Mwanamke Na Mahusiano

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 73

MWANAMKE NA MAHUSIANO

1
MWANAMKE NA MAHUSIANO

MWANAMKE

NA

MAHUSIANO-1

2
MWANAMKE NA MAHUSIANO

YALIYOMO

YALIYOMO……………………………….……..……..…….3

TABARUKU………………………….. ……………..………4

LENGO LA KITABU………………………....….….…….…5

JE MAJIRA YANGU YA KUINGIA……..………..……. …6

NANI NIOLEWE NAYE ?.........................................……15

MAJIRA YA BWANA NI MIAKA MINGAPI ?........…20

NINI UFANYE UKIWA SINGLE…………….………….….26

USAFI WA KINGONO KWENYE MAHUSIANO......49

USILOLIJUA KUHUSU MWANAUME………………....63

KUHUSU MWANDISHI………………….……….………….73

3
MWANAMKE NA MAHUSIANO

TABARUKU

NI SHAUKU YA MOYO WANGU KUKISAIDIA KIZAZI


CHANGU KWA HABARI YA UFALME WA MUNGU NA
KUWEKA NJAA NA KIU YA KUMJUA MUNGU PIA
KUINUA WATU WALIO TAYARI KWA AJILI YA MUNGU
AMBAO HAWAJAJIKINAI YAANI ASKARI WAAMINIFU
HIVYO NI MATUMAINI YANGU KUPITIA MAARIFA
HAYA KUNA JESHI KUBWA LITAINUKA NA KUFANYA
KANISA KUTAWALA NA KUMILIKI KATIKA TAIFA NA
MATAIFA KUPITIA VITABU HIVI VYA KI-ELECTRONIKI
AMBAVYO NI BURE KABISA KWA KILA ATAKAYE.

TANZANIA, WEWE NI JIKO LA KUPIKIA MAISHA


HALISI YA WOKOVU.

4
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Lengo la kitabu hiki ni

Lengo la kitabu hiki ambacho ni toleo la kwanza la


muendelezo wa vitabu vya MWANAMKE NA
MAHUSIANO nia ni kusaidia wanawake wasiendelee
kuwa wahanga wa mahusiano maana imekua kawaida
wanawake wengi wameshindwa kutimiza malengo na
makusudi ya wao kuwepo duniani kwa sababu
mahusiano yamewachanganya kabisa

5
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA KWANZA

JE MAJIRA YANGU YA KUINGIA KWA MAHUSIANO


TAYARI ?
Majira ni wakati Sahihi wa ukomavu unamruhusu
mtu kuingia katika eneo fulani la kimaisha.
Majira si umri
Majira si ndevu
Majira si kuwa na matiti.
Majira si Kusoma chuo.
Majira si kubalehe pekee
Majira ni ukomavu hivyo tuna wake za Watu wengi
ambao tukiangalia kiukomavu utagundua hakufaa
kuwa Mama ana miaka 30 lakini ni Binti wa
chekechea kabisa.
Ndo utasikia ile kauli kuwa HUYU NAYE KAMA TOTO
DOGO

6
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Yaani kuna vitu huwa vinafanywa na mwanamke


(mkomavu) na kuna vitu vinafanywa na Binti(kwa
Sababu ajakomaa) ndo Maana mimi huwaga
napendaga kuwaambia Watu kuwa ukikua utaacha.
Binadamu mwenye jinsia ya kike ambaye
hajakomaa utamjua tu huwa anapapatikia
mahusiano kabla ya kujijua yeye na Kusudi
alilobeba.
Huwa hawana picha ya miaka 10 au hata 20 ijayo
watakuaje

Huwa hawana picha ya Mume atakayekuja kumuoa


ndio Maana yeye kila mpendwa akija ataanza
kumfikiria ndo leo anavutia na mkaka Daktari, kesho
anavutiwa na mfanyabiashara, kesho kutwa
anavutiwa na wale wabeba chuma na anamalizia
anavutiwa na muhubiri.

7
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Ukiona hii ujue Huyu bi-shosti hajakua kabisa ni


mtoto mchanga mwenye matiti anayeingia period.
Ndio Maana leo tuna kizazi cha hovyo kwa Sababu
mama ambao ni walezi hawajakua bado ijapokua
Wanaonekana ni Watu wazima ila kiuhalisia ni
mtoto kamzaa mtoto mwenzie.

Bahati mbaya shetani amefanikiwa kutengeneza


wanawake Wenye matiti lakini hawajakua.
Ukuaji ndio inaamua uwaje, ndoa Yako iwaje.
Sasa mbaya zaidi ukutane au uolewe na binadamu
mwenye jinsia ya kiume ambaye amebalehe na ana
ndevu lakini ni mtoto nasi familia itakua ya hivyo
sana.

Unakuta unamsifia jamaa Yako ni handsome ana six


packs anabeba chuma lakini kiuhalisia ni mtoto
yaani Upo kwenye mahusiano na mtoto mwenzio

8
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Majira Yako yatafika mpaka pale utakapokua na


ukomavu.
Ni hatari kuingia kwenye mahusiano wakati wewe ni
mtoto ndo lila siku utakua unasusa susa tu au
ukiolewa ndo kila Muda utakua unakagua simu ya
mumeo, au ukiona jamaa anatumika sana utasikia
mbona unatumika sana unanicheat aisee Huyu na
mtoto wa Kiwango cha pro max.
Ukomavu huwa unavuta Watu Sahihi yaani
ukomavu ni sumaku ya kuvuta Watu Sahihi.

Mfano; kuna Wanaume huwa wanakuja wananiuliza


na tunaongea nao sana tu kuhusu Binti gani
amfuate na nani asimfuate Kati ya hizo utasikia
tatizo yule ni mtoto na wengine tunampigia hesabu
na anasoma ila hawa majamaa wanasema ni bora
nimsubiri amalize chuo kuliko kwenda kwa fulani

9
MWANAMKE NA MAHUSIANO

utasikia fulani hajakua yaani utoto mwingi Sana na


tunakubaliana kuwa amasubiri mtu fulani.
Hivyo ukomavu ni huleta Watu Sahihi waliokomaa
wenzako.

Kikawaida mtoto huambatana na mtoto mwenzie


na mtu mzima hukaa na huambatana na mtu mzima
mwenzie hata haya mambo ya mahusiano
yanayoelekea ndoa yanatumia hii kanuni kuwa
mtoto atampata mtoto mwenzie na hapo sasa
mtoto akijitambua ndo ataanza kumsaidia mwenzie
akue ijapokua suala la ukuaji ni suala maamuzi ya
Mtu
Kuna kitu kinaitwa UANAMKE WA MWANAMKE.
hii inahusisha huyo mtu alivyo na hii inatokana na
malezi pamoja na Jamii inayomzunguka ilimpa
Tafsiri gani ya neno mwanamke.

10
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mfano mwingine kitu pekee anachoweza kukitoa


kwenye mahusiano ni ngono tu hajui kama anaweza
kumfanya huyo mkaka ambaye ni mfanyakazi wa
potifa kuwa waziri mkuu hajui hilo na hivyo
anaweza akawa anampa Mwanaume ngono akijua
anamfurahisha kumbe anamuua ule UKUU ULIO
NDANI YA UANAUME WAKE ndo Unakuta
Mwanaume hawezi kufanya maamuzi ya kihatima.

Mwanaume ukimpenda sana na ukitaka kumlinda


basi msaidie kwa kumnyima kabisa Ngono (sex) ili
awe salama kama Unataka awe Baba bora na
Mwanaume halisi.
Yeremia 31:21-22
[21]Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya
kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia
kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa
Israeli, irudie hii miji yako.

