Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

Ebenezer Christian Center, Maswa


S.L.P 199 Maswa, Simu: 0767220644, Email: maswa.tag@gmail.com

KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO TZ 0176

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

NAFASI: MRATIBU WA KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO (PROJECT COORDINATOR)

KITUO CHA KAZI: TAG EBENEZER CHRISTIAN CENTER – MASWA MJINI, SIMIYU.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G), Ebenezer Christian Center liliolpo wilayani Maswa
Mkoa wa Simiyu limekuwa likitoa huduma kwa watoto wanaotoka kwenye kaya maskini kupitia
kituo cha Huduma ya maendeleo Jumla ya Mtoto (Holistic Child Development Ministry) kwa
kushirikiana na Shirika la Compassion International Tanzania (CIT). Kanisa kupitia Program za
maendeleo jumla ya mtoto linalenga kuwafungua watoto katika umaskini kwenye maeneo ya Kiroho,
Kiuchumi, Kijamii na Kimwili (ambao ndio ujumla wa mtu), kwa shabaha ya kuwawezesha wawe
watu wazima wanaojua wajibu wao na wanaojitosheleza. Mchungaji kiongozi, anakaribisha maombi
kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wakujaza nafasi tajwa hapo juu.

1. SIFA ZA MUOMBAJI:

Sifa/elimu/ujuzi wa Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana.


Awe Mkristo aliyeokoka na kujitoa kwa Bwana Yesu; mwenye maisha ya Ushuhuda ya
kila siku. Mwenye moyo wa kujitoa, kutumika kanisani na mpenda maendeleo,
anayependa kufanya kazi na watoto na vijana kutoka katika mazingira magumu.
Awe na Shahada ya Kwanza (kutoka kwenye chuo kinachotambulika/kukubalika na
Serikali).
Awe na Elimu pamoja na uzoefu (wowote) katika maeneo ya Uongozi/utawala,
Usimamizi wa Miradi, Uhamasishaji wa rasilimali na Uongozi, Usimamizi wa biashara,
Maendeleo ya jamii, Maendeleo ya watoto, Theolojia, Ualimu au Sosholojia.
Awe na moyo wa kuwapenda watoto, na kutumika kanisani.
Awe na uwezo wa kuongea, kusoma, na kuandika kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili
kwa ufasaha. Asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la unyanyasaji wa mtoto.
Awe na uwezo na elimu ya kutumia kompyuta hasa program kama ‘Micro-soft office’
(Word, Excel, Power Point) na Internet Access.
Awe na umri kuanzia miaka 25 na asizidi miaka 45
Awe tayari kuabudu hapa kanisani ambapo huduma ipo.

WAJIBU WA MRATIBU WA KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO;

Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Mtoto na ni mwajiriwa wa kanisa. Katika utendaji wake wote wa
majukumu /wajibu atawajibika moja kwa moja kwa Mchungaji kiongozi na kusimamiwa na Kamati
ya huduma ya mtoto kwa kushirikiana na Huduma ya Mtoto ya Compassion International Tanzania
(CIT).

KAZI MUHIMU NA WAJIBU WA MRATIBU WA KITUO NI KAMA IFUATAVYO;


