Fasihi Simulizi Questions With Answers

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 60

Get more notes and past papers at www.easyelimu.com.

(WhatsApp only +254703165909 for more)

Fasihi Simulizi Questions with Answers


FASIHI SIMULIZI SWALI 1
Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa
amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika.Walitegemea matunda
mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.

Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa.Ndovu aliathirika zaidi. Alijaribu kuinama majini lakini
hakuweza . Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda
kumtafuta sungura. Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata. Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo
yumo msituni.
Maswali

a. Tambua utanzu na kijipera chake. (al.2)


b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. (al.2)
c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. (al.5)
d. Eleza sifa za kifungu hiki. (al.5)
e. Eleza umuhimu wa fomyula:

i. Kutanguliza (al.3)
ii. Kuhitimisha (al.3)

MAJIBU

a.
Utanzu – Hadithi (1x1)
Kipera – Ngano za usuli (1x1)
b.
i. Fanani : paukwa
Hadhira : pakawa
ii. Fanani : Hadithi! Hadithi
Hadhira : Hadithi njoo
c.
i. Huburudisha wanajamii husika
ii. Huelekeza wanajamii husika
iii. Huelimisha wanajamii husika
iv. Huhifadhira huziona ya jamii husika
v. Huonya wanajamii wa jamii husika
vi. Hujenga ushirikiano wa jamii husika
vii. Hujenga kumbukumbu ya wanajamii. zozote (5x1)
d.
i. Huhusisha wahusika wanyama
ii. Wanyama hupewa tabia za binadamu
iii. Huwa na ucheshi mwingi
iv. Hutoa matumaini kwa wanyonge kwamba mwishowe watakuwa washindi
v. Hutoa maadili na kuonya kwa njia ya kuchekesha isiyoumiza. Zozote 5x1
e.
i. Umuhimu wa fomyula ya kutanguliza
Humtambulisha mtambaji
Huvuta makini ya hadhira
Hutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi wa ubunifu
Hutofautisha kipera cha hadithi na vipera vingine
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Huashiria mwanzo wa hadithi


Hushirikisha mtambaji na hadhira. zozote 3x1
ii. FOMYULA YA KUHITIMISHA
Hupisha shughuli nyinginezo
Huashiria mwisho wa hadithi
Hutoa funzo kwa hadithi
Humpisha mtambaji mwingine
Hupumzisha hadhira
Hutoa hadhira kutoka ulimwengu wa hadithi hadi ulimwengu halisi. Zozote 3x1

FASIHI SIMULIZI SWALI 2

Lazima
Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali
Mabibi na mabwana. Siku hii ya leo nina furaha riboribo. Furaha ghaya. Furaha inayoshinda mwanamke
aliyepata salama. Mbona nisiwe na furaha na buraha katika jamii hii iliyotuka ikashinda utukufu wenyewe?
Jamii hii yetu imedumu kwa miaka na mikaka. Kisa na maana? Umoja wetu. Mshikamano wetu. Undugu
wetu. Muungano wetu. Sote twafahamu fika bila chembe chochote cha walakini kwamba umoja ni nguvu
utengano ni udhaifu. Nani asiyejua utu ni ubinadamu? Kwamba kinachotutofautisha na hayawani ni utu?
Utu imara na dhabiti usiotikisika wala kusukasuka katika mawimbi na dhoruba za aushi. Hakuna adinasi
anayeweza kusimama tisti kama mbuyu akiwa pekee. Asiyejua kifai kwamba jifya moja haliinjiki chungu
nani?

a. Tambua kipera hiki cha mazungumzo cha fasihi simulizi. (alama 1)


b. Huku ukitoa hoja tano, fafanua umuhimu wa kipera. (alama 5)
c. Bainisha vipengele vya kimtindo vilivyotumiwa kuwasilisha ujumbe. (alama 3)
d. Unanuia kutumia mbinu ya mahojiano kukusanya habari kuhusu kitanzu hiki.
Eleza manufaa matano ya kutumia mbinu hii. (alama 5)
e. Eleza maana ya ngomezi. (alama 1)
f. Fafanua sifa tano za ngomezi. (alama 5)

FASIHI SIMULIZI SWALI 3


Umeanguka mwamba Jabali tuloegemea Lilotupa kimbilio Mahasidi kutishia Mti mkuu umegwa Wana wa
ndege wawapi? Bila shaka hangaiko 'Metukumba makinda Angalikuwa pamwe nasi Maulana Mungu wetu
Swali hilo tungemuuliza Mbona kaacha mauko Ngome yetu kuvamia? Ela mwenyewe Mwenza Ajua hatima
yetu Lilobaki kumwamini Riziki kutuangushia

a. Taja na ufananue muktadha ambao utungu huu unwaweza kutolewa. (al. 2)


b. Taja sifa za ushairi simulizi ambazo zinazojitokeza katika utongo huu. (al. 5)
c. Onyesha mitindo ambayo imetumika katika kifungu hiki. (al. 6)
d. Umeamua kufanya utafiti wa kipera hiki kwa kushiriki.

I. Taja na ufafanue hasara zake.(al. 4)


II. Taja na ufafanue faida zake.(al. 3)

Majibu

a. Muktadha wa mazishi - Mwamba umeauguka, miti mkuu umegwa


Ataje na atoe mfano
b. Mishororo
i. Uborongaji - ngome yetu kuvamia
ii. Inkisan - wawapi - wako wapi?/Lililotupa/Pamwe/pamoja.
iii. Ritifaa - 'metukumba
iv. Lugha ya mafumbo- makinda
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

miti
Jabdli.
c.
i. Jazanda - makinda watoto
-mti- mzazi
Jabelli- mzazi (mwamba.)
mti kugwa-mzazi kufa..
ii. Balagha - wana wa ndege wa wapi?
iii. Mdokezo wa methali - mti mkuu umegwa
iv. Udondoshaji + Ritifaa - metukumba.
v. Taswira - Jabali tuliloegemea/ mti mkuu umegwa.
vi. Mishata - Mbona kuacha mauko
jabali tuliloegemea.
vii. Hasara za kushiriki
d.
i. Mbinu hii huchukua muda mrefu kuliko kuuliza maswatle.
ii. Huenda mshiriki akatekwa na yaliyomo na kusahau kurekodi
iii. Ugeni wa mtafiti huweza kuzua wasiwasi miongoni mwa wenyeji wakakosa kutenda kama
kawaida.
iv. Uchanganuzi wa data inayokusanywa hivi huwa mgumu na ni rahisi kwa mtafiti kuacha
maswala muhimu.
v. Ni njia ghali ya kutafiti - lazima mtafiti asafiri nyanjani,
vi. Vifaa atakavyotumia pia hughanmu pesa mingi mfano Kanda za video
vii. Falda zake
viii. Mtafiti huja karibu sana na jamii na hupata habari za moja kwa moja tena za kuaminika
ix. Ni njia bora zaidi kutumia kwa watu ambao hawajui kusoma wala kuandikwa
x. Ni rahisi kwa mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera kilichowasilisha
xi. Ni rahisi kunasa anayosikiliza au kutazama hivyo. Kuhifadhi kumbo, toni na ishara
xii. Mtafiti hupata hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na
watendaji
xiii. Hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii - hivyo kupata habari za cutegemeka.

FASIHI SIMULIZI SWALI 4

Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali


Heri ujue mapema
Nasaba yetu haina woga
Woga haumei kwetu, humea kwa kina mamako.
Tulichinja jogoo na fahali ili uwe mwanaume.

Ah! Kisu cha ngariba ni kikali ajabu.


Iwapo utatikisa kichwacho.
Uhamie kwa wasiotahiri,
Ama tukwite njeku.

Mpwangu kumbuka hili,


Wanaume wa mlango wetu
Si waoga wa kisu
Wao hukatwa mchana hadi usiku
Wala hawalalamiki.

Siku nilipokatwa
Nilisimama tisti
Nikacheka ngariba kwa tashtiti
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Halikunitoka chozi.

Iwapo utapepesa kope


Wasichana wa kwetu na wa mbali
Wote watakucheka
Ubaki ukinuna.

Sembe umepokea
Na supu ya makongoro ukabugia
Sema unachotaka
Usije kunitia aibu

Maswali;

a. Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha (alama 2)


b. Taja na uthibitishe shughuli zozote za kiuchumi za jamii ya wimbo huu (alama 4)
c. Thibitisha nafsineni na nafsinenewa katika utungo huu. (alama 2)
d. Mwimbaji wa wimbo huu ana taasubi ya kiume. Thibitisha kauli hii. (alama 2)
e. Umepewa wajibu wa kutafiti michezo ya watoto katika jamii yako. Pendekeza mbinu ambazo jamii
yako inaweza kutumia kuendeleza kipera hiki. (alama 6)
f. Fafanua mbinu nne ambazo fanani anaweza kutumia kufanikisha uwasilishaji wa soga. (alama 4)

MAJIBU

a. Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha (alama 2)

Wimbo wa tohara / nyisho – mpwake anatayarishiwa kukabiliana na kisu cha ngariba


Mwanafunzi lazima athibitishe
b. Shughuli za kiuchumi (alama 2x1)

i. Ufugaji / wafugaji – Anayeimbiwa wimbo alipozaliwa fahali alichinjwa.


ii. Ukulima / kilimo - sembe na supu
c. Nani mwimbaji wa wimbo na anamwimbia nani? (alama 2x1)

i. Mwimbaji – mjomba
ii. Mwimbiwa – mpwa (mtoto wa dadake mwimbaji)
d. Mwimbaji wa wimbo huu ana taasubi ya kiume – Thibitisha kauli hii (alama 4x1)

i. Anaona kuwa waoga ni akina mama


ii. Anasifu wanume wa mbari yao kuwa si waoga
iii. Akilia atachekwa na wasichana
iv. Anaambiwa kuwa ni “Ndume / mme” akabiliane na kisu
e. Mbinu za kuendeleza michezo ya watoto

Matumizi ya tamasha za muziki ya kitamaduni katika shule, vyuo na mashirika mbalimbali –


katika ngazi ya kitaifa na kimataifa
Kuirithisha jamii/ Kushirikisha fasihi simulizi katika sherehe za harusi, jandoni, mazishi na
matambiko katika jamii mbalimbali
Kuimarisha na kusisitiza vipindi vya redio na runinga katika vituo vyetu stesheni zetu
Kuimarisha michezo ya kuigiza, mashairi, na nyimbo kupitia redio, runinga na shughuli
nyingi za kitaifa
Kuimarisha utafiti wa Nyanja/vipera mbalimbali ya fasihi simulizi
Kufadhili utafiti wa michezo ya watoto
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kuandikwa vitabuni,
Tarakilishi na kanda za video kuhifadhi baadhi ya vipera vya fasihi simulizi
Kufunzwa shuleni
Kuweka sera za kuilinda
(alama 6x1)
f. mbinu za kufanikisha uwasilishaji wa soga.
Urudiaji
Uzungumzi nafsia
Uigizaji
Chuku
Taswira
Upenyezi / uchopekaji wa fanani
Tashhisi
Nidaa
Kuzungumza moja kwa moja
Hoja nne za mwanzo 4x1= 4

FASIHI SIMULIZI SWALI 5

Malaika,
Nakupenda malaika x 2
Ningekuoa malaika…
Ningekuoa dada…
Nashindwa na mali sina wee…
Ningekuoa malaika x 2
Pesa, zasumbua roho yangu x2
Nami nifanyeje,kijana mwenzio
Nashindwa na mali sina wee…
Ningekuoa malaika x 2

Maswali.

i. Tambua utungo huu. (al.2)


ii. Toa sababu za jibu lako hapo juu. (al.2)
iii. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi kwenye kipera hiki. (al.2)
iv. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa kwenye utungo huu. (al.2)
v. Jadili vipi mwasilishaji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake. (al.6)
vi. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumba mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani. (al.6)

MAJIBU

a. Wimbo auwimbo wa mapenzi. 1x2


b.
Matumizi ya lugha mkato na kuvuta kwa mfano…
Urudiaji wa vipande;ningekuwa malaika
Uwepo wa beti
Kuna kiitiko
2x1=2
c.
i. Shughuli ya kijamii-kuoa/ndoa 1x1
ii. Shughuli ya kiuchumi-ulipaji mahari 1x1
d.
Nafsi neni; Kijana anayaetaka kuoa 1x1
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Nafsi nenewa: Msichana anayechumbiwa 1x1


e.
Kupandisha na kushusha sauti
Matumizi ya viziada lugha
Uwe mfaraguzi
Kubalisha kiimbo na toni kulingana na hali
Awe jasiriili aweze kuimba bila aibu.
Zozote 3x2
f.
Gharama ghali za utafiti mf;kununua vifaa kama tepurekoda
Kupotea au kufisidiwa vifaa vya kuhifadhia data.
Ukosefun wa wakati wa kutosha wa kufanyia utafiti
Vikwazo kutoka kwa watawala-kunyimwa nafasi
Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi
Mtatizo ya kibinafsimf;kushindwa kudhibiti wahojiwa.
Ukosefu wausalama mf; kuvamiwa
(zozte 3x2)

FASIHI SIMULIZI SWALI 6

a. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)


b. Eleza kwa hoja tano, umuhimu wa kushiriki kama njia ya kukusanya data. (al. 5)
c. kikundi cha Tamasha Bora kiliwasilisha maigizo katika ukumbi wa shule yenu.
Fafanua kwa hoja tano sababu za uwasilishi wao kufanikiwa. (alama 5)
d. Eleza msamiati ufuatao (alama 5)
i. Ulumbi
ii. Mbazi
iii. Lakabu
iv. Matambiko
v. Rara nafsi

MAJIBU

a. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)


Maandalizi
Utafiti na ukusanyaji data
Rekodi ya data
Kuchunguza data na kunakili ili kuchanganua baadaye
Uchanganuzi na kufasiri data.
b. Eleza kwa hoja tano, umuhimu wa kushiriki kama njia ya kukusanya data (alama 5)
Kupata habari za kuaminika
Njia bora kwa wasiojua kusoma
Rahisi mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera
Mtafiti anaweza kunakili anayotazama au kusikiliza na hivyo kuhifadhi kiimbo, toni na
ishara. -Mtafiti anaweza kuthibitisha aliyokusanya
Kushiriki hukuza utangamano
c. Kikundi cha Tamasha Bora kiliwasilisha maigizo katika ukumbi wa shule yenu. Fafanua kwa hoja
tano sababu za uwasilishi wao kufanikiwa. (alama 5)
Ujasiri wa waigizaji
Ublnifu wa waigizaji - kutumia mbinu mbalimbalu ili kufanya uihizaji kuvutia
Ujuzi wa kutumia ishara za uso,mwili na miondoko inayooana na yanayoigizwa
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Ujuzi na ufasaha wa lugha na waigizaji


Kuielewa hadhira na kubadili mtindo ipasavyo
Matumizi ya maleba mwafaka
Kushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali
Kuelewa utamaduni wa hadhira
Ufaraguzi wa wahusika
d.
a. Eleza msamiati ufuatao (alama 5)
i. Ulumbi
Uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee/ utumiaji lugha kwa mvuto wa
kipekee
ii. Mbazi
Hadithi fupi yenye mafunzo na inayotolewa kama kielelezo wakati wa kumkanya au
kumwelekeza mtu.
iii. Lakabu
Jina la msimbo/kupanga ambalo mtu hujibandika au hubandikwa kutokana na sifa
zake za kimaumbile, kitabaka, kitabia au kimatendo
iv. Matambiko
Sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu moja
kwa moja ili kutatua matatizo ya kijamii ama kwa shukrani.
v. Rara nafsi
Ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake
mwenyewe

FASIHI SIMULIZI SWALI 7

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali


Lulu, mwanangu tulia,
Wiwi mtoto lala, mvua imekuja
Si uongo hata na miti huichangamkia
mvua, hakuna haja ya kuelezwa,
Lulu mwana tulia,
Wiwi mtoto lala, mvua imekuja.

i. Tambua kipera hiki (alama 2)


ii. Taja sifa nne za kipera hiki (alama 4)
iii. Eleza majukumu manne ya kipera hiki (alama 4)

MAJIBU

i. Tambua kipera hiki (alama 2)


Kipera-Bembea/Bembezi/Bembelezi 1x2
ii. Taja sifa nne za kipera hiki (aloma 4 sifa za Bembea
Huimbwa taratibu kwa sauti na mahadhi ya chini
Huwa fupi Huimbwa na wazazi au walezi wa watoto kuwaliwaza ili watoto wanyamaze au
walaleHutofaitiana kutoka jamii moja hadi nyingine kulingana na thamani za jamii hiyo
Hurudiwarudiwa maneno au kibwagizo Hutumia lugha shawishi na wakati mwingine ahadi
hutolewa
iii. Eleza majukumu manne ya kipera hiki (alama 4)
Majukumu ya Bembea
Hutumbuiza na kuongoa watoto
Hutumiwa kama sifo kumsifu mtoto ambaye ni mtulivu
Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Husawin mahusiano katika jamii


Hutakasa hisia ambazo mwimbaji huweza kuwa nazo
Humwelimisha mtoto katika umri mchanga (alama 4x1)

FASIHI SIMULIZI SWALI 8


Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ewe Mainga wa Ndumi
Siwe uloambia akina mama
Siku tulopiga foleni
Chakula cha msaada kupata
Turudishe vifaranga kwenye miji
Wageuke vijusi tena
Njaa isiwaangamize?
Siwe ulopita
Matusi ukitema
Chumvi na sukarikuturushia ja samadi?
Uhitaji wetu ukatutuma
Kuokota vihela uloturushia
Ukatununua,kura ukapata?
Sasa miaka mitano imetimia
Waja tulaghai tena
Mainga wa Ndumi huna lolote safari hii
Ubunge umekudondoka ukitazama

Maswali

a. Huu ni wimbo wa aina gani? (alama 2)


b. Taja shughuli mojamoja ya kijamii na kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu.
(alama 2 )
c. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani, eleza mambo sita ambayo utazingatia katika
uwasilishaji wako. (alama 6)
d. Jadili jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)
e. Maandishi ni mojawepo ya vifaa vya kukusanya na kuhifadhi fasihi simulizi. Tathmini udhaifu wa
kutumia kifaa hiki. (alama 5)

MAJIBU

a. Huu ni wimbo wa aina gani? (alama 2)


siasa mfano umetaja kura na ubunge
b. Taja shughuli mojamoja ya kijamii na kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu
(alama 2 )
shughuli ya kijamii –siasa mfara kura, ubunge
Shughuli ya kiuchumii –biashara
c. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani, eleza mambo sita ambayo utazingatia katika
uwasilishaji wako. (alama 6)
Kuigiza baadhi ya matukio
Kushiriki kuimba wimbo huo
Kutoa mifano ya baadhi ya wahusika
Kuuliza maswali balagha
Kubadilisha toni/kiimbo
Matumizi ya viziadalugha/sehemu za mwili.
Kutumia mtuo wa kidrama kuongeza taharuki au kusisitiza ujumbe.
Kuwa mchangamfu na mcheshi.
Kuwa na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka.
d. Jadili jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kupitia tamasha za muziki mfano wanafunzi hukariri


Kupitia sherehe za harusi,mazishi ambayo ni mifano ya mivigha
Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia runinga
Michezo ya kuigiza katika runinga
Tamasha za drama huendeleza utanzu wa maigizo
Sarakasi zinazofanywa na wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho
Utambaji wa hadithi bado hufanyika
e. Maandishi ni mojawapo ya vifaa vya kukusanya na kuhifadhi fasihi simulizi. Tathmini udhaifu wa
kutumia kifaa hiki. (alama 5)
Mambo kama vile kiimbo,toni ,hisia na mapigo ya muziki huweza kupotea,
Kwa vile maandishi si hai,hayawezi kutenda wala kusema
Kuandika fasihi simulizi hufanya kukosa ile taathira asilia
Kuiandika fasihi simulizi huidhibiti na kupunguza hadhira yake na kuathiri vibaya
usambazaji wake.
Baadhi ya watafiti huenda wakaandika yale ambayo wanahitaji kwa wakati mahuhususi na
kupunguza mengine.