11
MWANAMKE NA MAHUSIANO

[22]Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye


kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya
duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.
Njia pekee ya Kumlinda Mwanaume
unayempenda ni kumnyima kabisa Ngono
Ngono inapunguza ubora wa mwanaume

Sasa kuna mwanamke mwenzio anawaza njia ya


kumtunza mwanaume ni ngono Huyu mwanamke ni
hatari na silaha ya shetani kabisa kutokomeza
wanaume duniani na Huyu hafai kuwaza mahusiano
kwanza inabidi akae chini akue na akomae.

Mithali 6:32
[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Mithali 31:3
12
MWANAMKE NA MAHUSIANO

[3]Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo


wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
Nafsi inaangamizwa lakini sura ya 31 anaelezea
inavyoangamia kwa kupoteza Nguvu zake, hizi
Nguvu zipo kama ifuatavyo.

Nguvu za kuwa Mume Bora aliyetulia.


Nguvu za kuwa Baba bora kwa watoto.
Nguvu za kiume.
Nguvu za kupata utajiri.
Nguvu za kumfanya awe kichwa cha familia.
Nguvu za kumfanya awe kiongozi.

Hizi Nguvu Huwa unaziondoa pale unaporuhusu


ulale nae ni hatari Sana kwake zaidi ya kufurahi na
kuchekacheka ndo wanaume wengi wanapambana
lakini bado maskini na hawajiwezi kwa sababu

13
MWANAMKE NA MAHUSIANO

wewe ulimpa ngono ulimpa kiuno chako akichezee,


ulimpa matiti Yako ayaguse, uliamua kumvulia nguo
Ili umuharibu huku shetani akikupumbaza kuwa ndo
upendo huo na bahati mbaya zaidi unampunguzia
siku za kuishi kwa sababu zinaa inapunguza miaka
ya kuishi ndo maana ndoa nyingi wanaume
wanawahi kufa kwa sababu wakati hamjaoana
ulimpa sana tendo na unampunguzia a siku zake
akabakiza tarehe tu
Kuna kale kamsemo ka mtaani UKIMPENDA
UTAMLINDA hasa kwa kumnyima sex usimpe hata
picha ambazo maungio Yako wazi unaamuua.

Akikuoa mbona uwanja ni wake yaani atachagua ale


alafu ale au ale Muda huu na baadae ale tena.

Nimeongea kimafumbo aliye na akili na afahamu

14
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA PILI
NANI NIOLEWE NAYE?
Mtu atakayekuja kukuoa ni lazima mkubaliane
kuishi wote hivyo ni jukumu lako kukaa chini na
kutambua na kung’amua yupi akuoe.

Nikwambie tu ukweli kuolewa sio bahati ila kuolewa


ni haki Yako ya msingi na utaolewa tu Bila shaka.

Isaya 34:16
[16]Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome;
hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo,
hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa
maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake
imewakusanya.

Ukijiona umezaliwa ujue Wewe ni ubavu wa


mwanaume mmoja na wala usiongopewe na sensa

15
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Kuwa wanawake ni wengi sana hivyo ukimpata


mkaka mng’ang’anie hata akitaka ngono we mpe
maana ni bahati hiyo akisusa utaolewa na nani sasa,
sikia hayo ni uongo wa shetani na yangu Mwanzoni
Mungu alikua hapendi sensa

1 Nyakati 21:1,6-7
[1]Tena shetani akasimama juu ya Israeli,
akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.
[6]Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu
miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme
limemchukiza Yoabu.
[7]Neno hilo likawa baya machoni pa Mungu; kwa
hiyo akawapiga Israeli.

Ukisoma hapo ndo utaona sensa ilivyo Wewe


unachotakiwa ujue ni Kuwa Wewe kuwepo kwako

16
MWANAMKE NA MAHUSIANO

kuna mtu alichomolewa ubavu wake ambao ni


Wewe

Mwanzo 2:21-23
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi
mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake
mmoja, akafunika nyama mahali pake,
[22]Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA
Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa
Adamu.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika
mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi
ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika
mwanamume.

Wewe ni ubavu wa mwanaume mmoja hivi.


Mwanamke yeyote yule wewe ni ubavu wa
mwanaume fulani iwe umemuona au bado

17
MWANAMKE NA MAHUSIANO

haujamuona, sasa katika mazingira kama haya


unatakiwa ujue yupi ndo mtu Sahihi kwako na
vifuatavyo vitaanza kukupa mwanga kwamba kuna
dalili Kuwa ni Huyu mkaka.

Amosi 3:3
[3]Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja,
wasipokuwa wamepatana?

Mwanzo 2:24
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake
na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja.

Kwenye haya maandiko kuna maneno mawili ya


muhimu sana nayo ni AMBATANA NA KUPATANA
ambayo yana maana zinazofanana ambazo ni
kukubaliana, kuafikiana, na kung’ang’aniana Bila

18
MWANAMKE NA MAHUSIANO

kuachana na hizi maana zinabebwa na sehemu kuu


mbili nazo ni IMANI na KUSUDI.

IMANI ni maamuzi ya kuzifuata itikadi fulani


zinakupelekea kuamini na kuziishi hizo itikadi.

Itikadi ya kuamini Yesu ni Mungu na kuamini habari


za wokovu ni mfano wa Imani

KUSUDI/MAONO ni ile picha ya Maisha ambayo


Mungu ameikusudia itokee.

Ni lazima muwe mmepatana katika maeneo hayo


mawili kwanza kabla ya kumchunguza kwa habari ya
Ukomavu wake katika maeneo matatu nayo ni
KIMWILI, KIROHO NA KIAKILI ambayo ndiyo tunaita
miaka ya kuingia kwenye mahusiano yanayoelekea
Ndoa.

19
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA TATU
MAJIRA YA BWANA NI MIAKA MINGAPI?
Kibiblia hakuna miaka kamili iliyotajwa moja kwa
moja ya majira ya Bwana ya kuingia kwenye
mahusiano yanayoelekea kwenye ndoa ila biblia
inatuonesha dalili au ishara inayomfanya mtu aingie
huko na dalili yenyewe ukomavu.
Ukomavu ni dalili ya kujua majira ya Bwana ya
kuingia kwenye mahusiano yanayoelekea ndoa
ambapo yatakua Mapenzi yataona vema yenyewe,
ila ukomavu ni Zaidi ya watu wanavyoona kwa
kawaida kwa sababu ukomavu umegawanyika
makundi makuu matatu nayo ni

UKOMAVU WA KIMWILI.
Huu ni ukomavu ulio katika maumbile ya jinsia
fulani ambayo yanaonesha tayari Upo tayari kwa
ajili ya familia na Ndoa.

20
MWANAMKE NA MAHUSIANO

1 wakorintho 7:25
Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini
natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za
Bwana kuwa mwaminifu.

