Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 93

1

DIBAJI

INSHA za Kifalme ni mkusanyiko wa insha/makala


mbalimbali zilizoandikwa kwa nyakati tofauti tofauti na
Mwalimu Charkes Mganda John.
Katika Insha hizo kuna mengi ya kujifunza,
kustaajabisha na kujenga. Katika mfululizo huu, jumla
ya Insha 8 zimechambuliwa kama vile “Saikolojia ya
Umri, Ugonjwa wa kutosamehe, Saikolojia ya hasira,
Ugonjwa wa Hofu, Ukweli kuhusu Pombe, Ukweli
kuhusu Uraibu, Shabaha ya Urafiki na Uhusiano wa akili
na imani! Hivyo kwa moyo wa ukarimu nakualika
usome ujumbe uliomo katika insha hizo!

0756 286 804


0787 339 343

Charles Mganda John


Joyland International Schools – Dar es Salaam

2
SURA YA KWANZA
SAIKOLOJIA YA UMRI
UMRI kwa fasili ya kawaida ni hesabu ya muda uliopita
tangu kiumbehai kianze kuwepo. Mintarafu, umri wa
binadamu na wanyama huanza kuhesabika mara baada
ya kuzaliwa!
Kama mtu alizaliwa mwaka 2011 basi mwaka 2021
atahesabika kuwa na umri wa miaka 10!
Kama hakuna mwingiliano wa tatizo lolote, Umri wa
binadamu na viumbe wengine hutakiwa kwenda
sambamba na mwonekano wa mwili, uwezo wa
akili/fikra, nafasi katika jamii hata uwezo kiuchumi.
Yaan kadiri umri wa kuzaliwa unavyosonga, basi
vilevile hutegemewa ukuaji huohuo uonekane katika
akili na nafasi ya mtu kijamii.
UMRI KATIKA SAIKOLOJIA
Katika saikolojia umri wa kiumbe hai hasa binadamu
hupimwa kwa kuzingatia mambo kadhaa anuai, siyo
idadi ya miaka tu!
Kwa hiyo unapotaja umri wako katika mukutadha wa
saikolojia ni muhimu kuzingatia aina husika ya umri!
AINA YA UMRI
Zipo aina nyingi za umri katika mukutadha za saikolojia,
na hapa nitachambua aina tano kama ifuatavyo!

3
1. UMRI WENDO (Chronological age)

Huu ndiyo umri unaofahamika na kuzoeleka na


kila mtu! Hii ndiyo hesabu ya muda uliopita
tangu kiumbehai kianze kuwepo. Sherehe za
kuzaliwa (Birthday) karibia zote huzingatia umri
wendo!

2. UMRI WA KIMAUMBILE/KIBAIOLOJI
(Biological/physiological age)

Huu ni umri wa kimaumbile unaoangazia zaidi


mwonekano wa mtu ukilinganisha na miaka
yake! Umri huu wa kimaumbile unaweza
kupatana au usipatane na ule wa
chronojia/wendo!

Kwa mfano kijana mbichi kabisa wa miaka ya


kuzaliwa 24 anaweza kuonekana kama mzee wa
miaka 65, ukilinganisha na vijana wengine wa
umri au rika lake! Hii husababishwa na mtindo
wa maisha, afya, aina ya kazi, mazingira,
magojwa nk!

Kwa mfano kijana anayefanya kazi nzito katika


mazingira duni, lishe mbovu na matumizi ya
vilevi vikali, viroba, tumbaku, ugoro nk huzeeka
zaidi kimwili ukilinganisha na vijana wengine
wenye mtindo mzuri wa maisha!

4
Vilevile unaweza kumwona mtu ana mwonekano
kama kijana wa miaka 40, kumbe ni mzee na
yuko kwenye 60+

**Ukipata nafasi ya kuandikisha sensa au kusajiri


SIM card au kuandikisha wapiga kura au namba
za NIDA unaweza kuelewa zaidi
ninachozungumza hapa! Kwamba mtu anakuja
na vielelezo sahihi kabisa kwamba kazaliwa
mwaka 1995, lakini wewe unamwona mama mtu
mzima kana kwamba alizaliwa 1963, na
umeshampa shikamoo yake! Hujawahi kukutana
na watu wa aina hiyo?

Hali hii inamaanisha umri wake wa kimaumbile


ni mkubwa sana ukilinganisha na umri wake wa
kuzaliwa! Kwa hiyo huyo huhesabika kuwa ni
mzee kabisa aliyekula chumvi nyingi japo ana
miaka 26 tu!

3. UMRI WA KISAIKOLOJIA (Psychological


age)
Huu ni umri wa kihisia na kimtazamo zaidi! Kwamba
mtu anajichukulije yeye mwenyewe, ni mzee au kijana!
Kwa hiyo hapa ni namna mtu anavyojihisi na kufikiria
kuhusu umri wake!
Kwa mfano vijana wanaobalehe na kuvunja ungo,
huanza kujiona kama watu wazima sana na kujiingiza
kwenye ngono, japo umri wao bado 13,15,17 nk! Hii
maana yake ni kwamba kifikra hudhania kwamba

5
wameshakuwa wakubwa sana japo kimwili na kiakili
bado sana!

Hali hii pia huwakuta baadhi ya wazee kwa umri wa


kuzaliwa kushindwa kukubali hali ya uzee!
Unamsalimia shikamoo lakini anakujibu mambo? Hii
inamaanisha kuwa japo amezeeka lakini bado yeye
anajiona kijana mdogo! Ndiyo chanzo cha baba mtu
mzima kuhangaika na vibinti vidogo vodogo!
Unaukumbuka msemo wa uzee mwisho chalinze mjini
wote baby? Huo ndiyo mfano wa fikra za wazee na
vijana kuhusu umri wa kisaikolojia!

4. UMRI WA KIJAMII NA KIUCHUMI (social


age)
Kwa mujibu wa (Tibbits 1960) umri wa kijamii
hupimwa kwa kuzingatia matarajio ya jamii kwa mtu,
kama vile tabia, kazi na mafanikio!
Umri huu pia hauhusiani moja kwa moja na idadi ya
miaka ya kuzaliwa!
Kwa mfano kijana mdogo anayefanikiwa kumiliki mali
na kuwa na busara inayokidhi matarajio ya jamii yake
basi huhesabika kama mzee kijamii na huheshimiwa na
watu wote kwa heshima ileile wanayopewa wazee!
Halikadharika mzee mwenye tabia za kitoto huhesabika
kama mtoto kwenye jamii! Utasikia Fulani ni mzee

6
kijana na hupewa heshima kidogo kama vijana wengine
wasio wa umri au rika lake!

**Unaweza ukawa mzee kwa miaka ya namba, lakini


kijamii na kiuchumi ukaonekana mtoto mdogo kabisa.
Ishara ya wazi ya kuwa wewe ni mtoto ingawa una mvi
na umezeeka kwelikweli ni pale utakapoona huombwi
ushauri wala kutoa mawazo kwenye vikao vya ukoo
mpaka vile vya serikali ya mtaa! Na pengine ukitaka
kuzungumza wanakuzomea au kukunyamazisha bila hata
ya kukusikiliza! Ukiona hivyo usiumie sana, ujue wewe
ni mtoto sana kijamii, lakini hujatambua tu!
Kwa hiyo kijamii kama nilivyotangulia kusema kule juu
umri hupimwa kwa kuzingatia matarajio ya jamii, tabia,
kazi nk. Kumbe ni muhimu sana ukuaji wa mwili
ukienda sambamba na ukuaji wa akili na maendeleo ya
kiuchumi.
Mwandishi mmoja wa zamani alipata kuhoji na hapa
chini namnukuu!
Yoshua bin Sira 25:3 “Katika ujana wako
hukukusanya; utapata wapi upatapo kuwa mzee?”

5. UMRI WA AKILI (mental age)

Umri wa akili wakati mwingine hujulikana kama hisa ya


akili maarufu kama IQ. Aina hii ya umri huweza
kukokotolewa kimahesabu baada ya kupewa jaribio
maalumu la kupima uwezo wa akili.
7
Kwa hiyo unaweza kabisa kuwa na miaka 48 ya
kuzaliwa lakini umri wako wa akili ukawa miaka 12 tu.

Kwa lugha rahisi ni kwamba, kwa kawaida umri wa


miaka ya kuzaliwa hupaswa kwenda sambamba la
uwezo wa kiakili. Sasa kama uelewa wako unafanana na
ule wa kijana wa miaka 12 maana yake ni kwamba
japokuwa wewe una miaka 48 lakini umri wako wa akili
ni miaka 12.
Vile vile mtoto wa miaka 5 akiwa na ufahamu wa
wastani wa mtu wa mika 35, umri wake wa akili
utahesabika kuwa miaka 35 japo ana miaka 5.
**Hujawahi kuona mtu mzima anayependa midoli na
anaimiliki?
Au mtoto mdogo akifanya matendo ya kikubwa?
Hujawahi kusikia watu wananong’ona kwamba “Mtoto
huyu ni kama mtu mzima kabisa!” swala siyo ni ‘kama’
mtu mzima, jibu la kweli ni MTU MZIMA KABISA
KWENYE ENEO LA AKILI!

MAELEZO YENYE KUFAA


Yoshua Bin Sira 10:30 “Maskini hutukukzwa kwa
akili zake: na tajiri hutukuzwa kwa mali zake.”

1. Kwa kawaida umri wa kuzaliwa (wendo)


hupaswa kwenda sambamba na ongezeko la

8
akili/ufahamu, hisia sahihi, mwonekano
unaoendana na umri pia mchango na utambulisho
sahihi kijamii!

Luka 2:52 “Naye Yesu akazidi kuendelea katika


hekima na kimo, akimpendeza Mungu na
wanadamu.”

Luka 2:40 “Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu,


amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu
yake.”

Umeona kitu hapo?


1. Yule mtoto akakua +kimo =Huo ni Umri wa
kuzaliwa na kimaumbile!

2. Akaendelea katika hekima = Huo ni Umri wa


kiakili, Mfano Yesu akiwa na miaka 12 tu,
hekima yake iliwashangaza walimu wa sheria na
mafarisayo waliokuwa wazee zaidi yake kiumri!
Rejea (luka 2:46-47 )
3. Akimpendeza Mungu na wanadamu = Huu ndiyo
Umri wa kijamii! Alikidhi matarajio ya jamii
yake akiwa kijana mdogo.

Kwa kimombo naweza kuhitimisha kuwa

“Chronological age is supposed to be direct


proposional to the level of mental ability,

9
psychological and physiological well being,
social functions and roles included!

UMRI NA KUZEEKA
Umri kusonga mbele siyo ugonjwa wala fedheha, ni sifa
ya kiumbe hai chochote, lazima kizaliwe, kikue
ikiwezekana kizeeke na mwisho ni lazima kife!
Kwa hiyo uzee wenye tija, ni ule unaobeba maendeleo
yote, yaan ya wendo, mwili, akili, hisia na kijamii! Siyo
kujaza mvi tu kumbe kichwani hamna kitu! Ni uzee
unaotambua majira na nyakati siyo una miaka 70
unahangaika na vitoto vya miaka 17!

Yoshua bin Sira 25:2 “Kuna watu wa namna tatu


wanichukizao, na mwenendo wao unanikirithi:
Maskini mwenye kiburi, tajiri aliye mwongo na
MZEE MZINIFU ASIYE NA UFAHAMU.”

Mwandishi huyu alikereka sana na wazee wazinifu,


wasiokuwa na akili!

CHANGAMOTO ZA UZEE!

10
Kadiri umri wako wa kuzaliwa unavyosonga, unaweza
kukutana na changamoto za uoni hafifu, kupoteza uwezo
wa kusikia, kuishiwa nguvu, kupoteza kumbukumbu na
magonjwa ya uzeeni!

KUHUSU KUPUNGUKIWA!
Saikolojia inatambua uwezekano wa mtu kupoteza
kumbukumbu kutokana na uzee, kuchoka, kuchakaa
ngozi nk!
Na hapa mtu mmoja alipata kuandika!
Yoshua bin Sira 3:12-13
“Mwanangu, umsaidie baba yako katika UZEE
WAKE, Wala usipate kumhuzunisha siku zote za
maisha yake. Akiwa amepungukiwa na UFAHAMU
umwie kwa upole wala usimdharau iwapo wewe u
mzima sana.”

*Kupungukiwa na ufahamu pia huenda sambamba na


kupoteza kumbukumbu!
UMRI, UZEE NA UTUMISHI
Kwenye Ufalme wa Mungu huwa hakuna kustaafu
kutokana na uzee!
Tunafanya kazi mpaka dakika ya 90 hadi zile za
nyongeza, kwa sababu katika ufalme wa Mungu kwa

11
kawaida unafanya kazi ambayo ni kipaji chako cha
kuzaliwa!

Na hapa mtu fulani alipata kuomba afanikishe hilo hata


uzeeni!

Zaburi ya 71:18 “Na hata nikiwa mzee mwenye mvi,


Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi
hiki nguvu zako na kila atakayekuja uweza wako.”

UNAKUFA KAZINI.
Kwa kawaida mtu hupaswa kufa akiwa anatumikia
kusudi lake! Kwa mfano kama kipaji chako ni kuimba
basi ukiwa na afya njema hakikisha unafariki katika
mazingira ya kazi yako!

1. Mwanzo 25:7-8 “Hizi ndizo siku za miaka ya


maisha ya Ibrahimu alizoishi, miaka mia, na
sabini na mitano. Ibrahimu akafariki, naye akafa
katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku,
akakusanyiaka na watu wake.”
2. Mwanzo 49:33 “Basi Yakobo alipokwisha
kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake
kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu
wake.”
3. Mwanzo 50:24-26 “Yusufu akawaambia
nduguze, ‘Mimi ninakufa lakini Mungu atawajia

12
ninyi bila shaka, atawapandisha kutoka nchi hii
mpaka aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka na
Yakobo. Yusufu akawaapisha wana wa Israeli,
akisema ‘Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi
mtapandisha huko mifupa yangu. Basi Yusufu
akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka
dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.”
WENGINE HAWACHAKAZWI SANA NA UZEE
Katika saikolojia hii huitwa “Individual differencies”
wengine huzeeka na kuhangaika wakati baadhi hudunda
tu kama miaka imeganda vile! Hii husababishwa kwa
kiwango kikubwa na mtindo wa maisha na nasaba!
Nabii Musa ni kielelezo cha hilo!
Kumbukumbu la torati 34:7 “Musa alikuwa mtu wa
miaka mia na ishirini alipokufa; Jicho lake
halikupofuka, wala nguvu za mwili wake
hazikupunguka.”
*Umeona? Pamoj na kuzeeka, hakupungukiwa nguvu
wala kupata shida ya macho!

