kabisa kurudi nyuma, nilitaka nishindwe
nikiwa kwenye harakati za kujaribu kujiokoa kuliko kuogopa kufanya nikingoja
kukamatwa kibwege.
Agripina, adui namba moja wa maisha yako ni HOFU, sauti moja kichwani
iliniambia.
Safari yetu ilishia kwenye kontena moja ambapo baada ya kuingia ndani
nilishangaaa nilipoona mandhali ya ndani yakiwa ni mithili ya sebule nzuri ya
kisasa yenye kila kitu ndani yake.

29 | P a g e
“Anaitwa Casper ndiye atakaye kusadia kukupeleka kwenu,” alitoa utambulisho
yule mwenyeji wangu.
“Sawa.”
“Mimi naondoka, mambo mengine atakueleza mwenyewe,” yule mlinzi alisema
tena huku akituangalia kwa zamu.
Nilitikisa kichwa kumkubalia, alinyanyuka na kusogea kwa yule jamaa kisha yule
jamaa akatoa burungutu la pesa na kumpa yule mlinzi.
Isije ikawa ndiyo unauzwa Agripina, sauti nyingine iliniambia akilini.
Tulibaki na yule jamaa aliyetambulishwa kwangu kama Casper nahodha wa meli
ya mizigo ‘Zaghol 153’
Tulikuwa kimya kwa dakika nzima, hakuna aliyeanza kumsemesha mwenzake,
jamaa alikuwa bize na sigara zake, akionekana kutokunijali hata kidogo. Hata
hivyo nilibaki kimya nikisubiri niambiwe ni nini malipo ya kusafirishwa kutoka
Mascut hadi Mombasa.
“Una mzigo wowote au ndivyo hivyo ulivyo utakavyo safari?” hatimaye jamaa
aliniuliza.
“Ndivyo hivi nilivyo, sina mzigo”
“Ok, twende kwenye meli.”
Tulitoka ndani ya kontena lile na kupita katikati ya makontena mengi tukipishana
na watu lukuki waliokuwa wakiendelea na majukumu yao mule bandarini.
Safari yetu ikaaishia mbele ya meli kubwa ya rangi ya kijivu, ilikuwa ni meli
kubwa kama mlima. Ubavuni mwa meli hiyo kukiwa na maandishi makubwa
yaliyosomeka ‘Zaghol 153’
Nilijichoma ndani ya meli ile, nikapelekwa kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa
mule ndani nikatulia mule nikingoja kupewa maelekezo mengine.
Saa tisa kamili usiku Meli ile kubwa ilipiga honi kali. Dakika chache badaye
ikaanza kuondoka. Bado nilikuwa siamini kama hatimaye naweza kuiacha nchi ya
Oman, nilisali na kumshukuru Mungu kimoyomoyo.
Nilikuwa nimekaa ndani ya chumba kile juu ya kitanda huku nikijiona ni mwenye
furaha isiyo ya kawaida kwa kuona narejea nyumbani kwetu Tanzania.

30 | P a g e
Nikifika Mombasa, Kenya ni kama tayari nimefika Tanga, Tanzania. Siwezi
kuisahau hii Oman. Nilijiambia kimoyomoyo.
Nakumbuka nilikaa ndani ya chumba kile ndani ya Meli kwa masaa mengi mno
hadi usingizi ukanipitia, nililala masaa mengine mengi mno hadi nilipo amshwa na
njaa kali.
Kwa mujibu wa saa ya ukutani iliyokuwa mule ndani ilikuwa ni saa sita mchana
wa siku mpya. Njaa ilikuwa inaniuma mno.
Hadi wakati huo bado Casper hakuwa ameniambia ni jambo gani nitakalo stahili
kumlipa kama malipo ya kunisafirisha Mombasa.

Nikiwa bado natafakari mara mlango wa chumba kile uligongwa kiustarabu, na


kuvaa nguo, kisha nikauendea mlango na kuufungua. Alikuwa ni Casper.
Alikuwa amesimama sigara ikiwa mdomoni mwake, mkononi akiwa ameshika
sahani lililokuwa na chakula aina ya British Beef and Ale na glasi yenye sharubati
nzito ya nanasi.
“Nimekuletea chakula,” alisema huku akitoa moshi wa sigara katika tundu za pua
yake. Nilipokea chakula kile huku nikitoa tabasamu lililosema ahsante kwa wema
wako.
“Kula, ukishiba tutazungumza,” alisema tena Casper.
Nilikula upesi upesi, baada ya kushiba nikaketi kitako kumsikiliza yule jamaa.
“Kwa nini unakimbia Oman kwa kujificha...Umeua?” Casper aliuliza.
Swali lilikuwa kama mjeledi wa moto kifuani mwangu mate mepesi yalinijaa
mdomoni nikapatwa na kigugumizi. Na hata kabla sijajibu akasema tena:
Hata hivyo siyo kazi yangu kujua kwa nini unakimbia nchi ile ya kishenzi ya
Kiarabu, kazi yangu ni kukupeleka unakotaka kwa malipo ya penzi tu.”
Kwa mara nyingine nilibaki tena nimeduwaa baada ya kauli hiyo. Nilijiona ni
mjinga kwa kutohisi jambo lile kama linaweza kunitokea.
Nilibutwaa baada ya Casper kuanza kunishikashika matiti yangu yaliyokuwa
wima, vidogo dogo kama vipera.

31 | P a g e
Akawa ananivutia kwakwe, macho yake yakionesha ananjaa kali ya penzi.
Nilendelea kuduwaa nisijue kama nilitakiwa kukataa ama kukubali.
Ningewezaje kumkatalia mshenzi yule ilihali ni yeye alikuwa ameshikilia hatma ya
maisha yangu, nilikuwa kwenye himaya yake, angeweza kunifanya chochote hata
kunitosa baharini.

Casper akaendelea kunibinyabinya matiti huku pumzi zikimtoka kwa kasi.


