Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

Utafiki kuhusu afya ya uzazi naya sehemu za uzazi na

Ulemavu ndani ya waliohamishwa jijini Kampala

Women’s Refugee Commission na Refugee Law Project


Disemba 2013

REPOTI KWA WALIOSHIRIKI

SISI NI NANI?
Tume la wakimbizi Wanawake (WRC) ni
Afya ya uzazi na ya sehemu za
shirika lisilo la kiserilali linalopatikana
Marekani. Sisi ni shirika la utafiti na uzazi
utetezi linalofanya kazi ya kulinda haki, Kila mtu ana haki ya kupata habari na
huduma anazohitaji ili apate kutunza vizuri
usalama na ustawi wa jamii
afya ya uzazi na ile ya sehemu za uzazi.
zilizohamishwa kwa dunia nzima.
Jambo hili linaangalia pia kujifunza jinsi
Tunafanya kazi na serikali na mashirika mwili unavyotumika wakati mtu
ya umoja wa mataifa na mashirika ya anapokuwa mtu mzima na jinsi ya kujenga
kimataifa. uhusiano wa kimapenzi wenye usalama.
Hii ni pamoja na kupewa mpango wa
Refugee Law Project (RLP) ni mradi wa uzazi, kama vile kondomu na vidonge kwa
kufikia jamii wa chuo kikuu cha njia ya usalama, bora, nafuu
makerere Tunafanya kazi ya kuwezesha inayokubaliwa; kuweza kupata huduma ya
wahamiaji naa jamii zinazowahifadhi ili afya inayosaidia wanawake kuwa na
waweze kufurhia haki za binadamu na mimba na kujifungua kwa usalama;
kuishi maisha yenye kuheshimika. Hii kuweza kupata huduma kwa waathirika
wa unyanyasaji wa kijinsia, na kuwahi
inafanyika kupitia kwa utafiti, na kutoa
kupata habari na huduma kuhusu jinsi ya
msaada wa kisheria, huduma za afia ya
kuzuia na kutibu magonjwa ya zinaa, kama
kiakili, kisaikolojia na kijamii, huduma ya Virusi Vya Ukimwi.
kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na
kingono, na ufuatiliaji wa utawala, vurungu na haki ya mpito. Wakimbizi
wenye ulemavu ni miongoni mwa
walengwa muhimu wa RLP, na RLP
inafanya kazi nao kuhakikisha ya
kwamba wanafurahiya haki zao.

KWA NINI TULIKUJA KAMPALA?


Turizuru kampala kuanzisha utafiti ili
tujue zaidi kuhusu mahitaji ya afya ya
uzazi na ya sehemu za uzazi na mambo
Wana memba wa tiimu ya utafiiti yanayowagusa watu wenye aina tofauti

