Professional Documents
Culture Documents
Fani Ya Fasihi Simulizi Kwa Shule Za Upili 0195736540 9780195736540
Fani Ya Fasihi Simulizi Kwa Shule Za Upili 0195736540 9780195736540
|i
|
j
wi
wa aa
wi
UTA
TAA AUA
WA AA WA ADI wa
Wa KA
UA
WA Wa ai
Kaa
Wa
WA
YA
EA
ai
VYA KATAA
Fani ya
Fasihi
kwa shule za Upili
Assumpta K. Matei
OKFORD
UNIVERSITY PRESS
OKFORD
UNIVERSITY PRESS
Published in Kenya by
Ozford University Press East Afri
ca Limited, The Osford Place,
Elgon Road, Upper Hill, PO Bos
72532-00200, Nairobi, Kenya
|
” OAssumpta K. Matei 2011
14 15 16 17 18 19 20
15 14 13 12
Printed in Kenya by
Icons Printers Ltd, PO Bos 3927
3-00623, Nairobi, Kenya
Photographs/Illustrations by OUP
Library
Assumpta K. Matei
Kenya High School, Nairobi
Juni, 2010
Maana na Dhima ya Fasihi
Utangulizi
Fasihi ni sanaa ambayo hutumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha masuala kuhusu maisha
ya binadamu na mazingira anamoishi. Fasihi huweza kuandikwa au kusimuliwa.
Maana ya sanaa
Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha hisia na fikira za binadamu.
Sanaa huwasilishwa kwa mbinu kama vile maandishi,
matamshi, michoro, uchongaji, ususi, ufumaji na ufinyanzi.
Sanaa ni zao la mikono na akili ya mtu na kwa kawaida
huwa na umbo au sura dhahiri. Tunaposema kuwa sanaa
ina umbo dhahiri ina maana kuwa sanaa huchukua maumbo
yanayobainika. Ushairi, kwa mfano, ni utanzu wa sanaa ya
fasihi ulio na umbo dhahiri la beti zilizo na mishororo. Vinyago
na vyungu ni maumbo ya sanaa ya uchongaji na ufinyanzi
mtawalia.
Ufinyanzi
Tofauti kati ya fasihi na sanaa nyingine
(a) Fasihi hutumia lugha kama malighafi ya kuelezea fikira za binadamu. Sanaa nyingine
hazitumii lugha. Mfinyanzi, kwa mfano, hutumia udongo kufinyanga vyungu na
mchongaji hutumia kipande cha mti au jiwe kuchongea vinyago. Fasihi hutumia
lugha yenye mvuto na mguso wa kipekee. Tanzu na vipera vya fasihi hutumia lugha
ya kitamathali kama vile nahau, misemo, misimu, lakabu, kinaya na dhihaka.
(b) Fasihi, tofauti na sanaa nyingine, hujikita katika mazingira au muktadha wa mahali,
wakati na hali maalumu. Kuna methali, nahau na misimu ambayo hujikita katika
mazingira ya shambani. Pia kuna riwaya, mashairi na tamthilia ambazo zinaonyesha
migogoro ya kijamii. Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya Said A. Mohammed,
ni mfano wa tamthlia inayojikita katika mazingira ya jamii ya Waswahili na kusimulia
migogoro iliyojitokeza kati ya vijana na wazee wa jamii hiyo. Mazingira ya kazi ya
kifasihi huweza kuwa ya kubuni au ya kweli. Kinjeketile nayo ni mfano wa tamthilia
Oo
inayojikita katika mazingira ya ukweli. Inasawiri mapambano kati ya Watanzania na
Wajerumani na vita walivyopigana katika enzi za ukoloni.
(c) Fasihi ni sanaa tendi. Fanani (mwasilishaji wa fasihi simulizi) anaweza kuigiza yale
anayowasilisha na pia akashirikisha hadhira yake kwa kuigiza. Pia hadithi katika riwaya
na tamthilia huweza kuigizwa. Sanaa nyingine, kama vile ufinyanzi na uchongaji,
haziigizwi.
(4) Fasihi hutumia wahusika kuwasilisha maudhui. Ngano, riwaya, tamthilia, baadhi ya
mashairi na hadithi fupi ni mifano ya kazi zinazotumia wahusika kuwasilisha maudhui.
Sanaa nyingine, kama vile uchongaji, ni maumbo yanayomithilisha watu, hali na vitu
mbalimbali katika jamii.
(e) Fasihi huwasilisha ujumbe kwa kutumia maudhui na fani pamoja, tofauti na sanaa
nyingine ambazo hutumia sura au maumbo ya vitu.
Kutokana na misingi hii, ni wazi kwamba fasihi ina dhima kubwa katika jamii:
(b) Fasihi hueneza itikadi zinazotawala jamii husika. Methali na vitendawili ni mifano
ya semi ambazo hutumiwa kutilia nguvu itikadi fulani kwa kuzipitisha kutoka kizazi
kimoja hadi kingine. Fasihi pia inaweza kupinga itikadi zinazotawala, ikachukua
msimamo wa kuwatetea wanyonge. Vipera vya fasihi, kama vile nyimbo, hutumiwa
kueneza propaganda za kisiasa na kupinga utawala dhalimu. Katika fasihi andishi,
maandishi mengi yamepinga ukandamizaji wa wanyonge na kueneza siasa za
ukombozi. Baadhi ya kazi za aina hii ni pamoja na tamthilia ya Kinjeketile, ambayo
pamoja na kupinga unyonyaji wa mabepari kwa tabaka la wafanyakazi, inawachochea
kuungana kupigania uhuru wao wakiongozwa na Kinjeketile mwenyewe.
(c) Fasihi hupumzisha, huburudisha na huliwaza. Nyimbo za kazi husaidia kupunguza
hisia za uchovu. Aidha, usomaji wa riwaya, tamthilia na mashairi hupumzisha akili
na kuiliwaza. Vivyo hivyo, watu wanapotazama michezo ya kuigiza huchangamka na
kujisahaulisha kwa muda matatizo yao.
(d) Fasihi huhifadhi na kurithisha maarifa au elimu ya jamii. Fasihi simulizi na andishi
huhifadhi maarifa ya kijamii na kuyapitisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kupitia
kwa tungo, kama vile nyimbo na vitabu (riwaya, ushairi, tamthilia na hadithi fupi),
maarifa hupitishwa kwa wanajamii. Amali za jamii (mila, imani, historia) na sherehe
za kijadi (jando, matambiko, ibada na sherehe za kutawazwa) huhifadhiwa katika
tanzu na vipera vya fasihi simulizi na andishi na kupitishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine.
(e) Fasihi husaidia kukuza lugha. Lugha ndiyo malighafi ya fasihi. Kila fanani au mwandishi
ana upekee wake wa matumizi ya lugha. Kadiri lugha inavyotumiwa na fanani na
waandishi mbalimbali, ndivyo nayo inavyofinyangwa upya na kupevuka, na hivyo,
matumizi yake kupanuka. Halikadhalika, misimu inapokubalika kama semi katika
lugha hukuza lugha kwa kuiongezea msamiati. Maneno yaliyokuwepo katika lugha
hupewa maana mpya.
(f) Fasihi humwezesha binadamu kujenga tabia ya kudadisi na kutafakari kuhusu
Masuala yanayomkumba. Katika kusoma kwa makini na hata kuhakiki kazi za
kifasihi kama vile riwaya, hadithi fupi na tamthilia, pamoja na tanzu za fasihi
Simulizi za ngano, semi na vipera vyake, binadamu huimarisha mazoea ya kusoma
o
na kuchunguza makala mbalimbali. Aidha, mtu hupanua mawazo yake na kuweza
kutathmini mambo kwa mitazamo mbalimbali.
Fasihi huhamasisha wanajamii kuhusu masuala ibuka na nyeti katika jamii yao. Kwa vile
fasihi husawiri mambo yanayoathiri jamii mahususi, msomaji, mtazamaji ama msikilizaji
wa kazi ya fasihi hufahamishwa kuhusu mambo mapya au yaliyozuka. Ngomezi, kwa
mfano, ilitumiwa kuarifu watu kuhusu tukio jipya kama kuwepo kwa wavamizi, kifo au
kualika kwenye sherehe.
(h) Fasihi huadilisha. Fasihi hufunza tabia njema inayokubalika na jamii. Huasa jamii dhidi
ya matendo hasi na kudumisha maingiliano mema pamoja na hulka zinazokubalika.
Methali nyingi, kwa mfano, huonya dhidi ya matendo maovu kwa nia ya kukuza
maadili.
(i) Tamaa mbele mauti nyuma - huonya dhidi ya tamaa.
(ii) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu —- huhimiza bidii.
(iii) Ndugu mui heri kuwa naye — huhimiza udugu.
Hadithi za kimapokeo pia hutumiwa kufunza maadili. Mathalani, ngano za mhusika fisi
huonya dhidi ya tamaa. Ngano za kiayari nazo huonya dhidi ya ulaghai, usaliti, ujinga
au utegemezi. Katika novela Kipendacho Roho ya Pauline Kyovi, Nyanya anawahadithia
wajukuu wake hadithi ya Kadzo na Mazimwi ili kuwaonya dhidi ya kuhadaiwa kuhusu
mapenzi na ndoa. Hadithi hii pia inawaonya dhidi ya kuwaamini watu wasiowafahamu.
(Gi) Fasihi huunganisha na kuibua hisia za kizalendo au utaifa. Kupitia kwa nyimbo za
kisiasa kama vile wimbo wa taifa, kwa mfano, wanajamii huhamasishwa kuungana
pamoja na kuitetea na kuijenga nchi yao. Ufuatao ni mfano wa wimbo unaohimiza
uzalendo:
Wimbo huu unalenga kuibua hisia za kizalendo. Mifano ya tungo zenye dhima hii
huweza kupatikana katika tamthilia, riwaya na vipera vingine vya fasihi.
Na Fasihi huhifadhi historia ya jamii. Tanzu kama vile visakale na visasili hueleza historia
au asili ya jamii na mambo au vitu vinavyopatikana katika jamii hiyo. Tanzu za fasihi
andishi pia huhifadhi historia ya jamii kimaandishi. Mathalani, tamthilia ya Kinjeketile
ni hifadhi ya vita vya Majimaji nchini Tanzania (1905 — 1907) na hali ilivyokuwa chini
ya utawala wa Kijerumani.
mai
(k) Fasihi hupumbaza. Fasihi bora ni ile inayoathiri hisia za binadamu. Fasihi huweza
kuchekesha na kuliza wakati mmoja. Watu wanapotazama au kusoma kazi fulani ya |
fasihi, huathirika na hata wakalia.
Makundi ya fasihi
Fasihi imegawanywa katika makundi mawili makuu kulingana na jinsi inavyowasilishwa
na kuhifadhiwa.
1. Fasihi simulizi
Hii ni fasihi ambayo hubuniwa na kuhifadhiwa akilini. Fasihi simulizi huwasilishwa na
kusambazwa kwa masimulizi, mazungumzo ya kisanaa, kuimba, kughani, kuigiza na
kukariri kwa hadhira hai. Fasihi simulizi imegawika katika tanzu zifuatazo: hadithi,
semi, ushairi, maigizo na mazungumzo.
2. Fasihi andishi
Fasihi andishi ni fasihi ambayo huhifadhiwa katika maandishi na kusambazwa kupitia
kwa maandishi. Fasihi andishi imegawanywa katika tanzu zifuatazo: riwaya, tamthilia,
ushairi, novela, hadithi fupi na hadithi za watoto.
o
kuvitegua papo hapo. Kwa upande mwingine, fasihi andishi kwa kawaida huwasilishwa
kupitia kwa maandishi. Mwandishi wa riwaya hana fursa ya kuonana na wasomaji wa
riwaya yake ana kwa ana.
(c) Hadhira ya fasihi simulizi ni tendi. Huchangia katika uwasilishaji kwa kuuliza na kujibu
maswali, kuimba ama kucheza na kupiga makofi kwa kushangilia. Huonyesha taathira
ya utungo utaowasilishwa kwa hisia zao kwa kucheka au kuhuzunika. Katika ngoma
ama utegaji na uteguaji wa vitendawili, hadhira ni washiriki. Hadhira ya fasihi andishi
kwa upande mwingine haiwezi kuwa tendi (ni tuli). Haiwezi kumwuliza mwandishi
maswali wala haiwezi kushiriki wakati mwandishi anapoandika. Hadhira hushirikishwa
katika kusoma kurasa za kitabu zilizokwisha kuandikwa.
(d) Hadhira ya fasihi simulizi ni pana kuliko ya fasihi andishi. Fasihi simulizi huweza
kupokewa na hata wale wasiojua kusoma na kuandika. Fasihi andishi huwafikia tu
wale wanaojua kusoma na kuandika.
(e) Fasihi simulizi ni mali ya jamii. Haimilikiwi na fanani mahususi, tofauti na fasihi
andishi ambayo ni mali ya mwandishi au waandishi binafsi. Visasili huhusishwa na,
jamii wala si mtu binafsi, ilhali riwaya au tamthilia ni mali ya mwandishi na ndiye
mmiliki wa maandishi hayo.
(£) Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilika kimaudhui na kimtindo kutegemea
hadhira kuliko fasihi andishi. Fanani anaweza kubadilisha mtindo wa uwasilishaji,
badala ya kukariri, anaweza kuimba shairi. Anaweza kurahisisha lugha na kubadilisha
baadhi ya maudhui, akaongeza mengine ama kuyapuuza mengine. Msanii wa fasihi
andishi hana nafasi ya kuifanyia mabadiliko kazi yake baada ya kuchapishwa hadi pale
toleo jipya la kazi hiyo litakapotolewa. Kwa vile hakabiliani ana kwa ana na hadhira
yake, hawezi kujua maoni yao, hivyo hawezi kujirekebisha moja kwa moja.
(g) Yaliyomo katika fasihi simulizi huweza kusahaulika kwa urahisi, yakafisidiwa au
yakavurugika. Kwa sababu ya kuhifadhiwa ubongoni na kupitishwa kwa mdomo,
kudumu kwake hutegemea kumbukumbu ya wasanii mbalimbali. Pia, fanani anaweza
kufa au akarukwa na akili au hata akasahau mtiririko wenyewe. Ikiwa msanii atasahau
au kurukwa na akili, yaliyomo katika utungo asilia huenda yasidumu; yatabadilika.
Fasihi andishi ina uwezo zaidi wa kudumu kwani imehifadhiwa katika maandishi
ambayo huweza kusomwa na vizazi vingi kwa muda mrefu bila kufutika.
(h) Fasihisimulizi hutolewa katika vipindi (nyakati) na mahali maalumu. Ngano hutambwa
jioni kwenye nyumba za watu. Matambiko hufanyiwa katika sehemu maalumu. Miviga
kama vile upashaji tohara hutokea katika vipindi maalumu vya mwaka kama vile
wakati wa mavuno. Msomaji wa fasihi andishi hafungwi na mazingira ya wakati wala
mahali. Huweza kusoma wakati wowote na mahali popote.
(i) Uwasilishaji wa fasihi simulizi hutegemea viziada-lugha kama vile ishara za uso, mavazi,
miondoko, toni na hisia za hadhira. Katika fasihi andishi, mwandishi anategemea ujuzi
wake wa lugha kuwasilisha ujumbe wake kimaandishi. Hana nafasi ya kuwaigizia watu
o
sauti yake wala sauti za wahusika hazisikiki. Hata katika tamthilia, nafasi ya wahusika
wa hadithini huigizwa na wahusika wengine — wa mchezoni. Vivyo hivyo, mavazi ya
mwandishi hayawezi kuchangia katika uwasilishaji kwani hayupo pamoja na hadhira.
Ubora wa kazi yake hutegemea zaidi tamathali za usemi na ujuzi wa lugha.
D Fasihi simulizi ina historia ndefu (ni kongwe) kuliko fasihi andishi. Fasihi simulizi
ilianza pamoja na binadamu ilhali fasihi andishi ilianza baada ya kubuniwa kwa
maandishi. ;
(k) Wahusika katika fasihi simulizi kwa kawaida huwa binadamu, wanyama, mazimwi,
majini, miungu, mashetani na vitu visivyo hai. Wahusika wa fasihi andishi kwa kawaida
huwa binadamu, japo kuna baadhi ya kazi ambazo zina wahusika wanyama na hata
mizimu.
() Mwasilishaji wa fasihi simulizi anaweza kuwa mhusika mmojawapo katika kazi ya
kifasihi. Hata hivyo, mwandishi kwa kawaida si mhusika katika riwaya au hadithi
anayoandika. Isipokuwa katika kazi zilizosimuliwa katika nafsi ya kwanza (tawasifu)
ambapo mwandishi (msimulizi) hushiriki matukio ya hadithini.
(m) Fasihi simulizi haihitaji maandalizi kabla ya kutolewa. Majigambo, kwa mfano,
"hutungwa papo hapo na kuwasilishwa kwa hadhira. Aidha, ngano huwasilishwa bila
maandalizi na fanani huweza kufaragua masimulizi yake. Fasihi andishi hata hivyo
huhitaji maandalizi ya kutunga na kuandika kwa kipindi kirefu kabla ya kuchapishwa
na kuwasilishwa kwa hadhira.
(n) Fasihi simulizi ina tanzu na vipera vingi kuliko fasihi andishi. Semi, hadithi, ushairi,
maonyesho na mazungumzo yana vipera vingi ambatani ilhali fasihi andishi ina tanzu
kama vile riwaya, tamthilia, ushairi, novela na hadithi fupi ambazo hazina vipera vingi.
(o) Kurithishwa kwa fasihi simulizi kuna ubunifu kuliko kurithishwa kwa fasihi andishi.
Kufaulu kwa kazi ya fasihi simulizi hutegemea zaidi ubunifu wa fanani. Fanani ana
uhuru wa kubuni upya mtindo wa kuwasilisha kazi yake. Badala ya kutumia ngano,
fanani anaweza kutumia fani ya ushairi kama vile nyimbo. Fasihi andishi ikiandikwa
kwa mtindo fulani kama vile wa riwaya, huwa inabaki hivyo; itarithishwa vivyo hivyo
kwa vizazi vyote. Hata hivyo, baadhi ya riwaya huweza kuigizwa.
(c) Usimulizi
Msingi wa fasihi simulizi ni masimulizi. Kwa mfano, tendi, majigambo, ngano na rara
huwasilishwa kwa masimulizi. Fasihi andishi ni mwendelezo wa fasihi simulizi. Riwaya
kama vile Lila na Fila ya Kiimbila na Kipendacho Roho ya Pauline Kyovi zimeandikwa kwa
mtindo wa ngano za kimapokeo; hali inayoonyesha athari za tanzu za fasihi simulizi kwa
fasihi andishi. Katika tungo za kinathari za fasihi simulizi, fanani husimulia hadithi katika
nafsi ya tatu. Kazi nyingi za fasihi andishi za kinathari zimetumia nafsi hii hii ya tatu.
(d) Fani
Fani ni mbinu anazotumia msanii kuwasilisha maudhui. Kuna vipengele vingi vya fani
katika fasihi simulizi vinavyojitokeza katika fasihi andishi. Baadhi ya vipengele hivi ni:
(i) Ploti: Tanzu za kinathari za fasihi simulizi (ngano, visasili, mighani) huwa na ploti
sahili au nyepesi. Sifa hii pia inajitokeza katika baadhi ya riwaya za Kiswahili kama
vile Heri Subira ya Omar Babu na Siku Njema ya Ken Walibora ambazo ni nyepesi
kueleweka.
za
(ii) Wahusika: Fasihi simulizi pia imeathiri fasihi andishi kwa upande wa wahusika. Kama
tulivyotaja awali, fasihi simulizi hutumia wahusika kama vile binadamu, wanyama,
mizuka, mazimwi na viumbe visivyo hai. Fasihi andishi nayo hutumia wahusika wa
aina mbalimbali kuwasilisha ujumbe. Riwaya kama vile Shamba la Wanyama ya George
Orwell na Lila na Fila ya Kiimbila zina wahusika wanyama ambao wanatenda matendo
ya kibinadamu. Aidha, sifa za wahusika kushikilia nafasi zaidi ya moja katika tamthilia
inatokana na sifa za wahusika katika fasihi simulizi ambapo fanani na hadhira huweza
kuwa washiriki katika hadithi au kipera kinachowasilishwa.
| (iii) Nyimbo: Mtambaji wa ngano za fasihi simulizi hutumia nyimbo katika usimulizi.
Vivyo hivyo, baadhi ya kazi za fasihi andishi kama vile tamthilia hutumia nyimbo.
Katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga, S. A.Mohammed anatumia nyimbo
kuwasilisha maudhui yake.
(iv) Fantasia: Fantasia ni sifa nyingine ambayo hupatikana katika ngano, visasili na
mighani. Sifa hii pia hupatikana katika baadhi ya tungo za fasihi andishi. Zipo
riwaya za Kiswahili ambazo zina matukio ambayo yamekiuka uhalisia. Kuwepo kwa
wahusika wasio wa kawaida kama vile wanyama, samaki, mizimu na mazimwi katika
fasihi simulizi na fasihi andishi ni mfano wa fantasia. Matendo yasiyo ya kawaida
yanapatikana katika baadhi ya riwaya. Mathalani, katika Rosa Mistika, Kezilahabi
amewasawiri wahusika Rosa na Zakaria wakiwa mbinguni mbele ya hukumu ya Mungu.
Haya ni mandhari yasiyo ya kawaida.
(v) Safari: Tungo za kinathari za fasihi simulizi huwasawiri wahusika wakisafiri nchi za
mbali. Ngano za mashujaa husawiri mashujaa wakisafiri mbali kutafuta masuluhisho
kwa matatizo yanayozikumba jamii zao. Baadhi ya riwaya pia huwa na kipengele cha
safari kama vile Kusadikika, ambapo wajumbe wanasafiri nchi mbalimbali kutafuta
suluhisho kwa matatizo yanayoikumba nchi ya Kusadikika.
(e) Utendaji
Fasihi simulizi ni tendi. Vivyo hivyo, upo uwezekano wa kutenda fasihi andishi kwa kutumia
mbinu za fasihi simulizi. Tamthilia huigizwa jukwaani, tendi nyingi huimbwa, ngonjera
huambatanishwa na vitendo, na riwaya pia huweza kuigizwa kama sinema.
Fasihi Simulizi
Utangulizi
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo huwasilishwa kwa mdomo. Kama tulivyotangulia
kusema, fasihi simulizi hubuniwa na kuhifadhiwa katika akili ya binadamu.
5
ai
(c) Fasihi simulizi lazima iwe na mtendaji (fanani) kwa vile fasihi hii hutendwa. Mtendaji
anaweza kuwa mwimbaji kama ilivyo katika nyimbo, yeli/manju katika maghani,
mtambaji katika ngano au mpigaji ngoma katika ngomezi. Mtendaji katika fasihi
simulizi ana umuhimu wa kuuwasilisha utanzu wa fasihi simulizi na kuurithisha
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Wakati mwingine fanani hubuni tungo za fasihi
simulizi na kuziwasilisha papo hapo. Katika majigambo, kwa mfano, anayejigamba
hubuni maghani na kuyawasilisha papo hapo.
(d) Fasihi simulizi huwa na mahali maalumu wa kutendea. Kwa mfano, sherehe za jando
huwa na mahali maalumu pa kufanyiwa. Matambiko hufanyiwa chini ya miti mikubwa
au pangoni na nyimbo huimbwa katika miktadha na mahali maalumu. Nyiso huimbwa
jandoni, kimai huimbwa katika shughuli za baharini kama vile uvuvi na ubaharia, na
mbolezi katika matanga.
(e) Fasihi simulizi ni mali ya jamii. Tanzu za fasihi simulizi zikishatendwa humilikiwa na
kila mwanajamii. Hakuna anayeweza kudai kwamba ndiye mmiliki wa ngano, methali,
vitendawili au tanzu nyingine za fasihi simulizi. Mathalani, methali ni tungo za jamii
wala si za mtu binafsi. Hata waliozikusanya na kuziandika vitabuni hawazimiliki.
(f) Wahusika katika fasihi simulizi huweza kuwa mazimwi, mizuka, wanyama, binadamu,
milima, mawe, ndege, miungu au vitu.
(g) Fasihi simulizi ina wakati maalumu wa kuwasilishwa. Ngano, kwa mfano, hutambwa
jioni baada ya shughuli za mchana. Nyiso huimbwa tu wakati vijana wanapokuwa
jandoni na ulumbi husemwa wakati watu wanapokutana kwa shughuli fulani rasmi.
(h) Fasihi simulizi huwa na athari ya utegemezi. Uhai wa fasihi simulizi hutegemea
uwezo wa fanani kuigiza. Wakati wa kutamba, fanani huiga vitendo vya mhusika
wa hadithini ili kuifanya kazi yake kuvutia. Kwa sababu vitendo haviwezi kuingizwa
katika maandishi, kule kutegemea fanani au mwasilishaji hufanya fasihi simulizi
kuwa chapwa inapoandikwa. Aidha, tanzu na vipera vya fasihi simulizi hutegemeana.
Hadithi hutegemea methali kutoa funzo. Vitendawili navyo hutegemea taswira katika
mafumbo.
(i) Fasihi simulizi ina historia ndefu. Fasihi simulizi ilianza pamoja na maisha ya
binadamu. Hata kabla ya kuvumbuliwa kwa maandishi, fasihi simulizi ilikuwepo.
(j) Fasihi simulizi huzaliwa, hukua na kufa. Fasihi simulizi huzuka au huzaliwa na jamii.
Hukua jinsi jamii inavyokua kwa kuongezewa tanzu mpya ili kufumbata matukio
mapya katika jamii. Hata wakati jamii inapokufa, fasihi simulizi nayo hufa kwa kukosa
kizazi cha kuiendeleza. Aidha, kwa vile fasihi simulizi huhifadhiwa bongoni, inaweza
kupotea fanani akifa au hata akirukwa na akili.
(k) Fasihi simulizi huchukua umbo mahususi. Tungo za fasihi simulizi zina maumbo
yenye sifa za kipekee. Ngano, kwa mfano, zina sifa ya mianzo na miishio ya kipekee.
Methali zina maumbo ambayo hayabadilishwi. Vitendawili navyo vina sifa ya mtindo
bainifu wa uwasilishaji.
(1) Fasihi simulizi hurithishwa na fanani kwa mdomo. Fanani ndiye huiwasilisha kwa
hadhira kwa kutumia fani kama vile methali, ngano, mawaidha au nyimbo. Kwa njia
hii, yeye hurithisha fasihi simulizi kwa vizazi na vizazi.
(m) Fasihi simulizi hubadilika kutegemea fanani, wakati na mazingira. Kila fanani ana
mtindo wake wa kuiwasilisha. Jinsi fasihi hii inavyopitishwa na mafanani mbalimbali
ndivyo inavyobadilika. Aidha, fasihi simulizi hubadilika kutegemea mazingira na
wakati. Tashbihi, kwa mfano, hubadilika kutegemea hali hizi. Mathalani weusi waweza
kulinganishwa na vitu mbalimbali kama vile -eusi kama makaa, -eusi kama mpingo
ama -eusi kama lami.
Co)
Mambo ambayo huchangia kubadilika kwa fasihi simulizi
Mojawapo ya sifa za fasihi simulizi ni hali yake ya kubadilika. Mabadiliko hayo husababishwa
na mambo yafuatayo:
(a) Hadhira
Fanani au mwasilishaji wa fasihi simulizi hukabiliana ana kwa ana na hadhira yake.
Hadhira inaweza kumwathiri akabadilisha mtindo wake wa uwasilishaji papo hapo.
Mtambaji anaweza kulazimika kutumia msamiati rahisi au mgumu kuliko ule uliokuwa
katika utungo wa awali ili kukidhi mahitaji ya hadhira yake kulingana na umri na
viwango vya uelewa wao.
(c) Fanani
Kila fanani ana mtindo wake wa kisanii. Ana uwezo wa kuisimulia kazi kwa mtindo
mpya, na hivyo kuleta mabadiliko kifani. Kwa mfano, ngano moja inaweza kusimuliwa
kwa mitindo tofauti kulingana na mtindo nafsi wa mtambaji. Ploti hubaki kuwa ile
ile lakini pakawa na tofauti kuhusu yaliyomo na lugha.
Fanani husimulia anayokumbuka. Ikiwa kumbukumbu yake si nzuri, huenda
akasahau baadhi ya yaliyomo, hivyo kutoyarithisha kabisa. Kule kutorithisha huweza
kusababisha mabadiliko ya yaliyomo (maudhui) katika fasihi simulizi.
Aina za wahusika
Kuna aina mbalimbali za wahusika katika kazi za fasihi simulizi:
(a) Fanani
Fanani huhusika katika fasihi simulizi kwa kutunga utungo na kuuwasilisha kwa hadhira.
Ndiye msanii wa fasihi simulizi. Fanani anaweza kuwa msimulizi kama ilivyo katika ngano,
mwimbaji katika nyimbo, yeli au manju katika maghani, mtegaji katika vitendawili, mnasihi
(mtoaji nasaha) katika mawaidha, mpigaji ngoma katika ngomezi au mlumbi katika ulumbi.
Kwa kushiriki kwa njia hii, fanani huwa msimulizi na vilevile mhusika mshiriki katika
fasihi simulizi.
Yafuatayo ni majukumu ya fanani katika uwasilishaji wa fasihi simulizi:
(i) Ingawa fanani katika ngano si mmojawapo wa wahusika wa hadithini,
yeye huhusika katika uwasilishaji wa hadithi. Fanani haiwasilishi tu hadithi
bali huibadilisha kuwa sanaa tendwa kila anapoiwasilisha kwa hadhira hai.
Fanani hutenda mambo kama vile kuigiza sauti za wahusika wa hadithini pamoja
na kuashiria kwa uso (kutumia viziada-lugha) ili kufanikisha hadithi kwa kumsawiri
mhusika wa hadithi kama alivyo kwenye hadithi yenyewe.
(ii) Katika utegaji wa vitendawili, mtegaji (fanani) huhusika kwa kutoa kitendawili,
kupokea majibu na kuomba mji baada ya mteguaji kukosa jawabu.
(iii) Hutunga tungo na kuzisimulia au kuziwasilisha. Kwa mfano, anayejigamba hutunga
majigambo/vivugo na kuviigiza kwa hadhira hai.
(iv) Huwafunza vijana mbinu za kuiendeleza fasihi simulizi kupitia kwa uwasilishaji wake.
(v) Hutoa elimu kwa hadhira. Fanani ana jukumu la kuonya, kuarifu, kukashifu, kuelekeza,
kufahamisha, kukosoa na hata kuzindua hadhira yake.
(vi) Huendeleza utamaduni kwa kuupokeza kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kupitia kwa
utambaji wa ngano, mtambaji hurithisha mazoea ya utambaji na thamani za kijamii
zinazofumbatwa na ngano zenyewe kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
(vii)Hudumisha na kuendeleza lugha. Kadiri fanani anavyofinyanga lugha ndivyo
inavyopevuka na kukua. Fanani hubuni miundo mbalimbali ya lugha na kuipokeza.
Kwa jinsi hii huidumisha na kuiendeleza lugha.
o
(viii) Hushirikisha hadhira katika uwasilishaji wake. Kwa vile fasihi simulizi ni tendi na
ina hadhira hai, ni jukumu la mwasilishaji kuhakikisha kuwa hadhira yake inashiriki
vilivyo.
(b) Hadhira
Hadhira ya fasihi simulizi ni binadamu. Hawa ni wasikilizaji na watazamaji wa fasihi
simulizi.
Katika fasihi simulizi, wasikilizaji au watazamaji huchukua jukumu la uhusika pale ambapo
wanashiriki katika uwasilishaji kwa kuimba, kuuliza maswali kutegua vitendawili na kumpa
fanani ushauri kuhusu namna na wakati wa kuwasilisha utungo. Kwa kushiriki katika
nyimbo, hadhira inakuwa kama wahusika wa hadithini kwa kushiriki matendo ya wahusika
hao. Kwa hivyo, hadhira ya fasihi simulizi hutekeleza majukumu mawili: ni wasikilizaji au
watazamaji na pia ni wahusika washiriki katika fasihi simulizi.
WABEBA
eo Mbweha pia ni laghai.
eo Kinyonga husawiriwa kama asiyetandarukia mambo, asiye na msimamo na
anayebadilikabadilika.
o Kobe ni mwenda pole na mwenye makini. Wakati mwingine husawiriwa kama
mwenye hila.
Wahusika wanyama walio na sifa za kibinadamu hutumiwa kiistiara (kimafumbo) kukashifu
tabia hasi katika jamii. Katika mojawapo ya ngano, fisi anaamua kuila kamba inayomfunga
ndama kwanza ili amle ndama baadaye. Mwishowe fisi hadiriki kumla ndama kwa sababu
kamba inapokatika, ndama anatoroka. Hapa tunaonywa dhidi ya tamaa na kufanya mambo
bila tahadhari.
Ingawa wahusika wanyama hutenda kama binadamu, sifa zao za unyama hazipotei kabisa.
Sifa hizi hudumishwa kupitia kwa milio pamoja na miondoko yao.
Maswali
(a) Andika wahusika katika hadithi hii.
(b) Nini umuhimu wa hadithi za aina hii?
(c) Andika sifa za fasihi simulizi zinazojitokeza katika hadithi hii.
(d) Dondoa mbinu za kifasihi zilizotumiwa katika hadithi hii.
(e) Mtambaji wa hadithi hii amedokeza stadi (mbinu) mbalimbali za kuishi.
Andika zozote tano.
p
g'
Utanzu wa Hadithi
Utangulizi
Hadithi ni masimulizi yanayowasilishwa kwa lugha ya kinathari kuhusu watu, matukio
na mahali mbalimbali. Lugha nathari ni lugha iliyo na maelezo ya moja kwa moja katika
mfululizo wa sentensi zilizopangwa katika aya. Hadithi huweza kuwa ya kweli au ya kubuni.
Hadithi katika fasihi simulizi hutofautiana na hadithi za fasihi andishi, kwa sababu hadithi
za fasihi simulizi huwa na mtendaji na hadhira pamoja na pahali maalumu pa kutambia.
Sifa za hadithi
(a) Hadithi huwa na wahusika wa aina mbalimbali. Wahusika katika hadithi wanaweza
kuwa wahusika binadamu, wanyama, mazimwi, miti, mawe au miungu.
