Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA

MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU

MTIHANI WA UPIMAJI : DRS LA VII

SOMO: HISABATI

Muda: Saa 1:30 Julia 31 had agost 2 2023

MAELEKEZO KWA WATAHINIWA

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye maswali arobaini na tano (45)

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum ya kujibia (OMR)

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na kwenye ukurasa wenye swali 41 - 45
katika karatasi ya maswali

5. Andika namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia
OMR kwa swali la 1 - 40. Kwa mfano kama jibu ni A weka kivuli kama ifuatavyo:-

[A] [B] [C] [D] [E]

7. Ukigundua kuwa herufi uliyoweka kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini
kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali namba 1 - 40 na tumia kalamu ya wino


wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 - 45

9. Simu za mkononi “HAZIRUHUSIWI” katika chumba cha mtihani.

Karatasi hii ina kurasa 4

1
SEHEMU A: ALAMA 35
Chagua herufi ya jibu sahihi
1. Shule ya msingi Ikuyu ina wanafunzi 238 na shule ya msingi Ndola ina wanafunzi 5932.
Nini jumla ya wanafunzi wa shule tatu iwapo shule ya msingi Lupeta ina wanafunzi 2304
pungufu ya Ndola? (a) 9698 (b) 9798 (c) 8798 (d) 8474 (e) 6170
2. Juma ana mbuzi 4317 aliuza mbuzi 398 kwa matumizi ya karo ya mtoto . Je, Juma
alibakiwa na mbuzi wangapi iwapo mbuzi 298 alimgawia kaka yake? (a) 3561
(b) 3919 (c) 3621 (d) 4019 (e) 3721
3. Kreti moja la soda lina soda 24. Iwapo wakati wa harusi ya Amina kamati ilinunua kreti 46.
Je, kamati ilinunua soda ngapi jumla? (a) 1104 (b) 70 (c) 1214 (d) 1114 (e) 1014
4. Mwalimu aliwataka wanafunzi wa darasa la saba watafute hisa ya 113265 na 135. Je
walipata jibu gani? (a) 849 (b) 739 (c) 829 (d) 839 (e) 983
5. Mwalimu aliwataka wanafunzi sita watafute kipeuo cha pili cha jumla ya namba witiri kati
ya 0 na 10 (a) 4 (b) 5 (c) 25 (d) 24 (e) 3
6. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mnamo mwaka 1922, Hivyo mwalimu
Masanja aliwataka wanafunzi wake wauandike mwaka huo kwa kirumi. (a) MCMLXII (b)
MMII (c) CMMXXII (d) MCMXXIV (e) MCMXXII
7. Nafasi ya thamani ya tarakimu iliyopigiwa mstari katika numerali 902436 (a) Makumi
(b) Makumi elfu (c) Mamia elfu (d) Mamilioni (e) Maelfu
8. Mzee Jongo ana watoto 5 ambao umri wao hutofautiana kwa miaka minne kati ya mtoto na
mtoto wanaofuatana. Iwapo mtoto wa kwanza ana miaka 59. Je, mtoto wa mwisho ana
miaka mingapi? (a) 43 (b) 55 (c) 63 (d) 39 (e) 51
9. Kata ya igale ina walimu 40 iwapo walimu 8 wapo masomoni .Je, ni asilimia ngapi ya
walimu waliopo kazini? (a) 80 (b) 20 (c) 60 (d) 75 (e) 25
2
10. Ashura alikuwa na mita 16 za kitambaa . Iwapo alimgawia rafiki yake Zuwena mita 5 za
5
12
kitambaa hicho. Je Ashura alibakiwa na mita ngapi za kitambaa chake? (a) 10 (b)
5
2 3 2
(c) 10 (d) 10 (e) 11
5 5 5
11. Tafuta zao la 3.02 na 12 (a) 3.624 (b) 324.4 (c) 35.24 (d) 32.04 (e) 36.24
12. Wanafunzi wa darasa la tano walipewa namba zifuatazo; 15, 17, 21,31, 37, 39, 45, 49, 51
na 59. Iwapo mwalimu wao aliwataka waandike idadi ya namba tasa kutokana na orodha
hiyo ya namba. Jibu sahihi ni lipi? (a) 5 (b) 6 (c) 4 (d) 3 (e) 10
13. Wanafunzi watano walipewa kadi za namba kama ifuatavyo ; Mwanafunzi wa kwanza
1
