Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 27

MIZIGO NA JOHN RUGANDA

Taser ya “The Burdens” iliyoandikwa na ASSENY MURO

UTANGULIZI

Hali hii si ngeni kwa Wamala. Hapo awali kable ya uhuru alikwisha ya onja maisha ya namna hii
ya kushika chaki. Kwa bahati nzuri lakini siku chache kabla ya kupatikana uhuru alitoa hotuba
iliyowaathiri wasikilizaji na akajikuta amefanywa waziri. Tabu iliyoko ni kwamba mara nyingi
mtu akipanda cheo, husahau hali aliyokuwa nayo zamani na pia huwa na watu chungu nzima
walio tayari kumshangilia hadi siku ambayo mambo yakimharibikia hujikuta yupo peke yake.

Halafu hubakia kulaumu watu wengine. ni hawa Marekani na dola zao. Waliniambia kuwa
ningeweza kuwa mtu mkubwa sana lakini majuto ni mjukuu. Tume za uchunguzi zinazidi
kufanya kazi, milango ya kamba za kuzuilia watu imekuwa inafunguliwa na kufungwa. Kama
una bahati mbaya, utauawa hadharani kwa risasi.

Baada ya kuwekwa kizuizini kwa miaka kadhaa. Wamala anasamehewa na mara anadhihirikiwa
kwamba anashindwa kurudia maisha yake ya zamani yaliojaa ukiwa. amenyang ’anywa kila kitu
isipokuwa mke na watoto wake wawili tu. Hawa ndio watenzi wenzake sasa na ndio watazamaji
wake pia. Wamala sasa hawezi tena kutembea barabarani kwa fahari wala kucheka kiwaziri. sasa
anatoa amri lakini hakuna wa kuzipokea. Hisi ya madaraka na ufahari inakuwa ni kumbukumbu
za maisha ya awali kwa njozi na noto.

 watu ambapo walikwisha kuwa na maisha ya juu huona kuwa njaa, umaskini, na
kushindwa kupata mahitaji ya lazima ya familia kuwa ni fedheha kubwa. pia inaonyesha
jinsi mtu anapokosa madaraka kama wamala asmavyo bado wapo wanaharamu
wapendao vyeo na wenye nia ya kunyakua ili watajirike haraka haraka bado hawatiwi
nguvuni. Wamala anaona vigumu kukubali ukweli kuwa ameanguka na sasa anaamua
kulewa ili kuufanya moyo wake shupavu uweze kupingana na ukweli mpya wa maisha.

Mkewe, Tinka anauona ukweli wa mambo yalivyo kuliko Wamala. Hana matumaini ya
kufanikiwa tena. ili kuipatia familia yake angalau mlo, amamua kutengeneza pombe ya enguli na

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 1


kusuka mikeka. Na mara nyingine tinka anapokumba maisha ya starehe waliyokuwa nayo,
hujitahidi kumrudisha mume wake katika ukweli wa maisha ya vibandani waishiyo sasa. Zawadi
anayopata kutokana na juhudi yake ni matukano kutoka kwa Wamala. Lolote analolifanya hapati
shukrani lakini anaendelea kufanya kwa sababu ya watoto wake. “Ninawasumbukia nyinyi
wanangu” anamwelezea mwanaye, Kaija. Kaija naye anachukizwa na mateso anayoyapata
mamake. Ukweli ni kuwa Tinka ndiye kichwa cha nyumba na anajaribu kuwafanya Wamala na
watoto wake kuuona ukweli wenyewe. Mgongani kati ya Wamala na Tinka unazidi, mitego ya
ujanja wanayowawekea watoto wao ili kupata huruma kutoka kwao, mwishoni yanaonesha picha
ya jitihada ya maisha kwa watu walio nje ya nyumba yao.

Wamala na Tinka mwishoni wanatengana na jumuia jwa sababu ya siasa. walipokuwa na maisha
ya starehe, walijiona ni watu tofauti na watu wengine. kuanguka na kushindwa kwao kumejenga
ukuta mnene kati yao na watu wengine. Mashirikiano machache yaliyobakia (Wamala Wanunuzi
zake wa enguli) yanawazidisha uchungu wa kuanguka kwao. Uchungu ambao unatokana na
kukosa mali na kupungukiwa na hadhi. Huu mchezo unajaribu kuonyesha dalili na hasara ya
ugonjwa huu mpya yaani ujinga mkubwa wa kutaka makuu na kujidharau.

WAHUSIKA

WAMALA BABA

TINKA MAMA

KAIJA MWANA

NYAKAKE BINTI

Kwa mara ya kwanza mchezo huu uliigizwa Januari 1972 na kikundi cha Makonde katika Jumba
la Taifa la Michezo lililopo Kampala. Aliyeunmgoza alikuwa ni David Rubadri. Wafuatao ndio
walioshiriki:

TINKA Chrisina Nyakana

KAIJA David Kihazo

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 2


WAMALA John Kalema

NYAKAKE Rose Mbowa

ONYESHO LA KWANZA

Pazia linainuka na kuonyesha nyumba ndogo ambayo si ya kudumu na iliyojengwa kwa fito na
kukandikwa kwa udongo. Kuta za sebule (ambayo sehemu yake inatumika kama jiko)
zimepakwa samadi ya ng’ombe. Fanicha zake zimetengenezwa hapo hapo nyumbani. Kigoda
kikubwa kilichotandikwa ngozi ya simba. Ngoma ya kifalme. Mkuki na zana nyingine za
kifalme. Kuna vyombo vingine vya jikoni kwa sababu ya moshi wa kila siku vitu vyote
vimekuwa vyeusi na chumba kina giza. Nyuzi hafifu masizi zinaning’inia kutoka darini.

Tinka amekaa peke yake akisuka mkeka. Anapitisha muda? Anamngojea Wamala? uso wake
unaonyesha hali ya huzuni na uchovu wa maisha. Mtoto wake, Kaija anaingia kimya. Amevaa
kaptula ambayo imetiwa kiraka vibaya na shati la nailoni na amechukua koroboi. Anapiga
miayo. Tinka anashtuka kidogo. Kimya.

Tinka anauliza kajia kwa nini hajalala bado ingawa ni usiku na kaija anamjibu Nyakake
amefanya tena yaani Nyakake amekojoa kitandani ndiyo sababu anataka apewe kitanda chake.
Kaija anamwambia mamake kuwa Nyakake analowesha upande wake na halafu anasongelea
upande wake. Pia amechoka kuvumilia uvundo wa kila siku. Uk.2

Kaija pia anahisi njaa kupita kiasi. Tinka anamjibu na kumwambia chakula anacho kula
kinakwenda wapi? Anakula, asipokula, siku zote anaconda kama kijiti cha kuchokorea meno.
Anampa viazi na mahagwe aliyomwekea baba yake.

Kaija anamwambia Tinka kuwa anataka kitanda kwa kuwa na mwalimu anasema mvulana wa
miaka kumi nan ne anapaswa kuwa na kitanda chake peke yake ili kuvizuia vijinyoka visitambae
tambae kutoka kwa mwili wa mtu moja hadi mwingine.

Pia usiku huo, Mbwa walikuwa wakifukuzana na vivuli na Mbwa wanabweka nje. Tinka na
Kaija wanakuwa na wasiwasi kuwa majambazi wamekuja kuiba yaani Tinka anamwelezea Kaija
kuwa hivi juzi juzi majambazi wawili walimnyang’anya sanduku msichana aliyekuwa amevaa
viatu vyenye visigino virefu na miwani ya jua na ndani mwa sanduku mlikuwa na maiti. Mtoto

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 3


mchanga. Msichana yle alikuwa akienda kwa baba mtu. Mumewe alikuwa mwuzaji katika
kampuni moja ya mafuta. Umati wa watu uliokuwepo uliwaua hao wanyang ’anyi saa hiyo hiyo.
uk.4

Nyakake anakohoa mfululizo mmoja. Tinka na Kaija wanaangaliana na kusema, wana wasiwasi.
Kaija anasema kuwa mwalimu alisema inaweza kuwa ni kifua kikuu. Anafaa apelekwa kwa
daktari. Tinka anasema wangempeleka kwa daktari lakini chupa ya pombe ni bora Zaidi kwa
babake kuliko afya ya binti yake. Uk.5 akiendelea hivi atakuta maiti watatu nyumbani.