Hilo andiko linatuonesha kwa habari ya


mwanamwali na Maana halisi ya hili neno toka
kwenye kamusi ni

1. Msichana aliyekwisha kubalehe lakini bado


hajaolewa.
2. Msichana ambaye bado hajapoteza ubikira
wake

Kutoka kwenye maana hizo tunaona kuwa


mwanamwali ni mtu aliyefikisha umri wa kupevuka
lakini bado hajaolewa, hii inatuonesha kuwa
inampasa kwanza awe amekomaa kama ishara
kuwa anastahili kuolewa

21
MWANAMKE NA MAHUSIANO

UKOMAVU WA KIROHO
Huu ni aina ya ukomavu unaotuhakikishia kutembea
SawaSawa na Neno la Mungu mfano Neno la
Mungu linasema usiibe na usizini yaani mtu
aliyekomaa kiroho pamoja na hisia zake kuwa ni
kubwa lakini sharti awe anaweza kuishi Sawasawa
na Neno la Mungu pasipo kuyumba wala kusita sita

Mfano yusufu alisha komaa kiroho hivyo Ilimfanya


aweze kuwaza kumuacha kwa siri lakini malaika
wakamtokea kwenye ndoto na kumwambia kuwa
asimuache huyo Maria hii inaonesha kuwa
amekomaa kiroho

Mathayo 1:19
Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa
haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa
siri.

22
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mfano mwingine ni yusufu pale ambapo amepewa


fursa ya kulala na mke wa potifa lakini yeye
anagoma wakati angeweza kumkubalia na kulala
naye bila hata potifa kufahamu lakini yusufu
alisimama na Mungu wake na kukataa kulala nae na
kupelekea kufungwa gerezani Ili mradi tu asimtende
Mungu dhambi

Mwanzo 39:9
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala
hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa
wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa
nikamkose Mungu?

UKOMAVU WA KIAKILI
Ukomavu wa kiakili umegawanyika katika aina kuu
tatu nazo ni Uwezo wa kutatua mambo,Uwezo wa

23
MWANAMKE NA MAHUSIANO

kusimamia jambo au mambo uliyoyakubali, Uwezo


wako wa kiuchumi.

✓Uwezo wa kutatua mambo


Mtu yeyote yule ni lazima awe na Uwezo wa
kutatua mambo na sio tu kutatua bali inabidi awe
jawabu kwa mambo yanayokuja mbeleni ni hatari
kukuta haswa Mwanamume hana jawabu kwa vitu
vinavyowakumba, mtu akikosa hii atapata wakati
mgumu Sana.

✓Uwezo wa kusimamia jambo ulilolikubali.


Watu wengi hupata tabu Katika hili eneo na kama
mtu hawezi kusimamia anachokiamini ujue hawezi
kulinda anachokipenda yaani inabidi uwe na
maamuzi na uyasimamie usiwe mtu wa
kuendeshwa ndo utasikia mama kaniambia nisioe
waluguru au wachaga au nisioe aliyenizidi umri au

24
MWANAMKE NA MAHUSIANO

utasikia rafiki yangu ameniambia hunifai yaani


vituko ni vingi sasa mtu ambaye kila maamuzi
mpaka aulize mtu huyo bado hajakomaa, Mtu wa
hivi je anaweza kukutetea kwa wazazi na Ndugu
zake pale watakaposema hatumtaki huyo
✓ Uwezo wa kiuchumi
Hasa mwanaume ni lazima awe nao Ili kufanya
mahusiano yawe na nguvu, bila fedha mahusiano
magumu ijapokua mahusiano sio fedha ila fedha ni
muhimu sana

25
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA NNE
NINI UFANYE UKIWA SINGLE NA UNASUBIRI
MWENZI WAK
✓Weka Mkazo kwanza kwenye ukuaji wa Maisha
yako Binafsi.
1 wakorintho 7:32,34-35
[32]Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye
asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana,
ampendezeje Bwana;
[34]Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali.
Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya
Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini
yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya
dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
[35]Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee
tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate
kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo
mengine.

26
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mtume Paulo anakazia kuwa haujaolewa usiwe na


haraka Wewe mpendeze Bwana Yesu tu na
mtumikie Mungu na hakikisha mahusiano yako na
Bwana yanakua sawa sawa yaani ndio Muda wa
kusoma vitabu vingi, kuwa na mikesha yako binafsi
na kadhalika.
✓Usiwaze kuingia mahusiano na mtu Ambaye
hajaokoka kwa Sababu ni chukizo mbele za
MUNGU.

2 Wakorintho 6:14
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa
jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani
kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya
nuru na giza?

Ni lazima utambue uliyeokoka sio sawa kuwa mtu


na ambaye hajaokoka na Mungu hataki kabisa

27
MWANAMKE NA MAHUSIANO

✓Weka mipango endelevu ya kujitunza.


1 Wakorintho 6:16,18-20
[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili
watakuwa mwili mmoja.
[18Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo
mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye
zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake
mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na
Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
[20]Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

✓Tazama tabia za kiungu zaidi kwa mtu.


Wagalatia 5:19-21

28
MWANAMKE NA MAHUSIANO

[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya,


uasherati, uchafu, ufisadi,
[20Ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu,
hasira, fitina, faraka, uzushi,
[21]Husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana
na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu
watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme
wa Mungu.

Tafuta tabia za kiungu ambazo ni tunda la Roho


Mtakatifu.
Wagalatia 5:22-23
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani,
uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
[23]Upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna
sheria.

29
MWANAMKE NA MAHUSIANO

✓Kuwa mtu mwenye Hekima na wala sio ukiroho


uliokosa Hekima ya Mungu.

MWANAMKE NA UTAWALA HISIA ZAKE.


Kama tujuavyo Kuwa hakuna mwanamke asiye na
hisia hivyo ni dhahiri kabisa kujua namna ya
kuzitawala hisia zako kwa wale walioolewa na hata
ambao hawajaolewa na hata wale mabinti wa
mashuleni.
1 Wathesolonike 4:4
Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika
utakatifu na heshima;
Maandiko yanatuonesha Kuwa ni jukumu la kila
mmoja kutambua mwili wake unawakaje hisia na
kujua namna ya kujitawala bila madhara yoyote
yule ,Hivyo vifuatavyo ni miongoni mwa Vitu
vinavyotusaidia tusichochee mapenzi.

30
MWANAMKE NA MAHUSIANO

VICHOCHEO VYA MAPENZI/NGONO.


A. Miziki ya kidunia.
Amosi 6:5
Ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti
ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna
nyingi, kama vile Daudi;

Tatizo sio tu Nyimbo bali nani anaziimba Nyimbo


yoyote ile iliyoimbwa na mtu ambaye hajaokoka
basi haifai kwako kusikiliza Maana Biblia inasema
kusikiliza huku kunaitesa roho Yako
2 Petro 2:8
Maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa
kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku
baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
Petro anasema Lutu alijitesa roho yake kwa sababu
kule kusikia na kuona kwa hiyo tunaona Kwenye

31
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Nyimbo kuna mambo ya ajabu ambayo mengi Sana


yapo ndani ya hizi nyimbo.

Kweli kuu kuhusu mziki


I. Kwenye kila mziki kuna roho nyuma yake

II. Nyimbo ni funguo za shughuli za mapepo na


kadhalika, Kama vile ambavyo malaika wa nuru
wanavyotumika na nyimbo hivyo hivyo pepo
zinahitaji Nyimbo Ili yajifunue mfano kuna Watu
wanavua mpk nguo zao pale wanapocheza Miziki
hii inakuonesha kuwa kuna mapepo Mahali hapo.