(b) Hadithi hueleza matukio kwa mpangilio wa moja kwa moja, kuanzia tukio la mwanzo
hadi la mwisho. Yaani, hadithi huwa na ploti sahili au nyepesi isiyo na mbinu
changamano kama vile hadithi ndani ya hadithi au mbinu rejeshi.
(c) Hutumia lugha ya kimaelezo au ya nathari.
(d) Hadithi huwa na mtendaji au fanani. Fanani anaweza kuiga wahusika katika hadithi
anayosimulia. Kwa mfano, anaweza kuiga jinsi fisi alivyokula. Anaweza kupandisha
au kushusha sauti kutegemea ukali wa kauli inayotolewa.
(e) Hadithi husimulia matukio ya kweli au ya kubuni yenye maadili. Hadithi za mazimwi,
kwa mfano, ni za kubuni. Aidha, hekaya na visasili ni hadithi za kubuni ilhali mighani
na visakale vina ukweli fulani.
(£) Kwa kawaida, hadithi hutambwa jioni baada ya shughuli za mchana, hususan baada ya
chakula chajioni au watu wanapongojea chakula chajioni kiive. Katika baadhi ya jamii,
utambaji hauruhusiwi mchana. Wanaojaribu kufanya hivyo hutishwa. Kwa mfano,
katika jamii ya Wagiriama, wanaohadithiana mchana hutishwa kuwa wataolewa na
fisi.
D
Dhima ya hadithi
Hadithi hutekeleza majukumu yafuatayo katika jamii:
katika hadithi ni kati
(a) Huielekeza jamii. Kama tulivyotaja hapo juu, mgogoro mkuu
vita
ya wema na uovu. Kwa kawaida wema huishia kushinda uovu. Hii huonyesha
vya jamii dhidi ya uovu. Kila hadithi huwa na funzo maalumu linalokusudiwa kutoa
mwongozo wa kimaadili kwa wanajamii.
ya kilimo,
(b) Hurithisha elimu ya jamii. Maarifa ya jamii ya kijadi kama vile sayansi
husimul iwa
uhunzi, mbinu za uwindaji, tiba, ukunga, sanaa ya uchongaji na ufinyanzi
katika ngano na kurithishwa kwa vizazi vya jamii.
kwa mdomo. Kwa sababu
(c) Hukuza uwezo wa kukumbuka. Fasihi simulizi hupokezwa
hii, watu hutarajiwa kuikumbuka hadithi ili kuweza kuitamba baadaye kwa wengine
na kwa njia hiyo kuipokeza kizazi baada ya kizazi.
(d)Huhalalisha baadhi ya desturi za jamii. Baadhi ya hadithi hueleza sababu ya kuwepo
Hueleza, kwa
kwa hali fulani. Visasili, kwa mfano, huhalalisha tabia na imani za kidini.
madhehebu
mfano, sababu za kuabudu milima, miti, majabali na sababu za kuwepo kwa
fulani. Baadhi ya visasili hueleza asili ya kifo kwa nia ya kuhalalisha kuwepo kwake.
wake.
Hadithi huonya, hushauri, huadibu na kunasihi jamii kupitia kwa wahusika
wa na
Wahusika katika hadithi husawiri tabia hasi na chanya. Tabia chanya huhimiz
hasi hupuuzwa na kulaaniwa.
Huhifadhi na kuendeleza historia ya jamii. Mashujaa na michango yao kwa jamii
hujulikana kupitia kwa hadithi za mighani ambayo hupitishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine. Mashujaa waliopata kuathiri historia ya jamii zao ni kama Lwanda
u:
Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Waswahili na Wangu wa Makeri wa Wakikuy
——
(8) Huhifadhi utamaduni wa jamii. Kupitia kwa hadithi ambazo hupitishwa kutoka kizazi
kimoja hadi kingine, tunaweza kuona mazoea, mila na utamaduni wa jamii hiyo.
(h) Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii huwa na hadithi zake ambazo husimulia tajriba
ya jamii hiyo. Kila jamii, kwa mfano, ina fasiri yake ya chanzo cha kifo. Ngano fulani
na mighani huhusishwa na jamii fulani. Mathalani, Wangu wa Makeri anahusishwa
na jamii ya Wakikuyu.
(i) Hukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani. Hadithi hutambwa mbele ya hadhira.
Kadiri mtu anavyotamba ndivyo anavyoboresha uwezo wake wa kuzungumza mbele
ya watu.
(j) Huliwaza na kuburudisha baada ya shughuli za kazi. Hii ndiyo sababu hadithi
zilitambwa jioni. Zile zinazotambwa wakati kazi ikiendelea zilinuiwa kuondoa ukinaifu
na uchovu unaosababishwa na kazi.
(k) Hukuza ubunifu. Utambaji wa hadithi ni kipawa. Jinsi kipawa hiki kinavyopaliliwa
kupitia utambaji ndivyo kinavyokua.
(1) Hadithi huunganisha watu katika jamii. Watu wanapokuja pamoja kutambiana ngano
hujihisi kuwa jamii moja na ushirikiano hujengeka zaidi.
Usimulizi wa hadithi
Sifa za mtambaj
Mtambaji wa hadithi huchukua nafasi muhimu sana katika kufanikisha uwasilishaji wa |
hadithi. Kwa sababu hii, mtambaji wa hadithi anafaa kuwa na sifa zifuatazo: |
(a) Mtambaji anapaswa kuwa na ubunifu wa kiwango cha juu. Aweze kuibuni upya hadithi
kila mara anapoitamba kwa hadhira mpya au katika muktadha mpya kwa njia ya
kuchangamsha. Ikiwa hadhira yake ni ya watoto ataongeza masuala ambayo yanapendwa
Zaidi na watoto kama vile ishara za uso, miondoko na mabadiliko ya sauti au mchezo wa
maneno na sauti. |
(b) Mtambaji anapaswa kuijua hadhira yake na mahitaji yake pamoja na kiwango chao cha
elimu au tajriba yao maishani. Hili litamwezesha kubadilisha mtindo wa uwasilishaji
ili kuwafaa wale anaowasimulia. Kama ni watoto, atatumia lugha rahisi na yenye
vichekesho vinavyopendwa na watoto. Aidha, sharti aelewe hulka za hadhira yake
kama vile nini huwachukiza, huwachangamsha au kuwavutia.
(o) Mtambaji anapaswa kuielewa na kuimudu lugha ya hadhira yake. Malighafi ya fasihi
simulizi ni lugha. Ni muhimu mtambaji afahamu kiwango kikubwa cha msamiati wa
lugha anayotumia ili aweze kuitumia lugha hiyo kwa wepesi katika utambaji.
(4) Anapaswa kuyaelewa mazingira ya hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika na
hadhira kutoka kwayo. Ikiwa hadithi inahusu mfalme, na katika mazingira ya hadhira
yake pana rais, mtambaji anaweza kutoa mfano wa rais. Hili litawafanya wasikilizaji
wake kuelewa dhana ya ufalme. Inabidi pia afahamu masuala ibuka katika jamii ili
aweze kuyashughulikia katika masimulizi yake.
(e) Anapaswa kuwa jasiri wa kuweza kuzungumza hadharani. Mtambaji hastahili kuona
haya kuzungumzia masuala ya aibu inapobidi. Pia anahitajika kuwa na ukakamavu
wa kusimama mbele ya hadhira na kuihadithia.
(£) Anapaswa kuujua utamaduni wa hadhira yake ili kuepuka kutumia maneno au ishara
zinazoweza kuvuruga mawasiliano. Aweze kutoa ujumbe kwa njia inayokubalika na
utamaduni wa jamii.
ya kuunda au
(8) Mtambaji anapaswa kuwa na uwezo wa ufaraguzi. Ufaraguzi ni hali
kuigeuza kazi ya fasihi simulizi papo hapo na kuiwasilisha kwa hadhira. Mtambaji
basi anapaswa kuwa na uwezo wa kubadilisha sauti, kuigiza na kutumia viziada-lugha
kutegemea hadhira na muktadha.
(h) Mtambaji bora huwa mcheshi. Hili humwezesha kuichangamsha hadhira yake na
kunasa makini yao. Ucheshi hata hivyo hutegemea hadhira. Hadhira ya watu wazima
itafurahishwa na lugha inayoghushi kiucheshi kuliko hadhira ya watoto.
Gi) Mtambaji anapaswa kuwa na uwezo wa kuishirikisha hadhira yake kwa kuiuliza
maswali ya balagha na kuishirikisha katika nyimbo. Hili litakinga dhidi ya ukinaifu.
Pia litampa fursa ya kujirekebisha kutokana na mwitiko wa hadhira.
J) Anastahiki kuwa mbaraza anayeingiliana vyema na watu. Hili humfanya kuvutia
hadhira.
Ngano
Ngano ni hadithi za kimapokeo ambazo hutumia wahusika kama vile watu, wanyama,
miungu, mashetani, mizimu, miti na vitu visivyo hai kuelezea au kuonya kuhusu maisha.
Sifa za ngano
(a) Ngano huwa na fomyula maalumu - fomyula ya ufunguzi (mwanzo) na fomyula ya
kuhitimisha (mwisho). Mfano wa fomyula ya mwanzo ni:
“Hadithi! Hadithi!”
“Hadithi njoo!”
Mfano wa fomyula ya mwisho ni:
“Hadithi yangu inaishia hapo.” au “... wakaishi raha mustarehe.”
(b) Ngano ni hadithi za kimapokeo. Yaani, hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Watambaji mbalimbali huzipitisha ngano kwa vizazi tofautitofauti.
(c) Usimulizi wake huwa na urudiaji au ukariri mwingi wa maneno, sauti na vifungu vya
maneno, kwa mfano, “... zimwi likakimbia, likakimbia ...”.
RA
hai, mizimu,
(d) Ngano huwa na wahusika wanyama, binadamu, mazimwi, viumbe visivyo
miungu na hata mashetani. Wahusika hawa hupewa sifa za kibinadamu ili waweze
kutumiwa kuadilisha.
(e) Aghalabu ngano huwa na matumizi ya nyimbo ambazo ni kitulizo kwa hadhira.
Nyimbo huipunguzia hadhira mwemeo unaosababishwa na matukio ya hadithi na
pia kuwasilisha mafunzo muhimu. |
(£) Ploti yake huwa sahili. Ngano hazina matumizi ya mbinu nyingi kama mbinu rejeshi
ambazo huenda zikafanya ploti kuwa changamano.
(g) Ngano ni hadithi za mafunzo na ambazo humulika mtazamo wa jamii husika kuhusu
maisha. Ngano za kiayari, kwa mfano, huhimiza uaminifu.
ya
(h) Ngano huwa na matumizi mengi ya fantasia. Fantansia ni mambo ya ajabu au yasiyo
kawaida. Mfano wa fantasia ni binadamu kuruka kama ndege hewani, zimwi kumeza
watu na baadaye kuwatapika wote.
a
(i) Ngano huwa na kipengele au motifu ya safari. Mashujaa katika ngano za mashuja
husafiri nchi za mbali kutafuta masuluhisho kwa matatizo yanayozikumba jamii zao.
i
(j) Ngano huwa na upenyezi wa mtambaji. Upenyezi wa mtambaji ni hali ya mtambaj
kuingiza maneno yake au kutoa maoni kuhusu tukio au mhusika fulani katika hadithi.
kana
(k) Matukio katika ngano hayajikiti katika kipindi maalumu. Visa husimuliwa
kwamba vilitokea wakati uliopita bila kutaja wakati maalumu. Kwa mfano, “Zamani
sana ...” au “Hapo zamani za kale ...”
Hadhira: Pakawa!
Msimulizi: —Hapo zamani za kale...
au
Msimulizi: —Paukwa!
Hadhira: Pakawa!
Msimulizi: Sahani!
Hadhira: Ya mchele!
Msimulizi: Giza!
Hadhira: La mwizi!
Msimulizi: Na kiboko je?
Hadhira: Cha mtoto mkorofi!
Msimulizi: Hapo zamani za kale...
(iii) Huashiria mwanzo wa hadithi. Kwa mfano, katika jamii ya Wameru, mtambaji
husema “Jukia rugano” kumaanisha “Chukueni ngano,” kisha wanaotambiwa husema,
“Twajukia” yaani “Tumechukua” kuonyesha kwamba wamekubali kuhadithiwa na hapo
hadithi huanza.
(iv)Huweka mpaka kati ya ulimwengu halisi na ulimwengu wa hadithi. Huwatanabahisha
wasikilizaji kuwa sasa wameingia katika ulimwengu wa ubunifu. Kwa mfano,
mtambaji anaposema, Hapo zamani za kale, wasikilizaji wanasadikishwa kuwa mambo
yatakayotambwa ni ya kipindi cha zamani; hayawahusu moja kwa moja japo huenda
hadithi ikawa na wahusika wenye tabia kama zao.
(V) Fomyula ya ufunguzi hushirikisha au huleta hadhira na mtambaji pamoja. Mtambaji
anaposema: Hadithi! Hadithi! hadhira hujibu: Hadithi njoo! kuonyesha kwamba hadhira
iko pamoja na mtambaji.
Aina za ngano
Ingawa wataalamu wamejaribu kuziainisha ngano, si rahisi kuzitenganisha kabisa. Ile
ambayo ingeonekana kuwa ngano ya usuli kwa kigezo kimoja inaweza kuwa ngano ya
mtanziko au hurafa kwa kigezo kingine. Ngano huweza kuainishwa kwa kutumia vigezo
vifuatavyo:
(a) Wahusika .
Ngano zinaweza kuainishwa kwa misingi ya wahusika wanaotenda matendo katika ngano
yenyewe. Kwa kufuata kigezo hiki, tuna ngano kama vile:
(i) Ngano za mazimwi na majitu
Hizi huwa na wahusika mazimwi au majitu.
(ii) Hurafa
Hurafa ni ngano ambazo wahusika wake ni wanyama lakini wanaowakilisha binadamu.
(iii) Hekaya
Wahusika wake ni binadamu wanaowakilisha tabia za binadamu wa aina hiyo katika
jamii. Kwa mfano, Abunuwasi katika Hekaya za Abunuwasi huwakilisha walaghai.
(iv) Ngano za mashujaa
Wahusika katika ngano za mashujaa ni binadamu waliotenda mambo ya kishujaa katika
jamii zao.
(b) Dhamira j
Kwa kuzingatia dhamira, ngano huweza kuainishwa kulingana na sababu, nia au lengo la
kutambwa kwake. Kwa kuzingatia kigezo hiki tunapata ngano zifuatazo:
(i) Ngano za kuadilisha
Kimsingi, ngano za kuadilisha hufunza tabia inayokubalika.
(ii) Ngano za usuli
Ngano hizi huonyesha asili ya tabia, maumbile, tabia, hali au mahusiano fulani.
(iii) Ngano za mtanziko
Ngano za mtanziko hulenga kukuza stadi ya kutathmini na kutoa uamuzi ufaao.
Ni muhimu kutaja hapa tena kuwa vigezo vya dhamira na wahusika ni mwongozo tu
wa kuainisha ngano ili kuzifanya zieleweke kwa urahisi. Aina hizi za ngano huingiliana.
Kwa mfano, ngano ya usuli inaweza kuwa na dhamira ya kuadilisha.
Ngano za mazimwi
Hizi ni ngano ambazo wahusika wake ni mazimwi. Mazimwi ni wahusika ambao wana uhai
lakini si binadamu, si wanyama, si miungu wala si mashetani. Kwa kawaida, mazimwini
wahusika walio na sifa za kutisha kiumbo, sura na matendo. Kwa mfano, zimwi linaweza
kuwa na urefu wa kufikia mbingu. Mazimwi ni zao la fikira za binadamu. Yaani ni viumbe
wa kufikirika tu.
(a) SIA WAASI. Mazimwi husawiriwa kama wahusika mahasidi wenye tamaa na uovu
Zamani sana katika kijiji cha Tima paliondokea sonara mmoja. Sonara huyu alikuwa
na mke mrembo ambaye alihusudiwa na walimwengu wote katika eneo hilo. Karibu
na kibanda chao palikuwa na msitu ambao ulisetiri mazimwi ya kila aina. Kila jioni
ungeyasikia mazimwi hayo yaking'ang'ania mawindo. Sonara na mkewe hawakwisha
kushangaa jinsi viumbe hawa walivyokithiri kwa tamaa.
Siku moja sonara aliondoka kijijini kwenda mbali kwa shughuli za ufuaji. Alimwacha
mkewe akiwa mjamzito. Mara tu baada ya kuondoka, uchungu wa uzazi ulibisha hodi.
Mama mtu akawa taabani, asiwe na mwombezi. Katika hali hii ya hamaniko, mama
mtu alishtukia kapata mkunga aliyeonekana mzuri na mpole ajabu. Mama akajawa na
furaha tele. Bahati iliyoje!
Mkunga akaingia kazini. Baada ya dakika chache, malaika, kitoto kichanga
kikahanikiza hewa ya asubuhi mbichi kwa kilio. Mama mtu alimshukuru mkunga kwa
usamaria wema. Laiti angalijua kuwa kajipagaza zigo lisilobebeka!
Mkunga huyo hakukawia. Akaingia ghalani, akachukua mtama, akasaga na kumpikia
mwanagenzi fuka. Mzazi, hamu ya kula hajapata bado, mkunga akamkabidhi bakuli la
uji. “Shika mke mzazi,” akasema. Hata kabla ya mama kutoa kauli, mkunga akabadilika
ghafla. Ile sauti ya upole ikabadilika kuwa mngurumo wa kutisha: “UKIKATAA, MIMI
NAENDA KUUNYWA!”. Kumbe yule mkunga alikuwa zimwi lililobugia uji pamoja na
bakuli! Mama alipoona hayo, vimbimbi vikamsimama kwa woga.
Kufikia jioni, njaa ilikuwa imemuuma mama na mtoto si haba. Yule mkunga-zimwi
akajigeuza binadamu na kuchinja mbuzi ili ampikie mama mzazi. Baada ya supu kuiva,
zimwi likaibeba pamoja na minofu na kumpelekea mama mzazi. Lakini hata kabla ya
kutua sufuria, lilikariri maneno yale yale: “UKIKATAA, MIMI NAENDA KUNYWA.”
Kwa kauli hiyo, likabugia nyama pamoja na sufuria. Mbuzi mzima akapata makao
ndani ya tumbo la zimwi! Mama na mtoto wake wakalala mataya yakigongana. Siku
tatu zilipita bila ya mama kupewa chakula chochote. Unyonge wa uzazi ukamvamia.
Kitoto nacho kikaendelea kudai haki.
Asubuhi moja Kasuku alipitia akitarajia kiamsha kinywa kama kawaida. Akampata
mke wa sahibu yake taabani. Baada ya mazungumzo mafupi na mama mtu, waliafikiana
kuwa ampelekee sonara ujumbe.
Kasuku alienda akatua juu ya mti uliokuwa karibu na kiwanda cha sonara. Akaimba:
Ewe sonara unayefua
Mke kajifungua
Unyonge wa uzazi wamliza
Tumbo la uzazi latekenya
Chango zamsokota
Kisa na maana
Chakula hapati
Mpishi hupikia tumbole
Zimwi huchumia chunguche
Kikawia hasara takufika
Ya kinda na mamaye.
Sonara alisikiliza wimbo huu kwa muda na ujumbe wake ukamgonga ndipo.
Akajihami na kufunga safari kurejea nyumbani. Alipofika, alimpata mkewe taabani,
mwili umenyong'onyea. Maghala yote yalikuwa yamefagiwa na zimwi lililokuwa
limejidai kuwa mfadhili na lililala nje ya ghala kwa mavuno ya shibe. Sonara alilidunga
mkuki likafia papo hapo. Ingawa Sonara alijuta kwa kutowazia hali ya mke wake tangu
awali, aliweza kuliangamiza zimwi. Hadithi yangu inaishia hapo.
Oo
Hurafa
Sifa za hurafa
(a) Wahusika katika hurafa ni wanyama.
Oa
kutaka kulipiza kisasi kwa kiumbe huyu ambaye daima alizoea kuyahujumu maghala
ya mahindi. Paka akamtazama Panya kwa jicho la hasidi, akatayarisha mafumba yake
kwa vita. Lakini ghafla akakumbuka maneno ya Malaika Mkuu na kujiasa. Alimnyoshea
Panya kidole na kumwambia, “Laiti Malaika Mkuu asingekuwa amenionya dhidi ya kula
chochote, ningekufunza funzo la maisha.” Basi Panya akanusurika.
Sasa walikuwa wakilitazama kasri la Mungu. Kwa mbali, mbwa alikaza mboni zake
zaidi na kumwona Swara akija kwa madaha. Ziraili akamwingia, “Kaka Mbwa, natumai
unakumbuka walivyotwambia wahenga kuwa ngojangoja huumiza matumbo. Je, una hakika
gani kuwa baada ya kufikisha ujumbe utapewa hata tone la maji? Hamadi kibindoni bwana.
Faidi chajio ukionacho sasa.” Bila nadhari, Mbwa alimtwaa Swara na kumla shibe yake.
Jua lilipozama Paka na Mbwa walijipata nje ya lango la kasri. Mungu akatoka kwenye
chumba chake cha maongezi na kwenda kupokea salamu zake. Akamwuliza Mbwa, “Je,
safari ilikuwaje?” Mbwa akajibu, “Safari ilikuwa ndefu, lakini yenye mafanikio makubwa.
Niliweza kuwashika Sungura na Swara na kuwala. Njaa haikunidhili mno, ila bahasha
niliyopewa ilipotelea njiani.” Mungu akamjibu, “Subiri hapo nje ya lango. Nitakuita baada
ya kuzungumza na Paka.” Paka alipoulizwa, alijibu kwa sauti hafifu, “Safari ilikuwa ndefu
mno. Sikuweza kuzungumza na yeyote. Nilitaka kulipiza kisasi kwa Panya niliyekutana
naye ila sikuweza kwani Malaika Mkuu alikuwa ametuonya dhidi ya hayo.” Mungu
alimpa pole kwa hayo. Akamkaribisha ndani ya kasri na kumpa sharubati kwanza. Mbwa
akabaki nje akisubiri. Tangu siku hiyo, Mbwa daima husubiri nje naye Paka huishi ndani
ya nyumba. Hadithi yangu inaishia hapo.
Zoezi ZI
Hekaya
Hizi ni ngano ambazo kwa kawaida humsawiri mhusika akitumia ulaghai kupata matilaba
yake kutoka kwa wengine. Hekaya pia huitwa ngano za kiayari. Ayari ni mtu mwenye tabia
ya kulaghai. Mhusika huyu hujifanya kuwa rafiki wa mwingine kwa nia ya kujifaidi.
Katika ngano za kiayari au hekaya, kwa kawaida mhusika mdogo au mnyonge hutumia
akili kumshinda mhusika mwenye nguvu asiye na akili.
Katika jamii ya Waswahili, kwa mfano, hekaya nyingi zilihusu mhusika wa kubuniwa
aliyepewa jina la Abunuwasi. Katika jamii nyingine za Kiafrika, hekaya zilimhusu sungura
aliyewalaghai wanyama wakubwa kama vile ndovu. Wanyama wengine kama vile nyani,
mbweha, nyoka na mamba pia husawiriwa kama wahusika walaghai. Ngano za kiayari au
hekaya hutumiwa kuadilisha na kuonya dhidi ya matendo hasi kama vile udanganyifu,
usaliti, hadaa na matumizi mabaya ya cheo.
Mfano wa hekaya
Hapo zamani za kale, Abunuwasi alikuwa mshairi mashuhuri katika kasri la SIA
Abunuwasi alikuwa na punda wake aliyekuwa na sura nzuri mno.
Siku moja punda wa Abunuwasi alihisi kiu. Kwa sababu Abunuwasi hakutaka
kumpeleka punda huyo mtoni kwa kuchelea kwamba angeibwa na mahasidi, aliamua
kumnywesha maji mle nyumbani. Hata hivyo, Abunuwasi hakuwa na ndoo wala karai
ya kutilia maji na hivyo basi akamwendea jirani yake na kumwambia, “Bwana wee nifae
kwa jua nikufae kwa mvua. Punda wangu yu taabani kwa kiu. Nami mwenzio wajua |
tangu hapo wezi walikuja wakabwakura mali yangu. Sasa hata chano cha kutilia tonge |
sina. Naomba uniazime karai yako niitumie kisha nitairejesha mara moja.”
Jirani aliyatilia shaka maneno ya Abunuwasi. Alikuwa ameangukia mizungu ya mja
huyu mara nyingi. Hata hivyo, moyo ulimkumbusha kuwa hata adui hupendwa. Alitwaa
karai na kumkabidhi mgeni wake.
Juma lilipita, Abunuwasi akawa hajarudisha karai. Jirani, subira ikamkimbia.
Akamwendea Abunuwasi na kumwambia, “Ndugu yangu, nimepatwa na haja. Naomba
unikabidhi ile karai.”
>
Abunuwasi alijidai kuhizika. Hata hivyo akili yake nyepesi ilimwambia, “Huu ndio |
wakati.' Aliingia ndani, akatwaa karai ya jirani yake. Ndani ya karai hiyo alitia karai |
nyingine. “Kikembe cha karai kubwa,” aliiita. Alimkabidhi jirani ambaye alimkumbusha
kuwa alikuwa amemwazima karai moja tu. Abunuwasi alikenua akamwambia, “Ndugu,
muda si haba umepita, nayo karai yako imezaa karai ndogo. Sina nia ya kukudhulumu.
Nairudisha karai pamoja na mtoto wake.”
Jirani, ambaye kwa mara nyingine hakutambua mtego wa Abunuwasi, alimsifu
Abunuwasi kwa uaminifu wake. Akatwaa 'mama' na 'mwanawe' na kujiendea zake.
Baada ya mwezi mmoja Abunuwasi alimwendea jirani yake kuomba ile karai tena. |
Jirani alimwazima mara moja kwa kutarajia natija hata maradufu. Wiki mbili zilipita bila
jirani kupata neno lolote kutoka kwa Abunuwasi. Asubuhi moja akaenda kwa Abunuwasi
kudai mali yake. Abunuwasi alitoka nje, uso umejaa huzuni ya mamba. Akamwambia
jirani kuwa karai ilikuwa imekufa! Jirani alikasirika na kukataa kuwa karai ambayo
imetengenezwa kwa chuma inaweza kufa. Abunuwasi alimkumbusha, “Ndugu, kizaacho
Pia hufa.”
j
|
|
|
Ji
(35)
Jirani hakumwamini Abunuwasi. Alimshtaki. Hakimu, katika kuamua kesi alisema,
“Mantiki inadai kuwa ikiwa kifaa kinaweza kuzaa basi kufa ni faradhi”. Abunuwasi
wakashinda. Hadithi yangu inaishia hapo.
Ngano za mtanziko
Katika ngano za mtanziko, mhusika hukabiliwa na hali ngumu ya kuamua baina ya mambo
au hali mbili au zaidi zinazomkabili; kimaadili, kisheria au kikanuni. Ngano za aina hii
mara nyingi huipa hadhira swali la kujadiliana. Hukuza uwezo wa kutathmini (kupima)
hali na kutoa uamuzi ufaao.
WA
Ngano za mashujaa
Hizi ni ngano ambazo wahusika wake ni mashujaa. Ngano za mashujaa husimulia kuhusu
maisha ya mtu au watu waliotenda mambo ya kishujaa na kutukuzwa. Mashujaa hawa
hutenda vitendo vya kijasiri kama vile kusafiri kwenye nchi za majitu na kupigana na
majitu ili kuziokoa jamii zao.
Ngano nyingi za mashujaa huwa na motifu ya safari na husawiri mapigano kati ya wema
na uovu. Uovu kwa kawaida huwakilishwa na wafalme au viongozi dhalimu, mazimwi au
majitu. Hatimaye wema hushinda uovu kupitia kwa juhudi za mashujaa.
Ngano za mashujaa husimuliwa kuhimiza uzalendo na ujasiri miongoni mwa vijana.
Hizi ni ngano ambazo huwa na maana nyingine ya ndani/maana iliyofichika. Kuna aina
mbili kuu za ngano za kimafumbo.
(a) Istiara
Istiara ni hadithi ambayo maana yake ya juu inawakilisha maana nyingine iliyofichika.
Hurafa ni mfano wa istiara, ambapo wanyama huwakilisha binadamu.
(b) Mbazi
Mbazi ni hadithi fupi yenye mafunzo na inayotolewa kama kielelezo wakati wa kumkanya
au kumwelekeza mtu. Mbazi huwa na maana fiche na hutolewa katika vikao rasmi vya
kutoa mawaidha. Mbazi nyingi hupatikana katika Biblia hasa katika mafundisho ya
Yesu Kristo.
Mjukuu wangu, ni vyema kulipa wema kwa wema. Wazazi wako wamekulea kwa
kujisabilia, mbona unawahangaisha hivi kwa kufusha mioshi midomoni kila mara?
Pulika usikie hadithi niitambayo.
Zamani sana, Simba na Nyoka walikuwa wanapigana, Simba akitaka kumla Nyoka.
Hata hivyo, Nyoka aliweza kuhepa kabla ya Simba kumuua. Akapata hifadhi katika
nyumba ya Binadamu. Binadamu alimficha Nyoka ndani ya kabati. Simba akamtafuta
nyoka asimpate.
Mara tu nyoka alipogundua kuwa hasimu wake ameondoka, alitoka ndani ya kabati,
akamuuliza Binadamu, “Matendo mema hulipwa vipi?” Bila shaka, mjukuu wangu,
Binadamu alimjibu, “Jaza ya hisani ni hisani.”
Nyoka hakusema lolote. Alimkazia jicho Binadamu tu. Kwa kudhani kuwa
hajaeleweka, Binadamu akamfafanulia, “Kwa kawaida, wema hulipwa kwa fedha, lakini
kwa vile huna pesa, unaweza kunipa mnyama yeyote mara tu utakapofanikiwa katika
mawindo yako.”
Nyoka alitabasamu na kusema huku akipanua mataya yake, “Ndugu yangu, unajua
kuwa Nyoka hulipa wema kwa uovu? Nitakumaliza sasa hivi!”
Binadamu akamwambia Nyoka, “La! La! La! Hiyo si haki. Hebu tumuulize Nyuki.”
Nyuki alipoulizwa naye alisema kuwa binadamu hurina asali yake na kumfukuza kwa
mioshi kutoka kwa makazi yake. Binadamu hakuridhishwa na jibu la Nyuki. Akamwomba
Nyoka aulize Mwembe. Nao Mwembe ukasema, “Mimi sijawahi kutendewa haki na
Binadamu. Yeye hutunda matunda yangu msimu baada ya msimu. Anapoona kwamba
utasa umeniingia, yeye hunikata na kunitumia kujitengenezea makaa.” Binadamu
kijasho kikaanza kumtoka. Hata hivyo, akamwomba Nyoka aulize maoni ya Mnazi.”
Nao Mnazi ukasema, “Ni kweli kuwa wema hulipwa kwa ubaya. Binadamu huchukua
nazi zangu, akazikuna na kutumia tui apendavyo. Majani yangu nayo huyachukua'
kuezekea nyumba. Hata shukrani ya mbolea tu hajawahi kunipa.”
Nyoka akamwambia Binadamu, “Unaona sasa? Kigumba kwa nguruwe kwa
binadamu ki uchungu.” Binadamu akakubali. Hata hivyo akamwomba Nyoka ampe
fursa ya kumuaga mkewe. Nyoka akaridhia ombi la binadamu. Binadamu akaenda
kumwambia mkewe kisa chake. Mama mtu michirizi ya machozi ikatiririka njia nne nne.
Akaamua kwenda kuongea na Nyoka, “Bwana Nyoka, nimeona itakuwa bora nikikupa
mayai ule kabla ya kumla mume wangu.” Nyoka akaongozwa na tamaa kukubali. Mke
wa binadamu akachukua fuko lenye mayai na alipolifungua, Nyoka akaingiza kichwa
kuyatwaa mayai. Mara mke wa binadamu akavuta kamba iliyokuwa kwenye mdomo
wa fuko hilo na kufungia kichwa cha Nyoka ndani ya fuko. Kisha akachukua kisu
na kumkata Nyoka kooni. Maisha ya mumewe yakaokolewa. Hata hivyo, Binadamu
akakiona kitendo cha mkewe kuwa cha dhuluma. Akaamua kumtaliki mkewe. Wema
ukalipwa kwa uovu tena. Mjukuu wangu hadithi yangu inaishia hapo. ji
Sifa za mighani
(a) Mighani husimulia kuhusu watu na matendo yao ya kihistoria yaliyowahi kutokea.
Kwa mfano, inaaminiwa kuwa Fumo Liyongo ni shujaa wa Waswahili wa Pate aliyewahi
kuishi.
(b) Ingawa mighani huaminiwa kuwa ni matukio ya kweli, matukio yenyewe na uwezo
wa wahusika hupigwa chuku kiasi cha kuwafanya kuonekana kama si binadamu wa
kawaida. Kwa mfano, tunaambiwa kuwa Fumo Liyongo aliweza kuinua tani mia moja
za chuma.
(d) Kila jamii huwa na mighani yake mahususi ya mtu au watu waliotenda matendo ya
kukumbukwa. Mekatilili wa Medza wa Wagiriama, Lianja wa Wakongo, Wangu wa
Makeri wa Wakikuyu na Shaka wa Wazulu ni mifano ya mashujaa ambao walileta
mabadiliko makubwa katika jamii zao.
(e) Baadhi ya mighani huhusiana na visasili. Masimulizi ya Lwanda Magere, kwa mfano,
yanaeleza sababu ya Wajaluo kuabudu jiwe waliitalo “Mtemi Lwanda Magere'.
Inaaminika kuwa jiwe hili ni mwili wa Lwanda Magere.
(f£) Mashujaa husimuliwa kuwa na maumbile ya kiajabu. Huweza kuzaliwa wakiwa na
upungufu wa kiungo cha mwili, lakini wakawa na nguvu za ajabu.
(g) Mashujaa huangamizwa kwa njia ya kiajabu. Lwanda Magere, kwa mfano, aliuawa
kwa kuchomwa kivuli chake kwa mkuki. Naye Fumo Liyongo aliuawa kwa kuchomwa
sindano ya shaba kwenye kitovu. Katika Biblia, Samson aliishiwa na nguvu kwa
kunyolewa nywele tu!
Mashujaa huangamizwa na husalitiwa na watu wa karibu au jamaa zao. Fumo Liyongo,
kwa mfano, alisalitiwa na mwanawe, naye Lwanda Magere akasalitiwa na mkewe.
Samson, katika Biblia, alisalitiwa na mkewe.
