Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 34

Kazi ya Kufundishia wanafunzi wa mwaka wa tatu.

Kazi hii imeandaliwa na mwalimu Masereka Levi Kahaika. +256782381038 au


+256702381038 Chuo Kikuu cha Makerere
MUHADAHRA WA 1 : FASILI YA RIWAYA NA HISTORIA YA RIWAYA
Riwaya
Zoezi: katika makundi ya wawili wawili jibu mswali haya.
1. Je, umewahi kuelezwa hadithi ndefu? Ilikuwaje?
2. Umewahi kusoma riwaya yoyote? Unatumia vigezo gani kubainisha kuwa hii ni riwaya?

Katika mhadhari huu utajifunza kuhusu fasili mbalimbali za riwaya. Ni matarajio yetu kuwa
mwishoni mwa mhadhara huu utakuwa na uwezo wa:
 Kufasili riwaya na sifa za riwaya.
 Kueleza sifa za riwaya na chimbuko la riwaya.

Riwaya ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko hadithi fupi. Urefu
wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi,
inaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi. Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya
Kiswahili ni Uhasama Kilimani, riwaya za mwandishi Masereka George Black.

Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K.W. Wamitila inataja aina nyingi tofauti za riwaya, k.m.
riwaya changamano, riwaya sahili, riwaya kiambo, riwaya ya kibarua na nyingi nyingine.

Waandishi waliobobea katika suala la riwaya kama Matteru na Muhando (1976) walisema kuwa
riwaya ni kazi ya kubuni kama hadithi ambayo hutungwa na kuibua mambo mengi katika
mazingira wanayoishi watu. Naye F. Nkwera anasema kuwa riwaya ni hadithi ndefu ya
kutungwa kwa kubuniwa iliyojengwa juu ya tukio la kihistoria kueleza maisha ya watu au taifa
fulani. Riwaya kwa kawaida huwa na mhusika mkuu mmoja au hata wawili. Senkoro naye
anasema kuwa riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye wahusika zaidi ya mmoja yenye kueleza
maisha ya watu.

Misingi ya riwaya huwa inatumia lugha ya kinathari inayogusa jamii, yenye visa virefu na ya
masimulizi ya kubuni.

Wamitila (2003:178), anasema riwaya ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu
wa kutosha, msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye
kuchukua muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu.

Page 1 of 34
Muhando na Balisidya (1976:62), wanasema riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo
hutungwa kufuatana na uwezo wa fanani kuibusha mambo kutokana na mazoea au mazingira
yake.Wanaendelea kusema kuwa riwaya yaweza kuanzia maneno 35000 hivi na kuendelea.
Riwaya iliyo na maneno chini ya 35000 ni novela si riwaya kwa kutumia kigezo cha urefu.
Nkwera (1978:109), anasema riwaya ni hadithi iliyo ndefu kuweza kutosha kufanya kitabu
kimoja au zaidi. Ni hadithi ya kubuniwa iliyojengwa juu ya tukio la kihistoria na kuandikwa kwa
mtindo wa ushairi iendayo mfululizo kwa kinaganaga katika kuelezea maisha ya mtu au watu na
hata taifa.Anaendelea kusema kuwa riwaya ina mhusika mkuu mmoja au hata wawili.

Senkoro,(1996) anasema riwaya ni kisa ambacho urefu wake unakiruhusu kitambe na kutambaa
vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwandishi wake. Anaendelea kusema kuwa ni
hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja na yenye mazungumzo na
maelezo yanayozingatiwa kwa undani na upana wa maisha ya jamii.Hivyo, inaonesha kuwa ili
kujua maana ya riwaya ni vyema kuzingatia mambo kadhaa ambayo ndiyo ya msingi, na mambo
hayo ni; lazima riwaya iwe na lugha ya kinathari, isawiri maisha ya jamii, iwe na masimulizi ya
kubuni na visa virefu, wahusika zaidi ya mmoja, iwe na mpangilio na msuko wa matukio, lazima
na maneno kuanzia elfu thelathini na tano na kuendelea, na mwisho riwaya ni lazima ifungamane
na wakati yaani visa na matukio ni lazima viendane na matukio.

Chimbuko la Riwaya ya Kiswahili


Baada ya kuangalia maana ya riwaya kutokana na wataalamu mbalimbali sasa ni vyema kutoa
maana ya riwaya ya Kiswahili kabla ya kujadili chimbuko la riwaya. Riwaya ya Kiswahili ni ile
ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili katika lugha ya Kiswahili. Pia, ni ile
riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.

TUKI (2004:48) inasema chimbuko la maana yake ni mwanzo au asili.Tanzu za asili zinaonesha
kuwa ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua riwaya za Kiswahili. Yafuatayo ni
mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya chimbuko la riwaya ya Kiswahili.

Page 2 of 34
Madumulla (2009) ameeleza kuwa riwaya ilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile hadithi,
hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa mdomo.Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na
maandiko ya fanai ya ushairi hususa ni tendi za Kiswahili katika hati za kiarabu kwa sababu
ndiyo maanadishi yaliyotamba katika pwani ya afrika mashariki. Wazungu na waarabu
hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za
maandiko ya ya kinathari. Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha za
ulaya na kufanya riwaya za Kiswahili kutokea.Mfano wa riwaa hizo ni kama vile; Habari za
mlima iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed (1980).

Senkoro (2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya


kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni
yaliyopelekea haja ya kimaudhui zaidi ya ngano na hadithi fupi.Anaendelea kusema kuwa
riwaya za kwanza zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu mpaka za Kiwsahili.Anasema riwaya
mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa. Ndiyo riwaya ya kwanza kutafsiriwa
kwa Kiswahili.Pia Senkoro (2011) anaeleza kuwa riwaya ni utanzu uliozuka kutokana na hali
mahususi za kijamii.Riwaya kama ile ya Kiingereza ya Robinson Crusoe iliyoandikwa na Daniel
Defoe ni miongoni mwa riwaya za mwanzo. Anasema riwaya ilizuka kutokana na maendeleo na
mageuzi ya kiutamaduni na viwanda.Suala la ukoloni na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo
zilihitaji kuelezwa kwa mawanda mapana zaidi ya yale ya ngano na hadithi fupi. Kupanuka kwa
usomaji hasa wakati wa vipindi vya mapinduzi ya viwanda huko ulaya kilifanya waandishi
waandike maandiko marefu kwani wakati huo ndipo walipoibuka wasomaji hasa wanawake
waliobaki majumbani waume zao walipokwenda viwandani kufanya kazi.

Mulokozi (1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya Kiswahili lipo katika mambo makuu
mawili ambayo; ni fani za kijadi za fasihi pamoja na mazingira ya kijamii. Mulokozi anaeleza
kuwa riwaya haikuzuka hivihivi tu bali ilitokana na fani za masimulizi yaani hadithi, na ndipo
zikapatwa kuigwa na watunzi wa riwaya wa mwanzo.Fani hizo zilizopata kuchipuza riwaya za
mwanzo ni kama vile; riwaya za kingano,tendi,hekaya, visakale,historia, sira, masimulizi ya
wasafiri, insha na tafsiri.

Page 3 of 34
Ngano, Mulokozi anasema, kuwa ngano ni hadithi fupi simulizi pia huwa ni hadithi za kubuni na
nyinga hasa zinawahusu wanyama wakali,pia zinahusu malaika,binadamu, mazimwi na majini.
Anasema kuwa mara nyingi ngano huwa na msuko sahihi na wahisika wake ni bapa na wahusika
hao ni mchanganyiko wa wanyama, mazimwi na binadamu.Anatoa mfano wa ngano
zilizochukua visa vya kingano kuwa ni kama vile riwaya ya Adili na Nduguze ya Shaban Robart
(1952), Lila na Fila ya Kiimbila (1966), Kusadikika ya Sharban Robart (1951) na baadaye
yakafuata machapisho mengine kama vile: Mfalme wa Nyoka ya R.K. Watts.Dhamira za riwaya
za kingano ni kama vile choyo,mgongano wa kimawazo na tama.

Hekaya, ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu yaani yasiyokuwa ya


kawaida. Mara nyingi masaibu hayo hufungamanishwa na mapenzi. Pia, hekaya ni ndefu kiasi
yaani sio ndefu kiasi cha kama riwaya. Katika jamii ya waswahili hekaya zilikuwa zimeenea
sana kipindi cha kabla ya ukoloni.Mifano ya hekaya ni kama vile; Hekaya za Abunuasi ya
C.M.C.A. 1915, Sultan Darai (1884), Kibaraka ya (1896) na hekaya ya Jonson, F. na Brenn,
E.W.Katika hekaya ya Alfa-Lela-Ulela ya kuanzia 1929. Hizo ndizo baadhi ya hekaya za
mwanzo lakini baadaye ziliathiri riwaya za Kiswahili kama vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya
Sharban Robart (1952), hekaya ya Ubeberu Utashindwa ya Kiimbila (1971),na Hekaya ya
A.J.Amiri,ya Nahodha Fikirini, (1972).

Tendi (utendi), ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, ambao


waweza kuwa ni wa kijamii au kitaifa.Kwa kawaida baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya ila tu
badala ya kuwa na umbo la kinathari zenyewe zina umbo la kishairi. Kuna tendi za aina mbili
ambazo ni tendi andishi na tendi simulizi.Riwaya pevu kama tendi huathiri mawanda mapana ya
kijamii na kihistoria.Huwa na wahusika wababe yaani mashujaa wenye kuwakilisha pande
zinazopingana.Mfano wa tendi ni kama vile; Utendi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki, Mlima ya
Hemedi Abdallah, (1895), Utendi wa as (Ghuli), utenzi wa Fumo Liyongo wa Mohamed
Kijumwa K. (1913).Tendi katika riwaya za Kiswahili imetumia wahusika wawili tu ambao ni
wahusika wa kubuni na wale wa kijadi wa kiafrika.

Page 4 of 34
Visasili, hizi ni hadithi zinazohusu asili na hatima ya watu, vitu, viumbe, ulimwengu na mataifa.
Pia, huangalia uhusiano wa wanadamu na mizimwi pamoja na miungu. Hadithi za kivisasili
zinapoonyeswa huaminika kuwa na kweli tupu hasa kwa kusimulia matukio mengi ya
kiulumwengu.

Mfano wa visasili; Lila na Fila ya Kiimbila (1966) ambayo imekopa motifu ya asili ya ziwa
ikimba huko Bukoba.Hadithi ya Mungu wa Kikuyu huko Kenya.Roza Mistika ya Kezilahabi
(1971), Nagona (1987) na Mzingile (1991), Siku ya Watenzi Wote ya Sharban Robart.

