Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

Seventh-day

Adventist Church P. O. BOX 99, IGANZO

MBEYA, TANZANIA
Southern Highlands Conference Mobile:+255 787 481 915
Office of Youth/Chaplaincy & Music director +255 614 235 016
Email: mesjanzi@gmail.com Website: www.shcadventist.or.tz

03/07/2024
Wachungaji wa Mitaa,
Wazee wa Makanisa,
Waratibu wa Kanda
Viongozi wa Vijana Makanisani,
Jimbo la Nyanda za Juu Kusini.

YAH: MASTER GUIDES & SYL WALIOHITIMU NA WALE WALIO MAFUNZONI

REFRESHER CAMP DODOMA 08 -15 DECEMBER 2024

Nawasalimu katika Jina la Bwana, Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Wapendwa nawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Nawashukuru sana kwa
ushirikiano mliouonyesha kwenye zoezi la Kambi la Vijana Itamboleo, Bwana awabariki
sana.

Napenda kuwajulisha kuwa Union imeandaa Kambi maalumu sana la kufanya upya na
kuhitimisha Master guides na SYL na kuzindua makadi mapya kwa Mafunzo ya viongozi
hao wa idara ya Huduma za vijana. Kambi litafanyika huko Dodoma tarehe 08 -
15/12/2024. Naomba ifahamike fika kuwa Masterguides na SYL wote waliohitimu ambao
hawatafika katika kambi hilo hawatatambuliwa tena kama Masterguides au SYL mpaka
atakapokuwa ameanza upya na kuhitimu kupitia makadi mapya yatakayokuwa
yamezinduliwa kambini hapo.

Kiingilio cha kambi ni Tsh. 25,000/= Viingilio vitakusanywa na Area Coordinator wa

kanda husika, yaani tunategemea Bank Pay In Slip moja tu kwa kila kanda, naye
ataziingiza kwenye Account ya Jimbo letu benki ya CRDB Account No.015C517327301
Southern Highlands Conference of SDA Church, na baadaye zitatumwa huko
Union. Mwisho wa kulipa kiingilio hapa kwetu ni tarehe 10/10/2024. Tafadhali anzeni
maandalizi mapema.

Nawatakia baraka za Bwana katika Maandalizi yenu

Mch. Meshack J. Zilakwega

MKURUGENZI IDARA YA HUDUMA ZA VIJANA, SHC

Nakala kwa : Maofisa, SHC

Wakurugenzi, SHC
MISSION:“To call all people to become disciples of VISION:“In harmony with Bible revelation,
Jesus Christ, to proclaim the everlasting gospel Seventh-day Adventists see as the climax of God’s
embraced by the three angels messages (Revelation plan the restoration of all this creation to full
14:6-12), and to prepare the world for Christ soon harmony with His perfect will and righteousness.”
return.”
Seventh-day
Adventist Church P. O. BOX 99, IGANZO
MBEYA, TANZANIA
Southern Highlands Conference Mobile:+255 787 481 915
Office of Youth/Chaplaincy & Music director +255 614 235 016
Email: mesjanzi@gmail.com Website: www.shcadventist.or.tz

03/07/2023
Wachungaji wa Mitaa,
Wazee wa Makanisa,
Waratibu wa Kanda
Viongozi wa Vijana Makanisani,
Jimbo la Nyanda za Juu Kusini.

YAH: MAHUBIRI YA VIJANA E.E.I 22/09 -05/10/2024

Nawasalimu katika Jina la Bwana, Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Wapendwa napenda kuwakumbusha kuhusu ratiba ya Mahubiri ya vijana E.E.I

iliyotolewa na Division. Tutakuwa na Mahubiri yatakayoendeshwa na vijana walioko
makanisani kwetu hapo tarehe 22/09 - 05/10/2024. Makubaliano yetu na viongozi
wa vijana ni kwamba kila kanda itafanya mahubiri hayo kupitia vijana wa kanda husika.
Naomba Wachungaji na wazee wa makanisa mtoe ushirikiano chanya kwa vijana wetu
ili kuwawezesha kufikia malengo yao ya Utume waliyojiwekea.

Pia jambo jingine ni kwamba baada ya kumaliza kambi la vijana kinachofuata ni ujenzi
wa nyumba ya Mjane huko Makete mkoani Njombe, naomba Area Coordinators fedha
zilizokusanywa zitumwe mahali sahihi kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa awali ili
kazi ianze mara moja. Na kwa kuwa kila kanda inajua goli lake tafadhali kamilisha goli
lako, mwisho ni tarehe 15/07/2024

Aidha nipende kuwataarifu kuwa Effort ya Nalasi - Tunduru inahamishiwa mwaka ujao
ili kutoa nafasi kwa vijana wetu kushiriki kikamilifu katika Effort za vijana za kila Kanda
Jimboni hapa.

Mungua awabariki.

Mch. Meshack J. Zilakwega

MKURUGENZI IDARA YA HUDUMA ZA VIJANA, SHC

Nakala kwa : Maofisa, SHC

Wakurugenzi, SHC

MISSION:“To call all people to become disciples of VISION:“In harmony with Bible revelation,
Jesus Christ, to proclaim the everlasting gospel Seventh-day Adventists see as the climax of God’s
embraced by the three angels messages (Revelation plan the restoration of all this creation to full
14:6-12), and to prepare the world for Christ soon harmony with His perfect will and righteousness.”
return.”

You might also like