FASIHI SIMULIZI SWALI 9


Soma hadithi hii kisha ujibu maswali
Ilikuwa alfajiri yenye baridi. Umande ulitapakaa kote. Ukungu ulitanda hivi kwamba hungeweza kumuona
mtu alikuwa hatua chache mbele yako.Ndovu alipoamka, alikuta fisi mlangoni pake. Fisi alikuwa
amemlimia ndovu shamba lake, lakini alikuwa hajalipwa ujira wake.
Kila alipomwendea ndovu kwa ajili ya malipo yake, fisi alitiliwa huku na kutolewa kule.”Leo ni leo”,fisi
alimwambia ndovu.”Nimevumilia vya kutosha. Kila siku ninapokuja kuchukua pesa zangu, hukosi hadithi
mpya ya kunisimulia. Leo sitoki hapa bila pesa zangu!”
Fisi alipomaliza kumwaga joto lake, ndovu alimwambia: “Sikiliza fisi. Mimi nimeheshimika kote kijijini.
Naona haja yako ni kunivunjia heshima –mbele ya familia yangu na wanakijiji kwa jumla. Sikulipi pesa
zako, mpaka ujifunze kuwaheshimu wazee. Nakuamuru uondoke hapa mara moja, kabla sijakasirika!
Nataka uende popote, unapofikiria kwamba unaweza kupata msaada. Ukienda kwa chifu, usisahau
kwamba tunakunywa na yeye. Ukienda polisi, mkuu wa kituo amejaa tele mfukoni mwangu. Ukienda
mahakamani, hakimu tulisoma darasa moja. Popote uendapo, hakuna yeyote atakayekusikiliza”
“Zaidi ya hayo, hakuna yeyote atakayekuamini.Mimi naitwa Bwana pesa.Kwangu umeota mpesapesa na
kustawi. Nani ataamini kwamba naweza kushindwa kulipa vijisenti vichache ninavyodaiwa na fisi?”
Fisi alisikiliza kwa makini majitapo ya ndovu. Aliamua kumpasulia ndovu mbarika: “Bwana ndovu najua
kuwa wewe una nguvu na uwezo mkubwa wa kifedha.Lakini hayo yote mimi hayanihusu ni yako na familia
yako. Sitakuruhusu unidhulumu kilicho haki yangu. Usiutumie uwezo uliopewa na Muumba kuwaonea na
kuwanyanyasa maskini wasio mbele wala nyuma” alimaliza usemi wake na kuondoka huku machozi
yakimdondoka.
Fisi alipofika nyumbani, aliwasimulia fisi wanyonge wenzake yaliyomsibu.Fisi walikusanyika na kulizingira
boma la ndovu huku wakisema: “Tunataka haki itekelezwe! Dhuluma lazima ikome! Unyanyasaji lazima
ukome!” Ndovu aliposikia kelele langoni mwake, alipiga simu kwenye kituo cha polisi.
Mara, kikosi cha polisi wa kupambana na ghasi kiliwasili. Fisi walipigwa mijeledi na kuezekwa marungu.
Waliojifanya mabingwa walipigwa risasi. Fisi waliosalia walikimbilia makwao, huku wakichechemea kwa
maumivu. Mpaka wa leo fisi wangali wanatembea kwa kuchechemea.
Maswali

a. Usimulizi huu ni wa aina gani? Toa sababu. (alama 4)


b. Eleza mtindo wa lugha uliotumika katika hadithi hii. (alama 4)
c. Eleza sifa za ndovu katika hadith hii. (alama 5)
d. Fafanua jinsi kisa hiki kinavyo dhihirisha methali: ‘Mwenye nguvu mpishe’ (alama 4)
e. Je, hadithi zina umuhimu gani katika jamii? (alama 3)

MAJIBU

Hurafa (alama 1)
Ameshirikisha wanyama kama wahusika (alama 1)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

0. Usuli

1. Unaeleza chanzo cha fisi kuchechemea (alama 1)


i. Methali - Leo ni leo
a. Semi
i. Kumpasulia mbarika
ii. Kuvunjia heshima
iii. Wasio na mbele wala nyuma
iv. Amejaa tele mfukoni.
Kutaja 1 Mfano 1 Zozote 2 x 2 = 4
ii.
i. Mwenye majitapo
ii. Mwenye nguvu
iii. Mwenye uwezo mkubwa
iv. Mdhalimu
v. Mnyanyasaji
vi. Mjeuri Zozote 5 x 1 = 5
iii.
Ndovu ni mwenye nguvu
Anamdhulumu fisi kwa kutomlipa pesa baada ya kufanya kazi shambani.
Fisi hana nguvu / mnyonge
Fisi wanapoamua kuitisha haki wanapigwa mijeledi na waliosalia kuchechemea
kwao.
Hoja 4 x 1 = 4
iv. Kuelimisha
v. Kuburudisha
vi. Kuendeleza maadili zozote 3 x 1 = 3

FASIHI SIMULIZI SWALI 10

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali uliyopewa.

Msichana wa sura nzuri


Kitu gani kinakufanya usiolewe
Elimu unayo ya kutosha
Hata ng’ambo ukaenda ukarudi

Msichana wa urembo kama wewe


Uonyeshe mapenzi kwa vijana
Ukionyesha majivuno kwa vijana
Utazeeka ukiwa nyumbani kwenu

Ooh baby, miaka yaenda mbio sana


Na sura yako nayo ikichunjuka
Ooh baby, miaka yaenda mbio sana
Na sura yako nayo ikichuchuka

Pengine tabia zako ndizo mbaya


Awali kweli dada ulijivuna
Kwanza mimi nilitaka nikuoe
Ukaringa ati sina masomo

Ooh baby, ona watoto wa nyuma yako


Wameolewa wamekuwacha ukihangaika
Ooh baby, ona watoto wa nyuma yako
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Wameolewa wamekuwacha ukihangaika

Msichana wa sura nzuri


Kitu gani kinakufanya usiolewe
Elimu unayo ya kutosha
Hata ng’ambo ukaenda ukarudi

A.
i. Taja shughuli mbili za kijamii katika utungo huu. (al 2)
ii. Fafanua mbinu zozote mbili za kimtindo katika utungo huu huku ukitoa mifano
mwafaka. (al 2)
iii. Eleza toni ya utungo huu. (al 2)
B. Wewe kama mwasilishaji wa kazi ya fasihi simulizi, ni mbinu zipi ungetumia ili kufanikisha
uwasilishaji wa utungo huu? (al 5)
C. Taja changamoto nne zinazokumba kukua na kuendelea kwa fasihi simulizi. (al 5)
D. Ni sababu zipi zinaweza mfanya fanani kufaragua katika uwasilishaji wa hadithi? (al 4)

MAJIBU

A.
i. shughuli za kijamii
Elimu
Ndoa
2X1=2
ii. mbinu za kimtindo
Kuchanganya ndimi-ooh baby
Taswira oni-sura nzuri
2X1=2
iii. toni ya utungo
Toni ya huzuni-nafsi neni anahuzunika kwa kukataliwa na msichana mrembo.
Toni ya masimango-anamsimanga Yule msichana kwa sababu amezeeka kabla ya
kuolewa. 2x1=2
B. jinsi ya kufanikisha uwasilishaji wa fasihi simulizi
Kuvaa maleba panapohitajika.
Kubadilisha toni ipasavyo ili iwiane na matukio ya uwasilishaji wako.
Miondoko ya viungo vya mwili pia ni muhimu.
Kuihusisha hadhira pia njia nzuri ya kufanikisha uwasilishaji wa fasihi simulizi.
Kutumia ala husika hasa katika kipera cha ushairi simulizi.
Kuwasilishia kazi hii mahali panapofaa. Mfano, jukwaani.
Kuhakisha kwamba umezingia utamaduni wa jamii husika.
Pia ni vizuri kutilia maanani umri na kiwango cha elimu cha hadhira yako.
5x1=5
C. Changamoto zinazokumba kuendelea na kuenea kwa fasihi simulizi
Kukua na kuendelea sana kwa kazi ya kimaandishi.
ukosefu wa utafiti wa kutosha kuhusu fasihi simulizi.
Uchache wa wataalam wa kutosha wa kutafitia kazi ya fashihi simulizi.
maendelea ya kiteknolojia na sayansi yanayo athiri mtazama ya jamaa kuhusu fasihi
simulizi.
Watu kuhamia mjini na kutangamana na watu wa jamii zingine tofauti kunafanya uhifadhi
wa fasihi simulizi kuwa mgumu mno.
Mtaala wa elimu pia umepuuza lugha za kiasili ambazo ndizo nyenzo kuu ya kurithisha
fasihi simulizi.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

D. Sababu za kufaragua
Fanani huenda akasahau na kubadilisha mtiririko wa hadithi
Anaweza kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira yake k.v umri
Mabadiliko ya kiwakati pia yanaweza kumfanya afarague ili kuingiliana kiwakati na hadhira.
Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha.
Ubunifu wa fanani ili uwasilishaji wake uweze kuvutia zaidi
Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale
ambayo ni muhimu na kuacha mengine.
Kutoeleweka hivyo kuhifadhiwa vibaya.
5x1=5

FASIHI SIMULIZI SWALI 11

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.


Walisema waliosema
Kitali hakina macho
Huvizia wapendwa
Kikafakamia
Kwenye kinywa kisochoka
Kwa mara nyingine hasidi
Ametudhalilisha
Amewapapu kutisha wanetu
Majagina kupiga busu la sime
Jeshi letu sasa ni mateka
Wasaliti wamewapa mahasimu
Cheko la kutucheka
Nii kilio ni kilio ni kilio tangamano

a. Tambua utanzu na kipera cha kifungu hiki. (alama 2)


b. Eleza toni ya kifungu hiki. (alama 2)
c. Eleza sifa sita za kipera kinachorejelewa. (alama 6)
d. Fafanua majukumu ya kipera hiki katika uwasilishaji wa ngano. (alama 10)

MAJIBU

a. Tambua utanzu na kipera cha kifungu hiki. (alama 2)


Utanzu-Ushairi alama 1
Kipera- Nyimbo za mbolezi alama 1
b. Eleza toni ya kifungu hiki. (alama 2)
Huzuni/ uchungu/masikitiko- ni kilio nikilio/ hurizia wapendwa. 1×2
c. Eleza sifa sita za kipera kinachorejelewa. (alama 6)
i. Hutofautiana katika jamii moja hadi nyingine kutegemea imani ya jamii kuhusu kifo na
hadhi ya waliofiwa.
ii. Huimbwa kwa nia ya kufariji waliofiwa.
iii. Husifu aliyekufa- sifa chanya za aliyekufa.
iv. Hufungamana na muktadha maalum.
v. Huimbwa wakati wa matanga au wakati wa kuomboleza
vi. Huimbwa kwa toni ya uchungu/ huzuni
vii. Huimbwa kwa mwendo wa taratibu.
viii. Huandamana na ala za muziki. Za kwanza 6×1
d. Fafanua majukumu ya kipera hiki katika uwasilishaji wa ngano.
i. Hutumiwa kuwasilisha ujumbe mzito katika hadithi.
ii. Hutenganisha matukio yanayojumuisha hadithi.
iii. Husisimua hadhira na kuiondolea ukinaifu wa masimulizi makavu
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

iv. Huishirikisha hadhira katika utambaji na uwasilishaji.


v. Hurefusha hadithi.
vi. Ni kipumuo. Hupunguzia hadhira uchovu.
vii. Huipa hadithi toni fulani mf. Toni ya huzuni.
viii. Huendeleza hadithi.
ix. Huangazia maadili katika hadithi.
x. Huburudisha jamii
xi. Huchangia kama kitambulisho cha jamii husika. Zozote l0×1=10

FASIHI SIMULIZI SWALI 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.


Hapo zamani, katika enzi za mababu zetu, wanyama wote waliishi jinsi sisi binadamu tunavyoishi.
Waliweza kulima, kufunga, kuchota maji na hata kupika. Wanyama wote waliishi katika jamii tofauti tofauti
kwenye vijiji. Vijiji kadha, kwa pamoja viliunda milki iliyotawaliwa na mnyama mmoja aliyechaguliwa na
wanyama wengine kuwa mfalme wao. Kwa kawaida, mnyama aliyechanguliwa kuwa mfalme alikuwa na
sifa za kipekee. Kama vile sungura alikuwa na werevu mwingi, Faru, Nyati na Ndovu walikuwa na nguvu za
kupindukia . Simba , Chui au Duma walikuwa wakali sana.

Kulikuwa na milki mbili kubwa zaidi zilizopakana; Almasi iliyoongozwa na Simba na Dhahabu iliyoongozwa
na Nyati. Milki hizi mbili zilitoshana kwa kila kitu – si ustawi wa kielimu, si wa kiuchumi, si wa
miundomsingi. Wanyama wote katika milki hizi waliishi kwa mtagusano uliowawezesha kuishi kwa amani
na umoja. Hili lilitiwa mbolea zaidi na kwamba viongozi wao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana.

Hata hivyo, baada ya muda, Simba alianza kujiona kuwa alistahili eneo kubwa kuliko Nyati. Alianza kuota
akiwa mfalme wa milki zote mbili. Katika ndoto zake alimwona Nyati akinyenyekea mbele yake. Alifikiri
kuwa wadhifa wake ungekuwa wa juu zaidi kama angemiliki rasilmali za miliki zote mbili. Mawazo haya
yalimfanya Simba kujaa chuki nyingi kila walipokutana na Nyati.

Kama wasemavyo wahenga, “Kikulacho ki nguoni mwako.” Simba alianza kumtembelea Nyati kuuliza
ushauri wa jinsi wangeweza kuunda muungano wa milki zao. Nyati aliliona wazo la Simba kuwa nzuri lakini
akampendekezea rafikiye kuwa wachukue muda kutafakari zaidi juu ya muungano huo. Wazo hili
halikumfurahisha Simba kwani alimwona Nyati kama kizingiti kwenye ngazi yake ya madaraka. Hapo
ndipo Simba alipoanza kupanga mikakati ya kumng’oa Nyati mamlakani.

Baada ta kuhakikisha kuwa mipango yake imekamilika, Simba aliamua kumvizia Nyati kumwangamiza.
Hata hivyo, Nyati aliweza kuonywa na marafiki zake waliokuwa kwenye utawala wa Simba kabla ya Simba
kumvamia. Alipofahamu mipango hasi ya Simba, Nyati pia aliamua kujihami ili kujikinga dhidi ya Simba.
Pupa za Simba za kuongoza zilimfanya amvamie Nyati katika milki yake. Simba alikuwa amesahau kuwa
mwenye pupa hadiriki kula tamu. Vita vikali kati ya milki hizi mbili vilizuka. Umoja uliokuwepo ukageuka
utengano, uhusiano wao ulikuwa umeingia nyufa.

Nyati alikataa Abadan kumwachia Simba mamlaka kwa nguvu. Alihimiza kikosi chake kupigana kwa
vyovyote vile ili kuhifadhi uhuru wao, jambo ambalo walilifanya kwa uwezo wao wote. Kama isemavyo,
“Fahali wawili wapiganapo nyasi ndizo huumia.” Wengi waliumia wasiojua kiini cha vita hivi.

Vita vilidumu kwa muda mrefu. Kwa kawaida Nyati aliwapenda wanyama aliowaongoza kwa moyo wake
wote. Kila usiku alifikiri jinsi ya kuvimaliza vita hivi ili kuepusha maafa zaidi katika milki yake. Hata hivyo,
alipata na namna mbili tu za kulishughulikia jambo hili – aidha aendelee kupigana na kuwaangamiza
wanyama wake wote au akubali wito wa Simba kung’atuka mamlakani. Aliamua kuwaita washauri wake
kwenye makao makuu ya milki ili wajadili jinsi ya kunusuru milki yao. Washauri wake walionekana
kugawanyika mara mbili. Kundi moja lilisistiza kuwa amani haiji ila kwa ncha ya upanga ilhali lingine liliona
heri nusu shari kuliko shari kamili. Nyati aliwaza na kuwazua asijue la kufanya.

Hadithi yangu inaishia hapo.

Maswali
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

a.
i. Kwa kutoa mfano katika hadithi hii, eleza kwa nini ngano hii ni ya mtanziko. (al. 2)
ii. Fafanua mitindo yoyote mitano aliyotumia msimulizi kufanikisha usimulizi wake. (al. 5)
iii. Huku ukitoa sababu tano fafanua umuhimu wa kushirikisha hadhira katika usimulizi wa
ngano kama hii. (al. 5)
b. Onesha kwa mifano mine jinsi jamii huhifadhi kipera cha ngano sasa. (al. 4)
c. Ni changamoto zipi zinazoweza kumkumba mtafiti akifanya utafiti wa ngano nyanjani. (al.4)

MAJIBU

a.
i. mtanziko kwa vile hatimaye Nyati hakuweza kutoa uamuzi wa kuach vita au kuendelea na
vita x 2
ii. minu tano za kimtindo
i. Usimulizi
ii. Dayalojia
iii. Uhaishaji – wanyama kutenda kama binadamu
iv. Misemo – tia molea
v. Chuku – kuwa na nguvu kupindukia
vi. Methali – kikulacho ki nguoni mwako
vii. Fonyula – hapo zamani
viii. Tabaini matumizi ya ‘si’
ix. Mninu rejeshi – hapo zamani 5 x 1=5
iii. umuhimu wa kushirikisha hadhira katika wasilisho
i. Kuondosha ukinaifu
ii. Kulipa wasilisho uhai
iii. Huwapa kumbukizi ya matukio
iv. Huelewa funzo
v. Watauliza maswali ili kueleweshwa
vi. Watajibu maswali ili kuonyesha uelewa wao
vii. Kuitikia huonyesha ukubalifu wao
viii. Kucheka kwao huonyesha kuburudika si haba
b.
i. kuandika vitabuni/ kuchapisha
ii. vinasa sauti/kurekodi
iii. filamu/ video
iv. Matandaoni/ mawinguni
v. tarakilishi/vipatarakilishi/ vipakatalishi
vi. sidi/diski tepevu. Zozote 4 x 1=4
c.
i. gharama kuwa juu
ii. mtazamo hasi wa jamii
iii. kushukiwa kwamba mtafiti anawapeleleza
iv. wahojiwa kudai kulipwa
v. mbinu nyingine kama hujaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika
vi. vikwazo vya kidini – fikiria kwamba matendo ya fasihi simulizi ni ya kishenzi
vii. kupotea na kufisidiwa kwa vifaa
viii. uchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi
ix. watawala kukataa kuoba idhini/ruhusa
x. matatizo ya usafviri/matatgizo ya mawasiliano na uchukuzi
xi. hali mbaya ya anga
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

xii. kukosa wakati wa kutosha


xiii. matatizo ya kibinafsi – mfano mtafiti kushindwa kuidhiiti hadhira.
xiv. Ukosefu wa usalama
xv. Tatizo la tafsiri ya data
Zozote 4 x 1 =4

FASIHI SIMULIZI SWALI 13

Soma utungo ufuatao kasha ujibu maswali yanayofuata.

