Adhabu 1

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 14

Adhabu

Adelheid Marie Bwir


Bwiree
Kiswahili
Siku moja mamangu
alinunua matunda aina
tofauti.

1
Mimi na ndugu zangu
tulijiuliza, "Mama
atatugawia wakati gani?"

2
Baadaye, kakangu, Rahim,
alijificha na kuyala
matunda yote!

3
Mimi na ndugu yangu
tulipogundua, tulisema kwa
hasira, “Rahim ni mtukutu
na mchoyo. Lazima
aadhibiwe.”

4
Mama alikasirika sana
alipogundua kwamba
matunda yote yalikuwa
yameliwa.

5
Mimi na ndugu yangu
tulimwangalia Rahim kwa
ukali.

6
Mimi nilimwuliza mama,
"Utamwadhibu Rahim?"

7
Baadaye, Rahim alipata
adhabu asiyoitarajia.

8
Hakuweza kutulia!

9
Mama alipomwuuliza
alijibu kwa sauti ya chini,
“Naumwa na tumbo.”

10
Sote tuliona kwamba hiyo
ilikuwa adhabu mbaya
kuliko kama Rahim
angechapwa na mama.

11
Alipopata nafuu, Rahim
alituomba msamaha.

Aliahidi kuwa hangeiba


tena.

12
Adhabu
Writer: Adelheid Marie Bwir
Bwiree
Illustr
Illustration:
ation: Melany Pietersen
Language: Kiswahili

© African Storybook Initiative and Molteno Institute, 2014

This work is licensed under a Cr Creativ


eativee Commons A Attribution
ttribution
(CC-B
(CC-BY Y) V
Version
ersion 3.0 Unpor
Unportedted Licence
Disclaimer: Y You
ou ar
aree fr
free
ee tto
o download, cop
copyy, tr
translate
anslate or adapt this st
stor
oryy and use the
illustr
illustrations
ations as long as yyou ou attribute or cr
credit
edit the original author/s and illustr
illustrat
ator/s.
or/s.

You might also like