III. Nyimbo hutumika kuwakilisha majira


Mfano kuna kipindi wanamuziki wanatoa Nyimbo
ambazo zinafanana karibia zote kama mwaka huu
wa 2023 Watu wengi wanatoa Nyimbo za kufanana
kama vile imapiano hii ni kwa sababu kuna ajenda

32
MWANAMKE NA MAHUSIANO

ya giza ambayo inafanya Kazi kwa majira hayo


inawezekana ni kumwaga roho za uzinzi na
kadhalika.
IV. Nyimbo ni lango la roho au maroho
Kwa waganga huimba Nyimbo Ili maroho yashuke
na aague uganga wake yaani roho hazishuki mpaka
Nyimbo ziachiliwe, sasa kila Muda uonapo Nyimbo
ujue kuna roho nyuma yake zinazoambatana na
Hizo Nyimbo, mfano uzinzi, ushoga, mauaji, usagaji
na mambo kama hayo
V. Nyimbo za kidunia hutumika kuua njaa na kiu ya
kumtafuta MUNGU binafsi

2.Video na picha za ngono


2Petro 2:8
Maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa
kuona: na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki,

33
MWANAMKE NA MAHUSIANO

siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na


sheria;

Petro anasema kwa kupitia kuona Lutu alikua


anaitaabisha roho yake, sasa Picha za ngono
huaribu kabisa Ufahamu wa mtu na kama ujuavyo
vita ya mtu na shetani huanzia Kwenye Ufahamu na
akikuweza Hapa utakua na Wokovu jina tu
Utaishi kutokana na kile unachokiona na kukisikia
na Hii inasababisha kuwasha hisia na kuamsha
mapenzi Kabla hayajaona vyema na hata kuleta
mashambulizi ya roho chafu.

• Ukweli ambao watu wengi hawatakwambia


kuhusu picha za ngono/ponografia .
Unapoenda kwenye tovuti za ponografia (Picha za
ngono) na unatazama, unapofungua macho
kutazama, roho chafu zinakuingia. Moja ya mambo
yanayofadhiliwa na ponografia ni punyeto

34
MWANAMKE NA MAHUSIANO

(kujichua). Moja ya mambo yanayofadhiliwa na


punyeto (kujichua) ni kifo cha mapema.

Wale mliofungwa na punyeto, mnanena kwa lugha


lakini imewafunga. Je, ninaweza kukushangaza?
Adui anaondoa uhai kutoka kwako. Wakati wowote
unapotazama nyenzo za ponografia, vitabu, au
video, unajifunga mwenyewe na roho ya dhihaka na
aibu.
Ngono ni agano. Ni maisha. Kwa kadri unavyoshiriki
ngono na watu tofauti ndivyo unavyojiingiza
kwenye maagano tofauti.SWAHILI

Ni maisha. Unapoanza kubadilisha wapenzi wengi


wa ngono unaingia maagano kadhaa. Ulihisi ni
dakika 10 au saa 1 ya furaha, hapana, ilikuwa saa
moja la agano zito. Ulipoingia kwenye agano,
iliwakamata watoto wako. Iliweka rehani maisha
yako ya baadaye. Imemeza maisha yako.

35
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Kuna watu wanajiona wana akili na wanatumia kila


aina ya uzazi wa mpango na kinga ili kuepuka
magonjwa ya zinaa wasijue wanapata mapepo ya
zinaa.
Uliepuka Magonjwa ya Zinaa (STD) lakini ukapata
Mapepo ya zinaa (STD). Haya mapepo hayazuiwi na
kinga au uzazi wa mpango

Hao mapepo Wanapitia raba (mpira) wanazoziita


kondomu – kondomu ni kipande cha nyenzo
kinachotumiwa na watu wawili wajinga –
mwanamke ni mjanja/mdanganyifu na mwanaume
suruali (mwanaume mjinga)

Najua watu, waumini, nasikitika kusema,


wafanyakazi kanisani ambao wamefungwa na
punyeto. Punyeto sio tamaa, sio hisia, ni roho
kamili. Kama nikisema “Kila mtu kanisani leta simu

36
MWANAMKE NA MAHUSIANO

yako”, utakachokiona kwenye simu za watu


walichopakua na wanachokitazama kitakutisha.

Kila unapotazama ponografia kuna mambo matano


hutokea:
I. Unashangilia dhambi
Mwanaume au mwanamke unayemtazama
hajaolewa, wanachofanya ni uzinzi au uasherati; na
wewe unaisherehekea. Unakubaliana na maisha
hayo. Kila unapotazama,
unaadhimisha/kuushangilia udhalimu. Wewe
unayeitazama, unakubali tendo la ndoa la watu
wawili ambao hawajaoana. Ni sawa na kusema
unaidhinisha uovu huo. Ndio maana unaitazama.

II. Unasababisha msongo wa mawazo


Hao wanawake/wanaume wote unaowaona
kwenye hizo movies, aina ya mwili walionao

37
MWANAMKE NA MAHUSIANO

itasababisha mawazo/msongo wa mawazo ukuingie


kwa sababu wewe sio kama wao (utaanza
kujihukumu hauna maumbile mazuri kama yao); bila
kujua kuwa miili yote hiyo ni matokeo ya upasuaji
sio miili yao. Wameitengeneza hivyo kwa upasuaji.

III. Wewe ni itikadi mbadala.


Unaongeza hamu ya kula kwa kutazama jinsi
wanavyofanya. Asili ya mwanadamu ni ya kudadisi.
Wanaume wameunganishwa kuchunguza.
Wanawake wanasukumwa na wanachofikiri.
Wanaume huguswa na kile wanachokiona.

Tamaa hiyo ya kuchunguza huanza kuingia kichwa


chako. Tamaa hiyo itaanza kukufanya utafute
mbadala kwahiyo hutaridhishwa na yeyote.

IV. Unazivutia roho za ajabu nyumbani mwako.

38
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Unawaza USHOGA na USAGAJI umeingiaje


majumbani mwetu ni hizi roho za ajabu ambazo
tumeziruhusu Kupitia sisi wazazi ndio tuna
mashoga, hivi hujiulizi mtu anapataje hisia za
kumuingilia kinyume na maumbile mwanaume
mwenzake Yaani anawezaje kuthubutu kama Sio
kuna roho zimemvamia Yaani unawezaje kufanya
mabusu ya midomo kwa midomo na mwanaume au
mwanamke mwenzio kama Sio mapepo haya na
maroho machafu.

V. Unajenga roho ya ukatili


Upuuzi wote unaoutazama kwenye hizo picha au
video za ngono haufanyiki kwa heshima. Ndio
maana unaona 90% ya wale wanaobaka ni waraibu
wa ponografia. Kijana anatembea barabarani, na
anamwona msichana wa miaka saba, na
kinachokuja kichwani mwake ni picha za vitendo vya
jeuri vya ngono ambavyo ametazama. Anaona hiyo
picha akilini mwake na mapepo yanaipa nguvu.
39
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Ibilisi anapotaka kumwangamiza mtu, ni kumpa


nafasi ya kushiriki mambo ya zinaa. Njia moja rahisi
ya kuharibiwa ni wakati shetani anakupa ngono ya
bure. Wewe ni kijana, unaona msichana mzuri, na
kabla ya kuzungumza naye anafungua miguu yake
kwako, na wewe unafikiri ni mjanja sana.
Wewe sio mjanja, alifungua tu miguu yake na
kukuonyesha moto wa kuzimu ili uingie.
Nilizungumza na kijana mmoja ambaye hakuwa
mzuri kivile kimwonekano bali alikuwa na
wanawake wanaomfuata kumtaka. Alionekana
kufurahishwa na jambo hilo, kwa hiyo nilimkaribisha
ofisini kwangu na kumjulisha kwamba ni roho za
majini zinazomfuata.

Walimtaka aendelee kuweka maisha yake kwa


wanawake hadi atakapoondolewa utukufu wake na
mali; mpaka afike mahali ambapo atakachoweza

40
MWANAMKE NA MAHUSIANO

kufanikiwa maishani ni kuwapa mimba wanawake


tu.

