Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 22

Muhtasari wa Matukio Katika Riwaya

Riwaya inapoanza, mhusika mkuu, Mangwasha, yuko na wanawe wawili, Sayore na Kajewa, katika
kanisa fulani, ambapo wanajificha. Nje ya kanisa hilo, wapo watu wengine wa kabila la Waketwa
waliokimbilia usalama hapo baada ya makao yao katika eneo la Matango kuchomwa.

Kuna fununu kwamba jamii ya Waketwa inafurushwa kutoka makwao kwa sababu kuna watu fulani
wanaotaka ardhi ya Matango kwa nguvu.

Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anachukia kabila la Waketwa kwani yeye anatoka katika kabila la
Wakule. Waketwa na Wakule wana uhasama wa tangu jadi. Inabainika kuwa Lonare, ambaye ni kiongozi
wa Waketwa, ana umaarufu mkubwa nchini. Katika uchaguzi mkuu uliopita,angeshinda lakini alitekwa
nyara kabla ya uchaguzi na kwa sababu hiyo, Mtemi Lesulia aliishia kuchaguliwa bila kupingwa.

Mangwasha ni mwanamke mwenye bidii, na anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu Mshabaha.
Chifu huyu ni rafiki mkubwa wa Mtemi Lesulia, naye pia anawachukia Waketwa. Hivyo, anapanga
kuwadhulumu Waketwa, jambo ambalo Mangwasha analifahamu kutokana na kufanya kazi katika ofisi
yake ambako njama za kuwadhulumu hupangiwa. Chifu Mshabaha pia ni rafikiye Sagilu. Mzee huyu
anataka kumuoa Mangwasha licha ya kwamba anajua msichana huyu ana mchumba, Mrima, na kuwa
wanapanga kufunga ndoa. Siku ya harusi ya Mangwasha na Mrima, Sagilu anamtuma kimada wake,
Sihaba, akiwa na bomu lililofungwa kama zawadi kwa maharusi. Kwa bahati nzuri, Mrima anamshuku na
kuagiza asiwakaribie. Kwa hivyo, maafa aliyokusudia kufanya hayafanyiki. Mbinu hii ilipofeli, Sagilu
anamnyemelea Mrima baadaye na kumzuga kwa kutumia pesa. Mrima anaanza kulewa, kuponda mali
kwa kiasi kwamba anaisahau familia yake, huku akimwachia Mangwasha jukumu la kuwalea wana wao
wawili. Mrima anaishia kuwa mlevi kupindukia kutoka Ponda Mali hadi akaishia Majaani alipookolewa
na mkewe na akina Lonare alipokuwa amepotelea.

Nchi ya Matuo inakumbwa na matatizo mengi. Kuna matatizo ya kiuchumi yanayosababishwa na


uongozi mbaya na ufisadi uliokithiri. Mtemi Lesulia anaendeleza ubaguzi dhidi ya Waketwa na vijana
wengi wa jamii hii walio na elimu hawapati kazi za kujiendeleza kimaisha. Kwa mfano, uteuzi wa
wagombea nafasi za uongozi ukiwa umekaribia, machifu wanalazimishwa kuwahamisha Waketwa kutoka
Matango ili viongozi wanaopendelewa na mtemi wasipate upinzani. Mbinu hii ingemfanya yeye-Mtemi
Lesulia-asishindwe na mpinzani wake mkuu wa kisiasa, Lonare. Sihaba anatumwa kwenda kuhakikisha
kwamba makazi ya Waketwa yameteketezwa, anawatumia vijana ambao wanatumia petroli kuchoma
makazi hayo. Lonare na wafuasi wake wamepeleka kesi mahakamani, naye Mangwasha akiwa na
wenziwe, wanawashawishi watu kurudi katika makao yao ya zamani kule Matango ambako wanakita
mahema. Hata hivyo, siku ya tatu, vijikaratasi vinasambazwa kuwataka watu watoke kwenye ardhi hiyo
ambayo inabainika imetwaliwa na kupewa Nanzia, mkewe Mtemi Lesulia, na rafikiye mtemi, Mbwashu.
Wawekezaji hawa walinuia kujenga jengo la kibiashara katika ardhi hiyo ya Matango. Watu wanaokuja
kuanza ujenzi wanafukuzwa na Waketwa walioamua kuitetea ardhi yao kwa vyovyote vile.

Baadaye, Mtemi Lesulia anamtumia Sagilu kumpa Mrima pesa nyingi pamoja na ahadi kwamba atapewa
kazi serikalini, ilimradi amfanyie Mtemi Lesulia kampeni na kuwaendea kinyume Waketwa pamoja na
wapinzani wa serikali.

Kipindi kifupi kabla ya uteuzi wa watakaopeperusha bendera za vyama mbalimbali, Sagilu anatofautiana
na mwanawe Mashauri, baada ya mwanawe kugundua kwamba babake ana uhusiano wa kimapenzi na
mpenzi wake, Cheiya. Mtemi Lesulia naye anakosana na mwanawe, Ngoswe, wakati anapanga njama ya
kuvuruga zoezi la uteuzi ili kuwaharibia wapinzani wake nafasi za kuteuliwa. Ngoswe anaona kwamba
hatua ya babake inaongozwa na ubinafsi wa kujitakia uongozi na kutojali kwamba baadhi ya watu huenda
wakapoteza maisha yao katika vurugu anazopanga. Sagilu anashindwa katika uteuzi na inakuwa wazi
kwamba Mtemi Lesulia atakuwa na upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Kwa ushawishi wake, Chifu Mshabaha anafutwa kazi na mtemi anaamua kumwondokea Sagilu ambaye
sasa anaandamwa na sheria kwa ufisadi alioendesha nchini.

Awali, tunaona Mangwasha akipoteza kazi yake katika afisi ya Chifu Mshabaha kwa kujitokeza kama
mpinzani wa serikali kwani anamfanyia Lonare kampeni, kando na kwamba mara zote, hakumkubalia
Sagilu ombi la kumtaka awe kimada wake. Sihaba anatiwa mbaroni kwa kuendesha biashara haramu ya
ukahaba inayosababisha wasichana wengi kuharibika lakini anaachiliwa kutokana na ushawishi aliokuwa
nao serikalini.

Sagilu anapatwa na kichaa kwa sababu ya masaibu yanayomwandama.Mkewe mtemi, Nanzia, anaugua
baada ya jengo lake la kibiashara la Skyline Mall kutwaliwa na serikali. Baada ya kulazwa hospitalini kwa
muda, Nanzia anafariki.

Kwa mara nyingine, Lonare anatekwa nyara kabla ya uchaguzi lakini anafaulu kutoroka na kukimbizwa
hospitali kupata matibabu. Uchaguzi mkuu unafanyika na Lonare anachaguliwa kuwa mtemi.

Sagilu anashindwa na Mwamba anayechaguliwa kuwa mbunge wa Matango. Lonare anawahutubia


wananchi wa Matuo na kuahidi kuufufua uchumi wa nchi na kukabiliana na ufisadi serikalini. Anaahidi
pia kwamba serikali yake itashughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuhakikisha kwamba
pana usawa wa kijinsia, akisema kwamba Matuo imesambaratishwa na ubabedume. Anawaomba
wananchi wenzake kujiepusha na ukabila na kuwahimiza kukataa na kufichua maovu yanapofanyika
nchini. Aidha, Lonare anachagua kutolipiza kisasi dhidi ya mahasidi wake wa kisiasa.

MUHTASARI WA SURA YA KWANZA

Mangwasha yuko na wanawe katika kanisa fulani ambapo yeye na watu wa kabila lake la Waketwa
wamekimbilia usalama baada ya kuchomewa nyumba zao katika mtaa wa Matango, jijini Taria.

Kuna fununu zinazosema kwamba pana watu fulani waliotaka kuitwaa ardhi ya Matango kwa nguvu.
Inabainika pia kwamba mjini Taria, kuna jamii mbili ambazo ni mahasimu wa tangu jadi, Wakule na
Waketwa. Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anatoka katika jamii ya Wakule na anawachukia Waketwa.
Lonare ni kiongozi kutoka katika jamii ya Waketwa lakini ana umaarufu mkubwa nchini kote
kwani katika uchaguzi mkuu uliopita, alikuwa na sera bora zaidi. Hata hivyo, kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi, alitekwa nyara na tukio hilo likafanya Mtemi Lesulia kuchaguliwa bila kupingwa.
Mangwasha anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu Mshabaha. Anajua kwamba Chifu
Mshabaha, ambaye pia anawachukia Waketwa, anafanya mpango wa kuwadhulumu Waketwa.
Kwa sababu hii, anapanga kumwona kiongozi wake, Lonare, ili kumweleza njama zinazopangwa dhidi ya
watu wake.

Juhudi za Mangwasha, hata hivyo, zinatatizwa na hali kwamba jamii haimthamini mwanamke, na
anashangaa kama atasikilizwa. Anaamua atafanya tu alilokusudia, liwe liwalo.

VIDOKEZO MUHIMU
 Mangwasha na wanawe (Sayore na Kajewa) wamo kanisani pamoja na waketwa wengine.
Fununu pale kanisani zinasema kuwa watu fulani walitaka kutwaa ardhi ya matango kwa nguvu.
 Mumewe Mangwasha-Mrima aliitelekeza familia yake na kumwachia Mangwasha majukumu ya
ulezi juu ya umaskini uliowaandama.
 Mangwasha aliweza kuokoa watoto wake pamoja na vifaa vichache.
 Katika mkoba fulani alimokuwa akitafuta vyeti vyake anaipata bahasha ndogo nyeupe iliyotiwa
gundi. Ndani mlikuwa na kijibarua kilichoandikwa vibaya vibaya na ilikuwa na ujumbe
ulioeleweka-ulimlenga Mrima.
 Waketwa walikuwa wanalaumiwa na Wakule kwa chochote kibaya kinachotokea.
 Lonare Kiongozi wa Waketwa amepitia mitego mingi ya hatari anayotegewa na Wakule.

