Dira Ya Sarufi 2023

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 67

DIRA YA SARUFI

(NA ISIMUJAMII)

UCHAMBUZI WA KCSE
(2000-2022)

(PAMOJA NA MAKALA YA SARUFI)

NA
MWALIMU ONYANGO
(MHARIRI: BW. PATRICK MANDILA, KAPSABET BOYS)

TABARUKU KWA WATAHINIWA WOTE WA KCSE, MWAKA WA 2023

1
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
KUHUSU DIRA YA SARUFI
Kitabu hiki ni cha kipekee ambacho kimeangazia takribani masuala yote ya sarufi
na matumizi ya lugha katika shule za upili kwa kuzingatia maswali ya KCSE.
Kitabu hiki ni bora kwa kuwa:
1. Kimeshughulikia sehemu ya sauti za Kiswahili kwa kina.
2. Sentensi ya Kiswahili imeshughulikiwa ipasavyo: virai, vishazi, shamirisho,
chagizo, uchanganuzi wa sentensi na kadhalika.
3. Kila sehemu ina maswali ya KCSE yaliyotahiniwa; 2000-2021.
4. Masuala fiche ya sarufi na matumizi ya lugha yameshughulikiwa.
5. Kuna maswali mengi ya sarufi na matumizi ya lugha na isimujamii pamoja na
majibu yake mwishoni mwa kitabu
6. Kina maswali ya KCSE ya Isimujamii; 2006-2021 pamoja na Majibu ya
kanseli
7. Kuna sehemu ya insha pia; mwaka wa 2000-2021.

Kuhusu Sarufi na Matumizi ya Lugha


Hii ni sehemu ya tatu ya karatasi ya pili (102/2). Ndiyo sehemu ndefu zaidi
katika mtihani wa Kiswahili na hubeba alama 40. Mtahiniwa anafaa kujibu maswali
yote kwa kuzingatia sarufi na hijai. Maswali yanapaswa kujibiwa yalivyoulizwa.
Kazi ya mwanafunzi iwe safi kama pamba. Mtahiniwa asikariri maswali
anapoyajibu.

Kuhusu Mwandishi
Mwalimu Onyango ni mwalimu, mchambuzi na mtafiti wa Kiswahili mwenye ari,
uzoefu na tajriba katika ufundishaji wa somo la Kiswahili. Pamoja na hayo,
Mwalimu Onyango ni mtahini, mtunzi, mhakiki na mhariri wa kazi za Kiswahili.
Ameandika makala ya Dira ya Fasihi, Dira ya Ushairi, Dira ya Isimujamii,
Ngao ya Fasihi, Kielelezo cha Fasihi Simulizi na makala mengine mengi ya
KISWAHILI. . Kwa sasa, ni mwalimu wa Kiswahili na pia Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Uchapishaji la DIRA SERIES.
Tabaruku
Sitamsahau babangu kwa kunikumbusha mara kwa mara kuwa ninafaa kukamilisha
kazi hii ya uandishi. Tabaruku pia kwa mwandani wangu Bw. Mandila ambaye pia
ni mwalimu wa Kiswahili na mtahini mzoefu wa 102/2 kutoka Kapsabet Boys.

2
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
UTANGULIZI
Sarufi ya Kiswahili hasa katika kiwango cha sekondari huangazia matawi ya isimu
kama vile fonetiki, fonolojia, mofolojia, semantiki, sintaksia na pragmatiki.
Vipashio vya lugha ni zao la matawi haya. Vipashio vya lugha ni kama vifuatavyo:
a) Sauti
b) Silabi
c) Maneno
d) Sentensi
Hivi ndivyo vijisehemu vinavyounda lugha ya Kiswahili. Aidha, vipashio hivi
vinahusiana na kutegemeana.

FONETIKI: SAUTI ZA KISWAHILI


Sauti ni mlio unaotokana na mgusano/mkaribiano wa ala za kutamkia.
Kuna aina mbili kuu za sauti katika lugha ya Kiswahili. Hizi ni:
-Irabu
-Konsonanti

Uzalishaji wa Sauti
Sauti hutokana na hewa. Hewa kutoka mapafuni hutatizwa/huchachawizwa katika
bomba la sauti na kusababisha mlio. Hewa hii huitwa mkondo-hewa toka. Mlio huu
huitwa sauti. Konsonanti hutolewa kwa ushirikiano wa ala mbili; tuli na sogezi.

Tofauti kati ya Irabu na Konsonanti

Irabu Konsonanti

a) Hutamkwa kwa ulaini. Hewa kutoka Wakati wa utamkaji, hewa huzuiliwa


mapafuni haizuiliwi katika ala za kutamkia katika ala za kutamkia.
b) Hutamkwa zikiwa pekee Hutamkwa pamoja na irabu.

c) Huunda silabi na maneno zikiwa Haziwezi kuunda


pekee silabi(zinapotamkwa) na maneno

IRABU ZA KISWAHILI
Kiswahili kina irabu tano (na tatu nyingine za kimsingi). Sauti hizi ni a,e,i, o na u.
Kuna vigezo vitatu vya kuanisha irabu za Kiswahili;
a) sehemu ya ulimi ya kutamkia
b) mwinuko wa ulimi
c) hali ya mdomo/midomo

3
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
IRABU SEHEMU YA ULIMI MWINUKO WA ULIMI HALI YA MIDOMO
a Kati Chini Hutandazwa
e Mbele Wastani Hutandazwa
i mbele Juu Hutandazwa
o Nyuma Wastani Huviringwa
u Nyuma juu Huviringwa

KONSONANTI ZA KISWAHILI
Konsonanti za Kiswahili ni 26. Kuna vigezo vitatu pia vya kuainisha konsonanti za
Kiswahili. Hivi ni;
a) mahali pa kutamkia
b) namna ya kutamka
c) hali ya glota
Konsonanti Aina Mahali Mghuno
1. /b/ Kipasuo Midomo Ghuna
2. /ch/ kipasuo-kwamiza kaakaa gumu Sighuna
3. /d/ Kipasuo ufizi/masine Ghuna
4. /dh/ kikwamizo ulimi-meno Ghuna
5. /f/ kikwamizo midomo-meno sighuna
6. /g/ Kipasuo kaakaa laini Ghuna
7. /gh/ kikwamizo kaakaa laini Ghuna
8. /h/ kikwamizo Koromeo Ghuna
9. /j/ Kipasuo Ufizi Ghuna
10. /k/ Kipasuo kaakaa laini sighuna
11. /kh/ kikwamizo kaakaa laini Ghuna
12. /l/ kitambaza Ufizi Ghuna
13. /m/* king’ong’o/nazali Midomo Ghuna
14. /n/ king’ong’o/nazali Ufizi Ghuna
15. /ng’/ king’ong’o/nazali kaakaa laini Ghuna
16. /ny/ king’ong’o/nazali kaakaa gumu Ghuna
17. /p/ Kipasuo Midomo sighuna
18. /r/ kimadende Ufizi Ghuna
19. /s/ kikwamizo Ufizi sighuna
20./sh/ kikwamizo kaakaa gumu sighuna
21. /t/ Kipasuo Ufizi sighuna
22./th/ kikwamizo ulimi-meno sighuna
23./v/ kikwamizo midomo-meno Ghuna
24./w/ kiyeyusho Midomo Ghuna
25./y/ kiyeyusho kaakaa gumu Ghuna
26./z/ kikwamizo Ufizi Ghuna

4
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Kuna konsonanti mbili zinazoitwa likwidi (liquids katika Kiingereza). Konsonanti
hizi ni /l/ na /r/.
Sifa bainifu za sauti ni sifa maalum zinazoitofautisha sauti moja na nyingine. Kwa
mfano, sauti /n/ ni king’ong’o cha ufizi na ni ghuna.

ZOEZI 1
Andika sifa bainifu za sauti zifuatazo:
i. /k/
ii. /ny/
iii. /sh/
iv. /ch/
v. /u/
vi. /s/

ZOEZI 2
Tofautisha sauti zifuatazo:
i. /m/ na /ng’/
ii. /l/ na /r/
iii. /e/ na /o/
iv. /f/ na /k/

ZOEZI 3
Andika maneno yenye mpangilio ufuatao wa sauti:
i. KIKII
ii. KKIKI
iii. IIKI
iv. IKKI
v. IKIKKII
vi. KKKI
vii. KKI

KCSE 2020
Andika maneno yenye miundo ifuatayo: alama 2
i. Kipasuo ghuna cha midomoni, irabu ya chini kati, kipasuo sighuna cha
ufizi, irabu ya juu mbele
ii. Nazali ya ufizi, kipasuo cha kaakaa laini, irabu ya juu nyuma, irabu ya
nyuma wastani

5
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
KCSE 2021

Tofautisha sauti zifuatazo: alama 2


i. /l/ na /r/
ii. /m/ na /b/

KCSE 2022
Andika irabu zenye sifa zifuatazo: alama 1
i) Mbele, juu, tandazwa
ii) Nyuma, kati, viringwa

SAUTI MWAMBATANO
Sauti mwambatano ni sauti ambazo huundwa kwa konsonanti mbili au zaidi na
huongezwa irabu ili kuunda silabi.
Sauti mwambatano hazipatikani katika orodha ya konsonanti ishirini na sita
zilizoorodheshwa katika jedwali la ukurasa wa nne.
Sauti /ch/ katika cha si mwambatano. Aidha, sauti kama vile /sh/, /dh/ na
konsonanti nyingine za herufi mbili si mwambatano. Sauti mwambatano ni kama
vile;
/nd/
/mb/
/nj/
/mbw/
/njw/
/ndw/na kadhalika.

Zingatia jedwali lifuatalo:

SAUTI NENO
/mb/ umba
/mbw/ umbwa
/nj/ onja
/njw/ onjwa
/nd/ unda
/ndw/ undwa
/shw/ oshwa

Sauti mwambatano huwa na muundo wa kki/kkki. Hakuna sauti mwambatano iliyo


na konsonanti zaidi ya tatu.

6
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
MOFOLOJIA
SILABI
Silabi ni pigo moja la sauti katika neno. Pia, silabi ni herufi katika neno
zinazotamkwa kwa pamoja au mara moja. Tunapoainisha silabi, tunazingatia sauti
ya mwisho; irabu au konsonanti.
Kuna aina mbili za silabi:
1. Silabi wazi-hizi huishia kwa irabu. Kwa mfano silabi u-ba-o; zote tatu ni wazi.
2. Silabi funge-hizi huishia kwa konsonanti. Kwa mfano m-tu; silabi m- katika
mtu ni silabi funge.
Miundo ya silabi huhusu sauti zinazounda silabi kwa jumla kinyume na aina ambapo
tunazingatia sauti za mwisho.

Kuna miundo mingi ya silabi kama vile:


MUUNDO MFANO
Irabu pekee u-a, i-ba
Konsonanti pekee m-tu
Konsonanti na irabu Ba-ba
Konsonanti, Konsonanti na irabu i-mba
Konsonanti, Konsonanti, Konsonanti na irabu Mbwe-ha, mbwa, ngwe-nje
Irabu na Konsonanti Al-fajiri

ZOEZI 4
Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
i. runinga
ii. biblia
iii. hariri
iv. shauku
v. shukrani
vi. daktari

Swali 2015
Bainisha silabi katika neno: wanyweshavyo

Maswali mengi huhusu miundo ya silabi na sauti zinazounda silabi. Mfano:


Andika neno lenye muundo ufuatao wa sauti:
irabu+konsonanti+konsonanti+irabu

Swali 2021
Andika neno moja lenye silabi za muundo ufuatao: alama 1
Konsonanti+Konsonanti, Irabu+Konsonanti, Konsonanti, Irabu

7
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
VIPENGELE VYA PROSODIA
SHADDA
Shadda ni mkazo unaotiwa katika silabi ya neno wakati wa utamkaji. Kwa kawaida,
shadda hutiwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno kwa mfano Kiswa’hili.
Wakati mwingine, shadda huwekwa katika silabi tofauti za neno moja ili kuleta
maana tofauti. Maneno haya ni kama vile:
ala
walakini
barabara

Maswali ya KCSE
Weka shadda katika maneno yafuatayo:
miambakofi
yatazoleka
malaika
nge
mteremko
waliotusifia
sherehekea
bingiria
walimwengu

ZOEZI 5
Tia shadda katika maneno yafuatayo:
i. wekeza
ii. karibisha
iii. safari
iv. shinikiza
v. endelevu
vi. mwalimu
vii. rekebisha
viii. shinikizwa

KIIMBO
Kiimbo ni upandaji na ushukaji wa sauti mtu anapozungumza. Majukumu ya kiimbo
ni;
i) Kuonyesha swali
ii) Kuonyesha kauli/taarifa
iii) Kuamrisha
iv) Kuonyesha ombi/rai

8
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
ZOEZI 6
1. Akifisha sentensi ifuatayo ili ilete maana tatu tofauti: Walimu wamefika
2. Kuna uhusiano gani kati ya kiimbo na alama zifuataz za kuakifisha?
i. Kikomo
ii. Koma
iii. Alama hisi

MOFOLOJIA: VIPASHIO VYA KISARUFI VYA MANENO


Hivi ni viambajengo vya maneno vilivyo na maana. Viambajengo hivi hutofautiana
na silabi kwa kuwa silabi ni mapigo ya sauti. Hata hivyo, kuna baadhi ya silabi
zilizo na maana. Kigezo cha maana huibua vipashio viwili vya kimofolojia; viambishi
na mofimu.
Vipashio vya kisarufi ni mofimu na viambishi.

MOFIMU
Mofimu ni kipande cha neno chenye maana. Mofimu pia yaweza kuwa neno
kamili.
Kipande hiki hakigawiki katika sehemu nyingine zenye maana. Kuna aina mbili za
mofimu: mofimu huru na mofimu tegemezi.
Mofimu huru huwa neno kamili kwa mfano kabati, meza, shangazi na kadhalika.
Mofimu huru ni maneno ambayo hayana viambishi.
Mofimu tegemezi ni mofimu ambazo hutegemeana ili kuunda neno kamili. Mofimu
tegemezi huwa na viambishi na mzizi. Maneno mengi ya Kiswahili huundwa kwa
mofimu tegemezi.
Mofimu tegemezi huwasilisha dhana mbalimbali. Dhana zinazowasilishwa na
mofimu tegemezi ni sawa na dhana za viambishi isipokuwa mzizi.
Aidha, kuna makundi mengine mawili ya mofimu, mathalan;
a. Mofimu mzizi ambao ni mzizi wa neno.
b. Mofimu nyambulishi ambavyo ni viambishi vya maneno.

VIAMBISHI
Kwa upande mwingine, kiambishi ni mofimu inayowekwa kwenye mzizi wa neno
ili neno hilo lilete maana iliyokusudiwa.
Kuna aina mbili za viambishi;
a. Viambishi awali; hivi huja kabla ya mzizi.
b. Viambishi tamati; hivi huja baada ya mzizi wa neno.

Mzizi waneno ni sehemu ya neno ambayo ni kiini cha maana ya neno hilo na
haibadiliki neno linaponyambuliwa. Mzizi wa neno pia ni mofimu.
Zingatia neno lifuatalo:
9
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Anasoma
Neno hili lina mofimu nne yaani; a-na-som-a
Mzizi wa neno hili ni –som-
Viambishi ni vitatu yaani; a-na-a
Kwa hivyo, ikiwa neno lina viambishi vinne, neno hili litakuwa na mofimu tano na
mzizi mmoja.
Kumbuka: Viambishi na mzizi wa neno ni mofimu.
Tanbihi: Fanya mazaoezi zaidi katika sehemu hii na utafute ushauri zaidi kutoka
kwa mwalimu wako.

MAJUKUMU YA VIAMBISHI
VIAMBISHI AWALI VIAMBISHI TAMATI
nafsi kauli
ngeli viishio/vitamatishi
wakati mahali
hali wakati
kirejeshi virejeshi
mtendwa/shamirisho
vikanushi
mahali

ZOEZI 7
Panga maneno katika sentensi zifuatazo katika jedwali ili kubainisha mofimu huru
na tegemezi. Sentensi ya kwanza imetolewa kama mfano kwenye jedwali.
1. Amina ni msichana mrembo.
2. Maria alikuwa akipika wali.
3. Mogaka huwachekesha wafuasi wake.
4. Kikombe hiki ni kichafu.
5. Waziri wa kawi ni mchapakazi.
6. Hema limeraruka
7. Waoga wamekimbia waliposikia mayowe.
8. Uchungu wa mwana aujuae ni mzazi.
9. Tarakilishi imenunuliwa leo.
10. Maji safi yatanywewa.