Kuna watu siku hizi hawajawahi kukutana na


mwanaume yeyote (vijana), vijana wa kiume ambao
ni bikira, wasichana ambao ni bikira lakini ni wapiga
punyeto (wanajichua).
Kwa hiyo Shetani anawaambia “Ah, hamjafanya
jambo kuu kwa hiyo haina shida”. Hapana!
Umeharibu maisha yako. Acha kufikiria kuwa
haujagusana kimwili, umeunganishwa kiroho.

Ninajua maaskofu ambao wamezungumza nami


kwamba wanateseka na ponografia. Ina maana
wao si watu wa Mungu? Bila shaka ni watumishi wa
Mungu. Ina maana wao ni watumishi bandia?
Hapana, sio bandia. Mungu aliwaita lakini kuna kitu
kiliingia.

41
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Ikiwa umefungwa na roho hii, Mungu akuokoe


haraka!

03.Filamu au tamthilia zenye mlengo wa kingono.


Watu wasiookoka si watu wabaya lakini hutumika
na shetani kuharibu nafsi ya mtu aliyeokoka na
kuamsha mapenzi kwa sababu mtu yeyote ambaye
hajaokoka huyo anatawaliwa yanavyotuambia na
shetani Kabisa kama maandiko

Wakolosai 1:13
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha
na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo
lake;
Hapo juu tumeona mtu aliyeokoka huwa
amehamishwa kutoka falme ya giza na kuingizwa
katika ufalme wa Mwana wa pendo lake yaani Yesu
Kristo hivyo tunapata ufahamu kuwa yeyote

42
MWANAMKE NA MAHUSIANO

ambaye hajaokoka anatawaliwa na kumilikiwa na


shetani sasa chochote anachofanya basi huwa
nyuma yake kuna msukumo au ushawishi wa giza
juu yao yaani wanakua mawakala wa shetani bila
hata kujitambua ndio maana waigizaji wa namna hii
huigiza na kuruhusu tendo la ndoa kuwa sehemu ya
maigizo yao na hapo sasa ndipo hutumika na giza
yaani shetani kuchochea Matendo ya zinaa juu ya
watu wa Mungu.

Mtu yeyote aliyebobea kwenye filamu au tamthilia


za aina hii hakika Maisha yake ya kiroho huwa
yanakua yapo hoi na ya kujikongoja yaani yanakua
hayana matokeo makubwa kama wewe umekua
mpenzi wa hizi filamu basi utanikubalia katika hili
kuwa tamthilia baadhi hutumika kama wakala wa
kupandikiza vitu vya zinaa kama kujichua,ushoga na
kadhalika, mfano wa tamthilia hizo ni kutoka nchi ya
ufilipino ni ngumu sana kukuta tamthilia zao hazina
mashoga yaani wanaume wenye mambo ya giza

43
MWANAMKE NA MAHUSIANO

sasa huu ni mpango Kabisa wa kuchochea Matendo


ya zinaa pia hata kuharibu matumizi ya asili ya
kihisia.

2 Petro 2:8
Maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa
kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku
baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;

Ni hatari kuona na kusikia Matendo ya zinaa kwa


sababu huleta kifungo cha mawazo ambacho
kinapelekea mtu kuendeshwa na shetani Kabisa.
2 Wakorintho 10:4-5
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina
uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,
kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka
nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

44
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Filamu na tamthilia za aina hii huleta kifungo cha


fikra ambacho kitahusika na kutawala hisia za mtu
na kuharibu Uwezo wake wa kujitawala kifikra na
kujitawala kihisia.

04.Mazungumzo mabaya.
Watu wengi wamepotea na kujiingiza kwenye
maisha ya zinaa kutokana na mazungumzo mabaya
Kupitia Mazingira, marafiki, na hata ndugu
wanaoishi nao.
Mazungumzo mabaya sio tu unaongea na kina nani
bali pia nini unasikiliza, taarifa gani unaifatilia,
kichekesho gani, au ukiwa na Simu unaangalia
whatsapp status za nani, hadithi za kimapenzi za
mtandaoni, una makundi gani ya whatsapp kwenye
Simu Yako haya yote ni mazungumzo unayofanya
kila siku na yanachochea kwa upana sana kuamsha
hisia zako za kimapenzi.

45
MWANAMKE NA MAHUSIANO

1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu
tabia njema.

Hata kama una tabia njema ila kama utakua


unafatilia sana hivyo vitu nikuhakikishie hizo sifa
unazopewaga kuwa una tabia njema zitaondoka
zote kama utakua unafatilia na kujihushisha na
mazungumzo mabaya na utaanza kuwa mtumwa wa
kihisia hasa za kimapenzi ambazo zitachochea
kufanya zinaa.

05.Hadithi/simulizi za mapenzi
Njia mojawapo inayotumiwa na shetani kukufanya
uchochee Mapenzi Kabla ya wakati wake ni hii na ni
hatari sana hii, hata mimi Kabla ya kuokoka nilikua
nasoma kwenye magazeti hizi simulizi yaani
zinatengeneza picha halisi kabisa ya mdada au
mkaka

46
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mfano; utasikia nilipomuona akiwa na nguo


iliyolowa maji mwili wangu ulisisimka

Niishie hapo hii ni njia hatari sana si tu inaleta picha


ila inaamsha hisia zako na haiishii hapo
inasababisha wengine kuvamia na maroho ya
uasherati na zinaa.
Hii inaendana na kule kuwasiliana na mkaka huku
mnaulizana umelala utasikia ndio utasikia umevaa
nguo gani utasikia ya buluu utasikia hivi
ningekuwepo hapo unafikiri ingekuaje niishie hapa
tu, aisee mazungumzo ya aina hii yanakupeleka
kwenye vitendo vya uasherati Wanaume na wadada
wengi Kupitia haya mambo imewapelekea kujichua.

Nyingine ni ile hali kukumbatiana kule kunakoleta


msisimko mdada unakumbatia mkaka mpaka matiti
yako binti yanajibana kwenye kifua cha mkaka na
unataka upone labda kama umezoea uasherati ila

47
MWANAMKE NA MAHUSIANO

binti ambaye hajawahi kabisa hayo mambo ni


shahidi yaani unasikia moto wa hisia unaamka
haraka sana, binti bora uonekane mshamba katika
hili ila sio uzungu unaoangamiza roho yangu Kamwe
usifanye hivyo ni hatari kwako.

48
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA TANO
TUNAWEZAJE KUWA NA USAFI WA KINGONO
KWENYE MAHUSIANO YANAYOELEKEA NDOA?
Ukitaka uwe salama na uwe na usafi wa kingono
wakati wa mahusiano yanayoelekea Ndoa mambo
yafuatayo uyaepuke
a) Kuzitafakari/kusikilizia hisia za mwili-Inahusisha
ufahamu wenyewe
Biblia imetuagiza tuyatafakari yaliyo juu-Wafilip 4:8.
Mungu alijua tukiyatafakari ya chini yakiwemo
tamaa za mwili tutachochea mapenzi.
Hizi hisia ni lazima zije na nina kushauri zikija ingia
hata mfungo siku zote hasa za period na jiepushe
kuongea na huyo mkaka umpendaye au jamii yote
ya wakaka hasa unaowaona ni wazushi na Wana
mambo ya kihuni.
Binti mmoja akaniambia Kuwa akiwa yuko na hisia
huwa anamtafuta mkaka ambaye ana hisia naye
anasema akiongea huwa anaona afadhali kidogo

49
MWANAMKE NA MAHUSIANO

lakini nikamwambia niambie ukweli akasema Kuwa


akiongea nae ndo huwa anasikia hisia zinaamka
zaidi na jamaa akikata simu yeye huwa anapata
tabu zaidi Aisee nikamwambia usifanye hivyo tena
ni hatari kwake hasa atakapokutana na wanaume
washenzi, hivyo basi hali hii ikikutokea nakushauri
usiongee na huyo mkaka umpendaye ila siku hiyo
nakushauri ingia mfungo walau masaa 12 tu na
utakua sawa.

i) Usijiulize maswali ya kipuuzi mf. ‘Hivi, tutafika


kuoa au kuolewa bila kuonja? Wenzio walioonja
wamekuwa watumwa wa dhambi hiyo kujitoa ni
gharama kubwa wengi wameshindwa kuilipa,
usiwaze kuonja hadi NDOA.

ii) Baridi imezidi/Upweke jamani niko peke yangu.