JE, UMEKUA NA KUONGEZEKA KATIKA


MAENEO YOTE YA UKUAJI? TAFAKARI
CHUKUA HATUA!

13
SURA YA PILI
UFAHAMU UGONJWA WA KUTOSAMEHE

1. Umewahi kuumizwa, ukaapa hutakuja kusamehe?


2. Kuna watu hutaki kuwaona, kuwasikia wala
kuwafikiria?
3. Unateseka kwa sababu tu umeshindwa kumsamehe
mtu fulani?
4. Ungependa kujua mapana ya ugonjwa huu? Soma kwa
moyo na hamasa!
Kama binadamu, daima tunakosea na kukosewa!
Tunakwazwa na kukwaza, aidha tunakera na kukerwa,
tunaudhi na kuudhiwa, tunaonea na kuonewa,
tunadhurumu na kudhurumiwa nk .
Kujikwaa kwetu huku huacha maumivu makali ya
kihisia moyoni na akilini hali inayopelekea kuathiri hata
utendaji kazi wa miili YETU.
Kwa mfano; kunyanyaswa kingono, kudhalilishwa,
kuporwa mali, kuumizwa, kutwezwa utu, kuvunjiwa
heshima, kusalitiwa na manyanyaso ya aina yoyote ile ni
chanzo cha maumivu makali ya moyo na hisia ambayo
hupelekea kwenye ugonjwa wa akili wa
KUTOSAMEHE!

14
SASA Kama ulikuwa hujui, basi leo nakujulisha kuwa
“Kutosamehe ni ugonjwa” kama yalivyo magonjwa
mengine!
Kutokusamehe ni moja kati ya magonjwa mengi
yanayotafuna nguvu kazi ya familia, jamii na taifa!
Na kwa bahati mbaya sana watu wengi hawajui kuwa
hali ya kutosamehe ni ‘UGONJWA’ wa akili
KWANI UGONJWA NI NINI?
Kisayansi, ugonjwa ni hali yoyote ile inayoingilia
utendaji kazi wa kawaida wa mwili wa kiumbe hai.
Kutoka kwenye fasili hiyo, hali ya kutosamehe inapata
sifa ya kuwa ugonjwa, kwani hali ya kutosamehe
huingilia utendaji kazi wa kawaida na wa asili wa akili,
hisia na mwili, na hivyo kuorodheshwa kama moja
wapo ya magonjwa ya akili kwenye tafiti za saikolojia
hasa zile za tawi la Psychiatriology !
Kwa hiyo kutosamehe kwa kifupi ni tatizo la akili kama
nitakavyofafanua baadae!
TAFITI ZINASEMAJE?
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa (Johns Hopkin
Medical Research) kutosamehe (unforgiveness)
imetajwa kusababisha mabadiriko katika mapigo ya
moyo, shinikizo la damu, na kuzorota kwa mfumo wa
kinga za mwili (immunity) hali hii hufanyika kama
mwitikio wa mwili kutokana na kusongwa na hasira,
fadhaa, sonona na wasiwasi!
15
Asilimia 61 ya magonjwa kama kansa na shinikizo
yamehusishwa na kutosamehe!
Kwa upande mwingine utafiti wa Worthington na
Scherer (2004) unabainisha kuwa ugonjwa wa
kutosamehe kama aina ya mwikitikio utokanano na
mfadhaiko. Athali za ugonjwa huu ni nyingi, kama vile
hasira, huzuni, fadhaa, wasiwasi, mgogoro nafsia au
baina ya watu na wakati mwingine mgogoro wa kiimani.
Zaidi sana; Kujihisi hauko salama (Chronic stress
response) jaziba ya muda mfupi (short term intense
Response) na uwenda wazimu wa kujihisi unaonewa tu
kila wakati, ambayo kisaikolojia huitwa Paranoid
Personality Disorder, ni sehemu ya athali za ugonjwa wa
kutosamehe!
TIBA YA KUTOSAMEHE.
Kutosamehe ni ugonjwa unaotibika na kupona kabisa!
Ugonjwa huu unaweza tu kutibika na kupona endapo
mgonjwa atajulishwa na kufahamishwa yafuatayo!
KUUJUA UKWELI:
Unaumia na kuteseka kwa sababu hujui ukweli kuwa
wewe ndiye unayekosa usingizi na kujaa mawazo kwa
sababu umeshindwa kumsamehe mbaya wako!
Ukiujua ukweli wa “Mechanism” ya mateso na
sononeko la kumbeba mtu moyoni, utaapa kusamehe
kwa ajili ya kulinda amani ya moyo na furaha yako!
16
Yohane 8:32 “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo
kweli itawaweka huru.”

UKWELI NI HUU!
Kwa uchache

1. Kutosamehe ni ishara ya kuwa wewe ni mtu


dhaifu, hujipendi, hujikubali na unapenda
kuteseka!
2. Wewe ndiye unayeteseka sana kuliko mtu
uliyekataa kumsamehe. Huenda hana muda na
suala hilo linalokuumiza kichwa wewe!
3. Kusamehe ni kwa faida ya afya yako ya akili na
mwili, unayemsamehe hanufaiki na lolote!
4. Kusamehe huimarisha afya yako ya moyo, akili
na kinga za mwili.
5. Kusamehe huimarisha mahusiano na wengine na
hivyo kuondoa upweke.
6. Huondoa uadui, hivyo wasiwasi, fadhaa na
kudhaniana hupungua
7. Muhimu zaidi huongeza kujistahi/kujitukuza (self
esteem) na kujiona mtu mwenye nguvu na
uliyekamilika!

17
Ukisha jua hayo yote, utachukua hatua za makusudi na
juhudi za haraka kuwasamehe unaodhani walikukosea!
Kitendo cha kusamehe ni kama kutua mzigo mzito na
mkubwa mabegani mwako!
Dawa, sindano, dripu na mionzi ya kumaliza ugonjwa
huu ni wewe kuamua ‘KUSAMEHE BILA
MASHARTI’ Unasamehe bila masharti kwa sababu
unafanya hivyo kama hatua ya kujitibu wewe
mwenyewe!
Ukitaka kusamehe kwa masharti maana yake utakuwa
bado hujipendi na unatamani kuendelea kuteseka juu ya
waliokukosea wakati wao wanalala usingizi wa pono na
hawana muda na wewe!
NITAJUAJE KAMA NIMESAMEHE?
Njia rahisi ya kujua kuwa umesamehe ni pale
unapojisikia ‘fresh’ tu hata pale unapomwona
aliyekuumiza! Uzoefu unaonesha kwamba, wengi
hujisikia vibaya, mapigo ya moyo kwenda haraka na
kupata hisia za chuki au huzuni wanapowaona wabaya
wao! Sasa ukiona hali hiyo imeisha na haikusumbui tena
basi jua umeshasamehe na umepona kabisa ugonjwa
huo!
Kusamehe na kupona kwa hiyo ni pale unapopata ahueni
moyoni!

18
Kumbuka: kusamehe wakati mwingine siyo tukio la
mara moja! Ni mchakato kulingana na chanzo cha
maumivu yenyewe.

USHUHUDA WA MTEJA.
Mteja wangu mmoja aliniambia kuwa aliona dunia kama
kiwanja cha mateso na jehanamu kwake, kwani mtu
aliyekuwa amegoma kumsamehe na alikuwa
anamchukia sana ndiye alikuwa mgeni wake wa mara
kwa mara! Alishindwa kumfukuza wala kumwambia
kwamba hamtaki! Alilazimika kutabasamu japo moyo
ulikuwa unavuja damu, alimchinjia kuku mara kwa mara
huku moyoni akiomboleza! Alimfanyia mema yote
kinafiki tu!
Jamaa alikula na kunywa na kuondoka! Halafu baada ya
muda mfupi tu alirudi tena! Eeh, alikuja mara kwa mara
kwa sababu alikuwa hajui kuwa kabebwa moyoni?
What a pain? Usiyempenda ndiye mgeni wako wa mara
kwa mara! Maisha ya jehanamu ya duniani!
UFALME WA MUNGU UNASEMAJE?
Kimaumbile ya asili binadamu ameumbwa na uwezo
mkubwa wa kusamehe na kuachilia! Hili suala la kukaa
miaka 15 na zaidi bila kusamehe ni athali ya mazingira
tu, tumefundishwa tu lakini kwa hakika binadamu
hajaumbwa kuwa kiumbe wa aina hiyo!

19
Mtoto mdogo, ambaye hajavurugwa wala kuathiliwa na
mazingira ya migogoro huwa ana uwezo wa asili kabisa
wa kusamehe! Hata hivyo uwezo huo hupotea kadiri
miaka inavyosonga na kujifunza jinsi ya kutunza hasira
na uchungu kwa muda mrefu.
Mtoto mdogo huwa haoni kazi kusamehe hata
ungemfanyaje, kwa sababu kiasili suala la kusamehe
limefungwa kwenye muda!
Waefeso 4:26-27 "Mwe na hasira, ila msitende
dhambi; Jua lisichwe na uchungu wenu bado
haujawatoka." Wala msimpe nafasi ibilisi."
Kwa kawaida unaweza kukasirika kuanzia asubuhi
mpaka jioni, lakini zaidi ya hapo linaanza kuwa tatizo la
akili!
Kwa uwezo wao wa kusameheana na kuacha upendo
utawale Bwana Yesu aliwasifia watoto na kuwatolea
mfano!
Marko 10:13-16 “Basi wakamletea watoto wadogo ili
awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila
alipoona alichukizwa sana, akawaambia, ‘Waacheni
watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana
watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amini
nawaambieni: Yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu
kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.
Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao,
akawabariki.”

20
Kwa hiyo watoto wadogo ndiyo mfano halisi wa
binadamu ambaye hajaumizwa! Jinsi tulivyo leo kwa
asilimia kubwa siyo asili yetu ni matokeo ya
kunyanyasika sana mpaka manyanyaso hayo yakaibadiri
asili yetu njema! Hata hivyo lipo tumaini kubwa, tumaini
hilo ni kwamba upo uwezekano wa kurudisha fikira na
mtazamo wako kwenye asili yake na kuwa binadamu wa
kusamehe na kuachilia bila masharti!
USHAURI WA BWANA YESU
Yesu Kristo alilsisitiza sana umuhimu wa kusamehe na
kuachilia! Suala la kusamehe alilipa uzito na msisitizo
wa kipekee SANA! Mintarafu, hali hii iliwafanya
wanafunzi wake wahoji sana juu ya kusamehe. Kwamba
unaweza kusamehe hata mara ngapi? Hata mara saba?
Yesu alijibu hata saba mara sabini! Rejea mathayo
18:21-22 (samehe 7×70)
*Tunaomba msamaha kwa Mungu kwa sababu hata sisi
tunasamehe watu wengine walio tukosea. Rejea Luka
11:4, 6:37

SOMA MAFUNGU YAFUATAYO KWA


TAFAKARI.
Waefeso 4:31-32 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira
na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila
namna ya ubaya. Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi,

21
wenye huruma, MKASAMEHEANE kama na Mungu
katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”
Unakumbuka athali ya kutokusameha? Kwa hiyo
uchungu, ghadhabu, hasira, kelele na kila aina ya ubaya
unaokutesa, unaweza kuondoka kwa kusamehe!
Wakolosai 3:12-15 “Basi kwa kuwa mmekuwa
wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni
moyo wa REHEMA, utu wema, unyenyekevu, upole,
uvumilivu. Mkichukuliana, na KUSAMEHEANA,
mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake;
kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo hivyo na
ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndiyo
mlioitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa
shukrani.”
**Kwa hiyo, waliozaliwa mara ya pili kwa kumwamini
Yesu ni wateule na watakatifu wa Mungu! Hawapaswi
kuteseka kwa kubeba watu mioyoni mwao! Wanapaswa
kusamehe kwa maana kusamehe ni ishara ya ukomavu
na upendo ambayo ndiyo amri katika agano jipya!
Kutosamehe ni kukosa kujipenda mwenyewe na
kuwapenda wengine!

22
WENGINE WAMEKUKOSEA KWA UJINGA
WAO!
Ni muhimu kutambua kuwa wapo watu waliokukosea
kwa sababu tu ya ujinga wao, sio ujinga wako! na hivyo
wakakuachia maumuivu makali moyoni mwako! Kwa
hiyo kundi hilo la wajinga hupaswa kusamehewa kwa
kuwa ni wajinga tu! Hawajui athali ya maneno
wanayotunenea, au matendo yao kwetu!
Yesu alijua waliokuwa wanamtesa na kumsulibisha
msalabani walikuwa wajinga tu! Kwa hiyo ilikuwa
muhimu kuwasamehe!
Luka 23:34 “Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui
walitendalo”
Kwa hiyo kuna watu unapaswa uwasamehe yaishe kwa
sababu walikukosea kwa kutokujua kwao madhala ya
waliyokufanyia! Na kwa kuwa ni wajinga basi
hawajaona hata umuhimu wa kukuomba msamaha,
hivyo wasamehe ili wewe uwe huru!
**Watu wa aina hii unapaswa siyo tu kwamba
uwasamehe lakini uwasamehe na kuwaelimisha na
kuwafariji ikiwezekana!
Rejea 2 Wakorintho 2:5-11

23
JE, ASIPOKUBALI MSAMAHA?
Ndiyo, kuna watu huwa wanakataa suluhu! Hawataki
yaishe! Wanapenda maisha ya ugomvi, migogoro na
kutunishiana misuli!
Bwana Yesu alishauri kushughulika nao kama
ifuatavyo!
Mathayo 18:15-17 “Na ndugu yako akikukosea,
enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu;
akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii,
chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili
kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila
neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie
kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako
kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”
Kumfanya mtu kuwa “wa mataifa” siyo kumweka
moyoni wala kumbeba, bali ni kumsamehe na kuachana
naye!
Usijipe kazi ya kumbadirisha mpumbavu, kama
haeleweki achana naye na asikusumbue! Mtu wa mataifa
ni mtu ambaye hajastarabika, mshenzi na kafiri! Akija
kwako utampokea na kumfanyia ukarimu kwa heshima
na kiwango cha watu wa mataifa!
Kwani akija kwako mtu usiyemjua, huwezi
kumkaribisha? Utakuwa na kinyongo naye? Kama jibu
ni hapana, fanya hivyo kwa ndugu yako asiyetaka
suluhu!

24
KUSAMEHE NA KUSAHAU
Hii ni dhana tu isiyo na uhakika wala ulazima! Cha
muhimu ni kusamehe tu sauala la kusahau siyo lazima
wala muhimu kwa sababu ubongo huhifadhi matukio
yote mazuri na mabaya! Kwa hiyo unaweza
kuukumbuka ubaya uliotendewa na usiumie maana
ilishabaki kama historia tu!
Hata hivyo, kama unataka kujisahaulisha uwezekano
upo. Kwani kwenye saikolojia kuna dhana ya
kukumbuka na kusahau “Concept of memory and
forgetting” kuna kitu kinaitwa ‘Motivated forgetting’
kwa hiyo ni wewe tu, unaweza kutengeneza mazingira
ya kusahau msala au tukio lililopelekea wewe kuchukia
na kushindwa kusamehe!