Mofimu Huru Mofimu Tegemezi


Amina msichana
ni mrembo

10
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Maswali ya KCSE
1. 2022
Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo: alama 2
i) anavyojenga
ii) mfariji
2. 2020
Andika maneno yenye mofimu zifuatazo: alama 2
i. Umoja(ngeli ya U-I), mzizi, kiishio
ii. Kikanushi, kiambishi ngeli(KI-VI umoja), mzizi, kauli tendeka, kiishio
3. 2019
Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo:
i. Asemavyo
ii. Mwangwi

4. 2018
Andika neno lenye muundo ufuatao
i) Kiambishi ngeli, wakati uliopita, mzizi, kauli tendwa, kauli
tenda(kiishio)
ii) Kiambishi cha wingi, mzizi

5. 2016
Tambua kiambishi awali na tamati katika neno:
Alalaye
6. 2015
Andika neno moja lenye mofimu zifuatazo:
Nafsi ya kwanza wingi,wakati uliopita, yambwa, mzizi, kauli tendesha, kauli
tenda
7. 2013
Bainisha mofimu katika neno : Atamnywea

8. 2011
Ainisha viambishi katika kitenzi: tutaonana
9. 2008
Tambua mzizi wa neno: msahaulifu
Tambua kiambishi awali na tamati katika neno alaye

11
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
10. 2007
Ainisha viambishi katika neno: Kujidhiki
11. 2006
Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi: Alimchezea

ZOEZI 8
Onyesha mizizi katika maneno yafuatayo:
i. Amepika
ii. Mlango
iii. Tumeshona
iv. Viatu
v. Analalamika

ZOEZI LA 9
1. Andika maneno yenye mipangilio ifuatayo wa viambishi:
i. Kiambishi cha wingi, mzizi, kiishio
ii. Kiambishi cha umoja, mzizi
iii. Mzizi, kielezi cha mahali
2. Eleza uhusiano uliopo baina ya mzizi, viambishi na mofimu.
3. Kwa kutolea mfano, taja silabi tatu ambazo ni viambishi.

VIAMBISHI NA MANENO MAALUM


Viambishi maalumu ni viambishi ambavyo hutekeleza majukumu maalumu ya
kisematiki au ya kimofolojia vinapotokea katika maneno.
Mifano ya viambishi hivi ni kama vile:ji, na, kwa na kadhalika.
Baadhi ya viambishi hivi hutumika kama maneno katika miktadha mingine.
Maneno maalumu ni maneno yaliyo na majukumu mbalimbali ya kimaana katika
sentensi. Mengi ya maneno haya ni viunganishi na vihusishi.
Maneno na viambishi maalumu huwa na majukumu zaidi ya mawili kwa kawaida.
Mtahini arejelee makala mbalimbali ili ajifunze matumizi ya maneno na viambishi
hivi kwa mfano kitabu cha Chemchemi ya Marudio.

Maswali ya KCSE
MWAKA NENO/KIAMBISHI SWALI
2001 -ni Tunaweza kusema katika chumba au
2002 ki matumizi matatu
2003 ka Matumizi
2003 ndivyo Matumizi
2005 kwa Aliimba kwa sauti tamu.

12
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2005 na Halima na Asha wanasaidiana.
2006 na Sofia na Rael wanaandaliwa chai na mpishi.
2006 Huenda mvua ikanyesha kesho.
2006 Miti hukatwa kila siku duniani.
2009 ji matumizi mawili
2010 ku Sikumwelewa alivyoeleza namna ya
kuwatunza mbwa wake.
2012 ku Amani atakutengenezea mpini wa jembe
kisha aelekee kule kwao.
2013 li matumizi matatu
2015 kama kiunganishi
kihusishi
2015 kwa sababu
pamoja na
2015 ka Malik alitia embe kapuni likaiva.
2016 ka Mpishi alipika, akapakua na akagawa
chakula.
2016 hu Balozi huja hapa kila mara.
2016 ji matumizi mawili
2017 o matumizi mawili
2017 kwa i. sehemu ya kitu kizima
ii. namna tendo lilivyofanyika
2019 ku Tunga sentensi mbili.
2021 ni Wasaidieni wale, walinisaidia wakati wa
shida.
2021 vile Kiwakilishi
kielezi
2021 kwa Sehemu ya kitu
Namna
2022 ka matumizi mawili

Tanbihi: Kutotahiniwa kwa viambishi na maneno mengine maalumu katika mitihani


iliyopita hakumaanishi kuwa hayatatahiniwa. Mtahiniwa aelewe matumizi ya
maneno na viambishi vingine.
Mtahiniwa ajibu swali lilivyoulizwa; ikiwa ni kutunga sentensi ili kuonyesha
matumizi, afanye hivyo.

Kwa mfano:
1. Kwa kutolea mifano, onyesha matumizi matatu ya kiambishi –ji- (alama 3)
Majibu
Kuonyesha ukubwa; jibwa
13
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Kuonyesha ngeli; jiwe
Kuonyesha udogo; kijitoto
2. Onyesha matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo:
Tulienda kwake baada ya kutoka kwa Yusufu.
Majibu
Kwake;umilikaji
Kwa;mahali
Rejelea Upeo wa Sarufi na Chemchemi ya Marudio katika sehemu hii kwa
maelezo zaidi.
ZOEZI 10
i. Onyesha matumizi mawili ya kiambishi ‘i’
ii. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi matatu ya neno ‘jinsi’
iii. Tunga sentensi tatu kudhihihirisha matumizi matumizi ya neno ‘na’
iv. Taja majukumu ya viambishi vilivyopigiwa mstari katika sentensi
zifuatazo:
a) Mwerevu amejinyoa.
b) Hamisi amenituma nyumbani.
c) Atakuona akitoka mkutanoni.
v. Tumia neno ‘mle’ katika sentensi moja kudhihirisha maana mbili.
vi. Ainisha viambishi awali katika ‘lililimwa’

NYAKATI NA HALI
Nyakati ni wingi wa wakati. Kuna nyakati tatu katika Kiswahili; wakati uliopo,
wakati ujao na wakati uliopita.
Kuna hali nyingi katika Kiswahili. Tutazame mifano ya nyakati na hali kwa
kuzingatia utahini katika KCSE.
MWAKA WAKATI/HALI SWALI
2003 nge/ngali Tofautisha maana za sentensi
2007 ngali Maana ya: Ningalikuwa na pesa ningalifurahi.
2007 Mwambaji aliimba, akacheza na
akachangamsha sana.
2007 Shangazi huja kila mara.
2011 wakati ujao hali Tunga sentensi
timilifu
2014 wakati ujao hali Geuza sentensi: Dobi huwapigia watu nguo
timilifu pasi.
2015 hali ya mazoea Geuza: Mmomonyoko wa udongo ulipozuiliwa
mashamba yalinawiri.
2017 wakati uliopo hali Tunga sentensi
isiyodhihirika.
2018 wakati ujao hali ya Geuza: Barabara nyingi zimesakafiwa.
14
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
mazoea
2019 wakati uliopita hali Ni wazi kwamba gharama ya maisha itapanda
timilifu bei ya mafuta ikipanda
2020 Wakati uliopita hali ya Bili atawashauri vijana kuhusu umuhimu wa
mazoea michezo.
2021 hali ya mazoea Jani ambalo lilipukutika lilipeperushwa na
upepo.
2022 hali ya mazoea Huduma za afya zilipoboreshwa, viwango vya
maambukizi vilipungua.

Tanbihi 1(nge/ngeli na ngali)


1. Viambishi nge, ngeli na ngali kimsingi huonyesha kuwa matendo yote mawili
hayakutendeka na hivyo kuonyesha kujutia.
2. Viambishi hivi havichanganywi katika sentensi moja.
3. Ngeli na ngali huonyesha kutokuwepo kwa uwezekano wa jambo kufanywa;
hakuna nafasi nyingine(-nge-li-). Nge huonyesha kuwa licha ya kwamba
matendo hayakutendeka, kuna uwezekano.
Tanbihi 2(po)
Kiambishi ‘po’ hurejelea hali tatu:
i. Mahali-mfano; alipo
ii. Wakati maalum(po-awali)-aliponiona
iii. Mazoea/kila mara- (po-tamati)-anionapo

ZOEZI 11
1. Onyesha dhana tatu zinazowasilishwa na kiambishi ‘a’
2. Taja viambishi vitatu vya ukanusho wa nyakati na hali.
3. Kwa kutolea mifano, onyesha matumizi matatu ya kiambishi “po”
4. Kuna tofauti gani kati ya matumizi ya nge na ngeli? Eleza kwa kutumia
mifano.
5. Tunga sentensi inayoonyesha kuwa tendo halikufaulu kutokana na
kutotimizwa kwa tendo lingine.
6. Tunga sentensi katika wakati uliopo, hali isiyodhihirika.
7. Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali na nyakati zilizo mabanoni:
i. Uchoyo wa Omolo umemtatiza sana.(hali ya mazoea)
ii. Kikokotoo kilipoharibika, alitaabika sana.(wakati ujao)
iii. Baraka za mungu ni muhimu kwa binadamu.(wakati uliopita)
iv. Maji yamesafishwa kabla ya kunywewa.(wakati ujao, hali timilifu)
v. Kamusi zitanunuliwa kwa ajili yetu.(wakati uliopita, hali ya kuendelea
katika umoja)
vi. Jitu lilimvamia Hamisi akitoka sokoni. (wakati ujao, hali ya mazoea
wingi)
15
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
SEMANTIKI: AINA ZA MANENO
Kuna aina nane za maneno katika lugha;
1. Nomino-2012i, 2014o, 2017d, 2019c
2. Viwakilishi-2000, 2002, 2008s, 2011a, 2015k, 2016r, 2018d
3. Vivumishi-2003, 2007g, 2010d, 2011a, 2013c, 2016e, 2017d, 2019e
4. Vitenzi-2005, 2007l, 2008r, 2009l, 2010n, 2012m, 2014b,
5. Vielezi-2005, 2006, 2008u, 2009i, 2010f, 2013b, 2018, 2019g
6. Viunganishi-2003, 2004, 2006n, 2011p, 2015m, 2019v
7. Vihusishi-2004, 2008o, 2011k, 2013c, 2016p
8. Vihisishi-2015v, 2017u, 2019r

KCSE 2020
I. Tunga sentensi moja yenye nomino dhahania na kivumishi kimilikishi.
II. Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:
Mwenyewe hakuwa amekupa ruhusa kuitumia.

KCSE 2021
Tunga sentensi kubainisha kiunganishi kitegemezi. Alama 2
Kutokana na mzizi –erevu unda:
i. Nomino
ii. Kivumishi
KCSE 2022
1. Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo: alama 2
Mkulima yupo shambani anapalilia mimea.

2. Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi


ifuatayo: alama 1
Serikali imebuni mikakati ya kukabiliana na nzige wengi wanaovamia mashamba.

3. Tunga sentensi ukitumia kihisishi kinachoibua kinyume cha matarajio. Alama 1

Nomino Viwakilishi Vivumishi Vitenzi Vielezi Viunganishi Vihusishi Vihisishi


1 pekee sifa sifa vikuu namna kujumuisha mahali furaha
ujirani
2 kawaida vionyeshi vionyeshi visaidizi wakati kuchagua wakati huzuni
3 wingi vimilikishi vimilikishi halisi mahali ulinganisho hali kutakia
heri
4 jamii a-unganifu a- vishirikishi idadi sababu au a-unganifu kubeza
unganifu matokeo
5 vitenzi- viulizi viulizi sambamba masharti ulinganishi mshangao

16
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
jina
6 mseto virejeshi virejeshi kukubali mwitikio
7 milikishi idadi idadi kulinganua kukiri
8 dhahania pekee pekee ombi
9 visisitizi visisitizi kiapo
10 nafsi nomino kukanusha
11 ngeli kukemea
12 majuto
13 kutaha-
dharisha

 Tanbihi: Herufi inayofuata mwaka, kwa mfano 2017u, ni swali la u


katika mwaka husika.
 Mtahiniwa awe na umilisi wa aina za maneno kwa kina ili aweze
kujibu maswali haya.
 Kazi hii ni ya Kidato cha pili. Vitabu vya kiada vyenye mchango katika
sehemu hii ni Ijaribu na Uikarabati na kitabu cha Upeo wa Sarufi.
 Kumbuka: Aina za maneno ndio msingi wa Kiswahili. Maswali ya aina
za maneno kamwe hayakosi katika mitihani ya kitaifa.

Majukumu ya Aina za Maneno


Nomino ni majina ya vitu/watu; Viwakilishi hutumika nomino zisipotajwa;
Vivumishi hufafanua nomino na viwakilishi; Vitenzi ni maneno yanayotaja
matendo; Vielezi ni maneno yanayotoa maelezo kuhusu vitenzi, vivumishi na
vielezi vingine; viunganishi ni maneno yanayounganisha maneno mengine na
sentensi; vihusishi ni maneno yanayoonyesha uhusiano baina ya vitu, hali na
kadhalika; vihisishi ni maneno yanoyoonyesha hisia mbalimbali.

VITENZI
Kuna aina tano za vitenzi
a. Vitenzi halisi
b. Vitenzi vikuu
c. Vitenzi visaidizi
d. Vitenzi vishirikishi
e. Vitenzi sambamba
Kuna makundi mawili ya vitenzi
1. Vitenzi vya asili ya kibantu
2. Vitenzi vya asili ya kigeni

17
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Masuala Kuhusu Vitenzi
a. Mnyambuliko wa vitenzi
b. Ukanushaji
c. Vinyume
d. Vitenzi vya Silabi Moja
e. Hali ya Kuamrisha

MAELEZO KUHUSU VITENZI


Kuna aina TANO za vitenzi. Zingatia jedwali lifuatalo:
AINA MAELEZO MIFANO
1 halisi(T) Hutokea pekee katika sentensi. 1. Anasoma.
2. Mama analima.
2 visaidizi(Ts) Ikiwa sentensi ina vitenzi viwili, 1. Mzee alikuwa
cha kwanza ni kisaidizi. Vitenzi akitembea.
visaidizi havionyeshi kitendo. 2. Mwalimu angali
anafunza.
3 vikuu(T) Ikiwa sentensi ina vitenzi viwili, 1. Maji
cha kwanza ni kisaidizi na cha pili yamekwishakum
ni kuku. Kitenzi kikuu ndicho wagika.
kinachoonyesha tendo.
2. Kiranja
anatakakuzungu
mza.
4 vishirikishi(t) ni vya aina mbili:
a. vipungufu Ni vitenzi vidogo visivyochukua ni, si, ki, vi, ndi na
viambishi vingi kama vile kadhalika
viambishi tamati.
b. vikamilifu Ni vitenzi visaidizi ambavyo 1. Alikuwa
hutokea pekee katika sentensi au darasani.
huja baada ya vitenzi visaidizi. 2. Nokoa angali
shambani.
3. Dada alikuwa
angali bafuni.
5 sambamba Vitenzi vikitokea viwili au zaidi 1. Gari limekuwa
katika sentensi, vyote kwa likinguruma.
pamoja ni sambamba. Vitenzi 2. Angela anaimba
sambamba huwa na muundo wa akisoma.
Ts+T na T+T.

Viwakilishi hutekeleza majukumu ya nomino katika sentensi.


Vivumishi na Vielezi hutekeleza la jukumu kutoa maelezo.

18
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Kuna aina nne kuu za vielezi;
a. Vya wakati
b. Vya idadi
c. Vya mahali
d. Vya namna
-hali -vikariri
-halisi -viigizi
-ala -mfanano

ZOEZI 12
Ainisha vitenzi katika sentensi zifuatazo:
iii. Hofu ilitanda baada ya kutangazwa kwa janga hilo.
iv. Matikiti hukuzwa vijijini.
v. Kinyozi alikuwa akimnyoa mteja wake.
vi. Barabara yetu ina mashimo mengi.
vii. Tuliimba tuukicheza usiku kucha.
viii. Vikapu vingali vitupu.

TANBIHI: Kuhusu aina tano kuu za maneno, rejelea Kitabu cha Upeo wa
Sarufi.
Makala mazuri ya viunganishi, vihusishi na vihisishi yanapatikana katika
kitabu cha Ijaribu na Uikarabati.

VITENZI VYA SILABI MOJA.


