Download as doc, pdf, or txt
Download as doc, pdf, or txt
You are on page 1of 8

TAMTHILIA

UTANGULIZI

 Tamthilia ni utanzu ambao hutegemea mazungumzo na uigizaji ili kuuwasilisha ujumbe

wake. Somo hili linachunguza utanzu huu katika somo hili, maana na chimbuko la

tamthilia vimetolewa. Aidha kuna historia fupi ya tamthlia na aina za tamthilia. Sifa za

tamthilia zimejadiliwa pamoja na uhakiki na uchambuzi wa tamthilia.

DHANA NA MAANA TAMTHILIA

 Tamthilia ni neno la kiarabu lenye maana ya kumithilisha au kufananisha. Katika

Kiswahili tamthilia linatumika kwa maana ya michezo ya kuigiza. Katika tamthilia huwa

kuna ufananishaji ambapo mwigizaji hujifananisha na mhusika wa mchezo wakati wa

kuigiza. Kulingana na kamusi ya Kiswahili sanifu, tamthilia ni utungo wa kisanaa

ambapo huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo.

 Kutokana na maelezo hayo tunaweza kusema kwamba tamthilia ni utungo ambao

unaweza kuwa umeandikwa au haukuandikwa unaoliweka wazo linalowasilishwa katika

umbo la tukio linaloliwezesha kutendeka mbele ya hadhira. Katika somo letu

tutashughulikia kuhusu tamthilia iliyoandikwa ambapo mtindo wa mazungumzo ya

wahusika umetumika. Kigezo kikuu cha tamthilia ni kuweza kuwasilishwa jukwaani na

kutazamwa na hadhira.

 Tamthilia huwa na umbo lenye mpangilio maalum, mtiririko wa vitendo vitendwavyo

pahala fulani pa kutendea na kila kitendo kikawa na maonyesho yake k.v onyesho la

kwanza , la pili la tatu nk. Tamthilia ni fasihi au sanaa tendaji ambayo si ya kusomwa tu

1
bali pia huigizwa. Tamthilia hutafsiriwa na kufasiliwa katika vitendo vinavyoonekana,

miondoko na sauti jukwaani. Hata hivyo tamthilia huweza kusomwa kimya kimya.

 Mazungumzo baina ya wahusika sio majibizano tu ya usemi au kauli tupu bali ni msingi

mkuu wa kuendelezwa ma kukuzwa kwa tendo kuu la kimaigizo katika tamthilia Fulani.

Kama sanaa ya utendaji, kwa hivyo suala la uigizaji na utendaji kwenye jukwaa ni

muhimu sana na lazima lichunguzwe katika uchambuzi wowote wa tamthilia.

CHIMBUKO LA TAMTHILIA

 Chanzo cha sanaa za maigizo ambazo ndizo asili ya drama au tamthilia ni sherehe za

kidini au matambiko. Wagiriki wa zamani walicheza na kuimba wakizunguka

madhabahu au mahali patakatifu na kuigiza visasili na visa kale vilivyolingana au

kufungamana na maisha ya miungu wao.

 Katika sherehe za matambiko, kulikuwa na drama yenye utendaji, uigizaji na mavazi

maalum ambayo pia yanaitwa maleba au mapiku yaliyotumika tu wakati wa sherehe

hizo. Uchina pia kulizuka drama iliyoambatana na sherehe za kidini na vilevile Misri

katika miaka ya 2000 k.y.m . Tamthilia za kwanza kuwahi kuandikwa zilitokana na

utamaduni wa Ugiriki katika karne ya 6 k.y.m

 Katika Afrika hali kama hiyo inajidhihirisha. Dhana ya sanaa za maigizo na hata

tamthilia ikiwa na maana ya utendaji na uigizaji, haikuanza tu na majilio ya wakoloni

hapa afrika. Matambiko katika jamii mbalimbali yalizaa aina ya utendaji katika baadhi

ya ngoma, majigambo ya kiasili na masimulizi mbalimbali ya mwafrika.

2
 Katika utamaduni wa waswahili, kabla ya kuja kwa watu wa ulaya ya magharibi na

kuleta drama yao, waswahili walitunga na kughani tendi ambazo baadhi yake

ziliandikwa kwa hati ya kiarabu.

 Baadhi ya tendi zinaelezea kwa namna ya maigizo, matendo na kutofautisha maneno ya

wahusika mbalimbali na wasimulizi, maswala mbalimbali ya utamaduni wa waswahili.

Maigizo hayo hutoa maelezo ya mandhari, mavazi na vifaa vingine ambavyo yote

yanafanana na jukwaa la kisasa tunalolisoma na kulitumia katika michezo ya kuigiza.

HISTORIA FUPI YA TAMTHILIA YA KISWAHILI

 Tamthilia andishi ililetwa katika utamaduni wa waswahili na lugha ya Kiswahili wakati

wa ukoloni. Mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi na mandeleo ya kiteknolojia yalileta

drama iliyojitenga na dini na kujisimamia. Tamthilia zikaanza kuandikwa na kuigizwa

majukwaani au kwenye kumbi zilizojengwa maalum kwa shughuli hiyo. Hii ndiyo

tamthilia iliyoletwa na wazungu.