(i) Mashujaa huangamizwa na watu wasiokuwa na uwezo kama wao. Kwa mfano, Fumo
Liyongo aliuawa na mwanawe, Samson katika Biblia alinyolewa na mkewe, naye
Goliathi akauawa na Daudi ambaye alikuwa kijana mdogo.
Umuhimu wa mighani
(a) Mighani hutambulisha jamii. Kila jamii ina mighani yake mahususi inayohusu watu
na matukio yaliyowahi kutokea katika historia yao. Mighani ya Lwanda Magere
inawatambulisha Wajaluo; Fumo Liyongo, Waswahili; Koome Njue, Wameru;
Syokimau, Wakamba.
(b) Mighani huelezea na kuhifadhi historia ya jamii kwa kuipitisha kutoka kizazi kimoja
hadi kingine. Pia hutaja mashujaa, vita walivyopigana, lini na dhidi ya nani.
(c) Hutumiwa kama sifo kusifu mashujaa kwa matendo yao. Mighani, kwa mfano, ya
Fumo Liyongo inamsifu Liyongo.
(d) Ni kumbukumbu kwa mashujaa kuonyesha kuwa jamii inatambua na kuthamini
mchango wao.
(e) Huhimiza uzalendo. Hadithi za mashujaa huwafanya watu kujitambulisha na mashujaa
hao na hivyo kukuza hisia za kizalendo. Vijana huhimizwa kupigania jamii zao kama
mashujaa hao walivyofanya.
Huonya dhidi ya matendo kama vile usaliti na kupuuza mambo madogo madogo. Shujaa
aghalabu husalitiwa na mtu wa karibu, hivyo tunapotambiwa mighani, tunafunzwa
kutahadhari na watu wa karibu walio na hila —- Kikulacho ki nguoni mwako.
Hupitisha thamani na amali za jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kama
tulivyotangulia kutaja, baadhi ya mighani huoana na visasili. Kwa mfano, mwili wa
Lwanda Magere unapogeuka jiwe, jiwe hilo linakuwa takatifu kwa jamii ya Waluo.
Mighani hii inapotambwa, watu huelewa thamani inayohusishwa na jiwe hilo.
Kama tanzu nyingine za fasihi simulizi, mighani hutumiwa kuburudisha. Huburudisha
baada ya shughuli za mchana.
Huhimiza ujasiri na kutokata tamaa. Watu wanapoona jinsi mashujaa walivyopigania
nchi zao, wao hupata moyo wa kutokata tamaa.
Kama tanzu nyingine za fasihi simulizi, mighani hukuza ushirikiano. Watu hujumuika
pamoja kutambiwa mighani na hujihisi kundi kuwa moja.
Mfano wa mighani
Mojawapo ya mighani ambayo imesimuliwa kwa miongo mingi katika jamii ya Waswahili
ni mighani ya Fumo Liyongo. Liyongo alikuwa jagina wa jamii ya Wapate ambaye aliishi
Ungwana wa Mashaha, eneo la Shaka, katika jimbo la Ozi. Liyongo anasifika kama
shujaa wa vita-ambaye katu hakunywea mbele ya mahasidi wake hata kama mahasidi
hao wangekuwa na silaha kali kiasi gani. Inasimuliwa kwamba Liyongo alikuwa na tambo
ambalo liliwafanya watu kumwogopa. Alikuwa mrefu kiasi kwamba hata Wagalla ambao
waliaminiwa kuwa warefu sana walimfikia magotini tu. Liyongo alikuwa na nguvu
zisizomithilika. Inasimuliwa kwamba aliweza kuinua tani mia moja za chuma! Na hilo
lisionekane kubwa sana kwani Liyongo aliwahi kuusukuma mtumbwi uliojaa watu na
mizigo kutoka upande mmoja wa bahari hadi ule mwingine huku yeye amejikita kwenye
ufuo. Ama kweli shujaa huyu alikuwa na misuli ambayo haikuweza kushindwa na jambo
hata likawa na uzito wa nanga. Alikuwa simba ambaye kutembea kwake usiku kulikuwa
kama kutembea mchana.
Si kimo tu ambacho kiliwafanya waja kumwogopa Liyongo bali pia mtazamo wake.
Wengi walizimia mara tu alipowakodolea macho, na wengine kushikwa na kitapo
alipowatokea ghafla. Umaarufu wa Liyongo katika uwanja wa vita ulimvutia sana
Mfalme Daudi Mringwari, kakake Liyongo. Mfalme aliusifia ujagina wa Liyingo kwa
Wagalla ambao walikuwa mabingwa vitani. Wagalla hawakuyaamini maneno ya Mfalme
hadi pale alipoagiza Fumo Liyongo kusafiri kutoka Shaka hadi Pate ili Mfalme apate
kuwasadikisha Wagalla kuwa avumaye baharini papa, kumbe wengine wapo! a
Basi Liyongo akashika tariki kuelekea Pate, kwenda kuitika wito wa Mfalme.Kutoka
Shaka hadi Pate ni safari ya siku nne kwa miguu, naye Liyongo alidiriki kufika Pate
baada ya siku mbili. Kuwasili kwa Liyongo Pate kuliandamana na shani kuu. Liyongo
alipokaribia Pate alipuliza panda mara tatu zikipasuka, nao mji mzima ukatanabahi kuwa
Liyongo keshawasili. Umati mkubwa ukakusanyika kwenye baraza la mfalme kujionea kwa
macho yao mja huyu wa kugandisha damu kwenye mishipa, ikawa ni kama waliostaajabu
ya Musa na sasa wenda kushuhudia ya Firauni. Mara tu Liyongo alipotia guu kwenye
kizingiti cha kasri la Mfalme, alitua mizigo aliyokuwa amebeba, nalo! Mizigo hiyo ilijaza
nyumba nzima. Wagalla wakahizika, wakaamini kuwa kweli Liyongo ni jabari. Ujagina
wa Liyongo ukawatuma Wagalla kutaka kuunga udugu naye, angaa wajinasibishe naye.
Wakamwomba Mfalme awaruhusu wapate mbegu ya Liyongo. Mfalme akaridhia ombi
lao na kumwoza Liyongo kimanzi wa Kigalla. Liyongo na kidosho huyu wakazaa mvulana
ambaye alikuzwa vyema, akainukia kuwa ghulamu mwenye heba na nguvu.
Walisema wasemao kuwa mti huanguka kwa tundaze. Umaarufu wa Liyongo ndio
uliomchongea kwa Mfalme ambaye kadiri siku zilivyosonga ndivyo mshale wa wivu
ulivyomfuma na woga wa kunyang'anywa ufalme ukaukuza zaidi mgogoro kati ya ndugu
hawa. Mfalme akataka kumwangamiza Liyongo alakulihali. Liyongo akagundua feli ya
Mfalme na kutorokea nyikani ambako aliishi na Wasanye, Wadahalo, Waboni na Watwa.
Ari ya kutaka kumwangamiza Liyongo ilimsukuma Mfalme kula njama na Wasanye na
Wadahalo. Akawaahidi kuwapa reale mia ili kumletea kichwa cha Liyongo. Ukatili ulioje!
Kwa kujua uwezo wa Liyongo, ilibidi Wasanye na Wadahalo kujifanya kuwa marafiki
wa Liyongo ili watekeleze mradi wao. Wakapanga kutunda makoma kutoka mtini na
kula kikoa, wakitarajia kuwa zamu ya Liyongo ikifika atapanda mtini, wapate kumuua,
bila kujua kuwa akili ya Liyongo iliyokuwa inashika kama sumaku ilikuwa imekwisha
kugundua hayo! Zamu ya Liyongo ilipofika alichukua mshale wake akayaangua matunda
kikwi kwa mshale uo huo. Maadui wakala shibe yao huku wakiugulika. Wakampasha
Mfalme habari kuwa Liyongo ni jabali ambalo mijusi hawawezi kulikwea.
Mfalme hakufa moyo. Wanasema kuwa mbwa hafi maji akaribiapo ufuo. Naye
Mfalme alihisi kuwa alikuwa karibu kama pua na mdomo katika kuizika historia ya
Liyongo katika kaburi la sahau. Akatayarisha shambulizi jingine, mara hii akihakikisha
kuwa ametumia akili kweli kweli. Akawatuma wale wale wajumbe aliokuwa amewatuma
awali kumwambia Liyongo kuwa mjini ku salama; kwamba angeweza kurejea nyumbani. |
Liyongo, pamoja na uwekevu wake akaanguka kwenye mtego huu. Akarejea mjini |
ambako aliviziwa na askari wa Mfalme akicheza gungu na mwao, ngoma ambayo Liyongo
akiisakata kwa faka kuu, na ambayo alikuwa mahiri kwayo.Liyongo akatiwa kizuizini,
akawa anangojea hukumu ya kifo.
Liyongo alihesabu siku gerezani akisubiri mauko yake. Hakungoja jinsi kondoo
angojeavyo kutiwa sime shingoni na kudhulumiwa sufu yake! La hasha! Liyongo aliwazia
mkakati wa kujiopoa. Akaona kuwa njia ya pekee ya kuepuka mauti yaliyomkodolea
macho ni kutoroka gerezani. Akamwandikia mamake shairi ambalo lilimtaka kuoka
mkate wa wishwa na kuitia tupa ndani ili Liyongo apate kifaa cha kukerezea minyororo.
Mamake Liyongo hakukawia kufanya hivyo. Japo mama mtu alijua kuwa tendo hilo
lilikuwa hatari, uchungu wa uzazi ulimtuma kujisabilia kwa mwanawe.
Liyongo akakata pingu na kuvunja lango la gereza. Kwa viganja vyake akarejesha
uhuru wake na kurudi tena nyikani.
Tamaa ya utukufu na uluwa ni kama kiu ya maji, haikatiki hadi pale mtu ayapatapo
maji, akakinai na hata kupiga mbweu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Mfalme. Alipogundua
kuwa Liyongo katoroka, aliamua kutumia mshale wake wa mwisho uliokuwa kwenye
riaka.Mara hii alihakikisha kuwa amelenga ndipo. Alimwendea mwanawe Liyongo na
kumrai amuulize babake ni kitu gani ambacho kinaweza kumuua, kwani Mfalme tangu
hapo alikuwa ametanabahi kwamba Liyongo hafi hata kwa mzinga hatari. Shababi
akaahidiwa uwaziri na kuozwa binti ya Mfalme. Wazo la kuozwa huyu hurulaini
likaupujua utu wa rijali huyu. Akafunga safari hadi Shaka ambako Liyongo, japo alijua
njama ya mwanawe alimwambia kuwa angeweza kufa tu kwa kudungwa kwa sindano |
ya shaba kitovuni. Kijana aliposikia hayo alifurahi na kurudi kwa Mfalme kumpasha
habari. Mfalme alifurahi na kumtuza kijana zawadi maridhawa. Akampa sindano ya |
shaba na kumtaka akamuue baba yake.Kijana akarudi kwa baba yake, akamwotea akiwa
usingizini na kumchoma kwa ile sindano.
j
W. |
|
ji
(r)
Liyongo alikurupuka kwa ghamidha kutoka usingizini, akachukua upinde na
kuelekea kisimani akijua kuwa hatima ya maisha yake ilikuwa imefika; anakufa kifo
cha mwana alompa uhai yeye. Alipofika kisimani, Liyongo alitia mshale kwenye upinde
huku anauelekeza mjini na kukata roho huku waliokuja kumtazama wakidhani bado yu
kwenda kuchota maji kisimani. Wakamlilia jagina wao huku wakimmiminia sifa,
wakamrai azungumze nao ila hawakuambulia lolote. Mama mtu alipiga moyo konde
na kwenda kisimani, roho mkononi, zingizi ya uzazi ikimkeketa si haba akampembejea
mwanawe kuondoka kisimani. Hewa ya mandhari hayo ikahanikiza mashairi. Mama
akaimba, akaghani, akakariri ... Kimya. Hatimaye mwili wa Liyongo ukasalimu amri
baada ya siku kadha, mwamba uliokuwa tayari umeanza kuoza ukaanguka. Maskini mama
mtu akakitazama kifo kikimpoka mwana alokuwa tegemeo la jamii. Wingu la huzuni
likatanda eneo zima. Mbolezi za akina mama zikapamba kutwa hiyo ya kiza, wakawa
kama wanawakiwa, wakamlilia shujaa wao kwa beti ali ali:
Visakale
Visakale ni masimulizi ya kimapokeo ya matukio yaliyotendeka zamani. Matukio haya
yanaweza kuwa ya kweli lakini yakaongezwa ubunifu na kuyafanya yaonekane kama ya
kubuni tu. Visakale husimulia masuala kama vile:
(a) vita
(b) hamahama za jamii
(c) majanga ambayo jamii ilikabiliana nayo kama vile njaa, na maambukizi ya magonjwa.
Wahusika katika visakale ni binadamu. Visakale na mighani hulingana kwa kuwa vinahusu
matukio ya kihistoria. Mighani huangazia mashujaa katika jamii ilhali visakale husimulia
matukio mengine yote ya kihistoria katika jamii. Hamahama za jamii ya Waisraeli kutoka
Misri, kupitia jangwani hadi Nchi ya Agano (Kanaani) katika Biblia ni mfano mwafaka wa
kisakale.
aa Ji
Visasili
Visasili ni hadithi za kale ambazo huelezea imani na mtazamo wa jamii kuhusu asili ya
ulimwengu na mwenendo wake. Hufungamana sana na masuala ya kiimani au kidini na
mitazamo ya jamii kuhusu asili ya miviga kama vile tohara, ndoa na unyago na utaratibu
uliozingatiwa katika desturi hizo. Visasili huelezea pia chanzo cha kifo, asili ya jamii
fulani na asili ya maumbile mbalimbali ya kiasili kama vile milima na mito. Aghalabu,
visasili huaminiwa kuwa ukweli usiopaswa kuuliziwa maswali. Kimsingi, visasili hutumiwa
kuhalalisha desturi, miiko na madhehebu ya jamii iliyovizaa. Wahusika katika visasili
huweza kuwa binadamu au miungu. Visasili vinaweza kuainishwa katika makundi mawili:
vya usuli na vya kidini, kutegemea majukumu yake.
Visasili hutofautiana na ngano za usuli. Ngano za usuli hueleza sababu za hali, maumbile au
mahusiano ya kawaida katika jamii ilhali visasili hueleza chanzo au asili ya hali, maumbile
na mienendo ulimwenguni.
Visasili hujikita katika imani fulani za kidini ilhali ngano za usuli ni zao la ubunifu tu.
Visasili huaminiwa kuwa vya ukweli lakini ngano za usuli hubuniwa na jamii katika kujaribu
kueleza sababu za hali, maumbile au mahusiano.
Visasili huwa na wahusika miungu na mandhari yasiyo ya kawaida. Wahusika binadamu
katika visasili ni mashujaa au majagina kama vile Gikuyu na Mumbi kwa Wagikuyu au Sera
na Mwambo kwa Waluhya.
Sifa za visasili
(a) Visasili ni hadithi za kinathari ambazo zinaaminiwa kuwa ni masimulizi ya kweli
kuhusu tukio linalosimuliwa kama lilivyotukia zamani za kale.
(b) Husimulia mambo ya kiimani au kidini kama yanavyoaminiwa na jamii.
(c) Hukubaliwa na jamii husika na kuaminiwa kuwa vya kweli. Kwa mfano, Wakikuyu
huchukuliwa kuwa ni kizazi cha Gikuyu na Mumbi.
(d) Huwa na misingi ya kihistoria. Tangu jadi, kwa mfano, jua hupatwa. Jamii hujaribu
kueleza na kuhalalisha kupatwa huku kwa jua.
(e) Visasili huweza kuwa na wahusika binadamu mashujaa, miungu, wanyama, mawe na
vitu vingine.
(£) Matendo ya wahusika katika visasili hukitwa katika ulimwengu wa asili au mwanzo
wa ulimwengu ambao ulikuwa tofauti na ulimwengu wa kisasa au katika ulimwengu
mwingine wa mbinguni au wa kufikirika tu.
Umuhimu wa visasili
(a) Hutumiwa kuhalalisha baadhi ya desturi na imani katika jamii fulani, kwa mfano
sababu za kuabudu miti, mawe, milima na miungu wengine.
(b) Huelezea asili ya mambo, kwa mfano asili ya kifo, maisha na tamaduni mbalimbali
kama vile uwindaji.
(c) Nikitambulisho cha jamii. Kila jamii huwa na visasili ambavyo hufungamana na imani
za jamii husika. Chanzo cha kifo, kwa mfano, hufafanuliwa kwa njia tofauti tofauti
kutegemea imani ya jamii. Tofauti hizi hutambulisha upekee wa kila jamii.
(d) Huonyesha na kuhifadhi historia, imani na utamaduni wa jamii. Imani hizo hupitishwa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
(e) Hupunguza athari za baadhi ya majanga kwa watu. Kwa mfano, watu hukubali kifo
kwa sababu kimehalalishwa; kwamba kila binadamu lazima afe. Wanaamini kuwa si
kosa lao kufa na hivyo hupunguza uchungu baada ya kufikwa na kifo.
(£) Huadilisha. Kila kisasili hutoa maadili. Katika baadhi ya jamii, kinyonga alisababisha
kifo. Wenye imani hii huonya dhidi ya kufanya mambo polepole.
(g) Ni nyenzo ya kudhibiti tabia na matendo ya watu. Yapo baadhi ya maeneo kama vile
mibuyuni ambayo huchukuliwa na jamii zingine kuwa madhabahu au pahali patakatifu
pa ibada, hivyo ni mwiko kucheza katika maeneo haya. Wanajamii huonywa dhidi
ya kukata miti humo. Aidha, jamii nyingine huamini kuwa mibuyuni ni makao ya
mashetani, hivyo wanajamii huonywa dhidi ya kwenda humo.
Mfano wa kisasili
Mulungu ndiye aliyemuumba binadamu. Kwa vile Mulungu ni mwema daima aliwaambia
malaika wake, “Nisingependa binadamu wawe wakifa kabisa. Ningependa binadamu akifa
awe anafufuka.” Basi akawaumba binadamu na kuwaweka katika eneo jingine mbali na
alikoishi yeye Mulungu.
Karibu na nyumba ya Mulungu, paliishi kinyonga na ndege aitwaye Mnana. Katika
mtagusano wao na Mulungu, Mulungu aliweza kung'amua kuwa ndege huyo alipenda
kutia chumvi maneno na hata kusema mambo kinyume na alivyoambiwa. Akamtambua
kuwa kiumbe asiyeweza kuaminiwa. Kwa upande mwingine, kinyonga alikuwa mwadilifu
na mwenye busara. Hakusema uongo.
Mulungu alipoona kuwa wakati umefika wa kumpasha binadamu ujumbe wa uzima
alimwita kinyonga na kumwambia, “Nenda katika eneo ambamo nimewaweka binadamu.
Waambie kuwa yeyote atakayekufa atafufuka.” Kinyonga alisujudu na kusema, “Ndiyo,
Mulungu.” Hata hivyo, kinyonga alitembea polepole kama kawaida yake. Mnana alibaki
nyumbani kwa Mulungu. Kinyonga akahesabu hatua zake polepole akihofia kuumiza
ardhi ya wenyewe. Alipofika alikuwa yu hoi, nguvu zimemwishia. Aliwakuta binadamu
wamekusanyika pamoja. Taratibu akaanza kutoa ujumbe wake, “Nime ... nime ...
nimeambiwa ...” lakini hakudiriki kusema aliloambiwa.
Mnana alimwomba Mulungu udhuru wa kuondoka. Mulungu akamridhia, naye
akaruka moja kwa moja. hadi alikoishi binadamu. Alimkuta kinyonga katika harakati
zake za kusema 'nime ... nime ... nimeambiwa” huku watu wakingoja kwa matarajio
makuu kusikia alichoambiwa. Mnana alipofika, kinyonga alikuwa amechoka kiasi cha
kusahau ujumbe wenyewe. Kinyonga alipomwona Mnana akamuuliza, “Tuliambiwa nini
na Mulungu?” Naye Mnana bila kuchelewa akasema, “Tuliambiwa kuwa binadamu wakifa
wataangamia na kudidimia kabisa kama mizizi ya mshubiri.” Kinyonga akashangaa na
kusema, “Lakini tuli ... tuli ... tuliambiwa kwa ... kwamba ... bin ... bin-adamu wakifa
... wa ... Wata ...watafufuka tena ...” Hata hivyo kinyonga alikuwa amechelewa. Watu
walikuwa wametawanyika wakaelekea makwao, nyuso wameziinamisha.
Sifa za vigano
(a) Vigano ni hadithi fupifupi.
(b) Vigano husimulia kisa kimoja tu.
(c) Wahusika katika vigano ni binadamu au wanyama.
(d) Vigano hukusudia kuadilisha hasa kwa kutumia methali au kuthibitisha na kusisitiza
katika methali.
Tarihi
Tarihi ni rekodi za matukio ya kihistoria. Katika tarihi, matukio hupangwa kulingana na
jinsi yalivyofuatana kiwakati. Tarihi huwasilishwa kwa njia ya masimulizi bila kutolewa
ufafanuzi.
Ingawa tarihi hazichukuliwi kama tungo za kisanaa, baadhi yazo hutumia mbinu za kifasihi
na hivyo kuzifanya zichukuliwe kama fasihi. Kwa kawaida, tarihi hutokea katika maandishi.
Kwa kiasi fulani, sifa hii hufanya tarihi kutofautiana kidogo na fasihi simulizi. Aghalabu
tarihi husimulia kuhusu familia za kifalme. Mfano wa tarihi ni Habari za Wakilindi, Tarihi
ya Kilwa na Tarihi ya Pate.
OO
Kumbukumbu
ambamo
Kumbukumbu ni maelezo ya kitawasifu au kiwasifu ambayo husimulia matukio
ambayo
msimulizi amehusika binafsi au jamii yake. Mfano wa kumbukumbu simulizi
iliwahi kuandikwa ni Uhuru wa Watumwa ya James Mbotela.
Soga/Visoga
ta
Hizi ni hadithi fupi za utani au ucheshi. Soga hutumiwa kukejeli jambo kwa kufumba
Soga kwa
ukweli wake katika kicheko. Hivyo, hukashifu tabia fulani kwa njia ya ucheshi.
kawaida hutolewa katika vikao vya kupitisha muda.
Mfano wa soga
miguu kwenda
Mama mmoja alikuwa amebeba mzigo mzito huku akitembea kwa
eka alikokuwa
sokoni. Msamaria mwema alisimamisha gari na kujitolea kumpel
u mgongoni,
anaelekea. Mama huyu aliketi kwenye kiti cha nyuma huku mzigo wake
kacheka na
hautui. Dereva alipomwuliza sababu ya kutoutua mzigo, mama aliche
na zigo jingine
kusema, “Gari lenyewe naliona dogo mno. Kulipagaza uzito huu wangu
itakuwa dhuluma kubwa. Acha nilipunguzie uzito.”
husu magari.
Kisa hiki kinaonyesha kwamba mama huyu ni limbukeni wa mambo yanayo
garini.
Haelewi kwamba hata asipouweka mzigo chini, uzito utabakia mlemle
1. Dhamira
mwisho. Ni sababu
Dhamikra ni wazo kuu linalojitokeza katika hadithi kuanzia mwanzo hadi
dhidi ya ubinafsi,
kuu ya kusimulia hadithi fulani. Hadithi inaweza kudhamiria kuonya
kwa dhamira.
unafiki au tamaa. Aghalabu, maadili katika hadithi hujitokeza kupitia
2. Maudhui
. Mfano wa
Maudhui ni masuala ambayo hushughulikiwa na mtambaji katika hadithi
.
maudhui ni tamaa, usaliti, ulaghai, ubinafsi, umaskini na uongozi
3. Fani
Fani ni mbinu zote ambazo mtambaji hutumia kufanikisha utambaji wake. Fani hujumuisha
matumizi ya lugha na tamathali zake, wahusika, ploti, uigizaji, urudiaji, nyimbo na vipengele
vingine kama vile kupanda na kushuka kwa sauti.
1. Ploti
Huu ni mfuatano wa matukio kulingana na jinsi yanavyosababishana. Kwa kawaida, ploti
ya hadithi nyingi huwa na mtindo sahili au wa moja kwa moja. Haina matumizi mengi ya
mbinu rejeshi na vipengele vingine ambavyo huenda vikaifanya hadithi kuwa changamano.
Kwa kawaida ploti ya hadithi huwa na mgogoro mmoja ambao ndio unaosukuma hadithi
mbele. Hata hivyo, kuna baadhi ya hadithi ambazo huwa na ploti changamano. Ploti za
aina hii huwa na migogoro miwili au zaidi.
Kimuundo, ploti ya hadithi huwa na sehemu tatu kuu:
(a) Mwanzo: Mwanzo wa hadithi huweza kujumuisha fomyula ya ufunguzi wa hadithi
kama ilivyojadiliwa awali. (Tazama fomyula katika ngano ukurasa 26 — 28) Ngano za
kimapokeo huchukua mianzo kama iliyokwisha jadiliwa katika fomyula.
(b) Katikati au mwili: Sehemu hii ndiyo hutoa habari zote zinazohusiana na hadithi.
Mgogoro unaomkabili mhusika mkuu hukuzwa hapa. Kwa kifupi, hadithi yenyewe
husimuliwa hapa.
(c) Mwisho: Katika hadithi, mwisho hujumuisha fomyula za kumalizia. Aghalabu hadithi
nyingi za kimapokezo huishia kwa '... wakaishi raha mustarehe” au “Hadithi yangu
inaishia hapo'. Sehemu hii pia huonyesha utatuzi/mwisho wa mgogoro unaomkumba
mhusika mkuu.
Mambo yanayozingatiwa katika uchambuzi wa ploti ya hadithi
(a) Wahusika: Je, hadithi ina wahusika wangapi?
(b) Mgogoro: Kuna migogoro mingapi inayomkabili mhusika mkuu?
(c) Utatuzi: Juhudi zinazotumiwa na mhusika mkuu kukabiliana na mgogoro au tatizo
linalokabili ni gani?
(d) Mtiririko: Matendo yanafuatana na kusababishana vipi kuanzia mwanzo hadi
mwisho?
(e) Kuna matukio yepi makuu au ya kimsingi? Matukio hayo yanahusiana vipi?
(£) Ni nini upeo wa juu wa hadithi yenyewe? Kwa mfano, katika baadhi ya ngano za
mazimwi, upeo wa juu ni kuuawa kwa zimwi na kurejea kwa amani katika jamii.
(g) J e, hatimaye kuna suluhisho gani kwa tatizo linalomkumba mhusika mkuu?
(h) Hadithi inachukua muundo wa aina gani? Ina mwanzo, katikati na mwisho?
(3)
2. Mandhari
Mandhari ni mazingira ya mahali, wakati na hali inayozunguka tukio fulani. Kwa sababu
ya ufupi wa hadithi, mara nyingi mandhari hayafafanuliwi kwa kina.
Katika kuchanganua mandhari ya hadithi tunajiuliza maswali yafuatayo:
mandhari ya
(a) Tukio linatokea wapi? Matukio katika ngano, huweza kutokea katika
kifantasia au kiajabu kama vile ndani ya matumbo ya majitu, katika ulimwengu wa
mazimwi au mazingira ya kawaida.
(b) Tukio linatokea katika hali gani? Je, ni katika hali ya njaa, kiangazi, shibe, vita au
majonzi?
za
(c) Tukio lilitokea lini? Je, ni zamani za kale, usiku au mchana? Aghalabu hadithi
kimapokeo hujikita katika muda mrefu uliopita.
3. Wahusika
za binadamu
Wahusika ni viumbe vya kisanaa ambavyo mtambaji hutumia kuwakilisha tabia
katika jamii husika. (Rejelea wahusika katika fasihi simulizi kurasa 15 — 18.)
maana
Katika usimulizi wa hadithi, mpaka kati ya wanyama na binadamu hufutwa. Hiiina
u.
kuwa wanyama huweza kusawiriwa wakizungumza na kujadiliana na binadam
yafuatayo:
Katika kuchanganua wahusika katika hadithi, mhakiki anastahiki kujibu maswali
Kwa kujibu swali hili
(a) Hadithi inamhusu nani? Je, ni fisi, sungura au shujaa wa vita?
utakuwa unamtambulisha mhusika mkuu.
mawe?
(b) Je, wahusika ni wa aina gani? Ni binadamu, mazimwi, mimea au
ni shujaa
(c) Je, mhusika mkuu amesawiriwa vipi? Ni nguli au ni hasidi? Mhusika nguli
a hasidi
au jasiri asiyeogopa ambaye kwa kawaida hutetea maadili ya jamii. Mhusik
naye ni adui au mpinzani wa nguli au anayepigana na maadili ya jamii.
au mafunzo
(d) Je, mhusika huyu anawakilisha hali gani katika jamii? Anatoa maadili
gani?
(e) Je, kuna wahusika wengine wangapi katika hadithi na wana sifa gani?
o kati yao?
(£) Wahusika wengine wanaingiliana vipi na mhusika mkuu? Je, kuna mgogor
atendayo?
(g) Je, ni misukumo (motisha) au hali gani inayomfanya mhusika mkuu kutenda
kilisha hali gani?
(h) Wahusika wana mchango au umuhimu gani katika hadithi? Wanawa
Wanasaidia vipi kuiendeleza hadithi?
ni mhusika
(i) Je, wahusika hawa ni wa aina gani? Ni bapa? Ni duara? (Mhusika bapa
asiyebadilika; kama ni mui hubaki mui hadi mwisho. Mhusika duara hubadilika.)
a wengine
(j) Je, mhusika huyu hufanya nini na husema nini kujihusu? Je, wahusik
wanasema nini kumhusu?
ai
4. Lugha |
Lugha huchukua nafasi kubwa sana katika hadithi na fasihi simulizi kwa jumla kwani
ndiyo malighafi ya fasihi simulizi. Katika usimulizi wa hadithi, fanani aghalabu hutumia
lugha yenye: |
(a). sentensi fupifupi. Sentensi fupi ni rahisi kueleweka na pia hazina uchovu wa kufasiri |
dhana nyingi kama ilivyo katika kauli moja ndefu. Aidha, sentensi fupi hujenga
taharuki upesi na huondoa uchovu au ukinaifu.
(b) tamathali za usemi. Hizi hutumiwa kujengea taswira au picha ya matukio
yanayosimuliwa akilini mwa msikilizaji. Taswira (picha) huweza kujengeka kwa
kusikiliza sitiari, tashbihi na tanakali za sauti.
(c) vichekesho. Hivi hutumiwa kuteka makini ya wasikilizaji na pia kuwafanya wasisahau
yanayosimuliwa.
(d) nyimbo. Nyimbo hushirikisha hadhira na hazisahauliki kwa urahisi. Pia, nyimbo
huupa usimulizi uhai na kuondoa uchovu unaotokana na masimulizi makavu. Aidha |
nyimbo huwazindua waliokuwa wakisinzia wakati wa masimulizi. Mawazo makuu pia |
hupitishwa kupitia nyimbo katika hadithi. |
(e) takriri. Hiki ni kipengele cha lugha kinachohusu kurudiarudia maneno fulani au
vifungu vya maneno ili kuyasisitiza. Kwa mfano, badala ya kutumia viwakilishi vya
nomino, fanani hurudia majina ya wahusika. Kibwagizo katika wimbo pia hukaririwa.
Hapo zamani za kale, Nyani na Mamba walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Watoto wao
walipendana na kufaana kama ndugu wa toka nitoke. Familia ya Mamba iliishi mtoni
nayo ya Nyani iliishi katika msitu uliokuwa maili thelathini kutoka mtoni. Kila mara
marafiki hawa walitembeleana na kusaidiana kwa hali na mali. Kwa vile Mamba alikuwa |
mvuvi mashuhuri, aliweza kumwauni Nyani na aila yake kwa samaki wa aina mbalimbali. |
Nyani naye alimpelekea Mamba matunda na nafaka kutoka shambani mwake. |
Urafiki wao ulikita mizizi na kunawiri zaidi wakati Mamba alipokuja kwa Nyani
kumposea mwanawe binti. Ukwe uliutilia viungo uhusiano wa Nyani na Mamba
wakawa wanagandana kama kupe na mkia wa ng'ombe. Wakatenda mengi pamoja.
Wakazungumza ya kupwa na ya kujaa. Hakuna hata mmoja wao aliyeutilia shaka |
uaminifu wa mwenzake. Wake zao nao walifuata kaida ya maji kufuata mkondo.
Walikuwa masahibu wa chanda na pete. ;
Msimu mmoja wa mapukutiko ulishuhudia mabadiliko ya kudumu katika maisha ya
Nyani na Mamba. Wakati huo, bahari ilichafuka si haba. Kazi ya Mamba ya uvuvi ikaanza
kukabiliwa na majabali ya kila aina. Kila mara Mamba alipokwenda uvuvini, alirudi
akichekelewa na nyavu zake. Hakuambulia chochote. Njaa ilianza kubisha hodi katika
familia ya Mamba. Hali hii ilitishia kuutia ufa urafiki kati ya Mamba na Nyani. Mamba
alivamiwa na pepo ambaye hata yeye alishindwa kumfahamu. Kila mara alipomwona
55 |
(5) Ji|
alivyojaribu
Nyani au watoto wake alitamani kumdakia na kumla mzima mzima. Kadiri
ri, “Una njaa
kujiasa dhidi ya fikira hii mbovu ndivyo moyo wake ulivyoendelea kumshau
wanawe za kuwa
bwana, familia yako itaangamia. Je, huoni rafiki yako na familia yake
anajiita rafiki
kitoweo? Utaendelea kula wishwa hadi lini? Mbona huyo Nyani ambaye
karafuu alizokuwa
yako sasa amekata guu humu? Mbona haji tena kukutazama? Hata
na akasadiki kuwa
akikuletea ameacha kuleta.” Mamba akaanza kumshuku rafiki yake
Nyani alikuwa mla naye tu.
abu nyota,
Usiku mmoja baada ya kula mate na kujilaza kitandani mwake akihes
ili apate kujiokoa
wazo lilimjia. Alikata shauri kumlaghai rafiki yake wa miaka mingi
yake alikwenda kwa
yeye na familia yake kutoka katika kinamasi cha njaa. Asubuhi
agana nilipata
Nyani akiwa amejiinamia kwa jitimai. Alisema, “Rafiki yangu, jana tulipo
a mahututi. Alisema
tanzia. Mjumbe kutoka kijijini aliniarifu kuwa baba yangu ni mgonjw
majonzi makuu.
kwamba baba ananitaka nyumbani upesi.” Habari hizi zilimtia Nyani
Nyani hangeweza
Alimwahidi Mamba kwamba wangeandamana pamoja. Kwa vile
uchefu na manyezi kila
kutembea majini, ilibidi abebwe na Mamba. Alipatwa na kichef
hivyo, Mamba
alipotazama bahari iliyojitandaza mbele yao kwa mbwembwe. Hata
kana na urafiki na mazoea
alimhakikishia kuwa wangefika salama. Naye kwa imani iliyoto
ya miaka mingi, alitulia.
ni mwa
Safari ilikuwa ndefu na yenye machovu yaliyomfanya Nyani kulala mgongo
mbarika Nyani,
Mamba. Walipofika kwenye vina vya maji, Mamba aliamua kumpasulia
kumbe uzuri wako wa
“Rafiki yangu, nimekuwa nikidhani wewe ni rafiki wa dhati,
huku maghala
mkakasi? Mimi na wanangu tumetafunwa na njaa kwa miezi kadha sasa
kama nimepata
yako yakishiba na kutapika chakula. Hujadiriki hata siku moja kuja kujua
ia hali yangu,
hata senti moja ya kusagia mkunguni. Jana usiku nilipokuwa nikiwaz
basi hali ya
nilioteshwa katika ndoto kwamba kama ningepata moyo wako na kuula,
hata hivyo lisilo
uhitaji ingeniishia. Moyo wangu unaniuma sana kukufanyia tendo hili,
budi hutendwa.”
