Kiswahili STD 4 - Kiongozi Cha Mwalimu

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 144

Kiswahili

Kiongozi cha Mwalimu

Darasa la Nne

Taasisi ya Elimu Tanzania

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 1 7/23/21 2:55 PM


© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2018

Toleo la Kwanza 2018


Chapa ya Pili 2021

ISBN: 978-9976-61-735-1

Taasisi ya Elimu Tanzania


S.L.P 35094
Dar es Salaam - Tanzania

Simu: +255 735 041 170 /+255 735 041 168


Baruapepe: director.general@tie.go.tz
Tovuti: www.tie.go.tz

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha,


wala kutafsiri kitabu hiki kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi
ya Taasisi ya ElimuTanzania.

ii

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 2 7/23/21 2:55 PM


Yaliyomo
Ukurasa
Utangulizi......................................................................................... v
Shukurani......................................................................................... xii
Sura ya Kwanza
Kutaja neno moja linalobeba maana ya jumla................................... 1
Sura ya Pili
Vitendawili, nahau, na methali........................................................ 8
Sura ya Tatu
Kutambua rangi za vitu..................................................................... 15
Sura ya Nne
Kueleza matukio................................................................................ 22
Sura ya Tano
Mavazi yetu....................................................................................... 30
Sura ya Sita
Vinywaji vyetu.................................................................................. 37
Sura ya Saba
Mimea yetu........................................................................................ 43
Sura ya Nane
Zahanati yetu .................................................................................... 49
Sura ya Tisa
Kazi zinazofanyika kila siku ............................................................. 55
Sura ya Kumi
Kutumia alama za uandishi ............................................................... 62
Sura ya Kumi na Moja
Kuandika hadithi .............................................................................. 69

iii

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 3 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Mbili
Mahali tulipo ....................................................................................76
Sura ya Kumi na Tatu
Dawa za kulevya ..............................................................................81
Sura ya Kumi na Nne
Kuchemsha chai ...................................................................88
Sura ya Kumi na Tano
Kuandika barua .............................................................................94
Sura ya Kumi na Sita
Kuandika hadithi fupi kwa kutumia majina ya ndege ....................99
Sura ya Kumi na Saba
Kujifunza mashairi .....................................................................105
Sura ya Kumi na Nane
Haki ya elimu kwa mtoto ...............................................................111
Sura ya Kumi na Tisa
Kufuata maelekezo ya uelekeo wa pande kuu nne za dunia ......... 118
Sura ya Ishirini
Kusoma ngonjera kwa sauti ......................................................124

iv

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 4 7/23/21 2:55 PM


Utangulizi
Kitabu hiki cha kiongozi cha mwalimu cha Kiswahili Darasa la Nne
ni mwendelezo wa kiongozi cha mwalimu cha somo la Kiswahili
Darasa la Tatu. Lengo kuu la kiongozi hiki ni kumpa mwalimu mbinu
na maarifa ya kufundisha somo la Kiswahili katika Darasa la Nne.
Katika kiwango hiki mwanafunzi anatakiwa aweze kumudu vizuri
stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika Kiswahili katika
miktadha mbalimbali.
Lugha iliyotumika ikiwemo msamiati, miundo, mazoezi ya lugha,
methali, nahau na vitendawili ni ya kiwango cha juu kuliko ya Darasa
la Tatu. Mbinu mbalimbali za ufundishaji zimependekezwa. Una uhuru
wa kubuni mbinu nyingine kulingana na mazingira, hali ya mahali, idadi
na uwezo wa wanafunzi wako ili kuleta ufanisi katika ujifunzaji. Katika
mchakato wote wa ufundishaji na ujifunzaji washirikishe wanafunzi
katika mazungumzo, kuimba, kuchora, kuigiza, kutamba na kughani.
Vifuatavyo ni vipengele muhimu ambavyo vitakusaidia kufundisha
stadi za lugha katika Darasa la Nne:

1. Msamiati
Ni jambo muhimu kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanafahamu maneno
yote mapya na kuyatumia katika sentensi. Msamiati ufundishwe kwa
kutumia vitu halisi, picha na vielelezo, maelezo, vitendo, maigizo na
onesho. Kwa hiyo, huna budi kutayarisha zana za kutosha za kufundishia
hasa zinazopatikana katika mazingira yako. Vidokezo vifuatavyo ni
muhimu:
(a) Kutumia vitu halisi
Ni muhimu utumie vitu halisi katika kufundisha msamiati kwa
kuwa wanafunzi wanapoona wanaelewa kwa urahisi.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 5 7/23/21 2:55 PM


(b) Kutumia picha na vielelezo mbalimbali
Iwapo utashindwa kupata vitu halisi, tumia picha na vielelezo.
Picha na vielelezo vitayarishwe mapema na viwe vikubwa
vya kutosha ili viweze kuonekana kwa urahisi kwa wanafunzi
wote. Viwe na mvuto na uhalisia ili kueleza dhana kwa usahihi.
Zingatia wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Mfano, tumia
picha na vielelezo mguso.
(c) Kutumia vitendo
Inafaa maneno mengine hasa vitenzi na vivumishi yafundishwe
kwa vitendo. Kwa mfano, chagua mwanafunzi na kumpa kifutio
na kumuelekeza aende kufuta ubao. Mwanafunzi atafanya
kama alivyoelekezwa. Uliza swali. _______ (Taja jina la
mwanafunzi) alikuwa anafanya nini? Pokea majibu na kisha
eleza kuwa ulikuwa unafundisha neno “futa”.

2. Miundo
Muundo ni mpangilio wa maneno na uhusiano wake katika sentensi.
Katika muundo mmoja inawezekana kutunga sentensi kadhaa zenye
maana tofauti.
Katika kitabu cha mwanafunzi alama za “____” na “……..” zinatumika
kuonesha miundo. Alama ya “____” huonesha kuwa neno halijakamilika.
Alama ya “……” huonesha kuwa neno au maneno hayapo. Katika
miundo nafasi hizo zinatakiwa zijazwe. Nafasi ya “____” itajazwa na
sehemu ya neno na “……..” itajazwa kwa neno au maneno. Waongoze
wanafunzi kujaza nafasi hizo. Kwa mfano:
(a) Muundo
ana____ inaweza kujazwa na kuwa: analima, anasoma,
anaimba, anatembea na kuendelea.

vi

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 6 7/23/21 2:55 PM


(b) Muundo
…..ata__ inaweza kujazwa ikawa Bibi atakuja.
Miundo ifundishwe kwa lugha rahisi na inayoeleweka. Irudiwe rudiwe
ili wanafunzi waizoee na kujenga kumbukumbu. Sentensi zinazotungwa
kusisitiza miundo lazima zilingane na mazingira na maisha ya wanafunzi
ili waweze kuzitumia katika maisha yao ya kila siku. Tunga mazoezi
ya ziada kutokana na misingi ya sura husika.
3. Methali
Methali zifundishwe kadiri zinavyotokea katika hadithi au zijengewe
maelezo yanayohusiana na mazingira inamotumika. Eleza methali
kwa kutumia masimulizi yanayohusiana na maisha ya kila siku ili
wanafunzi wagundue maana za methali hizo. Methali zinazofanana
au za kinyume na zile zilizomo katika hadithi zinaweza kufundishwa
pia. Ufundishaji wa methali bila kuzihusisha na mazingira ya maisha
haufai. Wanafunzi waelekezwe kutoa mianzo au miisho ya methali zao
na wengine wamalizie. Pia, wanafunzi waongozwe kutumia methali
katika miktadha mbalimbali.
4. Vitendawili
Fundisha vitendawili kwa kuwapa wanafunzi nafasi ya kutega na kutegua
vitendawili vyao. Waelekeze kupeana mji kila wanaposhindwa kupata
jibu sahihi. Uhusiano uliopo kati ya kitendawili na jibu lake ujadiliwe.
Vitendawili pia vinaweza kutumiwa kama chemsha bongo mwanzo
wa somo la Kiswahili. Vitendawili vipya vyenye mantiki vikubaliwe.
Kumbuka kwamba vitendawili hutofautiana kulingana na mazingira.
5. Misemo na nahau
Fundisha misemo na nahau kwa maelezo, picha, matendo, vitu halisi na
majadiliano. Waongoze wanafunzi jinsi ya kutumia misemo na nahau
hizo katika sentensi. Kwa mfano: Maneno yako yalimkata maini.
(Maneno yako yalimuudhi).

vii

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 7 7/23/21 2:55 PM


6. Ufahamu
Lengo la kusoma ni kuelewa kilichoandikwa yaani ufahamu. Ziko njia
mbalimbali za kufundishia kusoma. Unashauriwa kufuata mwongozo
uliotolewa katika kitabu hiki. Hata hivyo uwe tayari kubadili njia
iwapo utapata vikwazo. Kwani ufanisi wa mwanafunzi ndio lengo letu.
Zifuatazo ni njia mbalimbali za kusoma:
(a) Kusoma kimya
Katika somo la kusoma kimya waelekeze wanafunzi kusoma
kimya bila kufungua mdomo. Wanafunzi wasome sura yote
na kujibu maswali ya ufahamu. Licha ya maswali yaliyomo
kitabuni, tunga maswali mengine ya nyongeza kuhusiana
na sura husika.
(b) Kusoma kwa sauti
Lengo la kusoma kwa sauti ni kuwawezesha wanafunzi
kusoma kwa lafudhi sahihi ya Kiswahili kwa kuzingatia:
Sauti ya kutosha, matamshi, shada, kiimbo, matumizi ya
alama za uandishi kwa usahihi na hisia. Katika somo la
kusoma kwa sauti onesha mfano wa usomaji mzuri. Pia, teua
wanafunzi wengi kwa kadiri iwezekanavyo kusoma kwa
sauti. Hii itategemea muda, idadi na kiwango cha usomaji
wa wanafunzi.
(c) Kusoma kwa ziada
Lengo la kusoma kwa ziada ni kumwezesha mwanafunzi
kusoma kwa ufahamu na kwa kasi stahiki na kumwongezea
maarifa. Kusoma kwa ziada pia, humjengea mwanafunzi tabia
ya kupenda kujisomea. Ongoza usomaji huu. Inashauriwa
yafuatayo yazingatiwe:
(i) Waelekeze sura ya kusoma katika kipindi hicho.
(ii) Wanafunzi wasome kimya.

viii

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 8 7/23/21 2:55 PM


(iii) Waulize maswali, wanafunzi wajibu maswali hayo
kwa kusema au kwa kuandika.Waongoze wanafunzi
kutoa muhtasari wa habari waliyosoma.
(iv) Katika baadhi ya vipindi badala ya kujibu maswali
wanafunzi waelekezwe kuchora, kusimulia, kuigiza
au kuimba ili kusisitiza maarifa waliyoyasoma.
(v) Inafaa somo la kusoma kwa ziada lifanyike mara moja
ndani ya wiki mbili.
7. Mazoezi ya lugha
Katika kitabu hiki yamo mazoezi ya lugha mbalimbali kwa kila sura.
Aina hizo hujumuisha mazoezi ya uchaguzi wa jibu sahihi, kujaza nafasi,
kueleza maana za maneno, kuunganisha sehemu mbili za sentensi,
umoja na wingi, kubadili nyakati na kadhalika. Fundisha zoezi moja au
mawili ya lugha kwa kipindi kimoja na kuongeza mazoezi kulingana
na mazingira na uwezo wa wanafunzi.
8. Utungaji
Sehemu kubwa ya mazoezi ya utungaji katika darasa hili ni wa
kuongozwa. Uongozi huo umefanywa kwa:
(a) Kuchagua na kupanga sentensi zilizochanganyika, hasa
zilizotokana na habari iliyosomwa au kuzungumzwa
(b) Kutumia picha: Wanafunzi wanaweza kuchora kama
wataelekezwa na mwalimu kufanya hivyo au kuchorewa
picha zinazohusu habari fulani. Wanafunzi wanatakiwa
kutoa maelezo kuhusu picha moja au zaidi zilizotolewa.
(c) Kukamilisha habari
(d) Kusimulia na kuelezea hadithi au habari mbalimbali.
Wanafunzi wahimizwe kuigiza, kuimba kutenda na
kuitikia.
(e) Kuuliza maswali ambayo majibu yake yataunda hadithi

ix

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 9 7/23/21 2:55 PM


Toa uzito sawa wa mazoezi ya utungaji wa mdomo na wa kuandika.
Hii itawasaidia wanafunzi kukuza uwezo wa kujieleza kwa mdomo na
kwa maandishi.
9. Ushairi
Ushairi ni uwanja mwingine wa fasihi. Katika kiwango hiki wanafunzi
wasome na kuimba mashairi na ngonjera. Pia, watambue vina, mizani,
mishororo na urari katika mashairi.
10. Mwandiko
Kazi ya kufundisha mwandiko iliyoanza Darasa la Kwanza iendelezwe
na kuimarishwa katika darasa hili. Sisitiza uumbaji mzuri wa herufi hati
ya kuunga, ukataji wa maneno kwa kuzingatia silabi na nafasi kati ya
neno na neno. Pia, alama za uandishi zisisitizwe. Sisitiza usahihi wa
mwandiko katika kila somo linalohusisha kuandika.
11. Imla
Ni somo ambalo wanafunzi hupimwa uwezo wa kusikiliza na kuandika
kwa usahihi kile walichosomewa na mwalimu. Wanafunzi wengi
hawawezi kuandika habari vizuri kwa kufuata taratibu na alama za
uandishi. Vilevile, hawawezi kuandika kwa kasi kwa kufuata msomaji
anavyosoma. Fundisha uandishi wa imla kwa kuzingatia kanuni.
12. Matayarisho / maandalizi ya somo
Soma kitabu cha mwanafunzi na kiongozi cha mwalimu kwa makini
na kukielewa kabla ya kufundisha. Hii itakusaidia kuelewa kwa undani
vipengele vyote unavyotakiwa kufundisha.
13. Fikiri
Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyoorodheshwa katika kipengele
cha fikiri katika kila sura kabla ya kusoma. Maswali hayo yatakusaidia
kupata maarifa ya awali aliyonayo mwanafunzi juu ya sura husika.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 10 7/23/21 2:55 PM


14. Mgawanyo wa vipindi
Katika mwaka wa masomo kutakuwa na siku 194 ambazo ni sawa na
wiki 39 za masomo. Makadirio ya muda yamewekwa kwa mfumo wa
vipindi ambapo kila kipindi ni dakika 40. Katika darasa hili kuna vipindi
5 vya Kiswahili kwa wiki. Hata hivyo mapendekezo haya yanaweza
kubadilika kulingana na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
15. Mrejesho kwa wanafunzi
Sahihisha kazi zote za wanafunzi na kuwapa mrejesho. Ni vema
kufanya masahihisho darasani ili kila mwanafunzi atambue kosa lake
na kujisahihisha.

xi

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 11 7/23/21 2:55 PM


Shukurani

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatambua na kuthamini mchango


muhimu wa washiriki waliofanikisha uandishi wa kiongozi hiki cha
mwalimu.

TET inatoa shukurani za dhati kwa mchango uliotolewa na wataalamu


wote walioshiriki kutayarisha kitabu hiki wakiwemo waandishi,
wachapaji, wasanifu, wahariri, wachoraji na wapiga chapa. Pia, inatoa
shukurani kwa wakufunzi wote walioshiriki katika kazi ya uandishi
wa kitabu hiki.

Aidha, Taasisi inatoa shukurani za pekee kwa Wizara ya Elimu, Sayansi


na Teknolojia kwa kusimamia kwa karibu zoezi zima la uandishi na
kugharamia kazi ya kutayarisha na kuchapa kitabu hiki.

Dkt. Aneth A. Komba


Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Elimu Tanzania

xii

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 12 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kwanza
Kutaja neno moja linalobeba maana ya jumla
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kusoma habari kuhusu mahafali ya Darasa la Saba
(b) Kujifunza maneno yenye maana ya jumla
(c) Kujifunza maneno ya kundi moja
(d) Kutunga sentensi kwa kutumia maneno ya kundi moja
(e) Kutumia maneno yenye maana ya jumla katika mazungumzo

Mahitaji vitu halisi, chati ya picha, kadi za maneno, kadi za


sentensi na pichamguso
Muhtasari
Katika sura ya kwanza mwanafunzi atajifunza msamiati kutokana
na habari watakayosoma ya Mahafali ya Darasa la Saba. Vilevile,
watajifunza dhana ya neno moja linalobeba maana ya jumla. Pia,
watajifunza maneno ya kundi moja na kuyatumia katika sentensi.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa kwanza.
(b) Waongoze wanafunzi kujadili picha iliyopo ukurasa wa pili
katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Ongoza majadiliano kuhusu dhana ya mahafali, kisha
wanafunzi waeleze jinsi wanavyosherehekea mahafali katika
shule yao.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 1 7/23/21 2:55 PM


(d) Waongoze wanafunzi kusoma kimya bila kufuatisha kwa
vidole na bila kutoa sauti.
(e) Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:
(i) Mahafali yalifanyika katika shule gani?
(ii) Darasa la Tatu na la Nne walifanya kazi gani?
(iii) Taja rangi za maputo yaliyotumika katika kupamba.
(iv) Taja matunda matatu yaliyoliwa siku ya mahafali.
(f) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma kwa
maneno machache.
(g) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la
ufahamu lililopo kwenye kitabu cha mwanafunzi katika
ukurasa wa 3-4. Kisha sahihisha zoezi lililofanywa na
wanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu somo. Eleza nini unatarajia
kifanyike katika somo hili.
(b) Wakumbushe wanafunzi alama za uandishi kwa kuuliza
maswali.
(c) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, matumizi sahihi ya alama
za uandishi na kusoma kwa hisia.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu.
Hakikisha wanafunzi wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(e) Wakati wanafunzi wanasoma, mwalimu baini dosari
zinazojitokeza na kuzisahihisha.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 2 7/23/21 2:55 PM


(f) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na rekebisha makosa hayo.
(g) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; mshereheshaji, mahafali, alfajiri,
wasili, alasiri, tumbuiza, adhuhuri na hitimu kwa kutumia
mbinu ya maelezo, vitendo, maigizo na nyimbo.
(b) Andika maneno hayo ubaoni kisha wanafunzi wayasome
na kueleza maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waambie wanafunzi watunge sentensi kwa kuandika.
(f) Sahihisha kazi za wanafunzi na kufanya masahihisho
darasani.