Visakale, ni hadithi ya kale kuhusu mashujaa wa taifa,kabila au dini.Mara nyingi visa kale
huchanganya historia na masimulizi ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu katika kila
kabila na kila lugha.Baadhi ya visakale vya Kiswahili ni masimulizi huhusu chimbuko la miji ya
pwani, mijikenda,mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa kama hivi ndivyo vinavyosababisha
kuandikwa kwa riwaya za Kiswahili. Mfano wake ni riwaya ya Abdalla Bin Hemed bin Ali
Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari za Wakilindi, Kisima cha Giningi ya M.S.Abdulla
(1968) na ile Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo na Buhliwali (1980) ya
A. Kitereza.

Visasuli, hizi ni hadithi zozote ambazo huelezea chimbuko au asili ya kitu chochote na mara
nyingi visasuli havina uziyo wowote kulinganisha na visasili. Mfano wake ni; Kwa nini paka
anapenda kukaa jikoni(mekoni), Kwa nini mbuni hana mbawa yaani hapai angani, kwa nini kima
anamuogopa mamba,kwa nini mbwa huishi na binadamu,kwa nini fisi hupenda kula
mifupa.Katika hadithi hizi watu huwa hawaamini sana bali wanachukulia kuwa ni utani tu.
Masimulizi ya kihistoria, haya ni masimulizi ya matendo ya mwanadamu katika muktadha wa
wakati,na ni fani muhimu sana katika jamii yeyote ile. Masimulizi halisi ya kihistoria yaweza
kuwa ni ya mdomo au hata maandishi na yote huwa ni chemichemi nzuri ya riwaya. Mfano wa
riwya hizo ni; Habari za pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi ya
masimulizi na uchambuzi.Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria ni; Uhuru wa
Watumwa ya J. Mbotela (1934), Kifo cha Ugenini ya O. Msewa (1977), Kwa Heri Iselamagazi
ya B. Mapalala (1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo ya G. Ruhumbika (1992).

Page 5 of 34
Sira, ni masimulizi ya kweli kuhusu maisha ya mtu au watu.Sira huweza kuwa wasifu yaani
zinazohusu habari za maisha ya mtu zikisimuliwa na mtu mwingine au zaweza kuwa tawasifu
yaani habari za maisha ya mtu zikisimuliwa na yeye mwenyewe. Sira iliathiri kuchipuka kwa
riwaya hasa kwa kuonesha masilmulizi ya maisha ya mtu toka utotoni mpaka uzeeni. Masimuliza
ya riwaya hizi yalikuwa katika masimulizi na hata katika maandishi pia kwa maana kabla ya
ukoloni yalikuwepo mandishi yaliyohusu maisha ya mitume na masahaba.Mifano ya hadithi hizi
ni; Kurwa na Doto ya M. S.Farsy (1960), Rosa Mistika ya Kezilahabi (1971),Kichwa Maji ya
Kezilahabi (1974) pamoja na Dunia Uwanja wa Fujo (1975), Mzimu wa Baba wa Kale ya
Nkwera (1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya Miaka Hamsini ya Sharban Robart (1951).

Masimulizi ya wasafiri, hizi ni habari zinazosimulia masibu ya wasafiri katika nchi mbalimbali.
Hekaya za riwaya chuku za kale zilisaidia kukuza riwaya.Mfano Alfa –Lela –Ulela na hadithi ya
Robinson Kruso huko 1719 ilihusu safari ya baharini ya mhusika mkuu ambaye baadaye
merikebu aliyokuwemo ilizama, ndipo akalazimika kuishi peke yake katika kisiwa kidogo.
Katika riwaya za Kiswahili kuna baadhi ya riwaya za masimulizi kama vile;Mwaka katika
Minyororo ya Samweli Sehoza (1921),Tulivyoona na Tulivyofanya Uingereza (1932) ya Martin
Kayamba. Uhuru wa Watumwa na Kwa Heri Eselamagazi.

Insha, ni maandiko ya kinathari yenye kuelezea,kuchambua au kuarifu kuhusu mada fulani.Zipo


insha za aina nyingi kama vile,makala,hotuba,tasnifu,michapo,barua, sira maelezo n.k insha
nyingi ni fupi mfano kuanzia maneno kama 500 na 10000 japo zingine zaweza kuwa ni ndefu
kiasi cha kuwa tasnifu za kufikia kiwango cha kuwa kitabu.Mfano wa insha ni Siku ya Watenzi
Wote ya Sharban Robert na Kichwa Maji ya Kezilahabi.

Shajara, ni kitabu cha kumbukumbu za matukio ya kila siku. Uandishi wa shajara ulianzia huko
Asia na baadaye ndio ulipopata kuibuka ulimwenguni kote.Jadi hii ya kiasia iliathiri utunzi wa
riwaya hasa zile za kisira.Mfano wa shajara ni ile iliyotungwa na Lu Shun iitwayo Shajara ya
Mwendawazimu (1918).

Page 6 of 34
Romansia (chuku) hii ni hadithi ya mapenzi na masaibu ya ajabu.Zikua maarufu sana huko
Uingereza hasa karne ya 6 na 12 na Ufaransa pia zilikuwepo na pamoja na China ambapo hadithi
zilizofanana na riwaya zilitungwa.Mfano hadithi za Hsiao-shuo.Watunzi wa riwaya za kisasa
zimekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na riwaya hizo za chuku hii ni kwa sababu
watunzi wengi wlikuwa wamesoma kazi nyingi za riwaya za wakati ule.

Drama, maigizo mengi hasa ya tamthilia yaliathiri sana riwaya hasa kwa upande wa usukaji wa
matukio na uchanganyaji wa ubunifu na uhalisia.Mfano ni riwaya nyingi za Charles Dickens zina
msuko uliosanifiwa kwa uangalifu kama msuko wa tamthilia.

Baada ya kujadili fani za kijamii hatuna budi sasa ya kujadili mazingira ya kijamii kama
yalivyopatwa kuelezwa na Mulokozi.Anaeleza kuwa, kufikia karne ya 16 fani za kijamii
zilikuwa zimekwisha enea na kufahamika katika maeneo mengi,hivyo kulihitajika kuwe na
msukumo wa kijamii, kiteknolojia na kiuchumi.Msukumo huo wa kuendeleza fani za kijadi
ulikuwa ni wa aina tatu ambao ni:

Ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi huko ulaya,ukuaji huo ulifungamana na biashara ya


baharini ya mashariki ya mbali na kuvumbuliwa kwa mabara mawili ya Amerika na ukuaji wa
viwanda hasa vya nguo huko ulaya. Mabadiliko haya yalizua tabaka jipya la mabwanyenye
waliomiliki viwanda na nyenzo nyingine za kichumi.Tabaka hilo lilihitaji fani mpya za fasihi,
lilikuwa na wakati wa ziada wa kujisomea, uwezo wa kifedha wa kujinunulia vitabu na
magazeti.Hivyo tangu mwanzo ilitawaliwa na ubinafsi uliojidhihirisha kiitikadi.Kwa mfano
Robinson Kruso ni riwaya iliyosawiri ulimbikizaji wa mwanzo wa kibepari.Ilimhusidia mhusika
asiyestaarabika aitwaye Friday au Juma. Ubinafsi hu ulijitokeza pia katika utungaji wake, na
haikusomwa hadharani bali kila mtu alijisomea mwenyewe chumbani mwake.

Mageuzi ya kijamii na kisiasa, mabadiliko haya yalifungamana na mabadiliko ya kiuchumi.


Mataifa ya ulaya yalianza kujipambanua kiutamaduni na kisiasa yaliyojitenga na dola takatifu ya
kirumi.Mabadiliko hayo yalianza kujenga utamaduni wa kitaifa na mifumo ya elimu iliyo hiyaji
maandishi katika lugha zao wenyewe.Mfano wa mageuzi ya kijamii na kisiasa iliyofanyika ni

Page 7 of 34
kama vile; Misahafu ya Dini Kama Biblia ilanza kutafsiriwa kwa lugha za ulaya, Martin Luther
alichapisha Biblia kwa lugha za kidachi miaka ya 1534.Hivyo basi inaonesha kuwa kadiri elimu
ilivyopanuka na nduvyo wasomaji wa vitabu walivyoongezeka na kufanya kuwe hadhira kubwa
nzuri ya wasomaji na watunzi wa riwaya.

Ugunduzi wa teknolojia ya upigaji chapa vitabu, yaani kwa kutumia herufi


iliyoshikamanishika.Ugunduzi huu uliofanywa na Johnnes Gutenberg huko ujerumani mwaka
1450 uliorahisisha kazi ya uchapaji vitabu katika nakala nyingi nakuondoa kabisa haja ya
kunakili misswada kwa mikono. Bila ugunduzi huo kufanyika haingewezekana kuchapisha
riwaya nyingi na kuzieneza kwa bei nafuu.Nmifano ya riwaya hizo ni kama vile; Pamela ya
Samwel Richardson (1740).

Kutokana na wataalamu mbalimbali kueleza chimbuko la riwaya ya Kiswahili, inaonekana


kuwa,riwaya ni utanzu wa fasihi ambao kuzuka kwake kulifungamana na fani za kijadi pamoja
na mazingira ya kijamii. Fani za kijamii kama vile, ngano, visasili, visasuli, visakale,insha,na
nyinginezo zizosimuliwa bila ya kuandikwa kabla ya karne ya 16, zilichochewa na kupewa
mwendelezo baada ya kukua kwa sayansi na teknolojia huko ulaya,hasa baada ya ugunduzi wa
mitambo ya kupiga chapa kazi za fasihi.

Utangulizi
Zoezi: Katika makundi ya watatuwatatu, jibu maswali haya:
1. Hivi umewahi kujiuliza ikiwa riwaya ina aina?
2. Je, wewe katika hizo riwaya ambazo umewahi kusoma unaweza ukatuambia aina za
riwaya ulizowahi kusoma?
Katika muhadhara wa 1 umepata maana kamili ya riwaya pamoja na chimbuko lake. Muhadhara
huu ni maendelezo ya huo uliotangulia. Hapa utajifunza tanzu za riwaya na historia ya riwaya ya
Kiswahili. Tutajadili juu ya michepuo ya riwaya, yaani riwaya dhati na riwaya-pendwa.