Naweza kusema nini zaidi?


Wewe Ni Wa Thamani
Samehe Kwa Faida Yako
Samehe Kwa Afya Yako
Samehe Kwa Usalama Wako
Samehe Kwa Raha Zako

25
SURA YA TATU
SAIKOLOJIA YA HASIRA NA UFALME WA
MUNGU
"A Rhapsody For Kingdom Anger Management and
Strategies"
MASWALI YA KUJIULIZA.
1. Umewahi kuwa na hasira?
2. Huwa unapata hasira Mara kwa Mara?
3. Ukiwa na hasira huwa unafanyaje?
4. Je, Kuna ndugu, jamaa au marafiki umewafuta kabisa
na hutaki hata kusikia habari zao kutokana na hasira?
5. kuna wakati hasira inajaa mpaka unahisi Koo
linauma/Kuwaka Moto?
6. Umewahi kujuta kwa kufanya maamuzi mabaya
kutokana na hasira?
7. Hasira imewahi kukugarimu kama vile kutozwa faini,
kufungwa au kutengwa na jamii?
8. Je, Kuna faida au Hasara kwenye hasira?

SOMA KWA HAMASA !

26
HASIRA ni sehemu ya hisia kali za ndani zimpatazo mtu
hasa anapokutana na upinzani fulani.
Hakuna binadamu asiyekasirika, kwa Sababu hasira ni
hisia za kawaida za kuzaliwa nazo (Inborn).
Hata hivyo uwezo na kiwango cha kutawala hisia za
hasira hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.
Mwanafalsafa wa zamani Aristotle aliwahi kusema
"Kukasirika kila mtu anaweza, lakini Kukasirika
kwa sababu sahihi, kwa mtu sahihi, kwa Kiwango
sahihi na kwa wakati sahihi Ni vigumu kwa kila
mtu."
Lengo la sura hii ni kukufanya uwe na Uwezo wa
kuhimili hasira zako! Na ukikasirika basi iwe ni kwa
sababu sahihi, wakati sahihi, kwa Kiwango sahihi na
kwa mtu sahihi! Ili usijikute kwenye matatizo.
Ukiwa na Uwezo mkubwa wa kudhibiti hasira zako
utaonekana mtu mwema na muungwana kwa mwenzi
wako, familia yako na jamii kwa ujumla!
• Kama mshauri wa masuala ya kisaikolojia,
nimekutana na wateja kadhaa wanaosumbuka na
hasira, Wengi walikiri kuwa, kutokana na kuwa
na hasira za ghafla na za mara kwa mara hujikuta
wameleta fujo na madhara makubwa. Zaidi Sana
wengine imewapelekea kuepukwa na ndugu,
jamaa na marafiki kadhaa! Mmoja aliniambia

27
"Kwenye vikao vyetu vya ukoo wananijua, Mara kwa
Mara huwa wanaepuka kubishana na Mimi."
Hata hivyo hali hiyo ilionekana kumuumiza Sana!
Fikiria, wafanya kazi wenzako (Staff member)
wanakuogopa kwa hasira zako za kiwenda wazimu,
unajisikiaje!
Ukifahamu kwamba watu wanakwepa hata kukudadisi
Mambo ya kawaida kwa sababu ya hasira zako Kama za
mkizi, unajisikiaje?
AINA ZA HASIRA KISAIKOLOJIA
Kisaikolojia zipo aina kadhaa za hasira, aina hizi
zimechambuliwa kutokana na kisababishi cha hasira
yenyewe Kama Ifuatavyo.
1. Hasira ya haki. Hii kwa kimombo tunaita
Righteous Anger. Hii ni hasira chanya, Ni hasira
inayositahili na kuhitajika! Ni hasira ambayo
huinuka ukiona kitu/Jambo Fulani haliendi Sawa
Sawa, mfano ukaona mtu anaonewa na
kunyanyaswa, hasira hii hupelekea kukupa nguvu
hata za kujitoa mhanga ili umsaidie! Kwa hiyo
hii ni hasira Nzuri!
MFANO WA HASIRA YA HAKI
(Yesu aliwahi kucharaza viboko na kupindua meza za
watu waliokuwa wamegeuza nyumba za ibada kuwa
sehemu ya harambee na biashara maarufu Kama pango
la wanyang'anyi)
28
Soma Luka 19:45-46 au Marko 13:15-17
Kuna siku niliingilia Kati kuzuia mwizi asiuawe kwa
kupigwa mawe! Akili zangu zilikuja kujua kuwa
nilikuwa kwenye hatari ya Kufa Mimi Mwenyewe,
nikiwa tayari nimemwokoa mtu huyo aliyesadikika kuwa
kibaka !
2. Hasira kutokana na kuzidiwa au kuelemewa
na Mambo mengi, inaitwa ‘overwhelmed
anger!’
Mfano kutopata usingizi vizuri, kuwa na ratiba
iliyosonga sana, kukosa muda wa mazoezi na
kuburudika au kuwa na njaa!
3. Hasira za kutaka kuendesha/kutawala hii kwa
kimombo inaitwa Manipulative anger,
Ni hasira inayolenga kuwatisha watu ili wakuogope
uwaendeshe unavyotaka! Neno maarufu la mtaani
naweza kusema "Kupiga mkwara"
Baadhi ya viongozi madikteta, hutumia hasira hii ili
afanye anavyotaka bila kufuata katiba, utaratibu wala
sheria.
4. Hasira itokanayo na mapito!
Hii ni hasira kutokana na matukio aliyopitia mhusika
kama vile kusalitiwa na mpenzi, kufiwa, kunyanyaswa
kingono nk. (Post traumatic stress Disorder)

29
5. Hasira kwa kiasi fulani huweza kisababishwa na
hali ya kimaumbile/kifiziolojia kwa mfano
kiwango cha sukari kuwa chini sana mwilini,
kukosa mlinganyo sawia wa homoni na kemikali
kwenye ubongo kutokuwa sawa! (Hormonal na
brain chemical imbalances.
6. Sababu nyinginezo ni hofu ya maisha na
usalama, Mfano uchumi mbaya, ukosefu wa
ajira, changomoto za kimaisha kwa ujumla !

HABARI NJEMA
Pamoja na sababu zote nilizotaja hapo na zile uzijuazo
Mwenyewe, wanasaikolojia wote tunakubalina kuwa
hasira inaweza kudhibitiwa/kuzuiwa au kupunguzwa
UNAFANYAJE?
• Isome hasira yako vizuri bila
kujipendelea/kujihurumia
• Ukisha ielewa vyema, Epuka
vitu/Hali/vichochezi vya hasira yako.
• Ufundishe ubongo wako kubaini mapema
Mazungumzo, hali au mazingira yanayoweza
kukupelekea kwenye hasira.
HASIRA KWENYE UFALME WA MUNGU IKO
HIVI
Tuliozaliwa mara ya pili na kufanyika kuwa watoto wa
Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo (Yohane 1:12)

30
Tunayo nafasi nzuri zaidi ya kuishinda hasira na kuwa
wenye furaha.
Kwa sababu gani?
Unapozaliwa kwa mara ya pili, unakuwa kiumbe kipya
na unabeba vinasaba na hali ya baba wa mbinguni.
Maana imeandikwa "Kama Yeye alivyo, ndivyo na sisi
tulivyoona humu Ulimwenguni" (1 Yohane 4:17b)
MUNGU YUKOJE?
Zaburi 103:8 " Bwana amejaa huruma na neema, Haoni
HASIRA upesi, Ni mwingi wa fadhili."
Sifa ya Mungu wetu ni hiyo
KWA NINI HASIRA HAIFAI?
Pamoja na faida moja ya hasira kama tulivyoona kule
juu, bado hasara inaonekana kuwa ni kubwa Sana.
• HASIRA HAITENDI HAKI. Mtu mwenye
hasira kamwe hawezi kutenda haki, kwa sababu
vitendo vingi huvifanya akiongozwa na hasira
kuliko akili.
Yakobo 1:19-20 "Hayo mnajua ndugu zangu
wapenzi: Basi kila mtu awe mwepesi wa kusikia, Bali
Si mwepesi wa kusema, Wala KUKASIRIKA kwa
Maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya
Mungu."

31
Kwa hiyo kwenye hasira hakuna Haki. Viongozi wengi
Wenye hasira hushindwa kutenda haki kwa
wanaowaongoza! Kamata kamata na vitisho ni dalili za
kiongozi mwenye hasira.
• HASIRA HULETA UGOMVI na uasi! Bila
hasira ugomvi na uasi utatoka wapi?
Mithali 29:22 "Mtu wa hasira huchochea ugomvi, na
Mtu mwenye ghadhabu huasi Sana."
• HASIRA HUTENDA MABAYA. Kuna watu
wanaozea kwenye magereza mbalimbali
kutokana na kufanya unyama kwa msukumo wa
hasira tu, wanajutia hasira yao.

Zaburi 37:8 "Ukomeshe hasira, uache


ghadhabu, usikasirike mwisho wake Ni
kutenda mabaya."
Kumbuka Kaini alimuua ndugu yake Abeli kutokana na
kujaa wivu na hasira! (Mwanzo 4:3-8)
Hata nabii Yona alifikia hatua ya kumwomba Mungu
amuue, kwa Maana moyo wake ulijaa wivu na hasira!
Soma Yona 3:10 na Yona 4:1-4
Ukisoma hapo utaona Mungu anamuuliza Yona, Je
watenda vyema KUKASIRIKA?
• Hasira nyingi Ni Upumbavu. Umejilaumu na
kujuta mara ngapi kutokana kufanya maamuzi au
tendo fulani kwa hasira?

32
Mhubiri 7:9 "Usifanye haraka KUKASIRIKA
Rohoni mwako, Maana hasira kukaa kifuani mwa
wapumbavu."
• Hasira huondoa ulinzi.
Mdomo hukiponza kichwa, ndivyo hasira pia iwezavyo
kukuponza, mtu Asiye na hasira ni vigumu kujikwaa
katika kusema au kutenda.
Mithali 25:28 "Asiye tawala Roho yake ni mfano wa
mji uliobomolewa, usio na kuta.
JINSI YA KUFANYA
Jipatie hekima na ufahamu. Ndiyo maana nipo hapa
kukufundisha, ukipata UFAHAMU wa kutosha juu ya
jambo fulani ni rahisi kukabiliana nalo kwa ufasaha!
Mithali 29:11 "Mpumbavu hudhihirisha Hasira Yake
yote, Bali mwenye Hekima huizuia na kuituliza."
Umeona? Mwenye hekima huizuia na kuituliza hasira!
Kwa hiyo uwezo wa kuituliza na kuizuia hasira yako
unategemea Kiwango cha hekima na uelewa wako!
Pia Mithali 14:29 "Asiye mwepesi wa hasira
anafahamu nyingi. Bali mwenye Roho ya hamaki
hutukuza upumbavu."
Zaidi ya hayo Mithali 16:32 "Asiye mwepesi wa hasira
Ni mwema kuliko shujaa, na Mtu aitawalaye roho
Yake kuliko mtu atekaye mji."

33
SAMEHE KWA FAIDA YAKO!
Kusamehe ni njia moja nzuri na rahisi Sana kumaliza
hasira! Kama Kuna mtu alikukosea na kukusababishia
hasira hizo, basi dawa nzuri ni kumsamehe!
Ukimsamehe moyo wako utafunguka na hautasikia
hasira juu yake!
Mithali 19:11 "Busara ya Mtu huiahirisha hasira
Yake. Nayo ni fahari Yake KUSAMEHE makosa."
EPUKA UKARIBU NA MTU MWENYE HASIRA
KALI.
Hasira wakati Mwingine inaambukizwa! “contagious”!
Inaambukizwa, kuenea na kusambaa! Ukiwa na urafiki
na Mtu mwenye hasira ni rahisi kuiga tabia zake! Ndiyo
maana Kuna makabila hapa Tanzania yanajulikana
kabisa kwa hasira na mapanga! Kwa nini? Wanaigana
tu! Hii huitwa "imitation"
Mithali 22:24-25 "Usifanye Urafiki na mtu mwenye
hasira nyingi, Wala usiende na Mtu wa ghadhabu
nyingi. Usije ukajifunza njia zake na kujipatia nafsi
yako mtego."
Hali hii inanikumbusha kipindi fulani nikiwa
mwanafunzi, kijana mmoja rafiki yangu (mwenye asili
ya hasira hasira) alinishawishi tukampige mkwara
mwalimu mmoja tuliyekuwa tunaamini ni mnoko sana
pale shuleni!

34
Nilikubali na tukaenda, tulichokifanya kidogo Mimi
nifukuzwe shule!
JE, TUSIKASIRIKE KABISA?
Waefeso 4:26-27 "Mwe na hasira, ila msitende
dhambi; Jua lisichwe na uchungu wenu bado
haujawatoka." Wala msimpe nafasi ibilisi."
• Kukasirika kwa muda mrefu ni kumpa shetani
nafasi ya kufanya uhalifu kwa kutumia Mikono
au Mdomo wako."
Kumbuka hasira imetajwa Kama matendo ya mwili
yasiyo na kibali kwa Mungu! Mwenye hasira hawezi
kuingia mbinguni!
Wagalatia 5:19-20 "Basi matendo ya mwili Ni
dhahiri, ndiyo Haya. Uasherati, ufisadi, uchawi,
uadui, ugomvi, wivu, HASIRA, Fitina faraka uzushi
husuda etc.
NI IPI SULUHU YA KUDUMU?
Hakikisha Roho Mtakatifu anakaa ndani yako na
kukuongoza, Yeye Ni kinyume na hasira!
Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la Roho Ni
UPENDO, furaha, Amani, uvumilivu, utu wema,
fadhili, uaminifu, upole, kiasi juu ya Mambo hayo
hakuna sheria."
*Tafakari, chukua hatua !

35
SURA YA NNE
HOFU NI UGONJWA
HOFU ni hali ya kuwa na hisia hasi, hisia hizi
huambatana na woga, wasiwasi, mashaka, mfadhaiko,
msononeko,na kukata tamaa au kutoamini!
Katika maisha ya kila siku faida za HOFU ni chache
sana au hazipo ukilinganisha na kinyume chake yaani
"UJASIRI"

Sasa basi, Kwa kuwa HOFU ni mbaya basi haina nafasi


na usiipe nafasi katika maisha yako.
MUNGU alipomwumba mwanadamu alikusudia awe
jasiri wala siyo mwoga! Na ndiyo maana akampa
jukumu la kutawala sehemu nyingine yote ya uumbaji
wake! Angejua ameumba kitu dhaifu na kioga
asingethubutu kumkabidhi jukumu zito na kubwa kama
hilo, yaan KUTAWALA sawasawa na Mwanzo 1:27-28.