Akanivua gauni, nikabaki na nguo ya ndani, niliendelea kuganda kama sanamu
machozi yakijikusanya machoni.
Mara akavua surauli yake harakaharaka kama anakimbizwa, nikaona kitu cha ajabu
kwenye sehemu zake za siri.
Hatimaye nilifika getini na kutoka nje, jasho liliendelea kunitoka huku mwili wote
ukinitetetemeka, hatua ya kwanza....Ya pili...Ya tatu. Mara nikasikia sauti kali ya
kiume ikiniita nyuma yangu.
“Agripina...”
Bila kufikiria mara mbili, nikageuka. lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ulikuwa ni
mtego, hapo hapo nikaona sura za wale wanajeshi zikimakanika bunduki zao
wakazielekeza mbele yangu.
“Nimekwisha!!!!..”
Ndani ya sekunde chache amri kutoka kwa mwanajeshi mmoja ilitoka:
“Kamata! Huyoo ndiye yeye, msimwache akatoroka..” sikupoteza muda hapo
hapohapo nikakurupuka na kutimua mbio.
“Paaaaaaa!..PAA!”
Sauti kali ya risasi ilisikika nyuma yangu, Kukazuka kizaazaa kingine , watu
wachache waliokuwa eneo lile la lango la hospitali kila mtu akashika njia yake
huku sauti za taharuki zikiwatoka.
Nilifahamu wazi risasi ilikuwa imepigwa angani ili kunitisha nisikimbie, nilikuwa
tayari kufa nikiwa nakimbia nikijaribu kujiokoa kuliko kusimama kisha nikatiwa
nguvuni kikondoo.

32 | P a g e
“Simama wee mwanamke Simamaa!!” sauti za amri zilizidi kunishurutisha.
Sikujali nilizidi kukimbia kwa nguvu zangu zote, nilibahatika kuona kichochoro
mbele yangu, mita kama kumi, nikaona pale ndiyo mahali sahihi pakuwapoteza
wale mafala waliokuwa wakinifuata nyuma yangu kwa kasi.
Kwa mbio za farasi, nilikifikia kile kichochoro na kutokomea ndani yake,
nikakutana na mazingira ambayo yalizidi kunipa nguvu ya kukimbia. Nilikuwa
ndani ya makazi ya watu hohehahe kwetu Tanzania hupaita ‘Uswahilini’ Nikapita
kwenye vichochoro viwili vitatu, hatimaye nikajikuta nimetokea katika eneo
ambalo halikuwa na njia.
Risasi zilizidi kulindima nyuma yangu.
Nikatazama kulia kwangu nikajiona nipo katika nyumba eneo la uwani, nikaona
kuna vyumba kadhaaa katika eneo lile la uwani vikiwa wazi. Nikakimbia na
kuingia kwenye chumba kimoja.
Nilisukuma mlango kwa nguvu na kuzama ndani kisha nikaufunga. Kwa
mwonekano chumba hicho kilikuwa kikikaliwa na mvulana wa Kiarabu. Naye
alikuwemo humo ndani!.
Bahati nzuri ni kwamba, amelala fofo! Alikuwa mwanaume mrefu na mwenye
nywele nyingi kichwani.
Pamoja na kwamba nilisukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani kwa fujo
lakini mtu yule aliyekuwa amelala fofo hakushituaka!. Nilijikunyata nikiwa
nahema kama nimetoka kwenye mbio za marathoni.
Ukimya wa ghafla ukashika hatamu. Sauti za risasi huko nje sikuzisikia, Nikawa
najiuliza maswali mwenyewe mule ndani kama natakiwa nitoke ndani ya chumba
kile nitimkie mahali pengine ama niendelee kubaki mule ndani hadi hapo
mwenyeji wa chumba kile aliyekuwa akikoroma kitandani atakapo amka na
kunikuta mule ndani.
Katika kuwazawaza huko nikapata wazo ambalo niliamini ni zuri. Bahati mbaya
bado kivuli cha bundi kiliendelea kunifuata, kwani kabla sijalifanyia kazi wazo
langu mara nikashuhudia kitu cha ajabu.
Yule mtu aliyekuwa amelala kitandani alikuwa anatoa mkoromo usio wa kawaida,
nikasimama na kumtizama.
Sikuamini kile nilicho kiona.

33 | P a g e
Mtu yule alikuwa akitokwa damu puani, masikioni na mdomoni damu ile
ilichanganyika na povu lililokuwa likimtoka mdomoni.
“Ngo ngo ngo...” ndani ya sekunde hizohizo nikisikia mlango wa chumba kile
ukigongwa kwa nguvu!.
Nilibaki nimeganda kama sanamu, nilihisi akili yangu ikisimama kufanya kazi kwa
muda, wakati nikiwa nimeduwaa mbele ya mtu yule aliyeonekana yupo kwenye
hekaheka za kuipigania roho yake nikashitushwa tena na sauti kali ya mlango
ukigongwa.
Hapo ni kama akili yangu ilikurupuliwa ilipokuwa imelala, nikatambua hatari
iliyokuwa inaninyemelea.
“Ngo,ngo,ngo!..Open the door..” Sauti ya mtu ilisikika ikisema kwa wahaka huku
akiendelea kuugonga mlango kwa nguvu, jasho lilinichuruzika maungoni mwangu,
nikaona hatimaye ninaingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Oman, sikutaka
kujiongopea kwamba siwezi kuhusishwa na kifo cha yule jamaa aliyekuwa
akiweweseka kitandani huku damu ikimtoka puani na mdomoni.
Nikaamini kabisa hilo ni jumba bovu jingine linalokwenda kuniangukia,
nikajionya kama nisipofanya kitu lazima nitaingia kwenye mikono ya serikali na
sikuhitaji mwalimu wa kunieleza kuwa kama nikingia kwenye mikono ya dola nini
kitatokea.
“Ngo,ngo,ngo...”
Mgongaji aligonga tena safari hii kwa nguvu zaidi, nikatizama kulia na kushoto
nikaona mahali pekee pakujificha ni kuingia chini ya uvungu wa kitanda. Lakini
kabla sijazama uvunguni mara mlango ulisukumwa kwa nguvu na ukafunguka.
Aliingia msichana mmoja wa kiarabu akanikodolea macho yenye mshangao kisha
akayahamisha macho yake kwa kwa mvulana aliyekuwa hoi pale kitandani,
nikamwona akibutwai baada ya kuona hali ya yule mtu pale kitandani.
Nilikuwa nimesimama nikiendelea kumwangalia yule dada namna alivyo taharuki
kwa kile alichokuwa akikishuhudia mbele yake, nikawa makini na yule msichana
kufuatilia kila tendo alilokuwa akifanya, akayatupa macho yake tena kwangu,
akanitizama kwa chati kisha akasema kitu, lakini sikumwelewa kwakuwa
alizungumza kwa lugha ya Kiarabu.