Masuala makuu yanayojitokeza katika Sura ya Kwanza

1. Uhasama wa kikabila na kisiasa unajitokeza kwani Waketwa wanabaguliwa na kupokwa haki


zao za kumiliki ardhi na kuishi kwa amani.
2. Waketwa wanalaumiwa hata kwa mambo ambayo hayako katika uwezo wa binadamu
kudhibiti, kama vile maradhi sugu yanapowashinda madaktari. Kiongozi wa Waketwa, Lonare
ameepuka kifo mara nyingi, kifo kilichopangwa na Wakule.
3. Ukabila ulioshamiri Matuo unawafanya Waketwa wengi kuwa katika tabaka la chini, huku
wakiwa na viongozi wachache sana serikalini.
4. Mfumo wa ubabedume unawanyima wanawake nafasi ya kujiamini kama wahusika sawa katika
jamii. Mwanamke asiyekuwa na cheo au pesa hawezi kusikilizwa (uk. 8).
5. Ufisadi umeshamiri katika jamii. Ardhi ya Waketwa inapotwaliwa, Chifu Mshabaha anaangalia
kando kwani alikuwa amepokea mlungula (uk. 9).
6. Maudhui ya bidii yanajitokeza kupitia kwa mhusika Mangwasha ambaye msimulizi anasema
alifunzwa kuuambaa uvivu (uk. 12).

Wahusika Katika Sura ya Kwanza:

a) MANGWASHA
Mhusika huyu ana hulka zifuatazo:
i) Mcha Mungu- Anafumba macho na kumwomba Mungu kumwepusha mumewe na mabaya.
ii) Mwenye matumaini- ana imani kuwa angeishi hata kama alikuwa akiyapitia mengi.
iii) Jasiri- anaamua kuwa angemweleza Lonare maovu yaliyokuwa yakipangwa na Chifu
Mshabaha hata kama alihofu kuwa asingesikilizwa.
iv) Mwenye bidii. Anasema kuwa kutoka utotoni alifundishwa kuambaa uvivu na kujihadhari na
vitu vya kupewa.
v) Mwanamapinduzi- alitamani kuvunja kikwazo cha mila aiokoe jamii yake. Ndipo siku moja
alitaka kukutana na Mtemi.

b) MTEMI LESULIA
i) Dikteta- Kauli za kiimla alizotoa zilichukuliwa kama sheria za nchi na hazikupingwa kamwe.
ii) Katili- aliongoza kwa mkono wa chuma aliwafanyia wapinzani wake vituko vilivyokiuka
haki.
iii) Mbaguzi/mkabila- uongozi wake unahusisha viongozi wengi wa Wakule.

c) MRIMA
i) Mpyaro – anamtusi Mangwasha na kumwita sakumbimbi.
ii) Msaliti- anaisaliti jamii yake ya Waketwa kwa kushawishiwa na marafiki wa Mtemi
iii) Kaidi anashawishiwa na wafuasi wa Lesulia hata asimsikie mkewe anapojaribu
kumwambia hila ambazo Wakule waliwapangia.

d) LONARE
i) Mwenye maono- alikuwa na ruwaza ya kuasaidia wenyeji wote wa nchi ya Matuo bila
ubaguzi.
ii) Mwenye hekima- Msimulizi anasema kuwa Lonare alikuwa na hekima iliyowatia Wakule
wahaka.

e) CHIFU MSHABAHA

i) Fisadi-Mwanamume mmoja pale kanisani anasema kuwa anajua chifu alikuwa amepokea
mlungula.

(ii) Mnafiki-anaenda kutoa pole zake kwa wenyeji wa matango waliochomewa makao yao ilhali yeye
mwenyewe ameshiriki katika njama hiyo.

Maudhui katika sura ya Kwanza:

a) Ukatili/Dhuluma
i. Wanamatango wanachomewa makazi yao na kuwa wakimbizi pale kanisani.
ii. Uongozi wa Lesulia ni wa kiimla. Tunaambiwa anaongoza kwa mkono wa chuma.
iii. Wakule wanapata dhuluma za kijadi ambapo uongozi unawatenga kwa chuki. Wanalaumiwa kwa
chochote kibaya kinachotokea katika nchi ya Matuo.

b) Utabaka
i. Kuna matabaka mawili katika mji wa Taria. Mtaa wa Majuu panaishi matajiri na vigogo wa nchi.
Mtemi pia anaishi hapa. Watu hawa wenye ushawishi ni wa jamii ya Wakule.
ii. Idadi kubwa ya waketwa ni ya tabaka la chini. Wanaishi katika eneo la Matango na kufanya kazi za
hadhi ya chini.

c) Tamaa na ubinafsi
Inasemekana kwamba kuna baadhi ya waketwa walionunuliwa na Wakule ili wachome makao
yao wenyewe kwa tamaa ya pesa.
Wanaume wengine nao waliuza wake zao kwa Wakule ili wapate ajira.

d) Ubabedume
i. Mangwasha alitamani sana kufisha uhasama uliokuwa baina ya Waketwa na Wakule lakini nafasi
yake katika jamii kama mwanamke haingemruhusu.
ii. Mrima pia anashangaa kuwa Mangwasha anakotoa nguvu ya kutaka kumkabili Mtemi Lesulia.
Anamkanya na kumwambia asiruhusu wazo kama hilo akilini.

e) Uongozi Mbaya

Uongozi wa mtemi Lesulia ni wa kiimla. Anaongoza kwa mkono wa chuma na kauli anazotoa
zinachukuliwa kuwa sheria za nchi.

Maudhui zaidi katika sura hii:


Uozo katika jamii, Malezi,Mabadiliko, Elimu,Utamaushi, Mila na Desturi,Unafiki,
Usaliti,Uwajibikaji,Ukengeushi, Mihadarati,Mbinuishi, Teknolojia.
MUHTASARI WA SURA YA PILI

Mangwasha ni msichana mwenye bidii kazini. Anahudumu katika afisi ya Chifu Mshabaha. Anakutana
na Mrima, ambaye pia ni mwenye bidii, na kuchumbiana. Wanafanya mazoea ya kwenda kula chakula
katika mkahawa wa Mpenda Bure unaomilikiwa na Sagilu, mzee ambaye ni rafikiye Mtemi Lesulia.
Sagilu anamtaka Mangwasha kimapenzi na anapomkataa, anaweka kisasi dhidi yake. Chifu Mshabaha pia
anamchukia Mangwasha kwa kumchumbia mwanamume asiyekuwa na pesa na kumkataa rafikiye,
Sagilu, ambaye ni tajiri.

Siku ya harusi ya Mangwasha na Mrima, Sagilu anamtuma Sihaba, kimada wake, na bomu ambalo
linalipuka na kusababisha watu waliohudhuria sherehe kutawanyika. Baada ya miaka kadhaa katika ndoa
na kuwa na watoto wawili Sayore na Kajewa. Mrima kwa kushawishiwa na Sagilu anabadilika.
Anaitelekeza familia yake na kuingilia ulevi. Mangwasha anateseka sana na anapoamua kufuatilia
mumewe ili ajue ni nini kilichomfanya abadilike, anagundua kwamba anapewa pesa nyingi na Sagilu,
ambaye ni adui wa ndoa yao.

VIDOKEZO MUHIMU
 Mangwasha anapotamatisha masomo yake ya sekondari na kumwomba babake Mzee Shauri
aendeleze masomo yake zaidi katika chuo cha uhazili kwao Ndengoni.
 Anahitimu na kuajiriwa kama mhazili katika ofisi ya chifu Mshabaha. Anafanya kazi yake kwa
bidii. Kwa sababu utiifu na umahiri wake kazini anapandishwa cheo hadi gredi ya juu zaidi ya
uhazili.
 Mangwasha anachumbiana na Mrima anayefanya kazi ya ukarani katika ofisi za wizara ya maji
karibu na afisi ya chifu.
 Mrima ni kijana anayehudumia wateja kwa ukarimu na unyenyekevu na mwenye bidii. Kisadfa,
anaingia kazini wa kwanza na kuondoka wa mwisho kama alivyofanya Mangwasha.
 Sagilu ni tajiri anayemiliki mkahawa kwa jina Mpenda Bure wanapokutana mara kwa mara Mrima
na Mangwasha.
 Yeye ni rafiki mkubwa wa Chifu Mshabaha na mtemi Lesulia. Kutokana na urafiki huo, Sagilu
anafanywa mwenyekiti wa Halmashauri ya Mapato katika nchi ya Matuo.
 Sagilu ana kimada kwa jina Sihaba. Inabainika kuwa Sihaba hampendi Sagilu bali anapenda pesa
zake. Sagilu anamjengea nyumba na kumpa chochote atakacho.
 Mtemi Lesulia na Sagilu wanashirikiana katika biashara za ughaibuni. Wanamiliki viwanda
ambapo wanawaajiri Wakule pekee.
 Sagilu anafanya biashara za kimagendo kama ile ya kuagiza ngano na mali ya thamani bila kulipa
ushuru. Malori yake yanapokamatwa yakisafirisha bidhaa ghushi, anatoa mlungula.
 Kwa wakati mmoja Sagilu anauza maziwa ya unga yenye sumu, maziwa haya yanahatarisha
maisha ya watoto wote nchini na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa.
 Sagilu anamtaka Mangwasha kimapenzi bila kujali kuwa ana mchumba.
 Msimamo wa Mwangasha ni thabiti kuwa anampenda Mrima hata anaposhawishiwa na chifu
Mshabaha alikataa kata kata kuhusiana na Sagilu.
 Siku ya harusi kati ya Mrima na Mangwasha, Sagilu anamtuma Sihaba na bomu ili kutibua harusi
hiyo. Mpango untibuliwa baada ya Mrima Kugundua na kumtuma msimamizi wake asimruhusu
kuwakaribia maharusi.
 Baada ya ndoa wanabarikiwa na watoto wawili (Sayore na Kajewa) ambao wanajiunga na shule ya
msingi hapo Taria.
 Mrima anabadilika na kuwa mlevi anayekesha katika vilabu vya pombe. Anakosa kufika kazini na
kutowajibikia elimu na mahitaji ya familia yake.
 Baada ya mashauriano baina ya Mangwasha na rafikiye Bi. Mbungulu, Mangwasha anaamua
kufanya uchunguzi wa kilichomfanya mumewe abadilike. Anamsaka mumewe kunakouzwa
pombe eneo la Ponda Mali ila hampati.
 Mangwasha anapitia anapofanya kazi Mrima ambapo anamvizia Sagilu akimpa Mrima bunda la
noti. Mrima anaingia ofisini mwake na kuelekea ulevini alikokaa hadi kesho yake asubuhi.
 Mangwasha anamkabili Mrima nyambani kuhusu ulevi wake na kwa muda Mrima anakosa kwenda
ulevini.

