Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA

MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU

MTIHANI WA UTAMILIFU : DRS LA VII

SOMO: KISWAHILI

Muda: Saa 1:30 Julia 31 hadi agost 2


2023

MAELEKEZO KWA WATAHINIWA

1. Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye maswali arobaini na tano (45)

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum ya kujibia (OMR)

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na kwenye ukurasa wenye swali 41 - 45
katika karatasi ya maswali

5. Andika namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia
OMR kwa swali la 1 - 40. Kwa mfano kama jibu ni A weka kivuli kama ifuatavyo:-

[A] [B] [C] [D] [E]

7. Ukigundua kuwa herufi uliyoweka kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini
kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali namba 1 - 40 na tumia kalamu ya wino


wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 - 45

9. Simu za mkononi “HAZIRUHUSIWI” katika chumba cha mtihani.

1
Karatasi hii ina kurasa 4

SEHEMU A: ALAMA 35
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Sikiliza kwa makini habari inayosomwa na msimamizi, kisha jibu swali 1-5 kwa
kuchagua herufi ya jibu lililosahihi.

1. Methali iliyotumika katika habari ni ipi kati ya hizi zifuatazo _____ A. Haba na
haba hujaza kibaba B. Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe C. Lakuvunda
halina ubani D. Penye miti mingi hapana wajenzi E. Meno ya mbwa
hayaumani
2. Kijiji cha Ruangwa kilikua na ___ A. Mali nyingi B. Umasikini mkubwa C.
Utajiri mkubwa wa mali D. Uhaba wa mali E. Mashamba mengi
3. Wanakijiji wa Ruangwa walitoa misaada kwa watu wa vijiji vya ____ A. Jirani
B. Mbali C. Watu mbalimbali D. Masikini E. Wazawa
4. Katika habari uliyosikiliza neno ‘Hawakuwathamini’ lina maana sawa na neno
lipi kati ya haya yafuatayo? A. Hawakuwaamini B. Hawakuwajali
C. Hawakuwapenda D. Waliwafukuza E. Walipenda sana
5. Kichwa cha habari hii kingefaa kuwa _____ A. Kiongozi mwenye maono
B. Penye miti mingi hapana wajenzi C. Kijiji cha Ruangwa D. Utajiri
wa mali E. Wananchi wa Ruangwa
6. Ni neno lipi kati ya yafuatayo ni kisawe cha neno ‘Shari’ A. Ubunifu B.
Uzushi C. Ugomvi D. Uzembe E. Umaarufu
7. Ningekuwa na njaa ____ chakula A. Ngalikuwa B. Ningenunua
C. Ningelinunua D. Nisingenunua E. Tungenunua
8. Katika neno ‘wananifuata’ kiambishi kinachoonesha kitenzi ni kipi? A. – fuat
B. – ni C. – ana D. – fuata E. – fua
9. Neno SAMANGA lina konsonati ngapi? A. Saba B. Nne C. Mbili
D. Tano E. Kumi
10. Umefanya vibaya rafiki yangu -–– ningalikupa A. ungaomba B. ungeliniomba
C. Ungeliomba D. ungaliomba E. ungeomba
11. Stadi wa kutunga nyimbo na kuimba katika ngoma huitwa A. Kungwi B.
Malenga C. Manju D. Msanii E. Mtaalamu
12. Yule mwizi ___ baada ya kuzomewa A. alifurahi B. alitahayari C.
Alihimili D. alicheka E. Alimtisha
13. Mama alikuwa anafua nguo. Neno alikuwa linaonesha aina gani ya maneno?
A.Kivumishi B. KItenzi kisaidizi C. Kielezi D. Kihisishi E. Kiwakilishi
14. Hamidu amefundisha shuleni ___ miaka kumi na mbili A. mpaka B. tangu
C. kwa D. toka E. kipindi
15. Neno mpya lina silabi ___ A. mbili B. tatu C. moja D. tano E. nne
16. Neno lipi ni kisawe cha neno njiwa? A. Ndege B. Hua C. Kinda D.
Kasuku E. Chiriku
17. Kutokana na maumivu makali ya jeraha John hakuweza kupata hata ___ la
usingizi A. raha B. jicho C. lepe D. pitio E. punje