Somo la 4 Mazoezi ya lugha


A. Kuandika jedwali kutokana na habari kwa kuonesha muda au tukio
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kueleza tukio lolote wanalolifahamu.
(b) Ongoza wanafunzi kwa kuonesha mfano wa tukio na muda
kutokana na jedwali.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 3 7/23/21 2:55 PM


Mfano
Namba Muda Tukio
i. 12:30 asubuhi Wanafunzi kufanya usafi katika maeneo
ya shule
ii. 3:00 asubuhi Wazazi na wageni waalikwa kuwasili
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa wa 4
katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuandika maneno yanayowakilisha neno la jumla


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja maneno ya jumla
wanayoyafahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kutambua maneno yanayowakilishwa
na neno la jumla.
Mifano
(i) gauni, sketi, shati, suruali, kaptura – nguo
(ii) chiriku, kuku, kasuku, bata – ndege
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa wa 5
kitabu cha mwanafunzi.
Majibu
(ii) bluu, kijani, kijivu, njano, zambarau
(iii) mchicha, nyama, samaki, njegere, maharage
(iv) ng’ombe, mbuzi, pundamilia, twiga, kondoo
(v) juisi, soda, maziwa, maji
(vi) mpira wa pete, mpira wa miguu, rede, riadha
(vii) tikitimaji, chungwa, embe, nanasi
(viii) Morogoro, Ruvuma, Iringa, Arusha
(ix) siafu, mchwa, sisimizi, chawa
(x) ugali, wali, pilau, kande

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 4 7/23/21 2:55 PM


C. Kupigia mstari neno tofauti na neno jingine katika kundi
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano.
Mifano i. kanga, mwewe, kalamu, njiwa.
ii. karoti, hoho, vitunguu, chupa.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C katika ukurasa
wa 5 katika kitabu cha mwanafunzi.
D. Kuunda maneno ya jumla kwa kutumia herufi na namba
zilizomo katika jedwali
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja maneno ya jumla
wanayoyafahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kuunda maneno kutoka kwenye
jedwali. Rejea mfano uliopo katika zoezi la 3 D ukurasa
wa 6 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D, ukurasa wa 6
katika kitabu cha mwanafunzi.
E. Kucheza mchezo
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja michezo mbalimbali
wanayoifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kutoka nje ya darasa ili kucheza
mchezo.
(c) Waongoze wanafunzi kucheza mchezo wa zoezi 3 E(i)
ukurasa wa 7 – 8 katika kitabu cha mwanafunzi.
(d) Waulize swali la 3 E (ii) wanafunzi wanapomaliza kucheza
mchezo huo. Unaweza kuuliza swali hilo ndani ya darasa
au nje ya darasa.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 5 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa wa
8 katika kitabu cha mwanafunzi kwa kusimulia sherehe
waliyowahi kuhudhuria.
(b) Waongoze wanafunzi kuchagua simulizi moja ambayo
itawasaidia wanafunzi katika kujibu maswali kwa kuzingatia
mwongozo uliopo katika zoezi la 4 B ukurasa wa 8 katika
kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kuandika habari waliyoichagua kwa
kuzingatia mwongozo huo.
(d) Sahihisha kazi ya wanafunzi kwa kuzingatia: alama za
uandishi, uumbaji wa herufi, nafasi kati ya neno na
neno na herufi kubwa.

Somo la 6 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kusoma kimya bila kufuatisha kwa
vidole na bila kutoa sauti majigambo kati ya tunda, mti,
mnyama na mdudu.
(b) Waulize wanafunzi maswali ya zoezi la 5 ya ufahamu katika
ukurasa wa 10 katika kitabu cha mwanafunzi kwa mdomo.
(c) Sikiliza na rekebisha majibu ya wanafunzi.

Somo la 7 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Eleza nini unatarajia kifanyike katika somo hili.
(b) Wakumbushe wanafunzi alama za uandishi kwa kuuliza
maswali.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 6 7/23/21 2:55 PM


(c) Chagua wahusika 4 ambao ni tunda, mti, mnyama na mdudu.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
kulingana na uhusika wake.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya majigambo kwa kufuata
uhusika wake.
(f) Ukibaini makosa wakati wa majigambo rekebisha makosa
hayo.
(g) Waongoze wanafunzi wafanye majigambo kwa kubadilishana
kadiri muda unavyoruhusu.

Somo la 8 Zoezi la lugha


Kukanusha sentensi
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano wa kukanusha
sentensi kama ilivyooneshwa katika ukurasa wa 10 zoezi
la 6 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 ukurasa wa 10
katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 9 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja vyombo mbalimbali vya usafiri
na sifa zake kwa mfano; baiskeli, ndege, pikipiki, gari, treni
na meli.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 7 kwa kutoa mfano
ulio katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 10. Unaweza
kuongeza mifano mingine.
(c) Waongoze wanafunzi waandike majigambo kwa kutumia
vyombo viwili vya usafiri.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 7 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Pili

Vitendawili, nahau, na methali

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kutega na kutegua vitendawili
(b) kueleza maana ya nahau
(c) Kukamilisha methali
(d) Kuelezea maana za methali
(e) Kufafanua ujumbe uliomo katika methali
(f) Kueleza umuhimu wa vitendawili, nahau na methali

Mahitaji vitu halisi, chati ya picha, chati za nahau na methali,


pichamguso

Muhtasari
Vitendawili, nahau, na methali zinaonesha lugha ya kisanii katika
Kiswahili. Mwanafunzi atajifunza kutega na kutegua vitendawili,
kueleza maana ya nahau, kukamilisha methali, kueleza maana zake na
kufafanua ujumbe uliomo katika methali. Vilevile, mwanafunzi ataeleza
umuhimu wa vitendawili, nahau, na methali katika matumizi ya lugha
katika kuwasiliana.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 8 7/23/21 2:55 PM


Somo la 1 Kusoma kimya
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 11.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Vitendawili,
nahau, na methali. Tumia picha zilizopo ukurasa wa 12
na 13 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Doto
Mshindi, iliyopo katika ukurasa wa 11 – 14 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waulize wanafunzi maswali ya zoezi la kwanza la ufahamu
yaliyopo ukurasa wa 14.
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Sahihisha zoezi lililofanywa na wanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari itakayosomwa, na
wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu.
Bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 9 7/23/21 2:55 PM


(d) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na zisahihishe.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Vitendawili
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutega na kutegua vitendawili
wanavyovifahamu.
Mfano
Kitendawili – Tega
Kuku wangu ametagia mibani – Nanasi
Endapo mwanafunzi hatatoa jibu sahihi, mtegaji apewe mji.
(b) Waongoze wanafunzi kwa kutumia maelezo, picha na mifano
kutega na kutegua vitendawili.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 A ukurasa wa 14,
kutegua vitendawili kwa kutumia picha.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 B ukurasa wa 15 la
kutegua vitendawili namba 1 – 8. Angalia majibu yafuatayo:
1. kisogo 2. majani ya mti yaliyodondoka 3. bendera 4.
nyoka 5. kivuli 6. njia 7. moshi 8. chupa. (zingatia majibu
kulingana na mazingira wanayoishi wanafunzi).
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 C ukurasa wa 15
kwa kuandika vitendawili vyenye majibu yafuatayo:
mhindi, mwiba, utelezi, konokono na ngoma.

10

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 10 7/23/21 2:55 PM


Somo la 4 Zoezi la Lugha
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu zoezi litakalofanyika.
(b) Toa mifano michache yenye majibu ya KWELI na SI
KWELI.
Mfano
(i) Watoto hutega na kutegua vitendawili. KWELI
(ii) Vitendawili haviburudishi. SI KWELI
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 ukurasa wa 15
kwa kuandika KWELI au SI KWELI.

Somo la 5 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja nahau wanazozifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kubaini nahau kwa kukamilisha
maelezo waliyopewa.
Mfano Kandambili alitoka shamba kulima. Alifika nyumbani
alioga na kubadilisha nguo. Alikwenda kilabuni
kunywa pombe. Kandambili alilewa sana. Akiwa
njiani alianguka kila mara huku akiimba. Kandambili
alifanya nini? Kandambili alivaa miwani.
(c) Waongoze wanafunzi kutumia nahau kukamilisha maelezo
waliyopewa katika zoezi la 4 ukurasa wa 16 katika kitabu
cha mwanafunzi.

11

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 11 7/23/21 2:55 PM


Somo la 6 Methali
A. Kusoma hadithi
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutaja methali wanazozifahamu.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 A ukurasa
wa 16 katika kitabu cha mwanafunzi. Wasome hadithi
kisha waandike methali zilizomo katika hadithi hiyo.
(iii) Waongoze wanafunzi kuandika maana ya methali
walizoziandika.

B. Kujaza nafasi zilizoachwa wazi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu somo utakalofundisha.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 B katika
ukurasa wa 17-18 katika kitabu cha mwanafunzi.
Watumie methali kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika
maelezo waliyopewa 1- 4.

C. Kukamilisha methali
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutaja methali wanazozifahamu
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 C la
kukamilisha methali katika ukurasa wa 18 katika kitabu
cha mwanafunzi.

12

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 12 7/23/21 2:55 PM


D. Kuandika methali
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu somo utakalofundisha.
(ii) Toa mfano uliopo katika kitabu cha mwanafunzi katika
zoezi la 5 D ukurasa wa 18.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 D la kuandika
methali namba 1 - 7 zitakazotumika kuwaonya watu.

Somo la 7 Mazoezi ya lugha


A. Kubadili sentensi kuwa katika wakati ujao
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo mafupi kuhusu wakati ujao kabla ya
kutoa mifano.
(ii) Toa mfano wa kubadili sentensi kuwa katika wakati
ujao.
Mfano Asha alinunua kitabu.
Asha atanunua kitabu.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 A ukurasa wa
18 kitabu cha mwanafunzi la kubadili sentensi kuwa
katika wakati ujao.

B. Kuandika sentensi katika hali timilifu


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano wa kuandika sentensi kuwa katika hali
timilifu.
Mfano Mama anapika chakula.
Mama amepika chakula.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 B ukurasa
wa 19-20 katika kitabu cha mwanafunzi, la kuandika
sentensi katika hali timilifu.

13

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 13 7/23/21 2:55 PM


C. Kuoanisha methali
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu methali zinazooana.
(ii) Toa mfano uliopo zoezi la 6 C ukurasa wa 20 kwenye
kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 C ukurasa wa
20 la kuoanisha methali zinazofanana kutoka sehemu
A na B.
Majibu (i) f (ii) a (iii) b (iv) e (v) d (vi) c

D. Kuandika sentensi katika hali ya ukanushi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano wa kubadili sentensi kuwa katika hali ya
ukanushi.
Mfano Watoto walifurahia michezo.
Watoto hawakufurahia michezo.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 D, ukurasa wa
20 katika kitabu cha mwanafunzi la kuandika sentensi
katika hali ya ukanushi.

14

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 14 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Tatu
Kutambua rangi za vitu

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma habari kuhusu mwaka mpya
(b) Kutambua rangi za vitu
(c) Kutambua shughuli mbalimbali zinazofanyika nyakati
mbalimbali za siku

Mahitaji vitu halisi, chati ya picha, rangi mbalimbali,


mazingira halisi
Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza kutambua rangi mbalimbali za
vitu. Vilevile, watajifunza shughuli mbalimbali zinazofanyika nyakati
za siku.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 21.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Mwaka
mpya. Unaweza kutumia mazingira ya wanafunzi au picha
iliyopo ukurasa wa 22 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Mwaka
mpya iliyopo katika ukurasa wa 21 – 22 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.

15

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 15 7/23/21 2:55 PM


(d) Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:
(i) Mama alivaa sketi ya rangi gani?
(ii) Baraka aliingia darasa la ngapi?
(iii) Nani alipiga pasi nguo za Baraka na kaka yake?
(iv) Baraka na kaka yake walioneshwa nini shuleni?
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
lililopo ukurasa wa 23 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
kuandika.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari itakayosomwa.
(b) Wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi
kwa kuuliza maswali.
(c) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia kanuni ya usomaji.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu,
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(e) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

16

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 16 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; pasi, cherehani, sarakasi, sare,
mgahawa, kwa kutumia mbinu ya maelezo, vitendo na
onesho mbinu.
(b) Andika maneno hayo ubaoni, wanafunzi wayasome na
kueleza maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Watake wanafunzi watunge sentensi kwa kuandika kisha
sahihisha.

Somo la 4 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Rejea utangulizi sehemu ya namna ya kufundisha miundo.
(b) Andika ubaoni miundo unayotaka kufundisha kisha
wanafunzi wasome.
(c) Toa mifano ya sentensi zenye miundo unayofundisha.
Mfano Baba alimwambia mama, hatuna budi
kuwapeleka watoto shuleni.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 la kutunga sentensi
kwa kutumia miundo ukurasa wa 23 katika kitabu cha
mwanafunzi.

17

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 17 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja nahau wanazozifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kutoa maana za nahau na kutunga
sentensi.
Mfano
Nahau - kata tamaa ni kitendo cha kushindwa kuendelea na jambo fulani.
Sentensi - Obedi alikata tamaa baada ya kuachwa na gari la asubuhi.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya nahau kisha watunge
sentensi kwa kila nahau katika zoezi la 4 ukurasa wa 24.

Somo la 6 Mazoezi ya lugha


A. Kuandika wingi wa maneno
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo mafupi kuhusu umoja na wingi.
(ii) Toa mifano kwa kuandika wingi wa maneno.
Mfano Umoja Wingi
Maji Maji
Kitabu Vitabu
Tunda Matunda
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 A ukurasa
wa 24 katika kitabu cha mwanafunzi kwa kuandika
wingi wa maneno.

18

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 18 7/23/21 2:55 PM


B. Kuandika majina ya vitu viwili kwa kila jina la rangi
Hatua za ufundishaji
(i) Ongoza wanafunzi kutaja vitu vyenye rangi
mbalimbali.
(ii) Toa mifano kwa kuandika majina ya vitu viwili kwa
kila jina la rangi.
Mfano Kijani – majani, njegere.
Bluu – anga, bati.
Zingatia mazingira/uhalisia wa rangi ya vitu wanavyovitaja
wanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 B la kuandika
majina ya vitu viwili kwa kila rangi katika ukurasa wa
24 katika kitabu cha mwanafunzi.

C. Kubadili sentensi kuwa katika umoja


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mifano ya kubadili sentensi kuwa katika umoja.
Mfano Mama alinunua vitabu vya hesabu
Mama alinunua kitabu cha hesabu.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 C la kubadili
sentensi kuwa katika umoja, ukurasa wa 25 katika
kitabu cha mwanafunzi.

19

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 19 7/23/21 2:55 PM


D. Kuandika shughuli zinazofanyika katika muda tofauti kwa siku
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kueleza ratiba kuanzia asubuhi
wanapoamka.
(ii) Toa mfano wa shughuli zinazofanyika katika muda
uliooneshwa katika kitabu cha mwanafunzi.
Mfano Asubuhi – kuamka mapema na kujiandaa
kwenda shule.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 D, ukurasa
wa 25 katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuandika sentensi katika hali ya ukanushi


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kueleza ukanushi unavyoonekana
katika kitendo (kitenzi).
(ii) Toa mfano wa kubadili sentensi kuwa katika hali ya
ukanushi.
Mfano Tulifurahia kwenda kuogelea
Hatukufurahia kwenda kuogelea
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 E, ukurasa
wa 25 katika kitabu cha mwanafunzi.

20

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 20 7/23/21 2:55 PM


Somo la 7 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu furaha ya kuingia
mwaka mpya.
(b) Waongoze wanafunzi kuandika habari yenye maneno
yasiyopungua sitini (60), wakieleza jinsi walivyoingia darasa
jipya kwa kuzingatia mwongozo ufuatao:
(i) Mwaka uliopita ulikuwa darasa la ngapi?
(ii) Mwaka huu umeingia darasa la ngapi?
(iii) Mambo gani umefurahia baada ya kuingia darasa
jipya?
(iv) Unatarajia kufanya nini ili kufanikiwa katika masomo
yako?
(c) Sahihisha kazi ya wanafunzi kwa kuzingatia: alama za
uandishi, uumbaji wa herufi, nafasi kati ya neno na
neno na herufi kubwa.