Masuala Makuu Yanayojitokeza Katika Sura Ya Pili

1. Mangwasha, mhusika mkuu, anajitokeza kama mwanamke jasiri na aliyejikomboa kiakili.


Hathamini tamaduni zilizopitwa na wakati, kama vile kulazimishiwa ndoa kwa misingi ya
mali. Kwa msingi huu, anamkataa Sagilu ambaye anatumia ushawishi wa hela kumtaka awe
mwanamke wake.
2. Yeye ni mwenye mapenzi ya dhati, hali inayomfanya kumjali mumewe na kufuatilia ili ajue ana
tatizo gani linalomfanya kuingilia ulevi na kuitelekeza familia yake.
3. Sagilu anasawiriwa kama mtu katili, anayehodhi bidhaa na kuziuza kwa bei za juu wakati
kuna uhaba wa bidhaa hizo. Aliwahi kuagiza maziwa ya watoto ambayo yalihatarisha maisha
yao. Kwa kuwa ana uhusiano wa karibu na Mtemi Lesulia, sheria hazikumfuatilia katika suala
hili, ishara ya ufisadi.
4. Chifu Mshabaha anajitokeza kama mbaguzi na mpyaro. Anasema kwamba Waketwa hawana
akili (uk. 20).
5. Ufisadi na uepetevu unajitokeza kwani polisi hawajishughulishi kumtia mbaroni mwanamke
anayekuwa na kilipuzi kwenye harusi ya Mangwasha.
6. Sagilu ana kisasi na familia ya Mangwasha. Kwa sababu hiyo, anatumia pesa ili kumtokomeza
Mrima na kwa namna hiyo, kumsababishia Mangwasha na wanawe mateso.
7. Taasubi ya kiume inajitokeza kupitia mhusika Mrima ambaye anamwambia Mangwasha
kwamba hamzuii kuoa mke mwingine (uk. 41).

Wahusika Katika Sura ya Pili:

a) MANGWASHA
i. Mwenye bidii/mchapa kazi- anafika wa kwanza na kutoka wa mwisho kazini.
ii. Mpelelezi- anafanya upelelezi wake na kugundua anayempa mumewe pesa za kushiriki
ulevi.
iii. Mwajibikaji- baada ya Mrima kutelekeza familia bado anajikakamua kushughulikia
wanawe. Mfano anapoulizwa vitabu vipya na Sayore anamhakikishia kumnunulia siku
inayofuata.
iv. Mwenye msimamo thabiti- anaposhinikizwa na Chifu mshabaha kukubali kuolewa na
Sagilu anakataa na kufuata penzi lake kwa Mrima.
v. Mwenye hashima- anamkabili Mrima kwa maneno ya heshima wakati anaporejea asubuhi
kutoka ulevini.
vi. Mwenye mapenzi ya dhati- anamjali Mrima mumewe na kutaka kujua kinachomsababishia
ulevi hata akaenda kumsaka mtaa wa Ponda Mali.

b) SAGILU
i. Fisadi- anatoa mlungula wakati ambapo malori yake yanashikwa yakisafirisha bidhaa
ghushi.
ii. Mkiritimba- hataki kushindwa na yeyote katika biashara.
iii. Katili- waliojaribu kumpiku aliwafanya hila na mizungu na kuwafilisi. Kabisa. Pia, anauza
maziwa ya unga yenye sumu yanoyodhuru watoto.
iv. Mzinifu- inasemekana kuwa anawabadilisha wanawake kama anavyobidilisha magari.
v. Mbaguzi- Katika viwanda vyake ni Wakule peke wailajiriwa
vi. Mwenye wivu- Hataki yeyote kumpiku katika biashara kwani anataka kila biashara
anayofanya pasiwe na wa kushindana naye.
c) MRIMA
i. Mchapa kazi- anafika kazini wa kwanza na kutoka wa mwisho
ii. Mlevi- anashiriki ulevi usiku kucha katika eneo la Ponda Mali.
iii. Mwepesi wa kushawishiwa- kwa kupewa pesa na Sagilu anashawishika na kuingilia ulevi
huku akisahau familia yake na yale Sagilu aliwafanyia awali.
iv. Mhafidhina- anashikilia itikadi za kale kuwa mwanamke hafai kumhoji mumewe ataokako
au aendako na pia hawezi kumzuia kuoa wa pili.
d) CHIFU MSHABAHA
i. Mpyaro- anasema kuwa Waketwa hawana akili hata ya kuwachagua wachumba akimrejea
Mangwasha aliye Mketwa.
ii. Mbaguzi- anadhihirisha ubaguzi kwa Mrima ambaye anaona hafai kumwoa Mangwasha
kwani ni maskini.

Maudhui Katika Sura ya Pili:

a) Kazi/Bidii
i. Mangwasha na Mrima ni wachapa kazi-Mangwasha anafanya kazi katika ofisi ya Chifu Mshabaha
kama mhazili.
ii. Mrima anafanya kazi katika ofisi ya chifu mshabaha kama karani.
iii. Wote hufika kazini wa kwanza na kutoka wa mwisho.

b) Ufisadi
i. Sagilu anaagiza ngano na bidhaa nyinginezo za thamani kimagendo bila kulipia ushuru.
ii. Malori yake yanapokamatwa anatoa mlungula.

c) Ubaguzi
Sagilu na Mtemi Lesulia wanamiliki viwanda kadha nchini ambapo ni Wakule pekee walioajiriwa
mle.

d) Ulevi
Mrima anaignilia ulevi baada ya miaka kadhaa ya ndoa. Anamwachia mkewe majukumu yote ya
malezi.

e) Ukatili
i. Sagilu aliagiza maziwa ya unga yenye sumu yanayohatarisha maisha ya watoto wote nchini.
ii. Sihaba alipanga kutibua harusi ya Mangwasha na Mrima anapoingia akiwa na kifurushi kinapatikana
kuwa kilipuzi.
iii.
f) Uwajibikaji
Mangwasha anawajibikia malezi ya Sayore na Kajewa kwa kuwavisha, kuwasomesha na
kuwalisha peke yake wakati Mrima anapotelea katika ulevi.

g) Uzinzi
Sagilu ana kimada kwa jina Sihaba.
Maudhui zaidi katika sura hii:
Elimu, Kazi, Nafasi ya mwanamke katika Jamii, Tamaa, Ubeberu, Ukiritimba, Unasaba/Ukabila,
Mapenzi, Kutamauka, Mgogoro, Mabadiliko, Umenke, Utamaduni

MUHTASARI WA SURA YA TATU

Waketwa ni watu wenye bidii. Hata hivyo, wengi wao wanaishia kufanya kazi duni na wanabaguliwa kwa
kila hali kwani utawala wa Mtemi Lesulia ni fisadi na unaendeleza ubaguzi dhidi yao. Kuna matatizo ya
kiuchumi yanayotokana na uongozi mbaya; vijana waliosoma hawana ajira na wengine wao hawasomi
kutokana na umaskini uliokithiri.

Pia, kuna uharibifu wa mazingira kutokana na mapuuza na kutojali kwa serikali.Tunafahamu kwamba
machifu wamelazimishwa kuwahamisha Waketwa kutoka Matango ili Mtemi Lesulia asipate upinzani
katika eneo hilo, na Lonare asichaguliwe, kwani wafuasi wake wengi wanaishi huko. Baadaye, Sagilu
anamtembelea Mangwasha usiku na kutaka kumhonga kwa pesa ili amkubali. Mangwasha anamfukuza na
kukataa Pesa zake. Usiku huo anapolala, anaota kwamba jinyama hatari linamfukuza na mbele
anakokimbilia anakabiliwa na moto mkubwa. Anapoamka, anatanabahi kwamba makazi ya Matango
yalikuwa yanateketezwa kwa moto na watu wanahangaika ovyo.

VIDOKEZO MUHIMU

 Waketwa ni wenye bidii sana na wenye akili za ujasiriamali kutoka jadi. Hawana ubaguzi wa
kikazi au kikabila.
 Wakule ndio wengi serikalini kwa kuwa mtemi Lesulia anatoka katika jamii hii.
 Waketwa wanalalamikia uongozi wa Mtemi Lesulia ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili
kwa njia iliyojaa shaka.
 Vijana waliohitimu wamekosa kazi kwani zinazotolewa kimapendeleo bila kujali kama mtu
amehitimu mradi tu awe ametoka katika jamii ya Wakule. Jeshi la nchi limeajiri vijana wengi
kutoka jamii ya Wakule.
 Sekta nyingi zimeajiri watu wasiohitumu kwa kazi zenyewe. Mfano, walimu wa shule za msingi
hadi chuo kikuu hawajahitimu kwa masomo wanayofunza. Huu ni utepetevu wa kiwango cha juu.
 Mifumo ya kiuchumi ni kandamizi inyofukarisha nchi ya Matuo kwa sera za ubaguzi. Nchi
inashikilia utabaka ambapo matajiri ndio wanaendesha nchi.
 Uchafuzi wa mazingira umeshamiri, kutokana na kuharibu misitu na mvua kupungua na
kubadilika kwa majira.
 Uharibifu zaidi unaendelea kwa kuchimba na kukusanya mchanga.Mashimo makubwa
yanaachwa yanayowaangamiza watoto mvua inaponyesha.
 Matajiri wanawaajiri watoto ambao wazazi wao wanashindwa kuwaelimisha katika machimbo ya
mawe.
 Kutokana na baruti wenyeji wanapata uziwi na kuwasababishia magonjwa ya kukokohoa
yasiyopona. Wanapolalamika wanaambiwa wahame maeneo hayo.
 Uharibifu zaidi unafanywa kwa kubadilisha mikondo ya mito na vijito kwenye mashamba yao
makubwa na kunyima raslimali hii muhimu wenyeji. Mtemi Lesulia ni mmojawapo wa vigogo
hawa.
 Uozo mkubwa unaingilia jamii na asasai ya familia ikiathirika ambapo watu wasiojali
wanaangamiza hata watoto wao
 Mangwasha anaendelea kufanya kazi yake kwa uaminifu bila malalamiko. Aidha anaguswa
moyo kuwaona vijana wanaomaliza kidato cha nne na darasa la nane wakijikusanya kwenye
viambaza vya duka bila shughuli yoyote.
 Anawahurumia watoto wasichana waliopata watoto kwa umri mdogo wakiombaomba wapita
njia.
 Lonare kiongozi kutoka kwa amii ya Waketwa ni mfanyabiashara anayemiliki magari ya
uchukuzi.
 Biashara zake zinawindwa na serikali ya Mtemi Lesulia. Magari yake yanatafutiwa makosa
madogomadogo na madereva wake kukamatwa kwa makosa yasiyojulikana na hata
kunyang’anywa leseni.
 Lonare anawania kiti cha Mtemi wa Matuo kwa chama cha ushirika akipingana na Mtemi Lesulia
anayegombea kwa chama cha Mamlaka. Rafiki yake, Mwamba anawania kiti cha ubunge cha
Matango kwa chama kicho hicho cha Ushirika akipingana na rafiki yake Chifu Mshabaha,
Sagilu.
 Lonare anapomtembelea Mangwasha wanajadili kuhusu vijikaratasi vilivyosambazwa vikiwataka
Waketwa wahame Matango. Lonare anaamua kukabiliana na tishio la Waketwa kuvamiwa kwa
kupeleka habari hizo kwenye vyombo vya mawasiliano.
 Jioni hiyo Sagilu anatembea nyumbani kwa Mangwasha na kumpa bahasha yenye pesa ila
anaikataa na kumtupia. Manoti ya elfu yanatapakazwa na upepo.
 Mangwasha anapolala anaota akikimbizwa na jinyama linalotapika pesa na moto mbele yake.
 Hii ni jazanda inayorejelea Sagilu-jinyama nao moto ni kiangazambele cha moto utakaochomea
Waketwa makazi yao.

