Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 13

CamScanner

CamScanner
CamScanner
CamScanner
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA KILIMANJARO
MWONOZO WA USAHIHISHA KISWAHILI KIDATO CHA NNE

MEI 2024
1. SWALI I ii iii iv v vi vii Viii ix x
JIBU E A D C B B C E D A

Alama 01@ = 10
2.
ORODHA A I ii iii iv v vi
Alama 01@
ORODHA B D E C B F A
=6
3a. Mtahiniwa atapaswa kubainisha dhima iliyobebwa na mofu “ki” katika maneno aliyopewa kama
ifuatavyo:
i. Hudokeza umoja
ii. Hudokeza namna au jinsi
iii. Hudokeza masharti
iv. Hudokeza udogo/ kudunisha
v. Hudokeza upatanisho wa kisarufi.
Alama 01@ = 5
b. Mtahiniwa atapaswa kueleza athari hasi nne (4) za kutumia misimu katika lugha ya Kiswahili.
i. Misimu huharibu lugha kwa sababu siyo lugha sanifu
ii. Misimu ina chuku nyingi
iii. Misimu hutumia lugha ya matusi
iv. Misimu haidumu huzuka na kutoweka
v. Misimu hubagua ,kwani hutumiwa na watu wachache.
Alama 01@ = 04
4a. Mtahinwa aoneshe faida za viungo vya mwili vilivyotajwa vinavyotumika katika kazi za fasihi
simulizi.

Page 1 of 9
i. Macho; hutumika kuonesha hisia (uchungu, kulia hasira). Husaidia hadhira kujua hisia za fanani
ii. Mdomo; hutumika kuzungumza. Husaidia hadhira kupata ujumbe kwa kusikia kutoka kwa
fanani.
iii. Kichwa; hutumika kutunza kumbukumbu na kuonesha hadhira ishara kama vile kukubali au
kukataa.
iv. Miguu; hutumika kutembea, kuruka. Humsaidia fanani kutembea huku n akule na kuifanya
hadhira yake kuwa hai muda wote.
v. Mikono; hutumika kuonesha ishara. Humsaidia fanani kusisitiza jambo au ujumbe kwa kutumia
mikono.
Alama 1.5*4 = 06
b. Mtahiniwa afafanue matatizo matatu (3) ya kuhifadhi fasihi simulizi katika kanda za kunasia
sauti
i. Kukosekana kwa utendaji
ii. Fanani na hadhira hawataonana ana kwa ana
iii. Haitobadilika kulingana na mazingira na wakati
iv. Hutumia gharama
v. Ni mali ya mtunzi

Alama 01 @ = 03
5. Mtahiniwa anapaswa kueleza njia sita za uundaji wa msamiati/maneno katika lugha ya Kiswahili
kwa kuzifafanua kwa kutoa mifano.
i. Urudufishaji/Uradidi mf.nyepesinyepesi
ii.Uambatishaji mf.bwanamisitu
iii.Ufananisho mf.kengele
iv.Unyambulishaji mchezaji Hoja 00½ mfano (1) 00½ (ii) 00½
v. Ufupishaji mf.Bakiza
vi.Kukopa mf.alfajiri kutoka Kiarabu
vii.Unasibu mf kichwa
viii.Upanuzi wa maana mf kupe
Alama 09 @1.5

Page 2 of 9
6a. Mtahiniwa anapaswa kutaja hatua muhimu za kuzingatia katika uandishi wa barua za gazetini.
Nyingine:,
i. Kichwa cha barua
i. Lugha fasaha
ii. Mwanzo wa barua ii. Alama za uandishi
iii. Muundo wa barua
iii. Barua yenyewe iv. Mantiko wa mawazo
iv. Mwisho wa barua v. Uwazi na ithibati
vi. Iwe fupi na wazi
v. Jina na anwani ya mwandishi chini kushoto vii. Mwanzo maalum
viii. Anuani ya mwandishi mwisho kushoto
Alama 0.5*5 = 2.5