21

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 21 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Nne

Kueleza matukio

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma habari kuhusu Mwaka mpya
(b) Kueleza matukio mbalimbali kwa usahihi
(c) Kutumia nyakati mbalimbali kueleza matukio
(d) Kukanusha matukio katika sentensi kwa kutumia wakati
husika

Mahitaji mazingira halisi, picha na pichamguso

Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi wataweza kuelezea na kutumia nyakati
mbalimbali kueleza na kukanusha matukio katika sentensi kwa kutumia
wakati husika.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 26.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Kueleza
matukio, kutumia picha iliyopo ukurasa wa 26 katika kitabu
cha mwanafunzi.
(c) Waelekeze wanafunzi kusoma kimya habari kuhusu Kueleza

22

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 22 7/23/21 2:55 PM


matukio iliyopo katika ukurasa wa 26 – 28 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waulize wanafunzi swali 1-5 kutoka katika zoezi la kwanza
ukurasa wa 28, kitabu cha wanafunzi kisha wajibu kwa
kuongea.
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
lililopo ukurasa wa 28 kuanzia swali 6 – 9 kwa kuandika.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Tumia picha iliyopo ukurasa wa 26 kuwataka wanafunzi
waeleze kile wanachokiona kwenye picha hiyo.
(b) Wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi
kwa kuuliza maswali.
(c) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kufuata kanuni za usomaji.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(e) Wakati wanafunzi wanasoma, baini makosa yanayojitokeza
na kuyasahihisha.
(f) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(g) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

23

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 23 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; masika, mkaidi, elea, adha,
ng’ambo, bondeni, kujitosa, kwa kutumia mbinu ya maelezo,
vitendo na oneshombinu.
(b) Andika maneno hayo ubaoni, wanafunzi wayasome na
kueleza maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi,
Kisha waambie wanafunzi watunge sentensi nyingine
kwa kuandika. Sahihisha kazi za wanafunzi na kufanya
masahihisho darasani.

Somo la 4 Mazoezi ya lugha


A. Kusimulia na kuigiza tukio
(i) Kusimulia tukio
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu mambo ya kuzingatia katika masimulizi.
(b) Toa mfano kwa kusimulia tukio kwa ufupi kutokana na
habari iliyosomwa kwa maneno yako mwenyewe.
(c) Waongoze wanafunzi kusimulia tukio walilosoma kwa
maneno yao wenyewe bila kupotosha wazo kuu.
(d) Wasahihishe wanafunzi pale ambapo unaona wanakosea.

24

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 24 7/23/21 2:55 PM


(ii) kuigiza tukio
Hatua za ufundishaji
(a) Chagua wanafunzi wawili wawili ili waweze kuigiza
mazungumzo kati ya mwalimu Sara na mwalimu Mbilo.
(b) Waongoze wanafunzi wawili wawili waigize mazungumzo
hayo huku ukiwasikiliza na kuwarekebisha kama watakosea.
(c) Wape wanafunzi nafasi ya kuigiza kadiri utakavyoona muda
unaruhusu.
B. Kuandika maana ya maneno ya kifungu A kwa kuchagua
jibu sahihi kutoka kifungu B
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo namna ya kutumia maneno kutoka kifungu
B ili kukamilisha maana ya maneno ya kifungu A.
(ii) Toa mfano wa neno kutoka kifungu A kwa kuchagua
jibu sahihi kutoka kifungu B.
Mfano i. Adha (c) jambo linalosumbua au kuleta shida.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B, katika
ukurasa wa 29 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu i. (c), ii. (e), iii. (h), iv. (b), v. (a),
vi. (i), vii. (d), viii. (g)

C. Kupanga sentensi kwa mfuatano sahihi wa matukio


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusimulia matukio
wanayoyafahamu.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C, ukurasa wa
30 katika kitabu cha mwanafunzi na sahihisha kazi zao.
Majibu 1. (4) 2. (2) 3. (1) 4. (3) 5. (6) 6. (5)

25

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 25 7/23/21 2:55 PM


D. Kuandika kinyume cha maneno
Hatua za ufundishaji
(i) Waambie wanafunzi wataje maneno matano (5) na
kinyume chake.
(ii) Toa mifano ya kinyume cha maneno.
Mfano Achia - shika
Bondeni - mlimani
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D, ukurasa
wa 30 katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuandika sentensi kwa usahihi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu upatanisho wa kisarufi.
(ii) Toa mfano wa kuandika sentensi kwa usahihi.
Mfano Ndekia walikuwa mkaidi.
Ndekia alikuwa mkaidi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E, katika
ukurasa wa 30 katika kitabu cha mwanafunzi.

F. Kuandika sentensi katika hali timilifu


Hatua za ufundishaji
(i) Watake wanafunzi kufanya matendo mbalimbali
kisha uwaulize ‘umefanya nini’ ? Wanaweza kujibu
yafuatayo; nimesimama, au nimetoka nje, nimeandika.
(ii) Toa mifano ya sentensi timilifu.
Mfano Mvua kubwa inanyesha leo.
Mvua kubwa imenyesha leo.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F, ukurasa
wa 31 katika kitabu cha mwanafunzi.

26

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 26 7/23/21 2:55 PM


G. Kuandika sentensi katika wakati uliopita
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mifano ya sentensi katika wakati uliopita.
Mfano Mwalimu Mbilo amepiga simu shuleni.
Mwalimu Mbilo alipiga simu shuleni.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 G, ukurasa
wa 31 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 5 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(i) Ongoza majadiliano kwa kutumia picha iliyoko ukurasa
wa 33 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya
asiyesikia la mkuu huvunjika guu iliyopo ukurasa wa
32-33 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waelekeze wanafunzi kusoma kimya habari inayohusu
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Iliyopo ukurasa
wa 32-34 katika kitabu cha mwanafunzi bila kufuatisha
kwa kidole na bila kutoa sauti.
(iv) Waulize wanafunzi swali 1-3 kutoka katika zoezi la
nne ukurasa wa 34, kisha wajibu kwa kuongea.
(v) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma
kwa maneno machache na kueleza mafunzo
waliyojifunza.
(vi) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la nne la ufahamu
lililopo ukurasa wa 34 kuanzia swali 4 – 5 kwa
kuandika.

27

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 27 7/23/21 2:55 PM


Somo la 6 Kusoma kwa sauti
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo mafupi kuhusu habari itakayosomwa, na
wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi
kwa kuuliza maswali.
(ii) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri wa
usomaji, kwa kufuata kanuni za usomaji.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa
zamu. Hakikisha wanafunzi wengi wanapata nafasi
ya kusoma.
(iv) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha
usomaji kwa muda na kurekebisha makosa hayo.

Somo la 8 Mazoezi ya Lugha


A. Kuandika wakati uliotumika katika kila sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu viambishi vya wakati
ta, na, li katika kitendo (kitenzi).
(ii) Toa mifano ya kuandika wakati uliotumika katika sentensi.

Mfano
(a) Aliondoka asubuhi na mapema – wakati uliopita
(b) Nitawaeleza wenzangu madhara ya wizi – wakati ujao
(c) Tabia ya wizi inapaswa kukomeshwa – wakati uliopo

(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 A katika


ukurasa wa 35 kitabu cha wanafunzi.

28

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 28 7/23/21 2:55 PM


B. Kukanusha sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mifano ya kukanusha sentensi kwa kuzingatia silabi/
neno “ha” na “si”
Mfano (a) Wanafunzi wanaogopa mitihani
Wanafunzi hawaogopi mitihani.
(b) Tabia ya wizi ni nzuri
Tabia ya wizi si nzuri
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 ukurasa wa 35
katika kitabu cha mwanafunzi unaweza kuongeza
sentensi nyingine.

29

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 29 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Tano

Mavazi yetu

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma habari
(b) Kujifunza aina za mavazi na kueleza mazingira yanakovaliwa
(c) Kujifunza mahali na wakati sahihi wa kuvaa mavazi hayo
(d) Kujua watu wanaostahili kuvaa mavazi hayo

Mahitaji vitu halisi na chati za picha, pichamguso, bangokitita


na kalamu rashasha
Muhtasari
Katika sura hii mwanafunzi atajifunza mavazi mbalimbali na aina za
mavazi kulingana na mazingira mfano; shuleni, kazini na nyumbani.
Pia atajifunza mahali na wakati sahihi wa kuvaa mavazi hayo na watu
wanaostahili kuvaa mavazi hayo.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 36.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya mavazi
yetu. Tumia picha zilizopo ukurasa wa 37 katika kitabu
cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Mavazi
yetu, iliyopo katika ukurasa wa 36 - 38 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.

30

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 30 7/23/21 2:55 PM


(d) Waulize maswali yafuatayo kisha wanafunzi wajibu kwa
kuongea:
(i) Je, Luko alikwenda wapi wakati wa likizo?
(ii) Je, mzozo uliozuka ndani ya basi ulikuwa kati ya
watu gani?
(iii) Nani alivaa gauni lenye maua ya bluu na nyeupe?
(d) Waongoze wanafunzi kueleza habari waliyoisoma kwa
maneno machache.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza ukurasa wa
39 kuanzia swali 4 -8 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo mafupi kuhusu habari itakayosomwa na
wakumbushe wanafunzi kanuni za kusoma kwa sauti.
(ii) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri
wa usomaji, kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili,
matamshi sahihi, kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia
na matumizi sahihi ya alama za uandishi.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa
zamu, bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(iv) Wakati wanafunzi wanasoma, baini makosa
yanayojitokeza na kuyasahihisha. Endapo makosa
yatajirudiarudia simamisha usomaji kwa muda na
kurekebisha makosa hayo.
(v) Wape wanafunzi zaidi nafasi ya kusoma kadiri muda
unavyoruhusu.

31

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 31 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; kanzu, baraghashia, jezi, sare,
teremka, furahi, zozana, mtanashati, sitiri, nong’ona na
magwanda.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(e) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 39
katika kitabu cha wanafunzi.

Somo la 4 Methali
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutaja methali wanazozifahamu.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 ukurasa wa 40
katika kitabu cha mwanafunzi la kukamilisha methali.

Somo la 5 Mazoezi ya Lugha


A. Kuandika kinyume cha sentensi
Hatua za ufundishaji
(a) Waambie wanafunzi wataje maneno na kinyume chake.
Unaweza ukatumia matendo.
(b) Toa mifano kwa kuandika kinyume cha sentensi.

32

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 32 7/23/21 2:55 PM


Mfano
Tausi ni ndege mwenye rangi zisizovutia.
Tausi ni ndege mwenye rangi zinazovutia
Tulisafiri kwa basi kwenda kwa bibi
Hatukusafiri kwa basi kwenda kwa bibi
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa wa
40-41 katika kitabu cha wanafunzi.

B. Kukanusha sentensi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kukanusha sentensi.
Mfano Msichana alivaa sketi ya kubana
Msichana hakuvaa sketi ya kubana.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B ukurasa wa 41
katika kitabu cha mwanafunzi.

C. Kubadili sentensi kuwa katika wakati ujao


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika sentensi katika wakati ujao.
Mfano
Abiria waliwahi kituoni.
Abiria watawahi kituoni.
Mama amevaa mavazi ya heshima.
Mama atavaa mavazi ya heshima.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C ukurasa wa 41
katika kitabu cha mwanafunzi.

33

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 33 7/23/21 2:55 PM


D. Kuoanisha maneno yanayohusiana kutoka kundi A na B
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu mavazi yanayovaliwa na watu
kutegemea shughuli wanazofanya.
(b) Toa mfano ufuatao kabla ya kuwapa wanafunzi zoezi.
Mfano
Kundi A Kundi B
iv. Joho (f) Mhitimu
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 D ukurasa wa 42
katika kitabu cha wanafunzi.
E. Kupanga maneno yaliyopo katika sentensi ili yalete maana
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu kupanga maneno katika sentensi ili
yalete maana.
(b) Tumia mfano uliotolewa katika zoezi la 4 E ukurasa wa 42
kwenye kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E ukurasa wa 42
katika kitabu cha wanafunzi.

F. Kutunga sentensi kutokana na jedwali


Hatua za ufundishaji
(a) Andika jedwali la sentensi ubaoni lililopo zoezi la 4 F ukurasa
wa 42 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Toa mifano kwa kuandika ubaoni sentensi zifuatazo kutokana
na jedwali.
i. Ndani ya gari alikuwemo baba aliyevaa suti.
ii. Walipokuwa barabarani walimwona mvulana aliyevaa jezi.
iii. Walipofika kituo cha basi waliwakuta abiria wengi.

34

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 34 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 F ukurasa wa 42
katika kitabu cha mwanafunzi.

G. Kukamilisha sentensi kwa kutumia maneno yaliyopo


kwenye kisanduku
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo ya namna ya kutumia maneno kutoka kwenye
kisanduku ili kukamilisha sentensi.
(b) Waongoze kusoma maneno yaliyopo katika kisanduku katika
zoezi la 4 G ukurasa wa 43 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Toa mfano uliooneshwa katika kitabu cha mwanafunzi.
Unaweza kuongeza mifano mingine.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 G ukurasa wa 43
katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1. suti 2. mtandio 3. nadhifu 4. abiria 5. alifoka
6. mazingira 7. adui 8. ajira 9. walemavu 10. wakinong’ona

H. Kuandika majina ya mavazi kutokana na herufi zilizomo


katika jedwali
Hatua za ufundishaji
(a) Chora jedwali lililopo zoezi la 4 H, ukurasa wa 43 katika
kitabu cha mwanafunzi ubaoni au kwenye bangokitita.
(b) Toa mifano kama ilivyooneshwa katika kitabu cha
mwanafunzi kwa kuzungushia jibu sahihi. Ongeza mifano
mingine.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 H ukurasa wa 43
katika kitabu cha wanafunzi.

35

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 35 7/23/21 2:55 PM


I. Kutunga sentensi kwa aina ya mavazi yaliyotolewa
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja mavazi waliyovaa.
(b) Toa mfano kwa kutunga sentensi kwa kila aina ya vazi.
Mfano
Soksi: Kila mwanafunzi anatakiwa awe na soksi nyeupe.
Suruali: Baba yake Luko alivaa suruali nyeusi.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 I ukurasa wa 44
katika kitabu cha wanafunzi.

Somo la 6 Vitendawili
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutega na kutegua vitendawili
wanavyovifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa wa 44
kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 7 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kusimulia habari kwa kufuata
mwongozo uliopo zoezi la 6 ukurasa wa 44 katika kitabu
cha mwanafunzi kwa mazungumzo.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 kwa kuandika.
(c) Waongoze wanafunzi kuandika habari hiyo kwa kuzingatia
mwongozo uliyotolewa katika kitabu cha mwanafunzi zoezi
la 6 ukurasa wa 44.
(d) Baada ya kusahihisha chagua habari iliyoandikwa vizuri na
wanafunzi waisome darasani kwa sauti.

36

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 36 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Sita

Vinywaji vyetu

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kueleza maana ya vinywaji
(b) Kutaja majina mbalimbali ya vinywaji
(c) Kuainisha aina za vinywaji mbalimbali wanavyovifahamu
(d) Kutofautisha majina ya vinywaji vyenye kileo na visivyo
na kileo
(e) Kuelezea faida za vinywaji kwa watumiaji kwa kila kinywaji
alichotaja
(f) Kuelezea hasara za vinywaji vyenye madhara
atakavyobainisha
(g) Kutoa kauli mbiu anayofikiri inafaa kwa watumiaji wa
vinywaji vyenye madhara
Mahitaji vitu halisi, picha, bangokitita, kalamu rashasha.

Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza maana ya vinywaji na aina zake,
vinywaji vyenye madhara na visivyo na madhara kupitia habari ya
Vinywaji vyetu. Pia, watajifunza msamiati, nahau, methali, kinyume
cha maneno na utungaji.

37

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 37 7/23/21 2:55 PM


Somo la 1 Kusoma kimya
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 45.
(b) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Vinywaji
vyetu, iliyopo katika ukurasa wa 45 – 48 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(c) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yafuatayo:
(i) Taja majina ya vinywaji ulivyovisoma katika habari.
(ii) Watoto hupendelea vinywaji gani?
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
lililopo ukurasa wa 48 katika madaftari yao.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi kanuni na taratibu sahihi za kusoma
kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji.
Zingatia usomaji wa majibizano kwa kubadili sauti kwa kila
mhusika au kuchagua wanafunzi kusoma kwa kuzingatia
wahusika Bibi Afya, Wananchi, Mama Maua, Daudi, Maseke,
Shauri, Mahanju na Kashamba.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu, bila
kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wote wanapata
nafasi ya kusoma.

38

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 38 7/23/21 2:55 PM


(d) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati: mlevi, starehe, madafu, madhara, athiri,
togwa, wakazi, sharubati, kileo kwa kutumia mbinu ya
maelezo, vitu halisi, picha na maigizo.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni
ukizingatia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 la msamiati ukurasa
wa 48 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 4 Methali na nahau


A. Kuandika neno Methali au Nahau
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano uliopo katika zoezi la 3 A ukurasa wa 49
katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa
wa 49 katika kitabu cha mwanafunzi la kuandika
neno METHALI au NAHAU kuonesha sentensi yenye
methali au nahau.

39

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 39 7/23/21 2:55 PM


B. Kukamilisha methali
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mifano.
Mfano Kidole kimoja…………….
Kidole kimoja hakivunji chawa.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B la
kukamilisha methali katika ukurasa wa 49-50 katika
kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 5 Mazoezi ya lugha


A. Kuandika NDIYO au HAPANA katika sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano ufuatao:
Watoto wanapenda sharubati yenye sukari. NDIYO
Vinywaji vyote vina vileo. HAPANA
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa
wa 50 katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuandika sentensi kwa usahihi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano wa kuandika sentensi zilizokosewa kwa
usahihi.
Mfano Kiti cha mwalimu vimevunjika.
Kiti cha mwalimu kimevunjika.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B ukurasa
wa 50 katika kitabu cha mwanafunzi.