Masuala Makuu Yanayojitokeza Katika Sura Ya Tatu

1. Maudhui ya bidii na kutobagua kazi yanasisitizwa katika sura hii. Waketwa hawakuchagua kazi
kama walivyofanya Wakule. Walifanya hata zile zinazofikiriwa kuwa duni (uk. 43).

2. Ufisadi unajitokeza kwani watu wengi, hasa wa jamii ya Wakule, wanapata kazi hata bila kuhitimu,
jambo ambalo lina madhara makubwa, kama vile vifo vinavyofanyika hospitalini ambako watu
wasiosomea udaktari wanaajiriwa kufanya upasuaji wa kimatibabu. Viongozi wa kijeshi pia wanatoka
katika jamii ya Wakule (uk. 44).

3. Uchafuzi wa mazingira pia umeangaziwa. Wananchi wanaathirika kiafya kutokana na uchafuzi wa


mazingira (uk. 46).

4. Umaskini unawafanya baadhi ya vijana kutopata elimu ya haja, huku wasichana wakipata mimba za
mapema na kukosa kuendelea na masomo (uk. 48-49).

5. Lonare anajitokeza kama kiongozi bora kwani anapigania elimu ya wasichana na anataka kuongoza
Matuo si kwa sababu ya mshahara tu bali kwa kuwa anawapenda wananchi wenzake, kuonyesha kwamba
yeye pia ni mzalendo.

5. Mwandishi ametumia jazanda ya jinyama na moto. Jinyama linalomkimbiza Mangwasha ni Sagilu


ambaye ni mzee asiyekuwa na maadili, nao moto ni kiangazambele cha moto unaowachomea Waketwa
makazi yao huko Matango.

Wahusika Katika Sura ya Tatu:

a) LONARE

Ni kiongozi wa Waketwa anayewania kuwa mtemi wa nchi ya Matuo.


i. Mtetezi wa haki- anataka kuwania cheo cha mtemi sio kwa mshahara bali awakimboe.
Wanamatuo kutokan na udhalimu we Mtemi Lesulia.
ii. Mwenye bidii- Amejibiidisha katika biashara yake ya usafiri.
iii. Mwajibikaji- amewajibika kuwalea watoto wake watatu peke yake baada ya mkewe
kufariki. Lombo kitindamimba anasomea utabibu.
iv. Mvumilivu- anavumilia mateso anayopitishiwa katika biashara yake.

b) MANGWASHA
i. Mlezi mwema- baada ya kutoka kazini anawasaidia Kajewa na Sayore kukamilisha kazi
waliopewa na mwalimu.
ii. Mshauri mwema- anamshauri Lonare asiwe na kiburi kabla ya kukabiliana na Mtemi
Lesulia.
iii. Mpelelezi- anapeleleza kuhusu vijana watano waliondamana na chifu Mshabaha.

c) SAGILU
i. Mwenye dharau- anamdharau Mangwasha kutokana na hali yake ya uchochole baada ya
kuachwa na mumewe.
ii. Fisadi anamtembelea Mangwasha na kujaribu kumpa mlungula ili amkubali kimapenzi.

Maudhui Katika Sura ya Tatu

i. Utabaka- Waketwa wanafanya kazi zozote duni japo wana bidii inayowawezesha kuwa
mashuhuri wa biashara za magari na maduka makubwa ilhali Wakule wanaishi kwenye mitaa
ya kifahari huku wakiwa na idadi kubwa serikalini.
ii. Ubaguzi-vijana waliohitimu wa jamii ya Waketwa hawapati nafasi za kazi. Majopo ya uajiri
yamejaa Wakule hivyo basi wawanaajiri ka kuangalia majina. Jeshi la nchi pia limejaa
Wakule. Waketwa pia wanapitishiwa msururu wa maswali yasiyokuwa na uhusiano wowote
na kazi wanazoomba.
iii. Uongozi mbaya- Nchi ya Matuo inaongozwa kwa sera za ubaguzi zilizowafukarisha
wananchi.
iv. Uharibifu wa mazingira- Misitu iliharibiwa kisha kusababisha kiangazi na mabadiliko ya
majira. Mandhari ya kimaumbile yaliharibiwa pia kutokana na machimbo ya mawe na
mchanga.
v. Siasa- Lonare na Mwamba wanawania viti mbalimbali wakitumia chama cha Mamlaka
kuwania viti vyao katika uchaguzi.

Maudhui zaidi katika sura hii:


Utabaka, Bidii, Ujasiriamali, Uongozi mbaya, Unasaba/ukabila/ubaguzi, Changamoto katika
Elimu, Ubepari, Kutamauka, Nafasi ya vijana katika jamii, Nafasi ya dini, Usaliti.

SURA YA NNE

Sura hii inafanyika katika mandhari ya kanisa, inaanza asubuhi baada ya watu kukesha nje ya kanisa hilo.
Ni baada ya kufurushwa kutoka Matango. Mangwasha na Mbungulu wanakutana na wanawake wengine
ambao wanaelezea kwamba usiku walipochomewa nyumba walikutana na vijana. Hawa walikuwa na
mageleni yaliyohanikiza harufu ya mafuta ya petroli. Vijana hao waliingia kwenye gari jekundu
lililoendeshwa na mwanamke fulani ambaye hawakuweza kumtambua. Mkurugenzi wa ardhi mjini Taria
anakuja mahali pale akiandamana na Chifu Mshabaha na mwanamke aitwaye Mbwashu. Mbwashu ni
mshirika wa karibu wa mtemi na mkewe Nanzia. Anawaahidi watu chakula, mablanketi na mahema ya
msaada. Watu wanakasirishwa na hatua ya kuwachukulia kama wakimbizi lakini mkurugenzi huyo
anasema kwamba chanzo cha moto uliowachomea makazi yao hakijulikani, baadaye kidogo anaondoka.
Watu wana hasira, hawataki kuishi mahali hapo inadhihirika kuwa wako radhi kwenda kukita mahema
huko kwao Matango.

Siku ya tatu baada ya kurudi Matango, vijikaratasi vinasambazwa kuwataka Waketwa watoke sehemu
hiyo. Watu wanakuja hapo kutaka kujenga ua ili kuzingira ardhi ya Matango lakini wanafukuzwa na
wenyeji, ambapo Sihaba anajeruhiwa. Inafahamika kuwa kuwa huyu ndiye aliyesambaza vijikaratasi vya
kuwataka watu wahame eneo la Matango. Sagilu naye ameshaonywa na Mtemi Lesulia kuhakikisha
kwamba jalada halisi la ardhi ya Matango halipatikani, kwani ardhi hiyo sasa ni mali ya Nanzia, mkewe
mtemi, na Mbwashu.

Baadaye, Sihaba anamtembelea Chifu Mshabaha. Anamwachia barua zenye taarifa kuhusu jengo la
kibiashara ambalo linanuiwa kujengwa Matango. Kuna barua kutoka kwa Mtemi Lesulia inayoeleza
kwamba kipande hicho cha ardhi ni mali ya Nanzia na Mbwashu. Mangwasha anafaulu kuzipata na
anazirudufisha barua zote na baadaye zinatumiwa kama ushahidi mahakamani katika kesi inayohusu
ardhi ya Matango. Mwamba, mwanasheria anayewakilisha Waketwa katika kesi hiyo anashinda kesi kwa
ushahidi huo. Mpango wa Mtemi Lesulia, Sagilu na Chifu Mshabaha wa kuwafurusha Waketwa kutoka
kwenye ardhi ya Matango unakosa kufaulu.

Mtemi Lesulia anapanga njama nyingine. Kupitia kwa Sagilu, wanampa Mrima pesa nyingi pamoja na
ahadi ya kumpa cheo serikalini ikiwa atamfanyia kampeni Mtemi Lesulia na kuwaendea kinyume
Waketwa. Mangwasha anapata pesa hizi pamoja na barua yenye ahadi alizopewa Mrima na anamtaarifu
Lonare, Mwamba, Sauni na Sagura. Wanakutana na Mrima na kufanikiwa kumweleza ukweli kwamba
anatumiwa tu kisiasa, na kwamba Mtemi Lesulia na Sagilu hawana mpango wowote wa kumfaa.
Wanakubaliana kurudisha pesa alizohongwa nazo kwa Sagilu, ambaye wanamkuta akiwa kwenye
mkutano pamoja na wafuasi wake katika mkahawa wa Saturn.

VIDOKEZO MUHIMU

 Mangwasha na wenyeji wa Matango wamekimbilia kanisani baada ya makao yao kuchomwa.