Hakuna shujaa anayekumbukwa duniani kwamba


"ALIJAA HOFU" hofu kwa maana hiyo haijawahi
kusababisha ama kutengeneza watu walioleta mabadiliko
makubwa na matokeo chanya kwenye dunia.

Historia imejaa watu majasiri ambao walikataa


kuendekeza DHAMBI hii na kwa maana hiyo hawakuwa
na chembe ya hofu wala woga mioyoni mwao!

Wanasayansi mashuhuri, wanasiasa wa kuigwa,


wapigania Uhuru, wana mapinduzi, wachezaji, waalimu,
wanafutuhi (comedian), watu waliogundua mambo
makubwa, wana falsafa, saikolojia, sosholojia, na kada

36
zote uzijuazo zimesheheni watu waliokataa kuwa waoga!
Zinazungumzia watu majasiri!

MUNGU ANASEMAJE?

Isaya 35:4 " Waambieni walio na moyo wa hofu,


jipeni moyo, msiogope!..….."

Ndugu, kama una tatizo la hofu katika maisha yako ujue


si mpango wa MUNGU uwe hivyo! Ukiwa na hofu
huwezi kufanya mambo mengi ya msingi! HOFU
inakufanya uburuzwe, upelekeshwe, uendeshwe kama
gari bovu na kutumikishwa!

Mfalme Daudi alipomwomba Mungu, Mungu


alimwondolea hofu kwanza! Ukiwa na hofu kuna
Mambo mengi yatakwama kwenye kila jambo
unalofanya!

Zaburi 34:4 " Nalimtafuta Bwana akanijibu,


Akaniponya na hofu zangu zote."

Daudi alijitoa kwa moyo kumtafuta MUNGU, lakini


Mungu anapomjibu anaanza kwanza kutatua tatizo la
Hofu!

HOFU INA ADHABU!

Penda usipende, Hofu yoyote ile huambatana na adhabu


fulani sawasawa na

37
1Yohane 4:18 "Katika pendo hamna hofu, lakini
pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana
HOFU INA ADHABU"

MTU mwenye hofu ni mtumwa, mnafiki, mwongo, hana


msimamo na msaliti! MTU mwenye hofu hafai kabisa
katika UFALME wa MUNGU pia hafai hata kulitumikia
taifa kama la Tanzania!

TABIA ZA HOFU.

1. Kunyamaza hata kama unapaswa kupaza


sauti.

Kutoka 15:16 "Hofu na woga umewaangukia; kwa


uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama
"Jiwe".......hata watakapovuka watu wako uliowanunua"

MTU mwoga hawezi kukemea wala kusema chochote!


Katika jamii yetu kuna mambo mengi ya kifedhuli
yanatendeka, lakini kwa kuwa watu wengi wamejaa hofu
basi hawawezi kusema chochote! Hofu inaleta hali ya
uzubaifu fulani wa kijinga.

2. Hofu inatabia ya kusambaa na kuambukiza!


Kama yalivyo magonjwa ya mlipuko (pandemic
diseases) kama kipindupindu "Huenea kwa kasi"
hata hofu huambukizwa na kuenea kwa kasi!
(contagious) Ndiyo maana utasikia sehemu fulani
kuwa "HOFU imetanda/imeenea

38
Kumbukumbu la torati 20:8 “Tena maakida na
waseme zaidi na watu, wawaambie, ni mtu gani aliye
hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende
akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze
ikayeyuka mfano wa moyo wake.”

3. Hofu inakunyima usingizi. Watu wasiokuwa na


chembe ya hofu hulala usingizi mtamu!

Mithali 3:24 "Ulalapo hutaona hofu, naam


utalala na usingizi wako utakuwa mtamu"

Kama unakesha unawaza kutokana na hofu na kupelekea


kukosà usingizi, ni muda mzuri Sasa kwako kuitupilia
mbali hofu! Inamaanisha unatumikia ile adhabu ya hofu.

4. Hofu inakufanya useme/kuongea hovyohovyo


tu. mtu wenye hofu hata ukimsikiliza anaongea
ama kuhutubia huwezi kumwelewa sawia!
Maneno yao yamejaa hofu, kujipendekeza,
kusifiasifia watawala, kwa ujumla hofu huondoa
ufasaha kwenye akili mpaka kwenye ulimi.

Marko 9:6 Jamaa aliingiwa hofu ndiyo.maana


hata maombi yake hayakuwa na mantiki na
hayakujibiwa!

39
MUNGU AKITAKA KUKUTUMIA
ANAOKUONDOLEA HOFU KWANZA

1. Mungu anamwita Gideoni

"Waamuzu 6:11-16" Bwana yu pamoja nawe, ee


shujaa!”

Kumbuka huyu alikuwa kijana mdogo na


mwoga na mpaka anasikia hilo neno alikuwa
amejificha kwenye shinikizo akipepeta ngano
kwa hofu ya vita!

2. Mungu anapomwita Jeremiah


katika Yeremia 1:4-10 "Lakini bwana
akaniambia, usisema Mimi ni mtoto"

3. Mungu anapomwita Joshua anamwambia wazi


"Uwe na moyo wa ushujaa, usiogope wala
usifadhaike" soma mwenyewe Yoshua 1:9
4. Yusufu alipotaka kukataa kumwoa Maria,
Mungu alijua shida haikuwa mimba bali hofu!
Ndiyo maana akamwambia "Usiogope" Mathayo
1:20 inathibitisha hili.
5. Mungu alipotaka kumkabidhi Maria jukumu la
kumzaa mwokozi cha kwanza ilikuwa ni kumtoa
hofu tu !

Luka 1:30 " usiogope Mariamu"


Mifano Ni mingi mno, niishie hapa kwa hilo!

40
KWA NINI HOFU NI DHAMBI?

Ufunuo 21:8 “Bali WAOGA, na wasioamini, na


wachukizao, na wauaji na wazinzi na wachawi na
waabudu sanamu na waongo wote sehemu yao ni
katika lile ziwa la moto’’

UMEONA KITU?

UOGA unatajwa kama DHAMBI. Ndiyo ! ni dhambi


kabisa.

UNA HOFU YA KUUWAWA?

Ndugu ishi Leo, usiwaze wala kufikiri sana juu ya kifo


na zaidi usiogope kufanya mambo yako ya msingi eti
kisa unaogopa kufa! Kwa maana kufa kupo tu.

Yesu Kristo alitufundisha tusiogope wauaji hata kifo


chenyewe!

Mathayo 10:28 na Luna 12:4 "Msiwaogope hao wauao


mwili halafu baada ya hapo hawawez kufanya lolote"

Na ndiyo maana alifanikiwa kuwajengea ujasiri


wanafunzi wake baada ya yeye kuondodoka. Kwa mfano
walipata hata ujasiri wa kuwajibu viongozi wa kidini wa
kipindi kile.

"Imetupasa kumtii MUNGU na siyo mwanadamu"


Matendo ya mitume 5:29

41
UJASIRI SIYO UKATIRI WALA KIBURI

Mithali 16:32 "Asiye mwepesi wa hasira ni mwema


kuliko shujaa, na MTU aitawalae ROHO yake kuliko
MTU atekaye mji"

Ndivyo ninaweza kuhitimisha, ujasiri SIYO ukatiri wala


kiburi! Ni unyenyekevu na utii kwa hisia na dhamiri
njema iliyo moyoni mwako! Jasiri daima hapendi
kuogopwa wala kutukuzwa, Jasiri ni MTU mwema,
mpole na mnyenyekevu asiyeburuzwa wala
kuyumbishwa. Nelson Mandela anachukuliwa kama
shujaa na jasiri japo alikuwa MTU wa kusamehe na
kutabasamu! Kwa hiyo ushujaa hauji kwa kukunja sura
au kufokafoka!

Kama wewe ni kiongozi wa umma au wa kidini


unapaswa ujue kuwa ni kosa na dhambi kubwa mno
kuwajengea watu hofu. Hofu ni gereza la siri!

KAZI YA ROHO MTAKATIFU NI


KUTUONDOLEA HOFU

Warumi 8:15 "Kwa kuwa hamkupokea tena ROHO


ya utumwa uliletayo hofu; Bali mlipokea.ROHO ya
kufanywa wana......"

Hata maombi ya MTU aliyejaa hofu huwa ni kivutio


kwa wasikilizaji! Kemea kemea kemea hata kama hana
uhakika anakemea nini! Maombi ya MTU jasiri yamejaa
ujasiri, imani na uhakika! Kuna watu wanakesha
wanafukuza wachawi Kila siku, HOFU Haiwapi hata

42
muda wa kufanya tathmini juu ya vita hivyo
wanavyopigana bila kujua vimeisha au mapambano
yanaendelea!

BADILIKA!
Unaogopa kiongozi wa mtaa
Unaogopa mkuu wa idara
Unaogopa kasisi
Unaogopa mama/baba mkwe
Unaogopa mawifi/shemeji zako
Unaogopa Wachawi
Unaogopa shangazi/baba mdogo
Unaogopa waganga wa kienyeji
Unaogopa mijusi, bundi,njiwa
Unaogopa serikali
Unaogopa kufa
Unaogopa kuoa/kuolewa
Unaogopa kuanzisha biashara
Unaogopa kuweka hadharan msimamo wako
Unaogopa nini?
Kama unahangaika na hofu na inakukera, basi chukua
hatua ya imani leo! Kuwa chochote MUNGU
Alichokusudia uwe.

43
SURA YA TANO

UKWELI KUHUSU POMBE

Nikupe hongera Sana kwa moyo wako wa kujifunza,


Basi karibu tujifunze ukweli kuhusu Pombe!
Nimekuwa nikiulizwa maswali kadhaa juu ya Suala la
matumizi ya POMBE , kwa maana ya ruksa au haramu
katika Ufalme wa Mungu na afya ya binadamu!
Hapa nazungumzia pombe yenye kilevi yaan
CnH2n+1OH
Kila mtu ana maoni na msimo wake kuhusu pombe, kwa
sababu hiyo na mimi naomba nikushirikishe tafakari
yangu juu ya jambo hili, kwani ni wazi yamekuwepo
mabishano kwa muda mrefu, kundi moja linaitetea,
kuihifadhi na kuilinda pombe kama katiba waliyoapa
kuilinda. huku kundi jingine linaizodoa, kuisakama,
kuisimanga na kuhitimisha kuwa ni dhambi na najisi.
UKWELI NI UPI? SOMA KWA UTULIVU.
Bila kupoteza muda
Marko 7:15 "Hakuna kitu kilicho nje ya mtu
ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, Bali
vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu."

44
Ndiyo kabisa! Kwa habari ya unajisi huwezi kunajisika!
Na ndiyo maana hata mimi siwezi kukuhukumu kwa
suala la chakula na vinywaji! Kwa Maana aliyezaliwa
mara ya pili hawi chini ya maagizo na makatazo ya hapa
na pale yasiyokuwa kwa jinsi ya Kristo.
Hapa Mtume Paulo anasema
Wakolosai 2:16 "Basi Mtu asiwahukumu ninyi katika
vyakula au VINYWAJI au kwa sababu ya sikukuu
au mwandamo wa mwezi au sabato."
Tena kwa asili kabisa hakuna kitu najisi hata kimoja
(Warumi 14:14)
Kumbuka baada ya uumbaji kukamilika, Mungu aliviona
vyote alivyiviumba kuwa ni vyema na vya kupendeza,
hakuona unajisi! (Mwanzo 1:25)
KAMA NI HIVYO, JE POMBE NI SAWA?
Ufunuo wa wazi wa kibiblia unamtaka mtu aliyezaliwa
Mara ya pili, aishi kwa kutumia AKILI zake vizuri na
ipasavyo!
1Wakorintho 15:34 "Tumieni akili Kama ipasavyo,
Wala msitende dhambi Maana wengine hawamjui
Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe."
Ikiwa biblia inatambua na kuthamini matumizi ya Akili,
naamini utaelewa sawia ninachoenda kukizungumzia
mapema iwezekanavyo!

45
HALALI LAKINI HAIFAI
Hapa panahitaji utulivu kidogo! Kuna Mambo mengi
sana hayafai kabisa kiafya japo ni halali. Kwa mfano
uvutaji wa sigara kwa sheria za Tanzania ni halali kabisa
japo haufai. Mpaka wazalishaji wa sigara huweka onyo,
kwamba uvutaji wa sigara ni hatari kwa Afya! Ni hatari
japo imethibitishwa na tbs! Kwa nini hawaachi
kuzitengeneza? Wanataka Akili yako ifanye kazi!
Ukiacha kuvuta hawawezi kuzalisha zingine!
Sasa sikia neno lisemavyo!
1Wakorintho 6:12 "Vitu vyote ni halali kwangu,
Lakini si vyote vifaavyo. Vitu vyote Ni halali kwangu
Lakini Mimi sitatiwa Chini ya Uwezo wa kitu
chochote."
 Yawezekana Ni halali kabisa, sawa, lakini je
inafaa?
 Yawezekana Ni halali, lakini Swali je, imeletea
uraibu? Umekuwa tegemezi kwa bidhaa hiyo?
Unaweza kuongezea 1Wakorintho 10:23-26
Kwani sumu Kama benofos siyo halali? Ni halali. Je
inafaa? Ndiyo inafaa kwa kuua wadudu shambani . Je,
ukiinywa? Ni uamzi wako, maana siyo najisi sawa lakini
kwa hakika inaua!
 Inaweza ISIWE najisi lakini ikawa na Athali
hasi/mbaya.

46
 Kwenye uhalali na kufaa, ndipo panadai
uwekezaji wa Akili yako na utashi ili uamue
vyema!
UMUHIMU WA KUTAMBUA NAFASI YAKO
Hili ni Suala wazi Sana, Mtu anayejitambua vyema na
anafahamu aina ya majukumu yake huamua ikiwa awe
mnywa POMBE au la.

Katika Ufalme wa Mungu iko hivi.