Page 8 of 34
Malengo ya Muhadhara
Baada ya kusoma muhadhara huu utatambua na kueleza yahusuyo:
 Tanzu za Riwaya.
 Historia fupi ya riwaya ya Kiswahili.
 Utaweza kubaini aina ya riwaya yoyote unayoisoma.
 Utaweza kuteua riwaya inayofaa kwa kufundisha wanafunzi ikiwa wewe ni
mwalimu
Tanzu za Riwaya
Kuna michepuo miwili ya riwaya riwaya-dhati na riwaya-pendwa. Riwaya-dhati ni riwaya yenye
kuchimbua na kuchambua matatizo au masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zale, athari
zake na ikiwezekana ufambuzi wake. Ni riwaya iliyokusudiwa kumkera na kumfikirisha
msomaji, siyo kumstarehesha tu. Riwaya-pendwa ni riwaya ambayo shabaha yake kuu ni
kumstarehesha na kumburudisha msomaji. Lengo hili hulitimiza kwa kusawiri visa na vituko vya
kusisimua damu, mathalan vituko vya ujambazi na uhalifu, ujasusi, na mahaba ya waziwazi.
Riwaya-pendwa huweza kuwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada. Zipo pia riwaya nyingi
ambazo zinaingia katika makundi yote mawili yaani riwaya zenye kutumia mbinu za riwaya-
pendwa kujadili masuala mazito ya kijamii.

Tanzu ni matawi au aina mahsusi za sanaa fulani


Mpaka sasa bado wataalamu hawajakubaliana kuhusu namna ya kuzigawa riwaya kitanzu.
Ubishi uliopo ni kuhusu vigezo vya kutunda katika uainishaji huo: je, vitumike vigezo vya
maudhui, umbo, mtindo, mutindo, shabaha, au vyote pamoja? Baadhi yao wanadai kuwa riwaya
zote ziko katika utanzu mmoja tu wa fasihi – utanzu wa riwaya. Kwa mujibu wa maelezo hayo,
tanzu nyingine ni drama, hadithi fupi na ushairi. Wengine wanasema riwaya si utanzu, bali ni
kumbo ya fasihi yenye tanzu au matawi kadha dani yake Msimamo huu wa pili ndio
unaozingatiwa katika muhadhara huu.

Wengi waliojaribu kuainisha tanzu za riwaya wametumia kigezo cha maudhui na kidogo, fani.
Idadi ya tanzu iliyoorodheshwa na wataalamu hao inatofautiana. Hapa tutajadili zile tanzu
ambazo wataalamu wengi huziorodhesha. Kigezo kikubwa tutakachokitumia ni maudhui, umbo
na shabaha ya riwaya inayohusika. Ni muhimu kukumbuka pia kuwa ziko riwaya ambazo zina
Page 9 of 34
sifa za tanzu mbili au zaidi (mathalan riwaya inaweza kuwa ya kijamiii na kihistoria wakati huo
huo).
Orodha ya riwaya-dhati ni:
RIWAYA-DHATI
 Riwaya ya Kijamii
 Riwaya ya Kisakolojia
 Riwaya ya Kihistoria
 Riway ya-sira
 Riwaya-chuku
 Riway ya Kingano
 Istiara
 Riwaya-tendi
 Riwaya-teti
 Riwaya ya Vitisho
 Riwaya ya Kisayansi
 Riwaya-barua
 Riwaya ya Majaribio
 Orodha ya riwaya-pendwa ni kama ifuatavyo:

RIWAYA PENDWA
 Riwaya ya Mahaba
 Riwaya ya Uhalifu/ Ujambazi
 Riwaya ya Upelelezi
 Riwaya ya Ujasusi

RIWAYA-DHATI
Riwaya ya Kijamii (Sociological Novel)
Hii ni riwaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida ya kijamii. Matatizo hayo huweza
kuwa ya kifamilia, ya kimahusiano, ya kitabaka, ya kisiasa, ya kitamaduni, n.k. Utanzu huu ndio
wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya. Miongoni mwa watunzi waliojipambanua zaidi huko Ulaya

Page 10 of 34
na Marekani katika uwanja huu ni Charles Dickens, ambaye alitunga riwaya nyingi, zikiwemo
Bleak House (1853) na Hard Times (1854); Leo Tolstoi, ‘iyetunga Vita na Amani (1865-1869)
na Anna Karenina (1875-1877); Gustave Flaubert (1821-1880) wa Ufaransa, aliyetunga Madame
Bavary (1856). Huko Marekani walitokea watunzi kama Mark Twain (1804-1864) aliyetunga
Huckleberry Finn (1884), Harriet Stowe (1811-1896) aliyetunga Uncle Tom’s Cabin (1852),
Jack London (1876-1916), aliyetunga The Iron Heall (1907), na Zola Neal Hurston (k.1901-
1960) aliyetunga Their Eyes Were Watching God (1937). Hapa Afrika, watunzi kama Alan
Paton (1903-1988) wa Africa Kusini, mtunzi wa Cry the Beloved Country (1948); Chinua
Achebe (Nigeria), mtunzi wa Things Fall Apart (1958) na A Man of the People (1966); Ngugi
wa Thing’o (Kenya), mtunzi wa A Grain of Wheat (1987), Petals of Blood (1977) n.k.; Mongo
Beti (Cameroon), mtunzi wa Mission termiėe (tafsiri ya Kiingereza inaitwa “Mission to Kala”)
(1957); na Sembene Ousmane (Senegal), mtunzi wa Les bouts de bots de Dieu (tafsiri ya
Kiingereza inaitwa “God’s Bits Wood”) (1960). Halikadhalika, idadi kubwa ya watunzi wa
riwaya ya Kiswahili hutunga riwaya ya kijamii. Mifano ni Shaaban Robert, Siku ya Watenzi
Wote (Nelson 1968), M. S. Mohamed, Nyota ya Rehema (OUP 1978); Said A. Mohamed Dunia
Mti Mkavu (Longman 1980), E. Kezilahabi, Rosa Mistika (EALB 1971), John N. Somba
Alipanda Upepo Akavuna Tufani (HEB 1969); Alex Banzi, Titi la Mkwe (TPH 1972), na Shafi
Adam Shafi, Kasri ya Mwinyi Fuad (TPH 1979).

Riwaya ya Kisaikolojia (Psychological Novel)


Hii ni riwaya inayodododosa nafsi ya mhusika; fikra, hisia, mawazo, imani, hofu, mashaka na
matumaini na matamanio yake ya binafsi, na athari za mambo hayo kwake binafsi na labda kwa
jamii yake. Baadhi ya watunzi waliojipambanua katika mkondo huu ni Henry James (1843-
1916), Mmarekan aliyetunga The Awkward Age (1899), The Ambassadors (1903), na riwaya
nyingine; na James Joyce (1882-1941), mtunzi wa Ireland aliyeandika Portrait of the Artist as a
Young Man (1916) na Ulyasses (1922). Kwa upande wa riwaya ya Kiswahili, miongoni mwa
riwaya zinazoingai kwa kina katika nafsi za wahusika ni zile za Kezilahabi, Kichwamaji (EAPH
1974), M. S. Mohamed, Kiu (EAPH, 1972) na Said Ahmed Mohamed Tata za Asumini
(Longman 1990).

Page 11 of 34
Riwaya ya Kihistoria (Historical Novel)
Hii ni riwaya yenye kuchanganya historia halisi na sanaa makusudi ili kutoa maudhui fulani.
Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu ya kihistoria yaliyoathiri mwenendo na
mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika (Mulokozi 1994). Riwaya ya historia huchanganya
wahusika wa historia na wa kubuni, na matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo, riwaya hiyo
huzingatia zaidi namna matukio makuu ya historia yalivyomuathiri, na yalivyoathiriwa na,
matendo ya mtu binafsi aliyeyashiriki.

Baadhi ya watunzi mashuhuri wa riwaya ya historia ni Sir Walter Scott wa Uingereza (mfano
Ivanhoe 1819), Leo Tolstoi wa Urusi, Vita na Amani (khj) na M Vassanji wa Tanzania, The
Gunny Sack (Heinemann 1989). Kwa upande wa fasihi ya Kiswahili, riwaya ya historia bado ni
fani ngeni. Baadhi ya watunzi wa riwaya ya historia ni Olaf Msewa. Kifo cha Ugenini (TPH,
1977) M. Kareithi Kaburi Bila Msalaba (EAPH, 1992), A. Lihamba, Wimbo wa Sokomoko
(TPH, 1990), M. M. Mulokozi, Ngome ya Mianzi (MPB, 1991) na Ngoma ya Mianzi (TPH,
1992) na G. Ruhumbika, Miradi Bubu ya Wazalendo (ERB, 1992).

Riwaya-Sira (Auto) (Biographical Novel)


Hii ni riwaya ambayo husimulia habari za maisha ya mhusika au wahusika tangu kuzaliwa hadi
pale inapokomea, au hadi anapofariki. Hivyo muundo wa riwaya hii aghalabu huamuliwa na
lengo hilo la kusimulia hadithi ya maisha ya mtu fulani: visa hufuatana kimantiki na kiwakati.
Riwaya ya kisira inapoandikwa kwa kauli ya nafsi ya kwanza huitwa riwaya ya kitawasifu
(autobiographical) na inaposimuliwa kwa kauli ya nafsi ya tatu huitwa riwaya ya kiwasifu
(biographical). Baadhi ya riwaya-sira hujikita katika maisha ya mtunzi mwenyewe, lakini baadhi
husimulia habari za wahusika wa kubuni tu Mifano mashuhuri ya riwaya-sira ni Dickens, David
Copperfield (1849-50), Dostoyevski, The Brothers Karamazov na Ntulanalwo na Buhliwali
(TPH, 1980). Kwa upande wa riwaya ya Kiswahili, Ruhumbika Miradi Bubu ya Wazalendo
(ERB, 1992), Mapalala Kwa Heri Iselamagazi (TPH, 1991) na Kezilahabi, Dunia Uwanja wa
Fujo (EALB, 1975) ni mifano ya riwaya-sira.

Riwaya-Chuku (Romance)

Page 12 of 34
Ni riwaya za vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida. Ni riwaya isiyozingatia uhalisia. Mara
nyingi masaibu ya riwaya-chuku huambatana na mapenzi. Mifano: Baadhi ya hadithi za Alfu-
Lela-Ulela, na hadithi za mtunzi wa Kiitaliano, Boccaccio (Decameron Katika fasihi ya
Kiswahili, riwaya za Shaaban Robert za Adili na Nduguze (Macmillan 1952) na Kusadikika
(Nelson 1951) zinaingia katika kundi hili.