Hivi ni vitenzi ambavyo mizizi yake ni ya silabi moja. Aghalabu mizizi hii huwa ya
herufi moja hadi tatu. Mtahiniwa anafaa kuelewa maana za vitenzi hivi pamoja na
mnyambuliko wake.
Ili kuleta maana kisarufi, unatakiwa kuongeza kiambishi awali ku- kwa mfano ku-
la, ku-fa na kadhalika.

Vitenzi vya silabi moja ni kumi. Hivi ni:


Kitenzi Maana Mwaka
l.a Tia kitu mdomoni 2000, 2004, 2010, 2012
f.a Tokwa na uhai 2000
w.a Fanyika/tendeka
j.a Fika mahali
p.a Pokeza mtu kitu 2004
ny.a Toa kitu cha majimaji
nyw.a Tia kitu cha majimaji mdomoni 2000, 2012

19
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
pw.a Maji kujaa baharini
ch.a Tokeza kwa jua asubuhi
chw.a Jua kwenda magharibi

Tanbihi:
Herufi zilizo kabla ya vitone ni mizizi ya vitenzi hivi.
Kando na maana nilizoandika, angazia maana zaidi katika kamusi.

ZOEZI 13
1. Tofautisha makundi yafuatayo ya nomino. Tolea mifano.
Nomino za pekee na kawaida
Nomino za wingi na jamii.
2. Eleza tofauti kati ya:
i. Vitenzi vikuu na visaidizi
ii. Vitenzi vikuu na halisi
iii. Vishirikishi vipungufu na vishirikishi vikamilifu
3. Fafanua tofauti za kimatumizi kati ya viwakilishi na vivumishi. Tumia
sentensi. Rejelea jedwali la hapo juu.
4. Jadili aina mbalimbali za viunganishi na vihisishi kwa kuzingatia madhumuni.
5. Taja makundi mawili ya vitenzi vya Kiswahili. toa mifano.
6. Jadili makundi yoyote matatu ya vihusishi.
7. Kivumishi kilichopigiwa mstari:
Mtihani huo ulikuwa mgumu.

NOMINO
Masuala Kuhusu Nomino:
a. Ngeli za nomino
b. Umoja na wingi wa nomino
c. Ukubwa na udogo wa nomino
d. Mizizi ya nomino

NGELI ZA NOMINO
Ili kufahamu umoja na wingi wa nomino, ni lazima mtahiniwa ajue ngeli za maneno
husika. Kuna ngeli nyingi katika Kiswahili. Katika sehemu hii, nitaangazia ngeli
ambazo zimewahi kutahiniwa katika KCSE. Isitoshe, watahiniwa huulizwa
kuandika miundo ya maneno katika ngeli mbalimbali kwa mfano A-WA, LI-YA na
kadhalika. Sehemu hii isipuuzwe katika maandalizi. Kwa mfano:

20
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Onyesha miundo mbalimbali ya nomino katika ngeli ya A-WA
i. m-wa
mtoto-watoto
mzee-wazee
ii. mw-wa
mwalimu-walimu
mwanamke-wanawake
iii. m-mi
mtumi-mitume
iv. ki-vi
kipepeo-vipepeo
v. nomino zisizo na wingi
ng’ombe-ng’ombe
mbu-mbu
vi. nomino zinazochukua viambishi awali-wingi
daktari-madaktari

ZOEZI 14
1. Andika miundo ya maneno katika ngeli zifuatazo:
i. KI-VI
ii. U-ZI
iii. I-ZI
2. Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani?
a) Tumbo
b) Kelele
c) Zuzu
d) Mgaagaa
e) Mkwara
f) Chuki
g) Gozi
h) Ikirahi
i) Kitata
j) Bombwe
3. Andika maneno matano matano katika ngeli zifuatazo:
i. U-I
ii. U-U
iii. YA-YA
iv. I-I
v. KU
vi. U-ZI
vii. I-ZI

21
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Ngeli za maneno hupatikana katika kamusi. Kuna maneno yanayopatikana katika
ngeli zaidi ya moja kwa mfano neno Kiberenge.
Zingatia jedwali lifuatalo:
NENO NGELI MWAKA
neno 2002
kiongozi 2002
mate 2002
chakula
kwetu
U-U 2010
furaha 2011
furaha 2014
nyasi 2014
I-I 2016
A-WA(miundo ya maneno) 2017
ugwe 2018
limau 2018
sukari 2019
teo 2019
U-I 2020
KI-VI
teo 2021
chanda
bendera 2022
ujana

UMOJA NA WINGI
Ni kurejelea nomino pamoja na viambishi vyake vya upatanisho katika hali ya
umoja na wingi. Kuna nomino zinazochukua viambishi katika wingi na nyingine
zisizochukua viambishi. (andika mifano ya nomino hizo) . Pia, nomino nyingine
hutanguliwa na neno akina/kina katika wingi kwa mfano akina mama.
Fanya mazoezi zaidi kuhusu sehemu hii.
Jibu maswali yafuatayo ya KCSE kuhusu umoja na wingi.

UMOJA WINGI
2000
a. Uta wake ni mrefu na mkubwa
sana.
b. Mimi ninataka kumwona

22
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
mwanariadha aliyepata nishani ya
dhahabu.
2001
a. Kwato za wanyama hutufaidi.
b. Mnataka vyeti vya kuwasaidia?
2001
Ukanda
Uzee
2002
a. Mafuta haya yanachuruzika sana.
b. Miinuko ile ndiyo mwanzo wa
Milima ya Chungu.
2003
a. Huku kuimba kwenu kuzuri
kutawapendeza wageni.
b. Hii miche ni mizuri sana,
itatufaa.
2005-Pahala hapa ni pake.
2007-Nyundo hii imevunjika pini wake.
2008-Mvua imebomoa nyumba ya jirani.
2015-Mkihifadhi hizo nafaka vizuri
maeneo haya yatakuwa na vyakula vya
kutosha.
2014-Hao wenyewe hawakuzingatia
mafunzo ya lishe bora.
2017-Maseremala walilainisha mbao
hizo wakatutengenezea meza.
2018-Nahodha alilikwepa jabali hilo,
chombo kikafika ufuoni salama.
2019-Seremala aliulainisha ubao huo ili
kutengeneza kisha amuuzie mlizi huyo
2020- Nyua walizojenga hapa zimesaidia
kukabiliana na wahalifu hao.
2021- Nguo walizouza madukani mwao
ziliwavutia watalii.
2022- Waashi walijenga majumba ya kifahari
ya kupendeza.

Kumbuka: Huwezi kuandika sentensi katika umoja na wingi bila maarifa ya


ngezi za nomino.

23
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
UKUBWA NA UDOGO
Ukubwa na udogo wa nomino ni kuziweka nomino katika hali inayodhihirisha umbo
la kupindukia. Umbo hili laweza kuwa dogo zaidi au kubwa zaidi. Aidha, hali hii
hudhihirisha udunishaji na dharau.

Zingatia jedwali lifuatalo la maswali ya KCSE:


WASTANI UKUBWA UDOGO
2022: Ngoma hizo
zimetengenezwa kwa ngozi
laini.
2020:Mbuzi huyo wake ana
ngozi laini(udogo)
2019: Mtu huyo alifuata njia
iliyomwelekeza mjini.
2018:Nguo ambazo zinauzwa
kwenye duka hilo zinavutia.
2017: Ngoma hizo zao ziliibwa
na wezi wale.
2015: Nyumba hizo zilijengwa
mbali na mji ule.
2013: Madebe hayo
yatasafirishwa pamoja na
nyundo hizi.
2011: Paka mweupe amenaswa
mguuni.
2009: Ndovu wa Kiafrika
ameharibu kichaka.
2006: kiti
2004: ngoma
2001: Mwizi aliiba kikapu na
ng’ombe.

Kumbuka: maneno yanapoandikwa katika ukubwa na udogo, hupoteza miundo ya


kawaida ya kimofolojia. Miundo hii ya udogo na ukubwa haipatikani katika kamusi.

VINYUME
Vinyume ni maneno yanayokinzana/kupingana kimaana. Vinyume pia huitwa
antonimu. Vinyume huandikiwa baadhi ya:
a. nomino kwa mfano nomino za vitenzi jina na nomino za fikra
b. vitenzi
c. vielezi

24
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
d. vivumishi
Mtahiniwa huulizwa kuandika kinyume cha neno, sentensi au maneno katika
sentensi ambayo yamekolezwa au kupigiwa mstari. Nomino za kawaida kwa mfano
mama, dada na kadhalika haziandikiwi vinyume.

Zingatia mifano ifuatayo ya maswali ya KCSE:


MWAKA SWALI
2021 Punde tu alipouliza swali hilo Koru aliingia darasani.
2020 Zito ni kwa jepesi……..ni kwa choyo………ni kwa kali.
2019
2019 Zuri ni kwa baya, aminifu ni kwa………………………..na wivu ni kwa…………………….
2018 Karimu ni kwa choyo………………………ni kwa kukashifu…………………ni kwa tele
2017 Mwanafunzi mkakamavuh uzingatia masomo yake.
2016 Wasichana wanaingia darasani kwa haraka.
2014 Ubora wa kazi zao ulifichikabaada ya kuanzishwa kwa mradi ule.
2011 Watoto wameombwa waanike nguo.
2009 Furaha amehamia mjini.
2008 Wasichana watatu wanaingia darasani kwa haraka.
2006 Mwise alikunja nguo alizokuwa ameanika.
2001 shari, oa
2003 Mjomba alichomeka upanga kwenye ala.

Kumbuka: hakuna vinyume vya nomino za kawaida kama vile baba, msichana na
kadhalika.

MWINGILIANO WA MANENO
Katika mada hii, mtahiniwa huhitajika kubadilisha neno fulani liwe katika kundi
tofauti la maneno. Kwa mfano kugeuza kivumishi kuwa nomino, nomino kuwa
kitenzi na kadhalika.

Zingatia mifano ifuatayo ya maswali ya KCSE. Tutazingatia nomino na vitenzi


pekee.

MWAKA NOMINO KITENZI


2003 mfuasi
2003 kifaa
2003 mharibifu
2004 mtukufu
2004 mchumba
2005 shukuru

25
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2005 enda
2006 chelewa
2006 andika
2007 ghafilika
2008 zingua
2008 tosa
2008 sahili
2015 tathmini*
2015 suluhu*
2016 tafakari
2017 alisamehewa*
2017 alinyenyekea*
2020 Hadithi hiyo ilitungwa vizuri
ikawavutia wengi.(vitenzi viwe
nomino)
2022 Mkurugenzi aliwashauri
wafanyakazi wajibidiishe
kazini.(Geuza yawe nomino)

Ukiulizwa kuunda nomino kutokana na kitenzi, ongeza kiambishi awali ku- kwa
mfano soma-kusoma.
Sehemu hii inabadilika kwa sababu maneno haya hutahiniwa katika sentensi.
Rejelea KCSE 2015 na 2017, 2020

SENTENSI YA KISWAHILI
Sentensi ni neno au mtungo wa maneno yaliyopangwa pamoja kwa utaratibu
maalumu ili kutoa taarifa fulani. Kwa hivyo sentensi yaweza kuwa neno moja au
mawili au zaidi.
Kusudi la sentensi ni kutoa taarifa kwa umantiki. Umantiki ni hali ya kuwepo kwa
ukweli wa kihalisia katika sentensi.
Sentensi ni kipashio cha juu zaidi cha lugha ya Kiswahili.
Sentensi huundwa kwa aina za maneno na iwapo ni neno moja pekee linaloiunda,
neno hilo litakuwa kitenzi. Aidha, uwezo wa kitenzi pekee kuunda sentensi
huchochewa na hali kwamba kitenzi cha sentensi hubeba dhana ya kiima, wakati
na tendo. Kwa mfano;
A-NA-SOMA (He is reading)
a-kiima/mtendaji
na-wakati
soma-tendo

26
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Vipengele vya Sentensi ya Kiswahili
 Muundo wa sentensi
 Uainishaji wa sentensi
 Virai
 Vishazi
 Shamirisho
 Chagizo
 Uamilifu wa sentensi
 Uchanganuzi wa sentensi

MUUNDO WA SENTENSI
Sentensi ya Kiswahili huundwa kwa kiima na kiarifa/kundi tenzi na kundi nomino.
Kiima ni sehemu ya sentensi ya sentensi inayokaliwa na nomino. Hutokea katika
upande wa kushoto wa sentensi na hutangulia kitenzi. Aidha, kiima huweza
kujitokeza ndani ya kitenzi, kwa mfano; Tu-naimba.

Mifano ya Kiima
Mwalimu ameondoka.
Yule ni mzee.
Kalamu yangu imepotea.
Watu waliofika watahudumiwa.
Dhana ya kiima na kundi nomino hufanana kusemantiki na kutofautiana
kisintaksia.
Kiima hutokea mwanzoni mwa sentensi; kundi nomino huweza kutokea popote
kwenye sentensi.

Tazama;
Mhadhiri huyu huendesha gari kubwa.
Mhadhiri huyu-kundi nomino/kiima
Gari kubwa-kundi nomino

Kundi tenzi ni sawa na kiarifa. Ni sehemu ya sentensi inayofuata kundi nomino.


Kundi tenzi huanza kwa kitenzi kikiwa peke au na kufuatwa na maneno mengineyo.
Hili kundi huanza kwa kitenzi hadi mwisho wa sentensi.
Mfano;
Wahasiriwa wa mkasa wa moto walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta.
Nomino/viwakilishi na vitenzi ni maneno makuu/vipashio vya shuruti katika kundi
nomino na kundi tenzi mtawalia.

ZOEZI 15
1. Eleza tofauti baina ya kundi nomino na kiima.
27
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2. Pigia mstari kundi nomino katika:
Simu iliyopotea jana imepatikana kabatini.
Kile ni cha mtoto.

KUAINISHA SENTENSI
Sentensi huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili;
a. Dhamira
b. Muundo

Dhamira
Dhamira ni jukumu/kusudi la sentensi. Aghalabu dhamira ya sentensi hutokana na
uakifishaji wake isipokuwa katika miktadha michache. Dhana hii inhusiana na
kiimbo katika sentensi.
Kuna aina zifuatazo za sentensi;
a) Sentensi arifu
b) Sentensi ulizi
c) Sentensi amrishi
d) Sentensi igizi/ingizi
e) Sentensi agizi
f) Sentensi za rai

KCSE 2020
Tunga sentensi inayoonyesha kwamba kitendo kilifanikiwa kutokana na kufanikiwa
kwa kingine.

KCSE 2021
Tunga sentensi zifuatazo: alama 2
i. agizi
ii. hisishi
Muundo
Kuna aina tatu za sentensi zinazotokana na muundo.
a. Sentensi sahili
b. Sentensi ambatano au ambatani
c. Sentensi changamano/changamani

Muundo wa sentensi hufafanuliwa na vipengele viwili; kipengele cha mawazo na


kile cha vishazi.

28
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Sentensi sahili ni sentensi iliyo na wazo moja. Sentensi sahili huundwa kwa
kishazi kimoja huru. Aghalabu, sentensi sahili huundwa kwa kitenzi kimoja
kikuu/kitenzi halisi.
Mifano
a. Amefika.
b. Nitakuwa kanisani.
c. Mtoto analala.
d. Mama angali anapika sima.

Sentensi ambatano ni sentensi iliyo na mawazo mawili au zaidi. Hii huwa na


vishazi viwili huru vinavyounganishwa. Huwa na vitenzi viwili au zaidi vikuu.

VIRAI
Kirai(R) ni neno au fungu la maneno yasiyo na uhusiano wa kiima na kiarifa na
huwasilisha dhana moja katika sentensi. kuna aina tano za virai;
a. Virai Nomino (RN)-Hivi huanza kwa nomino na kufuatwa na maelezo ya
nomino hiyo. Yaweza kuwa nomino pekee au nomino na maneno mengine.
b. Virai Vielezi (RE)-Hivi huanza kwa kielezi. ni kifungu kinachotoa habari
kuhusu vitenzi.
c. Virai Vitenzi (RT)-Hivi huanza kwa vitenzi hadi mwisho wa sentensi.
d. Virai Vivumishi (RV)-Hiki ni kifungu kinachotoa maelezo kuhusu nomino
katika sentensi. Aghalabu huja baada ya nomino au baada ya kitenzi
kishirikishi kipungufu.
e. Virai Vihusishi (RH)-Huanza kwa kihusishi hadi mwisho wa sentensi.