2Timotheo2:20-21 "Basi katika nyumba havimo
Vyombo vya dhahabu na fedha tu, Bali na vya mti na
vya udongo; Vingine vina heshima, Vingine havina.
Basi Ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao,
atakuwa chombo Cha kupata heshima, kilicho
safishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa
kila kazi iliyo njema."
Wanaofahamu kuwa wametengwa kwa ajili ya kila kazi
njema kwenye Ufalme wa Mungu hawawezi kuwa
victim wa vileo na POMBE!
ANGALIA HAPA KWA MFANO
Samson hakupaswa kunywa pombe ili atimize vyema
wajibu wake.
Waamuzi 13:1-14 zingatia zaidi aya ya 4 na ya 14
"Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu,
Wala asinywe divai, Wala mvinyo, Wala asile kitu
47
chochote kilicho najisi: Na hayo yote niliyomwamuru
na ayatunze."
Yohane Mbatizaji, pia hakupaswa kunywa pombe, kwa
Maana alipaswa kutekeleza misheni maalum kabla ya
ujio wa Yesu Kristo! Soma mwenyewe hapa chini!
Luka 1:15 "Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za
Bwana: hatakunywa divai Wala kileo, naye atajazwa
Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mama.
Soma tena Hapo juu kwa msisitizo! "Kwa sababu
atakuwa mkuu mbele za Bwana hatakunywa divai
Wala kileo"
Watu wakuu/wateule katika Ufalme wa Mungu
hawanywi POMBE , Si kwa sheria, lakini Ni kwa sababu
pombe Ni ya hadhi ya Watu wa Chini Sana! Mtu mkuu
na pombe ni wapi na wapi?

NINI MBADALA WA POMBE KWAO?


Hapohapo Luka 1:15b badala ya Kujazwa pombe?
"Naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni
mwa mamae."
Kwa kujua umuhimu huo, Paulo alikazia hivi
Waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo.
Kuna ufisadi: Bali mjazwe Roho Mtakatifu."

48
Umeuona mbadala wa POMBE? Ni Kujazwa Roho
Mtakatifu !

SAIKOLOJIA NA ELIMU YA AFYA


Wataalamu wa masuala ya saikolojia na Afya huwa
wanashauri na kusisitiza hivi
 Mwanamke mwenye ujauzito Kama anataka
kujifungua mtoto mwenye afya Nzuri ya "Akili"
na mwili nilazima asinywe pombe, asivute sigara,
etc
 Pombe inabomoa ubongo wa mtoto tangu
tumboni mwa mamaye, Kwani kwenye clinic ya
baba, mama na mtoto mnashauriwa Nini?

KWENYE UFALME WA MUNGU TUNA ADABU!


POMBE tangia lini ina adabu? Tangu lini mlevi akawa
na adabu? Sasa jua kwamba kwenye Ufalme wa Mungu,
tunaenenda kwa adabu!
Soma hapa kwa utulivu!
Warumi 13:12-13 "Usiku umeenda Sana, mchana
umekaribia, Basi na tuyavue matendo ya Giza na
kuzivaa silaha za nuru. Kama ilivyohusika na
mchana na tuenende kwa ADABU; Siyo kwa ulafi na
ULEVI....."
=siyo kwa ulafi na ulevi!

49
Wagumu kuelewa Paulo aliwashauri hivi
Tito 2:3 "Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na
mwenendo wa Utakatifu; Wasiwe wasingiziaji,
wasiwe Wenye kutumia mvinyo nyingi, Bali
wafundishao mema."
Zaidi Mtume Paulo aliutaja ulevi katika kundi moja na
ugomvi, uchawi, uasherati, ufisadi, uchawi, uadui,
ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda,
ulevi, ulafi nk!
Soma hapa Wagalatia 5:19-20

 Kisaikolojia na kibaiolojia, Pombe hupenya


haraka Sana kwenye ubongo na kuharibu vibaya
Sana maeneo anuai ya ubongo kama Medulla
oblangata, hypothalamus, hippocampus,
Cerebellum, frontal lobe na cerebral cortex!
Mifumo hii ikiharibika unakuwa "Mwehu" kama
wehu wengine, kwa muda!
Pombe ina hali ya akili “change mental state” na hali ya
akili ikibadilika lolote linaweza kutokea.
Hujawahi kuona mtu mzima na heshima zake anakojoa
Hazarani ?
 Unalikubuka tukio la mlevi kupiga watu kwa
risasi na yeye kujiua huko Sinza Dar es salaam
kisa pombe?

50
Na ndiyo maana Kuna Mambo mengi hujitokeza baada
ya kulewa kama vile
Mithali 23:29-35 "Ni Nani apigaye yowe? Ni Nani
aliyae ole? Ni Nani mwenye ugomvi? Ni Nani
mwenye mguno? Ni Nani aliye na JERAHA zisizo na
sababu? Ni Nani aliye na macho mekundu? Ni wale
wakaao kwenye mvinyo, waendao kutafuta divai
iliyochangamka......." Tafuta usome pote!
ZAIDI ya hayo?
Mithali 20:1 "Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi
na akosae kwa vitu hivyo hana hekima."
 Ukijidhalilisha, kuaibisha kwa sababu tu ya
pombe jua wazi huna hekima !

POMBE INA "OLE"


Isaya 5:11 "Ole wao waamkao asubuhi na mapema,
wapate kufuata kileo. Wakishinda Sana hata usiku
wa manane mpaka mvinyo imewaka Kama Moto
ndani yao."
 Pombe inaaibisha na kudhalilisha
Mwanzo 19:30-38 (Hapa Lutu analewa Pombe na
kufanya ngono na binti zake)

51
POMBE INALETA UMASIKINI NA
KUTELEKEZA MAJUKUMU.
Kama mshauri, Nimeshauri wanafunzi wengi Sana wa
sekondari, msingi na vyuo vya Kati, ambao masomo yao
yameathirika Sana kutoka na ulevi wa wazazi wao!
Ndoa nyingi na familia zinaomboleza kwa ajili ya
Pombe!
Halafu mtu mmoja "anasisitiza" pombe ilibarikiwa
kabisa kwenye harusi ya kana ,,,,,aibu!
ELEWA KUWA
1 Timotheo 5:8 "LAKINI mtu yeyote asiyewatunza
walio wake, yaan wale wa nyumbani mwake, hasa
ameikana imani. Tena ni mbaya kuliko asiye amini."
Pombe imewafanya watu wangapi waikane imani kwa
kutokujali wenzi na familia zao? Mimi ni zao la jamii hii
ya Tanzania, utanidanganya nini juu ya Pombe?
 Wanandoa wangapi wamezini kisa Pombe?
 Familia ngapi zimevurugika kisa Pombe?
 Kuna Vijana wangapi wamepata magonjwa ya
zinaa na UKIMWI Kama matokeo ya ngono
zembe kwenye clab za Pombe?
 Makasisi wangapi wamedhalilika na kudhalilisha
kanisa kisa Pombe?

52
SIKIA WEWE KIZIWI NENO LA BWANA
Mithali 21:17 "Mtu apendaye anasa atakuwa
masikini, apendaye MVINYO na mafuta hatakuwa
tajiri."
Hapa Tanzania, familia nyingi ziko kwenye mstari wa
umasikini wa kutupwa, hasa vijijini kutokana na Pombe
tu! Kama hujui, jua hivyo kuanzia Sana!
Katika kiwango cha umasikini wa mtu mmoja mmoja na
familia unaweza kugundua kuwa umaskini
unasababishwa na Pombe kwa asilimia zisizopungua 75.
Usitake Sana kubishania Mambo ya kipumbavu! Kwani
huna ndugu, jamaa, rafiki, jirani, classmates etc aliyepata
majanga na kuharibu kabisa hatima Yake kutokana na
Pombe?
KWA NINI MAKANISA BAADHI YANAPIGIA
CHAPUO POMBE?
1. Akili za kinabii Tito
Yesu alilewa, na sisi tulewe jamani ! kwa maana
imeandikwa hivyo katika Luka 7:33-35
 Nilishangaa watu wakimcheka nabii Tito
kwamba anapotosha, wakati kwa masikio yangu
nimesikia kwenye mahubiri zaidi ya Mara kumi
Makasisi wakihubiri hivyo kuanzia kwenye dini
yangu?. Kwa hiyo kina TITO Wapo kila Kona,
kila dini na kila dhehebu, sema wengine

53
wanaheshimika, wengine wanadharaulika, lakini
akili yao moja!
 Yesu hakuwahi kuwa mlevi, aliitwa hivyo na
wapinzani wake wakuu, hasa mafarisayo
2. Mtume Paulo aliagiza tunywe pombe!
Ila Nyinyi watu, Paulo aliagiza wapi?
Aliagiza hapa!
1 Timotheo 5:23 "Tokea Sasa usinywe maji tu, Lakini
tumia MVINYO kidogo kwa ajili ya tumbo lako, na
magonjwa yanayokupata Mara kwa Mara."
Jamani, hata kwa akili za usiku ni kweli Paulo anaagiza
hapo tunywe pombe? Hata kwa Akili zangu za darasa la
kwanza Mwishoni mwa miaka ya 90 kule shule ya
msingi Kawekunelela-Ushetu Kahama, ningeelewa
hivyo?
Kwamba, Wakristo wote tunaumwa tumbo? Na
tunapatwa na magonjwa Mara kwa Mara ambayo tiba
yake ni kwunywa pombe?
Pombe Kama dawa haina shida, Maana hata majani ya
bangi hutengenezwa dawa na kemikali nyingi zifaazo
kwa tiba! Kama daktari kakwambia hivyo sawa, Lakini
usihalalishe uraibu wako kwa kigezo cha dawa wakati
huna ugonjwa unaotibika kwa Pombe.
4. Inaleta furaha ya moyo!
Zaburi 4:7 na zaburi 104:15

54
Elewa wazi kuwa, Hii ilikuwa njia nzuri kwa watu wa
agano la kale kujiliwaza kwa Sababu Roho Mtakatifu
alikuwa bado hajamwagwa! Leo hatutegemei Pombe
kufurahi, badala yake tunafuraha Kama matokeo ya
kuongozwa na Roho Mtakatifu!
Wagalatia 5:22 "Lakini tunda la Roho Ni UPENDO,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili,
uaminifu, upole na kiasi.
 Unasaka furaha kwenye Pombe? Fikiri
kiungwana!
 Ndiyo maana nimetangulia kusema kule juu na
Hapa nakumbusha tena
Waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo ambamo
man ufisadi Bali mjazwe Roho Mtakatifu."
Zaidi ya hapo Nisemeje?

4.Kuondoa mawazo!
Mithali 31:6-7 "Mpe kileo yeye aliye karibu na
kipotea, kaMpe divai yeye aliye na uchungu nafsini,
Anywe akausahau umasikini wake, asiikumbuke
Tena taabu Yake."
Kwa kawaida shida, dhiki, umasikini na uchungu nafsini
havitoki kwa kunywa Pombe. Zaidi vinakupa unafuu wa
muda mfupi “temporary relief” na Pombe ikiisha

55
matatizo unayakuta yanakusubiri! Wanasaikolojia wote
wanaomjua Mungu na WAPAGANI hawawezi
kukushauri kunywa Pombe kumaliza.matatizo yako!
MWISHO Kama umesoma na kuelewa Basi fanya uamzi
wako Mwenyewe!

56
SURA YA SITA
UKWELI KUHUSU URAIBU (ADDICTION)

MASWALI YA KUJIULIZA
1. Umetumia tumbaku, ugoro, pombe, bangi,
mirungi, sembe nk?
2. Umekuwa muumini mwaminifu sana wa
kutazama picha na video za ngono?
3. Umekuwa ukikaa na kuperuzi mitandao ya
kijamii muda wote napengine huelewi nini hasa
unakitafuta lakini huwezi kujizuia?
4. Vipi kuhusu mawazo, fikra na hisia za ngono,
zinakujia mara kwa mara?
5. Huwezi kushiriki tendo la ndoa bila kutumia
“booster” kwanza?
6. Unajichua? Unapiga punyeto?
7. Unathamini mpira, kiasi kwamba unaweza
kutoroka saa ya maziko au ratiba yoyote muhimu
ili ukaangalie mpira?
8. Unakaa kwenye runinga muda mrefu mpaka
wakunyang’anye rimoti?
9. Vipi, kuhusu kujiona mnafiki, na kujihukumu
wewe mwenyewe kutokana na ‘tabia’ yako
Fulani chafu ya gizani iliyokushinda kabisa
kuiacha?
10. Nini kinatawala sehemu kubwa ya maisha yako?

57
JIBU LOLOTE JUU YA MASWALI HAYO
LIKUPE KIU NA HAMASA YA KUSOMA SURA
HII KWA TAFAKARI.

URAIBU/UTEJA ni ile hali ya mtu kuathiriwa na kitu au


tabia fulani kwa kiasi kikubwa, hali inayopelekea
kwenye utegemezi kwa kitu hicho au tabia hiyo,
Kadharika hali hiyo humfanya muhanga ashindwe
kujizuia au kuachana na tabia hiyo, pale atakapohitaji
kufanya hivyo
Dunia ya leo, hasa katika karne tuliyonayo, tumeendelea
kushuhudia ongezeko kubwa la vijana walioathiliwa
vibaya sana na madawa ya kulevya na tabia mbaya za
kisirisiri.
Pamoja na jitihada za serikali, mashirika ya kimataifa na
asasi za kiraia kuwekeza nguvu kubwa katika
kupambana, kuzuia na kuelimisha jamii juu ya athali za
mambo hayo, lakini bado hali haijawa nzuri!
Katika makala hili, nitajikita zaidi kuonesha chanzo cha
tatizo, kwani huwezi kumaliza tatizo bila kumaliza
chanzo chake!,
Kwa kuzingatia maudhui ya aya hii hapa chini, Najisikia
deni nisipokushirikisha kile nikijuacho juu ya uraibu!

Warumi 15:1-6, ”Sisi tulio imara katika imani,


tunapaswa kuwasaidia wale walio dhaifu wayakabili
matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu, kila
mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwa
58
wema ili huyo apate kujijenga katika imani. Maana
Kristo hakujipendelea mwenyewe ila alikuwa kama
yasemavyo maandiko, “Kashfa zote walizokutolea
wewe, zimenipata mimi…..,”
Kwa msingi huo, Mimi kama mdau hai wa vijana, ninalo
jukumu na wajibu wa kuwasaidia hawa vijana na watu
wengine walioathilika na madawa pamoja na tabia chafu,
ili wajinasue kutoka katika tabia hizo na hatimaye
wapone na kurudi katika hali zao za kawaida ili
kuendelea na majukumu yao ya kila siku katika ujenzi
wa taifa.
Lakini kwa upande mwingine, lipo jukumu muhimu
zaidi la kuwaelimisha wale ambao hawajaathirika ili
wafahamu athali ya dawa za kulevya na tabia zote zenye
kuleta uraibu na utegemezi katika maisha yao!