 Tangu miaka ya awali ya utawala wa wazungu hadi uhuru, kuliigizwa michezo ya kuigiza

ya kiulaya na mingi ilikuwa miongoni mwa sanaa za maigizo za kibwanyenye. Tamthilia

hizi zilidumu baina ya 1920-1960 katika mashule, na ilitokana na ustaarabu wa kizungu

na yenye madhumuni ya wazungu kujifurahisha na kujiliwaza.

 Michezo hiyo ya mwanzo ilitia watoto a shule na waigizaji wengine katika miji mikubwa

k.v Nairobi, Mombasa, Dar es salaam na Kampala katika kumbi zilizoitwa ‘little

theatres’ kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakoloni.

 Michezo ya awali ilimbeza mwafrika na tabia zake hasa hali ya kutojua kusoma na

kuandika. Baadhi ya tamthilia hizo zilitafsiriwa kwa Kiswahili na wamishonari k.v

3
‘Bwana amekufa, (The Lord Is Dead) na ‘Wanawake wenye akili (Intelligent Girls). Huu

ukawa mwanzo wa thamthilia zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

 Katika miaka ya arobaini na hamsini, wazungu ambao awali walikua wameona sanaa za

maigizo za kiafrika kama sanaa za kishenzi, waliamua kuziendeleza sanaa hizo.

 Ngoma na maigizo hayo yakaanza mashuleni ili yaonyeshwe kwa wananchi kama

sehemu ya kuburudika kwa mwafrika. Makundi yakaundwa mashuleni kwa madhumuni

hayo ya mchezo kutafsiriwa katika lugha ya Kiswahili.

 Baadaye kwenye miaka ya hamsini na sitini, michezo ya Kiswahili iliandikwa ambayo

ilivuma mashuleni na badhi yake kuchapiswa. Mifano ya michezo hiyo ni Afadhali

Mchawi, Mgeni Karibu, Nakupenda Lakini, Nimelogwa Nasiwe na Mpenzi n.k.

 Mnamo mwaka 1957 kulianzishwa mashindano ya maigizo mashuleni amabayo yalitoa

changamoto kubwa kuhusiana na utoaji wa vitabu. Michezo hiyo iliendelea mashuleni

hadi mwaka wa 1963 ambapo msaada kutoka shirika la British Council Library

ulikatizwa.

 Katika kipindi cha ukoloni hasa kuanzia miaka ya arobaini na kuendelea, nje na ndani ya

mashule kulizuka vichekesho. Vichekesho hivyo vilikua na lengo la kuburudisha na

havikuwa na maudhui mazito kujadili matatizo katika jamii.

 Vichekesho vya wakati wa ukoloni viliwacheka watu washamba na kuwadhihaki

wasiojua ustaarabu wa kizungu na lugha ya kimombo.

 Kulianzishwa pia maigizo ya redioni ambapo mwafrika alikuwa mhusika mkuu. Kupitia

michezo hiyo, ilidhaniwa kuwa mwafrika alikuwa mhusika mkuu.

4
 Kupitia michezo hiyo, ilidhaniwa kuwa mwafrika angesahau harakati za kudai uhuru na

badala yake kuanza kuucheka ujinga wa mwafrika mwenzake. Hata hivyo juhudi zote

hizohazikufua dafu na mwafrika alipigana na kujinyakulia uhuru.

 Baada ya uhuru, sanaa za maigizo zilichukua sura mpya. Miaka ya sitini, kutokana na

juhudi za kisiasa, kielimu na kitamaduni wa mwafrika na maadili mbalimbali k.v.falsafa,

dini, siasa, utamaduni, kasumba matatizo ya jamii, n.k. tamthia zingine zilitafsiriwa

kutoka kwa lugha za kigeni, hasa lugha ya kingereza k..m. Juliasi Kaizari, Mabepari Wa

Venisi, Mfalme Edipode n.k.

 Baadaye, kumeibuka watunzi wengi ambao wametunga na kuigiza tamthilia mbalimbali.

Watunzi k.v E.Hussein, D Mulwa, A Mazrui, C.N Chacha, P. Muhando, n.k. wametunga

tamthilia nyingi ambazo zimeendelea kuzingatia matatizo ya jamii na namna ya kuishi

vyema.

 Maudhui ya tamthilia hizo yanahusu maendeleo ya kisiasa kiuchumi kitamaduni kidini na

kifalsafa. Mwafrika ameacha kumcheka asiyejua kusoma nankuandika na kuanza

kumcheka mwenzake anayemwiga mzungu na kuwa mzungu mweusi

AINA ZA TAMTHILIA

 Ujuzi wa vipengele mbalimbali vya tamthilia tulivyozungumizia unatusaidia kusoma na

kuelewa tamthilia vizuri. Tamthilia ni za aina kadha. Aina ina sifa zake maalum. Aina

hizo za tamthilia ni kama zifuatazo:

Tanzia

 Tamthilia ya tanzia huhusika na mambo yenye uzito kifikira na hisia katika na kihisia

katika maisha ya binadamu. Katika tamthikia za aina hii, mhusika mkuu hupewa sifa

5
nyingi zinazovutia na kupendeza. Lakini mhusika huyo hukabikwa na shida au tatizo

ambalo linaweza kumpata mtu yeyote. Namna anavyojaribu kukabiliana na tatizo hilo na

kupigana vita kuishinda shida inayomkabili, hali ya malimengu na hali au tabia ya

binadamu zinamfanya asiweze kufaulu na mwishowe anashindwa.