Tinka anamwuliza Kaija kuwa amemuliza babake juu ya kitanda? Pia amulize pole pole, Je,baba,
kina Mama wote huwanunulia watoto wao vitanda? Wanalipa karo za watoto wao na isitoshe
.kodi ya kichwa cha waume zao?

Kaija anamjibu na kusema kuwa baba yake anasema kuwa Tinka ndiye alisababishia kushuka
cheo? Kwamba akiwafukuza marafiki na jamaa zake na ndiyo sababu hakuwepo na mtu yeyote
wa kumsaidia wakati askari walipofika.

Tinka (kwa hasira) baba yake hawezi kulipa kodi na kununua kitanda. Wakati mwingine atasema
kuwa wewe (Kaija) ni mzigo kwake na unamwangusha chini kwa karo na kitanda. Uk.8 Kaija
anasema hana haja ya kupata kitanda na Tinka anasema ampe baba muda wa miaka mitatu.

Pia Kaija anamwomba Tinka kumkopesha shilingi mbili yaani Kaija anataka kuanza biashara ya
kuuza karanga shuleni. Kwani karanga zinafaida sana na baada ya mwezi moja au miwili
atakuwa amepata fedha za kutosha kujinunulia kitanda chake. Tinka ambaye ni mamake
anakataa na kusema itakuwaje mtoto auze karanga shuleni? Ataivunja heshima ya mamake.
Tinka atawezaje kuvumilia vicheko na dharau za wanawake wa mtaa wao wenye vibanda?
Minong’ono na masengenyo yao, umbea na huruma za kejeli. Uk.9 Tinka anamahidi kuwa atauza
mkeka anaosuka na kumnunulia kaptula mpya kabla kateba hajamfukuzaa shule na mkeka
mwingine atakaosuka atamnunulia kitanda kizuri. Uk.9

Mambo yangekuwa rahisi Zaidi kama pombe yake ya enguli ingelikuwa ikinunuliwa lakini
wanunuzi wake siku hizi wanapendelea Zaidi pombe ya waragi ya Uganda.

Tinka anamwelezea Kaija kuhusu uchoyo wa wanaume. Wakiwa nje ya nyumba ndipo kuwa na
furaha lakini nyanyake Kaija alikuwa ni mwenye huruma, mapenzi na ukarimu. Alimsimulia

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 4


Tinka hadithi za zamani: za wanaume walevi waliochomwa visu usiku wa manane na wake zao
wenye wivu, za baba wenye mapenzi waliofurahisha wana wao kwa kuwatolea tenzi za
kishujaa,za watoto wadogo waliopakatwa na kubembelezwa kuimbwa mpaka wakalala juu ya
mapaja ya mama zao. Uk 12.

Pia Tinka anamwelezea Kaija juu ya wanawake wana hila zao kama vile kusahaulisha mamako,
wana dawa wanayotumia kuwavutia wanaume. Uk. 14

Kaija anamwomba mamake (Tinka) amsimulie hadithi ya Ngoma aliyekuwa chifu na msichana
mzuri anayeitwa Nyenje. Pia wimbo (Bunduki za kucheza Ngoma) Uk. 16.

Pia hadithi ya Chifu mkuu Ngoma na bintiye wa pekee, Nyenje. Ngoma alipeleka ukumbe kote
akisema mtu yeyote anayetaka kumposa binti yake ni lazima aonyeshe ustadi wa kukwea mti
mrefu na kuteremsha kibuyu kilichokuwa na kitovu cha Nyenje, Machifu na watoto walijaribu
bahati yao lakini hawakufaulu. Wawindaji na wachugaji pia mti huo wa mvule ulikuwa mrefu
sana. Halafu akaja mwenye ukoma, kabwela, maskini na mwenye madonda yanayonuka mno.
Mwendo wake ulionyesha kwamba alikuwa mtu anayekokota taabu nyuma yake. Alitaka
kuukwea mti wa mvule.

Watu walipomwona walikimbia kwa hofu na wengine waliuokuwa wamejificha walicheka


mpaka wakatokwa na machozi na kumrushia mwenye ukoma mawe, akasema havijali vicheko
vyao, kwani vicheko ni kama mvua tu. Inanyesha na kwisha na isitoshe alisema kuwa walio
werevu huucheka ubaya na wajinga huucheka ugonjwa. Wakacheka. Ngoma alikuwa mtu wa
haki ana alimruhusu kujaribu bahati yake. Uk. 18

Mwenye ukoma alikwea mti akiimba wimbo wa kusifu Nyenje, uzuri wa Nyenje haulinganishiki.
Alitamani kama angekuwa mwezi unaong’aa kutoka juu hapo ndipo angeweza kumwona vyema
uzuri wake akioga. Kwa kweli Nyenje alikuwa na shingo ndefu kama ya korongo na ilikuwa na
mizunguko ya shanga. Meno yake yalikuwa meupe kuliko maziwa. Mwenye ukoma akawa
anaendelea kukwea juu Zaidi, mwishoni yule mwenye ukoma alikiteremsha kibuyu. Uk. 19

Sauti ya baba anasikika akishukuru mtu kwa kumsaidia kubeba kitanda. Tinka anamwambia
Kaija kwemda kulala kabla ya babake kuona miguu yake michafu na kuanza kupiga kelele sana.
Atasahau kuwa debe moja la maji ni senti kumi. Uk.19

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 5


Tinka anafungua mlango. Wamala anaingia huku akikokota kitanda cha kwendea safari. Kikuu
kuu lakini bado kina hali nzuri. Amelewa, Kwake ina maana kuwa amefurahi sana, tetemeko la
mwili wake linaonekana wazi katika hali yake ya kuyumbayumba. Wamala anamsalimu Tinka,
hakuna jawabu kutoka kwa Tinka. Wamala anasema bado ungali unasuka mkeka wako tu,
unaonekana mchawi anayetungia uongo pamoja. Uk. 20 Tinka anasema wamechoka na vitu
vikuukuu. Wamala anamjibu na kusema wacha matata Tinka, kitanda bado kina hali nzuri.

Wamala anamwita Kaija aje aone mchumba wake mpya. Kaija ambaye alikuwa akiusikiliza
ubishi wao akiwa ndani anafungua mlango taratibu na kuja kuangalia kitanda chake halafu Tinka
anamfukuza Kaija na kuufunga mlango, Kaija anakwenda kulala. Uk 22 wamala anawasha sigara
ya aina ya “Crown Bird” Tinka anarudia kusuka.

Tinka (kwa hasira) anamwuliza wamala, alikuwa wapi usiku jana? Wamala anadanganya na
kusema, ameshalipwa shilingi hamsini katika kupatikana huko. Mungu amlani yule karani wa
Halmashauri wa Uajiri wa kazi za serikali. Anasema yeye ni mpumbavu na tena ni mpinga
maendeleo na hawezi kufanya kazi katika hali ya mwamko mpya wa siasa. Kwa hiyo aliondoka
bila ya ugomvi na kwenda kupumzika kwenye bustani la Jamhuri na kuanza kufikiri.

Tinka anaendelea kumtukana na kusema bado hajajibu Swali Lake, wamala anasema kuwa Tinka
alisema kuwa akili zimemruka, wamala anamwonyesha kiberiti. Kiwanda cha kiberi kinaitwa
Associated matches kinaweka sehemu mbili za mkwaruzo juu ya kiberiti? Wamala anawasha
kiberiti kwa nguvu, anawasha sigara na kukitupa kijiti.