40

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 40 7/23/21 2:55 PM


C. Kuandika kinyume cha maneno
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano wa zoezi la 4 C uliopo kwenye kitabu cha
mwanafunzi ukurasa wa 51.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C ukurasa
wa 51 katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kupigia mstari neno ambalo ni tofauti na mengine


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano kwa kupigia mstari neno ambalo ni tofauti
na mengine.
Mfano gari, gauni, pikipiki, ndege, meli.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 D, katika
ukurasa wa 51 katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuandika vinywaji sita visivyo na kileo kutoka katika jedwali


Hatua za ufundishaji
(i) Nakili ubaoni au kwenye bangokitita jedwali lililopo
katika zoezi la 4 E ukurasa wa 51 katika kitabu cha
mwanafunzi.
(ii) Tumia jedwali hilo kutoa mfano kwa kulizungushia
neno soda kwa kutumia chaki au kalamu rashasha.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E ukurasa
wa 51 katika kitabu cha mwanafunzi,
Majibu maziwa, maji, juisi, togwa, chai, soda.

41

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 41 7/23/21 2:55 PM


F. Kutunga sentensi kwa kutumia jedwali
Hatua za ufundishaji
(i) Nakili jedwali ubaoni au kwenye bangokitita la zoezi la
4 F katika ukurasa wa 51 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Toa mifano miwili kwa kutumia jedwali hilo.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 F, katika
ukurasa wa 51 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 6 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Andika ubaoni mambo ya kuzingatia kama yalivyoandikwa
katika zoezi la 5 ukurasa 52 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Waongoze wanafunzi kujadili mambo hayo yaliyoandikwa
ubaoni na majibu kuyaandika ubaoni.
(c) Waongoze wanafunzi kumalizia habari kwa kuzingatia
mwongozo uliopo katika zoezi la 5 ukurasa wa 52 katika
kitabu cha mwanafunzi.

42

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 42 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Saba

Mimea yetu

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kueleza maana ya mazingira
(b) Kueleza maana ya mimea
(c) Kutaja majina ya mimea katika mazingira yake
(d) Kuainisha aina mbalimbali za mimea anazozifahamu
(e) Kubainisha faida za kila mmea alioutaja

Mahitaji vitu halisi, picha, bangokitita, kalamu rashasha.

Muhtasari
Maudhui ya majigambo ya Mimea yetu yatawafundisha wanafunzi
aina mbalimbali za mimea na faida zake kwa ufasaha. Pia, atajifunza
matumizi mbalimbali ya msamiati, nahau, methali na utungaji.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 53.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Mimea yetu.
Atumie picha zilizopo ukurasa wa 54 na 55 katika kitabu
cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Mimea
yetu, iliyopo katika ukurasa wa 53 – 55 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.

43

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 43 7/23/21 2:55 PM


(d) Waongoze wanafunzi kujibu swali 1-3 katika zoezi la 1 la
ufahamu ukurasa wa 55 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
mdomo.
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya swali la 4-8 katika zoezi
la kwanza la ufahamu, lililopo ukurasa wa 55-56 kwenye
madaftari yao.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi
kwa kuuliza maswali.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi
ya alama za uandishi. Zingatia usomaji wa majigambo
au kuchagua wanafunzi kusoma kwa kuzingatia uhusika.
(Mbuyu, Mkahawa na Mkorosho)
(c) Waongoze wanafunzi kusoma watatu watatu kwa zamu kwa
kuzingatia uhusika. Bila kujali jinsia zao na uwezo wao.
Hakikisha wote wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

44

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 44 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; mbuyu, watalii, mkahawa,
mkorosho na bibo.
(b) Andika maneno hayo ubaoni.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma maneno hayo na kueleza
maana ya neno mojamoja.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(e) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(f) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia
msamiati waliyojifunza katika madaftari yao.

Somo la 4 Kazi ya kufanya (igizo)


Hatua za ufundishaji
(a) Tengeneza makundi matatu kwa kuzingatia uhusika yaani
Mbuyu, Mkahawa na Mkorosho.
(b) Toa maelekezo katika vikundi hivyo, nini cha kufanya.
(c) Wape nafasi vikundi hivyo kujiandaa na kuwasilisha kazi
yao (majigambo).
(d) Fanya hitimisho la igizo kwa kila kundi.

Somo la 5 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano uliopo katika zoezi la 3 katika kitabu cha
mwanafunzi ukurasa wa 56.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 la kutunga sentensi
moja kwa kila nahau.

45

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 45 7/23/21 2:55 PM


Somo la 6 Methali
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano ufuatao wa jinsi ya kukamilisha methali.
Wingi si …….
Wingi si hoja.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 la kukamilisha
methali katika ukurasa wa 56 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 7 Mazoezi ya lugha


A. Kukamilisha sentensi kwa kutumia maneno uliyopewa
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano wa kukamilisha
sentensi kwa kutumia neno.
Mfano Mmea ni kitu chenye uhai, majani, shina na mizizi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 A ukurasa
wa 57 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 2. Mkahawa 3. Mbolea 4. Matunda 5. mboga

B. Kuoanisha mimea iliyopo katika sehemu A na zao lake


kutoka katika sehemu B
Hatua za ufundishaji
(i) Nakili ubaoni chati inayoonesha sehemu A na sehemu
B iliyopo katika zoezi la 5 B ukurasa wa 57 katika
kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Tumia swali la i na ii kama mfano.
Mchungwa - (f) machungwa
Mhogo - (i) kisamvu na mihogo

(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 B ukurasa


wa 57 katika kitabu cha mwanafunzi.

46

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 46 7/23/21 2:55 PM


C. Kuandika NDIYO au HAPANA
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano ufuatao:
Mkahawa ni mbuni._______
Mkahawa ni mbuni. NDIYO
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 C ukurasa
wa 58 katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kupanga vizuri herufi ili kupata jina la mmea


(i) Toa mfano uliopo katika zoezi la 5 D katika kitabu
cha mwanafunzi ukurasa wa 58.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 D, katika
ukurasa wa 58 katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuorodhesha majina ya mimea na yasiyo ya mimea


Hatua ya ufundishaji
(i) Nakili maneno yote yaliyopo katika zoezi la 5 E
ukurasa wa 58 ubaoni.
(ii) Tumia jedwali lililopo katika ukurasa wa 58 katika
kitabu cha mwanafunzi kutoa mfano.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 E, katika
ukurasa wa 58 katika kitabu cha mwanafunzi.

F. Kuchagua neno kutoka kwenye mabano


Hatua ya ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano wa kuchagua
neno kwenye mabano lenye maana sawa na sentensi
waliyopewa.

47

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 47 7/23/21 2:55 PM


Mfano Eneo linalobubujika maji kutoka ardhini
chemchemi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 F, katika
ukurasa wa 59 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1. jukwaa 2. siagi 3. busara 4. mnada
5. chemchemi
G. Kuchunguza picha kisha kujibu maswali
Hatua za ufundishaji
(i) Ongoza majadiliano kuhusu picha iliyopo ukurasa wa
59 katika kitabu cha wanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 G, ukurasa
wa 60 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1. nyuma 2. chini 3. mbele 4. pembeni 5. chini

Somo la 8 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu somo utakalofundisha.
(b) Ongoza majadiliano kuhusu picha iliyopo katika ukurasa
wa 60.
(c) Waongoze wanafunzi kumalizia habari waliyopewa katika
zoezi la 6 ukurasa 60 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
kuandika katika madaftari yao.
(d) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia sifa sahihi za
mmea wa mhogo, alama za uandishi, mwandiko, nafasi
kati ya neno na neno na matumizi sahihi ya herufi kubwa.

48

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 48 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Nane
Zahanati yetu

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kueleza dhana ya zahanati
(b) Kutaja vifaa vinavyopatikana zahanati anavyovifahamu
(c) Kufanya ziara katika zahanati iliyopo karibu au kualika
tabibu kutoka zahanati jirani kwa maelezo zaidi
(d) Kutaja majina ya vifaa vya zahanati na kazi zake
(e) Kueleza umuhimu wa zahanati katika jamii

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, picha, bangokitita,


kalamu rashasha.
Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza vifaa vinavyopatikana katika
zahanati na huduma zinazotolewa na umuhimu wa kuwa na zahanati.
Pia, watakuza msamiati, kuunda maneno na kuandika habari kwa
mtiririko mzuri.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililopo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 61.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Zahanati
yetu. Atumie picha iliyopo katika ukurasa wa 63 katika
kitabu cha mwanafunzi.

49

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 49 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Zahanati
yetu, iliyopo katika ukurasa wa 61 – 64 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi kujibu swali 1-3 katika zoezi la 1 la
ufahamu ukurasa wa 64 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
kuongea.
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya swali la 4-8 katika zoezi la
kwanza la ufahamu, lililopo ukurasa wa 64 katika madaftari
yao.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari ya Zahanati yetu.
Wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi
kwa kuuliza maswali.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu bila
kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wengi wanapata
nafasi ya kusoma. Fuatilia kubaini dosari zinazojitokeza na
kuzisahihisha.
(d) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(e) Wanafunzi warudie kusoma kadiri muda unavyoruhusu.

50

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 50 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; kipimajoto, vipimo, tabibu,
maabara, tiba, zahanati, pakaza na hadubini.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja
na kutunga sentensi kwa kutumia maneno hayo kwa
mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 lililopo katika
ukurasa wa 65, katika kitabu cha mwanafunzi katika
madaftari yao.

Somo la 4 Mazoezi ya lugha


A. Kuchagua jibu sahihi
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano swali la 1 zoezi
la 3 ukurasa wa 65 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa
wa 65 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1.B 2.A 3. B 4. C 5. D

B. Kuandika sentensi kwa mfuatano sahihi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu mfuatano sahihi wa sentensi
katika habari unaoleta maana.

51

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 51 7/23/21 2:55 PM


(ii) Nakili ubaoni sentensi zilizopo katika zoezi la 3 B
ukurasa wa 66 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma sentensi hizo ubaoni.
(iv) Toa maelekezo ya jinsi ya kupanga sentensi hizo katika
mpangilio mzuri na wanafunzi wafanye hivyo.
Majibu 1. (6), 2. (3), 3. (1), 4. (5), 5. (7), 6. (4), 7. (2).
(v) Waongoze wanafunzi kuandika habari kutokana na
sentensi hizo.
C. Kuandika maneno mapya
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu uundaji wa maneno mapya
kutokana na maneno uliyopewa kwa kudondosha
baadhi ya herufi na silabi.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 3 C ukurasa wa 66
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C ukurasa
wa 66 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1. popo, poa 2. rudi, rudia 3. tende, tenda,
tena 4.teke, Kenya 5. zima, zama, ama 6. uma, mia,
ua 7. pumba, umba, paza 8. cheche, mea, chema 9.
mtu, tundu 10. tiba, tibu, babu

D. Kuoanisha maneno na maana zake


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo yatakayomsaidia mwanafunzi kuoanisha
maneno kutoka sehemu A na maana zake kutoka
sehemu B.

52

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 52 7/23/21 2:55 PM


(ii) Nakili ubaoni zoezi la 3 D katika kitabu cha mwanafunzi
ukurasa wa 67.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma maneno yaliyopo sehemu
A na sehemu B na tumia swali la i na ii kutoa mfano.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi hilo kwenye
madaftari yao.

E. Kuandika umoja na wingi wa maneno


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu kuandika umoja na wingi katika
maneno.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E, ukurasa wa
68 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.

F. Kuandika sentensi katika wakati ujao


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya jinsi ya kubadili sentensi katika wakati
ujao. Zingatia kiambishi ‘ta’ kinachoonesha wakati
ujao katika kitenzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F ukurasa wa
68 katika kitabu cha mwanafunzi.

G. Kutunga sentensi kwa kutumia vifungu vya maneno


Hatua za ufundishaji
(i) Nakili ubaoni vifungu vya maneno vilivyopo
katika zoezi la 3 G ukurasa wa 68 katika kitabu cha
mwanafunzi.

53

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 53 7/23/21 2:55 PM


(ii) Waongoze wanafunzi kupata maana ya vifungu hivyo.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 G la kutunga
sentensi kwa kutumia vifungu vya maneno kwa
mazungumzo kisha waandike kwenye madaftari yao.
H. Kujaza herufi zinazolingana na namba
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo namna ya kuunda maneno kwa kutumia
namba na herufi.
(ii) Nakili ubaoni jedwali lenye namba na herufi, namba
1 - 24 na herufi A - Z katika zoezi la 3 H ukurasa wa
69 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kuunda maneno kwa kutumia
mfano uliopo katika kitabu cha mwanafunzi.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 H ukurasa
wa 69-70 katika kitabu cha mwanafunzi, la kujaza
herufi zinazolingana na namba ili kupata maneno
yanayotumika zahanati.

Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo jinsi ya kuandika habari katika mtiririko mzuri.
(b) Uliza maswali yaliyopo zoezi la 4 ukurasa wa 70 katika
kitabu cha mwanafunzi na andika majibu ubaoni.
(c) Waongoze wanafunzi kuandika habari kwa kuzingatia
maswali na mwanzo waliyopewa. Nakili mwanzo huo ubaoni
au tumia kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 70.
(d) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia, alama za
uandishi, mwandiko, nafasi kati ya neno na neno na matumizi
sahihi ya herufi kubwa.

54

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 54 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Tisa
Kazi zinazofanyika kila siku
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kueleza maana ya neno siku
(b) Kutaja kazi anazofanya kila siku kwa kuzingatia nyakati
(c) Kutofautisha nyakati mbalimbali za siku
(d) Kupanga kazi azifanyazo kila siku nyumbani
(e) Kuwasilisha ratiba yake ya siku

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, picha, bangokitita,


kalamu rashasha, ratiba ya siku.

Muhtasari
Katika hadithi ya Juhudi na Amani wanafunzi wataweza kueleza kazi
za kila siku kwa kuzingatia nyakati. Vilevile, wataweza kuandika
ratiba zao za siku wakihusisha shughuli mbalimbali za kila siku. Pia,
watajifunza misamiati, nahau, vitendawili na nyakati.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 71.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Juhudi na
Amani. Tumia picha iliyopo katika ukurasa wa 72 katika
kitabu cha mwanafunzi.

55

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 55 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Juhudi na
Amani, iliyopo katika ukurasa wa 71 – 73 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza
(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 73 katika kitabu cha mwanafunzi kwa kuongea.
(f) Sikiliza majibu na fanya marekebisho kwa majibu yasiyo
sahihi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari ya Juhudi na Amani.
Wakumbushe wanafunzi kanuni na taratibu za kusoma
kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Wakati wanafunzi wanasoma, mwalimu baini dosari
zinazojitokeza na kuzisahihisha.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na rekebisha makosa hayo.Wanafunzi warudie
kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

56

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 56 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; asubuhi, mchana na jioni.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni na
angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kutunga na kuandika sentensi hizo
katika madaftari yao.

Somo la 4 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu miundo. Tafadhali rejea katika kipengele
cha miundo katika utangulizi.
(b) Nakili miundo yote ubaoni iliyopo katika zoezi la 2 ukurasa
wa 73 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma miundo ubaoni na kutoa
mfano uliopo kitabuni.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia miundo
hiyo kwa mazungumzo na andika sentensi hizo ubaoni.
(e) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(f) Waongoze wanafunzi kutunga na kuandika sentensi kwa
kutumia miundo katika madaftari yao.

57

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 57 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu namna ya kupata maana ya nahau.
(b) Toa mfano uliopo katika zoezi la 3 katika kitabu cha
mwanafunzi ukurasa wa 74.
(c) Waongoze wanafunzi kutoa maana ya nahau zote zilizo
katika zoezi la 3 ukurasa wa 74 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 6 Mazoezi ya lugha


A. Kuchagua jibu sahihi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano kwa kuchagua jibu sahihi katika swali la
kwanza zoezi la 4 A ukurasa wa 74 katika kitabu cha
mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa
wa 74 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1.B 2. C 3. A 4. B 5. D

B. Kubadili sentensi kuwa katika wakati uliopo


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo namna ya kubadili sentensi kuwa katika
wakati uliopo ukizingatia kiambishi cha wakati ‘na’
katika kitenzi.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 B ukurasa wa 75
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B ukurasa
wa 75 katika kitabu cha mwanafunzi.

58

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 58 7/23/21 2:55 PM


C. Kuchunguza picha na kutaja aina za kazi na shughuli
Hatua za ufundishaji
(i) Ongoza majadiliano kuhusu picha a - h zilizopo zoezi la
4 C ukurasa wa 76 – 77 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 C ukurasa wa 77
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C.

D. Kutunga sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo jinsi ya kutumia maneno ya sehemu A
na sehemu B ili kukamilisha maana.
(ii) Nakili ubaoni zoezi la 4 D ukurasa wa 77 katika kitabu
cha mwanafunzi.
(iii) Tumia mfano uliopo katika zoezi 4 D.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi hilo kwenye
madaftari yao.
E. Kuandika sentensi katika wakati uliopita
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo jinsi ya kuandika sentensi katika wakati
uliopita zingatia kiambishi cha wakati ‘li’ katika
kitenzi.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 E ukurasa wa 77
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E, katika
ukurasa wa 77-78 katika kitabu cha mwanafunzi katika
madaftari yao.

59

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 59 7/23/21 2:55 PM


F. Kuimba wimbo
Hatua za ufundishaji
(i) Eleza kuhusu mahitaji ya watoto wenye ulemavu.
(ii) Andika ubaoni wimbo uliopo katika zoezi la 4 F
ukurasa wa 78 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kuimba wimbo huo.
(iv) Waongoze wanafunzi kujibu swali la zoezi la 4 F
ukurasa wa 78 katika kitabu cha mwanafunzi.

