Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

TUBERCULOSIS (TB)

KIFUA KIKUU
KIFUA KIKUU
Ni Ugonjwa wa Kuambukiza unao Athiri Mapafu, husababishwa na Bakteria
(Mycobacterium tuberculosis) ambae huathiti mfumo wa hewa.

NAMNA INAVYOAMBUKIZWA
Kifua Kikuu husambaa kutoka kwa Mtu mmoja (Muathirika wa Kifua Kikuu) hadi
kwa mtu mwingine (Sio Muathirika wa Kifua kikuu) kwa Njia ya HEWA kupitia:
➢ Kukohoa
➢ Chafya
➢ Kucheka
➢ Kuimba
➢ Kuongea

• Kikohozi na Chafya ndio njia kubwa ya Bakteria Kutoka kwa Mtu mmoja kwenda
kwa Mwingine kwa Haraka.

SABABU ZINAZOPELEKEA KUPATA KIFUA KIKUU (TB)


• Uvutaji wa Sigara na Ulevi.
• Umri (Wazee na Watoto, kinga zao ndogo)
• Moshi wa Kuni na Mkaa
• Vumbi na Moshi wa Viwandani
• Maeneo yenye Mkusanyiko wa watu wengi.
• Upungufu wa Kinga Mwilini.
Watu wenye Shida ya Upungufu wa Kinga ya Mwili wako hatarini
zaidi katika kupata KIFUA KIKUU (TB). Mfano:
▪ Ukimwi
▪ Kansa
▪ Lishe duni
▪ Magonjwa ya Muda mrefu. i.e Kisukari

DALILI ZA MAPEMA ZA KIFUA KIKUU (TB)


• Kikohozi chenye Kutoa makohozi kinachodumu wiki (2 – 3)
• Homa inayodumu wiki mbili
• Kutokwa Jasho Usiku
• Kupungua Uzito

DALILI ZA MWISHO ZA KIFUA KIKUU (TB)


• Kikohozi chenye Damu
• Kupumua kwa Shida
• Maumivu ya Kifua
• Kuvimba kwa Tezi (Lymph Nodes)
• Kuvimba kwa Maungio (Joints)

Mwenye Hizi Dalili apelekwe Hospitali Mapema kwaajili ya Matibabu na kuzuia


Maambukizi Mapya kwenye Jamii.
NAMNA/JINSI YA KUJIKINGA NA KIFUA KIKUU

• Epuka kabisa Uvutaji wa Sigara.


• Epuka Mikusanyiko mikubwa ya watu mfano Stendi, Sokoni n.k.
• Tumia Vifaa vya Kujikinga Sehemu zenye Vumbi na Moshi hasa Viwandani mfano
Mask (Barakoa).
• Jizibe na kitambaa Safi wakati wa Kukohoa na Chafya.
• Osha Mikono vizuri na maji safi baada ya Kukohoa au Chafya kupunguza nafasi ya
Maambukizi.
• Kuwa na Tabia ya Kusafisha Vumbi hasa Nyumbani, Kazini n.k.
• Kula Chakula Chenye Ubora wa kuimarisha Mwili na kinga (Healthy Balanced Diet)
mfano Maziwa, Mboga za Majani, Maji Mengi, Samaki n.k.
• Wagonjwa wenye Upungufu wa Kinga mfano Ukimwi, Kansa, Kisukari, Wazee,
Watoto, washauriwa kufanyiwa Vipimo mara kwa mara ili kama kuna Maambukizi
yatibiwe mapema.
• Hakikisha Haukai Mbele ya Mtu yoyote anaekohoa au Kupiga chafya.

❖ Watoto huchomwa Chanjo (BCG)

You might also like