Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 42

‫في أخبار مولد خير البشر‬

‫وما له من اخالق وأوصاف وسير‬

CHANU CHA
DURI
MAELEZO YA MAZAZI YA BINADAMU BORA ZAIDI
NA YANAYOHUSIANA NA YEYE KUTOKAMANA NA
TABIA, SIFA NA SERA YAKE

IMAM ALI BIN MUHAMMAD BIN HUSEIN AL-HABSHY

(ALLAH AMRIDHIE)

‫بالسواحلية‬
KISWAHILI
2018/0441
UTANGULIZI WA MFASIRI

Shukurani za dhati ni za Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuwa waumini na wapenzi wa


bwana Mtumi Muhammad (Rehma na amani zimshukie). Twamshukuru na twamuomba
atuthubutishe katika mahabba ya bwana wetu Mtumi Muhammad (Rehma na amani
zimshukie) na twamuomba atupambe kwa tabia zake njema, atujaalie nikatika watu
watakaonyweshwa na Mtumi wetu (Rehma na amani zimshukie) kutokamana na kauthar
yake kinywaji ambacho hatutosikia tena kiu baada ya hapo. Aatupatie shafaa ya Mtumi
wetu Muhammad (Rehma na amani zimshukie) siku ya Qiyama, atupatie baraka zake sisi
na wazee wetu na watoto wetu na waja wema. Ewe mola nakuomba umteremshie rehma
na amani bwana wetu Muhammad na jamaa zake na swahaba zake na wafuasi wao na
kila aliemwema, ututangamanishe nasisi na watakaokuja baada yetu, kwa rehema zako
ewe mwenye kuwarahamu wanaorahamu.

Ama baada ya himdi na swala na salamu.. hakika kueneza na kutangaza sifa na sera ya
kipenzi cha Mola (Rehma na amani zimshukie) ni katika mambo muhimu sana katika dini
yetu. Khaswa kwakua tumeamrishwa kumuiga Mtumi wetu Muhammad (Rehma na mani
zimshukie). Kueneza na kuzieleza sifa za bwana wetu inasaidia kukuza kizazi chenye
malezi mazuri na kuweza kujipamba na tabia mzuri za bwana wetu Muhammad (Rehma
na amani zimshukie) na kuwafanya wawe wataweza kumfuata na kumpenda. Kule kuiskia
na kuisoma na kuiregelea sera ya Mtumi wetu Muhammad (Rehma na mani zimshukie)
mara kwa mara ndio unapata ladha ya sifa na tabia njema, na ukipata ladha ndio
inapatikana kufungamana na hizo tabia njema ukafuza nazo na hatimae kupata mahabba
ya mwenye izzi Mungu atukushieo na radhi zake ambazo sote twazikimbilia.
Kwa ajili ya hayo yote na mengineyo, wenye busara na hikmah walifahamu na wakawa
wakimbila kutunga vitabu vya sera ya Mtumi Muhammad (Rehma na mani zimshukie)
kwa mifumo tafauti tafauti na kusomwa kwa njia tafauti tafauti. Watu tafauti wachaji
Mungu, wasomi na wenye ufasaha kilammoja akajaribu kutunga, kumueleza na kumsifu
kipenzi cha mwenye izzi Mungu atukushieo, na mbele yetu tuko na kimoja kati ya tungo
hizo, na katika vitabu ambavyo vimepata qabuli kikawa chasomwa sehemu mbalimbali
ulimwenguni, sikengine ni “Sumtu Al-Durar” (Chanu cha duri) yani chombo kilichojaa
vilivo na thamaani.

Hichi ni kitabu kilichotungwa na mmoja wa wanazuoni wakubwa, mcha Mungu, mmoja


kati ya waliomsifu na kumueleza Mtumi Muhammad (rehma na amani zimshukie) kwa
vizuri katika uhai wake wote. Nae simwengine ni Imam Ali bin Muhammad bin Husein Al-
Habshy, mtoto wa aliekua mufti wa Makkah, ambae ananasaba ya kisharifu, aliezaliwa
katika mji wa Qasam Yemen siku ya Ijumaa, 24/mfungo mosi/1259H na kufariki katika
mji wa Seiyun Yemen 20/mfungo saba/1333H.

1|Page
Mwenyewe alikua akifanya haflah kubwa sana ya maulidi inayohudhuriwa na watu wengi
sana, taqreeban ndio kongamano linalohudhuriwa na watu wengi zaidi katika jimbo la
Hadhramoot Yemen katika mji wa Saiun, maulidi yanayokua Alkhamisi yamwisho katika
mwezi wa Mfungosita uliotukuka kwa kuzaliwa kiumbe bora zaidi ulimwenguni, na
hatimae walioko mbali wakaruhusiwa na yeye mwenyewe wayasome popote pale walipo
kama vile mashariki ya bara Afrika na mashariki ya bara Asia na kwengineko.

Afrika mashariki alimpatia ijaza (Ruhusa) Alhabib Swaleh bin Alwy Jamalulleyl asome
baada ya kupata sifa za maulidi yanayosomwa kule Seiyun, Yemen na usafiri ulikua tabu
wakati huo haukua mwepesi, akampatia ijaza kupitia tungo alizomtungia akimwambia:

Chukua ewe kipenzi changu kutokamana na maneno yangu duri

Chukua na uwabainishie maana yake watakaohudhuria…Mpaka mwisho wa qaswida

Ndipo nae akaanzisha maulidi yake katika mji wa Lamu, nae akawaruhusu wanafunzi
wake waliombali wasome popote pale walipo kama vile Mambrui, Malindi na
kwengineko.

Kwakua maulidi haya yanasomwa sana upande wa Afrika mashariki na pengine wengine
wanapitwa na maana au ufahamu ya baadhi ya maneno, ndipo nikaazimia baada ya
ushauri wa babangu mzazi Alhabib Muhsin sayyid Ali Badawy (Mungu amueke) niufasiri
utungo huu kwa lugha ya Kiswahili ili iyenee faida kwa waislamu na wasiokua waislamu,
wanaoifahamu lugha ya kiarabu na wasioifahamu.

Nimejaribu kufasiri kwa lahajah ya Kiswahili sanifu (Standrad) inayofahamika na wengi


ela baadhi ya vilima ambavyo havitafsiriki Kiswahili ela kwa lahjah ya Kiamu.
Kama alivyosema Alhabib Ahmad bin Muhammad Al-Ahdal “lugha ya kiarabu haifasiriki
sawasawa Kiswahili ela kwa lahjah ya Kiamu”

Pia nimelazimika kuongeza maneno machache kwa lengo la kutaka kufafanua na


kufahamisha zaidi, na nimeweka nyongeza hizo kati ya alama mbili za [].

Vilevile sikumtaja Mtumi Muhammad (rehma na amani zimshukie) ela nimemtakia rehma
na Amani, kinyume na asili huku nikiwa nimeweka ndani ya alama mbili za ().

2|Page
Mwisho namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie kazi hini iwe itakua na ikhlaas ndani yake ili
nipate thawabu mimi na kila aliekuwa sababu kukamilika kazi hini, kwa kila atakaefaidika
kupitia tafsiri hini kumjua zaidi Mtumi watu (Rehma na amani zimshukie) na hatimae
kumpenda na kumfuata. Thawabu pia ziwaendee wazazi na mababu zangu wote
waliotangulia mbele za haki.

Pia namuomba yoyote atakaeona kosa lolote afanye bidii kunijulisha niweze kurekibisha,
kwa njia yoyote ama kupitia barua pepe kwa anwani hini: Fukheyr@yahoo.com

Abubakar Muhsin Sayyid Ali

22/Mfungotano/1440H

3|Page
UTANGULIZI WA MSAHIHISHAJI

Namshukuru Mwenyezi Mungu atukushieo kuijaalia ile ndoto niliyokua nayo kwa muda
mrefu sana; leo hini imekuwa kweli. Mungu amemuafiqia mwanangu “Fakhruddyn”
Abubakar Muhsin Sayyid Ali Badawy baada ya kumshiria akifasiri kitabu cha “sumtu
ddurar” Chanu cha duri. Kitabu ambacho chasomwa kwa wingi ulimwengu mzima na huku
kwetu Afrika mashariki, na amekifasiri kwa uzuri na kwa lugha ya kufahamika na wengi.

Namuomba mwenye izzi Mungu ajaalie tafsiri hini iwe itakua na manufaa kwa alieifasiri
na kila atakaeisoma, amuongezee juhudi pamoja na kumkunjulia wakati aliefasiri ili aweze
kufasiri na zengine, faida ya tafsiri hini iwaenee wote, kwani yeye ndie mueza wa hilo…

Ewe Mola mswalie Mtumi wako Muhammad (Rehma na amani zimshukie) na jamaa zake
wote na swahaba zake na waliokuja baada ya wao, uinue zaidi utajo wa Bwana wetu
Muhammad (Rehma na amani zimshukie) na utupambe na tabia zake njema, utuzidishie
elimu na uchaMungu, ujaalie vijana wetu wawe watakua ni vituzo vya macho yetu hapa
duniani na kesho akhira, kwa rehma zako Ewe mwingi wa kurahamu.

Muhsin sayyid Ali Badawy

28/Mfungotano/1440H

4|Page
SHANGILIO LA HABIB ALI AL-HABSHI (MUNSWIB)

Hussein Assad Al-Husseiny

28/Mfungonne/1441H

5|Page
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Hussein Assad Al-Husseiny

28/Mfungonne/1441H

6|Page
7|Page
ّ
)‫مدخل الصالة على النبي (صلى هللا عليه وسلم‬
KIINGILIO CHA SWALA ZA MTUMI (REHMA NA AMANI ZIMSHUKIE)

َ َ َ َ
ٍ‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** أشرف بدر في الكون اشرق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Mwezi bora zaidi uliochomoza ulimwenguni
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** أكرم داع يدعوا إلى الحـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Mbora wa walinganizi anaeelingania haki
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** املصطفى الصٍادق املصدٍق‬ ‫ٍيا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Mswafiwa, Mkweli alieswadikiwa
ً َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** احلى الورى منطقا واصدق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Mzuri wa viumbe kwa matamshi na Mkweli
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** افضل مـن بالتقـى تحقٍـق‬
ٍ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Mbora ambae amekolea na ucha Mungu
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** من بالسخا و الوفـاء تخلٍـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Aliejipamba kwa ukarimu na utekelezaji ahadi

ٍ
8|Page
ٍ

ٍ
َ َ َ َ
ٍ‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** واجمع من الشٍمل ما تف ٍـرق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Na ulijumuishe tangamano liliopambanuka
َ َ َ َ
ٍ‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** و اصلح وسهٍل ما قد تع ٍـوق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Usuluhishe na ufanye wepesi yalyiotatiyana
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** و افتح من الخير كلٍ مغلـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Na ufungue ya kheri kila lililofungika
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** وآلـه ومـن بالنٍبـي تعلٍـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Na ali zake na kila aliejifungamanisha na Mtumi
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** وآله ومن للحبيـب يعشـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Na ali zake na kila anae mpenda Mtumi
َ َ َ َ
‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** ومـن بحبـل النٍبـي توثٍـق‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Na kila alieshikamana na kamba ya Mtumi
َ َ َ َ َ َ َ َ
ٍ َ ‫ص ِّـل ٍَع ٍليٍ ٍِّـه ٍَو‬
‫سلٍِّـم‬ ‫ص ِّـل َعلى ُم َح َّمدٍ *** يا ر ِّب‬ ‫يا ر ِّب‬
Ewe Mola! Mswalie Muhammad
Ewe Mola mrehemu na umpe amani

---------------

9|Page
‫ك‬
‫ديَ َ‬ ‫عل َ ْي َ‬
‫ك َويَ ْه ِ‬ ‫ه َ‬
‫م َت ُ‬
‫ع َ‬
‫م نِ ْ‬ ‫ما تَأَ َّ‬
‫خ َر َو ُيتِ َّ‬ ‫و َ‬‫ك َ‬
‫ذنبِ َ‬ ‫من َ‬ ‫م ِ‬ ‫د َ‬ ‫ما تَ َ‬
‫ق َّ‬ ‫ك الل َّ ُ‬
‫ه َ‬ ‫مبِينًا * لِِّيَ ْغ ِف َر ل َ َ‬ ‫ك َ‬
‫ف ْتحًا ُّ‬ ‫ح َنا لَ َ‬ ‫إِن َّا َ‬
‫ف َت ْ‬
‫زيزًا *‬ ‫صرًا َ‬
‫ع ِ‬ ‫ك الل َّ ُ‬
‫ه نَ ْ‬ ‫ص َر َ‬
‫قيمًا * َو َين ُ‬ ‫ص َراطًا م ْ‬
‫ُّس َت ِ‬ ‫ِ‬