2
18. Mtu anayefundisha wanafunzi wa vyuo vikuu huitwa? A. Mkutubi B.
Mhandra C. Mhadhiri D. Daktari E. Mkufunzi
19. Wale wachangamfu wataondoka kesho. Neno lililopigiwa mstari ni ____
A. Kivumishi B. Kitenzi C. Kihisishi D. Kielezi E. Kivumishi
20. Neno “Maradufu” lina maana gani? A. Mara kwa mara B. Mara nyingi
C. Mara moja D. Mara chache E. Mara tatu
21. Mbuzi aliyepotea ameonekana sokoni. Je, hii ni aina gani ya sentensi?
A. Ambatano B. Changamano C. Sahili D. Shurutia E. Tegemezi
22. Kauli taarifa ya sentensi “Tafadhari nisikilizeni kwa makini“ ni ipi A. Alituambia
tumsikilize kwa makini B. Alisema tumsikilize C. Tumsikilize tafadhali
D. Kwa makini tafadhari E. Nisikilizeni kwa makini
23. Neno “jenga” likinyambulishwa katika hali ya kutendeka litakuwa neno lipi?
A. Jengwa B. Jengeka C. Jenga D. Jengeshwa E. Jengewa
24. Hali ya kuwa na fedha au mali nyingi huitwaje? A. Ukapa B. Ukata C. Ukwasi
D. Ubahili E. Uwezo
25. Hali ya kumfanya mtu atii kila analoambiwa ina maana sawa na nahau ipi kati
ya zifuatazo A. Kumkalia kitako B. Kumkalia kooni C. Kutia akili D.
Kumuweka kiganjani E. Kumkalia kichwani
26. Kamilisha ,methali hii „Jiwe la kutupwa ngomani __________“ A. humpiga
wako B. haliumizi C. huumiza walio wengi D. haliumizi mtu E. humpata
manju
27. Mimi na Asha tutafaulu mtihani wetu. Sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi?
A. Pili umoja B. Tatu wingi C. Kwanza wingi D. Tatu umoja E. Kwanza
umoja
28. Methali isemayo „baya lako si jema la mwenzako“ ina maana gani? A.
Matendo mabaya ya mtu humletea sifa mbaya B. Tuliridhike na vitu
tulivyonavyo C. Wanapopigana wakubwa huumia wadogo D.
Tusiwadharau wengine E. Tufanye mambo kwa uangalifu
29. Maana ya methali isemayo „jumbe ni watu si kilemba” ni _________ A.ukiona
mtu anafanya jambo fulani lazima jambo lile lina faida kwake B. tukitaka
kufanikiwa lazima tuwe na ushirikiano na wenzetu C. mtu humdharau mtu
mwingine kutokana na mazoea kupita kiasi D. kuwa kiongozi ni kuwa na
matendo mazuri na kuhusiana vizuri na watu E. anaye husiana na mtu mbaya
huishia kuambukizwa ubaya huo
30. Hamisi ni mmwizi nahau ipi kati ya hizi zifuatazo inafaa kuelezea tabia ya
Hamisi A. Ana mkono wa birika B. Ana mdomo wa panga C. Ana ndimi
mbili D. Ana mkono mrefu E. Anakula hongo
31. Maana ya nahau „kumlamba mtu kisogo“ A. Kumkonyeza B. Kumtukana
C. Kumdharau D. Kumsengenya E. Kumcheka
32. Amina alikuwa na „kichwa cha panzi” msemo kichwa cha panzi ni? A. Msikivu
sana B. Mtambuzi C. Msahaurifu sana D. Anakumbuka E. Mtiifu sana
33. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inapingana na hii “Umoja ni nguvu utengano ni
udhaifu“ ? A. Panya wengi hawachimbi shimo B. Kidole kimoja hakivunji
chawa C. Palipo na wengi hapaharibiki neno D. Mkono mmoja hauchinji
ng`ombe E. Jifya moja haliinjiki chungu
3
34. Tegua kitendawili kifuatacho, Dume wangu amelilia machungoni______ A.
moto B. radi C. mvua D. jua E. mwezi
35. Badili sentensi ifuatayo kuwa katika hali ya uyakinishi „Mama na baba hawa
kuamka asubuhi kunitakia heri ya mtihani“ A. Mama na baba waliamka
asubuhi kunitakia heri ya mtihani B. Baba na mama sihawakuanitakia kila la
kheri katika mtihani C. Baba na mama walinijulia heri ya mtihani D. Mama na
baba waliuliza habari za mtihani E. Baba na mama hawakukuuliza habari
za mtihani
SEHEMU D: UTUNGAJI
PANGA SEHEMU ZA BARUA ZIFUATAZO KWA MTIRIRIKO UNAOFAA KWA
KUZIPA HERUFI A, B, C, C, D NA E

36. YAH: MAOMBI YA KAZI


37. Mkurugenzi, kampuni ya vigae S.L.P 280 ZAIKO
38. Wako mtiifu SUNGURA KICHECHE
39. S.L.P 4302 DODOMA
40. Tarehe 7.4. 2003

SEHEMU E: UFAHAMU
Soma kwa makini Habari ifuatayo kisha jibu maswali 41 – 45 kwa
kuweka herufi ya jibu sahihi
Zamani za kale sehemu nyingi duniani zilikuwa na misitu. Maji na ardhi nzuri kwa
kilimo. Mfano wa sehemu hizo ni pori la Geita mkoani Geita. Watu wa jamii ile
walilima mashamba madogo lakini walipata mavuno mazuri
Ilikuwepo misitu mikubwa iliyokuwa na miti ya mitundu, mipodo na mibanga. Miti
ilikuwa hata ikifikia hatua ya kukomaa bila kuharibiwa licha ya kutoa mazao mengi,
Misitu iliwaletea watu wa jamii ile mvua ya kutosha kila mwaka. Wanyama na
ndege walizaliana kwa wingi katika misitu hiyo. Wakati huo watu walikuwa
wachache na mahitaji yao ya misitu yalikuwa machache pia. Kwahiyo kila kitu cha
asili kilitosheleza mahitaji ya kila mtu kwa kila siku. Je, baada ya mfumo wa soko
huria na mfumo wa mawasiliano kwa teknloljia ya kisasa kuna nini?

MASWALI
41. Mtu anaposema “kila kitu cha asili” kilitosheleza mahitaji ana maana gani? ____

42. Katika msitu uliozungumziwa, miti gani ilikuwepo kwa wingi? _______

43. Kichwa cha habari hii kinafaa kiwe? _____________________

44. Mfumo unaodhaniwa na mwandishi wa habari kuhusu mfumo wa mawasiliano


wa teknolojia ya kisasa unaitwajes? __________________

4
45. Baadaya mfumo wa soko huria la biashara Geita kumetokea nini?
___________

You might also like