34 | P a g e
Ingawa sikumwelewa lakini nilibaini alichokuwa ananiuliza ni nini. Alitaka
kufahamu mimi ni nani,kwa nini nipo mule ndani na nimemfanya nini mtu yule
anayetokwa na damu nyingi.
Kitendo cha mimi kubaki kuwa bubu huku yeye akiniuliza maswali lukuki
kilimkera vibaya sana yule msichana, nikaona anatoa simu yake ya mkononi kisha
akapiga namba fulani na kuanza kuzungumza na mtu upande wa pili. Sikutaka
kujiongopea kwamba haiti polisi.
Machale yakanicheza, hapohapo nikamrukia na kumkwapua ile simu na kuitupa,
baada ya kufanya kitendo kile kilichofuata kilikuwa hakielezeki, tulikamatana na
yule msichana na kuvingirishana huku na kule, pamoja na kwamba nilikuwa na
njaa lakini niweza kumthibiti msichana yule.
Nilimvuta nywele nikamkandamiza kwa chini huku nikiwa nimemkanyaga kifuani.
“Kimyaa!! nasema kimyaa, nyau wewe nani aliyekwambia uite polisi? Umeniona
mimi ndiyo nimemua huyu fala wako aliyelala hapa kitandani...Eeh?” nilisema
kiwazimu nikiwa nimevurugwa vibaya sana.
Nilichofanya ni kumfunga kwa kamba mikono na miguu yake kisha nikamsachi
mifukoni mwake, nikamkuta na kiasi cha fedha ambazo sikumbuki zilikuwa ni
shilingi ngapi, nilizikomba pesa zote nikiamini zitanisaidia mbele ya safari, baada
ya tukio hilo niliyatupa macho yangu kwa yule bwana pale kitandani.
Nilichanganyikiwa baada ya kumwona mtu yule akiwa amekodoa macho huku
akiwa ahemi. Mtu yule alikuwa amekwisha fariki dunia...
“Hapanifai tena hapa”
Sikupoteza muda, niliondoka mule ndani upesi nikimwacha yule binti akijizoazoa
pale sakafuni, niliingia mtaania na kuendelea kukimbia, niligeuka kuwa mkimbizi
katika nchi ya watu.
Nakumbuka baada ya kutoka mule ndani nilichofanya ni kwenda katika hoteli
iliyokuwa mafichoni kidogo, ilikuwa karibu na pwani ya bahari, haikuwa hotel ya
kitalii ila nakumbuka jina la hotel hiyo iliitwa ‘Kuruthumu’ ingawa ilikuwa ni
usiku nilipata stafutahi ya chai ya maziwa na mkate wa siagi ambao kwa hakika
ulijaza tumbo langu.
Na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikipata stafutahi ile nilikuwa
nimekwishapata wazo moja ambalo niliamini kama nikiliweka katika uhalisia ni

35 | P a g e
wazi litaleta matunda na kuweza kutoroka kabisa katika nchi ile na kurudi
nyumbani Tanzania.
Casper akaendelea kunibinyabinya matiti huku pumzi zikimtoka kwa kasi.
Akanivua gauni, nikabaki na nguo ya ndani, niliendelea kuganda kama sanamu
machozi yakijikusanya machoni.
Mara akavua surauli yake harakaharaka kama anakimbizwa, nikaona kitu cha ajabu
kwenye sehemu zake za siri.
Sehemu zake za siri zilikuwa kubwa na zilikuwa wima kama mnara wa mashujaa
wa vita ya pili ya dunia, zilikuwa zimekakamaa huku zikinitizama kwa uchu.
Kwenye mdomo wa mnara huo kulitoka chozi la uchu. Jamaa akawa anahema kwa
tabu, mzimu wa ngono ulikuwa ushampanda vibaya sana.
Hatimaye akawa ananiingilia kimwili. Sikuhisi chochote zaidi ya maumivu makali
sehemu zangu za kike. Kwa lugha nyepesi naweza nikasema alikuwa akinibaka.
Alinibaka, akanibaka na kunibaka, alinifanya anavyotaka mpaka hamu yake
iikakwisha.
Alipotoka juu ya mwili wangu nilikuwa nahisi kama nimetiwa kwenye bani ya
kukaishia tumbaku. Koo lilinikauka.
Sikuwa na la kufanya kwakuwa kitu nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ni
kurudi nyumabni kwetu Tanzania, nilikubaliana na udhalilishaji wote sanjari na
maumivu yote yatakayo nisibu ilimradi nifikishwe nyumbani.
“Bila shaka utanifikisha nyumbani salama, ” nilisema kwa sauti ya upole mbele ya
yule mwanayme mwenye asili ya Kigiriki.
Alinitizama kwa chati kisha akasema:
“Nina kisasi na wanawake wote kwenye hii dunia, sijawahi kumpenda mwanamke
yeyote tangu nilivvyopata akili. Tangu nilipogundua viumbe hao walinifanyia
mambo ambayo sikupaswa kufanyiwa niliwachukia mno.
Niliapa kuwaliza na kuwaumiza kisha kuwamaliza popote watakapo ingia kwenye
anga zangu...”
Aliwasha sigara yake, akavuta na kunipulizia moshi mwingi usoni mwangu huku
akinitizama kama kikaragosi. Akaendelea kusema:
“Hadi sasa nimekwisha ua mademu wengi na bado nina kiu ya kuua zaidi. ..”