‫حيم‬
‫ين َر ُءوف َر ِ‬ ‫م ْؤ ِ‬
‫منِ َ‬ ‫علَ ْيك ْ‬
‫ُم بِا ْل ُ‬ ‫حرِيص َ‬
‫ُّم َ‬ ‫ما َ‬
‫عنِت ْ‬ ‫علَ ْي ِ‬
‫ه َ‬ ‫عزِيز َ‬
‫ُم َ‬ ‫ن أَ ْن ُف ِ‬
‫سك ْ‬ ‫م ْ‬
‫سول ِ‬
‫ُم َر ُ‬
‫جا َءك ْ‬ ‫لَق ْ‬
‫َد َ‬

‫م‬
‫ظي ِ‬ ‫ش ا ْل َ‬
‫ع ِ‬ ‫و َربُّ ا ْل َ‬
‫ع ْر ِ‬ ‫ه َ‬
‫و ُ‬ ‫ك ْل ُ‬
‫تۖ َ‬ ‫و َّ‬ ‫علَ ْي ِ‬
‫ه تَ َ‬ ‫وۖ َ‬
‫ه َ‬ ‫ه ََل إِ َٰلَ َ‬
‫ه إِ ََّل ُ‬ ‫ي الل َّ ُ‬
‫سبِ َ‬
‫ح ْ‬
‫ُل َ‬ ‫ول َّ ْوا َ‬
‫فق ْ‬ ‫َ‬
‫ف ِإن تَ َ‬

‫َسلِيمًا‬ ‫سلِ ِّ ُ‬
‫موا ت ْ‬ ‫ه َو َ‬ ‫صلُّوا َ‬
‫علَ ْي ِ‬ ‫م ُنوا َ‬
‫ين آ َ‬
‫ذ َ‬ ‫ي يَا أَيُّ َ‬
‫ها ال َّ ِ‬ ‫صلُّونَ َ‬
‫علَى ال َّن ِب ِّ ِ‬ ‫ه ُي َ‬ ‫مالئِ َ‬
‫ك َت ُ‬ ‫إِنَّ الل َّ َ‬
‫ه َو َ‬

‫‪10 | P a g e‬‬
‫الفصل ألاول‬
MLANGO WA KWANZA
* ‫الحمد هلل القوي سلطانه * الواضح برهانه * المبسوط في الوجود كرمه وإحسانه‬

Shukurani ni za Mola mwenye ufalume wenye nguvu, ambae hoja zake ziko wazi,
ambae ukarimu wake na ihsani zake kwa viumbe wake zimekunduka *

‫حكمه * وطوى عليها علمه * وبسط لهم من فائض المنة ما جرت‬ِ ‫الخلق ل‬
َ َ َ‫خل‬
‫ق‬ َ * ‫تعالى مجده وعظم شانه‬
* ‫به في أقدار القسمة‬

Umetukuka utayo wake na nikubwa kila jambo lake, Ameumba viumbe kwa hikmah,
akaficha ndani yake ujuzi wake, na akawakunjulia kutokamana na vipawa vyengi,
vipawa alivyopanga kuwagawanyia kulingana na alivyoqadariya *

‫فأرسل إليهم اشرف خلقه واجل عبيده رحمة * تعلقت إرادته األزلية بخلق هذا العبد المحبوب * فانتشرت‬
* ‫آثار شرفه في عوالم الشهادة والغيوب‬

Akawatumilizia mbora wa viumbe vyake na mtukufu wa waja zake kwa rehma,


yalifungamana matakwa yake ya tangu azali kumuumba huyu mja mpendwa, zikaenea
alama za utukufu wake katika ulimwengu wa unao’onekana na uliofichamana *

‫فما أجل هذا المن الذي تكرم به المنان * وما أعظم هذا الفضل الذي برز من حضرة اإلحسان * صور ًة كامل ًة‬
*‫هيكل محمود * فتعطرت بوجودها أكناف الوجود * وطرزت برد العوالم بطراز التكريم‬
ٍ ‫ظهرت في‬

Ni wema wa hali gani wa zema ambazo ametukirimu nazo Mola mwingi wa kutoa, na ni
ukubwa ulioje wa fadhila ambazo zimetoka kwenye ukumbi wa Ihisani, sura kamili
zilizodhihiri katika umbile la kushukuriwa, ikaenea arufu njema kwa kupatikana kwake
pembe zote za ulimwengu, na likapambika shali la malimwengu kwa marumaru za
ukarimu *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

11 | P a g e
‫الفصل الثاني‬
MLANGO WA PILI
* ‫تجلى الحق في عالم قدسه الواسع * تجليا قضى بانتشار فضله في القريب و الشاسع‬

Amedhihiri Mola katika ulimwengu wa utukufu wake uliopanuka * kudhihiri kuliohukumu


kuenea kwa fadhila zake kwa alie karibu na mbali *

* ‫فله الحمد الذي ال تنحصر افراده بتعداد * و اليمل تكراره بكثرة ترداد‬

Shukurani ndake yeye, shukurani ambazo hazidhitiki kwa hisabu, wala hazichokeshi
kuzirudia mara kwa mara *

* ‫حيث ابرز من عالم اآلمكان * صورة هذا األنسان * ليتشرف بوجوده الثقالن * وتنتشر اسراره في األكوان‬

[Twamshukuru] kwa kulichomoza katika ulimwengu, umbile la huyu binadamu, ili


washarifike kwa kwa kupatikana kwake majini na binadamu, na ienee siri zake
ulimwengu mzima *

* ‫فما من سر اتصل به قلب منيب * اال من سوابغ فضل هللا على هذا الحبيب‬

Hakuna siri iliyofungamana na moyo wa mtu alietubia, ela ni kutokamana na kuenea


kwa fadhila za Mola juu ya huyu kipenzi cha Mungu *

‫م األنـام نـواال‬
َّ ‫ب عـ‬
ٍ ‫ب سروره قـد توالـى = بحبي‬
ٍ ‫يا لقل‬

Bishara njema nda moyo ambao umetawaliwa na furaha


kumfurahia kipenzi ambae zipowa zake zimewaenea viumbe wote

‫ل من شرف الوجود بنور = غمر الكون بهجـ ًة وجمـاال‬


َّ ‫ج‬

ametukuka Mola ambae ameusharifisha ulimwengu kwa nuru ya mtumi


aliefinika na kueneza ulimwengu furaha na uzuri

‫قد ترقى في الحسن اعلى مقا ٍم = وتناهى في مجـده وتعالـى‬

Amepaa katika uzuri daraja ya juu kabisa


na amefika kileleni katika utukufu wake na ametukuka

‫الحظته العيون فيما اجتلتـه = بشراَ كامال َ يزيح الضـالال‬

Yamempeleleza macho katika zilizo wazi yakaona kua ni


binadamu alokamilika amabae huondoa upotofu

‫ه و كمـاال‬
ِ ‫ة في شؤونـ‬
َ ‫وهو من فوق علم ما قدرتـه = رفع‬

Naye yuko juu zaidi ya yalivyomfahamu macho


mtukufu katika mambo yake yote na ni mkamilifu
12 | P a g e
* ‫فسبحان الذي ابرز من حضرة االمتنان * ما يعجز عن وصفه اللسان * ويحار في تعقل معانيه الجنان‬

Utakatifu wa mawi ni wa Yule ambae amemleta kutoka katika hadhira zake za wema,
akamleta kiumbe ambae ulimi umelemewa kumsifu, na akili zimetahayari kumfahamu *

‫انتشر منه في عالم البطون والظهور * ما مالء الوجود الخلقي نور * فتبارك هللا من اله كريم * بشرتنا اياته‬
‫ريص عليكم بالمؤمنين‬
ٌ ‫ عزي ٌز عليه ما عنتم ح‬،‫ل من انفسكم‬ ٌ ‫في الذكر الحكيم * ببشارة {لقد جاءكم رسو‬
* }‫رؤوفٌ رحيم‬

Imeenea kutokamana nae mbinguni na ardhini nuru, nuru ambayo yajaza mbingu na
ardhi, basi utukufu ni wa Mola Mkarimu, Mola ambae zimetubashiria sisi aya zake katika
kitabu chake kitakatifu chenye hikima kwa bishara ya neno lake alietukuka
{Amewajieni mtumi kutokamana na nyinyi, amabae anaona uzito kwa yanayowakuta,
mwenye pupa juu yenu, na kwa waumini ni mpole na mwenye sikitiko} *

* ‫ط مستقيم‬
ٍ ‫ي الى صرا‬
َ ‫فمن فاجأته هذه البشارة و تلقاها بقلبٍ سليم فقد هد‬

Hivo yoyote atakaefikiwa na bishara hii na akaipokea kwa moyo mkunjufu, basi mtu
huyo atakua ameongoka njia ya sawa *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل الثالث‬
MLANGO WA TATU
* ‫و اشهد ان ال اله اال هللا وحده ال شريك له * شهادة تعرب بها اللسان * عما تضمنه الجنان‬
* ‫من التصديق بها واالذعان‬

Na nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi yakwamba hapana Mola anaepaswa
kuabudiwa kwa haqqi illa Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wake, kukiri
kunakobainishwa na ulimi, kwa yaliomo ndani mwa moyo, kwa kusadikisha shahada hilo
na kulikubali *

* ‫تثبت بها في الصدور من اإليمان قواعده * و تلوح على اهل اليقين من سر ذلك األذعان والتصديق شواهده‬

Hukita kwa shahada hilo katika nyoyo misingi ya imani, na hudhihiri juu ya watu wenye
yaqini kutokamana na siri ya kukubali na kusadikisha huko alama za Imani hio*

13 | P a g e
* ‫واشهد ان سيدنا محمدا ً العبد الصادق في قوله وفعله * و المبلغ عن هللا ما امره بتبليغه لخلقه من فرضه ونفله‬

Na nakiri kwa moyo pamoja na kibaini kwa ulimi kwamba bwana wetu Muhammad ni
mja mkweli katika maneno yake na matendo yake, na nimwenye kufikisha kutoka kwa
Mwenyezi Mungu yale aliyomuamrisha kuyafikisha kwa waja zake kutokamana na ya
faradhi na ya sunnah *

* ً‫للعالمين بشيراً ونذيراً * فبلغ الرسالة * و ادى األمانة * وهدى هللا به من األمة بشراً كثيرا‬
ً ‫عب ٌد ارسله هللا‬

Mja aliemtumiliza Mwenyezi Mungu kwa viumbe wote hali yakua ni mwenye kubashiri
mema na kuogopesha maovu, akafikisha ujumbe, na akatekeleza amana, na Mungu
akaongoza kupitia yeye viumbe wengi *

* ً‫فكان في ظلمة الجهل للمستبصرين سراجاً وقمراً منيرا‬

Akawa ni mwangaza katika kiza cha ujinga kwa wanao taka mwangaza na akawa ni
mwezi wenye nuru *

* ‫ة انتشر سرها في البحر و البر‬


ٍ ‫ة تكرم هللا بها على البشر * و ما اوسعها من نعم‬
ٍ ‫فما اعظمها من من‬

Ni zema zikubwa ziloje kutokamana na zema ambazo Mwenyezi Mungu amewakirimu


binadamu, na ni neema panufu kiasi gani kutokamana na neema ambazo kwamba
zimeenea siri zake katika bara na bahari *

‫اللهم صل وسلم باجل الصلوات واجمعها و ازكى التحيات و اوسعها * على هذا العبد الذي وفى بحق‬
* ‫ه غاية اإلقبال‬
ِ ‫العبودية * و برز فيها في خلعة الكمال * و قام بحق الربوبية في مواطن الخدمة هلل و اقبل علي‬

Ewe Mola mtakie rehma na amani rehema zilo kubwa na kundufu na salamu takatifu na
panufu juu ya huyu mja ambae ametekeleza hakki ya utumi, na akadhihiri katika utumi
huo katika vazi la ukamilifu na akatekeleza wajibu wa kumuabudu Mola wake katika kila
nyanja, na akamlekea yeye upeo wa kumlekea *