Nilipokukopoa,
Cheko la mwivu wangu lilipaa sana
Ukewenza ukamshawishi kuchukua buruji kueneza habari.
“Njooni mwone jana la ajabu.”
“Hajawahi kuonekana kama huyu
Tangu kuumbwa kwa ulimwengu.”
Ndivyo walisema walokubeza
Kijiji kizima kilimiminika mwangu nyumbani
Kuyatuma maozi kukutazama weye
Uso na thamani walikwona,
Wakaupa unyonge moyo wangu toto,
Wakanituma kuola viungo vyako
Wakanitanabahisha upungufu ulokulemaza!
Chozi chungu likapukitika
Likalovya change kidari
Likalovya chaoko kipaji
Tabasamu ukatoa kunihakikishia
“Mimi si mjalana!
Katu sivyo wasemavyo walimwengu!”
Neno lako hili likanipa tulivu
Nikaamua alakulihali kupambana na yangu jumuiya
Ilpsema kwa moja kauli utokomezwe, chakani utupwe.
Tazameni mahasidi mloteka
Teko la dharau mlonimwaiya
Mkanitia ukiwa usomithilika!
Oleni! Tungeni macho!
Mwana mlioambaa ukoma
Ulomwinga ja nyuni wala mtama, tazameni
Mekuwa malaika, anowaauni
Kiguru mlomtajia hakimzuwii kufuma mishale!
Maadui wamwonapo hutetema kama jani
Mefagia vijiji vinane kwa pigo moja la kiganja chake
Mepigana vita visohisabika
Na Wetu mahasimu waliotupoka na mifugo.

Jamii yetu sasa metawala kote


Umekuwa nahodha mwenye kubwa saburi
Akili yako nyepesi sumaku kweli kweli
Hupakata yote ya neema na shwari
Mwili wako japo lemavu,
Mesheheni nguvu za majagina mia moja!
Naposhika zana, maadui elfu huanguka!
Umeifaa jamii hii, ilotaka kuangamiza
Majagina wote, wakusujudia
Walokufurusha wamebaki hizika
Watukuka ewe shibli
Mfano wa Shaka Zulu
Alowayeyusha kama barafu.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Limwengu mzima wakujua, mwana


Alozawa kishika mkuki
Ulosema na miungu, alfajiri lipoukumbatia ulimwengu
Wla mwana jihadhari usaliti wao waja
Wasije kutosa lindini kwa nduli kukukabidhi.

MASWALI

a. Ainisha utungo huu kimuundo na kimaudhui. (ala. 2)


b. Eleza sifa tatu za mighani ambazo zinajitokeza katika utungo huu. (ala.6)
c. Jadili fani katika wimbo huu. (ala.5)
d. Jadili sifa za jamii iliyoizaa kazi hii. (ala. 2)
e. Ni nani anayimba wimbo huu (nafsineni)? (ala.1)
f. Eleza tofauti 4 kati ya mighani na visasili (ala.4)

MAJIBU

i. Hasira Hasara/Jua Hasira Hasara/Epuka Hasira 1 x 1 = Al. 1


ii.
Tarbia – Mishororo 4 katika ubeti
Ukara – Vina vya utao vinatiririka|
2 x 2 = Al. 4
(Asipotoa sababu asituzwe)
iii. Fafanua umbo la shairi hili.
Shairi hili lina beti saba.
Mishororo 4 katika ubeti
Vipande 2 – ukwapi na utao
Mizani 16 katika mishororo
Vina vya mwisho wa mishororo vinatiririka
Shairi hili lina kibwagizo – “Ukiitaka salama, jua hasira hasara”
Zozote 4 x 1 = Al. 4
iv.
Inkisari – takusaidia (mshororo wa kwanza)
Kuboronga sarufi – ‘kuweka yako azima’ badala ya kuweka azima yako
Tabdila – Ubeti 5 – ‘Sinyamai’ badala ya ‘Simanyazi’
Zozote 3 x 1 = Al. 3
v.
√√Mshairi anawasihi watu wazima na watoto kupunguza hasira. Mtu aulizapo moyo wake
hasira zinapotea.
√√Anawashauri watu wawe na subira ili waipate na neema
√√Mtu akitoka salama akumbuke kuwa hasira ni hasara.
1 x 3 = Al. 3
vi. Toni ya kushauri – anashauri dhidi ya hasira
1 x 1 = Al. 1
vii. Mshairi/yeyote mwenye wosia
1 x 1 = Al. 1
viii.
a. Moyo
b. Pesa/Ngwenje/Fuhisi
x 2 = Al. 2

FASIHI SIMULIZI SWALI 14


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Hawa wanifuatao wananicha,


kwa ukoo wangu mtukufu
kawa jadi yenye majagina
wa mioyo na vitendo
wananicha,
Kwa kuwa wa kwanza kijijini
kuvishwa taji
kwa mabuku kubukua
kwa kuwa jogoo wa kwanza
kuwika kwenye anga za ilimu
idhini nikakabidhiwa,
ya tafiti kuendeleza
mamlaka nikapewa
ya kuwaza kwa niaba ya jamii.
Hawa wanifuatao wananicha
kwa kuweza
kuvyaza mikakati
ya kukabiliana na ulitima walonipagaza
kwa ndoto zangu za ujana kuzima.

a. Tambua kipera hiki cha fasihi simulizi. (alama 1)


b. Kwa kurejelea kifungu hiki taja sababu tatu kwa jibu lako. (alama 3)
c. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo katika kifungu hiki. (alama 2)
d. Eleza sifa sita bainifu za kipera hiki. (alama 6)
e. Kipera hiki kinaendelea kudidimia katika jamii yako. Eleza hoja nne utakazotumia kuishawishi jamii
yako kukinga hali hii. (alama 4)
f. Fafanua umuhimu wa kipera hiki katika jamii. (alama 4)

MAJIBU

a. Majigambo/vivugo. 1x1
b.
i. Kwa ukoo wangu mtukufu, kwa jadi yenye majagina.
ii. Kuwa wa kwanza kijijini kuvishwa taji.
iii. Kuwa jogoo wa kwanza kuwika kwenye anga za ilimu.
iv. Kuweza kuvyaza mikakati ya kukabiliana na ulitima. 3x1
c.
i. Takriri/uradidi- hawa, wanifatao, wananicha.
ii. Inkisari – walonipagaza – walilonipagaza
iii. Lahaja – ilimu
iv. Jazanda/stiara – kuwa jogoo wa kwanza kuwika. 2x1=2
d.
i. Hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe
ii. Kwa kawaida, hutungwa na kughanwa na wanaume.
iii. Hutolewa kwa nafsi ya kwanza kwa sababu anyejigamba ni mshairi mwenye.
iv. Huwa na usanii mkubwa. Anayehusika hutumia mfanano, sitiari na urudiaji.
v. Mhusika hujitungia kivugo kufuatia tukio mahusisi katika maisha yake. Mfano kushinda vita,
mchezo n.k.
vi. Huwa na matumizi ya chuku. Mhusika hujisifu kupita kiasi.
vii. Mhusika huweza kutaja usuli wake wa kina saba . Anahitajika kutaja na kusifu ukoo wake.
viii. Wahusika mara nyingi huwa walumbi au washairi wanaolewa kwa kina wanayoyasema.
6x1=6.
e.
i. Kuridhisha fani yenyewe kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

ii. kuzihifadhii kenye maandishi.


iii. Kuzifunza shuleni.
iv. Kizitamba mara kwa mara.
v. Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wake.
vi. Kuandaa mashindano ya utambaji wa kipera hiki kutoka kizazi hadi kingine.
vii. kuzihifadhi kwenye video ili kuhifadhi sifa za uwasilishaji kama vile sauti. 4x4=4
f.
i. Hukuza ubunifu. Mtu anavyotunga, majigambo mara kwa mara ndivyo anavyoimarisha
uwezo wake wa kubuni mitindo mipya.
ii. Hukuza ufasaha wa lugha. Wahusika wengi huwa walumbi.
iii. Hudumisha utu na utambulisho wa mwanaume katika jamii kupitia mambo mbalimbali
mfano vita.
iv. Ni nyenzo ya kufanya watu waheshimiwe. Hudumisha ari ya kufanya wanaume kutaka
kuwa mashujaa. 4x1=4

FASIHI SIMULIZI SWALI 15

Niaje wazungu wanaweza kutunza vitu vikajaa kwenye friji. Yani nimeweka soda mbili tu kwenye friji lakini
haitulii hadi nizinywe. Niko sebuleni nazunguka tu. Najaribu kuwaza vitu vingine lakini wapi akili
inaniambia “My friend kunywa soda”.

a. Taja na ueleze maana ya kipera hiki (alama 4)


b. Utanzu wa kipera hiki huweza kuchukua nafasi muhimu katika fasihi simulizi. Thibitisha kwa hoja
zozote sita. (alama 6)
c. Ufanisi wa uwasilishaji wa utanzu huu unategemea fanani. Tetea kauli hii. (alama 4)
d. Ni changamoto gani zinaweza kumkabili mwanafasihi nyanjani? (alama 4)
e. Dokeza umuhimu wa kukusanya data nyanjani. (alama 4)

MAJIBU

Niaje wazungu wanaweza kutunza vitu vikajaa kwenye friji. Yani nimeweka soda mbili tu kwenye frijilakini
akili haitulii hadi nizinywe. Niko sebuleni nazungukz tu . Najaribu kuwaza vitu vingine lakini wapi akili
inaniambia ‘’ My friend, kunywa soda”

a. Taja na ueleze maana ya kipera hiki. AL 2


Kichekesho
Ni mchezo mfupi ambao hupitisha ujumbe kwa njia au namna ya kuchekesha.
b. Utanzu wa kipera hiki huweza kuchukua nafasi muhimu katika fasihi simulizi. Thibitisha kwa hoja
zozote sita AL 6
Huburudisha watazamaji na waigizaji wenyewe. Burudani hii mara nyingine
hupumbaza.
Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii kama vile upashaji tohara,
matambiko, majigambo, ngoma, miviga na michezo ya watoto hudumishwa
kupitia maigizo
Ni kitambulisho cha jamii; kila jamii ina Sanaa ya maigizo ya jamii husika. Miviga
na sherehe za arusi na mazishi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
Hukuza umoja na ushirikiano wa watu wanapojumuika kushiriki katika maigizo.
Hao hujitambulisha kama jamii moja.
Ni nyenzo za kupitisha maarifa na amali za jamii kupitia michezo ya jukwaani.
Husawiri mtazamo wa jamii kuhusu masuala mbalimbali kama vile woga, wizi na
usaliti.
Hukuza ubunifu madhalan watoto wanaposhiriki michezo ya watoto, hujifunza
kubuni michezo wakiwa wachanga na pia Sanaa ya uigizaji.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Hukuza kipawa cha uongozi katika michezo, huweza kujifunza stadi za uongozi
Ni njia ya kuimarisha urafiki. Kwa vile mizaha na utani katika malumbano
hukuza urafiki na uhusiano bora
Huongoza jamii kupambana na na mazingira wanamojipata. Kutegemea imani ya
wanajamii,matambiko yanaweza kuondoa matatizo katika jamii kama vile njaa,
ugonjwa na ukame kwa kuomba Mungu
Maigizo huelimisha kupitia maudhui na hulka za waigizaji na kushauri nafsi zao,
kuiga au kukashifu hulka hizo.
c. Ufanisi wa uwasilishaji wa utanzu huu unategenea fanani. Tetea kauli hii. (Alama 4)
Huwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira yake ili kuwafanya wapendezwe na
hadithi
Anafahamu utamaduni wa jamii yake.
Anaifahamu hadhira yake vizuri na kusimulia kulingana na mapendeleo yao.
wasichana au wavulana? vijana au wazee?
Huwa na uwezo wa ufaraguni - uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila
kujifunga na muundo asilia.
Mwenye kumbukumbu nzuri - uwezo wa kukumbuka
Mwenye uwezo wa kuigiza kwa kutumia viungo vyake, uso (ishara-uso) na
sauti(kiimbo)
Mwenye uwezo wa kujenga taharuki kwa kusita kidogo ili kuvuta nadhari ya
hadhira yake.
Hushirikisha hadhira yake katika nyimbo n.k
Mtambaji hodari na mkwasi wa lugha.
d. Ni changamoto gani zinaweza kumkabili mwanafasihi nyanjani?( Alama 3)
Gharama ya utafiti-huenda gharama ikwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu.
Baadhi ya mafanani au wahojiwa huenda wakadai walipwe kabla ya kutoa habari
zozote.hivyo ikiwa mtafiti hana hela basi utafiti wake utakwamizwa.
Mtazamo hasi wa wanajamii kuhusu ujazaji wa hojaji huenda ukawafanya wengi
wao kutojaza hojaji zao. Wanajamii wengine huweza kushuku kwamba mtafiti
anawapeleleza na wakakataa kutoa habari.
Vizingiti vya kidini amabavyo hutokea pale ambapo baadhi ya wahojiwa
wanaamini kwamba matendo ya fasihi simulizi k.v matambiko na uimbaji wa
taarabu yanaenda kinyume na imani yao ya kidini.
Uchache wa wazee au wataalamu wa fasihi simulizi ,kukosekana kwa wazee
wanaoweza kutamba ngano ama kueleza vipera vingine k.v vitendawili.
Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi ikiwa mkusanyaji analazimika kwenda
mbali kukusanya habari,hasa katika sehemu kame itakuwa vigumu iwapo hana
gari.
Ukosefu wa usalama ,huenda mkusanyaji wa fasihi simulizi akavamiwa ,baadhi
ya watu si wakarimu na huenda wakamshuku mtafiti na kuvamiwa.
e. Dokeza umuhimu wa kukusanya data nyanjani. (Alama 3)
Ukusanyaji husaidia kurekodi na kuhifadhi tamaduni za jamii mbalimbali kwa nia
ya kuzipitisha kwa vizazi vijavyo.
Ukusanyaji huiendeleza fasihi simulizi kwa kurekodi vipera vya fasihi simulizi
Husaidia kuziba pengo la utafiti liliopo.
Ukusanyaji zaidi wa data za fasihi simulizi hutumiwa kama kiunzi cha uchunguzi
wa kulinganisha fasihi simulizi za jamii mbalimbali.
Humwezesha mwanafunzi kupata maarifa au stadi za kufanya utafiti katika
taalima nyingine za kijamii kama vile sosholojia.
Humpa mwanafunzi nafasi ya kushuhudia na kuathiriwa moja kwa moja na
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

utendaji wa fasihi simulizi

FASIHI SIMULIZI SWALI 16

a. Watu watatu walikuwa wakivuka mto. Mmoja alivuka pasi kukanyaga maji wala kuyaona.
Wa pili aliyaona maji akayavuka bila kuyakanyaga. Wa watatu aliyaona akayakanyaga
huku akiyavuka.
i. Bainisha kipera cha makala hayo. (alama 1)
ii. Eleza umuhimu wa kipera ulichotaja(i) hapo juu. (alama 4)
b. Fafanua muundo wa mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi. (alama 3)
c. Fafanua sifa za mawaidha. (alama 12)

MAJIBU

a. Watu watatu walikuwa wakivuka mto. Mmoja alivuka pasi kukanyaga maji wala kuyaona.
Wa pili aliyaona maji akayavuka bila kuyakanyaga. Wa watatu aliyaona akayakanyaga
huku akiyavuka.

i. Bainisha kipera cha makala hayo. (alama 1)


Mafumbo/chemsha bongo
ii. Eleza umuhimu wa kipera ulichotaja(i) hapo juu. (alama 4)
Hukuza uwezo na wepesi wa kufikiri
Hustawisha ubunifu
Hukuza maarifa ukabiliana na changamoto na kutumia marafiki kusuluhisha mambo
Huburudisha jamii
Hukuza uhusiano mwema.
b. Fafanua muundo wa mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi. (alama 3)
Utangulizi – Anayetoa mawaidha huanza kwa kauli ya kuvuta makini ya hadhira.
Mf: Sikiliza mwanangu na usikilize kwa makini …..
Mwili: Mawaidha huwasilishwa na kusisitizwa kwa kutumia kauli sisitizi pamoja na tamathali
za usemi kama vile methali.
Wasia, maonyo na maelekezo hutolewa kutegemea lengo.
Hitimisho: Mwasilishaji huonyesha msimamo wake kuhusiana na swala analousia, pia
anaweza kuuliza msimamo wa hadhira yako.
c. Fafanua sifa za mawaidha. (alama 12)
Mawaidha yaweza kutolewa katika miktadha rasmi na isiyokuwa rasmi. Miktadha rasmi ni
kama vile katika harusi, kwenye mazishi nk. Miktadha isiyo rasmi ni kama vile mzazi
anapotoa mawaidha kwa mwanawe.
Mawaidha hutolewa na watu waliopewa jukumu la kutoa mawaidha kama vile wazee na
watu walio na vyeo na waliochukuliwa kuwa na ukima.
Mwenye kutoa mawaidha hulielewa jambo analousia kwa undani.
Mwenye kutoa mawaidha hutumia lugha inayoathiri hisia za wanaousiwa k.v. methali.
Maudhui katika mawaidha ni mapana.
Mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi huwa na muundo maalumu wenye sehemu
tatu. Utangulizi, mwili na Hitimisho.
(hoja 6 x 2 = 12)

FASIHI SIMULIZI SWALI 17

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.