alipewa kadi yenye namba 0.3, wa pili kadi yenye namba , watatu 40%, wa nne 0.75,
2
watano -100 ni mwanafunzi yupi alishika kadi yenye namba ndogo kulizo zote? (a) 0.3
1
(b) 0.75 (c) -100 (d) (e) 40%
2
14. Mama alikuwa na machungwa 20, mtoto wa kwanza alimpa machungwa 5, Jirani alimpa
machungwa 2, iwapo mtoto wa pili alipewa mara mbili ya mtoto wa kwanza. Je mama
alibakiwa na machungwa mangapi? (a) 5 (b) 13 (c) 8 (d) 3 (e) 2
1
15. Mwajuma aliambiwa na Mwalimu Ali aandike sehemu inayofuata katika mfulilizo huu; ,
2
3 5 7 9 9 6 8
, , ,______ Je, aliandika sehemu ipi? (a) (b) (c) (d)
4 6 8 10 11 8 10
9
(e)
12
2
16. Kokotoa, 25.48 ÷ 0.091 (a) 28 (b) 280 (c) 2800 (d) 2.8 (e) 2.80
7
17. Shule ya Msingi Mtakuja ina wanafunzi 480. Iwapo ya wanafunzi hao ni wasichana . Je
12
ipi ni tofauti kati ya wasichana na wavulana? (a) 280 (b) 80 (c) 200 (d) 40 (e)
760
18. Mwalimu wa shule ya Msingi Matinganjola aliwataka wanafunzi wa darasa la saba
8 1 2 7 9
waandike 45% kuwa sehemu rahisi. (a) (b) (c) (d) (e)
25 2 3 20 20
19. Amina aliambiwa na mwalimu apite mbele ili akokotoe mlinganyo huu. 2x + 3 = 15. Je
nini ilikuwa thamani ya x. (a) 9 (b) 7 (c) 5 (d) 21 (e) 6
20. Mwanafunzi aliamka saa 9:50 usiku ili kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa
Mock. Je, muda huo ni saa ngapi katika mtindo wa saa 24 (a) 0950 (b) 0150 (c)
0350 (d) 0450 (e) 1550
21. Doto ana uzito wa kg 5 na gm 780 na kulwa ana uzito wa kg 2 na gm 800. Nini tofauti ya
uzito wa watoto hao? (a) Kg 3 gm 20 (b) kg 2 gm 20 (c) kg 3 gm 980 (d) kg 2 g
980 (e) kg 3
22. Tafuta kigawe kidogo cha shirika cha 24, 56 na 16 (a) 14 (b) 672 (c) 28 (d) 336 (e)
4096
23. Nini thamani ya -11 - -4 (a) -7 (b) -15 (c) +7 (d) +15 (e) -11
24. Mwalimu aliwataka wanafunzi wa shule ya Msingi Garijembe watafute namba mraba ya
49. Je, jibu sahihi lilikuwa ni lipi? (a) 2301 (b) 1901 (c) 2501 (d) 2014 (e) 2401
25. Mwalimu Hamisi alitakiwa kuripoti Ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kupeleka taarifa ya
Ujenzi wa vyumba vya madarasa saa 3 na dk 25 asubuhi , ikiwa alifika ofisini saa 4 dk 15,
Je mwalimu Hamisi alichelewa muda gani kufika ofisini hapo (a) Saa 1 dk 15 (b) Dk 50
(c) Dk 15 (d) Saa 1 dk 10 (e) Dk 40
26. Ikiwa umepewa 60, 72 na 96 ukaambiwa utafute kigawo kikubwa cha shirika , Jibu sahihi
litakuwa ni lipi? (a) 20 (b) 18 (c) 12 (d) 10 (e) 15
27. Tafuta kipeuo cha pili cha √ 2401 (a) 49 (b) 47 (c) 14 (d) 7 (e) 21
28. Tafuta namba inayofuata katika mwandamo huu XXIV, XXVII, XXXVI, ______. (a) XL
(b) XLIII (c) XXXIX (d) XLI (e) XLII
29. Ikiwa mzingo wa umbo mstatili wenye urefu wa sm (2x +5) na upana wa sm (x+2) ni sm
50. Tafuta eneo lake (a) Sm2 136 (b) Sm2 156 (c) Sm2 126 (d) Sm2 146 (e) Sm2
225
30. Pentagone ina pembe zifuatazo 2m, 10 0 + 4m, m+300, 1600 na 3m -1000. Tafuta thamani
ya ‘m’. (a) 4400 (b) 440 (c) 500 (d) 540 (e) 600
31. Hadija alipewa kasha la sabuni lenye urefu wa sm 12, upana wa sm 8 na kimo sm 6.
Tafuta eneo la kasha la sabuni alilopewa Hadija (a) sm 2 576 (b) sm2 96 (c) sm2 532
(d) sm2 432 (e) sm2 144
32. Mwanafunzi alipewa pipa la maji lililotobolewa upande mmoja lenye kipenyo cha sm 35 na
kimo cha sm 70. Kisha aliambiwa atafute eneo la pipa hilo. Je jibu sahihi lilikuwa lipi (a)
sm2 7700 (b) sm2 962.5 (c) sm2 8662.5 (d) m2 8662.5 (e) m2 962.5
33. Tafuta mzingo wa umbo lifuatalo