Hata hivyo,
Nyani alipigwa na butwaa nusura moyo wenyewe ujikabidhi kwa Mamba.
pole sana ikiwa
akili yake nyepesi ilifanya kazi. Alimwambia Mamba, “Ndugu yangu,
/
umekuwa unadhani sikujali. Kwa kweli, hata ungeniomba
moyo wangu siku hizo ningekupa tu. Unajua tena sisi
Nyani, Tumbili na Kima tuna mioyo mingi. Hata
hivyo, nasikitika kuwa Mungu alituambia kuwa
daima mioyo yetu itakaa mitini. Hii ndiyo sababu
tukajenga nyumba zetu juu ya miti. Basi ndugu
mpenzi, badala ya kuendelea na safari hii, turudi
pale mtini nikupe moyo wangu pamoja na mitatu
ya wanangu kusudi uwalishe wanao na mkeo.” 4
Mamba akaingia mtegoni. Wakarudi hadi ufuoni.
Kwa vile Mamba hakuweza kutoka majini, alibaki
ufuoni akimngojea rafiki yake amletee mioyo.
Mamba alitunga macho yake kwenye ujia alioufuata Nyani akiomba pasitokee |
lolote la kumchelewesha Nyani. Matumbo yalimnguruma kwa njaa. Roho ikampapa |
kwa tumaini. Alingoja, akangoja, akangoja ... wiki, mwezi, mwaka ... Nyani hakurudi.
Mamba akajua amepwaguliwa na Nyani. Akaapa kumtafuta kwa udi na ambari. Huo
ukawa mwisho wa urafiki kati ya Nyani na Mamba.
ia
Kwa kurejelea ngano uliyoisoma, jibu maswali yafuatayo.
1. Hii ni ngano ya aina gani? Thibitisha.
2. Fafanua sifa za wahusika wafuatao:
(a) Mamba (b) Nyani.
3. Andika na utolee mifano, sifa za kimsingi za hurafa ambazo zimejitokeza
katika kisa hiki. |
Andika maadili ya kisa hiki. ; '
Onyesha mbinu tano za lugha zinazojitokeza. YAI |
mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko,” wangemtania. |
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya |
ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa zaidi na nongwa za kila siku |
zilizotokana na ukewenza. Familia ya Mzee Kata ikawa medani ya vita vya wenyewe
kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba ya Mzee Kata amani. Asubuhi |
moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida na kuelekea katika kibanda cha mke wake wa ji
kwanza. Kama kawaida yake, alijikohoza kama ishara ya kutangaza kufika kwake. Daima |
hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea |
nuksi. Kinyume na siku nyingine, Mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani |
mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu ya |
kitanda cha mayowe ambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hana
Pumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee
(s7)7 ||
(57)
| |
|
Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu
Mzee Kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza.
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo
sasa alipata mwanya wa kumhini Majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye, huku
Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula haba; wengine wakila biriani
yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara. Siku zilivyozidi
kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa
Majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo
aliwafukuzia mbali. Wengine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa
kutaka kumwoa Majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake,
walinyeshewa matusi, wakahizika na kujiendea zao.
Siku moja, alitokea kijana mmoja maskini. Alikuja amevalia gwanda jeusi
lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia
iliyokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa
fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa
angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata
naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kijana huyu maana aliiona hii kama fursa ya
pekee ya kumwepushia vitimbi vya mama wa kambo.
Majaliwa aliandamana na mume wake hadi kijiji cha Peponi ambako kijana huyu
aliishi. Waliingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza maisha
ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofumbua macho, alijikuta
kalala ndani ya chumba kikubwa chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho
ulikuwa wa rangi ya zari. Mapambo ya dhahabu yalitundikwa ukutani. Kumbe kijana
aliyemwoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili
lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakuweza kuamini! Alikuwa ameamkia maisha ambayo
hakuwahi kuyawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni.
Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake
Majaliwa! Mumewe Majaliwa alishuhudia kwa mbali, machozi ya mama mtu na mwanawe
yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama maisha yao. Tangu
Usiku hiyo, watatu hawa waliishi kwa raha mustarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.
Utanzu wa Semi
Utangulizi
Semi ni kauli fupi za kisanaa zenye maana na mafunzo yaliyofichika. Semi hutoa mafunzo
kwa njia ya kufumba. Mafunzo katika semi hutokana na imani ya jamii ambayo imezibuni.
Mifano ya semi ni methali, vitendawili, misemo, nahau, misimu, lakabu, mafumbo,
chemshabongo na vitanza ndimi. Semi pia huitwa tungo fupi au tungo banifu.
Sifa za semi
(a) Semi hufumba ujumbe wake. Kwa mfano, maana ya ndani ya nahau 'piga kalamu' ni
“kufuta kazi' ilhali maana ya juu ni “kuchapa au kugonga kalamu'. Methali pia huwa
na maana iliyofumbwa. Aidha, vitendawili hufumba jibu.
(b) Hutumia picha (taswira) na ishara kupitisha ujumbe wake. Mtu anaposema, “kwetu ni
jehanamu', ile picha ya jehanamu inajichora akilini mwa msikilizaji. Jehanamu hapa
inaashiria mahali pabaya penye mateso. mengi.
(c) Maana ya semi hupatikana katika jamii iliyozibuni. Methali Mgaagaa na upwa hali
wali mkavu, kwa mfano, itaeleweka na jamii za pwani. Vilevile katika tashbihi, weupe
au weusi hulinganishwa na vitu mbalimbali kutegemea jamii na mazingira yake.
Mathalani, watasema -eupe kama maziwa au -eupe kama theluji; -eusi kama mpingo,
-eusi kama lami au -eusi kama makaa kutegemea vifaa vinavyopatikana katika jamii
husika. |
(d) Huwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machache. Mfano ni methali Juhudi si pato
ambayo imefupisha ujumbe mrefu kuwa mtu huweza kufanya bidii sana na akakosa
kufanikiwa. Semi huwasilisha ujumbe kwa njia ya mkato tofauti na hadithi ambazo
ni masimulizi marefu.
(e) Semi ni tanzu tegemezi. Hii ina maana kwamba semi hutokea kuambatana au
kutegemea tanzu nyingine. Kwa mfano, methali hutolewa katika muktadha wa
mazungumzo ya kutoa mawaidha, au mwishoni mwa hadithi kama funzo la hadithi.
3
Lakabu, misimu, misemo na nahau pia hupatikana katika utanzu wa mazungumzo.
Umuhimu wa semi
(a) Semi huelimisha. Vitendawili, methali, mafumbo na nahau zote hutoa mafunzo
ya aina fulani. Methali Mwenda pole hajikwai hutoa maarifa ya kufanya mambo
bila pupa. ;
(b) Hukuza uwezo wa kufikiria. Vitendawili, methali na mafumbo humhitaji mtu kufikiria
ili kupata ujumbe uliofumbwa. j
(c) Hutambulisha jamii na wanajamii. Kila jamii huwa na semi mahususi zinazohusu
shughuli zake. Misimu, kwa mfano, hutumiwa na kundi fulani katika jamii. Methali
mkulima ni mmoja walaji ni wengi inatambulisha jamii inayojihusisha na kilimo, ilhali
samaki mmoja akioza na mtungo pia inatambulisha jamii ya wavuvi. Vitendawili, misimu,
nahau na mafumbo pia hutofautiana kutegemea jamii. Kitendawili kimoja kinaweza
kuwa na majibu tofauti kutegemea jamii na mazingira yake.
(d) Hukuza utangamano katika jamii. Wakati wa kutegeana vitendawili, kwa mfano,
watu huja pamoja. Aidha, misimu hujenga uhusiano wa karibu miongoni mwa watu
wanaoitumia. Lakabu nazo hutumiwa na watu walio na uhusiano wa karibu.
Huburudisha. Baada ya shughuli za kazi, watu hujumuika pamoja katika vikao vya
kujiburudisha ambapo hutegeana vitendawili na hushiriki katika vitanza ndimi ili
kutuliza bongo na kusisimka pamoja.
Huhifadhi utamaduni. Semi hufumbata desturi za jamii. Zinapopitishwa kutoka kizazi
hadi kingine, utamaduni huo hurithishwa na kuhifadhiwa.
Husawiri mitazamo ya jamii kuhusu masuala fulani. Je, jamii inachukia nini? Inahimiza
nini? Kupitia kwa methali, bidii ya mja haiondoi kudura, tunafahamishwa kwamba
jamii hii inaamini kuwa binadamu yumo chini ya uwezo wa Mungu. Nahau, lakabu,
vitendawili na mafumbo pia hufumbata tajiriba ya jamii.
Hutasfidi lugha. Nahau, misemo, misimu na lakabu hutumiwa badala ya msamiati
mkali/wenye aibu. Badala ya kusema kuzaa tunasema kujifungua.
Hukuza lugha. Semi huyapa maneno maana mpya au maana ya ziada. Misimu
huweza kukubaliwa na kuwa nahau rasmi za lugha. Kwa njia hii, msamiati wa lugha
hupanuliwa.
Methali
Methali ni semi fupifupi za kimapokeo zenye kueleza fikira, maarifa, hekima na mafunzo
yanayotokana na uzoefu wa jamii mahususi. Methali hutumia taswira na mafumbo.
Chukulia, kwa mfano, Fimbo ya mbali haiui nyoka. Utungo huu ni mfupi, na unatumia neno
fimbo kama fumbo la suluhisho.
Methali ni utanzu tegemezi. Kama tulivyotangulia kutaja, kutumika kwake hutegemea tanzu
nyingine. Methali hutokea katika mazungumzo mazito kama vile katika kutoa mawaidha
au kama kielelezo na kifupisho cha hadithi. Si utanzu unaoweza kujisimamia kama tanzu
nyingine kama vile hadithi, ushairi au mazungumzo.
Sifa za methali
(a) Methali ni kauli fupi ambazo hutolewa kwa mtindo wa kishairi kinyume na jinsi kauli
za kawaida zinavyowasilishwa.
(b) Methali: Ushikwapo, shikamana; Aliye juu, mngoje chini, mathalani, zina sifa za kishairi:
kuwa na vipande vyenye mizani inayolingana na kwamba ni mshororo mmoja.
(c) Maudhui katika methali huchotwa kutoka kwa jamii zinamozaliwa. Maudhui hutokana
“na tajiriba na mambo yanayoathiri jamii.
(d) Huwa na muundo maalumu wenye sehemu mbili, kwa mfano Asiyesikia la mkuu,
huvunjika guu au Pilipili usiyoila, yakuwashiani?. Sehemu ya kwanza hudokeza wazo
na sehemu ya pili hulikamilisha kwa kukubali au kukataa.
(e) Hujengwa kwa tamathali nyingine za usemi na mbinu za lugha kama vile kinaya,
taswira na takriri. Methali Kukopa arusi kulipa matanga imejengwa kwa tamathali
ya sitiari. Arusi ni sitiari ya kukopa kuonyesha kuwa mtu anapokopa huhisi vizuri.
Matanga ni sitiari ya kulipa kuonyesha kwamba watu huona ugumu kulipa deni
walilokopa. Arusi ni jambo la furaha ilhali matanga ni jambo la huzuni.
(f) Methali hueleweka na jamii iliyozibuni, kwa mfano Kikiharibika cha fundi kikiongoka
cha Bwana Swedi kwa Waswahili, na methali ya Kikamba Yakua yiisawa ngathi ni aka
(Ng'ombe akizeeka nundu huliwa na wanawake). Katika jamii ya Wakamba, sehemu
fulani za nyama huliwa na wanaume, nundu ikiwa moja yazo. Hata hivyo ng'ombe
anapozeeka sana, utamu wa nundu huisha na wanawake wanakubaliwa kuila wakati
huo tu. Methali hizi mbili zina maana sawa. Hata hivyo, methali hizi hazitaeleweka
kwa watu wa jamii tofauti na iliyozibuni.
(8) Methali zina sifa ya utegemezi na huingiliana na tanzu nyingine za fasihi.
(i) Hutumiwa mwishoni mwa ngano kufupisha maadili ya ngano hiyo.
marafiki anaweza kuitwa
(ii) Hutumiwa kubuni lakabu. Mtu ambaye huwasaliti
“kikulacho' kutokana na methali Kikulacho ki nguoni mwako.
tamthilia ili kuongeza
(iii) Hutumiwa katika tanzu za kimaandishi kama vile riwaya na
ladha katika usimulizi.
mvuto.
(iv) Hutumiwa katika mazungumzo ya kawaida na ulumbi kuleta
(v) Hutumiwa katika nyimbo na mashairi.
daawa. Mshtakiwa
(vi) Hutumiwa katika hotuba rasmi au hata mahakamani katika
ishi
anaweza kujitetea kwa kurejelea methali Mavi ya kale hayanuki. Naye mlalam
kapoa. Aidha,
anaweza kusisitiza msimamo wake kwa kudai Mwenye kovu sidhani
mbio zako zimefika
mahakimu wanaweza kutumia methali kama vile Mshtakiwa,
ukingoni kutoa hukumu.
(vii) Hutumiwa katika kutoa mawaidha.
o imebuniwa.
(h) Methali huelezea ukweli ambao unakubalika na jamii ambam
mu wa kutolewa. Methali
(i) Tofauti na vitendawili, methali hazina muktadha maalu
anaweza kutumia
hazitengewi vikao vya kutolewa kama vitendawili vifanyiwavyo. Mtu
au usio rasmi.
methali wakati wowote anapozungumza katika muktadha rasmi
i, hakuna anayeweza
(j) Methali ni mali ya jamii. Kama tanzu nyingine za fasihi simuliz
kudai kumiliki methali.
hulka, itikadi, tamaduni na
(k) Methali huambatana na mazingira ya jamii iliyozizaa,
mea mazingira
tajiriba zake. Busara fulani inaweza kuwasilishwa kwa njia tofauti kutege
kana na jamii zilizo
ya jamii. Methali zifuatazo, kwa mfano, zina maana sawa ila zinato
na mazingira tofauti:
(i) Ulingo wa Kwae haulindi Manda.
(ii) Kamba ya mbali haifungi kuni.
(iii) Fimbo ya mbali haiui nyoka.
leza majukumu
(1) Methali zina matumizi mapana. Methali moja inaweza kutumiwa kuteke
Baada ya dhiki faraja
mbalimbali kama vile kuonya, kuelekeza na kufunza. Methali
inaweza kutumiwa:
(i) kuonya dhidi ya kukata tamaa
(ii) kuhimiza mtu asife moyo, avumilie, fanaka yaja
(iii) kutoa maoni tu kuhusu hali ya ukosefu
(iv) kushauri mtu awe na subira.
na na maana halisi
(m) Methali huwa na maana ya ndani na ya nje. Maana ya nje hutoka
ndani yenye fumbo
ya maneno yaliyoiunda. Vilevile, methali hupewa maana ya
lililofumbwa na maneno yanayoiunda.
Dhima ya methali
(a) Huelimisha. Methali hutumiwa katika hafla mbalimbali kama vile sherehe za jandoni
na arusi kupitisha maarifa ya kijamii kwa vijana. Methali Abebwaye hujikaza, kwa
mfano, inaelimisha wanajamii kuwa unapopata usaidizi fulani, nawe pia jikaze kutia .
bidii; usingoje kila mara kusaidiwa. Methali pia huelimisha kuhusu historia, siasa,
uchumi na utamaduni wa jamii. Methali Sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma
inaelimisha kuwa sheria haichagui. Aidha, Biashara haigombi inaelimisha kuwa ni
busara kwa muuzaji kuwabembeleza wateja wake.
(b) Huadilisha. Mbali na kuelimisha, methali hufunza maadili. Mstahimilivu hula mbivu
ni methali inayofunza uvumilivu. Nayo methali Tamaa mbele mauti nyuma hukashifu
tabia ya kuwa na uroho mwingi.
(c) Husawiri mitazamo na falsafa za jamii fulani kuhusu masuala mbalimbali. Je, jamii
inapenda nini? Inachukia nini? Inathamini nini? Methali Ucha Mungu si kilemba cheupe
huonyesha jamii inachukia unafiki. Vilevile, methali Uzuri wa mwanamke ni tabia
inaonyesha jinsi jamii inavyothamini mke mwadilifu.
(d) Hutambulisha jamii. Kila jamii ina methali zake zinazoitambulisha. Mathalani, Sie
munda sisuta sie emurwe (Kilicho tumboni ndicho kilicho akilini) ni methali kutoka jamii
ya Waluhya inayoonyesha umuhimu wa chakula. Ng'ombe akivunjika mguu malishoni
hujikokota zizini inatambulisha jamii ya wafugaji.
Uainishaji wa methali
Methali huainishwa kutegemea:
1. Muktadha
methali hizo.
Ili kuelewa methali, ni muhimu kujua mazingira, tamaduni na hali zilizozizaa
Methali ambazo zimezaliwa katika muktadha au mazingira sawa huweza kuwekwa katika
kundi moja. Methali Mpanda ovyo hula ovyo, Mke ni nguo mgomba kupalilia na Ukipanda
zinahusu
pantosha utavuna pankwisha huweza kuwekwa katika kundi sawa kwa sababu
muktadha wa kilimo.
2. Maudhui
kama
Maudhui na fani ndiyo hutawala methali. Maudhui katika methali ni mengi na mapana
zilivyo jamii na shughuli zake. Methali ambazo huwa na maudhui sawa huwekwa katika kundi
moja. Baadhi ya maudhui yanayojitokeza katika methali za Kiswahili ni ya:
(a) malezi, kwa mfano:
j
(b) kazi, kwa mfano:
(i) Kazi mbi si mchezo mwema.
(ii) Mchagua jembe si mkulima.
(iii) Kazi ya bakuli husiri.
(iv) Kazi isiyo faidi kutenda si ada.
(c) ushirikiano, kwa mfano:
(i) Kidole kimoja hakivunji chawa.
(ii) Jifya moja haliinjiki chungu.
(iii) Umoja ni nguvu utengano udhaifu.
3. Mtindo au fani
Mbali na maudhui, methali hutawaliwa na fani pia. Fani katika methali hudhihirika katika
muundo, tamathali za semi na taswira inayoibuliwa. Methali ambazo huundwa kwa kutumia
fani sawa huweza kuwekwa katika kundi moja. Methali zifuatazo zimeundwa kwa kutumia
kweli kinzani.
4. Jukumu
Methali huweza kuainishwa kulingana na majukumu yake. Je, methali inasifu, inakashifu,
inahimiza, inaonya ama inafariji? Methali zifuatazo hutumiwa kuonya:
(a) Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
(b) Asiyeangalia huishia ningalijua.
(c) Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
5. Maana
(a) Methali zenye maana sawa zinaweza kutiwa katika kundi moja, kwa mfano:
(i) Damu ni nzito kuliko maji.
Meno ya mbwa hayaumani.
(ii) Mtoto wa nyoka ni nyoka.
Mwana wa mhunzi asiposana, huvukuta. j
(b) Methali zenye maana zinazokinzana pia zinaweza kuainishwa pamoja, kwa mfano:
(i) Mvumilivu hula mbivu.
Ngoja ngoja huumiza matumbo.
(ii) Mtu pweke ni uvundo.
Manahodha wengi chombo huenda mrama.
1. Huku ukitoa mifano kutoka jamii yako, eleza vigezo vitano vya kuainisha
methali.
2. Weka methali zifuatazo katika makundi kulingana na vigezo vya maana.
(i) Ucha Mungu si kilemba cheupe.
(ii) Bila chambo hunasi samaki.
(iii) Mbaazi ukikosa maua husingizia jua.
(iv) Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi.
(v) Samaki mmoja akioza na mtungo pia.
(vi) Ukitaja nyoka shika kigongo.
(vii) Tumbili akiisha miti huja mwilini.
(viii) Paka hawekewi kitoweo kulinda.
(ik) Kitema kuni temato.
(2) Mchuma janga hula na wa kwao.
1. Sitiari
Sitiari ni mbinu ya kulinganisha kitu na kingine bila kutumia maneno ya kulinganisha kama
vile kama, mfano wa na mithili ya. Methali zinazoundwa kwa sitiari ni pamoja na:
(i) Mgeni ni kuku mweupe. Hapa mgeni anafananishwa moja kwa moja na kuku mweupe
kuonyesha mgeni hutambulika haraka akiwa kundini.
(ii) Ahadi ni deni. Ahadi inafananishwa na deni kuonyesha kuwa ni sharti mtu kutimiza
ahadi aliyoiweka.
2. Takriri
3. Tashbihi
|
au
(i) Kawaida ni kama sheria. Kawaida imefananishwa na sheria kuonyesha kuwa jambo la
kawaida ni kaida.
(ii) Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza. Lisilojulikana linalinganishwa na kiza.
4. Tanakali za sauti .
5. Taswira
Taswira ni picha zinazojengeka akilini mwa mtu baada ya kusoma, kutazama au kusikia
maelezo fulani. Taswira hizi hutokana na tajiriba pamoja na mazingira ya mtu. Ifuatayo
ni mifano ya methali zinazotumia taswira.
(i) Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba. Hapa, taswira au picha ya mti ulioanguka na
wana wa ndege kwenye viota inaonyesha jinsi kiongozi akifa au akipatwa na matatizo,
anaowaongoza pia huingia mashakani.
(ii) Mpanda farasi wawili hupasuka msamba. Taswira ya mtu apandaye farasi wawili na
kuathirika vibaya inajitokeza.
Kumbuka kuwa tamathali nyingine huweza kutumiwa kujenga taswira. Tashbihi na sitiari,
kwa mfano, zinaweza kuibua taswira ya jambo linalofananishwa.
6. Kweli kinzani
Katika kweli kinzani, maana ya maneno hukinzana kijuujuu (husikika kuwa haiwezekani)
lakini ikichunguzwa kwa undani kuna ukweli fulani uliofichika. Ifuatayo ni mifano ya
methali zinazotumia ukinzani:
(i) Wagombanao ndio wapatanao. Ukinzani unajitokeza kwamba kugombana na kupatana
ni vitendo tofauti na haviambatani. Watu hawawezi kugombana na wakati huo huo
wakawa wanapatana. Hata hivyo, ikichunguzwa kwa undani, ukweli wa kauli hiyo
unadhihirika. Watu waliowahi kukosana, baadaye huweza kuibuka kuwa marafiki
wakubwa.
(ii) Ukupigao ndio ukufunzao. Anayekupiga hakufundishi. Lakini, kwa ndani kuna
ukweli kwamba kila ambacho kinakuadhibu ndicho kinachokupa funzo la kudumu,
hutakirudia.
7. Chuku
Chuku ni mbinu ya kuongezea sifa za kitu zaidi ya kilivyo. Mifano ya methali zinazotumia
chuku:
(i) Usipoziba ufa utajenga ukuta. Hatari ya kupuuza “ufa' imetiliwa chumvi.
na kukejeliwa
(ii) Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi. Mzigo wa mwingine unapigwa chuku
kwa kulinganishwa na kanda la usufi ambalo ni jepesi sana.
8. Taashira au ishara
:
Katika taashira, kitu kimoja huashiria kingine. Mifano ya methali zenye taashira
kubwa baada
(i) Kimya kingi kina mshindo mkuu. Methali hii inaashiria kutokea kwa jambo
ya utulivu au kimya.
Mgeni
(ii) Kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Kamba mguuni pa kuku ni ishara ya ugeni.
hakosi kujulikana katika kundi la wenyeji.
11. Balagha
Balagha ni maswali yasiyohitaji majibu. Maswali haya humchochea mtu kufikiri.
(i) Pilipili usoila yakuwashiani?
(ii) Mavi usoyala wayawingiani kuku?
kuambiwa
Methali hizi zimeundwa kwa mbinu ya swali ambalo linamhitaji mwenye
kufikiria.
12. Tanakuzi
, sehemu moja
Hii ni mbinu inayotumia maneno au kauli zinazopingana. Katika tanakuzi
ya methali huwa na maana inayopingwa na sehemu ya pili.
ad
(i) Tamaa mbele mauti nyuma.
(ii) Mpanda ngazi hushuka.
Maneno yaliyokolezwa wino yana maana zinazopingana.
13. Kinaya
Kinaya ni kinyume cha matarajio au cha kauli inayosemwa au cha hali ilivyo. Kwa mfano:
(i) Kigumba kwa nguruwe kwa mwanadamu ki uchungu. Baadhi ya watu huwadhulumu
wengine na wao wanapodhulumiwa hulalamika.
(ii) Kikiharibika cha fundi kikiongoka cha Bwana Swedi. Jambo likiharibika mwenye
kulishughulikia ndiye hulaumiwa lakini likitia fora pongezi hazimwendei ila
humwendea mkubwa wake.
Muundo wa methali
Methali kwa kawaida huwa na muundo wenye sehemu mbili. Sehemu ya kwanza hudokeza
wazo, nayo ya pili hulikamilisha. Mifano:
(i) Baada ya kisa/mkasa.
(ii) Debe shinda/haliachi kutika.
(iii) Dawa ya moto/ni moto.
Uchambuzi wa methali
Maswali yafuatayo yatakusaidia katika kuchambua au kuhakiki methali:
(a) Methali imerejelea vifaa gani au inahusu nini? Kwa mfano, inarejelea wanyama,
binadamu ama vifaa vya nyumbani? Methali Hindi ndiko kwenye nguo na wendao uchi
wapo inarejelea vifaa vifuatavyo:
(i) Nchi - Hindi |
(ii) Rasilimali — Nguo
(iii) Watu — Waendao uchi/wahitaji/maskini.
(b) Methali imebuniwa kwa kutumia tamathali gani au mbinu gani za kifasihi? Kwa mfano:
(i) Haba na haba hujaza kibaba.
(ii) Haraka haraka haina baraka.
Methali hizi zimeundwa kwa mbinu ya urudiaji au takriri. |
Methali (i) imerudia neno haba na sauti ba ilhali (ii) imerudia neno haraka na sauti |
ka. |
pole ndiye mla nyama inaibua taswira
(c) Methali inaibua taswira gani? Methali Simba mwenda ni sharti uwe na subira.
kufanikiwa
ya utulivu, makini na subira; kwamba ukitaka
Methali Mtu pweke ni uvundo inaonyesha
(d) Methali inakupa wazo gani kuhusu jamii?
kuwa jamii husika inachukia utengano.
inayopingana na hii? Methali
(e) Je, kuna methali nyingine inayokaribiana kimaana au
zina maana sawa; nazo: Bidii
Wino wa Mungu, haufutiki na Bidii ya mja haiondoi kudura
ainame zinapingana kimaana.
ya mja haiondoi kudura na Mtaka cha mvunguni sharti
dha gani? Kwa mfano:
(£) Je, methali imejikita katika mazingira ama mukta
Mjini)
(i) Jogoo wa shamba hawiki mjini. (Mashambani/
(ii) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. (Pwani)
(iii) Ucha Mungu si kilemba cheupe. (Dini)
gani? Inanuia kuonya, kushawishi, kufahamisha
(8) Je, dhamira ya methali yenyewe ni inaelimisha; Uzuri wa
ea bila habari
au kukashifu? Kwa mfano Mali bila daftari hupot
refu lisilokuwa na ncha inaliwaza.
mkakasi ndani kipande cha mti ina kejeli ilhali Hakuna
Vitendawili
Kitendawili ni kauli yenye fumbo ambalo hutolewa kwa hadhira hai ili ilifumbue. Jibu la
kitendawili ndilo fumbo lenyewe.
Sifa za vitendawili
(a) Kwa kawaida, vitendawili ni semi fupifupi zinazotumia lugha ya mkato. Kwa mfano: |
'Pa' funua 'pa' funika. (Jibu: Nyayo wakati wa kutembea.) |
|
|
(b) Vitendawili hutolewa kwa hadhira ili vifumbuliwe. Hivyo, hadhira yake ni hai na tendi.
|
(c) Hutumia lugha ya picha au taswira na vina ukwasi wa tamathali za semi. |
Jj!
(d) Vitendawili huhitaji watu au makundi mawili ili kukamilisha uwasilishaji wavyo. Mtu |
wa kwanza hutega, na mwenzake hutegua.
(e) Vitendawili huwa na muundo au fomyula maalumu ya uwasilishaji. Kwa mfano:
Mtegaji: Kitendawili! |
Mteguaji: Tega!
Mtegaji: — Nyumba yangu haina mlango.
Mteguaji: Yai.
(g) Kitendawili ni fumbo au swali lililofichika ambalo huhitaji jibu. Kwa mfano, Mzungu
katupwa jalalani. (Jibu: Machicha ya nazi.) Machicha ya nazi ndilo fumbo lililofumbwa.
(h) Fumbo au jibu la kitendawili hufahamika tu na jamii ambamo kitendawili hicho
kimezaliwa. Kitendawili kinaweza kuwa na majibu mawili kutegemea mazingira ya
jamii. Kwa mfano, vitendawili vifuatavyo huweza kuwa na jibu zaidi ya moja:
(i) Wanangu wawili hushabihiana. Majibu: Tui na maziwa; Unga na majivu.
(ii) Mwarabu kasimama kwa mguu mmoja. Majibu: Uyoga; Mwavuli.
(i) Vitendawili ni sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea uwezo wa mtu kutambua j
na kuhusisha au kulinganisha vitu katika mazingira yake. Kwa mfano, ili kufumbua
fumbo la kitendawili Mbili mbili hadi pwani, lazima mtu awaze kuhusisha vitu viwili |
ambavyo daima hufanya jambo pamoja. (Jibu ni Macho.) Macho hutazama pamoja,
hulala pamoja, hulia pamoja.
|
() Vitendawili huingiliana na tanzu na vipera vingine vya fasihi simulizi. Kwa mfano, |
ngano. za mtanziko hutumia vitendawili, hasa katika fomyula ya ufunguzi wa ngano. |
|
|
ya vikao
Aidha, vitendawili hutangulia vikao vya kusimulia hadithi au hutegwa baada
hivyo.
(k) Vitendawili hubadilika kutegemea wakati au kipindi cha kihistoria na maendeleo
ya jamii. Kitendawili kimoja kinaweza kuundwa au kutolewa kwa maneno tofauti
kulingana na kipindi cha wakati kinapotumiwa. Kwa mfano:
(i) Mwarabu wangu nimemtupa biwini. (Jibu: Machicha ya nazi).
.
(ii) Mzungu katupwa jalalani. (Jibu: Machicha ya nazi).
o vina
Maneno tofauti (Mwarabu na Mzungu) katika vitendawili hivi viwili ambavy
jibu moja yanaonyesha viliathiriwa na nyakati tofauti za kihistoria.
na methali
(1) Vitendawili ni sanaa inayotendwa kwa hivyo hujisimamia yenyewe tofauti
kutolewa.
ambazo kwa kawaida ni sanaa tegemezi. Hutengewa vikao maalumu na
zote za maisha ya
(m) Kimaudhui, vitendawili hushughulikia masuala katika nyanja
ali
binadamu na mazingira yake. Maudhui haya hutofautiana katika jamii mbalimb
ingawa baadhi yao kama vile maudhui ya njaa, imani na usafiri huingiliana. Kwa mfano:
Kamba yangu ndefu lakini haiwezi kufunga kuni. (Jibu: Njia.)
Hapa kamba na kuni ni vifaa vya kawaida katika jamii nyingi za Kiafrika.
(n) Vitendawili vinaweza kuwa sahili (rahisi) na vingine changamano.
Mungu.)
Mfano wa kitendawili sahili ni: Anatuona lakini hatumuoni. (Jibu:
ngozi na
Mfano wa kitendawili changamano: Tunda lake la ajabu; juu nyama, katikati
ndani mchanga. (Jibu: Firigisi.)
nyingine watoto na
Vitendawili ni semi maarufu sana miongoni mwa watoto. Katika jamii
wazima walishindana
watu wazima hushiriki. Miongoni mwa Wakamba, kwa mfano, watu
katika uteguaji wa vitendawili hata kuliko watoto.
Dhima ya vitendawili
mazingira
(a) Vitendawili huelimisha. Vitendawili hujumuisha masuala mengi katika
kuhusu
ya jamii. Hali hii inavifanya kuwa na uwezo mkubwa wa kuelimisha watu
kutoa mji.
mazingira yao. Aidha, mtu akikosa jibu la kitendawili haadhibiwi zaidi ya
kupata jibu
Akishataja tu hupewa jibu. Kwa hivyo, katika vitendawili, kukosa jibu au
ni njia za kuelimisha.
utegaji
(b) Huburudisha. Vitendawili huwapumzisha na kuwapumbaza wanaoshiriki katika
na uteguaji wavyo. Hili ni jukumu lililohifadhiwa vitendawili tangu jadi.
twa
(c) Hufundisha kaida na maadili ya jamii. Vitendawili huwa na utaratibu fulani unaofua
njia moja ya
na ambao washiriki wanapaswa kuuheshimu na kuuzingatia. Hii ni
miwe.
kuadilisha kuwa kila jambo maishani lina kaida zake ambazo ni lazima ziheshi
ishwa.
