Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

LIGHT AFRICA SECONDARY SCHOOL MASANAFU

MTIHANI WA KISWAHILI.

Kidato Cha tatu(S.3)2024.

Mwisho wa muhula wa kwanza.

UFAHAMU NA UCHAMBUZI WA FASIHI.

Masaa mawili tu (2hrs only).

Jibu maswali matatu Three questions

SEHEMU A.

1.Mnakaribia siku ya wazazi kuwatembelea wanafunzi shuleni na mwalimu mkuu amewambia kualika
wazazi wenu kuwatembelea siku hiyo. Andikia mamako barua ukimwalika kukutembelea siku hiyo na
kukuletea vitu vya kutumia.

2.Umechaguliwa kama kiongozi wa afya na usafi katika shule yako na mwalimu mkuu amekupa nafasi
ya kuongea kuhusu njisi ya kudumisha afya na usafi katika shule yako.Andika hotuba utakayowatolea
wanafunzi wenzako.

3. SOMA TAARIFA HII KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA.

USAFIRI.

Usafiri ni shughuli ya mwendo wa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine ya watu na vitu vingine.
Inasaidia katika uchukuzi wa mizigo mbalimbali pamoja na binadamu. Usafiri ni WA aina mbalimbali
kama vile; Usafiri wa ardhi unaojumuisha usafiri wa barabarani Kwa matumizi ya
magari,pikipiki,baiskeri,teksi,basi,rori na magari mengine ya watu bunafsi. Magari haya yote, husaidia
watu na mizigo yao kutoka Mahali Fulani mpaka mahali pengine. Pia, kuna usafiri mwingine wa ardhi
ambao ni wa wanyama kama vile; matumizi ya punda, farasi na ngamia wanaochukua watu na mizigo
yao.

Hali kadhalika, Kuna usafiri wa angani ambapo watu hutumia helikopta na eropleni kusafiri kutoka
sehemu moja hadi sehemu nyingine Kwa shughuli mbalimbali. Kwa mfano watu husafiri hadi nchi
nyingine Kwa sababu ya masomo, kufanya biashara, utalii na kuhama.

Fauka ya hayo, Kuna aina nyingine ya usafiri wa majini. Hii inatumia vyombo vya majini kama vile;
mashua,mitumbwi,meli na kadhalika.

Kwa upande mwingine, Kuna aina nyingine ya usafiri wa reli. Usafiri huu una barabara yake maalumu
inayojengwa Kwa vyuma vilivyokongomewa ardhini. Aina hii inatumia chombo kimoja tu. Chombo hicho
ni Garimoshi/treni. Garimoshi hubeba mizigo mikubwa pia mingi pamoja na watu wengi Kwa sababu ya
ukubwa wake

Ingawa hivyo, vyombo vyote vya usafiri vinaendeshwa na watu waliofunzwa na kufuzu. Hii ni kwa
sababu ya kuzuia ajari.
1
MASWALI

(a). Kwa nini vyombo vya usafiri vinaendeshwa na watu waliofunzwa na kufuzu? (Alama 03)
(b). Taja kichwa cha habari hii. (Alama 02)
(ch). Toa aina tatu za usafiri kutoka habari hii.( Alama 03)
(d). Toa sababu mbili kwani watu husafiri hadi nchi nyingine. (Alama 04)
(e). Kulingana na ujumbe huu, "Usafiri" ni nini? (Alama 02)
(f). Taja vyombo sita vinavyotumika katika usafiri wa ardhi.(Alama 03)
(g). Andika majina ya wanyama ambao ni vyombo vya usafiri kulingana na makala haya.(Alarm 02)
(h). Ni vyombo Gani vinavyotumika katika usafiri wa angani. Toa vyombo viwili. (Alama 02)
(I). Mashua, mitumbwi na meli ni vyombo vya aina gani ya usafiri? (Alama 02)
(j). Taja aina ya usafiri yenye chombo kimoja tu. Taja chombo hicho. (Alama 02)
(k). Kwenye barabara za Uganda, kunatokea ajali nyingi Kila mwezi. Tacha vyanzo/visababishi vya ajali
barabarani. (Alama 05).
SEHEMU B
4. SOMA USHAIRI KISHA UJIBU MASWALI:

HAKI YAKO

Dhuluma isikuzike, nakwambia makanika,


Sogeeni nisikike, Kaa kitako pulika,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.

Kwanza nakwambia juwa, ni hakiyo kulelewa,


Chakula chema kupewa, pia malazi kupewa,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.

Pili pindi uguapo, tiba ni haki kupewa,


Hosipitali fikapo, ni sawa upewe dawa,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.

Tatu pia nakwambia, kusoma we ni lazima,


Shule ukisha ingia, vitabu ni kuvusoma,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.

Nne kusema siache, mawazo yako baini,


Ukweli katu sifiche, ni haki kuongeeni,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.

Mwisho nataka kwambia, tumezawa nazo haki,


Ni Kosa kuzubalia, zitwaliwe Kwa mkuki,
Ni yako haki ishike, usikubali kupokwa.
2
MASWALI

(a). Taja kichwa cha shairi hili. (Alama 03)

(b). Shairi hili lina beti ngapi? ( Alama 03)

(ch). Shairi hili lina mistari mingapi katika Kila ubeti? ( Alama 03)

(d). Andika kibwagizo cha shairi hili. (Alama 03)

(e). Mshororo wa kwanza katika Ubeti wa pili una mizani ngapi? (Alama 03)

(f). Ubeti wote wa pili una mizani ngapi? (Alama 03)

(g). Shairi hili lote Kwa jumla Lina mizani ngapi? (Alama 03)

(h). Taja vina vya kati katika Ubeti wa mwisho. (Alama 03)

(I). Onyesha vina vya mwisho Katika Ubeti wa Kwanza. (Alama 03)

KISWAHILI MBELE, NYUMA HATURUDI.


**TAMATI**

You might also like