36 | P a g e
Alivuta tena, akaendelea kuongea.
“Hata wewe tayari nisha kuua....”
“Casper!!!” nilimaka.
“Kwa nini unaongea maneno hayo mbona unanitisha..”
“Sikiliza we’ mbwa mwanamke. Hapo ulipo tayari nishakuambukiza Ukimwi na
kwa taarifa yako siwezi kukusafirisha hadi huko unakotaka kufika. Umebakiza
muda mfupi wa kuendelea kuishi kwenye hii dunia, kitu cha msingi ni kusali sala
zako za mwisho...”
Toba!!
Ilikuwa ni kama ndoto mbaya ya kutisha inayonipitia nikiwa nimelala usingizini.
Nilitamani iwe hivyo ili nishituke na kujikuta kitandani, chumbani mwangu huko
kijijini kwetu Makose maisha yangu ya upendo na amani yakiendelea kama
kawaida.
Pamoja na umasikini ulizingira familia yangu na nchi yangu, lakini amani na
upendo wa Tanzania yangu ilikuwa ni tunu niliyoitaka kwa udi na uvumba katika
maisha yangu ya kusaka fedha kwenye nchi za watu.
Nilijikuta nikianza kulia kama mtoto aliyetelekezwa na mamaye, mambo
aliyonieleza mzungu yule, Gaspaer, yalikuwa ya kutisha mno.
“Umeniambukiza Ukimwi!!!”
“Ndiyo nimekupa Ukimwi kwa makusudi,” alisema huku tabasamu la kifedhuli
likimtoka usoni mwake.
“Kwa nini lakini! Eeeh! nilikukosea nini kwenye maisha yako mimi.”
“Kimya!!Kenge wewe, kimya unamlilia nani hapa fala wewe!.”
“ Umeniambukiza Ukimwi!!!”
"Nasema kimya we’ mtu mweusi huelewi...Alaa!”
“Nimekukosea nini?” niliendelea kulalama huku mifereji ya machozi yakilowesha
mashavu yangu.
“Nikwambie mara ngapi mbwa wenzio wanawake, walinifanyia mambo mabaya
maishani. Na nikwambie mara ngapi niko kwenye oparesheni ya kulipa kisasi kwa
mbwa wote wa kike!!!!!” aliongea kwa kuofaka vibaya sana.
37 | P a g e
Ghafla hali ya hewa mule ndani ilichafuka, yule jamaa alitoka akiwa na hasira
dhidi yangu, nilimwona mtu yule kama alipandwa na majini kichwani mwake,
sikutegemea kabisa kwa ukarimu alionionyesha awali kama angeweza
kunibadilikia muda mfupi kiasi kile.
Nilibaki chumbani nikilia kwa uchungu, kwakweli sikujua nini hatma ya maisha
yangu, kwa dakika zile chache nilijikuta nikikata tamaa vibaya mno, sikuona
thamani ya uhai kwenye huu ulimwengu, kitendo cha kuambukizwa UKIMWI
kiliniuma mno.
Nikiwa sijawa vizuri kiakili mara Casper akarudi akiwa kama mbogo
aliyejeruhiwa na jangili kwa risasi.
“Toka toka humu ndani toka...” alisema huku akinisukuma, alikuwa kifua wazi,
mkononi alikuwa ameshikilia kamba pamoja na kisu chenye makali.
Nilitoka nje, nikiwa nimeghafirika kwa tukio hilo. Nje nilikutana na watu wengine
ambao kwa mwonekano walikuwa ni wafanyakazi wa meli ile, walionekana ni
watu wenye kumwogopa sana Casper.
“Mfunge kamba huyu mwanamke mbwa.” Amri ilitolewa na Casper, upesi vijana
wale walinidaka kama sungura dhidi ya kundi la mbwa mwitu wenye njaa.
Walininifunga kamba miguu na mikono, haikuishia hapo, walinifunga mwilini na
chuma kizito.
Nilitambua nini kinacho kwenda kutokea. Kutupwa baharini nikiwa nimefungwa
mikono na miguu, sanjari na chuma kizito mwilini wangu.
Nilikuwa kiumbe mwenye bahati mbaya kwenye maisha, nilizaliwa kwenye
familia masikini na nimekuwa ndani ya umasikini huo kwa muda mrefu, katika
kipindi ambacho niliamini nakwenda kubadilisha historia ya maisha yangu mara
mambo yanabadilika kwa kufanya kosa dogo sana, ambalo limeniletea majanga
mazito na yenye kuogopesha.
Machozi yalinibubujika, picha ya familia yangu ilijitengeneza kichwani mwangu,
hasa nilipogundua nakwenda kufa pasina wao kuona mifupa yangu.
Siku zote familia yangu itakuwa na amani kwa kuamini mtoto wao niko nchini
Oman nikifanya kazi za ndani na mwisho wa siku nitarejea nyumbani na
kubadilisha hali ya maisha ya nyumbani.

38 | P a g e
Nikaendelea kuona taswira ya wazazi wangu watakapo kaa kwa muda mrefu bila
kunipata na kuamua kufuatilia kwa wakala aliyenipeleka Oman, wataambiwa
nilikutwa na misukosuko ya kifo kabla ya kufufuka mochwari, baada ya hapo
watambiwa nilitokomea kusiko julikana.
Niliyaona machozi ya wazazi wangu, niliona mfadhaiko mkubwa nyoni mwao,
mimi nilikuwa mtoto wa pekee na nguzo yao ya badaye. Hawatoona japo unywele
wangu daima dumu.
Niliumizwa na nililia sana juu ya hilo, uchungu uliokuwa kifuani kwangu ulikuwa
haumithiliki, niliamini mambo yote hayo chanzo chake ni umasikini na sasa
nilikuwa nikionja chungu ya umasikini.
Mpenzi msomaji pengine haya ninayo simulia leo unaweza kuona ni kama riwaya
za kubuni, amini nakwambia, mambo yote haya yemenitokea na hakuna hata moja
la kubuni wala kuongeza chumvi.
Nikiwa nimejinamia, nimfeungwa kamba na chumba mwilini, mara nikashitushwa
na sauti ya Casper ikisema:
“Mtupeni baharini huyo mbwa mwanamke.....wanawake wote duniani ni mbwa,
hadi mama yangu mzazi, naye ni mbwa, tena mbwa koko...” mwendawazimu yule
aliongea.
Hapohapo wakanibeba juu tayari kunitosa baharini, wakawa wanasogea ukingoni
mwa meli tayari kwa kunibwaga majinii. Niligeuka kuangalia chini nikaona bahari
ikiwa na mawimbi mazito yaliyokuwa yakijipiga katika kuta za meli ile kubwa na
kutawanyika kila mahali.
Nikaona ubuluu wa maji, nikabaini kuwa sehemu ile ilikuwa na kina kirefu.
Agripina mimi sikuwahi kujua kuogolea ingawa hata kama ningekuwa najua
kuogelea bado nisingeweza kufanya lolote kwani mikono na miguu yangu ilikuwa
imefungwa kwa kamba huku shingoni nikiwa nimefungwa kwa kamba nyingine
iliyo unganishwa na chuma kizito.
“Moja...mbili...” wale jamaa walihesabu”
“Tatu.. twendee!”
Hapohapo wakanirusha baharini! Nilijibamiza kwenye maji ‘pwaaa’ maji yakaruka
na kusambaa kila mahali, nikaanza kuzama kuelekea chini huku nikinywa vikombe
kadhaa.