Kukosa jibu la kitendawili si sababu ya kulaaniwa lakini ni njia ya kufaham
(d) Hukuza ubunifu na stadi ya kufikiri haraka. Mteguaji wa kitendawili sharti afikiri na
kuoanisha yaliyotajwa na mazingira yake ili kupata jawabu. Vitendawili hukuza ari
ya kufikiria na kudadisi mazingira. |
(e) Vitendawili hudhihaki na kukejeli watu, hali au tabia hasi katika jamii. Hukashifu
matendo hasi na kusifu yale chanya. Kitendawili Rudi nyuma nikuonyeshe (ambacho jibu
lake ni Mavi ya mlevi) kinatumia stihizai kukashifu ulevi na kuhimiza usafi. Mzungu
katupwa jalalani. (Jibu: Machicha ya nazi.) Hapa mzungu anadhihakiwa, pengine kwa
sababu za kihistoria za kudharau Waafrika na hatimaye kufurushwa kwao.
(f) Husawiri mitazamo na itikadi ya jamii kuhusu hulka fulani. Kitendawili Nyumbani
kwetu kuna papai lililoiva sana lakini nashindwa kulichuma (Jibu: kaka au dada),
kinaonyesha kuwa ndoa kati ya dada na kaka haziruhusiwi; ni mwiko.
Hukuza uwezo wa kukumbuka. Vitendawili hutumiwa kama chemshabongo ya kujaribu
uwezo wa mtu kukumbuka na kuhusisha mambo.
Huleta umoja na ushirikiano katika jamii. Watu hujumuika pamoja wakati wa
kutegeana vitendawili. Kwa njia hiyo utangamano huimarika.
Hutambulisha jamii. Kila jamii huwa na vitendawili vyake vinavyoonyesha mazoea,
hali, tajriba na mazingira ya jamii husika.
Huchochea tabia ya udadisi. Uzoefu wa kutafuta kiini cha kitendawili hujenga tabia
ya kutaka kufichua jambo lililofichika. Kwa kujaribu kupata jibu la fumbo katika
kitendawili, wanajamii huimarisha ari yao ya kutafiti mambo ili kubaini kiini chake.
(k) Vitendawili hukuza na kusambaza ujuzi wa lugha. Vitendawili vina ukwasi mkubwa
wa lugha na tamathali za semi. Kwa hivyo, ni nyenzo kuu ya kukuza na kusambaza
masuala ya lugha katika jamii.
Muundo
Mtindo
Vitendawili hutolewa kwa mtindo wa majibizano. Majibizano haya huwa kati ya mtegaji
na mteguaji au mtegaji na hadhira ya wasikilizaji. Utaratibu ulioelezwa katika muundo
huzingatiwa na mtegaji na mteguaji/hadhira.
Lugha
1. Sitiari
Aghalabu, vitendawili hutumia sitiari. Kwa mfano:
(i) Fatuma mchafu — (Ufagio). Hapa Fatuma ni sitiari ya ufagio.
(ii) Saa yetu kadiri inavyotembea ndivyo inavyopunguza nguvu — (Moyo). Saa ni sitiari
ya moyo.
(iii) Jani la mgomba laniambia habari zinazotoka ulimwenguni kote — (Gazeti/jarida).
Jani la mgomba ni sitiari ya gazeti/jarida.
2. Tashihisi/Uhaishaji
Wakati mwingine, vitendawili hutumia mbinu inayoipa kitu kisicho hai sifa za kibinadamu.
Kwa mfano:
(i) Akizungumza kila mtu hubabaika — (Radi). Hapa, radi imepewa sifa ya kuzungumza
kama binadamu. Sauti kali ya radi huwaogofya binadamu.
(ii) Amenifunika kote kwa blanketi lake jeusi — (Giza). Giza limepewa sifa ya binadamu
ya kumfunika mwingine.
(iii) Daima nasababisha mafarakano — (Ukewenza). Hapa, ukewenza umerejelewa
kwa nafsi ya kwanza.
3. Taashira
(i) Faiza akiniona ajificha — (Mzee kobe). Kinachoashiriwa na kujificha kwa Faiza ni
Kobe.
(ii) Chonge la nyoka huuma hata walio mbali — (Ugonjwa). Chonge la nyoka linaashiria
ugonjwa.
4. Stihizai/dhihaka/kejeli
Vitendawili vinavyobuniwa kwa dhihaka hutumiwa kukashifu mienendo hasi katika jamii.
Pia hueleza sifa ya kitu kwa njia ya kebehi (dharau). Kwa mfano:
di
(i) Akivaa miwani hafanyi kazi vizuri — (Mlevi). Kitendawili hiki kinakashifu ulevi. |
(ii) Babangu amevaa koti la chuma - (Mzee kobe).
(iii) Upara wa Mwarabu unafuka moshi — (Chai ya maziwa). |
(iv) Uzi mwembamba umefunga dume kubwa — (usingizi).
5. Kweli kinzani
Vitendawili vya aina hii huundwa kwa hoja mbili ambazo zinapingana. Mifano:
(i) Ajenga ingawa hana mikono — (Ndege). Ndege hana mikono kama binadamu,
hata hivyo yeye hujenga kiota.
(ii) Ana meno lakini hayaumi — (Kichana). Meno ya kichana hutumiwa kuchana wala
si kuuma.
(iii) Hufa ikifufuka — (Bahari kupwa). Maji ya bahari kupwa (kutoka ufukweni) ni |
kurejea.
6. Tanakali za sauti |
Kuna vitendawili vinavyoundwa kwa tanakali za sauti. Kwa mfano:
(i) 'Chubwi' — (Jiwe likianguka ndani ya maji). |
(ii) 'Prrr mpaka Makka' — (Utelezi). |
iii) 'Pa' funua pa' funika — (Nyayo wakati wa kutembea).
7. Takriri
| Baadhi ya vitendawili huundwa kwa kurudia neno au sauti. Kwa mfano:
(i) Aliwa yuala, ala aliwa — (Papa).
(ii) Amezaliwa Ali, amekufa Ali, na amerudi Ali — (Nywele).
(iii) Mama kazaa mtoto, mtoto kazaa mtoto na mtoto kazaa mtoto — (Kuku na yai).
8. Taswira
Baadhi ya vitendawili vimeundwa kwa jinsi ya kuibua taswira au picha mbalimbali. Kwa |
mfano: j |
(i) Nimemwona Bi Kizee akijitwika machicha — (Mvi). |
(ii) Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri — (Mbegu).
Mtu anaposikiliza vitendawili kama hivi, anajenga picha akilini mwake. Katika picha hiyo |
ndimo mna jawabu la kitendawili chenyewe. |
9. Utata
Baadhi ya vitendawili huweza kufasiriwa kwa njia zaidi ya moja. Tunasema kitendawili
cha aina hii kina utata. Utata katika vitendawili husababishwa na hali kwamba jibu |
la kitendawili hutokana na mazingira. Watu tofauti huweza kuwa na majibu tofauti
kwa kitendawili hicho hicho kutegemea hali ambayo inawazunguka. Kwa mfano: |
(i) Inachurura inaganda — (Asali au gundi).
(i) Kimuundo, vitendawili huwa (i) Methali kwa kawaida haina fomyula
na fomyula mahususi ya mahususi ya uwasilishaji.
uwasilishaji.
(ii) Huwa na fumbo ambalo lazima (ii) Fumbo halifumbuliwi papo hapo.
lifumbuliwe na hadhira papo Huwasilishwa kwa mwenye kutumia
hapo. methali.
(iii) Vitendawili huwa maarufu zaidi (iii) Methali hutumiwa zaidi kama semi za
miongoni mwa watoto/vijana. kuonyesha hekima hasa miongoni mwa
wazee na watu wazima.
(v) Vitendawili kwa kawaida huwa (v) Si lazima methali zitolewe hadhira
na hadhira tendi inayotoa maana tendi. Huweza kutolewa kama funzo au
yake. changamoto kwa hadhira inayosikiliza au
kusoma.
(vi) Huwasilishwa kwa majibizano kati (vi) Huwasilishwa kwa kauli moja tu na
ya mtegaji na mteguaji. msemaji.
“Vitendawili ni aina ya sanaa. Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mwafaka.
Andika tamathali za semi zilizojenga vitendawili vifuatavyo:
(a) Sanduku la babu latufurahisha. (Gitaa)
(b) Wanisikia tu wala hawanijui. (Mtangazaji wa redio)
(c) Mshale wangu umekita katika nyama nawatafuta wazee waje kunitolea.
(Mvulana akishampata mchumba)
(d) Mgongo wa bibi mchafu. (Chungu)
(e) Nina mawe yangu madogo lakini yanamaliza mlima. (Macho)
Misimu
Sifa za misimu
(a) Misimu ni semi au msamiati ambao huzuka na kutoweka baada ya muda fulani.
na
(b) Hutumiwa na wanajamii katika mawasiliano yao katika kipindi fulani cha wakati
mahali fulani.
misimu
(c) Hutumiwa na kundi fulani la watu kufanikisha mawasiliano. Kwa mfano, kuna
ya vijana, ya wafanyakazi katika vyombo vya usafiri na hata ya watoto.
(d) Ingawa misimu huzuka na kutoweka baada ya muda, baadhi ya misimu hudumu na
kukubalika kama semi au msamiati sanifu wa lugha husika. Kwa mfano, neno chai (kwa
maana ya hongo) lilianza kama msimu, kisha likashika na kukubalika kama msemo
sanifu.
mahali
(e) Misimu hupata maana yake kutoka kwa watumiaji pamoja na muktadha wa
na wakati. Kwa mfano, neno sare ni msimu uliopata maana katika sekta ya usafiri wa
matatu likimaanisha kubebwa bila malipo. Aidha, pauni ya Uingereza ilipokuwa na
thamani ya shilingi ishirini za Kenya, noti ya shilingi ishirini ilirejelewa kama paundi.
Baada ya mabadiliko ya wakati na kiuchumi, ilikuja kurejelewa kama mbao. Huenda
neno hili litabadilika tena au lisalie hivyo. ;
(f) Misimu si semi sanifu, hivyo haipaswi kutumiwa katika miktadha rasmi.
(8) Misimu huundwa kwa mbinu mbalimbali kama vile kutohoa maneno au kugeuza
mpangilio wake, kwa mfano risto (hadithi) kutoka neno 'story' la Kiingereza.
Dhima ya misimu
Misimu hutumiwa kutekeleza majukumu mbalimbali katika jamii, kama ifuatavyo:
(a) Ni kitambulisho cha kundi fulani la watu. Misimu ya mabaharia, kwa mfano,
huwatambulisha na kuwatofautisha mabaharia na vikundi vingine vya wafanyakazi
katika vyombo vya baharini kama vile makuli.
(b) Misimu huhifadhi siri za wanaoitumia. Watu hutumia misimu ili kulinda siri zao
zisijulikane.
(c) Hutumiwa kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji. Kwa mfano, waasisi
wa misimu chungwa na ndizi nchini Kenya wakati wa kura ya maoni kuhusu katiba
mpya mwaka 2005 waliitumia misimu hii kunadia wito wao wa kupinga au kuunga
mkono katiba hiyo.
(d) Hukuza ushirikiano, uzalendo na uaminifu miongoni mwa wanaoitumia. Lugha ni
nyenzo kuu ya kuwaunganisha watu, hivyo wanajamii wanapotumia misimu sawa,
hujiona kuwa na mionjo, hali na maazimio sawa.
(e) Huongeza haiba au ladha katika lugha, hivyo kuondoa ukinaifu unaotokana na kutumia
msamiati uliozoeleka miaka nenda miaka rudi.
(£) Hutumiwa kupunguza makali katika lugha au kutasfidi lugha. Badala ya kutumia neno
la aibu au msamiati unaoibua masikitiko, watu hubuni misimu kuelezea jambo kwa
njia nyepesi isiyoumiza.
(8) Hukuza lugha zaidi. Wakati mwingine misimu hukubalika kama msamiati rasmi,
misemo, methali au nahau katika lugha fulani. Kwa mfano, maneno matatu na daladala
ni misimu iliyoibuka kurejelea magari ya uchukuzi wa umma nchini Kenya na Tanzania
mtawalia. Kwa sasa, maneno haya yanakubalika kama msamiati rasmi wa lugha ya
Kiswahili.
Huhifadhi utamaduni na historia ya jamii. Kwa vile misimu tofauti hutumiwa katika
vipindi mbalimbali vya wakati, kuwapo kwake huakisi maendeleo, ukuaji, historia na
mabadiliko katika jamii husika.
Ni kielelezo cha mpangilio (mfumo) wa jamii fulani, kijamii na kiuchumi. Kwa vile
misimu hutambulisha matabaka katika jamii, tunaweza kutambua ni matabaka gani
yanayounda jamii hiyo.
Hutumiwa kuondoa urasmi katika mazungumzo. Vijana, kwa mfano, wanapotumia
misimu badala ya semi sanifu, huondoa urasmi na kudumisha uhusiano wa kirafiki.
YA
(k) Hukuza uwezo wa kufikiri na kutathmini au kudadisi. Ili kuelewa misimu fulani, ni
lazima ufikirie na kutathmini chanzo cha msamiati huo. Mathalani Mukoloni (mama)
ni mfano wa msimu wa nyumbani. Ili kuuelewa, inabidi ufikirie zaidi na kupima ni
nani aliye na tabia za kudhibiti watoto zaidi kati ya mama na baba.
Uainishaji wa misimu
Misimu hutofautiana kutegemea:
(a) Wahusika. Kuna misimu ya vijana, mabaharia au wanafunzi. Neno beste hutumiwa
na vijana kumaanisha rafiki.
(b) Matilaba. Kuna misimu ya kuendeshea biashara. Neno kung'ara linamaanisha kuvaa
nguo inayopendeza na sare linamaanisha kubebwa kwenye matatu bila kulipa nauli.
(c) Vifaa. Kuna misimu ya vyakula, pesa na vyombo vingine. Maneno nyake ni nyama na
ashu (kwa kuboronga neno ashara) ni shilingi kumi.
(d) Mahali. Kila eneo huibua misimu yake. Gari la uchukuzi kwa umma nchini Kenya ni
matatu na Tanzania ni daladala.
(e) Wakati au kipindi. Misimu hubadilika kulingana na wakati au kipindi. Kwa mfano,
wakati wa uchaguzi wa 2002 nchini Kenya, kulizuka neno unbwogable lililomaanisha
wasioshindwa/wasiotishika na likatoweka katika muktadha wa baada ya hapo.
Lakabu
Lakabu ni jina la msimbo au jina la kupanga ambalo mtu hujibandika ama hubandikwa
kutokana na sifa zake za kimaumbile, kitabaka, kitabia au kimatendo. Lakabu aghalabu
huwa neno moja au fungu la maneno lililo na maana fiche au ya kisitiari. Sifa zinazodokezwa
katika lakabu zinaweza kuwa za kusifu, kudhalilisha au kukosoa.
Sifa za lakabu
(a) Lakabu si jina halisi la mtu. Ni jina tu la kupangwa.
(b) Lakabu aghalabu huwa neno au fungu la maneno lililo na maana iliyofumbwa.
(c) Lakabu huoana na sifa za mhusika. Inaweza kusifu, kukej eli au kufanyia tashtiti tabia
hasi ya mhusika. Lakabu Baba wa Taifa, moja kwa moja inaashiria sifa nzuri za mhusika
na kumsifu. Kwa upande mwingine, lakabu kama Kagumu inaashiria tabia ya uchoyo.
(d) Lakabu hupatikana katika tanzu na vipera vingine vya fasihi simulizi kama vile sifo,
malumbano ya utani na majigambo (vivugo), ambapo wahusika hujipa majina ya
kupanga ya kujitapa.
(e) Lakabu huundwa kwa lugha ya picha au taswira na sitiari, kwa mfano, lakabu Nyayo
ya Rais mstaafu Moi inatumia sitiari. Inamfananisha na nyayo za mtu, hivyo kutupa
taswira ya mtu anayefuata falsafa ya mwingine.
(£) Ingawa lakabu si jina halisi la mtu, huweza kudumu na kufanya jina halisi la mtu
kusahaulika.
Dhima ya lakabu
(a) Hutumiwa kusifia matendo chanya ya mhusika.
(b) Hukashifu au hukejeli matendo mabaya ya mhusika.
(c) Ni kitambulisho cha mhusika. Husawiri tabia au hali ya mtu fulani kwa maneno
machache.
(d) Hutumiwa kama ishara ya heshima. Katika jamii ambamo kumtaja mkazamwana kwa
jina lake halisi ni mwiko, baba mkwe huibua lakabu ya kumrejelea mkazamwanawe.
(e) Hutumiwa na baadhi ya wahusika kuficha utambulisho wao. Baadhi ya waandishi
hujibandika majina ya uandishi ili kuficha majina yao halisi.
(£) Hutumiwa na wahusika kujigamba na kujinaki. Katika majigambo, anayejigamba
hujipa lakabu ili kujinaki na kuonyesha ubingwa wake.
(g) Hutumiwa kuhifadhi siri. Wakati mwingine watu humpa mtu fulani lakabu ili
wanapomrejelea isijulikane ni nani.
(h) Hukuza uhusiano bora hasa miongoni mwa watani. Katika kufanyiana utani watu
huweza kubandikana majina.
(i) Hutumiwa kuondoa urasmi katika mahusiano ya kijamii.
Vitanza ndimi
Vitanza ndimi ni kauli au sentensi zenye maneno ambayo yana mfuatano wa sauti
zinazotatanisha kimatamshi. Vitanza ndimi huundwa kwa maneno yenye sauti
zinazokaribiana sana kimatamshi. Kimsingi, katika jamii nyingi za Kiafrika, watu hufurahia
kucheza na maneno kama njia ya kujiburudisha. Watoto, kwa mfano, wana mazoea ya
kucheza na maneno na sauti katika michezo na nyimbo zao.
(a) Vitanza ndimi hukuza matamshi bora. Mtu anapotamka kwa haraka na kwa usahihi,
hutia makali stadi zake za kimatamshi. Kupitia hali hii, uzoefu wa kutamka vyema
hujengwa.
(b) Hukuza uwezo wa kufikiri kwa haraka. Baadhi ya vitanza ndimi hutatanisha kwa
sababu ya ukuruba wa maana. Mtu huhitajika kuwaza haraka ili kuteua neno sahihi
la kutamka katika muktadha wa maneno fulani.
(d) Hukuza ubunifu. Anayebuni vitanza ndimi anahitajika kuwa na ujuzi mpana wa lugha
na ubunifu ili kuteua maneno yanayokaribiana kimatamshi na kimaana.
(e) Hukuza lugha. Vitanza ndimi vilivyobuniwa katika vipindi mbalimbali huhifadhiwa
na kupitishwa kwa vizazi vijavyo kama mifano katika kipera cha vitanza ndimi.
Mafumbo na chemshabongo
Mafumbo ni kauli zenye maana iliyojificha. Mafumbo hutumia lugha fiche au ya kiistiari
pamoja na tamathali nyingine za usemi. Humtaka anayeambiwa kudadisi mazingira yake
na kufikiria ili kupata maana. Mafumbo huchemsha bongo za wale wanaoshiriki katika
kuyafumbua. Ingawa vitendawili ni aina ya fumbo, tunadai kwamba mafumbo kwa kawaida
ni semi ndefu kuliko vitendawili. Mafumbo hutumika sana sana katika mazungumzo na
huundwa kutegemea mazingira. Kwa mfano, watu wanapozungumza wanaweza kumtaja
mtu fulani kwa ubaya wake kisha mtu mwenyewe akija, mmoja wao akawatahadharisha
wengine kwa kusema 'Chungeni msikanyage nyoka'. Watachunguza mazingira yao au
wafikirie ili kubaini maana ya fumbo la nyoka.
Kuna mafumbo ambayo huitwa chemshabongo. Chemshabongo ni maswali ambayo
humtaka mtu kutumia akili na ujuzi kuyajibu. Maswali mengi ya aina hii ni ya kimapokeo,
mengine hubuniwa na msemaji ili kukidhi mahitaji ya hadhira mahususi. Baadhi ya
chemshabongo, kwa hakika, ni hesabu tu. Nyingine hutolewa kwa njia ya mraba ambao
unahitaji kujazwa kwa maneno mwafaka. Tazama mfano ufuatao:
|
Nina kilo moja ya mchanga na kilo moja ya pamba. Kipi kizito zaidi, mchanga au
pamba?
Jibu: Vyote vina uzito sawa kwa vile uzito wavyo ni sawa (kilo moja).
Sifa za mafumbo
Mafumbo huwa na sifa zifuatazo:
(a) Ni semi ambazo hufumba jambo.
(b) Huhitaji mtu kuwaza ili aweze kubaini fumbo lenyewe.
(c) Shughuli, maumbile au vitu vilivyo katika mazingira ya jamii kama vile mifugo, njia
za usafiri na nyenzo za biashara vinaweza kufumbiwa.
(d) Baadhi ya mafumbo hufananisha kitu kilichotajwa katika fumbo na mazingira halisi.
(e) Baadhi ya mafumbo huwa marefu na mengine huwa mafupi. Tazama mfano ufuatao:
Jibu:
Jibu:
(i) Utavusha kuku kwanza.
(ii) Rudi, uchukue mtama uuvushe.
(iii) Chukua kuku, urudi naye ng'ambo ya kwanza na kumwacha
hapo.
(iv) Mvushe nguchiro.
(v) Mrudie kuku umvushe.
Fumbo hili, pamoja na kumhitaji mtu kutumia uhalisi wa mambo, anahitajika kutumia
mantiki ili kulifumbua. Mfumbuaji anahitaji kujua:
(i) Nguchiro hula kuku - hawezi kuwaacha pamoja.
(ii) Kuku hula mtama - hawezi kuacha kuku na mtama pamoja.
Dhima ya mafumbo
(a) Hukuza uwezo na wepesi wa kufikiri. Ili kufumbua fumbo ni lazima mtu afikiri kwa
makini na wakati mwingine kwa upesi.
(b) Hustawisha ubunifu. Fumbo hufumbuliwa kwa kuoanisha yaliyomo katika fumbo, tajiriba
na mazingira. Hivyo, mtu hutumia kiwango fulani cha ubunifu ili kupata maana. Aidha,
shughuli ya kufumba mafumbo huwahitaji watu kuwa wabunifu.
(c) Hukuza maarifa ya kukabiliana na changamoto na kutumia mantiki kusuluhisha mambo.
Tazama mfano:
za Li zikate mah
Sifa za nahau
(a) Nahau huundwa kwa lugha ya mkato iliyo na ujumbe mzito wa mafumbo. Kwa mfano
Kidudu mtu ina maana ya mfitini.
(b) Nahau mbili au zaidi zinaweza kuwa na maana moja. Ifuatayo ni mifano:
Kupata jiko
Kuoa
Kuasi ukapera
Jamvi la wageni
Bao la mkahawani Sa
Kunja jamvi
j Maliza shughuli
Funga virago
(c) Nahau moja inaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa mfano:
Kushika mguu —
kuomba radhi
—
kutoa shukrani
—
kupiga mbio
Kufunga virago —
kumaliza shughuli
—
kuondoka
(d) Maneno katika nahau hupoteza sifa zake za kawaida na kuchukua maana nyingine
iliyo tofauti kabisa. Kula chumvi, kwa mfano, ni kuzeeka wala maana haihusiani na
maana ya maneno 'kula' au 'chumvi'.
(e) Nahau huundwa kwa maneno mawili au zaidi. Soma mifano ifuatayo:
Shingo upande — bila kupenda
Kufua dafu —- kufaulu
Bega kwa bega — pamoja
Mtoto wa kikopo — mhuni
Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa — kudanganya, kumpa mtu sifa asizostahili.
(f) Nahau huweza kuundwa kwa mitindo mbalimbali au kwa maneno ya kategoria
mbalimbali kama vile:
(i) Kitenzi na nomino — piga chuku
—- andika meza
—- tafuna maneno
(ii) Kitenzi na kitenzi —- kufa kupona
—- kufumba na kufumbua
— pata shika
—- ruka akitoja
(iii) Kitenzi na kielezi — jikaza kisabuni
— tokea pwani
—- kufa kikondoo
(iv) Nomino na nomino — askari kanzu
— donda ndugu
—- domo kaya
(v) Nomino na kitenzi — mguu haumshiki
— damu kumkauka
— akili kumruka
(vi) Nomino navivumshi — —nyota njema
— bahari kubwa
— ndege mbaya
Dhima ya nahau
(a) Nahau hukuza lugha. Nahau huyapa maneno maana tofauti na maana ya kawaida.
Kwa njia hii, hupanua msamiati wa lugha.
(b) Nahau huipa lugha ladha. Badala ya kutumia maneno yaliyozoeleka kurejelea mambo
ya kawaida, nahau hutumika kukoleza ladha ya lugha. Badala ya mtu kusema fulani
amezeeka sana, anasema fulani amekula chumvi ya kutosha.
(c) Nahau pia hutumiwa kupunguza ukali wa jambo linalorejelewa. Badala ya kusema
fulani ana tabia ya uasherati tunasema ana jicho la nje.
(d) Nahau huweza kutumika pia kuhifadhi siri ili wanaotengwa wasielewe. Si watu wote
wanaoelewa maana ya nahau zote. Unaposema fulani amekuwa kidudu mtu huenda
mwingine asielewe kuwa unamaanisha amekuwa mfitini.
F- |
Misemo
Misemo ni semi ambazo zinabeba ukweli wa kijumla. Hutumiwa kuelezea mambo
mbalimbali yanayokubali ukweli huo. Misemo hutumiwa kutoa ujumbe kwa muhtasari.
Baadhi ya misemo hutumiwa kama methali. Kwa mfano, tunasema, “Umoja ni nguvu,
utengano ni udhaifu.”
Utangulizi
Ushairi simulizi ni utanzu unaojumuisha tungo zote zenye mapigo ya kimuziki. Mawazo,
hisia na hoja katika utanzu huu huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kutumia lugha ya
mkato yenye mpangilio maalumu wa maneno katika mishororo. Ushairi simulizi huimbwa,
hughaniwa au kukaririwa. Ni muhimu kutaja hapa kuwa ushairi simulizi hutofautiana
na mashairi ambayo yameandikwa kwa lengo la kuwasilishwa mbele ya hadhira katika
mashindano ya tamasha za muziki au yanayowasilishwa katika hafla maalumu.
1. Maudhui
Kwa kuzingatia maudhui, tunaweza kupata mashairi yenye maudhui ya:
(a) mapenzi. Hupitisha jumbe za mapenzi.
(b) kutuliza. Kuna nyimbo za bembea au bembelezi ambazo hutuliza watoto.
(c) kuomboleza. Mbolezi huimbwa wakati wa msiba.
(d) kusifu. Sifo huimbwa kusifu mashujaa au waliofaidi umma na kustahiki kutambuliwa.
(e) siasa. Nyimbo za siasa huwasilisha jumbe za kisiasa.
Mtindo wa uwasilishaji
Mashairi simulizi huchukua mitindo ya uwasilishaji ifuatayo:
(a) maghani. (Hutolewa kwa kauli bila kuimbwa.)
(b) nyimbo. (Huwasilishwa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka.)
shairi. (Utungo unaokaririwa.)
tendi au rara. (Husimuliwa kwa mapigo ya kishairi.)
ngonjera. (Huwasilishwa kwa kujibizana.)
Mwasilishaji
Majigambo. (Huwasilishwa na anayejigamba.)
Kwaya. (Uimbaji wa watu wengi pamoja.)
(8) Husawiri mfumo wa jamii fulani kisiasa, kiuchumi na kijamii. Baadhi ya nyimbo
huonyesha shughuli za kiuchumi za jamii kama vile ufugaji. Hodiya (nyimbo za kazi)
huonyesha shughuli mbalimbali kama vile uwindaji, kilimo, uvuvi. Majigambo pia
husawiri mifumo ya jamii kisiasa na kijamii.
(h) Huonyesha falsafa na imani za jamii husika kuhusu masuala fulani. Mbolezi huonyesha
imani za jamii kuhusiana na kifo. Majigambo husawiri falsafa ya jamii kuhusu ushujaa.
(i) Ni nyenzo kuu ya kuhamasisha wanajamii. Nyimbo za kisiasa na kizalendo zimetumiwa
na tawala kama nyenzo ya kueneza propaganda za kisiasa.
G) Hukuza ubunifu. Anayekariri, kuimba au kughani mashairi huhitajika kubuni mbinu
zifaazo za uwasilishaji. Kwa kufanya hivi, uwezo wake wa kubuni hukuzwa.
(k) Hukuza usanii wa lugha. Wanaotunga na kuimba mashairi hujizoesha kutumia lugha
kwa ufundi mkubwa ili kutosheleza urari wa mizani na vina.
(1) Husaidia wanajamii kukabiliana na hali ngumu na kuwahimiza wasikate tamaa. Kwa
mfano, mbolezi hufariji na kusawiri kifo kama faradhi. Kwamba humfika mja yeyote,
hivyo hisia za mwemeo hupungua. Aidha, nyimbo huhimiza waliokwenda vitani au
wanaofanya kazi wasikate tamaa.
(m) Ushairi simulizi hustarehesha na kufurahisha wanajamii. Tungo za ushairi simulizi
huvutia hisia, huburudisha na kusisimua mwili na akili.
—..—
1. (a) Andika miktadha mitano katika jamii yako ambamo nyimbo huimbwa
au mashairi hukaririwa.
(b) Taja aina za mashairi au nyimbo ambazo huimbwa katika miktadha
uliyoitaja.
2. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Umeanguka mwamba
Jabali tuloegemea
Lilotupa kimbilio
Mahasidi kutishia
Mti mkuu umegwa
Wana wa ndege wawapi?
Bila shaka hangaiko
'Metukumba makinda
Angalikuwa pamwe nasi
Maulana Mungu wetu
Swali hilo tungemuuliza
Mbona kaacha mauko
Ngome yetu kuvamia?
Ela mwenyewe Mwenza
Ajua hatima yetu
Lilobaki kumwamini
Riziki kutuangushia
Nyimbo
Nyimbo ni tungo za kishairi zenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti, muwala na
mapigo ya kimuziki na huwasilishwa kwa kuimbwa. Nyimbo hutambuliwa kwa sifa tatu:
(i) huwepo kwa hadhira inayotumbuizwa
(ii) muziki unaoimbwa kwa sauti
(iii) matumizi ya ala.
Sifa za nyimbo
(a) Sifa bainifu ya nyimbo ni kwamba hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka
kwa sauti.
(b) Nyimbo hutumia lugha ya mkato yenye mpangilio maalumu wa silabi, mishororo na
beti zenye mapigo ya kimuziki.
(c) Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua taswira na hisia nzito kama za mapenzi,
huzuni na furaha.
(d) Nyimbo zinapoimbwa, mara nyingi huandamana na ala za muziki kama vile ngoma,
baragumu, msewe na zumari.
(e) Katika jamii za Kiafrika, nyimbo hufungamana na muktadha fulani. Kuna nyimbo
za kazi, harusi, jando na unyago, kuzaliwa kwa mtoto, kumpa mtoto jina, ibada na
matambiko.
(£) Baadhi ya vifungu katika nyimbo hurudiwarudiwa. Vifungu hivi huitwa vibwagizo,
viitikio au mikarara ya nyimbo.
(8) Nyimbo nyingi huandamana na uchezeshaji wa viungo kama vile mabega kupiga
makofi na mapigo ya miguu. j
(h) Kimsingi, nyimbo ziliimbwa na makundi ya watu kwa hadhira hai. Hata hivyo, kuna
nyimbo zinazoimbwa na mtu mmoja kwa hadhira yake au hata bila hadhira.
Umuhimu wa nyimbo
(a) Nyimbo hutambulisha jamii kwa kusawiri shughuli na maisha ya jamii iliyozibuni.
Mathalan, nyimbo katika jamii ya wakulima zitasheheni msamiati unaohusu shughuli
za kilimo kama vile kuvuna, kupanda na kupalilia.
(b) Nyimbo humwezesha binadamu kutakasa hisia zake. Kupitia kwa nyimbo, binadamu
hutoa hisia za moyoni kama vile kujutia kosa ulilofanya, mapenzi ama huzuni.
Mbolezi humsaidia aliyeathiriwa kutoa hisia za huzuni. Nyimbo za mapenzi, kama
vile chombezi, humwezesha mpenzi kumfichulia mwenzake hisia zake za moyoni.
(c) Ni mbinu mojawapo ya kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Rekodi za
. matukio muhimu katika jamii huweza kuhifadhiwa kwa nyimbo na kupitishwa kwa
vizazi.
(e) Hupitisha amali na mambo ambayo jamii inayathamini. Amali hizo hurekodiwa katika
nyimbo mbalimbali kama vile za kazi na kurithishwa vizazi vya jamii hiyo. Mawaidha
na thamani za jamii hukaririwa katika nyimbo kama nyenzo za kuzirithisha.
(f) Nyimbo hutumiwa kuhamasisha watu na kuchochea hisia za kuchamgamkia jambo
fulani. Nyimbo za kisiasa, kwa mfano, huweza kuchochea hisia za kuungana pamoja
kutetea haki au kuunga mkono jambo fulani.
(8) Nyimbo huakisi ukwasi wa tamaduni za jamii. Umbuji (ufasaha wa kujieleza) na
ujumi (mvuto au uzuri wa kazi ya sanaa) wa jamii hujitokeza katika nyimbo. Uteuzi
wa maneno, ishara na ujumbe katika nyimbo huonyesha ukwasi wa jamii hiyo kifani.
(h) Hukuza ubunifu miongoni mwa wanajamii. Uimbaji ni kipawa na nyimbo hupalilia
kipawa hiki.
Soma ubeti ufuatao kisha ujibu maswali:
Siku hiyo ya nuru
Tulokata pingu
Kuyabwaga mazigo
Silisili tukakata
Beberu tukatimua
Istiimari tukaua
Uhuru tukarejesha
Hadhi yetu kufufua
Bendera mlingotini ikapepea,
juu ya kilele cha mlima
Ishara ya kujitawala.
1. Nyimbo hufungamana na muktadha. Andika muktadha ambapo wimbo huu
unaweza kuimbwa.
2. Nyimbo huakisi ukwasi wa tamaduni za jamii. Jadili kauli hii kwa kurejelea
ubeti huu wa wimbo.
Taja sifa nyingine tano za nyimbo zinazojitokeza katika wimbo huu.
Aina za nyimbo
Kila jamii ina nyimbo zake ambazo hutofautiana na nyimbo za jamii nyingine. Baadhi
ya nyimbo ambazo hupatikana katika jamii za Kiafrika ni pamoja na:
Bembea/Bembelezi/Pembejezi
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa ili kuwabembeleza watoto walale au watulie wanapolia.