G. Kuonesha nyakati katika sentensi


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu viambishi vya nyakati na, li na
ta katika kitendo (kitenzi).
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 G ukurasa wa 78
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 G kisha
sahihisha na kuwapongeza waliofanya vizuri.

Somo la 7 Vitendawili
Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi namna ya kutega na kutegua
vitendawili.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa 79 katika
kitabu cha mwanafunzi, kwa kuonesha picha au vitu halisi
ambavyo ni majibu ya vitendawili. Wape nafasi ya kutega
kitendawili chenye jibu husika hatua kwa hatua.
(c) Ongeza majibu kadiri uwezavyo ili wanafunzi waandike
vitendawili kwenye madaftari yao.

60

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 60 7/23/21 2:55 PM


Somo la 8 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu namna ya kuandika ratiba ya siku kwa
kuzingatia shughuli.
(b) Waongoze wanafunzi kuandaa ratiba ya siku ya Jumatatu
wakiwa shuleni.
(c) Uliza maswali yafuatayo:
(i) Umejifunza nini kutokana na ratiba tuliyoiandaa?
(ii) Unafikiri kingetokea nini kama kungekuwa hakuna
ratiba shuleni?
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 ukurasa wa 79
katika kitabu cha mwanafunzi.
(e) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia, alama za
uandishi, mwandiko, nafasi kati ya neno na neno na
matumizi sahihi ya herufi kubwa.

61

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 61 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi
Kutumia alama za uandishi

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kutaja alama za uandishi anazozifahamu
(b) Kubainisha matumizi ya kila alama za uandishi alizozitaja
(c) Kueleza ujumbe na mafunzo yaliyomo katika hadithi
(d) Kusikiliza, kusimulia, na kueleza ujumbe uliomo katika
hadithi
(e) Kuandika sentensi kwa kuzingatia alama za uandishi

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, kadi za alama za


uandishi, picha, bangokitita, kalamu rashasha na
ratiba ya siku
Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watasoma hadithi ya Ndoto yangu
itakayowasaidia kueleza ujumbe na mafunzo yaliyomo. Pia, kusikiliza,
kusimulia, kuandika hadithi kwa kuzingatia alama za uandishi na kwa
kutumia msamiati, nahau na miundo mbalimbali.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililopo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 80.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Ndoto yangu.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Ndoto

62

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 62 7/23/21 2:55 PM


yangu, iliyopo katika ukurasa wa 80 – 81 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 81 katika kitabu cha mwanafunzi kwa kuongea.
(f) Sikiliza majibu na kufanya marekebisho kwa majibu yasiyo
sahihi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari ya Ndoto yangu.
Wakumbushe wanafunzi kanuni na taratibu sahihi za kusoma
kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu bila
kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wengi wanapata
nafasi ya kusoma.
(d) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

63

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 63 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; radi, kale, makumbusho, ndoto,
watumwa, ziara, minyororo na sufi.
(b) Andika maneno hayo ubaoni kisha waongoze wanafunzi
kusoma maneno hayo.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja
na kutunga sentensi kwa kutumia maneno hayo kwa
mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 82
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

Somo la 4 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Nakili nahau ubaoni na kuwaongoza wanafunzi kutoa
maana ya nahau zote zilizopo katika zoezi la 3 ukurasa wa
82 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 ukurasa wa 82
katika kitabu cha mwanafunzi la kutunga sentensi mbili
kwa kila nahau.

Somo la 5 Mazoezi ya lugha


A. Kuoanisha maneno na maana zake
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo jinsi ya kuoanisha maneno ya kifungu A
na maana zake kutoka kifungu B.
(ii) Nakili ubaoni zoezi la 4 A ukurasa wa 82 katika kitabu
cha mwanafunzi.

64

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 64 7/23/21 2:55 PM


(iii) Tumia swali la kwanza kama mfano.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa
wa 82 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu
i. (c) ii. (f) iii. (e) iv. (g) v. (a) vi. (d) vii. (b)

B. Kuandika NDIYO au HAPANA katika sentensi


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano wa sentensi
ya kujibu ndiyo au hapana. Unaweza kutumia sentensi
ya kwanza zoezi la 4 B ukurasa wa 83 kitabu cha
mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B ukurasa
wa 83 katika kitabu cha mwanafunzi.

C. Kuandika kinyume cha maneno


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa kinyume cha maneno.
Mfano Usiku – Mchana
Kaa – Simama
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C ukurasa
wa 83 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1. mchana 2. washa 3. amka 4. huzuni 5. toka

65

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 65 7/23/21 2:55 PM


D. Kuandika aya kwa usahihi kwa kuzingatia alama za
uandishi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya mambo muhimu ya kuzingatia katika
uandishi.
(ii) Andika ubaoni mfano ufuatao:
mwalimu wetu anaitwa furaha anafundisha somo la
kiswahili Darasa la Nne siku moja alitusimulia
hadithi ya tatu na paka wake tatu alimgawia paka
wake samaki lo paka alijilamba.
(iii) Tumia mfano uliouandika ubaoni kuelekeza jinsi ya
kuweka alama za uandishi kwa usahihi.
Majibu
Mwalimu wetu anaitwa Furaha. Anafundisha somo
la Kiswahili Darasa la Nne. Siku moja alitusimulia
hadithi ya Tatu na paka wake. Tatu alimgawia paka
wake samaki. Lo! Paka alijilamba.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 D ukurasa
wa 83 kwenye daftari.
(v) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia alama
za uandishi na matumizi sahihi ya herufi kubwa na
kufanya masahihisho.

E. Kukamilisha sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu upatanisho wa kisarufi.
(ii) Nakili ubaoni kisanduku kilichopo katika zoezi la 4 E
ukurasa wa 84 katika kitabu cha mwanafunzi.

66

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 66 7/23/21 2:55 PM


(iii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 E ukurasa wa 84
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E, kwenye
madaftari yao.

F. Kubadili sentensi kuwa katika hali timilifu


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu kiambishi awali ‘me’ cha kuonesha
hali timilifu katika kitenzi.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 F ukurasa wa 84
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la 4 F kwenye
madaftari yao.

G. Kutumia baadhi ya herufi za maneno kuunda maneno


mapya
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu uundaji wa maneno mapya kwa
kutumia maneno aliyopewa.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 G ukurasa wa 85
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 G.
Majibu
1. tanga, wizi, tawi, wazi 2. fua, ua, siafu, mfu 3. changa,
moto, choma, chama 4. kumba, kumbusha, umba, umbo
5. simu, ila, mua, lia 6. taka, kasa, saka, kata 7. ua,
au, mua, ama 8. sufu, sifuri, sifa, sifu 9. tumwa, mtu,
tuma, watu 10. uma, uzi, uza, mia

67

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 67 7/23/21 2:55 PM


Somo la 6 Imla
Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi matumizi ya alama za uandishi,
mwandiko mzuri, mpangilio wa aya na nafasi kati ya neno
na neno.
(b) Soma kwa sauti kifungu cha habari kwa kuzingatia alama
za uandishi wanafunzi wakisikiliza.
Mfano
Kinyonga ni mnyama wa ajabu. Mnyama huyu,
hujibadilisha rangi ya mwili wake ili afanane na mazingira
yanayomzunguka. Lo! Mnyama huyu ni tajiri wa rangi.
Utashangaa anapozaa watoto, ndiyo mwisho wa maisha
yake. Nampenda sana kinyonga kwa maajabu yake.
(c) Soma tena hatua kwa hatua wanafunzi wakiandika.
(d) Soma kifungu chote ili wanafunzi wafanye masahihisho
kabla kazi zao hazijasahihishwa.
(e) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia yafuatayo:
(i) usahihi wa maneno
(ii) uumbaji wa herufi
(iii) nafasi kati ya neno na neno
(iv) alama za uandishi
(v) hati ya wima ya kuunga
(vi) matumizi ya herufi kubwa
(vii) usafi wa kazi

68

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 68 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Moja

Kuandika hadithi

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma na kusimulia hadithi
(b) Kubainisha matumizi ya kila alama za uandishi
(c) Kuandika hadithi kwa mtiririko sahihi wa matukio
(d) Kubainisha mambo muhimu ya kuzingatia ili kuleta mfuatano
au mtiririko sahihi wa jambo fulani
(e) Kuandika sentensi kwa kuzingatia alama za uandishi

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, kadi za alama za


uandishi, picha, bangokitita, kalamu rashasha
Muhtasari
Katika sura hii ya kuandika hadithi wanafunzi watajifunza kusimulia,
kusoma na kuandika hadithi kwa mtiririko sahihi wa matukio na kutumia
alama za uandishi kwa usahihi.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 86.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Kabula na
Bahati kwa kutumia picha iliyopo ukurasa wa 87.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Kabula na
Bahati, iliyopo katika ukurasa wa 86 – 88 katika kitabu cha

69

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 69 7/23/21 2:55 PM


mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 88 katika kitabu cha mwanafunzi kwa kuongea.
(f) Sikiliza majibu na kufanya marekebisho kwa majibu yasiyo
sahihi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari ya Kabula na Bahati.
Wakumbushe wanafunzi kanuni na taratibu sahihi za kusoma
kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na kurekebisha makosa hayo wanafunzi warudie
kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

70

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 70 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; porini, yatima, ghafla, jirani,
mpole na twika
(b) Andika maneno hayo ubaoni na uwaongoze wanafunzi
kuyasoma.
(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno moja moja na
uwaongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo katika mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni na
angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 89
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

Somo la 4 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo jinsi yakuoanisha nahau na maana zake.
(b) Nakili ubaoni zoezi la 3 ukurasa wa 89 katika kitabu cha
mwanafunzi. Waongoze wanafunzi kuzisoma nahau zote.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 la kuoanisha nahau
na maana zake kwenye madaftari yao.
Majibu i. (c), ii. (a), iii. (d), iv. (f), v. (b)

Somo la 5 Mazoezi ya lugha


A. Kuandika NDIYO au HAPANA
Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano wa kuandika jibu sahihi kwa kushirikisha
wanafunzi kujibu swali la kwanza zoezi la 4 A ukurasa
wa 89 katika kitabu cha mwanafunzi.

71

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 71 7/23/21 2:55 PM


(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa wa
89 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.
B. Kubadili majina kuwa vitendo
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu namna ya kubadili majina kuwa
vitendo, kwa mfano kwa njia ya uambishaji.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 B ukurasa wa 90
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B ukurasa wa
90 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.
Majibu 1. soma 2. andika 3. cheza 4. chora 5. eleza

C. Kubadili sentensi kuwa katika hali ya mazoea


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya kiambishi ‘hu’ katika kitenzi
kinachoonesha hali ya mazoea.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 C ukurasa wa 90
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C ukurasa
wa 90 katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kupanga sentensi katika mfuatano sahihi wa matukio


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo namna ya kupanga sentensi zisizo katika
mfuatano sahihi.
(ii) Nakili ubaoni sentensi zote za zoezi la 4 D ukurasa
wa 90 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma sentensi hizo.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 D kwa kupanga

72

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 72 7/23/21 2:55 PM


kwa usahihi sentensi ya kwanza na ya pili. Kisha
wanafunzi wamalizie zoezi hilo kwenye madaftari yao.

E. Kuandika kinyume cha maneno


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano kwa kuwauliza wanafunzi wataje kinyume
cha maneno.
Mfano Mpole – Mkali
Nyuma – Mbele
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E ukurasa wa
91 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.

F. Kupigia mstari maneno ambayo ni vitendo


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 F ukurasa wa 91
katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la 4 F kwenye
madaftari yao.

G. Kuondoa silabi moja katika maneno ili kuunda neno jipya


Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu namna ya kudondosha silabi ili
kuunda neno jipya.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 4 G ukurasa wa 91
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 G.
Majibu 1. kasi 2. fungu, nguo 3. kisa 4. bati, kaba 5. miwa
6. dari 7. dua, waa 8. siku 9. mende, mea
10. mche

73

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 73 7/23/21 2:55 PM


H. Kuandika habari kwa usahihi kwa kuzingatia alama za
uandishi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo kuhusu matumizi ya alama za uandishi.
(ii) Andika ubaoni au kwenye bango kitita mfano ufuatao:
kija ni muuguzi katika zahanati ya kaloleni alialikwa
na mwenyekiti wa kitongoji cha mbuyuni muuguzi
huyo alitoa elimu ya afya ya matumizi bora ya vyoo
ama kweli wanakijiji walifurahia elimu hiyo
(iii) Tumia mfano uliouandika ubaoni au kwenye bangokitita
kuelekeza wanafunzi jinsi ya kuweka alama za uandishi
kwa usahihi. Ni vema uwape nafasi wanafunzi kuweka
alama hizo.
Majibu
Kija ni muuguzi katika zahanati ya Kaloleni. Alialikwa
na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbuyuni. Muuguzi
huyo, alitoa elimu ya afya ya matumizi bora ya vyoo.
Ama kweli, wanakijiji walifurahia elimu hiyo.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 H ukurasa
wa 92 kwenye madaftari yao.
(v) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia matumizi
sahihi ya alama za uandishi, herufi kubwa, uumbaji
wa herufi, nafasi kati ya neno na neno na mwandiko.

74

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 74 7/23/21 2:55 PM


Somo la 6 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu taratibu za usimuliaji wa hadithi.
(b) Simulia hadithi fupi ya kuvutia na waulize wanafunzi
mafunzo ya hadithi hiyo.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa wa 92
katika kitabu cha mwanafunzi kwa kuzingatia jinsi.
(d) Sikiliza kwa makini hadithi inayosimuliwa na waongoze
wanafunzi kuuliza mafunzo ya hadithi husika.

75

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 75 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Mbili
Mahali tulipo

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma habari ya Jinsi nilivyonusurika
(b) Kuandika sentensi zenye kuonesha mahali watu walipo na
vitu vilipo
(c) Kutaja mahali panapowekwa vitu na wanapokuwa watu

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, kadi za alama za


uandishi, picha, bangokitita, kalamu rashasha
Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza kuonesha na kuandika mahali
watu na vitu vilipo wakitumia msamiati na miundo tofauti.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililopo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 93.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu habari ya Jinsi
nilivyonusurika kwa kutumia picha iliyopo ukurasa wa 94.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Jinsi
nilivyonusurika, iliyopo katika ukurasa wa 93 – 94 katika
kitabu cha mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila
kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.

76

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 76 7/23/21 2:55 PM


(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 94-95 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
kuongea.
(f) Sikiliza majibu na kufanya marekebisho kwa majibu yasiyo
sahihi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari ya Jinsi nilivyonusurika.
Wakumbushe wanafunzi mambo muhimu ya kuzingatia
wakati wa kusoma kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili, matamshi sahihi,
kiimbo, kasi nzuri ya usomaji, hisia na matumizi sahihi ya
alama za uandishi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na rekebisha makosa hayo.
(e) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; kibanda, kasi, jeruhi, kando,
chakavu na okoa
(b) Andika maneno hayo ubaoni na waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo.

77

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 77 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kueleza maana ya neno mojamoja
na kutunga sentensi kwa kutumia maneno hayo kwa
mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 95
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

Somo la 4 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu somo kwa kurejea utangulizi kipengele
cha miundo.
(b) Nakili miundo yote ubaoni iliyopo katika zoezi la 3 ukurasa
wa 95 katika kitabu cha mwanafunzi na waongoze wanafunzi
kusoma miundo hiyo.
(c) Toa mfano kwa kutumia swali la kwanza la zoezi la 3.
(d) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia miundo
hiyo kwa mazungumzo na andika sentensi hizo ubaoni.
(e) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(f) Waongoze wanafunzi kutunga na kuandika sentensi nyingine
kwenye madaftari yao.

Somo la 5 Nahau
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo ya namna ya kupata maana ya nahau.
(b) Nakili ubaoni zoezi la 4 ukurasa wa 95 katika kitabu cha
mwanafunzi au tumia vitabu kuwaongoza wanafunzi kusoma
nahau zote.
(c) Toa mfano kwa kutumia swali la kwanza kutoa maana ya

78

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 78 7/23/21 2:55 PM


piga yowe kama ilivyotumika katika hadithi.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 la kuandika maana
ya nahau kama zilivyotumika kwenye hadithi.
Majibu i. piga kelele ii. fanikiwa iii. kuangalia kwa haraka
iv. wasiwasi/duwaa/hofu v. kimbia kwa kasi

Somo la 6 Zoezi la lugha


Kuchagua jibu sahihi kukamilisha sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kutoa mfano wa kukamilisha
sentensi, tumia swali la kwanza zoezi la 5 ukurasa wa
96 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa wa 96
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

Somo la 7 Vitendawili
Kutegua vitendawili
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano wa kitendawili na wanafunzi wategue.
(b) Toa nafasi kwa wanafunzi kutega na kutegua vitendawili.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 ukurasa wa 96
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.
Majibu 1.nzi 2.nanasi 3. maboga 4. moto 5. macho.
6. kitanda 7. nywele 8. ardhi/mawingu
9. mwangwi 10. mate

79

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 79 7/23/21 2:55 PM


Somo la 8 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo ya matumizi ya picha zisizo na mfululizo
katika utungaji.
(b) Ongoza wanafunzi kujadiliana picha ya 1-5 na tunga sentensi
ya mfano kwa kutumia picha mojawapo.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia picha
kwa mazungumzo.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 7 ukurasa wa 97
katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

80

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 80 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Tatu
Dawa za kulevya
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kusoma shairi la dawa za kulevya
(b) Kujifunza madhara ya dawa za kulevya
(c) Kuandika habari fupi kuhusu dawa za kulevya
(d) Kubaini ujumbe uliobebwa katika shairi

Mahitaji picha na pichamguso


Muhtasari
Dawa za kulevya ni janga la kitaifa ambapo taifa hupoteza nguvu kazi
kwa kuathirika na dawa hizi. Katika sura hii mwanafunzi atajifunza
madhara ya dawa za kulevya kwa kusoma shairi linalohusu dawa za
kulevya. Pia, mwanafunzi atajifunza utungaji wa habari fupi.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 98.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu shairi la Dawa
za kulevya ni hatari. Tumia ubunifu wa kutafuta picha
zinazoonesha madhara ya dawa za kulevya.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya shairi la Dawa za
kulevya ni hatari, katika ukurasa wa 98 – 100 katika kitabu
cha mwanafunzi kwa kuzingatia kanuni za usomaji wa shairi.
(d) Waulize wanafunzi maswali yafuatayo kisha wajibu kwa
kuongea:

81

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 81 7/23/21 2:55 PM


(i) La mgambo likilia, ujue kunalo jambo. Maana yake nini?
(ii) Mwandishi ana maana gani anaposema, “Tuzipige
mateke tabia zisizofaa.’’
(c) Waongoze wanafunzi wasimulie shairi walilolisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
swali 3 - 6 yaliyopo ukurasa wa 100 katika kitabu cha
mwanafunzi kwenye madaftari yao.
Majibu
(i) Uwepo wa taarifa ya jambo fulani.

