Kiswahili Final Teaching With-nf-V4

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

KUFUNDISHA KWA KUTUMIA VITABU VYA HADITHI

SI BUNILIZI, DARASA LA 3-4


MATINI YA KUJIFUNZIA KATIKA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA (JZK)

UTANGULIZI
Kusoma-ili-Kujifunza ni hatua muhimu wanafunzi wa darasa la 3-4 hupitia. Kusoma maudhui ya habari kama vile
yale yanayopatikana katika Sayansi, Sayansi ya Jamii, Hisabati, Lishe na Uraia ni ujuzi wa kudumu na ni hatua
muhimu katika kujifunza mahiri mpya. Kwa kutumia vitabu vya hadithi si bunilizi vya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)
pamoja na vitabu vya kiada vya mahiri husika, unaweza kufundisha mahiri muhimu ya somo huku ukisaidia kukuza
ujuzi wa kusoma kwa wanafunzi wako. Vitabu vya hadithi si bunilizi vinaweza pia kutumika wakati wa masomo ya
Kusoma na Kuandika.

Kitini hiki cha Kujifunzia kina maudhui mawili:


• Kukupa wewe na wenzako ujuzi kuhusu kufundisha kwa kutumia vitabu si bunilizi, kujadili na kufanya mazoezi
katika Jumuiya za kujifunza (JZK).
• Kukupa mikakati na shughuli za kufanya na wanafunzi unapofundisha maeneo ya somo kama vile Sayansi,
Hisabati, Kusoma na Kuandika.

JINSI YA KUFUNDISHA KWA KUTUMIA VITABU SI BUNILIZI


1. Andaa somo
Tambua mahiri kuu kama zilivyobainishwa kwenye mtaala. Kwa mfano, “Mwanafunzi
ajenge umahiri wa kutaja/kutambua rasilimali na jinsi zinavyoweza kusaidia
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.“
• Soma kitabu wewe mwenyewe kwa umakini kabla ya kuanza somo. Chagua
sehemu utakayofundisha kwa siku hiyo.
• Chagua maneno matatu (3) mapya ya msamiati kutoka katika kitabu
ulichosoma na uandae zana za kufundishia msamiati husika kwa mfano; kadi
za maneno, picha, nk.
• Zingatia mkakati wa kusoma katika vikundi (kuchangia kitabu) wakati wa somo
husika (jozi, vikundi vidogo).

2. Kabla ya Kusoma
• Soma ,”Rasilimali zetu”, na ueleze lengo la kujifunza:
• Leo tutajifunza kuhusu maliasili za Tanzania kama vile milima, maziwa na
bahari.
• Waulize wanafunzi waeleze wanachofahamu kuhusu ‘Rasilimali zetu.’
Toa maana ya neno hilo kama inahitajika.
• Uliza: Unafikiri tutajifunza nini kutokana na kitabu hiki? Jadili kile ambacho
darasa linaweza kujifunza kutokana na kitabu husika – Uliza kama kuna
anayeweza kujitolea kueleza watakachojifunza kutoka katika kitabu husika, na
kisha muite mvulana na msichana ambaye hajanyanyua mkono.
• Malizia utangulizi wa kitabu kwa kuuliza: Je, unadhani kitabu hiki kitajibu
maswali gani kuhusu Rasilimali Zetu? (Nakili majibu yao kwenye ubao.)
• Tambulisha na jadili maneno matatu (3) ya msamiati mpya.

Mazingira: Vitu vyote vinavyomzunguka binadamu.


Maliasili: Vitu vya thamani ambavyo binadamu huvitumia, mfano ardhi na misitu.
Rasilimali: Vitu vya thamani vinavyotegemewa na taifa, shirika au watu binafsi katika uchumi na maendeleo.
KUFUNDISHA KWA KUTUMIA VITABU VYA HADITHI
SI BUNILIZI, DARASA LA 3-4
MATINI YA KUJIFUNZIA KATIKA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA (JZK)

3. Wakati wa Kusoma
Soma kitabu pamoja na wanafunzi, tulia kila baada ya aya na uliza maswali ambayo yanasaidia kujenga uelewa wa
wanafunzi kuhusiana na habari wanayosoma. Kwa mfano:
• Chagua sentensi au maelezo kutoka kwenye kitabu, inasema/yanasema nini kuhusu Rasilimali Zetu?
• Sehemu hii ya kitabu au maelezo haya yanatuambia nini? (Wazo kuu)
• Toa maoni ikiwa maswali ya wanafunzi yamejibiwa.
• Uliza: Je, uliona neno la msamiati katika sentensi au maelezo? Hebu soma tena sentensi hiyo na ufikirie, neno
hilo linamaanisha nini?
• Uliza maswali mengine yoyote ya umahiri husika ili kuboresha na kuongeza uelewa.

