Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 5

JARIBIO LA MWEZI KIDATO CHA TATU

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU


Saa: 3:00 Februari 2024.

Maelekezo
1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (11).
2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali mawili kutoka
sehemu C.
3. Andika Jina lako kamili katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia.
4. Simu za mkononi na VYOTE VISIVYOHUSIKA NA MTIHANI haviruhusiwi
katika chumba cha mtihani.
5. Soma vizuri maelekezo ya kila swali kabla hujaanza kujibu.

Mtihani huu una jumla ya kurasa tano (5) zenye maandishi

Ukurasa wa 1 kati ya 5
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika kipengele (i) – (xv), chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake
katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Elimu yenye manufaa kwa mujibu wa Uislamu inakuwa na sifa gani?
A. Inahusisha Dini na dini B. Inafundisha ya Dunia na Akher
C. Inawezesha kufanya ibada D. Inasababisha kupata ajira
E. Inatoa ujuzi na marifa

(ii) Kundi lipi linaonesha vigawe sahihi vya Tawhid?


A. Uluhiyyah, Rububiyyah na Asmaaiyya.
B. Swifatiyya, Uluhiyyah na Rubbuubiyyah
C. Uluhiyya, Asmaai waswifat na Ibadah
D. Uluhiyyah, Rububiyya na Asmaai waswifat
E. Rububiyyah, Asmaaiyya na Swifaatiyya.

(iii) Kwanini Wahyi ni njia muhimu kwa watu kumjua Mwenyezi-Mungu


(S.W)?
A. Ni njia pekee ya kumjua Mwenyezi –Mungu (S.W)
B. Ni njia ambayo haiwezi kubadilishwa kimaana.
C. Ni njia ya kwanza iliyopo moyoni kwa watu
D. Ni njia inayofafanua wazi itikadi sahihi kwa watu
E. Ni njia pekee iliyotumiwa na Mtume (S.A.W)

(iv) Kwanini sio sahihi kuitafsiri Dini kama “Njia ya mahusiano kati ya
mwanadamu na Mungu?”

A. Zipo njia nyingine za kuhusiana na Mungu tofauti na dini


B. Tafsiri hiyo imetolewa na jamii ya wasiokua Waislamu
C. Tafsiri hiyo inaonesha kuwa, dini ni hiyari kwa wanadamu
D. Mwanadamu anahuiana na Mungu kieoho na haitaji dini
E. Tafsiri hiyo inaonesha kuwa dini ni lazima kwa wanadamu

Ukurasa wa 2 kati ya 5
(v) Ibada ya Zakat na Sadaka inzingatia mambo mengi katika utekeleaji
wake isipokuwa
A. Kutoa vilivyo halali C. Kutoa vilivyo vizuri
B. Kutoa mwezi wa D. Kutoa kati kwa kati
Ramadhani E. Kujiepusha na Ria

(vi) Kwa namna gani Uislamu unamuwezesha muumini kuwa katika


ibada wakati wote wa maisha?
A. Umelezimisha kutekelezwa kwa nguzo tano za Dini
B. Dhana ya ibada inahusu kila jambo katika Uislamu
C. Katika Uislamu kuna nguzo za Imani
D. Uislamu umeondoa uhuru wa watu kupumzika
E. Kuna majengo ya ibada za Waislamu katika nchi zote.

(vii) Anapaswa kufanya nini mtu anayemsalia maiti baada ya Imam kuleta
Takbira ya tatu?

A. Kumuombea maiti D. Kutoa salamu


B. Kusoma Surat Fat’ha E. Kusoma Sala ya Mtume
C. Kutoa Salaam

(viii) Ufafanuzi wa mafundisho ya Uislamu kwa mujibu wa mabadiliko ya


mazingira na wakati ni matokeo ya kutekelezwa kwa msingi gani wa
Sharia?
A. Ijtihaad D. Hadithi
B. Qur’an E. Qur’an na Sunnah
C. Sunna na Hadithi

(ix) Ni kwa muktadha gani dhana ya Hadithi inafafanuliwa kama jambo


au kitu kipya, taarifa au hotuba?
A. Katika mazingira ya kisheria
B. Kihistoria
C. Katika mazingira ya kilugha
D. Kimatumizi
E. Katika kuifafanua Sunna

Ukurasa wa 3 kati ya 5
(x) Mafundisho gani mahususi yanayopatikana katika Suratul – Ikhlas?
A. Shetani ni adui mkubwa wa mwanadamu
B. Kuna shari katika giza la usiku linapoingia
C. Uislamu ni njia sahihi ya maisha
D. Kazi kubwa ya Shetani ni kutia wasiwasi moyoni
E. Allah (S.W) ndio jina la dhati la Mwenyezi – Mungu

2. Oanisha Funga za Sunna zilizopo katika Orodha A na majina ya Funga hizo


katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwa kila kipengele
katika kujitabu chako cha kujibia.
ORODHA A ORODHA B
(i) Kufunga tarehe 12, 13 na 14 A. Funga ya Ashura
katika miezi ya Hijriya B. Funga ya kafara
(ii) Kufunga tarehe 9 katika C. Funga ya Nabii Mussa
mwezi wa Dhul Hijja. D. Funga siku nyeupe
(iii) Kufunga kila baada ya siku E. Funga ya Nabii Dawud
moja. F. Sitta Shawwal
(iv) Kufunga tarehe 10 katika G. Funga ya Araf
mwezi wa muharram H. Masiku meusi
(v) Funga muakkada kila mwezi
wa 10 Hijriya.
(vi) Kufunga kila baada ya siku
moja.

Ukurasa wa 4 kati ya 5
SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. (a) Mfahamishe ndugu yako Bainisha nyakati tano zilizoharamishwa


kuswali swala za Sunnah

4. (a) Tumia hoja tatu kumbainishia rafiki yako tofauti iliyopo kati ya zakat na
sadaqat.

(b) Bainisha mambo matatu ya kuzingatia ili ibada ya utoaji wa zakat na


Sadaqat ikubalike.

5. Ainisha makosa mawili yaliyotajwa katika surat Mau’n ambayo muumini


anapaswa kuyaepuka.

6. Bainisha vigezo sita utakavyovitumia kutambua hadithi ya uongo kwa


kuangalia Matni yake.

7. Eleza tofauti ya istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika fani ya Hadithi


a) Isnad na Matin
b) Riwaya na Rawi

8. Kwa kurejea Maisha ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam)


eleza matukio mawili yanayothibitisha kuwa mitume huandaliwa kuwa
Mitume kabla ya kupewa utume.

SEHEMU C (Alama 30)


Jibu maswali mawili tu.
9. Eleza mambo sita ambayo Mtu aliyefunga akiyafanya anaweza kujiona kuwa
amefungua lakini kisheria bado hajafungua.
10. Qur an ni maneno matakatifu ya Allah ambayo msomaji wake lazima awe na
adabu wakati anapoyasoma. Ainisha mambo matano anayopaswa kuzingatia
msomaji wa maneno hayo.
11. Chambua vigezo vinne utakavyovitumia kutambua hadithi ya uongo kwa
kuangalia isnad yake.

***Wabillah Tawfiq***

Ukurasa wa 5 kati ya 5

You might also like