Riwaya ya Kingano (Fabulous novel)


Ni riwaya yenye umbo na mtindo wa ngano, mathalan huweza kuwa na wahusika wanyama, visa
vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni, na visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoria.
Mfano ni riwaya ya Shaaban Robert, Adili na Nduguze (khj) na J. K. Kiimbila Lila na Fila
(Longman, 1966).

Istiara (Allegory)
Ni riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kiwakilishi tu cha jambo jingine.
Kwa mfano, riwaya ya Nathanael Swift (1726) Safari za Gulliver (Mf. F. Johnson, Sheldon
1932). Riwaya ya George Orwell (1945), Shamba la Wanyama (Mf. F. Kawegere, EAPH, 1967)
ni ishara ya mfumo wa utawala wa udikteta wa Kisovieti wa enzi istiara kuhusu utawala wa
mabavu wa kikoloni.

Riwaya-tendi (Epic novel)


Ni riwaya yenye mawanda mapana kama utendi. Aghalabu riwaya hiyo husawiri matendo ya
ushujaa, na masuala mazito ya kijamii yenye kuathiri historia ya taifa linalohusika. Mfano ni Leo
Tolstoi Vita na Amani (khj) na Thomas Mofolo (1926) Chaka Mtemi wa Wozulu (Mf. M. S.
Attas, OUP, 1975).

Kiwaya-teti (Picaresque novel)


Ni riwaya inayosimulia vituko na masaibu ya maayari (watu wapuuzi, walaghai, wajanja, n.k.)
kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Agalabu maayari hao huwa ni watu wanaovutia (si
wahusika wawi (waovu), wa tabaka la chini, na bapa. Matukio ya riwaya hii hayana msuko

Page 13 of 34
ulioshikamana vizuri. Shabaha yake mojawapo ni juziteta na kuzikejeli tabia za matabaka na
watu mbalimbali katika kijamii. Mifano: Riwaya ya Don Quixote imetumia mbinu za riwaya-teti.
Riwaya-teti ny ingine ni Thoma Nash, The Unforutnate Traveler (1590), na Daniel Defoe Moll
Flanders (1722). Kwa kiasi fulani visa vya Abunuwas (Hekaya za Abunuwas) vinafanana na
vituko vya kiriwaya-teti.

Riwaya ya Vitisho (Gothic novel)


Hii ni riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu; mara nyingi visa hivyo huambatana na
matukio ya ajabu au miujiza. Huko Ulaya riwaya hizo kwa kawaida hutumia mandhari ya Kasri
za kale (Gothic castles). Riwaya ya Dracula (1897) ya Mwingereza Bram Stoker (1847-1912),
ambayo ni hadithi ya mzuka anyonyaye damu ya watu (vampire), na ambayo imezaa filamu za
sinema za Dracula huenda ilitokana na athari ya riwaya za aina hiyo. Katika fasihi ya Kiswahili,
riwaya zenye kushabihiana, lau kidogo, na gothic novels ni zile za kichawi, kwa mfano N. J.
Kuboja, Mbojo Simba-Mtu (EALB, 1971) na C. Mung’ong’o, Mirathi ya Hatari (TPH, 1977).

Riwaya ya Kisayansi (Science Fiction/ Novel)


Hii ni riwaya inayotumia taaluma ya sayansi kama msingi wa matuko, masaibu na maudhui
yake. Mathalan baadhi ya riwaya hubashiri namna sayansi itakavyoathiri maendeleo ya
mwanadamu katika karne zijazo, na baadhi huonesha namna sayansi inavyoweza kuleta hasara
kwa mwanadamu pindi ikitumika vibaya bila kuzingatia “maadili” au ubinadamu. Mara nyingi
uwezo wa binadamu wa kuyatawala na kuyadhibiti maumbile, na pengine hata uwezo wake wa
kuitawala sayansi aliyoibuni mwenyewe, husailiwa. Watunzi mashuhuri wa riwaya ya sayansi ni
Jules Verne wa Ufaransa, aliyetunga Voyage au centre de la Terre (1864) “Safari hadi kwenye
Kiini cha Dunia” (1864); De la Terre a la lune “Kutoka Duniani hadi Mwezini” (1865), n.k.; na
H.G. Wells wa Uingereza aliyetunga The Time Machine 1895); The Invisible Man (1897); The
War of the World (1898), Katika Kiswahili bado hawajajitokeza watunzi wa riwaya ya kisayansi,
isipokuwa labda Eddie Ganzel Katika hadithi yake fupi ya Kisiwa cha Sikri (Ilichapishwa katika
gazeti la Nyota Afrika miaka ya 1970). Naye said A Mohamed katika Nyuso za mwanamke suala
la kiteknolojia limeangazwa sana.

Page 14 of 34
Riwaya-barua (Epistolary novel)
Hii ni riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barira wanazoandikiana
baadhi ya wahusika. Kiwaya ya Samuel Richardson, Pamela, imo katika Ba iitwayo Une Si
Lorigue Letire “Barua Ndefu Kama Hii (1980). Tafsiri ya Kiswahili ilifanywa na C. Maganga na
Kuchapishwa na Mkuki na Nyota mwaka 1994.

Riwaya ya Majaribio (Experimental Novel)


Riwaya ya majaribio kame hii imejitokeza katika mikondo miwili. Mkondo wa kwanza ni riwaya
ya “mjadala-natsi.” Mkondo wa pili ni “riwaya-kweli” (non-fiction novel).

Riwaya ya “mjadala-nafsi” hutungwa bila kuzingatia kanuni za kawaida za uandishi wa riwaya.


watunzi wa riwaya hii hudai kuwa umbo la kawaida la riwaya halitoshelezi mahitaji ya karne
hii– halitoshi kuwasilisha kweli kamili ya maisha katika sura zake zote. Mathalan, ni vigumu
kuuelezea mtiririko wa mawazo na hisia zilizomo katika ubongo wa mtu kwa njia za kawaida za
uandishi (kwa kutumia sentensi, aya, maongezi ya wahusika.

Riwaya ya Uhalifu/ Ujambazi


Hizi ni riwaya zinazosimulia vituko vya kihalifu, kwa mfano wizi, ujambazi, uuaji, magendo,
utapeli, na kadhalika. Aghalabu polisi huhusishwa katika kuwasaka na kuwadhibiti wahalifu hao.
Mifano: J. Simbamwene, Kwa Sababu ya Pesa (Longman 1972); F. Katalambula, Buriani
(EALB, 1975); L. O. Omolo. Mtu Mwenye Miwani Meusi (Longman, 1970); S. J. Chadhoro,
Kifo Changu ni Fedheha (Longman, 1972); A. Komanya, Tabu (TPH, 1977); Hammie Rajab,
Ufunguo wa Bandia (EAPL, 1979), E. Musiba, Kikomo (CP, 1980), na Faraji Katalambula,
Buriani (EALB, 1975); na takriban riwaya zote za John Simbamwene.

Riwaya ya Upelelezi

Page 15 of 34
Riwaya hii kwa kawaida huwa na vitu viwili: Kosa au uhalifu, na upelelezi wa uhalifu huo hadi
mhalifu anapopatikana. Hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhulumiwa (waliotendewa kosa)
na wapelelezi, wakiwemo polici. Mkondo huu wa riwaya-pendwa ulianzia huko Marekani
mwaka 1841, ilipochapishwa hadithi ya Edgar Allan Poe iitwayo “The Murders in the Rue
Morgue”. Baadaye, mtunzi wa Kiingereza, Sir Arthur Conan Doyle (1859-1930), alikomaza fani
hii na kuifanya ipendwe na kuenea duniani kote. Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya upelelezi
katika fasihi ya Kiswahili, M. S. Abdulla (1918-1991) aliiga baadhi ya mbinu za Arthur Conan
Doyle. Riwaya za upelelezi za M. S. Abdulla ni Mzimu wa Watu wa Kale (EALB 1960), Kisima
cha Giningi (Evans 1968), Duniani Kuna Watu (EAPH, 1973), Siri ya Sifari (EAPH, 1974),
Mwana wa Yungi Hulewa (EAPH 1976) na Kosa la Bwana Musa (AP, 1984).

Watunzi wengine mashuhuri wa riwaya ya upelelezi ni Faraji Katalambula, John Simbamwene,


Ben Mtobwa na E. Ganzel Baadhi ya kazi zao ni: Katalambula, Simu ya Kifo (EALB, 1965),
Simbamwene, Muuaji ni Nani? (Jomssi, 1987), Ben Mtobwa, Dimbwi la Damu (AP 1984), na
Ganzel, Kijasho Chembamba (Tamasha, 1980).

Riwaya ya Ujasusi
Hii ni riwaya ya upelelezi wa kimataifa, Majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au
maajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao, hasa siri za kijeshi (k.m. silaha
walizo nazo), siri za kisayansi na kiuchumi, n.k. ili tarifa hizo ziwanufaishe wale waliowatuma.
Wakati mwingine majasusi hutumwa kwenda kuharibu silaha au nyenzo za uchumi za maadui.
Huko Ulaya, riwaya za kina John Buchan. The Thirty-Nine Steps (1915), Ian Fleming (riwaya
ambazo mhusika wake mkuu ni James Bond), na Nick Carter (kwa mian Assault on England
1972) zinaingia katika mkondo huu. Katika Kiswhaili, baadhi ya watunzi mashuhuri wa riwaya
za ujasusi ni E. Musiba, Kikosi cha Kisasi (KP 1979) na Njama (CP 1981); K. M. Kassam,
Mpango IPA 1982); B. Mtobwa Tutarudi na roho Zetu? (Heko 1987) na Hammie Rajab Roho
Mkononi (Busara 1984).

Historia Fupi ya Riwaya ya Kiswahili

Page 16 of 34
Katika Muhadhara 1, tumezungumzia chimbuko la riwaya duniani. Tumeonesha kuwa chimbuko
la riwaya lilitokana na mambo makuu mawili: fani za jadi za kifasihi, na mazingira ya kijamii.

Muhadhara huo umedhirisha pia kuwa fani za kifasihi ambazo zingeweza kavyaza riwaya
zilikuwapo hapa Africa Mashariki kabla ya ukoloni. Fani hizo ni ngano, hekaya, tendi, visakale,
historia sira, masimulizi ya wasafiri, insha, na tafsiri. Kitu ambacho hakikuwepo ni mazingira ya
kijamii, hususan hadhira kubwa ya watu wajuao kusoma na kuandika, wenye uwezo wa kununua
vitabu na wakati wa kutosha kuyisoma; mitambo ya kupigia chapa, na mfumo wa usambazaji wa
vitabu. Hivyo riwaya ya Kiswayili ilibidi isubiri majiho ya ukoloni kabia ya kuchipuka.