Malaika nakupenda Malaika
Malaika nakupenda Malaika
Nami nifanyeje?
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kijana mwenzio
Nashindwa na mali sina we!
Ningekuoa Malaika

Pesa zasumbua moyo wangu


Pesa zasumbua moyo wangu
Nami nifanyeje?
Kijana mwenzio
Nashindwa na mali sina wee
Ningekuoa Malaika

a. Tambua utungo huu. (alama 1)


b. Thibitisha jibu la (a) . (alama 2)
c. Tambua nafsineni katika utungo huu. (alama 1)
d. Eleza toni inayojitokeza katika utungo huu. (alama 2)
e. Umealikwa kuwasilisha utungo huu mbele ya wanafunzi wa shule yako.Taja mambo sita
utakayozingatia ili kufanikisha uwasilishaji huu. (alama 6)
f. Tambua na uthibitishe shughuli mbili za kijamii zinazojitokeza katika utungo. (alama 2)
g. Taja mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika utungo. (alama 2)
h. Eleza dhima ya utungo wa aina hii katika jamii. (alama 4)

MAJIBU

a. Tambua utungo huu


alama 1
Wimbo wa mapenzi
b. Thibitisha jibu la (a) . alama 2
Anasema anampenda Malaika
Anasema angemuoa Malaika
c. Tambua nafsineni katika utungo huu. Alama 1
mvulana
d. Eleza toni inayojitokeza katika utungo huu. Alama 2
kubembeleza/ kushawishi
e. Umealikwa kuwasilisha utungo huu mbele ya wanafunzi wa shule yako.Taja mambo sita
utakayozingatia ili kufanikisha uwasilishaji huu. Alama 6
I. awe jasiri -aweze kuimba wimbo mbele ya watu bila uoga
II. mbunifu-auimbe wimbo huu kwa njia ya kuvutia ili aondoe ukinaifu /mbinyo
III. atumie ishara za uso , za mwili na miondoka ambayo ianaoana na wimbo wake.
IV. Awe mjuzi wa lugha ya jamii husika
V. Aielewe hadhira yake
VI. Avae maleba yanayooana na wimbo anaoimba
VII. Abadilishe toni na kiimbo kulingana na wimbo wake.
VIII. Ashirikishe hadhira kwa kuuliza maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.
IX. Mfaraguzi-awe na uwezo wa kubadilisha wimbo wake papo hapo.
X. Awe na sauti inayosikia na hadhira yake.
f. Tambua shughuli mbili za kijamii zinazojitokeza katika utungo. (Alama 2)
ndoa – ningekuoa
kulipa mahari – nashindwa na mali sina
(kutaja ½ mfano ½ )
g. Taja tamathali mbiliza usemi zilizotumika katika utungo.alama 2
sitiari-malaika
swali la balagha-Nami nifanyeje?
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Takriri – malaika / nashindwa na mali sina


Nidaa – nashindwa na mali sina wee!
h. Eleza sababu nne utakazowahimiza wanafunzi wenzako wadumishe utungo huu katika
jamii.alama 4
I. Kitambulisho cha jamii
II. Huburudisha
III. Huliwaza
IV. Huhifadhi utamaduni
V. Hurithisha elimu ya jamii
VI. Hukuza lugha
VII. Hukuza ubunifu
VIII. Huadilisha
IX. Huhifadhi hisoria ya jamii
X. Hupumbaza
(Zozote nne =4)

FASIHI SIMULIZI SWALI 18

“Hapo zamani za kale, kale sana kabla ya ujio wa manabii Issa, Musa ama hata Yesu, walimwengu wote
waliishi pamoja kama ndugu na dada. Hakukuwepo haya makabila tunayoyasikia yakitajwa kila siku.
Hakukuwepo na utabaka. Hapakuwepo na maskini. Watu wote waliishi pamoja kama wafanyavyo
wanyama wa familia moja. Hakukuwepo na tofauti na tamaa ya uongozi na kujitakia kwa wananchi.
Ubinafsi.

Mwanadamu alipogundua umoja aliopewa na Mungu wake, alianza kusoma mengi mno na kutaka kujua
mengi kuhusu Mola. Alidhani kwamba Mungu aliishi mbinguni. Hivyo basi, wanadamu wote waliitana
pamoja katika kamkunji; mkutano wa siri, waratibu jinsi wangeweza kumfikia mwenyezi Mungu. Mwisho
wa kikao, walikubaliana kuwa waanze kujenga ukuta mkubwa ambao ungewawezesha kufika juu mbinguni
na kuzungumza moja kwa moja na Mola Mkuu.

Siku iliyofuatia waliingia katika kazi. Huyu alileta jiwe hili na huyu msumari huu. Kazi ilifanywa kwa
kujitolea na jitihada kuu kila mmoja akiamini kuwa atakaye kilicho mvunguni ni sharti ainame. Aidha,
mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Ukuta wao ulipanda kwa kasi. Wazee wenye busara walijaribu
kuwaonya wajenzi dhidi ya hatua hii yao ila wakashikilia msimamo wao wa kutaka kuonana na Muumba
wa mbingu na ardhi ana kwa ana.

Mungu alipoona kuwa mwanadamu amejawa na kiburi, aliwachanganya wajenzi kwa kuzichanganya lugha
zao. Hili liliwanya kutoelewana kiasi kwamba fundi mmoja alipoomba aletewa bisibisi aliletewa nyundo.
Hatimaye ukuta mzima ulianguka na kuwaangamiza wajenzi na waliosalia wakabaki kutoelewana lugha
zao. Hii ndiyo sababu wanadamu wana lugha tofauti.”
Kutoka: Meja S. Bukachi- Mola Mkuu (Riwaya)
Maswali

a. Tambua kipera hiki cha hadithi. (Alama 2) (


b. Wewe ni mtafiti uliye nyanjani kwa uchunguzi zaidi kuhusu kipera hiki:

i. Taja mbinu tatu utakazotumia katika utafiti wako. (Alama 3)


ii. Upi umuhimu wa kukusanya na kuhifadi tungo kama hizi? (Alama 5).
iii. Taja njia tano zinazotumiwa na jamii ya kisasa kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)

MAJIBU

a. Tambua kipera hiki cha hadithi. (Alama 2)


kisasili- inaeleza kuhusu chanzo cha lugha tofauti.
(kutaja 1, kueleza 1)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

b. Wewe ni mtafiti uliye nyanjani kwa uchunguzi zaidi kuhusu kipera hiki:

i. Taja mbinu tatu utakazotumia katika utafiti wako. (Alama 3)


Kusikiliza

Kushiriki

Kurekodi

Kutazama

Kutumia hojaji

Mahojiano
(Zozote 3×1= 3)
ii. Upi umuhimu wa kukusanya na kuhifadi tungo kama hizi? (Alama 5). ⮚]]
Humpa mwanafunzi wa fasihi simulizi nafasi ya kutagusana na jamii
iliyozaa fasihi husika.
Humpa mwanafunzi wa Fasihi Simulizi nafasi ya kushuhudia na kuathiriwa
moja kwa moja na utendaji wa Fasihi Simulizi.

Husaidia kurekodi na kuhifadhi tamaduni za jamii.

Huiendeleza Fasihi Simulizi.

Husaidia kuziba pengo la utafiti lililopo.

Hutumiwa kama kiunzi cha uchanganuzi wa kiulinganishi wa Fasihi


Simulizi za jamii mbalimbali.

Humwezesha mwanafunzi wa Fasihi Simulizi kupata maarifa ya fasihi.

Husaidia kurekebisha mawazo potovu kuhusu suala fulani. (Zozote


5×1= 5)
iii. Taja njia tano zinazotumiwa na jamii ya kisasa kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)
Tamasha za muziki.

Sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko zipo.

Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.

Michezo ya kuigiza katika runinga, redio.


Tamasha za drama huendeleza utanzu wa maigizo.
Sarakasi zinazofanywa na wasanii.

Ngoma za kienyeji kama Isukuti huchezwa katika hafla mbalimbali.


Watafiti wanaendeleza utafiti kuhusu Fasihi Simulizi.
Utambaji wa hadithi bado hufanyika.
(Zozote 5×1= 5)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

FASIHI SIMULIZI SWALI 19

a. Eleza maana ya miviga. (alama.2)


b. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
c. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
d. Fafanua vigezo sita vinavyotumiwa kuainisha methali. (alama.6)
e. Jadili mambo manne ambayo huzingatiwa katika katika uchambuzi wa hadithi. (alama.4)

MAJIBU

a. Eleza maana ya miviga. (alama.2)

Ni sherehe za kitamaduni amabazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum cha
mwaka (1x2)
b. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
Huandamana na matendo Fulani – kama vile kupiga magoti, kunyolewa. n.k
Huongozwa na watu mahususi katika jamii.
Huandamana na utoaji mawaidha / ulumbi.
Maleba huvaliwa na wanaohusika.
Hufanyiwa katika mazingizira maalum.
Huambatana / Hufungamana na utamaduni wa jamii husika.
Hufanywa wakati wa kipindi maalum / wakati maalum.
Huwa na kutolewa kafara.
Huwa na kutolewa sadaka.
Kuna kula kiapo – wahusika huweka ahadi ya kutenda wema.
c. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
Udhaifu katika miviga
Husababisha kudorora kwa maendeleo.
Huleta utengano kati ya jamii na majirani.
Huasi mabadiliko ya kiwakati (nyingine zimepitwa na wakati.
Madhara yanaweza kutokea hasa vifaa butu vinapotumika.
Huleta utengano wa kujinsia kumtukuza mwanaume na kumduinisha mwanamke. ( zozote
3x1)
d. Fafanua vigezo sita vinavyotumiwa kuainisha methali. (alama.6)
Mandhari / mazingira – ukipanda pantosha , utavuna pankwisha.
Maudhui – ulezi – samaki mkunje angalia mbichi.
Fani / tamathali za usemi – Takriri haba na haba hujaza kibaba.
Jukumu – Kuonya – Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.
Maana sawa – pole pole ndio mwendo -haraka haraka haina baraka.
Abjadi – Kupangwa kialfabeti zote zinazoanza na harufi A zinawekwa pamoja hadi Z.
(zozote 6x1)
e. Jadili mambo manne ambayo huzingatiwa katika katika uchambuzi wa hadithi. (alama.4)
Ujumbe. - Hadhira
Msuko/ ploti. - Fanani
Dhamira. - Kubainisha umuhimu wa formyula ya kufungua na
Wahusika. Kufunga hadithi.
Ugiligili
Tamathali za semi.

FASIHI SIMULIZI SWALI 20

a. Ulumbi ni nini? (alama 2)


Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

b. Eleza sifa za mlumbi(alama 6)


c. Fafanua aina zozote sita za wahusika katika Fasihi Simulizi.(alama 6)
d. Taja mambo ambayo huzingatiwa kufanikisha uwasilishaji wa ngano katika Fasihi Simulizi.(alama
6)

MAJIBU

a. Ulumbi ni nini? (alama 2)


Ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.
b. Eleza sifa za mlumbi(alama 6)
Mkamamavu
Mcheshi
Mwenye kumbukumbu nzuri
Mbunifu
Mwenye kuielewa hadhira
Mwenye ufasha wa lugha
Mfaraguzi
Mwenye kuelewa mazingira ya hadhira yake
Mwenye uwezo wa kushirikisha hadhira
Mbaraza
(Mwanafunzi asitaje hoja tu-aelezee)(alama 8)
c. Fafanua aina zozote sita za wahusika katika Fasihi Simulizi.(alama 6)
Fanani-anayetunga na kuwasilisha Fasihi Simulizi
Hadhira-kusiliza , kutazama , kushiriki kwa kuimba, kuuliza maswali, kutegua
vitendawili, kupiga makofi nk.-kuna hadhira tui na hai
Wanyama wanofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja
,ulaghai, tama na ujinga na kuna wale wanaobakia wanyama tu.
Binadamu
Mazimwi na majitu-viumbe wenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile
jicho kubwa moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu mnyama wenye tama
liyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu
anayewapendeza.
Wahusika vitu visivyo na uhai kama mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa
kuibua imani za kidini za jamii husika.
Mizimu-roho za waliokufa ambao hutembea na huathiri binadamu
Miungu-viumbe wenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu na hutumika sana
katika mighani na visasili
Swali funge=za kwanza 6*1=6
d. Taja mambo ambayo huzingatiwa kufanikisha uwasilishaji wa ngano katika Fasihi Simulizi.(alama
6)
Lazima kuwe na fanani
Kuwe na hadhira
Pawepo na ngano yenyewe ya kughanwa
Pawe na pahali pa kuaghania ngano yenyewe
Mganaji awe na uwezo wa kuiteka makini ya hadhira kutoka ulimwengu halisi
hadi wa kubuni
Fanani awe na uwezo wa kuishirikisha hadhira wakati wote wa usimulizi ili
kuondoa ukinaifu
Kiimbo-aweze kupandisha nakushikisha sauti ili kuibua hisia tofauti tofauti
Awe mfaraguzi
Awe jasiri wa kuweza kusimulia hadithi yake bila uoga
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Zozote6*1= 6

FASIHI SIMULIZI SWALI 21

a. Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)


b. Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
c. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
d. Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)
i. Matambiko
ii. pembezi
iii. Misimu
e. Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

MAJIBU

a.
mbunifu – awe na uwezo wa kuwasilisha hadithi kwa namna ya kuwachangamsha. Abuni
hadithi upya mara tu anapoitamba.
Afahamu lugha- Awe na ufahamu mpana wa lugha husika na utamaduni unaohusika ili
awasilishe vyema ngano yake.
Afahamu hadhira yake na mahitaji yao- wake , waume, watoto, vijana, nk . apatane vyema
na mazingira yake ya kisimulizi.
Mcheshi- ili kuinasa makini ya hadhira yake.
uwezo wa ufaraguzi na afahamu mbinu zifaazo za sanaa na maonyesho – uwezo wa
kuunda, kugeuza na kuwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo hapo.
Afahamu tabia za binadamu- mambo yanayofurahisha, kuudhi, kuchangamsha, kuvutia au
kumpendeza. Pia wafahamu mikondo mbalimbali ya jamii.
Sauti yake isikike na ibadilike ipasavyo.
Ashirikishe hadhira yake- anaweza kuwauliza maswali, waimbe nyimbo nk
Jasiri – aweze kuzungumza hadharani bila haya hasa masuala ya aibu.
Afahamu utamaduni wa hadhira yake ili atoe ujumbe kwa njia inayokubalika na hadhira na
asije akatumia ishara au maneno yasiyokubalika pale.
b.
Zingine hazina faida yoyote
Zingine zaweza kusifu tamaduni zinazodhalilisha watu fulani
Zaweza kuleta utengano kati ya majirani hasa zile zinahifadhi siri
Zaweza kuleta matabaka
Zingine huenda kinyume na mabadiliko ya wakati. Baadhi ya matendo wakati wa matanga
na unyago yamepitwa na wakati.
Huweza kusababisha tofauti ya kijinsia kv jando na ndoa kwani humdhalilisha mwanamke
na kumtukuza zaidi mwanamume.
Ina gharama – mavazi, chakula, zawadi,nk
Baadhi hujaza hofu.
c.
i. Maandalizi_ mada ya utafiti, mawanda ya utafiti, walengwa, kipindi cha utafiti, kibali, mbinu
za kukusanya na kuhifadhi na gharama ya utafiti.
ii. Utafiti na ukusanyaji wa data yenyewe. Kuhusisha mbinu mbalimbali kama vile kuhoji,
hojaji, kushuhudia au kujaza fomu.
iii. Kurekodi data kwa kuandika- kunasa habari ama kupiga picha za kawaida ama video au
zote tatu.
iv. Kuchunguza data – ili kutafsiri na kuandika upya neno kwa neno bila kupotosha maana
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

halisi ya lugha asili.


v. Kuchambua/ kuchanganua na kufasiri data ili kupata matokeo kamili ya utafiti na
mapendekezo.
d.
i. Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu
kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame,
magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na
uwezo.
ii. Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo
katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri,
waganga, nk
iii. Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano
baina ya wanakikundi hicho./ Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu
kutegemea mazingira maalum./ Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira
fulani na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale.
e.
Hutolewa kwa watu waliotenda kinyume na matarajio ya jamii zao.
Baadhi yalitolewa kabla ya ulaji wa viapo.
Yanaweza kutolewa moja kwa moja na aliyeathirika.
Huaminiwa yanaleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa kuyaepuka kwa
kutenda mema.
Hutumia lugha fasaha na mtoaji kwa kawaida huwa mlumbi.
Hutumia lugha kali ya kuonya na kujaza woga ili watu waache maovu.

FASIHI SIMULIZI SWALI 22

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

a. A: Kumbe mambo yenyewe rahisi hivi?


B: Rahisi, lakini usije ukabakwa tena
A: Hapana, safari hii itakuwa zamu yako. (Alimrudishia … huku akichekacheka)
C: Hapajaharibika mambo mama’ngu. Kwani la ajabu lipi? Sasa miye namsubiri Bakari mpya tu,
hichi kikongwe nikipe talaka.(Akitabasamu)
D: Haachwi mtu hapa. Tutabanana humo humo. Yeye atakuwa mke mdogo na mimi mkubwa.

i. Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 1)


ii. Toa sababu mbili kuthibitisha jibu lako la (i) hapo juu. (alama 2)
iii. Eleza manufaa saba ambayo jamii hunufaika nayo kwa kushiriki katika kipera hiki. (alama
7)
b. Soma kifungu ufuatao kisha ujibu maswali.

Siwezi kuhutubu. Mimi sikuwafundisha ubaguzi. Kwa nini mnabaguana? Kwa nini hamukuwapa
watu wa matabaka yote nafasi ya kuzungumza? Kwa nini? Kwa nini mnafanya hali hii ya kuwa kuna
watu na nusu watu? Nataka wazungumze wale ambao hawata sifu tu.
i. Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 2)
ii. Eleza mitindo mitatu katika kifungu hiki. (alama 3)
iii. Eleza majukumu matano ya kipera hiki katika jamii. (alama 5)

MAJIBU

a.
i. Kipera cha utungo
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Utani. Alama 1×1=1


ii. Anamtania mwenzake kuwa ni zamu yake ya kubakwa.
Anamtania mkewe kuwa atamtaliki. Alama 2×1=2
iii. Manufaa ya kushiriki katika kipera hiki.
Hupunguza urasimi miongoni mwawa jamii.
Huimarisha urafiki- waliona uhusiano mwema ndio hutaniana.
Hukuza utangamano miongoni mwa jinsia/tabaka/kabila wanapotaniana.
Hutambulisha Imani/mila/tamaduni ya jamii kwa kutaja sifa zake. Kupeana talaka
na kuwa na wake wawili.
Kukosoa/ kukashifu tabia hasi katika jamii mfano ubakaji.
Huburudisha kutokana na ucheshi katika malumbano ya utani.
Utani hutoaa maarifa ya kukabiliana na hali mbalibali katika maisha.
Alama 7×1=7
b.
i. Kipera cha utungo
Mawaidha- Alama 1×2=2
ii. Mitindo mitatu Alama 1x3
Balagha- kwa nini mnabaguana?
Takriri- kwa nini
Taswira- watu na nusu watu
Jazanda- tofauti za kitabaka
iii. Majukumu matano ya kipera hiki.
Kuelekeza /kutoa mwongozo wa jinsi ya kukabiliana na matatizo/jinsi ya kutenda
jambo.
Kuwapa wanajamii maarifa kuhusu majukumu yao ya kijamii na matarajio ya jamii
kwao.
Kujifunza maadili yanayoambatana na itikadi za jamii.
Kutambulisha jamii kwani mawaidha hutolewa kulingana na mila,desturi na itikadi
za jamii.
Kusuta na kukashifu tabia hasi katika jamii kwa mfano ubabuzi. Alama 5×1=5

FASIHI SIMULIZI SWALI 23

a. Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)


b. Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
c. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
d. Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)

i. Matambiko
ii. pembezi
iii. Misimu
e. Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

FASIHI SIMULIZI SWALI 24

Soma maigizo yafuatayo kisha ujibu maswali


MSAKATONGE: Limekucha sasa jua, nimetoka gizani, Haki zangu nazijua, tasema nataka nini, Mzigo huu
najitua, siumbuki mwako kondeni, Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Hayo unayoyanena, hapa hayatakikani,
Ni hatia kubwa sana, kabisa iso kifani,
Mambo yaso na maana, kayasikia na nani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
MSAKATONGE: Malipo ninayopata, sio pesa ni mapeni,
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Maisha yangu ni mwata, hayaniishi madeni,


Shida zinaniambata, kwa wangu umaskini,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea
Nitazame mwili wangu, sinayo siha mwilini,
Haitoshi kula yangu, kwa kuwa sina mapeni,
Ni mararu nguo zangu, nachekwa kiwa njiani,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Uchumi ‘meharibika, kote kote duniani,
Hata huko Amerika, walia nifanye nini,
Kuache kulalamika, uchangamke kazini,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
Utaweza kuushika, uvuvi dhiki majini?
Mararu kujifunika, si fedheha mwafulani,
Mradi wanufaika na malipo hatimani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
MSAKATONGE: Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
Silioni lenye heri, kwa nguvu za muilini,
Inaniandama shari, nyumbani hata kazini,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Basi tuache hasira, isiongoze njiani,
Tuitumie busara, tuketi hizi thenini,
Bila hata ya papara, tupime kwenye mizani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.