Sifa za bembea
(a) Bembea huimbwa taratibu kwa sauti na mahadhi ya chini.
(b) Huimbwa na wazazi au walezi wa watoto kuwaliwaza na kuwabembeleza watoto walale
au wanyamaze wakati wanapolia.
(c) Huwa fupi.
(d) Bembea hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine kulingana na thamani za jamii
hiyo.
(e) Huimbwa kwa kurudiarudia maneno au kibwagizo. Wakati mwingine hata wimbo
mzima huimbwa kwa kurudiwarudiwa.
(£) Hutumia lugha shawishi na wakati mwingine hutolewa ahadi za kununuliwa watoto
zawadi.
Majukumu ya bembea
Majukumu yanayotekelezwa na nyimbo zabembea nipamojana:
(b) Hutumiwa kama sifo kumsifu mtoto ambaye ni mtulivu. Husifu pia somo ya mtoto
huyo au wazazi wake.
(c) Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika. Ikiwa baba ni msasi, mtoto atatajiwa
kuwa baba ni msasi jasiri au baba yuko karibu kutoka usasini.
(d) Husawiri mahusiano katika jamii. Kupitia kwa bembea, mlezi huweza kuibua migogoro
iliyomo kati yake na wazazi wake au wazazi wa watoto, hivyo kuonyesha uhusiano
kati ya waajiri na waajiriwa.
Wimbo huu unaonyesha thamani ya mvua kwa jamii hii. Kila mtu duniani
huichangamkia mvua kwa sababu ndiyo chanzo cha kila kitu kilichoumbwa na Mungu.
(8) Husawiri falsafa au mtazamo wa jamii kuhusu jinsia na matarajio ya jamii kwa jinsia
fulani. Katika bembea, mlezi anaweza kutaja kuwa machozi ni ya kike iwapo anatuliza
mtoto wa kiume. Majukumu yake (mtoto wa kiume) kwa jamii pia huweza kutajwa.
Mlezi huweza kumtajia mtoto wa kike kwamba msichana anatarajiwa kuwa mlezi
mwema wala si kilizi.
(h) Huwaonya watoto dhidi ya tabia hasi. Watoto huonywa dhidi ya kulia ovyo kwa sababu
kulia hukumbusha mtu mambo mabaya.
Mfano wa bembea
Sifa za mbolezi
(a) Mbolezi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine kutegemea imani ya jamii
kuhusu kifo pamoja na hadhi ya aliyekufa.
(b) Huimbwa kwa nia ya kufariji waliofiwa.
(c) Husifu aliyekufa. Kwa kawaida, mbolezi hutoa sifa chanya au nzuri za aliyekufa. Watu
mashuhuri katika jamii huweza kutungiwa mbolezi zao mahususi zinazowasifu na
kutaja michango yao kwa jamii.
(d) Hufungamana na muktadha maalumu. Mbolezi huimbwa tu wakati wa matanga au
wakati wa kuomboleza jambo fulani. j
(e) Huimbwa kwa toni ya huzuni na pengine uchungu hivyo kuibua hisia za ndani za
mwombolezaji.
(£) Huimbwa kwa mwendo wa utaratibu.
Majukumu ya mbolezi
(a) Mbolezi husawiri msimamo wa jamii kuhusu kifo. Wapo wanaoamini kuwa kifo
husababishwa na maovu au pepo fulani na ambao hukashifu kifo. Watu wengine
hutambua kifo kama mlango wa kuingia katika uzima wa milele (kidini).
(b) Nikumbukumbu na sifo kwa aliyekufa. Husawiri tabia za aliyekufa kwa nia ya kumsifu
na kumkumbuka.
(c) Hufariji waliofiwa na kuwasaidia kukabiliana na uchungu au uzito wa kumpoteza
mpendwa wao.
(d) Ni njia ya kutakasa moyo na hisia za aliyefiwa. Aliyefiwa huweza kutumia mbolezi
kutoa hisia zake za huzuni. Kwa njia hii, anaweza kupunguza uzito wa kumpoteza
mwenzake.
Mfano wa mbolezi
Wa
Majukumu ya nyiso
(a) Nyiso hutumiwa kuwaandaa kihisia wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe
cha ngariba.
(b) Huwajuza wanaotahiriwa kuhusu majukumu mapya na matarajio ya jamii yao kwao.
Huwafahamisha kuwa wamevuka hatua muhimu na kuwaandaa kiakili kwa majukumu
ya utu uzima.
(c) Huonyesha furaha ya vijana kujivunia hatua ya kutoka utotoni na kuingia utu uzima.
(d) Huhimiza ujasiri na kukebehi woga.
(e) Huhimiza uzalendo na kuonea fahari utamaduni wa jamii. Wanaoshiriki jandoni
hujitambulisha na jamii yao zaidi, na hivyo uzalendo huimarika.
(£) Nyiso hutoa nasaha kwa vijana. Huwafahamisha kuhusu matarajio ya uchungu,
majukumu yao ya kiutuuzima, huasa dhidi ya woga na kuwasia umuhimu wa kuhifadhi
siri watakazopewa.
Mfano wa nyiso
Ewe kilizi
Ulozowea kujificha
Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio
ya radi ilo juu mbinguni
Jua kesho ni siku ya siku
Siku ya kujua mbichi na mbivu
Kutofautisha jogoo na vipora,
ngariba taposhika, chake kijembe
Ndipo utakapojua bayani
Ukoo wetu si wa kunguru
Ikiwa hu tayari
Kisu kukidhihaki
Sithubutu kamwe, wanjani kuingia
sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!
Nyimbo za kisiasa
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa katika shughuli au miktadha ya kisiasa. Nyimbo za kisiasa
huwa na maudhui mapana kama vile mapambano, propaganda, kuzindua, kuhamasisha,
kukejeli, kuhimiza au kutia ari.
Beberu lipoona
Vita vimechacha
Tamaa iliwatoka
Wakasalimu amri
Uhuru wakatoa
Hawakutoa kwa hiari
Hilo usisahau
Wazalendo walipigana '
Kwajino na ukucha
Uhuru tukapata
Kombozi akashika sukani
Hadhi yetu tukarudishiwa.
Tumia wimbo uliosoma kujibu maswali yafuatayo.
1. (a) Thibitisha kuwa huu ni wimbo wa kisiasa.
(b) Andika majukumu matano ya nyimbo za aina hii.
(c) Bainisha matumizi ya mbinu zifuatazo katika wimbo huu.
(i) Majazi (ii) Urudiaji (iii) Nahau
Sifa za sifo
(a) Sifo husifu na kutukuza watu ambao wamefanya jambo fulani. Kwa mfano, husifu
maarusi, waliohitimu jandoni, viongozi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, walioshinda
mashindano ya michezo au wenye kumiliki vitu, vipawa na hali fulani.
(b) Sifo hutumia sitiari kwa ufanifu mkubwa. Huwafananisha wanaosifiwa na wanyama
ili kuonyesha sifa fulani bora. Kwa mfano, kiongozi anaweza kufananishwa na simba
kuonyesha ujasiri wake au kurejelewa kiistiari kama Mkuki uwakao au Ngao yetu.
(c) Sifo hutumika katika miktadha mbalimbali ya kijamii kama vile miviga.
(i) Huimbwa kwenye jando kuwasifu mashujaa na kuwapongeza kwa kuingia katika
utu uzima.
(ii) Huimbwa kwenye mazishi kama taabili/taabini kuwasifu na kuwakumbuka
waliokufa.
(iii) Huimbwa kwenye harusi kuwasifu maarusi.
(iv) Huimbwa katika sherehe za kutawazwa kwa viongozi au wafalme.
(v) Kuna sifo za kidini ambazo humsifu Mungu na mtume. Kwa mfano, Kasida ya
Hamziya inamsifu Mtume Mohammed.
(d) Sifo pia huweza kuimbwa na mtu au watu binafsi wakijisifu. Sifo ya aina hii huitwa
majigambo au vivugo.
(e) Sifo huakisi thamani ya jamii husika. Kila jamii ina thamani yake. Kuna jamii zinazothamini
ujasiri wa kivita, nyingine usuli mwema au nasaba tukufu, ufugaji wa mifugo wengi, kilimo
au harusi.
(£) Sifo hupigia chuku sifa za anayesifiwa.
Majukumu ya sifo
Sifo husifu matendo chanya ya viongozi au watu mashuhuri katika jamii.
Hutangaza mafanikio au mchango wa mtu au watu wanaosifiwa kwa jamii. Anayeimba
sifo hutaja mambo ambayo anayesifiwa alitenda au ametenda.
Hukuza uzalendo. Sifo huwahimiza vijana kuiga matendo mazuri ya wanaosifiwa. Kwa
njia hii, watu hujifunza kuionea fahari jamii na kuwa tayari kuitolea mchango wao.
Kuweka kumbukumbu au rekodi ya matukio ya kihistoria. Wimbo unaomsifu shujaa
wa vita, kwa mfano, huonyesha vita alivyopigana, alipigana na nani na lini.
Huonyesha msimamo na mitazamo ya jamii fulani kuhusu masuala mbalimbali. Wimbo
unaosifu uzalendo wa mtu fulani vilevile unaweza kuonyesha chuki kwa usaliti.
Hutambua mchango wa watu mbalimbali kwa jamii. Sifo hutaja majina ya wanaosifiwa
kwa nia ya kuwatambua na kutambulisha juhudi zao.
(g) Huburudisha. Sifo nyingi hutumbuiza, hutuliza na hupumbaza akili.
Mfano wa sifo
aa
Tulipotekwa na adui
Mifugo wote kutwaliwa
Tukabaki kuuma vyanda
Je, hakupambana na majagina
Mifugo wetu kurudisha
Utu wetu kukomboa
Haiba yetu kurejesha?
Zoezi Zi
Sifa za hodiya
(a) Huimbwa wakati watu wanapofanya kazi. Kila aina ya kazi huwa na aina yake ya
nyimbo. Kuna nyimbo za wawindaji, za wakulima (wawe), nyimbo zinazohusishwa
na shughuli za majini (kimai) na pia za vita.
(b) Huimbwa na kundi la wafanyakazi au mtu mmoja wakati anapofanya kazi yake binafsi.
Majukumu ya hodiya
(a) Huhimiza watu kutia bidii na kuendeleza kazi bila kufa moyo.
(b) Hukashifu uvivu na utegemezi. Baadhi ya nyimbo za kazi hukashifu wasiopenda kazi.
(c) Hurahisisha kazi kwa kupunguza fikira za uchovu. Watu wanapofanya kazi wakiimba,
kazi huonekana kuwa nyepesi na muda huonekana kupita kwa kasi.
(d) Husawiri imani, mitazamo na thamani za jamii husika kuhusu kazi. Jamii inathamini
kazi gani? Uzembe na bidii kazini huchukuliwaje? Kazi inapewa nafasi gani?
(e) Huonyesha changamoto au matatizo ambayo wafanyakazi hukabiliana nayo katika
kazi zao. Je, wanahofia nini kazini? Wana matumaini gani katika kazi zao?
(f) Hujenga ushirikiano. Watu wanapoimba wakifanya kazi pamoja hujenga ushirikiano.
Ushirikiano pia huhimizwa katika baadhi ya nyimbo za kazi.
Nyimbo za mapenzi
Hizi ni nyimbo ambazo huwa na maudhui au ujumbe wa kimapenzi.
Aa.
4
(d) Hukuza ubunifu. Nyimbo za mapenzi hubuniwa kwa umbuji na ujumi wa hali ya juu
ili kuibua hisia za mapenzi, huzuni au huruma.
(e) Ninyenzo ya kupitisha maarifa au elimu ya jamii. Nyimbo za harusi hutumiwa kutoa
mawaidha ya unyumba kwa maarusi wapya. Aidha, matarajio ya jamii na majukumu
yao wapya kama bibi nabwana hupitishwakwanyimbo.
Kipi kinokwinamisha,
kwa tewengu kukubwaga?
Ama ni majukumu kuhofia mwenzetu? aa |
Ni aidha za ulezi?
Ni hofu ya kutelekezwa?
Jikoni kuachwa jukumu la kawaida?
j |
Nikahi ni sitara
Usumbufu kuepuka vipanga na mwewe
Ndoa huneemesha na jina kukupa ukatukuka kimwana
Shujaa ukapata wa kukulinda
Miliki ni hakikisho kutoka kwa dume hata katika mauko,
Penzi halali kupata, na warithi kuambulia,
wa kiume kukufaa
Silie mwana silie,
watutia simanzi
Waitia ndoa doa, nuksani kukuandamia.
Zoezi
Zoezi /1|
Maghani
Maghani ni ushairi ambao hutolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. Tofauti kati ya maghani
na nyimbo ni kwamba maghani hayaimbwi. Hata hivyo, kimaudhui maghani ni sawa na
nyimbo. Hushughulikia masuala ya kijamii kama vile kazi, maombolezi au siasa, kama
ilivyo katika nyimbo.
Aina za maghani
Maghani ni ya aina mbili kuu:
Sifo
Haya ni mashairi ya sifa ambayo hughaniwa kumsifu mtu fulani kutokana na matendo
yake ya kishujaa.
D
Sifa za sifo
(a) Sifo huwasifu watu, wanyama, mimea na hata vitu visivyo hai.
(b) Sifo hutoa sifa chanya na hasi. Sifa hasi hutolewa kwa nia ya kukashifu vitendo vibaya.
(c) Huingiliana na kutegemeana na tanzu nyingine za fasihi simulizi. Sifo huweza
kutumiwa katika miviga kama vile mazishi kusifu aliyekufa kwa matendo yake ya
kipekee. Pia, huweza kutumiwa katika harusi na tohara kuwasifu wanaohusika katika
shughuli hizo.
Aina za sifo
Sifo zinaweza kuainishwa katika vitanzu mbalimbali kama vile majigambo au vivugo,
pembezi na tondozi.
Sifa za majigambo
Sifa bainifu za majigambo ni kwamba:
(a) Hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe.
(b) Hutungwa kwa usanii mkubwa. Anayejigamba hutumia mfanano, sitiari, vidokezi,
ishara na urudiaji.
(c) Anayejigamba hujitungia kivugo kufuatia tukio mahususi katika maisha yake. Anaweza
kuongea kuhusu siku za jandoni, ndoa au kuoa, kutoka vitani, kushinda mchezo, kesi
au jambo fulani gumu.
(d) Kwa kawaida, majigambo au vivugo hutungwa na kughanwa na wanaume.
(e) Huwa na matumizi ya chuku. Anayejinaki hujisifu kupita kiasi kwa kutaja mafanikio
au mchango wake. Anaweza pia kutoa ahadi ya kuleta mafanikio makubwa hata zaidi
ya yale ambayo tayari ameiletea jamii yake.
(£) Majigambo hutolewa kwa nafsi ya kwanza kwa sababu anayejigamba ni mshairi
mwenyewe.
(g) Anayejigamba huweza kubeba baadhi ya vifaa vyake vya kazi au vinavyoonyesha
jambo analojisifia. Aidha, anaweza kuvaa maleba yanayooana na kazi au jambo ambalo
anajisifia.
ai
(h) Kwa kawaida majigambo hutungwa papo hapo. Hata hivyo, mengine huandikwa ili
kughanwa baadaye katika hafla fulani kama vile harusi. Ni muhimu kutaja hapa kuwa
haya ni mabadiliko katika sanaa hii.
(i) Anayejisifu huweza kutaja usuli wake wa kinasaba. Katika baadhi ya jamii, anayej igamba
huhitajika kutaja na kuisifu nasaba au ukoo wake — upande wa baba na mama kwa
majina yake halisi.
G) Wanaojigamba mara nyingi huwa walumbi au washairi wanaoelewa kwa kina
wanalolitongoa.
(k) Maudhui makuu katika majigambo ni ushujaa.
Umuhimu wa majigambo
(a) Hukuza ubunifu. Kadiri mtu anavyotunga na kughani majigambo ndivyo
anavyoimarisha uwezo wake wa kubuni mitindo mipya ya utunzi na uwasilishaji.
(b) Hukuza ufasaha wa lugha.Watunzi wengi wa majigambo huwa walumbi.
(c) Ni nyenzo ya burudani. Majigambo huongoa waliohudhuria sherehe ambapo
yanatolewa.
(d) Hudumisha utu na utambulisho wa mwanaume katika jamii. Kwa sababu ya uchokozi
uliokuwepo katika jamii, ilikuwa muhimu kwa wanaume katika jamii kuwa jasiri,
wakakamavu na mashujaa waliokuwa tayari kutetea jamii zao. Kupitia kwa majigambo,
wanaume walidhihirisha nafasi zao katika jamii.
(e) Ni nyenzo ya kufanya watu waheshimiwe. Hudumisha ari ya kuwafanya wanaume
kutaka kuwa mashujaa. Mtu alipofanya kitendo cha ushujaa alijigamba na
kuheshimiwa. Kwa sababu hii, kila mtu alitaka kufanya jambo la kishujaa ili ajigambe
na kuheshimiwa.
Mfano wa majigambo
(ii) Tondozi
Tondozi ni tungo ambazo hughanwa kuwasifu watu, wanyama au vitu kama milima,
Mfano wa tondozi
Kipungu kipungu
Nani kama yeye?
Hashindiki kwa nia
Hashindiki kwa shabaha
Hulenga mbinguni
Hutia ghera kufikia peo
Peo zisofikika kwa wanokata tamaa
Kipungu, kipungu, hachi tufani za anga.
Tendi
Tendi huitwa pia ushairi wa ushujaa. Utendi ni ushairi mrefu wa kimasimulizi unaotumia
mtindo (lugha ya) wa kiwango cha juu na ambao nguli wake ni jagina au shujaa mwenye
sifa za kiuunguungu.
Tendi husimulia matukio ya kihistoria yenye uzito au umuhimu wa kijamii na kitaifa.
Husimuliwa kwa mfano, kuhusu mwanzilishi wa dini au shujaa wa vita.
<<
Sifa za tendi
(a) Tendi husimulia matukio muhimu ya kihistoria au kijamii kama vile vita vya ukombozi,
safari ndefu au watu mashuhuri.
(b) Utendi ni masimulizi yenye ulumbi na lugha ya kiwango cha juu. (Ulumbi ni sanaa ya
kutumia lugha kwa upekee.)
(c) Ingawa tendi huhusu matukio ya kweli, tendi nyingi huchanganya historia na visasili
(imani za kidini za kijamii kuhusu asili ya matukio ya kijamii). Matukio na sifa za
wahusika husimuliwa kwa kupigwa chuku kiasi kwamba wanaonekana kutokuwa watu
wa kawaida.
(e) Utendi unaweza kughanwa au ukaimbwa kishairi. Uwasilishaji wake pia unaweza
kuandamana na ala za muziki.
(£) Tendi hutolewa katika mazingira maalumu. Ikiwa utendi utawasilishwa hadharani,
hafla ambamo unatolewa huwa ama rasmi au ukahusiana na miviga kama vile harusi
na matambiko.
Tendi hupokezwa kutoka kizazi hadi kingine.
Kwa kawaida tendi ni tungo ndefu.
Tendi hutungwa papo hapo, hivyo huathiriwa na muktadha wa utungaji. Hata hivyo,
sanaa ya utendi imebadilika na sasa huhifadhiwa vitabuni kimaandishi.
Baadhi ya tendi muhimu katika jamii za Waafrika ni:
(i) Utendi wa Fumo Liyongo (ii) Utendi wa Sundiata
(iii) Utendi wa Al-Inkishafi (iv) Utendi wa Mwanakupona
(v) Utendi wa Adamu na Hawa (vi) Utendi wa Shaka Zulu
(vii) Utendi wa Tambuka viii) Utendi wa Shufaka.
(ir) Utendi wa Mwindo (2) Utendi wa Lianja.
Mfano 1 wa utendi
62. Kwali na makadhi wamua haki, 63. Aimi! Wawapi wake zidiwa,
wahakiki zuo wakihakiki, Zituzo za mato, wasiza ngowa?
Waongoza watu njema tariki; Wasiriye wote kuwa mahuwa;
wesiwe kwa wote waitishiye. sasa ni waushi waliushiye.
Mfano 2 wa utendi
Rara
Rara ni hadithi fupi na nyepesi za kishairi zinazopitishwa kwa mdomo. Rara huzungumzia
tajiriba ya maisha kwa kutamba hadithi kwa mtindo pendwa au kwa njia ya kusisimua.
Wakati mwingine, hughanwa kwa kuandamana na ala za muziki.
Rara nyingi pendwa husimulia matukio ya kubuni, ingawa kuna chache zinazosimulia
matukio ya kweli. Zinaweza kusimulia kuhusu mahusiano mbalimbali kama vile kati ya
waajiri na waajiriwa, uhaba wa kazi, suala la usalama, masuala ya kijinsia na msongamano
wa magari.
ai
Sifa za rara
(a) Hadithi katika rara huwasilishwa katika beti, kila ubeti ukishughulikia suala bainifu.
Maana ya kila ubeti huwa wazi.
(b) Huwasilishwa kwa mtindo igizi kwa kuandamana na ala za muziki na utendaji wa
matukio.
(c) Hupatikana katika fani au mitindo tofauti tofauti. Hii ni kwa sababu waliozighani
walijifunza na kuzipitisha kwa njia ya mdomo na kuingiza mabadiliko.
(d) Rara nyingi simulizi zilihusu koo tawala japo za kisasa zimeanza kusimulia masuala
ibuka na ya kawaida, kama vile mahaba, kwa lugha isiyo rasmi.
Kwa kawaida, rara simulizi hutolewa kwa toni ya kitanzia.
Rara husisimua. Kwa kawaida rara huwa na mwanzo wa kiupeo unaoteka hisia za
msikilizaji na kumsisimua kwa lugha yenye mguso.
Rara nzuri zaidi huwa na ufumbaji na udokezaji wa masuala badala ya kuyaelezea kwa
ukamilifu na uwazi. Zinaweza kutumia sitari badala ya kutaja jambo moja kwa moja.
Rara pia huwa na ucheshi wenye kinaya.
(h) Nyingi za rara husimulia mambo ya kubuni. Hata hivyo, kuna baadhi ya rara ambazo
husimulia visa vya kweli.
Mfano wa rara
Alijua nilimpenda
Ila hata hilo alijipa kujipurukusha
Akayoyomea
Akamezwa na ulimwengu.
Jibu maswali yafuatayo kwa kurejelea utungo uliosoma.
1. Bainisha mzungumzaji (nafsineni) katika utungo huu.
2. Mzungumzaji analalamikia nini?
3. Eleza toni ya rara hii.
4 Bainisha sifa za rara zinazojitokeza katika utungo huu.
Rara nafsi
Huu ni ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake
mwenyewe. Kwa kawaida, rara nafsi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji unaoandamana na
ala za muziki. Hushughulikia masuala yanayoathiri hisia za mtu binafsi kama vile mapenzi,
usaliti, talaka na kifo. Mashairi mengi yanayohusu mahaba ni rara nafsi. Rara nafsi
hubainisha tabia za anayeghani, historia yake, imani na mionjo yake ya maisha. Ushairi
rasmi wa makiwa na sifo ni aina za rara nafsi.
(c) Katika baadhi ya jamii, rara nafsi zilighanwa katikati ya utambaji wa ngano, wakati
wa kazi kama vile mavuno au utwangaji wa nafaka au katikati ya sala.
Mfano wa rara nafsi
ka
Ngonjera
Ngonjera ni tungo za kishairi ambazo huwa na muundo wa kimazungumzo.Mazungumzo
katika ngonjera ni ya kulumbana au kujibizana. Mhusika mmoja husema au huuliza jambo
na mhusika mwingine hujibu au kuendeleza mazungumzo.
Katika ushairi simulizi, ngonjera huendelezwa (kwa kawaida kwa njia ya wimbo) pale mtunzi
mmoja husema jambo ambalo linaendelezwa na wenzake kwa njia hiyo hiyo - ya wimbo.
Katika baadhi ya jamii za Kiafrika, kuna nyimbo za harusi za aina ya ngonjera ambapo
upande wa bwana harusi huimba kuhusu jambo ambalo hujibiwa na upande wa bibi harusi.
Umuhimu wa ngonjera
(a) Hukuza ubunifu. Majibizano kati ya wanaobishana humfanya kila mmoja atake
kuonekana bora zaidi katika ubunifu.
(d) Hutia hadhira hamu ya kutenda jambo fulani au kuwasilisha maarifa fulani.
Mfano wa ngonjera
Mashairi mepesi
Haya ni mashairi ya kawaida ambayo hupatikana katika ushairi simulizi na ambayo
hukaririwa. Hujumuisha mashairi mafupi ya kihisia, kimapenzi, ya kuwasifu na kuwakosoa
watu, kuelekeza au hata kufahamisha kuhusu suala fulani. Kuna mashairi ya kisasa, kama
vile ubaguzi wa kijinsia, ukiukaji wa haki za watoto na ufisadi, ambayo yamehifadhiwa
kwenye maandishi.
Mfano wa shairi
Wa zamani waliamba, mwacha mila hujituma — Vazi hino kuazima, kamwe halitegemeki
Vipi wewe tauamba, utamaduni wa zama? Utakuwa ja kulima, wa shamba asomiliki
Kokote utapotamba, hutopata ila mama Mwenyewe kiliandama, mkulima hujidhiki,
Utamaduni ndo mama, mwingine ni wa kuomba. Kutafutala kukodi, kwanihanapakwegema.
AA AAA
AAA IIIA
Utangulizi
Maigizo au drama ni sanaa ya mazungumzo yanayoambatana na matendo. Katika maigizo,
wahusika waigizaji huigiza tabia, maneno na matendo ya watu wengine katika jamii kwa
nia ya kuburudisha na kupitisha ujumbe fulani. Maigizo au uigizaji hupatikana katika tanzu
nyingine za fasihi simulizi ya Kiafrika. Katika hadithi, kwa mfano, utambaji huandamana
na matendo. Uigizaji pia hupatikana katika vipera vya ushairi simulizi kama vile ngonjera,
majigambo, tendi na mazungumzo kama vile soga, ulumbi na malumbano ya utani.
Vipera vya maigizo ni kama vile: michezo ya jukwaani, michezo ya watoto, vichekesho,
miviga, matambiko na ngomezi.
Sifa za maigizo
(a) Maigizo hutolewa au huigizwa mbele ya hadhira. Lazima kuwa na mwigizaji (fanani)
na mtazamaji (hadhira) ili uwasilishaji wa utanzu huu ukamilike.
(b) Uigizaji huhitaji uwanja maalumu wa kutendea au mandhari.
(c) Maigizo hufungamana na shughuli za kijamii kama vile utambaji wa hadithi na sherehe
za miviga kama jando, harusi na matanga. |
(d) Katika maigizo, sharti kuwe na tendo la kuigizwa. Wahusika huiga tabia au matendo
ya watu na viumbe wengine kwa nia ya kuelimisha, kukashifu na kuburudisha.
(e) Waigizaji huvaa maleba yanayooana na hali wanazoigiza.
(£) Maigizo huiga hali ya maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kitamaduni kwa nia ya
kuonyesha mafanikio, udhaifu na migogoro katika nyanja za maisha.
(g) Maigizo huwa na muundo mahususi wa mtiririko wa matukio. Huanza kwa utangulizi |
wa mchezo (unaohusu kutambulisha mgogoro), ukuzaji wa mgogoro wenyewe, kilele |
cha mchezo (mgogoro) na mwisho (usuluhishaji wa mgogoro).
(h) Maigizo yanaweza kuambatana na ngoma pamoja na uimbaji wa nyimbo au ukariri
wa tungo za kishairi.
Umuhimu wa maigizo
(a) Maigizo huburudisha watazamaji na waigizaji wenyewe. Watu hutumbuizwa na
kupumbazwa na maigizo kama vile ya ngoma za kitamaduni na vichekesho.
(b) Maigizo huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Desturi za jamii kama vile
upashaji tohara, matambiko, majigambo, ngoma, miviga na michezo ya watoto
hudumishwa kupitia kwa maigizo.
(c) Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii ina sanaa yake ya maigizo ya shughuli za jamii
husika. Miviga kama vile mazishi na harusi hutofautiana kutoka jamii moja hadi
nyingine. Michezo ya watoto huwa mahususi kwa watoto wa jamii fulani.
(d) Hukuza umoja na ushirikiano. Watu wanapokuja pamoja kushiriki katika maigizo
hujitambulisha kama jamii moja.
Ni nyenzo ya kupitisha maarifa na amali za jamii. Kupitia kwa michezo ya jukwaani,
matambiko, ngoma, miviga na vipera vingine vya maigizo, maarifa na amali za jamii
hupitishwa. i
Husawiri mitazamo ya jamii kuhusu masuala mbalimbali. Baadhi ya uigizaji hufanyia
tashtiti vitendo vinavyochukiwa na wanajamii kama vile woga, wizi na usaliti.
(8) Husifu tabia chanya na kukashifu tabia hasi. Baadhi ya vichekesho hukashifu matendo
ya kijinga.
Hukuza uzalendo. Kupitia kwa maigizo kama vile miviga, vijana hujitambulisha na
jamii zao na kuzionea fahari. Baadhi ya miviga kama vile maigizo ya kutawazwa kwa
viongozi husifu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii zao. Vijana na wanajamii hupata
kielelezo bora cha kuiga.
Huimarisha na kupalilia ubunifu. Kwa mfano, watoto wanaposhiriki katika michezo
ya watoto, hujifunza kubuni michezo wakiwa wachanga na pia kujifunza sanaa ya
uigizaji.
GJ) Hukuza kipawa cha uongozi. Waigizaji wanapochukua majukumu ya uongozi katika
michezo huweza kujifunza stadi za uongozi.
(k) Ni njia ya kuimarisha urafiki. Mathalan, mizaha au utani katika malumbano ya
utani yanapoigizwa hukuza urafiki, uhusiano bora na stahamala kati ya watu, koo na
makabila yanayolumbana. Pia, waigizaji wa michezo ya jukwaani wanapoigiza pamoja
hujenga uhusiano wa kirafiki.
(D) Huongoza jamii kupambana na mazingira wanamojipata. Kutegemea imani ya
wanajamii, matambiko yanaweza kuondoa matatizo katika jamii kama vile njaa,
ugonjwa na ukame kwa kuomba Mungu au miungu.
(m) Huelimisha. Kupitia kwa maudhui na hulka za waigizaji, hadhira hupata fursa ya
kujitathmini na kushauri nafsi zao kuiga ama kukashifu hulka hizo.
Sifa za mwigizaji bora
Kufanikiwa kwa uigizaji, kwa kiasi kikubwa, kunawategemea waigizaji. Mwigizaji bora
huwa na sifa zifuatazo:
(a) Ni jasiri. Ili aweze kuigiza bila woga mbele ya watu, ni sharti awe na ujasiri.
(b) Ni mbunifu. Huweza kutumia mbinu mbalimbali za uigizaji ili kuufanya uigizaji
kuvutia, kuondoa ukinaifu na kusisitiza ujumbe.
(c) Ni mwenye ujuzi wa kutumia ishara za uso, za mwili na miondoko ambayo inaoana
na hali anayoigiza. Ikiwa anaigiza hali ya huzuni, ishara za usoni zionyeshe hali hiyo.
(d) Ni mwenye ujuzi na ufasaha wa lugha. Aweze kutumia lugha ipasavyo kuwasilisha
mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
(e) Anaielewa hadhira yake ili abadilishe mtindo wa uigizaji kulingana na kiwango na
matakwa yao.
(£) Anapaswa kuvaa maleba yanayooana na nafasi anayoigiza. Ikiwa anaigiza mzee, avae
mavazi ya kizee. Ikiwa anamwigiza mtu mwenye cheo, avae mavazi yanayooana na
hadhi hiyo.
(g) Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti tofauti za matukio
anayoigiza. Tukio la huzuni, kwa mfano, liwasilishwe kwa toni ya huzuni. Tukio la
kuudhi pia liwasilishwe kwa toni ya kukashifu.
(h) Hushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kutazama
na kusikiliza tu uigizaji na kumsaidia kuboresha uwasilishaji.
(i) Sharti aelewe utamaduni wa hadhira yake ili asitumie maneno na ishara ambazo
zinakinzana na imani yao.
Michezo ya jukwaani
Hii ni aina ya michezo ambayo huigizwa jukwaani au mahali wazi. Mchezo wa jukwaani
huigizwa moja kwa moja mbele ya hadhira hai. Uigizaji wa michezo ya jukwaani huonyesha
kisa cha mgogoro fulani wa kijamii. Mgogoro huu unaweza kuwa kati ya wanajamii au
mgogoro kati ya mhusika na nafsi yake. Michezo inayoigizwa jukwaani inaweza kuwa ya
kawaida au ikawa michezo bubu (michezo isiyoambatana na sauti).
(c) Hukuza ubunifu. Waigizaji huhitajika kuiga tabia, hali au sauti za wahusika wa
hadithini. Pia, huhitajika kubuni mbinu mpya za uigizaji ili kuivuta hadhira.
(d) Ninyenzo ya kukuza umoja. Watu wanapokuja pamoja kutazama michezo, urafiki na
utangamano hujengeka.
(e) Hukuza uwezo wa kukumbuka. Mwigizaji huhitajika kukumbuka maneno halisi ya
mhusika wa mchezoni ili ayawasilishe kwa hadhira jinsi yalivyo.
(f) Hukosoa jamii. Watu wanaofanya kinyume na matarajio ya jamii kama vile wivu,
uchoyo au wizi hutungiwa mielezo inayosawiri matendo yao kwa nia ya kuwakosoa
kwa kudhihaki.
Vichekesho
Vichekesho ni michezo mifupi ambayo hupitisha ujumbe kwa namna ya kuchekesha.
Vichekesho vinaweza kujitegemea kama kipera cha maigizo au vikategemeana na
kufungamana na tanzu au vipera vingine vinavyoibua kicheko kama vile ngano na ulumbi.
Sifa za vichekesho
(a) Vichekesho huigizwa.
(b) Huwasilishwa kwa lugha sahili au nyepesi iliyojaa taswira zinazoweza kutambuliwa
na hadhira.
(c) Hutumia mbinu ya kejeli, kinaya au tashtiti kwa ufanifu mkubwa.
(d) Hushughulikia masuala ya kijamii kwa njia nyepesi, lakini inayonuiwa kuadilisha au
kurekebisha tabia.
(e) Vichekesho huwa vifupi.
(£) Vichekesho havihitaji uchambuzi wa makini au wa ndani ili kuvielewa au kupata
maana.