39 | P a g e
“Moja...mbili...” wale jamaa walihesabu”
“tatu.. twendee!”
Hapohapo wakanirusha baharini! Nilijibamiza kwenye maji ‘pwaaa’ maji yakaruka
na kusambaa kila mahali, nikaanza kuzama kuelekea chini huku nikinywa vikombe
kadhaa.

nilikuwa siwezi kufurukuta kwakuwa chuma kizito kilikuwa kimefungwa shingoni


mwangu, mikono na miguu ikiwa imefungwa kwa kamba, nilipojaribu kuvuta
hewa kwa ndani nikajikuta navuta maji mengi puani na mdomoni tendo hilo
likanifanya nianze kutapatapa kwa namna halisi ya mfa maji.
Nilibwia vikombe vya maji huku nikiwa sipati pumzi, hatimaye nikawa nazama
kwa kasi kuelekea chini kabisa ya bahari, sikuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri
mauti, nafsi yangu ilikuwa tayari kabisa kufa.
Nilibwia vikombe vya maji nikiwa sipati pumzi, nikaanza kuliona giza la ajabu
mbele yangu, hatimaye sikujua tena kilicho endelea. Na kabla sijajua kilicho
endelea nafsi yangu ilikiri kwamba mimi tayari ni maiti.

40 | P a g e
SURA YA NNE

“JINA lako nani?”


“Nani?”
“Wewe hapo..”
“Jina langu....jina langu... jina langu, nimelisahau!!!!”
“Pole sana binti”
“Pole ya nini?”
“Umeokolewa na wanajeshi wa majini waliokuwa katika nyambizi
baharini...Unaijua Nyambizi?
“Sijui, ni kitu gani?”
“Nyambizi ni manowari, zinazotembea chini ya maji kama samaki, wanajeshi wa
UN kutoka Ujerumani, walikuwa wanasafari na nyambizi hiyo kwenda Syria, ndio
walioyaokoa maisha yako ukiwa katika hatua za mwisho.”
Yalikuwa ni mazungumzo ya daktari mmoja akiongea na mimi niliyekuwa
kitandani.
Kauli ya mwisho ya daktari huyo ndiyo iliyofungua milango ya kumbukumbu
zangu, mtiririko wa kumbukumbu zilianza kujaa kwenye kichwa changu mithili ya
simu iliyokuwa imezimwa data kwa muda mrefu na sasa imefunguliwa.
“Mungu wangu!”nilimaka.
“Nini?”
“Nimekumbuka kila kitu...”
“Kweli?”
“Kabisa.”
“Haya sema, jina alako unaitwa nani?”
“Naitwa Agripina”
“Kwa nini ulitupwa baharini?”

41 | P a g e
“Ni stori ndefu, ila nataka kujua hapa niko wapi?”
“Upo hosptali ya Ahlal Bayty mjini Mascut.”
“Unataka kuniambia nimerudi nchini Oman?”
“Hujarudi ila umeletwa na wanajeshi wa kulinda amani nchini Syria”
Nilishindwa kuelewa kama nilitakiwa kufurahia ama kulia, nchi ya Omani kwangu
ilikuwa siyo sehemu rafiki, sikutamani kabisa kuendelea kuishi juu ya mgongo wa
ardhi ya nchi hiyo.
Pamoja na kufikiria yote hayo mwisho wa siku nilimshukuru Mungu kwa
kuendelea kuonyesha miujiza ya ajabu kabisa kwenye maisha yangu na kunifanya
niendelee kuwa hai.
Nililala pale kitandani kwa masaa mengi hadi badaye aliporudi tena yule daktari
niliyekuwa nikizungumza naye.
“Ulisema jina lako unaitwa Agripina?”
“Ndiyo” nilijibu kisha nikamwona akiandika kwenye kitabu chake kidogo na
kuondoka.
Akaondoka, kama dakika kumi akarudi tena akiwa ameongozana na watu wengine
wawili mwanaume na mwanamke. Wakaja na kukizunguka kitanda changu.
“Agripina” aliniita.
“Abee”
“Unamfahamu huyu dada?” alisema akimsonta binti aliyeingia naye mule ndani.
Nilipo mtizama vizuri yule binti nikamkumbuka.
Ni msichana ambaye siku moja alinikuta ndani ya chumba nilichokimbilia
kujificha nikiwa nakimbizwa na wanajeshi, baada ya kuzinduka mochwari.
Katika maficho, nilimkuta mwanaume anayekaribia kukata roho, ambapo muda
kidogo akaja huyo msichana, kutokana na mazingira tete aliyonikuta nayo binti
huyo wa kiarabu, moja kwa moja akaamini nahusika na kifo cha mtu ambaye
inasemekana alikuwa ni kaka yake..
“Nishamkumbuka”

42 | P a g e
“Basi upo chini ya ulinzi kwa makosa ya mauaji ya kaka yake, lakini pia kwa
makosa mengine ya kutishia kuua na kufanya zinaa ndani ya nchi hii,” alidakiza
yule jamaa mwingine aliyeongozana na daktari.
Alitoa pingu na kunifunga. Angalau safari hii sikuwa na hofu hata kidogo, matukio
na mikasa kwenye maisha yangu ilinifanya kuwa na moyo mgumu kama jiwe,
kuna wakati kufa, niliona ni kitu cha kawaida. Muda wowote naweza kufariki. Ni
kawaida. Nilichokuwa nangoja kwa wakati huo ni siku muda tu mauti.
“Nafikiri hutakiwi kuendelea kulalia kitanda cha hosptali hii, utatakiwa kupelekwa
selo kisha mahakamani, badaye utumikekie adhabu ya makosa yako,” alisema tena
yule ofisa, ni kama naye alikwisha nihukumu kabisa bila kuthibitisha.
Nilichukuliwa na kupelekwa selo, haikuwa selo ile ambayo niliwahi kupelekwa
kipindi cha nyuma. Hii ilikuwa ni tofauti. Hii ilikuwa ni selo ambayo haikuwa na
tofauti na zile za nchini kwetu. Na nilichokikuta ndani ya selo hizo niliogopa sana.
Kulikuwa na utitiri wa wasichana wa Kitanzania ambao walikuwa ni mahabusu na
wafungwa wenye mashitaka mbalimbali wengine walisha hukumiwa kifo huku
wengine wakiongoja hukumu. Wengi wao walikuwa ni wasichana waliokwenda
kufanya kazi za ndani.
Pamoja na hali hiyo ya kutisha, kwa mara ya kwanza nilijihisi siko peke yangu
katika ulimwengu, kitendo cha kukutana na Watanzani wenzangu ambao wengi
wao walikuwa ni wenyeji wa Zanzibar, Tanga, Singida na Dar es salam ilinipa
faraja kubwa. Waswahili husema, kifo cha wengi harusi.
Mara nyingi tulikaa pamoja na kuzungumza mambo mengi ya nyumbani Tanzania.
Kila mtu alikuwa na kiu ya kurudi nyumbani lakini hilo lilibaki kuwa ndoto ya
mwendawazimu nyuma ya milango ya nondo.
Siku chache badaye, nilipelekwa mahakamani, sikuwa na imani na mahakama za
nchi hiyo, namna kesi zilivyo endeshwa kwakweli zilimnyima mtuhumiwa haki ya
kijitetea kwa kiwango kikubwa, na hili ilikuwa hsa kwa watu weusi.
Hata balozi zetu huko, hazijali watu wake, zimevaa miwani nyeusi na kujifanya
haijua wala kuona madhila wanayoyapata ndugu zao. Kuna wakati niliandika barua
ubalozini kuomba msaada wa mwanasheria ambaye ataninusuru na kitanzani.