Wengine wanamsuta kwani walidhani alifungua mlango wa kanisa na kuufunga baada ya kuingia
ila anawaamia kuwa aliingilia kwenye dirisha.
 Baadhi ya wakimbizi ni wanawake wawili ambapo mmoja anakiri kuwaona vijana wawili
waliobeba mageleni tupu yalionuka mafuta ya petroli. Mmoja alimpiga mwanamke huyo kumbo
kisha wakakimbilia kwenye gari jekundu lililoegeshwa karibu. Sauti ya mwanamke ilisikika
ikiuliza iwapo kazi ilikuwa imekamilishwa.
 Chifu Mshabaha anafika baadaye huku ameandamana na askari. Mkurugenzi wa Ardhi pia
anafika pamoja na Mbwashu aliyekuwa kikaragosi wa Mtemi Lesulia na mfanyabiahsara
aliyemiliki maduka na majumba ya ghorofa ya kupangisha.
 Mkurugenzi huyo anatoa pole na kutoa ahadi ya kuchunguzwa chanzo cha moto huo pamoja na
misaada ya serikali.
 Punde, Nanzia mke wa Mtemi Lesulia anafika mahali pale kwa gari aina ya pick up. Anatoa
msaada wa chakula hasa cha watoto. Hii ni mbinu ya kinafiki ya kuwafumba macho kwa kuwa
matukio haya yote anafahamu kiini chake na ilivyopangwa.
 Sauni anawahutubia wakimbizi wale na kuwashinikiza kutokubali kuweka mahema yao pale
kanisani kama walivyotakiwa na serikali. Wanaelekea kwenye ardhi yao ya Matango huku umati
mkubwa ukiwafuata. Askari wanawasimamia ili pasiwe na ghasia zozote.
 Wenyeji wa Matango wanapiga kambi eneo hilo kwa siku mbili kisha siku ya tatu wanapata
vijikaratasi vinanyowataka wahame pale ili pajengwe soko kubwa la wachuuzi.
 Sihaba mwanamke aliyewasimamia vijana kuchoma makazi anachomewa gari lake na kufikishwa
katika kituo cha polisi kwa kupatikana na na vile vijikaratasi ila umati unataka aachiliwe wao
wenyewe wamwadhibu.
 Wenyeji wa Matango wanaamua kupeleka kesi mahakamani. Naye Sihaba anaachiliwa jioni hiyo
ya siku anayokamtwa. Anamtembelea chifu Mshabaha na kumkabidhi bahasha nyeupe.
Mangwasha alishuhudia tukio hilo.
 Mangwasha anaingia ofisini mwa chifu na kuzirudufu karatasi zilizokuwa kwenye bahasha ile
kisha akaifunga na kurudisha kwenye saraka. Kisha anawajulisha kina Lonare kuhusu yaliyomo
kwenye karatasi ile.
 Bw. Mwamba anawakilisha wenyeji wa Matango naye Bw. Mafamba anawakilisha serikali
mahakamni. Hakimu anaamua kesi na Wanamatango wanashinda kesi. Uamuzi unatolewa kuwa
serikali iwajengee wenyeji wa Matongo nyumba zao upya.
 Baada ya uamuzi huo hakimu ananyang’anywa leseni na kushushwa cheo. Hata hivyo anapata
kazi ya uhadhiri katika chuo kikuu cha kibinafsi. Mangwasha anapomfikiria mumewe,
Mbungulu anaingia kisadfa na kumjulisha kuwa alimwona Mrima akiwa katika hali mbaya
akielikea katika mtaa wa Majaani.
 Siku ya Jumamosi, Mwangasha, Lonare, Mbungulu na Mbaji wanaelekea Majaani wanapomkuta
Mrima akiwa mlevi chakari.
 Mrima anakubali kurudi nyumbani shingo upande. Anaanzisha kibanda na kupitia bidii zake na
usaidizi wa mkwe kibanda hicho kinakua na kuwa duka kubwa inayofurika wateja.
 Mangwasha alipofika nyumbani, anagundua kuwa bahasha ambayo aliona Sagilu alimpa Chifu
Mshabaha ofisini, ipo kwake nyumbani. Hii ni baada ya Mangwasha kuingia kwenye chumba
cha kulala na kuipata juu ya kabati kisha akaificha kwenye mto.
 Mangwasha anapoenda kazini anaamua kumpasha Lonare habari zile hivyo wanakutana katika
mkahawa mmoja. Mangwasha anaazimia kumkabili Mrima ila Lonare anamshauri awaachie
jukumu hilo.
 Siku iliyofuata, Lonare, Sagura, Sauni, Mwamba na Mbaji wanamtembelea Mrima nyumbani na
kumpata akiwa ametapakaza kila kitu nje ye nyumba. Wanamkabili kwa ukweli uliokuwa
kwenye bahasha ile.
 Wanamshinikiza Mrima kuandamana nao katika hoteli ya Saturn ambapo Sagilu alikuwa na
mkutano wa wafuasi wake kurejesha bahasha ile. Pale hotelini Mbwashu, Chifu Mshabaha,
Ngoswe mwanawe Mtemi Lesulia walikuwa katika mkutano wakupanga kampeni.
 Baada ya kizaazaa cha kutaka kuwakataza kuongea Lonare anapata nafasi ya kuongea. Anasema
sababu yao kuwa pale ni kurejesha mlungula wake Sagilu kisha anamrushia bahasha ile. Noti za
pesa zinatawanyika kila mahali.
 Ngoswe anaachwa akipiga kelele na kumwita Lonare majina ambayo hayangeandikika.

Masuala Makuu Yanayojitokeza Katika Sura Ya Nne

1. Mangwasha na Lonare wanajitokeza kama wahusika waadilifu, wanarudisha pesa


zilizotumiwa kama hongo kwa Sagilu kutoka kwa Mrima.
2. Aidha, Mangwasha na Lonare ni wenye mapenzi ya dhati kwa nchi na kwa watu wao.
Wanamwokoa Mrima kutoka Majaani ambako amedhoofikia kiafya.
3. Chifu Mshabaha, Mbwashu, Sagilu, Mafamba na Mtemi Lesulia wanajitokeza kama wahusika
fisadi na katili kwani hawajali athari za vitendo vyao vya kifisadi kwa wananchi. Mtemi
Lesulia analinganishwa na mjusi kafiri anayekula chakula cha mchwa na mchwa wenyewe.
Maelezo haya yanajenga jazanda ya utawala dhalimu unaowaangamiza wananchi wake.

Wahusika Katika Sura ya Nne:

a. SAGILU
i. Fisadi- anampatia Mrima bahasha ya pesa elfu mia nane pesa taslimu ili kumfanyia Mtemi
Lesulia.
ii. Mwenye majitapo- analinganisha Mwamba na kidagaa ambaye hawezi kumshinda papa.
iii. Katili – anashirikiana na Mtemi Lesulia kuwapoka wenyeji wa Matango ardhi yao.

b. MANGWASHA
i. Jasiri- anakaidi mila zinazomkandamiza mwanamke na kuhutubia watu pale nje ya kanisa.
ii. Mwenye matumaini- anawatumainisha wanawe kuwa Mungu angewapa maisha.
Anawaambia kuwa hali hiyo waliomo ni ya muda.
iii. Mwenye mapenzi ya dhati-anapoelezwa kuwa mumewe Mrima ameonekana akiwa katika
hali mbaya, anaamua kumtafuta kule Majaani.
iv. Msamehevu- hana kintongo na memewe hata baada ya kumwachia majukumu ya malezi na
kutorokea ulevini.
v. Mwajibikaji- amewajibika kulea wanawe wakati mumewe hayupo na hata kumtafuta
memewe anapotorokea ulevini
vi. Mtetezi wa haki- anashirikiana na wengine kama vile Lonare kutetea haki ya wenyeji wa
Matango ya kumiliki ardhi yao.

c. MRIMA
i. Mwepesi wa kushawishika- Anaingia katika mtego wa Sagilu kwa kupokea hongo na
kusukumizwa ulevini.
ii. Mhafidhina- anashikilia mila na desturi za jadi anaposema kuwa hawezi kukubali kurudi
nyumbani kutuzwa na mke kama mgonjwa.
iii. Mwenye bidii- anaporudi nyumbani anafungua kibanda ambapo anafanya bidii na kupanua
biashara hiyo na kuwa duka kubwa inayofurika wateja.
iv. Mpenda ulevi- anapatikana katika mtaa wa Majaani akiwa mlevi chakari.

d. LONARE
i. Mwenye utu- anawanunulia wenyeji wa Matango mahema mengine baada ya serikali kukosa
kuongezea mengine zaidi.
ii. Mtetezi wa haki- Yuko mstari wa kwanza kuhakikisha kuwa wana Matango wamepata haki
yao ya kumiliki ardhi yao.
iii. Mwenye busara- anatumia busara kuwakabili maadui zake wa kisiasa.
iv. Mshauri mwema- anamshauri Mangwasha na wenzake kuhusiana na vile wangelikabili
suala la Mrima kupokea pesa kama hongo.

e. SAUNI
i. Mwenye hasira- anamkemea Mrima kwa hasira akimwuliza iwapo bado hajatosheka na
maovu aliyotendewa.
ii. Mtetezi wa haki- anashirikiana na Lonare na Mangwasha katika kupigania haki ya wenyeji
wa Matango.
iii. Jasiri- anamkabili mkurugenzi wa Ardhi kwa maswali hata anapoangaliwa kwa jicho kali na
chifu mshabaha anaendelea bila woga wowote.

f. SAGURA
i. Mpole- polisi wanapokuja kuweka ulinzi kwenye mahema ya wenyeji wa Matango,
anawauliza kwa upole waondoke kwani hawawaamini.
ii. Mtetezi wa haki- anashirikiana na kina mangwasha na Lonare kitika kuokoa ardhi yao.

g. SIHABA
Katili- anatumiwa na Sagilu kuchoma makao ya wenyeji wa Matango.
h. NANZIA
Mnafiki- kitendo cha kuwatembelea wakimbizi wa matango na kuleta chakula cha watoto ni cha
unafiki alijua walichokuwa wamewafanyia wakimbizi.

i. BW. MAFAMBA
i. Fisadi- alikuwa fisadi aliyejulikana ndani na nje ya nchi. Aliiyafunika maovu yote ye
viongozi mbalimbali.
ii. Katili- ndiye aliyetumika katika kutoweshwa kwa majalada na nyaraka muhimu zilizohusu
kesi za ufisadi.
iii. Mwongo- katika kesi mahakamni anatoa ushahidi wa uongo. Anadai kuwa wenyeji wa
Matango walipata vyeti vya umiliki ghushi.

j. BW. MWAMBA
Mtetezi wa haki- anawawakilisha wenyeji wa Matango katika kesi ya kutetea ardhi yao.

k. NGOSWE
Mpyaro- baada ya Lonare kumrushia Sagilu hongo aliyompa Mrima, anasikika akipiga kelele na
kumwita majina ambayo yaingeandikika.