Wamala anamwambia Tinka kuwa ni kasumba ya kibepari. Biashara kubwa, nyumba kubwa na
wanawake wanene. Pia anamwelezea Tinka namna ambayo amenda kwa Mkurungezi
Msimamizi na pendekezo la kuanzisha kiwanda cha viberiti na karani msichana ambaye si raia
wa hapa (nchi geni) akamfukuza baada ya kuyaangalia matambara ya Wamala, akavuta dawati
lake na kutoa tangazo lililoandikwa “Hakuna kazi”, mkurungezi mismamizi anashughuli nyingo
ingawa Mkurungezi alikuwemo ndani na hana kazi maalumu. Wamala anamwambia msichana
huyo kuwa hana haja ya kazi. Akamwambia kuwa anamsumbua na walinzi wakamtolea nje. Uk.
27 Pendekezo la maskiniu kukataliwa (Wamala).

Wamala anaeleza juu ya maisha ya famila yake (umasikin), wanaamka alfajiri mbichi, chai kavu,
viazi baridi na maharagwa. Harufu ya kali ya moshi na mkojo kutoka kwa umande kwani maji ni

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 6


ghali na hawana hata tone ndani ya nyumba. Kaija anakwenda shule. Baridi ya asubuhi
inagonganisha meno na kuchoma matako yake yaliyo wazi. Kake anafukuzana na vipepeo au
kuzungukazunguka kimya nje ya nyumba kwa sababu hawana lolote la kuzungumza.

Pia saa nne akifika, Tinka anaanza shughuli za kusuka mikeka na kutayarisha madebe na mianzi
ya kutengenezea pombe ya enguli. Anasoma gazeti na kupekua kurasa zinazotangaza nafasi za
kazi, anapoona moja inayomfaa ana tatizo la kupata wadhamini watatu yaani anaoshirikiana nao
na walevi wa Baa ya Jamburi.

Saa ya chakula cha mchana ni viazi na maharagwe, mara nyingi kaunga na dodo. Jioni anaenda
ulevini ili kusahau matatizo. Akirudi nyumbani ni kimya na wasio na matumaini. Chumbani
kulala, na hakufuatwa na Tinka (mkewe) alfajiri nyingine, siku ingia siku toka. Uk. 28

Tinka bado anaulizia Wamala alipolala usiku jana. Binti yao bado hajapelekwa kwa daktari.
Wamala alikuwa amabaki na shilingi hamsini. Shilingi kumi akazitumia kununua kitanda, kumi
akatia kiu yake (ulevi), amebaki na thelathini.

Wamala akimhonga Tinka, anasema wagawanye na achukue kumi na tano. Tinka anakubali
lakini anashauku ukarimu wa ghafla. Uk. 30

Pia wamala anamwelezea Tinka juu ya S.M.K (shirika la matangazo la mataifa), kwamba
ataanza kuuza matangazo kuvumisha bidhaa. Kwa mfano Waragi huyashawishi mapaja, kunywa
vat uwe mwanamume, rex na ngono kwa mwanamume mwenye matatmanio Uk. 30 yaani
amechoka na kudharauliwa na wazungu na wazungu kutushawishi kuvitumia kwa mfano,
magari, sigara, vinywaji, manukato, karatasi za chooni, dawa, nk.

Wamala anamwomba Tinka ampe nusu chupa ya enguli kwa kuwa watu wanaisifu kuwa nzuri
kupita zote zinazouzwa vibandani.

Wamala anamwelezea Tinka kuhusu mheshimiwa Vincent. Vincent anakuja katika Baa ya
Jamhuri na kuwanunuli watu pombe yaani anataka kupigania ubunge uchaguzi ujao. Ana umri
wa sitini. Alikuwa chifu wa Saza kabla hajastaafu. Sasa ni mlevi na mwindaji wa wanawake
kama Wamala. Ana wake wane, binti kumi na wawili na kila mmoja ameolewa.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 7


Pia Vincent anawaambia watu na kusema atatilia mkazo kwenye ujenzi wa mashule, kujenga
barabara na zahanati, elimu ya bure, matibabu ya bure na wasiokuwa na kazi kupata kazi na
kupata malipo ya kuwasaidia kila mwezi. Uk 32

Wamala anataka amfundishe mzee Vincent jinsi ya kufanya kampeni yake. Uk. 32. Wamala
anamwelezea Tinka namna alivyomtoa nje Mzee Vincent na kumwambia kuwa watu
wamechoishwa na maneno matupu, ahadi nyingi na hotuba ndefu. Wanachohitaji ni maneno
machache tu ya kuwavutia na kuwateka. Kupiga makelele hakufai kitu. Wamala akamwambia
Vincent angeanza kutumia maneno kama: Mchague shujaa, mchague anayefaa, mchague
Vincent. Alipoyajaribu maneno hayo huko Baa la Jamhuri yalifanya kazi na watu wote
waliyashangilia kwa kupiga kofi na kuyaimba mchague shujaa, mchague anayefaa, mchague
Vincent. Uk. 33

Tinka anasema ni shauri ya hiyo pombe aliyowapa. Wamala alipata shilingi hamsini na ataonana
naye kesho ili kushauriana naye juu ya shirika hilo. Tinka kwa kejeli hongera kwa kupata kazi ya
heshima kama hiyo. Wamala anasema kwa tatanishi kuwa hakuna kitu cha kusheshimka. Anaona
anaubongo wa kutoa madondoo ya kudondoleka yaani hana sababu ya kukejeli. Yeye (Wamala)
ana akili. Pia wamala anasema Tinka ni mwanamke mharibifu sana na ni mzigo mkubwa.

Wamala anaanzisha ugomvi kwa kuwa Tinka hana shukrani ataanza kumtoza kodi ya uuzaji wa
pombe kwa kuwa nyumba si ya kupikia pombe wala si baa. Anaweza kumtoza leseni ya biashara
na leseni ya pombe. Uk. 34 wamala anaendelea na kusema pengine atamwelezea chifu kuwa mke
wake (Tinka) anapika na kuuza enguli kwa njia isiyo halali ndani ya nyumba yake. Adhabu ni
atapata kifungo cha miezi sita na faini ya shilling mia tano. Viboko kumi na wiwili kila siku.
Vitaondoa ukaidi wake.

Baada ya ujanja wote kushindwa, Wamala anaamua kutumia nguvu. Anaingia ndani ya chumba
cha kulala kutafuta hiyo pombe. Tinka ana wasiwasi kwa sababu ameificha pombe yake mahali
ambapo anaona ni pa salama. Wamala anarudi amejawa na hasira.

Wamala na Tinka wanashikana. Tinka anamtukana na kumpiga makofi yasiyo na nguvu. Tinka
ana mwita nguruwe we! Kupe we! Mjinga! Kicheche! Nungu! Tinkae anamsukuma na kumvuta
wamala huku na kule. Tinake anangukia ngoma, anaangua kilio, mshindo mkubwa unasikikika

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 8


wakati kyanzi, vyombo vya jikoni, mkuki na vinginevyo vinaanguka na kutawanyika. Tinka
ameumia kiko cha mkono.

Wamala anaketi na anakunywa pombe iliyomo akitumia chupa. Tinka anajizoazoa,


anamwangalia wamala kwa chuki. Anathema mate na anajipiga kofi pajani kwa kiburi na
anajiandaa kuondoka. Wamala anamvurumiza kiatu na kinampata mgongoni. Tinka anarudia
kuketi na kulia. Uk. 37

Wamala anamwambia Tinka kuwa ndiye aliyemcokoza kwa kuwa alitaka pombe kidogo tu tana
kwa fedhe yake. Pia Tinka hangemetendea kama alivyo tenda yaani mwanamume anataka apewe
heshima japo kidogo tu ya kumfanyaajione kuwa ni bwana katika nyumba yake mwenyewe na
wala si kama kirado cha mlango cha kudutia viatu vya kila mbwa anayeingia. Mwanamume
hafanyiwi hivyo, akiwa masikini au si maskini. Uk. 38 damu inatirika kwa wingi. Ngojea
nikatafute bendeji nikufunge dawa.