* ‫صال ًة يتصل بها روح المصلي عليه به * فينبسط في قلبه نور سر تعلقه به وحبه * و يكتب بها بعناية هللا في حزبه‬

Swala ambayo itafungamana ruhu ya mwenye kumswalia, itandae katika moyo wake
nuru ya siri ya kufungamana nae na mapenzi yake, na aandikwe kwa swala hiyo kwa
inaya ya Mwenyezi Mungu katika kundi lake *

14 | P a g e
‫وعلى اله وصحبه الذين ارتقوا صهوة المجد بقربه * و تفيأوا ظالل الشرف األصلي بوده وحبه * و ما عطر‬
* ‫األكوان بنشر ذكراهم نسيم‬

Pia Mungu awarahamu Jamaa za Mtumi na Swahaba zake ambao walikwea kilele cha
utukufu kwa sababu ya kua karibu na Mtumi, wakajitaza kwenye kivuli cha utukufu wa
asili kwa kite cha Mtumi na mahaba yake, mwida ukienea ulimwengu kwa kuenezwa
utayo wao kwa upepo uliolaini *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل الرابع‬
MLANGO WA NNE
* ‫ فلما تعلقت ارادة هللا في العلم القديم * بظهور اسرار التخصيص للبشر الكريم * بالتقديم والتكريم‬،‫اما بعد‬

Ama baada ya himdi na swala na salamu… ilipofungamana matakwa ya Mwenyezi


Mungu katika ujuzi wa tangu, kutaka kudhihirisha siri alizomkhusu kiuimbe kitukufu,
kwa kutangulizwa na kukirimiwa * ilipita uwezo uliowazi,
kwa neema iliyokunjufu na zema za kuenea *
* ‫نفذت القدرة الباهرة * بالنعمة الواسعة و المنة الغامرة‬

Likapasuka yai lenye maumbile, katika ulimwengu mkunjufu mkubwa, umbile lenye uzuri
wakushuhudiwa kwa macho, lilokusanya sifa za ukamilifu wazi na uzuri ulokamilika wenye
kupendeza *
‫المطلق و‬
ِ ‫ل‬
ِ ‫حاو لوصف الكما‬
ٍ * ‫ل مشهو ٍد بالعين‬ٍ ‫فانفلقت بيضة التصوير * في العالم المطلق الكبير * عن جما‬
* ‫الحسن التا ِم و الزين‬
ِ
Ukahamahama huo uzuri wenye Baraka, katika mitulinga mitukufu na vizazi *
* ‫ب ضمه * اال و تمت عليه من هللا النعمة‬
ٍ ‫فتنقل ذلك الجمال الميمون * في األصالب الكريمة والبطون * فما من صل‬

Hakuna uti wa mgongo uliombeba mtumi Muhammad, illa ulikamilishiwa -kwa barka za
Mtumi- neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu *
* ‫م الذي يتنقَّل في بروجه * ليتشرف به موطن استقراره و موضع خروجه‬
ُّ ‫فهو القمر التا‬

Yeye ni mwezi uliotimia unaozunguka katika buruji zake, ili ishafirike kwa ajili yake sehemu
itakapotua na pahali atakapotoka *

15 | P a g e
* ‫سر هذا النور ما اظهرت * و خصصت به من خصصت‬
ِ ‫وقد قضت األقدار األزلية بما قضت و اظهرت من‬

Na imehukumu qadari ya tangu ilivohukumu, na ikadhihirisha kutokamana na siri ya nuru


hini kilichodhihirisha, na akakhusishwa kwa nuru hiyo aliekhusishwa *
* ‫فكان مستقره في األصالب الفاخرة * واألرحام الشريفة الطاهرة‬

Ikawa mashukio yake ni katika mitulinga ya fakhari, na zizazi zitukufu ziliotwahara *


* ‫حتى برز في عالم الشهادة بشراً ال كالبشر * و نوراً حير األفكار ظهوره و بهر‬

Mpaka akadhihiri katika ulimwengu wa kushudiwa -ulimwenguni- binanadamu amabae


hafanani na binadamu mwengine, na nuru iliyotahayarisha na kushangaza akiliza binadamu
kudhihiri kwake *
* ‫فتعلقت همة الراقم لهذه الحروف* بإن يرقم في هذا القرطاس ماهو لديه من عجائب ذلك النور معروف‬

Ikafungamana himma ya mwenye kuandika hizi herufi, aandike katika kurasa aliyonayo
kutokamana na maajabu ya nuru hiyo kwa wema *
‫ف ذلك الموصوف * تشويقاً للسامعين * من خواص المؤمنين‬ ِ ‫و إن كانت األلسن ال تفي بعشر معشارِ اوصا‬
* ‫* و ترويحا ً للمتعلقين بهذا النور المبين‬

Na ingawaje ndimi hazitoshei hata fungu la kumi katika kumi [uchache] wa sifa za msifiwa,
naandika tu kutia shauku kwa wenye kuyasikia, kutokamana na waumini khaswa, na
naandika kwa lengo lakuwapumbaza waliofungamana na hini nuru iliyowazi *
‫و إال فانى تعرب األقالم * عن شؤن خير األنام * ولكن هزني الى تدوين ما حفظته من سير اشرف المخلوقين * و‬
* ‫م العالمين‬
َّ ‫ما اكرمه هللا به في مولده من الفضل الذي ع‬

Lau si hivo ni vipi zitaeleza vizuri kalamu, kutokamana na mambo ya mbora wa viumbe,
lakini amenihimiza mimi kuandika kile nilichokihifadhi kutokamana na sera ya kiumbe
kitukufu, na yale ambayo mwenyezi Mungu amemkirimu kwayo katika mazazi yake
kutokamana na fadhila ambazo zimewaenea viumbe wote *
‫عج‬
ِ ‫و بقيت رايته في الكون منشورة على مر األيام والشهور والسنين * داعي التعلق بهذه الحضرة الكريمة * وال‬
* ‫التشوق الى سماع اوصافها العظيمة‬

Na imebaki bendera yake yapepea katika ulimwengu juu kupitia masiku na nyezi na miaka,
kilichonipelekea kuandika sifa za mtumi ni kwa sababu ya tangamano lakufungamana na
huyu mtukufu mwenye cheo, na msukumo wa shauku ya kuskiza sifa zake tukufu *

*‫ن بروحِ ذلك النعيم‬


ِ ‫ل هللا ينفع بها المتكلم والسامع * فيدخالن في شفاعة هذا النبي الشافع * و يتروحا‬
َّ ‫و لع‬

Na asaa Mwenyezi Mungu akamnufaisha atakaesoma na atakaeskia, wakaingia katika shafaa


ya huyu Mtumi mwenye kushufaiya, na wakapumbaa kwa raha ya neema za kuskia sifa za
Mtumi Muhammad (Rehma na amani zimshukie) *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

16 | P a g e
‫الفصل الخامس‬
MLANGO WA TANO
‫وقد آن للقلم ان يخط ما حركته فيه األنامل * مما استفاده الفهم من صفات هذا العبد المحبوب الكامل * و‬
* ‫شمائله التي هي احسن الشمائل‬

Imefika wakati kwa kalamu iandke kitakachopelekeshwa na ncha za vizodole,


kutokamana na kilichofaidikia ubongo kufahamu sifa za huyu mja mwenye kupendekeza
aliekamilika, na tabia zake ambazo kwamba ni tabia nzuri zaidi *

‫اخبار و أثار * ليتشرف بكتابته القلم والقرطاس و‬


ٍ ‫ن ان نث ِبت ما بلغ الينا في شأن هذا الحبيب من‬
َ ‫حس‬
َ ‫وهنا‬
* ‫تتنزه في حدائقه األسماع و األبصار‬

Na hapa imependeza tuthibitishe yaliotufikia kutokamana na yanayomukhusu huyu


kipenzi kutokamana na hadithi za bwana Mtumi na maneno ya Maswahaba, ili zipate
kutukuka kwa kuziandika [Hadithi hizo] kalamu na karatasi na zipumbae katika
mabustani ya sifa za Mtumi masikio na macho *

* ‫وقد بلغنا في األحاديث المشهورة أن اول شي ٍء خلقه هللا هو النور المودع في هذه الصورة‬

Imetufikia sis kupitia hadithi mashuhuri, yakwamba kitu cha kwanza alichokiumba
Mwenyezi Mungu ni nuru iliyotiwa katika umbile la Mtumi Muhammad (Rehma na amani
zimteremkie) *

* ‫فنور هذا الحبيب اول مخلوقٍ بر َز في العالم * و منه تفرع الوجود خلقاً بعد خلقٍ فيما حدث و ما تقادم‬

Basi nuru ya huyu kipenzi ndicho kiumbe cha kwanza kilichodhihiri katika huu
ulimwengu, na kutokamana na hiyo nuru ndio uligawanyika ulimwengu kiumbe baada
ya kiumbe katika zilizozuka baadae na pia zilizotangulia *

‫ { قلت يا رسول هللا بابي‬: ‫وقد اخرج عبدالرزاق بسنده عن جابر بن عبدهللا األنصاري (رضي هللا عنهما) قال‬
‫ يا جابر إن هللا خلق قبل األشياء نور نبيك‬: ‫و امي اخبرني عن اول شي ٍء خلقه هللا قبل األشياء * قال‬
* } ‫د (صلى هللا عليه وسلم) من نوره‬ ٍ ‫محم‬

Amepokea Abdul-Razaq kwa sanad yake kutoka kwa Jabir mtoto wa Abdillahi Al Answari
[katika Answar wa madina] (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake)
amesema: { Nilimuuliza Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) nikamwambia: nakuapia kwa
babangu na mamangu, nipe khabari kuhusiana na kitu cha kwanza alichokiumba Mungu
qabla hajaumba chochote, akasema Mtumi (Rehma na amani zimteremkie): “Ewe Jabir
hakika Mwenyezi Mungu ameumba nuru ya Mtumi wako Muhammad (Rehma na amani
zimteremkie) kabla hajaumba chochote kutokamana na nuru yake [Mwenyezi Mungu] ” *

17 | P a g e
‫ كنت اول‬: ‫رسول هللا صلى هللا عليه وسلم‬: ‫ * { قال‬: ‫وقد ورد من حديث ابو هريرة رضي هللا عنه انه قال‬
* } ‫النبيين في الخلقِ وآخرهم في البعث‬

Na imepokewa katika hadithi ya Abu Hureirah (Mwenye izzi Mungu amuelee radhi)
kwamba amesema: amesema Mtumi wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani
zimteremkie) Mimi ndie Mtumi wa kwanza kuumbwa na wa mwisho kutumilizwa *

* ‫وقد تعددت الروايات بانه اول الخلق وجودا و اشرفهم مولودا‬

Na kuna riwaya nyingi zinazosema kua Mtumi Muhammad (Rehma na amani


zimteremkie) ndiye kiumbe wa kwanza kupatikana na ndiye kiumbe bora zaidi
kilichozaliwa *

* ‫ة خفية * اختصت من شاءت من البرية * بكمال الخصوصية‬


ٌ ‫ولما كانت السعادة األبدية * لها مالحظ‬

Na ilipokuwa kunali saada kwa milele, kuna upelelezi wa ndani, alimukhusisha anae
mtaka katika viumbe, kukhusisha kuliko kamilika *

‫فاستودعت هذا النور المبين * اصالب و بطون من شرفته من العالمين * فتنقل هذا النور من صلب ادم‬
* ]‫ونوحٍ و ابراهيم [عليهم السالم‬

Akaiweka hii nuru iliyowazi, katika mitulinga na vizazi za wale aliowatukuza katika
viumbe vyake, ikaguragura hii nuru kutoka kwa mitulinga ya Adam na Nuhu na Ibrahim
[amani iwe juu yao] *

‫حتى اوصلته يد العلم القديم * الى من خصصته بالتكريم ابيه الكريم * عبدهللا ابن عبدالمطلب ذي‬
* ]‫القدر العظيم [رضي هللا عنه‬

Mpaka ikafikishwa na mikono yenye elimu ya tangu, kwa yule aliemukhusu na


kumchagua kwa kumkirimu babake mtukufu, Abdillahi mtoto wa Abdil-Muttalib mwenye
cheo kikubwa [mwenye izzi Mungu amuelee radhi] *

