Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

1

SHEMASI WILBARD NDESOMA -HISTORIA BINAFSI (14/06/2024).

Nilizaliwa mnamo 07/02/1991 katika hospitali ya Huruma (Mkuu -Rombo), kama mtoto wa
kwanza kati ya watoto wawili (wote wa kiume) katika familia ya baba Alfred Wilbald Ndesoma
Moshi na mama Radegunda John Tesha Sumni wa Kingachi Usseri, ambao walibariki ndoa
takatifu katika Kanisa Katoliki Chang’ombe Dar- Es -Salaam. Nilipewa Sakramenti ya ubatizo
katika Kanisa la Mt Yohane Mbatizaji (Parokia ya Usseri) mwaka 1992 ambapo nilipewa jina
(Majina) Wilbard (la ubatizo) na Ndesoma (jina la pili) ambayo yote yanaendana na majina ya
babu mzaa baba.

Nilianza kusoma shule ya awali na baadaye msingi katika shule ya Msingi Usseri maarufu kwa
jina (Eliee) ambako nilihitimu elimu ya shule ya Msingi (darasa la saba) mwaka 2006. Nikiwa
darasa la nne nilikuwa najihusisha na utumishi wa altareni. Nikiwa darasa la tano, siku moja
baada ya Misa ya kwanza Padre (msadizi wa Paroko wakati huo) aliniuliza kama ninatamani
kuwa padre nikamjibu ndio. Basi akaniambia kuwa kesho yake nije na mzazi kwa maonano.
Kesho yake nikafika na mama kwani baba alikuwa ameshafariki (04/04/2003) na tukaenda
kumwona Padre baada ya misa ya kwanza. Wakili paroko akamwambia mama kuhusu nia
yangu na akamwambia kuwa nitakapomaliza darasa la saba aniwezeshe kwenda Seminari. Kwa
msaada wa Mungu baada ya kuhitimu darasa la saba na baada ya kuandaliwa na Padre Sixtus
Kessy na hatimaye usaili na mtihani wa kuandika, tar 06/12/2006 nilijiunga na Seminari ndogo
ya Mitume wa Yesu Uru kwa maandalizi ya kidato cha kwanza (pre-form one orientation).
Januari mwaka 2007 nikaanza rasmi malezi yakiwemo ya kitaaluma ya elimu ya sekondari (O-
level) amabko nilihitimu mwaka 2010. Mama alikuwa ananipatia mahitaji muda wote nikiwa
katika masomo ya sekondari. Nikiwa nasubiri matokeo nikajiunga na chuo cha mafunzo ya
ufundi stadi cha Mtakatifu Yosefu, Boma Ngombe- Hai, kupata uzoefu wa kutumia kompyuta.
Mwaka 2011 nilijiunga na sekondari ya Mzumbe Morogoro nilikopangwa na serikali kwa
masomo ya kidato cha tano na sita ambako nilihitimu mwaka 2013. Wakati nasubiri matokeo
ya kidato cha sita nikawa niko nyumbani nikimsaidia mama ambaye alikuwa akisumbuliwa na
maradhi. Matokeo yalipotoka nikaenda hospitalini Huruma alikokuwa amelazwa mama
kumfahamisha kuhusiana nayo na nia yangu ya kujiunga na Seminari kuu na akaridhia. Wakati
huo nilikuwa pia nasaidia kazi Parokiani Usseri hadi nilipokwenda Nairobi Kenya kwenye
nyumba ya malezi ya Shirika la wamisionari wa Mariannhill kwa wiki moja, kwa ajili ya kuona
wanavyoishi (come and see) na baadae usaili wa kujiunga nao. Baada ya usaili nilikata tamaa
kuwa sitachukuliwa na sikurudisha fomu ya kujaza nikaondoka nayo kama ukumbusho na
nikajiambia kwamba nimefanikiwa tu kuvuka nje ya Tanzania kwa mara ya Kwanza. Nikiwa
2