4. Baada ya kusoma
Tumia mbinu ya kuuliza maswali ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza njia za kufikiria kuhusu matini.

MASWALI RAHISI MASWALI YA KUFIKIRISHA

• Wanafunzi wanaweza kupata majibu moja kwa • Wanafunzi wanatakiwa kufikiri kwa kina ili kujibu
moja kama yalivyosemwa katika matini. maswali haya kwa kuchanganya walichosoma
na mtazamo wao wa kiulimwengu na uzoefu wa
maisha.
Mfano: Taja aina mbili za misitu iliyopo Tanzania. Kwa Mfano: Je, ungependa kutembelea mbuga gani ya
wanyama? Kwa nini?

Wazo Kuu - Wazo kuu ni kiini cha kifungu husika. Kwa kawaida, ni jambo kuu ambalo mwandishi anataka msomaji
akumbuke. Maelezo katika matini yanajipambanua, yanathibitisha, na kuonyesha wazo kuu. Tumia maswali haya
kuwasaidia wanafunzi kutambua wazo kuu:
• Ni mada gani muhimu zaidi katika matini/ukurasa/aya hii? Mfano: Kuna rasilimali nyingi Tanzania.
• Je, kifungu hiki kinakufundisha dhana gani kuu? Ni lazima wote tufanye kazi kuhifadhi maliasili zetu.

Mazoezi ya Uandishi wa mfano wa hadithi si bunilizi.


• Tengeneza orodha ya maliasili tatu (3) zinazopatikana
katika eneo letu. Andika sentensi moja kuhusu kwa
nini rasilimali ni muhimu.
• Chora na uweke lebo picha za wanyama
wanaopatikana katika mbuga tatu za kitaifa za
Tanzania.
• Andika aya kuhusu jinsi utakavyosaidia kulinda
maliasili ulizojifunza katika kitabu hiki.
KUFUNDISHA KWA KUTUMIA VITABU VYA HADITHI
SI BUNILIZI, DARASA LA 3-4
MATINI YA KUJIFUNZIA KATIKA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA (JZK)

1. Changamoto na Suluhisho: 
• Panga idadi ya vitabu na idadi ya wanafunzi. Kama inawezekana panga wanafunzi 4-5 washiriki kutumia
kitabu kimoja.
• Azima nakala za ziada kutoka kwa mwalimu mwingine.
• Kaa na kundi kubwa zaidi na usome kwa pamoja na wanafunzi hao kwa sauti.

2. Mikakati ya ujumuishi
• Hakikisha watoto wenye matatizo ya uoni wanakaa karibu na kurasa/kitabu.

3. Mikakati ya upimaji endelevu


• Waambie wanafunzi washirikishane wazo kuu
walilolipata katika usomaji wa kitabu cha hadithi
si bunilizi na wenzao. Tembea katika jozi zao na
uwasikilize.
• Waambie wanafunzi waandike neno moja jipya
la msamiati na wachore picha yake kwenye
karatasi ya tiketi ya kutokea ambayo huwa
wanaiweka wakati wa kutoka kipindi cha
mapumziko, chakula cha mchana au mwishoni
mwa kipindi.

KUFUNGA

Kusoma matini ya hadithi si bunilizi ni ujuzi ambao ni muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma. Watoto pia wanapenda
kujifunza kuhusu ulimwengu unaowazunguka. Endelea na mjadala huu wa mikakati ya kutumia vitabu vya hadithi
si bunilizi na wenzako, mnasihi wako na katika Jumuiya za Kujifunza (JZK). Maswali haya ya mjadala yanaweza kuwa
muhimu:

1. Je, ni changamoto gani unapata wakati wa kutumia vitabu vya hadithi si bunilizi kwenye ufindishaji wa
masomo ya kusoma na kuandika? Jadili suluhisho linalowezekana.
2. Je! ni kwa kiasi gani wanafunzi wako wanajifunza kubainisha wazo kuu katika usomaji wao?
Je, unawasaidia vipi kufikia lengo hilo?
3. Je, ni kwa namna gani unaandaa maswali ya kufikiri kwa kina na yenye ushahidi?

You might also like