Professional Documents
Culture Documents
Grade 5 Kisw Sehemu A Nakala Ya Mwalimu-R, Pd&Vi
Grade 5 Kisw Sehemu A Nakala Ya Mwalimu-R, Pd&Vi
KISWAHILI
SEHEMU A
Zoezi la 1 na la 2
Gredi ya 5
NAKALA YA MWALIMU
Maagizo ya jumla
1. Mwalimu awafahamishe wanafunzi wote kwamba mazoezi yote katika sehemu hii
yatakuwa tathmini ya ana kwa ana. Kila mwanafunzi atakuwa na zamu yake ya
kutathminiwa; mmoja baada ya mwingine.
2. Mwalimu awafahamishe wanafunzi wote kwamba karatasi hii ina mazoezi matatu:
i. Mazungumzo ya ana kwa ana
ii. Ufahamu wa Kusikiliza
iii. Kusoma kwa Sauti
3. Mwanafunzi aandaliwe kiti au dawati kutazamana na mwalimu.
4. Mwalimu atangulize kila zoezi na amfahamishe mwanafunzi matarajio ya kila zoezi.
5. Mwalimu amfahamishe mwanafunzi kukamilika kwa kila zoezi.
6. Mwalimu atathmini umilisi wa mwanafunzi kwa mujibu wa mwongozo wa kutathminia
pamoja na kuweka rekodi.
Mbuni ni ndege mkubwa sana. Mbuni ndiye ndege mkubwa zaidi ulimwenguni. Ndege huyu
anaweza kukua hadi kufikia uzito wa kilo mia moja arubaini. Ana miguu mirefu na shingo ndefu.
Ni ndege mwenye mbio za ajabu. Anaweza kukimbia kwa kasi ya kilomita sabini kwa saa moja;
utadhani ni gari. Hata hivyo, mbuni hawezi kupaa juu kama wafanyavyo ndege wengine.
Mbuni ana manufaa mengi. Yeye hutaga mayai makubwa ambayo huliwa. Nyama yake vile vile
ni chakula. Aidha, mbuni huwavutia watalii ambao huleta pesa za kigeni nchini.
Ukija kwetu utaona picha maridadi ya mbuni kwenye ukuta sebuleni. Picha hiyo nimeichora
mimi mwenyewe. Niliichora baada ya kumwona mbuni tulipozuru mbuga ya wanyama ya
Maasai Mara. Hakika mbuni ni ndege anayependeza.
7. Kama ungezuru mbuga ya wanyama ya Maasai Mara unadhani ungeona ndege yupi
mwingine?
(Mwanafunzi ajibu)
50
Mbali na mapambo ya kuvaliwa, kuna yale ya kujipaka. Katika kundi hili, kuna poda
60 70
na wanja. Mtu hujipaka poda usoni na wanja machoni. Hina nayo hupakwa
80
Ni muhimu kutumia mapambo haya kwa namna ambayo inafaa. //Usijipambe kupita
90
kiasi ukauharibu urembo wenyewe. Huna budi kujihadhari usije ukatumia mapambo
100
ambayo yanaweza kudhuru ngozi yako. Ukifanya hivyo utakuwa umejiletea hasara.
107