Tazama mifano katika jedwali lifuatalo:


KIRAI Mifano katika sentensi
nomino 1. Huyu ametibiwa.
2. Magari mapya yamenunuliwa.
3. Waliokosa kufika wataadhibiwa.
kitenzi 1. Mishahara imelipwa.
2. Meli mbili zimeng’oa nanga.
3. Tarakilishi ni kifaa kizuri.
kivumishi 1. Wasichana warembo hunipendeza.
2. Televisheni iliyoibwa jana imepatikana.
3. Walimu hodari sana wametuzwa.
kielezi 1. Simu kubwa sana ni yake.
2. Walifika mkutanoni mapema mno.
3. Twende kanisani.
kihusishi 1. Vitabu viko ndani ya kabati.
29
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2. Tumepita mtihani kuliko wao
3. Amefika katika studio zetu.

Virai vitenzi na virai vihusishi hupigiwa mstari hadi mwisho wa sentensi. Neno la
kwanza katika kirai ndilo aina. Kwa mfano, ikiwa neno la kwanza ni kivumishi,
hicho ni kirai kivumishi. Hata hiyo, kirai kilichopigiwa mstari katika sentensi
ifuatayo ni nomino bali si kirai kivumishi.
Yule kibogoyo anatafuna mifupa.

ZOEZI 16
Ainisha virai katika sentensi zifuatazo
1. Mwalimu wetu ni mwenye bidii.
2. Somo hao wanachukiana.
3. Tutaondoka baada ya chamcha.
4. Dora amefika mapema sana.
5. Wanajeshi mia moja jasiri wamesifiwa.

VISHAZI
Kishazi ni neno au fungu la maneno yaliyo na uhusiano wa kiima na kiarifa na
huwasilisha wazo kamili au lisilo kamili katika sentensi. Sentensi huundwa kwa
vishazi. Kishazi chaweza kuwa sentensi kamili.
Kuna aina mbili za vishazi:
a. Vishazi huru-hivi ni vishazi vinavyowasilisha maana kamili. Kishazi huru
huwa sentensi sahili. Vishazi viwili huru huunda sentensi ambatano ilhali
kishazi huru na tegemezi huunda sentensi changamano.
b. Vishazi tegemezi-hivi ni vishazi ambavyo havitoi maana kamili.
Hutegemeana au kutegemea vishazi huru ili kuunda sentensi. Vishazi
tegemezi huunda sentensi changamano.

Mifano ya vishazi:
Sentensi Kishazi tegemezi Kishazi huru
Mama anapika. Mama anapika.
Balozi amehutubia Balozi amewahutubia
mawaziri. mawaziri.
Wanafunzi wenye bidii Wanafunzi wenye bidii
hupita mtihani. hupita mtihani.
Nilimwona ingawa Nilimwona.
sikumsalimia. Sikumsalimia.
Mpira uliotobolewa jana Mpira uliotobolewa jana umeshonwa
umeshonwa.
Mtoto ambaye alizaliwa Mtoto ambaye alizaliwa na Amepelekwa hospitalini

30
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
na meno amepelekwa meno
hospitalini.
Ukifika uniarifu. Ukifika uniarifu
Tumebeba vitabu ili Ili tuonekane wenye bidii Tumebeba vitabu
tuonekane wenye bidii. Tuonekane wenye bidii
Ungefika mapema Ungefika mkutanoni mapema.
mkutanoni ungemwona Ungemwona katibu mkuu
katibu mkuu.

ZOEZI 17
Onyesha vishazi katika sentensi zifuatazo:
i. Amefika mapema ili amwone mwenyekiti wenu
ii. Mahasimu hao wameridhiana.
iii. Karamu iliyoandaliwa jana itaisha Jumamosi.
iv. Waumini wanapokea sakramenti ya Kitubio.
v. Umati uliowavamia majangili watano umeondoka.
vi. Paka mweusi ameondoka.
vii. Walimu wa Kiswahili ni werevu.
viii. Vijana wanapaswa kujitegemea sana.
ix. Mashambulizi hayo yaliwaangamiza raia wengi.
x. Umu na nduguze waliachwa na mama yao.
xi. Hofu imetanda katika taifa la Urusi.
xii. Wazazi wote watahutubiwa baada ya chamcha.
xiii. Upendo wao uliwatangamanisha sana.

SHAMIRISHO
Shamirisho ni nomino katika sentensi ambazo hupokea athari ya kitendo. Kuna
aina tatu za shamirisho. Shamirisho pia huitwa yambwa. Aidha, shamirisho pia
yaweza kuwa kiambishi kinachowakilisha ngeli ya nomino katika kitenzi iwapo
nomino haijatajwa. Kwa mfano; Alilimiwa.

Kuna aina tatu za shamirisho:


a. Shamirisho kipozi/yambwa tendwa
b. Shamirisho kitondo/yambwa tendewa
c. Shamirisho ala/kitumizi

Tazama mifano ifuatayo:


Sentensi SH-kipozi SH-kitondo SH-ala Chagizo
Amelimiwa asubuhi. A asubuhi
Mtoto uji Mtoto

31
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
amenyweshwa uji na
mama.
Kasisi wetu ushauri waumini wote
amewapa waumini nasaha
wote ushauri nasaha
Babu gari lake Babu
ametengenezewa
gari lake na fundi
stadi.
Tulilimiwa shamba shamba Tu trekta juzi
kubwa kwa trekta kubwa
juzi.
Mwalimu mkuu zawadi wanafunzi gwarideni
amewapa wanafunzi
zawadi gwarideni.

Kumbuka:
Mara nyingi, nomino mbili zikifuatana katika kundi tenzi, ya kwanza ni shamirisho
kitondo na ya pili ni shamirisho kipozi. Kwa mfano;
Baba amemnunulia mama leso.
Mara nyingi, shamirisho kitondo huwa mtu au watu/nomino hisivu.

ZOEZI 18 A
Ainisha shamirisho katika sentensi zifuatazo:
1. Babu ameniletea bakora.
2. Mazuu atawaingia kuku kwa kisu.
3. Omari amemnunulia Amina gari kwa hundi.
4. Tutapewa vifaa vipya kesho.
5. Waokoaji wamenunuliwa mitungi mipya ya oksijeni na serikali.
6. Watoto wameitwa na mama yao.

ZOEZI 18 B
Anza sentensi zifuatazo kwa shamirisho zilizo mabanoni.
1. Museu amemuuzia Muutu shamba bandia.(kipozi)
2. Amempa tarakilishi ya bei ghali.(kitondo)
3. Wamezoa takataka kwa reki.(ala)

32
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
CHAGIZO
Chagizo ni neno au fungu la maneno yanayotoa taarifa kuhusu vitenzi au vielezi.
Chagizo ni sawa na kielezi au kundi elezi au kirai kielezi. Aina za chagizo ni
sawa na aina za vielezi. Mathalan;

a. Chagizo ya mahali
b. Chagizo ya wakati
c. Chagizo ya idadi
d. Chagizo ya namna

Utahini wa Sehemu hii Katika KCSE


SHAMIRISHO VIRAI VISHAZI CHAGIZO
2022-Wanakijiji Vipepeo wale weupe 2022-Wanakijiji
waliwajengea wanaashiria mvua ya waliwajengea
wakongwe nyumba masika wakongwe nyumba
kwa mawe.(yambwa) inayotarajiwa kwa mawe.
mwakani.
2021-Anza kwa 2021-Wale wengine 2021-Tunga
yambwa tendewa: watasafiri sentensi moja
Andai alimnywesha ughaibuni kwa kubainisha kishazi
babu uji kwa ndege. huru na kishazi
kikombe. kitegemezi
2020-Tunga
sentensi yenye
kishazi kirejeshi
ambacho ni kielezi.
2019-Zumari 2019-Usalama 2019-Zumari
alimtunzia Keto ukiimarishwa alimtunzia Keto
watoto hao kwa watalii wengi watoto hao kwa
upendo. watakuwa wanazuru upendo.
humu.

2017-Mhunzi 2018-Viongozi 2017-Viwanda 2015-Mwenyewe


alimfulia mjukuu wengi walikuwa vikianzishwa alikipenda kwa
wake pete ya waadilifu mno kabla mashambani idadi dhati.
shaba. ya uchaguzi mkuu. ya wanaohamia
mjini itapunguzwa.
2008-Mpishi 2017-Kirai kihusishi 2007-Mkulima 2008-Mchezaji
amempikia mgeni kama kielezi aliyepanda wakati aliucheza mpira
wali vizuri. ufaao amepata mjini
mavuno mazuri Malindi.(Ibadilishe
chagizo ya mahali

33
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
kwa ile ya wakati)
2014-Wafugaji 2014-Zana hizi 2013-Ingawa 2012-Watahiniwa
waliwakatia zimeundwa na mshahara wake si hao walisoma
ng’ombe wote mafundiwenye mkubwa anaikimu maswali yote kwa
majani ya mti huo. ustadi mkubwa. familia yake. makini.
(anza kwa yambwa
tendwa)
2011-Kipkemboi 2013-Ubaguzi wa 2015-Tunga 2010-Vibarua
alimbebea mwalimu kijinsia sentensi yenye wamefanya kazi
mzigo kwa gari. umekashifiwa na kishazi kirejeshi haraka ipasavyo.
viongozi wenye ambacho ni
msimamo dhabiti kivumishi.
mno.
2010-Vibarua
wamefanya kazi
haraka ipasavyo.

UCHANGANUZI WA SENTENSI
Zingatia mambo yafuatayo unapochanganua sentensi;
 aina ya sentensi
 kundi nomino na kundi tenzi
 aina za maneno
 mtindo wa uchanganuzi
Mtahiniwa afanye mazoezi mengi katika sehemu hii.

Maswali ya KCSE
Mwaka Swali Mtindo
2022 KN(N+s)+KT(T)+KN(N+V) Tunga sentensi
2021 Wakulima hawa wanapanda zao hili daima. mstari
2020 KN(N+RH)+KT(T+E) Tunga sentensi
2019 Mvua imepusa na watu wameanza mstari
kuondoka.
2018 a. Hili lake lilikuwa limeiva lakini mstari
hatukujua.
b. Mkufu wa umu unapendeza sana.
2017 KN(N+RH)+KT(Ts+T) Tunga sentensi zenye
KN(V+N)+KT(t+v) miundo ifuatayo.
2016 Mpira ulichezwa tulipokuwa tunapika. Matawi
2015 Mvua ilinyesha tulipokuwa tukilima. Matawi
2014 Lililimwa vizuri sana Matawi
KN(N)+KT(T+E)+U+KN(N)+KT(T+E) Tunga sentensi
34
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2011 Maria alipika taratibu huku mama Jedwali
akimwelekeza vizuri.
2010 Amina na Mustafa huimba vizuri Mistari/mishale
2009 Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita Matawi
mtihani.
2008 Paka mdogo amepanda mchungwani matawi
2007 Mvulana mrefu anavuka barabara Jedwali
2006 Mkulima mzembe amepata hasara matawi

Majaribio zaidi ya Uchanganuzi wa Sentensi


1 S

KN KT

N V T E

Mama mzazi amepanda uchagani (½ x 8 = alama 4)

S ½
S1 U S2 ½
KN KT KN KT1/2 ½
N T E t V½
Twiga hukimbia mbio ingawa ni mrefu ½

3
S√ ½
KN√ ½ KT√ ½
N√ ̅S√ ½ t√ ½ N V√ ½
½
Rehema ambaye huimba taarabu ni Mwanamke Mpole

35
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
S1
S1 U S2
KN KT KN KT
N T E N KT
Wanafunzi walisoma taratibu huku N T E
mwalimu akiwaeleza vizuri
6
S

SI U S2

KN KT KN KT

N V T E U N T N

Walimu shupavu walifunza vizuri lakini wanafunzi hawakupita mtihani

7. Mwanafunzi mmoja mtundu aliadhibiwa vikali, lakini hakutumwa nyumban

S1 U S2

KN KT KN KT

N KV T E T E

V V Ø

Mwanafunzi mmoja mtundu aliadhibiwa vikali lakini (mwanafunzi) hakutumwanyumbani 16x ¼ =4

36
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
9
S
KN KT
N V E S̅ T H N V
mkongojo mrefu sana ulioletewa utauzwa na fundi mcheshi
babu

10 S

KT
KN

T H KN2
N1
N2 S̅

Mlango umevunjwa na fundi aliyeujenga


11.
S-S1+U+S2
S1-KN+KT
KN-N
N-Rais
KT-T
T-alihutubu
U-lakini
S2-KN+KT
KN-Ø
KT-T
T-walimpuuza. 8x ½

12 Wachezaji vikapu watakifanikiwa katika mechi hiyo watatuzwa medali

S
KN KT
N V S̅ T N
Wachezaji vikapu wakifanikiwa katika mechi watatuzwa medali
hiyo

13
S
S1 S2
KN KT U KN KT
N T T KN Ø T N E

N
Omondi anaazimia kuwa mhasibu lakini hatii bidii masomoni

37
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
14
S
S1 U S2
KN KT KN KT
T N N T E
Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri

15.
S
KN KT
N T H N V E
Gofu hushabikiwa na watu wachache sana

16.
S1/2
S1 U S2
KN KT KN KT
N V T N T
Mtoto anacheza Huku mama anapiKa
huyu

17.
S
KN KT
N V t V
Sifa mzuri ni zake

18.
S  KN + KT

KN  N + S
N  Mtanzania

S  ambaye alifika jana
KT  t + V
t  ni
V  huyu

19.

S
S1 U S2
KN KT KN KT
 T N V N T N V

Amejenga nyumba nzuri lakini Kombo amejenga nyumba ndefu


38
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
20
S  KN + KT ½
KN  N+U+N ½
N  Kuku ½
U  na ½
N  mbuzi ½
KT  t+N ½
t  ni ½
N  Mifugo ½

Zoezi 19
Changanua sentensi zifuatazo kwa njia zilizo mabanoni:
1. Afrika mpya yapendeza(matawi)
2. Ukarimu wenu umewafurahisha wageni(mstari)
3. Waoga wote waliofika leo watafukuzwa(vistari)
4. Mahabusu walihepa baada ya msimamizi kuondoka.(jedwali)
5. Karne hii imeshuhudia ufeministi mkubwa sana(matawi)
6. Karim amefika mapema lakini Eddah amechelewa(jedwali)
7. Simu yake kubwa imeibwa na mwanafunzi mtundu(vistari)
8. Mkufunzi mwenye tajriba ataajiriwa.
9. Maovu huandamana na majuto.(mstari)
10. Mwangeka ni binamuye Mwangemi.(jedwali)

KUUNGANISHA SENTENSI
Katika sehemu hii, mtahiniwa huulizwa kuunganisha sentensi mbili kwa kuzingatia
maagizo aliyopewa. Aina za sentensi zinazozaliwa na kuunganishwa kwa sentensi
mbili au zaidi ni sentensi ambatano au changamano.
Jedwali lifuatalo linaonyesha maswali mbalimbali ya KCSE yanayohusu mada hii.
Mwaka Sentensi Unganisha/Masharti
Husika
2001 Mwanafunzi amesoma kwa bidii.
Mwanafunzi anataka kupita mtihani.

2001 Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi


hapa.
2003 Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina
chumvi.
2003 Romeo aliamka. Alitazama saa yake. Akala
kiamsha kinywa mbio mbio.
2006 1. Selina alijitahidi sana. Tumia ‘japo’
2. Selina hakushinda mbio hizo.
2008 1. Mwanafunzi yule ni mrefu.
39
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2. Mwanafunzi yule amepita mtuhani.
2013 Osore amempigia Ngungui simu. Ngungui Usirudie kitenzi
amempigia Osore simu.
2017 Kheri aliweza kutujengea hospitali.
Atajenga zahanati pia.
2017 Zumari anasoma Uanasheria. Vilevile Maki
anasomea Uanasheria.
2018 Maji yalijaa. Maji yalimwagika. Unda changamano
2019 Mhandisi alikarabati mtambo. Bila kutumia kiunganishi
Mtambo ulikuwa kiwandani.
2019 Vyakula viliandaliwa. Vyakula vilikuwa na Unda sentensi
viinilisha muhimu. changamano
2020 Maafisa hao walipewa uhamisho. Maafisa Unda ambatano
wengine hawakupewa.
2020 Tunda halitaoshwa vyema. Tunda Tumia ‘po’
halitalika.
2020 Kengewa alitoa ahadi. Wengi waliiamini Anza kwa ‘Ahadi…
ahadi hiyo.
2021 Zimwi lilizidi kukimbia. Unganisha kuwa sentensi
Shujaa aliongeza mwendo kulifikia. moja kwa kutumia neno
‘kadiri’
2022 Watalii walifika katika mbuga ya Tsavo Tumia amba
walikowaona wanyamapori.