1
za ulemavu ( ya kimwili, hisia na wa Kwa kusikiliza washikiriki tuliweza kujua
kiakili na ulemavu mwingi zaidi ya moja). kuhusu mawazo yao na uzoefu wao.
Tulitaka pia kujifunza zaidi kuhusu ni nini Tunashukuru kwa kuwa tuliweza
watu wenye ulemavu wanafikiri kukutana nao na kuturuhusu kujadiri
ingefanyika ili kuboresha hali, ikiwa ni nao na kutupa taarifa na historia zao
pamoja na nini wao wenyewe wanaweza kwa iliyo muafaka.
kufanya.
TULIJIFUNZA NINI?
TULIFANYA NINI KAMPALA? Matokeo ya awali yanaonyesha
Kwa zaidi ya wiki mbili mwezi wa kwamba kwa ujumla watu kadhaa
disemba na wiki moja ya mwezi wa wenye ulemavu walijihisi ya kwamba
Januari 2014, tume la wakimbizi wanadharauliwa sababu ya ulemavu
wanawake (WRC) lilifanya kazi na timu wao. Washiriki wote na wahudumu
ya RLP ya ustawi wa Afya ya Akili, ya walihisi kwamba ingekuwa vema watu
kisaikolojia, na kijamii kuwapa mafunzo wenye ulemavu waangaliwe zaidi.
watafiti wakimbizi 12 na waajiri Pendekezo lenye uzito hasa kutoka kwa
washiriki wa kuendesha utafiti miongoni wahudumu ni kwamba, wapelekwe kwa
mwa wanawake wakimbizi wenye nnchi ya tatu kwa kuwa wengi wanahisi
ulemavu wa umri wa myaka 20-49 na kwamba huduma wanayopata kampala
vijana wasichana na wavulana wa umri haitoshi kwa ulemavu wao unaohitaji
wa myaka 15-19 jijini Kampala. Watafiti tegemezi. Mapendekezo mengine ni
wakimbizi na waajiri washiriki walikuwa pamoja na kuwa wa kwanza kupata
pamoja na watu wenye ulemavu. huduma badala ya kusubiri na kila mtu
msatari. Mapendekezo ya ziada ni
Katika ujumla, timu ya utafiti ilikutana pamoja na kupata nafasi za elimu na
104 wakimbizi wenye ulemavu, 75 mafunzo ya kazi za mikono kwa watu
wanawake na wasichana, na 29 wenye ulemavu na wale
wanaume wenye matatizo ya kimwili, ya wanaowachunga ili waweze kuwasiliana
kuona, ya kiakili, ya kusikia na matatizo vizuri na watowa huduma na kupata
mengine mengi. Walikutana na nafasi za kazi na kupata mapato.
wakimbizi ambao hawawezi kutoka
nyumbani, na wahudumu 32, na Kulingana na huduma za afya, baadhi ya
wanamemba wa familia ya watu wenye watu wenye ulemavu walitaarifu ya
ulemavu. Shughuri ziliendeshwa kwa kwamba walitunzwa vizuri na
Kiswahili, kisomali, Kinyarwanda na kwa wahudumu wa afya sababu ya ulemavu
ishara za luga ya Luganda. Baadhi ya wao. Lakini wengi wa washiriki na
shughuri zilifanywa kwa vikundi na hali wanohudumia watu wenye ulemavu
kadharika nyingine zikafanywa kwa watu walilalamikia huduma za afya ambazo
binafsi. hazitoshi na kuchukuliwa vibaya na
wafanyakazi wahuduma za afya.

2
Kukosa utafsiri, pamoja na lugha kwa
ishara, kukosa usafiri wa kwenda kwa
vituo vya afya, hali kadharika kukosa
pesa za kulipa wahudumu wa afya
vilionekana kuwa vikwazo vya kupata
huduma. Watu wengi kama wakimbizi
na watu wenye ulemavu walionekana
kukubali ya kwamba walidharauliwa
sana na kutupiliwa mbali na wahudumu Picha: Mfano wa kupanga sehemu za mwili
wa afya wakati walikuwa hawana pesa, ilivyo fanywa na wanaume wenye ulemavu
wamoja wao walisema kwamba wa kiakili. (Credit: RLP)
walikuwa wanasubiri kupokea huduma
siku yote, lakini wakarudi nyumbani bila Washirika wengi walikuwa wanafahamu
kupata huduma “ukiwa mlemavu Virusi Vya Ukimwi au baadhi ya alama za
unasubiri,unasubiri,unasubiri.” magonjwa ya zinaa, hata kama walikuwa
hawafahamu majina ya hayo magonjwa
UFAHAMU WA AFYA YA UZAZI NAY A na sababu zake. Waliweza tena
SEHEMU ZA UZAZI kuorodhesha mbinu nyingi za kuzaa kwa
Watu wengi walisema InterAid, hospitali mpango zikiwemo mpira wa condomu,
ya Mulago, RLP, African Centre for vidongo ambavyo mwanamke angeweza
Torture Victims (ACTV) na Kampala City kutumia kila siku au shindano ambayo
Council Authority (KCCA) wanatowa mwanamke angeweza kudungwa kila
taarifa na huduma kuhusu afya ya uzazi myezi mitatu. Wengine walitaja kifaa
na ya sehemu za uzazi, hata kama cha kuweka kwa mfuko wa uzazi, kifaa
kupata taarifa za kingono iliripotiwa chenye umbo la T ambacho kinawekwa
kuwa ngumu hasa kwa watu ambao tumboni mwa mwanamke, hali
wana matatizao ya kiakili. kadhalika kufunga kizazi cha mwanamke
na mwanaume. Wakati watu wachache
Wakati baadhi ya washirika walijuwa waliweza kutaja mbinu za kupanga uzazi,
kwenye sehemu za uzazi za mwanaume kwa ujumla kulikuwa kutoamini,
na mwanamke zinapatikana, wengi wao kilikuwa pia na imani potofu kuhusu njia
walikua hawaelewi vizuri mwili yao nyingine za kupanga uzazi. Wengi
Wale wenye matatizo ya kakili walikuwa walihofia ya kwamba mpira wa
na magumu zaidi kutofautisha na kondomu unaweza kukatalia ndani ya
kuonyesha sehemu za mwili, na kwa mwili wa mwanamke au unaweza
ujumla walikuwa hawajui jinsi kusababishia mwanamke kupata
vinatumika. ugumba. Washiriki ambao walikuwa
hawawezi kutoka nyumbani au ambao
Vijana wasichana na wavulana, nao kwa walikuwa na ulemavu wa aina nyingi
ujumla walijua zaidi kuliko watu wazima. walionekana kujua mambo madogo
kuhusu afya ya uzazi na ya sehemu za

