Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

OFISI YA RAIS - TAMISEMI

HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA


MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2024
SOMO: URAIA NA MAADILI DARASA: VII MUDA: SAA 1:30
SEHEMU A: (Alama 20)
1. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa
i. Ni kiongozi yupi wa kata kati ya wafuatao huchaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge?__
A. ofisa mtendaji wa kata B. diwani C. mwenyekiti wa kijiji D. wajumbe wa kata E. Barozi [ ]
ii. Mwajiriwa wa serikali na mtendaji mkuu wa shughuli zote za kata ni yupi? ______
A. Afisa elimu kata B. Afisa maendeleo jamii C. Ofisa mtendaji wa kata
D. Diwani wa kata E. Bwana shamba [ ]
iii. Bendera ya taifa imepambwa na rangi kuu nne ambazo hubeba maana nzito kwa taifa letu. Je, ni rangi ipi
huwakilisha madini yanayopatikana nchini? __ A. nyekundu B. njano C. nyeusi D. bluu E. kijani [ ]
iv. Chombo cha kitaifa ambacho huwaunganisha Watanzania katika kuwasiliana ni ______
A. Wimbo wa taifa B. redio C. lugha ya Kiswahili D. simu za mkononi E. Bendera ya taifa [ ]
v. Kati ya vifuatavyo kipi hutumika kuhifadhi na kulinda sheria zote zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya muungano
wa Tanzania? ______
A. mahakama zote nchini B. magereza C. jeshi la polisi D. katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania [ ]
vi. Unapoona mtu mwenye asili ya India anaongea Kiswahili inamaanisha nini? ____
A. Hajui lugha yake ya kihindi B. Anakipenda Kiswahili kuliko kihindi C. Anaichukia lugha ya kihindi
D. Anaimarisha uhusiano wa kiutamaduni na nchi yetu [ ]
vii.Taifa letu lina historia ndefu kabla na baada ya uhuru. Kila tarehe 7 Aprili huwa tunaadhimisha _____
A. kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa B kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar
C. siku ya uhuru wa taifa D. maonesho ya biashara ya kimataifa [ ]
viii. Mwenendo wa maisha unaohusisha mila, desturi, jadi na asili ya watu hujulikana kama: ______
A. jamii B. itikadi C. utamaduni D. mazoea E. utandawazi [ ]
ix. Kati ya zifuatazo zipi ni miongoni mwa tunu za taifa letu? ________ A. lugha ya kiswahili, umoja, mshikamano,
upendo na utu B. katiba, bendera ya taifa C. fedha za nchi, wimbo wa taifa na lugha ya taifa
D. utamaduni, ndege za taifa na umoja na mshikamano [ ]
x. Katika ukuaji wa mtoto kuna mambo yanapaswa kuzingatia kati ya mtoto wa kike na wa kiume; ambapo _____
A. mtoto wa kiume kupewa kipaumbele kuliko wa kike kwa kuwa ni shujaa B. mtoto wa kike afunzwe kazi za
nyumbani pekee C. wapewe elimu ya jinsia kulingana na mabadiliko wanayopitia [ ]
D. watengwe, wasikaribiane kuwaepusha na uasherati

2. Oanisha fungu A na fungu B ili kuleta maana

FUNGU A JIBU FUNGU B


i Kutumia mali za umma kwa maslahi binafsi A. Nijukumu la wananchi wote
ii Ajira za utotoni B. Haki za binadamu
iii Rasilimali C. Ufisadi
iv Usalama wa taifa D. Milima, mabonde, madini na mbuga za wanyama
v Sikukuu ya wafanyakazi duniani E. Kutafsili sheria na kutoa haki
F. Tabia hatarishi ya kuwatumikisha watoto wadogo
katika kazi ngumu
G. Mei mosi

3. Jaza nafasi zilizoachwa wazi.


i. Jumuiya ya madola ni umoja wa mataifa huru yaliyokuwa makoloni ya uingereza ikiwemo uingereza
yenyewe Jumuiya hii ilianzishwa mwaka ……………………………………………………………………………
ii. Kitendo cha watu wawili au zaidi kufanya kazi pamoja huitwa: ……………………...………………………...
iii. Kitendo cha kumwambia mtu alichokifanya sio sahihi ni …………...………………………………….............
iv. Mfumo wa utawala ambapo wananchi hushirikishwa katika maamuzi ………………….……..………………
v. Mfumo ambao huwaunganisha watu katika ulimwengu na kuifanya dunia kama kijiji kwa kutumia teknolojia
ya habari na mawasiliano unaitwa ………………………………………………………………………
SEHEMU B: (Alama 20)
4. Umepewa majina ya marais waliopita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuanzia mwaka
1962 hadi 2015. Wapangae hao marais kwa kuwapa herufi A hadi E kwa kuzingatia aliyetangulia
kuwa rais.
i. Benjamin William Mkapa [ ]
ii. Ali Hassan Mwinyi [ ]
iii. John Pombe Magufuli [ ]
iv. Julius Kambarage Nyerere [ ]
v. Jakaya Mrisho Kikwete [ ]

5. Jibu maswali yafuatayo kwa kujaza jibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi
i. Aina kuu mbili za viongozi wa serikali za vijiji au mitaa ni ……………………………………. na ……………………………
ii. Chombo au Taasisi inayohusika na ulinzi wa watu na mali zao huitwa…………………………………..
iii. Ni makundi gani ambayo huhitaji mahitaji maalumu? Taja mawili tu……….,………………………………………………..
iv. Hali ya kuipenda nchi yako na kujitoa kutumika kwa nidhamu,uaminifu,na ukweli huitwa ……………………………..
v. Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini ni ……………………………………………………………………….

SEHEMU B: (Alama 10)


6. Chunguza picha ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata

MASWALI
i. Hao watoto wanaoonekana kwenye picha wanafanya nini? ………………………………………………………………………..…..
ii. Je, ni salama kwa watoto pekeyao kuwa mahali hapo? ……………………………………………………………………………………
iii. Ni athari gani inaweza kuwapata watoto hao kutokana na kitendo wanachofanya? ……………………………………………
iv. Ikitokea ajali kwenye eneo hilo wewe utafanya nini? …………………………………………………………………………….………..
v. Kama ungepewa nafasi ya kuwashauri hao watoto wewe ungewashauri nini? …………………………………………………..

You might also like