1. Bainisha kipera cha maigizo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama 4)
2. Eleza ujumbe wa maigizo uliyoyasoma hapo juu. (alama 4)
3. Eleza shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)
4. Wewe ni mwigizaji wa michezo jukwaani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika
uwasilishaji wako. (alama 5)
5. Unanuia kutumia mbinu ya kuchunza/ utazamaji kukusanya habari kuhusu miviga ya tohara. Eleza
manufaa manne ya kutumia mbinu hii. (alama 4)

MAJIBU

a. Bainisha lipera cha maigizo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama 4)
Ngonjera
Kujibizana kwa wahusika wawili
Wahusika kupingana mwanzoni.
Wahusika hufikia uafikiano kufikia mwisho.
Mhusika mmoja huzua jambo na mwingine hujibu.
Huendelezwa kwa njia ya ushairi.
Kipera = 1. Ithibati 3x1 =3
b. Eleza ujumbe wa maigizo uliyoyasoma hapo juu. (alama 4)
Mwajiriwa amezinduka, anazifahamu haki zake na kuzitetea.
Mwajiri anaghairi kusikiliza malalamishi ya mwajiriwa - unayoyanena, hapa hayatakikani
Mwajiriwa anapata mshahara duni ambao unaendelea kuyaza umaskini wake.
Uchumi umeharibika kote kote duniani
Kugomea kzi ni kujitosa taabani - mahitaji utayakosa.
Njia mojawapo ya waajiriwa kupigania haki zao ni kugoma / kususia kazi.
Mwajiriwa anapitia dhuluma kiwandani - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
Mwajiriwa ni mvumilivu - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
Basi tuache hasira, isiongoze njiani,
Mwajiri na mwajiriwawawache na watumie busara, kusuluhisha tofauti zao bila papara.
4x1 =4
c. Eleza shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kilimo-siumbuki mwako kondeni,


Uvuvi - Utaweza kuushika, uvuvi dhiki majini?
Viwanda - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
3x1 =3
d. Wewe ni mwigizaji wa michezo jukwaani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika
uwasilishaji wako kifungu. (alama 5)
i. Kuzungumza moja kwa moja na hadhira - mjukuu wangu sijui kama umewahi kuwazia
ii. Kujenga taswira zinazoweza kutambulika na hadhira. - kutetemeka kama kondoo/shikwa na
mtapo
iii. Kushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali - ungekuwa Msakatonge ungefanya nini?
iv. Matumizi ya lugha sahili
v. Taharuki / lugha inayojenga taharuki.
vi. Kujivika maleba yanayooana na kinachoigizwa ili kutia uhai maigizo.
vii. Matayarisho kabambe kabla ya maigizo.
viii. Lugha yenye ufundi wa juu kama vile picha, mafumbo na tamathali za usemi
ix. Matumizi ya ishara na viziada lugha
x. Udramatishaji kwa kucheza na kadhalika
Za kwanza 5x1 = 5
e. Unanuia kutumia tabinu ya kuchunza / utazamaji kukusanya habari kuhusu miviga ya tohara. Eieza
manufaa manne ya kutumia mbinu hii. (alama 4)
a. Kupata habari za kuiegemewa na kuaminika.
b. Ni rahisi kuzek ai kama vile kwa vinasa sauti, video na kadhalika.
c. Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
d. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji kama vile. toni/kiimbo, ishara na kadhalika.
e. Kuweza kupatsie Salisi za uwasilishaji.
Za kwanza 4x1 =4

FASIHI SIMULIZI SWALI 25

a. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)


b. Eleza kwa hoja tano, umuhimu wa kushiriki kama njia ya kukusanya data (alama 5)
c. Kikundi cha Tamasha Bora kiliwasilisha maigizo katika ukumbi wa shule yenu. Fafanua kwa hoja
tano sababu za uwasilishi wao kufanikiwa. (alama 5)
d. Eleza msamiati ufuatao (alama 5)

i. ulumbi
ii. mbazi
iii. lakabu
iv. matambiko
v. rara nafsi

MAJIBU

a. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)


Maandalizi
Utafiti na ukusanyaji data
Rekodi ya data
Kuchunguza data na kunakili ili kuchanganua baadaye
Uchanganuzi na kufasiri data.
1×5=5
b.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kupata habari za kuaminika


Njia bora kwa wasiojua kusoma
Rahisi mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera
Mtafiti anaweza kunakili anayotazama au kusikiliza na hivyo kuhifadhi kiimbo, toni na
ishara.
Mtafiti anaweza kuthibitisha aliyokusanya
Kushiriki hukuza utangamano
Zozote 5×1=5
c. Ujasiri wa waigizaji
Ubunifu wa waigizaji - kutumia mbinu mbalimbalu ili kufanya uihizaji kuvutia
Ujuzi wa kutumia ishara za uso,mwili na miondoko inayooana na yanayoigizwa
Ujuzi na ufasaha wa lugha na waigizaji
Kuielewa hadhira na kubadili mtindo ipasavyo
Matumizi ya maleba mwafaka
Kushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali
Kuelewa utamaduni wa hadhira
Ufaraguzi wa wahusika
Zozote 5×1=5
i. Ulumbi
Uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee/ utumiaji lugha kwa mvuto wa
kipekee
ii. Mbazi
Hadithi fupi yenye mafunzo na inayotolewa kama kielelezo wakati wa kumkanya au
kumwelekeza mtu.
iii. Lakabu
Jina la msimbo/kupanga ambalo mtu hujibandika au hubandikwa kutokana na sifa
zake za kimaumbile, kitabaka, kitabia au kimatendo
iv. Matambiko
Sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu moja
kwa moja ili kutatua matatizo ya kijamii ama kwa shukrani.
v. Rara nafsi
Ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake
mwenyewe
1×5=

FASIHI SIMULIZI SWALI 26

Malaika …..
Nakupenda malaika x 2
Ningekuoa mali we…..
Ningekuoa dada…..
Nashindwa na mali sina we…..
Ningekuoa malaika x 2
Pesa, zasumbua roho yangu x 2
Nami nifanyeje, kijana mwenzio
Nashindwa na mali sina we
Ningekuoa malaika x 2

i. Tambua utungo huu. (alama 2)


ii. Toa sababu za jibu lako hapo juu (alama 2)
iii. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi inayodokezwa kwenye kipera hiki. (alama 2)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

iv. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa. (alama 2)


v. Jadili vipi mwasilishji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake.(alama 6)
vi. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumbuka mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani? (alama 6)

MAJIBU

i. Tambua utungo huu. (alama 2)


Wimbo au
Wimbo wa mapenzi
(Hoja 1x2=alama2)
ii. Toa sababu za jibu lako hapo juu (alama 2)
i. Matumizi ya lugha ya mkato na ya kuvuta: mali we…
ii. Urudiaji wa vipande: ningekuoa malaika x2
iii. Uwepo wa beti
iv. Kuna kiitikio
(Zozote 2x2=alama 4)
iii. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi inayodokezwa kwenye kipera hiki. (alama 2)
i. Shughuli ya kijamii: kuoa/ndoa
ii. Shughuli ya kiuchumi: ulipaji mahari
(Zote 2x1=alama 2)
iv. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa. (alama 2)
Nafsineni: kijana anayetaka kuoa
Nafsinenewa: msichana anayechumbiwa.
v. Jadili vipi mwasilishaji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake.(alama 6)
vi. Kupandisha na kushusha sauti;
vii. Matumizi ya viziada lugha;
viii. Uwa mfaraguzi;
ix. Kubadilisha kiimbo na toni kulingana na hali;
x. Awe jasiri ili aweze kuimba bila aibu;atumie maleba yafaayo kuwasilisha ujumbe
(zozote 3x2=alama 6)
xi. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumbuka mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani? (alama 6)
i. Gharama za utafiti ni ghali, mfano kununua vifaa kama tepurekoa;
ii. Kupotea au kufisidiwa vifaa vya kuhifahi data;
iii. Ukosefu wa wakati wa kutosha wa kufanyia utafiti;
iv. Vikwazo kutoka kwa watawala – kunyimwa nafasi;
v. Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi – magari;
vi. Matatizo ya kibinafsi mfano kushinwa kudhibiti wahojiwa;
vii. Ukosefu wa usalama, mfano kuvamiwa.
(zozote 2x3 = alama 6)

FASIHI SIMULIZI SWALI 27

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Mabibi na mabwana, ndugu na marafiki hamjambo! Nimefika hapa leo kushuhudia sherehe za vijana hao
wanaofuzu kuingia utu uzimani. Tangu jadi mababu zetu waliandaa sherehe kama hizi ili kuwaandaa
vijana wao kukabiliana na maisha ya usoni. Wanangu, utu uzima hautokani tu na viviga au kisu cha
ngariba. Ni matendo na tabia. Naam, ni matendo na tabia. Katika jamii ya sasa watu humpima mtu
kutokana na ufanifu wake kiuchumi, kielimu na kijamii. Mtu asiye na mali yake hubezwa kwa kutofanya
bidii inavyostahili. Hivyo basi, nawashauri vijana wanaofuzu leo kuwa, mnafaa kutia bidii masomoni ili
mustakabali wenu uwe mzuri. Katika nyakati zetu, ubingwa wetu ulipimwa katika fani ya vita na ngoma.
Ungewasikia wanaume wakijisifu kwa wimbo wakisema:
Ooh ooh ooh!
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Mimi ni chuma inayoishi


Ningiapo vitani, macho yangu tu huwafisha wengi.
Viganja vyangu vimeiletea jamii yetu fahari
Wananiita Ngao.
Juzi ngomani niliwapiku wote
Wanawali waliniangukia kwa kutaka uchumba
Nani mwingine kama Ngao?

Hata hivyo, hali katika jamii ya sasa ni tofauti. Ngoma imekuwa nyenzo ya burudani tu. Navyo vita vya
kikabila vimepitwa na wakati. Wanaopigana aghalabu huchukiliwa hatua kali za kisheria. Elimu ni silaha ya
pekee. Elimu itawafungulia milango ya heri. Ndugu na marafiki, nawaomba nyote muwasisitizie vijana hao
umuhimu wa kuwatii walimu wao na kutia bidii masomoni watakaporudi shuleni. Msisite kuwaadhibu
wanapokosea. Ni muhimu kukumbuka kuwa, mchelea mwana kulia hulia mwenyewe. Tulisimuliwa na bibi
kuwa, hapo zamani za kale mwanamke fulani alificha mnyama hatari aliyekuwa akifukuzwa na mashujaa
wa jamii. Baada ya mashujaa hao kuondoka, mnyama huyo alimla mwanamke huyo. Ingawa ni hadithi,
kisa hicho kinatufunzwa kuwa, hatufai kuficha matendo mabaya ya wanetu. Tuwarekebishe mapema.
Nikimaliza naomba kuwajuza vijana hawa kuwa, tohara siyo ufunguo wa ulevi. Inahuzunisha kuwakuta
vijana wadogo wamelala matopeni kwa kushindwa kutembea kutokana na ulevi. Wengine hubaki pale hadi
asubuhi wakitumbuizwa na milio ya vyura. Nina matumaini kuwa, kundi hili litakuwa tofauti. Asanteni kwa
kunisikiliza.
Maswali

i. Tambua kipera katika dondoo. (alama 1)


ii. Eleza sifa za kipera ulichotaja katika (i) (alama 4)
iii. Eleza dhima zozote mbili za kipera ulichotaja katika (i) (alama 2)
iv. Tanzu za fasihi huingiliana na kutegemeana. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu hiki. (alama
5)
v. Eleza toni iliyobainika katika kifungu. (alama 2)
vi. Fafanua mbinu za kimtindo zinazodhihirika katika kifungu hiki. (alama 6)

MAJIBU

i. Tambua kipera katika dondoo. (alama 1)


hotuba
ii. Eleza sifa za kipera ulichotaja katika (i) (alama 4)
a. Hutolewa na watu maalum walioteuliwa kuzungumza.
b. Watu wanaotoa hotuba aghalabu huwa na umilisi mkubwa wa lugha.
c. Hotolewa kwa nafsi ya kwanza.
d. Mtoaji hotuba anaweza kutumia viziada lugha kama vile ishara za mikono.
e. Hotuba huteuliwa mada mahususi wala haizungumzii jambo lolote.
Zozote 4 x 1 = 4
iii. Eleza dhima zozote mbili za kipera ulichotaja katika (i) (alama 2)
a. Kuwaelimisha wanajamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na maisha.
b. Kuadilisha na kutoa nasaha hadharani.
c. Huimarisha ukakamavu wa kuzungumza kadiri watu wanavyotoa hotuba hadharani.
d. Kukuza ufasaha na umilisi wa lugha.
e. Kupalilia kipawa cha uongozi. Zozote 2 x 2 = 2
iv. Tanzu za fasihi huingiliana na kutegemeana. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu hiki. (alama
6)
Kifungu hiki ni cha hotuba. Hata hivyo, hotuba yenyewe imejumuisha tanzu nyingine za fasihi
simulizi kama vile:
a. Kuna matumizi wa nyimbo – wimbo uliotumika unaonyesha jinsi watu walivyojisifu kwa
uhodari wao vitani na ngomani.
b. Hadithi – hadithi inayohusu mwanamke na nyama inarejelewa.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

c. Semi – kifungu hiki kimejumuisha methali na nahau. Kwa mfano, mchelea mwana kulia
hulia mwenyewe.
d. Miviga – msimulizi anadokeza kuhusu tohara kwa vijana kwa kutaja kisu cha ngariba.
Zozote 3 x 2 = 6
v. Eleza toni iliyobainika katika kifungu. (alama 2)
Toni ya kushauri – nafsi neni anawashauri vijana waliopashwa tohari na walezi wao.
Kutaja 1, kueleza 1
vi. Fafanua mbinu za kimtindo zinazodhihirika katika kifungu hiki. (alama 5)
a. Methali – mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
b. Nahau – kutia bidii
c. Mbinu rejeshi – nafsi neni anarejelea simulizi ya bibi.
d. Takriri – ni matendo na tabia
e. Taswira – vijana wadogo wamelala matopeni; wakitumbuizwa na milio ya vyura
f. Tashihisi – elimu itawafungulia milango ya heri
g. Sitiari – elimu ni silaha ya pekee
Zozote 5 x 1 = 5

FASIHI SIMULIZI SWALI 28

Hamkuona jinsi tulivyowapiga magoli


Hamkuona vile tuliwala chenga kila mara
Itakuwaje timu mbovu kama hii
Kuchezea miamba kama sisi
Niliwafunga baada ya sekunde wakati ule nitashindwaje leo?
Maswali

a. Tambua kipera kinachodokezwa na maelezo haya na ukifafanue (al 2)


b. Fafanua umuhimu wa kipera cha fasihi ulichotambua katika (a) (al 8)
c. Fafanua sifa zozote tano za mawaidha (al 5)
d. Ni changamoto zipi zinazoweza kumkumba mtafiti akifanya utafiti wa soga nyanjani(al 5)

MAJIBU

a. Majigambo
Kipera hiki kinahusisha mhusika akijigamba kuhusu timu yake ambayo anaisifu kwa kufunga kwa
sekunde (1x2)
b. Umuhimu
Hukuza ubunifu.kadiri mtu anavyotunga na kughani ndivyo anyokuwa mahiri
Hukuza ufasaha wa lugha. Watunzi wengi wa majigambo huwa walumbi
Ni nyenzo ya burudani. Huongoa wanaokuja kwa sherehe
Hudumisha utu na utambulisho wa wanaume katika jamii
Hufanya watuwaheshimiwe katika jamii
Huhifadhi na kuendeleza Amani turathi na utamanduni wa jamii.
Kitambulisho cha jamii.
(zozote 1x8)
c. Sifa za soga
Huwasilishwa mbele ya watu
Hugusia takriban vipengele vyote vya maisha ya binadamu
Huibua maadili yanayohitaji kuzingatiwa
Hujenga maudhui maalumu na ya aina nyingi kutegemea jinsia umri
Hutumia lugha ya kuathiri hisia
Aghalabu hutolewa na watu wenye umri mkubwa
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Hutolewa katika miktadha rasimu au iso rasimu


Huwa na ufasaha mkubwa wa lugha (alama 5)
d. Changamoto za utafiti nyanjani.
Miundo misingi.
Mawasiliano ya lugha/utofauti wa lugha
Mtazamo hasi wa jamii husia.
Ukeosefu wa usalama.
Wahojiwa kudai kulipwa.
Miundo misingi.
Vizingitti vya kididni.
Mwalimu ahakiki.(zozote 1x5)

FASIHI SIMULIZI SWALI 29

a. Wewe ni mwigizaji wa michezo ya jukwaani. Eleza mambo sita ambayo utazingatia ili kufanikisha
uigizaji wako. (alama 6)
b. Mbinu ya uigaji sauti ina umuhimu gani katika fasihi simulizi: (alama 4)
c. Soma utungo ufuatayo kisha ujibu maswali. (alama 10)
Mwananguuu , ni wewe kweli !
ndimi niliyekupa uhai mwana unoringia,
Anokufanya upite ukinitemea mate,
Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,
Miungu na waone uchungu wangu,
Radhi zao wasiwahi kukupa
Laana wakumiminie,
Uje kuzaliwa mara mia na wanao,
Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,
Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,
Wakazamwanao wasikuuguze katika utu uzimawake
(kutoka – Fani ya Fasihi Simulizi)
Maswali
i. Tambua kipera hiki cha Fasihi simulizi (alama 1)
ii. Eleza sifa zozote nne za kipera hiki cha Fasihi Simulizi (alama 4)
iii. Eleza kwa kutoa ithibati jinsia ya nafsineni? (alama 1)
iv. Fafanua umuhimu wa kipera ulichokitaja hapo juu katika jamii.(alama 4)

MAJIBU

a. Mambo ya kuzingatia kufanikisha uigizaji.


Nitakuwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira ili kuwafanya wapendezwe na miagizo.
Nitahakikisha nimeufahamu utamaduni wa jamii.
Nitapania kufahamu hadhira yangu pamoja na mahitaji yao.
Nitapanua kufahamu hadhira yangu pamoja na mahitaji yao.
Nitatumia ufaraguzi – uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga kwenye
muundo asilia.
Kumbukumbu nzuri – uwezo wa kukumbuka
Nitabadilisha kiimbo kulingana na mahitaji
Kutumia viziada lugha k.v ishara za uso , ishara za mikono na miondoko mbalimbali.
Nitainjenga taharuki kwa mtuo wa kidrama ili kuvuta nadhari ya hadhiri yangu
Nitaishirikisha hadhira yangu kwa njia mbali mbali k.v uigizaji wa sehemu fulani nyimbo
n.k.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Nitaitumia lugha kwa uhodari ili kuipa mvuto.


Nitavalia maleba yenye kuonna na nafasi ninayoigiza.
Nitajenga miahaka mwema na hadhira yangu. (zozote 6 x 1 = 6)
b. Umuhimu wa uigaji sauti
Kuburudisha
Kusawiti uhalisia
Kumakinisha hadhira
Kusisitiza matendo.
c.
i. Tambua kipera hiki cha fasihi simulizi (alama 2)
Maapizo- miungu na wakuone/ laana wakumiminie (1×2= 2)
Kutaja al 1- kufafanua al 1
ii. Jinsia ya nafsi neni ni gani? (alama 2)
Mwanamke/ jinsia ya kike- ndimi nilompa uhai mwana unoringia (1×2= 2)
Kutaja al 1- kufafanua al 1
iii. Eleza sifa zozote sita za kipera hiki cha fasihi simulizi (alama 6)
Maapizo yalitolewa kwa watu ambao walienda kinyume na maagizo ya jamii zao; wabakaji,
waliowatusi wazazi wazee na wengineo.
Katika baadhi ya jamii za Kiafrika, maapizo yalitolewa kabla ya ulaji wa kiapo.
Maapizo yanaweza kutolewa moja kwa moja na yule aliyeathirika.
Kidini, Mungu, miungu au mizimu huweza kutoa maapizo kuhusu mustakali wa mtu fulani.
Maapizo huaminiwa kuwa yataleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa
kuyaepuka kwa kutenda mema.
Maapizo hutumia lugha fasaha. Lugha ya ulumbi.
Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kujaza woga ili kuonya dhidi ya maovu.
iv. Fafanua umuhimu wa kipera ulichokitaja hapo juu katika jamii (alama 4)
Hutumiwa kama nyenzo ya kuwaonya wanajamii dhidi ya matendo hasi.
Hutambulisha jamii. Kila jamii ina namna yake ya kuapiza.
Hukuza umoja katika jamii. Kuwapo kwa kaida na miiko sawa huwafanya watu kujihisi kuwa
kitu kimoja.
Huadilisha. Wanajamii hujifunza kutenda mema ili kuepuka laana. (4×1= 4)
Mtahiniwa afafanue hoja zake ili zilingane na kipera cha maapizo.
v. Fafanua njia sita jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi (alama 6)
Wanafunzi hukariri, hughani na kuimba mashairi katika tamasha za muziki.
Mawaidha na vipera vingine vya fasihi simulizi hupitishwa katika sherehe za harusi, jando,
mazishi na matambiko.

FASIHI SIMULIZI SWALI 30

a. Taja aina mbili za Fasihi ( alama 2)


b. kwa kutolea hoja nane Tofautisha kati ya Fasihi ulizotaja hapo juu. ( alama 8)
c. (Eleza maana ya Mighani. ( alama 2)
d. Jadili umuhimu wa mighani. ( alama 8)

MAJIBU

a. Taja aina mbili za Fasihi ( alama 2)

Fasihi simulizi
Fasihi andishi
b. kwa kutolea hoja nane Tofautisha kati ya Fasihi ulizotaja hapo juu. ( alama 8)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia
ya maandishi.
Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na
majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi
andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara,
nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi
hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe
mbele ya hadhira.
Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi
andishi haina mahali maalum.
Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi
haiandamani na shughuli ya kitamaduni.
Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m.
semi, maigambo.
Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali
fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha
ya binadamu
Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali
andishi haina wakati maalum.
c. Eleza maana ya Mighani. ( alama 2)
Hadithi za mashujaa/majagina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa
Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wakamba.
d. Jadili umuhimu wa mighani. ( alama 8)

Huhusu mashujaa wa jamii fulani.


Wahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maadui.
Wahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika
kivuli, nguvu katika nywele, kutoulika n.k.
Wahusika hupigania haki za wanyonge.
Mhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maadui.
Mhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu k.v. mwanamke au
jamaa zao.
Mashujaa huuliwa kwa njia ya ajabu kama vile kunyolewa nywele, kivuli kuchomwa mkuki,
kuchomwa shindano ya shaba kitovuni
Mighani huzungumzia matukio ya kihistoria.
Kuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithini.
Mighani hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Huchukuliwa na jamii kama hadithi zenye ukweli na jamii hujinasibisha na mighani hiyo.
Husimulia mambo ya kiimani na kidini.

FASIHI SIMULIZI SWALI 31

Ewe kilizi
Ulozowea kujificha
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio


ya radi ilo juu mbinguni
Jua kesho ni siku ya siku
Siku ya kujua mbichi na mbivu
Kutofautisha jogoo na vipora,
Ngariba taposhika, chake kijembe
Ndipo utakapojua bayani
Ukoo wetu si wa kunguru
Ikiwa hu tayari
Kisu kukidhihaki
Sithubutu kamwe, wanjani kuingia
sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!

a. Huu ni wimbo wa aina gani? Toa sababu. ( alama 2)


b. Wimbo huu unaimbwa na nani ? Toa idhibati. ( alama 2)
c. Fafanua sifa nane za huu. ( alama 8)
d. Je, nyimbo za aina hii zina dhima gani kwenye jamii. ( alama 8)

MAJIBU

a. Huu ni wimbo wa aina gani? Toa sababu. ( alama 2)


Nyiso/Nyimbo za tohara- Ngariba taposhika, chake kijembe
b. Wimbo huu unaimbwa na nani ? Toa idhibati. ( alama 2)
Ami ya anayepashwa tohara- sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!
c. Fafanua sifa nane za nyimbo za aina hii. ( alama 8)

Huambatana na shughuli za jando (wavulana) na unyago (wasichana).


Huimbwa faraghani katika mazingira ya tohara pekee.
Huimbwa usiku wa kuamkia siku ya tohara.
Zilitoa sifa kwa waliotahiriwa, wazazi na wasimamizi wao.
Ziliimbwa kuwapa wavulana ujasiri wa kukabili kisu cha ngariba.
Zilitoa mafunzo kuhusu majukumu mapya baada ya kutahiriwa.
Hujumuisha watu maalum walioteuliwa kushiriki katika sherehe.
Huhusisha watu wa jinsia na umri fulani.
Maudhui yake hutegemea jinsia.
d. Je, nyimbo za aina hii zina dhima gani kwenye jamii. ( alama 8)

Kuonyesha vijana wamevuka kutoka utotoni hadi utu uzima.


Kuwaandaa vijana kwa uchungu watakaouhisi kupitia kijembe.
Kuhimiza ujasiri na ukejeli uoga.
Kusifu wahusika kwa ujasiri wa kukabili kisu na kuingia katika utu uzima.
Kuburudisha waliohudhuria shughuli ya jando au unyago.
Kuelekeza vijana kwenye matarajio mapya ya jamii.
Kufunza majukumu katika utu uzima.
Kukuza umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuwaleta wanajamii pamoja.

FASIHI SIMULIZI SWALI 32

a. Taja aina mbili kuu za fasihi. (al.2)


b. Fafanua tofauti baina ya fasihi ulizotaja hapo juu. (al.4)
c. Tambua istilahi zifuatazo za fasili. (al.8)
i. Fanani
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

ii. Jagina
iii. Maleba
iv. Miviga
d.
i. Eleza maana ya vitanza ndimi. (al.2)
ii. Fafanua sifa za vitanza ndimi. (al.4)

MAJIBU

a. aina kuu za fasihi


Fasihi simulizi
Fasihi andishi

b. Fafanua tofauti
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa mdomo mbele ya hadhira
Fasihi andishi huwasilishwa kwa maandishi kv kwenye vitabu na jazanda

c. Tambua istilahi zifuatazo


Fanani - Huyu ni msimulizi wa fasihi simulizi
Jagina- Shujaa katika mighani
Maleba - Mavazi au vifaa vinavyovaliwa na wasanii
Miviga - sherehe za kutamaduni ambazo hufungwa na jamii katika kipindi fulani maalum.
d.
i. Vitanza ndimi
ii. Sifa:

Sauti hukaribiana kimatamshi


Kuna uradidi/ takriri ya maneno au sauti fulani.

FASIHI SIMULIZI SWALI 33

Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa
amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika.Walitegemea matunda
mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.

Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa.Ndovu aliathirika zaidi. Alijaribu kuinama majini lakini
hakuweza . Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda
kumtafuta sungura. Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata. Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo
yumo msituni.

MASWALI

a. Tambua utanzu na kijipera chake. (al.2)


b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. (al.2)
c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. (al.5)
d. Eleza sifa za kifungu hiki. (al.5)
e. Eleza umuhimu wa fomyula:

i. Kutanguliza (al.3)
ii. Kuhitimisha (al.3)

MAJIBU
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

a.
i. Utanzu – Hadithi (1x1)
ii. Kipera – Ngano za usuli (1x1)
b.
i.
Fanani : paukwa
Hadhira : pakawa
ii.
Fanani : Hadithi! Hadithi
Hadhira : Hadithi njoo
c.
Huburudisha wanajamii husika
Huelekeza wanajamii husika
Huelimisha wanajamii husika
Huhifadhira huziona ya jamii husika
Huonya wanajamii wa jamii husika
Hujenga ushirikiano wa jamii husika
Hujenga kumbukumbu ya wanajamii zozote (5x1)
d.
Huhusisha wahusika wanyama
Wanyama hupewa tabia za binadamu
Huwa na ucheshi mwingi
Hutoa matumaini kwa wanyonge kwamba mwishowe watakuwa washindi
Hutoa maadili na kuonya kwa njia ya kuchekesha isiyoumiza. Zozote 5x1

e. Umuhimu wa fomyula ya kutanguliza


Humtambulisha mtambaji
Huvuta makini ya hadhira
Hutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi wa ubunifu
Hutofautisha kipera cha hadithi na vipera vingine
Huashiria mwanzo wa hadithi
Hushirikisha mtambaji na hadhira. zozote 3x1

FASIHI SIMULIZI SWALI 34


Jua limechomoza leo likiwa kali angani
Majira ni ya asubuhi rafiki,
Akilini sijasahau
Aliyonipitishia, akishatindiika,
Aibu ikanitwaa na wahaka kunivaa.

Kadamnasi alifika hadharani kumimina


Cheche moto za matusi ziso mithilika.

Ila leo nasema kwa alofanya,


Amani nawe na muwe ardhi na mbingu
Pamoja nawe jamaa zako wakuandame
Katika uchochole ulitima wa kimawazo
Mazao yako na yanyaukie kondeni!
Mifugo wako na wafie malishoni!
Uhangaishwe nao mara elfu na elfu!
Ujinga na daima urithishwe kimapokeo.
Utulivu na ukugure daima dawamu!
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

a. Tambua kipera cha mazungumzo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama
4)
b. Kwa kutolea ithibati, taja shughuli zozote mbili za kiuchumi zinazotekelezwa na jamii inayorejelewa
katika kipera hiki. (alama 2)
c. Fafanua umuhimu wa nidaa katika kufanikisha uwasilishaji wa kipera hiki. (alama 3)
d. Onyesha matokeo matatu ya kutenda kinyume na matarijio ya jamii inayorejelewa katika kipera
hiki. (alama 3)
e. Kwa hoja nane, eleza namna shule yako inavyochangia kukuza vipera mbalimbali vya fasihi
simulizi. (alama 8)

FASIHI SIMULIZI SWALI 35


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Ndimi Chesirwo, kijana barubaru,


Ndume na gwiji, la ukoo mtukufu,
Najivunia umahiri, kusakata kandanda.

Tazama umbo langu, guu mithili ya jokovu,


Kifua cha miraba, weusi wa kijungu,
Wenzangu wanienzi, na hata kuduwaa.

Misuli ni tinginya,
Kijijini nasifika,
Wazee kunienzi,
Mabinti kunikabidhi.

Maswali

a. Tambua utungo huu na uthibitishe jibu lako. (alama 2)


b. Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua katika (a) (alama 8)
c.
i. Eleza maana ya maghani. (alama 1)
ii. Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani. (alama 4)
d. Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)

MAJIBU

a. Tambua utungo huu na udhibitishe jawabu lako. (Alama 2)


Majigambo/vivugo- mwandishi anajisifu kwa umahiri wake binafsi.
Kutaja alama 1 kudhibitisha alama 1

b. Kwa kurejelea hoja zozote nane, jadili sifa za utungo uliotambua kwenye swali la (a). (alama 8)

Sifa za majigambo
Hutungwa na kuganwa na muhusika mwenyewe.
Hutungwa kwa usanii mkubwa. Anayejigamba hutumia mitindo tofauti au ishara.
Mwenye kujigamba - hujitungia kivugo kufuatia tukio lililowah kuitokea maishani mwake.
Mara nyingi majigambo hutungwa na kuganwa na wanaume.
Husheheni matumizi ya chuku.
Hutolewa kwa nafsi ya kwanza.
Anayejigamba huweza kubeba baadhi ya vifaa vyake vya kazi au vinavyoonyesha jambo
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

analojisifia.
Majigambo yanaweza kutungwa papo kwa hapo.
Anayejigamba huweza kutaja usuli wake wa kinasaba. Anaweza kusifu ukoo wake
Anayejigamba huwa mlumbi.
Maudhui makuu katika majigambo huwa ushujaa.
(Akikosa (a) , atuzwe 0 katika (b) – Z a kwanza 8 x 1 = 8 athibitishe dai)
c.
i. Maghani ni nini? (Alama 1)
Maghani ni ushairi ambao hutolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. 1 x 1 = 01

ii. Taja na ueleze tofauti za aina mbili za maghani unazojua. (Alama 4)


maghani ya kawaida- tungo za mashairi yenye hubeba masuala ya kawaida; mfano,
njaa, mapenzi, elimu nk.
Maghani simulizi: mashiri ya kihadithi ambayo husimulia sifa za mtu ,mnyama, kitu,
historia au tukio fulani.
Kutaja – alama 2, kutofautisha 2/0

d. Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (Alama 5)


i. Tamasha za kimziki. Wanafunzi hukariri, hugana na kuimba mashairi katika tamasha za
muziki
ii. Sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko bado zinaendelezwa na jamii ya sasa.
iii. Utungaji na utegaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.
iv. Michezo ya kuigiza katika runinga na redio.
v. Tamasha za drama hihifadhi utanzu wa maigizo,mazungumzo na ushairi simulizi.
vi. Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho.
vii. Ngoma za kienyeji huchezwa kwenye hafla kama vile harusi au mikutano ya kisiasa.
viii. Wapo watafiti ambao huandika na kuhifadhi rekodi za vipera vya fasihi simulizi.
ix. Utambaji wa hadithi hutambwa na jamii nyingi za kisasa hasa sehemu za mashambani. (
Zozote 5 x 1 = 05)

FASIHI SIMULIZI SWALI 36

Tofautisha baina ya

i. Hurufa na hekaya (alama 4)


ii. Hadithi za mazimwi na hadithi za mtanziko (alama 4)
iii. Usuli na visasili (alama 4)

He! he! he! weee!


Unayeogopa kutahiriwa
Nani atatahiri badala yako
Eh, eh… ni babu yako
Eh, Eee!... kisu kikali mno!
Lakini nitavumilia.
iv. Huu wimbo unaitwaje? (alama 1)
v. Nini dhamira ya wimbo huu (alama 2)
vi. Taja sifa zozote tano za utanzu wa nyimbo kwa jumla (alama 5)

MAJIBU
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

i. Hurafa ni aina ya ngano ambazo wahusika wake ni wanyama lakini wanao wakilisha binadamu
ilihali Hekaya ni ngano pia lakini wahusika wake ni binadamu wanaowakilisha tabia za binadamu
wa aina hiyo katika jamii.
ii. Hadithi za mtanziko ni zile ambazo mhusika hukumbwa na hali ngumu ya kuamua baina ya mambo
au hali mbili ilihali hadithi za mtanziko ni hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.
iii. Usuli ni aina ya ngano ambazo huelezea sababu za kuwepo kwa hali, tabia ama mahusiano Fulani
k.m. mwewe na kifaranga ilihali visasili ni hadithi za kale ambazo huelezea imani na mtazamo wa
jamii kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake.
iv. Nyiso
v.
Huwafahamisha kijana kuhusu matarajio ya uchungu huasa dhidi ya uoga woga.
Huwaandaa kihisia wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe cha ngariba.
vi.
Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua twasira na hisia nzito.
Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti
Huandamana na uchezaji wa viungo kama vile mabega, kupiga makofi.
Baadhi ya vifungu katika nyimbo hurudiwarudiwa
Hufungamana na muktadhaa Fulani.

FASIHI SIMULIZI SWALI 37


Soma kifungu kifutacho kisha ujibu maswali yanayofata.

Basi kizito Matukio alipewa Cheo kikubwa kutokana na uchapakazi wake. Shirika alilokuwa akifanya kazi
likawa na matumaini makubwa. Kizito naye badala ya kuchapa kazi akawa anajigamba na kujitapa
mitaani. “Ukubwa ninaujua miye. Mimi ndiye Kizito hapa. Kizito Mzito mimi, akaringa. Akawadharau akina
Wanjiku. Amina na Shikuku. Akajitosa kwenye raha bila kujali na kuvaa suti nzito alizoagizia kwa fedha za
shirika. Muda si muda shirika likaingia hasara. Mwishowe ametimuliwa kazini na wazito wenyewe.
Ameondoka na mkoba mzito wa madeni na fedheha: nguo sasa anavaa za matambara mazito! Jamani
uzito unakowapeleka wazito.

