MUHTASARI WA KIKAO CHA KUFUNGUA KIKUNDI KILICHOFANYIKA TAREHE 30

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 1

MUHTASARI WA KIKAO CHA KUFUNGUA KIKUNDI KILICHOFANYIKA

TAREHE 30/06/2024 KATIKA UKUMBI WA BIG SCREEN:


A)MAHUDHURIO
Wajumbe walioitikia wito wa kikao kilichofanyika tarehe tajwa hapo juu walikua ni ………….

B)AGENDA
1.KUFUNGUA KIKAO
2.KUJADILI NAMNA YA KUWEZA KUSAIDIANA KIUCHUMI NA KIJAMII
3.MENGINEYO
4.KUFUNGA KIKAO

AGENDA NA 1:KUFUNGUA KIKAO.


Kikao kilifunguliwa mnamo saa 12:40 jioni ,kilifunguliwa kwa kuwashukuru wajumbe wote
walioitikia wito wa kikao na kwa sala fupi .
AGENDA NA 2:KUJADILI NAMNA YA KUWEZA KUSAIDIANA KIUCHUMI NA KIJAMII.
Kutokana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazotukabili vijana wengi hapa
mtaani ,tuliamua kuanzisha kikundi kitakachosaidia kupunguza changamoto hizo.Pia wajumbe
walitoa maoni ya kuwepo kwa mchango wa kila mwezi ,kwani wanaamini kikundi hakiwezi
kujiendesha chenyewe pasi na kuwepo na michango.Tuliazimia kuwepo na mchango usiozidi
sh.3000/=.
AGENDA NA 3:MENGINEYO.
Wanakikundi waliombwa kuwahamasisha watu wenye sifa waweze kujiunga na kikundi kwani
nafasi bado zipo wazi.
AGENDA NA 4:KUFUNGA KIKAO.
Kikao kilifungwa saa 02:00 usiku kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa uvumilivu na jinsi
walivyojituma kuchangia mawazo yao kwa kila agenda.

You might also like