* ]‫و امه التي هي في المخاوف آمنة * السيدة الكريمة آمنة [رضي هللا عنها‬

Na mamake amabae ameepushwa na kila lakumuogopesha, nana mkarimu Amina


[Mwenyezi Mungu amuelee radhi] *

* ‫فتلقاه صلب عبدهللا * فالقاه الى بطنها * فضمته احشاؤها بمعونة هللا محافظة على حق هذه الدر ِة و صونها‬

Ikapokewa na mtulinga wa Abdullahi (Mwenyezi Mungu amuelee radhi) akaitumbukiza


kwenye kizazi cha Amina (Mwenyezi Mungu amuelee radhi), ikakumbatiwa na tumbo za
Amina (Mwenyezi Mungu amuelee radhi) kwa usaidizi wa Mwenyezi Mungu kwa lengo la
kuihifadhi hakki ya hii lulu kubwa na kuihami *

18 | P a g e
* ً ‫فحملته برعاية هللا كما ورد عنها حمال ً خفيفاً ال تجد له ثقال ً * و التشكوا منه الماً وال علال‬

Amina (Mwenyezi Mungu amuelee radhi) akaibeba nuru hiyo kwa maangalizi ya
Mwenyezi Mungu kama ilivyopokewa kutokana kwake mwenyewe mimba iliyokua
khafifu ambayo hakupata tabu wala uzito wowote wala hakulalamikia maumivu wala
magonjwa yoyote *

‫حتى مر الشهر بعد الشهر من حمله * و قرب وقت بروزه الى عالم الشهادة لتنبسط على اهل هذا العالم‬
*‫فيوضات فضله * وتنتشر فيه اثار مجده الصميم‬

Mpaka ikapita mwezi baada ya mwezi kutokana na mimba yake, na ikakurubia wakati
wa kudhihiri kwake kwenye ulimwengu, ili ipate kuenea juu ya walimwengu fadhila zake
nyengi, na ienee katika ulimwengu alama za utukufu wake ulio safi *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل السادس‬
MLANGO WA SITA
‫سرور و ابتهاج‬
ٍ ‫ومنذ علقت به هذه الدرة المكنونة * و الجوهرة المصونة * و الكون كله يصبح و يمسي في‬
* ‫* بقرب ظهور اشراق هذا السراج‬

Na kwanzia ilipofungamana na ulimwengu hii lulu iliofichwa, na jauhara ilohifadhiwa,


ulimwengu wote wapambaukiwa ukichewa ukiwa katika shangwe na furaha, kwa
kukurubia kuchomoza kwa mwangaza wa hii taa yenye mwangaza *

* ‫ة الى التقاط جواهر كنوزه‬


ٌ ‫ة الى بروزه * متشوق‬
ٌ ‫و العيون متشوف‬

Na macho yapeleleza kudhihiri kwake, hali yakiwa na hamu ya kuokota kanzi yake
yenye thamani *

* ‫ة لقريشٍ نطقت بفصيح العبارة * معلنة بكمال البشارة‬


ٍ ‫و كل داب‬

Wanyama wote wa maqureish walitamka kwa faswaha ya vilima, wakitangaza


kukamilika kwa bishara *

* ‫حامل حملت في ذلك العام * اال اتت في حملها بغالم * من بركات وسعادة هذا األمام‬
ٍ ‫وما من‬

Na hakuna mwanamke yeyote aliebeba mimba katika mwaka huo, ela alizaa mtoto wa
kiume, kutokamana na baraka na kukongowewa kwa huyu kiongozi *

19 | P a g e
ً ‫ولم تزل األرض والسموات * متضمخ‬
‫ة بعطر الفرح بمالقاة اشرف البريات * و بروزه من عالم الخفاء الى عالم‬
* ‫الظهور * بعد تنقله في البطون والظهور‬

Na hazikuacha mbingu na ardhi, kua zimejipaka arufu njema ya furaha kwa ajili ya
kukutana na kiumbe bora, na kudhihiri kwake kutoka kwenye ulimwengu wa ghaibu
kuja katika ulimwengu wa kushuhudiwa, baada ya kuguragura kwake katika tumbo na
mitulinga *

*‫فاظهر هللا في الوجود بهجة التكريم * و بسط في العالم الكبير مائدة التشريف و التعظيم * ببروز هذا البشر الكريم‬

Akaidhihirisha Mwenyezi Mungu katika ulimwengu furaha yenye utukufu, akakunjua


katika ulimwengu mkunjufu meza ya utukufu na ukubwa, kwa kudhuhiri kwa huyu
binadamu Mkarimu *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل السابع‬
MLANGO WA SABA
* ‫فحين قرب اوان وضع هذا الحبيب * اعلنت السموات واألرضون ومن فيهن بالترحيب‬

Ulipokurubia wakati wa kuzaliwa huyu kipenzi, zilitangaza mbingu na ardhi na vilivyoomo


ndani yake kwa kukongowea *

* ‫و امطار الجود االلهي على اهل الوجود تثج *والسنة المالئكة بالتبشير للعالمين تعج‬
] )‫[سبحان هللا والحمد هلل و ال إله إال هللا وهللا أكبر (ثالث مرات‬

Na mivua ya zipowa za Mola ikateremka juu ya walimwengu, na ndimi za malaika zilijaa


bishara kwa viumbe wote na kuvuma *
[Subhana’Allah, Alhamdu’Lillah, Lailahailla’Allah, Allah’Akbar (Mara tatu) ]

* ‫والقدرة كشفت قناع هذا المستور * ليبرز نوره كامال ً في عالم الظهور * نوراً فاق كل نور‬

Na nguvu za Mwenyezi Mungu zikaondoa paziya ya hichi kilichofichwa, ili ipate kudhihiri
nuru iliyokamilika katika ulimwengu wa dhahiri, mwangaza uliyoshinda miangaza yote *

* ‫و انفذ الحق حكمه * على من اتم هللا عليه النعمة * من خواص األمة * ان يحضر عند وضعه امة‬

Na akapitisha Mwenyezi Mungu hukmu yake, juu ya yule aliemkamilishia neema, kutokamana na
ummati wake makhsusi, ili wahudhurie wakati wa kuzaliwa kwake na mamake *

20 | P a g e
* ‫تانيساً لجنابها المسعود * و مشارك ًة لها في هذا السماط الممدود‬

Kwa lengo la kumpumbaza mwanamke alienali saada, na kwa aajili ya kushirikiana nae
katika hichi Chanu hichi kilichotandikwa *

‫فحضرت بتوفيق هللا السيدة مريم والسيدة اسية * و معهما من الحور العين من قسم هللا له من الشرف‬
* ‫بالقسمة الوافية‬

Akahudhuria kwa tawfiqi ya Mwenyezi Mungu nana Maryamu na nana Asiya, na wakawa
pamoja nao kutokamana na Hurilain, ambao Mwenyezi Mungu amewagawia utukufu kwa fungu
la kutosheleza *

‫فاتى الوقت الذي رتب هللا على حضوره وجود هذا المولود * فانفلق صبح الكمال من النور عن عمود * و برز الحامد‬
* ‫المحمود * مذعناً هلل بالتعظيم والسجود‬

Ukafika wakati alioupanga Mwenyezi Mungu ukifika kupatikane mzawa huyu, ikapasuka
asubuhi iliyokamilika kwa mwangaza uliostawi, akachomoza mwenye kuhimidi mwenye
kuhimidiwa, ilhali akipondokea kwa Mwenyezi Mungu kwa kumtukuza na kumsujudia *

‫مقام‬
MAQAMU (KISIMAMO)
‫أشرق الكون ابتهاجـا ً = بوجود المصطفى أحمد‬

Uling'ara ulimwengu kwa furaha


kwa kupatikana mteuliwa Ahmad

‫سرور قـد تجـدد‬


ٌ ‫أنـس = و‬
ٌ ‫و ألهل الكون‬

Na watu wa ulimenguni wana pumbao


na furaha zilizo jadidika (Kuanza upya)

‫فاطربوا يا أهل المثاني = فهزار اليمـن غـرد‬

Teremani enyi muloteremeshiwa Qur’an


kwani nyuni mwenye sauti mzuri ameimba kwa sauti ya juu

‫ل = فاق في الحسن تفـرد‬


ٍ ‫و استضيئوا بجمـا‬

Mujing’arishe na uzuri
ulioshinda katika uzuri na ukapwekeka

21 | P a g e
‫مستمر ليـس ينفـد‬
ٍ = ‫ولنا البشـرى بسعـ ٍد‬

Na tunao sisi bishara kwa mwenyebaraka


yenye kuendelea isiyokoma

‫حيث أوتينـا عطـا ًء = جمع الفخـر المؤبـد‬

Kwa kupewa kipawa (tunu)


kilichokunsanya fakhiri ya kudumu

‫ل ان يحصره العـد‬
َّ ‫د = ج‬
ٍ ‫فلربـي كـل حـمـ‬

Kwa Mola shukurani zote


ambazo zimemshinda kuhisabika

‫إذ حبانا بوجود الـ = مصطفى الهادي محمد‬

Alipotutunuku kwa kutuletea


mswafiwa muongozi Muhammad

‫يا رسـول هللا أهـال ً = بك إنَّـا بـك نسعـد‬

Ewe Tumwa wa Mungu kongoni


kwako wewe sisi tumenali saada

‫و بجاهـه يـا إلهـي = جد و بلغ كل مقصـد‬

Kwa jahi yake ewe Mola wangu


tupe na utufikishie matakwa yetu

‫و اهدنا نهج سبيلـه = كي به نسعد و نرشـد‬

Na utuongoze muongozo wa njia yake


ili kwayo tunalisaada na tuongoke

‫رب بلغنـا بجـاهـه = في جواره خير مقعـد‬

Ewe Mola tufikishe kwa jahi yake


pembezoni mwake makazi mema

‫و صـالة هللا تغشـى = أشرف الرسل محمـد‬

Na swala ya Mola imfunike


mbora wa Mitumi Muhammad

22 | P a g e
‫حيـن يتـجـدد‬
ٍ ‫مستـمـر = كـل‬
ٌ ‫م‬
ٌ ‫و ســال‬

Na salamu zenye kuendelea


kila mara iwe itajiregelea

‫الفصل الثامن‬
MLANGO WA NANE
‫وحين برز صلى هللا عليه وسلم من بطن امه برز رافعاً طرفه الى السماء * مؤميا ً بذلك الرفع الى ان له‬
* ‫شرفاً عال مجده وسما‬

Na alipodhihiri (Rehma na amani zimteremkie) kutoka katika tombo la mamake,


alidhihiri hali ya kua ameyainua macho yake mbinguni, akishiriya kwa huko kuinua
macho yake kua anao utukufu uliokwea cheo chake na kuangatika *

* ‫وكان وقت مولد سيد الكونين * من الشهور شهر ربيع األول ومن األيام يوم األثنين * و موضع والدته و قبره بالحرمين‬

Na ilikua wakati wa kuzaliwa bwana wa mbinguni na ardhini katika miezi ni mwezi wa


mfungo sita, na katika masiku ni siku ya juma tatu, na sehemu aliyozaliwa na kuzikwa
ni Maka na Madina *

* ‫و قد ورد انه ولد مختوناً مكحوال ً مقطوع السرة * تولت ذلك لشرفه عند هللا ايدي القدرة‬

Na imepokewa yakwamba Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) alizaliwa hali yakua


ametahiriwa ametiwa wanda na amekatwa kitovu, imesmamia kutekeleza hilo kwa ajili
ya utukufu wake mbele za mola, mikono ya uwezo [Mungu alietukuka] *

* ‫و مع بروزه الى هذا العالم ظهر من العجائب * ما يدل على انه اشرف المخلوقين وافضل الحبائب‬

Na pamoja na kuchomoza kwake katika hunu ulimwengu kulidhihiri miujiza


yanayodulisha ya kwamba yeye ni kiumbe bora na kipenzi chema zaidi *

‫ " لما ولدت امنة رضي هللا عنها‬: ‫فقد ورد عن عبدالرحمن بن عوف عن امه الشفاء رضي هللا عنهما * قالت‬
* " ‫ل فسمعت قائال ً يقول رحمك هللا او رحمك ربك‬َّ ‫رسول هللا وقع على يدي فا سته‬

Imepokewa kutoka kwa Abdul-Rahman mtoto wa Auf kutoka kwa mamake Shaffaa
(Mungu awaelee radhi) yakwamba yeye [Shaffaa] amesema: " Alipozaa [Nana] Amina
(Mungu amuelee radhi) kumzaa Mtumi wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani
zimteremkie) aliangukia mikononi mwangu akapiga ukee, nikamsikya msemi akisema:
Mungu akurahamu ao Mola wako akurahamu " *