MASWALI

a. Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)


b. Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)
c. Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
d. Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
e. Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
f. Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)

MAJIBU

a. Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)


Wahusika katika soga huwa ni wa kubuni
Wahusika hupwa majina ya watu wanaopatikana katika jamii husika.
Huwa na ukweli Fulani unaowahusu wanajamii
Ucheshi unaotumika huwa muhimu kama njia ya kupunguza ukali wa ukweli uliomo.
b. Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)

Uradidi –nzito nzito


Jazanda – mkoba mzito
Taswira – nguo sasa navaa za matambara.
c. Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
Gharama ya utafiti
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Mtazamo hasi kwa wanajamii


Vizingiti vya kidini
Kikwazo kutoka kwa watala
Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi
Ukosefu wa usalama
Uchache wa wazee au wataalamu
d. Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
Kengele zinazotumiwa kupigia hodi kwenye majumba.
Toni katika rununu
Milo kwenye ambulensi
e. Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
Baadhi ya niviga kama vile kutiwa unyagoni kwa wasichana umepitwa.
Baadhi ya miviga ukinzana na malengo ya taifa mf unyago
Hujaza hofu mf kafara ya binadamu.
Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa
f. Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)

Ni kitambulisho cha kundi Fulani la watu. Mfano misimu ya mabaharia huwatambulisha


mabaharia wengine.
Misimu huhifadhi siri za wanaotumia.
Hutumiwa kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji.
Hukuza ushirikiano , uzalendo na uaminifu miongoni mwa wanaotumia.
Huongeza haiba au ladha katika lugha-kuondoa ukinaifu unaotokana na kutumia msamiati
uliozoeleka miaka nenda.
Hupunguza makali katika lugha /kutasfidi lugha.
Hukuza lugha zaidi-baadhi usanifisha na au kuwa lugha rasmi.
Hufadhi historia na utamaduni wa jamii.
Kielelezo cha mpangilio (mfumo) wa jamii Fulani, kijamii na kuchumi –matabaka.
Hutumiwa kuondoa urasmi katika mazungumzo.
Hukuza uwezo wa kufikiri na kutathmini au kudadisi.

FASIHI SIMULIZI SWALI 38

i. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali


“Mwanangu, dunia haitaki papara. Ikiwa unataka kufanikiwa katika mustakabali wako kuwa mtoto
mtiifu na mwongofu. Kumbuka kuwa asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu…”
a. Tambua na ueleze kipera hiki cha fasihi (alama 2)
b. Eleza sifa tatu za kipera hiki. (alama 3)
c.
i. Fafanua dhima tano za kipera hiki katika jamii. (alama5)
ii. Fanani anawezaje kuihusisha hadhira katika usimulizi wake?(alama 4)
iii. Eleza utaratibu unaofuatwa wakati wa kutega na kutegua vitendawili. (alama 6)

MAJIBU

I.
i. kipera- mawaidha alama 2
ii. sifa za mawaidha-
matumizi mapana ya mbinu za lugha kama vile vile methali
hutolewa na mzee, mzazi au mtu anayechukuliwa kuwa na hekima
lugha inayotumiwa huwa ya kipekee inayolengwa kuathiri wanaousiwa
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

huweza kufungamanishwa na visa au matukio maalum yanayotokea katika jamii


huweza kuambatanishwa na mbazi na istiara
alama 3
iii. umuhimu wa mawaidha
hutoa ushauri kwa walengwa
Hutoa maelekezo kwa anayepewa mawaidha
Humtolea mlengwa maonyo asije akapotoka na kutumbukia mashakani
Humkosoa muathiriwa ambaye huenda alikuwa ameuchukua mkondo usiofaa wa
maisha
Hutambulisha jamii- kila jamii huwa na aina yake ya mawaidha kulingana na
thamani zake
Alama 5
II. jinsi ya kuihusisha jamii katika masimulizi
Kuwauliza maswali
Kuimba wimbo pamoja na hadhira
Kuwauliza kukariri jambo alilolisema
Kuwashirikisha katika vitendo mathalani kupiga makofi au kuigiza wahusika
III. utaratibu wa vitendawili
i. Mtegaji hutanguliza kwa kuiambia/ kutangaza vitendawili
ii. Hadhira hujibu tega
iii. Mtegaji hutoa kitendawili chenyewe
iv. Hadhira hupewa muda wa kufikiri na kujaribu kukitegua
v. Hadhira ikitoa jibu lisilo sahihi, mtegaji huomba apewe mji ili aweze kutoa jibu
vi. Mtegaji akipewa mji anaotaka hukubali na kutoa jibu
Alama 6

FASIHI SIMULIZI SWALI 39


Soma kifungu kifutacho kisha ujibu maswali yanayofata.
Basi kizito Matukio alipewa Cheo kikubwa kutokana na uchapakazi wake. Shirika alilokuwa akifanya kazi
likawa na matumaini makubwa. Kizito naye badala ya kuchapa kazi akawa anajigamba na kujitapa
mitaani. “Ukubwa ninaujua miye. Mimi ndiye Kizito hapa. Kizito Mzito mimi, akaringa. Akawadharau akina
Wanjiku. Amina na Shikuku. Akajitosa kwenye raha bila kujali na kuvaa suti nzito alizoagizia kwa fedha za
shirika. Muda si muda shirika likaingia hasara. Mwishowe ametimuliwa kazini na wazito wenyewe.
Ameondoka na mkoba mzito wa madeni na fedheha: nguo sasa anavaa za matambara mazito! Jamani
uzito unakowapeleka wazito.
MASWALI

a. Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)


b. Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)
c. Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
d. Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
e. Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
f. Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)

MAJIBU

a. Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)


Wahusika katika soga huwa ni wa kubuni
Wahusika hupwa majina ya watu wanaopatikana katika jamii husika.
Huwa na ukweli Fulani unaowahusu wanajamii
Ucheshi unaotumika huwa muhimu kama njia ya kupunguza ukali wa ukweli uliomo.
b. Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)
Uradidi –nzito nzito
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Jazanda – mkoba mzito


Taswira – nguo sasa navaa za matambara.
c. Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
Gharama ya utafiti
Mtazamo hasi kwa wanajamii
Vizingiti vya kidini
Kikwazo kutoka kwa watala
Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi
Ukosefu wa usalama
Uchache wa wazee au wataalamu
d. Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
Kengele zinazotumiwa kupigia hodi kwenye majumba.
Toni katika rununu
Milo kwenye ambulensi
e. Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
Baadhi ya niviga kama vile kutiwa unyagoni kwa wasichana umepitwa.
Baadhi ya miviga ukinzana na malengo ya taifa mf unyago
Hujaza hofu mf kafara ya binadamu.
Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa
f. Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)

i. Ni kitambulisho cha kundi Fulani la watu. Mfano misimu ya mabaharia huwatambulisha


mabaharia wengine.
ii. Misimu huhifadhi siri za wanaotumia.
iii. Hutumiwa kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji.
iv. Hukuza ushirikiano , uzalendo na uaminifu miongoni mwa wanaotumia.
v. Huongeza haiba au ladha katika lugha-kuondoa ukinaifu unaotokana na kutumia msamiati
uliozoeleka miaka nenda.
vi. Hupunguza makali katika lugha /kutasfidi lugha.
vii. Hukuza lugha zaidi-baadhi usanifisha na au kuwa lugha rasmi.
viii. Hufadhi historia na utamaduni wa jamii.
ix. Kielelezo cha mpangilio (mfumo) wa jamii Fulani, kijamii na kuchumi –matabaka.
x. Hutumiwa kuondoa urasmi katika mazungumzo.
xi. Hukuza uwezo wa kufikiri na kutathmini au kudadisi.

FASIHI SIMULIZI SWALI 40

a.
i. Miviga ni nini? (Alama 2)
ii. Eleza sifa nane za miviga. (Alama 8)
b.
i. Ulumbi ni nini? (Alama 2)
ii. Eleza sifa nane za ulumbi

MAJIBU

a.
i. Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum
cha mwaka.
ii.
Miviga huandamana na matendo au kanuni Fulani.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Miviga hufuata utaratibu maalum.


Miviga huongozwa na watu mahususi katika jamii.
Miviga huandamana na utoaji mawaidha.
Maleba maalumu huvaliwa na wanaohusika.
Miviga hufanyiwa mahali maalum.
Miviga huenda na wakati maalum.
Huhusisha imani ya dini husika. (8x1)
b.
i. Ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.
ii.
Hutumia lugha kwa njia inayovutia na kushawishi.
Hutumika katika miktadha kama kutoa hotuba kwa jamii.
Hukuza ukakamavu wa kuzungumza hadharani.
Hutumia tamathali za usemi kama vile jazanda.
Ulumbi huwa na urudiaji mwingi wa maneno.
Walumbi hutumia chuku kwa ufanisi.
Mlumbi huelewa utamaduni wa jamii.
Ulumbi hutumika katika shuguli za jamii.
Ulumbi hutumia viziada lugha. (8x1)

FASIHI SIMULIZI SWALI 41

a. Ngomezi ni nini? (alama 1)


b. Taja mifano minne ya ngomezi za kisasa (alama 4)
c. Eleza hasara tano za miviga (alama 5)
d. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Lulu, mwanangu tulia,
Wewe mtoto lala, mvua imekuja
Si uongo hata na miti huichangamkia mvua,
Hakuna haja ya kuelezwa,
Lulu mwana tulia,
wewe mtoto lala, mvua imekuja.
i. Tambua kipera hiki (alama 2)
ii. Taja sifa nne za kipera hiki (alama 4)
iii. Eleza majukumu manne ya kipera hiki (alama 4)

MAJIBU

a. NGOMEZI ni sanaa ya ngoma


Ni aina ya fasihi ambayo hutumia milio ya ngoma badala ya mdoma
b. Ngomezi za kisasa
Kengele za milangoni
Milio kwenye ambulensi
Toni katika rununu
Kamsa kwenye magari ya polisi
Honi za gari
Ving’ora(vya usalama) NK 4x1
c. Eleza hasara tano za miviga (alama 5)

Baadhi ya miviga huhatarisha Maisha ya wanajamii km kurithi mke wa mtu


aliyeaga,kutiwa, unyagoni
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Baadhi ya miviga hukinza malengo ya kitaifa km ukeketaji wa Watoto wa kike ni


ukiukaji wa haki za binadamu

Hujaza watu hofu km miviga inayohitaji kafara ya binadamu au sherehe za


kufukuza mapepo huhofisha

Baadhi ya miviga huhusisha ushirikina km mazishi katika jamii nyingine..Hili


huweza kusababisha uhasama katika baadhi ya koo

Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa au mali.Hili huiacha familia katika hali
duni kiuchumi km sherehe za kuomboleza katika baadhi ya jamii 5x1
d.
i. Kipera- Bembea/Bembezi/Bembelezi 1x2
ii. Sifa za Bembea

Huimbwa taratibu kwa sauti na mahadhi ya chini

Huwa fupi

Huimbwa na wazazi au walezi wa watoto kuwaliwaza ili watoto


wanyamaze au walale

Hutofaitiana kutoka jamii moja hadi nyingine kulingana na thamani za


jamii hiyo

Hurudiwarudiwa maneno au kibwagizo

Hutumia lugha shawishi na wakati mwingine ahadi hutolewa


iii. Majukumu ya Bembea

Hutumbuiza na kuongoa watoto

Hutumiwa kama sifo kumsifu mtoto ambaye ni mtulivu

Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika

Husawiri mahusiano katika jamii

Hutakasa hisia ambazo mwimbaji huweza kuwa nazo

Humwelimisha mtoto katika umri mchanga (alama 4x1)

FASIHI SIMULIZI SWALI 42


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ndimi Nguli, dume la ukoo mtukufu
Ulojipambanua kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani
Makoo yakatetemeka
Yakang’ang’ania gozi kusakata nami.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Maswali

a. Tambulisha kipera kinachojitokeza katika kifungu hiki. (alama 2)


b. Eleza sifa tano bainifu za kipera hiki katika fasihi simulizi. (alama 10)
c. Fafanua umuhimu wa kipera hiki. (alama 8)

MAJIBU

a. Majigambo au vivugo (1x2 = 2)


b.
Hutungwa na kughaniwa na mhusika mwenyewe
Hutungwa kwa usanii mkubwa sana. K.m matumizi ya sitiari
Anayejigamba hutunga kivugo kufuatia tukio mahususi katika maisha yake michezoni,
vitani, kesi, jando na Kadhalika.
Huwa na matumizi ya chuku. Mtunzi hujisifu kupita kiasi kwa kutaja mafanikio na mchango
wake.
Majigambo hutungwa papo hapo. Lakini mengine huandikwa na kughaniwa baadaye.
Maudhui makuu ya majigambo huwa ushujaa
Kwa kawaida hutungwa na kughaniwa na wanaume
Anayejigamba huweza kuvaa maleba yanayooana na kazi yake. Pia anaweza kubeba
baadhi ya vifaa vya kazi.
Anayejigamba huweza kutaja na kusifu ukoo/nasaba yake.
Mara nyingi wanaojigamba kuwa walumbi au washairi
Za kwanza 5 x 2 = 10
c.
Hukuza ubunifu. Mtunzi huimarisha uwezo wake wa kubuni mitindo mipya ya utunzi na
uwasilishaji anapoendelea kubuni majigambo.
Ni nyenzo ya burudani. Waliohudhuria sherehe huongolewa na majigambo
Kukuza ufasaha wa lugha. Watunzi wengi wa majigambo huwa Walumbi ambao ni weledi
wa lugha
Hudumisha utu na hutambulisha mwanamume katika jamii. Wanaume walipaswa kuwa
jasiri katika jamii kwa sababu ya uchokozi uliokuwepo
Ni nyenzo ya kufanya watu waheshimiwe. Hufanya wanaume kuwa mashujaa.
(zozote 4x2= 8)

FASIHI SIMULIZI SWALI 43


Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

Mimi ni Olichilamgwara
Olichilamgwara mwana mbee wa Ojilong
Ojilong wa Marukatipe
Wazee waliposhindwa
Nilivuka misitu milima na mito
Ni mimi jabali
Kipande cha jifya la mama
Nilipokuwa nalisha mifugo
Nilisikia baragumu inalia
Baragumu ya wito
Mifugo wa mtemi wamechukuliwa
Nikachukua mkuki wangu
Wenye kigumba cha mti
Nikachukua upanga wangu
Wenye makali kama mmweso wa radi
Upanga uliopasua pembe za nyati kwa dhoruba moja
Ndipo nilipofyatuka kasi kama umeme
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kufumba kufumbua nikawakaribia nduli


Kusikia vishindo vyangu wakaanza kubabaika
Kuona kifua changu cha manyoya ya kanga wakatetemeka
Macho yangu makali kama kaa la moto yalipowatazama wakakimbia
Mkuki wangu ulipaa kama umeme
Wote wakalala
Mifugo wakanifuata…
Mko wapi vijana
Mmekuwa kama majivu baada ya moto kuzimika?

Maswali

a. Tambua kipera ulichokisoma na udhibitishe jibu lako. (alama 2)


b. Tambua sifa za jamii zinazosawiriwa katika utungo huu (alama 2)
c. Kwa kutoa mifano bainisha vipengele vinne vya kimtindo vilivyotumiwa na nafsineni (alama 4)
d. Fafanua sifa nne za kipera hiki (alama4)
e. Eleza mambo manne ambayo mtendaji wa kipera hiki anaweza kufanya ili kufanikisha utendaji
wake. (alama4)
f. Fafanua mikakati ambayo jamii inaweza kutumia ili kuzuia tungo kama hizi kufifia. (alama 4)

MAJIBU

a. .
Ni majigambo /vivugo
Matumizi ya mimi ni…. (1x2)
b.
Ni wafugaji – nilipokuwa nalisha mifugo
Ni wezi wa mifugo – mifugo wa mtemi wamechukuliwa
Wanajihusisha na vita (2x1)
c.
istiara(sitiari) Ni mimi Jabali
Tashbihi – kiasi kama umeme
Ulipaa kama umeme
Kama mmweso wa radi
Mdokezo – mifugo ikanifuata…
Swali la balagha – mmekuwa kama majivu baada jua moto kuzimika?
Chuku – upanga kupasua pembe za nyati kwa dhoruba moja
Msemo – kufumba na kufumbua
Urudiaji(takriri) nikachukua mkuki wangu
Nikachukua upanga wangu
Matumizi ya mishororo mishata m.f wazee waliposhindwa
Nilipokuwa nalisha mifugo…
Uhuishi – mkuki kupaa
Usambamba – nikachukua mkuki wangu , nikachukua upanga wangu
d.
anayejigamba hutunga kufuatia tukio mahususi katika maisha yake - anakumbuka
alivyokomboa mifugo ya Mtemi kutoka kwa wezi.
Huwa na matumizi ya chuku
Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na wanaume
Hutolewa kwa nafsi ya kwanza m.f Nikachukua mkuki wangu
Anayejisifu huweza kutaja usuli wake wa kinasaba m.f Ochilamgwara mwana mbee wa
Ojilong
Maudhui makuu ni ushujaa
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Hutungwa kwa usanii mkubwa – sitiari urudiaji tashbihi n.k


e.
Avae maleba – mkuki , upanga ngozo
Atomie kiimbo na toni kupanda na kushuka kwa sauti yake
Atumie miondoko ya mwili
Atumie ishara za uso
Ashirikishe hadhira kwa kuuliza maswali ya balagha.
Kadiria hoja zaidi (za kwanza 4 x 1 = 4)
f.
Kufanya utafiti Zaidi
Kuhifadhi kwenye kanda tepu rekodi video n.k
Kufunza shuleni
Kupanga mashindano kati ya jamii mbalimbali
Kuhifadhi katika maandishi
Kuhimiza watu kutunga tungo kama hizi.
Shere mbalimbali

FASIHI SIMULIZI SWALI 44


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:
Wanangu, mwanadamu lazima awe na malengo ya mambo anayohitaji kuyatekeleza siku za maisha yake
duniani kabla ya maisha ya baada ya kifo. Ni lazima akumbuke kuwa si vyema akubali kufa kama kwamba
hakuwahi kuishi duniani. Yaani, haifai kwa mtu yeyote kuondoka duniani na kuelekea peponi kuishi kwa
starehe ama ahera kwa wale wanaokufa kabisa, bila kuacha lolote lenye mashiko duniani. Lazima
kuhakikisha kwamba kuna bora, japo moja, ambalo waliosalia duniani watakukumbuka kwalo. Japo
kiduchu tu. Ukiwa mwimbaji imba lau ubeti mmoja tu ukasikizwe wakati utakapokuwa umepumzika. Ukiwa
kiongozi jenga daraja japo moja na kulizindua wewe. Mwili wako utakuwa umeondoka ila nafsi yako
itasalia duniani kwa jina lako.