Tinka anasema ngumi, Vita, njaa, chuki, umaskini na kulala peke yake bila ya mume hawezi
kuvumilia tena.

Kaija anamshwa na kelele zao. Aanchungulia mlangoni.

Wamala anasmea utando wa buibui utafaa. Ulikuwa ukitumika sana kabla ya kuja kwa
mahospitali. Ulimwengu unaotuzunguka umejaa mateso. Hauna huruma, unavunjavunja mtu.
Kila mmoja anakuamuru uinamishe kichwa unapokwenda. Hawataki uinue kichwa, wanaweza
kukuvunja kama maisha yako mikononi mwao. Wakipenda wanaweza kukuvunja kama kijiti
kikavu na hilo wanalitenda kila siku kwa sababu kunawapa wajione wana nguvu. Wanataka uone
kuwa sasa wana madaraka na wanaweza kukukalia kichwani na wewe uwe chini ya matako yao
bila ya kupata hewa. Kwa hivyo, mtu anporudi nyumbani kutoka kwenye jahanamu hii, huu
ulimwengu wa mafirauni wapendao vyeo, wenye mikono ya kupokonya haki za watu yaani
mikono iliyo na tama ya kunyang’anya ili kujitajirisha haraka wenyewe. Mtu anahitaji ruma na
kuangaliwa vizuri. Wala siyo kusundungwa na matusi. Uk. 39

Wamala anona Kaija mlangoni, nini Kaija? Kaija matata yoyote baba? Wamala anamjibu,
hakuna mwanangu. Kila kitu sawa.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 9


Kaija anainagalia bendeji aliyofungwa mama yake. N kuuliza mama afanyaje kwenye kiko?
Kimefungwa. Wamala anamjibu kuwa mama alijikwaa kwenye ngoma. Kaija kiatu chako kimoja
hapa baba, pole mama. Tinka anasema atapoa na sijambo kubwa ni ajali ndogo tu.

Kaija usirudie baba, inauma, Wamala anamnyamazisha na kumwambia aenda alale. Kaija
anatoka Ahsante kwa kitanda ulichoniletea.

Baadaye Tinka anamkumbusha maisha mazuri waliokuwa nayo. Kaija aliuwa mdogo, Kage
alikuwa hajazaliwa na ndiye annyeteseka. Wamala anamoa onje kidogo pombe, Tinka anakataa
wamala anasema kuwa pombe ni kitu cha mwisho kupigwa maruduku katika nchi yao kwa
sababi wakipiga marufu unywaji pombe na hata kunywa kupita kiasi, wanaohusika wangepigwa
risasi na kutiwa moto au kuchoma majumba ya serikali. Tunajenga taifa la walevi na wapendaji
fahari wanaojishaua kwa unafiki mbele ya viongozi.

Wamala anamkumbusha Tinka, Nyakati zile za furaha, kwa fano mazungumzo yote yale ya
Mtakatifu Mama mkubwa na moto wa jahanamu aliyafahamu kuwa ni kisingizio tu, kwenye
ngazi za kanisa, kwenye sakafu baridi, kwenye makaburi, sauti nyororo ziwaamsha wafu.
Alifurahia kila nukta waliokuwa pamoja. Uk 41

Tinka anasema tunda lilokatazwa lile lililowaletea adamu na hawa kufukuzwa kwenye bustani ya
edeni. Wamala anasema jambo la kustaajabisha kuona kuwa mischana mdogo kama Tinka
aliyejitolea mtawa kwenye umri wa miaka kumi na sita hakua Bikiria Maria.

Tinka anasema alipokuwa na miaka kumi na mitano kwenye shamba la ndizi baada ya mazishi
ya mama yake, Sam alimwambia kuwa kitendo hicho kingemsahaulisha huzuni za kifo cha
mama. Uk. 42

Wamala anasema, watawa, mapadre na waongodu walikusanyika kunipinga. Wakasema chama


chetu ni cha komunisti. Wakomunisti watakaonajisi watawa na kuyafanya makanisa kuwa
mahali pa kufanyia uchafu na kucheza Kamari. Babake Tinka alikuwa mbele sana katika ukristo.

Tinka anasema maskini baba! Ng’ombe aliokupa kuchinja baada ya mikutano ya siasa. Wamala,
inashukuru sana. Walinisaidia sana kushinda katika uchaguzi na kupata kura nyingi. Mungu
amweke mzee mahali pema.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 10


Wamala alimwoa mtawa wao waliomwamini sana, tena binti pekee wa chifu mashuhuri wa
kikatoliki. Ilikuwa kazi nzuri ya kisiasa. Alitafuna mkate wa sakramenti hata mfupa ungetoka
damu. Alifanya sherehe kubwa ya kupendeza, bendi ya polisi ikitumbuiza, wiskina divai kwa
kila mtu na macho ya wanawake yakiona wivu. Wanaumewakiwakodolea macho wanawake na
Askofu anatazama pembeni. Uk. 45

Wamala anasema, Unafiki wa watu, walitupigia magoti tuwape vyeo vya ukurungezi. Uk 45

Wamala pia anamkumbusha Tinka namna walivyoagiza vitu kutoka kwa duka kubwa la bidhaa
kwa kupiga simu. Shughuli za biashara zikafanywa huko hoteli ya “inter continenyal ” kwenye
kuseti nywele zangu akija hapo, wakuu wa benki wakija kwenye chumba cha wamala cha
kusomea. Ndugu na rafiki wakiwazukia kila mara na wamala akimwambia Tinka kuwa
akiwafukuza siku zote. Uk. 45

Tinka anamwelezea kuwa akienda kwenye Ikulu walinzi watamfukuzia mbali, akimpigia simu
itakatwa na karani mmarekani na akiandika barua, itatupwa kwenye kikapu cha taka. Wamala
anasema limi, tutaendelea kubeba dhambi za watu weupe? (ukoloni) Mungu wangu! Lini
tutajiheshimu na kujiongoza wenyewe? Inasikitisha. Uk. 47

Wamala anasema takunywa bilauri nyingine moja halafu alale. Wamala anamaliza pombe.
Wanakwenda kulala wakiwa wameshikana mikono.

ONYESHO LA YA PILI

Siku ya pili, mchana, maweko ya vitu ni yale yale. Kitanda cha safari bado kinglimo chumbani.
Kwenye pembe nyingine ya chumba kunaonekana madebe, mitungi ya maji, chupa, madumu na
magazeti ya zamani. Tinka anajiandaa kutengeneza enguli. Wakati pazia inapofunguliwa, Tinka
anatafuta kitu humo chumbani. Wamala anaingia amechukua kifurushi. Kwa mshangao,
anaangalia vifaa vya Tinak vya kutengenezea pombe.

Wamala anasmwambia Tinka, kumbuka polisi, Tinka, Polisi. Miezi sita ndani, faini kubwa.
Tinka kwa matumaini, Robo ya chupa tu watarudi kwenye kituo chao.

Baadaye Tinka anapotelea kwa chumba cha watoto. Wamala anafungua kile kifurushi, suti
nyeusi, shati jeupe, tai na viatu vyeusi na soksi. Anavua matambara yake na anazivaa nguo
mpya. Mtu mwingione sasa . maridadi kabisa. Tinka anarudi na mwanzi.
P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 11
Tinka anatia chumvi yaani watu wakikutana na Wamala njiani aliyasema kuwa mavazi ya
kuazima haya zinaonekana kwamba zilipimwa maksudi. Wamala na mwalimu umbo sawa.
Tinka anamwambia amependeza mno, badiliko la umbo na watu watadhania kuwa ni waziri.

Baada ya kusifiwa, wamala anazunguka ndani ya chumba akiigiza mwendo wa kiwaziri kwa
mbwembwe, mkono mmoja ndani ya mfuko wa suruali na mwingine unakitingisha kidude cha
funguo asichokuwa nacho.