23 | P a g e
* "‫ "فاضاء له ما بين المشرق والمغرب * حتى نظرت إلى بعض قصور الروم‬: ‫قالت الشفاء‬

Akasema Shaffaa: “ Akaangaziwa Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) baina ya


mashriq na maghrib mpaka nikaona baadhi ya maqasri ya Roma” *

‫ "ثم ألبسته وأضجعته فلم أنشب أن غشيتني ظلمة ورعب وقشعريرة عن يميني * فسمعت قائال‬:‫قالت‬
* "‫يقول "أين ذهبت به؟" قال "إلى المغرب‬

Akasema Shaffaa: “ Kisha nikamvesha nguo na nikamlalisha, basi haikunchukua mda


chikanivamia mimi kiza na khofu na babaiko upande wangu wa kulia, nikamsikia
mwenye kusema akisema: umeenda na yeye wapi? akajibiwa “ nimeenda nae upande
wa magharibi ” *

‫وأسفر ذلك عني ثم عاودني الرعب والظلمة والقشعريرة عن يساري * فسمعت قائال يقول أين ذهبت به‬
* ‫قال إلى المشرق‬

Na kikaniondokea mimi kiza na khofu na babaiko, kisha ikaniregelea tena khofu na kiza
na babaiko upande wa kushotoni mwangu, nikamsikia mwenye kusema akisema:
umeenda nae wapi? akajibiwa: “upande wa mashariki” *

* ‫قالت فلم يزل الحديث مني على بال حتى ابتعثه هللا فكنت من أول الناس إسالما‬

Akasema Shaffaa: basi haya maneno hayakunitoka akilini mwangu mpaka


alipotumilizwa na Mwenyezi Mungu nikawa nimiongoni mwa watu wa kwanza kusilimu *

‫السنة من عظيم المعجزات * و باهر االيات البينات * بما يقضي بعظيم شرفه عند مواله * و‬
ُّ ‫و كم ترجمت‬
* ‫حين ترعاه * وانه الهادي الى الصراط المستقيم‬
ٍ ‫إن عين عنايته في كل‬

Na ni hadithi ngapi zilizoelezea miujiza yake mikubwa mikubwa, na alama kubwakubwa


zilizo wazi, zinazoonyesha ukubwa wa cheo chake mbele ya Mola wake, na kwamba
jicho la inaya ya Mola wake la mchunga wakati wote, na kwamba yeye ndie mwenye
kuongoza watu katika njia ilionyoka *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

24 | P a g e
‫الفصل التاسع‬
MLANGO WA TISA
‫ضعات‬
ِ ‫ه المر‬
ِ ‫ثم انه بعد ان حكمت القدرة بظهور ة * و انتشرت في األكوان لوامع نوره * تسابقت الى رضاع‬
* ‫* و توفرت رغبات اهل الوجود في حضانة هذه الذات‬

Kisha hakika yake Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) baada ya kuhukumu nguvu za
uwezo wa Mwenyezi Mungu kudhihiri kwake ulimwenguni, na ikaenea ulimwenguni
miangaza ya nuru yake * Walishindania kumnyonyesha wenye kumnyonyesha, na
zikapatikana raghbah za walimwengu kuilea hii dhati tukufu *

‫* فنفذ الحكم من الحضرة العظيمة * بواسطة السوابق القديمة * بإن األولى بتربية هذا الحبيب و حضانته‬
* )‫السيدة حليمة (رضي هللا عنها‬

Ikapita hukmu kutoka kwa hadhrah tukufu, kupitia hukmu ya tangu, kua aliyekua bora
zaidi kumlea huyu kipenzi cha Mwenyezi Mungu na kumyonyesha ni nana Halima
(Mwenyezi Mungu amuelee radhi) *

‫و حين الحظته عيونها * و برز في شأنها من األسرار مكنونها * نازل قلبها من الفرح و السرور * ما دل على‬
* ‫ان حظها من الكرامة عند هللا حظ ٌ موفور‬

Na yalipompeleleza Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) macho yake [Nana Halima]


ikadhihiri kwake siri za nguvu za Mola undani wake, iliingia katika moyo wake furaha na
bashasha, iliodulisha kua bahati yake kutokamana na karama za kutoka kwa Mwenyezi
Mungu ni fungu lililobora Zaidi *

* ‫فحنت عليه حنو األمهات على البنين * و رغبت في رضاعه طمعاً في نيل بركاته التي شملت العالمين‬

Akawa na kite kwake [Mtumi] kama kite cha mamama wazazi juu ya watoto wao, na
akawa na raghbah ya kumlea akitaraji kupata baraka zake [Mtumi rehma na amani
zimshukie] ambazo zimewaenea viumbe wote *

* ‫فطلبت من امه الكريمة * ان تتولى رضاعه وحضانته و تربيته بالعين الرحيمة‬

Akamuomba mamake [Mtumi] mtukufu, asimamie kumnyonyesha na kumlelea kwa


jicho la huruma *

‫فأجابتها بالتلبية لداعيها * لما رأت من صدقها في حسن التربية و وفور دواعيها * فترحلت به الى منازلها‬
* ‫ة و بعين عنايته منظورة‬ ٌ ‫مسرورة * وهي برعاية هللا محفوف‬

Akamjibu kwa kumkubaliya ombi lake, baada ya kumuona ukweli wake katika kumlea
uzuri na kwa kua kwa nana Halima kulikua mambo ya kumuezesha kumlea mtumi uzuri,
akaondoka nae kuelekea kwao hali akiwa na furaha, huku akiwa amezungukwa na
kinga ya Mwenyezi Mungu na uangalizi wake *

25 | P a g e
* ‫فشاهدت في طريقها من غريب المعجزات * ما دلها على انه اشرف المخلوقات‬

Akaona katika njia yake miujiza tafauti tafauti, yaliomdulisha kuwa yeye [Mtumi] ni
kiumbe kitukufu Zaidi *

* ‫فقد اتت و شارفها و اتانها ضعيفتان * و رجعت وهما لدواب القافلة يسبقان‬

Alikuja kutoka kwao hali ya kuwa hayawani wake na punda wake ni madhaifu, na
akarudi kutoka Makkah hali ya kuwa wale hayani wake na punda wake wanashindana
na misafara mengine *

* ‫و قد درت الشارف والشياة من األلبان * بما حير العقول واألذهان‬

Hakika vilijaa maziwa viwele za hayawani wakongwe na mbuzi wote kwa namna
ilitahayarisha akili za watu na mabongo *

‫و بقي عندها في حضانتها و زوجها سنتين * تتلقى من بركات و عجائب معجزاته ما تق ُّر به العين * و‬
* ‫تنتشر اسراره في الكونين‬

Na akabakiya [Mtumi] katika malezi ya nana Halima na mume wake miaka miwili,
akipokea kutokamana na baraka na miujiza yake [Mtumi] mambo yanayotuliza macho,
na zikawa zinaenea siri zake mbinguni na ardhini *

* ‫حتى واجهته مالئكة التخصيص و األكرام * بالشرف الذي عمت بركته األنام * وهو يرعى األغنام‬

Mpaka wakamjia yeye [Mtumi] malaika wa kukhusisha na kutukuza, wakamjia na


utukufu ambao ulienea baraka zake viumbe wote wakati yeye [Mtumi] yuachunga
mbuzi na kondoo *

‫فاضجعوه على األرض اضجاع تشريف * و شقوا بطنه شقاً لطيف * ثم اخرجوا من قلبه ما اخرجوه و اودعوا‬
*‫فيه من اسرار العلم و الحكمة ما اودعوه‬

Wakamlaza juu ya ardhi kwa njia ya utukufu, wakampasua tumbo lake kwa upole, kisha
wakatoa katika moyo wake walichokitoa, wakaweka ndani ya moyo wake kutokamana
na siri za elimu na hikmah walichokiweka,

ٍ‫ى=ولكنهم زادوه طهراً على طهر‬


ً ‫و ما اخرج األمالك من قلبه اذ‬

Hawakutoa Malaika kwenye moyo wa Mtumi uchafu


lakini waliuzidisha uswafi juu ya uswafi ulonao

* ‫و هو مع ذلك في قو ٍة و ثبات * يتصفح من سطور القدرة االلهية باهر اآليات‬

Naye [Mtumi] kando na hayo yuko katika nguvu zake kamili na amekita vizuri, huku
akiangalia kutokamana na maandishi ya qudrah za Mwenyezi Mungu dalili zilizowazi *

26 | P a g e
‫فبلغ الى مرضعته الصالحة العفيفة * ما حصل على ذاته الشريفة * فتخوفت عليه من حادثٍ تخشاه * و‬
ِ ‫تدر انه مالحظ ٌ بالمالحظة التام‬
* ‫ة من مواله‬ ِ ‫لم‬

Ikafika kwa mlezi wake mwema aliejichunga, yaliomfika mwili wake [Mtumi] mtukufu,
akamkhofia asije akapatikana na jambo ambalo alikhofia, na hakujua kwamba [Mtumi]
anachungwa kikamilifu kutoka kwa Mola wake *

‫ة بفراقه * ولكن لما قام معها من حزن القلب عليه و اشفاقه * و هو‬ٍ ‫فردته الى امه و هي غير سخي‬
*‫حصن مانعٍ و مقا ٍم كريم‬
ٍ ‫بحمدهللا في‬

Akamrudisha kwa mamake hali yakua hataki kuepukana nae, lakini kwa sababu ya
huzuni zilomfikia kwa yaliyompata [Mtumi] na kwa kumhurumia, naye [Mtumi] pamoja
na kumshukuru Mungu yuko katika ngome yenye kukenga na cheo kitukufu *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل العاشر‬
MLANGO WA KUMI
* ‫فنشىء (صلى هللا عليه وسلم) على اكمل األوصاف * يحفه من هللا جميل الرعاية و غامر األلطاف‬

Akakulia Mtumi (Rehma na amani zimeteremkie) juu ya tabia zilokamilika, ikimzunguka


kutoka kwa Mwenyezi Mungu riaya iliyokua njema na kinga za kila aina *

‫فكان يشب في اليوم شباب الصبي في الشهر * و يظهر عليه في صباه من شرف الكمال ما يشهد له بأنه‬
* ‫سيد ولد آدم وال فخر‬

Akawa akuwa kwa siku makuzi ya mwezi kwa vijana wa kawaida, na ikawa yadhihiri kwake
katika utoto wake kutokamana na utukufu wa kukamilika mambo ambayo yanamtolea ushahidi
ya kuwa yeye ndie bwana wa vijana wa nabii Adam wala sio fakhari *

‫مريض اال شفاه هللا‬


ٍ ‫ة والمر ِه طائعة * فما نفث على‬
ٌ ‫ولم يزل وانجم سعوده طالعة * و الكائنات لعهده حافظ‬
* ‫* و التوجه في غيثٍ اال وانزله مواله‬

Na haikuacha nyota ya kunali saada kwake kuchomoza, na viumbe kwa ahadi yake
wanatekeleza na amri zake wanazitwii * hakumtufia mate mgojwa yoyote ela Mola
alikuwa akimponya, wala hakuomba mvua ela Mola wake alikuwa akiiteremsha *

27 | P a g e
‫حتى بلغ من العمر اشده * و مضت له من سن الشباب والكهولة مدة * فاجأته الحضرة االلهية بما شرفته‬
‫به وحده * فنزل عليه الروح األمين * بالبشرى من رب العالمين * فتال عليه لسان الذكر الحكيم شاهد‬
* } ‫م عليم‬
ٍ ‫{ و انك لتلقى القرآن من لدن حكي‬

Mpaka akafikia kwenye umri wa maqamu, ikampitia kutokamana na miaka ya


ubarobaro na ukongwe mda, ghafla Mungu akamfijai kwa lile alilomsharafisha yeye
peke yake, akamteremkia yeye ruhu muaminifu [Jibrili] akamteremkia na bishara
kutoka kwa Mola wa viumbe wote, akamsomea ujumbe unaotoka katika Qur’an, dalili
{ Na wewe wapokea Qur’an kutoka kwa Mola mwenye hikma na mjuz } *