Sm 36
A: sm 936
B: sm 102
Sm 24 C: sm 128
D: sm 107
E: sm 937
Sm 43

3
34. Tafuta mzingo wa pembetatu ifuatayo

A: m 56
m(5x-2) m(6x-8) B: m 71
C: m 43
D: m 81
E: m 61
15

35. Mwalimu alichora mchoro ufuatao ubaoni

A B C D
Je, katika mchoro huu kuna vipande vingapi vya mstari? (a) 4 (b) 3 (c) 7 (d) 6 (e) 5
36. Baba aliwagawia watoto watatu maembe 660 kwa uwiano wa 3: 7: 2. Je mtoto wa pili
anazidi maembe mangapi zaidi ya mtoto wa tatu? (a) 275 (b) 385
(c) 110 (d) 215 (e) 49
37. Johari alinunua jozi ya viatu kwa sh 25000 na kuuza kwa shilingi 16000. Je, hasara
aliyoipata ni asilimia ngapi ya bei ya kununulia? (a) 36 (b) 40 (c) 25
(d) 30 (e) 32
1 1
38. Maulidi alikula ya mkate na Ali alikula ya mkate aliokula Maulidi . je ni sehemu gani
6 2
1 1 2 1 3
ya mkate ulibaki? (a) (b) (c) (d) (e)
2 4 5 12 4
39. Kampuni ya Tigo iliweka 300,000/= katika akaunti ya bank ya akiba inayotoa kiasi cha riba
1
7 % kwa mwaka . Je , itachukua muda wa miaka mingapi kupata faida ya sh 45,000/=
2
(a) Mwaka 1 (b) Miaka 2 (c) Miaka 3 (d) Miaka 4 (e) Miaka 5

40. Umri wa Kija ni mara 4 ya umri wa mwanae Asha. Iwapo Jumla ya umri wao ni miaka 35.
Nini umri wa Kija miaka mitano iliyopita (a) 28 (b) 40 (c) 23 (d) 7 (e) 2

SEHEMU B: KOKOTOA NA KUONYESHA NJIA


2 2
a b −ab
41. Mwalimu aliwataka wanafunzi wa darasa la saba , warahisishe
ab−1
Je walipata jibu gani baada ya kurahisisha.

42. Agape alipokea mshahara wake wa sh134,000 na kununua mahitaji yafuatayo Sukari kg 6
@ 2400/=, Mafuta ya kupikia lita 3 @ 1200/= Unga wa sembe kilo 10 kwa sh 9000,
Mchele kg 7 @ 1600/= Baada ya matumizi hayo kiasi kingine alilipa madeni. Je ni kiasi
gani kilitumika kulipa madeni?

43. Mwalimu aliandika majira ya nukta zifuatazo A( -2,3), B(1,3), C(1,-2) na D(-2,-2)
baada ya kuunganisha majira hayo ni umbo gani lilitokea?

44. Keneth hutumia sh 18000 kwa starehe . Je hutumia sh ngapi kwa chakula?

Nguo Starehe
45. Iwapo kivimbe cha duara ni sm 88 Tafuta eneo la duara hilo.

You might also like