43 | P a g e
Hata hivyo, sikupata majibu hadi siku ya hukumu. Ubalozi wa nchi yangu ulitupa
kisogo kwa asilimia kubwa. Hatukuthaminiwa kama ambavyo raia wa kigeni
wanavyothamaniwa na balozi zao nchini mwetu.
Nilihukuwa kifo. Hakimu alisema ilisema, Kwa kuwa nilishawahi kunyongwa na
mahakama za kijeshi kwa kamba, nikarudiwa na fahamu nikiwa mochwari, safari
hii nilihukumiwa kuchomwa sindano ya sumu hadi kufa.
“Haki pekee anayopewa mshtakiwa ni mwili wake kusafirishwa nchini kwao ama
kijijini kwao kwa ajili ya mazishi yake.” Alisema, kisha akagonga nyundo mezani.
Nilishukuru japo kwa hilo kwani niliona angalau sasa ndugu zangu watapata fursa
ya kuona maiti yangu na kuzikwa kwenye ardhi ya nchi yangu. Kama nilivyosema,
nafsi yangu haikuogopa kufa, ila kilichoniumiza ni kufa nikiwa na mtoto tumboni,
hilo liliniliza machozi.
Nilishukuru japo kwa hilo kwani niliona angalau sasa ndugu zangu watapata fursa
ya kuona maiti yangu na kuzikwa kwenye ardhi ya nchi yangu, nafsi yangu
haikuogopa kufa, ila kilichoniumiza ni kufa nikiwa na mtoto tumboni, hilo
liliniliza machozi.
“Usilie Agripina ndivyo maisha yalivyo, hujafa hujaumbika” mtu mmoja
mwenyeji wa Kigoma alinipa moyo.
“Silili kwa sababu ya hukumu, namlilia mwanangu aliye tumboni”
“Una mtoto tumboni?”
“Ndio.”
“Nafikiri huwezi kutumikia adhabu ya kifo hadi pale utakapokuwa umejifungua
mtoto.”
“Labda ngoja tusubiri,” nilisema kinyonge huku matone ya machozi yakijikusanya
kwenye macho yangu.
Siku, wiki na miezi ikayoyoma, niliendelea kuishi ndani ya gereza kama mfungwa
ninayesubiri siku ya kutumikia adhabu yangu ya kifo. Wakati nikingoja siku ya
hukumu pia tumbo langu lilizidi kuwa kubwa.
Siku moja nikafuatwa na askari magereza walikuwa kama sita, mikononi mwao
walibeba bunduki. Walinizunguka huku wakionekana kuwa makini na mimi,

44 | P a g e
mmoja miongoni mwao akanisogelea na kunieleza ilibaki wiki moja tu kabla ya
kutumikia adhabu yangu ya kifo.
Nilihisi mate mepesi yakijaa mdomoni, pamoja na kwamba nilikuwa sina hofu
dhidi ya kifo lakini kwa mara ya kwanza nikahisi mwili ukinisisimka, hofu
ikanisambaa kifuani mwangu, taswira ya tukio la mtu kunyongwa likajitengenza
kwenye akili yangu, kwa kweli niliogopa mno.
Walipoondoka wale askari, wafungwa wenzangu walinifuata na kuniuliza nilikuwa
naambiwa nini. Niliwaeleza yote nilioambiwa na wale askari wa kiarabu, simanzi
na hofu ilienea katika nyuso za wafungwa hasa Watanzania wenzangu ambao pia
walihukumiwa kifo.
“Ndiyo maana wameanza kuwa makini na wewe, kuanzia leo unaweza usiwe na
sisi tena ndani ya selo. Siku za mfungwa kunyongwa zikikaribia huwa anawekwa
mbali na watu kwa imani kwamba anaweza kufanya lolote dhidi ya mtu yeyote ili
mradi asife peke yake,” alisema mfungwa mmoja miongoni mwa waliokuja kunipa
pole.
Saa kumi na mbili jioni nilijiwa tena na wale askari wenye bunduki, kama
alivyonieleza yule mfungwa mwezangu nilihamishwa na kupelekwa katika selo ya
peke yangu. Niliingizwa kwenye chumba kimoja kizuri ambacho kilikuwa na kila
kitu cha thamani, chumba hicho kilikuwa ndani ya jela hiyo.
Sikujua mantiki ya kuingizwa kwenye chumba nadhifu ingawa wakati mwingine
nilihisi hizo ni itifaki za kumkirimu mtu ambaye hukumu yake ya kifo ipo jirani,
hata hivyo wakati mwingine nilipingana na fikra hizo kwa kuwa mwanzoni
nilipohukumiwa kifo, sikufanyiwa ikhisani ya mambo haya.
Niliishi ndani ya chumba kile nadhifu, kila siku nikiletewa vyakula vizuri ambavyo
nafikiri vingine sijawahi kuvila hadi leo ninaposimulia mkasa huu. Wiki ile moja
ilienda harakaharaka, hatimaye siku ya hukumu ikafika.
Walikuja askari wenye bunduki na kunitoa nje ya chumba kile, nilifungwa
minyororo miguuni, mnyororo huo ukaunganishwa na shingo yangu ukapita hadi
mikononi, kisha nikavikwa soksi nyeusi usoni.
Nilishikwa bega kwa nguvu na askari mmoja miongoni mwa waliokuwa
wamenizunguka huku mkono mmoja wa askari yule ukiwa umekamata silaha yake
vizuri.