# ‫ { اقرأ باسم ربك الذي خلق‬: ‫فكان اول ما نزل عليه من تلك الحضرة من جوامع الحكم * قوله تعالى‬
* } ‫ علم األنسان ما لم يعلم‬# ‫ الذي علم بالقلم‬# ‫ اقرأ و ربك األكرم‬# ‫خلق األنسان من علق‬

Ikawa aya ya kwanza kumteremkia kutoka kwa hadhrah tukufu kutokamana na maneno yenye
mkusanyiko wa hikmah, ni neno lake atukushieo { Soma kwa jina la Mola wako alieumba #
ameumba binadamu wote kutokamana na tone la damu # soma na Mola wako mlezi ni
mkarimu Zaidi # ambae amemfundisha kwa kalamu # amemfundisha binadamu asoyajua } *

* ‫فما اعظمها من بشار ٍة اوصلتها يد األحسان من حضرة األمتنان * الى هذا األنسان‬

Ni bishara kubwa iliyoje iliofikishwa na mkona wa ihsani, kutoka kwa hadhrah ya utoaji,
kuja kwa huyu binadamu *

* } ‫ علمه البيان‬# ‫ خلق النسان‬# ‫ علم القرآن‬# ‫ { الرحمن‬:‫و ايدتها بشارة‬

Ikatiliwa nguvu na bishara: { Arrahmaan # amefundisha Qur’an # amemuumba


binadamu # akamfundisha kubaini } *

*‫و الشك انه هو األنسان المقصود بهذا التعليم * من حضرة الرحمن الرحيم‬

Na hapana shaka yakwamba yeye [Mtumi] ndie bin Adamu aliekusudiwa kwa
mafundisho haya, ktoka kwa Mola mwingi wa rehema mwenye kurehemu *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

28 | P a g e
‫الفصل الحادي عشر‬
MLANGO WA KUMI NA MOJA
‫ثم انه (صلى هللا عليه وسلم) بعد ما نزل عليه الوحي البليغ * تحمل اعباء الدعوة والتبليغ * فدعا الخلق‬
* ‫الى هللا على بصيرة * فاجابه باالذعان من كانت له بصير ٌة منيرة‬

Kisha hakika yake Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) baada ya kuteremshiwa Wahyi
uliokuwa na fasaha, alibeba majukumu yakulingania na kufikisha ujumbe,
akawalingania watu kwa Allah kwa njia ya busara, akamuitikia kwa kukiri kwa aliyokuja
nayo kila aliekuwa na ubongo uliotiwa nuru ya uongofu *

* ‫ة سبقت بها األقضية و األقدار * تشرف باسبق اليها المهاجرون واألنصار‬


ٌ ‫وهي اجاب‬

Nayo ni mwiitikio uliotanguliwa na qadhaa ya Mwenyezi Mungu na qadar yake,


walisharafika kutangulia kuitikia mwito huo Muhajirina na Answari *

* ‫و قد اكمل هللا بهمة هذا الحبيب و اصحابه هذا الدين * و اكبت بشدة بأسهم قلوب الكافرين و الملحدين‬

Na hakika aliikamilisha Mwenye Izzi Mungu kwa himmah ya huyu kipenzi na masahaba
zake hini dini, na akawakhizi kwa nguvu zao [Maswahaba] nyoyo za makafiri na
wanaotia kombo dini *

* ‫فظهر على يديه من عظيم المعجزات * ما يدل على انه اشرف اهل األرض و السموات‬

Ikadhihiri kupitia mikona yake miujiza mikubwa, yanayodulisha yakwamba yeye [Mtumi]
ni mbora wa watu wa ardhini na mbinguni *

‫فمنها تكثير القليل * وبرء العليل * و تسليم الحجر * و طاعة الشجر * و انشقاق القمر * و اإلخبار‬
* ‫بالمغيبات * و حنين الجذع الذي هو من خوارق العادات * و شهادة الضب له والغزالة * بالنبوة والرسالة‬

Miongoni mwayo ni kufanya chengi kilichokuwa kidogo, na kuponya waliokuwa


wagonjwa, na kusalimiwa na jiwe, na kutiiwa na mti, na kupasuka kwa mwezi * na
kuelezea mambo ya ghaibu, na kitunu cha kigogo cha mtende ambacho hicho kitunu ni
katika mambo ambao siyakawaida, na kutokewa ushahidi na yuru na paa, kuwa yeye ni
Mtumi na ametumilizwa *

* ‫الى غير ذلك من باهر اآليات * و غرائب المعجزات * التي ايده هللا بها في رسالته * و خصصه بها من بين بريته‬

Na mengine yasiokuwa haya kutokamana na alama zilizo wazi, na miujiza ya kimaajabu,


ambayokwamba alitilia nguvu Mwenyezi Mungu kwayo utumi wake, na akamkhusisha
yeye pwekeyake katika viumbe wake wote *

29 | P a g e
* ‫و قد تقدمت له قبل النبوة ارهاصات * هي على نبوته و رسالته من اقوى العالمات‬

Na hakika ilitangulia kwake kabla ya utumi mambo ambayokwamba siyakawaida, hayo


mambo yalikuwa juu ya utumi wake na kutumilizwa kwake ni alama zenye kutilia nguvu
utumi wake *

‫و مع ظهورها و انتشارها سعد بها الصادقون من المؤمنين * و شقي بها المكذبون من الكافرين و المنافقين‬
* ‫* و تلقاها بالتصديق والتسليم * كل ذي قلبٍ سليم‬

Na pamoja na kudhihiri [Hizo alama] na kuenea kwake walinali saada kwazo waumini
waliosadiki, na wakakhasirika wale waliokanusha kutokamana na makafiri na wanafiki,
na wakazipokea [Hizo alama] kwa kuziamini kila mwenye moyo ambao umesalimika *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل الثاني عشر‬


MLANGO WA KUMI NA MBILI
‫و من الشرف الذي اختص هللا به اشرف رسول * معراجه الى حضرة هللا البرِ الوصول * وظهور ايات هللا‬
* ‫الباهرة في ذلك المعراج * و تشرف اهل السموات و من فوقهن باشراق نور ذلك السراج‬

Na katika utukufu ambao Mwenyezi Mungu aliomkhusu nao Mtumi aliemtukufu, ni


Miraji, kupanda kwake Mtumi mpaka kwenye hadhrah ya Mwenyezi Mungu Alie mwema
mwenye kuunganisha, na kudhihiri alama za Mwenyezi Mungu zilizowazi katika kupanda
huko (Miraji), na kusharafika mbingu na zilizo juu yake kwa kuchomoza nuru yake kama
taa yenye muangaza *

* ‫فقد عرج الحبيب ومعه األمين جبريل * إلى حضرة الملك الجليل * مع التشريف و التبجيل‬

Hakika alipanda kipenzi akiwa pamoja naye muaminifu Jibrili, mpaka kwenye hadhrah
ya Mfalume mwenye cheo kitukufu, pamoja na kutukuzwa na kuheshimiwa *

* ‫فما من سما ٍء ولجها اال وبادره اهلها بالرحيب والتكريم والتأهيل‬

Hakuna mbingu alioingia, illa walikimtapilia watu wa mbingu hiyo kwa kumkongowea na
kumkirimu na kumkurubisha *

30 | P a g e
* ‫مر عليه * بشره بما عرفه من حقه عند هللا و شريف منزلته لديه‬
َّ ‫ل‬
ٍ ‫و كل رسو‬

Na kila Mtumi aliekua akimpitia, alimpatia bishara kwa yale aliyokua ayajua kutokamana
na cheo chake mbele ya Mwenyezi Mungu na utukufu wa cheo chake mbele ya Mola
wake *

‫حتى جاوز السبع الطباق * و وصل الى حضرة األطالق * نازلته من الحضرة االلهية * غوامر النفحات القربية‬
‫* و واجهته بالتحيات * و اكرمته بجزيل العطيات * و اولته جميل الهبات * و نادته بشريف التسليمات * بعد‬
* ‫اناثنى على تلك الحضرة بالتحيات المباركات الصلوات الطيبات‬

Mpaka akazipita mbingu zote saba, na akafika kwenye upeo wa hadhrah hio [Ya Allah],
zilimteremkia kutoka kwa hadhrah hio ya kimungu, vipawa vingi mno venye
kumkurubisha na Mola wake * na akamuwajihi kwa kumsalimia kwa maamkuzi mema,
na akamkirimu kwa vipawa vikubwa vikubwa, na akammilikisha vipaji vizuri, na
akamuita kwa salamu zilizo bora, baada ya kuisifu ile hadhrah tukufu kwa maamkuzi
yenye baraka na rehma zilizo njema *

‫فيالها من نفحاتٍ غامرات * و تجلياتٍ عالياتٍ في حضراتٍ باهرات * تشهد فيها الذات للذات * و تتلقى‬
‫* عواطف الرحمات * و سوابغ الفيوضات بإيدي الخضوع واألخبات‬

Ni vipawa vingi vilioje venye kufinika, na kufunukiwa [kuona siri] kulioko hali ya juu
katika hadharah zilizo mzuri, yashuhudia ndaniyake dhati [Mtumi] dhati [Mwenyezi
Mungu] na kupokea sikitiko la rehma, na vipawa vingi venye kuenea, kwa mikono ya
unyenyekevu na khushui *

‫وراءهـن وراء‬
َّ ‫ي حسرى = دونها مـا‬
ُّ ‫سقط األمان‬
ْ َ ‫تب ت‬
ٌ ‫ر‬

Vyeo vyamuacha mwenye kutamani katika hali ya tahayuri


pasina kuzifikia kwa sababu hakuna aliezipata zeo hizo ela bwana Mtumi

* ‫عقل الحبيب في تلك الحضرة من سرها ما عقل * و اتصل من علمها بما اتصل‬

Alifahamua kipenzi [Mtumi] katika hadhrah hiyo kutokamana na siri zake mambo
aliyojaaliwa kuyafahamu, na akafungamana kutokamana na elimu ya hadhrah hiyo kwa
kile alichojaaliwa kushikamana nacho *

} ‫{ فاوحى الى عبده ما اوحى * ما كذب الفؤاد ما رأى‬

{ Mwenye izzi Mungu akampa wahyi mja wake kile alichopewa wahyi # haukusema
urongo moyo [wa Mtumi Muhammad rehma na amani zimshukie] kwa alichokiona
[Katika safari yake ya miraji] } *

31 | P a g e
‫ة خصصت بها حضرة األمتنان * هذا النسان * و اولته من عواطفها الرحيمة ما يعجز عن‬
ٌ ‫فما هي إال منح‬
* ‫حمله الثقالن‬

Haikua hii safari ela ni kipawa amekikhusisha kitendo hicho hadhrah ya utoaji,
kumkhusu huyu binadamu, na akamjaza kite cha huruma kiasi ambacho wanashindwa
kubeba (kufahamu) majini na binadamu *

* ‫و تلك مواهب ال يجسر القلم على شرح حقائقها * والتستطيع األلسن ان تعرب عن خفي دقائقها‬
* ‫خصصت بها الحضرة الواسعة هذه العين الناظرة و األذن السامعة‬

Na hivo vyote ni vipawa ambavyo haviwi na ujasiri kalamu juu ya kusherehesha uhakika
wake, wala ndimi haziwezi kuelezia maana ya ndani yaliofichika * ambayo yamekhusiwa
kwayo hadhrah kunjufu hili jicho lenye kuona na sikio lenye kusikia *

‫ع في األطالع على مستورها * واألحاطة بشهود نورها * فانها حضرة جلت عن نظر الناظرين‬
ٌ ‫فال يطمع طام‬
* ‫ة ع َّزت على غير سيد المرسلين‬ ٌ ‫* و رتب‬

Basi asifanye tamaa mwenye tamaa kutaka kujua yaliofichwa, na kutaka ukweto kwa
kushuhudia nuru yake * hakika ni hadhrah iliombali na ufahamu wa wenye
kufahamu,na nicheo ambacho hakiwezi kupatikana na mwengine asiyekua bwana wa
Mitumi wote *

*‫فهنيئاً للحضر ِة المحمدية * ما واجهها من عطايا الحضرة األحدية * وبلوغها الى هذا المقام العظيم‬

Basi pongezi ni kwa hadhrah ya Mtumi Muhammad, kwa kile alichokishudia na kukipata
kutokamana na hadhrah ya upweke, na kufika kwake katika hii sehemu tukufu *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل الثالث عشر‬


MLANGO WA KUMI NA TATU
* ‫و حيث تشرفت األسماع باخبار هذا الحبيب المحبوب * و ماحصل له من الكرامة في عوالم الشهادة والغيوب‬