(ii) Kuacha tabia zisizofaa.

(iii) kifo, afya mbaya na kudhoofika mwili, kutokufanya


kazi, kupata magonjwa ya maambukizi kama UKIMWI.

(iv) Kuondoa changamoto za madawa ya kulevya, kufuatilia


nyendo za watoto shuleni na nyumbani.

(v) Elimu itolewe kwa vijana kuhusu dawa za kulevya.

(vi) Kuacha kutumia madawa ya kulevya / kwenda hospitali


kupata matibabu / kuachana na makundi mabaya.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu shairi litakalosomwa.
(b) Toa mfano wa usomaji bora wa shairi kwa kusoma ubeti
wa kwanza na wa pili kwa kuzingatia urari wa vina, mizani
na kanuni nyingine za kusoma kwa sauti.

82

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 82 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kusoma shairi mmoja mmoja, unapo
baini makosa ya usomaji wa kishairi sahihisha makosa hayo.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya mazoezi zaidi ya kusoma
shairi kadiri muda unavyoruhusu.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati familia, dawa, madhara, asilani, makini
na kinywaji.

(b) Andika maneno hayo ubaoni kisha uyasome na kueleza


maana ya neno mojamoja.

(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno


hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni, kwa
kurekebisha makosa.

(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 100


katika kitabu cha mwanafunzi.

(e) Sahihisha kazi za wanafunzi na kufanya masahihisho


darasani.

Somo la 4 Mazoezi ya Lugha


A. Kuoanisha maneno ya sehemu A na maana zake katika
sehemu B
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuoanisha maneno ya sehemu A na maana
zake katika sehemu B

83

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 83 7/23/21 2:55 PM


Mfano
Sehemu A Sehemu B
iii. Madhara (f) Uharibifu au athari mbaya
ii. Asilani (a) Kamwe
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa wa 101
katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuandika wingi wa maneno


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja maneno ambayo umoja na wingi
hautofautiani kama vile; soda, mafuta na sukari.
(b) Toa mifano ya maneno kwa kuandika wingi wa maneno
yaliyopo kwenye umoja.
Mfano Ukuta – kuta
Jiwe – mawe
Changamoto – changamoto
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa wa 101
katika kitabu cha mwanafunzi.

C. Kuandika maneno kuonesha mahali


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika maneno kuonesha mahali.
Mfano Shule shuleni
Msitu Msituni
Kaburi kaburini

84

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 84 7/23/21 2:55 PM


(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C ukurasa wa 101
katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kuandika kinyume cha maneno


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika kinyume cha maneno.
Mfano Nyeupe nyeusi
Juu chini
Mkali mpole
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D ukurasa wa 102
katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuunda neno jipya kwa kudondosha silabi au herufi


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuunda neno jipya kwa kudondosha silabi
au herufi.
Mfano Taifa tai
Kulevya kule
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E ukurasa wa 102
katika kitabu cha mwanafunzi.
F. Kuandika KWELI au SI KWELI
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika KWELI au SI KWELI katika
sentensi.
Mfano
(i) Dawa za kulevya hupoteza nguvu kazi ya taifa. KWELI
(ii) Mtu anayetumia dawa za kulevya hawezi kupata
UKIMWI. SI KWELI.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F ukurasa wa 102
katika kitabu cha mwanafunzi.

85

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 85 7/23/21 2:55 PM


G. Kukamilisha sentensi kwa kuchagua jibu sahihi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika ubaoni sentensi ili kuchagua jibu
lililo sahihi.
Mfano Kushirikiana______ kunachangia kueneza
UKIMWI. (maji, mavazi, malazi, sindano)
Kushirikiana sindano kunachangia kueneza
UKIMWI
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 G ukurasa wa 103
katika kitabu cha mwanafunzi na kusahihisha kazi zao.
H. Kubadili sentensi kuwa katika wakati ujao
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi wataje mambo watakayofanya kwa
siku zijazo.
(b) Toa mifano kwa kubadili sentensi kuwa katika wakati ujao.
Kumbuka kiambishi “ta” katika kitenzi ndicho kinachoonesha
wakati ujao.
Mfano
Wasichana wanafundishwa madhara ya mimba za utotoni.
Wasichana watafundishwa madhara ya mimba za utotoni.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 H ukurasa wa
103-104 katika kitabu cha mwanafunzi.

86

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 86 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Rejea maelekezo yaliyopo katika utangulizi kuhusu utungaji.
(b) Waongoze wanafunzi kuandika habari yenye maneno sabini
(70), wakieleza kuhusu madhara ya dawa za kulevya kwa
kuzingatia maswali ya zoezi la 4 ukurasa wa 104 katika
kitabu cha mwanafunzi.
(c) Sahihisha kazi ya wanafunzi kwa kuzingatia uumbaji wa
herufi, nafasi kati ya neno na neno, alama za uandishi na
matumizi ya herufi kubwa.

87

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 87 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Nne
Kuchemsha chai

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kujifunza jinsi ya kufuata maelekezo na hatua sahihi katika
kutenda jambo
(b) Kuandika utungaji unaohusu jambo linalofanyika hatua
kwa hatua
(c) Kufafanua hatua zinazofanyika katika kupika chai

Mahitaji vitu halisi na picha, pichamguso, mazingira halisi.

Muhtasari
Sura hii itamsaidia mwanafunzi kujifunza utungaji kwa kufuata
maelekezo ya kutenda jambo hatua kwa hatua. Mfano, atajifunza
kupika chai hatua kwa hatua.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 105.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu hadithi ya Kuchemsha
chai. Unaweza kutumia picha iliyopo katika hadithi ukurasa
wa 105 katika kitabu cha mwanafunzi au tumia mazingira
ya wanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma hadithi ya Kuchemsha chai
iliyopo katika ukurasa wa 105 – 106 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.

88

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 88 7/23/21 2:55 PM


(d) Waulize wanafunzi kwa mdomo maswali kutoka zoezi la
kwanza la ufahamu swali la 1 na la 2 katika ukurasa 106
katika kitabu cha mwanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma kwa
maneno machache.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
lililopo kwenye kitabu cha mwanafunzi katika ukurasa wa
106.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Eleza nini unatarajia kifanyike katika somo hili na
kuwakumbusha wanafunzi matumizi ya alama za uandishi.
(b) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia kanuni za usomaji.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu.
Hakikisha wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Unapobaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
na kurekebisha makosa hayo. Pia wanafunzi warudie kusoma
kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati epua, chemka, upishi, vifaa, na viungo.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na wanafunzi wayasome na
kutoa maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni, zenye
makosa zirekebishe.

89

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 89 7/23/21 2:55 PM


(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 katika ukurasa wa
107 katika kitabu cha mwanafunzi na sahihisha kazi hiyo.

Somo la 4 Mazoezi ya Lugha


A. Kuoanisha maneno ya sehemu A na B ili kukamilisha
sentensi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuoanisha maneno ya sehemu A na B ili
kukamilisha sentensi.
Mfano
Sehemu A Sehemu B
i. Mwalimu Zena (e) anafundisha somo la upishi
ii. Hatua ya kuchemsha chai (h) kuweka sufuria lenye maji kwenye
jiko linalowaka
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa wa 107
katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuandika sentensi kwa usahihi kwa kuzingatia alama za


uandishi
Hatua za ufundishaji
(a)
Waongoze wanafunzi kwa kuwakumbusha matumizi ya
alama za uandishi. Unaweza kutumia chati ya alama za
uandishi au kadi za alama za uandishi.
(b) Toa mifano ya kuandika sentensi kwa usahihi kwa kuzingatia
alama za uandishi.
Mfano maziwa yaliyoganda hayafai kupikia chai
Maziwa yaliyoganda, hayafai kupikia chai.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa wa 108
katika kitabu cha mwanafunzi.

90

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 90 7/23/21 2:55 PM


C. Kupanga maneno ili kupata sentensi zenye maana
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kupanga maneno ili kupata sentensi zenye
maana.
Mfano Wanafunzi chai walichemsha shuleni.
Wanafunzi walichemsha chai shuleni.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C ukurasa wa 108
katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kuandika sentensi katika wakati uliopita


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano ya kubadili sentensi kuwa wakati uliopita.
Mfano Amina anaimba wimbo mzuri.
Amina aliimba wimbo mzuri.
Jerome anauza maziwa.
Jerome aliuza maziwa.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D ukurasa wa
108-109 katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kutunga sentensi kutokana na jedwali


Hatua za ufundishaji
(a) Andika ubaoni jedwali lililoko zoezi la 3 E ukurasa wa 109
katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Toa mifano kwa kutunga sentensi kutokana na jedwali.
Mfano i. Nilijitahidi nikawa wa kwanza.
ii. Nilizingatia masomo nikawa mwanafunzi bora darasani.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E ukurasa wa 109
katika kitabu cha mwanafunzi.

91

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 91 7/23/21 2:55 PM


F. Kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika sentensi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika
sentensi.
Mfano
1. Mgeni alipobisha ________ alikaribishwa
Mgeni alipobisha hodi alikaribishwa.
2. Bibi alifinyanga __________ vizuri.
Bibi alifinyanga chungu vizuri.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F ukurasa wa 109
katika kitabu cha mwanafunzi.

G. Kuongeza silabi mbele au nyuma kuunda maneno mapya


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuunda maneno kwa kuongeza silabi moja
mbele au nyuma.
Mfano nepa – nenepa
kata – kataa
zizi – mzizi
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 G ukurasa wa 109
katika kitabu cha wanafunzi. Kazi za wanafunzi zisahihishwe
na wahimize wanafunzi kufanya marudio.

92

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 92 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujadili hatua za utungaji kwa kutumia
picha.
(b) Waongoze wanafunzi kujadili picha zilizopo katika kitabu
cha mwanafunzi ukurasa wa 110 – 111.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kila picha kwa
mazungumzo na kuziandika sentensi hizo ubaoni.
(d) Andika sentensi hizo ubaoni na kusahihisha makosa
yaliyojitokeza.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 kuandika habari fupi
isiyozidi maneno sabini (70) kwa kutumia picha zilizopo
katika ukurasa wa 110 –111 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 6 Kazi ya kufanya (Utungaji)


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kwa kufanya mazungumzo mafupi
ya jinsi ya kupika viazi vitamu. Ni vema ukatumia ziara ya
taswira ili wanafunzi waseme wanachokifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa wa 111
katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Sahihisha kazi walizoandika wanafunzi, kisha chagua tungo
zilizo nzuri zisomwe darasani.

93

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 93 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Tano

Kuandika barua
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kujifunza jinsi ya kuandika barua ya kirafiki
(b) Kueleza muundo wa barua ya kirafiki
(c) Kueleza umuhimu wa barua za kirafiki
(d) Kuandika barua ya kirafiki

Mahitaji chati ya muundo wa barua.

Muhtasari
Uandishi wa barua ni jambo muhimu kwa mawasiliano katika jamii.
Katika sura hii mwanafunzi atajifunza muundo na jinsi ya kuandika
barua ya kirafiki, ambapo itamsaidia katika maisha yake ya kila siku.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 112.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu barua za kirafiki kwa
kuuliza maswali.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Ziara
kiwandani mtibwa, iliyopo katika ukurasa wa 112–113
kitabu cha mwanafunzi kwa kuzingatia kanuni za usomaji.
(d) Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:
i. Je, barua ya kirafiki ina umuhimu gani ?
ii. Je, unafikiri Kabula ana tabia gani ?

94

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 94 7/23/21 2:55 PM


(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyosoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 114 kitabu cha mwanafunzi na kusahihisha
zoezi hilo.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu habari itakayosomwa na
kuwakumbusha wanafunzi kanuni za kusoma kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu.
Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(d) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; ziara, kujikimu, kukengeuka
na ndoto.
(b) Andika maneno hayo ubaoni na kuyasoma kisha eleza maana
ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi na
kuzisahihisha.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 39
katika kitabu cha mwanafunzi.

95

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 95 7/23/21 2:55 PM


Somo la 4 Mazoezi ya Lugha
A. Kuchunguza miundo katika barua za kirafiki na kujibu
maswali
Hatua za ufundishaji
(a) Ongoza majadiliano mafupi kuhusu muundo wa barua ya
kirafiki.
(b) Tumia barua ya kirafiki iliyopo ukurasa wa 113 katika kitabu
cha mwanafunzi, kusaidia mwanafunzi kubaini vipengele
vya barua ya kirafiki.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa wa 114
katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuandika vipengele vya barua ya kirafiki katika mpangilio


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kuwakumbusha muundo
wa barua ya kirafiki. Tumia barua ya kirafiki.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa wa
115 katika kitabu cha mwanafunzi, kisha sahihisha
kazi za wanafunzi na kuwapongeza waliofanya vizuri.

C. Kuchunguza muundo wa barua ya kirafiki, kisha kujaza


visanduku alivyopewa
Hatua za ufundishaji
(a) Tumia barua ya kirafiki kuwauliza wanafunzi maswali.
Mfano
(i) Upande wa kulia unaona kipengele gani? (anuani
ya mwandishi )
(ii) Upande wa kushoto kuna kipengele gani? (salamu
za awali)

96

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 96 7/23/21 2:55 PM


(iii)
Katikati ya barua kuna kipengele gani? (kiini cha
barua/barua yenyewe)
(iv) Mwisho kuna kipengele gani? (jina na saini ya
mwandishi)
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C ukurasa wa 115
katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kuandika KWELI au SI KWELI kuonesha kukubali au


kukanusha wazo
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika KWELI au SI KWELI kuonesha
kukubali au kukanusha wazo
Mfano
(i) Barua za kirafiki huandikwa kwa familia au rafiki
tu. KWELI
(ii) Anuani ya barua ya kirafiki haihitajiki kwani jina
la anayeandika linatosha. SI KWELI
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D ukurasa wa 116
katika kitabu cha mwanafunzi.
E. Kuoanisha sehemu ya muundo wa barua katika sehemu
A na sehemu B ili kuleta maana kamili
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu somo utakalolifundisha.
(b) Toa mifano kwa kuoanisha sentensi kutoka sehemu A na B
ili kuleta maana kamili.
Mfano
Sehemu A Sehemu B
i. Barua yenyewe (a) Madhumuni au lengo la barua hii ni
---------
iv. Maamkizi ya awali (c) Mpendwa baba shikamoo -----------

97

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 97 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E ukurasa wa 116
katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu
i – a
ii – b
iii – d
iv – c
v–g
vi – e
vii – f
F. Kuandika kinyume cha maneno
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano ya kinyume cha maneno.
Mfano
i. Kifunguamimba – kitindamimba.
ii. Adui – rafiki.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F ukurasa wa 117
katika kitabu cha mwanafunzi. Sahihisha kazi za wanafunzi
na kuwapongeza waliofanya vizuri.

Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja vipengele muhimu vya barua
ya kirafiki. Tumia mfano wa barua ya kirafiki.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 ukurasa wa 117
katika kitabu cha mwanafunzi. Sahihisha barua walizoandika
wanafunzi kwa kuzingatia muundo wa barua ya kirafiki,
uumbaji wa herufi, nafasi kati ya neno na neno, matumizi
ya alama za uandishi na herufi kubwa.

98

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 98 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Sita
Kuandika hadithi fupi kwa kutumia majina ya ndege

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma hadithi
(b) Kutambua aina mbalimbali za ndege na majina yao
(c) Kuandika hadithi fupi
(d) Kubuni mambo muhimu katika kuandika hadithi

Mahitaji chati za picha, pichamguso na vitu halisi.