b. Mtahiniwa anapaswa kuandika barua katika gazeti la Nipashe kwa kuzingatia hatua zilizotajwa
hapo juu.
Mfano :
KUKITHIRI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA ARUSHA (alama 1.5)
Mhariri Nipashe, (alama 01)
Miongoni mwa mambo yanayonikera katika jiji la Arusha ni uchafu uliokithiri huku viongozi wake
wakionesha kushindwa kukabiliana kabisa na hali hiyo.
Ndugu mhariri,nimekuwa nikitembelea maeneo ya Mromboo, Kwa Mrefu, Standi kuu ya mabasi, na
Sakina kutokana na shughuli zangu za kutembeza bidhaa lakini maeno haya yanatia mashaka.
Kumekuwako na maji machafu yanayotiririka kutoka kwenye vyoo Pamoja na rundo la takataka
barabarani jambo hili linaharibu taswira ya jiji hili. Kwa bahatai mbaya viongozi wa mitaa na wajumbe
wamekuwa hawawajibiki katika kuhakikisha mazingira haya yanaboreshwa na kuwa safi, matokea yake
kumekuwepo na ongezeko la watu wanaopata maradhi ya kuambukiza ikiwa ni Pamoja na kuumwa
tumbo, ukurutu na ukuenea kwa harufu mbaya.
Nakumbusha mamlaka husika kwamba, kukosekana kwa afya njema ni miongoni mwa sababu ya
kushindwa kuzalisha na hivyo kudhoofisha uchumi wan chi.viongozi wa serikali za mitaa Pamoja na
wasaidizi wao ambao ni wajumbe wanapaswa kushirikiana kwa Pamoja ili kuhakikisha mazingira
yanakuwa safi. Kwa kufanya hivyo wanaweza kuaminika kwa wananchi na hivyo kuheshimiwa kama
viongozi na hiyo ndo kazi ya uongozi inavyopaswa kuwa
Ni wajibu si kwa viongozi serikalini pekee lakini hata kwa wananchi kuhakikisha mazingira wanayoishi
yanakuwa safi jambo litakalosaidia kuepeka maradhi na mambo mengine yatokanayo na uchafu. Pamoja
na hayo halmashauri zinapaswa kutunga sheria ndogondogo zinazolenga kutunza usafi wa mazingira na
kusimamia.
Musa Nsena,

Page 3 of 9
S.L.P 1015,
Arusha.
Kichwa cha barua alama 1.5 Nyingine:,
Mwanzo alama 01 i. Lugha fasaha
ii. Alama za uandishi
Barua yenyewe alama 02
iii. Muundo wa barua
Mwisho wa barua alama 01 iv. Mantiko wa mawazo
v. Uwazi na ithibati
Anwani ya mwandishi alama 01

7. Mwanafunzi afafanue changamoto sita kati ya hizi zifuatazo


i. Kutiliwa mkazo kwa matumizi ya kiingereza badala ya Kiswahili katika baadhi ya
shughuli za kiutawala. Mfano uandishi wa ripoti.
ii. Maafisa wa ngazi za juu waliwasiliana kwa kiingereza na si kwa Kiswahili.
iii. Kiingereza kilikuwa Lugha ya kufundishia darasa la tano hadi la nane katika shule za
msingi.
iv. Kutumika kwa lugha za kijamii katika shughuli za kidini hali iliyozorotesha maendeleo
ya Kiswahili.Vitabu vya dini kama biblia, vitabu vya liturujia na nyimbo vilitafsiliwa
kwa Lugha za jamii.
v. Kiswahili kuonekana kama ni lugha ya wanyonyaji.
vi. Kukosekana kwa vyombo vya kizalendo vya kuendeleza Kiswahili.
vii. Kushamiri kwa kasumba ya kuthamini kiingereza.
viii. Kutokuhusisha wazalendo wakati wa kusanifisha Kiswahili
Alama 1.5 @_= 09

