Taarifa PFC

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

TAARIFA YA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA MTAA WA ARUSHA CENTRAL 2023

Tunamshukuru Mungu wa mbinguni kwa ulinzi wake mkuu aliotulinda tangu


tulipomaliza kambi la mwaka 2022 hadi kutuwezesha kufikia katika kambi hili la
mwaka huu 2023. Jina la BWANA lipewe sifa.

MALENGO

 Usajili wa wanachama.
 Kuwa na maombi ya kufunga na kuomba
 Kujifunza Biblia kwa mpango na Roho ya unabii.
 Kufanya uinjilisti Pamoja na kugawa vitabu vya roho ya unabii vipatavyo 150/=
 Kuwa na mfuko wa chama
 Kuwa na madarasa ya chama Pamoja na kujifunza nishani.
 Kuwa na kwaya rasmi ya pfc
 Kuwa na kikosi rasmi cha gwaride.
 Kufanya PFC day mara 2 mwaka.
 Kutembelea na kuabudu Pamoja na kundi letu la kyoga Pamoja na makanisa
Jirani.(Kijenge sda church Pamoja na USA sda church).
 Kufanya Rally ya mafunzo ya siku 3 (mara 2 kwa mwaka)
 Kuhudhuria mikutano yote ya kanisa na kushiriki.(effort)
 Kuwa na sherehe za uvishaji pini za madarasa pamoja na nishani
 Kuhudhuria kambi la mafunzo ya vijana
 Kutoa huduma kwa jamii.
 Kufanya hiking
 Kufanya bonanza la michezo
 Kuwa na picknick Mbili kwa mwaka,

MAFANIKIO

1. Tumefanikiwa kusajjili wanachama 64 mwaka huu.


2. Tumefanikiwa kuwa na siku maalumu ya maombi ya kufunga na kuomba
mara 1 katika robo ya kwanza.
3. Tunaendelea na usomaji wa Biblia kwa mpango.
4. Tumefanikiwa kugawa vitabu katika shule ya winning spirit
5. Tumefanikiwa kuwa na kwaya rasmi ya pfc
6. Tumefanikiwa kufanya rally ya siku nne hapa kanisani ambapo jumla ya
wanachama 46 walihudhuria na kupata mafunzo mbalimbali.
7. Tumefanikiwa kuhudhuria kambi la mafunzo la vijana Ikungi Singida ambapo
jumla ya wanachama 35 walifanikiwa kuhudhuria kambi hilo

CHANGAMOTO
1. Baadhi ya Watoto kushindwa kuhudhuria katika vipindi vyetu vya jumapili
kutokana na ratiba mashuleni
2. Wanachama kutokuchangia ada za chama kwa wakati.
3. Watoto kutohudhuria vipindi kwa wakati siku za mafunzo.
4. Upungufu wa waalimu wa madarasa na nishani.
MAMBO AMBAYO TUNATAZAMIA KUTEKELEZA KABLA YA MWAKA
KUISHA

 Tunatazamia kufanya PFC day.


 Tunatarajia Kwenda kulitembelea kundi letu la kyoga.
 Tunatazamia Kwenda kutembelea makanisa yaliyopo nje ya mtaa wa
arusha central
 Tunatazamia kufanya uvishwaji wa pini kwa walio hitimu madarasa
yao.

SHUKRANI;
Tunamshukuru Mungu kwa kuwa Pamoja nasi katika kipindi chote hadi kufikia leo
hii.tunamshukuru mchungaji wetu wa mtaa na wazee wakanisa kwa umoja wao bila
kuwasahau wazazi wote kwa Pamoja tunasema MUNGU awabariki.

You might also like