3
uzazi hasa kwa kuwa walikuwa na wakati Washiriki walisema ya kwamba Wakati
mdogo wa kupata taarifa kutoka nje msichana au mwanamke mwenye
ulemavu amekuwa tayari kujifungua
Baadhi ya njia za kupanga uzazi mototo wake, angejifungulia hospitalini
Mpira wa kondomu Vidonge au nyumbani akiwa na mkunga wa jadi,
mama yake au akiwa pekeyake kwa siri.
Ikiwa angejifungulia hospitalini,
angetembea kwa mguu au kuenda na
gari. Pia walisema ya kwamba angeenda
Shindano Kifaa cha kuweka na mtu wa familia au baba ya mtoto.
tumboni mwa
mwanamke Washiriki wengi walihisi kwamba
wanawake na wasichana wenye
ulemavu na wajawazito hawatunzwi
vizuri na hawaheshimiwe na wahudumu
kipandikizi Kwa taarifa zaidi wa afya wakinukuru maneno kama
kuhusu njia za
“Unawezaje kubeba mimba na wewe ni
kupanga uzazi
tembelea kituo cha
mkimbizi mwenye ulemavu?” na “Ni
afya. shida anajifungua shida nyingine.”

UZOEFU KWA UJUMLA WA WASIWASI WA USALAMA


WANAWAKE NA WASICHANA WENYE Washiriki wenye ulemavu kwa ujumla
ULEMAVU AMBAO WANABEBA MIMBA walikubali ya kwamba hawana usalama
Washiriki kwa ujumla walikubali ya hasa wakiwa kwa vyoo na kandokando
kwamba wakati msichana au ya makazi yao. Izo sehemu mbili zilitajwa
mwanamke mwenye ulemavu anabeba kuwa ni sehemu za hatari na kuna
mimba awe ameolewa au hajaolewa uwezekano wa kushambuliwa na
inaathiri jinsi anavyohudumiwa na kubakwa.
familia yake na majirani. Ikiwa
ameolewa, mimba inapokelewa kwa
furaha na wanandoa na familia. Ikiwa
hajaolewa anabaguliwa. Familia na
majirani wanasema ya kwamba ni
“Malaya” ya kwamba “alifanya tabia
mbaya” au ya kwamba “alibakwa.” Kwa
msachana kama huyo ambaye
hajaolewa, washiriki walisema ya
kwamba angeweza kuchunga mtoto au
wazazi wake wanamlazimisha kutoa Photo: Choo (imechukuriwa na: RLP)
mimba.