8. Mwanafunzi ajibu swali hili kama ifuatavyo:


i. Kichwa cha shairi ni LUGHA YA KISWAHILI (alama 01)
ii. (a) Umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika mawasiliano (alama 01)
(b) kuenzi na kuthamini lugha ya Kiswahili. (alama 01)
iii. Mkarara ni “tunu toka kwa manani, tangu kale na azali (Alama 01)
iv. Anamaanisha ni zawadi kutoka kwa Mungu (alama 01)

Page 4 of 9
v. Muundo vina vya kati na mwisho
Muundo wa mizani 16
Muundo wa kituo bahari
Muundo tarbia (alama 02)
Akitaja hoja nyingine sahihi apewe alama.
vi. Vipengele vya lugha ni takriri mfano Kiswahili na tashihisi bara bila simanzi (alama 02)

9. Mwanafunzi ajibu swali hili kama ifuatavyo:


➢ Maana ya mzalendo ni mtu anayeithamini na kuijali nchi yake.
NB. Mwanafunzi anaweza akatoa maelezo mengine yanayofanana na hayo
➢ Atoe hoja tatu (03) kwa kila diwani kuthibitisha dai hili.

DIWANI YA WASAKATONGE
i. Mshairi anapinga uongozi mbaya unaoonea na kukandamiza wananchi. Shairi la “madikteta”
na “unyama”
ii. Mshairi anakemea unafiki na usaliti wa viongozi wa dini na serikali. Shairi la “wasodhambi”
iii. Mshairi anakemea matabaka. Shairi la “wasakatonge”
iv. Mshairi anaping rushwa. Shairi la “mvuja jasho”
DIWANI YA MALENGA WAPYA
i. Mshairi anakemea matabaka. Shairi la “samaki mtungoni”
ii. Mshairi anapinga uongozi mbaya. Shairi la “puuzo”
iii. Mshairi anapinga rushwa. Shairi la “sukari”
iv. Mshairi anakemea tabia ya uonevu. Shairi la “ kifungo”
DIWANI YA MASHAIRI YA CHEKACHEKA
i. Mshairi anakemea tabia ya uzembe na ukasuku “Tuambae ukasuku”
ii. Mshairi anakemea rushwa na ulanguzi “Mwinyi umewasha moto, Angalia usizimwe”
iii. Anapinga uozo katika dini ya kikristo “chanzo cha huo uozo”
Page 5 of 9
iv. Ametoa onyo juu ya wale wanaowadharau watu wengine “utu umekuwa kima”

10. Mwanafunzi atatakiwa kuonesha falsafa au imani za waandishi waaili wa tamthilia kama ifuatavyo.
➢ Falsafa ni imani na mwelekeo wa mwandishi katika kazi anayoitunga. Ni kile
anachokiamini mtunzi wa kazi ya fasihi.
TAMTHILIYA YA KILIO CHETU
Mwandishi anaamini yafuatayo:
i. Elimu ya jinsia ikitolewa kwa watoto itawasaidia kupambana na hatari ya kuambukizwa
virusi vya UKIMWI
ii. UKIMWI hauna tiba na humpata mtu yeyote bila kujali umri.
iii. Maambukizi ya ugonja wa UKIMWI ni kwa njia ya ngono na sio kugusana.
iv. Marafiki wabaya ni chanzo cha kuporomoka kwa maadili mfano Jumbe, Chogo, Mwarami
na Joti.

TAMTHILIYA YA NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE.


Mwandishia anaamini yafuatayo:
i. Kuchanganya Mapenzi na kazi hufanya kazi kuharibika kam aliyofanya mhusika ngoswe.
ii. Ukosefu wa elimu, hospitali na barabara ni chanzo kikubwa cha umaskini.
iii. Ulevi ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika jamii.
iv. Imani za uchawi na ushirikina hurudisha nyuma maendeleo

TAMTHILIYA YA ORODHA
i. Mwandishi anaamini kuwa ukweli , uwazi na uadilifu ni mambo ya muhimu katika
kupambana dhidi ya UKIMWI.
ii. Mwandishi anaamini kuwa jamii ikipatiwa elimu itajinusuru dhidi ya janga la Ukimwi.

