Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

MTIHANI WA PAMOJA WA GATUZI NDOGO

YA JOMVU/CHANGAMWE
Hati ya Kuhitimu Kisomo cha Sekondari

Jina: …………………………………………………….. Nambari ya Usajili: ………..

Sahihi: …………………………… Darasa: ……………….. Tarehe: ………………..

102/1
KISWAHILI
Karatasi ya 1
INSHA
Machi, 2024
MUDA: SAA 1¾

MAAGIZO:

a) Andika jina lako na nambari ya usajili kwenye nafasi ulizoachiwa hapo juu.
b) Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo
juu.
c) Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
d) Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
e) Kila insha isipungue maneno 400.
f) Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE


SWALI UPEO ALAMA
1 20
2 20
3 20
4 20
JUMLA 40

UKURASA WA 1
1. Lazima
Wewe ni katibu mkuu wa wizara ya kilimo. Mmefanya mkutano wa kuzungumzia
mikakati ya kupambana na baa la njaa nchini. Katika mkutano wenu, katibu mkuu wa
chama cha msalaba mwekundu amealikwa. Andika kumbukumbu za mkutano huo.

2. Kugatuliwa kwa huduma za matibabu kutoka serikali kuu kumeleta maumivu kuliko
tiba kwa wananchi. Jadili.

3.Tunga kisa kinachobainisha maana ya methali: Mbaazi ukikosa kuzaa husingizia jua.

4.Nilikuwa natazama Runinga ya Tupashe Habari, mara nikaona picha ya mtu ambaye
nilimfahamu… Endeleza

UKURASA WA 2
MWONGOZO WA KUTAHINI
1. Insha ya kumbukumbu
Vipengele muhimu vya kutahini
(a) Muundo
(b) Maudhui
MUUNDO
(i) Insha iwe na kichwa kinachotaja
a) Wanaokutana
b) Kiini cha mkutano
c) Mahali
d) Tarehe nawakati
Mwanafunzi azingatie mtindo wa uandishi wa kumbukumbu m.f:
 Mahudhurio
 Aorodheshe ajenda.
Baadhi ya maudhui.
i. Mafunzo ya njia bora za ukulima / njia za kiteknolojia.
ii. Wakulima kufadhiliwa na serikali kwa njia za mikopo, mbolea, mbegu n.k
iii. Kujenga mabwawa katika sehemu zinazoathiriwa na kiangazi ili yatumiwe kunyunyizia
maji.
iv. Maonyesho ya kilimo ili wakulima wajue namna mpya ya ukulima.
v. Wakulima kuhimizwa kukumbatia kupanda vyakula vinavyostahimili kiangazi; - mihogo,
viazitamu n.k
vi. Uhifadhi bora wa mavuno- maghala ya kuhifadhi vyakula vya nafaka.
vii. Chakula cha msaada kwa walioathiriwa.
viii. Ufadhili wa wataalamu ;mashirika kama KARI.
ix. Kuhimiza upanzi wa miti ili kuzuia mmonyoko wa udongo.
x. Kunadhifisha miundo misingi k.v barabara ili chakula kisafirishwe
xi. Mfumo wa kilimo biashara uhimizwe
xii.
2. Hii ni insha ya mjadala
Mtahiniwa ashughulikie hoja za kuunga na kupinga.
KUUNGA
i. Upungufu wa dawa hospitalini/zahanatini
ii. Upungufu wa wauguzi na madaktari katika hospitali na zahanati.
iii. Msongomano wa wagonjwa katika hospitali kuu.
iv. Vifo vinavyotokana na migomo ya wauguzi na madaktari.
v. Migomo ya madaktari na wauguzi.
vi. Upungufu wa wauguzi na madaktari wenye ujuzi wa kutumia vifaa vya kisasa vilivyo
katika gatuzi.
vii. Utata katika mkondo wa ugatuzi, mfano; mgao wa pesa kwa gatuzi
viii. Mazingira hasi kazini kwa madaktari na wahudumu wengine.
ix. Upungufu wa vifaa vya matibabu katika zahanati na hospitali.
KUPINGA
i. Kuajiriwa kwa madaktari na wauguzi.
ii. Kuongezewa mishahara kwa madaktari na wauguzi.
UKURASA WA 3
iii. Kununuliwa vifaa/ mitambo/ mashine za matibabu.
iv. Uhuru wa kujiunga na vyama vya kutetea wafanyikazi.
v. Uhuru wa kujiendeleza kitaaluma kwa madaktari na wauguzi.
vi. Uhuru wa kufanya kazi ya udaktari na uuguzi popote duniani.

3. -Hii ni insha ya methali.


-Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha maana ya methali hii.
-Zingatia sehemu mbili za methali.
-Watu wanaposhindwa kufaulu katika jambo huwalaumu watu wengine kwa makosa yao
wenyewe.
-Kisa kinaweza kuhusu:
(i) Mwanafunzi ambaye amekosa kufaulu katika mtihani mara nyingi huwalaumu walimu,
shule, ukosefu wa vitabu, wazazi ,n.k
(ii) Mkulima aliyekosa mavuno mazuri kwa sababu ya kuchelewa kulima au kupanda
kusingizia mvua, mbegu, n.k

Hakiki kazi ya watahiniwa

4. Hii ni insha ya mdokezo


-Sharti mtahiniwa abuni kichwa
-Sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa
-Mtahiniwa ana uhuru wa kutumia mbinu rejeshi-Mtahiniwa abuni kisa kitakachobainisha
kutokea mhusika aliyemfahamu runingani mf.Ushindi wa uchaguzi mkuu.
 Kuhusika katika ugaidi na kasha kuhukumiwa.
 Ushindi katika mtihani.

Sharti atunge kisa kinachomhusu mhusika aliyemwona runingani.

Mtahiniwa ana uhuru wa kueleza habari ya runinga na yaliyotokea baada ya kuona picha ya mtu
aliyemfahamu

UKURASA WA 4

You might also like