MPANGO WA ASILI WA MUNGU KWA


BINADAMU NI KUTAWALA
Mpango wa asili wa Mungu, ni binadamu kutawala
uumbaji wake wote na siyo binadamu kutawaliwa na
uumbaji!
Mpango na makusudi ya Mungu ni binadamu atawale
wanyama, ndege, samaki, mimea na kila kitu!
Kwa mantiki hiyo, Uumbaji wa Mungu unapogeuka na
kukutawala WEWE maana yake uko nje ya mapenzi na
makusudi ya MUNGU!
Binadamu wote tumepewa hadhi na mamlaka ya
kutawala siyo kutawaliwa; Na ninaposema kutawala
59
simaanishi binadamu kumtawala binadamu mwenzake,
lahasha! Ni binadamu kutawala viumbe wengine huku
akitawala hadi hisia zake mwenyewe!
Mwanzo1:27-31 Mungu akaumba mtu kwa mfano
wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu
akawabarikia, Mungu akawaambia, “Zaeni
mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale
samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila
kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu
akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao
mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti,
ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndiyo
chakula chenu na chakula cha kila mnyama wa nchi
na kila ndege wa angani na cha kila kitu
kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote
ya miche ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo, Mungu
akaona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema
na cha kupendeza sana, ikawa jioni ikawa asubuhi,
siku ya sita.
Binadamu kapewa mamlaka ya kutawala uumbaji wote
wa Mungu, kwa hivyo binadamu hakupaswa na hapaswi
kutawaliwa na kiumbe kingine chochote wala mmea! Pia
katika hili, nipende kubainisha wazi kuwa, kakuna mche
haramu hata mmoja, kwa sababu kila alichokiumba
Mungu aliona ni chema na cha kupendeza sana, Mapenzi
ya Mungu ni kuona uumbaji wake unatunufaisha na siyo
kutuletea matazizo ya afya na akili.
Hata katika agano jipya mtume Paulo aliendelea
kulisisitiza na kulikumbusha hili, anaweka wazi kuwa

60
kila kitu ni halali kabisa, lakini hatupaswi kutawaliwa
na chochote!
1wakorintho 6:12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini
si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini
mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote.
Kimsingi baada ya uasi wa wazazi wa kwanza pale
Edeni, miongoni mwa athali alizozipata mwanadamu ni
pamoja na kutawaliwa na viumbe, mimea, mpaka hisia
zake mwenyewe! Kifupi itoshe kusema kwamba
alishindwa kutawala na kujitawala, ndiyo chanzo cha
uraibu!
Ndiyo chanzo cha kuanza kutawaliwa na tumbaku,
bangi, vinywaji na kadharika. Pamoja na viwanda
vinavyotengeneza sigara kuweka onyo kali kuwa
‘uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya,’ lakini bado kuna
ongezeko kubwa la uvutaji wa sigara!
Kwa kifupi ni muhimu kuwapandikizia watoto wetu na
vijana mawazo ya kwamba hawajazaliwa watawaliwe na
kitu chochote! Wamezaliwa ili watawale kila kitu mpaka
hisia zao!
Kwa sababu, mtu asiyetawala hisia zake tayari ni tatizo!
Neno la Mungu linasema katika
Mithali 25:28 Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji
uliobomoka, usio na kuta.
Na mithali 16:32 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema
kuliko shujaa, na mtu aitawalaye roho yake kuliko
mtu atekaye mji.

61
Kwa ufupi biblia inamsifia mtu mwenye kutawala hisia
na tamaa zake kwamba ni zaidi za shujaa, lakini vilevile
imeweka wazi kuwa mtu asiyetawala roho yake ni kama
mji uliobomoka usio na kuta!

JINSI URAIBU UNAVYOINGIA

Kuna msemo wa wataalamu wa mambo ya lishe, kwa


kimombo wanasema, “We are what we eat” Yaani tuko
jinsi tulivyo (KIAFYA) kutokana na vyakula
tunavyokula! Kwamba, afya zetu kwa kiasi kikubwa
huchangiwa na kile tunachokula! Kwa kawaida vyakula
huingia tumboni na virutubisho hufyonzwa kwa
matumizi ya mwili na mabaki hutolewa nje kama
kinyesi, Lakini Sasa linapokuja suala la afya ya akili au
ubongo hali ni ileile katika maelezo tofauti kidogo kama
ifuatavyo!
Ni Kweli, chakula cha kawaida kina mchango mkubwa
katika maendeleo ya ukuaji wa ubongo hasa kwa mtoto
mdogo, mathalani chini ya umri wa miaka mitano.
Lakini ubongo wa mwanadamu kila siku unakula kupitia
kile unachotazama na kukiona, kukisikia, kukisoma,
kukihisi, kukionja na kadhalika. Kwa hiyo ubongo
hupokea taarifa kupitia milango mitano ya fahamu na
kuhifadhi katika kumbukumbu.
Katika saikololojia, kuna aina tatu za kumbukumbu
ambazo ni kumbukumbu hisia (sensory memory) hizi
hutokana na kile unachokiona au kukisikia papo kwa
hapo na kwa maana hiyo hupotea na kusahaulika ndani

62
ya sekunde chache au muda huo huo, Kwa sababu hiyo
hazina athali yoyote kwa mtu!
Pili kuna kumbukumbu za muda mfupi hizi huitwa
(short term memory) hudumu kwa muda mfupi na
baadaye husahaulika kabisa!
Lakini kuna kumbukukmbu za kudumu au za muda
mrefu yaani (long term memory) ambazo huhifadhiwa
na kukaa kwa muda mrefu! Kumbukumbu hizi
zinazokaa kwa muda mrefu huitwa “Subconcious mind”
au “unconscious mind” na kwa maana hiyo huweza
kuathili kabisa tabia ya mtu husika bila hata yeye
kujitambua, kwa kuwa huingia kwenye mfumo wa
maisha ya kawaida ya tabia, hisia na hulka za mhusika.
Sasa basi, kama mtu ataijaza akili yake mambo mabaya
kwa muda mrefu, matokeo yake ataanza kufanya mambo
ya kijinga na huo ndiyo hasa utakuwa utaratibu wa
maisha yake ya kila siku!
Mtu aliyezoea kuangalia picha au video za ngono kwa
mfano, hufikia hatua hata asipoangalia tena lakini
akizichota picha na videoz kwenye kumbukumbu za
muda mrefu (subconscious mind) na kuzileta kwenye
kumbukumbu inayofanya kazi kwa wakati huo (working
memory) huweza kuziona kana kwamba ni mubashara
(live) na rangi na sauti zake.

Kwa walioathilika hivyo, huwa inawawia vigumu sana


kuzifuta picha hizo kwenye bongo zao, kwa nini ni
vigumu? Ni vigumu kwa sababu tayari zimeshaingia
kwenye unconscious na subconscious mind na kwa

63
maana hiyo zimefanyika kuwa utaratibu wa kawaida
katika kuratibu maisha yao!

MUUNDO WA BINADAMU
Binadamu kamili ni mwili, nafsi na roho. Ili unielewe
vizuri zaidi ngoja niweke hivi! Binadamu ni ROHO
inayoishi kwenye MWILI wenye NAFSI.
Ambapo ili uelewe sawasawa zaidi naweza kukuonesha
hivi;
Mwili+Roho+Nafsi=Binadamu aliyekamilika
Mwili-Nafsi-Roho=Maiti
Mwili+Roho-Nafsi=Kichaa wendawazimu

Sasa linapokuja suala la uraibu iko hivi; Mwili ambao


ndio unaomiliki milango ya fahamu hupokea taarifa
kutoka kwenye mazingira na kuzituma kwenye nafsi
(akili, hisia na utashi) akili ikikubaliana na taarifa hizo,
basi huzituma moja kwa moja kwenye ROHO. Kwa hiyo
kwenye roho ndiyo hasa ghala au stoo ya kuhifadhia
taarifa zote anazozichukulia mtu kuwa muhimu kwake.
Kwenye biblia sehemu hii imetajwa kama MOYO!
Siyo kwa maana ya moyo unaosukuma damu mwilini.
Ni kwa maana ya roho na ndiyo maana mtu katili huitwa
ana roho mbaya! Maana yake moyo wake umehifadhi
mambo mabaya na hayo mambo (taarifa) yamegeuka

64
kuwa utaratibu wake wa maisha ya kila siku.
Umenielewa?
Kama umenielewa tuendelee mbele kidogo, Roho
ikishahifadhi mambo ya hovyo hovyo, itakuwa
inaiamrisha nafsi yako na nafsi kwa sababu ilisharuhusu
siku nyingi basi na yenyewe itauamrisha mwili
utekeleze kwa lazima hata kama hautaki. Ndiyo chanzo
cha mtu kujichua bila kutaka, au kuvuta ugoro, sigara, na
kufanya ngono uzembe zenye majuto baadae!
Kuna watu wengi sana wanatamani kuacha mazoea
fulani fulani, lakini imeshindikana kwa sababu tayari
mambo au tabia hizo zilishaingia kwenye (subconscious
mind) MOYO/ROHO na ndiyo maana hawezi kuacha
kujichua, hawezi kuacha kuvuta sigara au kunywa
pombe au kutumia dawa za kulevya nakadharika! Bila
usaidizi wa kiroho pamoja na ule wa kisaikolojia ni
jambo gumu sana kujinasua!
Kama umenielewa itakuwa rahisi sana kwako kuelewa
mafundisho na mantiki za kibiblia hasa kwenye kitabu
cha;
Mithali 5:23 “Linda moyo wako kuliko yote
uyalindayo maana ndiko zitokazo chemchemi za
uzima.”
Kumbe MOYO, kama nilivyotangulia kusema ni ghala
au stoo ya kuhifadhia akiba. Kwa hiyo ni stoo
inayohifadhi taarifa mbaya na nzuri. Kama mtu
amehifadha mambo mema ndipo zitatoka chemchemi za
uzima!

65
Kwa kutambua umuhimu huo wa moyo, ndiyo maana
umeshauriwa kuulinda ipasavyo!
Na ikiwa umehifadhi picha na video za ngono basi hizo
ndizo zitaendesha maisha yako!
Kama unafikiri nadanganya linganisha na Ufafanuzi wa
Yesu Kristo mwenyewe kwenye
Mathayo 12:33-35 “Ufanyeni mti kuwa mzuri na
matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa
mbaya kwa matunda yake mabaya; kwa maana kwa
matunda yake mti hutambulika. Enyi wazao wa
nyoka, mwawezaje kunena mema mkiwa wabaya?
Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo
wake. Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema,
na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.”
Kama hujaamizi kuwa Moyo (mind) wako ndiyo hazina
inayohifadhi taarifa njema na mbaya linganisha tena na
Mathayo 15:18-19 ‘Bali vitokavyo kinywani vyatoka
moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi kwa
maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, izinzi,
uasherati, wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano.”
Unapoona ujinga unazidi kuongezeka, hata miongoni
mwa watu wazima ni lazima uchunguze na kutafakari
hata vitu wanavyovipa nafasi kubwa kwenye mioyo yao
na bongo zao!
YESU ALIONYA KUJILINDA NA CHACHU
Mathayo 16:5-12 Nao wanafunzi wakaenda hata
ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate. Yesu
akawaambia, “Angalieni, jilindeni na chachu ya
66
mafarisayo na masadukayo” wakabishana wao kwa
wao wakisema, ni kwa sababu hatukuchua mikate.
Naye Yesu akafahamu, akawaambia, “Mbona
mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache,
kwa sababu hamna mikate?. Hamjafahamu bado,
wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu
tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota? Wala ile
mikate saba kwa wale elfu nne, na makanda mangapi
mliyookota? Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si
kwa sababu ya mkate naliwaambia? ILA JILINDENI
NA CHACHU YA MAFARISAYO NA
MASADUKAYO, Ndipo walipofahamu ya kuwa
hakuwaambia kujilinda na chachu ya mikate, BALI
MAFUNDISHO YA MAFARISAYO NA
MASADUKAYO.
Yesu anawatahadharisha na kuwaonya wanafunzi wake
wajihadhari na mafundisho ya mafarisayo na
masadukayo! Kwa nini wajihadhari? Ili ujue mafarisayo
walikuwa watu wa aina gani rejea katika
Mathayo 23:1-36 ukisoma hapa, utagundua mara moja
kuwa Mafarisayo kwa ujumla walikuwa wanafiki!
Walipenda kukaa viti vya mbele kwenye sherehe na
ibada, mafisadi, waongo na watu wasiojua kitu yaani
vipofu!
Kwa hiyo, Yesu aliwaonya kwa tafsiri ya kiingereza
(KJV) imeandikwa [take heed] of what you hear! maana
yake [be selective] yaani chagueni vya kusikiliza!

67
KWA NINI MAFUNDISHO MABAYA
ALIFANANISHA NA CHACHU?

Chachu kwa Kiswahili kingine ni amira, chachu inatabia


ya kuumusha unga! Hata kama ulikuwa kidogo tu amira
ikifanya kazi kisawasawa utashangaa ndoo imejaa hata
kama unga ulikuwa kilo mbili tu,
Hii ina maana gani? kadri unavyosikiliza au kutazama
vitu potofu, taratibu vitaanza kukuumusha kifikra, kiakili
na kitabia na mwisho utaharibika kabisa! Kwa hiyo
kama ni kwenye TV chagua vipindi vile tu unavyoona
vinamanufaa kwako na kwa watoto wako! Acha
kuangalia mikanda ya ngono! Acha kufuatilia kitu
chochote ambacho hakiwezi kukusaidia kufikia kilele
cha maono yako!
Acha kushabikia vitu ambavyo havihusiani na kile kitu
Mungu amekuumbia na kukuleta hapa duniani kwa
kigezo cha “Kusuuza nafsi”!
Ndiyo maana Mungu aliweka kope kwenye macho, ili
pale ambapo hatutaki kutazama baadhi ya vitu
zituwezeshe kufumba macho, maana kama kope
zisingekuwa na kazi angeweza kutuwekea macho kama
ya panzi, lakini kwa kuona umuhimu wa kufumba na
kufumbua alituwekea kope!
Mimi siwezi kusikiliza wala kutazama vitu
vinavyohatarisha afya yangu ya mwili, roho na akili!
Huwa nikigundua tu hiki kitu si fungu langu, basi mara

68
moja huwa naachana nacho, nahii nidhamu nimeijenga
kwa muda mrefu!
Kwa hiyo, vyote kwa pamoja yaani Mwili, roho na nafsi
vinatakiwa kuwa safi! Havitakiwi kuchafuliwa na jambo
lolote, hasa habari na picha au video zisizofaa.
Tumeshashauriwa kuwa
“linda moyo wako kuliko yote uyalindayo maana
ndiko zitokazo chemchemi za uzima’
lakini pia ni jambo zuri na la kheri kama tukilinda na
viungo vinavyorekodi taarifa mbalimbali na kuzituma
kwenye Moyo. Katika hili neno la Mungu linashauri
hivi;
1Wathesalonike 5:23 Mungu wa amani mwenyewe
awatakase kabisa; Nanyi NAFSI zenu na ROHO
zenu na MIILI yenu, mhifadhiwe mwe kamili, bila
lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu
Kristo.
Kwa hiyo nafsi, roho na mwili ni lazima vitakasike, na
kitu kikitakasika maana yake kitumike inavyopaswa!
Mtume Paulo aliuona uhitaji huu alipowaandikia
wakristo Wathesalonike, anawahimiza na kuwaombea
kwamba Mungu wa amani, Awatakase kabisa katika
maeneo hayo matatu ambayo nimeyazungumzia hapo
juu yaan mwili, nafsi na roho!