Umuhimu wa vichekesho
Majigambo/Vivugo
Ingawa majigambo huainishwa kama kipera cha ushairi, yanaweza kuigizwa. Ikiwa
yatasimuliwa au yatakaririwa yakiambatanishwa na matendo basi yanaweza kuainishwa
katika utanzu wa maigizo. Majigambo, aghalabu yaliambatana na ngoma. Katikati ya ngoma,
aliyejigamba anajitokeza na kujigamba na kisha kurudia kucheza ngoma. Aliyejigamba
anabeba zana zake za vita, kama vile mkuki na ngao, ambazo alizitumia kuonyesha jinsi
alivyotenda matendo ya kishujaa aliyojigambia. Aidha, alivaa maleba kuambatana na jambo
alilojisifia.
(Kwa maelezo zaidi, rejelea Majigambo ukurasa 112 — 114.)
Michezo ya watoto/chekechea
Hii ni michezo ambayo huigizwa na watoto katika shughuli zao za kila siku. Watoto huigiza
mambo wanayoyaona katika mazingira yao kama vile upishi, ukulima, sherehe za kijamii,
kama vile arusi, shughuli za kiuchumi kama vile biashara na kilimo.
Ngonjera
Kama tulivyotaja, ngonjera ni mashairi ambayo hukaririwa, huimbwa au kughanwa kwa
njia ya kujibizana. Ili majibizano hayo yawe sehemu ya maigizo, ni lazima yaambatane na
vitendo au utendaji.
Ngonjera isiyoambatana na maigizo/ishara za mikono na uso haiwi maigizo, huwa shairi
simulizi tu.
(Rejelea sehemu ya Ushairi Simulizi kwa maelezo zaidi na mfano wa ngonjera uk. 121.)
Ngoma
Katika fasihi simulizi, neno ngoma linaweza kuwa na maana kadha. Kwanza, ni chombo
cha muziki. Pili, ni sherehe kama vile jando au harusi, na tatu ngoma ni uchezeshaji wa
viungo vya mwili kuambatana na mdundo au mwondoko maalumu. Maelezo tunayonuia
hapa ni ya maana ya tatu ya ngoma.
Ngoma hutofautiana kulingana na jamii zilimozaliwa. Kila jamii ina ngoma yake mahususi.
Kwa mfano, jamii ya Wabukusu wana Isukuti; Wakamba, Wathi na Kilumi ilhali Waswahili
wana Chakacha.
Ngoma huweza kuchezwa ikiandamana . wa
na sherehe maalumu au ikachezwa bila WA UU
kufungwa katika sherehe yoyote kwa 3 iz.uu
LI AA AUA
NAI
nia ya kustarehesha na kufurahisha.
Aina hii ya ngoma huchezwa popote ili
kuburudisha watu. Ngoma hutofautiana
kulingana na dhamira ya ngoma na
wachezaji wake. Kuna ngoma za harusi,
za kufukuza mapepo, za kuaga mwaka,
na za unyago na jando. Kwa kufuatia
mkabala wa wachezaji, kuna ngoma
za wanawake, ngoma za vijana na pia
ngoma za wazee.
Sifa za ngoma
(a) Ngoma huandamana na muziki au ala za muziki kama vile ngoma. Aidha, wachezaji
ngoma huvaa maleba maalumu. Mara nyingi, maleba huteuliwa kulingana na mafunzo
yanayonuiwa kupitishwa pamoja na kaulimbiu ya kikundi chenyewe.
(b) Ngoma kwa kawaida huchezewa mahali wazi, kwenye kumbi za kuigizia michezo au
mahali popote palipo na nafasi ya kutosha kuchezewa.
(c) Katika ngoma, kuna wahusika wa aina mbili: watendaji (wachezaji) na watazamaji
(hadhira). Ili sanaa ya ngoma ikamilike, makundi haya mawili yanastahiki yawepo
kwa wakati mmoja.
Dhima ya ngoma
(a) Kuburudisha. Watu hutazama ufundi wa uchezeshaji viungo kufuatia midundo ya
ngoma inayoandamana nao kwa nia ya kujiburudisha.
(b) Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii huwa na aina zake za ngoma.
(c) Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii husika. Kila aina ya ngoma hufumbata
desturi za jamii hiyo. Kwa kuzipitisha ngoma hizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine,
jamii hudumisha utamaduni wake.
(d) Huleta utangamano katika jamii. Watu wanapojumuika kucheza ngoma, hujihisi kitu
kimoja na urafiki au udugu hujengeka.
(e) Huelimisha. Kupitia kwa nyimbo zinazoandamana na ngoma, jamii huweza kupitisha
mafunzo au maarifa maishani. Maudhui katika nyimbo hizi ni mapana na hulenga
kuadilisha pamoja na kuburudisha.
(f£) Hukuza ubunifu. Uchezaji ngoma ni ufundi unaohitaji kuchezwa kwa mtindo wake
kulingana na mdundo wa muziki. Wachezaji hubuni mbinu za kucheza ngoma upya.
Pia mashindano mbalimbali ya uchezaji wa ngoma hizi huimarisha zaidi vipawa vya
ubunifu. y
(g) Hukuza uzalendo. Ngoma za kitamaduni huwafanya wanajamii kuionea fahari jamii
yao, hivyo uzalendo kujengeka.
Miviga
Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalumu
cha mwaka. Mara nyingi, miviga kama vile jando hufanywa katika kipindi baada ya mavuno.
Miviga ya mazishi, kwa mfano, hufanywa kabla ya wakati fulani wa siku kutegemea imani
ya jamii. Aidha, miviga ya kuwapa watoto majina huathimishwa muda fulani baada ya
mtoto kuzaliwa.
Sanaa ya maigizo katika baadhi ya miviga hujitokeza pale mwanajamii anapoingizwa katika
kundi fulani kutoka kundi jingine. Uhamishwaji huu huandamana na majukumu mapya
pamoja na madaraka. Kwa mfano:
(i) Kutoka katika kundi la watoto kuingia kundi la watu wazima (jando au unyago).
(ii) Kutoka kundi la makapera kuingia kundi la waliooa (arusi).
(iii) Kutoka kwa uraia kuingia jeshi (askari).
(iv) Kutoka kwa uraia kuingia kwa utawala (kutawazwa kuwa kiongozi).
(v) Kutoka uhai kuingia ufu (mazishi).
Aghalabu miviga huwa na hatua tatu:
(i) Kumtoa mtu rasmi kutoka kundi moja la wanajamii.
(ii) Kumfundisha majukumu yanayohusiana na wadhifa mpya.
iii) Kumwingiza rasmi katika kundi jingine.
Dhima ya miviga
(a) Huelimisha wanajamii. Wakati wa jando, vijana huelimishwa kuhusu mambo
yanayohusu utu uzima na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za
maisha.
(b) Huonyesha matarajio ya jamii kwa vijana/wanajamii. Katika mafundisho yanayotolewa
katika miviga, matarajio ya jamii hubainika. Kupitia kwa sherehe za harusi, matarajio
ya jamii kuhusu wake/waume hupitishwa.
(c) Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii huwa na miviga yake mahususi. Sherehe za
mazishi ama za kumpa mtoto jina huendeshwa kwa namna fulani na jamii fulani. Pia
huonyesha mpangilio wa jamii husika.
(d) Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Miviga hupitishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine ili kuhifadhi utamaduni.
(e) Hukuza uzalendo. Huwahimiza wanajamii kuzionea fahari tamaduni za jamii yao.
Vijana wanapojumuika pamoja katika miviga kama vile sherehe za jando hujitambulisha
na jamii yao na uzalendo huimarika.
(ai)
(f£) Huhimiza na kukuza umoja miongoni mwa wanajamii wanapojumuika pamoja katika
sherehe kama vile harusi, matambiko ama mazishi.
(g) Miviga huwasaidia wanajamii kukabiliana na hali ngumu katika maisha kama vile
kufiwa.
(h) Ni njia ya kupitisha maadili na thamani za jamii kwa vijana. Hufunza umuhimu wa
kazi, suala la unyumba, uzazi na malezi kwa jumla.
(i) Ni mizani/kigezo cha kuonyesha kuvuka kutoka daraja moja la maisha hadi jingine.
Mathalani kupitia sherehe za jando, wavulana huhisi kuwa wakati umewadia wa kuacha
utoto na kuingia katika utu uzima. Harusi pia ni kivuko cha kutoka useja/ujane na
kuingia katika maisha ya ndoa.
(Jj) Huonyesha imani za kidini za jamii. Kila jamii ina imani zake za kidini na viviga
vinavyoambatana nazo. Kupitia kwa miviga, tabia zinazohusishwa na imani zao
huonekana. ;
Hasara za miviga
(a) Baadhi ya miviga kama vile kutiwa unyagoni kwa wasichana na kurithi mke wa mtu
aliyeaga zimepitwa na wakati. Huhatarisha maisha na afya ya wanajamii.
(b) Baadhi ya miviga hukinza malengo ya kitaifa. Kwa mfano, kutia unyagoni kwa lazima
na ukeketwaji wa watoto wa kike ni ukiukaji wa haki za binadamu.
(c) Hujaza watu hofu. Kwa mfano, miviga inayohitaji kafara ya binadamu katika baadhi
ya jamii huogofya. Aidha, sherehe za kufukuza pepo huhofisha.
(d) Baadhi ya miviga huhusisha ushirikina. Mazishi katika jamii nyingine huandamana
na ushirikina ambao huweza kusababisha uhasama baina ya koo.
(e) Baadhi ya sherehe za miviga hugharimu kiasi kikubwa cha pesa/mali na kuiacha familia
katika hali duni kiuchumi. Sherehe za kuomboleza katika jamii nyingine huandamana
na matumizi ya fedha nyingi.
Matambiko
Tambiko ni sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu
moja kwa moja au kwa Mungu kupitia kwa miungu. Yapo matambiko yalitolewa na wazee
maarufu waliopewa jukumu hilo. Matatizo yaliyoshinda mababu zetu yalipelekwa kwa
miungu ili iwasaidie kuyatatua. Baadhi ya matatizo haya yalikuwa magonjwa, ukame, kukosa
kupata watoto au mafuriko. Wakati mwingine, matambiko yalifanywa kutoa shukrani au
kuomba radhi. Iliaminiwa kuwa baadhi ya matatizo yalisababishwa na hasira za miungu.
Ili kuomba radhi, matatizo haya yalipelekwa kwa miungu mbalimbali kutegemea tatizo
lenyewe, mathalani, kwa mungu wa jua, wa mvua au wa milima.
Aghalabu matambiko yaliambatana na kafara ambazo zilibadilika kutegemea jamii na tatizo
lilitolewa kafara. Kwa hivi leo, matambiko yanaendelea kufa.
Sifa za matambiko
Sifa za ngomezi
(a) Kila mdundo wa ngoma huwakilisha kauli mahususi kwa lugha ya jamii ambamo
ngomezi imezuka.
(b) Ngomezi hutegemea mapigo, wizani na upatano unaotokana na ngoma inayopigwa
kuwasilisha ujumbe. j
(c) Fasiri (maana) hujikita na kutokana na jamii husika. Jamii ndiyo huyapa mapigo ya
ngoma maana yake. Maana ya mapigo hayo basi hueleweka tu na wanajamii walioubuni
mpigo huo wa ngoma.
(d) Kila mpigo wa ngoma hufuata mtindo wa kishairi. Kila mpigo huwakilisha silabi au
mizani katika lugha tamkwa. Hii ndiyo sababu lugha ya ngomezi ikachukuliwa kuwa
lugha ya kishairi. Katika jamii ya kisasa, matumizi ya ngomezi huweza kupatikana
kupitia:
(i) kengele zinazotumiwa kupigia hodi kwenye majumba.
(ii) kamsa/milio kwenye magari kama ambulensi. Magari ya kawaida pia hutiwa vifaa
ambavyo hutoa milio pindi magari hayo yakiguswa.
iii) toni katika rununu huwakilisha aina mbalimbali za taarifa/ujumbe.
Oo
Majukumu ya ngomezi
Ngomezi ina majukumu yafuatayo:
(a) Ninyenzo ya kupitisha ujumbe wa dharura kuhusu matukio ya dharura kama vile vita.
Hutumiwa kutoa matangazo rasmi.
(b) Nikitambulisho cha jamii. Huonyesha ufundi wa jamii wa kutumia vyombo vya muziki.
Kila jamii huwa na ngomezi zake mahususi. Ujumbe wa kuzaliwa kwa mtoto huweza
kupitishwa kwa mapigo tofauti tofauti ya ngoma kutegemea na jamii.
(c) Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii kutoka kizazi hadi kingine.
(d) Ninyenzo ya kukuza uzalendo. Wanajamii hufunzwa kuionea fahari mbinu hii yao ya
kuwasiliana.
(e) Hukuza ubunifu. Jinsi wanajamii wanavyokabiliwa na aina tofauti tofauti za ujumbe
ndivyo wanavyojifunza/wanavyobuni mitindo mipya ya kuwasilisha ujumbe kwa
ngoma, hivyo kuimarisha ubunifu.
(f) Ni njia rahisi ya kuwasilisha ujumbe bila kutegemea sauti ya mtu.
Hata hivyo, ngomezi huweza kutatiza hasa pale wanajamii wanaposhindwa kufasiri ujumbe
au wanapofasiri ujumbe visivyo.
Utanzu wa Mazungumzo
Utangulizi
Mazungumzo ni maelezo ya mdomo kwa lugha ya kawaida kuhusu suala lolote. Mazungumzo
huwa fasihi pale ambapo yanadhihirisha usanii wa aina fulani; pale ambapo yanaeleza
ukweli kwa namna ambavyo hayaunukuu tu moja kwa moja, bali yanaueleza kwa ubunifu.
Katika kuzungumzia tukio la kawaida, mtu anaweza kuifinyanga lugha kwa ufasaha na kwa
njia isiyo ya kawaida. Mazungumzo ya aina hii huwekwa katika kundi la fasihi simulizi.
Mazungumzo yanayotokea katika miktadha rasmi hutengewa vikao maalumu. Pia, kuna
mazungumzo yasiyo rasmi. Katika jamii za Kiafrika, mazungumzo rasmi hupatikana katika
miktadha mingi kama vile:
(i) kwenye sherehe za jandoni (mawaidha)
(ii) kwenye harusi (hotuba na mawaidha)
(iii) maabadini (mahubiri na sala)
(iv) kwenye mazishi (hotuba na taabili/taabini)
(v) mikutano ya kisiasa (hotuba)
(vi) shughuli za posa (hotuba)
(vii) kortini (ulumbi).
Mazungumzo pia hupatikana katika vipera vingine vya fasihi simulizi kama vile utegaji na
uteguaji wa vitendawili, maigizo na hata utambaji hadithi.
Malumbano ya utani
Malumbano ya utani ni majibizano kati ya watu wawili au makundi mawili ya watu kwa
nia ya kutaniana. Ni mazungumzo yanayofanywa kwa kutumia maneno ya mzaha ili kuleta
ucheshi. Watu hutaniana kwa kutumia lugha kwa ufundi na mtiririko maalumu. Kuna aina
mbalimbali za utani: ;
Cs)
(i) Utani wa mababu/mabibi na wajukuu
(ii) Utani wa marafiki
(iii) Utani wa koo, makabila au mbari
(iv) Utani wa mawifi na mashemeji
(v) Utani wa marika
(vi) Utani wa maumbu.
(e) Hukosoa na kukashifu tabia hasi. Baadhi ya malumbano ya utani hudhihaki ulafi,
uchoyo, wivu na tabia nyingine mbaya.
(f£) Huburudisha. Ucheshi katika malumbano ya utani huburudisha na kuchangamsha.
(g) Huelimisha. Kupitia kwa malumbano ya utani, watu hupana maarifa ya kukabiliana
na hali mbalimbali katika maisha.
Ulumbi
Huu ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee. Ni utumiaji wa lugha kwa mvuto
na ufasaha. Ulumbi humwezesha mtu kulielezea jambo la kawaida kwa namna ambavyo
linaonekana kuwa geni kabisa na kuwashawishi watu kulikubali au kulipenda. Kuna aina
mbili za ulumbi: rasmi na usio rasmi.
Ulumbi rasmi huweza kupatikana katika miktadha mbalimbali kama vile:
(i) kortini, ambapo mawakili hutoa hoja zao kutetea wanaowawakilisha.
(ii) kanisani/msikitini wakati wahubiri wanapotoa sala/mahubiri.
(iii) mijadala ya kisiasa ambapo wanasiasa wenye vipawa vya ulumbi huvitumia
kuwapiku wanasiasa wenzao na kuwashawishi raia kuwapigia kura.
(iv) katika sherehe za harusi au mazishi, kwa mfano, katika kutoa taabini/taabili
(hotuba kumhusu marehemu).
(v) katika kuapiza na katika kufukuza pepo.
(vi) katika utoaji wa risala. j
(vii) ulumbi usio rasmi hupatikana ambapo watu hutumia lugha kwa ufasaha hata katika
kuapiza/kulaani au hata katika mazungumzo ya kupitisha muda na marafiki. |
Sifa za ulumbi
(a) Ulumbi ni usemaji au uzungumzaji wa kifasihi. Mlumbi hutumia lugha kwa njia
inayovutia na kushawishi hadhira yake. |
(b) Ulumbi hubainika katika miktadha ya kutoa hotuba au katika hali ambapo mtu
anahitajika kutetea msimamo wake katika vikao, au hata katika mijadala rasmi.
(c) Hukuza ukakamavu wa kuzungumza hadharani. Mlumbi hupenda kuzungumza na
hupenda kujisikia akizungumza mbele ya watu.
(d) Hutumia vipengele anuwai vya lugha kama vile sitiari, maswali ya balagha, methali,
nahau, taswira na viziada-lugha kama vile toni, kiimbo na kidatu ili kuishawishi hadhira
au kutilia mkazo wazo fulani na kutetea misimamo yao. Hutumia lugha kutegemea
muktadha na hadhira yake.
Ce) Katika baadhi ya jamii, walumbi walitumiwa kuzungumza kwa niaba ya viongozi kama
vile machifu, wanaoomba posa au kwa niaba ya ukoo au mwanajamii aliyedhulumiwa.
Walumbi wengi aghalabu huwa na vipawa vya uongozi na huinukia kuwa viongozi wa
jamii zao.
(£) Utoaji hotuba kwa umbuji ni jambo ambalo limetambuliwa katika jamii nyingi. Ulumbi
husisitizwa sana katika matabaka ya juu kama kitambulisho cha tabaka hilo. Katika
baadhi ya jamii, watu katika tabaka tawala walifunzwa kutumia msamiati wenye
haiba, matumizi ya ishara, toni na sauti zifaazo. Hili lilinuiwa kuimarisha stadi za
ulumbi. Hata katika jamii ya kisasa, viongozi hufunzwa naa kufanyizwa mazoezi ya
kutoa hotuba kwa ufasaha (ulumbi).
(g) Walumbi hutumia chuku kwa ufanifu mkubwa. Hata hivyo, lazima wadumishe adabu.
(h) Ulumbi huweza kuwa na urudiaji mwingi wa maneno, virai na vishazi ili kusisitiza.
Katika sala, kwa mfano, unaweza kupata matumizi ya takriri na usambamba
yanayonuiwa kuvuta usikivu wa Mungu/miungu au kusisitiza jambo fulani.
Kifungu hiki kinarejelea wazo moja tu; mlumbi anaitetea dua — anatambua uwezo wa Mungu.
Umuhimu wa ulumbi
(a) Hukuza uwezo wa kujieleza hadharani. Kadiri mtu anavyozungumza hadharani ndivyo
anavyojiboresha kama mlumbi.
Ni nyenzo ya kukuza ujuzi na ufasaha wa lugha. Jinsi mtu anavyoitumia lugha kwa
umbuji ndivyo anavyokuza umilisi wake na umahiri wake wa kuisarifu lugha.
Ni msingi wa kuteua viongozi. Uwezo wa mtu kuwashawishi wanajamii kukubaliana
na mtazamo wake humfanya kutambuliwa kama mwenye uwezo wa kuongoza jamii.
Walumbi wana uwezo mkubwa wa kuishawishi hadhira.
Huhifadhi utamaduni wa jamii. Ulumbi ni sanaa jadiiya, yaani imekuwepo katika jamii
kwa muda mrefu ikipokezwa vizazi na vizazi.
Ni nyenzo ya kuburudisha wanajamii na kuwaelimisha bila kuwachosha. Walumbi
huweza kupitisha maarifa mbalimbali kwa wanajamii kwa njia yenye mvuto.
Hukuza uzalendo. Vijana wanapowasikiliza walumbi wakitongoa lugha, huionea fahari
lugha yao na kujitambulisha zaidi na jamii zao.
Huweza kutumiwa kuwasilisha ujumbe muhimu au ulio na athari kubwa au ambao
una makali na usio rahisi kueleza.
Ni kitambulisho cha utabaka. Katika baadhi ya jamii, ulumbi ulihusishwa zaidi na
tabaka tawala au watu wenye vyeo vya juu na haiba/heshima katika jamii zao. Katika
jamii hizi, ulumbi ni kigezo cha kuainisha matabaka.
(i) Ulumbi ni msingi wa kuheshimiwa katika jamii. Walumbi huheshimiwa kwa sababu ya
matumizi yao ya lugha yenye ujumi na umbuji katika kuyafafanua masuala ya kijamii.
Mfanowaulumbiusiorasmi
“La, hasha kimwana! Hatukukaidi wala si upepo, mabinti, ila ni wawindaji, lakini si wa
wanyama. Naomba kuyafasiri niliyoyagomba. Kwa ruhusa nitasema hivi; kwamba thawabu
ya mja ni sawasawa na jitihada na suna zake. Siku nyingi tumewinda. Na silalamiki kwa
kuwa adinasi, kiada huwinda mengi katika sayari hii kwa kadiri ya haja na hekima yake.
Hana budi, hata hivyo, kuutumia ubongo wake kwa nafasi sawasawa na namna ambavyo
Jalia alivyomkirimu. Naam, kwa maana wenye hekima hunaswa kwenye hila zao. Kwa
kuwa mpaka wa hadaa na yakini u katika ridhaa ya mwanadamu aliyejawa choyo, husuda,
hitilafu na mpungufu wa karama. Nawaomba kwa hivyo warembo mmakinike, pasiwe kwenu
faraka. Bali mhitimu katika nia moja na ushauri mmoja katika ombi letu. Naitwa Dzombo...
(Kutoka: Kipendacho Roho, Pauline Kyovi, OUP, uk. 10.)
(f) katika harusi. Mawaidha yanayotolewa kwa maarusi huchukua muundo wa hotuba.
(g) katika tamasha za muziki na ukariri wa mashairi au mashindano ya utoaji hotuba.
Sifa za hotuba
(a) Kwa kawaida, hotuba hutolewa na watu maalumu au walioteuliwa kuzungumza kama
vile viongozi au wawakilishi wao na watu wengine wenye hadhi katika jamii. Hata
hivyo, baadhi ya hotuba hutolewa katika miktadha isiyo rasmi. Katika makazi ya watu,
hotuba za waadhi/mawaidha/nasaha huweza kutolewa wakati wa chajio au baada ya
chajio.
(b) Watu wanaoteuliwa kutoa hotuba aghalabu huwa na umilisi mkubwa wa lugha.
Walumbi ni watoaji hotuba stadi. Siku hizi, viongozi pia hufunzwa stadi za kutoa
hotuba za hadharani.
(c) Hotuba hutolewa kwa nafsi ya kwanza.
(d) Mtoaji hotuba anaweza kutumia viziada-lugha kama vile ishara za uso na mikono ama
miondoko ili kufanya hotuba ivutie hadhira. Maswali ya balagha pia hutumika.
(e) Hotuba huteuliwa mada mahususi wala haizungumzii jambo lolote lile.
Umuhimu wa hotuba
(a) Huadilisha na kuasa. Hotuba zinazotolewa jandoni au katika harusi kwa kawaida
hunuiwa kutoa nasaha.
(b) Huelimisha. Hotuba za jandoni, kwa mfano, huwapa vijana maarifa ya kukabiliana na
maisha.
Mawaidha
Haya ni mazungumzo ambayo hutolewa ili kumpa mtu ushauri au nasaha kuhusu jambo
fulani. Mawaidha hutoa mwongozo na maelekezo ya kukabiliana na changamoto katika
maisha na jinsi ya kuhusiana na wanajamii.
Sifa za mawaidha
(a) Mawaidha hutolewa katika miktadha rasmi kama vile jandoni, katika harusi, kwenye
mazishi, darasani na kanisani. Hata hivyo, mawaidha yanaweza kutolewa katika
miktadha isiyo rasmi. Mzazi anaweza kumpa mwanawe mawaidha nyumbani wakati
wa chajio.
(b) Katika jamii nyingi, wazee na watu walio na vyeo vikubwa na waliochukuliwa kuwa
na hekima ndio waliopewa jukumu la kuwatolea vijana mawaidha. Hata hivyo, vijana
pia wanaweza kutoa mawaidha kwa vijana wenzao ambao wanahitaji ushauri au hata
vijana wakatoa mawaidha kwa wazee.
(c) Mwenye kutoa mawaidha hulielewa jambo analousia kwa undani. Sharti awe na ujuzi
wa kutosha katika mada anayozungumzia.
(d) Mwenye kutoa mawaidha hutumia lugha inayoathiri hisia za wanaousiwa. Inaweza
kuwa na tamathali za usemi kama vile methali.
(e) Mawaidha huingiliana na vipera vingine vya fasihi simulizi. Kwa mfano, methali
hufumbata mawaidha. Pia, utambaji ngano, miviga kama vile jando na harusi,
huandamana na utoaji wa mawaidha. Aidha, yapo mashairi ya waadhi (nasaha/
mawaidha). Hali kadhalika, anayetoa mawaidha anaweza kutumia mbazi (ngano za
kimafumbo) ili kusisitiza ushauri anaotoa.
(f) Maudhui katika mawaidha ni mapana. Huweza kugusia masuala kama vile dini,
uongozi, ujasiri, amali, elimu na taaluma, unyumba, mahusiano ya kijamii, malezi na
afya.
(g) Mawaidha yanayotolewa katika miktadha rasmi huwa na muundo maalumu wenye
sehemu tatu kuu: :
(i) Utangulizi
Katika sehemu hii, anayetoa mawaidha huanza kwa kauli ya kuvuta makini ya hadhira.
Anaweza kuanza kwa kutoa kiini cha mawaidha, kwa mfano, 'Utu uzima huenda na
uwajibikaji ...”
(ii) Mwili
za usemi kama vile methali. Wasia, maonyo na maelekezo hutolewa kutegemea lengo.
(iii) Hitimisho
Mwasilishaji huonyesha msimamo wake kuhusiana na suala analousia. Kwa kawaida,
anayetoa mawaidha huishirikisha hadhira kwa kutaka kujua msimamo au maoni yao
kuhusu suala alilowausia. Hadhira inaweza kutaja changamoto zinazohusiana na
mawaidha yanayotolewa.
Majukumu ya mawaidha
(a) Jukumu la kimsingi la mawaidha ni kuelekeza. Mawaidha hutoa mwongozo wa jinsi
ya kukabiliana na matatizo au jinsi ya kutenda jambo fulani.
(b) Huelimisha. Mawaidha huwapa wanajamii maarifa ya kuendeshea maisha. Huwajuza
wanajamii kuhusu majukumu yao ya kijamii na matarajio ya jamii zao kwao.
Mawaidha yanayotolewa kwa maarusi, kwa mfano, huwajuza wanaohusika kuhusu
yale wanayowajibika kutenda kwa mke au mume na kwa jamii kwa jumla.
(c) Huadilisha. Wanaopewa mawaidha hujifunza maadili kama vile usafi, unyenyekevu,
utulivu na kusamehe.
(d) Hutambulisha jamii. Kila jamii huwa na aina yake ya mawaidha kulingana na thamani
zake. Pia, mawaidha hutolewa kwa namna mbalimbali kutegemea jamii.
Mfano wa mawaidha
uu umumumumumumu——————————— )
1. (a) Eleza sifa za mawaidha zinazojitokeza katika utungo huu.
(b) Utungo huu au mawaidha haya yanaweza kutolewa katika muktadha au
shughuli gani katika jamii.
(c) Kwa kurejelea utungo huu, eleza mawaidha yanayotolewa kuhusiana na
ndoa.
2. (a) Taja miktadha mitano ambamo hotuba hutolewa katika jamii yako.
(b) Eleza majukumu manne ya mawaidha katika jamii yako.
3. Hotuba na mawaidha hufanana. Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano
mwafaka.
Soga
Soga ni mazungumzo yanayonuiwa kupitisha wakati. Mazungumzo haya huchukuliwa
kama fasihi yanapotolewa kwa usanii fulani yakimithilisha uhalisia badala ya kuunakili.
Katika soga, jambo la kawaida linalozungumziwa hupigwa chuku na kufanywa lionekane
kana kwamba halina uhalisia.
Maapizo
Maapizo ni maombi maalumu ya kumtaka Mungu/miungu/mizimu kumwadhibu mhusika
hasidi, mkinzani au mwovu. Hivyo, maapizo ni dua ya laana au maombi mabaya kutoka
kwa mtu ambaye anahisi ametendewa uovu au amesalitiwa na mwingine.
Sifa za maapizo
(a) Maapizo yalitolewa kwa watu ambao walienda kinyume na matarajio ya jamii zao.
Mifano ya watu hawa ni wabakaji, wezi, wauaji na waliowatusi wazazi, wazee au ukoo.
Wazazi pia huweza kutoa maapizo kwa wana wao ili kuwaonya dhidi ya hulka mbaya
kama vile utumiaji wa vileo. Huenda mzazi akasema, Nimelaani unywaji wa pombe
katika familia hii. Atakayeonja hata tone na aandamwe na ufukara usoisha!
(b) Katika baadhi ya jamii za Kiafrika, maapizo yalitolewa kabla ya ulaji viapo. Mtoaji kiapo
anaweza kusema, Ambaye amefanya tendo hili chuma hiki kimwingie kwenye mboni ya
jicho, asiuone mwangaza wa jua tena!
(c) Maapizo yanaweza kutolewa moja kwa moja na yule aliyeathirika. Mtu anapopoteza
kitu chake anaweza kuapiza ili kumtisha aliyekiiba arudishe. Kwa mfano, mtu anaweza
kusema, Aliyeiba mbuzi wangu apeperuke na huo mchanga, zizi lake lisipate kulala mbuzi
hata mmoja! Katika baadhi ya jamii, watu mahususi waliteuliwa kutoa maapizo, hasa
wakati wa ulaji kiapo. Watoaji kiapo ndio pia walioapiza.
(d) Kidini, Mungu, miungu au mizimu huweza kutoa maapizo kuhusu mustakabali wa
mhusika fulani. Aidha, maapizo ya kidini yanaweza kutolewa kama laana baada ya
mhusika kukaidi amri za Mungu au miungu. Kwa mfano, katika tamthilia ya Edipode
iliyoandikwa na Sofokile, miungu waliapiza kuwa Edipode angemuua baba yake na
kumwoa mamake mzazi. Maapizo ya aina hii huathiri, si jaala ya mhusika tu bali ya
jamii pia. Katika kisa cha Edipode, kwa mfano, waliyoapiza miungu yalitimia. Edipode
alikuja kumuua babake bila kujua (alikuwa ametoroka asimuue babake). Aidha, alimwoa
mamake bila kujua. Katika Biblia, Mungu anawalaani Adamu, Hawa na nyoka baada
ya kukaidi amri yake. Laana hii inaaminika kuwa imedumu hadi kizazi cha sasa.
(e) Maapizo huaminiwa kuwa yataleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa
kuyaepuka kwa kutenda mema.
(f£) Maapizo hutumia lugha fasaha (ulumbi). Watoaji maapizo katika ulaji wa viapo
aghalabu huwa walumbi.
(g) Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kujaza woga ili kuonya dhidi ya maovu.
Umuhimu wa maapizo
(a) Kimsingi, maapizo hutumiwa kama nyenzo ya kuwaonya wanajamii dhidi ya matendo
hasi.
(b) Hutambulisha jamii. Kila jamii ina namna yake ya kuapiza na mitindo tofauti ya kutoa
maapizo.”
(c) Hukuza umoja katika jamii. Kuwapo kwa kaida na miiko sawa huwafanya watu kujihisi
kuwa kitu kimoja.
(d) Huadilisha. Wanajamii hujifunza kutenda mema ili kuepuka laana.
Mfano wa maapizo
Ukusanyaji na Uhifadhi wa
Fasihi Simulizi
Utangulizi
Sifa za fasihi simulizi ni kwamba huzaliwa, hukua, huishi na huweza kufa. Kadiri jamii
inavyobadilika, fasihi simulizi nayo inabadilika na kuathiriwa na maendeleo ya binadamu
kisayansi, kijamii na kiteknolojia. Vipera vipya vya fasihi simulizi huzaliwa kutokana na
athari za utandawazi, hukuzwa na kupewa uhai katika mazingira mapya. Aidha, vipera
vya zamani kama vile matambiko na ngomezi huweza kufa au kupewa sura mpya. Kwa
sababu hii, kuna umuhimu wa kuhifadhi tanzu za fasihi simulizi ili zisipotee. Lakini kabla
ya kuzihifadhi, ni lazima kwanza zikusanywe. Katika kukusanya data ya fasihi simulizi,
anayenuia kuikusanya huenda ilipo jamii anayolenga kukusanya data kutoka kwao.
Ukusanyaji wa data ya fasihi simulizi hufanywa ili kuendeleza na kutekeleza malengo
muhimu yanayokusudiwa na anayekusanya.
Mkusanyaji wa data huhitajika kufuata hatua zifuatazo za utafiti: j
(a) Kujiandaa/Maandalizi — Hapa anatakiwa kuzingatia yafuatayo:
(i) Mada ya utafiti — anatafiti kuhusu nini? Je, ni uwasilishaji mbolezi?
(ii) Mawanda ya utafiti — Kama ni kitendawili, je, anatafitia fani? Aina?
(iii) Walengwa — Atatafiti katika jamii gani? Wakamba? Wajaluo? Je, walengwa ni
wa umri gani? Wazee? Vijana?
(iv) Kipindi cha utafiti — Utaanza lini na unatarajiwa kumaliza lini?
(v) Kuomba kibali cha utafiti kutoka kwa taasisi husika, k.v. Wizara ya Elimu.
(vi) Mbinu za ukusanyaji na kuhifadhi data — Je, atatumia hojaji? Mahojiano?