Na yaliposharifika maskizi kwa khabari za huyu kipenzi mwenye kupendwa, na yale


aliyoyapata kutokamana na karama katika ulimwengu huu tunaoushuhudia wa ardhini
na tusioushuhudia wa mbinguni *

32 | P a g e
‫تحركت همة المتكلم الى نشر محاسن ها السيد وأخالقه * ليعرف السامع ما أكرمه هللا به من الوصف‬
* ‫الحسن والخلق الجميل الي خصصته به عناية خالقه‬

Zilitaharaki himma za mwenye kuzungumza kutaka kueneza mazuri ya huyu bwana na


tabia zake, ili apate kujua mwenye kuskia yale ambayo Mwenyezi Mungu amemkirimu
[Mtumi] kwayo, kutokana na sifa njema na umbo zuri ambalo imemkhussu kwayo inaya
(uangalizi maalumu) wa Muumba wake *

‫ن واعية * فانه سوف يجمعه من اوصاف الحبيب على‬


ٍ ‫فليقابل السامع ما امليه عليه من شريف األخالق بأذ‬
* ‫الرتبة العالية‬

Basi na apulike mwenye kuskia yale ninayo yaandika ya tabia tukufu kwa masikio ya
mwenye kupulika, hakika zitamjumuikia yeye sifa za kipenzi kwa kiwango cha juu *

‫ة هللا في خلقه وخلقه‬


ِ ‫فليس يشابه هذا السيد في خلقه و اخالقه بشر * و اليقف اح ٌد من اسرار حكم‬
* ‫عين و ال اثر‬
ٍ ‫على‬

Hafanani na huyu Bwana katika maumbile yake na tabia zake kiumbe chochote, wala
hatojua yoyote kutokamana na siri za hikmah za mwenye izzi Mungu katika maumbile
yake na tabia zake juu alama ya kuonekana wala athari yoyote *

* ‫ة بدرية‬
ٍ ‫فإن العناية االزلية * طبعته على اخالقٍ سنيَّة * و اقامته في صور ٍة حسن‬

Hakika inaya ya tangu ilimuumba na kumpamba juu ya tabia njema ziliojuu zaidi, na
ikamuweka katika sura njema zinazong’aa kama mwezi uliokamilika *

‫س َنه‬ َ ‫فلقد كان (صلى هللا عليه وآله وسلم) مربوع القامة * ابيض اللون مشرباً بحمره * واسع الجبين‬
َ ‫ح‬
* ‫ة و الوفرة‬
ِ ‫م‬
َّ ‫شعره بين الج‬

Alikuwa Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) ni mwenye kimo cha wastani, mweupe
weupe uliovaana na wekundu, mkunjufu wa panja la uso lilozuri, nywele zake ziko
baina ya masikio na mafuzini *

‫بشر على‬
ٌ ِ‫وله اإلعتدال الكامل في مفاصله واطرافه * و األستقامة الكاملة في محاسنه و اوصافه * لم يأت‬
* ‫خل ِقه * في محاسن نظره و سمعه و نطقه‬ َ ‫مثل‬

Na anaulinganifu uliokamilika katika viungo vyake na mikono yake na miguu, na usawa


uliokamilika katika uzuri wake na sifa zake, hakujaumbwa kiumbe yeyote kama mfano
wake, katika uzuri wa maangalizi yake na maskizi yake na matamshi yake *

* ‫اجمل صورة * فيها جميع المحاسن محصوره * وعليها مقصورة‬


ِ ‫قد خلقه هللا عل‬

Hakika amemuumba yeye Mwenyezi Mungu juu ya umbile zuri, katika umbile hilo
kumekusanywa mazuri yote, na kwa umbile hilo tu ndio kumekusanywa mazuri yote *

33 | P a g e
‫إذا تكلم نثر من المعارف والعلوم نفائس الدرر * و لقد اوتي من جوامع الكلم ما عجز عن األتيان بمثله‬
*‫مصاقع البلغا ِء من البشر‬

Akizungumza humiminika kutokamana na maarifa na ujuzi lulu zilizonjema, na hakika


alipewa maneno yaliokusanya [Machache yenye maana mengi] kitu ambacho walishindwa
kufanya mfano wake wale mabingwa wenye fasaha na balagha katika viumbe *

*‫تتنزه العيون في حدائق محاسن جماله * فال تجد مخلوقاً في الوجود على مثاله‬

Hupumbaa macho katika bustani za mazuri ya uzuri wake, wala hupati ulimwenguni
kiumbe aliyefanana na yeye *

‫سي ٌد ضحكه التبسم و المـشــي الهوينا و نومه األغفـاء‬

Bwana ambae kiteko chake ni kutabasamu


na mwendo wake ni wa upole ni usingizi wake ni usingizi mwepesi

‫ه النسيم و ال غيــر محيَّاه الروضـة الغ َّنـاء‬


ِ ‫ماسوى خلق‬

Hazikuwa tabia zake ela ni kama upepo ulio laini


na haukuwa uso wake ela ni kama bustani iliyojaa kila maua mazuri

‫ة و حيـاء‬
ٌ ‫ووقـار و عصمـ‬
ٌ ‫م‬ ٌ ‫ة كلُّه و حـز‬
ٌ ‫م و عـز‬ ٌ ‫رحم‬

Yeye ni Rehmah yote mwenye msimamo na ukakamavu


mtulivu aliehifadhiwa, mwenye haya

‫معجز القول و الفعال كريـم الخلق و الخلِق مقسط ٌ معطاء‬

Maneno yake yote ni miujiza vilevile vitendo vyake


mwenye umbile zuri na tabia njema, muadilifu na mtoaji sana

* ‫و إذا مشى فكأنما ينحط ُّ من صبب * فيفوت سريع المشي من غير خبب‬

Na akitembea ni kama anayeteremka kwenye ardhi yenye kilima kwa kuangalia chini,
hivo humpita anayetembea haraka pasina kwenda mbio *

* ‫فهو الكنز المطلسم الذي ال يأتي على فتح باب اوصافه مفتاح‬
* ‫والبدر التم الذي يأخذ األلباب إذا تخيلته او سناه لها الح‬

Yeye ndiye kanzi iliyofichwa ambayo kwamba hakuna ufunguo wa kuweza kuifungua
kwa kujua sifa zote zilizo ndani yake, na nimwezi uliotimia ambao huziteka nyoyo
zinapomfikiria au zinapomulikiwa na mwangaza wake *

34 | P a g e
‫ه = تحيرت االلباب في وصف معناه‬
ِ ‫وجه‬
ِ ‫حبيب يغار البدر من حسن‬
ٌ

Kipenzi ambae mwezi wamuonea wivu kutokamana na uzuri wake


yameduwaa mabongo katika kusifu maana ya sifa zake

‫ف يعجز الواصفين * او يدرك الفهم معنى ذاتٍ جل َّت ان يكون لها في وصفها‬
ٍ ‫فماذا يعرب القول عن وص‬
* ‫ك او قرين‬
ٌ ‫مشار‬

Vipi yatakua na faswaha maneno katika kumsifu mtu ambae wenyekusifu wameshindwa
kumsifu, ao vipi yatafikia mabongo kufahamu maana ya mtu ambae amekatasika kua
atakua na mfano wake katika sifa zake ao hata aliemkurubia katika sifa zake *

‫ف‬
ِ ‫السنا =للبدر عند تمامه لـم يخسـ‬
َّ ِ ‫َكملت محا‬
‫سنه فلو اهدى‬

Yalikamilika mazuri yake, lau muangaza wake ulipewa


mwezi wakati umetimia, mwezi haungejaliwa kupatwa

‫ف‬
ِ ‫ه مالم يوص‬
ِ ‫ه = يفنى الزمان وفي‬
ِ ‫ه بوصفـ‬
ِ ‫ص ِفي‬
ِ ‫ُّن وا‬
ِ ‫و على تفن‬

Na juu ya uhodari wa wenye kumsifu katika kamsifu, zama zitamalizika na bado


kutakua kuna sifa atakua bado hajasifiwa

*‫فما اجـــل قـــدره الــعـــظـــيـــم * و اوســــع فـــضـــلـــه الــعــمــيـــم‬

Ni utukufu ulioje wa cheo chake kikubwa, na niupana ulioje wa fadhla zake zenye kueneya *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الفصل الرابع عشر‬


MLANGO WA KUMI NA NNE
* ‫ولقد اتصف (صلى هللا عليه وآله سلم) من محاسن األخالق * بما تضيق عن كتابته بطون األوراق‬

Na hakika alisifika Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) kwa uzuri wa tabia, ambazo
zinakua ndogo kuziandika tumbo za karatasi *
* ً‫خلَقاً * و اولهم الى مكارم االخالق سبقا‬
َ ‫كان (صلى هللا عليه وآله سلم) أحسن الناس خلقاً و‬
* ً‫و اوسعهم بالمؤمنين حلماً ورفقا‬

Alikua Mtumi (Rehma na amani zimteremkie) ni mbora wa watu kwa tabia na


maumbile, na alikua kiongozi wao katika tabia njema, na mwenye kuwatosheleza
waumini wote msamaha wake na upole wake *

35 | P a g e
* ‫بــــراً رؤفــــاً * ال يقول و ال يفعل اال معروفا * له الخلق السهل * و اللفظ المحتوي على المعنى الجزل‬

Mtenda wema mwenye huruma, hasemi wala hafanyi ela jambo la lema, alikua na tabia
nyepesi na matamshi ambayo yamekusanya maana mengi *

* ‫إذا دعاه المسكين اجابه اجاب ًة معجلة * و هو األب الشفيق الرحيم لليتيم و األرملة‬

Pindi anapoitwa na maskini anamuitikia haraka haraka, nae ndie baba mwenye kite na
sikitiko kwa mayatima na wajane *

* ‫وله مع سهولة اخالقه الهيبة القوية * التي ترتعد منها فرائص األقويا ِء من البرية‬

Na alikuwa [Mtumi] pamoja na tabia yake laini alikua na haiba ya hali ya juu sana, haiba
ambayo alikua ikitetema kwayo mishipa ya watu wenye nguvu *

* ‫ه تعطرت الطرق و المنازل * و بعرف ذكره تطيبت المجالس و المحافل‬


ِ ‫و من نشر طيب‬

Na kutokamana na kuenea kwa arufu yake mzuri zilinukia vizuri njia na majumba, na
kwa arufu njema ya utayo wake yananukia majaalis na mikusanyiko ya watu *

* ‫ه بإشرف خصوصية‬
ِ ‫ه و خل ِق‬
ِ ‫خل ِق‬
َ ‫فهو جامع الصفات الكمالية * و المنفرد في‬

Kwani yeye [Mtumi] ndie amekusanya sifa zote za ukamilifu, na amepwekeka katika
maumbile yake na tabia zake kwa mambo matukufu aliyokhusiwa yeye pekee *

* ‫ى عن زين الوجود‬
ً ‫فما من خلق في البرية محمود * اال وهو متلق‬

Hivo hakuna tabia njema katika viumbe wote yenye kuhimidiwa, ela tabia kama hiyo
inakua imepokewa kutoka kwa pambo la ulmwengu [Mtumi Muhammad] *

‫أجملت في وصف الحبيب وشأنه = وله العال في مجـده و مكانـه‬

Nimefupisha katika sifa za kipenzi na mambo yake matukufu


na anayo yeye upeo katika utukufu wake na cheo chake

‫عز قد تعالى مجدهـا = اخذت على نجم السهـا بعنانـه‬


ٍ ‫اوصاف‬

Sifa za utukufu zimetakasika utukufu wake


zimepaa zikapaa mpaka katika nyota ya suhaa kwa hatamu yake

‫وقد انبسط القلم في تدوين ما افاده العلم من وقائع مولد النبي الكريم * و حكاية ما اكرم هللا به هذا العبد‬
* ‫المقرب من التكريم والتعظيم والخلق العظيم‬

Imeendelea sana kalamu katika kuandika mambo ambayo imefaidisha elimu kutokamana na
matukio ya kuzaliwa kwa Mtumi alie mkarimu, na kueleza mambo ambayo Mwenyezi Mungu
amemkirimu kwayo huyu mja aliekurubishwa kwa Mola wake kutokamana na mambo
aliyokirimiwa na utukufu aliopewa na tabia njema zenye utukufu *