Wamala anaigiza namna atakavyokutana na bwana kanagonago Vincent. Uk. 56 wamala ni


mvutaji wa sigara ya aina ya “crown bird”, chupa ya wiski anayoletewa na Tinka. Anaonekana
kabisa kama Vincent katili na mwenye majivuno. Tinka na wamala wakiendeleza kujifanya
kama wamakutana na bwana Vincent. Wamala anasema, Halmashauri ya Jiji ifikirie kuhara,
mafuriko, uchafu, vijishonde na nzi. Uk. 60

Wamala anasema amemwendea Bwana Vincent, jambo la kwanaza ni la siasa (mchague shujaa,
anayefaa ni Vincent), la pili ni la kiwanda cha viberiti. Tinka akifanya kama Vincent. Nieleze
elimu na maarifa yako.

Wamala ni mwalimu wa gredi ya tatu, anafundisha kiingereza na elimu ya raia kwa miaka kumi.
Pia akawa mkuu wa chuo cha ualimu kwa miaka mitatu na alikuwa waziri wa kazi kwa miaka
miwili katika serikali ya mitaa. Lakini sasa kazi yake ni kufikiri.

Wamala anamwelezea kuwa anataka kuanzisha viberiti ambavyo njiti zake zina baruti pande zote
mbili. Unawasha kijiti kimoja kasha unakiweke ili ukitumie wakati mwingine. Na italeta
mamilioni. Wamala anataka yeye na Vincent Kanagonago washirikiane katiak biashara ya
viberiti vya ncha mbili.

Baadaye Tinka anamwelekeza bastola, toka kabla sijakupiga risasi. Kabla sijaita polisi.
Uondoke.toka au nitakupiga risasi. Uk.67 wamala anamfunulia kifu, haya basi nipige risasi.
Wamala anamsongelea Tinka, nimekuja kunywa wiski yako au sivyo? Hilo tu laweza kukupa
haki ya kunipiga risasi na nimeketi kwa kiti chako cha kunenepa. Fyatua risasi mnyonyaji riasai
wee!

Wamala anamvamia Tinka kwa ghafla, anamnyanganya ile bastola na kuitupa chini. Halafu
anamshika shingp na hapo panatokea mapigo makali. Anamkaba Zaidi, macho ya Tinka

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 12


yanatokeza nje na anatupatupa mikono ovyo. Wamala anakaba Zaidi.wanapigana. Pia wamala
anasema atampiga hadi macho ya Tinka yatoke nje kama ya chura. Kutoka nje kunasikika mlio
wa mabuti ya polisi. Mlio huu unasikika hadi Kaija kutoka shule.

Wamala anajaribu kuisogelea bastola, Tinka anamwambia wamala, asiinue mguu, vidole viko
tayari kufyatua risasi, usiwe na haja ya kuwa na haraka ya mwisho wako, omba Mungu, wamala,
akusamehe madhambi yako. Unayakumbuka maovu yako uliyofanyia Mungu? Uk. 70 wamala
anamrukia Tinka na kumtuma kama kinga yake anapokwenda kuiokota ile bastola. Wanaelekea
mlangoni. Wamala anamwambia Tinka waambie nitakupiga risasi. Nitafyatua risasi, nitakufa na
mmoja wao. Uk. 71

Kaija anaingia kutoka shule mabuti yanasikika kutoka nje. Kwa haraka, baba baba unafanya
nini? ni mimi, tafadhali. Wamala anasema lazima nife na moja wao haki ya Mungu.

Kaija anajidhihirisha kwa kushtuka, wamala anamtambua Kaija. Wamala anaona aibu sana na
anaketi, kichwa kikiwa kati ya magoti bila ya kufahamu la kufanya. Tinka anaangua kicheko.
Mambo yamerudi kama kawaida.

ONYESHO LA TATU

Siku impeita. kesho yake asubuhi na mapema. mpango wa vitu ni ule ule isipokuwa ile ngoma ya
kifalme, ile ngozi ya simba, kigoda na vitu vyote vya kifalme bimeondolewa. vyombo vya Tinka
vya kutengeneza pombe, vimeondolewa. Kile kitanda cha Kaija bado kipo.

Kaija anaingia amevaa kaptual tu na shati amelishika mkononi. Anaonekana amechoka,


anakwenda miayo, ananyoosha mikono. Tinka ambaye pia anaonekana amechoka, anafundasha
vitu vyovyote tu.

Kaija shikamoo mama. Tinka, marahaba Kaija (bila kuinua uso) Kaija anavaa shati yake na
kuuliza akiwa baba yake bado hajaamka. Tinka anashtushwa na swali hilo, anainua macho
kumtazama.

Kaija anamwambia Tinka kuwa aliota ndoto mbaya sana. Pia anauliza juu ya babake na Tinka
anamjibu kuwa ametoka. Ameamka mapema na Kaija amekuwa katika usingizi mzito na
hangeweza kumsikia.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 13


Tinka anakunja nguo zake na kuzipanga ndani ya sanduku la mbao. Kaija anauliza akiwa babake
alirudi siku ya jana. Tinka anamjibu kuwa alirudi akiwa amelewa sana lakini sasa ametoka.
Tinka anamwomba mama maji ya kunawa uso. Kaija anaingia ndani kuchukua beseni na mswaki
wa mti.

Tinka (anajiambia mwenyewe) Nitamwomba mwalimu auze baadhi ya vitu vyetu na achukue
hizo dedha kuwa malipo ya suti yake tuliyoichana.

Kaija anasema ilkuwa balaa. Ile ndoto mara mbili kwa usiku moja. Unafahamu Mama, mimi
sipendi jinsi anavyokupiga. Kama ataendelea kukupiga siku moja siku moja tutatianan mikononi.
Tinka anasema huu ni mchezo wa wazazi wake na babake hatarudia tena. Kaija anaendelea na
kusema pia na wapiti njia wakiwashangilia ili kuwashawishi muendelee kupigana. Mungeuana
bure na wanafunzi wenzake walikuwepo wakishuhudia wakinianglia kwa macho ya huruma.
Alijaribu kuwaamua lakini babake akampiga kofi. Uk. 76

Kaija anamwambia Tinka kuwa wakati yeye na babake walipokuwa wakipigana, Kaija aliondoka
na akawa anazurura ovyo. Akamwona kaboga analima kwenye shamba lake Kwani yeye awe
akilima wakati baba na Mama walikuwa wanakwaruzana kama chui huku wakiwa
wamezungukwa na watu waliokuwa wakicheka na kushangilia? Kaboga alipomwona alimuliza,
Je, Mwanngu wameacha kupigana? Kaija aliokota mawe machache na kuyatia mfukoni mwake.
Akakipiga kichwa kwa manati yake, kichwa kilijaa mvi. Nusura jiwe limpige sikoni. aliianama
na kupiga mayowe, nisaidieni! Nisaidieni! Huku akikimbia ili kuokoa maisha yake. Kuona vile
nilimaliza hasira zangu kwenye kung’oa miche ya pamba. Uk 78

Baada ya kung’oa miche ya Kaboga, alikutana na Tibasaga na kumwambia kuwa amemwona


aking’oa miche ya pamba yam mzee Kaboga lakini kabla hujaondoka mitakupiga vibaya sana
yaani nitamwambia mamako. Kwa hivyo, Kaija alimrukia na kumpiga kweli kweli na kumvunjia
mtungi wake. akafarijika Uk. 79

Kaija anamwambia Tinka, aliposikia sauti ya mama ya tibasaga alikimbia. Alipita njia ya
Jamburi karibu na bwawa la kuongelea na hakuweko mtu yeyote. Akajitazama majini, nikaona
mtu mwenye nguvu, akakunja ngumi na kupiga hewani, maji yalikuwa yametulia kabisa.
Akatamani kukojoa kwenye maji yaliyotulia lakini hakutoa hata tone maji. Akajitahidi tena kwa
nguvu hapo kukatoka tone moja tu, kule kutulia kwa maji kukaharibiwa na viwimbi vikawa

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 14


vinatoka upande wake. Moyo wake uliburudika kwa muda mfupo. Akaona mama na baba ndani
ya bwawa wakipigana kama vichaa, nyuso zao zikaonekana, mikunjo na midomo iliwa wazi
ikitoa damu. Uk. 79

Pia Kaija akapiga kelele, Msaada! Msaada! Kabla Kaija hajakimbia, Babake alikwisha fika
karibu naye na kumuliza kwa nini unpaiga kelele? Babake akamwambia kuwa asiogope na arudi
nyumbani. Asione aibu kwa kuwa bake ni mlevi.