45 | P a g e
Akawa ananiongoza na kunipeleka mahali nisikokujua, mapigo yangu ya moyo
yakawa yananidunda “duk duk duk” nikaanza kutokwa jasho mwilini, hofu ya kifo
ikawa kubwa, hatimaye nikaanza kulia, machozi na kamasi vilinitoka ndani ya ile
soksi nyeusi iliyofunika uso wangu. Hata hivyo hakuna aliyejali hilo..
Nilifikishwa ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na baridi kali kisha
nikaondolewa ile soksi usoni, nikashangaa nilipojikuta nipo ndani ya mochwari,
moyo wangu ukalipuka “paaa” niliogopa.
Ndugu msomaji hapa ngoja niseme kitu. Hakuna hukumu mbaya ambayo
inavuruga saikorojia ya mtu kama hukumu ya kifo, kama wadau wa sheria
watapata bahati ya kusoma maandishi haya ni vema wakafanyia marekebisho
sheria hii katika taifa letu, kwani sheria hii inamtafuna binadamu kisaikolojia kabla
ya kuitumikia.
Baadhi ya nchi za ulaya na Marekani, sheria ya hukumu ya kifo haipo kidogo na
baadhi ya nchi za Afrika, lakini kwa bara la Asia bado sheria hii inaendelea kutesa
saikolojia ya binadamu kwa kiwango kibaya sana.
Baada ya kujiona nipo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti nilianza kuhisi
kizunguzungu, maiti nyingi zilikuwa zimetapakaa chini huku zikiwa zimefunikwa
kwa mashuka meupe, kulikuwa na harufu kama ya jiki (ile dawa ya kuondoa
madoa), nikatambua hiyo ni dawa ambazo maiti zile zimedungwa kwenye miili
yao ili pengine zisiharibike.
Nafsi yangu ikazidi kuzongwa na jinamzi la hofu baada ya kubaini kuwa kumbe na
mimi dakika chache nitakuwa maiti kama zile zilizolazwa pale chini kisha
nitachomwa sindano yenye dawa ambayo ina harufu ya jiki kisha nitalazwa chini
na kufunikwa shuka jeupe nikingoja kuzikwa.
“Mlazeni juu ya kitanda” alisema daktari huku akivuta sumu kwa kutumia sindano
kwenye kichupa kidogo.
Nilishikwa na askari wawili nikalazwa juu ya kitanda, nikawa nimelala chali,
mtoto wangu aliyekuwa tumboni nikamsikia akichezacheza. Machozi yalinitoka.
“Tutaonana mbinguni kwa baba mwanangu, samahani kwa kutumikia adhabu
yangu, Labda pengine ni sahihi tu kufa na mama yako. Kama usipokufa sasa
utakufa baadae kwa Ukimwi ambao naamini tayari nimekwisha kuambukiza.”
Nilinong’ona huku nikisubiri kudungwa sindano yenye sumu hadi kufa.
Nilimwona daktari yule akiinyanyua sindano iliyokuwa imejazwa dawa ya
46 | P a g e
Tetrodotoxin ambayo ni sumu maalumu kwa kuulia watu waliohukumiwa kifo,
akaibonyeza kidogo ile sindano, matone madogo ya sumu yakaruka angani, kisha
akanisogelea pale kitandani nilipolazwa tayari mkononi akiwa amekamata sindano
ya sumu.
“Nina mimba jamani, msiniue,” nilisema huku nikilia, macho yangu yakimtizama
mtu yule kwa huruma.
“Nina mtoto tumboni baba yangu niache tafadhali, usinichome sindano ya sumu,”
niliendela kulalama, hakuna kilicho badilika. Mtu huyo hakuwa na muda na mimi,
alionekana alikwisha zoea huruma zile. Kwahiyo jambo lile mbele yake ilikuwa ni
kitu cha kawaida. Hakunijali kabisa hata usoni hakuniangalia.
Alitizama saa yake ya mkononi nikaona ameganda kwenye saa hiyo. Ni kama
alikuwa akingoja muda fulani uwadie ndipo afanye kazi yake. Naam! hisia zangu
zilikuwa sahihi, baada ya sekunde kadhaa akanigeukia tena na kunikabili:
“Mfungeni mikanda,” alitoa amri. Askari wenye bunduki wakaanza kufanya kazi
hiyo. Pamoja na kwamba nilifumgwa minyororo kwenye mikono na miguu lakini
nilifungwa tena mikanda.
Nikawa siwezi kufurukuta. Daktari yule alinisogelea tena akiwa na sindano
mkononi, akanijia usawa wa shingo yangu kisha akaniinamia na kunidunga
sindano ile ya sumu kwenye shingo yangu.
Nilifumba macho wakati tendo hilo linafanyika ingawa niliusikia uchungu wa
sindano ile hasa wakati daktari anaibinya sumu ya Tetrodotoxin kuingia ndani ya
mishipa ya mwili wangu.
Sekunde tatu zilitosha kunifanya nianze kuona maluweluwe, nikajiona napatwa na
maumivu makali mwili wote, yalikuwa ni maumivu kama vile nababuliwa na
moto, nikataka kupiga kelele mdomo nao ukawa mzito, mara povu zito likaanza
kunitoka modomoni, damu ikanitoka puani .
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu, muda mfupi badaye sikujua tena kilicho
endelea duniani.
Toba!!
Nimekufa!!!.

47 | P a g e
Nilifumba macho wakati tendo hilo linafanyika ingawa niliusikia uchungu wa
sindano ile hasa wakati daktari anaibinya sumu ya Tetrodotoxin kuingia ndani ya
mishipa ya mwili wangu.
Sekunde tatu zilitosha kunifanya nianze kuona maluweluwe, nikajiona napatwa na
maumivu makali mwili wote, yalikuwa ni maumivu kama vile nababuliwa na
moto, nikataka kupiga kelele mdomo nao ukawa mzito, mara povu zito likaanza
kunitoka modomoni, damu ikanitoka puani .
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu, muda mfupi badae sikujua tena kilicho
endelea duniani.
Nilikufa!!!!!