36 | P a g e
*‫فحسن مني ان أمسك أعنة األقالم في هذا المقام * و اقرأ السالم * على سيد األنام‬

Imekuwa ni bora sasa kwangu ni ziwiye hatamu ya kalamu, katika maqamu haya -hapa
nilipofika-, na nimpishie salamu, Bwana wa viumbe vyote *

)‫السالم عليك ايها النبي ورحمة هللا وبركاته (ثالث مرات‬

“Amani iwe juu yako ewe Mtumi wa Mwenye Izzi Mungu na rehma za Mwenye Izzi
Mungu na Baraka zake” (mara tatu)

*‫وبذلك يحسن الختم كما يحسن التقديم * فعليه افضل الصالة والتسليم‬

Na kwa hili [lakumtakia rehma na amani na baraka kipenzi cha Mola] inapendeza
kukhatimisha kama inavyopendeza -kuanza- kutanguliza, basi ni juu yake Mtumi (rehma
na amani zimteremkie) swala bora na salamu kutoka kwa Mola wake *

‫ل وسل ِّم أشرف الصِّالة والتِّسليم‬


ِّ ‫م ص‬
ِّ ‫الله‬
Ewe Mola mtakie rehma na amani zilizotukufu zaidi
‫مد الرِّؤوف الرِّحيم‬
ِّ ‫على سيِّدنا نبيِّنا مح‬
Bwana wetu na Mtumi wetu mwenyesikitiko mwingi wa sikitiko

‫الدعاء‬
DUA (MAOMBI)
‫ولما نظم الفكر من دراري األوصاف المحمدية عقودا ً * توجهت الى هللا متوسال ً بسيدي و حبيبي محم ٍد ان‬
* ً‫يجعل سعيي فيه مشكوراً و فعلي فيه محمودا‬

Baada ya kutunga akili kutokamana na lulu za sifa za Mtumi Muhhammad mkufu


uliotungamana vizuri * nilielekea kwa Mwenyezi Mungu nikitawasali kwa bwanangu na
kipenzi changu Muhamad ajaalie bidii yangu kwake yeye ni yenye kushukuriwa, na kazi
yangu iwe ni yenye kusifiwa *

* ‫وان يكتب عملي في األعمال المقبولة * و توجهي في التوجهات الخالصة و الصالت الموصوله‬

Na aandike kazi yangu katika amali zenye kukubaliwa * na kuelekea kwangu kwake kue
ni kwenye kuelekea kulikokua na ikhlasi na iwe ni kamba yenye kunifikisha kwake *

37 | P a g e
* ‫اللهم يا من اليه تتوجه المال فتعود ظافرة * و على باب عزته تحط الرحال فتغشاها منه الفيوضات الغامرة‬

Ewe Mola ambae wenye tamaa njema hukuelekea na wakarudi filhali yakua wameyapata
wayatakayo * Ewe Mola ambae katika mlango wa utukufu wako hufungwa misafara ya
ngamia wa kubeba mizigo ikajazwa kutokamana na utukufu wako zipawa tele tele *

‫نتوجه اليك * باشرف الوسائل لديك * سيد المرسلين * عبدك الصادق األمين * سيدنا محمدا الذي عمت‬
* ‫رسالته العالمين‬

Twaelekea kwako, kupitia wasila uliomtukufu zaidi kwako wewe * bwana wa Mitumi
wote * mja wako mkweli na muaminifu * bwana wetu Muhammad ambae utumi wake
umewafinika viumbe vyote *

* ‫أن تصلي وتسلم على تلك الذات الكاملة * مستودع امانتك * و حفيظ سرك * و حامل راية دعوتك الشاملة‬

Ushushe rehma na amani juu ya dhati ya kiumbe huyo aliekamilika * mwenye kueka amana yako *
na mhifadhi wa siri zako * na alieshika bendera ya malinganizi yako yaliokusanya mambo yote *

* ‫موطن من مواطن القرب ومظهر‬


ٍ ‫األب األكبر * المحبوب لك و المخصص بالشرف األفخر * في كل‬

Baba mkubwa wa ummati wake * anaependekeza zaidi kwako * na aliekhusishwa kwa


utukufu wenye fakhari zaidi * katika kila sehemu kutokamana na sehmu za ukaribu
wako na dhahiri *

‫قاسم امدادك في عبادك * وساقي كؤوس ارشادك الهل ودادك * سيد الكونين * و اشرف الثقلين * العبد‬
* ‫المحبوب الخالص * المخصوص منك باجل الخصائص‬

Mwenye kugawanya vipawa vyako kwa waja wako * Mnwesha kinywaji cha uongofu
watu wenye penzi lako* Bwana wa mbinguni na ardhini * Mtukufu wa majini na bin
Adamu * mja anae pendwa zaidi mwenye nasaba safi * aliekhusiwa kwako kwa mambo
khaswa makubwa (matukufu) *

* ‫اللهم صل وسلم عليه وعلى اله واصحابه * واهل حضرة اقترابه من احبابه‬

Ewe Mola mtakie yeye rehma na amani na ali zake na masahaba zake * na
waliojikurubisha nae katika vipenzi vyake *

‫اللهم انا نقدم اليك جاه هذا النبي الكريم * و نتوسل اليك بشرف مقامه العظيم * ان تالحظنا في حركاتنا‬
* ‫و سكناتنا بعين عنايتك‬

Ewe Mola hakika sisi tunatanguliza kwako cheo cha huyu Mtumi mtukufu * na
tunatawasali kwako kwa utukufu wa cheo chake kikubwa * utupeleleze katika harakati
zetu na pia katika utulivu wetu kwa jicho la inaya yako *

38 | P a g e
* ‫وأ ن تحفظنا في جميع اطوارنا و تقلباتنا بجميل رعايتك و حصين وقايتك‬

Na utuhifadhi katika hali zetu na mizunguko yetu kwa malezi yako yaliyomazuri * na
ngome yako yenye kukinga *

* ‫و أن تبلغنا من شرف القرب اليك والى هذا الحبيب غاية امالنا‬

Na utufikishie sisi kutokamana na utukufu wa kujikurubisha kwako na kwa kipenzi


chako mwisho wa matarajiwa yetu *

* ‫و تتقبل منا ما تحركنا فيه من نياتنا و اعمالنا‬

Na ututaqabalie kila ambalo tumeharakisha ndani yake niya zetu na pia amali zetu *

‫و تجعلنا في حضرة هذا الحبيب من الحاضرين* وفي طرائق اتباعه من السالكين * و لحقك وحقه من‬
* ‫المؤديين * ولعهدك من الحافظين‬

Na utujaalie katika hadhra ya kipenzi huyu niwenye kuhudhuria * na utujaalie ni katika


wenye kufuata njia yake iliyonyoka * pia utujaalie ni katika wenye kuitekeleza haqqi
yako na yake * na utujaalie ni kati ya wenye kuhifadhi ahadi yako *

* ‫اللهم ان لنا اطماعاً في رحمتك الخاصة فال تحرمنا * و ظنوناً جميل ًة هي وسيلتنا فال تخيبنا‬

Ewe mola hakika sisi tuna tamaa na rehema zako khaswa (maalumu), basi usitukoseshe rehma
zako * na dhanna mzuri juu yako ndio wasila wetu kwako wewe basi usitupitishe patupu *

* ‫ام َّنا بك و برسولك وما جاء به من الدين * و توجهنا به إليك مستشفعين‬

Tumekuamini wewe na Mtumi wako na yote aliyokuja nayo katika mambo ya dini * na
tumeekelea kwako kupitia yeye tukiomba shufaa *

* ‫ان تقابل المذنب منا بالغفران * و المسيء باإلحسان * و السائل بما سأل * والمؤمل بما امل‬

Umqabili alietenda makosa kati yetu kwa msamaha * na mkosa umqabili kwa ihsani * na
aliekuomba umpatie alichokuomba * na mwenye tamaa kwako umpatie alichokitamani *

* ‫وان تجعلنا ممن نصر هذا الحبيب و وازره * و وااله و ظاهره‬

Na utujaalie sisi ni kati ya waliomnusuru huyu kipenzi wako na kumsaidia * pia utujaalie
ni kati ya waliomueka mbele Mtumi katika mambo yao yote na wakamuawini *

‫م ببركته و شريف وجهته اوالدنا ووالدينا * و اهل قطرنا و وادينا * و جميع المسلمين والمسلمات * و‬
َّ ‫وع‬
* ‫المؤمنين والمؤمنات * في جميع الجهات‬

Ueneze kwa baraka zake na kwa utukufu wa muongozo wake vijana wetu na wazee
wetu * na watu wa eneo letu na bonde letu * na waisilamu wote wakiume na wakike *
na waumini wa kiume na wa kike * katika pembe zote [popote pale walipo] *

39 | P a g e
* ‫ى و صورة‬
ً ‫و ادم راية الدين القويم في جميع األقطار منشورة * و معالم األسالم واأليمان باهلها معمورة معن‬

Na uidumishe bendera ya dini iliyonyoka katika majimbo yote hali yakua yapepea * na
mafundisho ya uislamu na imani yaimarike kwa watu wa majimbo yote * kwa siri na dhahiri *

* ‫و اكشف اللهم كربة المكروبين * و اقض دين المدينين * و اغفر للمذنبين * و تقبل توبة التائبين‬

Ewe Mola waondeshee makero waliofikwa na makero * na uwalipie madeni wanaodaiwa


* na uwasamehe waliokukosea * utakabali tauba za wenye kutubia *

* ‫و انشر رحمتك على عبادك المؤمنين اجمعين * و اكف شر المعتدين و الظالمين‬

Na utapakaze sikitiko lako juu ya waja zako waumini wote * na ukomeshe shari la
mashari na madhalimu *

‫و ابسط العدل بوالة الحق في جميع النواحي واألقطار * وايدهم بتأييد من عندك و نصرٍ على المعاندين من‬
* ‫المنافقين و الكفار‬

Na ueneze uadilifu katika viongozi wa haqqi katika pembe zote na majimbo yote * na
uwatilie nguvu zitokamanazo nawewe na nusura juu ya wale washindani kutokamana
na wanafiki na makafiri *

* ‫و اجعلنا يارب في الحصن الحصين من جميع الباليا * و في الحرز المكين من الذنوب والخطايا‬

Utujaalie Ewe Mola katika ngome yenye kukenga na kila balaya * na ututie kwenye hirzi
ya kisawasawa yakutuzuwiliya na madhambi na makosa *

* ‫و ادمنا في العمل بطاعتك و الصدق في خدمتك قائمين‬

Na utudumishe katika kutekeleza twaa yako na tusimame wima na tuwe na ukweli


katika kukutumikia *

* ‫و إذا توفيتنا فتوفنا مسلمين مؤمنين * و اختم لنا منك بخير اجمعين‬

Na ukitufisha utufishe hali ya kua waisilamu na waumini * na mwisho wetu sote uwe
mwisho mwema *

* ‫وصل وسلم على هذا الحبيب المحبوب * لألجسام واألرواح و القلوب * و على اله وصحبه و من اليه منسوب‬

Na umtakie rehma na amani huyu kipenzi anae pendezeka * katika miili na roho na
nyoyo -za waumini- * pia uwatakie rehma na amani aali zake na swahaba zake na
yoyote anaenasibiana naye *

* ‫و آخر دعوانا أن الحمدهلل رب العالمين‬

Na mwisho wa maombi yetu twamshukuru Mwenyezi Mungu mlezi wa viumbe vyote.

40 | P a g e
FAHRASI

# Yaliomo Ukurasa
1 Utangulizi wa mfasiri 1
2 Utangulizi wa msahihishaji 4
3 Shangilio la Habib Ali Al-Habshi (Munswib) 5
4 Utangulizi wa mchapishaji 6
5 Kiingilio cha Swala za Mtumi 8
6 Mlango wa kwanza 11
7 Mlango wa pili 12
8 Mlango wa tatu 13
9 Mlango wa nne 15
10 Mlango wa tano 17
11 Mlango wa sita 19
12 Mlango wa saba 20
13 Maqamu (Kisimamo) 21
14 Mlango wa nane 23
15 Mlango wa tisia 25
16 Mlango wa kumi 27
17 Mlango wa kumi na moja 29
18 Mlango wa kumi na mbili 30
19 Mlango wa kumi na tatu 32
20 Mlango wa kumi na nne 35
21 Dua (Maombi) 37
22 Fahrasi 41

41 | P a g e

You might also like