69
USHAURI WA KIBIBLI
Marko 9:42-50 “Jicho, mkono, mguu nk
kikikukosesha, kata au ng’oa”
kwa hiyo ni bora kuliong’oa jicho lako kwa habri ya
pornograph!
Zaburi 119:37 “Unigeuze macho yangu, nisitazame
visivyofaa, unihuishe katika njia yako”

70
SURA YA SABA
SHABAHA YA URAFIKI
Urafiki ni hali ya uhusiano, mapatan na /ushirikiano wa
karibu kati ya watu wawili au zaidi wenye malengo
yanayofanana. Urafiki hulenga hasa kusaidiana,
kufarijiana, kutiana moyo, kushauriana, kukosoana nk!
Upo urafiki wenye faida na urafiki wenye hasara. Na
kwa mujibu wa saikolojia ya jamii, marafiki kwa sehemu
kubwa huweza kuathiriana kwa namna moja au
nyingine! Rafiki anaweza kuwa chachu ya mafanikio
kwako au chachu ya kukudumaza kama tutakavyoona
baadaye.
UFALME WA MUNGU UNAUTAZAMAJE
URAFIKI?
Ufalme wa Mungu unautazama urafiki kwa jicho
chanya! Kwamba kuwa na rafiki au marafiki ni jambo
jema na la kheri, hata hivyo umeweka tahadhari na
angalizo juu ya aina ya marafiki, kwani rafiki anaweza
kukubomoa au kukujenga.
SHABAHA YA URAFIKI
Shabaha ua lengo mahususi la urafiki ni kusaidiana,
kutiana moyo, nguvu, kushauriana nk
Rejea hapa!
Mhubiri 4:9-10 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja,
maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana

71
wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake.
Lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala
hana mwingine wa kumwinua!”
Shabaha ya urafiki ni kuinuana na kutiana moyo! Ni
kusaidiana na kushauriana.
Hii ndiyo ilimfanya Bwana Yesu aboreshe zaidi mfumo
wa kimahusiano kati yetu na yeye ili aweze kutusaidia
zaidi na kwa karibu zaidi. Yaan kutoka hali ya
mahusiano ya kitumwa na kujenga hali ya mahusiano ya
kirafiki zaidi!
Yohane 15:15 “Siwaiti tena watumwa; kwa maana
mtumwa hajui atendalo Bwana wake; lakini ninyi
nimewaita RAFIKI, Kwa kuwa yote niliyoyasikia
kwa baba yangu nimewaarifu.”
*Kumbe ile hali ya kujulishana na kufahamishana
mambo na kila kinachoendelea ni tabia ya urafiki hai.
Huwezi ukawa na rafiki wa kweli na wa dhati ambaye
hakushirikishi kwa lolote katika mambo yake. Huyo siyo
rafiki, labda ni jamaa tu!
Hata katika namna za ibada, Bwana Yesu alitushauri
tusali vikundi vikundi vyenye kupatana kama marafiki!
Mathayo 18:19-20 “Tena nawaambia, ya kwamba
wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo
lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu
aliye mbinguni. Kwa maana walipo wawili watatu
wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo
hapo katikati yao.”

72
Huo ndiyo aina ya urafiki unaopaswa katika Ufalme wa
Mungu! Urafiki kwa ajili ya mambo yauhusuo Ufalme
wa Mungu yaani urafiki chanya!
VIGEZO VYA KUWA MARAFIKI.
Suala la kuwa marafiki wa kweli huwa halitokei kwa
bahati tu! Ni mchakato wa asili ambao huweza
kukamilika baada ya wawili hao kuwa wamefanana na
kuendana katika mambo kadhaa kama ifuatavyo!
MFANANO/SIMILARITY.
Katika saikolojia, kigezo kikubwa cha watu kuwa
marafiki ni mfanano. Rejea Gestalt Psychologists
Principles of grouping.
Kufanana huku kuko kwenye kuendana kimawazo na
mitazamo siyo sura na mwonekano!
Yoshua bin Sira 13:14 “Kila kiumbe hupenda
kilichofanana nacho, na kila mwanadamu humpenda
aliyefanana naye. Wanyama wote huandamana wa
aina kwa aina, vilevile mwanadamu ataambatana na
mmoja wapo wa aina yake.”
Huu ndiyo ukweli unaoishi, ni suala gumu kuwa kwenye
urafiki na mtu usiyeendana naye kimawazo! Na ndiyo
maana watu wenye hekima wa zamani sana walipata
kusema hivi.
Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma, ndivyo mtu
aunoavyo uso wa rafiki yake.”

73
Kwa hiyo kama wewe ni chuma basi siyo rahisi kunoana
na ubao! Urafiki wa kweli hufanana katika vigezo vingi!
Kama rafiki yako siyo chuma halafu wewe ni chuma
uwe na uhakika urafiki huo hautadumu, ni kama ngoma
ya watoto tu, haitakesha!
KUPATANA/CONNECTEDNESS
Bila kupatana katika mambo mengi, urafiki huweza kufa
kabisa, kwa hiyo kupatana ndiyo kigezo ambacho
huufanya urafiki udumu na kudumu kwa muda mrefu.
Amosi 3:3 “Je, watu wawili waweza kutembea
pamoja, wasipokuwa wamepatana?.”
Urafiki bila mapatano kwa hakika kabisa hauwezi
kudumu!

IDADI YA MARAFIKI
Hakuna kigezo maalumu cha idadi ya marafiki, hata
hivyo hekima inashauri bora uwe na rafiki mmoja wa
maana, halafu wengine wawe kwenye lile kundi la jamaa
tu!
Kuwa na Idadi kubwa ya marafiki wakati mwingine ni
kuongeza idadi ya maadui, Uzoefu unaonyesha kwamba
maadui wakubwa wa mtu ni watu wa karibu, ni wale
ambao kwa kipindi fulani wamewahi kuwa marafiki!

74
Yoshua bin Sira 6:6 “Wale wenye amani nawe na
wawe wengi. Bali rafiki wa kukushauri mmoja kati
ya elfu.”

JINSI YA KUMPATA RAFIKI WA KWELI.


Urafiki hujengeka na kukua kwa taratibu sana. Kwa hiyo
inashauriwa usiwahi kujiaminisha kwake, kwani
wengine huja na malengo yao na yakishatimia hawezi
kuwa na muda na wewe!
Yoshua bin Sira 6:7-13
“Ukitaka kujipatia rafiki, umpate kwa kumjaribu,
wala usiwe na haraka katika kumwamini. Yaani
kuna rafiki wakati wa kufaa, ambaye yeye hatadumu
wakati wa msiba wako. Tena kuna rafiki ageukaye
kuwa adui, naye atakukashifia fitina iletayo lawama.
Pia kuna rafiki tena, ambaye anakula mezani pako,
bali siku ya mabaya haonekani. Wakati wa
kufanikiwa kwako atakuwa sawa nawe na kupiga
domo juu ya watumishi wako. Lakini ukipatwa na
masaibu atakugeuka na kujificha mbali nawe na uso
wako. Basi ujitenge na adui zako. Tena ujihadhari na
rafiki zako.”
Wenye hekima wanaendelea kutuinya!
Mika 7:5a “Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi
tumaini”

75
Kwa nini kila sehemu inasisitizwa kutokumwamini
rafiki? Watu wengi wamesalitiwa na rafiki zao wa karibu
sana!
NJIA YA KUDUMISHA URAFIKI
Katika safari ya urafiki huwa kuna mambo mabaya na
sintofahamu kadha wa kadha hutokea. Sasa yanapotokea
hayo ni muhimu kwa wahusika kuhojiana bila woga ili
kupata ukweli na kuonyana kindugu hali hii husaidia
sana kuboresha, kukomaza na kuupa thamani urafiki kwa
kiwango kikubwa sana!
Yoshua bin Sira 19:13-17 “Mhoji rafiki yako, labda
hakulitenda. Hata iwapo amelitenda yawezekana
asizidi kulitenda. Mhoji jirani yako, labda
hakulisema. Hata iwapo amelisema yawezekana
asiliseme tena. Basi mhoji rafiki yako mara nyingi
huwa masingizio tu, wala usiliamini kila neno. Aidha
kuna atelezaye kwa ulimi, wala si kwa moyo kwa
maana yu nani asiyekosa kwa ulimi wake? Basi mhoji
jirani yako kabla ya kumtisha, uipishe torati yake
aliye juu.”
Changamoto kubwa kwa baadhi ya rafiki zetu kwenye
hili huwa ni moja! Ukimhoji badala ya kukuelewesha
kwa upendo, anakufanya adui mara moja na kukuepuka!

Hapa Bwana Yesu alishauri hivi!

76
Mathayo 18:15-17 “Na ndugu yako akikukosea,
enenda ukamwonye, wewe nay eye pake yenu.
Akikusikiliza umempata nduguyo. Lakini kama
hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au
wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au
watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao,
liambie kanisa; na asipowasikiliza kanisa, na awe
kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”

*Hiyo ndiyo kanuni rahisi ya kushughulikia mgogoro wa


kirafiki/kindugu.
EPUKA MARAFIKI WABAYA!
Epuka kabisa marafiki wabaya, kwa sababu wanaweza
kukupoteza na kukuharibu! Tumeshaona vijana wema na
wazuri wakiharibika baada ya kujiunga na marafiki
wenye tabia mbaya!
Zaburi 1:1 “Heri mtu asiyekwenda katika shauri la
wasio haki; wala hakusimama katika njia ya
wakosaji. Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”
Mithali 22:24-25 “Usifanye urafiki na mtu mwenye
hasira nyingi, wala usiende na mtu wa ghadhabu
nyingi. Usije ukajifunza njia zake na kujipatia nafsi
yako mtego.”

77
TAFUTA WENYE UWEZO WA KUKUSAIDIA!
Ikiwa una njaa na kiu ya kuwa mtu mwenye hekima,
basi ni busara zaidi kutafuta marafiki watakaokusaidia
kuwa na hekima unayoihitaji!
Mithali 13:20 “Enenda pamoja na wenye hekima,
nawe utakuwa na hekima. Bali rafiki wa wapumbavu
ataumia.”
Karibu katika Ufalme wa Mungu, Ujipatie rafiki mmoja
wa kwali asiye mnafiki, Bwana Yesu,!

78
SURA YA NANE
UHUSIANO WA AFYA YA AKILI NA IMANI
Kupitia uzoefu nilioupata kwa kujifunza historia ya
mwanadamu na maendeleo ya dini, afya ya akili, biblia,
kutafakari na uhalisia wa kinachoendelea kwenye
ulimwengu wa dini na madhehebu, nimeng’amua na
kuhitimisha kuwa “Upo uhusiano mkubwa sana kati ya
afya ya akili na Imani”
KIVIPI?
Mtu amabaye afya yake ya akili siyo bora na thabiti
yupo hatarini zaidi kuamini hoja za
kizushi/kijinga/kipumbavu!
Ni rahisi kuamini propaganda za kidini na mafundisho
ya kipumbavu yenye sura ya dini! Na vilevile mtu
ambaye afya yake ya akili ni bora na thabiti anao uwezo
wa kufikiri, kutafakari na kung’amua kuamini
mafundisho hayo, kuyakataa au kuamini vinginevyo!
Kwa kifupi kabisa, afya ya akili inaanza kutengenezwa
kipindi cha mimba na hata baada ya kuzaliwa! Uchaguzi
mzuri wa vykula kwa mama huimarisha ukuaji wa
ubongo wa mtoto akiwa tumboni, kwa upande mwingine
mjamzito hushauriwa kuacha matumizi ya baadhi ya
dawa, pombe, sigara, bangi nk kama njia ya kulinda afya
ya akili ya mtoto tumboni!
Baada ya kuzaliwa, lishe nzuri na bora ni muhimu sana
kwa ukuaji na maendeleo ya ubongo wa mwanandamu

79
mpaka miaka 5 hivi. Baada ya hapo ubongo wa
mwanadamu hustawi ama kudumaa kutokana na aina ya
mafundisho anayopata, mila, desturi na utamaduni wa
jamii husika! Mafundisho na utamaduni bora huweza
kuchochea ubunifu na kukuza fikra halikadhalika
mafundisho na tamaduni duni hudumaza ubongo. Hata
hivyo matumizi makubwa ya pombe, bangi na dawa za
kulevya huweza kuharibu ubongo wa mwanadamu kwa
kiwango kisichomithilika!
AKILI NDOGO HUDANGANYIKA KIRAHISI
Tito 3:3 “Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa
hatuna AKILI. Tulikuwa waasi,
tumedanganywa…………”
Mtume Paulo anamwambia Tito, tatizo la wao kuwa
waasi, wauaji nk hapo zamani lilisababishwa na kukosa
akili tu! Kwa kukosa akili walidanganyika! Leo hii
vijana wadogo kabisa kwa kukosa akili wanajiunga na
imani za kipumbavu zenye kuleta maangamizi, ukatiri na
maafa kwa familia na jamii zao wenyewe!
NI LAZIMA KUSAILI KILA FUNDISHO
Watu wenye kujiridhisha na ukweli wa mafunmdisho
kwa tafiti na tafakari, biblia imewataja kama
waungwana!
Matendo ya Mitume 17:10-11 “Mara hao ndugu
wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao
walipofika huko wakaingia katika sinagogi la
wayahudi, Watu hawa walikuwa WAUNGWANA

80
kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea
lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza
maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo
ndivyo yalivyo.”
Mwandishi Luka anawatazama watu hawa wa Beroya
kama waungwana kwa sababu mbili muhimu!
Kwanza, waliipokea injili kwa uelekevu wa moyo, na
pili, wakayachunguza maandiko kila siku, waone
kwamba mambo hayo waliyofundishwa ndivyo yalivyo!
Kumbuka kinyume cha uungwana ni ushenzi! Kwa hiyo
kukubali fundisho la kiimani kwa shingo upande au bila
kulisaili ni dalili za wazi kuwa wewe si muungwana! Ni
dalili za kuwa mshenzi! Usipende tu kupiga kelele
ameeeee! Sema babaaa! Bila kusaili
kinachozungumzwa!
Fundisho lolote linalokunyima fursa ya wewe kufikiri,
kutafakari na kung’amua ni fundisho hatari na ni sumu
kwa ubongo wako! Ndiyo maana daima huwa niko
kinyume na mafundisho yenye dogma ndani yake!
Historia imesheheni watu waliowahi kuanzisha vikundi
vya imani za kidini zilizopata uungwaji mkono na watu
wengi, lakini mwisho wa siku wengine walichomwa
moto ama kunyweshwa sumu au kutapeliwa fedha na
mali na viongozi waanzilishi wa vikundi hivyo.
Ukifuatilia kwa karibu sana unaweza kugundua kuwa
dini na madhehebu mengi pamoja na kupingana lakini
wanafanana katika vipengele vingi! Kila dini kwa mfano

81
hutengeneza shuhuda za kusisimua na kustaajabisha
kama njia ya kupamba ama kusindikiza fundisho Fulani
la kidini. Kwa mfano katika dini ya kikristo, fundisho
lolote linalokosa uungwaji mkono kwenye biblia
hutengenezewa shuhuda maridadi pamoja na
kutangazwa kama dogma ya kiimani lengo likiwa ni
kuhalalisha uzushi huo!
Leo hii, maeneo mengi ya dunia yanaomboleza na
kusikilizia maumivu na uchungu mkubwa wa
kulazimishwa kuishi kinyume na dhamiri zao kutokana
na makundi ya wanamgambo wa kidini kuchukua
udhibiti wa maeneo yao! Mauaji ya kutisha naukatili wa
kinyama kote duniani kwa kiasi kikubwa hutekelezwa na
watu wenye masilahi ya kidini!