Parokiani, frateri mmoja ambaye alikuwa anafuatilia Kwenda kwangu kwenye usaili
akanishauri nijaze fomu na ikatumwa Nairobi. Cha kushangaza miezi michache baadaye
nikapokea barua ya kutaarifiwa kuchaguliwa kuanza malezi kwa hatua ya uaspiranti katika
Shirika la wamisionari wa Mariannhill ambako nilianza tar 10 January 2014 kwa miezi sita.
Baada ya Uaspiranti mwezi Agosti 2014 nikaanza mafunzo ya falsafa katika chuo cha
Konsolata (Consolata Institute of Philosophy). Nikiwa mwaka wa kwanza wa falsafa (2015)
katikati ya mitihani ya muhula wa kwanza, mama alitutoka. Nikaendelea na masomo Tar 05/05
/2017 nilihitimu stashahada ya falsafa na mafunzo ya dini katika chuo cha Konsolata. Baadaye
mwezi Novemba 2017, nikatunukiwa shahada ya falsafa katika chuo cha Kikatoliki cha Afrika
Mashariki (Catholic Institute of Eastern Africa-CUEA) ambako Chuo cha Konsolata
kilijiambatanisha kwa wakati huo baada ya uliokuwa uhusiano wake wa muda mrefu na Chuo
cha Urbaniana kusitishwa. Baada ya kuhitimu masomo ya falsafa (nikiwa kama mkandidati)
Pamoja na wenzangu wawili tukaingia hatua ya upostulanti kujiandaa na hatua ya Novisiati.
Miezi mitatu ya kwanza tulikua katika nyumba ya malezi katika eneo la Kalimoni au Juja Farm
katika Kaunti ya Kiambu nchini Kenya na ni sehemu ya Jimbo Kuu la Nairobi. Baadaye mimi
na wenzangu tukatumwa Tanzania kwa uchungaji mfupi katika Maparokia tatu ambazo
tulikuwa tukibadilishana kila baada ya mwezi mmoja. Mimi nilianzia Parokia ya Maria
Magdalena -Kimara-Mtoni, nikaenda Parokia ya Mt Laurenti-Longido katika Jimbo Kuu la
Arusha na nikamalizia Parokia ya Mt. Fransisco wa Assisi-Kidoka katika Jimbo la Kondoa
kwa utaratibu huo wa kupishana na mafrateri wenzangu wawili. Mwaka 2018 mimi na
wenzangu tulitumwa Novisiati Mariannhill Afrika Kusini katika makao yetu ya asili ya Shirika
ambako tuliungana na wenzetu nane kutoka sehemu nyingine. Ilipofika tarehe 02/02/2019
tukamaliza hatua ya novisiati kwa kuweka nadhiri za mwanzo katika Shirika la wamisionari
wa Mariannhill. Baada ya kuweka nadhiri sote tulipata uhamisho kutoka Makao Makuu ya
Shirika Roma. Mimi na mwenzangu mmoja tulihamishiwa Provinsiali ya Mariannhill. Kabla
ya uhamisho nilikuwa nikihesabiwa kuwa natoka katika Kanda ya Shirika ya Afrika Mashariki.
Tarehe 02/02/2022 niliweka nadhiri za daima na Novemba mwaka huo huo nilihitimu masomo
ya taalimungu katika chuo cha Mtakatifu Yosefu kilichopo Cedara, Pietermaritzburg-Kwa
Zulu Natali, Afrika Kusini. Baada ya kuhitimu nikawa nafanya Utume mfupi Parokiani (Mt
Yosefu-Richmond). Tarehe 05/05/2023 nilipewa Daraja ya Ushemasi Katika Kanisa la
Monasteri ya Mariannhill nikiwa na mwenzangu mmoja ambaye tulikuwa tumepata uhamisho
unaofanana baada ya hatua ya Novisiati. Tar 08/05/2024 niliwasili Misioni ya Mt Yosefu-
Richmond ambako nilitumwa kusaidia Parokiani. Mwezi mmoja baadaye niliteuliwa kuwa
Mkurugenzi wa wakandidati katika nyumba ya Shirika ya ukandidati katika eneo la Shirika
3

karibu na Parokia hiyo hiyo. Hadi natuma maombi ya kupatiwa Daraja ya Upadrisho kwa Mkuu
wa Shirika huo ndio umekuwa utume wangu. Katika safari yangu ya wito nimepitia milima na
mabonde lakini namshukuru Mungu kwa uaminifu wake na Neema zake kwangu kwani
hakuwahi kuniacha. Nashukuru wazazi, walezi (walei na wale wa maseminarini nilikopitia
malezi), walimu wakiwemo mapadre (hasa maparoko niliofanya utume kwao), wanashirika
wamisionari wa Mariannhill na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika safari
yangu ya wito. Aidha ningependa kumshukuru Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar-
Es- Salaam, Mha Juda Thaddaeus Ruwa’ichi, kwa kuridhia mimi kujiunga katika upadrisho wa
tar 06/07/2024.

You might also like