Ulitaka uwe na nani? Haya ni majira ya Bwana
yenye kusudi timilifu uwe peke yako, wakati wa

50
MWANAMKE NA MAHUSIANO

kuwa 2 na watakapokuja hao wa kike na wa kiume-


utakuja tu, vumilia.

b)Kusoma makala za mapenzi [makala za Internet,


magazeti, vipeperushi, vitabu]-inahusisha macho
yanayosoma makala.
• Unashangaa binti au kaka anasoma vitabu vya
tendo la ndoa/Mapenzi.
• Internet Café anaenda kutazama mambo ya
Ngono/Mapenzi. n.k.
Kijana huyu atakuwa salama kweli au ndio hao
mwisho anabaka mtu na wengine wanabaka hadi
wanyama na mabinti wengine hubaka vijana wa
Kazi hapo kwao.

c) Kutazama mambo ya ngono au yanayohusu


ngono-inahusisha macho.

51
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mikanda ya x, sinema za x, picha za x hasa kwa


internet na hata ‘live’ kuna watu wanapenda
kuchungulia sehemu zenye upenyo wa kufanya
hivyo. Raha yake aone tu utupu wa watu na
mchezo unavyokwenda, atapona?
Huyu ni mfano wa swala anayeingia katika geto la
simba Wenye njaa kali hawezi kupona ni suala la
Muda tu lakini huyu hawezi kupona kabisa.

d) Kushika au kushikana/kugusana-inahusisha
ngozi-Wakolosai 2:21.
• Mkono unaganda dk.5 dada na kaka
wanasalimiana salamu yetu.
Mkono wako una chapa ya Yesu usiruhusu kujinajisi
kwa kutii mwili.
• Vidole vinaongea kwa kupapasa au kubonyeza
au kutekenya ni uchochezi.

52
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Vidole vyako vinachapa ya Yesu, usiruhusu kujinajisi


kwa mambo hayo.
• Tongue Kiss/Denda ni hatari wala mtu
asijifariji kuwa salama-usionje.
Ulimi wako unachapa ya Yesu usionje uchafu [mate]
subiri Ndoa utanyonya mpaka uchoke ukitaka
maana utakuwa huru katika hayo si leo kwenye
ndoa utakunywa hata jaba la mate yake na
akikusumbua sana oh tubadilishane mate kidogo tu
basi tafuta chupa tema mate mule mpaka yajae
alafu mpe kwenye hiyo chupa anywe yamdomoni
asubiri akikuoa.
• Ngozi ikisikia umeshika/kwa, unapapasa/swa,
umekula denda, lazima itashtuka na kuleta hisia ya
kuvutwa katika ngono kwavile wewe ni kijana.
Usiidhalilishe Chapa ya damu ya Yesu uliogongwa
siku ulipookoka, itunze.

53
MWANAMKE NA MAHUSIANO

e) Kusikiliza mambo/maneno ya ngono au


yanayohusu ngono-sikio.
Sikio lako linachapa ya Yesu usilisikizishe uchafu
wowote-ni kichocheo.
Kusikia ni sikio kupata jambo bila kukusudia lakin
kusikiliza ni kukusudia. Hata kama sikio limenasa
uchafu kwa bahati mbaya hakikisha unalitoa.

f) Kuongea mambo ya ngono au yanayohusu


ngono-inahusisha mdomo.
• Mazungumzo ya Mdomo ni hatari-Mithali
6:26; 7:16-18,21. Iko nguvu katika
midomo/maneno. Biblia inasema Maneno huzaa
uhitaji na sura hiyo hiyo ya 6, inashauri jiepushe na
midomo ya malaya; Kwa maneno alimshinda-si kwa
mtutu, si kwa ‘hug’ wala busu ni maneno tu na
akamshinda. Usiruhusu kupokea maneno hata ya
mzaha kuhusu ngono.

54
MWANAMKE NA MAHUSIANO

• Mawasiliano katika Simu ni vema kuangalia


sana unavyoenenda.
Idadi ya “Call au Sms” mfano kutwa mara tatu
unampokea Fulani.
Simu inazidi ‘dose’ ya Panadol kutwa mara tatu
yeye mara tano.!!
Muda wa “Call au Sms” mfano usiku sana au alfajiri
ni kichocheo.
Usiruhusu Simu za usiku wa manane/alfajiri hata
kwa manadai ya kuamsha ktk maombi kwa muda
huo ataamsha na vingine si maombi tena!
Sauti ya “Call” kuna sauti za uchochezi mfano
kulegeza, kuguna, kutetemesha sauti, sauti kama
analia na nyinginezo kwa kijana utajua tu.

• Mazungumzo “Simu au meseji” yakihusu


ngono ni uchochezi sana.

55
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mambo hayo juu hata kama mtu hajaweka neno la


kimapenzi/kimahaba ni kichocheo, Je, mazungumzo
yenyewe hayo ni hatari zaidi mara 100.
Biblia inaonya mazungumzo mabaya yanaharibu
tabia njema-1Kor 15:33.
Mfano: Naskia baridi njoo basi unipe joto, wewe
umekuwa ‘heater’?
Najiona mpweke ‘lonelyness’ afadhali uje hapa
nichangamke. Kweli wewe una Baba, Mwana na
Roho Mtakatifu bado mpweke?
Ukiyachekea hayo, hutaki kuyakemea, anaongeza
‘dose’ sasa utaambiwa wazi zaidi ‘nina nyege, ni
wewe wa kutoa nyege zangu’

g) Zawadi ni moja kati ya vichocheo vya mapenzi


kwa namna hii.
• Size ya zawadi - Ukubwa, zawadi ya
thamani kubwa. Itaua msimamo.

56
MWANAMKE NA MAHUSIANO

• Idadi ya zawadi - vitu tele unapokea au mara


nyingi-utalipa tu.
• Aina ya zawadi - Kitu gani unapokea-chupi?
Zawadi hiyo itaongea tu.
Tunaishi zama za uovu, usanii na malaghai mpaka
Kanisani wa kike/kiume wao wanajua kuipaka asali
nia yao ili usishtuke mapema mpaka umefika chini,
zawadi ni chambo kukunasa we. Hutaki Kanuni hii
yatakayo kupata usilie.
Wachumba: Vijana hawa wako huru kutoa/kupokea
zawadi ila Kanuni ni hizo hizo hapo juu. Uchumba si
Ndoa muda huo bado unaendelea kumthibitisha
Mungu, usije kuishia njiani ukalilia mtu na vitu
vyako.

h) Picha na Mikao ya Picha kwa jinsia mbili ni


Kichocheo cha Mapenzi.
• Picha za nusu uchi eg. Kifua/Tumbo/Mapaja
wazi au chupi/sidiri tu.