Ukoloni ulisaidia kuweka mazingira ambayo yangeweza kuilea riwaya, lakini riwaya yennyewe
ilibidi iandikwe na kusomwa na wenyeji kutokana na ujuzi na uzoefu wao. Hi katimiza azma
hiyo, watumzi wa riwaya ya mwanzo walirejolea fani za jadi walizozizoea-walipala baadhi ya
mbinu na maudhui yao, nap engine hata kariha (inspiration) kutokana na fani hizo.

Kabla ya ukolani, sehemu kubwa ya fasihi andishi ya kimasimulizi ya Kiswahili ilikuwa ni tendi
(Angali Muhadhara wa 9). Baadhi ya tendi hizo, kwa mfano Kisa cha Anzaruni au Siri ‘Isirari
(Binti Lemba 1963), Kadhi Kassin bin Jaafar (Hemed Abdallah, Kame ya 19) zilitumia mbinu za
kiriwaya, kwa mfano ubunifu wa vituko na msuko wa matukio. Hivyo kwa kiwango hicho tendi
hizo ziliandaa mazingira ya Kisanaa yaliyosaidia kuzuka kwa riwaya wakati ulipotimu.

Jambo jingine lililosaidia katika kuchipuza riwaya ya Kiswahili ni tafsiri. Tafsiri ni mbinu
inayotumiwa na mataifa yote kukuza fasihi, lugha na maarifa yao. Kwa sababu zinazoele weka,
tafsiri za mwanzo katika luga ya Kiswahili zilikuwa ni za kidini: tafsiri ya kwanza
inayofahamika ni Sayyid ‘Aidarus bin Athumani (Karne ya 17) Kaswida ya Himziya
inayofahamika ni Sayyid ‘Aidarus bin Athumani (Karne ya 17), Kaswida ya humziya (1952),
Utenzi huo, unaomsifu Mtume Muhammad, ulitokana na utenzi wa Kiarabu uitwao al-
Hamziyyah uliotungwa na mshari wa Misri aitwaye Sharaf ad-Din Muhammad bin Said Al-
Busiri katika karne ya 13. Baada ya Hamziyya kazi nyingine za Kiarabu zilifasiriwa au
kusimuliwa upya kwa Kiswahili (mfano ni Utenzi wa Ras “IGhuli, Hekaya za Abunuwas na

Page 17 of 34
Alfu-Lela-Ulela). Wazungu nao walipoingia walianza kufasiri vitabu vya Biblia kwa Kiswahili;
tafsiri za mwanzo kabisa ni Agano Jipya na baadhi ya sura za Agano la Kale ziliyofanywa na
Ludwig Krapf kati ya mwaka 1846 na 1848.

Kazi za fasihi ya Kizungu zilianza kufasiriya kwa Kiswahili kuanzia mwishoni mwa kame ya 19
(k.m. C. Kingsley, Mashujaa; Hadithi za Wayunani 1889). Wakati wa ukoloni zilifasiriwa kazi
nyingi zaidi za kigeni, mathalan; H. R. Haggard, Mchawi (mfasiri M.M.B. UMCA 1900); Neale,
Nyumba ya Aptonga (The Farm of Aptonga) (S.P.C.K., London, 1924); Bunyan, J. Safari za
Msafiri (Pilgrim’s Progress), (S.P.C.K, London 1925); Johnson, F. na Brena, E. W. (Waf), Mfu-
Lela-Ulela (labda kutoka katika lagba ya Kiingereza, London 1928); Hekaya za Abunawas
(mfasiri S. Chiponde, Macmillan, 1928); R. I. Stevenson, Kisiwa Chenye Hazina (Mf. F.
Johnson, Longman 1929); R. Kipling, Hadiihi za Maugli (Mf. F. Joshnson. Sheldon 1934); N.
Swift, Safari za Gulliver (mf. F. Johnson, Sheldon, mwaka 1932); L. Carroll Elisi katika Nchi va
Ajabu (Mfasiri: E. V. St. Lo. Conan-Davies (Sheldos 1940); Wyss, J. R. Jamaa Hodari Kisiwen
(Swiss Family Robinson) (Mt. D. Diya London 1951); na D. Dafoe, Robinson Kruso na Kisiwa
Chake (EALB. K. 1962). Kazi nyingine muhimu ziliyofasiriwa ni baadhi ya tamthilia za William
Sshakespeare, k.m. Mjanya Biashara wa Venisi katika mtindo wa nathari (Taz. Hadithi za
Kiingereza, Sheldon, 1940).1

Mbali na tafsiri, maandiko ya mwanzo ya kinathari ya Waswahili wenyewe, hususan maandishi


ya tarikh za miji mbalimbali, Safari za Waswahili, Maisha ya Hamed bin Muhammed (Tippu
Tip), na Habari za Wakilindi, Kama tulivyoeleza kabla, yaliweka msingi wa mikondo na mitindo
ambao ingefuatwa na watunzi wa baadaye wa riwaya ya Kiswahili.

Baada ya Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki kuanzishwa mwaka 1930, uandishi katika lugha
ya Kiswahili ulihimizwa kwa njia ya mashindano. Kutokana na mashindano hayo, riwaya ya
kwanza ya Kiswahili, Uhuru wa Watumwa (James Mbotela K. 1885-1976), ilichapishwa mwaka
1934, Baadhi ya riwaya zilizotoka baadaye, wa mfano M. S. Abdulla, Mzimu wa Watu wa Kale
(EALB 1960), na Faraji Katalambula, Simu ya Kifo (EALB 1965) zilitokana na mashindano.

Page 18 of 34
Miaka thelathini iliyofuata baada ya Uhuru wa Watumwa ilitawaliwa na kazi za Shaaban Robert
(1909-1962). Riwaya yake ya kwanza, Utubora Mkulima (Nelson 1968) yasemekana ilitungwa
mwaka 1946, lakini haikuchapishwa hadi mwaka 1968. Riwaya iliyofuata ni Kufikirika (OUP
1968) iliyoandikwa mwaka 1947, na kuchapishwa mwka 1967. Riwaya ya tatu, Kusadikika
(Nelson 1951) ilichapishwa mwaka 1951, na ya nne, Adili na Nduguze (Macmillan 1952)
ilichapishwa mwaka 1952. Riwaya yake ya mwisho, Siku ya Watenzi Wote (Nelson 1968)
iliandikwa kama 1960-62 na kuchapishwa mwaka 1963. Karibu riwaya zote za Shaaban Robert
ziliathiriwa sana na ngano na hekaya, hasa katika muundo wake na uchoraji wa wahusika (karibu
wahusika wote wakuu ni bapa).

Shirika la Uchapishaji Vitabu la Africa Mashariki (EALB) lilianzishwa mwaka 1948 ili
kushughulikia uchapishaji wa vitabu kwa lugha za kienyeji. Shirika hilo lilichapisha karibu
vitabu tofauti tofauti 1000 katika lugha 16 kwa ajili ya shule na wasomaji wa kawaida. Miongoni
mwa vitabu hivyo, zilikuwemo hadithi’, hasa za kingano, hekaya na visa. Riwaya za Kiswahili
zilizopevuka zilianza kuchapishwa miaka kumi baadaye. Riwaya hizo ni Farsy, Kurwa na Doto
(EALB 1960) na M. S. Abdulla, Mzimu wa Watu wa Kale (EALB 1960).

Kihistoria, masuala makuu ya miaka ya 1960 kwa Afrika yalikuwa ni ukombozi was bara la
Afrika na ujenzi wa jamii mpya bada ya uhuru. Masuala haya makuu yalijitokeza katika riwaya
ya Kiswahili ya wakati huo. Hivyo palitokea riwaya za kisiasa na kifalsafa zilizojadili maisha,
utawala na ujenzi wa jamii mpya. Riwaya hizo zilizosuta ukandamizaji na ubinafsi, ziliuhakiki
unyama wa maisha ya kimji, na zilijaribu kuielekeza jamii katika mkondo wa ubinadamu, usawa
na ustawi. Baadhi ya riwaya hizo ni Shaaban Robert, Utubora Mkulima (khj) na Siku ya Watenzi
Wote (khj).

Kwa upande wa ukombozi, riwaya ya Kiimbila, Lila nad Fila (Longman 1966) iligusia dhamira
hiyo kiistiara. Riwaya iliyozungumzia bayana la ukombozi ni Kareithi, Kaburi Bila Msalaba
(EAPH 1969).

Page 19 of 34
Kundi jingine la riwaya za miaka ya 1960 ni riwaya-pendwa. Matawi wawili ya riwaya-pendwa
(Upelelezi na uhalifu) yalijitokeza wakati huu. Tawi la upelelezi liliwakilishwa na M. S. Abdalla,
Mzimu wa Watu wa Kale (khj), na Kisima cha Giningi (Evans 1968), na Katalambula, Simu ya
Kifo (EALB 1965). Tawi la riwaya ya uhalifu liliwakilishwa na Leo Odera Omulo, Mtaka Yote
Hukosa Yote (Longman 1968) na Chadhoro, S. J. Tatizo la Kisauni (EAPH 1969).

Katika kipindi hicho ilitokea pia riwaya ya tabia na maadili, iliyowakilishwa na J. N. Somba,
Kuishi Kwingi Kuona Mengi (EAPH 1968) na Alipanda Upepo Akavuna Tufani (Heinemann,
1969).

Mwisho, riwaya ya mila na utamaduni, iliyowakilishwa na M. S. Farsy, Kurwa na Doto (khj) na


Felician Nkwera, Msishi wa Baba Ana Radhi (EALB 1968) vilevile iliitokeza katika kipindi
hicho. Riwaya yenye kukosoa utamaduni na imani za jadi, kwa mfano Isaya, P., Nyumbani kwa
Mchawi (Ndanda 1961) vilevile yaweza kuingia katika kundi hili.