SENTENSI TATANISHI
Sentensi tatanishi ni sentensi iliyo na maana zaidi ya moja. Dhana hii ya isimu
huitwa utata katika sentensi. Utata katika sentensi hutokana na mambo
yafuatayo:
i) Matumizi ya vitawe kwa mfano mbuzi.
ii) Uakifishaji wa sentensi.
iii) Matumizi ya vifupisho km mwanawe.
iv) Matumizi ya maneno kwa mfano nay a kiunganishi na kihusishi.
v) Kauli ya kutendea kwa mfano alimpigia
vi) Matumizi ya kiambishi –wa- kwa mfano atawaonya

Maswali ya KCSE
MWAKA SWALI
2022 Jena angalifuata ushauri wa mwelekezi wake angalifaulu-maana
mbili
2021 Fundi alimkatia Makaa utepe huo.
2018 Medi anasema atawarithisha nyumba yake-maana mbili
40
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2017 Bedui alimrushia tufe-maana mbili
2016 Tuliitwa na Baba-maana mbili
2014 Wakimbizi walisema kuwa walitamani kurudi kwao mwaka huo-
maana mbili
2012 Julius Kiptoo mwanawe Kungu na Justine walikiletea kijiji chao
sifa-akifisha ili ilete dhana tatu tofauti
2011 Tuliitwa na Juma-maana mbili
2010 Nenda Ukaniletee mbuzi-maana mbili
2009 Kiharusi chake kimewatia hofu-maana mbili
2007 Hawa ni watoto wa marehemu Bw. Nzovu na Bi. Makambo.
2008 Yohana alimpigia Husha mpira-maana mbili
2005 Mamake Juma na Mariamu walitutembelea-maana mbili
2003 Alinunuliwa samaki na mtoto wake-maana nne
2001 Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala-maana mbili

UAKIFISHAJI
Huu ni uwekaji wa alama za uandishi katika maandishi.
Alama za uakifishaji ni alama zinazotumiwa wakati wa kuandika pamoja na herufi.
Mtahiniwa huulizwa maswali mawili katika sehemu hii:
i) Eleza matumizi ya
Au
ii) Akifisha kifungu

Tanbihi
Ni muhimu kulijibu swali jinsi alivyoulizwa. Iwapo ameambiwa ataje kwa
kutolea mifano, afanye vivyo hivyo.
Uakifishaji wa vifungu vya maneno una uhusiano wa karibu na uandishi
wa semi; yaani, taarifa na halisi. Hata hivyo, katika kuakifisha vifungu
vya maneno/sentensi, mwanafunzi hapaswi kuondoa au kuongeza neno au
maneno.

Alama za uakifishaji ni kama vile:(kuna miaka ya utahini wake baada ya kistari


kifupi)
1. Kikomo/kitone/nukta(.)
2. Kituo/kipumuo/koma/mkato(,)
3. Alama ya kunukuu/alama za mtajo(‘’ ‘’)2017
4. Alama ya kiulizi(?)
5. Alama ya hisi/mshangao(!)-2000, 2010
6. Alama ya nukta mbili/koloni(:)-2007, 2014
7. Alama ya nukta-kituo/semi koloni/nukta mkato(;)-2010, 2004
8. Kistari kifupi(-)
41
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
9. Kistari kirefu-2013
10. Mstari(________________)
11. Mabano/parandesi/vifungo () {}[]-2000
12. Mkwaju/mshazari(/)-2022
13. Kinyota(*)
14. Alama ya mlazo/italiki(h)
15. Alama ya herufi kubwa-2010
16. Herufi nzito
17. Ritifaa/kibainishi(‘)-2000, 2006
18. Nukta za dukuduku/mdokezo(…)-2000

ZOEZI 20
Andika matumizi matatu matatu ya alama 18 za kuakifisha. Tunga sentensi
kwa kila mojawapo.

KUAKIFISHA SENTENSI/TUNGO MBALIMBALI


2015: jihadhari akasema kulei uamuzi wako unaweza kukuathiri vibaya. al. 2
2002: watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini
kufanya hivyo ni sawa
2008: huenda serikali iwazie kuidhibiti bei ya petrol hatuwezi kuyaruhusu
makampuni ya petroli kunyanyasa umma alisema waziri wa kawi bei
yapetroli imeongezwa mara nne katika kipindi cha mwezi mmoja
2011: mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau
umjue mtoto aliuliza nani babu?
2015: basi mwanangu akasema daudi hivyo ndivyo tunavyoweza kufikia
vision 2030 wewe unaonaje

2016: shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwenu jioni mtoto


aliuliza kwetu wapi?
2018: jihadhari akasema kulei uamuzi wako unaweza kukuathiri vibaya
2020 :Mwanangu akasema Neema huku amemkazia macho huoni

unamtilia mwenzako wasiwasi

Tanbihi
Rejelea matumizi ya alama mbalimbali za kuakifisha katika kitabu cha
Kiswahili Kitukuzwe, kidato cha kwanza/Upeo wa sarufi.

KCSE 2021
Akifisha: lo kadio hamadi ndiye mwandishi wa kisiwa chenye tunu. Alama 2

42
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
KCSE 2022
Alama ya mshazari hutumiwa kutenga nambari. Tunga sentensi moja kuonyesha
matumizi mengine ya mshazari. Alama 1

USEMI HALISI NA USEMI WA TAARIFA


KCSE 2000-2020

Yafuatayo ni maswali ya KCSE ya uandishi wa usemi halisi na taarifa:


USEMI HALISI USEMI WA TAARIFA
2022: Watunza mazingira
watanadhifisha soko letu kesho.”
Chifu aliwaambia wafanyibiashara.
2021: Mama alimwita Juma na kutaka kujua
namna alivyofaulu kuuzima moto huo.
2019: Mkurugenzi alisema kwamba wangetoa
nyongeza ya mshahara mwaka ambao
ungefuata.
2017:“Kusoma kwa mapana
kutapalilia ubunifu wa wanafunzi
hawa wenu,”
2016: “Shughuli yetu itakamilika
kesho,” mama alimwambia
mwanawe Juma.
2012: “Shughuli yetu itakamilika
kesho,” mama alimwambia
mwanawe Juma.
2010: “Mito yetu imechafuka
sana; itabidi tuungane mikono
wakubwa kwa wadogo, wanaume
kwa wanawake ili tuisafishe.”
Mwanamazingira alituhimiza.

2009: Baba alipotuuliza kama tungpenda


kwenda Mombasa wakati wa likizo tulimjibu
kwamba tulitaka kwenda Kisumu kwa kuwa
tulikuwa hatujaliona Ziwa Viktoria.
2007: “Nitakuarifu nikimwona,”
Elma alisema.
2006: “Sitathubutu kumpa pesa
zangu,” Mkolwe alisema.
2004: Watoto waliambiwa na mama yao
43
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
watakaporudi nyumbani waoge, wale, halafu
waanze kusoma moja kwa moja badala ya
kuharibu wakati wao kwa kutazama vipindi
vya runinga. Aliwakumbusha kuwa
wanaofanya maonyesho kwenye runinga
tayari wamefuzu shuleni na wameajiriwa
kazi.
2001:
Mama alisema nichukue nafaka yetu
nikauze sokoni.
Mwalimu aliomba aletewe vitabu
vyake kutoka darasani.

2003: Tajiri alishangaa kuwa niliweza


kuubeba mzigo huo peke yangu.

SWALI
Fafanua mabadiliko yoyote matano yanayotokana na ugeuzaji wa usemi halisi
hadi usemi wa taarifa. Rejelea Kiswahili Kitukuzwe, kidato cha Pili.

MAANA ZA MANENO: VITATE, VISAWE NA VITAWE

Katika sehemu hii, tunashughulikia maana za maneno. Kwa hivyo, mchango wa


kamusi ni wa manufaa makubwa zaidi.
Vitate ni maneno ambayo hutatanisha kimatamshi. Visawe ni maneno yenye maana
sawa. Vitawe ni maneno yaliyo na maana zaidi ya moja.
Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja (uk. 584-588) imeshughulikia mada hii
kwa kina.

Lifuatalo ni jedwali linaloonyesha utahini wa sehemu hii katika mtihani wa kitaifa.


VITATE VISAWE VITAWE
2022-Baraste ni kwa hema-2022
barabara, hekima ni
kwa…………..na sihi ni
kwa………………
somo-2021
dua, tua Musei alikumbwa na zima-2020
matatizo mengi lakini
hakukata tamaa. 2020
2019-Jepesi ni kwa
rahisi, ukuta ni
kwa………………..na njia ni

44
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
kwa………………………..
gharama/karama 2014 doa, omba 2017 kata 2018
koga/konga 2012 medali, mchuano 2014 kinga 2014
karama/gharama 2007 enda kombo 2013 kanda 2013
suka/zuka 2006 sahibu, kisunzi 2012 barabara 2010
nduni/duni 2003 ukuta, mvulana, chuma 2011
akiuparaga 2009
mbari/mbali 2002 maarufu, ukoo, faida chuo 2008
2018
kaakaa/gaagaa 2002 andika 2004
ini/hini 2001 audi 2002
tairi/tahiri 2001 sarafu 2001
rithi/ridhi 2017 kejeli 2001
fito/vito 2015 daktari 2001
pembe 2007

UKANUSHAJI NA UYAKINISHAJI
Kukanusha ni kupinga/kukataa. Kuyakinisha ni kukubali. Dhana ya kukanusha ni
tofauti na dhana ya vinyume. Zingatia mifano ifuatayo ya maswali ya KCSE.

KANUSHA YAKINISHA
2022-Wanariadha wameenda uwanjani
kufanya mazoezi.
2021: Makuli hawajakuarifu kwamba
mizigo hiyo haikuwa yetu?
2020-Ngoma hizo zilihifadhiwa ili
ziuzwe mjini.
2019: Badi huwa hapitii hapa, huenda
usimpate.
2018: Mkulima anahitaji magunia haya.
2016: Askari wasipopiga doria wala
kushirikiana na raia hawatakuwa
wametuhakikishia usalama.
2014: Wanafunzi waliingia darasani,
wakatoa vitabu waanza kusoma.
2013: Askari wasipopiga doria wala
kushirikiana na raia hawatakuwa
wametuhakikishia usalama.

2011: Mgonjwa huyo alipona na kurejea

45
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
nyumbani.
2010: Usingeacha masomo,
usingetaabika vile.
2009: Hapo napo ndipo nitakapo.
2008: Sisi tumemaliza kujenga nyumba
ambayo ingalikuwa yake angalifurahi.
2006: Ningalikuwa na pesa ningalinunua
nyumba.
2005: Tumechukua nguo chache kuuza.
2003: Ungemuuliza vizuri angekujibu
bila wasiwasi.
2002
a. Matawi ya mti ambayo yalikauka
yalikatwa.
b. Matofali haya yanatumiwa kwa
ujenzi wa nyumba.

Tanbihi: Fanya mazoezi zaidi kuhusu uyakinishaji na ukanushaji.

KUBADILISHA MIUNDO YA SENTENSI


Katika sehemu hii, mtahiniwa huulizwa kuanza sentensi iliyoandikwa kwa neno
fulani. Ili kufanya hivi, ni muhimu mtahiniwa aweze kuelewa maana na muundo wa
sentensi husika. Anapotekeleza hili, anatakiwa kufanya hivyo bila kubadilisha
maana ya sentensi husika. Hii ni sehemu muhimu sana inayotakiwa kuzingatiwa
katika sarufi.

Yafuatayo ni baadhi ya maswali ya KCSE yanayotahini ufahamu na uzingatifu wa


maagizo uliyopewa.
Swali Anza kwa/Maagizo mwaka
Nimemleta paka ili aue Panya… 2003
panya wote
wanaotusumbua hapa
kwetu nyumbani.
Mbwa ambaye aliripotiwa Katika bwawa la maji… 2003
kuwa ameibwa
amepatikana katika bwa
la maji.

Alicheza kwa bidii Kucheza… 2004


46
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
akawafurahisha wengi
waliohudhuria tamasha
hizo.
Karamu hiyo ilifana sana, Chakula… 2004
kila mtu alikula chakula
akatosheka.
Nilikuwa nimejitayarisha Safari… 2005
vizuri kwa hivyo sikuona
ugumu wowote katika
safari yangu.
Mhunzi mrefu alishinda Tuzo… 2006
Tuzo.
Mwanafunzi huyu Anza kwa kiashiria kisisitizi 2006
anasoma Kifaransa.
Mama alishangilia harusi Mwana… 2011
ya mwana.
Wachezaji hawakucheza Mpira… 2014
mpira kwa sababu ya
mvua.
Chakula kinachozalisha Viinilishe vingi… 2015
kwa njia ya kiasili kina
viinilishe vingi.
Kaumu amewafanya Mifugo wangu…usitumie 2017
mifugo wangu wanywe ‘amewafanya’
maji.
Maeneo haya yana uyoga. Uyoga… 2017
Muutu aliwalea watoto wa Watoto wa maki… 2018
Maki.
Wageni wamefika. Wanafunzi… 2018
Wanafunzi wamefurahi.
Kengewa alitoa ahadi. Ahadi… 2020
Wengi waliamini ahadi
hiyo.
Seremala alilainisha Mbao… 2021
mbao. Seremala alikuwa
kiwandani.
Wahandisi walikarabati Barabara… 2022
barabara zote baada ya
mafuriko.

47
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
KUSAHIHISHA SENTENSI
Katika mada hii, mwanafunzi huulizwa kusahihisha sentensi iliyopewa. Ili
kusahihisha sentensi, mtahiniwa anafaa kufahamu ngeli za maneno yaliyo katika
senyensi pamoja na upatanisho wake wa kisarufi. Aidha, anafaa kufahamu
matumizi ya maneno katika sentensi pamoja na kufahamu msamiati.
Anaposahihisha sentensi, mtahiniwa hafai kuongeza au kuondoa baadhi ya
maneno. Hata hivyo, hili halizingatiwi katika maswali yote.

Yafuatayo ni maswali ya KCSE kuhusu suala hili:


MWAKA SWALI JIBU
2000 Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na
mzuri.
2000 Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa
sababu zimeiva vizuri sana.
2001 Kikombe chenye kimevunjika ni kipya.
2001 Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu.
2002 Kile kitabu kilipasuka ni changu.
2002 Mtoto mwenye ameanguka ni ndugu
yangu.
2006 Mtoto ambaye niliyemsomea ameasi
jamii.
2008 Waya yangu imepotea.
2010 Abiria walisafiri na ndege.

Pamoja na vipengele niliangazia, mtahiniwa azingatie yafuatayo anapojiandaa


kufanya mtihani:
1. Methali, misemo na nahau
2019: Mzee Pumu ni mraibu wa vileo. Baada ya muda watoto
wake wanakuwa watumizi sugu wa vileo. Andika methali inayoweza
kutumiwa kuelezea hali hii.

2022: Rafiki yako ana mazoea ya kutoa visababu ili asifanye kazi
fulani. Andika methali unayoweza kutumia kumwonya dhidi ya
tabia hiyo.

2. Minyambuliko ya vitenzi; kutendata, kutendama na kadhalika.


KCSE 2020
Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha kwa
kuzingatia maneno yaliyopigiwa mstari. alama 2
Alimfanya Tindi anywe pombe ikamfanya alewe.
48
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
3. Matumizi ya ote na o-ote
4. Matumizi ya enye/enyewe
5. Matumizi ya ingine/ingine-o
KCSE 2020
Tunga sentensi ukitumia mzizi –ingineo kumaanisha ‘baadhi ya’

6. Tashbihi
7. Tanakali za sauti
8. Hali ya kuamuru
9. a- unganifu

10. Sentensi za masharti


KCSE 2020
Tunga sentensi inayoonyesha kwamba kitendo kilifanikiwa
kutokana na kufanikiwa kwa kingine.

11. Nomino za jamii/makundi


12. Matamshi bora/maneno ya heshima
KCSE 2020
Hewala ni kwa kukubaliana na jambo,…………ni kwa kutaka kitu
kinusurike, na ………..ni kwa aliyefanya vyema katika jambo.