57
MWANAMKE NA MAHUSIANO

• Picha za utupu [mwili wote], picha hii hana


nguo hata moja-ni kichocheo.
• Picha na Mikao yake inavunja miiko ya jinsi ya
kuenenda Vijana waaminio.
‘pozi’ la Kushikana Mabegani, Kushikana Viuno,
Kushikana Kifua mtu anajikuta ameshika matiti
katika pozi la picha, Kushikana Makalio, Kubusiana
Shavu au Mdomo, Kupakatana/Kukumbatiana ni
KICHOCHEO. Kijana usikubali Kuidhalilisha Chapa ya
Yesu kwa pozi la Picha.

i) Mavazi ya Vijana wa Kike na Kiume


yanavyokuwa Kichocheo.
• Mavazi ya Kuonesha Nguo za Ndani-Milegezo,
Vifungo wazi, Mipasuo n.k.
• Mavazi ya Kuonesha Maungo/Maumbile-
Kubana sana inachora umbile, Kuangaza
[transparent] inaonesha viungo vyote japo kavaa, ni
vichocheo.

58
MWANAMKE NA MAHUSIANO

• Mavazi ya Kutositiri Mwili-Nguo fupi-


pensi/bukta/skert/gauni/blaus, Nguo hizi huacha
Kifua wazi, matiti nje, Kitovu nje, Tumbo nje, Kiuno
nje, Kwapa nje-ndio unakuta kijana haabudu
anachungulia titi kupitia kwapa.

• Ni maombi yangu mavazi hayo yasivaliwe


nawe unayesoma kitabu hiki. Ni maombi yetu
uushinde mwili, endapo utakutana na mavazi hayo
kazini, shuleni, kwenye daladala, barabarani,
dukani, sokoni na hata Kanisani kwa Waongofu
Wapya au Wakongwe wenye mitazamo tofauti.
Utaona hatuwezi kuepuka hili moja kwa moja kwa
jamii yetu ila tumejifunza ili ukiona mavazi hayousi-
‘take advantage’, usikodolee macho mpaka mate
yanatoka huna habari ni hatari kwa afya yako,
epuka.

59
MWANAMKE NA MAHUSIANO

j)Mazingira hatarishi/njia kuu ni Kichocheo - Mithali


7:7-13a, 21-23.
Njia Kuu ni mahali pa Kificho, Gizani, Uchochoroni,
Chumbani, Ufukweni, Kuwepo wawili tu mnataka
kufa maana mazingira tu ni kichocheo tosha.
Kabla ya kugusana, mabusu, zawadi, mazungumzo
vyote hivyo bado, ile kuwa wawili tu maeneo hayo
ni kichocheo tosha na kinaongea kwa kasi.

Kijana mmoja mjinga yeye alizubaazubaa NJIA KUU


yaliyomkuta ni balaa.
Tunapomalizia kichocheo cha 10 cha mapenzi hebu
tusome andiko hilo.
Kijana huyu alitembea muda hatarishi kwa kijana,
akakaa mahali hatarishi, akakutana na mtu hatarishi
[kahaba], akaambiwa maneno hatarishi, akanaswa.
Mithali 6; inatoaushauri kuwa jiepushe na maneno
ya Malaya n.k. ndipo sura ya 7; inaonesha kwa
maneno ya ubembelezi tu kahaba akamshinda

60
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Kijana kiulaini kabisa akaongoza njia kama Ng’ombe


aendavyo machinjioni uhitaji umeshapamba moto,
mfalme amesimamisha majeshi hayarudi chini,
anaona nikidhi tu uhitaji wa mfalme nisalimike,
kumbe maskini anaiangamiza nafsi yake ya thamani-
Marko 8:34-35.

Tunaishi zama za uovu makahaba wa kike/kiume


wapo Kanisani pia. Makahaba hupenda NJIA KUU
soma Ezekiel 16:22-26. Ni mahodari wa ubembelezi,
kwa kiroho cha kusuasua cha kutozingatia mipaka
ya uhuru wetu, hutoki, utalainika mwenyewe na
utajikuta unaongoza njia kama kijana mjinga. Epuka
mazingira hatarishi, kuna kisa kilitokea Kanisani
mkesha wa Vijana wa Maombi ya masaa 48. Kaka
kamfata dada anamwambia “nina nyege na wewe
ndio wa kutoa nyege zangu” Ikiwa mkesha wa
maombi kuna watu wanamawazo hayo, je, huko
njia kuu?

61
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Haya ni baadhi ya mambo ya kuepuka ili usichochee


Mapenzi.

“MWANAUME AMBAYE HAJAKUOA NA


UNAMPENDA ANALINDWA KWA KUNYIMWA SEX
KABLA YA NDOA”

62
MWANAMKE NA MAHUSIANO

SURA YA SITA
USILOLIJUA KUHUSU MWANAUME
Unahisi unamjua mwanaume ni nani? Jaribu kuwaza
tena. Zaidi ya asilimia 75 ya migogoro ya mahusiano
baina ya wenzi ni matokeo ya tafasiri isiyo sahihi ya
hulka na vitendo vya wenzi wao.
Tuanze ni kitu kinaitwa UANAUME NDANI YA
MWANAUME
Au
ASILI YA UANAUME KWA MWANAMUME
“UIMARA WA MWANAUME UPO KATIKA UTU WAKE
WA NDANI SIO KATIKA UTU WAKE WA NJE”

UANAUME WA MWANAUME hautokani na sura au


six packs ila UANAUME Wake unatokea ndani vile
anavyojiona

63
MWANAMKE NA MAHUSIANO

UANAUME WA MWANAUME NI ILE PICHA YA


NDANI YA MWANAUME HUYO JINSI ANAVYOJIONA

Mwingine anaona Yeye ni mwanamume pale tu


anapofanya zinaa ndio maana atapambana alale na
wadada wengi Wengine anajiona mwanaume pale
tu anapopiga mkewe mwingine anaona ni
mwanaume pale tu anapokua na wadada wengi
Kwenye mahusiano ndo anajiita kidume cha mbegu
na mwingine anaamini UANAUME Wake unaanzia
pale anapofanya kazi Yaani anavyopambana ndo
unasikia sifa ya mwanaume ni kazi bhana mwingine
anaamini UANAUME Wake ni pale anapokua na
hela tu ndo anajiona Yeye ni mwanamume ndo
unasikia mwanaume pesa bhana mwingine anajiona
mwanaume pale anapoona wadada wanateseka
kwa ajili yake sasa chanzo cha mahusiano mengi
kuyumba ni pale unapohusiana na mtu na
kushindwa kujua HUYU mwanaume nini kinamfanya
ajione mwanaume

64
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Mwanamke kwa bahati mbaya hauwezi


kuutengeneza UANAUME WA MWANAUME ila
unaweza ukaupaka rangi na kuupendezesha kama
ujuavyo kuwa TABIA ZA WATU ZINAJENGWA
MTOTO AKIWA NA MIAKA 4 MPAKA 13 baada ya ni
matokeo ya kile kilichopandwa miaka mingi nyuma
Kuna watu wengi sana hufikiri utampa mwanaume
tendo la Ndoa Ili atulie alafu huyo mwanamume
hatulii kwa sababu sio tu tendo la ndoa ndio
linalomfanya ajione mwanaume