i. AtamshuhudiaYesu Kristo kwa uaminifu na kuwa mtetezi wa watoto na vijana.
ii. Atasimamia utendaji wa watenda kazi wengine katika kufanikisha shughuli za maendeleo
ya ujumla ya mtoto na kijana.
iii. Atasimamia maono ya maendeleo ya ujumla ya mtoto na kijana na mali za huduma wakati
wote wa Uhai wa kituo cha Huduma ya Mtoto.
iv. Kuandaa mpango wa mwaka wa mshirika-mwenza wa kituo cha maendeleo ya mtoto na
kijana kwa kushirikiana na wadau wote na kuwasilisha kwa Kamati ya Huduma ya Mtoto
kwa uthibitisho na kuidhinishwa na uongozi wa kanisa.
v. Kuingiza na kusimamia utekelezaji wa mpango wa mshirika-mwenza kama
ilvyoidhinishwa Kwenye mfumo wa Compassion Connect.
vi. Kujaza taarifa za mahudhurio za mlengwa mmoja mmoja katika mfumo wa taarifa wa
Compassion (Compassion Connect)
vii. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za watenda kazi wengine na watu wanaojitolea
katika Kituo cha maendeleo ya mtoto na kijana.
viii. Kuwasilisha taarifa ya kimaandishi ya utendaji na maendeleo ya kituo kwa kamati, uongozi
wa kanisa na huduma ya Compassion International Tanzania kama itakavyotakiwa kwa
pande zote husika.
ix. Kuhakikisha ripoti zote za Watenda kazi wengine zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa
wakati na ubora unaotakiwa.
x. Kuhakikisha kuwa taarifa zote za fedha na watoto zinatunzwa vizuri na kuhuishwa kila
mara zinapohitajika.
xi. Kutunza kitabu cha hundi cha Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana na kupitisha
malipo yote sambamba na maelekezo yaliyotolewa na kamati ya Kituo na kulingana na
miongozo ya kifedha ya Ushirika wenza.
xii. Kushiriki katika zoezi la usaili wa kuwapata Watenda kazi wengine wote wa Kituo kwa
kutoa maoni ya kitaalamu kuhusu nafasi hizo.
xiii. Kuhakikisha mazingira ya Walengwa kituoni ni salama kwao kujifunza na kushiriki katika
program zote za kituo.
xiv. Kusimamia na kuwa mwangalizi mkuu wa utekelezaji wa mitaala yote inayotumika
kituoni.
xv. Kusimamia shughuli zote za ufundishaji na waalimu wa walengwa.
xvi. Atakuwa miongoni mwa walimu wa walengwa
xvii. Kuandika Maandiko mbalimbali na kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika
jamii kwaajili ya mahitaji mbalimbali ya watoto, wazazi na kituo kwa ujumla.
xviii. Kuhamasisha upatikanaji wa raslimali za ndani kwaajili ya miundombinu inayohitajika
kwa walengwa kujifunza.
xix. Kutathmini maendeleo ya watendakazi wengine wa Kituo cha Huduma ya Mtoto na
kuwasilisha maoni yake kwa kamati ya kituo.
xx. Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kiroho, kiafya, kielimu na kijamii ya mlengwa mmoja
mmoja aliye katika programu.
xxi. Kutembelea walengwa mashuleni na nyumbani na kuchukua hatua stahiki pale inapobidi.
xxii. Atawajibika kwa matokeo tarajiwa ya walengwa, viashiria vya utendaji na matokeo ya
ukaguzi, kwa mujibu wa mwongozo.
xxiii. Kuhakikisha walengwa wote wanaaandika barua kwa wafadhili wao kwa wakati na
viwango vinavyotakiwa.

xxiv. Kuhakikisha kuwa taarifa zote za watoto na Kanisa zilizoko katika mfumo wa taarifa wa
Compassion connect ni sahihi na zimehuishwa.
xxv. Kuhakikisha zawadi zilizotumwa na wafadhili zinawafikia walengwa kwa wakati na kwa
asilimia mia moja.
xxvi. Kushiriki katika mafunzo yanayoandaliwa kwaajili ya huduma ya mtoto na vijana.
xxvii. Kuwasaidia watenda kazi wengine wa Kituo na kushirikishana wajibu wao pale
inapohitajika. Hii ni pamoja na kuhakikisha watenda kazi wapya wanajua majukumu yao
katika Kituo cha huduma ya mtoto.
xxviii. Kutoa taarifa kwa kamati ya Huduma ya Mtoto, juu ya ubadhilifu wa fedha au tabia
isiyoridhisha kwa mmojawapo wa Watenda kazi wengine wa Kituo.
xxix. Kuhakikisha watoto walioandikishwa katika Kituo kwaajili ya ufadhili ni wale tu
wanaokidhi vigezo vilivyowekwa katika Ushirika-wenza.
xxx. Kuendesha vikao vya watenda kazi mara moja kwa mwezi au zaidi pale inapobidi.
xxxi. Kushiriki kikamilifu ibada za kila siku asubuhi pamoja nawatenda kazi wote kabla ya
kuanza kazi.
xxxii. Kuratibu vikao na mafunzo kwa wazazi kwa kushirikiana na uongozi wa Kanisa pamoja na
kamati ya wazazi kwa lengo la kuhamasisha watu hao kuhusika na maendeleo ya watoto.
xxxiii. Atafanya kazi nyingine za kiofisi kama atakavyopangiwa na uongozi wa kanisa.

Namna ya kutuma maombi:

Waombaji wenye sifa watume maombi yao kabla ya tarehe 15/8/2019 kwenye anuani zilizopo
hapo chini. Kila mwaombaji aambatanishe barua ya maombi pamoja na CV, nakala za vyeti vya
taaluma, Cheti cha kuzaliwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wa kanisa analoabudu.

Tuma maombi yako kwa anuani ifuatayo:


Mchungaji kiongozi,
Kanisa la TAG, Ebener Christian Center
S. L. P 199,
Maswa - Simiyu
Email: maswa.tag@gmail.com

You might also like