SEHEMU YA B
MASWALI YA SARUFI NA ISIMUJAMII (NA MAJIBU)
3A
a) Taja sauti mbili zinazotamkiwa kwenye kaakaa laini (alama 1)
b) Eleza tofauti za sentensi zifuatazo (alama 2)
i) Amerudi shuleni!
ii) Amerudi shuleni.
c) Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mstari.
i) Afisa mkuu anafuata sharia sembuse wewe. (alama 1)
ii) Ameenda huko mbali sokoni (alama 1)
d) Tambua aina ya vihusishi katika sentensi zifuatazo
i) Jumba alifuatalo li mbele ya msikiti wa Musa (alama 1)
ii) Kisiwa cha Giningi kimekauka (alama 1)
e) Tambua hali katika sentensi ifuatayo.
Vyungu vya aina hii vyafinyangwa na huyu. (alama 1)
f) Toa maana mbili za neno lifuatalo (alama 2)
Somo
g) Kanusha
Mama alimwambia sipo alime haraka (alama 1)
h) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizowekwa katika mabano
i) Lia (Kutendeshwa) (alama 1)
ii) -Ja (Kutendea) (alama 1)
i) Andika katika hali ya wastani umoja

49
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Kigombe kile kiliumia kikwato ( alama 2)
j) Akifisha sentensi ifuatayo.
Je kuna manusura wowote yeye alitaka kujua. (alama 2)

k)
i) Eleza maana ya kirai (alama 1)
ii) Onyesha aina ya virai katika sentensi ifuatayo.
Nilimpata akilalama ndani ya darasa (alama 2)
l) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi.
Mwelekezi wake alimwambia kuwa angeweza kuwa mwindaji mashuhuri ikiwa angeyafuata
mashauri yake. (alama 2)
m) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale.
Mtoto mmoja aliyekuwa mgonjwa sana alitibiwa jana. (alama 4)
n) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia “o” rejeshi
Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo (alama 1)
o) Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo
Wachimba migodi wanafanya kazi haraka ipasavyo. (alama 2)
p) Tumia kivumishi kimilikishi nafsi ya pili wingi katika sentensi (alama 2)
q) Onyesha viambishi katika fungutenzi hili ( alama 2)
Sajilika
r) Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Ndovu aliuawa na wawindaji haramu nami nikawaripoti
s) Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo ( alama 2)
i) Takrimu
ii) Sakini
t) Weka vitenzi hivi katika hali ya kuamrisha kulingana na maelezo katika mabano (alama 2)
i) -nywa (umoja)
ii) Tubu (wingi)
u) Weka neno lifuatalo katika ngeli mwafaka (alama 1)
Nyasi

ISIMU –JAMII
a) Eleza mitazamo mitatu kuhusu chimbuko la Kiswahili (alama 6)
b) Taja sifa nne za sajili ya utingo (alama 4)

3B
a) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya vielezi viwili vya silabi moja. (alama2)
b) Onyesha sifa bainifu za sauti zifuatazo (alama2)
a. f/v
c) Ainisha mofimu:Awaibiaye (alama2)
d) Eleza huku ukitoa mifano matumizi mawili ya kiambishi ‘ ji’ (alama2)
e) Huku ukionyesha upatanisho wa kisarufi weka nomino zifuatazo katika ngeli mwafaka (alama2)
i. Uwele
ii. vita
f) Tumia ‘o’ rejeshi tamati kuunganisha sentensi zifuatazo
(i)Jino linauma
(ii)Jino limeng’olewa (alama2)
g) Tambua vivumishi na uonyesha ni vya aina gani .
Wanafunzi wawa hawa waliochelewa watafanya kazi ya sulubu kama adhabu. (alama3)
h) Kanusha: Msichana ambaye amefika ametuzwa (alama 1)
i) Onyesha aina za virai katika sentensi hii:
Wale wazazi wetu watawasili kesho saa tatu (alama2)
j) Unda nomino kutokana na kitenzi ‘Haribu’ (alama1)
k) Tambua aina za vitenzi katika sentesi,

50
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Hawa sio wachezaji waliokuwa wakicheza jana (alama3)
l) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya viunganishi vya kulinganua (alama1)
m) Eleza matumizi mawili ya ‘ka’Toa mifano katika senstensi (alama2)
n) Andika visawe vya maneno yafuatayo (alama1)
i)Daawa.....................................................................................................................................................
ii)Ainisha....................................................................................................................................................
o) Jaza nafasi zilizoachwa (alama2)
Liwa liana
Hoji

p) Andika kinyume: Tajiri aliyesifiwa amelaaniwa (alama1)


q) Changanua sentensi hii kwa kutumia vishale
Yule mgeni aliyefika jana ameondoka leo (alama3)
R) Tambua vishazi na uonyeshe ni vya aina gani
Rudisha atapendwa na wengi ikiwa atashinda leo (alama2)
s) Eleza majukumu mawili ya chagizo huku ukjitoa mifano (alama2)
T) Akifisha:
Sikiliza bwana mdogo siku hizi tunaishi katika jamii ambayo imebadillika hayo mawazo yako ya
zama kongwe hayatakufikisha popote alivyorukia. (alama3)
u) Andika ukubwa wa sentensi katika wingi: Nyundo imo dani ya kibweta (alama1)

ISIMUJAMII
Eleza makosa matano yanayoweza kutokea wakati wa mazungumzo . (alama10)

3C
1. Tungia neno lifuatalo sentensi (alama 1)
Wa’lakini
2. Taja sifa tatu za sauti ifuatayo (alama 3)
|th|
3. Onyesha mzizi katika neno machweo (alama 2)
4. Andika katika ukubwa (alama 2)
Mke wa mzee huyu hupenda watoto sana.
5. Fakinisha (alama 2)
Kama Otoyo haji mwalimu hatasahihisha kazi.
6. Tunga sentensi sahili mbili kubainisha matumizi mawili tofauti ya ‘po’ (alama 2)
7. Eleza matumizi mawili ya koloni na utoe mfano kwa kutunga sentensi (alama 2)
8. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi kinai (alama 2)
9. Tunga sentensi kudhihirisha ngeli ya KU- (alama 1)
10. Bainisha yambwa katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Askofu aliandikiwa barua na waumini
11. Bainisha virai katika sentensi (alama 2)
Chake chote kilivunjika vibaya sana.
12. Changanua kwa matawi (alama 4)
Ibada ya wafu iliyofanyika jana usiku ilisababisha kilio kingi.
13. Tunga sentensi moja kutofautisha ‘thibiti’ na ‘dhibiti’ (alama 2)
14. Andika katika usemi wa taarifa (alama 2)
“Aisee! yale mawimbi ya tsunami yaliangamiza biashara nyingi sana” alisema Koinange.
15.
i) Mofimu ni nini? (alama 1)
ii) Taja aina mbili za mofimu na kwa kila aina utoe mfano. (alama 2)
16. Andika katika hali ya mazoea kwa kutumia kirejeshi mwafaka (alama 2)
Mtoto ambaye hula lishe bora ndiye hukua nyema.
17. Andika kinyume (alama 2)
51
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Wanaskauti wengi walivunja kambi jana asubuhi.
18. Tungia kitenzi kishirikishi kipungufu sentensi. (alama 1)
19. Tumia mzizi-enye katika sentensi kama kiwakilishi (alama 2)
20. Bainisha matumizi ya “ndi” katika sentensi ifuatayo.
Tumbo lake ndilo linaloguruma (alama 1)

ISIMU JAMII
Eleza sababu za vijana kutumia lugha ya sheng’ (alama 10)

3D
(a) Sauti /ch/ ina sifa zipi? (alama 2)
(b) Akifisha kifungu kifuatacho: baba kwa mshangao salale umechoma shati langu yaya akitetemeka
samahani si kosa langu (alama 3)
(c) Tambua miundo yoyote minne ya nomino za ngeli ya A-WA. Toa mifano. (alama 2)
(d) Nyambaka alimwambia Ochiel kuwa angemlipa pesa zake siku hiyo jioni. Andika katika usemi
halisi. (alama 2)
(e) Vitaje na uvinyambue vitenzi vyovyote viwili vyenye asili ya kigeni katika kauli ya kutendeana.
(alama 2)
(f) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: Tulipikiwa pilau kwa chungu. (alama 3)
(g) Tunga sentensi moja iliyo na chagizo ya namna halisi na ya namna hali. (alama 2)
(h) Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo: Ingawa hajalipwa mshahara, angali anaikimu familia
yake. (alama 3)
(i) Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa wingi: Hiki kijiti kilitolewa kwenye mti ule
mrefu. (alama 3)
(j) Tumia neno haraka kama nomino na kielezi katika sentensi moja. (alama 2)
(k) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia visanduku: Rosamaria alipata kitabu chake kipya
kilichopotea jana. (alama 4)
(j) Tambua na uainishe viwakilishi katika sentensi ifuatayo: Aliniitisha zawadi uliyokuwa
umenituma nimpelekee Hadija. (alama 2)
(k) (i) Kishazi ni nini? (Alama 1)
(ii) Tunga sentensi iliyo na kishazi huru na kishazi tegemezi. (alama 2)
(m) Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiambishi ‘ku’. (alama 2)
(n) Tambua hali na wakati gani katika sentensi ifuatayo: Zawadi atakuwa anasoma nitakapofika.
(alama 2)
(o) Tofautisha silabi funge na silabi wazi. Toa mfano mmoja mmoja kwa kila mojawapo. (alama 3)

ISIMUJAMII (alama 10)


(a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo:
i. Linguafranka
ii. Sajili
iii. Lahaja
iv. Uwili lugha.
v. Lugha sanifu
(b) Eleza majukumu yoyote sita ya Kiswahili nchini Kenya. (alama 6)

3E
a) Taja ala zinazotumika kutamkia sauti /ch/ (alama 1)
b) Tunga sentensi moja ukitumia nomino na kielezi kutokana na neno: enda (alama 2)
c) Tunga sentensi ukitumia nomino katika ngeli ya ‘u-ya’ ili kuonyesha upatanisho wa kisarufi
(alama 2)

52
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
d) Huku ukitoa mfano eleza maana ya sentensi sahili (alama 2)
e) Onyesha matumizi ya kiambishi ‘ji’ katika sentensi ifuatayo:
Mkiambiaji alijibidiisha katika riadha (alama 2)
f) Tumia vitenzi vifuatavyo kutunga sentensi katika kauli ya kutendeka
(i) Cha (alama 1)
(ii) Pa (alama 1)
g) ( i)Eleza maana ya kundi nomino (KN) (alama 1)
(ii) Tunga sentensi yenye muundo ufuatao KN(N) + KT(T + T + E) (alama 1)
h) Kwa kutolea mfano, eleza maana ya mofimu huru (alama 2)
i) Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha uteuzi (alama 2)
j) i) Kirai ni nini? (alama 1)
ii) Onyesha aina ya virai katika sentensi ifuatayo.
Nilimpata akilala ndani ya darasa (alama 1)
k) Kwa kutoa mfano mmoja wa sentensi eleza maana ya shamirisho kitondo (alama 2)
l) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi: (alama 4)
Yeye si mbaya sana kazini
m) Tunga sentensi moja ukitumia vitate hivi: (alama 3)
(i) Kipofu
(ii) Kibovu
(iii) Kibofu
n) Eleza mofimu zilizomo katika neno hili (alama 3)
Lililolila
o) Tunga sentensi moja ukitumia kihisishi cha masikitiko (alama 2)
p) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya alama ya kibainishi (alama 2)
q) Andika katika usemi wa taarifa
“Utaweza kuwa mwindaji mashuhuri ikiwa utayafuata mashauri yangu,” alisema Mbunda.
(alama 2)
r) Tunga sentensi ukitumia kinyume cha kitenzi hiki: Ezeka (alama 2)
s) Yakinisha sentensi ifuatayo:
Tusingalienda hospitali, tusingalitibiwa. (alama 1)

ISIMU JAMII
a) Fafanua istilahi zifuatazo za isimu jamii (alama 2)
(i) Isimu
(ii) Jamii
b) “.......ah.....naomba kumwongelesha Chucho.....Naam, naam
Chucho.......Hujambo? .....si.....sina neno......naam. Mjomba amezidiwa si wa maji si wa
chakula....kweli?......Muuguzi mkuu amedhihirisha..... Yes......ok......yeah.....Ala! Ameishiwa na
pesa.
(i) Tambua sajili husika katika dondoo hili. (alama 1)
(ii) Kwa hoja zozote saba, eleza sifa za sajili hii. (alama 7)

3F
(a) Eleza matumizi mawili ya –KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo. (alama4)
(b) Eleza maana ya vikwamizo. (alama 2)
(c) Andika vikwamizo vya ufizi. (alama 1)
(d) Andika sentensi ifuatayo upya.
Mwalimu huyo anafunza kifaransa. (Anza kwa kiashiria kisisitizi). (alama 2)
(e) Kwa kutungia sentesi eleza tofauti kati ya: adabu na adhabu. (alama 2)
(f) Kwa kutunga sentensi mbili tofauti, onyesha matumizi ya vihusishi kama nomino. (alama 2)
(g) Eleza matumizi ya hali iliyopigiwa mstari.
Abdi yuko wapi? “Acheza uwanjani.” (alama 1)
(h) Unda kivumishi kutokana na kitenzi. (alama 1)
Teta:

53
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
(i) Tunga sentensi iliyo na mpangilio ufuatao wa maneno: (alama 3)
W+V+U+N+T+E
(j) Huku ukitolea mfano, tofautisha kati ya sentensi ambatano na sentensi changamano. (alama 4)
(k) Eleza matumizi manne ya herufi ya mlazo (italiki). (alama2)
(l) Ainisha shamirisho katika sentensi hii:
Mchezaji alimpigia mwenzake mpira kwa mguu wa kushoto. (alama 2)
(m) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendwa.
Mama mzazi alimpokea mtoto wake leo alfajiri. (alama 2)
(n) Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo: Alimfungia dada yake. (alama 2)
(o) Unganisha sentensi hizi ukitumia O-rejeshi. (alama 2)
Buzi hili linakamuliwa. Buzi hili linatoa maziwa mingi.
(p) Andika katika ukubwa.
Nyoka yule amemmeza kondoo mzima. (alama 2)
(q) Andika kwa msemo wa taarifa. (alama 2)
“Lo! Kumekucha mara moja hii?” aliuliza mgeni.
(r) Fuata maagizo. (alama 2)
Kesho kuna sherehe za krismasi. (tumia sherehe kama kitenzi).
(s) Yakinisha katika umoja. (alama 2)
Tusingemwita mapema, tungelimwacha porini.
ISIMU JAMII
(a) Eleza tofauti uliopo kati ya Lugha ya taifa na Lugha rasmi. (alama 2)
(b) Fafanua sifa tatu kuu za lugha ya taifa. (alama 3)
(c) Eleza juhudi zilizochukuliwa na serikali baada ya uhuru kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili.
(alama 5)

MAJIBU

3A
a) /k/ /g/ng’/ gh/ (alama 1)
b)
i) Amri
ii) Maelezo (alama 2)
c) Kiunganishi
Kielezi cha mahali (alama 2)
d) i) Mbele ya –kihusishi cha ujirani (alama1)
Cha-kihusishi changamani / a-unganifu (alama 1)
ii) -kihusishi cha a-unganifu
e) Vyafinyangwa-hali ya ‘a’ (alama 1)
f) Somo-JIna waitanalo watu walio na jina moja (alama 1)
Funzo (alama 1)
g) Mama hakumwambia sipo alime haraka (alama 1)
h)
i) Lizwa (alama1)
ii) Jia (alama 1)
i) Ng’ombe yule aliumia kwato (alama 2)

j) Je1/2 ! 1/2 Kuna manusura wowote? 1/2 Yeye1/2 alitaka kujua. (alama 2)
k)
i) Kirai-Neno au fungu la maneno lisilodhihirisha maana kamilifu (alama 1)
ii) Ndani ya darasa-kirai kihusishi
Nilimpata akilalama-kirai kitenzi (alama 2)
l) “Utaweza kuwa mwindaji mashauri ikiwa utayafuata mashauri yangu,”Alisema mwelekezi wake.
Kila kitahiniwa ni nusu alama.akiweka alama za usemi halisi apewe ½ alama (alama 2)