SURA YA TANO

“AGRPINA, we’ Agripina...Agripina amka...Amka upesi!” nilisikia sauti


ikiniamsha, sauti hiyo haikuwa ngeni masikioni mwangu, nilifumbua macho
kivivu, ingawa niliona kwa mbali lakini sura ya mtu ninaye mfahamu ilijidhihilisha
mbele yangu.
“Mama!”
“Abee mwanangu.”
“Nmekufa na mungu ameniingiza peponi!”
“Hahaha! hapana mwanangu. Upo kijiji cha Makose wilaya ya Lushoto mkoani
Tanga, hujafa”
“Nipo Makose! Ina maana niko Tanzania?” niliuliza huku macho yangu
yakitizama huku na kule ndani ya chumba ambacho pia hakikuwa kigeni machoni
mwangu.
Kabla mama yangu hajanipa jibu mara akaingia mtu ambaye sikumtegemea
kumwona. Alikuwa ni Mariam Rashidi huyu ni yule wakala wa wasichana wa kazi
wanaokwenda kufanya kazi za ndani nchini ya Oman, alikuja na kuketi karibu
yangu.
48 | P a g e
“Mambo Agripina, naona mzimu wa kifo uliokukumba Oman umekurejesha
duniani,” alisema kwa masihara huku akiachia tabasamu pana na kuketi karibu
yangu.
Nikiwa sijakaa sawa nikendelea kushangazwa na utitiri wa ndugu walioingia ndani
ya chumba kile nilichokuwa nimelala. Kila ndugu aliyekuja kuniona alionekana
kufurahi kwa kuona nikiwa hai.
“Naombeni tusikilizane jamani,” alisema Mariam. Ndugu wote waliokuwa mule
ndani wakanyamaza.
“Kila mtu angependa kujua nini kilifanyika hadi Agripina kwa sasa yupo hai ilihali
taarifa zilienea kuwa tayari binti huyu kishachomwa sindano ya sumu na kafa...”
aliposema sentesi hiyo watu wote walijenga utulivu zaidi ili kujua nini kilitokea.
“Kwanza kabisa shukrani na pongezi zote anastahili Mwenyezi Mungu kwakuwa
ni yeye ndiye anayejua nini hatma ya maisha ya mja wake. Agripina alikuwa
katika hukumu ya kifo na alikwishaingizwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
tayari kwa kuchomwa sindano yenye sumu.
“Kitu ambacho wanajeshi na serikali ya nchi ya Oman hawafahamu hadi sasa ni
kwamba mtu anayehusika na kutoa adhabu ya kuwachoma watu sindano ya sumu
nilimuhonga dola zaidi ya 2000 ili mradi afanye lolote lile kumwepusha binti huyu
na kifo.
“Siku ya hukumu ya Agripina ilipowadia mipango yote ilikuwa sawa, alichofanya
mtu yule ni kumdunga Agripina sindano yenye dawa ya Ketamine Benzodiazepine
ambayo ilimfanya apatwe na maumivu makali sanjari na kumtoa povu mdomoni
lakini ambacho askari waliokuwa hawajui ni kwamba chupa yenye sumu aina ya
Tetrodotoxin chupa hiyo ilikuwa na dawa ya Benzodiazepine ambayo ilikuwa ni
dawa ya usingizi.
“Baada ya Agripina kupoteza fahamu kilichofuata ilikuwa ni kuusafirisha mwili
ndani ya jeneza, kama ambavyo mahakama ya nchi ile ilivyokuwa imeahidi, kwa
hiyo tulimsafirisha Agripina akiwa kama maiti hadi hapa Tanzania. Hivyo ndivyo
ilivyokuwa jamani...” alimaliza kusimulia Mariam.
Kila mtu mule ndani maelezo yale yalimsisimua mno. kwa kweli hata mimi nafsi
yangu ilikiri kuwa Mungu hashindwi na jambo. Nilipewa pole nyingi na ndugu na
jamaa, ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa mama yangu, wakati wote alikuwa

49 | P a g e
akibubujikwa na machozi. Kwa upande wangu, jambo lile nililiona ni kama ndoto
nzuri inayopita kichwani mwangu.
Muda mfupi baadaye ilikuwa ni zamu yangu kusimulia mambo yote yaliyo nisibu
tangu siku ya kwanza naikanyaga ardhi ya nchi ya Oman, hadi nagota nukta ya
mwisho, kila kila mtu alibubujikwa machozi
Ndugu zangu waliumizwa zaidi kusikia naisha na maambukizi ya virusi vya
Ukimwi, hata hivyo hapakuwa na mwenye kuweza kubadili ukweli wa jambo hilo.
Maisha yaliendela kama kawaida nikiwa kijijini kwetu Makose. Miezi michache
badaye, nilijifungua salama mtoto mzuri wa kiume, ambaye kwa bahati mbaya,
alizaliwa akiwa ana mambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Wito wangu kwa wasichana wenzangu wa Kitanzania hasa wenye ndoto za
kwenda kufanya kazi za ndani nchi za nje, ni vema mkawa makini huko
muendako, bila hivyo unaweza kujikuta unatumbukia katika shimo la mauti bila
kutegemea.
Jifunze kusimamia dhamira yako, kazi na mapenzi ni mafuta na maji, lakini pia
ningependa mjifunze kupamabana hapa hapa nyumbani, kwani fursa zipo nyingi.
Ukipatwa na tatizo hapa, ni rahisi kukabiliana nalo. Waswahili husema, zimwi
likujualo halikuli likakwisha.
Kabla ya kusema kwa heri. Napenda nimshukuru mwandishi wa mkasa huu wa
maisha yangu. Kaka yangu, Ally katalambula, ambaye alibadilisha maelezo yangu
na kuwa maandishi yaliyonakshiwa na kachumbali za kifasihi na kuchapwa kwa
mara ya kwanza katika Gazeti la Risasi toleo la kila Jumatano kutoka Global
Publishers.
Haikuwa kazi rahisi kumsimulia mkasa huu hadi mwisho, kwani mara nyingi
maelezo yangu yalikatishwa na kilio na simanzi kila nilipokuwa nikimweleza
hadithi hii.

50 | P a g e
***

ALLY KATALAMBULA:

Agripina alifariki dunia 12 Januari 2016 huko mjini Tanga kwa maradhi ya
UKIMWI. Ameacha mtoto mmoja wa miaka 7 ambaye analelewa kwenye kituo
cha watoto yatima cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar es salam.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina leke lihimidiwe. Mungu na ailaze roho ya
marehemu Agripina Joseph mahali pema peponi.

MWISHO

51 | P a g e

You might also like