Nchini Uganda hapakuwa riwaya yoyote iliyokuwa imeandikwa kwa Kiswahili kufikia mwaka
2018 ambapo waandishi chipukizi walijitokeza ikiwa ni, Masereka George Black ambaye
aliandika Riwaya ya Uhasama Kilimani, Muhereza Vincent ambaye aliandika riwaya ya Baraka
za Mama, Jitihada Zafua Dafu iliyoandikwa na Wanyenya Willy pamoja na riwaya ya Uchungu
wa Mwaridi iliyoandikwa na Ndanda E. Antonio. Vitabu hivi hata viko kwenye silabasi ya
kidato cha sita ya Uganda. Riwaya ya Kiswahili limepevuka na kupanuka zaidi kwenye miaka ya
1970-1995. Kama tuliyoona katika Kifungu cha 1, karibu tanzu zote za riwaya tulizozitaja
zimepata wawakilishi. Kadhalika, zimejitokeza riwaya za mikondo mbalimbali. Mambo makuu
yaliyoipambamua riwaya ya Kiswahili katika kipindi hiki ni:

Mambo yaliyochangia katika Uendelezaji wa Riwaya za Kiswahili


(a) Katokea kwa watunzi wapya, vijana, ambao wameipa uhai mpya riwaya Baadhi yao ni
Euphrase Kezilahabi (kz. 1944), Said Ahmed Mohamed Khamisi (kz. 1947), Shafi Adam
Shafi (ka 1940), M. S. Mohamed (kz. 1943), K. G. C. Mkangi (kz: M. X. Burhan (Kz. ?),
A. J. Saffari (kz. 1951) na B. Mapalala (kz. 1957).

Page 20 of 34
(b) Kuongezeka kwa riwaya-pendwa, ambako kuliambatana na kutokeza kwa wachapishaji-
waandishi (k.m. John Simbamwene na E. Musiba) ambao waliandika na kuchapisha
riwaya zao wenyewe Baadhi ya watunzi maarufu wa riwaya-pendwa waliotokea katika
kipindi hiki ni E. Musiba, Ben Mtobwa, J. Mkabarah, C. Merinyoi, Mbunda Msokile
(1950-1995), Nieco ye Mbajo, Hammie Rajab, John Simbamwene.

(c) Kujitokeza kwa riwaya inayoihakiki jamii kwa undani-wengine wameiita riwaya ya
uhalisia-hakiki. Baadhi ya watunzi mashuhuri wa riwaya hiyo ni; Shafi A. Shafi, Kasri ya
Mwinyi Fund (TPH 1978) na Kuli (TPH 1979); S. A. Mohamed, Tata za Asumin
(Longman 1990); E. Kezilahabi, Dunia Uwanja wa Fujo (EALB 1975), Gamba la Nyoka
(EAPL 1979); C. Mung’ong’o, Njozi Lliyopotea (TPH 1980) na A. J. Saffari, Kabwela
(Longman 1978), Mkangi, Mafuta (Heinemann 1984) na C. S. Chachage, Sudi ya
Yohana (DUP 1981) na Kivuli (DUP 1981); N. Tegambwage, Duka la Kaya (Tausi
Publishers 1985); Z. Burhani, Mwisho wa Kosa (Longman 1987) na G. Ruhumbika,
Miradi Bubu ya Wazalendo (ERB 1992). Nyuso za mwanamke (2010).

(d) Kuzuka Kwa riwaya ya historia. Watunzi mashuhuri wa riwaya hiyo ni B. Mapalala, kwa
Heri iselamagazi (TPH 1992) na G. Ruhumbika, Miradi bubu ya Wazalendo (Khj).

(e) Kuzuka kwa riwaya ya kifalsafa na ya majaribio. Wawakilishi wa mkondo huu wa riwaya
ni E. Kezilahabi, Nagona (DUP 1987) na Mzingile (DUP 1991) na Mkangi, Mafuta
(HEN 1984). Riwaya za Kezilahabi zinachanganya mjadala- nafsi na falsafa ya maisha.
Riwaya ya Mafuta inatumia fasihi simulizi (hususan ngano na semi), ishara za kijadi,
istiara, ubeuzi, mjadala- nafsi na muundo wa mlegezo ili kufichua uoza wa mahunsiano
ya kitabaka nehini Kenya. Mtunzi mwingine ambaye ametumia mbinu ya mjadala – nafsi
ni N, tegam bwage, Duka la Kaya (Tp 1985).

(f) Kuongezeka kwa riwaya za vijana na watoto, Mifano ni P. Shija, Mashujaa wa


Kazakamba (TPH 1978) na Vijana Jasiri (TPH 1980), A. Lihamba, Wimbo wa sokomoko

Page 21 of 34
(TPH 1990), M.M Mulokozi, Ngome ya mianzi (MTB 1990), Ngoma ya Mianzi (TPH
1991) NA Moto wa mianzi (Echol 1995).

(g) Kuzuka kwa riwaya ya wanakisomo: Hii ni riwaya inayoandikwa Mahsusi Kwa ajili ya
wanakisomo wa madarasa ya elimu ya watu wazima. Riwaya hii ina sifa zinfuatazo:

- Ni fupi (kwa vile wanakisomo (chekechea) hawajapata uzoefu wa kusoma matini


ndefu),
- Ni sahili kimuundo (ili ieleweke kwa urahisi kwa walengwa);
- Huwa na lugha rahisi (msamiati mwepesi, sentensi fupi fupi);
- Maudhui yake ni sahili lakini ya kiwango cha watu wazima (huhusu maisha na
matatizo ya kila siku ya wakulima na wafanyakazi wa kawaida vijijini na mijini, na
aghalabu hupendekeza ufumbuzi wa matatizo hayo).

Mwandishi alijyejipambanua Zaidi katika uwanja huu wa utuzi ni shaaban K. Msuya:


Mazungumzo ya mchana (TPH 1973), Mazungumzo ya Usiku (TPH 1975), Mazungumzo
ya jioni (TPH1976), Tuzungnumze yajayo (Bsa 1978) na Siri ya Bahati (BSA 1978).

(h) Kuanzishwa kwa taaluma ya uhakiki ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili, Taaluma hiyo
ilianza kufundishwa baada ya kuanzishwa kwa idara ya Kiswahili katika chuo kikuu cha
Dares Salaam Mwaka 1968. Miaka ya 1970, taaluma ya uhakiki imeenezwa mashuleni
kote nchini Tanzania, na miaka ya 1980 imeenezwa nchini Kenya. Baadhi ya wahakiki
mashuhuri wa riwaya ni: Kezilahabi, 1976; Topan, 1977: Sengo, T.S.Y na Kiango, S.D
1973, 1974;ohly, 1981, TUKI, 1983: Madumulla, 1986, Mazigwa, 1991; Mlacha 1990:
Madumulla na Mlacha, M, 1976; Senkoro, 1977, 1982?, 1987, senkoro na Mohamed, M.
A 1987; Lugano, R.S, 1989; Mazrui, A.M. na Syambo, B.K. (1992); na Wamitila (1991).

MUHTASARI
Katika muhadhara huu umejifunza Yafuatayo..
Tanzu za riwaya

Page 22 of 34
Umejifunza kuwa riwaya hugawanyika katika makundi makuu mawili: riwaya – dhati na
riwaya – pendwa. Riwaya – dhati huwa na shabaha kuu ya kuchambua masuala mazito
ya kijamii au kimaisha na riwaya- pendwa huwa na shabaha kuu ya kutoa burudani. Zipo
pia riwaya zenye kuchanganya sifa za makundi yote mawili.

Umejifunza pia kuwa riwaya hugawanyika katika tanzu nyingi Kwa mujibu wa maudhui,
shabaha na maumbo, Baadhi ya tanzu hizo ni.

RIWAYA- DHATI
 Riwaya ya kijami
 Riwaya ya kisaikolojia
 Riwaya ya kihistoria
 Riwaya –sira
 Riwaya – chuku
 Riwaya ya kingano
 Istiara
 Riwaya tendi
 Riwaya – teti
 Riwaya ya vitisho
 Riwaya - barua
 Riwaya ya majaribio

RIWAYA PENDWA
 Riwaya ya mahaba
 Riwaya ya uhalifu/ ujambazi
 Riwaya ya upelelezi
 Riwaya ya ujasusi

Historia fupi ya riwaya ya Kiswahili

Page 23 of 34
Umeelezwa kuwa kabla ya miaka ya 1930 hapakuwa na riwaya Kiswahili, bali palikiwa na
maandiko mbalimbali ya nathari ambayo wengine wameyaita riwaya kwa makosa. Zilikuwepo
pia tafsiri za riwaya za kizungu zilizofanywa na wakoloni ili zisomwe mashuleni na kwingineko.
Riwaya halisi ya kwanza ni uhuru wa watumwa. Baadaye Shaaban Robert alitokea, akatawala
uwanja wa utunzi wa riwaya hadi miaka ya 1960, walipotokea kina M.S. Abdulla, na watunzi
wengine. Miaka ya 1970- 1995 wametokea watunzi wengi zaidi, na dhamira nyingi zaidi
zimeshughulikiwa, japo riwaya – pendwa bado imechukua nafasi kubwa katika jumla ya riwaya
za Kiswahili. Katika kipindi hicho vilevile pametokea mikondo na riwaya ya wanakisomo.
Mwisho, wahakiki wengi wa riwaya wamejitokeza pia.

MUHADHARA WA Mwingine
Zoezi:katika makundi ya wanafunzi watatu watatu jibu maswali haya.
1. Unajua kuwa baada ya kozi hii baadhi yenu mnatakiwa kwenda kufundisha riwaya?
2. Je, utaanzia wapi? Wanafunzi wako utawapa mwongozo ulioandikwa na mwingine? Je,
wewe kama mwalimu utakuwa unawategemea wengine kukuandikia miongozo ya
kufundishia? Wakifanya makosa na wewe utayachukua kama yalivyo?
3. Unaweza ukajiandikia mwongozo wa kufundisha riwaya?
Uchambuzi wa Riwaya
Unajua kuwa kwa mwalimu yeyote au msomi yeyote ni jambo la msingi kujua kanuni za
uchambuzi wa riwaya. Katita muhadhara wa 2 tulijifunza kuhusu tanzu za riwaya na historia ya
riwaya katika Afrika Mashariki. Ni matarajio yetu kuwa mwishoni mwa mhadhara huu utakuwa
na uwezo wa:
 Kutambua vipengele vya uchambuzi wa riwaya.
 Kusoma na kuchambua riwaya yoyote ile.
 Kuweza kujitayarishia mwongozo wa kufundishia riwaya endepo wewe ni mwalimu
anayejitayarishia kwenda kufundisha.
Riwaya ni nini?
Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni iliyonyumbuka kifani na kimaudhui na ambayo hutumia
lugha kwa mtindo wa kinathari (masimulizi) katika kuelezea visa changamani na wahusika

Page 24 of 34
ambao huweza kuwa binadamu au wanyama kwa lengo la kusawirisha maisha ya jamii katika
kipindi fulani cha maisha ya jamii husika.