Kaija anamwuliza mamake wakiwa walipigana tena, yaani Babake alimdharau na kumiita
Mbwa. Pia alikuwa na wanawake wengine wakamstarehesha kuliko yeye. Uk. 80

Kaija anamwambia Tinka kuwa aliota ndoto ya Gharika. Damu ikichuruzika matone madogo
yakanyonywa na kusihia kwenye udongo. matone yakaongezeka mpaka ile vumbi haikuweza
kuyanyonya tena. Kukatokea kitu kama kijito kisha kikawa mto na hatimaye gharika. Uk. 81

Kaija, kuna giza na nipo peke ndani ya nyumba, nikigaagaa sina usingizi. halafu kukatokea
mkoromo kama wa fahali afanyaye matata wakati wa kuchinjwa. Mkoromo unasikika kwa
mbali, mara nikasikia vishindo vya miguu vikikanyaga vyombo vya jikoni. Kuna mtu ndani ya
nyumba, kuna umbo la kivuli kisichoonekana vizuri nilijisikia kuwa sijiwezi kama vile macho
maovu na mikono yeney nguvu kushambulia. Wakati niko kitandani nimeganda. sina nguvu. Ile
miguu sasa inanijia. Kwanza niliona ncha za vidole vya miguu vikinfuatia kwa siri na kwa
kutisha halafu nikaiona skati, sikati yenyewe kama ninaifahamu lakini mtu hawezi kuwa na
hakika kwa sababu ya kutokuwepo na mwanga wa kutosha. Kifua cha kivuli hiki kinainama
nayaona maziwa yakichezacheza kwa hasira. Kisha shingo nyembamba, mdomo mdogo, pua
iliyochongoka nay ale macho ni Tibasaga. Lakini anakuja kwa hasira na chuki? Kwa nini
amechukua jambia? Uk. 82

Kaija, pia mkoromo kutoka kwenye nafsi yake. Kile kivuli kinakimbia na anabaki peke yake kati
ya kidimbwi cha damu. Kumetapakaa damu. Hii nyumba inabomoka kwa damu. hivi kumetokea
mauaji ya watu wengi. Kuna damu nying. Gharika inaibomoa nyumba na mafuriko yanatririka
kwa kasi juu ya kilima kuelekea mabondeni. kila mtu anaogopa. Watu wanakimbia na gharika
inaendelea kuwazamisha. Wote wanazama na kunabaki bahari ya damu. Ninazama, ninazaama.
Nisaidie! Nisaidie! Maafa! Maafa! (ndoto ya Kaija) Uk. 82

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 15


Kaija anaaza kunywa uji wake bila ya furaha. Baada ya mude Tinka anarudi akiwa amebeba
Nyakake. anamlaza juu ya kitanda na anamfunika blanketi. Tinka anaaza kuiondoa fenicha na
kuzipeleka chumabni kwake.

Nyakake anauliza juu ya babake na Tinka kumwambia kuwa amekwenda kuhudhuria mazishi ya
rafiki yake moja.

Tinka anawambia watoto wake kuwa jana usiku hakulala vizuri kwa kuwa anamengi anayofikiria
na fikra nyingi humfanya mtu kuwa mzee upesi.

Tinka anawambia pia lazima wahame mahali pengine. tuondoke hapo nyumbani. Haya
mtayaelewa mtakapokuwa watu wazima. Nyakake anasema yeye hawezi kuondoka bila ya baba.
Uk 87

Kaija anaingia chumbani na kurudi na vitabu, nguo nk anauliza Tinka ikiwa anaweza kuchukua
kitanda chake na mamake anamwambia kuwa atapata kitanda kingine.

Tinka anasema anataka Amani na amevumilia tabu za aina nyingi. Pia wapenzi wake
watawahurumieni, watawatunzeni vizuri huko wanakolelewa yatima. ikiwezekana atakuwa akija
kuwatazameni.

Nyakake bado anauliza juu ya babake na Tinka kumjibu kwa amekwenda kwenye mazishi na
hatutamwona tena. Amewatupa mkono.

Kaija anasikia sauti ya king’ora ya gari la polisi na kuogopa kuwa wamekuja kumkamata.

Tinka anawakumbatia watoto wake pamoja. Tinka anamwambia Kaija kuwa polisi hawakuja
kumchukua. Daima mkumbuke kuwa halikuwa kosa langu. anaanza kulia kwa nguvu. Ukweli
ulipoanza kudhiri kwa watoto, wote wanajikunyata mahali pamoja.

MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA YA MIZIGO

1. Umaskini:

 Samadi ya Ng’ombe katika kuta za sebule ya nyumba ya wamala. Uk. 1

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 16


 Kaija hana kitanda na hata wanafunzi wenzake shuleni wana vitanda na mwalimu wao
alisema kuwa mvulana wa miaka kumi na mine anapaswa kuwa na kitanda chake peke
ili kuvizuia vijinyoka vitambaetambae kutoka kwa mwili wa mtu mmoja hadi
mwingine. Uk. 4

 Wezi hawana cha kuiba nyumbani mwa wamala labda matambara na nyuzi za masizi.

 Kaija aliuza ngoma ya kifalme na taji kwa watalii ilia pate pesa za daktari aliyetibu
Nyakake na Karo ya shule yake ili mwalimu mkuu asimfukuze shuleni. Uk. 76

 Wamala ni maskini. Kwa mfano anavaa matambara. Anavaa matambara na kwenda kwa
mkurungezi msimamizi na msichana ambaye ni sekretari wake. Anamdharau baada ya
kuangalia matambara yake na kutoa tangazo liloandikwa “Hakuna kazi ” na kumwambia
kuwa mkurungezi anashghuli nyingi na walinzi wakamtolea nje.

 Kaija ni maskini. anavaa kaptula ambayo imetiwa kiraka vibaya vibaya na shati la
aniloni.

2. Ulevi:

 Wamala ni mlevi. Tinka anasema chupa ya pombe ni Bora Zaidi kwa Wamala kuliko
afya ya binti yake (Nyakake).

 Tinka anatengeneza pombe (enguli) lakini wanunuzi wake siku hizi wanapenda pombe
ya waragi ya Uganda. Uk. 9

 Pia Wamala alikunywa pombe ya aina ya enguli ambayo Tinka anatengeneza. Wamala
na Tinka wanavutanan na kupigana baada ya kunywa chupa ye enguli. Uk. 36

3. Elimu:

 Kaija anasoma shuleni. Mamake anauza mikeka na kummnunlia kaptula mpya kabla ya
mwalimu mkuu kateba hajamfukuza shuleni. Uk. 9

 Wamala ni mwalimu wa gredi ya tatu. Anafundisha Kiingereza na elimu ya uraia. Uk. 61

 Wamala alifanya kazi kama mkuu wa chuo cha ualimu kwa miaka mitatau na waziri wa
kazi kwa miaka miwili katika serikali ya mitaa.
P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 17
 Kaija anasoma shule ya msingi. Amelipa karo ya muhula wa tatu na mitihani ya mwisho
wa muhula unakaribia. Uk. 76

4. Uasherati au Umalaya:

 Wamala ni msherati. Wamala ana wanawake wengine ndiyo sababu Tinka anahama
nyumbani.