Ukiwa na mkono wa kuandika andika japo ubeti mmoja wa shairi. Kumbusha watu kuhusu umuhimu wa
maisha na kuwaeleza kutenda mema kabla hawajaisha. Andika hata aya tatu za hadithi. Jihusishe katika
mashindano maarufu japo ujue kuwa wahariri wataiangalia kazi yako na kusema, “Uchafu mtupu! Huyu
hana talanta. Ameharibu wakati wake tu katika shindano hili la jumuia nzima. Sisi tunasaka talanta! Huyu
limbukeni anatuletea hapa ‘viswahili’ gani hivi visivyo na mkia wala kichwa hali mwenyewe si Mswahili?
Potelea jalalani! Huenda hata wakati mwingine kazi yako isisomwe ila wewe andika tu. Andika tena na
tena. Andika.Andika usihofu. Bora tu usife kama hukuwahi kuishi.Zingatieni wosia wangu huu wanangu.
(Kutoka Riwaya: Hawakuziki Mama- Meja S. Bukachi)

a. Tambua kipera hiki cha fasihi simulizi. (Alama 2)


b. Fafanua vipengele kumi vya kimtindo ambavyo fanani ametumia katika uwasilishaji wake. (alama
10)
c. Eleza umuhimu wa kipera hiki katika jamii. (alama 3)
d. Wewe ni kati ya wanaopewa kipera hiki. Fafanua mambo matano ambayo wewe na wenzako
mnaweza kufanya wakati wa kutolewa. (alama 5)

MAJIBU

a. Tambua kipera hiki cha fasihi simulizi. (Alama 2)


Mawaidha- kuna matumizi ya lugha ya kushawishi na kushauri mtu kukabiliana
na maisha.
Moja kutaja, moja kueleza (1x2)
b. Fafanua vipengele kumi vya kimtindo ambavyo fanani ametumia katika uwasilishaji wake. (alama
10)

Baba anazungumza moja kwa moja na wanawe.


Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Matumizi ya chuku- uchafu mtupu.

Tashihisi- potelea jalalani.

Methali- atakaye cha mvunguni sharti ainame.

Nahau- uchafu mtupu (isiyo na maana)

Urudiaji- Andika tena na tena. Andika. Andika usihofu.

Ritifaa- wahariri watasema, Potelea jalalani!

Tasfida- utakapokuwa umepumzika (utakapokuwa umekufa)

Kuigiza- Uchafu mtupu. Huyu hana talanta. Ameharibu wakati wake tu katika
shindano hili la jumuia nzima. Sisi tunasaka talanta! Huyu limbukeni anatuletea
hapa ‘viswahili’ gani hivi visivyo na mkia wala kichwa hali mwenyewe si
Mswahili? Potelea jalalani!”

Nidaa/ Siyai- potelea jalalani! (10x1=10)


c. Eleza umuhimu wa kipera hiki katika jamii. (alama 3)

Mawaidha hutoa mwongozo wa jinsi ya kukabiliana na matatizo au jinsi ya


kutenda jambo.

Mawaidha huelimisha kwa kuwapa wanajamii maarifa ya kuendesha maisha.

Wanaopewa mawaidha hujifunza maadili kama vile adabu, heshima na kadhalika.

Mawaidha hutambulisha jamii kwani kila jamii huwa na aina yake ya mawaidha
kulingana na thamani zake.
Hoja zifafanuliwe (3x1=3)
d. Wewe ni kati ya wanaopewa kipera hiki. Fafanua mambo matano ambayo wewe na wenzako
mnaweza kufanya wakati wa kutolewa. (alama 5)

Kuuliza maswali.

Kutoa majibu kwa baadhi ya maswali ya anayetoa mawaidha.

Kusikiliza kwa makini.

Kuuliza maswali palipo na utata.

Kuonesha kukubaliana kwa ishara za uso.


(5x1=5)

FASIHI SIMULIZI SWALI 45

Tambua vipera vifuatavyo: (alama 3)


Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

i. Wewe ni mweusi sana hadi ukibeba mtoto, analala akidhani ni usiku.


ii. “Kwa nini mnabaguana? Mimi sikuwafundisha kubaguana…”
iii. …hadi leo jamii hiyo inasadiki kuwa Luanda Magere alikuwa jagina wa kuenziwa.
a. Tegua vitendawili vifuatavyo: (alama 5)

i. Popoo mbili zavuka mto.


ii. Pango lenye mawe meupe na mkeka mwekundu.
iii. Naingia ndani ya nyama natoka bila kushiba.
iv. Amenifukuza kote kwa blanketi lake jeusi.
v. Aliwa yuala, ala aliwa
b. Eleza umuhimu wa nyimbo katika utambaji wa ngano. (alama 6)
c. Ukusanyaji data katika fasihi simulizi huwa na changamoto zipi? (alama 6)

MAJIBU

Tambua vipera vifuatavyo: (alama 3)

i. Wewe ni mweusi sana hadi ukibeba mtoto, analala akidhani ni usiku. (vichekesho)
ii. “Kwa nini mnabaguana? Mimi sikuwafundisha kubaguana…” (mawaidha)
iii. …hadi leo jamii hiyo inasadiki kuwa Luanda Magere alikuwa jagina wa kuenziwa. (mighani)
a. Tegua vitendawili vifuatavyo: (alama 5)
i. Popoo mbili zavuka mto. (macho)
ii. Pango lenye mawe meupe na mkeka mwekundu. (meno na ulimi)
iii. Naingia ndani ya nyama natoka bila kushiba. (sindano)
iv. Amenifukuza kote kwa blanketi lake jeusi. (giza)
v. Aliwa yuala, ala aliwa (papa)
b. Eleza umuhimu wa nyimbo katika utambaji wa ngano. (alama 6)
i. Husaidia kuondoa ukinaifu/uchovu kutokana na urefu wa hadithi.
ii. Kusisimua hadhira kwa njia ya burudani.
iii. Kuteka makini ya hadhira.
iv. Kuweka mipaka baina ya matukio kwenye hadithi.
v. Kushirikisha hadhira katika utambaji.
vi. Kuwasilisha mafunzo katika wimbo.
vii. Kurefusha hadithi.
viii. Kusisitiza ujumbe ikiwa unarudiwarudiwa.
ix. Kueleza sifa za wahusika. Zozote 6x1
c. Ukusanyaji data katika fasihi simulizi huwa na changamoto zipi? (alama 6)
i. Ukosefu wa utafiti wa kutosha.
ii. Uchache wa wataalamu wa kuitafiti na kuiendeleza.
iii. Ukuaji wa kazi za kimaandishi na hivyo kuondoa haja ya utambaji.
iv. Maendeleo ya kiteknolojia na sayansi yanayotoa njia za kisasa za kujiburudisha.
v. Baadhi ya watu kuhusisha fasihi simulizi na ukale na hivyo kutoona haja ya kutafiti.
vi. Watu wengi kuhamia mjini na hivyo kufanya urithishaji wake kutowezekana.
vii. Mtaala wa elimu kupuuza lugha za kiasili ambazo huhifadhi na kurithisha fasihi
simulizi.
viii. Kwa kuwa inahifadhiwa akilini, anayeihifadhi anaweza kuibadilisha, kutoweka au
kufa.
Zozote 6x1

FASIHI SIMULIZI SWALI 46


Tumia kifungu kifuatacho kujibu maswali yanayofuata
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

a. Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye
wa kike.

i. Bainisha kipera kinachorejelewa (Al 1).


ii. Andika shughuli moja ya Kijamii na moja ya Kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya
utingo huu. (Al 2)
iii. Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako. (Al 4)
iv. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia
katika uwasilishaji wako. (Al 5)
b. Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)

MAJIBU

a. Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye
wa kike.

i. Bainisha kipera kinachorejelewa

Kitendawili
ii. Andika shughuli moja ya Kijamii na moja ya Kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya
utingo huu

Kijamii – ndoa (kulichuma/ ndugu wa kiume asimuoe nguye wa kike).

Kiuchumi – kilimo – paipai lilioiva


iii. Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako
Umuhimu
Kuburudisha jioni baada ya kazi

Kukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili


kuviunda.

Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.

Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata
jibu.

Kuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati
vinategwa.

Kuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lugha.

Kupanua ujuzi wa mazingira wa mtoto.

Kuendeleza utamaduni wa jamii kama Nyumbani mwetu mna papai lilioiva


lakini siwezi kulichuma – Ndugu wa Kiume asimuoe nduguye wa kike.

Kukejeli au kudharau tabia mbaya kama wazungu wawili wanachungulia


dirishani – Makamasi
iv. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani. Eleza mambo ambayo utazingatia katika
uwasilishaji wako
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

a. Kutumia fomyula/muundo maalum. Mifano


Mtegaji : Kitendawili
Mteguaji : Tega

b. Kutumia ukakamavu wa kuweza kuzungumza hadharani.

c. Kuwa na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza


kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake.

d. Ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha


kwa wepesi.

e. Kuwa mchangamfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia


isikinai.

f. Ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na


ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na Imani za hadhira.

g. Kushirikisha hadhira kama vile kuimba, maswali ya balagha ili isikinai.

h. Kudramatisha ili kuonyesha picha Fulani kama vile kuiga toni, sauti, na
kiimbo kulingana na swala analowasilisha.

i. Kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigiza.

j. Ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.

k. Kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti unazoigiza kama


huzuni.

l. Ufaraguzi/kubadilisha uwasilishaji papo hapo kutegemea hadhira na kutoa


mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
b. Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)

i. ni hifadhi za matukio muhimu ya kihistoria katika jamii


ii. hutumiwa kama nyenzo ya kupitisha utamaduni
iii. hutumiwa kama burudani
iv. huakisi umbuji wa tamaduni mbalimbali
v. huhamasisha watu kutenda mambo mbalimbali
vi. huelimisha na kupitisha maarifa mbalimbali miongoni mwa wanajamii
vii. ni kiakisi cha fahari walio nayo wanaohusika katika utamaduni wao. Aina na
maana za nyimbo

FASIHI SIMULIZI SWALI 47

a. Tumia kifungu kifuatacho kujibu maswali yanayofuata.


Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuna – Ndugu wa kiume asimuoe nduguye
wa kike.
i. Bainisha kipera kinachorejelewa. (ala. 1)
ii. Andika shughuli moja ya kijamii na moja ya kiuchumi ambazo huedelezwa katika jamii ya
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

utungo huu. (ala. 2)


iii. Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako. (ala 4)
iv. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwaani. Eleza mambo matatu ambayo utayazingatia
katika uwasilishaji wake. (ala. 3)
b. Umepewa jukumu la kukusanya data kuhusu michezo ya watoto ukitumia hojaji.
i. Eleza manufaa matano ya kutumia mbinu hii. (ala. 5)
ii. Eleza changamoto tano za kutumia mbinu hii . (ala. 5)

MAJIBU

a.

i. Kitendawili……………….. 1*1=1
ii. Shughuli ya kijamii………….. kilimo/ukulima.
Shughuli ya kiuchumi………….ndoa ama nikahi.
(2*1=2)
iii. Dhima ya kipera hiki:
kuelimisha
kuburudisha
kukuza uwezo wa kukumbuka
kukuza uwezo wa kufikiri
kutanguliza tanzu nyingine za kifasihi
kukashifu tabia hasi katika jamii
kukuza utangamano
kukuza udadisi
kuwajuza wanajamii kuhusu mazingira yao.
Kukuza ubunifu
Kukuza uzalendo.
Kuhifadhi historia.
(4*1=4)
iv. Mambo ya kuzingatia katika uwasilishaji ;
Sauti inayosikika.
Awe mbunifu.
Aweze kukumbuka.
Aielewe lugha ya hadhira yake.
Aufahamu utamaduni wa hadhira yake.
Awe mcheshi.
Awe jasiri.
Arejelee mifano halisi katika jamii.
Aielewe hadhira.
Awe mfaraguzi.
Kuishirikisha hadhira.
3*1=3.
b. Hojaji
i. Manufaa ya hojaji.
Ina gharama ya chini Zaidi ikilinganishwa ma njia nyinginezo.
Mtafiti anaweza idadi kubwa ya watoaji habari kwa kipindi kifupi kwa maana hojaji
zinaweza zikatumiwa watu hao kwa njia kama vile posta.
Inaweza kutumiwa katika mahojiano kama mwongozo. Mhoji anaweza kuitumia
katika mahojiano kufidia udhaifu wa mhojiwa.
Humpa mhojiwa muda wa kuwazia maswali na kuyafanyia uchunguzi kabla ya
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

kuyajibu.
Hazina athari za mtafiti kwa sababu aghalabu zinapojazwa mtafiti hayupo. Mhojiwa
hujaza habari za kweli bila kushinikiwa kuchukua mtazamo Fulani kutokana na
kuwepo kwa mtafiti.
Zinaweza kubadilishwa kulingana na kiwango cha wajazaji/wahojiwa.
5*1=5.
ii. Changamoto za hojaji.
Maswali yenye utata husababisha fasiri mbalimbali ambazo hufanya matokeo
yasitegemeke.
Huenda wengine wasikamilishe kujaza hojaji,hivyo kumhini mtafiti habari
anazotaka.
Hojaji ikiwa ndefu sana huenda baadhi ya watu wakakataa kuijaza.
Hojaji wazi huwa ngumu sana kwa mtafiti kuchanganua data. Uchanganuzi
huchukua muda mrefu.
Huenda wahojiwa wasijaze mambo ya kweli. Si rahisi kwa mtafiti kuthibitisha iwapo
habari zilizojazwa ni za kweli.
Wahojiwa wanaweza kuchelewa kutuma hojaji zao, hasa hojaji zilizotumwa kwa
posta.
Zinaweza kujazwa tu na watu waliosoma,hivyo kuwatenga wengine ambao labda
wangetoa habari za kutegemeka.
Kwa vile mtafiti,hakabiliani na mhojiwa ana kwa ana ,hawezi akapata sifa za
uwasilishaji wa vipera vya fasihi simulizi kama vile toni na kidatu.
5*1=5

FASIHI SIMULIZI SWALI 48

A.
i. Miviga ni nini? (Alama 2)
ii. Eleza sifa nane za miviga. (Alama 8)
B.
i. Ulumbi ni nini? (Alama 2)
ii. Eleza sifa nane za ulumbi (Alama 8)

MAJIBU

a.
i. Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum
cha mwaka.
ii. Miviga huandamana na matendo au kanuni Fulani.
Miviga hufuata utaratibu maalum.
Miviga huongozwa na watu mahususi katika jamii.
Miviga huandamana na utoaji mawaidha.
Maleba maalumu huvaliwa na wanaohusika.
Miviga hufanyiwa mahali maalum.
Miviga huenda na wakati maalum.
Huhusisha imani ya dini husika. (8x1)
b.
i. Ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.
ii. Hutumia lugha kwa njia inayovutia na kushawishi.
Hutumika katika miktadha kama kutoa hotuba kwa jamii.
Hukuza ukakamavu wa kuzungumza hadharani.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Hutumia tamathali za usemi kama vile jazanda.


Ulumbi huwa na urudiaji mwingi wa maneno.
Walumbi hutumia chuku kwa ufanisi.
Mlumbi huelewa utamaduni wa jamii.
Ulumbi hutumika katika shuguli za jamii.
Ulumbi hutumia viziada lugha. (8x1)

FASIHI SIMULIZI SWALI 49


Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yaliyoulizwa.

Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na
Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa
mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa
sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi
aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza
agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika
duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La!
Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana
na neno la mjusi, wanadamu hufa.

a.
i. Tambua aina hii ya hadithi (al 2)
ii. Toa sababu za jibu lako katika (a) i. (al 1)
b. Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii. (al 3)
c. Fafanua hulka mbili za Kinyonga kwa mujibu wa makala haya (al 2)
d. Hadithi hii ina umuhimu gani? (al 4)
e. Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi (al 4)
f. Fafanua jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi (al 4)

MAJIBU

a.
i. Kisasili (al 2)
ii. Inaeleza jinsi kifo kilivyoingia duniani/ Asili ya kifo (al 1)
b.
Mwanzo maalum- Hapo zamani za kale
Wahusika wanyama
Wanyama kuwasilisha tabia za binadamu
Tanakali za sauti. (Zozote 3x1=3)
c.
Mvivu/ Mnyonge
Mtiifu (Zozote 2x1=2)
d.
Huburudisha
Huhifadhi historia ya jamii
Huendeleza utamandunu wa jamii
Huipa jamii mwelekeo
Huonya/ Huadhibu
Hukuza usirikiano
Hukuza stadi za lugha
(Zozote 4x1=4)
e.
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Kutazama
Kushiriki
Kurekodi
Kutumia Hojaji
Mahojiano (al 4)
f.
Tamasha za muziki
Sherehe za arusi, jando,mazishi na matambiko
Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia vyombo vya habari
Michezo ya kuigiza katika vyombo vya habari
Tamasha za drama
Sarakasi zifanywazo na wasanii
Ngoma za kienyeji k.v Isikuti
Watafiti wanaokusanya na kuhifadhi vipera vya fasihi simulizi
(Zozote 4x1=4)

FASIHI SIMULIZI SWALI 50

a. Fafanua sifa za nyimbo za watoto. (alama 5)


b. Eleza maana ya; (alama 5)

i. Vitanza ndimi
ii. Tarihi
iii. Vivugo
iv. Matambiko
v. Maapizo
c. Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa. (alama 5)
d. Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)

MAJIBU

a. Fafanua sifa za nyimbo za watoto. (alama 5)


Hujaa urudiaji
Huashiria kazi za jamii husika
Hutumia kiimbo cha juu
Huimbwa kwa toni ya furaha
Huambatanishwa na uchezaji wa viungo vya mwili.
Huhimiza tabia chanya
Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
b. Eleza maana ya; (alama 5)
i. vitanza ndimi- ni kauli au sentensi zenye maneno ambayo yana mfuatano wa sauti
zinazotatanisha kimatamshi.
ii. Tarihi- ni rekodi za matukio ya kihistoria ambayo hupangwa yakifuatana kiwakati
na huwasilishwa kwa njia ya masimulizi bila ya kutolewa ufafanuzi.
iii. Vivugo- ni maigizo ya kujigamba ambayo yanaweza kuambatanishwa na ngoma na
maleba.
iv. Matambiko- ni sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au
mizimu
v. Maapizo- ni maombi maalum ya kumtaka Mwenyezi Mungu , miungu au mizimu ili
kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au mwovu. (5x1)
c. Jadili mifano mitano ya ngomeziza kisasa. (alama 5)
Get more notes and past papers at www.easyelimu.com. (WhatsApp only +254703165909 for more)

Milio ya ambulensi
Toni katika rununu
Kengele shuleni
Toni katika saa
Kengele za milangoni (5x1)
d. Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)
Vitendawili huwa na fomyula ya uwasilishaji ilhali methali haina fomyula
mahususi.
Vitendawili huwa na fumbo ambalo lazima lifumbuliwe hapo hapo na hadhira
ilhali methali fumbo halifumbuliwi papo hapo na huwasilishwa na mwenye
kutumia methali.
Vitendawili ni maarufu kwa vijana ilhali methali huwa maarufu miongoni mwa
wazee na watu wazima.
Vitendawili hutolewa kwenye kikao maalum ilhali methali si lazima zitengewe
vikao maalum.
Vitendawili huwa na hadhira tendi ilhali methali huwa huwa na hadhira tuli.
Vitendawili huwasilishwa kwa majibizano ilhali methali huwasilishwa kwa kauli
moja tu na msemaji. (5x1)

last - 4057

Powered by TCPDF (www.tcpdf.org)

You might also like