4
Washiriki wengi walikuwa wanafahamu UTENDEWAJI NA MAMBO
huduma inayotolewa baada ya kubakwa YANAYOKUBALIWA
na faida ya kutafuta huduma ya afya Washiriki wote walikubali ya kwamba
baada ya kupitia unyanyasaji wa ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu
kingono. Kwa ujumla sehemu nyingine haukubaliki. Wakati kulazimishwa
ambazo washiriki walijihisi kutokuwa na kufunga kizazi ilionekana sana kuwa
usalama ni zile ambazo zinahusiana na haikubaliwi washiriki wengi waliripoti ya
na kwenye wanapita kwa mfano sehemu kwamba wasichana wenye ulemavu
zenye madaraja ya kupanda au karibu na ambao hawajaolewa au wamama
barabara au karibu na maji. Washiriki wanaweza kulazimishwa kutumia mbinu
walijihisi kutokuwa na usalama hasa kwa za kupanga uzazi kuzuia mimba ya pili.
walemavu wa mwili na wenye macho Kufunga kizazi pia ni swala lililoletwa
yaliyo na shida. kwa wanaume na vijana wenye ulemavu
hata kama kijana au mwanaume
Washiriki wengi hasa wale ambao mwenye ulemavu angebebesha
hawewezi kutoka nyumbani walisema ya msichana mimba washiriki waliweza
kwamba wanajihisi kuwa na usalama kufikiri ya kwamba alikuwa anatumia
wakiwa na watu wa familia zao na wale nguvuzake za wanaume: “ Kijana
ambao wanaowahudumia. Wengine angeonekana kama mwanaume
hasa wenye ulemavu wa kiakili walijihisi mwenye nguvu nyingi”
kuwa na usalama wakiwa na mshauri wa
RLP ambaye wangeweza kuambia TUTAFANYA NINI SASA?
wasiwasi wao. Tume la wakimbizi wanawake na RLP
watachambua zaidi taarifa na kuaandika
Je, ni huduma gani muhimu za afya kwa repoti kamili ya matokeo ya utafiti na
waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia? mapendekezo (mapendekezo kutoka
Kama mwenye alinusurika unyanyasaji wa kwa washiriki) kuhusu ginsi ya
kijinsia anataka huduma za afya mara kuboresha huduma za afya ya uzazi na
moja baada ya shambulio, anaweza: ngono kwa watu wenye ulemavu jijini
 Kupokea huduma za majeraha ya Kampala. Tutaongelea ripoti hii na
mwili wafadhili, Umoja wa Mataifa, Shirika la
 Kutumia vidonge kuzuia mimba umoja wa mataifa linalowahudumia
ambayo haihitajiki (Katika siku 5) wakimbizi( UNHCR) na mashirika yasiyo
 Kutumia dawa ya kuzuia magonjwa
ya kiserikali ya kimataifa na yale ya
ya zinaa.
yakitaifa.
 Kutumia dawa ya kuzuia Virusi Vya
Ukimwi /VVU (Katika siku 3).
 Kupata msaada wa msingi wa hisia. Utafiti kama huu unafanyika pia nchini
 Kupata baruwa za kuwatuma ili Kenya na Nepal. Tutaandika matokeo ya
wapate huduma zingine. utafiti kutoka kwa nchi hizi tatu kwa
ripoti moja na tutatoa utetezi wetu kwa

5
serikali, Mashirika ya umoja wa mataifa
ya kimataifa na yale ya kitaifa kuweka
nguvu ili kuboresha afya ya uzazi na ya
sehemu za uzazi kwa watu wenye
ulemavu kwa ulimwengu.

UNAWEZA KUFANYA NINI KAMA


UNATAKA KUSOMA MENGI KUHUSU
UTAFITI HUU NA RIPOTI HII?
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:
Yusrah Nagujja414340547/0776897107.
y.nagujja@refugeelawproject.org.

Ikiwa ungependa taarifa zaidi kuhusu


repoti kamili na utetezi wa Tume la
wanawake wakimbizi (WRC) kuhusu
matukio ya utafiti huu, tafadhali
wasiliana na Mihoko Tanabe kwa
info@womenscommission.org au
tembelea
www.womensrefugeecommission.org.

Matukio ya utafiti huu yameandikwa na


Mihoko Tanabe na yakaangaliwa upya
na Yusrah Nagujja, Apio Molly na Sandra
Krause. Yalisahihishwa na Diana Quick.
Sanamu zirichorwa na Stacey Patino.
Picha zilichukuliwa na RLP.

Utafiti ulifanywa na: Afugu Miriam


(Mtafsiru wa ishara); Apio Molly
(Aliyeweka sauti za rekodi kwa
maandishi); Banzi Josepha; Berlin
Abdulkadir; Chirwa Francis; Gato
Ndabaramiye Joshua; Fiona Iradukunda;
Mami Agnes; Namiyingo Agnes
(Aliyeweka sauti za rekodi kwa
maandishi ); Nimo Hassan Ali; Pascaline
Kwinjda; na Viviane Mushimiyimana. Jan 2014

6
Women’s Refugee Commission | 122 East 42nd Street | New York, NY 10168-1289
212.551.3115 | info@wrcommission.org | womensrefugeecommission.org

You might also like