 Wahusika wa tanzia husawiriwa vizuri ndipo waweze kuaminika kama binadamu wa

kweli. Msuko wa tamthilia hiyo hukita kwenye wazo moja bila kuingilia viploti vingine

vidogo vidogo. Mbinu hizi huelekeza hadhira katika kukubali kwamba yaliyomfika

mhusika mkuu au nguli hayakuweza kuepukika. Kwa kuelewa kwamba nguli ni kama

aliyeingia katika mtego wa majaaliwa usioepukika kunatufanya tumwonee huruma; na

kule kuelewa kwetu kwamba haya yanaweza kumpata yeyote kati yetu, kunatutia hofu.

 Juhudi na ushujaa wa nguli katika kupambana na shida ile kufa na kupona hutupa moyo

wa kuendelea na mpambano na kutujaza imani inayotufurahisha kwamba binadamu si

kiumbe dhaifu. Katika tamthilia za tanzia, nguli wakati mwingine hufa au kuuawa, lakini

kifo chake si kama cha ajali barabarani.

 Kifo cha kitanzia huja baada ya mapambano marefu yanayochipuza hisia za ushujaa wa

binadamu. Kwa hivyo, msuko wa mapambano dhidi ya shida fulani huwa muhimu zaidi

katika tamthilia za tanzia kuliko kifo kinachotokana na mapambano katika fasihi ya

Kiswahili.

 Tamthilia tafsiri ya Mfalme Edipode (Sofokile) ni mfano mzuri wa tamthilia tanzia.

Zingine ni k.v mzalendo kimathi(N. Thiong’o na M. Mugo), kinjikitile ( E. Hussein),

Pungw ( S.A. MohMED) na kilio cha haki( A. Mazrui)

6
Futuhi

 Futuhi ni tamthilia ambayo hutuchorea picha yakini ya maisha ingawa usawiri huo hauna

undani na uzito kama ule unaojitokeza katika tanzia. Kwa sababu hii, majaaliwa ya

wahusika wa futuhi huathiri hadhira kihisia kwa kiwango cha chini zaidi kuliko tanzia

inavyoathiri wahusika wake.

 Lengo la kimsingi la futuhi ni kuchangamsha na huishia kwa namna ya kufurahisha.

Futuhi kwa hivyo hujikwepesha na masuala ya kuhuzunisha au kutia hofu. Athari ya

futuhi ya kuchekesha hutokana na matendo, mienendo ya wahusika na hitilafu au ila za

kuingiliana kwa kiusemi

Melodrama

 Melodrama inafanana sana na tanzia ingawa mara nyingi nguli wa melodrama

Humalizika na mshindi, matokeo yake yanasisimua sana na mwendo wa msuko wake

huwa ni wa haraka haraka zaidi. Wahusika wake huvutia na kufurahisha lakini hawana

sifa za kishujaa. Dhamira ya melodrama huzungukia mavutano kati ya wema na uovu au

ubaya. Miishio ya tamthilia hizi haina sifa ya matakasohisia kama ilivyo na tanzia bali

huwa ni aina ya ushindi wa mhusika mwema

Kichekesho

 Kichekesho ni aina ya tamthilianambayo huwa na uwezo wa kusababisha kicheko kingi

kutokana na mbinu za kufutuhi ya chini kama ucheshi, hali zisizokuwa za kawaida k.v

wahusika wasio wa kike kuvaa mavazi ya kike na wale wa kike kuvaa ya kiume, visa vya

mapenzi ya kuchekesha, mikimbizano jukwaani n.k.

Tanzia-ramsa

7
 Hii ni aina ya tamthilia ambayo huonyesha mabadiliko ya aina Fulani yanayogeuza

mwelekeo wa matukio ya kitanzia na kuufanya kuwa tofauti au wa kifurahisha. Tanzia-

ramsa ni kama tanzia inayoishia kwa furaha

Tamthilia za historia

 Hizi ni tamthilia zinazojengwa kutokana na mhusika au matukio ya kihistoria. Mfano ni

tamthilia za Kinjekitile (E.Hussein) na Mkwava wa Uhehe (M.M. Mulokozi).

Tamthilia tatizo

 Tamthilia tatizo huzungumzia swala Fulani katika jamii. Tamthilia hizi pia huitwa

tamthilia tasnifu na kuna mifano mingi katika fasihi ya Kiswahili k.v Mnara wawaka

Moto (R.Chimerah), mashetani (E. Hussein), kitumbua kimeingia mchanga ( S.A.

Mohamed), Mama Ee (A.K. Mwachofi), Natala ( K. Wa Mberia)

You might also like