54
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
m)
S KN+KT
KN N+V+S
N Mtoto
V mmoja
S aliyekuwa mgonjwa sana
KT T+E
T alitibiwa
E jana (alama 4)
n) Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi hajapata karo hadi leo. (alama 1)
o) Migodi-Shamirisho kipozi (alama 1)
Haraka ipasavyo- chagizo (alama 1)
p) –ako -enu 
Mfano watoto wenu wana nidhamu (alama 1)
q) Sajili- mzizi (alama 1)
k- kauli
a-kiishio (alama 1)
r) Na- kuenyesha mtendaji (alama 1)
Na- ufupisho wa nafsi (alama 1)
s) Ukarimu (alama 1)
Maskani (alama 1)
t) Kunywa! (alama1)
Tubuni (alama1)
u) U-ZI (alama 1)

Jinsi ya kusahihisha matumizi ya lugha.


 ondoa nusu( ½ ) kwa kila kosa la sarufi(s) litokeapo kwa mara ya kwanza kwa kila kijisehemu
lakini isipite nusu alama (½) alizopata katika kijisehemu hicho.
 ondoa nusu alama (½) kwa kila kosa la tahajia (h) litokeapo mara ya kwanza hadi makosa sita
katika swali lote yaani (½ x 6=3)

Isimujamii
a)
- kiswahili ni tokeo la mwingiliano baina ya waafrika na waarabu.(alama 2)
- Kiswahili ni lugha ya kibantu(alama 2)
- Kiswahili ni lugha ya mseto wa lugha mbalimbali k.v kuhindi, kiarabu,kiajemi n.k mf. Maneno ya
kihindi k.v chapatti, laki.maneno ya kiajemi k.v maridadi na desturi. Maneno ya kiarabu k.v shukrani
na binti. (alama 2)
 Lazima mtahiniwa atoe ufafanuzi wa kila hoja.
 Kutaja ni alama 1, ufafanuzi alama1.
b)
- Lugha isiyo rasmi
- kuchanganya ndimi
- Ucheshi
- Ushawishi
- Wakati mwingini lugha huwa na matusi/lugha chafu
- Huambatanisha ushawishi na nyimbo. ( alama 4 =1x4)
Jinsi ya kusahihisha isumu jamii.
 ondoa nusu (½) alama kwa kila kosa la sarufi (s) litokeapo kwa kila kijisehemu lakini isipite
nusu ya alama alizopata (si alizotengewa) katika kijisehemu hicho.
 Ondoa nusu (½) alama kwa kila kosa la hijai (h) litokeapo kwa mara ya kwanza hadi makosa
matatu yaani (3x ½ =11/2)

55
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
3B
a) - Po ya wakati – Alipowasili – kielezi cha wakati.
- Po ya mahali – Alipohamia – kielezi cha mahali.
- Vyo ya jinsi –Alivyocheza – kielezi cha namna.
Sentensi zozote 2x1 =2
b) f – Ni konsonanti si ghuna. 1
v – Ni konsonanti ghuna. 1
c) A- wa – ib- i –a- ye.
A- mofimu tegemezi nafsi.
wa- mofimu tegemezi kitendwa.
ib – mofimu tegemezi - mzizi kitenzi.
-i – mofimu tegemezi kauli ya kutendea.
-a – mofimu tegemezi kauli
ye – mofimu tegemezi ‘O’ rejeshi tamati.
Zozote 4x ½ =2
d) (i) Ngeli ya U-ZI – Uwele umemzidia. ½
Ndwele zimewazidia ½
Ngeli ya VI-VI –Vita vimezidi. 1
e) Jino liumalo hung’olewa/meno yaumwayo hung’olewa. Alama 2
g) Wawa hawa – kivumishi kisisitizi 1
Ya - kivumishi a- unganifu 1
‘O’ – kivumishi kirejeshi 1
h) Msichana ambaye hajafika hajatuzwa.
Wale wazazi wetu – Kirai nomino 1
Kesho saa tatu – Kirai kielezi 1
j) - Harabu.
- Uharibifu.
- Kuharibu. yoyote moja 1x1 =1
k) Sio – kitenzi kishiriki kipungufu.
Walikuwa – kitenzi kisaidizi.
Wakicheza – kitenzi kikuu.
l) Lakini/ila/ijapokuwa/ingawa/bali/ilhali/sembuze/seuze. Yoyote 1x1 =1
m) Kuonyesha mfululizo wa vitendo.
Kuonyesha wakati ujao.
Hali ya kufanyika kwa kitendo – Alipigika.
Kutoa rai/amri – ‘Kacheza nje’ Zozote 2x ½ mfano 2x ½ = 2
n) - Daawa – Fitina/chokochoko/madai.
- Ainisha – Onyesha/gawa/changanua/panga/taja/chambua.
o) La, hojiwa, hojiana

p) Tajiri aliyekashifiwa jana amebarikiwa. zozote 2x1 =2


q) S – KN + KT
KN V+N+S
V Yule
N Mgeni
S aliyefika jana
KT T+E
T ameondoka
E leo. zozote 6x ½ = 3
r) Kishazi huru –Rudisha atapendwa na wengi.
Kishazi tegemezi – ikiwa atashinda leo.
s)
 Huelezwa jinsi kitendo kinavyofanywa – mfano ;Amecheza vibaya.
 Hueleza wakati – Aliondoka jana jioni.
 Hueleza mara ngapi – Alimpa mara tatu.
 Hueleza mahali – Michezo itafanyika uwanjani.
 Hueleza vivumishi vya sifa na idadi.Mfano;
56
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Pombe haramu imewauwa watu wengi sana.
Amenunua vitabu vizuri sana.
 Hueleza chagizo nyingine – mfano;Atafunza kesho alfajiri na mapema.
t) “Sikiliza bwana mdogo, siku hizi tunaishi katika jamii ambayo imebadilika.Hayo mawazo yako ya
zama kongwe hayatakufikisha popote,’’ alifyoa Kamene.
u) Majundo yamo ndani ya majibwete. 1

ISIMUJAMII
 Matamshi – mfano: Ulefu badala ya urefu.
 Kudondosha sauti.
 Kuhamisha mfumo wa lugha moja hadi nyingine – Mfano; Katoto badala ya kitoto.
 Kutodhibiti mfumo wa ngeli katika lugha. Mfano; ‘Ng’ombe hii’ badala ya ‘Ng’ombe huyu’
 Kujumulisha kanuni za lugha.Mfano :Mnyambuliko wa vitenzi - Soma – Somesha
-Penda – Pendesha (kosa)
 Kosa la kutoelewa maana ya neno kimatumizi au umilisi wa maneno.Kudhani neno ‘tetesi’
linalotokana na neno ‘teta’ ilhali maana yake ni uvumi. Zozote 5x2 = 10

3C
1. Kutungia neno wa’lakini sentensi.
Wa’lakini ni nomino yenye maana ya dosari/kasoro/ila
Mfano Gari langu lina walakini (1×1=1)
2. Sifa tatu za /th/
(i) Ni konsonanti
(ii) Ni sauti sighuna /hafifu
(i) Hutamkiwa kwenye meno. (3×1=3)
3. Mzizi wa neno ‘machweo’
_chw_ (2×1=2)
4. Ukubwa:
Jike la zee hili hupenda matoto sana
5. Kuyakinisha :
Otoyo akija mwalimu atasahihisha kazi. (1×2=2)
6. Matumizi mawili ya ‘po’
(i) ‘po’ mahali
Mfano : Anapolala pana uchafu.
(ii) po wakati
Mfano: Alalapo hukoroma.
7. Matumizi mawili ya koloni kwa kutoa mfano wa sentensi
(i) kutanguliza orodha ya maneno
Mfano: Kuna njia mbili tu za kufaulu maishani:bidii na nidhamu.
(ii) kutanguliza maelezo fulani
Mfano:
Mama alianza: “mimi sitaki Kuwa ninarudia jambo moja moja Kila siku na hakuna yule anayotaka
Kunisikiliza” (2×1=2)
8. Kuunda nomino mbili kutokana na kitenzi kinai
(i) ukinaifu
(ii) mkinaifu (wakinaifu) (2×1=2)
9. Kutunga sentensi kudhihirisha ngeli ya ku -
Mfano : Umoja - kucheza huko hakufai
Wingi - kucheza huko hakufai (1×1=1)
10. Kubainisha yambwa.
Askofu - yambwa tendewa
Barua - yambwa tendwa (2×1=2)
11. Kubainisha virai:
Chake chote kilivunjika vibaya sana
Kirai nomino kirai kielezi (2×1=2)
13. kutunga sentensi moja kutofautisha thibiti na dhabiti.
57
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Thibiti kuwa ya ukweli
Dhibiti tunza,weka chini ya mamlaka
Mfano :Askari alithibitisha kuwa gari hilo lilikuwa na kidhibiti mwendo. (2×1=2)
14. kuandika katika usemi wa taarifa .
Koinange alishangaa kwa jinsi ambavyo mawimbi ya tsunami yaliangamiza biashara nyingi sana.
(2×1=2)
15. (i) mofimu ni kipashio kidogo zaidi katika lugha
(ii) Aina
Mofimu huru:Mofimu ambazo huweza kujisimamia na kuwa na maana kamili bila kutegemea mofimu
nyingine mifano kuku,mama (1×1=1)
Mofimu tegemezi:ni viungo vya maneno yenye maana fulani lakini haviwezi kujitegemea vikiwa
peke yake. (1×1=1)
16. Hali ya mazoea kwa kutumia kirejeshi mwafaka.
Mtoto alaye lishe bora ndiye akuaye vyema. (1×2 =2)
Tanbihi :mwanafunzi atumie ‘o’ rejeshi tamati hili kuzua dhana ya mazoea.
17. Kinyume:
Wanaskauti wengi walipiga kambi jana asubuhi. (1×2=2)
18. Kutunga kitenzi kishirikishi kipungufu (t) sentensi
Vitenzi ‘vishirikishi vipungufu haviwezi kuambishwa viambishi vyovyote
Mifano :ni,ki,li,yu,zi n.k
Mfano
(i) mimi ni mzee
t
(ii) Daudi yu ukumbini
T (1×1=1)
19. Kutungia mzizi-enye sentensi kama kiwakilishi.
Mfano:
Mwenye macho haambiwi tazama
W (1×2=2)
20. Matumizi ya _ndi_
kurejelea nomino (1×1=1)
Adhabu.
(i) mtahiniwa akifanya makosa ya sarufi aondolewe ½ maki hadi makosa 6 baada ya kutuzwa.
6×1/2=3
(ii) mtahiniwa akifanya makosa ya tahajia aondolewa1/2 maki hadi makosa 6 baada ya kutuzwa
6×1/2=alama 3

ISIMU JAMII
1. Ukosefu wa ufasaha wa lugha/elimu
2. kufahamu lugha zaidi ya moja
3. kuficha siri
4. kujitambulisha na kundi fulani hasa vijana
5. Kurithishwa na wazazi (vijana)
6. Haina (sheng)masharti (lugha legevu)
7. Uwezo mkubwa wa kukabilianana mazingira (ubunifu wa hali ya juu)
(zozote 5×2=alama 10)
3D
(a) Sauti /ch/ ina sifa zipi? (alama 2)
Ni sauti/konsonanti hafifu.
Ni kipasuo kwamizo.
Hutamkiwa kwenye ulimi na kaakaa gumu. Zozote 2×1=2
(b) Akifisha kifungu kifuatacho: baba kwa mshangao salale umechoma shati langu yaya akitetemeka
samahani si kosa langu (alama 3)
 Baba: (Kwa mshangao) Salale! Umechoma shati langu?
 Yaya: (Akitetemeka) Samahani. Si kosa langu. Vitahiniwa 6×½=3
(c) Tambua miundo yoyote minne ya nomino za ngeli ya A-WA. Toa mifano. (alama 2)
Ki-Vi Kwa mfano: Kipepeo – Vipepepo.
58
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
M-Mi Kwa mfano: Mtume – Mitume.
M/Mw- Wa Kwa mfano: Mtu – Watu.
Ch –Vy Kwa mfano:Chura – Vyura.
Zinazochukua kiambishi ma- katika wingi: Daktari – Madaktari.
Zisizobadilika katika umoja na wingi: Punda – Punda. Miundo 4×½=2
(d) Nyambaka alimwambia Ochiel kuwa angemlipa pesa zake siku hiyo jioni. Andika katika usemi halisi.
(alama 2)
 “Nitakulipa pesa zakoleo jioni,” Nyambaka alimwambia Ochiel. Vitahiniwa 4×½=2

(e) Vitaje na uvinyambue vitenzi vyovyote viwili vyenye asili ya kigeni katika kauli ya kutendeana.
(alama 2)
Vitenzi vyenye asili ya kigeni ni vile vinavyoishia kwa irabu –i, -e au –u.
Kwa mfano: Hubiri – hubiriana, Amini – aminiana, Saliti – salitiana, Samehe – sameheana, abudu
– abudiana.
Kutaja kitenzi 2×½=1, Kunyambua vitenzi 2×½=1
(f) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: Tulipikiwa pilau kwa chungu. (alama 3)
 Tu (sisi) ni shamirisho kitondo/yambwa tendewa.
 Pilau ni shamirisho kipozi/yambwa tendwa.
 Chungu ni shamirisho ala/yambwa kitumizi. Vitahiniwa 3×1=3
(g) Tunga sentensi moja iliyo na chagizo ya namna halisi na ya namna hali. (alama 2)
 Mwanafunzi aliyecheka sana/mno/kupindukia aliadhibwa vikali/vibaya. Vitahiniwa 2×1=2

(h) Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo: Ingawa hajalipwa mshahara, angali anaikimu familia
yake. (alama 3)
 Hajalipwa ni kitenzi halisi.
 Angali ni kitenzi kisaidizi.
 Anaikimu ni kitenzi kikuu.
 Angali anaikimu ni vitenzi sambamba. Vitenzi vyovyote 3×1=3
(i) Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa wingi: Hiki kijiti kilitolewa kwenye mti ule
mrefu. (alama 3)
 Haya majiti/majijitiyalitolewa kwenye majitiyalemarefu. Vitahiniwa 6×½=3
(j) Tumia neno haraka kama nomino na kielezi katika sentensi moja. (alama 2)
 Haraka yake ilimfanya atembee haraka kwenda kazini.
N E Vitahiniwa 2×1=2
(k) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia visanduku: Rosamaria alipata kitabu chake kipya
kilichopotea jana. (alama 4)
S
KN KT
N T KN S
N V V
Rosamaria Alipata Kitabu chake kipya kilichopotea jana.
Vitahiniwa 8×½=4
(j) Tambua na uainishe viwakilishi katika sentensi ifuatayo: Aliniitisha zawadi uliyokuwa umenituma
nimpelekee Hadija. (alama 2)
 A – kiwakililishi cha nafsi ya tatu umoja, U – kiwakilishi cha nafsi ya pili umoja, U – kiwakilishi
cha nafsi ya pili umoja, Ni – kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja.
Vitahiniwa 4×½=2
(k) (i) Kishazi ni nini? (Alama 1)
Ni kipashio cha kimuundo chenye kiima na kiarifu. Maana 1×1=1
(ii) Tunga sentensi iliyo na kishazi huru na kishazi tegemezi. (alama 2)
 Mwalimu aliyeajiriwa mwaka jana alitoweka bila na fedha zetu. (Tathmini majibu ya wanafunzi)
Vishazi 2×1=2
(m) Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiambishi ‘ku’. (alama 2)
 Kucheka kwake kulituudhi sana. Matumizi yoyote 2×1=2
59
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
(n) Sentensi ifuatayo iko katika hali na wakati gani?: Zawadi atakuwa anasoma nitakapofika.
 Wakati ujao hali ya kuendelea. Kutaja wakati = 1, Kutaja hali = 1
(o) Tofautisha silabi funge na silabi wazi. Toa mfano mmoja mmoja kwa kila mojawapo.
 Silabi funge ni silabi inayoishia kwa konsonati. Kwa mfano: Dak-ta-ri. Silabi wazi ni silabi
inayoishia kwa irabu. Kwa mfano: Ba-ba.
Kutofautisha silabi 2×1=2, Kutoa mifano 2×½=1
ISIMUJAMII
(a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo:
(i) Linguafranka (alama 1)
 Ni lugha inayotumiwa baina ya watu ambao wanazungumza lugha tofauti kabisa za kwanza.
(ii) Sajili (alama 1)
 Ni mtindo wa lugha ambao hutumika katika muktadha mahsusi.
(iii) Lahaja (alama 1)
Ni namna tofauti tofauti ya kuzungumza lugha moja kutegemea eneo au tabaka fulani.
(iv) Uwili lugha (alama 1)
Ni hali ambapo mzungumzaji mmoja anaweza kutumia lugha mbili.
(v) Lugha sanifu (alama 1)
Ni lugha au lahaja iliyochaguliwa na kufanyiwa marekebisho ya kimatamshi, kisarufi, kimaana na
kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi.