Uchambuzi wa Fani katika Riwaya


Muundo wa riwaya: Huu ni mpangilio wa visa na matukio katika riwaya. Mpangilio huu ndio
hutupa umbo halisi la riwaya. Riwaya huwa na umbo ambalo huweza kuwa katika sura.
Mtiririko wa matukio katika sura hizi huweza kuwa:
(a) Moja kwa moja(msago)
(b) Rejeshi (kioo)
(c) Changamano
Muundo wa Moja kwa Moja (Msago)
Huu ni muundo ambao hutiririsha matukio kwa mpangilio sahili ambapo kuanzia tukio la
kwanza hadi la mwisho hufuatana moja kwa moja bila kuruka au kurudi nyuma. Kwa mfano,
Maria alitunga mimba, akazaa motto wa kiume, motto akaitwa Emanuel, alikuwa katika ukoo wa
Daudi, alianza kazi rasmi ya Mungu akiwa na miaka 30 na alipofikisha miaka 33 alikufa na
kufufuka na alipaa mbinguni baada ya siku saba.

Huu utakuwa muundo wa msago kwa sababu tunaelezwa visa na matukio kwa mtiririko wa moja
kwa moja. Yaani toka mimba, kazaliwa, kukua na kifo. Riwaya nyingi za Ken Walibora hutumia
muundo huu.
Muundo Rejeshi (Kioo)
Huu ni muundo ambao mtiririko wa visa na matukio hupanguliwa katika mfululizo wa kawaida.
Usimulizi wake husonga na kumulika matukio ya nyuma. Kwa mfano: Emanuel anakamatwa na
kuteswa, Maria anatunga mimba na kumzaa Emanuel, kifo cha Emanuel, kukua na kuanza
kufanya kazi rasmi ya Mungu akiwa na umri wa miaka 30 na kukua na kuanza kufanya kazi
rasmi ya Mungu akiwa na umri wa miaka 30 na kupaa kwake siku ya saba baada ya kufufuka.
Riwaya nyingi za Said A Mohammed ni mifano mizuri wa riwaya zilizotumia muundo rejeshi.
Muundo Changamano
Huu ni muundo ambao hutumia miundo miwili ambayo ni msago na urejeshi katika riwaya moja.
Aina hii ya muundo aghalabu huanza na kioo katika sura za kwanza za riwaya na baadaye

Page 25 of 34
hutiririsha matukio kwa mfululizo wa moja kwa moja katika sura/sehemu ya riwaya iliyobaki.
Mfano mzuri wa aina hii ya muundo umetumika katika Nyota ya Rehema

Zingatia:
Uchambuzi wa muundo katika riwaya huzingati mambo yafuatayo:
(a) Riwaya nzima imegawanywa katika sura au sehemu ngapi? Je kila sura au sehemu
ameipa jina?
(b) Mpangilio wa visa na matukio ni wa moja, urejeshi au changamani?
(c) Matukio haya yanasababishana na kutegemeana ili kufikia kilele na kuanza kupata
masuluhisho fulani?

Mtindo katika Riwaya: Mtindo ni jumla ya mbinu anazotumia mwandishi wa riwaya katika
kuwasilisha ujumbe wake. Ni ujuzi wa kujieleza na kusanifu kazi nzima ya fasihi.
(a) Usimulizi na nafsi
(b) Mtindo wa lugha
(c) Matumizi ya tanzu nyingine za fasihi
(d) Uteuzi wa wahusika.
Usimulizi na Nafsi
Katika riwaya, huwa hakuna mtu ambaye anahahithia visa na matukio katika hadithi hiyo.
Msimuliaji huweza kuwa:
(a) Mwandishi mwenyewe Mwandishi ndiye anajua matukio yote.
(b) Mmoja wa wahusika kakika riwaya. Mhusika huyu hujielezea yeye mwenyewe na
wahusika wengine katika hadithi.
Kutokana na usimulizi tunaweza kusema kuwa mwandishi anatumia kwa kiasi kikubwa
moja kati ya nafsi zifuatazo:
(i) Nafsi ya I umoja au wingi.
Kwa mfano:
 Sikumbuki vizuri … Nilitoka .. (nafsi I umoja)
 Tuliondoke siku ile ile … (Nafsi I … wangi)
(ii) Nafsi ya III umoja au wingi

Page 26 of 34
Kwa mfano:-
 Aliondoka asububi … (Nafsi III umoja)
 Waliondoka asubuhi … (Nafsi III wingi)

Zingatia:
Hakuna usimulizi unaotumia nafsi ya II. Hii ni nafsi inayohitaji majibizano. Waandishi huweza
kutumia nafsi ya pili ili kuonesha majibizano ya wahusika fulani. Ikitokea mwandishi ametumia
nafsi ya II katika riwaya yake basi tunapaswa kusema kuwa mwandishi anatumia dayolojia.
Nafsi ya ii hutumiwa kwenye tamthilia.

Mtindo wa Lugha
Riwaya hupambanuliwa kwa matumizi ya lugha ya kinathari (masimulizi) masimulizi ndiyo
hutawala kwa kiasi kikubwa katika kazi ya riwaya. Matukio na visa mbalimbali tunapata kwa
kusimuliwa na mwandishi au mmoja wa wahusika katika riwaya hiyo.

Matumizi ya Tanzu nyingine za Fisihi


Hapa mwandishi wa riwaya wakati mwingine huweza kuingiza vipengele mbalimbali vya tanzu
nyingine ndani ya riwaya. Vipengele huweza kuwa:
(a) Nyimbo
(b) Mashairi
(c) Majibizano
(d) Hadithi
(e) Mchezo wa kuigiza
(f) Matumizi ya barua

Mwandishi hufanya hivyo kwa malengo yafuatayo:


(a) Kuvuta hisia za msomaji
(b) Kumtambulisha mhusika na hisia za mhusika

Page 27 of 34
(c) Kuibua dhamira mbalimbali
(d) Kuakisi mtindo wa maisha ya jamii anayoichora.

Uteuzi wa Wahusika
Mwandishi wa riwaya ndiye humfinyanga mhusika wa aina yoyote ile anayoitaka mwenyewe.
Uumbaji wa wahusika hautokei tu kwa bahati mbaya, ila hutokea kwa makusudi ya mwandishi
mwenyewe. Mwandishi humuumba mhusika katika kazi yake kutokana na kazi anayotaka
‘amtume’ katika kazi yake. Mwandishi huwa na mawazo kichwani mwake ambayo anadhani ni
vyema jamii ikapata. Mawazo hayo huyaweka kinywani mwa mhusika ambaye yeye mwandishi
anadhani kwa muonekano na tabia za mhusika huyo atafanikiwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa
kwa athari ileile anayokusudia mwandishi. Kuna waandishi huamua kuumba wahusika wanyama
ili kuwakilisha tabia na sifa za binadamu ambao pengine zinarandana. Hivyo basi, uumbaji huo
hutokea kuwa ndiyo mazoea ya mwandishi au waandishi fulani na wasomaji wakiona wahusika
wale huweza kusema hii ni kazi ya mwandishi fulani kwa kuangalia wahusika tu bila hata kuona
jina la mwandishi. Kwa sababu hiyo, uteuzi wa wahusika ni muhimu sana katika kazi ya fasihi ili
ujumbe ufike kama ulivyokusudiwa na pengine kumtambulisha mwandishi kuwa huo ndio
mtindo wake.

Wahusika wa Riwaya
Wahusika ni viumbe anavyotumia mwandishi kuelezea migogoro na matatizo yaliyomo katika
jamii inayoshughulikiwa. Wahusika huchukua nafasi ya wanajamii halisi au kuelezea migogoro
iliyomo katika jamii. Ni wawakilishi wa matendo ya wanajamii. Wahusika hujifanya watendaji
halisi wa matendo yanayosimuliwa na msanii. Hivyo huigiza matendo yanayosimuliwa na msanii
na kufanya hivyo huweza kuonesha waziwazi mabaya na mazuri yatendwayo na baadhi ya
wanajamii. Wahusika ndio wanaotumiwa na msamii kuumba sanaa anayotaka.

Tunaposoma riwaya, lazima tujitahidi kuwajua wahusika pamoja na umuhimu wao katika riwaya
hiyo. Tunapoangalia wahusika katika riwaya, tunazingatia mambo yafuatayo:
 Maneno yao – Je wahusika wanasema nini? Maneno yao yanatufunza nini? N.k.

Page 28 of 34
 Maelezo ya mwandishi – Je mwandishi anasema nini kuwahusu? Je anaonesha chuki au
upendeleo kumhusu mhusika fulani? Anataka tumwelewe vipi?, n.k.
 Matendo yao – je wanafanya matendo ya aina gani? Kwa nini wanafanya wafanyavyo?
Wana nia gani? Je ni sababu gani zinawafanya watende watendayo?
 Nafasi zao – wahasika hao wana nafasi gani katika riwaya: ni mhusika yupi anawakilisha
ubaya na yupi anawakilisha uzuri? Je ni wahusika wepi ambao ni wakuu na ni wepi
ambao ni wadogo?, n.k
 Dhima zao – wahusika waliopo wana jukumu gani? Je unafikiri wana mchango wowote
katika hadithi nzima?, n.k. Haya ni baadhi ya mambo ambayo mhakiki/Mchambuzi
anatakiwa kujiuliza anapohakiki wahusika wa riwaya.

Matumizi ya Lugha
Lugha ndiyo ‘mzizi wa riwaya, na bila yenyewe kuwepo haiwezekani kuwa na riwaya. Mtunzi
wa riwaya hutumia lugha kuyaibusha mawazo yake katika hiyo kazi. Lugha ndiyo njia atumiayo
msanii wa riwaya kuyaelezea mambo mbalimbali ya jamii yake kwa njia ya ubunifu.

Matumizi ya lugha yako ya aina aina, humo tunagundua:


(a) Matumizi ya tamathali za semi. Kwa mfano, sitiari, tafsida, tashibiha, tashihisi, n.k.
(b) Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa. Kwa mfano, takriri, mdokezo, majalizo, n.k.
(c) Matumizi ya taswira na ishara mbalimbali
(d) Uteuzi na mpangilio wa maneno/ msamiati
(e) Lugha za wahusika hasa lahaja zao, lafudhi zao, n.k.
(f) Matumizi ya semi nyinginezo. Kwa mfano, msimu, mafumbo, mizungu, n.k.