MPANGO WA MUNGU NI KUKUPA AKILI


YENYE AFYA KWANZA!
Ipo tofauti ya ubongo na akili, ubongo ni kitu yaan
“substance” ambacho kila binadamu anacho pia viumbe
wengine kama mbwa, sungura, simba na ndege
wanaubongo!
Akili ni kama program ya kompyuta “software”
inayoingizwa kwenye ubongo ili ubongo huo ufanye
kazi iliyokusudiwa!
Kwa hiyo upo ubongo wenye akili na ubongo usiokuwa
na akili!Ubongo wenye akili ni ule uliotunzwa vizuri na
unaowezeshwa kwa paji la roho wa Mungu!

82
ROHO MTAKATIFU NI KAMA “SOFTWARE”
KWENYE UBONGO!
Mungu aliahidi kumtuma Roho wake mtakatifu kwa
malengo anuai, kama ilivyobainishwa na manabii wa
kale katika
Ezekileli 36:26-27
Yoeli 2:28

Muhimu zaidi ni hii hapa chini.


Isaya 11:2 “Na Roho ya Bwana atakaa juu yake,
Roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na
uweza, roho ya maarifa nay a kumcha Bwana.”

Kwa hiyo, pamoja na mambo mengine, Roho mtakatifu


anayeahidiwa kuja, ataleta hekima, ufahamu na maarifa!
Rejea Ayubu 32 :8, Mwanzo 41 Danieli 5

WATU WA AGANO LA KALE WALIIJUA HII


SIRI
Hesabu 31:3-5 “Nami nimemjaza Roho ya Mungu,
katika hekima na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya
kila aina. Ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa

83
dhahabu na wa fedha, na wa shaba,Na kukata vito kwa
kutiwa mahali, na kuchora miti; Na kufanya kazi ya
ustadi iwayo yote.”
Lakini hapa pia Mfalme Suleimani alidokeza kuwa dawa
ya ujinga na upumbavu ni kuwa na roho wa Mungu
Mithali 1:22-23
NI SEHEMU YA KAZI ILIYOMLETA YESU
Pamoja na mambo mengine, Kristo Yesu alikuja kutupa
akili!
1 Yohane 5:20 “Nasi twajua kwamba, mwana wa
Mungu amekwisha kuja, naye ametupa AKILI
kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, Nasi tumo ndani
yake yeye aliye wa kweli, yaani ndani ya mwana
wake Yesu Kristo, Huyu ndiye Mungu wa kweli, na
uzima wa milele.”
KWA NINI ENEO LA AKILI LIMEANGAZIWA
SANA KWENYE BIBLIA?
Neno la Mungu linaweka mkazo wa kipekee kwenye
“Akili” maarifa na ufahamu kwa sababu vitu hivyo
vikienda likizo kuna uwezekano wa kupokea imani
potofu!
Tazama hapa kwa mfano!
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa
kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa
maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani

84
kwangu mimi; kwa kuwa umeikataa sheria ya
MUNGU wako mimi nami nitawasahau watoto
wako.”
Pia katika Isaya 5:13 “Kwa sababu hiyo watu wangu
wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na
maarifa.”

KWA HIYO UFANYE NINI?


Watu wa dini wanapenda sana kujivunia akili! Utasikia
akitaja majina ya vyuo vya juu alivyopitia sambamba na
idadi ya shahada alizonazo na GPA za juu! Pamoja na
tambo hizo, matumizi ya akili katika mafundisho na
maisha yao ni aibu hata kuandika hapa! Ni imani na
mafundisho ya uongo na kupotosha!
Paulo alionya hapa!
Warumi 12:16 “…..Msiwe watu wa kujivunia akili:”
Mtu wa kujivunia akili ni mtu asiyetumia akili! Kwa
sababu siku ukianza kutumia akili kwa kawaida huwa
ndiyo siku ya mwisho kujivunia akili!
BADALA YA KUJIVUA, TUMIA!
1 Wakorintho 15:34 “Tumieni AKILI kama
ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana
wengine hawamjui MUNGU”

85
UBONGO UNATANUKA PALE UNAPOTUMIWA
Waebrania 5:14 “Lakini chakula kigumu ni cha watu
wazima, ambao AKILI zao kwa KUTUMIWA,
zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.”
Kwa hiyo, akili inapotumika ndipo utaanza kuwa mtu
mzima kichwani! Na hapa Paulo anashauri hivi
1Wakorntho14:20 “Ndugu zangu msiwe watoto
katika AKILI zenu, lakini katika uovu mgeuzwe
watoto wachanga bali katika AKILI zenu mkawe
watu wazima”
MATUMIZI YA AKILI HADI KWENYE NYIMBO
NA MAOMBI
1Wakorintho 14:15 “Imekuwaje basi? Nitaomba
Kwa roho tena nitaomba Kwa AKILI pia; Nitaimba
Kwa roho, tena nitaimba kwa AKILI pia.”
1Petro4:7 “Lakini mwisho wa mambo yote
umekaribia, basi iweni na AKILI, Mkeshe katika
sala”
Umeona kitu? Hata kukesha kutanguliwe na matumizi ya
akili! Maana bila akili tumeshuhudia watu wakifanya
maovu hukohuko kwenye mikesha ya maombi!
MAFUNDISHO UNAYOPATA YANA AKILI
NDANI YAKE?
Elimu dunia huanzia chekechea mpaka chuo kikuu! hapo
katikati vipo vyeti, diploma, shahada za awali, uzamili,

86
udhamifu mpaka uprofesa “professorship”! Hata
uprofesa utakuta viwango e.g associate professor mpaka
full professor! Hata elimu ya Ufalme wa Mungu huanza
na mambo mepesi mpaka yale ya juu au kwa lugha
nyepesi naweza kusema mambo yale magumu!
Kwa mfano
Yesu alilazimika kuacha kufundisha baadhi ya mambo
kwa sababui wanafunzi wake walikuwa wachanga bado
kiakili na kiimani. Soma hapa
Yohane 16:12-13 “Hata bado nikali ninayo mengi ya
kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa,
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,
atawaongoza awatie kwenye kweli yote………..”
JE, kanisa lako linakupa fursa ya kukua kiimani na
kiakili? Au viongozi tu ndiyo wanaosoma na
kujiendeleza, wewe huna cha maana ukijuacho kuhusu
imani yako na Ufalme wa Mungu kwa ujumla na
umebaki kuwa muhanga wa kutoa michango tu
wanayoipanga na kuiamua?
UNA HAKI YA KUYAJUA MAMBO MAGUMU
1Petro 2:2 “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa
yatamanini maziwa ya AKILI Yasiyoghushiwa ili
kwa hayo mpate kuukulia wokovu”
Haya maziwa ya akili ni mafundisho ya juu, ya
kukufanya ukue kiakili na kiimani!

87
JUHUDI ZA KIDINI NI LAZIMA ZITAWALIWE
NA AKILI
Najua unampenda Mungu sana! Kumpenda Mungu ni
lazima kudhibitiwe na kutawaliwa na matumizi ya akili.
Kwa maana tumeshaona pale juu kwamba akili ni paji
ama kipawa kutoka kwa Mungu, kwa hiyo kutumia akili
siyo dhambi bali ni utii kwa mwenye kutuluzukia kipawa
hicho cha akili!
Warumi 10:2 “Kwa maana nawashuhudia kwamba
wanajuhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika
maarifa.”
Watu wa Rumi walikuwa na juhudi kubwa sana kwa ajili
ya Mungu kama ilivyo kwa madhehebu takribani yote,
hata hivyo akili/maarifa yalikuwa yamewekwa pembeni!
IMANI POTOFU NI TATIZO LA AKILI SIYO
IMANI
Kuna watu mpaka leo wanafundishana na kushikiria
mambo yaliyotolewa ufafanuzi zaidi ya miaka 2000
iliyopita na yakaeleweka! Tatizo hapo siyo shetani wala
imani aslani! Hilo ni tatizo la akili!

1. Kuhusu vyakula, vinywaji. Yesu alifafanua kwa


kina mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,
kwamba ukitafuna mdomoni huenda tumboni, na
baada ya mmeng’enyo (digastion) virutubisho
hufyonzwa kwa matumizi ya mwili (metabolism)

88
na mabaki hutolewa nje kama kinyesi! Alisisitiza
kuwa hakuna chakula kinachoweza kuingia
moyoni!

Watu wahakutaka kuelewa, pia wanafunzi wake


walikuwa na mashaka na fundisho hilo! Kwa
hiyo alibaini moja kwa moja kuwa wale watu
waliong’ang’ania makatazo ya vyakula
hawakuwa na akili, tatizo haikuwa imani bali
akili ndogo! Kwa hiyo siyo busara kubishana na
mtu mwenye akili ndogo!

Soma mwenyewe hapa!

Marko 7:15-23 zingatia mstari wa 18 na 19

“Akawaambia hata nyinyi hamna akili?


Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje
ya mtu, kikimwingia hakiwezi kumtia unajisi.
Kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni
tu na kisha chatoka kwenda chooni?

Mpaka leo kuna maprofesa tena waliobobea


katika dini zao na biology, Mfumo wa
mmeng’enyo (alimentary carnal) upo kichwani,
lakini wanaamini baadhi ya vyakula huimgia
moyoni badala ya tumboni! Hali hii huitwa
upumbavu uliotukuka! (This is technically
known as “a highly educated fool”) dini bila

89
usaili matokeo yake ni hayo! Unakuwa msukule
ulioenda shule na ukapata vyeti na ajira!

2. Kuhusu sheria na Neema! Karne ya 21 hii,


zaidi ya miaka 2000 bado watu wanajadili ikiwa
tunaokolewa kwa neema au kwa sheria! What a
tragedy! Na mbaya zaidi wanajaribu
kuchanganya sheria na neema kwa pamoja!

Hali hii ilishawahi kulikumba kanisa la Galatia


huko nyuma! Walianza sarakasi za kuchanganya
sheria na neema na kufundishana! Mtume Paulo
alibaini mara moja kuwa hawa watu walikuwa na
shida kichwani siyo rohoni! Yaani tatizo lao
lilikuwa kugoma kutumia akili tu!

Ujinga ulianzia hapa!


Wagalatia 1:6 na mtume akahitimisha kuwa
kama siyo kurogwa basi hawana akili!
Wagalatia 3:1-3

ACHA KUOMBA VITU, OMBA AKILI


KWANZA!

Inafahamika wazi kwamba, mfalme Suleimani


alipoambiwa na Mungu aombe chochote, Yeye
aliamua kuuomba hekima na Mungu
akampongeza kwa uchaguzi mzuri 2 Nyakati 1:2-
14!

90
Ukweli huo bado upo mpaka leo, kwani hekima
ndiyo ufunguo pekee wa maisha! Na ndiyo
maana leo ukimwomba Mungu kwa imani na
bidii, anakupa Roho mtakatifu aliye chanzo cha
hekima yote! Luka 11:13

USIOMBEWE KUPATA GARI, NYUMBA,


OMBEWA HEKIMA

Kuombewa kupata vitu ni upumbavu kama


upumbavu mwingine ulivyo! Ikiwa kuna maombi
ya maana basi ni haya ya kuomba kupata akili ili
usichezewe wala kutapeliwa kwa mgongo wa
dini!

PAULO ALIWAOMBEA AKILI

Wakolosai 1:9 “Kwa sababu hiyo sisi nasi,


tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya
maombi na dua kwa ajili yenu ili mjazwe
Maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote
na ufahamu wa rohoni!”

What a great prayer! Wakolosai walikuwa na


mwangalizi wa kiroho jembe haswa!
Anawaombea wawe na akili ili wajue cha
kufanya! Lakini wewe unaombewa vitu ambavyo
wapagani na makafiri wanavimiliki? Hiyo ni akili
ya kijinga kabisa!

91
Paulo hakuishia kwa wakolosai tu, sala hii pia
aliwaombea Wafilipi!

Wafilipi 1:9 “ Na hii ndiyo dua yangu,


kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana
katika HEKIMA na UFAHAMU wote.

Matashi mema na dua ya kuwaombea hekima


aliifanya pia kwa kanisa la Efeso na maeneo
mengine!

SALA YA KUOMBEA HEKIMA SIYO PESA

Waefeso 1:15-18 “Kwa sababu hiyo mimi


nami, tangu nilipopata habari za imani yenu
katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa
watakatifu wote, siachi kutoa shukrani kwa
ajili yenu. Nikiwakumbuka katika sala zangu,
Mungu wa Bwana wetu wetu Yesu Kristo,
Baba wa utukufu, awape ninyi Roho ya
hekima, naya ufunuo katika kumjua yeye.
Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue
tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri
wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu
jinsi ulivyo, Na ubora wa ukuu wa uweza
wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa
kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake,”

92
RUKWA NA AKILI KWA AJILI YA
MUNGU, KUWA NA HEKIMA KWA AJILI
YA KANISA!

2 Wakorintho 5:13 “Maana ikiwa tumerukwa


akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu;au ikiwa
tunazo akili zetu ni kwa ajili yenu!

Ndiyo! Yawezekana kabisa ukaona akili yangu


kuwa haiko sawa, Usihofu, Watu wengi
wanaonifahamu tangu zamani wameniuliza kama
nimerukwa na akili, kwa kufundisha kinyume na
wanavyotaka wao nifundishe! Hata hivyo
nafurahi kuona lipo kundi kubwa la watakatifu
wanaoona hekima na ukweli kwenye mafundisho
haya! Kwa hiyo ukiona nimerukwa na akili ujue
ni kwa ajili ya Mungu na ukiona utimamu ndani
yake ujue ni kwa ajili ya kulijenga kanisa!

93

You might also like