(b) Eleza majukumu yoyote sita ya Kiswahili nchini Kenya. (alama 5)


 Ni chombo cha mawasiliano, maingiliano na maelewano baina ya Wakenya.
 Ni nyenzo ya kuwaunganisha Wakenya wote wenye asili mbalimbali na kuwafanya kuwa kitu
kimoja.
 Ni chombo cha kushirikisha umma katika shughuli zote za taifa.
 Ni kitambulisho cha Wakenya wote.
 Hutumiwa na serikali ya Kenya kupitisha sera zake kwa wananchi.

3E
(a) Kaakaa gumu
Ulimi (2 x ½) = 01
(b) Mwendo wake uliwafanya wengi kwenda mbio
(N) (E) (1 x 2)
(c) Ugonjwa umemwathiri sana
Magonjwa yamewaathiri sana
(Mwanafunzi atunge sentensi sahihi) (2 x 1)
(d) Sentensi sahili ni sentensi yenye wazo/dhana moja k.m.
Mwalimu anafundisha (1 x 2)
(e) Mkimbiaji – uzoefu wa kutenda jambo
Alijibidiisha – kirejeshi cha mtenda (2 x 1)
(f) (i) cha-Mola huchika kwa sababu ya utukufu wake
(Atumie chika au cheka)
(ii) pa-Ngwenje si kitu kinachopeka vivi hivi
(Atumie peka ) (2 x 1)
(g) (i) Kundi nomino ni sehemu yenye nomino au kundi la maneno yanayorejelea nomino
(1 x 1)
(ii) Mwalimu amekuwa akifunza darasani (1 x 1)
(Atunge sentensi sahihi)
(h) Ni kipashio kinachobeba maana bila kuambatanishwa na viambishi vyovyote k.m. mama, hodari,
mimi, jioni, Maureen n.k. (2 x 1)
(i) (i) ama
(ii) au
(Mwanafunzi atunge sentensi)
(j) (i) Kirai ni neno au fungu la maneno lisilodhihirisha uhusiano wa kiima na kiarifu k.m.
(ii) - Nilimpata akilala – kirai kitenzi
60
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
- Ndani ya – kirai kihusishi
- Ndani ya darasa – kirai kielezi (zozote 2 x ½ = 01)
(iii) Shamirisho kitondo ni nomino inayotendewa kitendo au inayonufaika kutokana na utendaji wa
kitendo.(yambwa tendewa)
k.m. Baba alimpikia mama ugali
mama ni shamirisho kitondo (2 x 1)

(iv) S

KN KT

W t
v E E

Yeye si mbaya sana kazini

(v) Kipofu mwenye kibofu kibovu ametibiwa


(vi) Li – kiwakilishi cha ngeli
Li – kiwakilishi cha wakati
Lo – kiwakilishi kirejeshi
Li – Yambwa tendwa/shamirisho kipozi/mtendewa
L – mzizi
a – kauli ya kutenda/kiishio (6 x ½ = 03)
(vii) Mfano: Maskini! Ole wangu! Toba! Mtume
(viii) (i) Kibainishi hutumika katika maneno yenye ung’ng’o k.m. ng’ombe
(ii) Katika ushairi au kukata silabi k.m. ‘sikate tamaa
(iii) Katika tarakimu zilizoachwa k.m. ’99 (atumie mfano mmoja)
(ix) Mbundo alisema kuwa angeweza kuwa mwindaji mashuhuri ikiwa (kama) angeyafuata mashauri yake.
(x) Ezeka – ezua
k.m. Juma aliezua paa
(xi) Tungalienda hospitali, tungalitibiwa.

ISIMU JAMII
(a) Fafanua istIlahi zifuatazo za isimujamii (alama 2)
(i) Isimu jamii – Ni taaluma inayochunguza lugha kisayansi/Huchunguza uhusiano uliopo baina aya lugha
na jamii yake.
Jamii kundi la watu wenye uhusiano na maingiliano mbalimbali/kundi la watu wenye uhusiano wa
aina Fulani, kijiografia, kimila, kitamaduni, na kilugha
(b) “........ah......naomba kumwangelesha Chucho......Naam, naam Chucho
Hujambo?...si ....sina neno.....naam. Mjomba amezidiwa si wa maji si wa chakula.....
kweli?.......Muuguzi mkuu amedhihirisha.....Yes...ok....yeah.....Ala! Ameishiwa na pesa.
(i) Tambua sajili husika katika dondoo hili (alama 1)
Simu
(ii) Kwa hoja zozote saba, eleza sifa za sajili hii. (1 x 1 = 01)
 Hutumai sentensi fupifupi ili kuokoa wakati mf. Naam
 Huendeleza majibizano mf. Majibizano kati ya Chucho na anayepiwa simu.
 Hutumia mbinu ya takriri mf. Chucho, naam
 Huhusisha kuchanganya ndimi mf. Kiingereza yes, yeah
 Aghalabu kanuni za lugha hukiukwa mf. Kumwongelesha
 Hulenga moja kwa moja kiini cha habari k.m. Baada ya maamkuzi, anamweleza kuhusu siha ya
mjomba moja kwa moja.
 Kukatana kalima
 Matumizi ya maamkuzi

61
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
3F
1. (a) (i) Kuonyesha udogo wa mtu, kitu au mnyama.
(ii) Kuonyesha aina ya kivumishi / kielezi. Anatembea kivivu.
(iii) Kuonyesha wakati; Alikuwa akitembea, nilipokuwa nikija.
(iv) Kuonyesha masharti; Ukiona vyaelea vimeundwa. (zozote 4x1 = alama
4)
(b) Vikwamizo:
Maana: Hewa hukwamizwa / hubanwa huku neha ya ulimi ikigusa utizi.
(c) Vya ufizi / z / na / s / (1 x 2 = alama 2)
(d) Yuyo huyo mwalimu anafunza kifaransa. (alama 2)
(e) Adabu – tabia njema, nidhamu, heshima, staha.
Adhabu – mateso anayopewa mtu aliyevunja kanuni au sheria; ikabu, rada. (1x2 = alama 2)
Sentensi itoe maana.
(f) Cha mlevi huliwa na mgama. (cha, wa, kwa)
Mwalimu akaadirie vihusishi. (alama 2)
(g) Wakati uliopo usiodhihirika. (alama 2)
(h) Teta (kitenzi) – mtesi / mtetezi (kivumishi) (alama 2)
(i) Sentensi ambatano huundwa na sentensi sahihi mbili na kiunganishi; lakini sentensi changamano
huwa na
kirejeshi. (mifano itolewe) (alama 2x2 = alama 4)
(j)
(k) Herufi za mlazo / italiki:
- Hutumiwa kutoa msisitizo au kutilia mkazo.
- Hutumiwa kuonyesha neno geni.
- Utungoni – lisilo la lugha ya Kiswahili.
(l) Mwenzake – kitondo, mpira – kipozi, mguu wa kushoto. (1 x 2 =
alama 2)
(m) Mtoto alipokewa na mama mzazi leo alfajiri.
(alama 2)
(n) (i) Alifunga badala ya dada yake.
(ii) Alifungia dada yake ndani.
(alama 2)
(o) Buzi linalokamuliwa linatoa maziwa mengi.
(alama 2)
(p) Joka lile limelimeza kodoo zima. (alama 2)
(q) Mgeni alishangaa na kuuliza kulivyokuwa kumekucha mara moja hiyo.
(alama 2)
(r) Kesho tutasherehekea krismasi.
(alama 2)
(s) Ningemwita mapema ningemwacha porini.
(alama 2)
Makosa ya sarufi yaadhibiw hadi 6.
Makosa ya hijai yaadhibiwe hadi 6.
Mwanafunzi asiadhibiwe ikizidi nusu ya alama alizopata katika swali husika.

ISIMU JAMII
(b) Lugha ya Taifa ni lugha inayotumika kuunganisha makabila mbalimbali katika taifa fulani. Lugha
iliyoteuliwa kama kitambulisho cha utamaduni na ustarabu wa taifa zima.
Lugha rasmi ni lugha iliyopewa jukumu la kutumika kikazi, katika shughuli rasmi za nchi.
(c)
 Lugha inayovuka msingi ya kikabila.
 Iwe na muundo wa kuisimu unafanana na lugha zingine katika taifa letu.
 Yafaa kuzua lugha ya kienyeji katika taifa lile.
 Lugha inayozungumziwa na kundi fulani la watu katika taifa lile. (alama 3x1 = alama 3)
(c)

62
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
 Kuundwa kwa tume za Elimu nchini Kenya kama vile Ominde.
 Uandishi wa vitabu na tafsiri ya vitabu vya kiingereza nchini Kenya.
 Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika taasisi ya Elimu.
 Maandalizi ya mitaala au mafunzo katika tashughuli za kidini.
 Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika taasisi za umma / serikali. (zozote 5x1 = alama 5)

SEHEMU YA C: MASWALI YA ISIMUJAMII, KCSE


2006-2022
MWAKA SWALI MADA
2023 ? ?

2022 “Wateja wetu wameagiza bidhaa tena. Katoni Sajili


mia mbili ziwe tayari kufikia leo jioni. Kazi ianze
mara moja!”
a) Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa
mfano kwenye makala. Alama 2
b) Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo
zingejitokeza katika makala haya. Alama 8

2021 a. Soma makala yafuatayo kisha ujibu Sajili


maswali.
“Karibu, karibu! Keti.
Naam, jitambulishe kwa jopo hili…
Bwana Nuru, ni jambo lipi ambalo
linakufanya kuamini kwamba nafasi hii
inakuafiki wewe?”
i. Bainisha sajili ya makala haya.
Alama 1
ii. Eleza sifa nne za sajili hii kwa
kurejelea makala haya. Alama 4
b. Wewe ni kinara wa chama cha
Wanamawasiliano Bora shuleni mwako.
Umepewa jukumu la kuwatangazia
wenzako mashindano ya uogeleaji
yakiendelea shuleni mwako. Fafanua sifa
tano za lugha utakayotumia. Alama 5

2020 Umewahutubia wanaeneobunge lako kuwaomba Sajili


wakuchague kuwa mbunge wao. Umegundua
kwamba hujafanikiwa kuwavutia upande wako.
Fafanua sifa kumi za lugha ungetumia
kuwavutia. Alama 10

2019 Wewe ni muhubiri katika Maabadi ya Shamu. Sajili


63
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
Umealikwa kuwahubiria wanafunzi wa shule ya
Upili ya Lulu. Fafanua sifa kumi za lugha
utakayotumia. Alama 10

2018 Ndugu wapenzi, waumini wenzangu, mbazi hii Sajili


haionyeshi huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu
wakosefu tu bali pia inatufunza umuhimu wa
unyenyekevu na msamaha.
a. Bainisha sifa tatu za sajili ya kidini
zinazojitokeza katika makala haya. al. 3
b. Fafanua vipengele vingine saba vya
kimtindo ambavyo mhubiri huyu
angetumia kufanikisha mazungumzo
yake. al. 7

2017 “Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, mahakama Sajili


hii imethibitisha bila chembe ya shaka kwamba
wewe mshtakiwa, Bi. Mlachake Chauchau ndiye
uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha
vifo vya raia hamsini na kupofuka kwa wengine
mia moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji.”
a. Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa
mifano miwili kutoka kwenye makala. al 2
b. Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii
ambazo zingejitokeza katika makala haya.
al 8

2016 Kwa kutolea mifano maridhawa, eleza kaida Kaida za lugha


zozote tano ambazo matumizi ya lugha
hutegemea katika jamii.

2015 Mtu I: wewe njoo hapa! (kwa sauti kubwa). Sajili


Fanya upesi!
Mtu II: (Anakimbia mbio) Naja sir.
Mtu I: (Anamtazama) Unajifanya mwerevu?
Mtu II: Hapana sir…eh…afande.
Mtu I: Jina?
Mtu II: Samwel Kibao.
Mtu I: (Huku anaandika) Lete kitambulisho.
Mtu II: Sina hapa sir.
Mtu I: Huna kitambulisho? Utafanyiwa booking
vipi?
Mtu II: Naomba…
Mtu I: Naomba! Nomba! Unaomba nini?
Wazururaji kama nyinyi tunawajua. Mnajidai
hamjui kuna curfew. Mnajiponza wenyewe na

64
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
kuwahasiri wenzenu. Kisha, “serikali saidia”.
Usiniharibie muda wangu.(akiashiria). Ingia
ndani! Utakuwa mgeni wetu leo. Tutakukirimu
chakula na chumba. (anamsukuma ndani)
a. Bainisha sajili ya makala haya. al 2
b. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea
makala haya. al 8

2014 Umepewa jukumu la kuwazungumzia vijana Sajili


wenzako kuhusu umuhimu wa uwekezaji.
Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia.

2013 Haya ngar’a ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara Sajili


leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona
ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe
ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya haya.
usikose mwanangu! Hamsa! Fifty! Hamsa! Fifty!
Hamsa na nyingine.
a. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. al 2
b. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea
kifungu hiki. al. 8

2012 Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo Kaida za lugha


yanavyodhibiti mifeido ya lugha.
(a) Mazingira (alama 4)
(b) Madhumuni (alama 2)
(c) Malezi (alama 4)

2011 (a) Bainisha changamoto tano zinazoikabili Chimbuko la


lugha ya Kiswahili kama somo katika shule za Kiswahili
upili nchini Kenya.
(alama 5)
(b) Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto
ulizobainisba hapo juu. (alama 5)

2010 "Benki yenyewe haina kitu ... CD4 count yake iko Sajili
chini ... Ni emergency ... Tutampoteza
ikikosekana."

(a) Taja sajili inayorejelewa na manerio


haya. (alama 2)

(b) Fafanua sifa nne zinazohusishwa na

65
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
sajili hiyo (alama 8)

2009 Eleza majukumu matano matano matano Hadhi ya lugha


ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na
Kimataifa.

2008 Eleza huku ukitoa mifano sifa tano za kimsingi Sajili


zinaaotambulisha sajili ya mazungumzo (alama
10)

2007 Huku ukitoa mifano mwataka, fafanua kaida Kaida za lugha


tano kaiika jamii ambazo matumizi ya lugha
hutegemea.

2006 Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 Sajili


sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na
hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani
kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga.
Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa
kuwaleta mashahidi ambao wametoa ushahidi
usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio
hilo. Korti hii imeonelea una hatia na imeamuru
ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila
faini ili liwe funzo kwako na kwa wenzako
wenye tabia kama zako. Una majuma mawili
kukata rufani.
a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika
katika muktadha upi?(alama 1)
b) Toa ushaidi wa jibu lako(alama 3)
c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki,
eleza sifa zingine sita za matumizi ya ligha
katika muktadha huu.
(alama 6)

SEHEMU YA C: INSHA: KCSE 2000-2021

MWAKA INSHA
2000 BARUA RASMI
2001 HOTUBA
2002 MAELEZO YA KAWAIDA
2003 MAZUNGUMZO
2004 KUMBUKUMBU

66
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302
2005 HOTUBA
2006 RIPOTI
2007 BARUA KWA MHARIRI
2008 TAHARIRI
2009 HOTUBA
2010 WASIFU
2011 MAHOJIANO
2012 KUMBUKUMBU
2013 MEMO
2014 HOTUBA
2015 RIPOTI
2016 RIPOTI
2017 BARUA KWA MHARIRI
2018 KUMBUKUMBU
2019 HOTUBA
2020 RIPOTI
2021 BARUA YA KIRAFIKI
2022 MAHOJIANO(1)
2022 BARUA YA KIRAFIKI(2)
2023 ?

MAREJELEO
Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja
Karatasi za mitihani ya KCSE
Karatasi za mitihani ya miigo
Upeo wa Sarufi
Kiswahili: Ijaribu na Uikarabati

HOJA YA MWANDISHI:
Natumai kitabu hiki kitakufaa wewe mwanafunzi na mwalimu wa Kiswahili. Ikiwa
una maswali, maoni, mapendekezo, malalamishi au marekebisho, piga simu kwa
nambari 0707311302 au utume ujumbe kwa barua pepe
johnsonoduory@gmail.com.

67
DIRA SERIES PUBLISHERS. Mwalimu Onyango. Toleo la TANO. © 2022-2023 0707311302

You might also like