Maudhui Katika Sura ya Nne:

Ufisadi
Bw. Mafamba anajulikana kuwa fisadi ndani na nje ya nchi.
Mrima anapokea hongo ya shilingi elfu mia nane kutoka kwa Sagilu.

Unyakuzi wa Ardhi
Mtemi Lesulia na wenzake wanaazimia kunyakua Ardhi ya Matango.

Ukatili
Mtemi Lesulia na Sagilu wanawafanyia wana Matango ukatili kwa kutaka kuwapoka ardhi iliyo
yao kihalali.

Maudhui Zaidi Katika Sura ya Nne:


Ukatili, Malezi, Usaliti, Uwajibikaji, Unafiki, Utabaka, Ujasiriamali, Nafasi ya dini katika jamii

MUHTASARI WA SURA YA TANO

Nchi ya Matuo inakaribia uteuzi wa viongozi. Sagilu, aliyekuwa na matumaini makubwa ya kupata uteuzi
wa kugombea uongozi wa Matango anapata msururu wa mapigo. Ana uhusiano wa kimapenzi na mpenzi
wa mwanawe, Mashauri, aitwaye Cheiya. Mashauri anapogundua jambo hili anamchukia babake hata
kufikia kiwango cha kumkana kama babake mzazi. Zaidi ya hayo, Mashauri anajiunga na kundi
linalomuunga mkono Lonare na Mwamba, ambao wanawania kiti cha mtemi na uongozi wa eneo-bunge
la Matango mtawalia. Hawa ni mahasimu wa kisiasa wa waliokuwa katika mrengo wa kisiasa wa akina
Sagilu na Lesulia. Mashauri ni rafikiye Ngoswe, mwanawe Mtemi Lesulia. Ngoswe anafahamika zaidi
kama mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya, kando na kukusanya ushuru kutoka katika mashamba
yanayomilikiwa na wazazi wake.

Cheiya anatoka katika familia ya kimaskini lakini baada ya elimu yake na kukutana na Mashauri,
anakengeuka na kuanza kuhusudu pesa, na hii ndiyo sababu anashawishiwa na Sagilu kwa urahisi.
Baada ya mtemi Lesulia kujua kwamba mwanawe Sagilu anamuunga mkono Lonare, anapanga njama ya
kuzua vurugu wakati wa uteuzi ili Lonare asipate kuteuliwa akaishia kushindana naye. Anafanya hivi ili
Sagilu kwa upande wake achukue uongozi wa eneo-bunge la Matango. Ngoswe hamuungi babake mkono
katika azimio lake la kuuzua vurugu. Anashangaa ni kwa nini babake yuko radhi watu wapoteze maisha
yao ili yeye na rafiki yake watwae uongozi. Yeye pia anaasi na kujiunga na Mashauri katika kumuunga
mkono Lonare.

Mangwasha anafutwa kazi kwa kuwa anamuunga mkono Lonare ambaye ni mpinzani wa Mtemi Lesulia.
Analazimika kujiunga na mumewe katika kuendeleza biashara kwenye duka lao. Katika hali hii,
Mangwasha anaweza kujionea hali ya mtoto wa kiume;

anamwonea huruma mtoto wa kiume kwani ameishia kutelekezwa huku jamii ikimwangazia zaidi mtoto
wa kike. Hivyo, kwa msaada wa mashirika mbalimbali, anafungua afisi mjini Taria ili kuwashughulikia
vijana hao, ambao aliona wanaendelea kuangamia taratibu.

Baada ya uteuzi kufanyika, Sagilu anashindwa na mpinzani wake, Mwamba. Jambo hili linamuudhi
Mtemi Lesulia ambaye anaamua kuacha sheria ifuate mkondo wake, kwani mara zote amekuwa
akiwalinda marafiki zake dhidi ya sheria, hasa Sagilu ambaye ni fisadi mkubwa. Kufuatia hili pia, Chifu
Mshabaha anafutwa kazi na waziri anayehusika na masuala ya utawala.

Sihaba, ambaye anaendesha biashara ya ukahaba, anakamatwa na majengo anayoendelezea biashara hiyo
yanafungwa. Miezi minne baada ya kushindwa katika uteuzi, Sagilu anapatwa na kichaa. Mkewe Mtemi
Lesulia, Nanzia, naye anapatwa na msongo wa mawazo na kulazwa hospitalini, baada ya kupokonywa
jengo la kibiashara la Skyline Mall. Ugonjwa wake unamsababishia kifo. Hata hivyo, kabla hajafa,
anamweleza Ngoswe kwamba yeye ni mtoto wa Sagilu, wala si mwanawe Mtemi Lesulia. Hali ya Sagilu
inaendelea kuwa mbaya hospitalini. Mwishowe anamwomba mwanawe, Mashauri, msamaha kwa
kumwendea kinyume. Mashauri akamsamehe. Mali ya Sagilu inatwaliwa na serikali kwani aliipata kwa
njia ya ufisadi. Wakati huu pia inafahamika kwamba Cheiya aliwahi kutumiwa kumtilia Lonare sumu
kwenye kinywaji chake. Anakamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi.

VIDOKEZO MUHIMU

 Nchi inajitayarisha katika uteuzi wa viongozi.


 Sagilu anakumbwa na misukosuko mingi mingine ya kujitakia huku umaarufu wake ukididimia.
 Mwanawe Sagilu Mashauri aliyesomea taaluma ya usanifu majengo anamchumbia Cheiya
ambaye ni yatima. Cheiya alikuwa amesomea amesomea taaluma ya uuguzi.
 Cheiya anabadili mkondo wake wa kimaskini. Anapopata ajira na kuishi maisha tofauti,
yasiyolingana na kipato chake kwa sababu ya tamaa yake.
 Katika uhusiano wake na Mashauri anakodishiwa nyumba katika mtaa wa Majuu na kununuliwa
gari.
 Sagilu anaanza kumtongoza Cheiya vile vile na kumnunulia zawadi za bei ghali.
 Ngoswe ambaye ni mwanawe Mtemi Lesulia na rakifiye Mashauri waliosoma pamoja,
anamjulisha Mashauri kuhusu uhusiano anaoshuku baina ya Sagilu na Cheiya.
 Ingawa Mashauri haamini, Ngoswe anampleka hadi katika hoteli ya Saturn anapowaona wakitoka
katika ghorofa ya juu. Jambo hili linamkasirisha Mashauri na kumkana baba yake kama mzazi.
 Ngoswe hafanyi kazi yoyote. Mtemi amempa mamlaka ya kukusanya kodi ya mjumba yao. Pesa
hizi anazifuja kwaraha na anasa.
 Ngoswe vile vile ni mlanguzi wa dawa za kulevya. Wakuu wa serikalini hawajaweza
kumkamata wala kumshataki kwa kuwa yeye ni mwana wa Mtemi na Mtemi ni mkubwa.
 Ingawa serikali inapitisha sheria kuhusu mihadarati, hakuna chochote kinachofanywa kuhusu
dawa hizo wanaouhusika hawakuwa na pa kuanza.
 Mashauri anafika katika kikao cha Lonare na wafuasi wake ambapo anakiri uovu alioufanyia
Lanare kama vile kubomoa jumba lake na mengine mengi.
 Kwa kuasi babake, anajisajili na chama cha ushirika na kuapa kumwuunga mkona Lonare katika
uchaguzi mkuu.
 Mashauri anahama mtaa wa Majuu na kwenda kuishi katika mji wa Majengo kwa kuhofia
usalama wake.
 Mtemi anapanga njama ya kuzua vurugu wakati wa uteuzi ili Lonare asiteuliwe akaishia kuwa
mpinzani wake.
 Ngoswe anaghadhabishwa na mipango ya baba yake na kushanga ni vipi babake atahiari vijana
wapoteze maisha yao ili atwae uongozi.
 Lombo mwanawe Lonare ambaye amehitimu kama daktari ujerumani anarudi nyumbani ili
amsaidie baba yake katika kampeni. Wanakutana na Mashauri na kuungana katika kampeni za
Lonare.
 Mangwasha anafutwa kazi kwa kuwa anamuunga mkono Lonare. Anaelekea nyumbani
anakomsaidia mumewe kuuza bidhaa katika duka lao.
 Mangwasha anaanza kumwonea huruma mtoto wa kiume kwani hana mwekekezi. Licha ya kuwa
jamii inamchulia mwanamume kama nguzo, imemtelekeza mvulana na kumshika msichana.
 Sihaba anakamatwa kwa kuendesha biashara ya ukahaba katika mtaa wa Majuu katika nymba
zake za Red Beads Lodgings. Wasichana hao wanashiriki mapenzi na wazee. Wanapofurushwa
wanawauliza iwapo waliowaokoa wataweza kuwanunulia chakula, mavazi au hata vipodozi.
Wasichana wale wanarudishwa makazini kwao na kurudishwa shuleni na wale wasiokuwa na
wazazi wakapelekwa katika makao ya mayatima.
 Sihaba anaachiliwa siku hiyo hiyo na kutokomea kutojulikana. Mashauri anamkabili baba yake
na kutishia kumwanika katika magazeti iwapo ataendelea kuficha uovu wa Sihaba.
 Katika uteuzi, Mtemi Lesulia anateuliwa kupeperusha bendera ya chama cha Mamlaka Lonare
naye anawakilisha chama cha Ushirika huku Mwamba akishinda kuwania kiti cha eneo-bunge
cha Matango. Sagilu anashindwa na mpinzani wake.
 Miezi minne kabla ya uchaguzi Mbungulu na Mangwasha wanamwona Sagilu mjini huku akikaa
kama aliyerukwa na akili.
 Mashauri anasimulia Lombo kuhusu hadithi walisoma katika somo la Historia huhusu kiongozi
mmoja wa nchi ya Ufaransa. Kisa hiki kinarejelea Nanzia ambaye ana wasiwasi kuhusu jumba
alilonyakua na kulibadilisha jina kuwa Skyline Mall.
 Wakiwemo katika mazungumzo yao, Mashauri anapokea simu kutoka kwa Lonare na
kumfahamisha hali ya Sagilu si nzuri kuwa anavua hata nguo hadharani. Lombo anamshauri
kwenda kumshughulikia babake kimatibabu.
 Baada ya Sagilu kupelekwa hospitalini, hale yake indaendelea kuimarika. Lombo ndiye
anashughulikia Sagilu pale hospitalini Taria. Sagilu anamwomba Mashauri msamaha pale
hospitalini.
 Mali ya Sagilu inatwaliwa na serikali kwani aliipata kwa njia haramu.
 Mangwasha anafungua ofisi ya kushughulikia vijana na watoto mitaani huku akipata ufadhili
kutoka kwa mashirika mbalimbali.
 Chifu Mshabaha anatembelea ofisi hii kumwomba Mangwasha msahama. Aidha anakiri
kutolipia biashara zake ushuru na sasa alidaiwa pesa nyngi au biahsara hizi zifungwe.
 Siku ya kupokezwa vyeti vya uteuzi, Lonare anamwona mwanamke ambaye alitumiwa na Lesulia
kumtilia sumu kwenye kinywaji wanapoenda nyumbani. Mashauri anamtambua kama Cheiya
aliyekukwa Mpenziwe. Wanakimbizana naye hadi pale ambapo anakamatwa na kufikishwa
katika kituo cha polisi.
 Nanzia anapatwa na msongo wa mawazo na kulazwa hospitalini baada ya jengo lake la Skyline
Mall kutwaliwa na serikali. Hali hii ilisababisha mauti yake. Kabla hajafa anamfahamisha
Ngoswe kuwa babake halisi ni Sagilu wala si Lesulia.
 Ngoswe anamtembelea Sagilu nyumbani na kufichuliwa kuwa hata ndugu yake aishiye Ulaya si
wa Lesulia bali Mhindi waliofanya biashara na Nanzia.
 Inabainika kuwa Lesulia na Nanzia walikaa kwa muda mrefu kabla kupata watoto na ndipo
Nanzia akahusiana na Sagilu akampata Ngoswe.
 Ngoswe anamfahamisha Mashauri kuwa wao ni ndugu. Baada ya mazishi ya Nanzia
wanampeleka mzazi wao katika hospitali ya matibabu maalumu ya akili.
 Umaarufu wa Mangwasha unaendelea kuongezeka. Anatangazwa kuwa miongoni mwa
wanawake walioleta mabadiliko makubwa ya vijana nchini.

