Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

1

KANUNI
UMOJA WA TUNAJALIANA

1. SIFA ZA MWANACHAMA
a) Mwanachama kulipa ADA mara moja anapojiunga;
b) Mwanachama anafanya MAJERESHO ya michango iliyotolewa na Chama kwa niaba yake
ndani ya Mwezi (1) Mmoja;
c) Mwanachama asipohudhuria vikao (3) vitatu mfululizo, anapoteza uanachama wake na
haki zake zote, isipokuwa kama ana sababu za msingi kwa kutoa taarifa RASMI;
d) Endapo Mwanachama ataamua kujitoa kwa hiyari yake mwenyewe kwenye chama,
atapoteza haki zake zote.

2. ADA
a) ADA ya mwanachama ni Tshs 600,000/= (LAKI SITA);
b) Kutakuwa na nyongeza ya thamani ya mwanachama ya Tshs 200,000/= (LAKI MBILI) kwa
kila mwanzoni mwa mwaka;
c) Aidha kutakuwa na RIBA ya asilimia 10 kwenye nyongeza ya thamani ya mwanachama
kwa kila baada ya MIEZI MITATU (3) kupita. Vilevile, kila baada ya Miezi MITATU (03)
mingine kupita kutakuwa na ongezeko ASILIMIA 10 nyingine;
d) Mtu asipolipa ADA anakuwa si MWANACHAMA.

3. SHUGHULI ZA KIUCHUMI
a) Kukopeshana kwa riba ya ASILIMIA 10 (sio zaidi ya miezi mitatu na sio zaidi ya asilimia 80
ya fedha zake zote zilizo kwenye mfuko wa chama). Aidha kutakuwa na ongezeko la RIBA
ya ASILIMIA 10 kwa kila MIEZI MITATU (03) kupita;
b) Kama mwanachama anayetaka kukopa atakuwa na DENI, atakatwa tofauti kufidia DENI
lake la awali;
c) Shughuli nyingine itakayoamuliwa na KIKUNDI kupitia VIKAO halali;
d) Kutakuwa na nyongeza ya Tshs 200,000/= LAKI MBILI kila mwaka kama ongezeko la
thamani ya kila mwanachama.

4. KUSAIDIANA WAKATI WA SHIDA


a) Mwanachama akipoteza maisha Chama kitatoa LAKI TANO (500,000.00) kwa familia;
b) Tegemezi wa mwanachama akipoteza maisha Chama kitatoa LAKI TATU (300,000.00)
kwa mwanachama;
c) Mwanachama akilazwa zaidi ya siku (3) tatu (SIO MAPUMZIKO) anapatiwana Chama
ELFU HAMSINI (50,000.00); ya kumfariji;
d) Tegemezi wa mwanachama akilazwa zaidi ya siku (3) tatu (SIO MAPUNZIKO) anapatiwa
na Chama ELFU ISHIRINI NA TANO (25,000.00);
e) Ni LAZIMA kushiriki tukio la SHIDA la mwanachama au wategemezi wake;
f) Aidha, kulazwa muda mrefu kutokana na ugonjwa ama ajali chama kitajadili kutokana na
uzito wa ugonjwa ama ajali husika.

5. KUSHIRIKIANA WAKATI WA RAHA


a) Mwanachama AKIOA/OLEWA anapatiwa na Chama LAKI TATU (300,000.00) kama
mchango wa ZAWADI;
b) Tegemezi wa mwanachama AKIOA/OLEWA anapatiwa na Chama LAKI TATU
(300,000.00) kama mchango wa ZAWADI;
2

c) Mwanachama AKIOA/OLEWA anachangiwa si chini ya LAKI MOJA (100,000.00) toka kwa


kila Mwanachama ili kufanikisha ndoa/harusiI hiyo.
d) Tegemezi wa mwanachama AKIOA/OLEWA anachangiwa si chini ya LAKI MOJA
(100,000.00) toka kwa kila Mwanachama ili kufanikisha ndoa/harusi hiyo;
e) Shughuli nyingine zinazohusu wanachama/wategemezi kwa mfano:- Kipaimara, Maulid,
Komunio, Kujifungua. Wanachama watachangia kreti 2 za soda na 2 za bia;
f) Ni LAZIMA kushiriki tukio la RAHA la mwanachama au wategemezi wake ENDAPO
kutakuwa na MWALIKO;
g) Ni wajibu wa kila Mwanachama kutoa taarifa ya shughuli yake walau wiki moja kabla
kama angependa wanachama wenzake washiriki.

6. WATEGEMEZI WA MWANACHAMA
a) Wategemezi wa mwanachama ni wale ambao wameainishwa na kutambuliwa na
KATIBA.

7. UPEWAJI HUDUMA KWA MWANACHAMA MPYA


a) Mwanachama mpya atapewa huduma baada ya miezi 3 kupita tangu kujiunga na chama
kwa kulipa ADA pamoja na ongezeko la thamani la mwanachama.

8. MAWASILIANO
a) Mwanachama anawajibika kutoa TAARIFA ya TUKIO lolote liwe la SHIDA ama RAHA
kupitia njia rasmi za mawasiliano kama kupiga simu kwa kiongozi ama viongozi;
b) Kutuma ujumbe mfupi kwa kiongozi ama viongozi, kutuma barua pepe kwa kiongozi ama
viongozi;
c) Kutuma ujumbe kupitia kikundi cha WHATSAPP

9. MICHANGO NA UREJESHAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI


a) Kila linapotokea TUKIO liwe la SHIDA ama RAHA pesa itatolewa mara MOJA kwenye
KIKUNDI halafu ITARUDISHWA na wanachama si zaidi ya mwezi MMOJA baada ya TUKIO
kutokea;
b) Mwanachama atafaidika na mafao yaliyotajwa hapo juu endapo tu atakuwa
amekamilisha Ada yake ya uanachama na ongezeko la thamani la mwanachama.

10. FAIDA MWISHO WA MWAKA


a) Kila mwisho wa mwaka kila mwanachama atapewa faida ya mfuko wa chama (kutokana
na faida za riba na shughuli zingine za kiuchumi);
b) Pesa ya msingi (ukiondoa faida) itabaki kwenye chama.

11. WANACHAMA WAPYA


a) Kila mwanachama MPYA atapaswa kulipa kiingilio cha Shilingi LAKI SITA (600,000.00);
b) Aidha mwanachama Mpya pia atapaswa kulipa nyongeza ya thamani ya Mwanachama
mmoja katika Chama kwa wakati huo.

12. MKUTANO WA WANACHAMA WOTE


a) Kutakuwa na Mkutano wa Wanachama wote mara moja kwa Mwezi, Mkutano huo
utafanyika JUMAMOSI ya Mwisho wa Mwezi;
b) Aidha kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa mujibu wa KATIBA ya CHAMA;
c) Mkutano wa dharura unaweza kuitishwa wakati wowote kama kuna jambo la dharura
linalohusu Umoja limetokea.

You might also like