TAARIFA KUHUSU KUHUDHURIA KIKAO CHA MAREKEBISHO YA
BOTI AINA YA MV MIKOKO 3 TSC/DAR 103 MKOANI TANGA.
Husika na somo tajwa hapo juu, Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania ilinunua boti mpya ya Mikoko Tanga yenye namba za usajili TSC/DAR.103 kwa Kampuni ya utengenezaji Boti inayoitwa Sam & Anzai Boat Builders Co.Ltd mnamo tarehe 29/06/2019 kwa lengo la kuthibiti matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa kwa kuhakikisha Doria inafanyika kwa ukamilifu pasipo kizuzi chochote Mkoani Tanga. Aidha muda mfupi baada ya Boti hiyo kukabidhiwa kwa Wakala ilibainika kuwa na hitilafu na mapungufu kadhawakadha yaliyopelekea watumiaji wa Boti kushindwa kufanya kazi ya Doria kama ilivyotarajiwa. Kwakuwa Mtengenezaji na Muuzaji wa Boti hiyo alitoa hati ya ubora na matengenezo (Warranty Certificate) kwa muda wa mwaka mmoja toka kununuliwa kwa Boti hiyo,Wakala ulifanya mawasiliano nae ili kurekebisha hitilafu hizo zilizojitokeza.Pamoja na mawasiliano hayo mtengenezaji wa Boti hiyo hakuweza kufanya kazi hiyo kwa wakati,kupelekea kuandaa kikao cha pamoja kati ya Kampuni hiyo pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu. Hata hivyo baada ya kufanya kikao kifupi na kutembelea eneo ilipo boti hiyo,mtengenezaji na Muuzaji wa Boti hiyo alirekebisha hitilafu zote zilizokuwa zimeainishwa katika ripoti ya ukaguzi iliyojumuisha pande zote mbili. Pamoja na Dokezo hili, naomba kuwasilisha muhutasari wa kikao hicho unaotoa ufafanuzi zaidi. Naomba kuwasilisha,