Page 6 of 9
iii. Mwandishi anaamini kuwa ukali kupita kiasi wa wazazi hausaidii katika malezi ya
watoto, bali kukaa nao na kuwaelimisha. Kukukurukakara
iv. Mwandishi anaamini kuwa usaliti ni chanzo cha ugomvi na magonjwa ktika jamii.

11. Mwanafunzi atatakiwa kufafanua vipengele vifuatavyo ( Vinaweza kutofautiana pia kulingana na
ulivyotumika katika riwaya husika

RIWAYA YA WATOTO WA MAMA NTILIE


Mwandishi ametumia vipengele vya lugha kama
i. Tamathali za semi kama vile Paa tashibiha, sitiari na tashihisi.
➢ Tashibiha |: Akamshika mumewe kwa mkono mmoja kama bua
: Akaanguka chini kam mzigo .
:Miguu ile peku peku……. Migumu kama ya mamba
: Kurwa alilruka nyama kama chui.
➢ Tashihisi : Makucha ya dunia yaliwatazama bila huruma
: Jiji lilikua limeshona midomo yake
: Mvua ilikua imeaga dunia
:……. Miguuni raba zilicheka kwa huzuni.
ii. Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa, kama vile :
➢ Takriri: Kukukurukakara, Kukukurukakara, Kukukurukakara
: Paa! Paa! Paa! Bastola ililia
: Twende twende
: Baba! Baba! Amka Baba!
➢ Onomatopeia/ Tanakali sauti
: Filimbi kilia pee! Pee!
: Mbwa alilia bwee!
: Akatema phuu!
iii. Matumizi ya lugha ya kingereeza kama vile faster faster mama, Iodine , Empire unama.

Page 7 of 9
RIWAYA YA TAKADINI
Mwandishi ametumia
i. Misemo : Pokea upewacho
: Maisha ni matamu
: Mume ni kiungo kwa mawanamke
: Penzi la lake halikufua dafu
: Mwanga hufukuza woga wote

ii. Tamathali za semi kama vile


➢ Tashibiha : Mtoto alionekana mweupe sawa na funza mkubwa
: Muda huenda polepole mithili ya kakakuona

➢ Tashihisi : Ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya.


: Ubongo wake uliathirika kwa mawazo uliufukuza usingizi.
➢ Ametumia mbinu nyingine z akisanaa kama vile
Takriri : Wewe ni sope , sope sope
: Najua najua

RIWAYA YA JOKA LA MDIMU


i. Mwandishi ametumia
➢ Misemo na methali kama vile
a. Misemo : Asiye na bahati habahatishi
: Asiyezika hazikwi
b. Methali : Asilojua mtu ni usiku wa kiza
: Biashara haigombi
ii. Tamathali za semi kama
a. Sitiari : “ Sote ni kobe”
: Sarahande wetu mboga kweli kweli
b. Tashihisi : Utumbo ulimlaumu
Page 8 of 9
: Mvua ikarindima kwa kiburi na kumwamdhibu vibati vibovu.

c. Mbinu nyingine za kisanaa


➢ Tanakali sauti : Saa ya mezani iliendelea kugonga ta! Ta! Ta!
➢ Takriri : Shetani oyee! Shetani oyee! Sheyani uhinja!

MGAWANYO WA ALAMA KWA SWALI LA 9 HADI 11


i. Utangulizi mzuri …………………… alama 2
ii. Kiini hoja tatu kila kitabu…………………. Alama 2 @ =12
iii. Hitimisho linaloendana na swali……… alama = 1

JUMLA ALAMA 15 @ SWALI

Page 9 of 9

You might also like