 Mischana mmoja katika kituo cha basi aliyekuwa amevaa vitau viredu vyenye visigino
virefu na miwani ya jua, wajambazi wawili walimnyanganya sanduku, ndani mwa
sanduku kulikuwa matiti ya mtoto mchanga alikuwa anampeleka matiti kwa baba mtu.
Alisema alikuwa ni mwuzaji katika kampuni ya mafuta.

 Tinka alipoteza ubikira wake katika shamba la ndizi na sam baada ya mazishi ya
mamake kwa kuwa sam alimdanganya kuwa kitendo hicho kingemsahaulisha huzuni
alizokuwa nazo.

5. Mabadiliko:

 Wamala ni waziri wa kazi katika serikali ya mitaa, familia ya Wamala walikuwa


wakitumia simu kuagiza vitu kutoka dukua kubwa la bidhaa, shughuli za biashara
zilifanywa katika hoteli ya intercontinental, mwenye kuseti nywele za Tinka angekuja
nyumbani, wakuu wa benki wakija kwa chumba chake cha Wamala cha kusomea, Ndugu
na rafiki wakiwatembelea mara kwa mar auk. 45 lakini sasa ni maskini hayo yote ni
ndoto.

 Wamala anabadilika kiumbo baada ya kuvaa suti nyeusi. shati jeupe, tai na viatu na soksi
baada ya kuazima mwalimu. Anavua matambara yake na kuvaa ngua mpya. Uk 50

 Kaija, maisha yanabadilika baada ya kupata kitanda chake.

 Tinka, maisha yake yanabadilika baada ya kuacha Wamala.

 Wamala maisha yake yanabadilika baada ya kuachwa na Tinka.

 Wamala ni maskini baada ya kufutwa kazi ya waziri.

6. Unyanyasaji au Ukatili:
P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 18
 Wamala na Tinka wanapigana, kukabana shingo. Uk. 68

 Kaija aliokota mawe machache na kuyatia mfukoni na akakipiga kichwa cha manati
yake, nusura jiwe limpige sikioni mzee Kaboga. Mzee aliinama na kupiga mayowe,
anakimbia na kuokoa maisha. Uk. 78

 Pia Kaija ni mwenye Hasira, mpotovu wa adabu. Anamrukia Tibasaga na kumpiga kweli
kwli na kumvunjia mtungi wake baada ya kumakuta na kumwona aking ’oa miche ya
Pamaba ya Kaboga. Uk. 78

7. Ndoa na mapenzi:

 Wamala alioa mtawa binti pekee wa chifu mashuhuri wa kikatoliki. Alifanya sherehe
kubwa nay a kupendeza, bendi ya Polisi ilitumbuiza. Uk. 44 (Wamala na Tinka)

 Mapenzi ya Mama kwa watoto. Tinka anawapenda watoto wake kaija na Nyakake.

 Mapenzi ya watoto kwa wazazi. Kwa mfano Nyakake anampenda babake.

8. Siasa:

 Kampeni za Vincent. Kwa mfano mchague shujaa, mchague anayefaa, mchague Vincent.

 Mzee Vicent anatoa ahadi. Nitatilia mkazo ujenzi wa mashule, kujenga barabara na
zahanati, elimy ya bure, matibabu ya bure, wasiokuwa na kazi kupata kazi. Uk. 32

 Wamala ni waziri. Alitoa hotuba iliyowaathiri wasikilizaji na akapewa au kufanywa


waziri.

9. Wizi:

 Majambazi waliiba mbuzi ya bwana Rayonga na redio mpya.

 Pia wajambazi wawili walinyanganya sanduku ya msichana mmoja katika kituo cha basi
aliyekuwa amevaa viatu viredu vyenye visigino viredu na miwani ya jua, ndani mwa

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 19


sanduku kulikuwa maiti ya mtoto mchanga alikuwa anampeleka maiti kwa baba mtu.
Alisema allikuwa ni mwuzaji katika kampuni ya mafuta.

10. Ufisadi:

 Wamala alipewa pesa (hongo) na wamerika yaani alikuwa waziri wa kazi wa serikali ya
mitaa. anafungwa jela au kizuizini kwa mika kadhaa. Anasamehewa na kufukuzwa
serikali na kupoteza kazi.

11. Uongozi mbaya:

 Wasomi wanalalamika kwa sababu fedha za serikali zinatumiwa ovyo huku


wakishindana kwa kulewa wiski na divai na baada ya uhuru walikuwa na midomo ya
kulaumu mafanikio yaw a matajiri ay wakurungezi wakiwapigia magoti ili wawape vyeo
vya ukurungezi.

12. Njaa:

 Kaija ana njaa. Anapiga miayo na kuuliza mamake chakula. Chakula ni uji siku nzima.

SIFA / HULKA / TAWASIFU / UMUHIMU WA WAHUSIKA KATIKA TAMTHLIA YA


MIZIGO

1. WAMALA

 Ni mumwe Tinka.

 Ni baba yao Kaija na Nyakake.

 Ni mwenye mapenzi. Anampenda Tinka na watoto wake.

 Ni mlevi. Anaenda ulevi katika baa ya Jamhuri kujiunga marafiki zake na kunywa
pombe.

 Ni Msherati. Anafanya mapenzi na wanawake wengine katika baa la Jamhuri ndiyo


sababu Tinka anahamia pahali pengine au kumacha.

 Ni mvutaji wa sigara ya aina ya “Crown bird”.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 20


 Ni maskini. Kwa mfano anavaa matambara. Anavaa matambara na kwenda kwa
mkurungezi msimamizi na msichana ambaye ni sekretari wake. Anamdharau baada ya
kuangalia matambara yake na kutoa tangazo liloandikwa “Hakuna kazi ” na kumwambia
kuwa mkurungezi anashghuli nyingi na walinzi wakamtolea nje.

 Wamala ni mwalimu wa gredi ya tatu. Anafundisha kiingereza na elimu ya uraia. Uk. 61

 Wamala alifanya kazi kama mkuu wa chuo cha ualimu kwa miaka mitatu na waziri wa
kazi kwa miaka miwili katika serikali ya mitaa.

 Wamala pia ni kiongozi. Kwa mfano wamala alifanya kazi kama mkuu wa chuo cha
ualimu kwa miaka mitatu na waziri wa kazi kwa miaka miwili katika serikali ya mitaa.

 Ni mwenye tamaa ya kuanzisha kiwanda cha viberiti. Kwani yeye na Bwana Kanagonago
Vincent wanataka waanzishe kiwanda cha viberiti ambavyo vinaweza kuwaka hata juu ya
sehemu zenye maji. Viberiti ambavyo njiti zake zina baruti pande zote mbili. unawasha
kijiti kimoja kisha unakiweka ili ukitumie wakati mwingine. Uk. 62

 Ni mfisadi. Kwa mfano wamala alipewa pesa (hongo) na wamerikia yaani alikuwa waziri
wa kazi wa serikali ya mitaa. anafungwa jela au kizuizinin kwa miaka kadhaa.
Anasamehewa na kufukuzwa serikali na kupoteza kazi.

2. TINKA

 Ni mkewe wamala.

 Ni mama zao Kaija na Nyakake.

 Ni mwenye mapenzi anampenda mumewe Wamala, wanafunga ndoa. Pia anawapenda


watoto wake.

 Ni msuka mikeka. Mikeka ambayo anamsaida kupata pesa za kununua kaptula ya Kaija,
kulipa karo shuleni.

 Ni mtengenezaji wa pombe ya aina enguli.

 Ni mwenye huruma. Kwa mfano anamhurumia Kaija kaw kutokuwa na kitanda.

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 21


 Ni maskini. Ndiyo anaanza kusuka mikeka ilia pate pesa za kununua kaptula ya Kaija na
karo shuleni.

 Ni mwoga. Kwani usiku Mbwa walikuwa nje ya nyumba walifukuzana nay eye kufikiri
kuwa ni majambazi amabao wamekuja kuwaiba na baada ye kugundua walikuwa Mbwa
tu wanakimbizana. Uk. 4

 Ni mwenye matusi. Ana mwita wamala nguruwe, Kupe. mjinga, kicheche, Nungu baada
ya kunywa chupa ya enguli yake.