Mandhari
Mandhari ni neno linalotumiwa kuelezea mazingira, eneo, mahali au wakati wa hadithi ya kazi
ya kifasihi inayohusika. Kila riwaya husimuliwa kwenye mazingira fulani, eneo fulani au mahali
fulani. Mandhari ni nguzo muhimu katika ujenzi wa riwaya. Mandhari huweza kutuelekea
kwenye wasifu wa wahusika, dhamira kuu, toni yake, n.k.

Page 29 of 34
Jina na Jalada la Kitabu
Hapa tunaangalia uhusiano wa jina la kitabu, jalada la kitabu na maudhui yaliyomo ndani ya
kitabu hicho.
(a) Jina la Kitabu
Hapa tunangalia, je Jina la kitabu linasadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?
Mfano: Nyuso za Mwanamke linasadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?.

(b) Picha ya Jalada la Kitabu


Kazi ya fasihi huwa na michoro au picha fulani kwenye majalada yao. Inawezekana majalada
hayo yakawa na uhusiano fulani na dhamira na maudhui ya kazi zinazohusika. Picha hizi huweza
kuwa kielekezo muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi.

Uchambuzi wa Maudhui ya Riwaya


Maudhui ni jumla ya mawazo au dhamira, msimamo, mtazamo, falsafa na ujumbe katika kazi ya
fasihi. Wakati wa kuchunguza maudhui ya riwaya, maswali mbalimbali yanaibuka, kwa mfano
hadhira huweza kujiuliza.
 Je msanii anatueleza nini?
 Je msanii kamtungia mtu wa tabaka gani?
 Anamtukuza nani?
 Anambeza nani?
 Msanii anataka tuchukue hatua gani katika utatuzi wa matatizo ayashughulikiayo katika
kazi yake?

Katika kipengele cha maudhui, huwa tunashughulikia vipengele vifuatavyo:


(a) Dhamira za mwandishi
(b) Ujumbe na maadili
(c) Mtazamo na msimamo wa msanii
(d) Falsafa ya mwandishi
(e) Migogoro aliyoishughulikia msanii.

Page 30 of 34
Ufafanuzi wa Vipengele vya Maudhui
Dhamira
Hili ni wazo au mawazo makuu ambayo yamejitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira hugusa
maeneo yote ya kimaisha. Hugusa uchumi, siasa, utamaduni na shughuli nyingine za kijamii
kama vile elimu, afya na miundo mbinu mbalimbali.

Aina za Dhamira
Kuna aina kuu mbili za dhamira. Aina hizo ni
(a)Dhamira Kuu
(b) Dhamira ndogondogo

Dhamira kuu
Hii ni dhamira ambayo kimsingi ndiyo hubeba dhamira nyingine. Huweza kuwa: ujenzi wa jamii
mpya, ukombozi au mapenzi. Ni wazo kuu moja ambalo hutokana na dhamira ndogondogo.

Dhamira ndogondogo
Hizi ni dhamira mbalimbali ambazo zinatumika kujenga dhamira kuu. Dhamira masuluhisho ya
matatizo hayo. Hivyo dhamira kuu kimsingi hutokana na jumla ya dhamira hizi ndogondogo.
Falsafa
Ni kipengele kimojawapo cha maudhui ambacho kinahusu mwelekeo wa imani ya mwandishi
katika kazi ya fasihi. Kwa mfano: Shaaban Robert aliongozwa na falsafa ya maisha kuwa
binadamu tenda wema maishani. Naye Said A Mohammed anaongozwa na falsafa ya kupigania
haki za wanyonge kwa mfano wanawake, maskini katika riwaya ya Nyuso za mwanamke
anatumia mwanamke kuendeleza falsafa yake.

Ujumbe/ maadili
Ni funzo ambalo msomaji wa kazi ya fasihi hupata baada ya kung’amua dhamira zinazojitokeza
katika kazi ya fasihi.

Page 31 of 34
Mtazamo wa Mwandishi
Huu ni msimamo ambao mwandishi wa kazi ya fasihi anakuwa nao anaposhughulikia matatizo
mbalimbali. Kuna aina mbili za mitazamo:
(a) Mtazamo wa Kidhanifu.
Mtazamo huu mara nyingi hutoa masuluhisho ambayo utekelezaji wake huwa ni mgumu
katika hali halisi. Kwa mfano: “Mapenzi bora ndiyo suluhisho la kila tatizo”. Kuna
matatizo ambayo hayahitaji mapenzi bora kama suluhisho.
(b) Mtazamo wa Kiyakinifu
Huu ni mtazamo wa kimapinduzi ambao huainisha Matatizo na masuluhisho yanayoikabili
jamii. Kwa mfano: umoja na mshikamano, kujitoa mhanga; kuondoa aina zote za dhuluma
ni mfano wa masuluhisho yanayosababishwa na mfumo.

Migogoro
Migogoro ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Katika kigezo cha
migogoro, tunapata migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao,
matabaka yao, n.k. Migogoro hii mara nyingi hujikita katika mahusiano ya kijamii. Migogoro
yaweza kuwa ya:
(a)Kiuchumi – mfano riwaya ya Shida (N. Balisidya), Kasri ya Mwinyi Fuad (S.A. Shafi),
Siku ya Watenzi Wote na Utu Bora Mkulima. (S. Robert), n.k.
(b) Kiutamaduni – kama tunavyoona katika riwaya ya Pepo ya Mabwege, (H. Mwakyembe),
Shida, (No. Balisidya), Vuta n’kavute (Shafi Adam Shafi), n.k.
(c)Kisiasa – kama tuionavyo katika riwaya za Ubeberu Utashindwa (J. K. Kiimbila)
Tamthilia za Kinjikitile (E. Hussein), Mwanzo wa Tufani, (K. K. Kahigi and Ngomera)
Tone la Mwisho (E. Mbogo), n.k.
(d) Kinafsia – Kama ilivyo kwa “Rami” katika riwaya ya Mzalendo (F. K. Senkoro)
akikabiliwa na mgogoro wa kinafsia anaoupima uzalendo wake; na tunamwona josina na
Kalenga katika riwaya ya Pepo ya Mabwege wakizingwa na mgogoro wa kinafsia
utokanao na mvurugano wa maisha unaotokana na uongozi mbaya na athari ya pesa
kataka mapenzi na ndoa. Katika riwaya ya Njia Panda (The River Betweeri) J. Ngugi

Page 32 of 34
tunaona wahusika kama vile Waiyaki, Muthoni, Nyambura, Kabonyi na Joshua
wakikabiliwa na migogoro mbalimbali ya kinafsi.

Maswali ya Kudurusu.

 Eleza maana ya Riwaya kwa kurejelea watalaam mbalimbali.


 Fafanua chimbuko la riwaya.
 Jadili aina mbalimbali za riwaya.
 Kwa kutoa mifano maridhawa, ni mambo gani yaliyochangia
uenezaji wa riwaya za Kiswahili?.
 Eleza sifa za riwaya zinazolenga wanakisomo.
 Eleza juu ya kipengele cha uchambuzi wa fani katika riwaya.
 Jadili mambo ya kuzingatia unapochambua muundo wa wa
riwaya.
 Eleza juu ya kipengele cha mtindo katika riwaya.
 Ni mambo yepi ya kuzingatia wakati wa kuchambua wahusika
katika riwaya?.
 Eleza jinsi utakavyoshughulikia kipengele cha lugha katika
uchambuzi wa riwaya.
 Eleza vipengele vinavyoshughulikiwa katika uchambuzi wa
riwaya.
MAREJELEO
Armah, A.K. (1976). Wema Hawajazaliwa. Nairobi, Kenya: Heinemann Educational
Books.
Chinua, A. (1977). Chinua Achebe. Heinemann Educational Books.
Madumulla, J.S. (2009). Riwaya ya Kiswahili, Historian a Misingi ya Uchambuzi.
Nairobi: Sitima Printer and Stations L.td.
Mulokozi, M.M.(1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili.Dar es Salaam.TUKI.
Mhando, P. na Balisidya,(1976), Fasihi na Sanaa za Maonyesho. Dar es Salaam:
Tanzania Publishing House.
Nkwera, F.V. (1978).Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo.Dar es Salaam: Tanzania
Publishing House.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.Nairobi.Kenya: Oxford University Press.
Ndanda, E.A.(2019). Uchungu wa Mwaridi. Kampala. Uganda. Fountain Publishers.
Senkoro, F.E.M.K.(2011). Fasihi Andishi.Dar es Salaam.Kauttu L.t.d.
Wamitila, K.W.(2003).Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus

Page 33 of 34
Publication.
Wamitila, K.W. ( 1999). Nguvu ya Sala. Nairobi. Kenya.Longhorn Publishers; 1999

Riwaya za Kusoma
Riwaya Zilizoandikwa na WanaUganda
1. Uhasama Kilimani Masereka George Black
2. Uchungu wa Mwaridi Ndanda Antonio
3. Baraka za Mama Muhereza Vincent

Riwaya Zilizoandikwa na Wasio wanaUganda


1. Nagona Euphrase Kezilahabi
2. Nguvu ya Sala Wamitila Wadi Kyallo
3. Kiu Mohammed S. Mohammed

Vitabu Vingine vya Kusoma kwa Ziada


1. Wema Hawajazaliwa Armah, Ayi Kwei
2. Said, A. M. (1980).Utengano. Nairobi, Kenya: Longman Publishers.
3. Said, A.M. 2010. Nyuso za Mwanamke.Nairobi, Kenya: Longhorn Publishers.
4. Mwenda, M. (2010). Msururu wa Usaliti. Nairobi, Kenya: East African
Educational Publishers.
5. Mbogo, M. (1996). Vipuli vya Figo. Nairobi, Kenya: East African Educational
Publishers.
6. Euphrase , K. (2007) Dunia Uwanja wa Fujo. Nairobi, Kenya: Vide-Muwa
Publishers.
7. Walibora, K. W. (1996). Siku Njema. Nairobi, Kenya: Longhorn Publishers.
8. Walibora, K. W. (). Mbaya Wetu. Nairobi, Kenya: Moran (E.A.) Publishers
Limited.
9. Walibora, K. W. (2003). Kufa Kuzikana. Nairobi, Kenya: Longhorn
Publishers.
10. Walibora, K. W. (2006). Ndoto ya Almasi. Nairobi, Kenya:Macmillan Kenya
Publishers
11. Ngugi, T. (1980). Shetani Msalabani. Nairobi, Kenya: East African
Educational Publishers.
12. Chinua, A. (1978). Mshale wa Mungu. Nairobi, Kenya:Heinemann
Educational Book.

Page 34 of 34

You might also like