Masuala Makuu Yanayojitokeza Katika Sura Ya Tano

1. Suala la ukengeushi linaangaziwa katika kisa cha Sagilu na Cheiya. Sagilu kuandamana na
msichana wa umri wa Cheiya ni kuonyesha hali ya kutojiheshimu na kutojali maadili. Cheiya,
kwa upande mwingine, yuko tayari kujishusha hadhi kwa sababu ya tamaa na kuandama pesa.
2. Hali ya kukengeuka pia kunajitokeza pale ambapo mmoja wa wasichana wanaofanya ukahaba
kwa Sihaba anasikika akisema, “…za kutununulia chakula, nguo au hata vipodozi?" (uk. 142).
Kauli hii inaashiria kwamba wasichana hawa wamekengeuka kiasi kwamba hawajithamini, na
hawathamini kazi kama njia halali ya kujitafutia riziki.
3. Suala la malezi mabaya pia linajitokeza katika sura hii kwani Ngoswe ni mwana kindakindaki
aliyeengwaengwa na kudekezwa kupita kiasi (uk. 122). Yeye anaendesha biashara ya kulangua
dawa za kulevya na babake, Mtemi Lesulia, anamlinda kiasi kwamba hata wakuu serikalini
hawawezi kumkamata (uk. 122-123).
4. Sifa ya Sagilu kama mtu fisadi inajitokeza. Anashirikiana na mwanawe kuifisidi nchi kwa
kushiriki biashara ya vipusa na meno ya ndovu, na Mashauri anaposhtakiwa, kesi zenyewe
zinazimwa kabla ya kuanza (uk.127).
5. Hatua ya Ngoswe na Mashauri kuungana katika kumpigia kampeni Lonare inaashiria nafasi ya
vijana na uwezo wao katika kuchangia mabadiliko chanya katika jamii.
6. Ujasiri wa Mangwasha unaendelea kuonekana katika sura hii. Anapokabiliana na Chifu
Mshabaha baada ya kupoteza kazi yake, anamwambia chifu huyo kwamba yeye na wengine
wanaotaka mabadiliko watazibomoa hisia zao za ukabila, ubinafsi na chuki ulioendelezwa na
utawala wa Lesulia (uk. 136).
7. Tatizo la umaskini uliokithiri linawafanya watu kufanya mambo kinyume na maadili ya kijamii.
Kwa mfano, baadhi ya wazazi wanawaruhusu wana wao wa kike kushiriki ukahaba kama njia ya
kujitafutia riziki (uk. 143).
8. Kufutwa kazi kwa Chifu Mshabaha, kukamatwa kwa Sihaba, Nanzia kupoteza jengo la Skyline
Mall na hatimaye kufariki, na Mangwasha kuanzisha afisi ya kushughulikia mtoto wa kiume
ni hatua muhimu katika ujenzi wa jamii mpya, jamii inayozingatia maadili na kuwajali watu.
9. Kupitia mawazo ya Mangwasha, tunapata kuelewa falsafa ya mwandishi kuhusu maisha: kila
mtu ni mhusika mkuu katika kisa cha maisha yake mwenyewe, na jambo la muhimu ni
mhusika huyo kuipa hadhira yake kitu cha kuwatia moyo maishani.

Wahusika Katika Sura ya Tano:

a. MTEMI LESULIA
i. Fisadi-anatoa vifurushi vya pesa ili vijana wahongwe waweze kuleta vurugu siku ya uteuzi
wa viongozi.
ii. Kiongozi dhalimu-anatumia vyombo vya dola vibaya. Ametoa Maagizo kwa vikosi vyake
vya polisi ili walinde vijana watakaosababisha vurugu na kuharibu kura za mpinzani wake.
iii. Mwenye hasira- anamkemea Ngoswe kwa hamaki na kumwamuru aondoke baada ya
Ngoswe kusema haikuwa haki alichokuwa akifanya.
iv. Mpyaro- anamwita Ngoswe Lumbwi.
v. Katili- anamtumia Cheiya kumtilia Lonare sumu kwenye kinywaji ili kumwangamiza.
Baada ya kugundua kuwa Mashauri anamuunga mkono Lonare, anamfuta kazi.
vi. Mlezi mbaya-alimlelea Ngoswe kwa kumwengaenga na kumdekeza kupita kiasi.
vii. Mnafiki- serikali yake inapitisha sheria kuhusu mihadarati ila Ngoswe mwanawe ndiye
anayeendeleza biashara ile haramu.

b. SAGILU
i. Mzinifu/mkware- ingawa ana mke anashiriki mahusiano ya kimapenzi na Cheiya, Nanzia
pamoja na wanawake wengine.
ii. Msaliti- anamsaliti Mashauri kwa kushiriki mapenzi na Cheiya ambaye ni mpenziwe.
iii. Mtamaduni- alienda kutakaswa katika kitovu chao Munyuni kwa kuvunja mwiko.

c. CHEIYA
i. Msaliti- analisaliti penzo lake kwa Mashauri kwa kufanya mausiano na babake Mashauri.
ii. Katili- anatumiwa na Lesulia kutaka kumwangamiza Lonare kwa kumtilia sumu kwenye
kinywaji.
iii. Mwenye tamaa- ana tamaa ya kupata pesa ndipo anajihusisha na mapenzi na Sagilu.
iv. Msomi- Ameelimika na kuwa muuguzi.

d. MASHAURI
i. Mapenzi ya dhati-anamvisha Cheiya pete ya uchumba kisha anamkodishia nyumba katika
mtaa wa Majuu na hata kumnunulia gari.
ii. Msamehevu- anamsamehe baba yake na hata kumshughulikia katika kumtafutia matibabu.
iii. Mwenye utu- anadhihirisha utu wake anapomtafutia baba yake matibabu hata baada ya
kumtendea maovu.
iv. Msomi- amesoma hadi chuo kikuu urusi na kuhitumu kama msanifu majengo.
v. Fisadi- pamoja na babake walifisidi vupusa na meno ya ndovu kabla hajabadili mienendo.

e. NGOSWE
i. Mlanguzi wa mihadarati- anafanya biashara ya kulangua dawa za kulevya ambazo
anazisambaza hata kwnye shule na vyuo.
ii. Mzinzi- anawabadilisha warembo mbalimbali wa mji usiku na kila uchao.
iii. Fisadi- anaendesha biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya bila kukamatwa.
iv. Mwenye utu- anamkabili baba yake anapotaka kuhatarisha maisha ya vijana katika kuzua
vurugu wakati wa uteuzi. Anamwambia babake kuwa si haki kufanya hivyo.
v. Katili. Dawa unazouza zinawafanya vijana mazube na wengine kupoteza maisha yao.

f. MANGWASHA
i. Jasiri- anakabiliana na Chifu Mshabaha bila woga baada ya kufutwa kazi. Anamwambia
kuwa yeye na wengine wanaotaka mabadiliko watazibomoa hisia zao za ukabila, ubinafsi na
chuki,
ii. Mwenye utu- anafungua ofisi ya kushughulikia masuala ya vijana na watoto wa mitaani.

g. CHIFU MSHABAHA
i. Katili- Namfuta Mangwasha kazi kwa kuwa anaunga mkono Lonare.
ii. Mbaguzi –afisi yake imejaa Wakule kama waajiriwa.

Maudhui Katika Sura ya Tano:

1. Ufisadi
a) Mtemi Lesulia anatoa mafurushi ya pesa ili kuharibu uteuzi wa Lonare.
b) Sagilu na mwanawe Mashauri wanifisidi serkali kwa kufanya biashara ya vupusa na meno ya ndovu.
c) Nanzia alinyakua jumba refu lililoka katikati ya mji kutoka kwa mlowezi anayefurushwa nchini.
Analibadilisha jina na luliita Skyline Mall.
d) Chifu Mshabaha anakiri kutolipia ushuru katika biashara zake.
e) Sihaba anaachiliwa baada ya kukamatwa siku hiyo hiyo aliyotiwa ndani.