Muhtasari
Katika sura hii mwanafunzi ataweza kuhadithia na kuandika hadithi.
Pia, mwanafunzi atajifunza aina mbalimbali za ndege na majina yao.
Vilevile, atajifunza kubuni mambo muhimu katika kuandika hadithi.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 118.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu hadithi itakayosomwa.
Unaweza kutumia picha zilizopo katika ukurasa wa 120 na
121 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya habari ya Kunguru na
bata, iliyopo katika ukurasa wa 119 – 122 katika kitabu cha
mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:

99

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 99 7/23/21 2:55 PM


(i) Ni nani walikuwa marafiki katika hadithi uliyoisoma?
(ii) Kwa nini kunguru aliona kuwa anadhulumiwa na bata?
(iii) Kwa nini bata alilia kwa uchungu?
(e) Waongoze wanafunzi wasimulie habari waliyoisoma
kwa maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza la
ufahamu katika ukurasa wa 122 katika kitabu cha
mwanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu hadithi itakayosomwa.
(b) Wakumbushe wanafunzi kanuni za kusoma kwa sauti.
Unaweza kutumia chati au kadi za alama hizo.
(c) Soma aya moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia kanuni za usomaji.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu, bila
kujali jinsia zao na uwezo wao. Wanafunzi wengi wapewe
nafasi ya kusoma.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; kale, tenga, hamaki, laumu,
uchungu na nyanyasa
(b) Andika maneno hayo ubaoni, waongoze wanafunzi kusoma
maneno hayo na kueleza maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
Mfano Hapo kale kunguru na bata walikuwa marafiki.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.

100

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 100 7/23/21 2:55 PM


(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 ukurasa wa 122
katika kitabu cha mwanafunzi, sahihisha kazi za wanafunzi
na wafanye masahihisho.

Somo la 4 Methali na semi


A. Kueleza maana za methali na semi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelekezo mafupi kuhusu methali na semi.
(b) Waongoze wanafunzi kutaja methali na semi wanazozifahamu.
(c) Waongoze wanafunzi kwa kutumia maelezo na mifano
kutambua maana za methali na semi.
Mfano
i. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
Mtu asiyeshaurika na wakubwa mwishowe hupata madhara
mabaya.
ii. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Siku zote mtu anayesema ukweli atapendwa na wengi.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 A ukurasa wa 123
katika kitabu cha mwanafunzi.

B.Kukamilisha methali kwa kuchagua jibu sahihi


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja methali wanazozifahamu.
(b) Waongoze wanafunzi kukamilisha methali kwa kuchagua
jibu sahihi kwa kuonesha mifano.
Mfano Ndege mjanja .................
(a) Hakamatwi na mtego
(b) Hunaswa kwenye tundu bovu
(c) Hukamatwa na ulimbo b
(d) Huwa mwangalifu kwa kila jambo

101

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 101 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa wa
123-124 katika kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 1- b, 2- b, 3-b, 4-c, 5- c.

Somo la 5 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu miundo.
(b) Andika miundo ifuatayo ubaoni.
....... walipokuwa ........
....... huku na huko ......
kila siku .........
........ lakini .......
........ kwa sababu .......
(c) Waongoze wanafunzi kusoma miundo iliyoandikwa ubaoni.
(d) Toa mifano ya sentensi zenye miundo unayotaka kufundisha.
mfano i. Kila siku .........
Kila siku kunguru huruka juu ya mti.
ii. ........ huku na huko .........
Alitazama huku na huko hakumuona ng’ombe wake.
(e) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 ukurasa wa 124
katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 6 Mazoezi ya Lugha


A. Kuandika kinyume cha maneno
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutoa kinyume cha maneno hayo.
Mfano nenda – rudi
jenga – bomoa
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 A ukurasa wa 125
katika kitabu cha mwanafunzi.

102

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 102 7/23/21 2:55 PM


B. Kutunga sentensi kutokana na jedwali
Hatua za ufundishaji
(a)Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kutokana na jedwali
kwa kutoa mifano.
Mfano i. Baada ya kusikia maneno hayo bata alilia kwa uchungu.
ii. Kabla ya kukubaliana kunguru wote waliruka.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 B ukurasa wa 125
katika kitabu cha mwanafunzi.
C. Kuandika KWELI au SI KWELI
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mifano kwa kuandika KWELI au SI KWELI katika
sentensi.
Mfano
i. Ndege wote hula nafaka. KWELI
ii. Ndege wafugwao ni bata, njiwa na bundi. SI KWELI.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 C ukurasa wa 125
katika kitabu cha mwanafunzi.
D. Kuandika sentensi kwa usahihi kwa kuzingatia alama za
uandishi
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kwa kuwakumbusha matumizi ya
alama za uandishi. Unaweza kutumia chati au kadi za alama
za uandishi.
(b) Toa mifano ya kuandika sentensi kwa usahihi kwa kuzingatia
alama za uandishi.
Mfano
i. loo kunguru ana tabia mbaya
Loo! Kunguru ana tabia mbaya.
ii. chiriku kunguru kuku na bata wote ni aina ya ndege
Chiriku, kunguru, kuku na bata wote ni aina ya ndege.

103

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 103 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 D ukurasa wa 125
katika kitabu cha mwanafunzi.

E. Kuandika majina ya ndege wafugwao kwa kutumia chati


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu jinsi ya kutumia chati iliyopo ukurasa
wa 126.
(b) Waongoze wanafunzi kutaja majina ya ndege wafugwao
wanaowafahamu.
(c) Waongoze wanafunzi kutaja majina ya ndege wafugwao
kwa kutumia chati iliyopo katika kitabu cha mwanafunzi.
Mfano KUKU, NJIWA.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 E ukurasa wa 126
katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 7 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kutaja mambo ya kuzingatia katika
uandishi.
(b) Waongoze wanafunzi kujibu kwa mazungumzo maswali ya
mwongozo katika zoezi la 6 ukurasa wa 126 katika kitabu
cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kuandika hadithi kwa kuzingatia
mwongozo wa maswali yaliyotolewa zoezi la 6 ukurasa wa
126 katika kitabu cha mwanafunzi.

104

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 104 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Saba
Kujifunza mashairi

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kujifunza kuhusu mashairi
(b) Kueleza maana ya shairi
(c) Kusoma na kuimba shairi
(d) Kubaini ujumbe uliobebwa katika shairi

Mahitaji mfano wa shairi


Muhtasari
Wanafunzi watasoma kuhusu mashairi. Wataeleza maana ya shairi, pia
wataimba shairi na kughani kwa kuzingatia urari wa vina na mizani.
Watafanya mazoezi mbalimbali kuhusu shairi kwa mfano msamiati,
ufahamu na mazoezi ya lugha.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 127.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu shairi la Janga la
UKIMWI.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya shairi la Janga la
UKIMWI lililopo katika ukurasa wa 127 – 128 katika kitabu
cha mwanafunzi, bila kufuatisha kwa kidole.
(d) Uliza maswali yafuatayo, kisha wanafunzi wajibu kwa
mdomo.
i. Shairi letu linahusu nini?
ii. Je, shairi hili lina beti ngapi?

105

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 105 7/23/21 2:55 PM


iii. Je, kuna umuhimu gani kujifunza elimu ya UKIMWI?
(e) Waongoze wanafunzi kueleza kwa kifupi kuhusu shairi la
Janga la UKIMWI.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 1 swali 4 - 6 la
ufahamu ukurasa wa 129 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi kanuni za usomaji wa shairi kwa
sauti. Unaweza kutumia ubeti wa shairi.
(b) Soma ubeti wa kwanza na wa pili kuonyesha mfano mzuri wa
usomaji wa shairi, kwa kuzingatia urari wa vina na mizani.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma shairi mmoja mmoja kwa
zamu, bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Baini dosari
zinazojitokeza na kuzisahihisha. Wape wanafunzi wengi
nafasi ya kusoma kadiri muda unavyoruhusu.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; kinga, samba, maradhi,
maambukizi, lishe na kusinyaa ulioko katika ukurasa wa
129 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Andika maneno hayo ubaoni wanafunzi wayasome na
waeleze maana ya neno mojamoja.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia maneno
hayo kwa mazungumzo. Andika sentensi hizo ubaoni.
Rekebisha makosa yaliyojitokeza katika sentensi hizo.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 katika ukurasa wa
129 katika kitabu cha mwanafunzi.

106

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 106 7/23/21 2:55 PM


Somo la 4 Mazoezi ya lugha
A. Kuchagua jibu sahihi kisha kujaza nafasi iliyoachwa wazi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi katika sentensi.
Mfano Mstari mmoja kwenye kila ubeti huitwa mshororo.
(b)Waongoze wanafunzi kuchagua jibu sahihi kwa kujaza nafasi
zilizoachwa wazi katika zoezi la 3 A ukurasa
130 -131, kitabu cha mwanafunzi.
Majibu 2. vina, 3. mizani, 4. ubeti, 5. kituo, 6. takwimu za
kitaalamu zinaonesha watu wengi wanaugua,
7. kutumia dawa na lishe bora.

B. Kuandika NDIYO au HAPANA.


Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano wa zoezi kwa kuandika NDIYO au HAPANA
katika sentensi.
Mfano Kinga ni bora kuliko tiba. NDIYO.

(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 B ukurasa 131,


katika kitabu cha mwanafunzi.

C. Kuandika kwa ukamilifu maneno yaliyotumika katika


shairi
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano kwa kuandika maneno yaliyotumika katika shairi
kwa ukamilifu. Tumia mfano uliotolewa katika kitabu cha
mwanafunzi ukurasa wa 132.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 C, katika kitabu
cha mwanafunzi ukurasa wa 132.

107

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 107 7/23/21 2:55 PM


D. Kuoanisha maneno katika sehemu A na B ili kuleta maana.
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano wa kuoanisha maneno katika sehemu A na B ili
kuleta maana.
Mfano
Sehemu A Sehemu B
i. dhoofu (j) Kukonda na kuishiwa na nguvu na
kupungukiwa na afya
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 D ukurasa wa 132
katika kitabu cha wanafunzi.
Angalia majibu yafuatayo:
ii. (e), iii. (h), iv. ( i), v. (a), vi. (c), vii. (b), viii. (f)

E. Kuandika kinyume cha maneno


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kuandika kinyume cha maneno.
Mfano dhoofu – nawiri
nzito – nyepesi
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 E ukurasa 133
katika kitabu cha mwanafunzi.

F. Kuandika neno lenye maana sawa na maneno aliyopewa


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kuandika neno lenye maana sawa na
maneno waliyopewa. Tumia mfano uliotolewa katika kitabu
cha mwanafunzi ukurasa wa 133.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 F ukurasa wa 133
katika kitabu cha mwanafunzi.

108

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 108 7/23/21 2:55 PM


Majibu ni kama yafuatayo:
1. umri 2. tabu 3. nadhifu 4. hifadhi 5. bibi kizee 6. mwisho
7. mwanzo 8. peremende.
G. Kukamilisha sentensi kwa kutumia maneno uliyopewa
katika kisanduku
Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kukamilisha sentensi kwa kutumia
maneno waliyopewa katika kisanduku.
Mfano Kiti kikubwa kilivunjika kabisa.
Kiti kidogo kilivunjika kabisa.
(b) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 G ukurasa wa
133-134 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 5 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa mfano wa kusoma shairi kwa wanafunzi kwa kutumia
shairi lenye ubeti mmoja.
Mfano
Leo tumekusanyika, malaria kuongelea,
Njia kutaja nataka, jinsi unavyoenea,
Nyasi na pia vichaka, makazi kukaribia,
Safisheni mazingira, mbu kutozaliana.

(b) Waongoze wanafunzi kusoma sentensi mbili mbili kishairi


kutoka katika ubeti huo.
(c) Waelekeze wanafunzi idadi ya silabi zilizoko katika sentensi
moja. Kila sentensi moja ina idadi ya silabi 16, ambayo
huitwa mizani. Tumia ubeti huo kuhesabu mizani hiyo.
(d) Waelekeze wanafunzi kuwa katika sentensi kuna silabi
zinazojirudiarudia katika mistari ya ubeti, ambazo huitwa vina.

109

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 109 7/23/21 2:55 PM


(e) Waongoze wanafunzi kutaja vina vya kati na vya mwisho
katika kila mstari wa ubeti wa shairi.
(f) Waeleze wanafunzi kuwa kila sentensi katika ubeti huitwa
mshororo.
(g) Waelekeze wanafunzi kuwa mstari wa mwisho katika ubeti
huitwa kituo.
(h) Waongoze wanafunzi kuandika shairi lenye beti mbili kuhusu
ugonjwa wa malaria kutoka zoezi la 4 ukurasa wa 134 katika
kitabu cha mwanafunzi.
(i) Sahihisha kazi za wanafunzi. Baada ya kusahihisha chagua
shairi lililoandikwa vizuri na wanafunzi walisome darasani
kwa sauti.

110

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 110 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Nane
Haki ya elimu kwa watoto

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi


(a) Kusoma shairi linalohusu haki ya elimu kwa mtoto kwa
kuzingatia usomaji sahihi wa kishairi
(b) Kuzijua na kuzielezea haki za watoto katika jamii

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, picha, bangokitita,


kalamu rashasha.

Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watasoma shairi la Haki ya elimu kwa mtoto
litakalowasaidia kuzijua na kuzielezea haki zao. Pia, watajifunza kutunga
shairi kwa kuzingatia vina na mizani.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 135.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu shairi la Haki ya elimu
kwa mtoto kwa kutumia mazingira halisi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya shairi la Haki ya elimu
kwa mtoto, lililopo katika ukurasa wa 135 – 136 katika
kitabu cha mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila
kutoa sauti.

111

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 111 7/23/21 2:55 PM


(d) Waongoze wanafunzi wasimulie shairi walilolisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la 1 la ufahamu ukurasa
wa 136 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu shairi la haki ya elimu kwa
mtoto. Wakumbushe usomaji sahihi wa shairi kwa kuzingatia
urari wa vina na mizani, na alama za uandishi.
(b) Soma beti moja au mbili kuonesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia kanuni za usomaji wa shairi. Pia, wakumbushe
wanafunzi maana na idadi ya mizani katika kila mstari kwa
kuonesha na kuhesabu mizani hiyo. Vilevile, fundisha maana
ya vina na jinsi ya kuvitambua. Vina ni mfuatano wa silabi
unaojirudiarudia katika mstari wa ubeti yaani mshororo.
(c) Waongoze wanafunzi kutaja vina vya kati na vya mwisho.
(d) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa kila beti
kwa zamu bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha
wanafunzi wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(e) Wakati wanafunzi wanasoma, mwalimu baini dosari
zinazojitokeza na kuzisahihisha. Ukibaini makosa
yanayojirudiarudia simamisha usomaji kwa muda na
kurekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

112

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 112 7/23/21 2:55 PM


Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; urithi, mvuto, sera, maradhi,
balaa, kuli, fani, tamati, ghani na haki.
(b) Nakili zoezi la 2 ubaoni ukurasa wa 137 katika kitabu cha
mwanafunzi na waongoze wanafunzi kusoma maneno ya
kifungu A na maana zake katika kifungu B.
(c) Tumia swali la (i) na la (ii) kama mfano.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 kwenye madaftari
yao.

Somo la 4 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo namna ya kutumia miundo katika sentensi.
(b) Nakili ubaoni miundo yote iliyopo katika zoezi la 3 ukurasa
wa 137 katika kitabu cha mwanafunzi.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma miundo ubaoni.
(d) Toa mifano iliyopo kitabuni na waongoze wanafunzi kutunga
sentensi kwa kutumia miundo hiyo kwa mazungumzo na
andika sentensi hizo ubaoni.
(e) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 la kutunga na
kuandika sentensi nyingine kwa kutumia miundo hiyo katika
madaftari yao.

113

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 113 7/23/21 2:55 PM


Somo la 5 Methali
Hatua za ufundishaji
(a) Rejea ufundishaji wa methali katika sehemu ya utangulizi.
(b) Toa mifano ifuatayo ya kukamilisha methali.
Kikulacho, ……….
Kikulacho, kinguoni mwako

…………., hakivunji chawa.


Kidole kimoja, hakivunji chawa.
Chagua wanafunzi wa kumalizia methali hizi.
(c) Wape wanafunzi nafasi ya kutoa methali wanazozifahamu.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 ukurasa wa 138
katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 6 Mazoezi ya lugha


A. Kuchagua jibu sahihi
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kwa kuandika sentensi ubaoni
ili kuchagua jibu lililo sahihi. Tumia swali la kwanza
kama mfano.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 A ukurasa wa
138-139 katika kitabu cha mwanafunzi.

Majibu 1. B 2. C 3. D 4. A 5. C 6. D

114

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 114 7/23/21 2:55 PM


B. Kuimba wimbo na kuandika haki za mtoto
Hatua za kufundishia
(i) Toa maelezo kuhusu somo utakalofundisha.
(ii) Nakili wimbo ubaoni uliopo katika zoezi la 5 B ukurasa
wa 139 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Imba wimbo huo ubeti wa kwanza na wa pili kwa
mfano.
(iv) Imba pamoja na wanafunzi beti zote mara mbili au tatu.
(v) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 B kwa
kuandika haki za mtoto zilizotajwa katika wimbo.

C. Kutunga sentensi kutokana na jedwali


Hatua za ufundishaji
(i) Nakili jedwali lililopo zoezi la 5 C ukurasa wa 140
katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Tunga sentensi mbili za mfano kutoka katika jedwali.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 C ukurasa
wa 140 katika kitabu cha mwanafunzi.

D. Kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuandika kitendo


kwa kila neno
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya namna ya kubadili majina kuwa
kitendo.
(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi 5 D ukurasa wa 140
katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 D kwenye
madaftari yao.
Majibu 1. lia 2. agiza 3. piga 4. lima 5. jenga 6. soma

115

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 115 7/23/21 2:55 PM


Somo la 7 Vitendawili
Hatua za ufundishaji
(a) Wakumbushe wanafunzi namna ya kutega na kutegua
vitendawili.
(b) Wape nafasi wanafunzi kutega na kutegua vitendawili vyao.
(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 ukurasa 140 katika
kitabu cha mwanafunzi.
Majibu (a) chupa (b) jogoo (c) kivuli (d) macho
(e) kinyonga (f) kibiriti.