Maandishi? Je, vifaa hivi vi tayari? Je, ikiwa ni hojaji, atazituma kwa posta au
ataziwasilisha kwa walengwa wenyewe? |
(vii) Gharama ya utafiti — Je, atatumia kiasi gani cha pesa? Nani atafadhili utafiti?
(b) Utafiti na ukusanyaji wa data — Mtafiti anaweza kukusanya data kupitia kwa hojaji,
mahojiano, kushiriki ama kutazama?
(c) Rekodi ya data — Mtafiti anaweza kurekodi data kupitia kwa maandishi, hunasa sauti
ya mhojiwa au fanani wa ngano, n.k. Vifaa hivi sharti viwe tayari kabla ya shughuli ya
utafiti kuanza.
(d) Kuchunguza upya data/maelezo yaliyotolewa na walengwa na kuyanakili jinsi yalivyo
ili kuyachanganua baadaye.
(e) Uchanganuzi na kufasiri kwa data — Hapa mtafiti huchanganua data kulingana na
vigezo vya uchanganuzi alivyoweka awali, na kulingana na mada yake. Matokeo ya
uchanganuzi hutumiwa kutoa hitimisho na mapendekezo kuhusu mada ya utafiti.
Uchanganuzi unaweza kutumia maelezo pekee au tarakimu/takwimu pamoja na
maelezo.
1. Kusikiliza
Mkusanyaji anaweza kusikiliza wasanii katika jamii fulani wakitamba, kusimulia au
kuimba tungo zao.
2. Kushiriki
Mkusanyaji anaweza kujiunga na jamii kwa kushiriki katika ngoma, soga na masimulizi
ya hadithi na tanzu nyingine. Hapa, anayekusanya data ya fasihi simulizi haulizi
maswali bali hujirekodia anachokibaini katika ushirika huo.
Umuhimu wa kushiriki
(a) Kwa kushiriki katika fasihi simulizi, mtafiti huja karibu zaidi na jamii na hupata habari
za kuaminika moja kwa moja.
(b) Kushiriki ni njia bora ya kukusanya habari kutoka kwa watu ambao hawajui kusoma
na kuandika, ama wale ambao huona vigumu kujieleza moja kwa moja.
(c) Ni rahisi kwa mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera kinachowasilishwa. Mathalan,
anaweza kuuliza kuhusu kipindi ambamo wimbo fulani uliimbwa au hadhira mahususi
ambayo ilitambiwa aina fulani ya ngano.
(d) Mtafiti anaweza kunakili/kunasa anayosikiliza au anayotazama, hivyo kuhifadhi sifa
za kiimbo, toni na ishara.
(e) Mtafiti hupata taathira na hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana
kwa ana na watendaji na hivyo kuelewa zaidi mada ya utafiti.
(f) Mtafiti anaweza kuthibitisha yale aliyokusanya kupitia kwa hojaji na mahojiano kwa
kuyahakiki.
(g) Kushiriki hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii. Ni rahisi kwa mtafiti
kupata majibu ya masuala anayotafiti kwa kushiriki na kutangamana na wanajamii.
Udhaifu wa kushiriki ”)
(a) Mbinu hii huchukua muda mrefu. Kushiriki katika utendaji huchukua muda zaidi
kuliko kuuliza maswali katika mahojiano.
(b) Huenda mtafiti akatekwa na yaliyomo na kusahau kurekodi.
(c) Ugeni wa mtafiti huweza kuleta wasiwasi miongoni mwa washiriki na wakakosa
kutenda kama kawaida.
(d) Uchanganuzi wa data inayokusanywa kwa njia hii ni mgumu na ni rahisi kwa mtafiti
kuacha masuala muhimu.
Hii ni njia ghali ya utafiti kwani inamhitaji mtafiti kusafiri mbali ili kushiriki katika
utendaji. Pia baadhi ya vifaa vya kuhifadhia data yenyewe kama vile kanda za video
huwa ghali au huenda zikakosa nguvu za umeme.
Kurekodi
Mkusanyaji anaweza kusikilizana na wasanii na kuwarekodi katika vinasasauti, kanda
za video, filamu au kuwapiga picha.
Kutazama
Mkusanyaji wa fasihi simulizi anaweza kukusanya data ya fasihi simulizi kwa
kushuhudia kwa macho fasihi fulani ikiendelezwa. Hapo, atashuhudia mwenyewe bila
kushiriki. Baadaye anaweza kuandika ili kuhifadhi. Mbinu hii hutumiwa zaidi katika
utafiti wa kipera cha maigizo.
Umuhimu wa utazamaji
(a) Ni rahisi kwa mtafiti kurekodi kwa vile hashiriki katika utendaji.
(b) Mtafiti hupata habari za kutegemewa zaidi hasa pale anapotumia kinasasauti kurekodi
moja kwa moja.
(c) Mtafiti anaweza kukaa mahali asipoonekana na kushuhudia utendaji halisi. Kwa sababu
washiriki hawajui kuwa wanatazamwa, utendaji wao hautaathiriwa na chochote;
utakuwa wa kawaida. Data ya aina hii inategemeka zaidi.
Udhaifu wa utazamaji
Wanajamii wanaweza kumshuku mtafiti kuwa anawapeleleza na hivyo kusitisha uwasilishaji
wao.
5. Kutumia hojaji
Hojaji ni fomu yenye maswali yaliyochapishwa ili kukusanya habari fulani. Hojaji
huandaliwa na mkusanyaji wa data na kutumwa au kupelekwa kwa mhojiwa au
atakayeijaza. Akikamilisha kuijaza unaituma au kupelekwa tena kwa mhoji. Hojaji ni
za aina mbili:
(a) Hojaji funge
Hii ni aina ya hojaji ambayo inamfunga mhojiwa kwa majibu fulani tu. Kila swali huwa
na orodha ya majibu na mhojiwa huhitajika kuweka alama tu kwa lile analoona kuwa
jibu sahihi.
Sifa za hojaji
(a) Hojaji huwa na maswali ambayo hujibiwa na kundi linalolengwa katika jamii. Mtafiti
anaweza kulenga watambaji ngano au walumbi.
(b) Hojaji inaweza kutumiwa moja kwa moja na mkusanyaji wa fasihi simulizi kwa
anayehojiwa. Katika hali hii, mtafiti humwelekeza mtoaji wa habari kuhusu namna
ya kujibu. j
(c) Hojaji inaweza kutumwa kwa mhojiwa bila kuwepo kwa mtafiti. Mhojiwa hujisomea
na kujijazia hojaji bila mwongozo wa mtafiti. (Aina hii ya hojaji ndiyo iliyozoeleka
zaidi.)
Umuhimu wa hojaji
(a) Hojaji ni njia ya ukusanyaji data iliyo na gharama ya chini zaidi.
(b) Mtafiti anaweza kufikia idadi kubwa ya watoaji habari kwa kipindi kifupi kwa sababu
hojaji nyingi zinaweza kutumwa hata kwa njia ya posta.
(c) Inaweza kutumika katika mahojiano kama mwongozo. Mhoji anaweza kuitumia katika
mahojiano kufidia udhaifu wa mhojiwa.
(d) Humpa mhojiwa muda wa kuwazia maswali na kuyafanyia uchunguzi kabla ya kuyajibu.
(e) Hojaji, kwa kawaida, hazina athari za mtafiti kwa sababu, aghalabu mtafiti hayupo
zinapojazwa. Mhojiwa hujaza habari za kweli bila kushinikizwa kuchukua mtazamo
fulani kutokana na kuwepo kwa mtafiti.
(£) Hojaji inaweza kubadilishwa kulingana na kiwango cha wajazaji au wahojiwa.
Udhaifu wa hojaji
(a) Maswali yenye utata husababisha fasiri mbalimbali ambazo hufanya matokeo
yasitegemeke.
(b) Huenda watu wakakosa kuijaza hojaji kwa kikamilifu kwa sababu mbalimbali kama
vile kuhofia lawama au wakakataa kujaza kabisa.
(c) Hojaji ikiwa ndefu sana huenda baadhi ya watu wakakataa kuijaza.
(d) Hojaji wazi huwa ngumu sana kwa mtafiti kuchanganua data. Uchanganuzi huchukua
muda mrefu.
(e) Huenda wahojiwa wasijaze mambo ya kweli. Si rahisi kwa mtafiti kuthibitisha iwapo
habari zilizojazwa ni za kweli.
(£) Wahojiwa wanaweza kuchelewa kutuma hojaji zao, hasa hojaji zilizotumwa kwa posta.
(g) Baadhi ya wazee, japo wana habari za kutegemewa, hawajui kusoma na kuandika. Kwa
sababu hii, hawawezi kujaza hojaji isipokuwa wanaposaidiwa na watafiti au wasaidizi
wa watafiti.
(h) Kwavile mtafiti hakabiliani na mhojiwa ana kwa ana, hawezi kupata sifa za uwasilishaji
wa vipera vya fasihi simulizi kama vile toni na kidatu.
6. Mahojiano
Katika mahojiano, mkusanyaji wa fasihi simulizi hukabiliana ana kwa ana na watu
anaonuia kupata maarifa kutoka kwao. Mkusanyaji atakuwa ameandaa maswali
atakayouliza katika kikao rasmi. Mkusanyaji pia anaweza kushiriki katika mahojiano
yasiyo rasmi bila kunakili majibu papo hapo. Maelezo yanayotolewa yanaweza
kuhifadhiwa katika kanda ya kunasa sauti. Siku hizi, mahojiano huweza kufanywa
hata kwa simu.
Umuhimu wa mahojiano
(a) Kwa vile mtafiti anatazamana ana kwa ana na mhojiwa, ni rahisi kupata habari za
kina na za kutegemeka.
(b) Mbinu (sifa) za uwasilishaji kama vile toni, ishara za uso na kiimbo hubainika kwa
mtafiti, hivyo kuimarisha uelewa wake.
(c) Mtafiti anaweza kumfafanulia mhojiwa maswali na kumwezesha kupata data ya
kuaminika zaidi.
(d) Kwa vile mtafiti anamhoji mlengwa moja kwa moja, anaweza kurekodi majibu ya
mhojiwa au kuyaandika. Kwa njia hii, yaliyosemwa kuhusu mada husika huhifadhika
na si rahisi kupotea.
(f) Kwa sababu wanatazamana ana kwa ana, mtafiti anaweza kung'amua wakati mhojiwa
anapotoa habari zisizo za kweli na kwa hivyo kuzichuja.
(g) Mtafiti anaweza kupata habari za kibinafsi na data zaidi kwani si rahisi kwa mhojiwa
kukataa kabisa kujibu maswali.
Udhaifu wa mahojiano
(a) Mahojiano yanahitaji stadi za mawasiliano za kiwango cha juu. Ikiwa mtafiti hana
stadi hizi, huenda akaathiri majibu ya wahojiwa kutokana na jinsi anavyoyafinyanga
maswali.
(b) Urasmi unaotokana na vikao vya mahojiano huenda ukatatiza mawasiliano kati ya
mbhoji na mhojiwa.
(c) Ukosefu wa muda wa kutosha wa mahojiano. Mahojiano huchukua muda mrefu na
huenda mtafiti akakosa kupata muda huo.
(d) Mhojiwa huenda asimwamini mtafiti, akahisi kuwa anapelelezwa, na kukataa kutoa
habari.
(e) Kiwango cha elimu cha mtafiti huenda kikawahofisha na kuwatia wahojiwa hisia za
unyonge na kuwafanya kutotoa habari za kutegemewa.
(f) Wahojiwa wengine huenda wakampa mtafiti habari za uongo ili kumfurahisha.
(g) Matatizo ya kutafsiri, ikiwa data imeandikwa kwa lugha tofauti, huenda yakaathiri
mahojiano.
(h) Mahojiano ni njia ghali ya kutafiti kutokana na gharama ya usafiri kwenda nyanjani.
|
|
|
Vifaa vya kukusanya na kuhifadhi fasihi simulizi
Ukusanyaji wa fasihi simulizi huhitaji vifaa vya kuhifadhi ujumbe. Vifaa hivi ni pamoja na:
Umuhimu wa maandishi
(a) Data kama vile hadithi huhifadhiwa kama ilivyotambwa, hivyo si rahisi kusahauliwa.
Mashairi na ngano nyingi zimeandikwa vitabuni.
(b) Huweza kufikia vizazi vingi kwa sababu kuandikwa huifanya fasihi simulizi iweze
kudumu.
(c) Si ghali kama zilivyo baadhi ya mbinu za kuhifadhi kama vile video.
(d) Si rahisi kufisidiwa au kupotea, hasa zikiandikwa katika vitabu. Hadithi, methali na
vitendawili vingi vimehifadhiwa kwa njia hii.
Udhaifu wa maandishi
(a) Kuna baadhi ya mambo kama vile kiimbo, toni, ishara, hisia na mapigo ya muziki
ambayo hayawezi kuandikwa kama yalivyowasilishwa na fanani, na kwa hivyo hupotea.
(b) Aidha, kwa vile maandishi si hai, hayawezi kutenda wala kusema. Ule uhai asilia wa
fasihi simulizi hufifishwa na kupotezwa na maandishi.
(c) Baadhi ya watafiti huenda wakaandika yale ambayo wanahitaji kwa wakati mahususi
na kupuuza mengine. Kwa mfano, ikiwa mada yake ni 'Wahusika katika ngano za
kimapokeo”, huenda akajihusisha na wahusika na kupuuza vipengele vingine kama
vile fanani. Haya huipujua fasihi simulizi.
(d) Kuandika fasihi simulizi huifanya kukosa ile taathira asilia kwani kunaipokonya
hadhira yake ile fursa ya kushirikiana ana kwa ana na fanani. Hivyo, hata mtu akitaka
kuulizia jambo, hana fursa ya kuuliza.
(e) Kuiandika fasihi simulizi huidhibiti na kupunguza hadhira yake na kuathiri vibaya
usambazaji wake. Fasihi inapoandikwa inawafikia tu wale wanaojua kusoma.
(ii) Vinasasauti/tepurekoda
Vinasasauti hupata sauti, toni na mahadhi ya tungo za fasihi simulizi. Vinaweza kutumiwa
katika mahojiano au mtu anaposhiriki au kutazama fasihi simulizi ikiigizwa. Ingawa ni bora
kuliko kalamu na karatasi, vinasasauti vina udhaifu kwa vile haviwezi kurekodi matendo
na miondoko ya wasanii.
Umuhimu wa vinasasauti/tepurekoda
(a) Sauti ya mhojiwa/fanani huweza kuhifadhiwa.
(b) Sifa ya uhai wa fasihi simulizi huhifadhiwa kwani kinasasauti hunasa sifa kama vile
za kidatu, toni na kiimbo cha mtambaji.
(c) Mkusanyaji wa fasihi simulizi anaweza kurudia kusikiliza uwasilishaji au mahojiano
iwapo hakuelewa. Sifa hii haipatikani katika maandishi.
Udhaifu wa vinasasauti/tepurekoda
(a) Kinasasauti huhitaji nguvu za umeme au betri hivyo basi, hakiwezi kutumiwa katika
sehemu zisizo na huduma hizi. Aidha, nguvu za umeme zikikosekana kabla ya utafiti
kukamilika utafiti utaathirika. Mtafiti atalazimika kuanza tena utafiti wake.
(b) Kinasasauti hakiwezi kumnasa mtambaji wala uigizaji wake. Watu wanaotumia kazi
iliyorekodiwa basi hukosa ile taathira ambayo inaibuliwa na kukabiliana ana kwa ana
na mtambaji.
(c) Baadhi ya wahojiwa au mafanani huenda wasitambe vyema ikiwa wanajua kuwa
wanarekodiwa. Mtafiti anaweza kukosa kupata data ya kutegemewa kama alivyotarajia
kuipata.
(ili) Kamera
Tofauti na vinasasauti, kamera inaweza kuchukua picha ambazo zinaonyesha kipengele
kimoja tu bila kuonyesha misogeo au miondoko wala sauti. Hata hivyo, kamera zinaweza
kuonyesha maleba.
(iv) Video
Video zinaweza kuchukua picha na pia kunasa sauti na miondoko. Ni njia nzuri ya kukusanya
fasihi simulizi isipokuwa ni ghali.
(a) Filamu na video hunasa picha na sauti, hivyo kuhifadhi uigizaji, ishara na kiimbo.
(b) Uhalisi wa mandhari ambamo kazi ya kifasihi inajikita huonekana na watumizi wa
kazi iliyohifadhiwa kwa filamu au video.
(c) Huipa kazi ya fasihi simulizi uhai na taathira zaidi kuliko kazi zilizohifadhiwa kwa
maandishi, kamera na kinasasauti.
Cs)
Udhaifu wa filamu na video
(a) Hii ni njia ghali ya kuhifadhi data.
(b) Data iliyohifadhiwa katika vifaa vyororo vya kompyuta na hata vinasasauti huweza
kufisidiwa, hivyo kutofaidi waliolengwa.
(3)
(f) Vizingiti vya kidini. Hivi hutokea pale ambapo baadhi ya wahojiwa wanaamini kwamba
matendo ya fasihi simulizi kama vile matambiko na uimbaji wa taarabu, yanaenda
kinyume na imani yao ya kidini, na hivyo kukataa kuhojiwa.
(8) Kupotea au kufisidiwa kwa vifaa vya kuhifadhia data. Vifaa kama vile vinasasauti,
video na santuri za kompyuta huweza kupotea au kuharibika kutokana na hali mbaya
ya anga. Yote yaliyokuwa yamehifadhiwa vilevile yatapotea.
(h) Uchache wa wazee au wataalamu wa fasihi simulizi. Fasihi simulizi ilikuwa maarufu
sana miongoni mwa wazee na pengine watu wa umri wa makamo. Kukosekana kwa
wazee wanaoweza kutamba ngano ama kueleza vipera vingine kama vile vitendawili
hutatiza mkusanyaji wa fasihi simulizi, na kwa hivyo huenda data ya kutegemewa
isipatikane.
(i) Vikwazo kutoka kwa watawala. Watawala huenda wakakataa kutoa idhini ya kufanya
utafiti. Baadhi ya taasisi fadhili pia huenda zikakataa kudhamini utafiti katika fasihi
simulizi.
G) Wadhamini mara nyingi ndio huamua mambo yanayochunguzwa, mahali pa
kuchunguziwa na mawanda au upeo wa uchunguzi wenyewe. Aidha, fasiri ya ufafanuzi
wa data mara nyingi lazima ilingane na maslahi ya wadhamini. Ikiwa mtafiti atatoa
fasiri isiyowiana na mapendeleo ya wadhamini, huenda mapendekezo yake yakafutiliwa
mbali na pengine udhamini wa utafiti zaidi kusitishwa. Aidha, matokeo ya utafiti mara
nyingi huwa mali ya mdhamini ambaye huweza kuyatumia kuikandamiza jamii ya
mtafiti.
(k) Mtafiti huenda asiwe na wakati wa kutosha kuwahoji watu wengi. Muda ukikosekana
hatapata habari za kutosha kuhusiana na mada yake.
(Ii) Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi. Ikiwa mkusanyaji analazimika kwenda mbali
kukusanya habari, hasa katika sehemu kame, itakuwa vigumu kufika huko kwa sababu
ya ukosefu wa vyombo vya usafiri kama vile magari.
(m) Matatizo ya kibinafsi. Anayekusanya fasihi simulizi anaweza kushindwa kuidhibiti
hadhira. Badala ya kuwauliza maswali, wahojiwa wanaweza kuwa ndio wanaomuuliza
mtafiti maswali. Kutojua lugha ya wahojiwa au kukosa mlahaka mwema na wahojiwa
kunaweza kuathiri ukusanyaji wa kazi za fasihi simulizi.
(mn) Ukosefu wa usalama. Huenda mkusanyaji wa fasihi simulizi akavamiwa. Aidha, baadhi
ya watu si karimu na huenda wakamshuku mtafiti na kumvamia.
(o) Tafsiri za data pia ni tatizo jingine. Fasihi simulizi huendelezwa kwa lugha za kijamii.
Kupata msamiati unaofaa kufasiri lugha changizi/chanzi hadi lugha pokezi ni tatizo.
Changamoto zinazoukabili ukusanyaji na uhifadhi wa
fasihi simulizi
Pamoja na matatizo yanayomkabili mkusanyaji moja kwa moja, kuna vikwazo ambavyo
vinakabili ukuaji wa fasihi simulizi:
(a) Ukosefu wa utafiti wa kutosha. Ingawa mengi yameandikwa kuhusu fasihi simulizi,
kuna vipera ambavyo bado havijaandikiwa sana.
(b) Uchache wa wataalamu wa kuitafitia na kuiendeleza. Wasomi wengi hupuuza utafiti wa
fasihi simulizi. Utafiti mwingi kuhusu fasihi umefanywa katika tanzu za fasihi andishi,
hususan riwaya, tamthilia, ushairi na hadithi fupi, lakini fasihi simulizi haijatafitiwa
vya kutosha.
Ukuaji wa kazi za kimaandishi. Kwa mfano, ngano nyingi za kimapokeo zimeandikwa,
hivyo hakuna haja ya utambaji; mtu anaweza kujisomea. Hili limefanya stadi ya
utambaji kufifia.
(d) Maendeleo ya kiteknolojia na kisayansi. Fasihi simulizi ilikuwa nyenzo ya kuburudisha
baada ya kazi, lakini kwa sasa teknolojia inatoa njia za kisasa za kujiburudisha kama
vile vipindi katika runinga.
(e) Kuhamia mijini kwa wanajamii wengi na kutangamana na watu wa jamii tofauti
kumefanya uhifadhi wa tamaduni za jamii na urithishaji wake kutowezekana.
(f) Mtaala wa elimu kupuuza lugha za kiasili ambazo ndizo zinazohifadhi na kurithisha
fasihi simulizi ya jamii mbalimbali. Kutofunzwa kwa lugha hizi katika madarasa ya juu
kwa jumla kunatinga ukuaji wa fasihi iliyosimuliwa au kuandikwa kwa lugha za kiasili.
(28). Kuna baadhi ya watu ambao wanaihusisha fasihi simulizi na ukale, hivyo kutoona
haja ya kuitafitia wala kuirithisha vizazi vya sasa.
(h) Fasihi simulizi ilihifadhiwa akilini. Kwa sababu hii, anayeihifadhi anaweza kuibadilisha,
anaweza kufa na kutoweka nayo au akili yake inaweza kufifia na kubetua kiini cha
simulizi hiyo.
(a) Tamasha za muziki. Wanafunzi hukariri, hughani na kuimba mashairi katika tamasha
za muziki.
(b) Sherehe za harusi, jando, mazishi na matambiko ambayo ni mifano ya miviga bado
zipo. Vipera vya mazungumzo kama vile mawaidha huendelezwa kupitia kwa sherehe
hizi.
(c) Utegaji na uteguaji vitendawili kupitia redio na runinga.
(d) Michezo ya kuigiza katika runinga, redio.
(e) Tamasha za drama huendeleza utanzu wa maigizo, mazungumzo na ushairi simulizi.
If
1
SU Si
ya Ka
S ”
Soga
9
yA , alumb, a
ano Yi t:
WA, Ja
ai
YA
yA Visakale E £
KA 9
ya AS IIS >
Z|SAA ZUIA
Ngano za usuli Ya ka 5 ?
afumbo |
5 i-
Ai
Zao
” AA AB / N ahau
- ZI
AI y SI S 13 4S7,
$/ fil No S
s > (ai
9 jv
$
S fe) 3 zA
|
di simulizi ALI
Na ya zani
NA N YA > 09 3
io
VAI
Nyimbo
>
wa
z
>$
> KA 3 YA GY
icheks Sho
ana fsi o. YA
E wa Aa Yap
LI “5 — 0
3 ua) Pembezi a. z S Ss AA Jah.
5 o 8 Yi
WALA Ja (50 3 6. WA
fa
$ YA < Z .
“ za
ka >
Mazoezi ya Marudio
1. Tofauti kuu kati ya tanzu na vipera vya fasihi simulizi ni ya kifani.” Thibitisha.
2. (a) “Fasihi simulizi ni utanzu ambao hauna budi kubadilika.” Jadili.
(b) Andika sifa sita zinazoipambanua fasihi simulizi.
3. “Kuna mfanano mkubwa kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi.” Thibitisha.
4. (a) Fafanua maana ya hadithi.
(b) Eleza umuhimu wa aina zifuatazo za ngano katika jamii yako:
(i) Ngano za mtanziko (ii) Ngano za usuli (iii) Ngano za kiayari.
(c) Ngano zilitambwa usiku kwa sababu gani?
5. Taja aina za wahusika katika hadithi za kimapokeo.
6. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:
Hapo zamani za kale paliishi mzee aliyekuwa tajiri sana. Kwa jina alijulikana kama
Mzee Mali. Mzee Mali alikuwa na mashamba si haba. Fauka ya hayo, alikuwa mfugaji
mashuhuri. Alikuwa na mifugo wengi. Wengi mno wajukuu wake; wengi kama nyota
angani.
Mzee Mali hakuwa tajiri wa mali tu; alikuwa na moyo uliosheheni imani na
ukarimu. Alikuwa na mkono wazi kwa wanakijiji wote. Hata hivyo, maisha ya mzee huyu
kiburi na inda. Mama huyu kwa jina Husuda, alimiliki hiana iliyomfanya hata kuwahini
watoto wake mwenyewe mahitaji ya kimsingi.
Siku moja, kifunguamimba wa Mzee Mali alikwenda malishoni. Akiwa huko,
macho yake yalitua juu ya unyoya mmoja mweupe pepepe mfano wa theluji. Kijana
alivutiwa na weupe wa unyoya huo na akataka kuuchukua. Lakini, akienda kuuchukua,
unyoya ulimhepa na kuelekea kulia.
Kijana aliufuata unyoya, akaufuata, akaufuata. Hatimaye, unyoya ulifika katikati
ya msitu na kujikita ardhini. Kando ya unyoya huo, palisimama yai kubwa la mbuni. Yai
lilisafisha koo kwa kikohozi kama cha mtu aliye na homa ya mkunguru, likamwambia,
“Rafiki yangu, msituni humu mnatisha, tafadhali nichukue, nipeleke nyumbani
kwenu uniepushie hatari inayonikodolea macho.” Kijana aliposikia yai likinena,
kijasho chembamba kilimtiririka tiriri na moyo kumdunda ndundundu. Kwa hakika,
aliweza kusikia mpigo wa moyo wenyewe masikioni. Mandhari hayo yalimpa mwemeo
mkubwa. Hebu jifikirie ukiwa katikati ya msitu mkubwa, mfano wa Msitu wa Kauleni
ulio karibu na Mto Ngamiza; miti mingi mikubwa zaidi ya mivule imekuzunguka, kisha
yai likuzungumzie na kukurai ulipeleke nyumbani! Mjukuu wangu utafanyaje?
Fikira za kila aina zilifurika akilini mwa kijana huyo. Moyo ulimwambia,
“Ukithubutu kuchukua yai hili utajichongea kwa mama yako. Kumbuka jinsi alivyo katili
na mchoyo.” Fikira nyingine ikamwambia, “Usiache uovu wa mama yako kuubadhiri
wema wako. Lichukue yai hili; liokoe.” Fikira hizi ziliendelea kupigania nafasi akilini
mwake na kuupa moyo wake ulemavu wa muda. Hatimaye alikata kauli kulibeba yai hilo
alakulihali. Alilitwaa na kulipakata mikononi kama kitoto kidogo akaelekea nyumbani.
Kijana alipofika nyumbani alimkuta mama ameketi nje. Mara tu alipoliona
yai hilo, alifoka, “Umeokota wapi yai wee?” Kijana alijaribu kumweleza mamake
alivyolifikia yai hilo, lakini kumbe alikuwa kayasukumia maelezo ndani ya masikio ya
kiziwi! Alijaribu, akajaribu kumsihi mama yake amkubalie aliweke yai lake ndani ya
nyumba, lakini wapi! Hatimaye alichoka na kubaki kumkodolea macho tu. Mama mtu
alimwamuru kulitupa yai hilo katika kichaka kilichokuwa karibu na nyumbani kwao.
Laiti angalijua! Mama alifurahi kwamba mwanawe kalitupa yai na kumwonya dhidi
ya vitendo vya kitoto. “Wewe unajua hata kizimba cha kuku hakiwatoshi kuku wetu,
waniletea yai liso faida niliweke wapi?” Kijana alinyamaza tu.
Usiku ulipofika familia ya Mzee Mali haikulala. Pepo za chamchela zilitisha
kung'oa mapaa ya nyumba. Majinamizi yalimwandama mama mtu. Lile yai lilimjia
na kumsuta kwa kuliita yai la kuokotwa. Hata kulipopambazuka, ulimwengu mzima
ulishuhudia mabadiliko makubwa katika familia ya Mzee Mali. Mifugo wote walikuwa
wamelala chini - mizoga. Mimea yake yote ilikuwa imekauka japo mimea katika
mashamba jirani ilitwaa rangi ya kijani kibichi. Mke wake naye alikuwa ameambulia
ugonjwa wa ngozi na kifafa.
Mzee Mali alijikongoja kutoka ndani ya kibanda chake, ambacho usiku wa
kuamkia mkesha wake kilikuwa kasri. Alimwita kitindamimba wake kwa mashauriano.
Kijana alimweleza kadhia ya lile yai. Baada ya kutia na kutoa, Mzee aliamua kwenda
kulisihi yai lirudi. Alishika kiguu na njia hadi alipoelekezwa na mwanawe.
Lile yai lilikuwa pale alipoelezwa. Alipoliona, alijaribu kulitwaa. Yai lilipoona
linachukuliwa, lilichupa na kukimbia kwa kasi ya umeme huku nyuma likiacha Mzee
Mali kaduwaa. Mzee alijuta kwa kutomkanya mkewe dhidi ya uchoyo wake.
Hata hivyo, wajukuu zangu, Waswahili husema, “Maji yakimwagika hayazoleki.'
Mzee Mali alikuwa amechelewa. Alibaki kutazama kivumbi kilichotifuliwa na yai lile
huku akiimba wimbo kulisihi:
Mzee aliendelea kunasihi kwa wimbo ule ule, akaimba, akaimba, akaimba mpaka
koo likakauka. Kila mara alijibiwa kwa wimbo ule ule. Baadaye wazo lilimjia mzee huyu
kumtuma kifunguamimba msituni. Kifunguamimba alienda pale pale na kulipata yai
lake. Aliliangukia miguuni kwa wimbo:
Maswali
(a) Eleza funzo linalotokana na ngano hii.
(b) Eleza sifa za ngano zinazojitokeza katika utungo huu.
(c) Taja wahusika katika ngano hii.
(d) Andika mbinu nyingine za kifasihi zilizotumiwa katika ngano hii.
Siwe ulopita
Matusi ukitema
Chumvi na sukari kuturushia ja samadi?
Uhitaji wetu ukatutuma
Kuokota vihela uloturushia
Ukatununua, kura ukapata?
Sasa miaka mitano imetimia
Waja tulaghai tena
Mainga wa Ndumi huna lolote safari hii
Ubunge umekudondoka ukitazama
Wanyonge tumeamua
Kwingine kujaribu
Maswali
(a) Huu ni wimbo wa aina gani? Kwa nini?
(b) Andika mbinu za lugha zilizotumiwa katika utungo huu.
(c) Ni nani anayezungumza (nafsineni) katika utungo huu?
(d) Fafanua toni ya utungo huu.
(e) Fafanua umuhimu wa nyimbo za aina hii.
'Nilipokukopoa,
Cheko la mwivu wangu lilipaa sana
Ukewenza ukamshawishi kuchukua buruji kueneza habari.
“Njooni mwone jana la ajabu”.
“Hajawahi kuonekana kama huyu
tangu kuumbwa kwa ulimwengu”
Ndivyo walisema walokubeza
Kijiji kizima kilimiminika mwangu nyumbani
Kuyatuma maozi kukutazama weye
Uso na thamani walikwona,
Wakaupa unyonge moyo wangu toto,
Wakanituma kuola viungo vyako
Wakanitanabahisha upungufu ulokulemaza!
Chozi chungu likapukutika
Likalovya changu kidari
Likanavya chako kipaji
Tabasamu ukatoa kunihakikishia
“Mimi si mjalana!
Katu sivyo wasemavyo walimwengu!”
Neno lako hili likanipa tulivu
Nikaamua alakulihali kupambana na yangu jumuiya
Ilosema kwa moja kauli utokomezwe, chakani utupwe.
Tazameni mahasidi mloteka
Teko la dharau mlonimwaiya
Mkanitia ukiwa usomithilika!
Oleni! Tungeni macho!
Mwana mlioambaa ja ukoma
Mlomwinga ja nyuni wala mtama, tazameni
Mekuwa malaika, anowaauni
Kiguru mlomtajia hakimzuwii kufuma mishale!
Maadui wamwonapo hutetema kama jani
Maswali
£ Hapo zamani za kale katika kitongoji cha Shwari, paliishi Sungura na Fisi. Sungura
na Fisi walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walizama na kuibuka pamoja katika
bahari mbalimbali za maisha. Marafiki hawa walizilea aila zao pamoja. Walifanya
kazi kwa ujima mashambani na kushiriki vunoni pamoja. Mvua nayo ilinyesha
msimu baada ya mwingine. Makonde yao yakanawiri na maghala yao yakaanza
kulalamikia shibe. Pia walichunga mifugo wao pamoja.
Watoto wa Sungura na Fisi walicheza pamoja bila kujali tofauti zao za kimaumbile.
Waliamka alfajiri na mapema kwenda kuchunga mifugo wa wazazi wao. Kadiri siku
zilivyosonga, ndivyo gundi iliyougandisha udugu kati ya familia hizi ilivyoendelea
kunata. |
Hata hivyo, siku za neema zilipisha shari. Mvua ilikataa katakata kukitembelea
Maswali
(a) Andika sifa tano za ngano zinazojitokeza katika hadithi hii.
(b) Hii ni ngano ya aina gani?
(c) Andika maadili yanayojitokeza katika ngano hii.
(d) Jadili mbinu za kifasihi zilizotumiwa katika ngano hii.
33. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata:
Zimepita siku ayami
Siku chungu tangu giza lipotanda
Wakati lipotazama kwa kiwewe na shauku
Pumzizo kipania, roho kupigania
Ziraili alipokakamaa aushiyo kufakamia.
Maswali
Oo
11
Simuliz
aa | ” gi - ” UA IA
kwa shule
za Upili
OKFORD
. i
UNIVERSITY PRESS ;
www.onford.co.ke 73654