2. Umaskini
a) Cheiya aliishi kimaskini hadi alipopata kazi na kuanza kuishi maisha yasiyo ya kiwango chake.
b) Kutokana na umaskini, wazazi wengine wanapeleka watoto wao kufanya ukahaba katika Red Beads
Lodgings.
c) Wapo vijana waliohitimu vyema vyuoni lakini kwa sababu ya ukosefu wa ajira na ulitima miongoni
mwa wazazi wameishia majiani na mitaani wakivuta bangi na kupora mali za watu.

3. Uozo Katika jamii


a) Sihaba nashirikisha wasichana wadogo katika ukahaba.
b) Mangwasha anaona wasichana wachanga wanaobeba watoto wachanga migongoni kule mitaani.
c) Sagilu anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Cheiya aliye mpenzi wa mwanawe Mashauri.
d) Nanzia anashiriki mapenzi na Sagilu na kumzaa Ngoswe.
e) Mashauri anamwambia Ngoswe kuwa hawezi kuelewa kuhusu mapenzi kwani
huwabadilishabadilisha wanawake.

4. Utu
a) Afisi ya huduma za vijana inawashughulikia wasichana waliofanyishwa ukahaba na Sihaba.
b) Mashauri anamtafutia baba yake matibabu hata baada ya kumtendea maovu.
c) Watoto wanapomfuata Sagilu huku wakimcheka, Mangwasha na Mbungulu wanawafurusha na
kuwaambia si vyema kumcheka mgonjwa.

5. Usaliti
a) Sagilu anamsaliti mwanawe Mashauri kwa kushiriki mapenzi na Cheiya.
b) Sagilu pia anamsaliti rafikiye Mtemi Lesuilia kwa kufanya mapenzi na mkewe Nanzia na kumpata
Ngoswe.
c) Ngoswe anamgeuka baba yake na kuingia upande wa wapinzani ingawa hapo awali alimlea kwa
kumdekeza na kumlinda afanyapo biashara harumu.
d) Baada ya Mangwasha kumfanyia Chifu Mshabaha kazi kwa muda mrefu mwishoni anamfuata kazi.
e) Mtemi Lesulia anawasaliti marafiki zake kama vile Chifu Mshabaha na kukosa kuwasaidia ila
anaacha sheria ichukue mkondo wake.

Maudhui Zaidi Katika Sura ya Tano:


Tamaa, Ukware, Ukengeushi, Elimu, Usaliti, Anasa na starehe, Malezi, Ndoa, Mabadiliko,
Ushauri na nasaha, Matumaini

MUHTASARI WA SURA YA SITA


Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, Lonare anaripotiwa kupotea. Kama ilivyofanyika katika uchaguzi
uliopita na kumfanya Mtemi Lesulia kuchaguliwa bila kupingwa. Hata hivyo, wafuasi wake wanaamua
kuwa wakati huu watampigia kura, awepo au asiwepo. Hii ni licha ya Mtemi Lesulia kusema kwamba kiti
cha mgombea nafasi ya mtemi katika Chama cha Ushirika kifutiliwe mbali kwani Lonare mwenyewe
hayupo. Kutokana na hayo, wafuasi wa Lonare walikuwa katika taharuki kubwa. Wengine walikuwa
wamekata tamaa wakidhani kuwa hakukuwa na namna ya kuwaauni kutoka kwa changamoto ile.

Asubuhi ya siku ya uchaguzi mkuu, Lonare anapatikana nje ya nyumba ya Mangwasha akiwa katika hali
mahututi. Wafuasi wake waliokuwa wameishiwa na matumaini wanajitokeza kwa wingi kwenda
kumpigia kura huku mwenyewe akipelekwa hospitalini.

Akiwa hospitalini, anamshauri Ngoswe kuacha biashara ya mihadarati kwani kwa kufanya hivyo,
atakuwa anaokoa kizazi kizima kutoka katika maangamizi. Lonare anamshauri pia kuacha biashara
nyingine haramu anazofanya na kujitenga na mitandao inayoendesha biashara hizo.

Hatimaye Lonare anachaguliwa mtemi wa nchi ya Matuo. Baada ya ushindi huu, anaihutubia nchi.
Anaahidi kufufua uchumi wa nchi na kukata mirija ya ufisadi. Anaahidi pia kwamba serikali yake
itashughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana.

Isitoshe, anaahidi kwamba atahakikisha kuwa kuna usawa wa kijinsia nchini huku akisema kwamba
Matuo imesambaratishwa na mfumo wa ubabedume. Anawaomba wananchi wenzake kuepuka ukabila na
kufichua maovu yanapofanyika nchini. Anaamua kuwasamehe maadui wake wa kisiasa.

VIDOKEZO MUHIMU

 Lonare anatoweka siku chache kabla ya uchaguzi mkuu. Msako mkali unaendelezwa na wafuasi
wake.
 Siku moja kabla ya uchaguzi Mtemi Lesulia anatoa uamuzi kuwa kiti cha mgombea nafasi ya mtemi
katika chama cha Ushirika kifutiliwe mbali kwa sababu Lonare hayupo.
 Asubuhi ya siku ya uchaguzi mkuu, Lonare anapatikana nje ya nyumba ya Mangwasha akiwa hali
mahututi.
 Lombo na Mashauri wanamkimbiza hospitalini kwa matibabu ya dharura. Vituo vya redio na runinga
vinatangaza kupatikana kwa Lonare.
 Habari za kuonekana kwa Lonare zinaenea kote na wafuasi wake waliojishughulisha na shughuli
mbalimbali kwa kukata tamaa wanaacha shughuli zao na kuelekea katika vituo vya uchaguzi.
 Pale hospitalini, Lonare anamshauri Ngoswe kubadili mienendo yake miovu kama vile kulangua
mihadarati. Anamwomba afunge majumba yake yote ya ufasiki na kwa kufanya hivyo atakuwa
akiokoa kizazi kutoka katika mangamizi.
 Ngoswe anajiunga na Mangwasha katika juuhudi zake za kuimarisha maisha ya vijana.
 Lonare anachaguliwa kuwa Mtemi wa nchi ya Matuo naye Mwamba anakuwa Mbunge wa eneo la
Matango.
 Sagilu haamini habari za kuchaguliwa kwa Lonare na Mwamba. Naye Mtemi Lesulia anadai kutotaka
ushindi kwani cheo cha mtemi kina majukumu mengi. Marafiki zake wanaamua kumwacha atulize
nfsi yake.
 Mbwashu anaabiri ndege na kuelekea ulaya na hakurudi. Alingoja kuona kama mkono wa sheria
ungemrudisha Matuo kwa kufunguliwa mashtaka.
 Lonare anatangaza siku mbili za kusherehekea ushindi wake. Siku ya pili anaagiza wananchi wa
Matuo na waandishi wa habari wajumuike katika uga wa kitaifa.
 Lonare anatoa hotuba yake inyoangazia masuala mbalimbali kama vile kuinua uchumi, kukamatwa
kwa mafisadi waliopora mali ya umma, kupigana na ukosefu wa kazi kwa vijana, usawa wa kijinsia
miongoni mwa mengine.

Masuala Makuu Yanayojitokeza Katika Sura Ya Sita

1. Ujumbe wa kutokata tamaa katika maisha unajitokeza katika sura hii. Licha ya kwamba
Lonare amenyanyaswa sana na utawala wa Mtemi Lesulia, hakati tamaa.
2. Wafuasi wa Lonare hawakati tamaa katika azimio lao la kumchagua kama mtemi. Hii ndiyo
sababu wanaamua kumpigia kura tu, awepo au asiwepo.
3. Katika hotuba yake Lonare, ni wazi kwamba serikali atakayounda itakuwa serikali bora kwani
ufisadi utamalizwa na umaskini kushughulikiwa, sawa na suala la Vijana na ajira.
4. Ni dhahiri kwamba mambo haya yakishughulikiwa, Matuo itakuwa nchi thabiti zaidi.

Wahusika Katika Sura ya Sita:

a. SAUNI
Mwenye matumaini- anawahimiza wafuasi wa Lonare wasikatize juhudi za kumsaka.
b. MWAMBA
Mwenye matumaini-anawaambia wafuasi wa Lonare kuwa hawawezi kukata tamaa kabla
hawajfahamu yaliyomfika.
c. MANGWASHA
Jasiri- watu wanapoogopa kumwendea Lonare alipokuwa yu hali mahututi, yeye anamwendea na
kumtikisa.

d. LONARE
Mshauri mwema- anamshauri Ngoswe afunge majumba yake ya ufasiki na akatize biashara
yake ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na biashara nyingine haramu.
e. MTEMI LESULIA
Mpyaro- anawaita vijana waliotuma kumwangamiza Lonare mabwege.
Katili-alikuwa amewatumia vijana kumwangamiza.
f. MBWASHU
Msaliti-anapoona mambo hayamkai baada ya Mtemi Lesulia kushindwa katika uchaguzi,
anaabiri ndege na kuelekea Ulaya.

Maudhui Katika Sura ya Sita:

a. Ukatili
Lonare anatekwa nyara siku chache kabla ya uchaguzi.
b. Ulaghai
Siku ya kupiga kura kulikuwa na visa kadha vya ulaghai mjini Taria.
c. Utamaushi
Baadhi ya wafuasi wa Lonare wanatamauka na kususia uchaguzi hadi pale wanaposikia habari za
kupatikana kwake.
d. Uongozi mbaya
i. Katika hotuba ya Lonare anaangazia uongozi mbaya wa Mtemi Lesulia uliofisidi pato la nchi.
ii. Mtemi Lesulia anakiri kuwa aliwasaidia wengine wa marafiki zake kusafirisha bidhaa ghushi ili
watajirike.
e. Usaliti
i. Mbwashu na marafiki za Mtemi Lesulia wanamwambaa na kumwacha peke yake.
ii. Mbwashu anapoona mambo hayamkai vyema anaabiri ndege na kutorokea Ulaya.

Maudhui Zaidi Katika Sura ya Sita:


Uwajibikaji, Matumaini, Mabadiliko, nafasi ya vijana katika jamii, Uogozi bora

You might also like