Somo la 8 Utungaji
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo kuhusu kanuni na taratibu za utungaji wa shairi
la kimapokeo. (Shairi linalozingatia urari wa vina na mizani)
(b) Andika ubeti ufuatao ubaoni.
Kibeta ni shule yetu, ipo Kishanje sikia,
Makini walimu wetu, darasani fundishia,
Tunza mazingira yetu, afya kuizingatia,
Taaluma zingatia, kuienzi shule yetu.

(c) Wasomee ubeti wa shairi wanafunzi. Kama unaweza waimbie


shairi hili.
(d) Waulize maswali machache ya ufahamu.
(e) Waongoze wanafunzi wataje maneno yanayohusiana na
SHULE YETU na kuyaandika ubaoni. Kumbuka maneno
hayo yawe na miisho ya silabi zinazofanana.
(f) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi zenye silabi nane
kwa kutumia maneno waliyoyataja kwa kuzingatia vina na

116

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 116 7/23/21 2:55 PM


mizani. Waeleze kwa kifupi maana ya kina/vina na mizani,
pia wakumbushe kuweka mkato kila baada ya silabi nane,
na mstari wa mwisho (kituo) waweke nukta.
(g) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 7 ukurasa wa 140
katika kitabu cha mwanafunzi.
(h) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia, alama za
uandishi, mwandiko, nafasi kati ya neno na neno, matumizi
sahihi ya herufi kubwa na urari wa vina na mizani.

117

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 117 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Kumi na Tisa
Kufuata maelekezo ya uelekeo wa pande kuu
nne za dunia
Shughuli za kutendwa na mwanafunzi
(a) Kusoma hadithi ya Safari yetu
(b) Kuelezea maana ya dira
(c) Kutaja pande kuu nne za dunia
(d) Kusikiliza maelekezo yatakayotolewa darasani kuhusu
uelekeo wa pande za dunia na kutekeleza kwa usahihi

Mahitaji vitu halisi, dira, mazingira halisi, picha,


bangokitita, kalamu rashasha.
Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza kufuata maelekezo ya uelekeo
wa pande kuu nne za dunia na namna ya kuyatekeleza ipasavyo baada
ya kusoma hadithi ya Safari yetu.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu maswali yaliyopo katika
kipengele cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa
wa 141.
(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu hadithi ya Safari yetu
kwa kutumia picha ya ukurasa wa 142.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya hadithi ya Safari yetu,
iliyopo katika ukurasa wa 141 – 143 katika kitabu cha

118

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 118 7/23/21 2:55 PM


mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila kutoa sauti.
(d) Waongoze wanafunzi wasimulie hadithi waliyoisoma kwa
maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.
(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu
ukurasa wa 143 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo mafupi kuhusu hadithi ya Safari yetu.
Wakumbushe kanuni na taratibu sahihi za kusoma kwa sauti.
(b) Soma aya moja au mbili kuonyesha mfano mzuri wa usomaji,
kwa kuzingatia kanuni za usomaji.
(c) Waongoze wanafunzi kusoma mmoja mmoja kwa zamu
bila kujali jinsia zao na uwezo wao. Hakikisha wanafunzi
wengi wanapata nafasi ya kusoma.
(d) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza
na kuzisahihisha.
(e) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji
kwa muda na rekebisha makosa hayo.
(f) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji
(a) Fundisha msamiati ufuatao; Kaskazini, Kusini, Mashariki,
Magharibi, shaka, mchoyo, nyenyekea, msitu, zama na
chomoza kwa kutumia mazingira halisi na vitendo.
(b) Nakili zoezi la 2 ubaoni ukurasa wa 144 katika kitabu cha
mwanafunzi.

119

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 119 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kusoma maneno na tumia swali la 1
na la 2 kama mfano.
(d) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 kwenye madaftari
yao.

Somo la 4 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Nakili miundo yote ubaoni iliyopo katika zoezi la 3 ukurasa
wa 144 katika kitabu cha mwanafunzi.
(b) Waongoze wanafunzi kusoma miundo ubaoni na toa mfano
kwa kila muundo kama ilivyooneshwa kitabuni.
(c) Waongoze wanafunzi kutunga sentensi kwa kutumia miundo
hiyo kwa mazungumzo na andika sentensi hizo ubaoni.
(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.
(e) Waongoze wanafunzi kutunga na kuandika sentensi nyingine
katika madaftari yao.

Somo la 5 Mazoezi ya lugha


A. Kukanusha sentensi
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya namna ya kukanusha sentensi.
(ii) Toa mfano ufuatao kwa wanafunzi.
Nyadu alielekea upande wa Mashariki.
Nyadu hakuelekea upande wa Mashariki
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 A ukurasa
wa 145 katika kitabu cha mwanafunzi.

120

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 120 7/23/21 2:55 PM


B. Kuchunguza picha na kujibu maswali
Hatua za ufundishaji
(i) Wakumbushe wanafunzi pande kuu nne za dunia
ambazo ni Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi.
(ii) Waongoze wanafunzi kujadili picha iliyopo katika zoezi
la 4 B ukurasa wa 145 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 B kwa
mazungumzo. Waweza kuwatoa nje ya darasa
wanafunzi na kuongeza maswali ya kuhusu uelekeo
katika shule yako.
(iv) Sikiliza majibu yao na kufanya masahihisho.

C. Kuchagua jibu sahihi


Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze kwa kutoa mfano wa kuchagua jibu lililo
sahihi. Tumia swali la kwanza kama mfano.
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 C ukurasa wa
146 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.

D. Kuchagua neno moja kutoka katika kisanduku kisha


kuweka katika kundi linalostahili
Hatua za ufundishaji
(i) Nakili maneno yaliyopo katika kisanduku katika zoezi
la 4 D ukurasa wa 147 katika kitabu cha mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kusoma maneno hayo na toa
mfano uliopo katika zoezi 4 D.
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 D kwenye
daftari.
Majibu 1. papasi 2. Kusini 3. mbele 4. chomoza
5. ziwani 6.nanasi.

121

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 121 7/23/21 2:55 PM


E. Kuongeza silabi moja katika maneno ili kuunda neno jipya
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya namna ya kuongeza silabi moja katika
neno na kuunda neno jipya.
(ii) Nakili ubaoni maneno yaliyopo katika zoezi la 4 E
ukurasa wa 147 katika kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Waongoze wanafunzi kusoma maneno hayo na toa
mfano uliopo katika zoezi 4 E.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 E kwenye
madaftari yao.
Majibu ya mfano 1. dodoki 2. kibao 3. kulia
4. maua / umia 5. mgomba 6. mmoja.

F. Kuandika wingi wa maneno


Hatua za ufundishaji
(i) Toa mifano ifuatayo ya kuandika wingi wa maneno.
Umoja Wingi
kisu visu
mto mito
(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 F ukurasa wa
147 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.

G. Kukamilisha fumbo kwa kujaza nafasi kwa kwenda


chini na kulia
Hatua za ufundishaji
(i) Toa maelezo ya namna ya kufumbua fumbo walilopewa
kwa kutumia mchoro wa fumbo uliopo kwenye
bangokitita.
(ii) Nakili ubaoni maelekezo ya kwenda chini na kulia,

122

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 122 7/23/21 2:55 PM


yaliyopo katika zoezi la 4 G ukurasa wa 148 katika
kitabu cha mwanafunzi.
(iii) Toa mfano wa kwenda chini wa swali la kwanza kwa
kuuliza swali. Andika jibu sahihi ambalo lina herufi
nne nalo ni DIRA.
(iv) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 G kwenye
madaftari yao.

Somo la 6 Kazi ya kufanya (kazi mradi)


Hatua za ufundishaji
(a) Toa utaratibu wa kufanya ziara halisi.
(b) Mwalimu na wanafunzi mtoke nje ya darasa.
(c) Waongoze wanafunzi kubainisha vitu wanavyoviona mbele,
kushoto, kulia na nyuma mwa darasa lao hatua kwa hatua.
(d) Waongoze wanafunzi kurudi darasani.
(e) Waongoze wanafunzi kuandika vitu walivyoviona upande wa
mbele, kushoto, kulia na nyuma ya darasa katika vikundi.
(f) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 ukurasa 148 katika
kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

123

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 123 7/23/21 2:55 PM


Sura ya Ishirini
Kusoma ngonjera kwa sauti

Shughuli za kutendwa na mwanafunzi

(a) Kusoma ngonjera ya Wajibu wa mtoto katika familia kwa


sauti ya kutamba

(b) Kueleza dhana ya ngonjera na familia

(c) Kutaja wajibu wa mtoto katika familia

(d) Kusoma majigambo kueleza umuhimu wa viungo vya mwili

Mahitaji vitu halisi, mazingira halisi, picha, bangokitita,


kalamu rashasha

Muhtasari
Katika sura hii wanafunzi watajifunza namna ya kutamba ngonjera na
kuandika habari fupi baada ya kusoma ngonjera ya Wajibu wa mtoto
katika familia. Pia, wanafunzi watasoma majigambo na kuweza kueleza
umuhimu wa viungo vya mwili.

Somo la 1 Kusoma kimya


Hatua za ufundishaji
(a) Waongoze wanafunzi kujibu swali lililopo katika kipengele
cha fikiri katika kitabu cha mwanafunzi ukurasa wa 149.

(b) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu wajibu wa mtoto


katika familia kwa kutumia mazingira halisi ya wanafunzi.

124

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 124 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kusoma kimya ngonjera ya Wajibu wa
mtoto katika familia, iliyopo katika ukurasa wa 149 – 151
katika kitabu cha mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole
na bila kutoa sauti.

(d) Waongoze wanafunzi wasimulie ngonjera waliyoisoma


kwa maneno machache na kueleza mafunzo waliyojifunza.

(e) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la kwanza la ufahamu


ukurasa wa 151 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye
madaftari yao.

Somo la 2 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji

(a) Toa maelezo mafupi kuhusu ngonjera ya Wajibu wa mtoto


katika familia. Wakumbushe kanuni na taratibu sahihi za
kusoma ngonjera kwa sauti.

(b) Chagua wahusika Neema, Musa, Asha, Mwalimu na wote


na kuwapa uhusika katika kusoma ngonjera.

(c) Toa muda mfupi kwa kila mhusika kusoma sehemu yake.

(d) Mwalimu na wanafunzi someni ngonjera kwa kuzingatia


uhusika na kanuni za kusoma ngonjera kwa sauti. Mnaweza
kusoma ngonjera hii zaidi ya mara moja.

(e) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza


na kuzisahihisha.

(f) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji

125

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 125 7/23/21 2:55 PM


kwa muda na kurekebisha makosa hayo.

(g) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

Somo la 3 Msamiati
Hatua za ufundishaji

(a) Fundisha msamiati ufuatao; zoa, bweteka, kitako, potoka,


mgomo na mpito.

(b) Nakili zoezi la 2 ubaoni ukurasa wa 152 katika kitabu cha


mwanafunzi.

(c) Waongoze wanafunzi kusoma maneno na kupata maana


ya maneno yote.

(d) Tumia swali la 1 na la 2 kama mfano.

(e) Mwalimu awaongoze wanafunzi kufanya zoezi la 2 kwenye


madaftari yao.

Somo la 4 Nahau
Hatua za ufundishaji

(a) Toa maelezo kuhusu namna ya kuoanisha nahau zilizoko


sehemu A na maana zake katika sehemu B.

(b) Toa mfano kwa kutumia swali la (i) na la (ii) katika zoezi la
3 ukurasa wa 152 katika kitabu cha mwanafunzi.

(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 3 la kuoanisha sehemu


A na B.

126

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 126 7/23/21 2:55 PM


Majibu i. (i) ii. (h) iii. (f) iv. (j) v. (e) vi. (d) vii. (c) viii. (b)
ix. (a) x. (g)

Somo la 5 Miundo
Hatua za ufundishaji
(a) Nakili ubaoni miundo yote iliyopo katika zoezi la 4 ukurasa
wa 153 katika kitabu cha mwanafunzi.

(b) Waongoze wanafunzi kusoma miundo ubaoni na toa mfano


kwa kila muundo kama ilivyooneshwa kitabuni.

(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 4 F ukurasa wa 153


kwa mazungumzo na andika sentensi hizo ubaoni.

(d) Angalia usahihi wa sentensi walizotunga wanafunzi.

(e) Waongoze wanafunzi kutunga na kuandika sentensi nyingine


kwenye madaftari yao.

Somo la 6 Methali
Hatua za ufundishaji
(a) Toa maelezo ya namna ya kukamilisha methali.

(b) Toa mifano ifuatayo:

…………., ndio mwendo.


Pole pole, ndio mwendo.

Kuishi kwingi,……………..
Kuishi kwingi, ni kuona mengi.

127

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 127 7/23/21 2:55 PM


(c) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 5 la kukamilisha
methali ukurasa 153 katika kitabu cha mwanafunzi.

Somo la 7 Mazoezi ya lugha


A. Kuchagua jibu sahihi

Hatua za ufundishaji

(i) Toa maelezo kuhusu somo utakalolifundisha.

(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 A ukurasa


wa 154 katika kitabu cha mwanafunzi.

B. Kuchunguza picha na kubaini kazi zinazomfaa mtoto


na kuandika sababu kwanini zinamfaa

Hatua za ufundishaji

(i) Waongoze wanafunzi kufanya majadiliano ya picha


1-5 zilizopo katika zoezi la 6 B ukurasa 155 katika
kitabu cha mwanafunzi.

(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 B ukurasa


155 katika kitabu cha mwanafunzi.

128

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 128 7/23/21 2:55 PM


C. Kuandika neno lenye maana sawa na neno lililopigiwa
mstari

Hatua za ufundishaji

(i) Toa maelezo kuhusu maneno yenye maana sawa


(visawe). Unaweza kutumia mchezo wa Nyama nyama.

(ii) Toa mfano uliopo katika zoezi la 6 C ukurasa wa 156


katika kitabu cha mwanafunzi.

(iii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 C kwenye


madaftari yao.

Majibu 1. angushwa 2. hodari 3. nyati 4. ngoja


5. panda 6. nyweshea 7. tunza 8. kubali.

D. Kuandika kinyume cha maneno

Hatua za ufundishaji

(i) Waongoze wanafunzi kuelewa dhana ya kinyume kwa


kuonesha mfano kwa kutumia picha na vitu halisi.

(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 D ukurasa wa


156 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari
yao.

129

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 129 7/23/21 2:55 PM


E. Kuandika umoja na wingi

Hatua za ufundishaji

(i) Toa maelezo ya kubadili umoja kuwa wingi na wingi


kuwa umoja. Zingatia silabi zinavyobadilika katika
neno.

(ii) Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la 6 E ukurasa


wa 156 - 157 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye
madaftari yao.

Somo la 8 Utungaji
Hatua za ufundishaji

(a) Toa maelezo jinsi ya kutumia picha zisizo na mfululizo


kufanya utungaji.

(b) Ongoza majadiliano kuhusu picha ya 1- 6 zilizopo katika


ukurasa wa 157-159 katika kitabu cha mwanafunzi.

(c) Waongoze wanafunzi kumalizia habari waliyopewa katika


zoezi la 7 ukurasa 157 katika kitabu cha mwanafunzi kwa
kuandika kwenye madaftari yao.

(d) Sahihisha kazi za wanafunzi kwa kuzingatia wajibu wa


mtoto katika familia, alama za uandishi, mwandiko, nafasi
kati ya neno na neno na matumizi sahihi ya herufi kubwa.

130

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 130 7/23/21 2:55 PM


Somo la 9 Kusoma kimya
Hatua za ufundishaji

(a) Ongoza mazungumzo mafupi kuhusu majigambo ya viungo


vya mwili.

(b) Waongoze wanafunzi kusoma kimya majigambo ya viungo


vya mwili, yaliyopo katika ukurasa wa 160 – 161 katika
kitabu cha mwanafunzi bila kufuatisha kwa kidole na bila
kutoa sauti.

(c) Waongoze wanafunzi wasimulie kwa maneno machache


majigambo waliyoyasoma na kueleza mafunzo waliyojifunza.

(d) Waongoze wanafunzi kujibu zoezi la 8 la ufahamu ukurasa


wa 162 katika kitabu cha mwanafunzi kwenye madaftari yao.

Somo la 10 Kusoma kwa sauti


Hatua za ufundishaji

(a) Toa maelezo mafupi kuhusu majigambo ya viungo vya


mwili. Wakumbushe kanuni na taratibu sahihi za kusoma
majigambo kwa sauti.

(b) Chagua wahusika macho, pua, sikio, mdomo, kichwa, kifua


na shingo na kuwapa uhusika katika kusoma majigambo
hayo.

(c) Toa muda mfupi kwa kila mhusika kusoma sehemu yake.

(d) Waongoze wanafunzi kusoma majigambo kwa kuzingatia

131

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 131 7/23/21 2:55 PM


uhusika na kanuni za kusoma majigambo kwa sauti. Mnaweza
kusoma majigambo haya zaidi ya mara moja.

(e) Wakati wanafunzi wanasoma, baini dosari zinazojitokeza


na kuzirekebisha.

(f) Ukibaini makosa yanayojirudiarudia simamisha usomaji


kwa muda na kurekebisha makosa hayo.

(g) Wanafunzi warudie kusoma kadiri wanavyopata nafasi.

132

KISWAHILI STD 4 _ KIONGOZI CHA MWALIMU.indd 132 7/23/21 2:55 PM

You might also like