Mwanaume haingii Kwenye mahusiano sio tu kwa


sababu ya ngono bali huwa wanaingia Ili wajione
wao ni Wanaume ndio maana kuna watu wanatoa
ngono lakini bado wanachitiwa ndo husema mbona
nimejitoa kila kitu nimempa mpaka Mwili lakini
hatulii kwangu kwa sababu sio ngono pekee ndo
inamfanya ajione mwanaume kwa sababu Wengine
mnapa ngono lakini we ni jeuri, muongo, sio
msikivu, huna utulivu kabisa
65
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Sasa kimbembe ukimpata mwanaume ambaye


ameumizwa Yaani unakua na mzigo mkubwa wa
kuponya UANAUME WAKE ULIO NDANI YAKE

MWANAUME anajali sana Moyo wake(siri) zake


kuliko Mwili wake na wanawake wanajali sana miili
yao kuliko wanavyothamini mioyo (siri) zao ni rahisi
mwanamke kumueleza bodaboda ugomvi wake na
mumewe lakini ni ngumu kumpa Mwili ndio
wanawake wengi ni wambeya ni ngumu
Mwanaume kutoa siri zake kwa sababu ukijua siri
zake utamtawala Mfano samson na delila hivyo sio
rahisi kukupa siri zake, na ishara mojawapo ya
mwanamume kuwa amekupenda na ni dhaifu
kwako ni kukupa siri zake za ndani ni kama vile
unavyohitaji utumie nguvu ili mwanamke akupe
Mwili wake Maana mwanamke akikupa Mwili wake
anakua dhaifu kwako ndivyo kwa mwanamume

66
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Na njia ya haraka au kipimo cha haraka


wanachotumia Wanaume kukuamini na kukupa siri
zake hata kama anakupenda na kukujali ni pale
anapokuambia mambo ya ujinga/upuuzi au ya
msingi sana je unamchukuliaje je unareact vp

Hivi si unajua kama nyie wadada mnaweza


mkafunguka siri zote kwa mtu ndivyo mwanaume
anaweza akakupa sex na mkawa Kwenye mahusiano
lakini asikupe siri zake

Ndio maana kuna watu wanaongea na ma-ex wao


vizuri na kuwaomba mpaka ushauri na kuwaambia
siri zao kuliko wewe uliyenae huu ni ukweli
mchungu

67
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Ukitaka kumkamata na Mwanamume jifanye kama


umejisahau we m-support sana huyo mwanamume
na akiona unamsupport hivyo kidogo unajifanya
unaulizia huduma yake, kazi yake imeendaje, m-
support shabikia hata mpira kishikaji muulize
ameangalia mechi ya simba na yanga mjue mpaka
mayele Yaani muongee Lugha Moja oya huu ni
unyama wa kumtia unyamani mtoto wa mwanamke
mwenzio
We jifanye kama hauna wivu sio kidogo tu ulikua
unaongea na nani mbona kimya unanisaliti eeehh

Kuna jamaa alimpenda Binti kwa kuwa kila safari ya


huduma binti anampeleka na bolt mara mbona Uko
online unatakiwa upumzike kesho una ratiba ngumu
ujue aisee jamaa alimpenda automatically

Niongezee kitu mwanaume anapenda masifa sio tu


Sifa bali masifa Yaani usiishie kusema umependeza

68
MWANAMKE NA MAHUSIANO

bali sema ukivaaga nguo fulani unapendeza Yaani


ukiwaga hivi ni nouma au Yaani unavyoongeaga ni
nouma Yaani nakuahidi atakua kula siku anavaa
nguo za namna Hiyo mwanaume anasifiwa kwanza
Ili apendeze Hiyo upendeza anapopewa Sifa fulani
pia Mwanaume anapenda mwanamke Ambaye
anajifanya sio mjuaji kwake na yule ambae akihitaji
msaada anaenda kwake aisee mwanaume yupo
hivyo.

69
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Vitabu vinginevyo vilivyoandikwa na mwandishi.


✓USICHOCHEE MAPENZI

✓KIJANA ALIYEOKOKA NDANI YA BABILONI

✓MAHALI PA SIRI PA MUNGU

✓UELEWE ULIMWENGU WA ROHO

✓USIMZIMISHE ROHO MTAKATIFU

✓SAFARI YA MTUMISHI WA MUNGU

✓RAFIKI YANGU ROHO MTAKATIFU

✓SIRI YA KUNENA KWA LUGHA

✓KUHUSU MALAIKA

✓SIRI YA MUZIKI

✓TUNDA LA ROHO

✓ROHO SABA ZA MUNGU

✓KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

✓MIMI NI MWANAMKE

✓NIPO SINGLE

✓KUTUMIKA CHINI YA MTUMISHI WA MUNGU

✓UPONYAJI WA MOYO ULIOUMIZWA

✓ KUVUNJA MADHABAHU ZA UKOO

✓MWANAUME HALISI

✓ SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI

70
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Kwa Mawasiliano Na Kujifunza Zaidi

Ikiwa umeguswa na ujumbe wa kitabu hiki, una swali,


una Maoni, ushauri, ushuhuda au unahitaji vitabu
vingine, Unaweza kuwasiliana moja kwa moja na
mwandishi;

PAULO EVARIST KOBA.

Kupiga & meseji: +255 783 428 460, +255 673 428 461

Barua pepe: paulokoba395@gmail.com

Pia unaweza kupata mafundisho zaidi kutoka kwa


PAULO EVARIST KOBA kupitia;

Barua pepe: paulokoba395@gmail.com

Facebook: EVARIST KOBA

Instagram: paulo_evarist_koba12348

WhatsApp: +255 783 428 460

71
MWANAMKE NA MAHUSIANO

Ungana nami Kuwahudumia Wengi

Shauku kuu ya mwandishi PAULO EVARIST KOBA ni


Kuona watu wengi wanafikiwa, wanabadilishwa na
Kuinuliwa kwa kweli iliyojengwa juu ya msingi wa
neno la Mungu.

Unaweza kuungana nami kuhakikisha Dunia inajazwa


maarifa ya Mungu nisaidie Ili yawe na uhalisia kwa
Maombi yako, mali yako na fedha yako kwa ajili ya
kutiwa nguvu na kwa ajili ya bando.

Ikiwa umeguswa kufanya chochote tafadhali tumia


vyanzo Vifuatavyo kufanya jambo na Mungu
atakubariki.

Tigo Pesa: +255 673 428 461 (Philomena)

Airtel Money:+255 783 428 460 (Philomena )

Mungu akubariki kwa utoaji wako

72
MWANAMKE NA MAHUSIANO

KUHUSU MWANDISHI
Naitwa Paulo Evarist Koba nimeokoka na nampenda sana YESU,
Muhitimu wa ngazi ya astashahada pale kwenye chuo cha
ufundi cha DIT.
Niliokoka Mwaka 2014 nikiwa kidato cha tatu huko shuleni
nilipokua nasoma elimu ya sekondari, tangu hapo Maisha
yangu yamebadilika kabisa.
Ninaabudu kanisa la Gilgal Revival Church pia ni mtoto wa
kiroho wa mchungaji Paulo Israel Shaban.
Haya maarifa nimejifunza Kupitia kwa Baba yangu wa kiroho
Askofu Paul Israel Shaban na watu kama Bishop Kabigumila, na
mchungaji Peter Mahenge, na Mwl Christopher Mwakasege.
Kama umeguswa na huduma hii na una ushuhuda kuhusu hiki
kitabu basi karibu kwa namba za hapo chini pia unaweza kutoa
sadaka Yako Ili kutoa sapoti karibu kwa mawasiliano ya hapo
chini pia kwa ushauri na msaada wa kiroho karibu sana kupitia
Email ifuatayo paulokoba395@gmail.com na mawasiliano ya
0783428460 au mitandao ya kijamii nitafute kama Evarist
Koba.

73

You might also like