 Ni mdanganyifu. Anamdanganya Nyakake kuwa babake Wamala amenda kwa mazishi


ya rafiki wakati Nyakake alipouliza juu ya babake. Uk. 84

3. KAIJA

 Ni bin yao wamala na Tinka.

 Ni nduguye Nyakake.

 Ni msomi. Anasoma katika shule ya msingi.

 Ni maskini. Amevaa kaptual ambayo imetiwa kiraka vibaya vibaya na shati la nailoni.

 Ana njaa. Anapiga miayo na kuuliza mamake chakula.

 Kaija ni mwenye hasira. Anang’pa miche ya pamba yam zee Kaboga na kumpiga
Tibasaga na kumvunjia mtungi wake baada ya kumwona aking’oa miche ya pamba yam
zee Kaboga. Uk. 78

 Ni mdadisi. Anamtaka kujua aliko babake ndiyo sababu anamwuliza mamake (Tinka) juu
ya baba yake.

MTINDO WA LUGHA KATIKA TAMTHILIA YA MIZIGO

Mtindo wa lugha unazungumzia juu ya Fani au Mbinu za Sanaa zinazofanya kazi ya faishi
kuvutia. Kwa mfano:

1. Methali: Ni misemo ya hekima yenye maana fiche au iliyofumbwa. Kwa mfano

 Ahadi ni deni. Uk. 8

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 22


 Chui jike alie kilema hufa huku akikwangua udongoni. Uk. 9

2. Misemo au Nahau au semi: Ni fungu la maneno linalotumiwa kutoa maana nyingine badala
ya ile ya maneno yaliyotumiwa. Kwa mfano

 Angua kicheko. Uk. 32

 Kata tama. Uk. 47

 Ona cha mtema kuni. Uk. 64

 Tema mate. Uk. 66

 Salimu amri. Uk. 70

3. Mseto au kuchanganya ndimi: Ni kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentseni ya


Kiswahili. Kwa mfano.

 Brroklax. Uk. 4

 Kwete. Uk. 24

 Associated matches. Uk. 24

 Kaunga na dodo. Uk. 28

 Propaganda. Uk. 44

 Oyee! Afrika Oyee! Uk. 53

 Hallo Vincent. Uk. 56

 Prince. Uk. 58 crown bird

4. Utohozi: Ni kuswahilisha maneno ya lugha nyingine kutamkika kama ya Kiswahili. Kwa


mfano

 Fanicha. Uk. 1 Bendeji. Uk. 38

 Nailoni. Uk. 1 Hospitali. Uk. 38

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 23


 Senti. Semina. Uk. 43

 Shilingi Uk. 35 Komunisti. Uk. 43

 Polisi, Faini Uk. 35 Sakramenti. Uk. 44

 Hoteli. Uk. 53 Kontrakta. Uk. 6

5. Tashbihi: Ni mbinu ya kulinganisha vitu au hali mbalimbali tofauti kwa kutumia maneno ya
kulinganisha “kama, mithili ya, sawa na, mfano wa” kwa mfano

 Siku zote unakonda kama kijiti cha kuchokorea meno. Uk. 2

 Alipoamka alijikuta yu baridi kama maiti.\

 Nyenje alikuwa amejibanza kipembeni akilia na machozi yakimtiriri kama maji. Uk. 18

 Bwana kanagonago anabadilisha magari kaam suruali. Uk. 58

6. Mubalagha au maswali ya balagha: Ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika


ambayo hayahitaji majibu. Kwa mfano

 Itakuwaje mtoto wangu auze karanga shuleni?

 Mpaka lini tutaendelea kubeba dhambi za watu weupe? Uk. 47

 Lini tutajiheshimu na kujiongoza wenyewe? Uk. 47

 Mwulize mamako kwa nini huna kitanda? Uk. 6

7. Chuku: Ni kutumia maneno yanayotilia chumvi ili kusisitiza ujumbe Fulani. au kusifia kitu.
Kwa mfano

 Meno meupe kuliko maziwa. Uk. 18

8. Taswira: Ni matumizi ya maneno yanayojenha picha hali au jambo Fulani kwa msomaji. Kwa
mfano

 Meno meupe kuliko maziwa. Uk. 18

 Bwana kanagonago anabadilisha magari kama suruali. Uk. 58

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 24


9. Majazi: Ni mbinu ya mhusika kupewa jina linaloambatana na sifa au tabia zake: Kwa mfano

 Kaboga: mkulima wa mboga.

 Enguli: pombe ya kienyeji inayofanywa kutoka ndizi.

 Kwete: pombe ya kienyeji.

10. Tasfida: Ni mbinu ya kudicha aibu au ukali wa maneno. Kwa mfano

 Mzee

 Ahsante

11. Takriri: Ni mbinu ya kurudiarudia neon moja au kifundu cha maneno ili kusisitiza ujumbe
Fulani. Kwa mfano

 Miaka mitatu! Miaka mitatu! Uk. 8 Askari! Askari! Askari! Uk. 66

 Ngonjea! ngonjea! Uk. 8 Nisaidieni! Nisaidieni! Uk. 78

 Haiwezekani! Haiwezekani! Uk. 8 Hapana! Hapana! Uk. 87

 Vyema! Vyema! Uk. 18 Amani! Amani! Amani! Uk. 87

 Ubadhirifu! Ubadhirifu! Uk. 25 Ninafahamu! Ninafahamu! Uk. 87

 Bila ya shaka! Bila ya Shaka! Uk. 52

 Mwizi! Mwizi! Mwizi! Uk. 64

12. Uzungumzi Nafsiya: Mhusika hujizungumzia, ama kwa kupongea au kuwaza, bila
kukusudia kusikika na yeyote. Kwa mfano

 Ni ya mwana kufuata nyayo za babake. Uk. 14 (Tinka anajimbia).

 Nita mwomba mwalimu auze baadi kubwa ya vitu vyetu na achukue hizo fedha kuwa
malipo ya suti yake tuliichana. Uk. 74 (Tinka anajisemea)

13. Nyimbo na / au mashairi: Yanaweza kutumik katika hadithi kwa madhumuni mbalimbali.
Kwa mfano

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 25


 Wimbo wa Tinka, mwanagu ewe mwanangu, babako amekimbia nk Uk. 16

14. Njozi au ndoto: Mwandishi hutumia ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua
jambo lililokuwa limefumbwa. Kwa mfano

 Ndoto ya Kaija. Kaija aliota kuwa alikuwa aking’oa miche yam zee Kaboga Uk. 78 (81 –
82)

Maswali

1. Anwani “Mizigo” inafaa tamthili hii? Jadili.

2. Eleza kwa ufupi yale yanayojitokeza katika tramthili ya Mizigo.

3. Eleza umuhimu wa wahusika wafuatao katika tamthilia ya mizigo.

a) Wamala

b) Tinka

c) Kaija

d) Nyakake

4. Mwandishi John Ruganda amechora vipi jinsia ya kike katikla tamthilia yake ya mizigo?

5. Eleza maudhui yanayojitokeza katika tamthilia ya mizigo

6. Eleza hulka za wahusika katika tamthilia ya mizigo.

7. Fafanaua mbinu za lugha zinazojitokeza katiuka tamthilia ya mizigo.

8. (a). Ni mizigo ipi John Ruganda anayozungumiza katika tamthili ya mizigo? Toa anagalau
mizigo minane.

(b). Fafanua lengo la mwandishi katika kutunga tamthilia ya mizigo.

9. (a). Fafanua ploti ya tamthili ya mizigo kama inavyojengwa na mwandishi.

John Ruganda.

(b). Onyesha umuhimu wa ploti katika kuikamilisha tamthilia ya mizigo

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 26


MWISHO

P320/2 TAMTHILIA YA MIZIGO. johnsonmuhindo@gmail.com 0775558860/0704902557 Page 27

You might also like